Swali: Mchuuzi maana yake nini kama tunavyosoma katika Hosea 12:7? na je tunaruhusiwa kuwa wachuuzi?
Jibu: Turejee.
Hosea 12: 7 “Ni MCHUUZI, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu”
Mchuuzi ni mtu anayefanya biashara ya kununua bidhaa na kuzisafirisha kwenda kuziuza mahali pengine hususani nje ya nchi yake.
Utalisoma neno hili tena katika kitabu cha Wimbo ulio bora 3:6, Ezekieli 27:3, Ezekieli 27:20-22 na Isaya 23:8.
Swali ni je biblia inaturuhusu wakristo kuwa Wachuuzi (yaani biashara ya kutoka nchi moja kwenda nyingine)?
Jibu ni ndio inaruhusu!, isipokuwa katika biashara yoyote ile ni muhimu kuzingatia viwango vya utakatifu na ukamilifu, Uchuuzi wowote ukihusisha rushwa au biashara haramu ni kosa kibiblia, na pia ni hatari kama maandiko yanavyosema katika Ezekieli 28:18.
Ezekieli 28:18 “Kwa wingi wa maovu yako, KATIKA UOVU WA UCHUUZI WAKO, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. 19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”
Ezekieli 28:18 “Kwa wingi wa maovu yako, KATIKA UOVU WA UCHUUZI WAKO, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).
Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)
Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
Rudi Nyumbani
Print this post
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo Mwanga wa njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zaburi 119:105).
Wengi tuna juhudi katika “mwili” lakini hatuna juhudi katika “roho”. Juhudi katika mwili ni nzuri na inafaa lakini ile ya roho ni bora Zaidi na inafaa sana. Kwasababu biblia inasema Roho ndiyo inayoutia uzima (Yohana 6:63).
Sasa Neno la Mungu linasema..
Warumi 12:11 “kwa bidii, si walegevu; MKIWA NA JUHUDI KATIKA ROHO ZENU; mkimtumikia Bwana”.
Sasa hizi juhudi katika roho ni zipi?..
1. JUHUDI KATIKA MEMA.
1Petro 3:13 “Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema”.
Matendo mema ni pamoja na kuwasaidia wanyonge (masikini, mayatima na wajane), kusamehe na mengineyo..
2. JUHUDI KATIKA KUPENDANA.
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika”
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
9 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika”
Mtu mwenye juhudi katika roho ni yule pia mwenye juhudi katika kuutafuta upendo.
3. JUHUDI KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU.
Kazi ya Mungu si lazima iwe ile ya kusimama mimbarini na kuhubiri/kufundisha.. Lakini pia ile ya kusafisha nyumba ya Mungu, ni kazi yenye thawabu kubwa na heshima kubwa kwa Mungu… Ukiwa na juhudi katika kumtumikia Mungu kwa njia hiyo pasipo kusukumwa au kukumbushwa kumbushwa bali unajituma wewe mwenyewe, basi hapo unaonyesha juhudi uliyonayo katika roho, na ukomavu wako kiroho.
4. JUHUDI KATIKA KUOMBA.
Ikiwa utaweza kuomba kila siku kwa muda usiopungua lisaa limoja, hiyo ni ishara kubwa ya kuwa una juhudi katika roho, lakini kama kuomba kwako ni mpaka jumapili kwa jumapili, basi kuna ulegevu ulio ndani yako.
5. JUHUDI KATIKA KUSOMA NENO.
Mtu mwenye kutia bidii katika kujua mafunuo yaliyo ndani ya biblia kwa njia ya kujifunza na kutafiti na kurudia rudia kutafakari yale aliyoyasoma na kujifunza, mtu wa namna hiyo kibiblia ni mwenye juhudi katika roho na si mlegevu.
Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
6. JUHUDI KATIKA KUMTOLEA MUNGU.
Sadaka inakamilisha ibada kwa mkristo yoyote yule (ikiwemo mchungaji, mwalimu, nabii, mwinjilisti au mtumishi mwingine yoyote). Na mtu mwenye bidii nyingi katika kumtolea Mungu, mtu huyo kulingana na biblia ni mwenye juhudi katika roho.
Kwa namna gani mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pake? (Zaburi 116:15).
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
IKIWA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).
SWALI:Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini?
Tunaona Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili, Mungu alimpa adhabu kwa kumwambia maneno haya;
Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Lakini tukiendelea kusoma tunaona, Kaini anamlilia Mungu na kumwambia adhabu yangu ni kali sana, haichukuliki, kila mahali nitakapoenda nitakuwa mtu wa kuuliwa, ndipo Mungu akamuhakikisha ulinzi kwa kumwekea alama. Kama tunavyosoma kwenye vifungu vinavyofuata;
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga
Swali linakuja hii alama ni ipi?
Lakini kabla ya kufahamu alama yenyewe ni nini ni vizuri ukaelewa maana ya adhabu aliyopewa ya kuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Fungua hapa ufahamu tafsiri yake >>>> UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.
Hivyo tukirudi kwenye swali alama ni ipi?
Zipo nadharia nyingi, lakini tujifunze kwanza baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa adhabu ile Kaini aliitambua kabisa ilihusu kutengwa na fadhili na uso wa Mungu kabisa. Na mahali popote pasipo na mkono wa Mungu hapana usalama wowote, ni sawa na mwili unaokosa kinga, kila ugonjwa unaopita pale utaushambulia, hata yale maradhi madhaifu kabisa,. Ndicho alichokigundua Kaini alijua pasipo Mungu duniani hata kwa sehemu ndogo, haiwezekaniki kuishi, chochote chenye uhai atakuweza tu, wanyama watakuweza, mapepo yatakuweza. Ndio maana ya kauli yake hiyo ‘kila anionaye ataniua’.
Lakini Mungu akamuhakikishia usalama, kwa kumwekea alama, ili yoyote akimwona asimuue Kaini. Sasa kufikiri alama hiyo ni mchoro(tattoo) Fulani mwilini, si rahisi kumfanya mtu asidiriki kumuua, kwani mchoro hauzuii mtu kuangamizwa.
Lakini kufikiria alama iliwekwa katika eneo la ki-mwonekano (ukubwa), au eneo la kuongezewa sifa/ufanisi Fulani uliotofauti na wengine yaweza kuwa jambo la kweli.
Kwanini?
Tunaweza kuona baada ya pale sifa za uzao wa Kaini jinsi zilivyokuwa, walikuwa ni watu wavumbuzi, watu wa elimu (Mwanzo 4:20-22) lakini pia Hodari na wengine wao wenye maumbo makubwa (Mwanzo 6:4),. Kwahiyo sikuzote tunafahamu hata sasa walio na uwezo mkubwa wa kielimu na kiteknolojia si rahisi kuwaweza kivita, hata iweje. Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, walikuwa ni wakulima tu na wafugaji. Hawakuwa na ujuzi mwingi ijapokuwa walikuwa ni uzao wa Mungu.
Kwahiyo wana wa Kaini, waliitawala dunia, hawakuwa watu dhaifu dhaifu, na yoyote ambaye angejaribu kumuua mmojawapo, kisasi kingemrudia mara saba, kwa nguvu tu walizokuwa nazo, ijapokuwa hawakuwa na Mungu maishani mwao.
Si jambo la ajabu Mungu kumuhakikisha ulinzi mtu mwovu, leo hii wengi watasema Bwana mbona wenye dhambi ndio wanaofanikiwa, mbona waovu ndio wenye nguvu duniani, wapo salama, ndio wenye mavumbuzi makubwa. Fahamu kuwa hiyo ni alama yao. Ambayo ilianzia tokea mbali kwa Kaini. Kwasababu wangekuwa waovu, halafu pia wanyonge, wangeishije kwenye hii dunia.
Kamwe usiitamani alama ya Kaini, usitamani kulindwa ndani ya uovu, kwasababu utadumu kwa kitambo tu, baadaye utaangamizwa kama ilivyokuwa kwa hawa, katika gharika. Yesu alitoa mfano wa magugu na ngano katika shamba, kama tunavyoifahamu ile habari, wale wakulima walitaka kwenda kuyang’oa magugu shambani ili waziache ngano. Lakini mwenye shamba akasema waache vyote vikue pamoja mpaka siku ya mavuno, ndipo yatakusanywa na kutupwa motoni.
Na tafsiri ya mfano ya ule mfano akasema shamba ni ulimwengu, na ngano ni wana wa ufalme, lakini magugu ni wana wa ibilisi, na wavunaji ni malaika. Kuonyesha duniani yapo mapando ya aina mbili, na yote yatashiriki mbolea, maji, matunzo yote kutoka kwa Mungu, na kimsingi magugu huwa ndio mepesi kustawi kwa haraka kuliko ngano.
Jiulize na wewe ambaye unastarehe katika dhambi na hauoni madhara yoyote, unaelekea wapi? Hujui umetiwa alama kwa muda, nguvu zako, utajiri wako, mafanikio yako, zaidi ya watu wa Mungu, usidhani ndio umebarikiwa unathamini na Mungu. lakini wakati utafika kuzimu utaiona. Embu kubali sasa kuwa mwana wa ufalme, kwa kumaanisha kutubu dhambi, na kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili akuondolee deni la dhambi uwe mtakatifu mbele zake kwa damu yake, akuepushe na hukumu inayokuja .
Ikiwa upo tayari kuokoka leo. Fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Nitamjuaje nabii wa Uongo?
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.(Opens in a new browser tab)
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Mathayo ni nani?
Kama jina la kitabu linavyojieleza “INJILI KAMA ALIVYOIANDIKA MATHAYO MTAKATIFU”. Maana yake ni kuwa kitabu hiki kiliandikwa na Mathayo. Lakini utata unakuja ni Mathayo yupi?
Ijapokuwa biblia haielezi ni Mathayo yupi lakini wanazuoni wengi na watafiti wa historia kibiblia, wanahitimisha kusema ni Mathayo mtume wa Yesu Kristo Yule mtoza ushuru, ambaye alijulikana pia kwa jina la Lawi (Marko 2:14) ndiye aliyekiandika kitabu hicho.
Kitabu hiki kinaeleza Mwanzo wa kutokea mwokozi duniani, mpaka Kifo chake na kufufuka kwake. Ndani yake kuna historia ya mwokozi, mafundisho na matendo ya miujiza aliyoyafanya. Katika kitabu hiki zipo hotuba kuu tano ambazo Yesu alizisema;
Kwa upana wa hotuba hizi na uchambuzi wa kitabu hiki, fungua hapa, >> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA MATHAYO.
Bwana akubariki
Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?
Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Wafalme(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Nini maana ya “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Mithali alikuwa nani?
Sulemani mwana wa Daudi, anajitaja mwenyewe kama mwandishi, katika mwanzo kabisa wa kitabu hiki
Mithali 1:1 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu
Kitabu hichi kinakadiriwa kuandikwa miaka mia tisa (900) kabla ya Kristo.Ni kitabu kilichojaa maneno ya hekima na kanuni, maagizo ya rohoni, vilevile maonyo mbalimbali yanayohusiana na maisha ya kawaida, pamoja na maarifa na mafunzo yaliyo katika vitu vya asili.
Mithali 1-22:16, Iliandikwa na Sulemani mwenyewe.
Kuanzia Mithali 22:17-24:34, zilizojulikana kama kitabu cha Tatu, huwenda ziliandikwa na wengine lakini zikakusanywa na Sulemani mwenyewe.
Lakini Kuanzia Mithali 25-29, biblia inatuambia ziliandikwa na Sulemani, lakini watu wa mfalme Hezekia ndio waliozirekodi.
Na Mithali 30, Ambacho hujulikana kama kitabu cha Tano. Kiliandikwa na Aguri bin Yake.
Lakini Mithali 31 ambacho ni cha mwisho, kiliandikwa na mfalme Lemueli.
Japo wanazuoni wengine husema Aguri bin yake na Lemueli, yalikuwa ni majina mengine ya Sulemani.
Kwa vyovyote, kitabu hichi kwa sehemu kubwa kimeandikwa na Sulemani. Ndio maana hujulikana kama kitabu cha Sulemani. Lakini pia hatuna uhakika asilimia zote hekima zote ziliandikwa na yeye mwenyewe, kufuata na hao watu wawili wa mwisho wasiojulikana.
Kwa urefu wa chambuzi wa kitabu hichi fungua link hii >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Hizi ni baadhi ya fafanuzi ya hekima tuzisomazo katika kitabu hicho
Maana ya Mithali 21:17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;
Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;
Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno;
Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?
Nini maana ya Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;
Je! Sulemani alienda mbinguni?
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Wafalme alikuwa nani?
Biblia haijaweka bayana aliyekuwa mwandishi wa kitabu hiki, lakini kufuatana na hadithi za kiyahudi huaminika kuwa nabii Yeremia ndiye alikuwa mwandishi wa vitabu hivi viwili vya wafalme.
Kitabu hichi kinaeleza kwa kina tawala za kifalme Kuanzia Mfalme Sulemani, na kugawanyika kwa taifa la Israeli pande mbili, hadi kuanguka kabisa kwa taifa lote la Israeli kwa kuchukuliwa utumwani Ashuru na Babeli. Miongoni mwa Wafalme wapo waliosimama vema, lakini pia wapo wengi waliolikosesha taifa la Israeli, Wa kwanza alikuwa ni Yeroboamu ambaye ndiye aliyeupokea ufalme uliogawanyika yeye aliunda sanamu na kuzisimamisha kaskazini na kusini mwa Israeli, ili waisraeli wakamwabudu Mungu huko. Machukizo ambayo yaliendelea hivyo kwa muda mrefu, ijapokuwa zilikuja kuondolewa hizo sanamu na mfalme aliyeitwa Yosia, lakini bado hasira ya Mungu haikupoa kwa mambo mengi mabaya waliyokuwa wanayatenda wana wa Israeli, Hadi walipofikia hatua ya kuhamishwa.
Kwa urefu wa uchambuzi wa vitabu hivi waweza fungua hapa upate kujisomea >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
Je! Wewe umepokea wokovu wa Roho yako kwa Kristo Yesu? Kama ni la! Basi wakati ndio huu wa kufanya geuko la dhati, moyoni mwako. Ikiwa upo tayari basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.
Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).(Opens in a new browser tab)
WhatsApp
Mwandishi wa kitabu cha Filemoni
Kitabu cha Filemoni ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika akiwa kifungoni Rumi. Waraka huu alimuandikia Filemoni mtu ambaye alimgeuza yeye mwenyewe katika injili yake. Baadaye akawa mtendakazi katika utumishi wa Bwana, katika nyumba yake mwenyewe. Na kuwa Baraka kwa watakatifu wengi huko Kolosai.
Filemoni 1:2 “na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako”
Kilichomsukuma hasaa mtume Paulo kuandika waraka huo ilikuwa ni kwa mtendakazi wake mpya aliyemzaa katika Kristo aliyeitwa Onesmo ambaye hapo mwanzo alikuwa ni mtumwa wa Filemoni aliyemwibia vitu vyake na kukimbia. Kwamba sasa ampokee na kumchukulia kama mtendakazi mwenzao, kwasababu ametubu na anafaa kwa utumishi. Kwa urefu wa mafunzo yaliyo ndani ya kitabu hichi cha Filemoni, Fungua hapa, ujifunze kwa kina >>>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.
Je! Umempokea Kristo maishani mwako?
Kama ni la! Basi wakati ndio huu, bofya hapa kwa mwongozo wa namna ya kumpokea Kristo maishani mwako. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)
Shalom.
Usiishie kutafuta tu utakaso wa roho, bali tafuta pia UTAKASO WA MWILI, kwamaana vitu hivi viwili vinaenda sambamba, kwasababu vitu hivi vikichafuka vinaiharibu pia nafsi ya mtu.
2Wakorintho 7:1“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Upo usemi kuwa Mungu wetu hatazami sana Mwili, lakini anatazama Zaidi Roho ya Mtu. (Hatuna budi kuwa makini na kauli hii!!)
Kutokana na kwamba asilimia kubwa ya maombi yetu yanalenga MAHITAJI YA MWILINI, basi ni wazi kuwa Mungu anaitazama pia miili yetu. Kwasababu kama mtu atamwomba Mungu Baba ampe fedha, au chakula, au makazi hayo yote si kwasababu ya “roho” kwasababu roho haili chakula, wala haivai nguo, wala haiishi kwa fedha.. bali mwili ndio unaohitaji hayo yote.
Sasa kama tutamlazimisha Mungu Baba aangalie miili yetu kwa mahitaji yetu, halafu wakati huo huo tunasema Mungu haangalii mwili, tutakuwa WANAFIKI!!.
Sasa ikiwa asilimia Zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yetu, yanalenga MIILI YETU, Basi ni wazi kuwa Mungu anaangalia Miili yetu na anajishughulisha nayo sana….
Ni lazima kulijua hili ili tusipotee na elimu ya uongo ya shetani,.. Ni lazima pia tujishughulishe kutafakari namna ya kuyafanya mapenzi ya Mungu katika miili yetu kama tu vile tunavyojishughulisha katika kumwomba mahitaji ya mwili..
1Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU mhifadhiwe MWE KAMILI, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.
Katika mstari huo biblia imetaja mambo yote matatu; Nafsi, mwili na roho. (yanapaswa yawe makamilifu, bila lawama mpaka wakati wa kuja kwake Bwana YESU).
Hivyo zingatia yafuatayo:
1. NI NINI UNAFANYA KUPITIA MWILI WAKO.
Jipime ni nini unakifanya katika mwili,.. je shughuli au matendo unayoyafanya kupitia mwili wako ni kulingana na mapenzi ya Mungu??.. Kama unafanya kazi haramu (mfano ukahaba, au kazi ya kuuza vitu haramu kama pombe, sigara, na mengineyo), basi kazi hiyo unaifanya kupitia mwili wako hivyo ibadili ili isikupeleke jehanamu ya moto.
Kama matendo unayoyafanya katika mwili ni haramu mfano uzinzi (1Wakorintho 6:18), wizi, au mauaji n.k geuka leo yasije yakawa sababu ya kukupeleka hukumuni.
2. NINI UNAKIAMBATANISHA NA MWILI WAKO
Angalia ni nini unakiambatanisha/unakishikamanisha na mwili wako.. Hapa nazungumzia aina ya mavazi na urembo na michoro (tattoo). Je mavazi uvaayo ni sawasawa na Neno la Mungu?.. Je yanaipasa jinsia yako sawasawa na Kumbukumbu 22:5.
Je mavazi unayovaa ni ya kujisitiri?, kuzuia tamaa kwa upande mwingine na kutunza heshima yako? (1Timotheo 2:9 na Mathayo 5:28)
Je michoro uichorayo na rangi yako ya asili uiondoayo ni mapenzi ya Mungu? (Walawi 19:28)
Angalia ni nini kinanin’ginia mwilini mwako.. Je hizo cheni, hereni, mikufu, bangili, vikuku n.k ni mapenzi ya Mungu?? Je si ishara ya utumwa?? (hebu soma Kutoka 21:5-6 na Kumbukumbu 15:16-17).
3. NI NINI KINAINGIA MWILINI MWAKO.
Angalia ni kitu gani unakiingiza mwilini mwako.. Je Mungu amekusudia moshi uingia katika mapafu yako ambayo yanapaswa yavute hewa safi ili kutimiza miaka uliyopewa yakuishi duniani?..
Je Mungu amekusudia uingize vilevi na madawa ya kulevya ndani ya mwili wako na kukutoa ufahamu wako kwa muda?.. Jiulize kama si ruhusa kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa umelewa/umekunywa pombe.. vipi kuuendesha huo mwili ukiwa umelewa??.. Huoni kama huo ni uvunjaji wa sheria kubwa Zaidi, kwasababu mwili ni bora kuliko gari au chombo kingine chochote cha usafiri.
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
KIJITO CHA UTAKASO.
Nini Maana ya Adamu?
WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Vazi/Nguo kiroho linawakilisha “matendo ya mtu”, maana yake kiroho mtu mwenye mavazi masafi, maana yake matendo yake ni masafi, na kinyume chake mwenye mavazi machafu maana yake matendo yake si safi (Ufunuo 19:18).
Sasa Matendo yanatunzwa, lakini pia yanafuliwa (safishwa).. kama vile nguo inavyoweza kutunzwa lakini pia kufuliwa.
1. TUNZA MAVAZI YAKO.
Maana ya kutunza mavazi ni kuhakikisha hayaharibiki wala kuwa na kasoro yawapo mwilini. Vazi lililotoboka au kuchanika maana yake limekosa matunzo mwisho wa siku yule mtu atabaki Tupu.
Vivyo hivyo ni wajibu wetu kuyatunza Matendo yetu mema, yasiharibike.. Kwa kujiangalia mazingira tuliyopo na mambo tuyafanyayo…
Ufunuo 16:15” (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, NA KUYATUNZA MAVAZI YAKE, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”.
Vitu vinavyoharibu matendo yetu mazuri/tabia nzuri ni pamoja kampani tulizonazo na mazungumzo tuzungumzayo..
1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”.
Chunguza makundi uliyonayo na aina ya mazungumzo unayozungumza.
2. FUA NGUO ZAKO.
Nguo isiyofuliwa inapoteza umaridadi na unadhifu kwa mtu, hata kama haijaharibika au kuchanika. Vile vile Matendo yasiyofuliwa yanapoteza unadhifu wa mtu kiroho.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.
Sasa mtu anafuaje Matendo yake?… Si kwa njia nyingine Zaidi ya kuomba na kusoma Neno.
Na Utajuaje matendo yako yameanza kuingia dosari?.. si kwa kusubiri uambiwe na mtu au watu, bali kwa kusoma Neno (biblia). Unaposoma Neno ndipo utakapojijua kama una kasoro au la!, kwasababu Neno la Mungu ni kioo.. Ili ujijue kama una uchafu mwilini, si kusubiri uambiwe, kwasababu si wote wenye ujasiri wa kukwambia kasoro zako.
Kitu pekee kitakachoweza kuutambulisha uchafu usoni mwako ni KIOO
na ni lazima usomaji wa Neno uambatane na maombi.
Hivyo Maombi ni “Maji” na Neno la Mungu ni “sabuni” kwa mambo hayo, matendo yetu yatakuwa safi daima.
Bwana atuongezee Neema yake.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
MAVAZI YAPASAYO.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
JE! UNA MHESHIMU MUNGU?
Kijeshi kushindwa kumtambua adui yako mpaka adui yako anajitambulisha kwako tena mbele ya macho yako ni ishara kubwa ya kushindwa mapambano.
Ndivyo ilivyokuwa kwa wale askari, walipofika na ujasiri wao mwingi, wakiwa na wazo la kumkamata mlengwa wao, tunaona mambo yalikuwa ni tofauti, kwasababu viashiria na matarajio yaliyokuwa kichwani mwao, hayakuweza kumfunua ni nani miongoni mwao ndiye mlengwa, huwenda wengine walidhani hayupo amekimbilia mapangoni kama Daudi. Lakini Yesu baada ya kuona wanahangaika sana ndipo akawauliza mnamtafuta nani.. Na wao kwa ujasiri wakajibu Yesu Mnazareti.. Yesu akasema ni mimi hapa! Tusome;
Yohana 18:3-8
[3]Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
[4]Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta?
[5]Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
[6]Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.
[7]Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.
[8]Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
Hivyo kibinadamu kwa taarifa hizo za ghafla nguvu lazima zikuishie, na kunyong’onyea ujikutapo kwenye mazingira kama hayo. Ni mfano tu wa ile habari ya Elisha (2Wafalme 6:8-23), Mfalme wa Shamu alituma majeshi kwenda kumkamata kwasababu alikuwa anatoa siri za ufalme wake kwa mfalme wa Israeli. Na hiyo ikapelekea washindwe sana mbele ya wayahudi. Lakini tunaona walipomfuata Elisha, alimwomba Mungu jeshi zima lipigwe upofu wasimtambue. Ndipo Elisha akalipeleka hilo jeshi katikati ya mji. Na baadaye akaomba wafumbiliwe macho, wakafumbuliwa wakagundua kumbe adui yao ndiye aliyekuwa kiongozi wao wa mbele.
Nguvu ziliwaishia kujikuta katikati ya maadui zao, wakifahamu kinachofuata ni kifo. Lakini Elisha hakuagiza wauliwe, bali aliwaombea kwa mfalme wapewe chakula wale wanywe kisha waondoke. Ndipo walipoondoka, hawakurudi tena kuwasumbua Israeli kwa kipindi kirefu. Kwasababu waliwapaliwa makaa ya moto kichwani.
Inamfunua Kristo kwa wakati ule, maadui zao walipofika pale bustanini, hakuwaua kwasababu alikuwa na uwezo huo, lakini alipokatwa sikio, mmojawapo wa wale askari alikuwa radhi kumponya, (kumfanyia huduma).
Na zaidi sana alikuwa tayari kuondoka na wale askari kuuawa nao, jambo ambalo Elisha hakufanya. Ili tu yeye afe taifa zima lipone..ni upendo wa namna gani huu usioweza kuelezeka aliuonyesha!.
Na kwa kifo chake hawakupona wayahudi tu, bali mpaka ni sisi watu wa mataifa kwa vizazi vyote, tumepona. Utukufu na heshima ni zake milele na milele.
Kwa hitimisho ni kuwa wale askari waliorudi nyuma wakaanguka chini, haikuwa bure hure, yote hiyo ilikuwa ni kufuatana na mwitikio wa Yesu kwao ambao hawakuutazamia.
Ni kutufundisha kuwa mawazo ya Mungu, sio mawazo yetu, rehema zake na fadhili zake na huruma zake ni nyingi kiasi ambacho kinaweza kumfanya mwanadamu aanguke na kutetemeka, kwa mwitikio wake mkuu wa upendo kwa wenye dhambi.
Je! Umempokea Kristo? Kumbuka lengo lake ni kukuvuta ili usiangukie hukumu. Okoka leo
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)