Neno kupomoka linamaana gani kwenye biblia?(Hesabu 16:22)

Neno kupomoka linamaana gani kwenye biblia?(Hesabu 16:22)

Hesabu 16:20 Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,  21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.  22 Nao WAKAPOMOKA kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?

Soma pia

Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 

14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?

Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi baadhi; Hesabu  16:4, 16:45,

Ni Kiswahili cha zamani cha Neno kuporomoka.  Yaani kuanguka chini, kwamfano maji yanayoelekea chini kwa wingi tunasema maporomoko ya maji, au udongo unaoanguka kutoka milimani kwa wingi tunasema maporomoko ya udongo.

Hivyo, katika vifungu anaposema Musa na Haruni wakapomoka kifudifudi, anamaanisha wakaanguka chini kifudi fudi mbele za Mungu kumlilia Bwana rehema.

Je! Na sisi tuombapo rehema au  tumtakapo Bwana kwa jambo Fulani muhimu ni lazima tupomoke chini ili tusikiwe ?

Jibu lake ni kwamba sio takwa kufanya hivyo. Kwasababu Mungu anaangalia moyo, kupomoka kwetu kunapaswa kuwe moyoni. Lakini pia si vibaya kuomba kwa namna hiyo, na ni vema, kwasababu pia ni ishara moja wapo ya unyenyekevu wa moyo. Ni sawa tu na tunapopiga magoti, au kunyosha mikono juu wakati wa kumwomba Mungu, kama ishara ya unyenyekevu mbele zake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?

LAANA YA YERIKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments