Zaburi 22:1 Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? 2 Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati.
Maneno haya ukiyatafakari, utagundua ni ya mtu aliyefikia hatua mbaya sana ya kukaribia kukata tamaa kwasababu ya aidha magumu, au huzuni, au mateso yasiyoelekeza anayoyapitia, akiangalia kulia, haoni tumaini lolote, akiangalia kushoto haoni mkono wowote wa Mungu ukimsaidia licha ya kuomba na kulia sana, kwa muda mrefu.
Sehemu nyingine anasema, amekataliwa kila kona, amekuwa kama msikwao kwa ndugu zake.
Zaburi 69:10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. 11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. 12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. 13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. 14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. 15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu. 16 Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. 17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
Zaburi 69:10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu.
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. 12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. 13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. 15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
16 Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. 17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
Mwandishi huyu alikuwa ni Daudi, alipitia kipindi kirefu sana cha kujiona kama vile Mungu kamtupa, hadi kuna wakati akaona heri aende kuomba hifadhi kwa maadui zake wafilisti ambao hapo mwanzo aliwafukuza na kuwaita makafiri (wasio tahiriwa), lakini safari hii kwa unyenyekevu wote, anaenda kuwa mmoja wa askari wao, ili tu apate hifadhi, asiangamie kabisa. Huyo ni mtu ambaye maji ya shingo yalimfikia kwelikweli.
Sio kwamba alikuwa haombi, au hamlili Mungu?. Au kwamba ana dhambi kuliko wengine, mpaka awe mtu wa bahati mbaya hivyo Hapana, nyakati zote alikuwa mwombaji, lakini akafika mahali katika uhalisia wa kibinadamu aliona kama Mungu amemwacha kabisa.
Lakini kwasababu huruma za Mungu zilikuwa nyingi juu yake alimpa moyo mkuu, wa kuendelea kumngoja Bwana. Ndio maana sehemu nyingi katika Zaburi anasisitiza sana Neno hili ‘mngojeeni Bwana’ (Zaburi 37:7, 25:3, 31:24,38:15, 40:1).
Sasa moja ya maneno machache ya Daudi yaliyonikuliwa na Bwana Yesu lilikuwa ni hili.
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27: 45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. 46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Mathayo 27: 45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Je! Unadhani kauli hiyo Yesu aliyoitoa alimaanisha kweli ameachwa?
Hapana, tangu mwanzo alikuwa anajua Mungu yupo pamoja naye, na kwamba saa yake imekaribia, muda si mrefu anakwenda kuinuliwa na kutukuzwa, tena sehemu nyingine anasema alishangalia pale msalabani (Wakolosai 2:15). Lakini kuinukuu kauli ile ni kuonyesha ubinadamu wetu, unavyoweza kutuhubiria tuwapo katikati ya shida, kwamba Mungu ametuacha hususani pale tunapopitia shida, na mateso.
Yesu alinukuu ubinadamu wetu kukumbuka mfano wa yale aliyoyapitia Daudi..
Lakini tunaona dakika chache baada ya pale, pindi tu alipokata roho, makaburi yakapasuka, wafu wakatoka makaburini, pazia la hekalu likapasuka, na baada ya siku tatu akafufuka, ukombozi wetu mkuu ukapatikana, ‘Lakini ni kwa maneno ya kudhaniwa kuwa Mungu amemwacha’.
Mathayo 27:50 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Mathayo 27:50 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka;
miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Ndugu, upitiapo hatua hizo ambazo mawazo yako yanakufundisha kuwa Mungu hayupo na wewe tena, amekuacha, kwasababu ya shida unazozipitia muda mrefu, magonjwa yasiyokoma, umeomba mpaka umechoka, umelia hadi ukomo,wewe ona ni kawaida,…. Piga moyo konde Mngojee Bwana. Daudi alistahimili hatimaye akathibitishwa kwenye ufalme ambao ulidumu pamoja na vizazi vyake vingi tofauti na wafalme wengine wa Israeli. Mngojee Bwana, kimaombi, kwasababu baada ya joto huja mvua.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?
kiaramu ni lugha gani? je ilizungumzwa na Yesu?
Nzi wa Misri, na Nyuki wa Ashuru vilimaanisha nini? (Isaya 7:18-20).
Print this post
Mithali 29:9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Mstari huo kwa lugha rahisi tunaweza kuuweka kwa namna hii. “Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu, akijibu kwa kicheko au kwa hasira, matokeo ni yaleyale tu hakuna amani au suluhisho”
Unafunua sifa za mpumbavu, kwamba sikuzote mwitikio wake wowote hauwezi kuleta mabadiliko. Kwamfano labda hoja imetolewa na ikamuumiza kiasi cha kumfanya ajibu kwa hasira. Sasa wewe waweza tarajia pengine jambo hilo limemgusa kweli moyo, litambadilisha lakini matokeo yake ni kwamba anakuwa vilevile, Halikadhalika waweza kutoa hoja ikamfanya acheke ukitarajia kitaambatana na badiliko lolote ndani yake lakini hakuna.
Maana yake mpumbavu, haguswi kwa ukali au kwa wepesi wa maneno ya aina yoyote…Na hivyo ni kuachana naye Tu.
Tukiachia wapumbavu wa kawaida tunaowafahamu..Mpumbavu hasaa ni yule mtu anayeikataa kweli ya Mungu mfano wa wale waandishi na mafarisayo wakati wa Bwana Yesu (Mathayo 23:17), mtu wa namna hii unapomuhubiri injili, hata imchomeje au imchekesheje hawezi kufikiri hata chembe kubadilika, kinyume Chake ni mapambano tu.
Bwana Yesu alitufundisha na kutuambia kuwa si kila mtu ni wa kumtupia lulu zetu, maana yake wanaweza kutugeukia na Kuturarua. Ukiona mtu anaishia kwenye ubishi tu na mashindano, ni kuachana naye na kugeukia waliotayari kupokea.
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.
KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI.
Theolojia ni elimu ya kujifunza sifa za Mungu na mapenzi yake na jinsi anavyohusiana na wanadamu na ulimwengu kwa ujumla.
Neno Theolojia limezaliwa kutoka katika maneno mawili ya kigiriki ‘theos’, na ‘logos’
Theos likiwa na maana ya Mungu, na logos ni neno/wazo/elimu/maarifa.
Hivyo tukiunganisha maneno hayo, ni sawa kusema theolojia ni mafundisho au maarifa au elimu kuhusu Mungu.
Ni utafiti kuhusu Mungu katika mpangilio na mtiririko maalumu. Ukweli ni kwamba theolojia haiwezi kumfafanua Mungu katika ufasaha wote, ikiwa mtu ataitegemea theolojia tu kumjua Mungu, ukweli ni kwamba amepotea, lakini ikiwa itasomwa vema (si kwa lengo la kitaaluma), bali kwa lengo la kupanua upana wa fikra kuhusu Mungu na maandiko, inafaa sana katika uelewa wa nyanja mbalimbali, hususani kwa wale viongozi na waangalizi kama vile wachungaji, na wahubiri. Si lazima isomwe kwenye vyuo maalumu, mtu yeyote akitia nia kujifunza theolojia anaweza jifunza, kwa kupitia mafundisho mengi, majadiliano na waalimu walio na upeo mpana wa biblia, semina, na kujisomea mwenyewe n.k.
Na Haya ni matawi makuu ya theolojia katika kuichambua biblia.
Imejikita katika kutafiti Maudhui au fundisho kuu la biblia, inaangazia jinsi gani vitabu mbalimbali kwenye biblia, vinavyoelezea mpango wa Mungu katika nyakati tofauti tofauti tangu mwanzo hadi mwisho. Mfano kujifunza MAAGANO, katika agano la kale na jipya yalivyotenda kazi na jinsi Yesu alivyoanza kutambulishwa tangu Edeni kama mzao wa mwanamke, hadi nyakati za manabii Isaya 53, hadi wakati wa kutokea kwake duniani Luka 24:27.
Upo umuhimu wa kuijua hii theolojia kwasababu itakupa kujua kiini cha biblia ni nini? Zipo habari nyingi, hadithi nyingi, nyimbo nyingi, mifano mingi, lakini ni vema ujue maudhui zao ni zipi ili usijikute unatoka nje ya shabaha ya imani.
Inaegemea kujifunza biblia katika migawanyo maalumu ya mada, kwa mfano,
Fundisho la Mungu (theolojia),
Fundisho La Yesu Kristo (Kristolojia),
Fundisho La Roho Mtakatifu (niumatolojia),
Fundisho La wokovu (Soteriolojia),
Fundisho La kanisa,(Ekleziolojia)
La Siku za mwisho.(Esokatolojia)
La mwanadamu (Anthropolojia)
La malaika (Angeolojia)
Inajikita kujifunza jinsi maagizo ya kibiblia yanavyoweza kutendewa kazi katika,, huduma kwa mfano kuhubiri na kufundisha , katika uangalizi wa kichungaji, katika umisheni, na katika taratibu za kiibada, na katika kutoa mashauri ya kikristo kama vile kuwaonya wenye matatizo ya kiroho, kifikra, vifungo n.k.
Inaangazia jinsi gani imani ya kikristo imekuwa ikipiga hatua katika vipindi mbalimbali vya kihistoria, inaangazia mabaraza mbalimbali ya makanisa yaliyokaa katika kujadili fundisho na misingi ya imani. Kwamfano lile baraza la Nikea (325WK). Mpaka nyakati za matengenezo mfano akina Martin Luther, calvin, na wengine.
Hii inakusaidia kujua historia na chimbuko la imani yetu, na sababu ya ukristo kuonekana katika muundo huu leo.
Hii inaegemea katika ukristo na jamii, kwamfano mtazamo wa ukristo katika maeneo ya kijamii mfano ndoa, biashara, taratibu za kijamii, haki za kibinadamu, vita,
Zipo theolojia nyingine kama vile theolojia za tafsiri, za kulinganisha, za utetezi, za kifalsafa. n.k. Kwasababu ya upana wa theolojia, haya ni matawi baadhi tu, kati ya mengi. Hivyo, kama watu wa Mungu, pamoja na kutegemea Bwana kutufunulia mwenyewe maandiko, upo pia wakati ambao hatuna budi kuyamulika maandiko kiundani (Kitheolojia), tukiwa na lengo la kumjua Mungu kwa upana na sio kuwa wasomi, au wanataaluma.
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
Kwanini kuna tafsiri nyingi za Biblia, na tafsiri ipi ni sahihi?
Yesu anapoitwa mwana wa Azali, maana yake nini?
Mungu hakumchagua Musa kwasababu ya wema, au kipawa, au ujuzi fulani aliokuwa nao tofauti na wengine. Hapana almchagua ili ‘kutumiza kusudi lake la kuchagua’ ambalo tunalisoma kwa urefu katika (Warumi 9:11-17). Linalomaanisha Mungu humchagua mtu na kumfanya awe kama anavyotaka mwenyewe, na sio kwa jinsi Yule mtu atakavyo. Kwamfano alimchagua Farao, kisha akamwekea moyo mgumu,ili atimize kusudi lake mwenyewe, kujichotea utukufu kwa mapigo yale kumi,aliyoyaachia kwa wamisri, vivyo hivyo na kwa Musa alimchagua na kumpa neema ile kubwa ya hofu ya Ki-Mungu na upole ili atimize kusudi lake la kuwakomboa wana wa Israeli.
Lakini hakuwa na tendo lolote jema alilowahi kutenda lililomshawishi Mungu amchague yeye tofauti na wengine.
Na ndivyo anavyofanya hata sasa kwa wanadamu wote. Tunaokolewa na kutumiwa na Mungu kwa neema tu, na si kwasababu ya matendo Fulani mema tuliyowahi kumtendea Mungu.
Nini tofauti ya Majira na Wakati?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
(Mafunzo maalumu kwa watoto na walezi).
Kama wewe ni mtoto basi jifunze haya, na kama ni mzazi basi pia jifunze haya na pia mfunze mwanao…
Mambo ya Walawi 19:3 “Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu”
Biblia imetumia neno “kumcha” kuonyesha msisitizo wa jambo hilo, jinsi lilivyo la msingi.
“Kumcha mzazi” sio “kumwabudu” bali ni kumpa heshima ya hali ya juu sana, ikiwemo kumsikiliza, kumtii na kufanya yale anayosema bila kumsumbua sumbua ikiwa jambo hilo si nje na mapenzi ya MUNGU.
Maana yake kama tunavyomcha MUNGU, kila atuambiacho tunakizingatia, kwasababu tunajua kwake kuna baraka na laana, kadhalika na wazazi hivyp hivyo wanaweza kutubariki na kutulaani.
Sasa wengi wetu inapofika eneo hili la kutafakari mzazi na mtoto akili zetu huwa zinalenga kufikiri wale watoto walio chini ya malezi ya wazazi, pasipo kujua kuwa hata uwe na miaka 70 na kama mzazi wako yupo hai bado hiyo amri inakuhusu hata wewe ya kumcha mzazi wako, kwani wewe bado ni mtoto kwake.
Amri ya watoto kuwatii na kuwaheshimu wazazi inawahusu hata wenye ndevu na hata wazee wenye mvi, haijalishi wewe sasa ni bibi au babu na unao wajukuu…kama mzazi wako yupo hai unayo amri ya kumcha..
Lakini ukimvunjia heshima mzazi kwasababu ni mzee, basi fahamu kuwa bado hujayajua maandiko.
Mithali 23:22 “Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee”
Jifunze kumcha Mzazi, wapo watu wanapambana na wazazi wakati wote, wanagombana na wazazi, na hata kuwaita wachawi, usiwe jamii ya hao watu waliotabiriwa..
Mithali 30:11,”Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao”.
Yafuatayo ni madhara machache ya kutomcha Mzazi.
1. Jicho kung’olewa.
Mithali 30:17 “Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa Na vifaranga vya tai watalila”
Mtu aliyetolewa macho ni kipofu, hawezi kuona ya mbele wala ya nyuma katika maisha yake, atabaki anapapasa tu.
2. Kifo.
Mithali 20:20 “Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu”.
Maana ya Taa kuzimika ni “kifo”. (Soma Ayubu 21:17).
Yapo na madhara mengine mengi ikiwemo kukosa Heri mashani..
Je unamcha mzazi wako?..je unameombea?..je umepatana naye?. Kama bado hujafanya hayo yote basi anza leo.
Bwana akubariki na atusaidie.
JE! UNA MHESHIMU MUNGU?
WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.
Uchaji ni nini kama tunavyosoma katika 1Timotheo 2:10?
BARAKA ZA WAZAZI KWA WATOTO.
Huu ni waraka wa Pili ambao mtume Paulo aliuandika kwa mwanae Timotheo akiwa kama mfungwa kule Rumi (2Timotheo 1:17)
Ni waraka wa Kitume zaidi, akimweleza Timotheo mambo mengi anayopaswa ayafanya, na ayaelewe kuhusiana na kazi ya Mungu.
Maudhui makuu ya Paulo yalikuwa ni haya;.
Haya ni maelezo mafupi katika maeneo hayo makuu:
> Paulo Anaanza kwa kumtaka Timotheo aichochee karama iliyo ndani yake, aliyoipokea kwa kuwekewa mikono na yeye. Akionyesha kuwa huduma ni kama moto ambao ili kuufanya uendelee kuwaka inahitaji wakati wote uchochewe.(2Timotheo 1:6-8)
> Anamsihi kama askari mwema, ajikite katika kazi moja ya injili, Asipeleke fikra zake katika shughuli za kidunia, akimtaka afahamu hilo ili aweze kuvipiga vita vizuri vya imani, bila kuvutwa na mambo mengi.
2 Timotheo 2:3-7
[3]Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. [4]Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. [5]Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. [6]Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda. [7]Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.
[3]Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
[4]Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
[5]Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
[6]Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda.
[7]Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.
> Anamtaka pia ajionyeshe Kuwa amekubaliwa na Mungu, Mtu awezaye kuligawanya Neno la Mungu vema, (2:15)
> Azikimbie tamaa za ujanani (2:22)
> Awe tayari kuhubiri injili Wakati wote ufaao na usiofaa.(4:1-2)
> Awe na kiasi katika mambo yote, avumilie mabaya, atimize huduma yake. (4:5)
> Akumbuke pia akikubali kuishi maisha ya utauwa ataudhiwa.(3:12)
Paulo anatoa habari za tabia alizokutana nazo kwa baadhi wa wahudumu wenza,
makundi hayo ni kama yafuatayo;
> Walioshirika na yeye nyakati zote kwa uaminifu, mfano wa hawa ni Onesiforo na watu wa nyumbani mwake, pamoja na Luka(1:16).
> Waliotengana naye kwasababu njema za mtawanyiko wa kihuduma mfano wa hawa ni Kreste na Tito,(4:9b)
> Lakini wapo ambao walimwacha kwa kupenda dunia mfano wa hawa ni Dema.(4:9)
> Na wengine kwa kujiingiza kwenye mafundisho ya uongo mfano wa hawa ni Himenayo na Fileto.(2:17-18)
> Na wengine walifanyika kabisa wapinzani wake. Mfano wa hawa ni Iskanda mfua shaba.(4:14)
Lengo la Paulo kumjuza juu ya watu hawa ni kumtaka ajifunze kuvumilia, na pia kujiepusha nao hususani wale wapingamizi, na kuweka misingi ya kimafundisho kwa kuwatahadharisha watu wasiyafuatishe mafundisho mengine, kwani makundi hayo atakutana nayo, na yatakuwepo.
Paulo anampasha habari Timotheo uhalisia juu ya nyakati za mwisho, ambazo tangu wakati ule zilikuwa tayari zimeshaanza..
2 Timotheo 3:1-5
[1]Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. [2]Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, [3]wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, [4]wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; [5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
[1]Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
[2]Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
[3]wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
[4]wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
makusudi yake ni kumtaka avumilie, na kusimama imara katika huduma, kwasababu nyakati ngumu atakutana nazo za watu wengi kujiepusha na mafundisho ya uzima.
Anasema pia kutazuka wimbi la waalimu wa uongo, wapinzani wa injili mfano wa Yane na Yambre, ambao watashindana na kweli, (3:8-9).
Hatua za kuchua:
> Adumu katika mafundisho na mwenendo wote alioupokea kwake (3:10, 14)
> Awakabidhi wengine mapokeo hayo. .(2:1)
> Ajiepushe na mashindano ya kidini, na maneno yasiyokuwa na maana (2:16, 23-26)
Mwisho.
Paulo anaeleza mwisho wake, na sababu ya kuvipiga vita vema na kusimama imara katika Imani, ni kwasababu aliiona ile taji ya haki aliyowekewa Na Mungu mbinguni. Akitumai na Timotheo atasukumwa kuvipiga vita vema kwa kuiona thawabu hiyo hiyo aliyowekewa mbinguni.
2 Timotheo 4:6-8
[6]Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. [7]Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; [8]baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
[6]Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
[7]Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
[8]baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Paulo kwa Timotheo (1Timotheo)
MAMBO NANE (8), AMBAYO WEWE KAMA KIONGOZI UTAIGWA.
UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.
WhatsApp
Mithali 27:19 Kama uso ufananavyo na uso katika maji; Kadhalika moyo wa mtu na mwenzake.
JIBU: Anaanza kwa kutoa mfano halisi, ili kueleza vema jambo la kitabia. Anasema kama vile maji yanavyoweza kuwa kioo kiakisicho, vivyo hivyo mioyo ya watu walio pamoja.
Kama tunavyojua ukiyatazama maji, utauona uso wako vilevile kama ulivyoyatazama, wala hayawezi kudanganya, ukiyaangalia umekunja sura, utaonekana hivyo hivyo, ukiyaangalia umevaa kofia, utajiona hivyo hivyo.
Ndivyo Mungu anavyowaona watu wawili waliojiungamanisha katika kitu kimmoja,(urafiki), tabia ya mmoja itamwakisi mwingine, mwisho wa siku watafanana tu na kuwa na mwenendo sawa. Akiwa mmoja ni mwizi, Yule mwingine atakuwa kama yeye tu, akiwa mmoja ni mwamini mwombaji Yule mwenzake atakuwa naye mwombaji, akiwa ni mkarimu, mwenzake naye atakuwa hivyo hivyo.
Ndio sababu biblia inasema wawili hawawezi kukaa pamoja isipokuwa wamepatana (Amosi 3:3). Hivyo vifungu hivi vinatukumbusha umuhimu wa kuchagua watu sahihi wa kuambatana nao, imesisitiza tusifungwe nira ya watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwasababu kwa njia hiyo watatuambukiza tabia zao.
Hata katika kuoa/kuolewa, ikiwa umeokoka, tafuta wa kufanana na wewe, au mbadilishe kwanza awe kama wewe ndio umwoe/uolewe naye vinginevyo, unajiandaa kugeuzwa tabia kama ilivyokuwa kwa Sulemani kuoa wake wa kimataifa.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NI UTUKUFU WA MUNGU KUFICHA JAMBO.
Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
Amali, na kila kazi ya ustadi, inatokana na mtu kupingana na mwenzake.
Je ni habari za nani unapenda kuzihubiri zaidi katika biblia?…
Kama ni taswira za wanadamu ndizo zinazokujia zaidi basi kuna uwezekano macho yako bado hayajafunguka vizuri..
Leo nataka tuangalie ni nani tunayepaswa kumwona zaidi na kumhubiri zaidi kila tusomapo biblia…
Tuyarejee maneno yafuatayo ya Bwana YESU..
Luka 24:25 “Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27 AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe”.
Luka 24:25 “Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27 AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe”.
Hapa Bwana YESU hakuanza kuwafunulia maandiko kwa kuanza kumtukuza Musa au Eliya na uhodari wao…La! Bali alianza kuelezea habari zinazomhusu yeye mwenyewe..
Wala kumsifu Samson na ushujaa wake, bali kupitia habari za Samson alijionyesha nafasi yake..
Vile vile hakuanza kumsifia na kumtukuza Sulemani na wake zake na mke wake, bali kupitia maisha ya Sulemani alielezea habari zake zaidi..na hivyo hivyo kwa manabii wengine wote, kupitia maisha yao na nyaraka zao alijielezea yeye mwenyewe…
Tuangalie maandiko machache ya manabii yaliyomhusu yeye
》 Nabii Musa aliandika habari za Bwana YESU!!..
Kumbukumbu 18:15 “BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye”.
》 Nabii Samweli naye aliandika naye habari za Bwana YESU!!..
1Samweli 2:1 “Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele”.
》 Na Nabii Isaya naye aliandika habari za mkuu wa uzima YESU,
Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani”
Soma pia Isaya 7:14.
》 Pia Nabii Mika aliandika habari za YESU..
Mika 5:2 “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”
》 Bila kumsahau na Daudi naye aliandika habari za YESU.
Zaburi 22:18 “Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura”.
Linganisha na Mathayo 27:35..
》 Nabii Hosea naye hakuacha kumtaja YESU..
Hosea 11:1 “Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri”.
Linganisha na Mathayo 2:14-15.
》 Na Yeremia naye alimzungumzia YESU KRISTO.
Yeremia 31:15 “BWANA asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako”
Linganisha na Mathayo 2:18.
》Na nabii Zekaria ni hivyo hivyo..
Zekaria 9:9 “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda”.
Linganisha na Mathayo 21:5.
》 Bila kumsahau Danieli naye alimwona YESU
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
》 Na malaki alimwona pia..
Malaki 3:1 “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi”
》 Nabii Yona naye ni hivyo hivyo aliandika habari za YESU..Soma Mathayo 12:40.
》 Nabii Ezekieli alieleza habari zake YESU…Soma Ezekieli 36:26-27 linganisha na Yohana 15:26.
》 Nabii Amos aliandika mahubiri ya yake YESU…Soma Amosi 8:9 linganisha na Mathayo 24:29.
》 Nabii Yoeli naye alizigusia kazi zake..
Soma Yoeli 2:28-32
》 Ayubu naye alimwona Soma Ayubu 19:25.
Na manabii wengine wote walimwona YESU kabla ya wakati na kuandika habari zake.
Hiyo ni kuonyesha jinsi YESU KRISTO alivyo kiini cha Imani, na kiini cha mafundisho..
Tukiweza kufikia kiwango cha kumwona Bwana YESU zaidi katika biblia zaidi ya mtu mwingine yeyote sisi ni watu wengine na wenye akili, na hapo ndipo tunapoweza kusema kuwa tunaijua biblia..
Luka 24:44 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko”.
Luka 24:44 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko”.
Bwana atufune akili zetu tumjue sana Mwana wa Mungu.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”.
Maran atha.
Tofauti na nyaraka nyingi za mtume Paulo, ambazo aliziandika kwa Makanisa, waraka huu aliuelekeza kwa Timotheo ambaye alisimama sio tu kama msaidizi wake wa kihuduma bali pia kama mwanae Katika vifungo vya injili. Ni waraka wa kichungaji zaidi ya wa kimafundisho,
Katika waraka huu Paulo anamwagiza Timotheo namna ambavyo kanisa linapaswa likae katika utaratibu, Mungu alioukusudia.(1Timotheo 3:15)
Maudhui makuu ya Paulo kwa Timotheo yalikuwa ni haya;
Haya ni maelezo mafupi Kwa kila kipengele.
Paulo anamhiza Timotheo lengo kubwa la kumtaka abaki Efeso ni ili awazuie watu wasifundishe elimu nyingine.
1 Timotheo 1:3
[3]Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
Elimu hiyo potofu aliyoina iliegemea kuwazuia watu wasile aina ya vyakula, Wasioe, pamoja na kuhubiriwa Hadithi za kizee, na nasaba (1:4, 4:7)
Kwa urefu wa mafundisho Hayo bofya hapa >>> HADITHI ZA KIZEE.
1 Timotheo 4:1-3
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; [2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; [3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
[1]Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
[2]kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
[3]wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Kwa wanaume: Paulo anatoa agizo la kwamba wao wanajukumu la kusalisha kila mahali, lakini bila hasira wala majadiliano, yaani wawe safi kiibada (2:8)
Kwa Wanawake: Paulo anatoa agizo kuwa hawana ruhusa ya kufundisha katika kanisa (2:12), halikadhalika wanawajibu wa kuvaa mavazi ya kujisitiri, mapambo yao yawe yale ya rohoni na sio ya mwilini (2:9-10).
Anaendelea kusema Wanawake ambao ni wajane waandikwe katika kanisa ili Wahudumiwe kimahitaji, lakini wale ambao si wajane kwelikweli hawapaswi kuandikwa (5:4-16)
Wazee, na vijana wafanyapo makosa wasikemewe, Bali Waonywe kwa upole Kulingana na marika yao(5:1), lakini pale wafanyapo dhambi. kwa kukusudia au kuzoelea wakemewe mbele ya wote. (5:20),
Watumwa wote wanawajibu wa kuwaheshimu mabwana zao, si tu kwa wale wasiamini bali pia kwa wale waaminio wawaheshimu wote. (6:1)
Kanisa lina wajibu wa kuwaombea watu wote, na watawala, ili liishi katika utulivu, na amani, katika utauwa wote.(2:1-4)
Sehemu hii Paulo anamwagiza Timotheo juu ya vigezo vya maaskofu, na Mashemasi namna wanavyopaswa wawe, kwamba wawe watu wasio laumika, wameshuhudiwa mema na watu wa nje, waume wa wake mmoja mmoja, si watu wa kupenda fedha,si walevi, si waongofu wapya, wanapaswa wawe wakaribishaji,, wastahivu, wenye kiasi, waaminifu, wawasimamiao watoto wao vema, na wake zao, (3:1-13).
Lakini pia anawahimiza wazee wanaotawala vema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima mara dufu (5:17).
Paulo anamwagiza Timotheo wajibu wake kama mwangalizi kuwa na upendo, Imani isiyo na unafki, na dhamiri njema, upole, saburi, na haki (1:5, 18-20, 6:11),
Anamwagiza afanye mambo yote bila upendeleo (1Timotheo 5:21).
Ajizoeshe kupata utauwa (4:8).
Awe kielelezo katika usemi na mwenendo (4:12)
Asiwaekee watu mikono kwa haraka,(5:22)
Akimbie tamaa ya fedha, na mashindano ya kidini (6:20).
Hitimisho.
Hivyo kwa ufupi, waraka huu ni wa kikanisa zaidi, na kwamba vigizo hivyo vikisimamiwa vema kanisa litakuwa imara, lenye heshima lisiloshitakiwa mabaya nje.
Ikiwa viongozi watachaguliwa hodari, na kila rika na jinsia likahudumu katika nafasi yake, yaani wanawake Kudumu katika upole, kujisitiri na kiasi na wanaume kuhudumu bila hasira wala majadiliano, huku waangalizi wakihakikisha mafundisho potofu hayapati nafasi. Ni ukweli kwamba kanisa hilo litakuwa imara sana.
Bwana akubariki
Shalom
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada nyingine:
Nasaba ni nini kibiblia?(1Nyakati 9:1, Tito 3:9)
Timotheo alikuwa wapi wakati anaandikiwa nyaraka zake na mtume Paulo?
Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
Fahamu kanuni muhimu ya kufungua milango ya Baraka za rohoni na mwilini.
Neno la MUNGU linasema..
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ALIYETUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, NDANI YAKE KRISTO”.
Ni lini tulibarikiwa na baraka zote za rohoni?..Je ni jana au leo??.. Nataka nikuambie kuwa si jana, wala juzi wala mwaka uliopita wala si siku ile ulipozaliwa…. bali ni tangu siku ile damu ya Mwokozi YESU ilipomwagika msalabani tayari tulishabarikiwa,
Na si kubarikiwa tu, bali pia tayari tulishaponywa tangu siku ile Kristo aliposulibiwa, tayari tulishashinda tangu siku ile Kristo aliposulibiwa..
Sasa swali ni hili, kama tayari Baraka na ushindi tulishapewa tangu siku ile ya pale Kalvari, kwanini sasa hatuzioni hizo Baraka zetu katika roho na katika mwili?
Hili ndilo swali la msingi kujiuliza.. kwanini hatuzioni hizo Baraka tulizobarikiwa miaka mingi iliyopita.
Sababu kuu ya sisi kutoshiriki Baraka zote za rohoni ambazo tayari zilishaachiliwa juu yetu, miaka elfu mbili (2) iliyopita pale Kalvari ni “shetani”.
Anachokifanya adui ni kuzuia kupokea zile Baraka, na si kuzuia zisitoke!.. Tayari Mungu alishatubariki..wala hatuwezi kumwomba tena atubariki, ni sisi kupambania kilicho chetu.
Sasa ili tuweze kupokea kilicho chetu, ni lazima tupambane vita, na vita hivyo ni vile vya kiroho, kwani shetani na majeshi yake yamesimama kuhakikisha hatupokei kilicho chetu.. shetani hamzii MUNGU kutoa, bali anatuzuia sisi kupokea… Na MUNGU tayari alishatoa, ila shetani anazuia tusipokee..
Ni sawa na mzazi aliyemtumia mwanae aliyeko shuleni fedha za matumizi kupitia anwani ya shule, halafu mwalimu mmoja azifiche zile fedha zisimfikie mtoto, hapo mtoto mwenye busara akishajua katumiwa fedha ana wajibu wa kuzifuatilia, na kuulizia na kama kuna shida kwa mwalimu, na kama akiona kuna shida basi aweza kushitaki ili tatizo litatuke, kwasababu atajua shida si mzazi bali ni mwalimu (sasa huu ni mfano tu).
Na mambo ya rohoni ni hivyo hivyo, BWANA MUNGU wetu alishatubariki kwa Baraka zote za rohoni.. kazi tuliyobakiwa nayo ni kushughulika na vizuizi vya sisi kupokea hizo Baraka.
Na silaha zifuatazo ndizo zinazoweza kuvunja vizuizi vyote na kuachia kilicho chetu.
1. MAOMBI
Maombi (hususani yanayohusisha mfungo) ni silaha ya kwanza ya kuzipinga hila za adui zinazozuia Baraka zetu.. Mtu aliyejizoeza kuomba ni rahisi kupokea Baraka zote zilizoahidiwa na MUNGU, na mtu anayepungukiwa maombi ni kinyume chake.
2. KUSOMA NENO.
Maombi bila Neno la Mungu ni sawa na bendera iliyokosa mlingoti… Mtu aombaye huku Neno la Mungu limejaa ndani yake, ni rahisi sana kuteka Baraka zake tofauti na yule asiyekuwa msomaji wa NENO, na kusoma Neno kunakozungumziwa hapa si kushika vifungu vya biblia, La!.. Unaweza kuwa umeshika vifungu elfu vya biblia na bado usiwe umelijua Neno.
Bali kusoma Neno kunakozungumziwa hapa ni kule kujifunza kitabu baada ya kitabu na kujua maudhui ya kila kitabu katika ufunuo wa Roho.
3. UTAKATIFU
Utakatifu wa mwilini na rohoni ni mkuki wa kumpiga yule mwovu aachie vinavyotuhusu.. kinyume chake uchafu na maisha ya dhambi ni kifungo kinachozuia Baraka zetu.
Sasa utauliza Baraka za rohoni na mwilini ni zipi?
Mfano wa Baraka za rohoni ni Amani, furaha, upendo, uvumilivu, upole, utu wema na mambo mengine yote mema yanayofanana na hayo, kwa ufupi ni Roho Mtakatifu na matunda yake (Wagalatia 5:22).
Na baraka za mwilini hamna haja ya kuziandika maana zinajulikana, ambazo ni zile zote zinazohusu mahitaji ya mwilini.
Je umepungukiwa na Baraka?…fahamu kuwa Maombi, Neno na Utakatifu ndio dawa ya kutibu hilo tatizo, wala usimnung’unikie MUNGU kwanini hakubariki.. yeye tayari alishatubariki, ni sisi kupambana kupata vilivyo vyetu..Anza mapambano hayo kuanzia sasa ikiwa tayari umeshampokea Bwana YESU.
Na kumbuka mapambano haya hamna siku yatapoa, hata baada ya kuwa mtumishi.. ni jambo endelevu daima mpaka safari ya maisha inaisha, kwani pia kuna kupokonywa na yule aliyetuzuia tusipokee, ikiwa hatutasimama katika mambo hayo makuu matatu, na mengine yanayofanana na hayo.
Hivyo ukristo ni mapambano, ni vita, lakini vyenye nafasi kubwa ya kushinda Zaidi ya kushindwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, kwa yeye aliyetupenda”.
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.
MILANGO YA KUZIMU.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
CHAKULA CHA ROHONI.