Si kila wakati maombi yatakuwa ni mazungumzo ya utulivu na amani, wakati mwingine maombi hugeuka kuwa mapambano, na ung’ang’anizi, na usumbufu. Kuna nyakati Mungu anabadilika tabia, kuonyesha kama hakujali hivi, hakusikii hivi, Sio kwamba anakuonea, au anafurahia wewe kuendelea kuteseka katika hali hiyo, hapana bali anafanya hivyo ili kukutengeneza wewe, kwa namna usiyoijua.
Ni lazima ufahamu, Mafanikio ya maombi si lazima yawe majibu, bali mafanikio ya maombi ni mabadiliko yako. Mungu akitaka kukutengeneza, ili tegeo lako lote liwe kwake, hukawia kutimiza ombi Fulani, ili uongeze tegemeo lako lote kwake.
Imani, tumaini, ukomavu, na Upendo wa ki-Mungu, mara nyingi hujengwa katika namna hiyo ya maombi ambayo yanakugharimu kumtaabisha Mungu.
Yakobo alipomtaka Mungu ulinzi, Mungu hakuonyesha kujali hata kidogo, Hivyo mazungumzo yao, yakabadilika kutoka kuwa ya amani, hadi mapambano, wakapigana mweleka usiku kucha mpaka akajeruhiwa uvungu wa paja, ijapokuwa maombi yalikuwa ni ya ung’ang’anizi sana, ya kuumwa, ya kudhoofika, ya kuchakaa, ya kukonda, ya njaa, lakini hakujua anakwenda kubadilisha hali yake ya ndani, alikuwa anaandiliwa kuwa ISRAELI, na sio Yakobo tena mdhaifu.(Mwanzo 32:24-28)
Fahamu kuwa maombi hufanya jambo la ziada juu ya majibu. Wakati mwingine unaweza usijibiwe kabisa hata hilo ombi unaloliomba lakini fahamu kuwa hutabaki kuwa yule yule.. Mtume Paulo, alimlilia sana Mungu (maombi ya ung’ang’anizi), kuhusu mwiba uliokuwa ubavuni mwake uondolewe, ukweli ni kwamba haukuondolewa, lakini alitoka na ufunuo mpya wa “Neema ya Mungu” ukambadilisha mtazamo wa maisha yake moja kwa moja kuhusu Mungu, Maana yake ni kuwa kama mwiba ule usingemtesa na kumlilia sana Mungu asingeielewa neema ya Mungu, ambayo mpaka leo hii tunajifunza kupitia masumbufu yake.
2Wakorintho 12:7-10
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
Hii ni siri ambayo wengi hawaijui, Uonapo upo kwenye Wakati mgumu na umeomba kwa namna ya kawaida huoni dalili yoyote ya kujibiwa, anza maombi ya kung’ang’ana, funga zaidi, lia zaidi, kemea zaidi, zama zaidi …Fanya hivyo kwasababu ipo kazi ya ziada Mungu anataka kuitenda ndani yako zaidi ya majibu unayoyataka,. Usiridhike tu na maombi ya utulivu, shindana na Mungu wako, ng’ang’ana sana, ikiwa hujajibiwa jana, endelea leo, tena kwa nguvu zaidi, ukiona hali imekuwa mbaya, usipoe, shughulika na Mungu zaidi na zaidi, hakuna kukata tamaa, hakuna kurudi nyuma, kwasababu Maombi hufanya kazi nyingine ya ndani zaidi ya majibu tu..
Mwisho utauna uzuri wa Mungu, jinsi atakavyokuleta katika matokeo bora zaidi, ambayo utamshukuru Mungu maisha yako milele. Hivyo fahamu kukawia kwake ni kwa faida yako.
Maombolezo 3:31-33
31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele.32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha
Mungu akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NGUVU YA MAOMBI
MWONGOZO WA MAOMBI YA FAMILIA
MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
Print this post
Huu ni mwongozo wa maombi yetu ya kambi July 30 – Aug 2.
Kanisa la Nuru ya Upendo
Daresalaam Tegeta. Bofya hapa
👇 📥
Miongozo mingine.
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
Ikiwa wewe ni mwanandoa, ni busara kuwa na maombi yako maalumu kwa ajili ya ndoa yako.
Waweza kutenga siku kadhaa katika wiki, au mara mbili katika wiki, kuwa na maombi maaalimu marefu kwa ajili ya ndoa yako.
Maombi ni nyenzo muhimu katika kuendesha na kufanikisha sehemu zote zamaisha yetu, huduma inahitaji maombi, kanisa linahitaji maombi, taifa linahitaji maombi, wewe unahitaji maombi, vivyo hivyo na ndoa yako pia inahitaji maombi ili iwe na ustawi Bora katika nyanja zote..hata kama huoni tatizo lolote ndani ya ndoa ..bado unahitaji maombi sana.
Kwanini maombi? Ni kwasababu njia pekee ambayo Mungu huweza kuyaingilia maisha yetu ili ayatengeneze vema basi ni kwa njia ya maombi.
Ndoa inaweza ikadumu lakini isiwe na amani, ndoa inaweza ikawa na amani lakini isiwe na mafanikio, ndoa inaweza ikawa na mafanikio lakini imekosa Mungu, vilevile inaweza ikawa na umoja lakini imejaa wivu, inaweza ikawa haina shida lakini watoto wanaokuja wakawa na matatizo, inaweza pia ikawa sawa leo, lakini kesho shetani akaishambulia….Hivyo suala la kuombea ndoa ni jambo la muhimu sana.
Huu ni mwongozo wa maeneo muhimu ya kuombea kila uingiapo katika maombi ya namna hii. (Kila kipengele tumia dakika 30)
Mungu alipomuumba mwanaume na mwanamke na kuwaleta katika ndoa aliwafanya mwili mmoja tena..Maana yake aliweka Muunganiko usiowezekana kibinadamu Wa umoja..
Mathayo 19:5
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
Hivyo hakikisha unaombea ndoa yako Bwana adumishe umoja wenu, uwe umoja kwelikweli, na kamwe pasiwepo matengano. Maana huo ndio mwanzo wa ndoa thabiti
Omba kwa nguvu, huku ukivunja roho za matengano, ukiangalia zaidi maeneo ambayo unaona kabisa yanahatarisha umoja wenu, yenye dalili ya kutaka kuwaachanisha hayo ndio uyaombee zaidi, ikiwa ni kazi, au watu, au magonjwa, mwambie Bwana apatengeneze hapo..tumia si Chini ya dk. 30 kuombea eneo hilo moja tu.
Hivi viwili navyo ni nyenzo kubwa sana katika ndoa thabiti. Bwana aliagiza mwanamume ampende mke wake kama mtu apendavyo mwili wake mwenyewe.. vivyo hivyo aliagiza mke amtii mumewe Kama mtumwa kwa Bwana wake.
Waefeso 5:22-25
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. [23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. [24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. [25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
[23]Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
[24]Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Hivyo ikiwa wewe ni mke, mwombee sana mumeo Bwana alidumishe pendo lake kwako, lakini pia ikiwa wewe ni mume mwombee mkeo Bwana amjengee utii kwako.
Lakini pia jiombee wewe sawasawa na jinsia yako Bwana akuzidishie upendo na utii..kwasababu vyote hivi ni nyenzo kwa wote, vizidi bila kupungua nguvu kwa jinsi siku zinavyokwenda.
Ndoa ikikosa maelewano hupoteza dira yake.
i) Omba Mungu ajenge usemi mmoja yaani lugha ya maelewano kwanza katika eneo lenu la kiroho.. Maana yake wote msisimame katika Bwana (muokoke), ikiwa mmojawapo hajaokoka mwombee neema Ya wokovu, injili imchome abadilike na kumpokea Kristo, na huku ukimhubiria pia.
ii) Omba pia Mungu awape Maelewano Katika majukumu yenu ya kiroho(utumishi). Mfano ratiba za ibadaza nyumbani, maombi, mikesha, mifungo, ushuhudiaji, na utoajik.
Ikitokea mmoja wenu haafiki majukumu hayo, si rahisi mwingine kutekeleza na matokeo yake inakuwa ni kushindwa kutimiza lengo kuu la kindoa. Kumbuka mmewekwa katika ndoa ili mumtumikie Mungu pamoja..hivyo jambo hilo ni lazima Lipewe nafasi ya kwanza na kubwa katika ndoa.
iii) Lakini pia omba maelewano katika mambo Yote ya kimaisha.
Mfano mikakati ya kimaendeleo, matumizi ya kifedha, n.k. huku ukigusia Maeneo yako yote ambayo unaona mikwaruzano inatokea, Au dalili hizo kutokea..ukiharibu hivyo vyanzo kwa maombi yako.
iv) Lakini pia Bwana awajengee mioyo ya kusamehe na kuachilia.
Ndoa nyingi zimeingia dosari, kupoa hata kufikia hatua ya kuvunjika kabisa kutokana na kuwa zimepoteza mioyo wa kusamehe na kuachilia Kwasababu ya majeraha au makosa yaliyofanyika nyuma..
Wakolosai 3:13
[13]mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Mwambie Bwana sikuzote, wote mpewe mioyo ya kusamehe na kuachilia.
Hapa pia ni mahali pa kupaombea sana.. Wengi wanadhani wanaweza linda ndoa zao kwa kuweka sheria kali, kwa kufuatilia nyendo zao, kwa kuwavisha mavazi ya kuficha mpaka nyuso, Lakini uhalisia ni kwamba ikiwa mtu amekosa uaminifu, huyo kamwe halindiki, atakuzunguka tu, Hivyo omba kwa Bwana juu ya mwenzi wako, na kwako pia Bwana awaumbie moyo wa uaminifu. Hilo linatosha kuwa ulinzi mkubwa kwa ndoa yako.
Nyuma ya mafanikio ya kitu chochote chema, ni lazima utaona uvumilivu ulipewa nafasi, hata huduma ya kufanikiwa hutegemea uvumilivu. Ndoa haimaanishi kila siku itakuwa ni furaha tu, zipo nyakati za kupishana kibinadamu, za kusemwa vibaya, za kuudhiwa zipo nyakati za kupungukiwa, yapo madhaifu pia.. Hivyo omba moyo wa uvumilivu thabiti uwe juu ya kila mwanandoa.. kuanzia wewe mwenyewe.Ili nyakati ngumu zitakapopita pasiwe na wepesi wa kuiacha ndoa au kuchukua Hatua za madhara.
Ndoa ikikosa mwelekeo wa ki-Mungu huishia pagumu. Omba Mungu awape dira sahihi isiyo na majuto katika mikakati yenu yote ya kimaisha.
Omba Bwana ayanyoshe mapito yenu, awafanikishe, awaepushe na njia ya majuto na upotevu wa yule mwovu.. kwasababu maandiko yanatuonyesha ndoa ya kwanza ilivamiwa na uharibifu kwasababu ya udanganyifu wa ibilisi, kwa kitendo cha Hawa kusikiliza na kuifuata njia nyingine ambayo hakuagizwa na Mungu, na matokeo yake alipokula tu lile tunda ikasababisha matatizo makubwa ambayo mpaka sasa tunayaona ..
Mafanikio Ya ndoa hutegemea pia mahusiano mema kwa ndugu na wakwe..Musa alifanikiwa kuiongoza huduma vizuri kwasababu alikuwa na mahusiano mazuri na mkwe wake Yethro. Ruthu alifanikiwa kuolewa na Boazi mtu mkuu na mwenye uwezo kwasababu alikuwa na ukaribu na mama mkwe wake Naomi hata baada ya kufiwa na mumewe.
Vivyo hivyo na wewe pia uhusiano wako ukiwa mzuri na watu wa upande wa mwenzi wako unaharakisha baraka na neema nyingi za Mungu.
Lakini pia ikiwa mahusiano ni mabovu, basi ndio utumie fursa hii kuombea utapatanisho haraka, sana. Eneo hili ni muhimu sana kuliombea, ijapokuwa wengi hulipuuzia.
Ikiwa ni ndoa ambayo tayari inayo watoto ni muhimu kuwaombea watoto wako daima, wasiwe chanzo cha nyinyi kufarakana, lakini kuwa mwiba na uchungu kwenye ndoa yenu.
Lakini ikiwa bado hamjawa na watoto, ombea uzao wako ujao ukawe faraja na neema kwenu. Watoto wakiwa wabovu wanaweza kuihatarisha ndoa yako, au kuifanya isiwe na amani. Hivyo waombee sana wokovu, ulinzi, afya, adabu.
Shalom.
Ukizingatia kuviombea vipengele hivyo, kila kipengele si chini ya nusu saa. (dakika 30), utaona neema kubwa sana ya Mungu ikifanya kazi katika maisha yako.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?
NDOA NA TALAKA:
Kabla ya Bwana wetu YESU KRISTO, Mkuu wa Uzima, Mfalme mwenye Nguvu, Mwamba Mgumu, na Mkombozi, na Mfalme wa wafalme, kuutoa uhai wake, ili baadaye aurudishe tena (Yohana 10:17), yapo maneno saba (7) aliyasema pale msalabani, ambayo tunayapata katika zote nne (yaani Mathayo, Marko, Luka na Yohana), na maneno hayo ni kama yafuatayo.
1. BABA UWASAMEHE, KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO.
Luka 13:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”.
Hili ndilo Neno la Kwanza Bwana YESU kulisema akiwa pale msalabani, kuonyesha upendo wa hali ya juu na huruma kwetu, ijapokuwa yeye tayari alishawasamehe, lakini alijua pia umuhimu wa kuwaombea msamaha kwa Baba, kwani si kila msamaha unaoweza kutoa wewe ukawa pia umetolewa na MUNGU, waweza kumsamehe mtu lakini Baba wa mbinguni akawa hajamsamehe huyo mtu bado, hivyo tunajifunza hata sisi kuwaombea wengine msamaha kwa Baba yetu wa mbinguni, kama alivyofanya Bwana wetu YESU KRISTO.
2. AMIN, NAKUAMBIA LEO UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.
Luka 13:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Luka 13:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Hili ni neno la Pili Bwana kuzungumza msalabani, kuonyesha huruma za Bwana YESU hata katika hatua za mwisho kabisa za maisha ya mtu.
3. MAMA TAZAMA MWANAO, NA KISHA AKAMWAMBIA YULE MWANAFUNZI TAZAMA MAMA YAKO.
Yohana 19:26 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake”.
Yohana 19:26 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.
27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake”.
Hili ni neno la tatu, lenye ujumbe wa kuangaliana sisi kwa sisi, kwani kwa kufanya hivyo tunaitimiza amri ya Kristo la upendo.
4. MUNGU WANGU, MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA?
Mathayo 27:46 “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
Hili ni neno la nne, lenye kuonyesha Uzito wa dhambi Bwana wetu alizozibeba kwaajili yetu, zilikuwa ni nyingi kiasi cha kuuzima uwepo wa MUNGU mbele zake pale msalabani.
5. NAONA KIU.
Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu”.
Hili ni neno la tano, lenye kuonyesha uzito wa mateso ya Bwana YESU kuwa yalikuwa ni makuu.
6. IMEKWISHA
Yohana 19:30 “Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”.
Hili ni neno la sita, lenye kutangaza mwisho wa utumwa wa dhambi.. na kuanza kwa majira mapya, hakuna tena mateso, wala kilio wala uchungu kwake YESU, na kwa wote watakaokuwa ndani yake.
7. BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU.
Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”.
Hili ni neno la mwisho, kabla ya kukata roho.
Maneno haya yalifunga kauli ya Bwana duniani na baada ya siku tatu, alitoka kaburini, Mauti ilimwachia, na akaja na ushindi MKUU, Wokovu kwetu, Haleluyaa!…
Je bado upo dhambini?.. bado huoni ni gharama gani aliyoiingia YESU kwaajili yako?.. Tubu leo na kumkaribisha maishani mwako kabla ya nyakati mbaya na hatari zinazoikaribia dunia kufika.
Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?
Nini tofauti kati ya kileo na divai?
Je kibiblia ni sahihi kuadhimisha jumapili ya mitende?
Ipi tofauti kati ya Sheria na kanuni kibiblia.
Huu ni mwongozo maalumu wa njia bora ya kuiomba sala ya Bwana. Wengi wetu tunaiomba aidha kwa kukariri au kwa kukosa ufahamu wa jinsi ipasavyo kuombwa, kulingana na majira ya nyakati za agano jipya. Lakini kama tukijua namna ya kuiomba ipasavyo basi tutaweza fungua milango mingi sana rohoni, ukizingatia kuwa ni sala ambayo Bwana wetu mwenyewe alitufundisha kwasababu ndio hiyo hiyo hata yeye alikuwa anaiomba.
fungua chapisho hili lililo katika pdf kwa kubofya download uweze kusoma;
Kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?
https://wingulamashahidi.org/2023/04/01/jinsi-ya-kupigana-maombi-ya-vita/.
Huu ni mwongozo wa maombi maalumu kwa ajili ya familia yako. Kama watakatifu, ni wajibu wetu kuziombea familia, Lakini sio kuziombea tu, bali kufahamu maeneo muhimu ya kugusia kwenye maombi hayo. Huu ni mwongozo maalumu wa maombi ya familia. Bofya juu ufungue chapisho hilo (pdf)
Pia Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
MISTARI YA KUOMBEA AMANI YA FAMILIA.
MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira NA KELELE na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya”.
Kelele zinazozungumziwa hapo ni kelele za “Maneno” , kelele za “Maombi” na kelele za “Nyimbo”
1.KELELE ZA MANENO.
Hizo ni zile kelele zinazotokana na malumbano yasiyo na msingi wa kiroho, au mashindano ya maneno. Watu wagomvi huwa wana kelele, watu wabishi huwa wana kelele, watu wakorofi huwa wana kelele, na yote ni matunda ya dhambi ambayo hayapaswi kuwa ndani ya mtu aliyeokoka.
2. KELELE ZA MAOMBI
Kuna mambo ambayo mtu akiomba ni kelele mbele za Mungu, na mfano wa hayo ni yale yasiyotokana na Neno, maana yake mtu anaomba kitu kwa tamaa zake na ambacho si mapenzi ya Mungu, na tena anatumia sauti kubwa, (maombi kama haya ni kelele mbele za Mungu na pia hayana majibu.)
Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
3. KELELE ZA NYIMBO.
Amosi 5:23 “NIONDOLEENI KELELE za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.
Si nyimbo zote ni kelele mbele za Mungu, zipo zinazomtukuza Mungu na wanaoimba pia wanamtukuza Mungu.. Lakini zipo nyimbo ambazo hazimtukuzi Mungu ingawa zina majina na sifa za kumtukuza Mungu,
Vile vile zipo nyimbo ambazo zina maneno mazuri ya kumtukuza Mungu, lakini wanaoimba ni watu wasio na mahusiano yoyote na MUNGU, nyimbo za namna hiyo ni KELELE mbele za MUNGU.
Vile vile nyimbo zenye midundo ya kidunia, lakini zina maneno ya kibiblia, hizo nazo ni kelele, na si kelele tu bali pia ni machukizo.
Jihadhari na kelele.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.
Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)
Rudi Nyumbani
Ikiwa wewe umeokoka, na una kiu kweli ya kumkaribia Mungu wako katika viwango vya juu. Basi fahamu huna budi ujikuze kiroho. Na ukuaji huo hutegemea mambo mawili makuu “Neno pamoja na maombi”. Katika tovuti hii yapo mafundisho mbalimbali yatakayokusaidia kupiga hatua hizo.
Makala hii imeegemea zaidi katika Maombi. Hivyo huu ni mwongozo wa Wiki kwa Wiki, mfululizo wa vipengele muhimu vya kuombea. Uwapo nyumbani, uwapo kanisani. Jiwekee ratiba Kisha kuwa mwombaji. Na hakika baada ya wakati fulani utaona matokeo makubwa sana ndani yako.
Mwendelezo utakuja…
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Orodha ya mafundisho yote.
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Rudi nyumbani