Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?

SWALI:Kama kijana mmoja yeye alimtuhumu muhubiri mmoja kuwa yeye ana KOSA HAWAONGOZI WATU SALA YA TOBA..Hilo ni kweli unaweza kumhesabia mhubiri kosa kwasababu hawaongozi watu sala ya toba ndugu zangu??Hiyo sala ya toba ikoje ndugu zangu?.


JIBU: Wokovu sio suala la kumsaidia mtu kufanya, wokovu ni jambo linalotoka katika moyo wa mtu…Kwasababu neno TOBA lenyewe linamaana ya KUGEUKA na sio KUZUNGUMZA…wapo watu wanasema hiyo sala usiku kucha lakini maisha yao hayageuki, kwasababu haitoki moyoni…na pia yupo asiyeisema hiyo sala lakini moyoni mwake akadhamiria kweli kugeuka na kuacha mienendo yake mibaya kuanzia huo wakati, Sasa mtu kama huyo mbele za Mungu ndiye aliyetubu.

Kumbuka ule mfano Bwana Yesu alioutoa juu ya wale wana wawili tukisoma katika

Mathayo 21: 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.

30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.

31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.”

Unaona hapo?, mimi binafsi kabla sijatubu nilishaongozwa sala ya TOBA mara nyingi, lakini muda mfupi baada ya pale nilirudi katika maisha yangu ya kale ya dhambi…lakini siku moja nilipoona mwenyewe ubaya wa dhambi na kuona umuhimu wa mbingu na YESU KRISTO maishani mwangu, sikuongozwa sala ya toba na mtu yeyote, lakini yale ya nyuma yote nilidhamiria kuyaacha kwa kumaanisha kuyaacha na kuanza kumtazama Mungu, na tangu huo wakati na kuendelea Mungu akawa upande wangu kunishikilia mpaka hivi sasa nimesimama kwa neema zake.

Hivyo kazi ya muhubiri sio kumwongoza mtu sala ya TOBA, hapana bali kumjengea mtu mazingira ya yeye mwenyewe kuchukua uamuzi wa kutubia dhambi zake…kwasababu TOBA halisi inatoka moyoni.

Japo upo wakati mtu atakuuliza nifanye nini ili niokoke? Na hapo unaona kabisa mtu kama huyo amedhamiria kweli KUGEUKA kwa wakati huo, na hafahamu lolote kuhusu mambo ya wokovu, hapo unaweza kumwongoza Sala, na sala hiyo kiuhalisia ni kama tu kumwongezea IMANI, ya kile alichokiamua rohoni mwake..lakini sio tiketi kwamba kwa kupitia hiyo amesamehewa. Hapana alishasamehewa pale tu alipodhamiria kugeuka kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake. Hivyo kama ulihubiri na hukuongoza mtu yeyote sala ya Toba, maadamu umehubiri Neno lililohai la Mungu, haupaswi kuhukumiwa na mtu yeyote, kwasababu huwezi jua tangu huo wakai ni wangapi waliotoka hapo wamegeuka kwa Neno lile au la! hata kama hakukuwa na hata mmoja aliyejionyesha katubu mbele za watu.

AMEN.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

KISASI NI JUU YA BWANA.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.

JAWABU LA MAISHA YA MTU.

FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments