SWALI: Je! ni sahihi kwa mkristo kufanya biashara za kifedha mitandaoni kama vile Forex, na crypto-currency mfano wa bitcons?
JIBU: Ni vema kufahamu biashara za kifedha mitandaoni kama forex ni nini?
Ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni katika soko la dunia. Yaani ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, sawa tu ile tuliyowahi kuisikia, ijulikanayo kama Bureau de change, ambayo watu wanakwenda kununua/kuuza pesa za kigeni, isipokuwa hii hufanyika mitandaoni, tofauti na bureau ambayo hufanyika kwa makarati ndani ya ofisi Fulani maalumu. Biashara hii ya forex na nyinginezo Mara nyingi hufanywa na taasisi kubwa za kifedha kama mabenki na makampuni, lakini pia hata watu binafsi.
Ni biashara ya bahati nasibu, inayofanana na michezo ya kubahatisha kitabia.. Lakini ni tofauti kabisa kimaudhui.
Biashara hii ni ya uwekezaji, ambayo imehalalishwa ki-ulimwengu, japokuwa hatusemi kuwa kila biashara iliyohalalishwa na taifa kuwa ni halali kwa mkristo kufanya, hapana mfano zipo pombe zimehalalishwa kitaifa lakini kwa mkristo sio sawa kufanya biashara kama hizo.
Lakini, biashara hii, haihusishi katika kumdhulumu mtu, au kumlaghai mtu kiakili, apoteze kitu Fulani ili wewe ujilimbikizie fedha zake ambazo hazina mzungumko wowote wa kimaendeleo. Mfano wa hizo ni kama vile “Betting na kamari”. Kwa mkristo kushiriki katika biashara hizo za betting na kamari sio sawa. Kwa urefu wa somo lake pitia link hii >>>JE! KUBET NI DHAMBI?
Lakini Forex na nyinginezo zijulikanazo kama biashara za uwekezaji, zinahitajika sana, kwasababu kama zikikosekana, basi mzunguko wa fedha za kigeni, ungekuwa mgumu sana, na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji uchumi, katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia.
Hivyo tukirudi kwa mkristo, je kufanya biashara hii ni dhambi?
Kimsingi ikiwa anafanya kwa lengo la uwekezaji wake, huku akijua pia ni kwa faida ya uchumi, na hamdhulumu au kumlaghai mtu. Hafanyi kosa. Lakini akiwa na fikra za kikamari, kama vile afanyavyo kwenye betting, Kwake itakuwa ni kosa, kwasababu dhamiri yake inamshuhudia, ameigeuza kama kamari moyoni mwake.
Ndio hapo hili andiko linakuja.
Warumi 14:22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali. 23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.
Warumi 14:22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. NA KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.
Maana yake ni kuwa ukiwa na mashaka moyoni mwako kuifanya kazi hii, basi ni heri usifanye kabisa, kwasababu mashaka yoyote ni dhambi. Lakini kimsingi biashara hii sio kosa kwa mkristo, ambaye ana maarifa/elimu ya kutosha juu ya biashara za kifedha katika ulimwengu wa sasa.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
Tarshishi ni mji gani kwasasa?
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Rudi nyumbani
Print this post
Hesabu 16:20 Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. 22 Nao WAKAPOMOKA kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?
Soma pia
Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu?
14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?
Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi baadhi; Hesabu 16:4, 16:45,
Ni Kiswahili cha zamani cha Neno kuporomoka. Yaani kuanguka chini, kwamfano maji yanayoelekea chini kwa wingi tunasema maporomoko ya maji, au udongo unaoanguka kutoka milimani kwa wingi tunasema maporomoko ya udongo.
Hivyo, katika vifungu anaposema Musa na Haruni wakapomoka kifudifudi, anamaanisha wakaanguka chini kifudi fudi mbele za Mungu kumlilia Bwana rehema.
Je! Na sisi tuombapo rehema au tumtakapo Bwana kwa jambo Fulani muhimu ni lazima tupomoke chini ili tusikiwe ?
Jibu lake ni kwamba sio takwa kufanya hivyo. Kwasababu Mungu anaangalia moyo, kupomoka kwetu kunapaswa kuwe moyoni. Lakini pia si vibaya kuomba kwa namna hiyo, na ni vema, kwasababu pia ni ishara moja wapo ya unyenyekevu wa moyo. Ni sawa tu na tunapopiga magoti, au kunyosha mikono juu wakati wa kumwomba Mungu, kama ishara ya unyenyekevu mbele zake.
Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?
LAANA YA YERIKO.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
Kuwatema farasi, maana yake ni nini?
Tunapokisoma kisa cha Daudi, cha kumwiba mke wa shujaa wake (Uria), na kumlazimisha kuzini naye kwa siri, na baadaye kumuua mumewe , (2Samweli 11) tunaishia kuona picha mbaya sana ya Daudi. Na kumshutumu, na wengi wetu kusema Daudi ni mzinzi sana, iweje apendwe na Mungu namna ile, tena awe kipenzi cha Mungu?
Ni kweli kabisa alichokifanya Daudi hakistahili kufanywa na mtu yeyote, ambaye anamjua Mungu, mfano wa Daudi. Lakini kuna funzo kubwa sana ambalo wengi wetu hatulioni nyuma ya maisha ya Daudi baada ya pale.
Daudi alipozama katika dhambi ile, na kugundua makosa yake. Alikuwa na badiliko lisilo kuwa la kawaida. Sio kule alikokuwa anaomboleza usiku kucha, Hapana, lile lingekuwa la “kufoji” tu, ambalo yoyote anaweza kulifanya hata leo. Kinyume chake Daudi alikuwa na badiliko la kimatendo. Na hilo ndilo lililomfanya apendwe sana na Mungu.
Kwa namna gani?
Sasa angalia Daudi Yule Yule ambaye alikuwa ni mzinzi, mwenye tamaa ya hali ya juu,akiona tu mwanamke mzuri hajali, huyu ni mke wa mtu au la yeye alimwiba na kuzini naye. Lakini Dakika zake za mwisho hazikuwa hivyo. Alibadilika kwelikweli baada ya dhambi ile.
Utakumbuka hata alipokuwa mzee, Wakuu wa Israeli walikwenda kumtafutia Binti mzuri bikira katika taifa lote la Israeli, ili amlalie Daudi ampe joto kwasababu nguo za joto hazikutosha. Lakini biblia inasema Daudi alipolala naye ‘hakumjua’.
Kwa jinsi ya kibinadamu, binti alale, na mtu mwenye sifa ya tamaa kama Daudi, halafu asimwingilie. Lazima kutakuwa kuna jambo lingine limetendeka ndani ya maisha ya huyo mtu.
Tusome;
1 Mfalme 1:1
“Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto. 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto. 3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme. 4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
“Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.
2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.
3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.
4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
Ni wazi kuwa habari hiyo ilijulikana Israeli nzima, Daudi amelala na binti bikira mrembo miaka kadhaa lakini hajamwingilia. Ni shujaa kiasi gani. Hawakujua kuwa anawathibitishia Israeli kuwa yeye sio Yule wa zamani, sio Yule mzinzi mliyemzoea, ameshabadilika. Si mtu wa kulipuka lipuka tamaa ovyo kama alivyokuwa hapo mwanzo.
Hiyo ndio sababu Mungu alimpenda Daudi. Kwasababu alikuwa na badiliko la dhati Kwa Mungu wake. Je! Na sisi, tunaweza kusema tumeuacha ulimwengu kweli kweli pale tunapomgeukia Mungu, au tutakuwa na vimelea vya kidunia ndani yetu, pale tunapokutana na majaribu kama yale yale ya mwanzo. Tulipokuwa wazinzi na sasa tumeokoka, Je! Tuna ujasiri wa kuishi maisha ya mbali zinaa, au bado tupo nusu nusu.
Tuwe na badiliko la dhati, leo tumeanguka katika dhambi Fulani mbaya, sasa tumetubu, tusiwe tena walewale wa kuanza kuangalia angalia nyuma kama mke wa Lutu. Mungu atakuchukizwa na sisi na mwisho wa siku tutakuwa jiwe la chumvi kama sio kutapikwa mfano wa kanisa la Laodikia.
Tumaanishe kwelikweli kuacha mambo maovu tuliyoyazoelea. Jifunze kwa Daudi. Yule sio mzinzi kama wewe unayejitumaisha kwa visa vyake vya zamani, ukadhani kuwa utanusurika hukumu ikiendelea na tabia hiyo.
Shalom.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?(Opens in a new browser tab)
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 4
Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?
(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
WhatsApp
Manabii Wanaume katika biblia walikuwa wengi kiidadi kuliko manabii wanawake.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA JEDWALI:
Kutazama Jadwali zima, basi Slide kuelekea upande wa kushoto.
Mbali na hawa walioorodheshwa katika Jedwali hilo hapo juu, walikuwepo pia Manabii wengine ambao hawakuonekana wakitajwa katika kutoa Nabii za Nchi au Taifa.. Mfano wa hao tunawaona katika Jedwali lifuatalo.
MAJINA YA MANABII WANAWAKE
MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU
WAFALME NA MALKIA WALIOTAWALA YUDA
WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.
Nini maana ya Mithali 11:17 inaposema;
Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
JIBU: Mwenye rehema ni mtu wa huruma, mwenye kusamehe, mwenye kuachilia hata kama tendo alilofanyiwa linastahili adhabu kwa yule mwingine.
Biblia inasema mtu kama huyo huipa faida nafsi yake. Huitendea mema nafsi yake. Ambayo huipata kwanza hapa hapa duniani, kwasababu Bwana alisema kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa na watu.
Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Maana yake ni anajijengea wigo mpana wa yeye naye kukutana na rehema nyingi mbeleni.
Vilevile anapata faida katika ulimwengu ujao, Bwana alisema..
Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Lakini anasema pia, mtu mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mkali ni kinyume cha mtu mwenye rehema, ni mtu asiye na huruma, mwenye visasi, asiyejali, mkorofi, akiudhiwa anarudisha Maudhi, akikosewa kidogo, analipiza mara mbili, maneno yake hayana staha, kugombeza wengine kwake ni jambo la kawaida n.k.
Sasa matokeo ya mtu wa namna hii ni kuadhibiwa na Mungu, aidha hapa hapa duniani, au kule aendapo.
Bwana alisema…auaye kwa upanga, atauwawa kwa upanga, ukimtendea mtu kwa ukali na wewe ukali utakurudia, ukimpiga mwingine kwasababu kakuudhi kidogo, na wewe utapigwa mahali fulani kwasababu ulimuudhi mwingine.. (hicho huitwa kisasi cha Mungu).
Hivyo tendea mema nafsi yako, lakini pia mwili wako, kwa kumpenda Bwana. Na kuwa mwema.
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.(Opens in a new browser tab)
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
(Opens in a new browser tab)NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?(Opens in a new browser tab)
SWALI: Nini maana ya Mithali 20:11 inaposema;
Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
JIBU: Mwandishi anatuonyesha kuwa tabia ya mwanadamu yoyote, huwa haijifichi kufuatana na umri wake, kwamba yaweza kukaa ndani tu kipindi cha utotoni isionekane ikaja kudhihirika ghafla ukubwani. Hapana, anasema “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili”.
Ikiwa na maana katika utoto ule ule unaweza kuuchunguza mwenendo wa mtoto, ukautambua. Na hiyo itakupa fursa ya kuurekebisha ukiwa ni mbaya, au kuuimarisha ukiwa ni mzuri, akiwa katika vipindi kile kile. Usione mwanao anayotabia ya udokozi, ukasema huyu ni mtoto tu, haelewi anachokifanya. Hapana unapaswa umrekebishe mapema, kwasababu hicho kitu kipo ndani yake, Ukiona mtoto anapenda kutazama biblia, anapenda kukaa kanisani, anapenda kusikiliza nyimbo za injili. Usiseme, huyu ni mtoto, ukampuuzia tu, kwa kuishia kusema ‘ubarikiwe mwanangu’ kinyume chake, mwendelezee mazingira hayo, kwasababu mwelekeo wa maisha yake, ni huko.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tabia zake zilianza kuonekana tangu utotoni, wazazi wake walimstaajabia, kumwona katika umri ule mdogo, yupo hekaluni, amekaa na waalimu na wakuu wa dini akiwauliza maswali, Kinyume chake wazazi wake hawakumkemea, bali waliyaweka yote mioyoni mwao, na kukubali kuutambua mwelekeo wa mtoto wao.
Hii ni kufundisha nini?
Lipo funzo la rohoni, lakini pia la mwilini.
La mwilini ni kuwa yatupaswa tuwatazame watoto, bila kupuuzia kitendo chochote wanachokidhihirisha katika umri ule wa chini. Ikiwa ni chema tukipalilie, ikiwa ni kibaya, tukikemee, na kushughulika nacho kwelikweli kabla hakijaweka mizizi. Hivyo hakuna mzazi au mlezi anaweza kusema, huyu mwanangu kabadilika tu ghafla. Ukweli ni kwamba mabadiliko yalianza kuwepo tangu zamani, isipokuwa kwa namna moja au nyingine tulipuuzia, tulipoyaona ndani yao tukadhani ni tabia za utoto tu. Wazazi wanaowajenga wanao katika maadili na vipawa tangu utotoni, ukiwatazama watoto wao wanapokuwa watu wazima, huwa wanakuwa na ufanisi na ujuzi wa hali ya juu sana, zaidi ya wale ambao watajijengea wenyewe wanapokuwa watu wazima. Hivyo mzazi jali maisha ya kiroho ya mwanao.
Vilevile rohoni, wapo ambao ni wachanga kiroho. Ikiwa na maana katika kanisa ni wale ambao wameokoka hivi karibuni. Halikadhalika hawa nao utaweza kutambua karama zao, sio mpaka wawe wakomavu kiroho. Aliye Mwinjilisti, utaona anapenda kushuhudia, lakini pia anauwezo wa kuwavuta wengine kwa Bwana. Aliye mwalimu, utaona anapenda sana kujifunza, aliye nabii, utaona karama za maono, ndoto, huwa zinamjia mara kwa mara, hata kwa namna ambazo hazielewi elewi, mwimbaji atapenda wakati mwingi kujifunza kuimba hata kama hawezi. Hivyo, kila mmoja wetu, kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake, hujidhihirisha mapema sana pindi ameokoka. Sio mpaka awe amekomaa sana kiroho kama wengi wanavyodhani.
Pindi unapookoka, kipindi hicho hicho karama yako inaanza kufanya kazi, unapachopaswa tu, ni kujishughulisha na utumishi wa Bwana, ndivyo utakavyoruhusu mambo hayo kutokea kwa wepesi na urahisi zaidi?
Mafundisho mengine
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
(TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.(Opens in a new browser tab)
Wafalme waliotawala ISRAELI, ukiwatoa wale watatu wa Mwanzo (Yaani Sauli, Daudi na Sulemani) walikuwa ni Wafalme 19 tu, na hakukuwa na Malkia aliyetawala Israeli kama ilivyokuwa kwa YUDA.
Kati ya Wafalme hao 19 waliotawala Israeli, hakuna hata mmoja aliyekuwa Mkamilifu mbele za MUNGU katika ukamilifu wote kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Wafalme waliotawala YUDA. Isipokuwa Mfalme mmoja tu aliyeitwa YEHU ndiye angalau alionekana kufanya Mema lakini pia alifanya na Mabaya.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.
Wafalme waliotawala YUDA ni 19, na Malkia aliyetawala YUDA ni Mmoja (1), hivyo kufanya jumla ya Watawala 20 kupita katika Taifa la Yuda.
Kati ya hao Wafalme 19; waliofanya MEMA ni Wafalme saba (7) tu, wengine 12 waliosalia walifanya Mabaya. Na Malkia Mmoja aliyetawala naye pia alifanya Mabaya, hivyo kufanya jumla ya watawala 13 waliofanya mabaya.
Tafuta jina la Mfalme hapa >>
Mafundisho mengineyo:
Bwana alimaanisha nini katika Mathayo 5:20 aliposema..
[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Ni haki ipi hiyo.
JIBU: Katika andiko hilo tunaona Bwana akiainisha kigezo cha mtu kuingia kwenye ufalme wa Mungu..kwamba kigezo chenyewe ni “HAKI” …
Haki ni kitu kinachomstahilisha mtu kupokea kitu fulani. Kwamfano tunasema mtoto ana haki ya kulindwa…ikiwa na maana kilichomsababishia apate haki ya kulindwa ni ile hali ya utoto wake.
Mfano mwingine, tunasema ni mtu mzima ana haki ya kuoa au kuolewa na mtu amtakaye, katika wakati auchaguaye yeye. Tafsiri yake ni kwamba kinachompa haki ya kuwa hivyo ni kwasababu yeye ni “mtu-mzima”. Angekuwa mtoto asingekuwa na haki hiyo.
Sasa tukirudi katika habari hiyo tunaona kilichowafanya waandishi na mafarisayo wajihesabie haki kwamba wao ni warithi wa ufalme wa mbinguni. Ilikuwa ni kuitimiza sheria kwa matendo yao. Ambayo kimsingi wao wenyewe hawakuweza kuishika..kwa nje walionekana sawa lakini ndani walikuwa mbali na sheria yao. Kwasababu hakuwahi kutokea mtu hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu kwa matendo yake, yeye mwenyewe.
Hivyo njia yao ya kupata haki, ambayo ni kwa matendo ya sheria haikuwa sawa. Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake na wale waliomsikia kwamba haki “ yao” isipozidi ya mafarisayo na waandishi kamwe hawataweza kuuingia ufalme wa mbinguni.
Swali je ya kwao inapaswa iweje. Je ya matendo ya sheria zaidi ya yale au vinginevyo?
Haki Yesu aliyoileta ambayo itampelekea mtu kurithi uzima wa milele ni kwa njia yake yeye mwenyewe .Ambayo sisi tunahesabiwa haki kwa kumwamini, kama mwokozi wa maisha yetu. Bila kutegemea matendo yetu ya haki. Yaani ni haki tuipatayo kwa neema.
Hivyo, wote wanaoipokea haki hiyo basi uzima wa milele ni wao. Na kwasababu ndio njia ambayo sisi tutamfikia Mungu. Basi neema yenyewe inatufundisha pia kuyazaa matunda ya Roho. Na hivyo tunaitimiza sheria ya Mungu mioyoni mwetu bila unafiki. Mbali na mafarisayo ambao walitegemea akili zako na nguvu zao.
Hata sasa ikiwa unategemea jitihada zako, zikupe haki mbele za Mungu, ndugu umepotea. Hutaweza Itegemee neema ya Mungu. Na hiyo itakusaidia kuyatimiza hayo mengine kwa Roho Mtakatifu.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili?
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya Isaya 40:12 inaposema maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri?
Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?
JIBU: Ukianzia kusoma vifungu vya juu na kuendelea vile vya chini, utaona Mungu anawaambia watu wake Israeli kuwa atawajilia kama mchungaji awachungaye kondoo wake , na kuwalisha, na kuwakuongoza, na kuwakusanya kifuani mwake, hata wale walio wachanga, ndivyo atakavyowatendea watu wake na hilo litawezekana.
Lakini Israeli waliona kama jambo hilo linaweza lisiwe rahisi, Ndio hapo akawaambia sasa katika vifungu vifuatavyo maneno hayo. Kwamba “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake”? Maji anayoyazungumzia hapo ni maji mengi, mfano wa bahari, na maziwa Je! Kuna mtu yeyote anayeweza kuyakusanya maji mengi namna hiyo kwenye viganja vyake? Jibu ni hapana! Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana.
Vilevile anawauliza ni nani awezaye ‘kuzikadiri mbingu kwa shubiri’?. Shubiri ni kipimo cha urefu, wa kiganja, toka kidole gumba mpaka kile cha katikati vinaponyooshwa. Na ni wazi hakuna mtu anayeweza kupima ukubwa wa mbingu, toka sayari moja hadi sayari nyingine, kwa kipimo chochote kile cha kibinadamu. Lakini kwa Mungu hilo ni jambo dogo sana, ni kama kuzipima kwa shubiri.
Halikadhalika anauliza ni nani awezaye kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi?. Pishi ni kopo dogo, je kuna mwanadamu anaweza kuyakusanya mavumbi yote duniani, kama vile akusanyavyo yale machache kwenye kopo lake. Ni wazi hakuna awezaye kuwa na pipa la uwezo huo.
Vilevile anauliza ni nani anayeweza kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?. Je! Kuna mizani yoyote ya kibinadamu inaweza kuiweka milima juu yake, na kutoa vipimo?. Jibu ni hakuna. Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana. Milima ni kama vipunje vidogo sana vya mchanga.
Ikiwa haya yanaonekana magumu kwa mwanadamu, lakini kwa Mungu ni mepesi. Vivyo hivyo jambo la kuwakusanya watu wake, au kuwasaidia, lisitizamwe kibinadamu, kwasababu uweza wa Mungu ni mkuu sana usioweza kufikirika kibinadamu. Maswali ya namna hii ndio kama yale Mungu aliyokuwa anamuuliza Ayubu, (Ayubu 38-41), na katika Mithali 30:4
Yesu kama mchungaji wetu mkuu, anauwezo wa kutukusanya kama kondoo wake. Haijalishi tutaonekana tumetawanyika mbali kiasi gani, lakini akisema jambo ni lazima liwe. Halikadhalika na katika mambo yetu yote ya kiroho na kimwili.
Hivyo kitabu cha Isaya sura ya 40 yote, kinaeleza uweza wa Mungu, usiopomika kibinadamu. Lakini Swali ni Je! Kristo amekusamehe dhambi zako? Kama ni la! Basi nafasi bado unayo leo. Mwamini yeye akuokoe. Na kukupa ondoleo la dhambi zako.
Kwa mwongozo wa namna ya kupokea wokovu basi fungua hapa>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)
Kuna Mbingu ngapi?
Mbinguni ni sehemu gani?