SWALI: Je andiko hili humaanisha nini? kupata mke ni kujipatia kibali cha kumkaribia Mungu tofauti na hapo mwanzo?
Mithali 18:22
Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
JIBU: Andiko hili hutafsiriwa vibaya na watu wengi, wakiamini kuwa pale mtu anapoingia kwenye ndoa basi ndio amejizidishia kibali cha kukubaliwa na Mungu katika maisha yake. Jibu ni hapana, kibali kwa Mungu sio ndoa, kibali kwa Mungu ni “kufanya vema mapenzi ya Mungu” .
Mungu alimwambia kaini maneno haya
Mwanzo 4:7
[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Zaidi pia, maandiko yanaeleza ipo nafasi kubwa kwa mtu kumkaribia Mungu anapokuwa hajaoa/kuolewa kuliko yule aliyeoa au kuolewa.Kwasababu ambaye hajaoa/ olewa hupata nafasi ya kutosha kumtafuta Bwana na kumfikiria yeye ampendezeje.
1 Wakorintho 7:32-33
[32]Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; [33]bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
[32]Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
[33]bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
Lakini je! andiko hilo humaanisha kibali gani?
“Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA”.
Tafsiri ya Neno hilo ni kuwa Mungu analikubali jambo hilo (Ndoa), analibariki, na pia analiona ni jema. Hivyo mtu asidhani kuwa aingiapo katika ndoa atamkosea Mungu, au Mungu atapunguza ukaribu naye. Hapana, kinyume chake atapata kibali tu. Hivyo awe na furaha na amani afanyavyo hivyo.
kwasababu pia zipo faida zinazoambata na mtu aliyeoa, mojawapo ni kujiongezea heshima kwa jamii lakini pia kuaminiwa zaidi. Na hilo ni jema hususani katika utumishi & huduma.
Lakini haimaanishi kuwa unapooa ndio Mungu anakukubali zaidi ya ule wakati ambao ulikuwa hujaoa/kuoelewa, au zaidi ya yule mtu ambaye hafikirii kuoa.
Mtume Paulo, Barnaba hawakuoa na zaidi mwokozi wetu Yesu Kristo hakuoa lakini tunaona ni jinsi gani walivyojirahisishia nafasi zao kwa Mungu.
kwa mafundisho zaidi kuhusu ndoa pitia masomo chini;
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MAFUNDISHO YA NDOA.
MWANAMKE UKITAKA KIBALI, USIWE MTU WA KUPENDA VITU. (Esta 2:17)
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya;
Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
JIBU: Kwa kawaida kipindi cha hari ( kiangazi), huwa ndio kipindi cha mavuno mengi. kwasababu mavuno yanakuwa yameshakomaa na kukauka.
Hivyo wakulima wengi kwa nyakati hizo wanakuwa mashambani kuvuna, kama vile tu walivyokuwa wakati wa masika walipokuwa wanapanda..
Na ni kipindi ambacho mkulima hufurahi pia kwasababu anakwenda kuona matunda ya kazi yake wakati si mwingi.
Lakini ni ajabu kuona, mtu ambaye hajasumbukia kupanda, halafu anaambiwa tu yeye akavune, tena kwa faida yake mwenyewe akauze, anaona uvivu kwenda kuvuna, hataki kabisa kwenda kujishughulisha na kazi hiyo, mpaka msimu mwingine unakuja, mazao yanaharibikia yote shambani. Mtu kama huyo utamchukuliaje? Ni sawa tu akiitwa “mwana mwenye kuaibisha”, Kwasasababu ni uvivu wa makusudi.
Sasa jambo kama hili kwasasa lipo pia rohoni.
Na lipo kwa namna mbili.
Bwana Yesu alisema..
Yohana 4:35-38
[35]Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. [36]Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. [37]Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. [38]Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
[35]Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
[36]Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja.
[37]Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine.
[38]Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
Umeona? Kufuatana na vifungu hivyo Bwana anatuonyesha kuwa tupo wakati wa mavuno sasa, wakati wa hari, wa kiangazi, mashamba yamekwisha kuwa meupe, Hivyo sote kwa pamoja kwa moyo mmoja yatupasa tutoke tuanze kuifanya kazi ya Mungu bila ulegevu kwasababu Yesu alishatupa agizo kuu kuwa tutoke tuenende ulimwenguni kote kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi.
Lakini ukilala na kusema huu si wakati, ndugu ni sawasawa na hilo neno unakuwa mwana mwenye kuaibisha. Kila mmoja wetu ameitwa kuwahubiria wengine habari njema za wokovu wa Yesu Kristo, haijalishi upo ofisini, shuleni, ugenini, jeshini, una wajibu wa kuvuna. Shika mundu yako washuhudie wengine habari njema, kwasababu huu ni wakati sahihi, na hautadumu milele.Hivyo tumia muda vizuri.
Neno la Mungu linasema..
Mhubiri 12:1
[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
na pia linasema..
1 Yohana 2:14
[14]Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Katika umri wako wa ujana ambao una nguvu ndio wakati wa kwenda shambani kumtumikia Bwana wako. ndio wakati wako wa hari, lakini unapokuwa mlegevu, hujishughulishi na Mungu wako, unachowaza ni anasa, starehe, mihangaiko, unasema nitamtumikia Mungu uzeeni, fahamu kuwa wewe ni sawa na mwana mwenye kuaibisha, kwasababu wakati huo utakuwa umeshapita.
Komboa wakati wako, thamini majira uliyopo, etende kazi ya Bwana.
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
Maana ya Mithali 25:25 Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu
Nini maana ya Mithali 16:30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;
Swali: Huyu Kuhani wa Oni ambaye binti yake aliolewa na Yusufu, tunayemsoma katika Mwanzo 41:45 je alikuwa ni kuhani wa Mungu au wa kuhani wa miungu ya kiMisri?
Jibu: Terejee mistari hiyo…
Mwanzo 41:45 “Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti POTIFERA, KUHANI WA ONI, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri”.
“Oni” lilikuwa ni eneo katika nchi ya Misri, kama vile ilivyo Mwanza, au Lindi nchini Tanzania au Nakuru Kenya.
Mji huu (wa Oni) Ulikuwa ni mji wa miungu ya kiMisri, na nchi ya Misri yote ilikuwa ni nchi inayoabudu miungu mingi, ikiwemo Bethshemeshi (soma Yeremia 43:13), sanamu za ng’ombe (1Wafalme 12:28) na mingine mingi (soma Yoshua 24:14).
Hivyo huyu kuhani “Potifera” hakuwa kuhani wa Mungu wa mbingu nan chi (YEHOVA), bali alikuwa ni kuhani wa miungu ya kimisri iliyokuwepo hapo “Oni”, na Yusufu alipofika kule alipewa binti yake awe mkewe.
Na Kwanini ulikuwa hivyo?(yaani kwanini Farao amchagulie mke na si Yusufu ajitafutie mwenyewe?)..
Jibu ni kwamba Farao aliona njia pekee ya kumheshimisha Yusufu na kumfanya apate kibali katikati ya waMisri ni kumuunganisha yeye na familia za watu wa kubwa na wenye hadhi wa nchi ya Misri.(wenye hadhi za kiimani), kwasababu naye Yusufu alikuwa mtu wa kiimani.
Hivyo na mtu wa kiimani na kidini aliyekuwa mkubwa huko ni huyo kuhani wa Oni, ndipo akapewa binti yake aliyeitwa Asenathi. Lakini hata baada ya Yusufu kupewa mwanamke huyo bado hakufuata miungu hiyo ya kiMisri, na Farao alilijua hilo, na wala hakumpatia huyo binti kwa lengo la kugeuza Imani ya Yusufu, bali kumheshimisha.
Lakini kwasababu pia ilikuwa ni mpango wa Mungu iwe hivyo (Yusufu aoe mwanamke wa kimataifa) basi hata mke aliyempata alikuwa ni sahihi kwake na wala hakumsumbua Yusufu baada ya hapo (huwenda hata alimtumikia Mungu wa Israeli baada ya hapo), na Zaidi sana tendo la Yusufu kumwoa Asenathi (binti wa kimataifa) limebeba ufunuo mkubwa juu ya Bwana YESU KRISTO na BIBI-HARUSI WAKE (yaani kanisa).
Kwa urefu marefu juu ya ufunuo wa maisha ya Yusufu fungua hapa >>>Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
Musa aliua lakini bado Mungu alimchangua kuwaongoza wana wa Israeli, je! Mungu anaruhusu mauaji?
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.
Ni lini na wapi Ibrahimu aliiona siku ya Bwana akashangilia?.
WhatsApp
Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe daima. Karibu katika mafundisho ya biblia, Neno la Mungu wetu lililo Taa na Mwanga wa Njia zetu (Zab.119:105).
Zipo njia Mbili tu zilizowekwa mbele ya kila mwanadamu, Nazo ni njia ya UZIMA, na njia ya MAUTI.
Yeremia 21:8 “Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu NJIA YA UZIMA, na NJIA YA MAUTI”.
Njia ya Uzima, inamwongoza mtu “Uzimani”..na Njia ya Mauti inamwongoza mtu “Mautini (ziwa la moto)”.
Njia ya Uzima imenyooka haina migawanyiko mingi (sawasawa na Yohana 14:6), ambapo Bwana YESU alisema yeye ndio hiyo “Njia”, na mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye.
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”
(Maana yake hakuna njia mkato wala njia mbadala ya kumfikia Baba)…Ni moja tu! Tena iliyonyooka, nayo ni YESU KRISTO, na si kupitia mtu mwingine yoyote mashuhuri, au mtakatifu mwingine yoyote aliye hai au aliyekufa au nabii yoyote katika biblia.
Lakini ile ya Mauti inamigawanyiko mingi, inaanza kama njia moja lakini mwisho wake inamigawanyiko,
Mithali 14:12 “IKO NJIA ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni NJIA ZA MAUTI”
Hapo anamaliza na kusema mwisho wake ni “NJIA ZA MAUTI” na si “NJIA YA MAUTI” kana kwamba ni moja, bali nyingi. Na njia ya Mauti si mwingine Zaidi ya “shetani”…Kama jinsi njia ya UZIMA ilivyo Bwana YESU kadhalika njia ya Mauti ni “shetani”.
Na shetani anaabudiwa kupitia vitu vingi, anaweza kuabudiwa kupitia miti, mawe, udongo, au kupitia vitu vitu vingine kama fedha, watu, dini n.k..ndio maana hapo biblia inasema hiyo Njia (shetani) mwisho wake ni “Njia za Mauti” (maana yake zipo nyingi).
Na hiyo ndio sababu pia kwanini biblia inataja uwepo wa milango mingi ya kuzimu (Soma Mathayo 16:18). Milango ya kuzimu ndio hizo njia zote zinazoweza kumpeleka mtu kuzimu.
Nabii Isaya amezidi kuziweza vizuri njia hizi kwa ufunuo wa Roho… Amezitofautisha kama “NJIA” pamoja na “NJIA KUU”..
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na NJIA KUU, na NJIA….”
“Njia Kuu” ni “Njia ya Uzima”…. Na “Njia” pekee yake “Ni njia ya Mauti”..
Lakini anaendelea kusema… hiyo “Njia kuu” itaitwa Njia ya utakatifu, na ya watu wasafirio..
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio….”
Maana yake wote wanaiendea hiyo njia ya Uzima (YESU) Ni lazima “utakatifu” uwe muhuri wao sawasawa na kitabu kile cha Waebrani 12:14.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”.
Vile vile ni lazima wawe “wasafiri”.. Tabia ya msafiri huwa anadumu katika chombo cha usafiri awapo safarini, na hawezi kujishikisha na mambo akutanayo njiani au barabarani…. na chombo chetu cha usafiri ni NEEMA YA MUNGU. Tuwapo katika safari hii ya kwenda mbinguni kupitia njia ya Bwana YESU, mambo ya ulimwengu hayapaswi yashikamane na sisi.
1Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho”.
Na mwisho anasema.. “wajapokuwa wajinga hawatapotea katika njia hiyo”
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO”.
Ikiwa utaonekana mjinga kwa kuwa umeamua kuifuata NJIA KUU ya UTAKATIFU na umeamua kuishi kama MSAFIRI duniani, basi biblia inasema “hautapotea/hatutapotea” katika njia hiyo..
Haijalishi dunia nzima itakuona kama umepotea, umerukwa na akili, umechanganyikiwa…Mungu yeye anakuona upo katika njia sahihi na una hekima nyingi.. kwasababu mwisho wa njia hiyo ni UZIMA WA MILELE, Na Utakutana na Bwana naye atakufuta machozi.
Ufunuo 7:15 “Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao 16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. 17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.”
Ufunuo 7:15 “Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao
16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.
17 Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.”
Je wewe leo umechagua njia ipi??… Njia kuu ya Uzima? Au Njia ya Mauti..
Kumbukumbu 30:14 “Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya. 15 ANGALIA, NIMEKUWEKEA LEO MBELE YAKO UZIMA NA MEMA, NA MAUTI NA MABAYA”.
Kumbukumbu 30:14 “Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.
15 ANGALIA, NIMEKUWEKEA LEO MBELE YAKO UZIMA NA MEMA, NA MAUTI NA MABAYA”.
CHAGUA NJIA YA UZIMA, na TEMBEA KATIKA NJIA KUU YA UTAKATIFU.
BWANA AKUBARIKI.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?
KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI
(Masomo maalumu kwa wazazi/walezi).
Ni nini unafanya kama mzazi uwapo nyumbani?.. Je maisha yako ndani ya kanisa ni sawa na yale nje ya kanisa?..Je kile unachokifanya kanisani ndicho unachokifanya nyumbani?…je nyumbani kwako ni sehemu ya kuishi tu au ni sehemu pia ya ibada?.
Kama wewe ni mwalimu kanisani, ni lazima pia uwe mwalimu nyumbani kwako…kama wewe ni kiongozi katika nyumba ya Mungu ni lazima pia uwe kiongozi katika nyumba yako, kama wewe ni mchungaji katika nyumba ya Mungu ni lazima pia uwe mchungaji katika nyumba yako mwenyewe…Ndivyo biblia inavyotufundisha.
Mitume wa Bwana YESU ni kielelezo kwetu, wao walikuwa wakihubiri Neno HEKALUNI NA NYUMBANI, kama maandiko yanavyosema, hivyo kama na sisi tumejengwa juu ya msingi wao ni lazima tufanye kama wao walivyofanya..
Matendo 5:42 “Na kila siku, NDANI YA HEKALU na NYUMBANI MWAO, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo”.
Umeona?.. Si hekaluni tu!, bali hata nyumbani…. Uharibifu mkubwa shetani anauanzia nyumbani… Hivyo ni lazima uwe na AMRI, katika nyumba yako mwenyewe… Ni lazima pafanyike ibada nyumbani kila siku, ni lazima pafanyike maombi, ni lazima watoto na wengine wanaoishi katika nyumba yako wajue kuomba na kuombea wengine.
Ni lazima watoto wajifunze biblia na kufundisha biblia tangu wakiwa wadogo, ni lazima pia wajifunze kutoa.. ni lazima wote wawe wa kiroho, ni lazima uwafundishe wawe vipaumbele katika Imani wawapo shuleni, maana yake wakiwa shuleni wawe vipaumbele katika kuongoza maombi kwa wanafunzi wenzao, na kuomba vile vile kufunga… Na si kuwaacha jumapili kwa jumapili tu wafundishwe kanisani hayo mambo..
Jenga tabia ya kuwafuatilia mienendo yao ya kiimani wakiwa mashuleni, fuatilia sifa zao za kiimani wawapo mashuleni, (na si tu taaluma yao)..wapo watoto taaluma zao zinaonekana nzuri lakini shetani kashawaharibu kitabia muda mrefu (matokeo yake yatakuja kuonekana baadaye).
Hivyo kama mzazi au mlezi, simama katika hiyo nafasi… kiasi kwamba NENO LA MUNGU nyumbani kwako ni AMRI sio OMBI!. Kama Nabii Yoshua alivyoazimia zamani zile..
Yoshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; LAKINI MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA. 16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine”.
Yoshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; LAKINI MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA.
16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine”.
KUOTA UPO KANISANI.
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
Mafundisho maalumu kwa watumishi wa Mungu na Watenda kazi wote katika shamba la Bwana.
Maombolezo 2:19
[19]Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa makesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; KWA UHAI WA WATOTO WAKO WACHANGA WAZIMIAO KWA NJAA, Mwanzo wa kila njia kuu.
Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi unaelewa ni uchungu mwingi kiasi gani unakupata pale unapoona mtoto wako anaangamia kwa kukosa mahitaji yake muhimu, mfano wa chakula. Ndicho kilichotokea kwa mama Hajiri siku alipofukuzwa kwa Ibrahimu, akiwa kule jangwani amepotea hali ilikuwa mbaya sana, kwani chakula na maji viliwaishia kabisa, huwenda zilipita siku kadhaa hawakuona dalili yoyote ya kupata msaada. Hivyo alichokifanya Hajiri, ni kwenda mbali kidogo na kumlilia sana Mungu wake, na Mungu akasikia, akaonyeshwa palipo na maji, akaenda kumpa mwanae, kuonyesha ni jinsi gani alivyouthamini uhai wa Ishmaeli.
Mwanzo 21:14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba. 15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja. 16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, AKAPAZA SAUTI YAKE, AKALIA. 17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. 18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa. 19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
Mwanzo 21:14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, AKAPAZA SAUTI YAKE, AKALIA.
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
Umeona kama Hajiri asingemtafuta Mungu katika hali ile, ni wazi kuwa Yule kijana ambaye alikuwa amekusudiwa awe taifa kubwa angefia jangwani na yale maono yasingetokea.
Ndicho tunachojifunza katika vifungu hivyo, kwenye kitabu cha Maombolezo, anasema kesha, ulie, kwa ajili ya watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa. Leo hii tuna watu wengi ambao wameokoka kwa kuisikia injili yetu. Lakini je, watu hao wanasimama au wanakufa?, Unapomhubiria mtu, hatutakiwi kusema yaliyobaki namwachia Mungu, bali ni kuhakikisha hafi kiroho kwa kukosa chakula cha uzima. Na hiyo inakuja kwa kuendelea kumfuatilia kumfundisha, Lakini zaidi sana KUMWOMBEA kwa Mungu usiku na mchana akue kiroho.
Tukiiga mfano wa Epafra jinsi alivyokuwa akiwaombea sana watu wa kolosai walioamini kwa injili yao.
Wakolosai 4:12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.
Umeona? Ukomavu wa watu walio wachanga wa kiroho hutegemea sana maombi ya kina kwa waliowazaa. Hivyo wewe kama mtenda kazi hakikisha unakuwa na maombi mengi kwa ajili ya wale uliowahubiria injili wakaokoka vinginevyo watakufa kiroho, katika ulimwengu huu wa njaa na kiu ya Neno la Mungu, tenga masaa kuwaombea. Na maombi hayo yawe ya rohoni kabisa, sio ya juu juu, bali ya kuzama, ili Mungu awakuze, na matokeo ya kazi yako utayaona tu baada ya kipindi fulani, jinsi watakavyozidi kubadilika na kukomaa kidogo kidogo, hatimaye kuwa watumishi imara katika shamba la Mungu.
Shalom.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
NJAA ILIYOPO SASA.
LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.
SWALI: Nini maana ya
Mithali 25:25 Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu, Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
JIBU: Biblia inalinganisha burudiko kubwa mtu analolipata pale anaposikia habari fulani njema na mfano wa mtu mwenye kiu halafu ghafla akaletewa kikombe cha maji ya baridi, sasa katika mazingira kama hayo ni wazi kuwa maji yale atayafurahia sana kwasababu yupo katika kiu.
lakini kiini cha mstari huo ni hapo anaposema ni habari njema ITOKAYO KATIKA NCHI YA MBALI.
Tukumbuke kuwa zipo habari njema nyingi..kwamfano habari za kupewa tenda fulani ya kibiashara ni habari njema, habari za kufaulu darasani ni habari njema, habari za kuzaliwa mtoto duniani ni habari njema, habari za kupandishwa cheo ni habari njema n.k…lakini zote hizi hazina jipya kwasababu ni za hapa hapa tu duniani.
Bali zipo habari njema zinazotoka katika nchi ya mbali na huko si kwingine zaidi ya MBINGUNI, hizo ndizo watu wana kiu nazo, wakizisikia tu ni lazima mioyo yao ni lazima iburudike sana.
Na habari zenyewe ni zile zinazomuhusu Yesu Kristo.
Alisema.
Yohana 6:33-35
[33]Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. [34]Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki. [35]Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
[33]Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.
[34]Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.
[35]Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
Yesu ndio maji yakatao kiu, alileta habari njema iliyotoka mbinguni, alikuja kutuletea ukombozi na msamaha wa dhambi, alikuja kutufungua katika vifungo vyetu, na shida zetu mbalimbali, na kutumwagia karama za rohoni, mambo ambayo mwingine yoyote hawezi kutoa. Lakini zaidi sana alikuja kutuambia habari za ufalme wake, kwa habari ya mambo yanayokuja, kuhusu mbingu mpya na nchi mpya, na Yerusalemu mpya, na umilele, na uzuri na thawabu alizotuandalia sisi tuliomwamini. Mambo ambayo ukisikia kama wewe unapenda kweli maisha…utayafurahia sana.
hivyo yatupasa mimi na wewe tuwe na mwitikio huu, wa habari hizi njema kwa kuwashuhudia pia na wengine maji haya, kwasababu ni wazi kuwa wengi wana kiu, na hivyo wanahaja ya kuzisikia hizi habari njema zimuhusuyo Yesu Kristo.
Sote kwa pamoja tuamke tukahubiri injili. Tukijua kuwa inahitajiwa sana.
shalom
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
INJILI NI NINI?
Maana ya Mithali 17:22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu, lililo Taa ya njia zetu na Mwanga wa njia yetu (Zab. 119:105).
Zipo aina tatu (3) za sanamu zinazoabudiwa na watu.
1.Sanamu zenye mfano wa Mtu
2.Sanamu-watu
3.Sanamu-vitu
Tutazame moja baada ya nyingine.
1.SANAMU ZENYE MFANO WA MTU.
Hivi ni vitu vyote visivyo na uhai vyenye mfano wa mtu, ambavyo vinatengenezwa na watu kwa lengo la kuabudiwa.
Tabia ya hizi sanamu kulingana na biblia ni kwamba zina midomo lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni, zina masikio lakini hazisikii, zina pua lakini hazinusi..na wanaoziabudu wanafanana na hizo kiroho.
Zaburi 115:4 “Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. 5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, 6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, 7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. 8 Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia”
Zaburi 115:4 “Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.
5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,
6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu,
7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.
8 Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia”
Hizi ndio zile zote zinazoabudiwa na wapagani, pamoja na baadhi ya madhehebu yajiitayo ya kikristo. Utakuta sanamu imewekwa ndani ya nyumba ya ibada, na watu wanakwenda kuiangukia na kuisujudia, hata kuitolea sadaka na kuiomba, jambo ambalo ni machukizo makubwa..
Ni dhambi kubwa kusujudia sanamu yoyote ile, Kasome Kutoka 20:1-6.
2. SANAMU-WATU.
Hii ni aina ya pili ya sanamu ambayo ni tofauti kidogo na ile ya kwanza… ile ya kwanza ina midomo lakini haisemi, ina macho lakini haioni, ina masikio lakini haisikii…. Hii ya pili nayo ni hivyo hivyo, ina macho lakini haioni, ina masikio lakini haisikii, ina macho lakini haioni..tofauti tu ni kwamba ile ya kwanza ile ya kwanza haipumui ila hii ya pili inapumua, ile ya kwanza imetengenezwa kwa miti, udongo, chuma, fedha au dhahabu lakini hii ya pili ni Wanadamu.
Sasa tunaisoma wapi katika biblia…
Ezekieli 12: 1 “Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, WATU AMBAO WANA MACHO YA KUONA, ILA HAWAONI, WANA MASIKIO YA KUSIKIA, ILA HAWASIKII; kwa maana ni nyumba iliyoasi”.
Ezekieli 12: 1 “Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, WATU AMBAO WANA MACHO YA KUONA, ILA HAWAONI, WANA MASIKIO YA KUSIKIA, ILA HAWASIKII; kwa maana ni nyumba iliyoasi”.
Umeona? Kumbe sanamu sio tu mawe na udongo vinavyoweza kuwa sanamu bali hata watu..
Kama hujamaanisha kumfuata YESU wewe ni SANAMU.. Kwasababu una macho lakini huoni mambo ya rohoni, una masikio lakini husikii sauti ya MUNGU, Una kinywa lakini hakineni mambo ya Mungu, Hivyo wewe ni sanamu pamoja na viungo vyako vyote.
“KICHWA” chako ni sanamu/mungu wako, ndio maana unakitumikia kwa vitu vya kidunia kama YEZEBELI..
“MASIKIO” yako ni sanamu/mungu wako, ndio maana unayatumikia kwa kubadilisha vipuli kila siku.
“MACHO” yako ni sanamu/mungu wako, ndio maana unayatumikia usiku na mchana kupaka uwanja, na kupadilisha kope pamoja na kuchonga nyusi.
“MDOMO” wako ni sanamu/mungu wako, ndio maana unautumika kwa rangi na kila aina ya lipstick
“MIKONO” yako na “MIGUU” ni sanamu/mungu wako, ndio maana unaitumika kwa bangili na kucha za bandia..
“TUMBO” lako ni mungu wako ndio maana unalitumikia kwa kulinywesha pombe na kuliburudisha kwa kila linachohitaji usiku na mchana… Huna muda wa kufunga na kuomba walau kwa wiki mara moja, kwako kufunga ni adhabu kubwa!!..
Wafilipi 3:19 “mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Ikiwa hujamaanisha kumfuata YESU kila kiungo katika mwili wako ni sanamu/mungu.. Ndio maana biblia inasema tuvifishe viungo vyetu vilivyo katika nchi, maana kwa hivyo huzaa dhambi na NDIO ibada ya sanamu.
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;
6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
3. SANAMU-VITU.
Hizi ni sanamu zote zisizo na mwonekano au maumbile ya mwanadamu lakni zinaabudiwa.
Mfano wa hizi ni kazi, fedha, umaarufu, Elimu, Mali kama nyumba, magari, ardhi n.k. Mtu akiwa na hivi na hana KRISTO maishani mwake ni mwabudu sanamu tu!
KUMBUKA: Usipomwabudu MUNGU WA KWELI, basi unaabudu sanamu, na usipoabudu sanamu basi unamwabudu MUNGU WA KWELI, Hakunaga hapo katikati! Ni aidha uwe wa shetani au wa Mungu.
Kama kazi yako inaheshima kuliko Mungu kiasi kwamba unakosa hata siku moja ya wiki kumtolea Mungu wako, hiyo kazi ni sanamu/mungu kwako.
Kama elimu yako, au umaarufu wako au cheo chako kina nguvu kuliko Neno la MUNGU, basi hicho ulichonacho tayari ni mungu wako.
Je umeokoka?…Kumbuka wote wanaoabudu sanamu sehemu yao ni katika lilwe ziwa liwakalo moto na kiberiti kulingana na biblia.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, NA HAO WAABUDUO SANAMU, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?
USIMWABUDU SHETANI!
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
DANIELI: Mlango wa 3
Mithali 17:22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
JIBU: Mstari huu unatuonyesha jinsi gani hali ya moyo inavyoweza kuathiri hali za nje za mwili. Si kila wakati dawa itatibu, ikiwa moyo umepondeka afya inaweza kuathiriwa pia. Kwamfano labda mtu yupo katika nyumba au makazi ambayo hana amani, anateswa, anaudhiwa, anaabishwa, muda wote anakuwa mnyonge, utaona pia kwa namna Fulani afya yake itaathirika, labda atasumbuliwa na ugonjwa Fulani ambao hauna sababu wala chanzo.
Lakini moyo ukichangamka, hata kama huyo mtu yupo katika hali/mazingira magumu kiasi gani, mwili wake pia baada ya mda utaitikia hali ya roho yake. Na hivyo atakuwa na afya yake.
Sasa Nitaufanyaje moyo wangu uchangamke?
1) Kwa kutembea ndani ya ahadi za Mungu katika Neno lake. Mara kadhaa katika maandiko Bwana Yesu alisema” jipeni moyo”. Unapojipa moyo katika ahadi za Mungu ukijua kabisa, ni hakika atatenda, hasemi uongo, Fahamu kuwa utakuwa ni mwanzo wa kuchangamka kwako. Kwamfano ukikumbuka kuwa alisema hatatuacha wala kutupungukia, unakuwa na amani wakati wote, nyakati zote, ukiwa na vingi ukiwa umepungukiwa yote yatakuwa sawa tu, kwasababu sikuzote yupo pamoja na wewe. Furaha inakutawala.
Hata upitiapo magonjwa, ukikumbuka ahadi zake kuwa atakuponya, ukaendelea kuzishika kwa imani, afya yako hurejea.
Yeremia 30:17 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. 18 Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. 19 Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao WACHANGAMKAO; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.
Yeremia 30:17 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.
18 Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.
19 Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao WACHANGAMKAO; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.
Hivyo ishi kwa kushikilia ahadi za Mungu kwenye Neno lake, zipo nyingi sana, na zimefika katika kila Nyanja ya maisha yetu. Hakuna sababu ya kutochangamka, wakati Neno la ahadi lipo. Aliyekuahidia ni Mungu wa miungu muumba wa mbingu na nchi hakuna lolote linalomshinda, kwanini uogope?
2) Pili, kwa kupenda ushirika na wengine. Kamwe usiishushe wala kuipuuzia nguvu iliyopo ndani ya ndugu katika Kristo. Zipo nyakati utahitaji kutiwa nguvu na wenzako, hata kukaa pamoja tu, kutafakari Neno la Mungu na kumwimbia Mungu ni tiba nzuri sana, itakayochangamsha moyo wako, tofauti na kama ungekuwa mwenyewe mwenyewe tu wakati wote.
Ndivyo ilivyokuwa hata kwa Paulo, wakati ule..
Matendo 28:15 Na kutoka huko ndugu, waliposikia habari zetu, wakaja kutulaki mpaka Soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, AKACHANGAMKA.
Chuma hunoa chuma, tuwapo pamoja, tunajengana nafsi, na matokeo ya kufanya hivyo yataonekana mpaka nje.
PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.
JE! UNAIONA ILE NCHI NZURI YA KUMETA-META MBELE YAKO?
Je sisi wakristo tunaruhusiwa kufanya 40 za marehemu?
Elewa maana ya mstari huu;
Mithali 10:12 Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
Mstari huu unalenga kutufundisha sifa za kipekee sana za upendo. Ambazo zinazungumziwa pia sehemu mbalimbali.
Kwamfano hapo anasema kuchukiana hakuzai kingine zaidi ya fitina,( yaani uchongezi, na kudhuriana), lakini upendano husitiri MAKOSA YOTE. Anaposema yote. Ni kweli yote. Endapo upendo utatoka kwelikweli katika kilele chake. Hiyo ndio sifa ya ajabu ya upendo ambayo kitu kingine chochote chema hakiwezi kutoa, kwamfano imani, nguvu, mamlaka, uweza n.k. haviwezi kusitiri “makosa yote”. Ni upendo tu peke yake.
Neno hilo hilo pia limerudiwa katika agano jipya.
1Petro 4:8 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi
Ndio maana Bwana Yesu alisema Torati yote imelalia hapo, katika kumpenda mwenzako kama nafsi yako, alisema vile unavyotaka wewe utendewe watendee wenzako. Utashangaa tu, wivu unayeyuka wenyewe, hasira inakufa, vinyongo vinaondoka, mashindano yanapotea, wizi, uzinzi unafutika, kwasababu umegundua kuwa mwenzako ni kama hiyo nafsi yako mwenyewe, kama vile wewe unavyopenda kufanikiwa vivyo hivyo usichukie kuona mwenzako amefanikiwa.
Lakini Jambo hili linaweza kutoka ndani yetu kwa njia tatu. Ya kwanza ni kujazwa Roho Mtakatifu. Kwasababu tunda mojawapo la Roho Mtakatifu ni upendo (Wagalatia 5:22). Hivyo unapokuwa mwombaji sana, hususani wa “masaa” sio dakika, unajazwa Roho Mtakatifu vema. Na matokeo yake ni kuwa urahisi wa kuudhihirisha upendo unakuja.
Lakini hilo peke yake halitoshi, unapaswa uambatanishe na usomaji wa Neno kila siku. Neno ni njia nyingine ya Roho Mtakatifu kukukumbusha, yale unayopaswa kufanya, kwamfano ukidhihirisha hasira ukisoma Neno utajifunza uvumilivu, utajifunza unyenyekevu, kuachia, na madhara ya kutokusamehe. Hivyo litakufanya uweze kurejea kwenye mstari haraka pale unapokaribia kuteleza. Usipuuzie kusoma Neno kila siku.
Tatu, ni kutendea kazi. Lazima ujiwekee malengo. Kwasababu ukiwa mwombaji tu, na msomaji peke yake bado haitakusaidia sana , kama huna mikakati ya kukifanyia kazi. Ndio maana hapo anasema iweni na JUHUDI nyingi katika kupendana,.Juhudi ni lazima yaani unaanza kuchukua hatua ya kushindana na vipinga-upendo, na hapo hapo utaanza kuona, wepesi umekuja ndani yako,
Sisi kama watoto wa Mungu, tumeagizwa tukue kila siku kuufikia upendo wa ki-Mungu ndani yetu. Ndio ukomavu wetu na kilele cha imani yetu. Kwasababu hii ndio dawa ya dhambi zote.(2Petro 1:5-11)
Bwana atuongezee neema.
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?