Title July 2018

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.

Bwana YESU ni yeye yule jana, na leo na hata milele hajabadilika wala hana kigeugeu, na NENO lake ni lile lile. Kama maandiko yanavyosema mwanamke wa kikristo anapaswa avae mavazi ya kujisitiri.(1Timotheo 2:9) hilo Neno hata leo bado linaendelea kufanya kazi kwa binti za Mungu.

Leo hii vichaa wapo wengi mitaani tunawaona, lakini ni mara chache sana kumuona kichaa mwanamke akitembea uchi barabarani, ingawa vichaa wanaume ni rahisi kuwaona wakiwa uchi, lakini sio kwa wanawake vichaa utawakuta wamevaa matambara na kujisitiri mwili mzima japo ni vichaa. Je! ni kwanini iwe hivi?? Jibu ni Kwasababu uchi wa mwanamke ni wathamani zaidi kuliko wa mwanamume hivyo unastahili muda wote usitiriwe.

Lakini leo hii mwanamke mwenye akili timamu ambaye uchi wake unathamani ambaye angepaswa afunikwe, ndiye anayeongoza kwa kutembea uchi barabarani, SASA HAPO KICHAA NI NANI?  lakini mwanamume ambaye uchi wake usiokuwa na thamani nyingi utakuta kajisitiri, kafunika shingo yake kwa shati na tai, huwezi kuona mgongo wake uko wazi wala mapaja yake wazi akitembea barabarani, miguu yake imesitiriwa yote kwa viatu na soksi, ni mtu huyo ambaye uchi wake hauna thamani sana, Leo hii huwezi kuona mwanaume anaenda na vesti kazini, lakini hili jambo ni la kawaida kwa wanawake kutembea migongo wazi na vifua wazi hata sasa imekuwa kawaida mpaka kwenye sehemu za ibada.


Swali ni Je! roho gani ipo hapo katikati? jibu ni rahisi ni ile ile roho iliyokuwa kwa mwanamke Yezebeli wa kwa maana yeye ndiye mwanamke pekee aliyekuwa anapaka uso rangi katika biblia.Lakini tuna wadada hao hao ambao Bwana Yesu amewaambia yeye mwenyewe wasifanye  mambo kama hayo na wametii yaani, kujipodoa uso, kupaka wanja, kuvaa vimini, suruali, kaptura, vesti, tight, pedo, kupaka lipstick, kupachika kucha, wigi n.k. lakini cha ajabu utamkuta mdada mwingine anajiita mkristo na anadai  amepokea Roho Wa Mungu lakini bado anajiona salama kufanya vitu hivyo.

Jiulize ni roho gani iliyoko ndani yako? kwanini YESU yule yule amkataze dada yule kufanya hivyo vitu na wewe asikukataze? jiulize sana, kama Roho wa Mungu kweli anakaa ndani yako atakushuhudia kwamba haya mambo hayafai na yanakupeleka kuzimu.

 Lakini kaa ukifahamu tu, wanawake wote wanaofanya hivyo sehemu yao ni katika lile ziwa la moto HIVI ASEMA BWANA.. (warumi 1).

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi

+255693036618/+255789001312


Mada Nyinginezo:

MAVAZI YAPASAYO.

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE

BWANA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI KUSEMA MARKO 2:19″WALIOALIKWA HARUSINI WAWEZAJE KUFUNGA MAADAMU BWANA-ARUSI YUPO PAMOJA NAO?”

PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ATUMIE MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO LAKE, JE! TUNARUHUSIWA NA SISI PIA KUTUMIA POMBE?


Rudi Nyumbani

Print this post

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

Tukisoma kitabu cha mwanzo 1, Biblia inasema Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na nchi. Lakini tunaona hakueleza aliumbaje umbaje hii mbingu na nchi yaani, miti, jua, mwezi, milima, wanyama, mwanadamu n.k.

Lakini tukija kusoma kwenye kitabu cha waebrania 11:3 tunaona

” Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. “

 Kwahiyo siri inaonekana hapo ni kwamba mbingu na nchi ziliumbwa kwa NENO la Mungu.

Sasa swali linakuja hili NENO ni nini?

Tukisoma Yohana 1:1-3″

1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. “

Kwahiyo kulingana na mstari huu biblia inaeleza kuwa Neno lilikuwapo kwa Mungu, na lilikuwa ni Mungu, maana halisi ya “Neno” kulingana na tafsiri ya Kigiriki iliyotumika ni WAZO au NIA. Kwahiyo wazo lilikuwapo ndani ya Mungu, Na hivyo vitu vyote vilivyoumbwa vimetoka katika hilo wazo la Mungu mfano dunia, malaika, wanadamu, sayari, miti n.k. 

Mfano mzuri ni kama wewe kitu chochote ulichokitengeneza kama nyumba, kiti, meza, nguo, vilitoka kwanza katika wazo lako au nia yako. Hii ikiwa na maana kwamba kama usingekuwa na hilo wazo usingeviumba vitu hivyo vyote, Vivyo hivyo na kwa Mungu pia kama WAZO  lake (ambalo ni Neno lake) asingekuwa nalo hapo mwanzo asingeweza kuumba chochote.

Kwahiyo kabla ya mwanadamu kuasi hili NENO lilikuwa pamoja na mwanadamu, Mtu alikuwa na ushirika na Mungu kwa asilimia zote, kwasababu NENO lilikuwa ndani yake kama lilivyokuwa ndani ya Mungu kitu kilichomfanya mpaka mwanadamu kuonekana kuwa kama mfano wa Mungu, Adamu alikuwa na mamlaka yote duniani, kama vile YESU leo alivyo na mamlaka yote duniani na mbinguni biblia inasema hivyo. Na ndio maana utajua sababu ya Mungu kutuita sisi ni miungu duniani, Na yeye ni MUNGU WA miungu.

Lakini baada ya anguko Adamu aliyapoteza yote aliyokuwa nayo kwasababu alijitenga na NENO la Mungu kwa kutokutii. Hivyo yeye na NENO (nia ya Mungu) vikawa ni vitu viwili tofauti. Kuanzia wakati huo baada ya anguko, lile NENO likaanza kumtafuta tena mwanadamu limrudishe tena katika ile hali ya kuwa na mahusiano na Mungu na mamlaka yote aliyokuwa nayo kabla hajayapoteza. Na ndio maana kuna mahali Yesu alisema sio ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua nyinyi.

Sasa tangu huo wakati lile NENO likaanza kutafuta njia nyingi za kumrejesha mwanadamu, likaanza kuzungumza na wanadamu kwa kupitia MBINGU, nyota,sayari na kwa  vitu vya asili, kwa dhumuni la kumrejesha tu, lakini mwanadamu bado hakutaka kutega sikio lake kusikia.

Baadaye lile NENO likaanza kuzungumza kupitia watu, mfano manabii wa Mungu, tunaona manabii kama Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Eliya, Danieli, Yeremia, Isaya n.k..lilisema nao kwa nguvu na kwa udhihirisho mwingi liliwapigia kelele wanadamu wamrudie Mungu, warudi  katika ule ushirika waliokuwa nao kwanza na Mungu. Lakini wanadamu bado hawakutega sikio lao kulisikia, zaidi ya yote waliwaua manabii waliotumwa kwalo.

Lakini japokuwa NENO hili limezungumza mara zote hizi kwa vizazi na vizazi kupitia vitu vya asili na manabii, bado ule uhusiano uliokusudiwa mwanadamu awe nao na Mungu wake haukufanikiwa kurejeshwa kwasababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu. 

Ndipo wakati ulipofika lile Neno likaona liuvae mwili, lije lenyewe katika mwili,liishi na wanadamu, lihubiri mambo yote lililohubiri ndani ya manabii na vitu vya asili kwa kusudi lile lile la  kumrejesha mwanadamu  kwa muumba wake. Hili jambo linazungumziwa kwenye..

Waebrania 1:1-2″ Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ” 

Sasa umeona mwisho wa yote Neno limekuja kuzungumza na sisi kupitia nini? sio kanisa wa chochote bali mwana.

Hili NENO likajichagulia mwili unaoitwa YESU KRISTO, Haleluya! ni furaha kiasi gani Mungu alivyojirahisisha kwetu sisi ili tukae na hilo NENO kwa jinsi ya kimwili, likiongea, likifundisha, likijibu maswali, likitembea na sisi wazi kabisa, linafurahi na sisi, kitu ambacho hapo mwanzo ilikuwa ni ngumu kulielewa lizungumzapo lakini hapa lipo pamoja nasi (IMANUELI)..Embu tutazame mstari ufuatao;

1 Yohana 1:1-3″

1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, TULILOLISIKIA, TULILOLIONA kwa macho yetu, TULILOLITAZAMA, na mikono yetu IKALIPAPASA, kwa habari ya NENO la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”

Habari hiyo inaelezea lile NENO ambalo zamani lilikuwepo lakini sasa limefanyika mwili na lipo katikati yetu kama mwanadamu.

Hivyo basi BWANA YESU KRISTO alipokuja akaanza kutufundisha na kuturejesha katika utimilifu wote na Mungu tuliokuwa nao pale Edeni hata na zaidi ya pale.,Jambo la kwanza alilolifanya ni kutupatanisha sisi na Mungu kwa kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu maana biblia inasema pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo (waebrania 9:22)

Na jambo la pili ni kutufanya sisi kuwa wana wa Mungu (miungu)
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “

Tukisoma 

2 Wakoritho 5:18-19 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu NENO la upatanisho. “

Kama tulivyosema lile NENO ni wazo/nia ya MUNGU nalo ni Mungu, ikiwa na maana usiipotii nia ya Mungu haujamtii Mungu. Na nia ya Mungu ni nini? Ni kuturujesha sisi tuwe na mahusiano naye kama ilivyokuwa hapo mwanzo ili tumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli. Na ndio maana WAZO/NIA yake iliuvaa mwili kwa dhumuni la kutuhubiria sisi tumgeukie Baba.

Kwasababu hiyo basi Yesu Kristo ndiye NJIA, NA KWELI, NA UZIMA, MTU HAFIKI KWA BABA ISIPOKUWA KWA NJIA YAKE YEYE.(Yohana 14:6), alisema aliyeniona mimi amemwona BABA, usipomtii YESU KRISTO na kumwamini umeukataa mpango wa Mungu kwa wanadamu na viumbe vyake vyote kama shetani alivyofanya. 

Natumaini utakuwa umeshaiona sababu ya YESU KRISTO Kutokea ni nini?, ni hiyo hapo juu, Neno la Mungu liliuvaa mwili, kutuhubiria sisi na kuturejesha kwa Mungu wetu ili tumwabudu yeye katika roho na kweli. 

Wakolosai 2:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. “


Kwahiyo Mungu hana nafsi tatu, Nafsi ya Mungu ni moja tu. Mungu kuonekana katika mwili hakumfanyi yeye kuwa na nafsi tatu. Alifanya hivyo tu ili kutupatanisha sisi na yeye. Kama tusingeanguka katika dhambi kulikuwa hakuna haja ya yeye kuuvaa mwili na kuja duniani, Yeye ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

NEEMA YA BWANA YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi 

+255693036618/+255789001312


Mada Nyinginezo:

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

VIUMBE VINATAZAMIAJE KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU?

NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?

KAINI ALIPATIA WAPI MKE?


Rudi Nyumbani

Print this post

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Je! Manabii wa uongo ni wapi?

Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “

Kuna watu wanasema usizihubiri hizi habari, we fundisha TU watu watubu wawe wakristo inatosha ndiyo kazi yako!. Swali ni je! ukishakuwa mkristo ndio mwisho wa safari?, unahitaji kukua na ndio safari inapoanzia  na sio inaishia. Hivyo basi unahitaji chakula ili ukue, na ujue ni chakula gani unapaswa ukile, maana vyakula ni vingi vijengavyo na vibomoavyo, Hivyo ni kuwa makini kujua ni chakula kipi ule na kipi usile kwa usalama wa roho yako na hatma yako ya milele.

Tunaishi katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi hata kutokea katika vizazi vyote vya nyuma, ambacho kina mchanganyiko mkubwa wa MANABII WA UONGO NA MANABII WA KWELI, Na wote wanafanya kazi moja ya KUVUNA ROHO ZA WATU, aidha kuzipeleka kuzimu au mbinguni, ni kipindi cha hatari sana tunachoishi. Ni muhimu kufahamu unavunwa upande gani, ili usije ukajikuta unadondokea sehemu ambayo haujatarajia.

UPOTOFU ULIOPO SASA:

Jambo kubwa linalowachanganya watu wengi ni kuona pale mtu anayejiita mtumishi wa Mungu halafu bado ni mwasherati, mtukanaji, mlevi, anapenda anasa, na bado miujiza inatendeka na yeye, anafufua wafu, anaombea watu wanaponywa, anatabiri na unabii unakuja kutimia, ananena kwa lugha n.k.

Kiasi ambacho kinamfanya mtu mchanga ashindwe kuelewa inawezekanikaje huyu mtumishi anafanya mambo ya kidunia lakini bado ishara na miujiza zinatendeka na yeye, Na wala hatumii uchawi ila  anatumia jina la YESU na nguvu za Mungu zinashuka. “HII NI SIRI” na ni jukumu kwa kila mkristo anayethamini maisha yake ya kiroho kufahamu..kumbuka (kuna wanaotumia nguvu za giza kutenda miujiza, siwazungumzii hao, hao ni rahisi kuwagundua lakini nawazungumzia wale wanaotumia nguvu za Mungu ambao ni ngumu kuwatambua.)

Tusome, mstari ufuatao unawazungumzia hao wanaotumia nguvu za Mungu ; Kumb.13:1-5″

1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “

Unaona hapo? Huyo nabii hapo katoa unabii kwa uweza wa nguvu za Mungu na ikatokea, lakini anawafundisha watu waende kinyume na maagizo ya Mungu. Vivyo hivyo na hata sasa katika kipindi hichi cha mwisho Mungu ameamua kuachia mvua yake (UPAKO) kwa watu wote waovu na wema kutujaribu sisi kama TUNAMPENDA BWANA NA KUYASHIKA MANENO YAKE AU LA!. 

Mtu anaweza akaja kwako na kutoa unabii na ukatimia na kufufua wafu, na kuponya wagonjwa lakini akafundisha injili nyingine akakwambia  ulevi ni sawawanawake kwenda na mitindo ya kisasa ni sawa (anasema Mungu haangalii mavazi anaangalia roho )akakufundisha kuupenda ulimwengu ni sawa, kuoa wake wengi ni sawa, Dunia haiishi leo wala kesho kula maisha, kuwa na pesa nyingi ndio kigezo cha kubarikiwa na Mungu, Mungu siku zote ni Mungu mzuri na hawezi kuwahukumu watu aliowaumba. n.k. na bado mtu huyo akatoa mapepo na kufufua wafu.

Na wewe kwasababu NENO na kumpenda Mungu hakupo ndani yako, ukadhani anazungumza ukweli au katumwa na Mungu kwasababu tu! ametoa unabii ukatokea, NDUGU USIDANGANYIKE UMEPOTEA!! .  Biblia inasema jiepushe na huyo mtu, CHUKUA TAHADHARI KWA USALAMA WA MAISHA YAKO..KIMBIA! HARAKA SANA NI BWANA NDIYE ANAYEKUJARIBU KUONA KAMA UNAMPENDA KWELI NA KULIFUATA NENO LAKE AU LA!

 
Leo hii wewe unayejiita mkristo unapenda injili za kufarijiwa tu! siku zote unapendwa kuambiwa “ALL IS WELL” ulimwengu hautakuja kuteketezwa,tunaishi chini ya neema, mafundisho unayoyapenda wewe ni KUTABIRIWA MAFANIKIO TU!. Lakini fahamu jambo moja BWANA YESU hakuacha enzi na mamlaka mbinguni ili aje kutufia sisi mlabani tuwe MABILIONEA, bali kwa ajili ya dhambi zetu.(hicho ndicho kiini cha injili) yeye mwenyewe alizungumza ..Mathayo 16:24-27

” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 

Leo mkristo anadai anamfuata YESU, lakini kigezo cha kumfuata YESU ni kuwa na MSALABA wako, sasa wewe MSALABA WAKO UKO WAPI?, Jihadhari na haya mafundisho ya uongo yanawapeleka maelfu wa waaminio kuzimu kila siku pasipo wao kujua.

Hawa manabii wa uongo, Bwana Yesu alisema tutawatambua kwa  MATUNDA YAO na sio kwa upako wao, kwasababu Mungu anaweza akamtumia mtu kama chombo tu cha kuazima akishamaliza shughuli nacho anakiacha, mfano tunaona Mungu alimtumia Punda kuongea na Nabii Balaamu kumpa ujumbe, lakini baada ya punda kutoa ujumbe alirudia katika hali yake ya kawaida ya upunda, vivyo hivyo na Balaamu mwenyewe alikuwa ni MCHAWI lakini Mungu alimtumia yeye kuwabariki Israeli, (hesabu 22:21-29),

Na pia Mungu aliwatumia wale manabii 400 kumdanganya mfalme Ahabu kwasababu Mungu alikuwa amekusudia mabaya juu yake. (1 wafalme 22:6). Kwahiyo kuwa na upako mtu kuona maono, au kuwa nabii, au kunena kwa lugha au kuponya au kufanya miujiza yoyote ile, sio kigezo cha huyo mtu kuwa NABII WA MUNGU. Tutatawatambua kwa matunda yao (AMBAYO NI NENO LA MUNGU). Nabii wa ni yule anayekuja na ishara pamoja na NENO lakini lililokuu ni NENO.

Kipime mtu anachokuambia je! kinaendana na NENO la Mungu? kama hakiendani na NENO la Mungu weka kando haijalishi anawashirika wengi kiasi gani, au anakubalika kiasi gani, au kanisa ni kubwa kiasi gani, au anaupako kiasi gani. KIMBIA! HILO NI SINAGOGI LA SHETANI!.. 

  • Ukiona unadumu kwenye mafundisho yanayokupeleka wewe kuutazama ulimwengu kuliko kumtazama KRISTO! KIMBIA!  KWA USALAMA WA MAISHA YAKO!!.
  • Ukiona unahubiriwa injili za mafanikio tu! Haufundishwi kufikia toba, au utakatifu maana biblia inasema pasipo huo utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu (waebrania 12:14). KIMBIA!
  • Ukiona unahubiriwa injili ya kutoa tu! kutoa tu! toa zaka, panda mbegu, n.k. Lakini NENO halihubiriwi, ONDOKA HAPO! Bwana Yesu alisema hivi..Mathayo 23:23-24″Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. VIONGOZI VIPOFU, WENYE KUCHUJA MBU NA KUMEZA NGAMIA. “ …KIMBIA! JIOKOE NAFSI YAKO.
  • Ukiona unaenda katika nyumba ya Mungu, hauhubiriwi NENO bali SIASA, usitazame nyuma hata kama kuna miujiza inatendeka kiasi gani....KIMBIA KAMA UNAIPENDA NAFSI YAKO!
  • Ukiona kiongozi wako wa dini, Anaelekeza watu kwake, na sio kwa KRISTO, anajisifu na kujitukuza yeye, utukufu wa Mungu anauchukua yeye.Hapo  hapana tofauti na ibada za sanamu, fahamu kuwa unamwabudu mtu na sio Mungu, isaya 42:8″ Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. “.usimsikilize nabii huyo biblia inasema hivyo… KIMBIA!

Jiulize Wewe unayejiita mkristo  tangu ulipoamini, maisha yako ya kiroho yamesonga mbele kiasi gani. utakuwaje mkristo halafu biblia husomi!??  sasa utawatambuaje manabii wa uongo au manabii wa ukweli kwa namna hiyo watakapokujia na mafundisho yao??. Utakuwa unapelekwa na kila upepo unaokuja wa elimu yoyote. Maana njia pekee ya kumpima nabii wa uongo au Nabii wa ukweli ni kwa NENO TU!.

Na sio kitu kingine. Jijengee kila siku tabia ya kusoma NENO na kuomba. Hizi ni nyakati za hatari tunaishi zile zilizotabiriwa kuwa watatokea manabii na makristo wengi wa uongo nao watawadanganya wengi yamkini hata walio wateule. Kumbuka ni wateule ndio wanaozungumziwa hapo kuwa wanaweza wakadanganywa sasa jiulize wewe ambaye sio mteule utaonekania wapi? wewe ndio hautaelewa chochote kinachoendelea utaishia kuwashangilia na kuwasifia kama Bwana Yesu alivyotabiri juu ya manabii wa uongo.

2 Petro 1:10″ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

KWAHIYO NDUGU HUU NI WAKATI WA MUNGU KUTUJARIBU SISI KAMA TUNAMPENDA YEYE NA KULISHIKA NENO LAKE AU LA!. Biblia inasema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.

 
Mungu hadhihakiwi usipoweza kufanya hivyo jua tu utaangukia kwenye huu mstari ufuatao;

2 Thesalonike 2:10-12″… na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;12  ILI WAHUKUMIWE WOTE ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “

MARAN ATHA!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi

+255693036618/+255789001312

Masomo Mengineyo

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

UNYAKUO.

Nini maana ya “Roho za manabii huwatii manabii?

HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO

Rudi Nyumbani

 

Print this post

EPUKA MUHURI WA SHETANI

Kutoka 21:2-6 ” Ukimnunua MTUMWA wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako HURU bure.

3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.

4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.

5 Lakini huyo mtumwa AKISEMA WAZIWAZI, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; SITAKI MIMI KUTOKA NIWE HURU;

6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; ndipo ATAMTUMIKIA SIKU ZOTE. “

JE! UNAJUA JAMBO GANI LITAMPATA MTU YULE, ALIYESIKIA UKWELI HALAFU HATAKI KUBADILIKA?

Biblia inaeleza wazi kabisa kulingana na maandiko hayo hapo juu, Mtumwa yule aliyetangaziwa uhuru wake baada ya kutumika miaka 6 akakataa (Yaani akaona ni vyema kuendelea katika utumwa wake.). Jambo linalotokea ni hili bwana wake huyo mtumwa atachukua sindano na kutoboa SIKIO lake, kuwa kama MUHURI wa kukataa kuwekwa huru, Hivyo basi huyo mtumwa atamtumikia bwana wake milele, Na kama tunavyofahamu sikio likishatobolewa haliwezi kurejea tena katika hali yake ya kwanza. Na ndio maana ilikuwa inatumika kama ISHARA YA MAPATANO(MUHURI).

Vivyo hivyo kwa wanadamu wa leo, Kristo alikuja kututangazia uhuru wetu kutoka katika UTUMWA WA DHAMBI kulingana na

 Mathayo 11:28-29 (Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “),

Kwasababu Bwana Yesu alisema Yohana 8:34-36″ ….Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. “

Bwana Yesu pia alisema maneno haya luka 4:18-19″ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, KUWAACHA HURU WALIOSETWA,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. “

Kwahiyo injili ililetwa  kwetu mahususi kwa kutuweka HURU mbali na dhambi. Hapo anaposema

“kuutangaza  mwaka wa Bwana uliokubaliwa” akiwa na maana kuwa ndio mwaka wa maachilio, ule mwaka wa saba ( Kwa maana mahali pengine anasema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.

2 Wakoritho 6:2). Kwahiyo tunaona MBIU YA MAACHILIO IMESHAPIGWA watu wote wawe HURU kwa YESU KRISTO BWANA. Lakini  cha kusikitisha wapo baadhi ya watumwa (watumwa wa dhambi), wanakataa kuupokea uhuru WAO waliotangaziwa na Bwana wanapenda kuendelea kumtumikia bwana wao shetani ambaye hapo mwanzo alikuwa anawatumikisha na kuwatesa. Embu tuitazame hii mihuri inampataje mtu.

MUHURI WA MUNGU:

Mungu anao MUHURI wake, na shetani pia anao muhuri wake kwa watoto wake. Wale waliokubali kuwekwa huru na BWANA wanatiwa MUHURI WA MUNGU nao ni ROHO MTAKATIFU kulingana na

waefeso 4:30″(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa MUHURI hata siku ya ukombozi). , na pia biblia inasema katika

2 Wakoritho 3:17 .. walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. “.

Kwahiyo unaona unapoukubali UHURU Mungu anakupa zawadi ya kupokea Roho Mtakatifu kama Muhuri wa uhuru wako. Lakini kama hauna Roho wa Mungu wewe bado ni mtumwa wa dhambi na UNAJUA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Warumi 8:9″….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”

MUHURI WA SHETANI:

Kwa wale waliokataa uhuru kwa makusudi angali wakijua kabisa wapo kwenye utumwa na wangepaswa wawe huru, lakini wakapenda kumtumikia bwana wao shetani katika dhambi zao kuliko kumtumikia Mungu nao pia wanatiwa MUHURI. Na mihuri hiyo YA SHETANI wanatiwa katika MASIKIO YA MIOYO YAO, maana yake ni hii HAWATAKUWA TENA NA NEEMA YA MUNGU JUU YA MAISHA YAO!,baada ya kuisikia injili na kuikataa Haiwezekani wao kumgeukia Mungu tena, Hata waelezweje injili hawawezi kusikia tena wageuke hao wameshakuwa mali halali ya shetani. Hii ni hatari sana tuwe makini tunaposikia wito wa Mungu.

Na huu muhuri wa shetani mpaka sasa hivi unaendelea kuwapiga watu,

leo hii umeshaisikia injili mara ngapiumehubiriwa uache uzinzi mara ngapi ewe kijana ewe binti,? umehubiriwa utubu dhambi zako mara ngapi? lakini umekuwa wa kwanza kufanya mizaha? umehubiriwa uache ulevi mara ngapiunavuta sigaraunaangalia pornoghaphyunafanya mustarbationbinti unasaganaumekuwa shoga kijanaunaenda kwa wagangaunajifurahisha katika anasa na miziki ya kidunia,

Mwanamke unavaa surualiviminiunapaka rangi kuchakijana unanyoa mitindo isiyofaa na kusuka nywele ,na tatoo kwenye mwili wakowanawake usengenyaji na umbeamtukanajiunajichanganya na watu waovu kwa jinsi isivyopasa, unachati nao mambo maovuhuku ukijua kabisa watu wanaoyafanya hayo wataishia katika jehanum ya moto, JE! UNADHANI NEEMA YA MUNGU ITAENDELEA KUDUMU JUU YAKO MILELE?.

Mungu hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?.

Unashindwa kuona jinsi unavyozidi kutiwa ule MUHURI wa shetani? kwa kuukataa uhuru wako ambao BWANA aliokutangazia pale KALVARI?. Maana kama unasikia sauti ya Mungu kila siku ikisema moyoni mwako UTUBU lakini unaipuuzia nakwambia ukweli utafika wakati HAUTAKAA UISIKIE TENA NDANI YAKO!!,

Na unajua ni kitu gani kitaenda kukutokea? Ni kwamba utafika wakati utaona mambo yote kuwa ni sawa, kuwa ulevi ni sawa,utaona uasherati hauna ubaya wowote, Mungu aliyetuumba hawezi kutuhukumu, hautaamini tena kama kuna jehanamu, utaishia kuwaona watumishi wote wa Mungu ni waongo, utaishia kuukosoa kila siku ukristo na biblia ukisema hayo mambo ni ya kale.

Utaanza kujiona kuwa ni haki yako kuishi unavyotaka hata kujichubua, kubadili maumbile, kuvaa unavyotaka ni sawa, Utajiona kutukana ni sehemu tu ya maisha ya binadamu hakuna kosa lolote kwasababu Roho Wa Mungu hayupo tena ndani yako kwasababu UMESHATIWA MUHURI, utaanza kuona kujipenda mwenyewe ni sawa, Kutazama pornography na kufanya musturabation ni sehemu maisha ya kila mwanadamu ukijidanganya kuwa Mungu hawezi kumuhukumu mtu kwa kufanya hivyo, unajikuta unaanza kupenda kufuatilia mafundisho ya mashetani kuliko mafundisho ya Mungu, Biblia hutaki kusoma kusoma lakini habari za freemasons, na zi kichawi, na filamu pamoja na vitabu kama , harryporter, twightlight, vampires,n.k. ndivyo vinavyokuvutia kusoma na kuangalia, jiulize ni roho gani inakuendesha? n.k.

Ndugu ukishaanza kuona dalili ya mambo kama hayo yanakuja ndani yako, jua kabisa neema ya Mungu ndivyo inavyoondoka kwako kidogo kidogo na ndo unavyoupokea MUHURI wa shetani hivyo, maana jua tu wewe unayeisikia injili kila siku unaambiwa utubu hautaki, neema yako haiwezi kuwa sawa na mtu yule ambaye hajawahi kusikia  injili kabisa. soma mstari ufuatao;

2 Wathesalonike 2:10-12 ” na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “

Kwahiyo ndugu maneno hayo hayakuogopeshi??  TUBU! yamkini hii sauti ya upole inayokuambia kila siku utubu bado inaendelea KULIA NDANI YAKO! ..itii na ugeuke maana upo katika HATARI, Maana hiyo sauti haitadumu milele ndani yako. Na ikishaondoka hakutakuwa na njia ya kurudi tena. YAANI MOYO WA KUTUBU hautakuwepo tena ndani yako utafanana na hao watu unaowaona huko ulimwenguni watendao matendo ya giza si kana kwamba hawasikii au hawakusikia injili  hapana lakini mioyo yao imeshatiwa MUHURI, hawatakaa wasikie tena na kubadilika, ndugu usifanane nao. Mtii Mungu tubu dhambi zako muda umeenda sana kuliko unavyofikiria.Yesu yupo mlangoni kurudi.
Maana biblia inasema…

 Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. MWENYE KUDHULUMU NA AZIDI KUDHULUMU; na MWENYE UCHAFU AZIDI KUWA MCHAFU; na MWENYE HAKI AZIDI KUFANYA HAKI; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA.Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. “

Naomba umalizie kwa kuyatafakari maneno yafuatayo ujue hatma ya WALIOUKATAA UHURU WAO KUTOKA KWA BWANA;

Warumi 1:24” Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI YAO.
28 NA KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO, MUNGU ALIWAACHA WAFUATE AKILI ZAO ZISIZOFAA, WAYAFANYE YASIYOWAPASA.

29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI YA MUNGU, YA KWAMBA WAYATENDAYO HAYO, WAMESTAHILI MAUTI, WANATENDA HAYO, WALA SI HIVYO TU, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAYO.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi

+255693036618/+255789001312

Mada Nyinginezo:

UNAFANYA NINI HAPO?

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.

NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?

NINI TOFAUTI KATI YA 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?


Rudi Nyumbani

Print this post

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!

Yoeli 2:28-32″ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

30 Nami nitaonyesha MAMBO YA AJABU KATIKA MBINGU na KATIKA DUNIA, DAMU, na MOTO, na MINARA YA MOSHI.

31 JUA LITAGEUZWA KUWA GIZA, na MWEZI KUWA DAMU, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.

32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.

UVUVIO MKUBWA UNAKUJA DUNIANI:

Tukisoma mistari hiyo Nabii Yoeli alionyeshwa maono ya uvuvio mkubwa wa Roho ya Mungu ambao ungekuja katika siku za mwisho,  Na ni dhahiri kabisa kwa wasomaji wa biblia wanafahamu sehemu ya huo unabii ulitimia wakati wa PENTEKOSTE, pale Roho wa Mungu alipowashukia wale watu 120 kwa mara ya kwanza, na kuwapa vipawa vikubwa na vya ajabu, ishara na miujiza mingi ikifanywa na mitume na wale wote waliojazwa Roho Mtakatifu.

Mvua hii ya Roho Mtakatifu Mungu aliyoiachilia kwa mara ya kwanza  pale Pentekoste inajulikana kama “MVUA YA AWALI/MASIKA” ( kwa kiingereza former Rain). Lakini pia Mungu aliahidi kuileta mvua nyingine tena ambayo ni “MVUA YA BAADAYE/ VULI” ( kwa kiingereza Latter Rain). Kwa ufafanuzi wa maelezo haya tusome;    

Yoeli 2:23 “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, MVUA YA MASIKA, na MVUA YA VULI, kama kwanza.” 

Kwahiyo hii mvua ya pili (MVUA YA VULI) mbali na ile ya kwanza iliyotokea wakati wa Pentekoste, Tukisoma katika historia ya ukristo Bwana aliishusha tena mwaka 1906, kwenye uamsho uliotokea mtaa wa AZUSA, huko Calfornia Marekani ambapo Bwana alimwaga ROHO wake na kushusha vile vipawa tena  vya Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa katika Pentekoste ya kwanza baada ya kanisa la Kristo kukaa muda mrefu bila uamsho kwa muda wa karne nyingi, lakini kuanzia huu mwaka 1906 tunaona vipawa vyote vilirejeshwa watu wakaanza kunena kwa lugha, kutabiri, kuponya magonjwa, ishara na miujiza, unabii n.k. vitu ambavyo havikuwahi kutenda tangu wakati wa kanisa la kwanza.

Hivyo basi Mungu alimtuma mjumbe wake William Branham kama mjumbe wa kanisa la mwisho LAODIKIA, ufunuo 3, Mungu alimtumia kwa ishara nyingi na miujiza ya ajabu ambayo haikuwahi kufanyika hapo kabla ikiwemo na utambuzi wa siri za mioyo ya watu, tafsiri za ndoto kama ilivyokuwa kwa Nabii Danieli, na ishara zilizoweza kuonekana wazi na kunaswa katika picha za kimagnetiki, n.k.

Ndipo Mungu akaendeleza kuimwaga hiyo roho kwa watumishi wake wengi waaminifu duniani kote kwa mfano wa William Branham kama oral Robert, Billy Granham, TL Osborn, nk.. 

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!  Yoeli 2:28-32" Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

( tazama ushuhuda mfupi juu ya huduma na maisha ya William Branham,)

Mvua hii ya mwisho itatimizwa katika huu wakati wa mwisho Bwana aliahidi sehemu hii ya maandiko itaenda kutimia

Yoeli 2:29 “tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.

31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo. 

Kumbuka katika mvua iliyoachiliwa mara ya kwanza, tuliona unabii, lugha, maono, ndoto, ishara, n.k. lakini hatukuona mambo ya ajabu katika dunia na katika mbingu kama jua kutiwa giza, mwezi kuwa damu, moto, minara ya moshi, n.k. tumezoelea kuona unabii na uponyaji, lakini haya mambo mengine yaliyosalia  yanaenda kutimilika katika hii mvua ya mwisho na yatakuja na hukumu sio kwa kuwaburudisha watu, Tunaona mfano uliotokea kwa mapigo ya Musa na Eliya. Ni mambo ya kutisha yanakuja. Na ishara ambazo hata hazijawahi kurekodiwa wala kufanywa mahali popote pale katika historia ya dunia.

Kumbuka hakuna ishara isiyokuwa na  ujumbe nyuma yake. Hivyo hizi ishara zitakuja na ujumbe, na ujumbe wake utakuwa ni wa kipekee, ukisoma kitabu cha ufunuo 10:4-11″ Inaelezea zile NGURUMO SABA ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, ni siri zilizofichwa tangu zamani nazo hazijaandikwa mahali popote katika biblia.

Zipo siri nyingi ambazo hazijulikani  kwamfano “Tutakapofika kwenye utawala wa miaka 1000 ni shughuli gani zitakuwa zinaendelea , na tukienda mbinguni tutakuwa tunafanya nini huko, siri za kwenda kwenye unyakuo na siri za kurudi kwa pili kwa Yesu, kuanguka kwa shetani, na mambo yaliyokuwa yanatendeka kabla ya Adamu kuumbwa nk,(huu ni mfano tu, zinaweza zikawa nyingine tofauti ya hizo au zaidi ya hizo ) .Siri hizi zitakuja kufunuliwa katika wakati huu ambao upo karibu katika mvua hii inayokuja kunyesha.

Ndugu William Branham kabla ya kufariki kwake alionyeshwa na Bwana huu uvuvio mkubwa jinsi utakavyokuja kuwa kiasi kilichomfanya yeye mwenyewe atamani kuwepo katika huo uamsho. Katika hilo ono alionyeshwa uponyaji wa kiungu wa ajabu ukitendeka watu wengi walikuwa wakiponywa kabisa kabisa.

lakini tukisoma

Mathayo 24:14″Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”

Mstari huu unaelezea jambo litakalofanyika kwanza kabla ya Bwana YESU kurudi, Huu uamsho unaokuja ndio utakaokuwa wa mwisho na utapita duniani kote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, kwasababu mambo dhahiri na ishara za ajabu zitaonekana kwa watu wote na bibi-arusi naye atakusanyika pamoja kwa ajili ya unyakuo na ndipo ule mwisho utakapokuja.

Ndugu hizi siku zipo karibu, wakati huo utakapofika kama leo haujajiweka tayari kule hautaweza kwasababu zitakuja na hukumu kutoka kwa Bwana, utaishia kupinga na kusema ni vya shetani, kwasababu utasikia mambo ambayo pengine hayajarekodiwa mahali popote kwenye biblia, na hautapata uhakiki wa mambo hayo sehemu yeyote kama hauna ROHO MTAKATIFU kwasababu ni mambo mapya kabisa na hautaweza kupambanua utabakia kuwa mtu wa nia mbili kama unyasi utikiswao na upepo hutajua wapi usimame, ikiwa leo tu huwezi kumtambua yupi nabii wa kweli na yupi nabii wa uongo, utawezaje kuelewa yatakayokuja huko mbele ambapo mambo mapya yatakuja kuhubiriwa??.

Tafakari ndugu tunaishi katika siku za mwisho, ijue kalenda ya Mungu katika maisha yako na wakati tuliopo, usije ukafanana na wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Maana ya yale mafuta ya ziada ni roho ya mafunuo ambayo mkristo wa dini tu hawezi kuwa nayo.

Ndugu kaa ukifahamu Huu uamsho utaanza duniani kote hivi karibuni, na mambo ya ajabu yataenda kutendeka na kuhubiriwa, kwa waovu itakuwa ni hukumu bali kwa wenye haki itakuwa ni kwa kuandaliwa kwa ajili ya unyakuo. Maandalizi ni sasa.

  “Tumeandika makala hii kuwakumbusha bibi arusi wa Kristo wote popote walipo kuwa kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni na kuna baadhi ya watumishi wa Mungu waaminifu wachache wamekwisha anza kuonyeshwa katika maono na Bwana Yesu, jinsi utakavyokuwa. Tazama chini shuhuda chache za watu hawa;”

 USHUHUDA WA STEPHEN POWELL’S 

Stephen Powell’s ni muhubiri wa kimarekani hivi karibuni tarehe 21 April 2017. Bwana alimwonyesha maono yafutayo na haya ni maneno yake yaliyonukuliwa;

NEMBO YA VITA ALIYOKUWA NAYO WILLIAM BRANHAM INAACHILIWA TENA.

Kulingana na historia, “NEMBO” (Coat of Arms) ni ishara muhimu ya utaratibu wa urithishaji uliotumika katika zama za kati huko Ulaya, Ilitumika mahususi kama utambulisho katika vita, Nembo zilianzishwa kuashiria ukoo wa familia fulani, urithi, umoja, umiliki, na pia katika taaluma fulani .

Bwana kwasasa anaenda kupitisha NEMBO hii ya thamani sana kwa kizazi chenye utukufu anachokinyanyua  leo duniani!, Mungu anaenda kuachilia uhalali fulani, ujuzi fulani, na urithishwaji katika roho!. Nisikilize kwa makini kitu ninachokwenda kusema sasa…

Hivi karibuni katika mfululizo wa maono niliyopewa, nilichukuliwa mbinguni nikaonyeshwa vitu vingi. Mara ya mwisho nilijikuta nimerudi katika hali yangu ya kawaida nikiwa na akili zangu  juu ya kitanda changu katika hotel moja huko west Virginia. Na nilipokuwa nimelala pale nilisikia BWANA akisema ” NINARUDISHA TENA NEMBO YA VITA ALIYOKUWA AMEIVAA WILLIAM BRANHAM “. Kisha nikaona ono Bwana akishika bega la askari mmoja ambaye kwenye nguo yake kulikuwa na kitu kama NEMBO hivi ingawa sikuweza kuikariri jinsi ilivyokuwa. Kisha  Bwana akaniambia ataenda kuachia vipawa vya miujiza katika mikono ya wana wake na binti zake katika hichi kipindi, kama ilivyokuwa kwa William Branham alivyopewa sio tu kuona maono bali pia kipawa katika viganja vyake.

KIZAZI KIPYA CHA WATENDA-MIUJIZA KATIKA MWENDELEZO WA WILLIAM BRANHAM.

Katika vita askari huwa wanavaa vazi fulani la nje (surcoat) kuzuia dirii isipate kutu. Hichi ndicho nilichokiona usiku ule, na ninaamini NENO la Bwana kuwa ni hili: Bwana anaenda kuendeleza haya katika roho mwaka huu  hapa Marekani na itakuwa ni kwa mwendelezo wa William Branham. Dirii ya huyu mtu haitaendelea kushika kutu itatokea tena kwa mara nyingine Marekani katika huu mwaka, wamekwisha vikwa hawa matenda miujiza wapya ambao wataanza kutenda kazi mwaka huu.

Kama vile Mungu alivyoweka fimbo katika mkono wa  Musa na kumwambia aende kufanya miujiza kule Misri, vivyo hivyo Mungu ataenda kufanya miujiza kupitia mikono ya hawa mashujaa ambao watatokea katika mwendelezo wa William Branham.

Branham alipewa maagizo mwaka 1946, Mungu alimwambia “miujiza itafanyika kupitia mikono yake”. Moja ya hii miujiza ilifanya kazi katika mkono wake wa kushoto na akapewa uwezo wa kupambanua roho hata kuweza kugundua uwepo wa magonjwa ya kipepo au udhaifu. Ishara ya pili aliyopewa ni kipawa cha ajabu cha maono aliweza kutambua siri za mioyo ya watu kwenye mimbari na kuwasaidia watu kuishinda roho ya kutokuamini (kitu ambacho kinazuia miujiza mingi isitendeke hapa Marekani). Mungu aliyafanya haya yote kupitia maisha ya huyu mtu na huduma yake, Hata hapa Marekani Mungu anaenda tena kufanya haya katika wakati wetu. Anaendeleza Nembo iliyokuwa kwa William Branham.

ONYO KWA VIONGOZI WA MAKANISA

Bwana alisema msiwe na mitazamo hafifu juu ya uvuvio unaokuja wa Mungu, kwasababu ikiwa haupo katika sehemu ya huo uamsho, ni rahisi wewe kuingia  katika hatari ya kumruhusu shetani aufanye moyo wako kuwa mgumu kama hautakuwa makini.

“Kuweni makini sana katika huu wakati mchunge laana mnazotoa katika midomo yenu juu ya huo uamsho unaokuja na kuuita kazi ya Mungu kuwa ni ya shetani. Kwasababu hata mafarisayo  walisema maneno hayo hayo japo walikuwa wanauona uwepo dhahiri wa Mungu ukitembea katika dunia. Sio mara zote ni rahisi kufahamu kipi kinatoka kwa Mungu na kipi kinatoka kwa shetani kwahiyo usiwe mwepesi kuhukumu kimakosa huo uvuvi unaokuja. Jinyenyekezeni viongozi wangu, ” Bwana anasema ” Na kwa utulivu hukumuni kazi ya Mungu hichi kipindi kinachokuja, sana sana kama katika kazi za kanisa”

“Kwasababu mimi BWANA nitaijaribu mioyo ya viongozi wangu katika huu uvuvio unaokuja; kwasababu uvivio unaokuja unahitaji kuujaribu uongozi. Mimi BWANA nitafichua siri za mioyo yenu, na kuyakemea mawazo yenu kwa vitu ambavyo hamjawahi kusikia wala msivyovielewa. Lakini kama mkijinyenyekeza  na kuwa wavumilivu  katika hukumu zenu katika hichi kipindi, Mimi Bwana nitawafunulia kazi zangu ni zipi na za shetani ni zipi.

“Mimi Bwana nitawafanya mtambue tofauti kati ya mwanga na giza. Lakini hawatapewa ujuzi huo viongozi wote wenye majigambo na wenye kujikweza na kujidhani kuwa wana mamlaka yote. Hawatapewa watu wanaojiona wanajua vitu vya Mungu. Siri za Mungu hawatapewa watu wale waliowepesi kuhukumu bali wale wanyenyekevu ndio watakaopewa kuzijua hizi siri.

Katika huu uamsho unaokuja kutafunuliwa vitu vya ajabu, siri zilizojificha, na vitu ambavyo huwezi kuvitegemea, Mimi Bwana nitaleta watenda miujiza na sio tu waponyaji, hawa watafanya miujiza ambayo hamjawahi kusikia wala kuona. Lakini msiogope kwa hivyo vitu msivyovielewa, Kwa kuwa mimi Bwana nitakuwa pamoja nanyi nami nitawapa uwezo wa kutambua. Nitaenda kuwasaidia, viongozi wangu, Mitume wangu, Manabii wangu, Wachungaji wangu, lakini muwe wanyenyekevu na msiwe wepesi kuhukumu. Hili ndilo Neno nalowapeni leo kuwaanda ninyi katika huo uvuvio unaokuja.

Love & Blessings,

Stephen Powell,

Lion of Light Ministries.

USHUHUDA WA SADHU SUNDAR SELVARAJ:

Hivi karibuni ndugu Sadhu ambaye ni nabii mwenye asili ya India Bwana amekuwa akimtumia kutoa nabii nyingi na kuja kutimia ikiwemo ushindi wa Obama 2008 na Donald Trump 2016 , mafuriko na matetemeko ya ardhi, mengi pamoja na tetemeko litakalokuja kutokea Calfornia Marekani hivi karibuni,  Alionyeshwa na Bwana Yesu Katika maono kwamba nguvu ya uvuvio iliyokuwepo juu ya nabii William Branham itarejeshwa tena ikiwa na nguvu mara saba”, kwa vijana wadogo ambao Mungu ataenda kuwanyanyua. Bwana alimwonyesha katika maono mengine mengi kuwa nguvu ambayo itaenda kuachiliwa katika huu wakati ukifika itakuwa ni kubwa sana na miujiza isiyokuwa ya kawaida itatendeka alisema. bofya hapa kutazama video .

 Na kuna manabii wengi wameonyeshwa uamsho huo utakao kuja duniani, baadhi yao ni Rick jonyer, Kenneth Hagin, Neville JohnsonVincent selvakumar n.k.

Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitika. Katika neema tulionayo sasa hivi umejiwekaje tayari umepokea Roho Mtakatifu?. Jitahidi utubu ndugu injili zinazokuja huko mbele sio za kuwafanya watu watubu tena bali ni kwa ajili ya hukumu na ushuhuda kwa watu tu , wakati wa kutubu ndio sasa, wakati wa kupita katika mlango ulio mwembamba ndio sasa, Tafuta mahusiano yako binafsi na Mungu epuka kamba za madhehebu uwe tayari maana Bwana yupo mlangoni kurudi. Ndugu huu ni wakati wa kukaa chini na kumtafuta muumba wako, kalenda ya Mungu isikupite usilemewe na mambo ya ulimwengu huu, Bwana Yesu alisema tukeshe ili siku hiyo isitujie kama mwivi maana ndivyo itakavyoujia ulimwengu mzima. Kukesha sio kujizuia kulala bali ni kuwa macho rohoni, ujumbe wa Mungu unapokushukia uufahamu. 

Luka 13:23-28″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”. 

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi

+255693036618/+255789001312


Mada Nyinginezo:

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”?

HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM


Rudi Nyumbani

Print this post

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Hii neema tulionayo leo itafika mwisho, kuna baadhi ya misemo imekuwa ikisemwa kuwa Mungu wa agano la kale leo hii hayupo, kama yupo zile ishara alizokuwa anatenda agano la kale ziko wapi leo?. Lakini SIKU YA BWANA inakuja ndugu usitamani uwepo! USITAMANI UWEPO! ni mambo ya kuogopesha ambayo usingetamani hata adui yako yampate, Mungu kuzuia ghadhabu yake ni kwa ajili yetu sisi tutubu lakini tusipotubu hukumu itatukuta.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

vitasa saba

Kuna vitu vitatu vinavyokuja huko mbeleni, 1) DHIKI KUU, 2) SIKU YA BWANA, 3) ZIWA LA MOTO. Leo tutaitazama hii SIKU YA BWANA ni ipi, itakuja lini na itakuwa inamuhusu nani.

Kwa ufupi ndugu, DHIKI KUU itakuja na tunafahamu itakuwa kwa wakristo watakaokataa kuipokea ile alama/chapa ya mnyama. Hii itamuhusu mpingakristo akiwatesa wakristo wale waliokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wale ambao hawakwenda kwenye unyakuo, Ambapo mwishoni mpinga-kristo atafanikiwa kuwaua kikatili wote wasioipokea chapa. Na hii dhiki itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu, ni wakati wa kutisha sana unakuja mbeleni. Kwahiyo wakati wakristo wachache wanapitia dhiki kuu, wengine wote waliosalia watakuwa wanaendelea kujifurahisha na mambo yao ya dunia wakimfurahia mpinga kristo na utawala wake.

Sasa SIKU YA BWANA  itaanza mara tu baada ya DHIKI KUU kuisha ambapo wale wanawali wapumbavu wote watakuwa wameshaondoka,(wameuliwa na mpingakristo) na unyakuo utakuwa umeshapita wakati huo, lakini hao waliobakia walioipokea chapa ya mnyama itawapasa waingie kwenye adhabu kali sana ya Mungu mwenyewe, Kwasababu wameshirikiana na mpinga kristo kuwaua watu wa Mungu na kwasababu wamekataa kumcha Mungu na kuzishika amri zake, ndugu Hii SIKU YA BWANA usitamani uwepo. Kumbuka haitakuwa jehanamu ya moto, bali itakuwa  ni adhabu ya hapa hapa duniani.

maandiko yanasema:

Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 

19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 

20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.

Pia tukisoma…

Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.

 7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka. 

8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.

 9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

 10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. 

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;

 12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”

Maandiko yanaposema SIKU YA BWANA hayamanishi ni siku kama siku moja, bali inamaanisha ni kipindi fulani cha WAKATI ambacho Bwana amekitenga kwa kusudi fulani. Kama maandiko yanavyotueleza ni kipindi ambacho kimetengwa cha GHADHABU NA HASIRA ya Mungu kulipiza kisasi kwa wanadamu wote wasiomcha Mungu.

Kipindi Hichi cha SIKU YA BWANA kitadumu kwa muda wa siku 75, Hizi zimepatikana kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli 12:12, ambapo tunaona kipindi cha ile dhiki kuu kitadumu kwa muda wa siku 1260, na hapo zimeongezeka siku nyingine kutoka siku 1260 mpaka kufikia siku 1335, kwahiyo ukichukua hizo siku 1335-1260=75.

Kwahiyo hizi siku 75 zilizoongezwa ni mahususi kwa ajili ya BWANA kujilipizia kisasi kwa wanadamu wote waliosalia juu ya uso wa  nchi.

Kabla ya SIKU hiyo ya BWANA kuanza Kutakuwa na baragumu saba zitakazopigwa kuitangulia ,  Hizi Zitabeba hukumu kwa watu wote, kama onyo watu watubu kumgeukia Mungu, Dunia itapigwa kwa mapigo mengi ya ajabu ukisoma Ufunuo 8 utaona hili, ikiwemo, theluthi moja ya maji kuwa damu, theluthi ya maji duniani kutiwa uchungu,theluthi ya mwezi na jua na nyota kupigwa,hebu tafakari kutakuwaje duniani wakati huo mchana kutakuwa kama jioni, giza litakuwa nene usiku na baridi kali sana, nzige wa ajabu watapandishwa kutoka kuzimu, maumivu yao ni kama ya kung’wata na nge, na meno yao ni kama meno ya simba, n.k.

Biblia inasema watu watakitamani kifo lakini hawatakiona, kumbuka hapo bado SIKU YA BWANA haijaanza huo ni mwanzo wa utungu tu, unatangaza hukumu KUU ya Bwana inayokuja mbeleni kwa urefu soma ufunuo sura ya 8 na ya 9. inaelezea haya mapigo ya baragumu saba za Mungu.

Lakini pamoja na mapigo yote hayo ya baragumu biblia inasema watu watakaokuwa juu ya uso wa nchi hawatatubu maovu yao kwasababu roho ya uovu imeshakaa juu yao kwa kuwa wote wamekwisha ipokea ile chapa ya mnyama neema ya Mungu imeondoka juu yao hawawezi kutubu tena.

Kwahiyo mara baada ya dhiki kuu ya mpinga-Kristo kuisha hapo tayari unyakuo ulishapita siku nyingi na wanawali wapumbavu kuuliwa, Sasa  Hawa wanadamu waliobaki ndio watakaoingia katika mapigo ya vitasa Saba vya Mungu  , katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia : Hebu tutazame vitasa hivi kimoja baada ya kingine.

KITASA CHA KWANZA:

Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.

2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”

Sasa adhabu hizi zitakuwa ni kwa Dunia nzima na sio theluthi tena ya dunia kama ilivyokuwa kwa zile baragumu saba. Majipu haya tunaona ni mfano wa yale yale waliopigwa wamisri, Kutakuwa na majipu ya ajabu usidhani ni haya ya kuwaida uliyoyazoea, biblia imeyaita ni MAJIPU MABOVU bado hajatokea kabisa duniani, huo ugonjwa bado haujazuka, Tuna magonjwa mengi ya hatari duniani lakini biblia haijayataja yote hayo, lakini ni huu ugonjwa wa MAJIPU tena jipu bovu ndio umetabiriwa utakuja, homa yake itakuwa sio kama hizi za kawaida tulizozizoea. Ndugu usitamani kuwepo huko wewe unayesema Mungu wa agano la kale haishi, siku hiyo utayaona haya wazi wazi.

KITASA CHA PILI:

Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” . 

Duniani kutakuwa na harufu kama ya damu ya mtu aliyekwisha  kufa, fikiria jambo hilo dunia nzima kutoa uvundo,  hakutakuwa na kiumbe chochote baharini chakula kitapungua duniani, maji yataisha, shughuli za usafirishaji baharini nk. vitakwama, mvua zitaacha kunyesha duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena mwanadamu, taabu itaongezeka duniani, hofu kuu itawaingia watu wakitazama ni mambo gani haya yameipata dunia?.. lakini bado mapigo yatakuwa yanaendelea,

KITASA CHA TATU:

Ufunuo 16:4-7 ” Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. “

Baada ya bahari kugeuzwa kuwa damu ya mizoga, watu wote tunajua wangekimbilia kutafuta maji katika mito na kwenye chemchemi za maji, kutokana na kiu kikali, lakini Bwana atayapiga pia maji ya mitoni na chemchemi, wakati huo fedha itakuwa haifanyi kazi tena, Mtu tajiri atakuwa ni mwenye kikombe cha maji safi mkononi mwake na sio fedha, Kwahiyo Bwana atawalazimisha kuyanywa hayo maji ya DAMU kwasababu  walishirikiana na yule mnyama kumwaga damu ya watakatifu wa Mungu, hivyo nao Bwana amewapa wainywe. Na kwasababu ya kiu kali watakunywa hiyo damu, na wanadamu wengi wataangamia na kufa kwa pigo hilo.

KITASA CHA NNE:

Ufunuo 16:8-9 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”

Baada ya pigo la maji kuwa damu, jua litashushwa chini, maunguzo yatakuwa ni makubwa  sana, joto litaongezeka duniani kwa nyuzi joto kubwa kuliko kiwango cha kawaida. Mimea yote itakauka, dunia itafanana na jangwa ndani ya muda mfupi sana, jaribu kutafakari jipu linapigwa na jua kali halafu hakuna maji hata kidogo ya kujipooza,ni dhiki kiasi gani? ni mambo ambayo huwezi dhania yatatokea lakini yapo mbioni kutokea. Lakini pamoja na hayo mapigo yote  biblia inasema watu watamtukana Mungu hawatatubu. Mfano tu wa kizazi chetu hichi watu wanapopatwa na majanga badala wageuke na kumuuliza Mungu ni kwanini na kutubu, wao wanalaani.

KITASA CHA TANO:

Ufunuo 16:10-11 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. “

Sasa pigo hili linamuhusu sana sana yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa, mahali kiti chake cha enzi kilipo ambapo ni VATICAN, Roma, Mungu ataachilia laana kwa mataifa ya ulaya ambayo ndio zile pembe kumi, zitamchukia na kumwangamiza yule mwanamke kahaba (Kanisa Katholiki) ambalo makao yake makuu ni VATICAN.

Hii ni kutokana na kwamba yale mataifa ambayo yalimtumaini mpinga kristo ayaletee amani duniani, hayajaletewa zaidi ya yote mpingakristo (PAPA) ameiongezea dunia matatizo hivyo basi watamchukia na kumwangamiza, tangu wakati huo utawala wa Roma, pamoja na mpinga kristo (PAPA) na Vatican yake hawatakuwepo tena ufalme wao umekwishatiwa giza.

Soma

ufunuo 17:16″ Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. ” 

KITASA CHA SITA:

Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 

15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 

16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”

Kitasa hichi kunazungumzia ile vita kuu ya HAR MAGEDONI ambayo itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi akilipigania taifa la Izraeli dhidi ya wafalme wote wa dunia. karibu kila taifa litaunga mkono vita hii wakiongozwa na mataifa kutoka mawio ya jua. Haya mataifa ya mawio ya jua ni mataifa ya mashariki, nayo ni CHINA,JAPAN, KOREA n,k. Wakati huo Vatican itakuwa haipo, Marekani itakuwa haipo, Urusi itakuwa haipo yatatoweshwa katika vita vilivyoelezwa katika ezekieli 38 & 39,

Kwahiyo zile roho chafu ambazo zilikuwa zinaendesha Vatican na Marekani zitahamia kwenye haya mataifa ya mashariki yaliyosalia kwa ajili ya vita dhidi ya Izraeli. Wakati huo ndio Bwana YESU atakapotokea kuwapigania watu wake Izraeli. Ndugu wakati huo dunia itakuwa mfano wa sayari ya Zebaki, hakutakuwa na maji, chakula, magonjwa, joto litakuwa juu sana,maji yote damu, machafuko pamoja na vita, usitamani ndugu yangu uwepo nakuombea Mungu usiwepo itakuwa ni vilio na kusaga meno, siku hiyo watu watatamani siku hizi za neema tulizonazo leo hawataziona.

KITASA CHA SABA:

Ambacho ndio hasaa kinaizungumzia ile siku ya Bwana..

Ufunuo 16:17-21 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 

18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.

 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.

 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 

21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”

Hili ni pigo la mwisho, na katika hili ghadhabu ya Mungu imetimia tukisoma pale muhuri wa sita ulipofunguliwa ulitoa picha halisi jinsi hii siku itakavyokuwa soma Mathayo 24:30-31 na pia Ufunuo 6:12-17

Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 

16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Pigo la saba la mwisho kama tunavyosoma ni baya kuliko yote yaliyotangulia maana jua linaondolewa, mwezi utakuwa damu, nyota zitatoweka, unaweza kuona kutakuwa na giza kiasi gani duniani, na baridi kiasi gani,litakuwaa ni giza zito sana, hakutakuwa na chanzo chochote cha umeme, shughuli zote za kimaendeleo zilishamalizwa katika mapigo yaliyotanguliwa, hadi kufikia hapa watu wachache sana watakuwa wamesalia duniani, kumbuka hapo bado ziwa la moto linasubiri watu, Hichi ni kisasi cha hapa hapa duniani.

Mvua ya mawe kubwa sana itanyesha, mawe kama talanta,(talanta 1 ni kama kg 34), Huwezi kujificha kwenye nyumba yako ya bati au ya kigae, kg 34 ni uzani mkubwa sana itaambana na  tetemeko ambalo halijawahi kutokea, kiasi cha kwamba visiwa vitahama, kisiwa cha zanzibar kitapotea, Milima itatapika volkano, kumbuka hayo yote yatafanyika katikati ya giza nene, hakuna mawasiliano.  hapo hakuna  mfalme wala mtumwa, raisi wala mwananchi wote waliosalia watatamani wafe kuliko kuishi, watatamani milima iwaangukie waikwepe ghadhabu ya Mungu,  Hapo ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mawinguni.

Soma

Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. “

Rafiki haya mambo ni kweli yatatokea, ndivyo yatakavyokuja kuupata ulimwengu na dalili zote zinaonyesha kuwa yatatokea katika kizazi chetu tunachoishi mimi na wewe, Bwana amekwisha kutuonya mbele, Nia yake ni sisi tuiepuke hiyo ghadhabu na ndio maana kuna mahali alisema alipokuwa katikati ya kitasa cha sita (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake). Kwahiyo ametuonya tukeshe na kuyatunza mavazi yetu, maana hii siku ya ghadhabu itakuja ghafla.

Ndugu kimbia injili ambazo zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka kutazama mambo ya ulimwengu huu. Hii ni roho ya shetani inawapumbaza wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2000 mbele, usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana.

Chunguza maisha yako angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na maombolezo, kimbilia kalvari sasa tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu, na Upokee Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika. Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la moto litafuata.

Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako au fuatiliza sala hii kwa imani:

Sema: 

“Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.

Baada ya kutubu unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu na utakuwa umekamilisha wokovu wako.

MUNGU AKUBARIKI.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada zaidi, wa kanisa, au mafundisho, au ushauri, piga namba hizi

+255693036618/ +25578901312


Mada Nyinginezo:

KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU

CHUKIZO LA UHARIBIFU.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MPINGA-KRISTO

Mpinga-Kristo ni nani?

Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu.

Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe.

Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.

Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).

Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.

Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika “SIRI”. Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji “UFUNUO wa ROHO” Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.

SIRI YA YESU KRISTO:

1 Timotheo 3:16 ” Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”

Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema “Yohana 5:43  Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. “ unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao

1 Wakoritho 2:6-8″  Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;

7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; “.

Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU,  kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.

SIRI YA MPINGA-KRISTO:

2 Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU;

4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7 Maana “ILE SIRI YA KUASI” HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;

9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;

10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.”

Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa “kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe”. Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na  kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.

JE HUYU MPINGA-KRISTO NI NANI?

Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.

Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.

Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa “SIRI YA UASI”. na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye.

Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA “TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI”..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo.

Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu,  n.k.

Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja “MFU” lenye jina linalofanana na  lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI).

Na yeye (shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani.

Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.

Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO.

Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama).  Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa “CHAPA YA MNYAMA”.

Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.

Ufunuo 18:4-5″  Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA

PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ATUMIE MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO LAKE, JE! TUNARUHUSIWA NA SISI PIA KUTUMIA POMBE?

BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?

Rudi Nyumbani

Print this post

KITABU CHA UZIMA

Kitabu cha uzima ndio kipi?


Ufunuo 20:11-15

11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa KATIKA VILE VITABU, sawasawa na MATENDO YAO.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 

15 NA IWAPO MTU YEYOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA, KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.”

Amina! Tukifuatilia mistari hiyo hapo juu tunaona katika ile siku ya mwisho ya Hukumu Bwana Yesu atakapoketi kuwahukumu wanadamu katika kiti chake cheupe cha enzi, kutakuwa na aina kuu mbili za vitabu: KITABU CHA UZIMA na VITABU VINGINE,. Hapo unaona kitabu cha uzima kinaonekana ni kimoja tu!. Lakini pia kuna vitabu vingine, ikiashiria ni vingi, kwa ufupi  tuvichunguze hivi vitabu ni vitabu gani;

Kitabu cha Uzima ni kipi? Na je! kinafunua nini sasa?

1) KITABU CHA UZIMA:

Kama kinavyojielezea ni kitabu kinachoelezea UZIMA, kama vile kitabu cha hesabati kinaelezea njia za hesabu, kitabu cha jeografia kinaelezea masuala ya kijeografia vivyo hivyo na vitabu vingine vyote. Na tunafahamu vitabu huwa vinagawanyika katika kurasa mbali mbali. Lakini tunaona vitabu vyote hivi tulivyonavyo duniani vinatueleza tu kanuni na mbinu za mambo mengi yahusuyo ulimwengu huu, na tunaona hakuna kitabu chochote ulimwenguni kilichoweza kuelezea UZIMA wa mwanadamu isipokuwa BIBLIA TU!. Kwahiyo kitabu cha uzima kinachozungumziwa hapo ni BIBLIA ambalo ni NENO LA MUNGU.

2) VITABU VINGINE

Tunaona biblia imevitaja kuwa ni vingi, hivi navyo  vinaelezea habari fulani na sio nyingine zaidi ya wanadamu kulingana na biblia inavyosema. Hivi ni VITABU vya wanadamu na kila mwanadamu anacho cha kwake, kikimwelezea maisha yake jinsi alivyoishi hapa duniani kwa muda wote aliopewa hapa duniani kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Na hivi navyo vina ukurasa, ambazo ni hatua unazopitia hapa duniani, Lakini hivi vitabu vyote havina uzima ndani yake, kitabu cha UZIMA ni kimoja tu, na ndio maana hivi vyote vinakitegemea hicho cha UZIMA kutoa hatma ya mwanadamu.

Kwahiyo kile kitabu cha UZIMA kinaelezea kanuni na taratibu za mwadamu anavyopaswa aishi hapa duniani ili aupate huo uzima uliondikwa ndani yake, hivyo basi kama wanadamu tunaoandika vitabu vya maisha yetu tunapaswa tuviandike vifanane na kile  cha UZIMA yaani BIBLIA, kuanzia utoto wetu mpaka kuondoka kwetu duniani vitabu vyetu vinatakiwa vifanane na  cha UZIMA, na huko ndiko KUONEKANA KWA  MAJINA YETU KATIKA KITABU CHA UZIMA. 

Hivyo ndugu kitabu chako unakiandikaje? angalia muda unavyokimbia! usiseme nitampokea Kristo au nitaishi maisha matakatifu nifikisha umri fulani au nikishapata kitu fulani. Jua mpaka sasa kitabu chako kinaendelea kuandikwa na ndivyo kurasa zinavyozidi kufunguka na kufunga, muda unavyozidi kwenda ghafla utajikuta kitabu chako kimefungwa kinasubiriwa kufunguliwa kwenye ILE SIKU YA HUKUMU. 

Na siku ile ya Hukumu kile cha UZIMA kitafunguliwa na cha kwako pia kitafunguliwa, vitalinganishwa, kama vinafanana au la! ‘”HUKO NDIKO KUHAKIKIWA JINA LAKO”. Kama Jina lako halikuonekana inamaanisha kitabu chako (maisha yako), Hayaendani na kile cha UZIMA  (yaani Biblia, NENO LA MUNGU). Hivyo basi kwa kuwa hauna UZIMA ndani yako sehemu yako itakuwa katika lile ziwa liwakalo Moto na kibiriti.

Kama mkristo maisha yetu kila siku tunapaswa tuyalinganishe maisha yetu na biblia, je! tukifanyacho kinaendana na kitabu cha uzima?. unafahamu kabisa waasherati, wazinzi, walevi, watukanaji, waabudu masanamu, waongo, wasengenyaji, mashoga, wasagaji, wavutaji sigara, wafanyaji wa mustarbation, watazamaji wa pornography, waizi, mafisadi,waendaji kwa waganga na wapiga ramli, wala rushwa, wauaji, nk, watu wa dizaini hii maisha yao yapo mbali na kile kitabu cha UZIMA, unategemea vipi uonekane katika kile kitabu, kumbuka majina yanayozungumziwa pale sio John, Yohana au Mary bali ni maisha yako  Jihakiki ndugu komboa wakati siku hizi ni za mwisho. soma. 

Ufunuo 21:27 ” Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”

Siku zote Kitabu hakiandikwi katika siku moja, ili kitabu chako kifanane na kile cha UZIMA Sio hatua ya siku moja bali ya maisha yako ya kila siku, usiishi maisha ya kuidharau injili leo ukasema siku moja nitamgeukia Mungu, usijinganye kile kitabu haukifananishi ndani ya siku moja inahitaji maisha. Bwana YESU alisema

 Luka 9:23″ Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate. ” Unaona sio siku moja.

Maombi yangu ni wewe umgeukie Mungu. Anza kukiandika kitabu chako vizuri katika muda wako wa maisha uliobakiza hapa duniani, kila siku kifananishe kitabu chako na  cha UZIMA ili siku ile ikifika JINA LAKO LIONEKANE. UIEPUKE HUKUMU.

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi 

+255693036618/+255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

KITABU CHA UKUMBUSHO

INJILI YA MILELE.

BARUA INAYOSOMWA

JE! KUNA UBAYA WOWOTE KUWAOMBEA NDUGU ZETU WALIOKUFA KATIKA DHAMBI, MUNGU AWAKUMBUKE KATIKA UFALME WA MBINGUNI?

JE! MUNGU ANAMJARIBU MTU?


Rudi Nyumbani

Print this post

MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

Yakobo 1:5-8″  Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 

7 MAANA MTU KAMA YULE ASIDHANI,YA KUWA ATAPOKEA KITU KWA BWANA. 

8 MTU WA NIA MBILI HUSITA-SITA KATIKA NJIA ZAKE ZOTE.”

MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

Mtu akishakuwa mkristo vita kubwa anayoanza kupitia ni katika AKILI, shetani anahamisha vita vyake kutoka katika mambo ya nje, kwenda katika mambo ya ndani kwa kusudi moja tu, la kumfanya mtu huyo alitilie SHAKA Neno la Mungu!, kwa kumletea mashaka asiuamini wokovu wake jambo linalompelekea mtu kama huyo kuwa katika hali ya KUSITA KWENYE MAWAZO MAWILI.

Shetani anafahamu kuwa mtu atakapoliamini Neno la Mungu kwa asilimia zote pasipo mashaka atapata anachokitafuta, sasa hapo shetani ndipo anapoanza kuwinda imani ya huyo mtu kwa kumletea mashaka moyoni mwake. Tunaona mfano mtu kama Petro alianza kutembea vizuri juu ya maji lakini alipoanza kutia shaka tu akaanza kuzama.

Kwahiyo silaha kubwa shetani anayoitumia kwa mkristo ni kumletea mashaka asiliamini Neno la Mungu aendelee kubaki katika hali ya kusita-sita asipokee kitu chochote kutoka kwa Bwana. Mbinu hii shetani alitoka nayo tangu Edeni pale Hawa aliporuhusu wazo la shetani la kutilia mashaka NENO la Mungu, na kula tunda ikapelekea mauti jambo ambalo linaendelea mpaka sasa. KULITILIA MASHAKA NENO LA MAUNGU!.

  Kwamfano Neno la Mungu limeahidi “wakutanikapo wawili au watatu kwa jina lake yeye atakuwepo katikati yao”. Lakini shetani atamletea mtu huyo wazo kwenye akili yake likisema : {…Aah! hilo haliwezekani, Mungu yupo mbinguni hawezi kuwepo hapa katikati yetu,hawezi kuwepo sehemu kama hii, sisi ni wachafu kama sivyo mbona hatumuhisi….}.  Sasa mtu huyo akidhani kuwa hilo wazo ni la kwake, kumbe hajui linatoka kwa yule mwovu..kwasababu shetani amemletea hilo wazo likianza na “mimi.. mimi.. mimi”.

Halianzi kama shetani anamwambia mtu huyo bali linakuja kama vile yeye huyo mtu ndio analiwaza hilo wazo. Hivyo inakuwa ni ngumu kwa mtu kama huyo kutambua mawazo ya shetani ni yapi na yake ni yapi. Kwasababu hiyo basi shetani anafanikiwa kumwacha katika hali ya kusita-sita na mwisho wa siku hapokei chochote kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu hakai katika mashaka, yeye ni wa kuaminiwa tu!.

  Tuchukue mfano mwingine, Neno la Mungu linasema.“Kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Hivyo Mtu akiwa mgonjwa atakapojaribu tu kulitafakari hili NENO limfae kwa ajili ya uponyaji wake, wazo lingine litamjia kwa haraka kichwani mwake,..{….Aaah! Hivi ni kweli inawezakana, hii inahitaji mtu mwenye upako sana, au mtakatifu sana, mimi nimemkosea sana Mungu hawezi kunisamehe wala kunisikia….} .

Kwahiyo mtu huyu anadhani kuwa mawazo hayo ni yeye kayatengeneza kumbe hajui ni shetani ndiye aliyemtengenezea na kuyapandikiza kwenye Akili yake pasipo mtu huyo kujua, Na kama ilivyo ada  shetani anamletea hilo wazo lianze na neno “mimi,.. mimi”. Hivyo basi mashaka hayo yakishaingia ndani ya moyo wake yanamsababishia mtu huyo asipokee uponyaji wake. Shetani anakuwa amemshinda.

  Mfano mwingine, Bwana Yesu alisema Marko 11:24″  Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. “. Hapa utamkuta mtu yupo katika kusali na kupeleka mahitaji yake binafsi mbele za Mungu akiwa katikati ya kusali wazo linamjia,{…“Aah! Hivi kweli Mungu atajibu maombi yangu, Mungu lazima atakuwa hapendezwi na mimi!. Ili anisikie ingenipasa nifunge kwanza wiki tatu, Aaah! acha tu niombe anaweza akanijibu”….}..

Unaona hapo hilo neno “anaweza”.tayari ni mashaka hayo hana uhakika na anachokiomba akidhani kuwa hayo ni mawazo aliyoyatengeneza yeye, kumbe ni mawazo ya shetani kayatupa kwenye akili yake, na kumfanya mtu huyo kuwa katika hali ya kusita-sita hivyo hawezi kupokea chochote kutoka kwa Mungu, Kwasababu shetani anajua tu! atakapoliamini hilo NENO kwa asilimia zote, pasipo kutilia shaka kwa namna yoyote, Atapokea chochote anachokiomba.

Tazama hichi kisa hapa chini, jinsi mtu huyu alivyompa Kristo maisha yake, siku ya jumatatu, lakini angalia shetani alivyoanza kuiwinda imani yake, na kumpelekea kuwa MTU WA KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

Siku ya jumanne anaanza kujifunza Neno la Mungu…

..Siku ya jumatano anautilia mashaka wokovu wake…

…Alhamisi anajihisi hajaokoka na kurudia kumpa Kristo tena maisha yake…

NAMNA YA KUSHINDA HALI HIYO:

Wazo lolote linalokuja katika kichwa chako linalokufanya ulitilie shaka NENO la Mungu, lipinge na kulikataa kwa JINA LA YESU kwasababu hayo sio mawazo yako bali ni ya shetani ameyaelekeza kwako ili usipokee kitu kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu anasema katika 

Yakobo 1:7-8 “Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.“.

Hivyo basi  Rudisha mawazo yako na sema ndani ya moyo wako “maneno ya Mungu, ni kweli na hakika”. yashikile hayo hayo pasipo kujihukumu mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo shetani atakukimbia na kukufanya kuwa mshindi siku zote na kupokea Ahadi za Mungu.

Usiruhusu mawazo yoyote ya kulichunguza NENO la Mungu kuwa linafanyaje fanyaje kazi, siku zote njia za Mungu hazichunguziki wewe AMINI tu!. Hayo mengine mwachie yeye, amesema kwa kupigwa kwake tumepona! amini hilo NENO kila siku litamke,sema moyoni mwako Mungu siku zote hawezi kusema uongo! usitafute kujua litafanyaje fanyaje kazi, itaonekana kuwa hakuna matumaini! lakini wewe liamini tu na utashangaa unapokea uponyaji wako. NENO la Mungu linasema “yote yawezekana kwake yeye aaminiye”.

Kwahiyo ukiwa katika sala unaomba jambo lolote amini umelipokea. usianze kusita-sita, au kujiuliza uliza au kutafuta njia mbadala,wewe mwamini Mungu lishikilie hilo neno, nalo litatokea kama lilivyo usitazame muda hata kama litachelewa lakini litakuja tu! wewe liamini tu usiruhusu mawazo mengine yoyote ya shetani ya mashaka kuingia ndani yako.

Pambana shetani hapo ndipo anapofanyia vita na hakuna vita vigumu kama hivyo, Tutamshinda shetani tu pale tutakapokuwa na NENO ndani yetu na kuliamini asilimia mia, lakini tukiwa watu wa mashaka kama maandiko yanavyosema TUSITAZAMIE KUPOKEA KITU CHOCHOTE KUTOKA KWA BWANA.

……Hapa yule mtu anatambua uongo wa shetani na anachukua hatua..

…..mwishoni wokovu wake unakuwa thabiti usiokuwa na mashaka…….

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: 

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

MTETEZI WAKO NI NANI?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

NINI MAANA YA ELOHIMU?


Rudi Nyumbani

Print this post

NDOA NA TALAKA:

Ndoa na talaka, kibiblia ni inakuwaje?


Mathayo 19:3-8″ Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, KWASABABU HIYO, MTU ATAMWACHA,BABAYE NA MAMAYE, ATAAMBATANA NA MKEWE; NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA;

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. BASI ALIOWAUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIWATENGANISHE.

7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 

8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. “

Ndoa na talaka, kibiblia ni inakuwaje?  Mathayo 19:3-8" Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 

Hapa tunaona jambo la kuachana kwa mke na mume halimpendezi Mungu hata kidogo, kwasababu biblia inasema alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hivyo ndoa haipaswi kuvunjwa isipokuwa kwa sababu zifuatazo zilizohorodheshwa kwenye biblia; 

1) UASHERATI:

Biblia inasema kwenye

Mathayo 19:9″ Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWASABABU YA UASHERATI, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. “. 

Ikiwa mmojawapo kati ya wanandoa amefumaniwa katika uzinzi hapo biblia imeruhusu kumwacha mtu huyo, na kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine, lakini kama ni kwasababu nyingine yoyote tofauti na uzinzi mfano kugombana, kuudhiana,  fitna, matatizo, shida, dhiki,magonjwa n.k. hapo biblia hairuhusu kuachana, na hata kama imetokea wameshindwa kulewana na kupelekea kuachana hairuhusiwi kwenda kuoa au kuolewa tena, Biblia inasema kila mmoja akae kama alivyo, ikiwa kama wakipatana wanaweza wakarudiana kinyume na hapo watakuwa wanafanya uzinzi.(marko 10:11-12) ,

 Biblia inasema

 1Wakoritho 7:10- 11″ Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.  

Hivyo basi ikiwa jambo kama hili limetokea mmojawapo kukamwatwa katika uzinzi ni vizuri ukajifunza kusamehe ili ndoa isivunjike, Mungu hapendi kuachana, kwasababu hata Bwana Yesu Kristo anatusamehe sisi mara nyingi pale tunapomfanyia uasherati wa kiroho, je! sisi hatupaswi kufanya zaidi?  lakini ikiwa huwezi kuvumilia  unaweza ukaivunja utakuwa hauna hatia biblia imeruhusu wewe kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine.

2) IKIWA AMETAKA KUKUACHA KWA SABABU YA IMANI YAKO:

Kama imetokea mlifunga ndoa wakati wote hamjawa waamini, na wewe ukaja kuwa muamini angali ukiwa ndani ya hiyo ndoa, na mkeo/mumeo asitake kukubaliana na imani yako na akaamua kukuacha asiishi tena na wewe, katika hali kama hiyo biblia inaruhusu wewe kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine lakini iwe katika BWANA TU!. Lakini kama ikitokea yule mtu katika hali yake ya kutokuamini anakubali kuishi na wewe hautakiwi kumuacha ukimuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine utakuwa UNAFANYA UZINZI! . 

soma

1Wakoritho 7:12-16 ” Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.

13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 

15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 

16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? “.

Kumbuka kuachana huku ni kwa wale tu! walioana kabla ya kuamini! Biblia haitoi ruhusu yoyote kwa wale walioamini kuachana isipokuwa kwa habari ya uasherati tu, na pia biblia hairuhusu mtu mwamini akaoe/kuolewa na mtu asiyeamini! Hilo ni kosa.

Hivyo basi kama maandiko yanavyosema waebrania 13:4″ Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. “. Ni vizuri mtu unapoingia kwenye ndoa ujue ni jambo la kuheshimika na Mungu hapendezwi na wanandoa kuachana kwasababu yoyote ile! (malaki 2:16 ).

Pale ndoa inapofungwa tu! Mungu anaachilia neema na baraka ya ziada tofauti na mtu ambaye hayupo kwenye ndoa, na pale ndoa inapovunjika kumbuka kuna hasara nyingi, ikiwemo kuzuia baraka za kiroho, watoto unawafanya kuwa kama yatima, unajirudisha nyuma na kuanza safari mwanzo hivyo basi ili kuyaepuka hayo kuwa mwaminifu kwa Bwana na kwa mke/mme wako. Na pia ufanye maamuzi sahihi katika kuchagua mwezi ikiwa kama bado haujaingia kwenye ndoa.

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:  +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU SAWASAWA NA KUTOKA 20:5-6?

AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?.


Rudi Nyumbani

Print this post