Neno hilo utalisoma katika ule utabiri wa Yakobo kwa watoto wake, alipokuwa anawabariki, na alipofikia kwa Dani, yeye alimfananisha na Bafe. Swali ni je Huyu bafe ni nani?
Tusome
Mwanzo 49:17 Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. 18 Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana.
Bafe ni nyoka aina ya kifutu. Hivyo Yakobo alimwona Dani kama nyoka, ambaye ijapokuwa maisha yake ni ya mavumbi, lakini ameng’ata farasi kisigo hatimaye farasi Yule akashindwa kuendelea na hapo hapo mpanda farasi naye akashindwa kuvifikia vita vyake.
Akimaanisha kuwa Dani anaweza dharaulika, lakini ana wokovu mkuu kwa watu wake, pale ambapo wangetarajia mpanda farasi arushiwe mikuki na majeshi ya watu, au avamiwe kijeshi, yeye anauma tu kisigo cha farasi wao, sumu inaingia na nguvu yao inaisha.
Ni kufunua kuwa kila mmoja wetu amepewa karama yake tofauti na mwingine, na kama ikitumika kifasaha huweza kumweka adui chini, sawa tu na zile karama ambazo huonekana zina heshima mbele ya macho ya watu kama vile, utume, uchungaji, uinjilisti n.k.
Kamwe usidharau karama yako, kumbuka sikuzote vile visivyoonekana kwa urahisi ndio huwa vina umuhimu mkubwa. Unaweza usiwe mguu au mkono, lakini ukawa moyo, au figo, vilivyojificha ndani, ambavyo tunajua uthamani wake ulivyo.
Halikadhalika, katika Baraka zile, Yuda aliitwa simba, Isakari aliitwa punda, Dani aliitwa Bafe, Lakini wote waliitwa Israeli. Taifa la Mungu.
Je ! unaitumia vema karama yako, au umeidharau? Na kutamani za wengine?
Kwa msaada wa jinsi ya kuitambua karama yako fungua hapa >>> NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
UFUNUO: Mlango wa 6(Opens in a new browser tab)
Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)MIHURI SABA(Opens in a new browser tab)
Rudi Nyumbani
Print this post