Moja ya jukumu la muhimu sana la kufanya baada ya kuzaliwa mara ya pili, ni kuzidi kumjua Yesu Kristo kwa undani, kwasababu Agano jipya lote linamuhusu Yesu Kristo, kiini chote cha biblia kinamuhusu Yesu Kristo, Agano la kale lilimuelezea Yesu Kristo kimafumbo lakini agano jipya limemwelezea kwa uwazi wote, Ukristo utakuwa haujakamalika kwa namna yoyote kama tutashindwa kumwelewa vizuri Yesu Kristo.
Tukishindwa kumwelewa Bwana Yesu , ni nani, kwanini alikuja duniani, anatendaje kazi, anataka nini kwetu, na sisi tunahitaji nini kutoka kwake, yuko wapi sasa hivi, anafanya nini n.k basi hatutaweza kumwelewa pia yule anayempinga yeye (Mpinga-Kristo) ni nani na anatoka wapi? Kadhalika Hatutaweza kujua mpinga-Kristo anatendaje kazi.
Kwasababu ni wazi kuwa huwezi kumjua adui ya mtu kabla hujamjua huyo mtu mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kufahamu maadui wa mtu asiyemjua, sharti kwanza amjue huyo mtu anapotokea na maisha yake ndani nje yalivyo ndipo aweze kuwatambua na maadui zake. Vivyo hivyo hatutaweza kumjua Mpinga-Kristo kama hatutamjua Yesu Kristo vizuri kwa undani.
Miaka mingi, sana kabla ya mwanadamu wala wanyama kuumbwa, Bwana Mungu alikuwa peke yake, alikuwa hana cheo chochote kwasababu katika hali ya kawaida, ili mtu awe na cheo sharti awepo mtu aliye chini yake.
Sasa Mungu kabla ya kuumba wanadamu wala malaika, kulikuwa hakuna mtu chochote chini yake wala juu yake, hivyo alikuwa hana cheo chochote, alikuwa ni yeye kama yeye tu! na alikuwa pia hana jina, kwasababu jina kazi yake ni utambulisho kwa wasio kujua, hivyo yeye wakati huo alikuwa hana bado wasio mjua wala wanaomjua, hivyo alikuwa ni yeye kama yeye,Na ndio maana alimwambia Musa jina lake ni “MIMI NIKO AMBAYE NIKO”..sasa hilo sio jina kama ukilitafakari kwa makini, bali ni sentensi inayojaribu kuelezea uwepo wa Mungu. Hapo ni Bwana alikuwa akijaribu kumweleza Musa nafasi yake aliyokuwepo nayo kabla ya uumbaji wa kitu chochote kile.
Sasa ulipofika wakati wa uumbaji alipoanza kuumba malaika, ndipo hapo akaanza kuitwa Mungu, kwasababu maana ya Neno Mungu ni “mtengenezaji/au muumbaji” ndipo vikawepo viumbe chini yake vilivyoumbwa na yeye, viumbe hivyo vikaanza kumwita yeye Mungu, lakini kabla ya hapo alikuwa haitwi Mungu. Kwasababu hata katika maisha ya kawaida, Mtu hawezi akaitwa Baba kabla hajapata watoto, siku atakapopata watoto ndipo hapo atakapoitwa Baba au Mama, na ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu hakuitwa Mungu, mpaka siku alipoumba.
Na ulipofika wakati wa mwanadamu kuumbwa, ambao aliwaita watoto wake, Cheo chake kilizidi kubadilika na Kuwa Baba, hivyo akawa na vyeo viwili yaani Baba pamoja na Mungu mwenyezi, kwasababu sisi wanadamu tuliomwamini yeye, Mbele za Mungu wetu ni kama watoto wake, Malaika sio watoto wa Mungu, bali sisi wanadamu ndio tunaoitwa watoto wa Mungu..
Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?” .
Hivyo ulipofika wakati wa Yeye kujidhihirisha kama Baba ni pale alipowatoa wana wa Israeli kutoka Misri akafunua jina lake kama YEHOVA,(Kutoka 6:1-6) Kwahiyo jina la Baba likawa ni YEHOVA, lakini ndio yule yule Mungu mwenyezi na ndio yule yule Baba Yetu. Aliwaokoa wana wa Israeli kama watoto wake kutoka katika mikono ya Farao kwa jina lake Yehova.
Kutoka 4:22 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, MPE MWANANGU RUHUSA AENDE, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako”.
Hosea 11: 1 “Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, NIKAMWITA MWANANGU ATOKE MISRI”.
Unaona Sasa kwasababu Israeli ni Mzaliwa wa Kwanza, ni lazima awepo mzaliwa wa pili, na huyo sio mwingine zaidi ya watu wa mataifa, Hivyo watu wa Mataifa nao pia waliingizwa katika neema hii ya kuitwa wana wa Mungu..
Warumi 9:23 “tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; 24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ILA NA WATU WA MATAIFA PIA? 25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. 26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, NINYI SI WATU WANGU, HAPO WATAITWA WANA WA MUNGU ALIYE HAI”.
Warumi 9:23 “tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;
24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ILA NA WATU WA MATAIFA PIA?
25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, NINYI SI WATU WANGU, HAPO WATAITWA WANA WA MUNGU ALIYE HAI”.
Lakini kama tunavyojua agano la kwanza halikuweza kumkamilisha mwana wa kwanza (wana wa Israeli) kuwa mkamilifu, kadhalika lisingeweza pia kumkamilisha mwana wa pili (yaani watu wa mataifa) kuwa wakamilifu, hivyo Bwana Mungu mwenyezi akatengeneza njia nyingine ya kuwakamilisha wana wake wote wawili (yaani wayahudi na watu wa mataifa), ambayo katika hiyo watakuwa wakamilifu kweli kweli…. Na ndio hapo akauvaa mwili yeye mwenyewe YEHOVA na kuwa mwanadamu, ili kuwa kipatanishi kati ya wanadamu na nafsi yake mwenyewe.
Akauvaa mwili akazaliwa kama mwanadamu, akatembea kama mwanadamu akaishi kama mwanadamu, akajinyenyekeza kama mwanadamu, hakufanya vile kwa wazi bali alifanya kama siri mpaka utakapofika wakati wa kufunuliwa kwa siri hiyo, kwamba Yesu Kristo alikuwa ni Yehova mwenyewe katika mwili wa kibinadamu, na ndio maana Malaika Gabrieli alimwambia Bikira Mariamu amwite jina lake YESU, sasa tafsiri ya jina Yesu kwa kiebrania ni YEHOVA-MWOKOZI, kwahiyo ni yule yule YEHOVA KATIKA MWILI WA KIBINADAMU, Isipokuwa Jina lake limeongezeka na kuwa YEHOVA-MWOKOZI hivyo amekuja kwa kuokoa. Siri hiyo hawakufunuliwa watu wote isipokuwa wale ambao Bwana alipenda kuwafunulia. Na ndio maana Mtume Paulo aliileza siri hiyo kwa ujasiri katika..
1 Timotheo 3: 16 “Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na HAKI KATIKA ROHO, Akaonekana na malaika, AKAHUBIRIWA KATIKA MATAIFA, AKAAMINIWA KATIKA ULIMWENGU, AKACHUKULIWA JUU katika utukufu”.
Unaona hapo Mtume Paulo anamzungumzia Yesu Kristo, Mungu katika mwili, lakini anasema ni SIRI?
Sasa unaweza ukajiuliza kama Yesu alikuwa ni Mungu katika mwili kwanini aliruhusu watu wamwite yeye mwana wa Mungu? au aruhusu kujulikana kama mwana wa Adamu? Au mwana wa Daudi?.
Bwana Mungu, alipouvaa mwili wa kibinadamu, alijishusha kuwa mdogo sana, sasa mtu hawezi kujishusha na kuwa mdogo na bado atafute kuitwa mkubwa, bila shaka atakuwa ni mnafki. Ndio maana aliwaambia wanafunzi wake, mimi mnaniita Bwana na ndivyo nilivyo lakini sikuja kutumikiwa bali kutumika, na akawaambia mtu akitaka kuwa mkubwa kuliko wote basi awe mtumishi wa wote, hivyo yeye alikuwa kielelezo namba moja cha maneno hayo,
Ili kuelewa vizuri hebu jaribu kutafakari mfano huu, kulikuwa na tajiri mmoja mwenye mali nyingi sana, na mwenye makampuni mengi na wafanya kazi wengi sana, na wengi wa wafanyakazi wake walikuwa hata hawamjui kwa sura kutokana na ukuu wake, wengi walikuwa wanamsikia tu, lakini yule tajiri akaona kuna kasoro Fulani katika moja ya makampuni yake yaliyopo katika moja ya majimbo yake, akasikia kwamba kwenye moja ya hilo kampuni lake, wafanya kazi wananyanyaswa hawalipwi mishahara yao kwa wakati, na kuna ubadhilifu wa fedha mahali Fulani, sasa yule tajiri akaona njia pekee ya kwenda kutafuta suluhisho la hilo tatizo na kujua ukweli wa Mambo sio tu kutuma mawakili wake, bali akaona njia pekee ni kujibadilisha na kutoka kwenye ukurugenzi wake, na kusafiri mpaka kwenye hiyo nchi ambapo kampuni lake lipo na kwenda kujifanya kama nayeye anatafuta ajira ndani ya hilo kampuni, na akishapata naye awe kama mmoja wa watumwa wadogo wa lile kampuni walioajiriwa,..
Sasa kwasababu yeye yupo pale sio kwa kutafuta ukubwa bali kwa kutafuta chanzo cha tatizo, hivyo hawezi kuanza kujitangaza kwamba yeye ndiye Mmiliki wa lile kampuni, hapana bali atafanya mambo yake kwa siri siri, atajifanya mtumwa, na zaidi ya yote, atazitii zile sheria ambazo yeye ndiye aliyezipitisha katika enzi zake, kama vile sio yeye aliyezipitisha, atakipa heshima kile cheo cha mkuu wa makampuni kama vile sio chake, mpaka utakapofika wakati wa yeye kuondoka labda ndio atawaambia moja wa wafanyakazi wake kwamba YEYE NDIYE MKUU WA MAKAMPUNI YALE. Hapo ni baada ya kile alichokuwa anakitafuta kukipata.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu Kristo, yeye alikuwa ni Mungu katika mwili, isipokuwa katika SIRI asingeweza kujiita Mungu kwa namna yeyote ile, alikubali kuitwa mnazareti, alikubali kuitwa mwana wa Mungu, alikubali kuitwa mwana wa Yusufu, alikubali kuitwa mwana wa Daudi , n.k ingawa yeye hakuwa mwana wa Yusufu wala mwana wa Daudi.. kwasababu yeye mwenyewe mahali Fulani aliwauliza mafarisayo…
Mathayo 22:41 “Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema, 44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako? 45 Basi, DAUDI AKIMWITA BWANA, AMEKUWAJE NI MWANAWE? 46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.”
Mathayo 22:41 “Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?
42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,
44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?
45 Basi, DAUDI AKIMWITA BWANA, AMEKUWAJE NI MWANAWE?
46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.”
Unaona hapo Bwana anawauliza mafarisayo kama yeye ni mwana wa Daudi, inakuwaje tena Daudi anamwita Kristo Bwana? Kwahiyo unaweza ukaona Bwana Yesu Kristo, kujidhihirisha kama mwanadamu, au kama mwana wa Mungu, au kama mwana wa Yusufu haimaanishi kwamba yeye ni mwanadamu au yeye ni mtoto kweli wa Daudi au yeye ni mtoto kweli wa Yusufu, au yeye ni wa ulimwengu huu.
Hivyo Baada ya Mungu kumaliza kazi ya upatanisho kwa njia ya msalaba pale Kalvari, alirudi katika enzi yake kama Mungu Mkuu, lakini akaituma Roho yake kama Roho Mtakatifu, ambaye ndio yeye mwenyewe lakini katika mfumo wa Roho, kwa namna ya kawaida huwezi kumtenganisha Mtu na Roho yake, mahali mtu alipo ndipo na Roho yake ilipo, huwezi ukasema mtu na Roho ni vitu viwili tofauti hapana ni kitu kimoja, na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, ni yeye yule aliyekuwa kama Baba mbinguni, kisha akajidhihirisha kama mwana duniani, na sasa yupo pamoja nasi kama Roho Mtakatifu.
Na jina lake ni lake ni YESU KRISTO (YAANI YEHOVA-MWOKOZI). Ana nafsi moja tu, Na hatujapewa jina lingine litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina lake YESU KRISTO, kwa jina hilo tunapata msamaha wa dhambi, na kufunguliwa vifungo vyetu, kwa jina hilo tunabatiziwa, kwa jina hilo tunatolea pepo, kwa jina hilo la Yesu tunatenda mambo yote ya mwilini na rohoni. Na wala hapana wokovu kwa mwingine yoyote isipokuwa kwa Mungu wetu (YESU KRISTO, MUNGU MKUU BWANA WA UTUKUFU).
Kwahiyo Mtu akimkataa Yesu Kristo, amemkataa Mungu mwenyewe, mtu akimpinga Yesu Kristo amempinga Mungu mwenyewe.
Kaka/Dada leo hii umefahamu kuwa Yesu ndiye Mungu, mtazamo wako juu yake upoje? Yeye ndiye atakayeketi katika kiti chake cha enzi na kuhukumu mataifa yote. Jifunze sana kumjua huyu kwasababu yeye ndio Njia pekee ya kuufikia uzima wa milele sio kuwa na dini wala dhehebu au kujiunga na mojawapo ya hayo, njia pekee ya kuupata uzima wa milele ni kumwamini yeye na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi na maisha ya kale, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake hilo “Yesu Kristo” kulingana na ( Matendo 2:38. Mdo 8:16, mdo 19:5 na Mdo 10:45) Na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu. Ni maombi yangu kwamba Bwana atakukirimia neema yake kuyapata hayo na kuzidi kumfahamu sana yeye..
Waefeso 4: 13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”.
Waefeso 4: 13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”.
Ubarikiwe!
Tafadhali “share ” ujumbe huu kwa wengine.
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TUZIJARIBU HIZI ROHO.
MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.
ITAMBUE KARAMA YA MUNGU.
UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?
JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?
JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?
Rudi Nyumbani
Print this post
Mtu anapozaliwa mara ya pili, siku hiyo hiyo anafanyika kuwa kiumbe kipya, na mtu aliyezaliwa mara ya pili ni lazima awe ametubu dhambi zake kwanza kwa kumaanisha kuziacha kabisa, kisha akabatizwe kwa maji na kwa Roho. (Yohana 3:1-5), Ndipo awe na uhakika kuwa amezaliwa mara ya pili na kafanyika kiumbe kipya.
Lakini hiyo peke yake haitoshi kukupa uhakika huo kwasababu biblia pia inasema katika Yakobo 2:17 “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake…haizai”
Hii ikiwa na maana kuwa siku ile unapofanyika kuwa kiumbe kipya ni lazima matendo yaambatanayo na huko kuwa kiumbe kipya yajidhihirishe ndani yako.
Wapo watu wanaodhani mioyoni mwao kuwa siku ile walipotubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi ilitosha wao kukubaliwa na Mungu na huku wakiendelea kuishi katika maisha yao ya kale. Kumbuka ndugu nyakati hizi za mwisho biblia ilishatabiri kutakuwa na makundi mawili ya waaminio, Ukisoma katika Mathayo 25 utaona habari ya wale wanawali 10, ambao wote walikuwa kweli ni mabikra, na wote walikuwa wanamngojea Bwana arusi aje kuwachukua waende pamoja Arusini, lakini tofuati yao ilikuwa ni kwamba watano walikuwa ni werevu na watano wao walikuwa wapumbavu.
Wale warevu walibeba mafuta ya ziada katika katika vyombo vya pembeni pamoja na taa zao, lakini wale wapumbavu hawakubeba mafuta ya ziada isipokuwa yale tu yaliyokuwa katika taa zao. Na Bwana arusi alipokuja usiku wa manane wale wapumbavu taa zao zilikuwa zinakaribia kuzima, hivyo ikiwalazimu waende kutafuta mafuta ili waweze kwenda kumlaki Bwana arusi, lakini waliporudi wakakuta wenzao wameshaingia karamuni na mlango umefungwa.
Mfano huo unaonyesha aina mbili za wakristo watakaokuwepo katika siku hizi za mwisho, angali sisi sote tukifahamu kuwa unyakuo upo karibuni kutokea siku yoyote, lakini ni wazi kuwa wapo watakaoenda na Bwana na wapo watakaoachwa. Kumbuka hapo wote ni wakristo [wanawali] wote walizaliwa mara ya pili, lakini wapo waliodumisha mafuta ya Roho mtakatifu ndani yao na wapo ambao waliyazimisha.. Na hawa walioyazimisha ndio watakaoachwa na watakaopitia dhiki kuu ya mpinga-Kristo siku ile ikifika.
Mtu unapokuwa kiumbe KIPYA. Ni lazima uwe MPYA kweli kweli kama neno lenyewe linavyosema KIUMBE KIPYA. Kuanzia huo wakati ulipotubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la YESU KRISTO na kupokea Roho Mtakatifu wa Mungu ndani yako, safari ndio inaanza na sio imeisha.
kuanzia huo wakati ni kuanza maisha yako UPYA tena, yaani kuyasahau (kuyaaga) mambo yote ya nyuma uliyokuwa unayafanya na kuyatenda na kumwishia Kristo siku za maisha yako yaliyobaka hapa duniani, ulikuwa ni mwasherati ulikuwa ni mtukanaji, ulikuwa ni mwizi, ulikuwa unakwenda disco, ulikuwa unatazama Pornography, ulikuwa unafanya mustarbation, ulikuwa unasengenya, ulikuwa ni mla rushwa, ulikuwa ni mshirikina, ulikuwa ni mvaaji vimini na suruali, ulikuwa ni mtembeaji uchi, ulikuwa ni mwabudu sanamu, ulikuwa unasikiliza miziki ya kidunia, n.k.. Kuanzia huo wakati na kuendelea ni kuyasahau na kukaa nayo mbali, sasa hiyo ndiyo dalili itakayokuthibitisha kuwa kweli wewe umefanyika kiumbe kipya.
Lazima ufikie hatua inayokuonyesha kuwa jana yako ni tofuati na leo yako.
Neno la Mungu linasema
2Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; YA KALE YAMEPITA TAZAMA! YAMEKUWA MAPYA.
Unaona hapo je! ya kale yako yamepita? Mtume Paulo kabla ya kuokolewa kwake alikuwa ni mwuaji, mtukanaji, mpinga-kristo,n.k. lakini baada ya kuzaliwa mara ya pili na kufanyika kiumbe kipya alisema maneno haya..
Wafilipi 3:11 “ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ILA NATENDA NENO MOJA TU; NIKIYASAHAU YALIYO NYUMA, NIKIYACHUCHUMILIA YALIYO MBELE; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.
Wafilipi 3:11 “ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ILA NATENDA NENO MOJA TU; NIKIYASAHAU YALIYO NYUMA, NIKIYACHUCHUMILIA YALIYO MBELE;
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.
Unaona Imani ni lazima iambatane na matendo yake, unasema umekuwa kiumbe KIPYA je! Yale ya kale bado yapo ndani yako? Huo upya ulio nafsini mwako upo wapi Kama bado kuupenda ulimwengu kuko ndani yako?. Bwana YESU akirudi leo kulichukua kanisa lake, kuwachukua wale wanawali werevu na wewe utakuwa mmoja wapo?.
Utajisikiaje siku hiyo, utakapoona umeachwa na mkristo mwenzako uliyekuwa unamwona kila siku ambaye yeye alijikana nafsi yake ameenda na Bwana katika utukufu milele na wewe umebakia hapa chini?. Ni hali mbaya sana ambayo hakuna mtu yeyote atatamani aipitie.
Lile neno linalosema kutakuwa na kilio na kusaga meno, halitakuwa kwa mtu asiyemjua Kristo, hapana yao itakuja huko baadaye, lakini zaidi litakuwa kwa Yule mkristo aliyejidhania kuwa angekwenda kwenye unyakuo lakini badala yake ameachwa.
Na alibaki kwasababu gani?. Ni kwasababu hajakamilishwa katika wokovu wake, aliiishi mguu mmoja nje, mwingine ndani, leo wa Mungu kesho wa ulimwengu huu, Anasema amezaliwa mara ya pili lakini bado hataki kuacha baadhi ya mambo ya kidunia,Ni heri kuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu biblia inasema hivyo.
Kama yanavyosema maandiko: Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna. Ni maombi yangu sisi sote (mimi na wewe) tusiwe katika hilo kundi kubwa la wanawali wapumbavu ambalo limeenea katika ukristo wa sasa. Badala yake tuwe miongoni wa wale wanawali werevu, tukiwa na mafuta ya ziada katika chupa chetu ili taa zetu zisizime wakati wowote hata Bwana ajapo.
Tufanyike viumbe vipya kweli kweli kila siku, yale tuliyoyaacha baada ya kutubu na kubatizwe tusitamani yaingie akilini mwetu hata kidogo. Tuishindanie Imani tuliyopewa mara moja tu na Bwana wetu, Tuishindanie hiyo hata ajapo. Naye atatupa TAJI YA UZIMA.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.”
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.”
DUNIA INAPITA NA MAMBO YAKE.
AMEN.
Tafadhali sambaza ujumbe huu wa Mungu kwa ndugu zako nao wapone, na Bwana atakubariki.
VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI
MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.
MNARA WA BABELI
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “HERI WALIOTASA, NA MATUMBO YASIYOZAA, NA MAZIWA YASIYONYONYESHA”?
NIFANYAJE ILI NI NIJUE KUWA UAMUZI NINAOUFANYA NI MAPENZI YA MUNGU?
Yohana 15.1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 KILA TAWI NDANI YANGU LISILOZAA HULIONDOA; NA KILA TAWI LIZAALO HULISAFISHA, ILI LIZIDI KUZAA 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu,”.
Yohana 15.1 “Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
2 KILA TAWI NDANI YANGU LISILOZAA HULIONDOA; NA KILA TAWI LIZAALO HULISAFISHA, ILI LIZIDI KUZAA
3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu,”.
Kama wewe ni mkulima, au kama ulishawahi kujihusisha na shughuli yeyote ya kilimo, unaweza ukaelewa kwa undani uhusiano uliopo kati ya shina, matawi na matunda, utagundua kwamba mti hauwezi kuzaa matunda pasipokuwepo na shina, na kama shina halina matawi basi pia haliwezi kuzaa matunda. Kwahiyo ili matunda yawepo ni lazima liwepo shina pamoja na matawi.
Biblia inasema Bwana wetu Yesu Kristo ni mzabibu (shina), na Baba yake ndiye mkulima, na sisi ndio watu wake ndio matawi, kila tawi lisilozaa huliondoa na kila tawi lizaalo hulisafisha ili lizidi kuzaa.
Sentensi hii inaonyesha wazi kabisa huyu mkulima, yupo kwaajili ya kutafuta faida, yaani kupata matunda, utagundua kuwa sio mkulima wa kupanda tu na kuondoka bali utagundua ni mkulima ambaye yupo kimaslahi zaidi, na anafanya juu chini kuhakikisha anapata anachokitafuta.
Sasa ili kupata anachokitafuta ndio hapo tunaona anauchunguza mti wake siku baada ya siku kutafuta matawi yanayozaa ili aendelee kuyasafisha na yale yasiyozaa ayaondoe, na utaona hashughuliki na shina (yaani Yesu Kristo) bali utaona anashughulika na matawi (yaani wafuasi wa Yesu Kristo).
Sasa kama wewe ni mkulima utagundua kuwa ili kuufanya mti usiendelee kuwa mrefu kwenda juu huwa wanakata lile tawi la juu kabisa linalokua kwenda juu, na matokeo yake ni kwamba ule mti utaendelea kutanuka badala ya kuendelea kwenda juu, vivyo hivyo watu wakitaka mti uzidi kuwa mrefu kwenda juu, huwa wanaondoa yale matawi ya pembeni, na matokeo yake ule mti utaendelea kwenda juu sana lakini hautataanuka.
Kwanini wanafanya hivyo?..Ni kwasababu endapo yale matawi ya pembeni yakiachwa na kuendelea kuwepo ule mti hautaendelea kukua kwenda juu kwasababu nguvu yote au chakula chote cha ule mti kitaenda kwenye yale matawi yaliyopo pembeni na hivyo kudhoofisha ukuaji wa matawi ya juu, na vivyo hivyo kama wanataka mti upanuke kwa mapana, wanapaswa waondoe matawi ya juu ili chakula chote kisiende kwenye yale matawi yaliyopo juu na badala yake kiende kwenye yale matawi ya pembeni ili utanuke kwa kasi.
Kadhalika wakulima wa mazao ya biashara kama kahawa wanaelewa kwamba, wakitaka mmea kama mti wa kahawa uzae sana, huwa wanakwenda kukata kile kikonyo cha juu kabisa cha mti wa mkahawa, ili usiendelee kwenda juu, na pia wanaondoa yale matawi madogo madogo ambayo yameota kwenye shina, ambayo hayazai, na kuacha yale matawi yenye matunda tu, na lengo la wao kufanya hivyo sio kwasababu hawapendi ule mkahawa uwe na matawi mengi, hapana! Bali wanajua endapo wakiyaacha yale matawi madogo yasiyozaa yaendelee kuwepo basi kuna hatari ya kuvuna kahawa chache kwasababu nguvu yote ya chakula badala iende kwenye yale matawi yanayozaa, inaishia kwenda kwenye yale matawi madogo madogo yasiyozaa, hivyo kusababisha matunda hafifu kutoka kwenye yale matawi makubwa yanayozaa. Hivyo utamkuta mkulima amekata matawi yote madogo madogo kama ni 20 au mia na kubakiwa tu na matawi matano au kumi makubwa yanayozaa.
Sasa hiyo hatua yote ya kupunguza matawi yasiyozaa ndiyo inayoitwa KUUSAFISHA MTI. Unaweza kutazama mfano wa picha chini.
Sasa tukirudi kwenye ule mfano Bwana Yesu aliosema kwamba kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa na lile lizaalo hulisafisha alikuwa ana maana kuwa, Kila mtu aliyekuwa ndani yake yeye asiyeonyesha dalili yote ya kuzaa matunda, Baba yake atamwondoa na sababu ya kumwondoa sio kwasababu anamchukia au hapendi awepo ndani ya Yesu Kristo, hapana! Sababu pekee ya kumwondoa ni kwasababu ile nguvu au kile chakula ambacho kinatumika kwa mtu asiyezaa matunda kingeweza kutumika kwa mtu anayezaa matunda ili azae mengi zaidi na zaidi. Na ndio maana mahali pengine Bwana Yesu alisema..
Mathayo 25.29 “Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa”.
Nilikutana na ndugu mmoja mwislamu wakati Fulani, nikamwambia Bwana Yesu alisema kuwa mwenye kitu atapewa lakini asiye na kitu atanyang’anywa hata kile alicho nacho, Yule ndugu alihuzunika sana kusikia ile sentensi, alisema kwanini iwe hivyo, sio vizuri? Ina maana kwamba Yesu hana upendo kwanini amnyang’anye Yule asiyekuwa nacho hata kile kidogo alichokuwa nacho?. Nikajaribu kumweleza kuwa Bwana Yesu hazungumzii mambo haya ya mwilini bali ya rohoni lakini bado alihuzunika. hivyo ndivyo ilivyo kwamba Bwana yupo kwa ajili ya faida, anachotaka kutoka kwetu ni matunda, sio nyuso zetu!! Na tutakuja kuyaona hayo matunda ni yapi muda mfupi baadaye.
Kwahiyo utaona kuwa, kuna hatari kubwa sana ya kutokuzaa matunda, hatari hiyo ni kwamba ile Neema na Baraka za Mungu juu yako za kumzalia Mungu matunda zinaondolewa kwako na kupewa mtu mwingine anayezaa, ndio hapo utakuta mwanzoni ulikuwa una hamu sana ya kumtafuta Mungu ghafla ile hamu inakufa, anaenda kuongezewa Yule mtu ambaye alikuwa anaonyesha bidii kidogo, anaongezewa nguvu mara mbili zaidi ya kumtafuta Mungu, utaanza kuona ile nguvu ya kuomba ambayo ilikuwa ndani yako ulikuwa una uwezo wa kuomba hata nusu saa, ghafla unajikuta hamu yote ya kuomba imekufa unaacha anaenda kuongezewa Yule ambaye kwa unyoofu wa moyo kila siku anajitahidi angalau aombe nusu saa, anaongezewa nguvu anaanza kuomba lisaa, masaa au hata mkesha, ukiona umepoa ghafla fahamu tu kuwa umeondolewa kutoka katika lile shina, au upo hatarini kuondolewa.
Sasa ni Matunda yapi Bwana anayoyahitaji kutoka kwenye mashina (yaani mimi na wewe)?
Matunda ambayo Bwana anayahitaji yanatoka katika kitabu cha
Wagalatia 5:22 “Lakini TUNDA LA ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
Wagalatia 5:22 “Lakini TUNDA LA ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
Unaona hayo ndio matunda Bwana anayoyahitaji kutoka kwetu, anategemea katika kipindi chote tunachokaa ndani yake yeye kama mzabibu mkuu, anategemea kutuona tunazaa, upendo ndani yetu, tunazaa fadhili, tunazaa utu wema, tunazaa upole, tunazaa kuwa na kiasi na uvumilivu, tunazaa amani..hata baadaye tuwahubirie wengine habari njema za wokovu.
Lakini atakapokuja na kutukuta hatuzai hayo matunda ya haki badala yake tunazaa, kutokusamehe, tunazaa wivu, tunazaa uasherati, tunazaa matusi, tunazaa kutokujiheshimu, tunazaa kiburi, tunazaa kuupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu, na bado tunasema sisi ni wakristo tupo ndani yake, bado tunasema sisi ni matawi yake, nataka nikwambie ndugu Kristo hana matawi ya namna hiyo, hii Neema iliyopo na wewe leo inayokulilia ugeuke utubu ili uzae matunda ya haki, itaondolewa kwako na kupewa watu wengine waliostahili. Ndivyo biblia inavyosema..
Mathayo 3.8 “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa PENYE MASHINA YA MITI; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”
Mathayo 3.8 “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa PENYE MASHINA YA MITI; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”
Na pia inasema “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO; Waebrani 12:14”
Itii sauti ya Roho wa Mungu leo inayokuambia utubu uache dhambi zako na umgeukie Muumba wako leo kwa moyo wako wote! Itafika wakati hutaisikia tena ndani yako,siku hiyo injili kwako itakuwa ni kama upuuzi tu!.. Hujawahi kukutana na mtu hata umwelezeje hataki kusikiliza injili?? itii sauti ya Mungu inayokuambia leo, uache uasherati!, Uache uvaaji mbaya kama wanawake wa ulimwengu huu wasiomjua Mungu, uache sigara na pombe!, uache usengenyaji Mtii Mungu leo, kisije hicho kidogo alichowekeza ndani yako akakiondoa na kumpa mwingine, acha kudanganyika kwamba utatubu tu siku moja!! Hakuna kitu kama hicho hiyo ni sauti ya shetani mwenyewe ikizungumza ndani yako. Na acha kuamini injili za kwamba Mungu ni upendo tu! Mungu ni upendo tu! Hawezi kutufanya chochote…Yeye mwenyewe kasema mara kadhaa na sio sehemu moja kwamba “yeye asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho atanyang’anywa” ikiwa na maana kwamba hatakuachia hata hicho kimoja ulicho nacho..
Mathayo 25: 28 “BASI, MNYANG’ANYENI TALANTA HIYO, MPENI YULE ALIYE NAZO TALANTA KUMI. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa”.
Mathayo 25: 28 “BASI, MNYANG’ANYENI TALANTA HIYO, MPENI YULE ALIYE NAZO TALANTA KUMI.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa”.
Je! Sentensi hiyo haikuogopeshi?? Tubu leo ukabatizwe upokee kipawa cha Roho Mtakatifu. Ili ufanyike Tawi lizaalo.
Bwana akubariki.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa ndugu zako wengine.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
VIUMBE VINATAZAMIAJE KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU?
NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?
KAINI ALIPATIA WAPI MKE?
Katika kitabu cha mwanzo tunasoma, baada ya Bwana Mungu kuumba mbingu na nchi na viumbe vyote alistarehe siku ya saba, biblia inasema hivyo katika..
Mwanzo 2: 1 “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. 4 HIVYO NDIVYO VIZAZI VYA MBINGU NA NCHI ZILIPOUMBWA. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi”.
Mwanzo 2: 1 “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.
2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
4 HIVYO NDIVYO VIZAZI VYA MBINGU NA NCHI ZILIPOUMBWA. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi”.
Lakini kuna mambo kadhaa ya kujiuliza kuhusu uumbaji wa Mungu, Jambo la kwanza la kujiuliza ni kwanini Mungu hakuumba vitu vyote ndani ya dakika moja? Maana anao huo uwezo na badala yake akachukua siku saba kukamilisha uumbaji wake?
Swali la pili la kujiuliza, Ni hapo aliposema… “HIVYO NDIVYO VIZAZI VYA MBINGU NA NCHI ZILIPOUMBWA” Hivyo vizazi vilivyoumbwa ni vipi?
Na yapo maswali mengine mengi sana ya kujiuliza juu ya kitabu cha mwanzo, lakini leo tuyatazame haya mawili kwa msaada ya Bwana. Kwasababu tukiweza kumwelewa Mungu katika uumbaji wake tutaweza kumwelewa Mungu katika uumbaji wake anaotufanyia sisi kila siku katika maisha yetu, kwasababu Mungu ni yeye yule jana, leo na hata milele hatabadilika. Njia alizozitumia kuumba mwanzo ndizo hizo hizo zinazoendelea leo katika uumbaji na utengenezaji wa maisha yetu.
Ni wazi kuwa Mungu anao uwezo wa kuumba kitu kufumba na kufumbua lakini, tunaona hakuutumia huo uwezo wake katika uumbaji wa Mbingu na nchi pamoja na uumbaji wa wanadamu na viumbe.. Hakuiumba dunia kufumba na kufumbua, bali ilimchukua muda kidogo katika utengenezaji, kwanini alifanya hivyo..kwasababu ndivyo ilivyompendeza.
Kwahiyo tunaweza kujifunza kuwa sio mpango wa Mungu, mambo kuzuka haraka haraka, sio mpango wa Mungu kwamba jambo ameliahidi leo na leo leo litimie kama lilivyo, ingawa huo uwezo anao, lakini hautumii sana na ndio maana tunasoma pale mwanzo baada ya Bwana Mungu kuiumba dunia, hakuiumba pamoja na miti wala bustani siku ile ile bali aliiumba kwanza yenyewe pamoja na mbegu kisha akizinyeshea mvua, ndipo baada ya kipindi Fulani zile mbegu zikaota, zikawa miche midogo ya miti, pengine ilichukua miezi kadhaa kuwa mikubwa, pengine miaka, lakini baada ya kipindi Fulani ndipo ikatokea misitu mikubwa..Lilikuwa ni jambo la pole pole, ingawa Mungu hakushindwa kuiumba dunia ikiwa na misitu tayari kwa dakika moja.
Kadhalika alipoviumba vizazi vya nchi (yaani wanadamu na wanyama) hakutokeza mamilioni ya wanadamu ndani ya siku moja, au mamilioni ya wanyama ndani ya siku moja, bali alimwumba mwanadamu mmoja kama mbegu duniani, akamwekea ndani yake vizazi vyake, vizazi vyote vya wanadamu akaviweka ndani ya mtu mmoja , ili kwamba baada ya muda Fulani labda baada ya miaka 1,000 au 2,000 ndipo wanadamu wawe wameijaza dunia yote.
Kwahiyo unaweza kuona kwamba mpango wa Mungu, wa wanadamu kuijaza dunia yote, ulikuwepo Edeni lakini haukutimia ile ile siku ya kwanza Mungu alipomuumba mwanadamu, hivyo unaweza ukaona jambo ni lile lile kwamba sio mpango wa Mungu kutimiza kusudi lake lote katika ile siku ya kwanza aliyozungumza.
Kadhalika sio mpango wa Mungu, leo tuzaliwe kesho tuwe na watoto, haitawezekana kwasababu nguvu ya Mungu ya uumbaji haiendi kasi hivyo, inapasa kwanza mwanadamu akamilike kwa miaka kadhaa ndipo awe na uwezo wa kupata mtoto.
Na vivyo hivyo, katika maisha yetu, sio mpango wa Mungu leo tukapande mbegu shambani na leo leo tukavune, sio mpango wa Mungu kutupa mali kwa haraka haraka, ingawa anao uwezo wa kufanya hivyo, ila ni mara chache chache sana na kwa watu wachache tena kwa ajili ya utukufu wake, lakini mpango wa Mungu hasa ni kuchuma kidogo kidogo.
Mithali 13: 11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”..
Kwahiyo tukitaka Bwana aumbe jambo jipya katika maisha yetu tunapaswa tuwe watu wenye subira na wavumilivu.
Kadhalika tukitaka Bwana atuponye, sio lazima atuponye siku hiyo hiyo tuliyomwomba, wakati mwingine itachukua muda, wiki, miezi au wakati mwingine hata miaka, lakini mwisho wa siku atatuponya. Mtu akipata jeraha tunajua hawezi kupona siku ile ile, itamchukua wiki, au miezi, au wakati mwingine miaka jeraha lile kupona, na kufunga, na ngozi kurudia kama ilivyokuwa..Sasa ile hatua ya kidonda kupona taratibu taratibu kwa namna ambayo hatuwezi kuona, ndio ile ile nguvu ya uumbaji iliyokuwa pale Edeni, Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi, na ndio hiyo hiyo nguvu inayoponya maisha yetu leo.
Nguvu hii ya uumbaji ipo taratibu sana haiwezi kuonekana kwa macho lakini baada ya kipindi Fulani inaleta matokeo, ndio hiyo hiyo inayolisogeza jua na mwezi, huwezi kuona jua likisogea kwa macho isipokuwa baada ya masaa Fulani ukitazama juu utaona limehama kutoka pale lilipokuwepo kwanza.
Vivyo hivyo huwezi kuona mti ukikua kutoka hatua moja hadi nyingine kwa kuudadisi kwa macho, ukifanya hivyo hutaona chochote, utasubiri na kusubiri pasipo kuona chochote ila mfano ukiondoka na kurudi baada ya siku kadhaa utashtukia tu umeongezeka urefu, hivyo ndivyo nguvu ya Mungu ya uumbaji inavyotenda kazi.
Ndivyo Mungu, anavyotenda kazi hatuwezi kumchunguza kwa akili za kibinadamu, tunachopaswa kufanya ni kumuamini tu, na kisha kuiachia ile nguvu yake ya uumbaji itende kazi, kwa uvumilivu wote pasipo kunung’unika.
Leo Bwana akikuahidia kukuponya unachopaswa kufanya ni kumwamini, usiangalie umekaa na ugonjwa siku ngapi au miezi mingapi au miaka mingapi, usijaribu kumdadisi Mungu jinsi gani anaponya…wewe mwamini tu, na kusubiri, kwa uvumilivu wote, na kushukuru kwasababu ile nguvu yake ya uumbaji inatenda kazi ndani yako kwa namna ambayo wewe huwezi ukajua. Itafika wakati utajikuta tuu, unaanza kuona unafuu kidogo kidogo, na hatimaye kupona kabisa, ukiona umeombewa na bado hali yako bado iko vile vile..sio wakati wa kuhama kanisa hili kwenda lile au mtumishi huyu kwenda yule, sio wakati wa kupanic huku na kule, tulia mahali ulipo mngoje Bwana, kwasababu Bwana anatenda kazi kwa namna usioijua wewe.
Vivyo hivyo na riziki nyingine za ulimwengu huu kama mali, sio za kuzihangaikia huku na huko, kwenda kwenye maombi haya na yale pale unapoona hakuna mabadiliko, tulia mahali ulipo tekeleza wajibu wako Bwana atakupa kidogo kidogo, kwanza yeye alisema “hata tusitie shaka” BWANA Mungu hakuijaza dunia hii watu ndani ya siku moja, ilichukua maelfu ya miaka vivyo hivyo hawezi kukujaza wewe mali nyingi ndani ya siku moja, atakupa kidogo kidogo mpaka utakapojaa kiwango anachokitaka yeye. Ndivyo nguvu yake ya uumbaji inavyotenda kazi.
Na zaidi sana na lililo kuu ni “KUWA MKAMILIFU”…Huwezi kuzaliwa mara ya pili leo na leo leo kuwa mkamilifu kwa kiwango kile Mungu anachotaka, Baada ya kuzaliwa mara ya pili Bwana anatutakasa kidogo kidogo ule uchafu uliopo ndani yetu ambao tulikuwa tunautumikia tulipokuwa kwenye dhambi, anauondoa mpaka tunakuwa wakamilifu kwa viwango vile anavyotaka yeye. Siku baada ya siku tunadumu katika ushirika, fundisho la mitume, kuumega mkate, na kusali ili tukue viwango vya kumzaliwa Mungu matunda.(Matendo 2:42)
Dada/Kaka..Je! umeiruhusu hii nguvu ya Mungu ya uumbaji itende kazi ndani yako leo?..Nguvu ambayo itakutengeneza na kukuumba upya uwe mtakatifu katika vile viwango vya kwenda mbinguni?, biblia inasema waasherati, wazinzi, walevi, waabudu sanamu, watukanaji sehemu yao ni katika lile ziwa la moto, na inasema pia katika “Waebrania 12:14 kwamba hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa Mtakatifu” Je wewe unao? Una uhakika kwamba Kristo akija leo utakwenda mbinguni? Kama huna huo uhakika ni wazi kuwa atakapokuja utaachwa..na kukumbana na dhiki kuu na siku ya Bwana inayowaka kama moto,na maandiko yanasema katika 2 Petro 1:10 kwamba tujitahidi kuufanya imara uteule wetu na wito wetu,..
Ndugu tunaishi katika siku za hatari ambazo Kristo yupo mlangoni kurudi, siku sio nyingi waovu wote wa huu ulimwengu wataomboleza na kujuta watakapojua kwamba Kumbe Kristo alikuwa ni Kweli, na wakati huo watakuwa wameshachelewa, ni maombi yangu usiwe mmoja wao. Tubu leo ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kukamilisha maagizo ya Bwana Yesu Kristo naye Bwana ataanza kuyaumba upya maisha yako, kwa kupitia Roho wake Mtakatifu.
Bwana Yesu akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki.
KISASI NI JUU YA BWANA.
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
SEHEMU ISIYO NA MAJI
MTUME PAULO ALIKUWA ANA MAANA GANI KUSEMA “KWA SABABU HIYO, TUKIACHA KUYANENA MAFUNDISHO YA KWANZA YA KRISTO, TUKAZE MWENDO ILI TUUFIKILIE UTIMILIFU;?
NITAMJUAJE NABII WA UONGO?
Mwanzoni kabla sijaokoka nilidhani ndani ya moyo wangu kuwa Mungu hataweza kunihukumu mimi, nilidhani ndani ya moyo wangu kuwa ijapokuwa ninamuudhi Mungu sasa lakini mwisho wa siku ataniokoa tu, kwasababu mimi sina dhambi nyingi zaidi ukilinganisha na watu kama wauaji, na wachawi, nilidhani kuwa pombe nilizokuwa ninakunywa kwa kiasi sizingeweza kuniletea madhara makubwa kiasi cha kutupwa jehanum kama wale wanaokuwa walevi wa kupindukia, uasherati niliokuwa ninafanya na disco nilizokuwa ninakwenda zisingekuwa ni kosa kubwa sana kunifanya mimi niangamizwe kabisa mfano wa wale wanaoigiza mikanda ya ngono.
Nilidhani kuwa matusi niliyokuwa ninatukana Mungu atayafumbia macho siku ile kwasababu Mungu ni wa rehema atanirehemu, kadhalika usengenyaji niliokuwa ninauzungumza niliona pia ni hali tu ya kibinadamu kwamba kila mtu huwa anafanya hivyo, kila kitu niliona kama si dhambi sana, nusu nusu maadamu mimi simdhulumu mtu, siui, wala siendi kwa waganga, isitoshe mimi ni mkristo na nina dhehebu langu, ninawapa kitu maskini hiyo inatosha,Mungu kunihurumia katika siku ile .
Sikuwa najali sana habari za Mungu, niliona kukaa hapo katikati ni sawa tu niliona kama YESU ni kitu cha ziada katika maisha yangu lakini sio msingi wa maisha yako. Hayo yote yalikuwa ndani ya moyo wangu Mpaka siku Bwana alipokuja kuniokoa kwa neema zake, na kunifungua macho ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa katika hali ya HATARI SANA pasipo kujijua.
Biblia ipo wazi kabisa inasema;
Mithali 14: 12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Ni wazi kila mtu ndani ya nafsi yake ataona kuwa kile anachokifanya au anachokiamini kuwa ni sawa hata kama watu wengine watakiona vipi, mwingine ataona kuwa kushika amri kumi tu za Mungu inatosha, hakuna haja ya kumjua Kristo YESU, mwingine ataona kunywa pombe huku upo kwenye dini yako ni sawa tu!. Mungu atasema Mungu haangalii nje anaangalia vya ndani hivyo kuvaa vimini, na suruali kwa mwanamke wa kikristo sio tabu, Mwingine atasema mimi naamini hakuna ziwa la moto bali tukifa tunapotea tu, mwingine atasema tukifa tunakwenda kwanza toharani kisha mbinguni baadaye, mwingine atasema kusaidia tu yatima na wajane na kuishi maisha ya kujitunza hiyo inatosha kukupeleka mbinguni. Mwingine atasema mambo ya Mungu yametungwa hakuna kitu kama hicho fanya biashara tengeneza pesa enjoy maisha siku ukifa umepotea hakuna maisha baada ya kifo..n.k. Kila mtu akiwa na mawazo yake mwenyewe moyoni akijitumainisha kuwa ni sawa..Biblia inaendelea kusema.
Yeremia 17: 9 “MOYO HUWA MDANGANYIFU KULIKO VITU VYOTE, UNA UGONJWA WA KUFISHA; NANI AWEZAYE KUUJUA? 10 Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.”
Yeremia 17: 9 “MOYO HUWA MDANGANYIFU KULIKO VITU VYOTE, UNA UGONJWA WA KUFISHA; NANI AWEZAYE KUUJUA?
10 Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.”
Unaona hapo, shetani ni mdanganyifu, lakini MOYO wako ni mdanganyifu zaidi ya shetani. Kwasababu shetani naye hakuwa na mtu wa kumdanganya kabla yake bali moyo wake ndio uliomdanganya, vivyo hivyo na wewe pia kinachokudanganya kwanza ni moyo wako kisha baadaye shetani atakusaidia kufanya hivyo. Na ndio maana biblia inazidi kusisitiza na kusema katika Mithali 4: 23 LINDA MOYO WAKO KULIKO YOTE UYALINDAYO; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Kaka/Dada haijalishi ni kitu gani unachokiamini kuwa ni sawa, haijalishi unajiona upo katika njia iliyonyooka kiasi gani, haijalishi ni sifa gani umeipata mbele za watu kwa matendo yako mema na ya kiasi, lakini Neno la Mungu na kanuni za Mungu zitabakia kuwa pale pale, Biblia inasema katika,
Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, MIMI NDIMI NJIA, NA KWELI, NA UZIMA; MTU HAJI KWA BABA, ILA KWA NJIA YA MIMI.
Usidhani kuwa dini inatosha, yupo aliyekuwa mtu wa dini na kushika amri zote lakini hakuwa na uzima ndani yake unaotoka kwa YESU KRISTO peke yake. Tunamsoma huyo katika
Mathayo 19: 16 “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ILI NIPATE UZIMA WA MILELE? 17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. 18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? 21 Yesu akamwambia, UKITAKA KUWA MKAMILIFU, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; KISHA NJOO UNIFUATE. 22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. 23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Mathayo 19: 16 “Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ILI NIPATE UZIMA WA MILELE?
17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,
19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?
21 Yesu akamwambia, UKITAKA KUWA MKAMILIFU, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; KISHA NJOO UNIFUATE.
22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
23 Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.
24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Kadhalika aliwaambia mafarisayo na masadukayo wale washika dini maneno haya:
Yohana 8:24 “kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.”
Unaona hapo? Usikubali kuuruhusu moyo wako kukudanganya kuwa YESU hana umuhimu sana katika maisha yako, usiruhusu kuona njia zako kuwa ni sawa mbele za Mungu na huku bado haujasafishwa dhambi zako katika damu ya YESU KRISTO. Leo hii unaweza ukawa na ujasiri mwingi na kiburi kingi cha kujiona hivyo, lakini ngoja siku utakayokaribia kufa hapo ndipo utajiona kuwa wewe si kitu, unahitaji uzima ndani yako na wakati huo utakuwa umeshachelewa.
Ni maombi yangu usitumainie akili zako kukuongoza popote katika njia za uzima, usitumainie nguvu zako, usitumainie elimu yako, usitumainie matendo yako, usitumainie uzuri wako, usimtumainie mwanadamu, usitumainie kile unachoamini bali tumainia kile Mungu anachosema kuwa kitakuokoa hiyo ndio salama yako ndugu. Siku ile kutakuwa na majuto makubwa sana pindi utakapogundua moyo wako ulikudanganya, kuupinga wokovu unaopatikana katika YESU KRISTO peke yake.
Huu ni wakati wa kubadili mwelekeo wa njia zako, na kukubali kuitii INJILI, Bwana Yesu anasema
Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Unaona hapo wote walio nje ya neema wapo katika giza, na wewe usitie moyo wako ugumu ukaipinga hiyo sauti inayokuita UOKOKE, kwasababu hiyo ni sauti ya neema ili umwendee akupe uzima wa milele, sio wote watakoikubali isipokuwa wale waliochaguliwa na Mungu tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu. Leo hii uwe nawe mmojawapo kwa kuitii, Inawezekana ulisharudi nyuma, au haukutambua umuhimu wa YESU maishani mwako, leo anza upya.
Mithali 28: 13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Tubu sasa kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako mbele zake YESU KRISTO, Kisha baada ya kufanya hivyo hatua inayofuata upaswa ukabatizwe katika UBATIZO SAHIHI kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Kumbuka wale wote walio nje ya Kristo hawana ondoleo la dhambi zao, hata iweje. Hivyo ili kuukamilisha wokovu wako unapaswa ukabatizwe kwa maji mengi na uwe ni kwa jina la YESU KRISTO, kama ulibatizwa ubatizo mwingine nje ya hapo pasipo kujua ni batili unapaswa ukabatizwe tena, kisha Bwana mwenyewe atakupa Roho wake mtakatifu kuanzia huo wakati na kuendelea atakayekupa uwezo wa kushinda dhambi. Na hapo utakuwa umeuokolewa mwenye tumaini la uzima wa milele. Kisha Damu ya YESU Kristo ndipo itaanza kunena mema juu ya maisha yako.
Hizi ni siku za mwisho YESU KRISTO yupo mlangoni kurudi, usiruhusu njia za udanganyifu wa mali zikakusonga usiufuate uzima ulio kwa BWANA YESU.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
Ukiwa umetubu na unautahitaji wa kubatizwa, unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi 0789001312.
NJIA YA MSALABA
NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?
JE! NI DHAMBI KWA MKRISTO KWENDA HOSPITALI AU KUTUMIA MITI SHAMBA ANAPOUGUA?
NINI MAANA YA MTU AKIJA KWANGU NAYE HAMCHUKII BABA YAKE HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU?
KUNGOJA maana yake ni kukaa katika hali ile ile huku ukisubiria kitu ulichokuwa unakitarajia kifike mara, na tunajua kwa namna ya kibinadamu, kungojea kitu Fulani kwa muda mrefu huwa kunachosha, kwamfano leo mtu akitumia saa moja kwenye kufanya shughuli fulani labda tuseme kupika au kufua, na akitumia saa hilo hilo moja katika kumngojea rafiki yake kituoni kwa namna ya kawaida yule mtu ataona ule muda aliotumia kumgojea rafiki yake kituoni umekuwa mrefu zaidi kuliko ule muda ambao alikuwa anapika. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu alipokuwa kituoni, hakuwa anajishughulisha na jambo lingine lolote isipokuwa kumtarajia rafiki yake tu. Muda wake mwingi haukupotea katika migawanyo ya shughuli nyingi bali katika jambo moja tu, hivyo muda ukaonekana kuwa mrefu zaidi.
Kadhalika sisi tunapokuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa mara ya pili [yaani kwa kubatizwa kwa maji na kwa Roho] Mungu analigeuza tumaini letu na tegemeo letu lote kuanzia huo wakati na kuendelea tunakuwa tunamtazamia yeye.
Biblia inasema Luka 12.36 ”nanyi IWENI KAMA WATU WANAOMNGOJEA BWANA WAO, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara”.
Hivyo kukaa huku katika hali ya kungojea kutaingia ndani ya kila mkristo halisi aliyezaliwa mara ya pili, tumaini lake likiwa ni kukamilishwa kwanza hapa duniani, pili akamilishwe katika siku ya UNYAKUO. Hivyo hatuna budi kungojea kwa saburi nyingi na kujizuia na mambo mengi. Lakini biblia inasema katika.
Isaya 40: 29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 BALI WAO WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA; WATAPANDA JUU KWA MBAWA KAMA TAI; WATAPIGA MBIO, WALA HAWATACHOKA; WATAKWENDA KWA MIGUU, WALA HAWATAZIMIA”.
Isaya 40: 29 “Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31 BALI WAO WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA; WATAPANDA JUU KWA MBAWA KAMA TAI; WATAPIGA MBIO, WALA HAWATACHOKA; WATAKWENDA KWA MIGUU, WALA HAWATAZIMIA”.
Unaona hapo, wote watumainio nguvu zao ziwasaidie katika maisha yao, watumainiao mambo yao wenyewe yawafikishe katika malengo yao, wote wanaodharau rehema za Bwana,na wokovu wake, wanaosema tangu umekuwa mkristo umepata faida gani, wote wanaosema huyo YESU mnayemngojea yupo wapi? Angalia sisi tumeshapiga hatua kubwa tuna hiki na kile, tuna maendeleo na mafanikio lakini ninyi mnaomtaja YESU mbona haji huo wokovu mnaousubiria miaka 2000 upo wapi? Huo utawala wa YESU mnaousubiria upo wapi? Huyo Yesu ameshakufa, na miaka hiyo yote hajawafaidia kitu.
Unaona hao wote wanaosema hivyo biblia inasema wao watachoka, watazimia na kuanguka, japo watajifariji kwa nguvu zao za sasa lakini ni kwa kitambo tu ipo siku watachoka tu, siku moja wataona na wengine walishaona tayari kwamba vitu wanavyovitumaini siku zote haviwapi uzima wa milele, wanaanza kuona mbona hivi vitu tulivyoviwekea matumaini na kuvitaabikia na kuvingojea havitupi furaha ya kudumu?, Biblia inasema watazimia wote bali wale WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA, watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Haleluya.
Hatushangai kuona Ulimwengu ulishangaa kipindi cha mitume na bado utaendelea kushangaa wakati wa sasa ni kwanini hawa watu hawakati tamaa kwa hicho wanachokingojea?. Hawajui Ni kwasababu sio kwa uweza wao wapo vile, bali ni kwasababu ya NGUVU wanazozipata kutoka kwa yeye WANAYEMNGOJEA.
Lakini mtu anayemngojea Bwana ni mtu wa namna gani? Ni mtu yule aliyeweka tumaini lake lote kwa Mungu, na kama vile tunavyosema kungojea ni kusubiria kwa uvumilivu na kusubiria huko kunakugharimu kuacha kufanya shughuli nyingine na kukitazama hicho kitu, vivyo hivyo na mtu yule anayesema anamngojea Mungu ni yule aliyejitenga na ulimwengu, aliyeamua kutokumchanganya Mungu na dunia, aliyesema tangu sasa, ulevi basi, zinaa basi, fashion basi, uchawi basi, wizi basi, usengenyaji basi, pornography basi, kampani mbovu basi, aliyesema tangu sasa namwishia Mungu katika mwenendo wangu wote, tangu sasa nautafuta utakatifu na weupe wa moyo, tangu sasa naanza mwanzo mpya na Bwana..Sasa watu kama hawa biblia inasema japo dunia itaona kama hiyo njia ya kujizuia na mambo yao ni ngumu, lakini Mungu yeye mwenyewe ndiye atakaye wapa NGUVU mpya ya kupaa juu, Mungu atawapa nguvu ya kuendelea kuishi maisha ya kujitakasa kila siku. Utakatifu kwao hautakuwa mgumu kuutimiza japo watu wa nje wataona inawezekanaje kanaje kwao wao kuishi vile?.
Na itaendelea vivyo hivyo mpaka siku ile ya kuipokea ahadi yake hapa duniani na katika siku ile ya UNYAKUO.
Pale Mungu atakapomnyeshea mvua zote mbili, yaani mvua ya masika na mvua ya vuli
Ni kwa nini Bwana anataka sisi tumngojee? Je! ni kwa lengo la kututesa?. Jibu ni hapana. Bali ameruhusu tukipitie hicho kipindi ili kututengeneza sisi, tuweze kuzimudu wingi wa hizo Baraka na hizo AHADI alizoziweka mbele yetu.
Zaburi 37: 9 Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi.
Bwana alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, hakuwafikisha moja kwa moja katika nchi ya AHADI, badala yake aliwapitisha kwanza nyikani katika kipindi cha kumngojea yeye kwa muda wa miaka 40, kuwapa sheria itakayowasaidia kuitawala ile nchi ili iwazalie wenyewe. Jaribu kufikiri kama moja kwa moja baada ya kutoka Misri wangeingia kaanani ni kitu gani kingetokea?. Ni wazi kuwa wangeingia na miungu waliyotoka nayo Misri katika nchi takatifu, wangekuwa na tabia zao za uuaji, uchawi, visasi nk.. katika nchi ambayo Mungu ameibariki wao wangeifanya kuwa laana. Lakini iliwapasa wapitie kipindi Fulani cha kumngojea Mungu ili siku watakapofika waingie na kanuni za kuwasaidia kuishi mule.
Lakini tunasoma wengi wao hawakuwa wavumilivu kumngojea Mungu, wakaanza kurudia mambo ya Misri ambayo walishayaacha zamani, wakaona mbona nchi yenyewe ipo karibu lakini miaka hii yote hatuifikii, hivyo wakakata tamaa na kuasi kama tunavyosoma. katika
Zaburi 10: 7 Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu. 8 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu. 9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda. 10 Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, Na kuwakomboa na mkono wa adui zao. 11 Maji yakawafunika watesi wao, Hakusalia hata mmoja wao. 12 Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake. 13 Wakayasahau matendo yake kwa haraka, HAWAKULINGOJEA SHAURI LAKE. 14 Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani. 15 Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao. 16 Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa Bwana. 17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu. 18 Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya. 19 Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka. 20 Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani. 21 Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri. 22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu. 23 Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu. 24 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake. 25 Bali wakanung’unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana. 26 Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani, 27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali. 28 Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu. 29 Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia. 30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa. 31 Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele. 32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao, 33 Kwa sababu waliiasi roho yake,…..”
Zaburi 10: 7 Baba zetu katika Misri Hawakufikiri matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
8 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, Ayadhihirishe matendo yake makuu.
9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.
10 Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia, Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.
11 Maji yakawafunika watesi wao, Hakusalia hata mmoja wao.
12 Ndipo walipoyaamini maneno yake, Waliziimba sifa zake.
13 Wakayasahau matendo yake kwa haraka, HAWAKULINGOJEA SHAURI LAKE.
14 Bali walitamani sana jangwani, Wakamjaribu Mungu nyikani. 15 Akawapa walichomtaka, Akawakondesha roho zao.
16 Wakamhusudu Musa matuoni, Na Haruni, mtakatifu wa Bwana.
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
18 Moto ukawaka katika mkutano wao, Miali yake ikawateketeza wabaya.
19 Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
20 Wakaubadili utukufu wao Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani.
21 Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.
22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
23 Akasema ya kuwa atawaangamiza Kama Musa, mteule wake, asingalisimama, Mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
24 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake.
25 Bali wakanung’unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana.
26 Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu.
29 Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.
30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa.
31 Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele.
32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33 Kwa sababu waliiasi roho yake,…..”
Hivyo kaka/dada, ikiwa wewe umeshakuwa mkristo, usichoke kumtazama Bwana, usichoke kumngojea Bwana ukayatamani mambo uliyoyaacha nyuma, mngojee Bwana baki katika hali hiyo hiyo ya utakatifu mpaka Bwana ajapo, faida zake utaziona utakapoingia katika nchi yako ya Ahadi pale Bwana atakapokuangazia rehema zake ukiwa hapa duniani kwanza, na kisha baadaye kule mbinguni utakapong’aa kama JUA.
Biblia inasema;
Maombolezo 3: 25 ”Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. 26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu”.
Maombolezo 3: 25 ”Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu”.
Usibabaishwe na chochote, usiyumbishwe na ulimwengu huu wala mambo ya ulimwengu huu kwasababu yanapita.Lakini wote wamngojeao Bwana watadumu milele.
Zaburi 27: 14 Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
Ubarikiwe sana.
KWA KUVUMILIA AKAIPATA ILE AHADI.
WALIOITWA NI WENGI, ILA WATEULE NI WACHACHE.
TUKAZE MWENDO ILI TUUFIKILIE UTIMILIFU.
NI KWA NINI TUNASEMA TUNAMWABUDU MUNGU ALIYE HAI ,JE! WALE WANAOMWABUDU SHETANI SIO MUNGU WAO ALIYE HAI?
KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA? (HOSEA 3)
Moja ya dhambi zinazowaangusha wengi ni “kutokusamehe”. Na hii inatokana mara nyingi na kutokuelewa nini maana ya msamaha. Ni rahisi kujilazimisha kusamehe lakini kama msamaha haujatoka ndani basi huo sio msamaha.
Ili kuelewa vizuri, tuchukue mfano una mtoto mdogo labda wa umri wa miaka 6 hivi, ukamkuta siku moja kachukua takataka kaweka ndani ya Friji, kwa namna ya kawaida ni lazima utakasirika na kuamua kumuadhibu ili kwamba siku nyingine asirudie…lakini je! Baada ya kumwadhibu utamwekea kinyongo?..Ni wazi kuwa hutamwekea kwasababu unajua ni mtoto tu! Laiti angefikia umri Fulani wa kujielewa asingefanya hivyo. Kwahiyo unamsamehe tu! Kwasababu unaelewa ni utoto tu ndio ulio ndani yake! Ndio unaomsumbua. Huwezi kwenda huku na kule na kwenda kutangaza kila mahali kwamba mwanao ni mbaya na kuanza kumchukia na kumwekea uadui.
Sasa usingeweza kuamua kumsamehe kabisa kutoka ndani ya moyo wako kama usingeelewa sababu ya kina ya yeye kufanya vile. Na ulipogundua kwamba sababu ni UTOTO ndipo ulipoamua kumsamehe kabisa kabisa.
Kadhalika tunapokuwa wakristo hatuwezi kusamehe watu wanaotuudhi au wanaotufanyia ubaya kutoka ndani ya mioyo yetu,kama hatutaelewa sababu ya wao kutufanyia huo ubaya ni ipi.
Leo tutajifunza sababu kubwa ya watu kutufanyia ubaya, au kutuudhi, au kutuumiza, au kutupangia mabaya, au kutuonea au kutufanyia chochote kile ambacho hakistahili kufanyiwa. Ambayo ukiielewa hiyo itakufanya uweze kumsamehe mtu kutoka ndani ya moyo wako kabisa.
Na sababu hiyo si nyingine zaidi ya DHAMBI ndani ya Mtu.
Mtu yoyote ambaye hajampa Bwana Yesu maisha yake, anakuwa ni milki ya shetani asilimia 100, Na kama anakuwa ni milki ya shetani, tunajua matunda ya shetani ndani ya mtu, ni yapi, Mwovu akiwa ndani ya mtu, Yule mtu lazima atakuwa ni mtu wa chuki, ni lazima atakuwa ni mtu wa kiburi, ni lazima atakuwa ni mtu wa hasira, ni lazima atakuwa ni mtu wa matusi, ni lazima atakuwa mtu wa kujipenda mwenyewe na kujijali nafsi yake, na kujiona yeye ni bora kuliko mwingine,ni lazima atakuwa ni mtu wa mashindano, ni lazima atakuwa mtu wa shari siku zote, mtu wa majivuno na wa dharau, na wakati mwingine atakuwa hata muuaji, n.k Kwa ufupi tabia zote mbaya ambazo zinajulikana zitakuwemo ndani ya huyo mtu ambaye hajampa Kristo maisha yake.
Sasa kama vile mtoto anapokosa, moja kwa moja unaelewa kabisa tatizo la Yule mtoto ni UTOTO uliopo ndani yake na laiti kama angekuwa mtu mzima asingefanya vile, Vivyo hivyo mtu yoyote ambaye hajampa Yesu Kristo maisha yake anapokutendea ubaya, anapokuonea wivu, anapokutukana pasipo sababu, anapokudharau, anapotafuta kukuangusha, anapokutegea mitego ya kila aina ili uanguke, anapokuchukia bure, anapokusengenya huku na huku, anapokuonea hasira, anapokuumiza kwa njia yoyote ile n.k Unapaswa uelewa kwamba tatizo sio yeye bali ni DHAMBI iliyo ndani yake, unapaswa uelewe laiti angekuwa Mkristo kweli kweli kama wewe asingefanya vile, laiti angekuwa amempa Bwana maisha yake asingekuwa na chuki,asingekulaani,asingekutukana, asingekuonea wivu n.k…
hivyo sio yeye bali ni ile dhambi iliyo ndani yake, Kama vile unavyoielewa hali ya mtoto mdogo anapofanya kosa vivyo hivyo unapaswa uielewa hali ya Mtu asiye ndani ya Kristo anapokukosea.
Ndio maana pale Kalvari Bwana Yesu hakutusamehe sisi kwasababu tu aliamua kutusamehe, au alituvumilia,hapana! bali alitusamehe kwasababu alijua hatujui tutendalo, Alijua laiti tungemjua yeye ni nani kwa wakati ule Tusengelimsulibisha pale msalabani. Alijua laiti tungefunguliwa macho yetu tusingefanya yale mambo…Hivyo alitusamehe katoka ndani ya moyo wake kabisa.
Sasa ukishindwa kuelewa haya, utajikuta kila mtu anakuwa adui yako, utashinda kuelewa tofauti ya mtu aliye ndani ya Kristo na mtu asiye ndani ya Kristo, utajikuta unakesha katika maombi ya kuangamiza maadui zako, utajikuta na wewe unaanza kulipiza mabaya badala ya mema. Utajikuta na wewe shetani amekuingia unaanza kuwa na chuki, unaanza kuwa msengenyaji, unaanza kulipiza visasi n.k
Hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako, anapokutukana, hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako anapokusengenya, hakuna sababu ya mtu kuwa adui yako anapokuchukia, hakuna sababu mtu kuwa adui yako anapokusaliti, hakuna sababu mtu kuwa adui yako anapokutendea ubaya wowote ule, kwasababu unaelewa kabisa kwamba tatizo sio Yule mtu, TATIZO NI DHAMBI ILIYOPO NDANI YAKE, laiti angekuwa mkristo kweli kweli asingefanya vile, hivyo unachopaswa kufanya ni kuchukua hatua ya wewe kumwombea Bwana ampe wokovu ili Dhambi hizo ziondoke ndani yake, lakini sio kushindana naye…Kwasababu ukishindana naye huwezi kumbadilisha kuwa kama wewe, wala hawezi kuvutiwa na kile kilichoko ndani yako. Suluhisho pekee ni kumwombea Rehema na Neema mbele za Mungu.
Ndugu jifunze kusamehe kutoka ndani ya moyo, kwa kuelewa hali ya mtu aliyopo. Kama kuwa na maadui hakuna mtu aliyekuwa na maadui kama Bwana wetu Yesu Kristo, na maadui zake namba moja tulikuwa ni mimi na wewe. Tulimtemea mate…je! wewe katika maisha yako ulishawahi kutemewa mate kama yeye?.. tulimtukana na kumdhihaki, na zaidi ya yote tukampeleka msalabani na kumwaibisha..je! wewe katika maisha yako ulishawahi kuaibishwa hivyo? Lakini yeye hakuwahi kutuita sisi maadui zake.. zaidi sana alisema “Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo” na zaidi ya yote akatuita sisi tuliokuja kumwamini baadaye rafiki zake.
Kama Bwana Yesu alitusamehe madeni makubwa kama hayo, unadhani sisi tunapaswa tuwafanyieje wanaotukosea?..tunapaswa tufanye zaidi ya hapo. Bwana alisema mwenyewe kwamba sisi tusipowasamehe waliotukosea hata Baba yetu wa mbinguni hatatusamehe makosa yetu. Ikiwa na maana kuwa kama kuna mtu yoyote ambaye hatujamsamehe kwa dhati kabisa kutoka ndani ya mioyo yetu, na sisi hatutasamehewa dhambi zetu, hivyo ni ziwa la moto litakuwa linatungoja, na Kristo hawezi kuzungumza uongo.
Ndugu yangu, epuka maombi yakupiga maadui zako, epuka kupeleka mashtaka mabaya mbele za Mungu juu ya watu wanaokuudhi, au kukuumiza, usimtaje ndugu yako kwa ubaya mbele za Mungu, wala usimtakie shari, bali mwombee rehema..ili atubu awe mkamilifu, Biblia inasema katika
Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.
Unaona? Hapo Bwana hafurahii, kuanguka kwake mtu mwovu, wala hafurahii mashataka mabaya tunayompelekea dhidi ya watu wengine, maombi tunayopaswa kuomba mbele zake ni Bwana atuepushe na madhara yao lakini sio awapige, au awaue, au awalaani. Adui yetu mkubwa ni shetani na sio watu.
Ni maombi yangu kuwa Bwana atakupa Moyo wa Rehema na Toba dhidi ya ndugu wanaotukosea.
Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine
Mada Zinazoendana:
KISASI NI JUU YA BWANA
VITA DHIDI YA MAADUI
OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “
Kuna watu wanasema usizihubiri hizi habari, we fundisha TU watu watubu wawe wakristo inatosha ndiyo kazi yako!. Swali ni je! ukishakuwa mkristo ndio mwisho wa safari?, unahitaji kukua na ndio safari inapoanzia na sio inaishia. Hivyo basi unahitaji chakula ili ukue, na ujue ni chakula gani unapaswa ukile, maana vyakula ni vingi vijengavyo na vibomoavyo, Hivyo ni kuwa makini kujua ni chakula kipi ule na kipi usile kwa usalama wa roho yako na hatma yako ya milele.
Tunaishi katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi hata kutokea katika vizazi vyote vya nyuma, ambacho kina mchanganyiko mkubwa wa MANABII WA UONGO NA MANABII WA KWELI, Na wote wanafanya kazi moja ya KUVUNA ROHO ZA WATU, aidha kuzipeleka kuzimu au mbinguni, ni kipindi cha hatari sana tunachoishi. Ni muhimu kufahamu unavunwa upande gani, ili usije ukajikuta unadondokea sehemu ambayo haujatarajia.
UPOTOFU ULIOPO SASA:
Jambo kubwa linalowachanganya watu wengi ni kuona pale mtu anayejiita mtumishi wa Mungu halafu bado ni mwasherati, mtukanaji, mlevi, anapenda anasa, na bado miujiza inatendeka na yeye, anafufua wafu, anaombea watu wanaponywa, anatabiri na unabii unakuja kutimia, ananena kwa lugha n.k. kiasi ambacho kinamfanya mtu mchanga ashindwe kuelewa inawezekanikaje huyu mtumishi anafanya mambo ya kidunia lakini bado ishara na miujiza zinatendeka na yeye, Na wala hatumii uchawi ila anatumia jina la YESU na nguvu za Mungu zinashuka. “HII NI SIRI” na ni jukumu kwa kila mkristo anayethamini maisha yake ya kiroho kufahamu..kumbuka (kuna wanaotumia nguvu za giza kutenda miujiza, siwazungumzii hao, hao ni rahisi kuwagundua lakini nawazungumzia wale wanaotumia nguvu za Mungu ambao ni ngumu kuwatambua.)
Tusome, mstari ufuatao unawazungumzia hao wanaotumia nguvu za Mungu ; kumb.13:1-5″
1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “
1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “
Unaona hapo? Huyo nabii hapo katoa unabii kwa uweza wa nguvu za Mungu na ikatokea, lakini anawafundisha watu waende kinyume na maagizo ya Mungu. Vivyo hivyo na hata sasa katika kipindi hichi cha mwisho Mungu ameamua kuachia mvua yake (UPAKO) kwa watu wote waovu na wema kutujaribu sisi kama TUNAMPENDA BWANA NA KUYASHIKA MANENO YAKE AU LA!.
Mtu anaweza akaja kwako na kutoa unabii na ukatimia na kufufua wafu, na kuponya wagonjwa lakini akafundisha injili nyingine akakwambia ulevi ni sawa, wanawake kwenda na mitindo ya kisasa ni sawa (anasema Mungu haangalii mavazi anaangalia roho ), akakufundisha kuupenda ulimwengu ni sawa, kuoa wake wengi ni sawa, Dunia haiishi leo wala kesho kula maisha, kuwa na pesa nyingi ndio kigezo cha kubarikiwa na Mungu, Mungu siku zote ni Mungu mzuri na hawezi kuwahukumu watu aliowaumba. n.k. na bado mtu huyo akatoa mapepo na kufufua wafu. Na wewe kwasababu NENO na kumpenda Mungu hakupo ndani yako, ukadhani anazungumza ukweli au katumwa na Mungu kwasababu tu! ametoa unabii ukatokea, NDUGU USIDANGANYIKE UMEPOTEA!! . Biblia inasema jiepushe na huyo mtu, CHUKUA TAHADHARI KWA USALAMA WA MAISHA YAKO..KIMBIA! HARAKA SANA NI BWANA NDIYE ANAYEKUJARIBU KUONA KAMA UNAMPENDA KWELI NA KULIFUATA NENO LAKE AU LA!
Leo hii wewe unayejiita mkristo unapenda injili za kufarijiwa tu! siku zote unapendwa kuambiwa “ALL IS WELL” ulimwengu hautakuja kuteketezwa,tunaishi chini ya neema, mafundisho unayoyapenda wewe ni KUTABIRIWA MAFANIKIO TU!. Lakini fahamu jambo moja BWANA YESU hakuacha enzi na mamlaka mbinguni ili aje kutufia sisi mlabani tuwe MABILIONEA, bali kwa ajili ya dhambi zetu.(hicho ndicho kiini cha injili) yeye mwenyewe alizungumza ..mathayo 16:24-27
” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Leo mkristo anadai anamfuata YESU, lakini kigezo cha kumfuata YESU ni kuwa na MSALABA wako, sasa wewe MSALABA WAKO UKO WAPI?, Jihadhari na haya mafundisho ya uongo yanawapeleka maelfu wa waaminio kuzimu kila siku pasipo wao kujua.
Hawa manabii wa uongo, Bwana Yesu alisema tutawatambua kwa MATUNDA YAO na sio kwa upako wao, kwasababu Mungu anaweza akamtumia mtu kama chombo tu cha kuazima akishamaliza shughuli nacho anakiacha, mfano tunaona Mungu alimtumia Punda kuongea na Nabii Balaamu kumpa ujumbe, lakini baada ya punda kutoa ujumbe alirudia katika hali yake ya kawaida ya upunda, vivyo hivyo na Balaamu mwenyewe alikuwa ni MCHAWI lakini Mungu alimtumia yeye kuwabariki Israeli, (hesabu 22:21-29), Na pia Mungu aliwatumia wale manabii 400 kumdanganya mfalme Ahabu kwasababu Mungu alikuwa amekusudia mabaya juu yake. (1 wafalme 22:6). Kwahiyo kuwa na upako mtu kuona maono, au kuwa nabii, au kunena kwa lugha au kuponya au kufanya miujiza yoyote ile, sio kigezo cha huyo mtu kuwa NABII WA MUNGU. Tutatawatambua kwa matunda yao (AMBAYO NI NENO LA MUNGU). Nabii wa kweli ni yule anayekuja na ishara pamoja na NENO lakini lililokuu ni NENO.
Kipime mtu anachokuambia je! kinaendana na NENO la Mungu? kama hakiendani na NENO la Mungu weka kando haijalishi anawashirika wengi kiasi gani, au anakubalika kiasi gani, au kanisa ni kubwa kiasi gani, au anaupako kiasi gani. KIMBIA! HILO NI SINAGOGI LA SHETANI!..
Jiulize Wewe unayejiita mkristo tangu ulipoamini, maisha yako ya kiroho yamesonga mbele kiasi gani. utakuwaje mkristo halafu biblia husomi!?? sasa utawatambuaje manabii wa uongo au manabii wa ukweli kwa namna hiyo watakapokujia na mafundisho yao??. Utakuwa unapelekwa na kila upepo unaokuja wa elimu yoyote. Maana njia pekee ya kumpima nabii wa uongo au Nabii wa ukweli ni kwa NENO TU!. Na sio kitu kingine. Jijengee kila siku tabia ya kusoma NENO na kuomba. Hizi ni nyakati za hatari tunaishi zile zilizotabiriwa kuwa watatokea manabii na makristo wengi wa uongo nao watawadanganya wengi yamkini hata walio wateule. Kumbuka ni wateule ndio wanaozungumziwa hapo kuwa wanaweza wakadanganywa sasa jiulize wewe ambaye sio mteule utaonekania wapi? wewe ndio hautaelewa chochote kinachoendelea utaishia kuwashangilia na kuwasifia kama Bwana Yesu alivyotabiri juu ya manabii wa uongo.
2 Petro 1:10″ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”
KWAHIYO NDUGU HUU NI WAKATI WA MUNGU KUTUJARIBU SISI KAMA TUNAMPENDA YEYE NA KULISHIKA NENO LAKE AU LA!. Biblia inasema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.
Mungu hadhihakiwi usipoweza kufanya hivyo jua tu utaangukia kwenye huu mstari ufuatao;
2 Thesalonike 2:10-12″… na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;12 ILI WAHUKUMIWE WOTE ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
MARAN ATHA!
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
NITAAMINI VIPI KAMA KUNA MBINGU AU KUZIMU?
KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE? NA TENA WANA WA ISRAEL WALIMFUKIZIA UVUMBA MALKIA WA MBINGUNI, NDIO YUPI HUYO?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, aliye Mfalme wa wafalme, na mkuu wa uzima, libarikiwe!
Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tutajifunza umuhimu wa kutaka kutafuta kujua mambo yajayo, Kwasababu biblia inasema katika..
Mathayo 7: 7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 KWA MAANA KILA AOMBAYE HUPOKEA; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa’.
Umeona! Bwana amesema kila aombaye hupokea, na kila atafutaye ataona ikiwa na maana kwamba, chochote mtu atakachokihitaji kama akikitafuta kwa bidii atakipata, kama atakitamani na kukihangaikia kwa bidii atakipata, na sheria hiyo haipo tu kwa wakristo bali hata kwa watu wasio wa Kristo, na viumbe vyote mtu yeyote hata asiye mcha Mungu akiamua kutafuta kitu chochoe katika ulimwengu huu kwa bidii atakipata tu! kwasababu ndivyo ilivyo “kila atafutaye atapata”…
Lakini leo hatuzungumzii namna ya kutafuta vitu vya ulimwengu huu, kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema…”itatufaidia nini kuupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi zetu ?”
Akimaanisha kuwa tusiwekeze nguvu zetu kubwa kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayopita badala yake tuwekeze nguvu kubwa kutafuta kujua mambo ya ulimwengu ujao yasiyoweza kuharibika. Na sheria ni ile ile kwamba “tukitafuta kwa bidii tutapata”
Lakini kama tunavyojua zipo gharama za kutafuta kitu, katika maisha ya kawaida hakuna mtu yeyote anayetafuta elimu ya kidunia katika hatua za awali akajihusisha na mambo ya ulimwengu huu, kwanza kabisa wengi wa wazazi huwa wanawapeleka watoto wao shule za bweni, na shuleni kule wanazuiliwa kuwa na vitu vyovyote vitakavyoweza kuathiri taaluma ya watoto wao, ndio hapo mwanafunzi atazuiliwa kuwa na simu, redio, atazuiliwa pia kuwa mzururaji, zaidi ya yote atazuiliwa hata kuingia jikoni,au kujishughulisha na kazi yoyote ya kujipatia kipato, yeye kazi yake iliyompeleka pale ni moja tu!! yaani kutafuta elimu. Kwahiyo waalimu wanafahamu endapo mwanafunzi akijihusisha na mojawapo ya mambo hayo, wanajua kabisa mwanafunzi yule hatapata kile alichoenda kukitafuta pale.
Hivyo analazimika kufungiwa shuleni, ananyimwa uhuru kwa asilimia kubwa, anakuwa ni sawa na kama yupo gerezani hivi, ananyimwa kujihusisha na mahusiano yoyote yale,tena wakati mwingine analazimika kupelekwa shule ya jinsia moja tu! isiyo ya mchanganyiko, Na zaidi ya yote kama mwanafunzi yule anajielewa atazidi kujiweka kwenye utumwa mwingine ulio mkali zaidi ya ule, ndio hapo masaa yake mengi atatumia kusoma hata ya usiku wa manane, muda anaolala utakuta ni masaa machache sana…ataendelea kwenye hicho kifungo kwa muda wa miaka kadhaa akitafuta tu! kilicho bora na hatimaye atakipata! Lakini je! asingeingia gharama za kuingia kwenye hicho kifungo kikali na cha kijitaabisha hivyo je! angekipata kilicho bora??
Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Mathayo 17: 21 “[Lakini namna hii haitoki ila kwa KUSALI NA KUFUNGA.]”
Unaona hapo aliposema kufunga hakumaanisha kuacha kula tu! bali alimaanisha kuacha kujishungulisha na mambo mengine ya kando ambayo yanaweza kuathiri kile kitu unachokitafuta. Hiyo ndio maana ya “kufunga” Kama vile mwanafunzi anavyofunga kwa kujizuia na mambo mengi ili apate anachokitafuta, anafunga kuwa mzururaji, kumiliki simu, kuangalia tv n.k
Mfano mzuri tunaweza kujifunza kwa kiumbe kama kuku, yeye atakapofika wakati wa kuyahatamia mayai yake, analazimika kufunga siku 21, lengo la yeye kufunga sio kwasababu anataka kuutesa mwili wake bila sababu, au kwasababu kapewa masharti ya kufanya hivyo, au kwasababu anatimiza wajibu Fulani, hapana bali ni kwasababu anajua endapo akienda kutembea huko na huko yale mayai aliyokuwa akiyahatamia yatapoteza lile joto na hivyo kuwa viza, na aambulie kutopata kile alichokuwa anakitafuta.
Kadhalika na tunapoutafuta ufalme wa mbinguni, tunapaswa tufunge! Na kufunga sio kuacha kula tu, hiyo ni moja, maana kuu pale ya kufunga ni tunatakiwa tufunge mambo ya ulimwengu huu yanayotuzuia tusifikie malengo yetu, kama vile kuku anavyolihifadhi joto lake kwa siku 21 kwa uvumilivu wote, na sisi vivyo hivyo tunapaswa tulihifadhi joto letu, kwa Roho Mtakatifu tuliyepewa kwa kipindi chote tunachoishi hapa duniani, Biblia inasema katika Luka 12: 35 “taa zenu ziwe zinawaka;…nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao,” hivyo tunapaswa tufunge uasherati, tufunge anasa, tufunge kiburi, tufunge kuzurura huku na kule kutafuta mambo ya ulimwengu huu yanayoharibika na utafutaji wa mali uliopitiliza…zaidi tuelekeze macho yetu mbinguni..kwasababu muda uliobaki ni mchache sana.
Kadhalika na maana ya kusali pia sio tu kujifungia ndani tu, na kupeleka mahitaji mbele za Mungu, hapana ni zaidi ya hapo, maana ya kusali pamoja na kupeleka mahitaji yetu na haja zetu mbele za Mungu ni kukaa katika uwepo wa Mungu muda mrefu ukitafuta kujua na kujifunza huku na kule kuhusu mahali ulipotoka, ulipo sasa na unapoeleka. Hiyo ndio maana ya sala.
Kaka/Dada tafuta mambo yajayo kwa “KUFUNGA NA KUSALI” wafunge marafiki wasio na maana wanaokuvuta katika mambo ya ulimwengu huu, ni afadhali uwe peke yako lakini unaenda mbinguni kuliko kuwa miongoni mwa kundi kubwa linalokwenda Jehanamu ya moto. Rafiki anayekudharau wewe unapomtafuta Mungu au anayekushauri namna ya kumtafuta Mungu wakati yeye mwenyewe hamtafuti ni Mlevi, msengenyaji, mla rushwa huyo atakupeleka jehanamu, tangu lini kipofu akamwongoza kipofu mwenzake? Bwana Yesu alisema wote watatumbukia shimoni..
Dada unayesoma hapa usipotaka kufunga mambo ya ulimwengu huu na kutazama macho yako..usipotaka kufunga uvaaji mbaya, usipotaka kufunga uvaaji wa mawigi, na kupaka wanja na lipstick, usipotaka kufunga usengenyaji wako, usipotaka kufunga tamaa za kuwa maarufu kama wanawake wa ulimwengu huu Kristo atakapokuja hutajua chochote…Hebu jifunze kwa mwanamke Ana wa kwenye biblia aliyefunga mambo yake yote na kuamua kutazama na kutafuta mambo yanayokuja ya mbinguni..
Mwanamke Ana, alifiwa na mume wake akiwa na umri mdogo, na akaamua kutokuolewa tena akafunga mambo yote na kuanza kujishughulisha katika kutafuta mambo yanayokuja tu…Wakati huo Masihi (Yesu Kristo) bado alikuwa hajazaliwa, lakini kwa jinsi alivyokuwa anatia bidii kutafuta sana…Bwana akamfunulia MAJIRA YA KUJA KWAKE, akashuhudiwa kumwona Bwana uso kwa uso. Hivyo wakati wakuu wa dini, hawajui majira ya kuzaliwa Bwana, Mwanamke Ana tayari alikuwa anajua kalenda ya Mungu. Wakati wanawake wengine wanafurahia fashioni za ulimwengu mwanamke Ana, alikuwa anajua Kristo yupo mlangoni kuja ulimwenguni. Tunasoma habari hiyo katika..
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana KWA KUFUNGA NA KUOMBA. 38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana KWA KUFUNGA NA KUOMBA.
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”
Na mambo haya haya yatatokea katika siku hizi za mwisho, wakati wewe dada unaendelea kujifurahisha na mambo mabovu ya ulimwengu huu, wapo wanawake wenzako mahali fulani Bwana ameshawapa kalenda yake ya kurudi kwake mara ya pili, wakati wewe unasema Kristo haji leo wala kesho wapo wanawake wenzako mahali Fulani ambao dunia inawaona washamba leo, wanazungumza na Bwana uso kwa uso, na wameshuhudiwa mambo mengi.
Kadhalika ndugu unayesema Kristo, haji leo wala kesho, hivyo ni wakati wa kuishi unavyotaka, ni vizuri ukafahamu kuwa ni maelfu wanaowaza kama wewe, lakini wapo wachache wanaofahamu nyakati za kujiliwa kwao, wapo wachache ambao wameamua kweli kufunga mambo ya ulimwengu huu na kuamua kumtafuta muumba wao, ambao tayari wameshapewa kalenda yote ya kurudi kwa Bwana..wakati ulevi wako unastawi, rushwa yako inastawi, kiburi chako kinastawi, anasa zako na uasherati wako unastawi..wenyewe wanainua vichwa vyao juu wakiitazama jinsi ile siku inavyokaribia…
Jifunze kwa Simeoni ndugu yangu, mtu aliyeishi wakati mmoja na mwanamke ANA, yeye naye Roho alimshuhudia kwamba hatakufa hata atakapomwona Kristo akifika ulimwenguni.. Wakati dunia nzima haielewi chochote..Tunayasoma hayo katika..
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, 31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;”
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;”
Ni maombi yangu kuwa Bwana ataigeuza nia yako na mtazamo wako kuanzia leo na kuendelea, uanze kutamani kujua mambo yajayo, Roho yule yule aliyemfunulia ANA na SIMEONI kuja kwake, mara ya kwanza, Roho huyo huyo anaweza kuyafunua macho yako leo ukaona jinsi kuja kwake mara ya pili kulivyo karibu, endapo tu utakusudia KUFUNGA mambo yote ya ulimwengu na kujitenga kumtafuta Mungu kama Ana na Simeoni.
Kama hujampa BWANA YESU maisha yako, ni vizuri ukafahamu kuwa Hakuna Uzima nje ya yeye, wasanii maarufu wamepita, maraisi washupavu wamepita,.Raisi tu wa Marekani aliyemaliza muda wake, leo hii umeshaanza kumsikia anafifia lakini huyu YESU mpaka leo hii anatangazwa, habari zake hazichakai na ndivyo ilivyo kwa wale wote wanaomcha yeye, hivyo nakushauri kama hujampa maisha yako, tubu leo na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako nawe utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.
Mungu akubariki.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana akuongezee Neema yake.
MIISHO YA ZAMANI.
MATUMIZI YA DIVAI.
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU
JE! SHETANI ANAWEZA KUYAJUA MAWAZO YA MTU?
SANDUKU LA AGANO LINAWAKILISHA NINI?
ELIMU ni UFUNGUO wa maisha, hiyo ni kweli, lakini ELIMU ILIYO SAHIHI sio tu ufunguo wa maisha, bali pia ni ufunguo wa kila kitu. Na kwa jinsi elimu ya mtu huyo itakavyozidi kuwa kubwa zaidi ndivyo uwezekano wa mtu huyo kufanya mambo yote unavyozidi kuwa mkubwa zaidi.
Kumbuka zipo Elimu kuu tatu zilizopo ulimwengu sasa.
1)Elimu ya ufalme wa mbinguni.
2)Elimu ya kidunia
3)Elimu ya ufalme wa giza
Leo hii tunaweza kufurahia mafanikio tuliyoyafikia ya kiteknolojia kwa mfano kuchat na watu mitandaoni, kupaa angani kwa ndege, kuzungumza na ndugu zetu walio mbali kwa simu, kutunza vyakula katika majokofu, katazama tv n.k..sio kwasababu dunia imebalika maumbile yake tofauti na ya zamani hapana!, Ni kwasababu wapo watu waliokaa chini kwa muda mrefu mahabara, na katika makarakana usiku na mchana, wengine hata kutokuoa au kuhatarisha maisha yao, wakisoma na kujifunza kanuni za huu ulimwengu jinsi ya kuendana nazo na kwa namna gani watazitumia kubuni njia mbadala ya kuunda vitu. Na kwa bidii yao ya kujifunza na kusoma sana kwa muda mrefu ikawapelekea kugundua vitu ambavyo hata kwa namna ya kawaida unaweza ukasema haviwezakani kutokea. Lakini tunaviona katika jamii zetu kila siku vipo..
Kadhalika shetani naye hakuna jambo ameweza kufanikiwa kulipata kwa mwanadamu kirahisi rahisi kama sio kwa Elimu. Alisoma kanuni za Mungu za uumbaji kwa muda mrefu sana, hivyo kwa kuwatazama viumbe wake na vitu vya asili na nguvu na mamlaka Mungu aliyoweka ndani yao, akagundua kuwa akiwafanya waende kinyume na zile kanuni basi yeye atakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa manufaa yake. Na ndio maana jambo la kwanza pale Edeni Shetani hakuja kwa utisho wowote wa silaha kwa Adamu na Hawa hapana bali alikuja na UDANGANYIFU. Ambao alijua kwa huo ataweza kuwadhoofisha UWEZO wao hivyo kirahisi atawapokonya mamlaka yao waliyopewa na Mungu katika hii dunia..
Na ndivyo alivyofanya na kufanikiwa kuuweka ulimwengu chini yake mpaka tunaona alipokuja Bwana wetu Yesu Kristo kuyachukua yale mamlaka tena Adamu aliyoyapoteza. Na haishii hapo tu! kwasababu shetani lengo lake ni kutaka kuwa kama Mungu, na kwasasa ameshafahamu kuwa hawezi tena kufikia malengo yake kwasababu ya YESU basi anachokifanya ni kuwa piga upofu wanadamu wote wasifikie katika viwango vya MAARIFA/ELIMU ambayo Bwana anataka watu wake wavifikie.
Na ndio maana biblia inasema katika Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;”..Shetani ataendelea kutuangamiza kama tutakosa maarifa ya kimbinguni.
Sasa Elimu hizo mbili yaani (Elimu ya dunia na Elimu ya ufalme wa giza), japo kila moja inajitahidi kwa upande wake, kutatua kila jambo, lakini hata moja haijaweza kuleta suluhisho la mambo ya msingi yamuhusuyo mwanadamu. Kwamfano hakuna elimu yoyote inayoweza kuleta dawa ya kifo na kutoa uzima wa milele, au kufufua mfu, au kuumba, au kusimamisha jua, au kuupiga mwezi, au kuamisha visiwa na milima, hakuna hata moja inayoweza kutabiri mambo yanayokuja,..hakuna hata moja ya hizo inazoweza kufanya jambo kama hilo. Wanasayansi wote pamoja na shetani mwenyewe hawana maarifa hayo.
Ni ELIMU moja tu YA KWELI ambayo Mungu aliiweka tangu mwanzo ndiyo inayoweza kufanya mambo yote, nayo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI BASI!!.
Hivyo pale Biblia inaposema katika Mithali 4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.”
Haimaanishi ELIMU yoyote tu ile, iliyopo kila mahali, hapana sio elimu ya ulimwengu huu, kama vile isivyokuwa elimu ya wachawi, bali Elimu inayozungumziwa pale ni Elimu inayohusiana na hicho kitabu chenyewe (yaani BIBLIA).
Na kama vile Elimu yoyote ile ilivyo na gharama kuipata kadhalika na kuisoma, vivyo hivyo na hii ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI izidiyo elimu zote inayo gharama nyingi za kuipata. Kila mkristo anapoamini na kumpa Bwana maisha yake ni sawa na mtoto kwa mara ya kwanza aliyeenda kuanzishwa elimu ya awali, anaitwa mwanafunzi, tunafahamu kuwa siku hiyo hiyo hawezi kujua kila kitu kinachohusu shule, siku hiyo hiyo hawezi kupaisha ndege, au kufanya operesheni, hapana bali atakavyozidi kuonyesha bidii ya kujifunza kila siku, kidogo kidogo atajikuta anaongeza kitu katika kichwa chake, atavuka darasa moja, anakwenda lingine hivyo hivyo mpaka baadaye akifika chuo kikuu, ambapo kiwango cha yale maarifa kitakuwa kimeshakolea ndani yake sasa hapo ndio anakuwa na uwezo wa kurusha ndege.
Na ndivyo tunavyojifunza kwa Bwana wetu YESU KRISTO, tunamwona kama vile alivyo, hakuzaliwa na kipawa tu basi cha kuwa na hekima nyingi kiasi kile na kujawa uwezo mkuu kama ule. Biblia haitufundishi hivyo bali tunamwona Bwana tangu akiwa mdogo alikuwa ni mtu mwenye bidii sana KUSOMA ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI, alikuwa akijifunza kupita kiasi hata akiwa na umri wa miaka 12 tu, biblia inarekodi siku tatu usiku na mchana alikuwa akijifunza habari za YEHOVA kwa marabi(Waalimu wa Torati), akiuliza maswali, pale ambapo hakuwa anapaelewa, alisahau hata kula kwa ajili ya KUSOMA TU! Aliwasahau wazazi wake, aliona ule muda walioenda Yerusalemu na wazazi wake ni mchache sana wa yeye kujifunza,
Tunasoma;
Luka 2:45 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, AKIWASIKILIZA NA KUWAULIZA MASWALI. 47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake”.
Luka 2:45 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, AKIWASIKILIZA NA KUWAULIZA MASWALI.
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake”.
Biblia inasema pia aliendelea kuwa mtu wa namna hiyo hiyo, akitoka katika hatua moja ya hekima hadi nyingi.. Tunasoma
Luka 2:52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika HEKIMA NA KIMO, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Unaona hapo aliendelea katika Hekima, siku baada ya siku na KIMO kinachozungumziwa hapo sio urefu wa mwili, bali ni KIMO cha KUMJUA MUNGU. Aliweza kuona mahali waandishi walikwama, yeye hakuridhika akavuka pale na kuzidi kujifunza zaidi mpaka siku moja akawa ZAIDI ya wale MARABI waliokuwa juu yake wakimfundisha.
Mathayo 13:51 “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam. 52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake VITU VIPYA NA VYA KALE”.
Mathayo 13:51 “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.
52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake VITU VIPYA NA VYA KALE”.
Bwana yeye kama mwandishi mkuu pia aliweza kutoa katika hekima yake vitu vipya na vitu vya kale (Agano jipya na Agano la Kale), kwasababu Elimu ya Ufalme wa mbinguni ilikuwa imemkaa sana ndani yake.
Hiyo ni sababu leo hii tunamwona Bwana kuwa mtu ambaye hakushindwa na jambo lolote, hakukuwa na tatizo lolote lililoweza kusimama mbele yake, alipewa maarifa yote na Mungu, alipewa maarifu ya namna ya kuutoa uhai wake na kuurudisha, ni nani leo hii anaouwezo huo?, aliweza kuamrisha mbingu, bahari, na upepo vyote vikamtii,hakukuwa na mgonjwa yoyote aliyeletwa mbele zake asiweze kumponya, Mungu alimpa kila kitu angali akiwa bado hapa duniani.. Na ndipo hapo shetani akajua kuwa hakuna tena tumaini kwake kwasababu vyote alivyovitarijia siku moja avipate vyote vimeshafunuliwa kwa BWANA wetu YESU KRISTO. Haleluya!. Kazi aliyobakiwa nayo sasa ni kutuangamiza kwa kukosa kwetu maarifa ya kumjua YESU KRISTO BWANA WETU.
Bwana YESU alitupa ushauri sisi wote, kwamba “TUJIFUNZE KWAKE” (Mathayo 11:29). Na pia alisema yeye ndiye njia ya kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye (Yoh 14:6). Hivyo ni lazima tujifunze katika NJIA ZAKE ili na sisi tupate akili tupone.
Kama wachawi na wanasayansi hawalali kila siku wapo wanachunguza na kutafiti juu ya mambo yao na ufalme wao, inatupasaje sisi wakristo ambayo ELIMU YETU inaweza kufanya makubwa zaidi ya hayo?
Ukristo mwanzo wake ni kuamini na kubatizwa, lakini pia ni zaidi ya hapo. Bwana anataka kutupa maarifa ya ziada katika maisha yetu ya kumjua yeye, ili na sisi pia tukue katika kimo na hekima, kama Bwana, lakini tunakuwa wavivu wa KUSOMA na KUJIFUNZA NENO LA MUNGU kila siku.
Japokuwa Paulo alikuwa ni mtume wa Kristo aliyejaa mafunuo mengi, na ambaye mpaka sasa tunatumia nyaraka zake kama urejesho wetu wa kimaandiko, lakini hakuacha KUSOMA na KUJIFUNZA kila siku Elimu ya Ufalme wa mbinguni. Tunasoma akimwambia Timotheo..
2Timotheo 4: 13 Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, NA VILE VITABU, HASA VILE VYA NGOZI.
Unaona hapo?, alihitaji Kusoma, kwasababu Elimu ya ufalme wa mbinguni ni kuu sana haina mwisho wake. Hakujiona kuwa amefika au anafahamu kila kitu bali alitaka zaidi na zaidi kujifunza kumjua Mungu katika upana wake na marefu yake. Na hakuishia hapo bali alimwagiza pia Timotheo afanye vivyo hivyo, kama tunavyosoma katika
1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. 13 Hata nitakapokuja, UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA na kuonya na kufundisha.”
1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
13 Hata nitakapokuja, UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA na kuonya na kufundisha.”
Hivyo na sisi pia kama watoto wachanga, tuitafute sana Elimu ya ufalme wa mbinguni, kwa kutafiti na kuchunguza mambo yote yamuhusuyo MUNGU wa ISRAELI na YESU KRISTO BWANA WETU katika maandiko angali tunaishi sasa, ili tukifikie kile cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Amen.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, NA KUCHUKULIWA NA KILA UPEPO WA ELIMU, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.”
MAFUNDISHO YA MASHETANI
JE! UMEFUNDISHWA?
UPEPO WA ROHO.
NINI MAANA YA “NITAWAVUTA WOTE KWANGU” (YOHANA12:32)?
JE KUNA ANDIKO LINALOMRUHUSU MWANAMKE KUWA SISTER?
YOHANA MBATIZAJI ALIBATIZWA NA NANI?