Biblia inaposema ndugu wa kunyonya inamaanisha nini (Matendo 13:1)?

Biblia inaposema ndugu wa kunyonya inamaanisha nini (Matendo 13:1)?

Swali: Katika kitabu cha Matendo 13:1, tunamsoma mtu mmoja akitajwa kama ndugu wa kunyonya wa Herode, je maana yake nini?.


Jibu: Maana ya “Ndugu wa kunyonya” ni “mtu aliyelelewa katika familia fulani, tangu utotoni, alipokuwa akinyonya” kwa lugha nyingine amekuwa “adopted” tangu utotoni, (katika umri wa kunyonya).

Hivyo mtu kama huyu anahesabika kuwa kama mwanafamilia, na watoto wa familia hiyo watamhesabu kama ndugu yao wa kunyonya, kwani amekulia katika familia yao.

Hivyo huyu Manaeni alilelewa pamoja na Mfalme Herode, katika familia moja, ingawa hawakuwa ndugu wa damu, lakini tangu utoto walikuwa pamoja.

Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na MANAENI ALIYEKUWA NDUGU WA KUNYONYA WA MFALME HERODE, na Sauli”.

Lakini kulikuwa na kusudi kwanini habari zake ziandikwe katika biblia, ukizingatia ya kuwa ndugu yake, ambaye alikuwa ni Herode pamoja na maherode wote walikuwa ni wakatili sana, waliwaua wakristo na kuwapiga vita vikali, lakini huyu Manaeni ambaye ni ndugu ya Herode, yeye alikuwa wa tofauti, kwani alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kugeuka na kuifuata Imani ya Kikristo, na kuwa miongoni mwa wasimamizi wa Imani katika kanisa la kwanza la watu wa mataifa, huko Antiokia.

Na kumbuka Antiokia ndiko jina la Ukristo lilikozaliwa, kwani hapo kabla waliomfuata YESU walikuwa wanaitwa wanafunzi tu.

Matendo 11: 26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia”

Sasa kufahamu kwa urefu ushuhuda alilolibeba Mtumishi huyu wa Mungu (Manaeni) na ujumbe tuupatao watu wa sasa katika Kanisa, fuatilia somo linalofuata…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Uzao wa Ibrahimu unamilikije mlango wa adui? (Mwanzo 22:17)

Swali: Katika Mwanzo 22:17, MUNGU anasema kuwa uzao wa Ibrahimu utamiliki malango ya adui, sasa unamiliki vipi huo mlango wa adui?.


Jibu: Turejee…

Mwanzo 22:17 “katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”.

Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa Mzao wa Ibrahimu aliyebeba ahadi kamili za Ibrahimu ni BWANA YESU KRISTO.

Wagalatia 3:16 “Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo”.

Wengine wote, akina Isaka na Yakobo,(yaani Israeli katika mwili). walibeba sehemu za baraka hizo lakini si zote.. Iliweza kumiliki baadhi ya milango ya adui katika mwili lakini si yote.

Sasa kwa namna gani Israeli ya mwilini ilimiliki malango ya adui?

Kwa njia ya vita: kumbuka zamani miji ilikuwa inazungukwa na kuta, na mageti makubwa, hivyo nguvu na udhaifu wa mji ulikuwa katika mageti ya mji, hivyo lango la mji likitekwa na kumilikiwa basi tayari ule mji umeshatekwa,

Na Mungu aliwapa ahadi wana wa Israeli kwa jinsi ya mwili, kumiliki mlango/malango ya adui, ndio maana waliweza kuangusha miji ya kanaani iliyo mikubwa na yenye nguvu, na hatimaye kuiteka nyara miji hiyo.

Lakini mbali na hayo, lipo Lango ambalo Israeli ya mwilini asingeweza kumiliki, na mlango huo si mwingine zaidi ya ule wa MAUTI na KUZIMU.

Na kawaida mtu mwenye miliki ya mlango, ni yule mwenye FUNGUO ZA HUO MLANGO.

Mtu akikosa funguo hawezi kuwa na milki ya mlango wowote ule.

Hivyo Israeli ya mwilini alikuwa na Funguo za kufungua Mageti ya Wakaanani na Yeriko na mageti ya Wafilisti na kuwapiga na kuwatoa katika ardhi yao, lakini hakuwa na FUNGUO za MAUTI na KUZIMU,

Hakuweza kuzuia watu wasiingie kuzimu wala kuwatoa huko na kuwarudisha tena juu sawasawa na Ayubu 7:9.

Ayubu 7:9 “Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa”

Hivyo Israeli ya mwilini haikuweza kumiliki malango yote…. alikwama hapo kwenye Mauti na Kuzimu, sawasawa na maneno ya Bwana Mungu katika Ayubu 38:17.

Ayubu 38:17 “Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?”

Sasa swali la msingi, kama Israeli ya mwilini imeshindwa kumiliki milango hiyo, ni nani basi mwenye uwezo huo sawasawa na Mwanzo 22:17?.

Jibu la swali hili tunalipata katika kitabu kile cha Ufunuo 1:17-18.

Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI, NA ZA KUZIMU”

Huyo mwenye hizo funguo za Mauti na kuzimu, ndiye mwenye milki ya Mlango wa Adui.

Maana adui wa kwanza na wa mwisho wa mwanadamu ni MAUTI ambaye analetwa na dhambi, huyu ndiye aliyeanza na Adamu pale Edeni na atamalizwa na Mwana wa Adamu siku ya mwisho.

1 Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.

Na matokeo ya Mauti katika dhambi ni KUZIMU.

Kwahiyo YESU KRISTO ndiye mwenye funguo za Mauti na Kuzimu.

Wafu wote wanamilikiwa na Bwana YESU, na KUZIMU ipo chini ya mamlaka ya Bwana YESU, utauliza kivipi?..Mtu anayekufa sasa katika dhambi si shetani anayemtupa katika lile shimo la kuzimu, bali mamlaka ya YESU kupitia malaika wake ndio wanaowatupa watu katika lile shimo la kuzimu.

Kwasasa shetani hana mamlaka yoyote na wafu, hizo milki alishapokonywa na Bwana siku ile aliposhuka kuzimu, na hayo malango sasa yanamilikiwa na YESU KRISTO (Mkuu wa Uzima).

Warumi 14:9 “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia”.

Nguvu za Bwana YESU kwasasa ni KUU SANA!!!, ukitaka kufahamu kwa sehemu kiwango cha nguvu alizonazo juu ya Mauti, ikumbuke ile kauli aliyosema..

Yohana 10:17 “Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.

18 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu”.

Tafakari mtu anakuambia anao uwezo wa kuitoa roho yake na kuirudisha tena,…yaani kama vile mtu anavyozima taa na kuiwasha….na tena anasema “hakuna mtu aniondoleaye”..Maana yake Bwana YESU hakuuawa, bali yeye mwenyewe ndiye aliyeitoa roho ndani ya mwili wake.

Ndio maana akasema yale maneno…

Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”

Sasa mtu aliyeuawa hawezi kusema maneno hayo…lakini Bwana YESU hakuuawa bali yeye mwenyewe aliiondoa roho yake katika ule mwili, na ndio maana hata wale askari walishangaa imekuwaje amekufa mapema vile kabla ya kuvunjwa miguu.

Sasa ni kweli yapo maandiko yanayosema kuwa Bwana YESU aliuawa, lakini fahamu kuwa popote yanapotaja hivyo ni kuitia nguvu mada iliyoanza, lakini ukweli ni kwamba Bwana hakuuawa na mtu bali aliitoa roho yake mwenyewe.

Hiyo yote ni kuonyesha kuwa Mlango wa Adui wa Mauti, Bwana anao funguo zake.

Hivyo basi tukitaka mauti na kuzimu zisiwe na nguvu juu yetu, hatuna budi kumwendea yeye mwenye funguo hizo, na hatimaye atupe wokovu.

Lakini tukimkataa yeye mwenye funguo hizo, tujue kuwa hatutaokoka hata kidogo.

Malango ya adui, ni malango ya kuzimu, na ni malango ya mauti na yote chanzo chake ni dhambi.

Je umempokea Bwana YESU na kuoshwa dhambi zako?.

Kama bado unasubiri nini?.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je Adamu na Hawa waliokoka?

Je mtu anaweza kupoteza wokovu?

USIWE ADUI WA BWANA

ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.

MUNGU HAJARIBIWI NA MAOVU BALI MEMA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Ni msiba gani unazungumziwa katika 1Petro 4:12?.

Jibu: Turejee…

1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho”.

Neno “Msiba” kama linavyozungumziwa hapo halimaanishi ule Msiba wa mtu kufa. La! Bali neno hilo limetumika hapo kuwakilisha “jaribu zito”.

Kama tu lile lililompata yule mwanamke aliyetokwa na damu mda wa miaka 12.

Marko 5:27 “aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;

28 maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.

29 Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule…………………

33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.

34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena”

Hivyo tukirejea andiko hilo la 1Petro 4:12 msiba unaozungumziwa hapo “Ni jaribu zito”.

Kwahiyo kwa kiswahili kingine mstari huo unaweza kusomeka hivi…

“Wapenzi, msione kuwa ni ajabu lile jaribu zito lililo kati yenu, linalowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho”

Na msiba huo (au jaribu hilo)…Ni “Kuteswa kwaajili ya Kristo”…tunalithibitisha hilo katika mstari unaofuata wa 13.

1 Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia”.

Soma pia 1Wathesalonike 3:7 unataja msiba wa dhiki katika Kristo.

Na hata leo wote watakaotaka kuishi maisha ya kumpendeza MUNGU na utauwa, watakutana na misiba ya Kuudhiwa kwaajili ya imani.

2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa”.

Lakini ukiishi maisha ya kuupenda ulimwengu, basi ulimwengu nao utakupenda kwasababu ulimwengu unawapenda walio wake.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

PIGO LA KUFA KWA WAZALIWA WA KWANZA

NYWELE ZAKO ZIKUFUNDISHE, SAUTI YA MUNGU.

VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.

MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE.

HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.

Rudi Nyumbani

Print this post

MRUDI MWANAO NAYE ATAKUSTAREHESHA

Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha”.

Kumrudi mtoto sio “kumwadhibu tu”. Bali pia kumrekebisha (Kauli zake na njia zake).

Ni kweli maandiko yanaruhusu kumwadhibu mtoto kwa kiboko pale anapokosea, lakini hiyo iwe hatua ya mwisho baada ya kuona harekebishiki kwa maneno..

Katika hatua hiyo maandiko yameruhusu kutumia mapigo kwa huyo mtoto, ili kuiokoa roho yake na kuzimu.

Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.

Soma pia Mithali 22:15.

Wengi wanaogopa kuwaadhibu watoto wao kwa mapigo wakiamini kuwa watapata madhara ya kisaikolojia na hata kiafya.. pasipo kujua kuwa hapo biblia imesema ukimpiga “hatakufa”..maana yake Mungu atazuia madhara yote ya kiafya, ikiwa lengo lako si lingine zaidi ya kumjenga.

Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo ya matumizi ya fimbo, ni muhimu kuanza na maonyo, na makemeo.

Maana yake kama mtoto amekosea kusema ni lazima arekebishwe kusema kwake mapema, kwasababu watoto wanasikia mambo mengi na kuyachukua tu pasipo kupambanua.

Tuliwahi kufanya maombi sehemu fulani, tukakuta mtoto wa miaka 5 anatukana matusi makubwa na anarudia tusi hilo hilo moja, mara ya kwanza tulidhani ni mtoto ana mapepo, lakini baadae tuligundua kuwa hana mapepo na hata matusi aliyokuwa anayatamka alikuwa hajui maana yake, alitamka tu akidhani kuwa ni maneno ya kawaida, pasipo kujua kuwa alikuwa anatukana.

Sasa mtoto ni kwamba alisikia hayo matusi pengine kwa watoto wenzake anaocheza nao, wasio na maadili na yeye akidhani ni neno la kawaida akalichukua na kulitumia popote alipoona mazingira hayampendezi.

Sasa mzazi hakuchukua jukumu sahihi la kumrekebisha, badala yake tu alianza kumpiga kila alipotaja hilo neno akidhani kuwa anafanya makusudi, na hata sisi tulipofika alitukana na mamaye alimfinya, lakini alipolia bado aliendelea kutukana.

Mama alidhani mtoto anakiburi na mkorofi, kumbe mtoto alilia akijitetea kwa kudhani kuwa lile neno ni sahihi kutamka mahali pale.

Sasa laiti kama mzazi angepata wasaa wa kumketisha na kumwonya na kumwambia anachokisema si sahihi na hakifai, kabla ya mapigo… mtoto angeelewa na kubadilika.

Kwahiyo ni muhimu kuwasikiliza watoto wanasema nini na kuzirekebisha kauli zao mapema,

Ni vizuri kuangalia watoto wako wanachokiangalia na kukikosoa mbele yao kama hakifai…

Pia ni muhimu kufuatilia michezo yao wanayoicheza na kuikemea mapema mbele yao,…..kwani wao ni kuiga tu siku zote…ni vichache wanabuni wenyewe..

Vingi wanaiga kutoka kwa watu pasipo kupambanua, na wanajifunza kutoka kwa watu wanaowazunguka, ikiwemo wanafunzi wenzao mashuleni na pia kupitia Tv.

Kwahiyo kagua maisha ya watoto wako, na “warudi mapema”..wala hawatakuchukia, au kuwashusha kisaikolojia bali utawajenga kwa maisha yao ya baadae..

usipowarudi mapema na wakikua katika misingi hiyo itakuwa ni ngumu kubadilika ukubwani, kwani ile dhambi wameanza kuifanya tangu utotoni na hivyo hawawezi kushawishika kuona madhara yake ukubwani, na ili hali hawakuona madhara yake utotoni.

Mtoto akiwa na kiburi au mtukutu basi mkanye kila wakati, na panapobidi basi tumia kiboko ila usimwache akakua na hiyo tabia.

Na pia akiwa hasikii, tafuta kila namna awe anasikia, usiache na kusema huyu karithi hiyo tabia kwa watu fulani waliotangulia..

Na pia mfundishe kauli za kibiblia, na kuomba, mfundishe

salamu za kibiblia, na misemo ya kibiblia…akue katika hiyo hata kama bado hajaweza kuipambanua lakini mfanye akariri hivyo hivyo kwani itakuja kumsaidia mbeleni kwasababu itakuwa moyoni mwake.

Kwa kumlea hivyo biblia inasema baadaye atakustarehesha..

Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha”.

Kustarehesha maana yake “hatakuja kukusumbua huko mbeleni”…

Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIOGOPE KUMWADHIBU MWANAO.

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Lango la samaki lilikuwaje? (Sefania 1:10)

Swali: Hili lango la samaki linalotajwa katika Sefania 1:10 lilikuwaje na lilikuwa linahusika na nini?.


Jibu: Yalikuwepo malango kadhaa ya Kulikuwa mji wa Yerusalemu nyakati za zamani, ambayo yalizunguka pande zote za mji.

Baadhi ya malango hayo ni  “Lango la samaki”,  “Lango la kale”, “Lango jipya”Lango la Efraimu” na “Lango la kondoo”, ambalo liitumika kupitishia kondoo katika mji, kwa maelezo marefu juu ya lango hilo fungua hapa >>>

Mlango la kondoo ulikuwaje?(Yohana 5:2)

Lakini kuhusu “Lango la Samaki” turejee maandiko.

Sefania 1:10 “Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani”.

Hili “Lango la Samaki” halikuwa na matumizi kama lile “Lango la Kondoo”…kwamba linatumika kupitisha samaki ndani ya mji.

La! Bali ni lango la mji wa Yerusalemu ambalo lilikuwa upande Kaskazini-magaribi, karibu na “Soko la Samaki”..Hivyo liliitwa jina hilo kufuatia soko la samaki lililokuwa karibu na lango hilo.

Ingawa pia kwasababu lilikuwa upande wa kaskazini, wafanya biashara kutoka Galilaya walilitumia hili, na wengi waliotoka Galilaya walikuwa ni Wavuvi..

Hivyo lilitumika pia na wafanya biashara wa samaki, lakini halikuitwa kwasababu hiyo bali kutokana na soko hilo la samaki lilikokuwa karibu na lango hilo.

Lango la samaki kwanza limeanza kuonekana kipindi cha Mfalme Manase ambaye alikuja kuujenga ukuta wa nje wa mji wa Daudi (Yerusalemu), aliujenga upande wa magharibi mpaka kufikia mlango huo wa samaki.

2 Nyakati 33:12-14 “Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.

13 Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.

14 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya LANGO LA SAMAKI; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma”.

Baada ya miaka mingi kupita, tunakuja kusoma, kipindi ambacho mji wa Yerusalemu umebomolewa na Nehemia amerudi kuujenga ukuta, tunaona biblia inataja kuwa sehemu ya ukuta ya upande wa “Lango la samaki” ulijengwa na wana wa Senaa..

Nehemia 3:3 “Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake”.

Utaona tena lango hilo linatajwa kipindi cha mji kuwekwa wakfu (Nehemia 12:39).

Je umempokea Bwana YESU?..Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa YESU kwa pili?.

Je akija leo na kukukuta hivyo ulivyo utakwenda naye??

Bwana atusaidie sote.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

MGAWANYIKO WA ISHARA ZA UJIO WA BWANA YESU KRISTO.

Ujio wa BWANA YESU duniani umegawanyika katika sehemu kuu Tatu (3).

Sehemu ya Kwanza: Ni kuzaliwa kwake kupitia bikira Mariamu.

Luka 1:30 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake”

Sehemu ya Pili: Unyakuo wa kanisa.

Luka 17:34 “Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.

Unyakuo wa kanisa utakapotokea si kila mtu atajua, na si kila mtu atamwona BWANA YESU, isipokuwa wale tu watakaonyakuliwa na wafu waliokufa katika Bwana… wengine wataendelea na shughuli zao, na biashara zao, na usingizi na wengine waliokufa nje ya Kristo wataendelea katika mauti zao. Na Hatua hii ndiyo tunayoingojea sasa, na hata mmoja wetu hapaswi kuikosa!.

Sehemu ya Tatu: Ujio wa utawala wa miaka elfu moja ambapo kila jicho litamwona.

Ufunuo 1:7 “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina”

Hiki ni kipindi ambacho, wale wote waliosalia kwasababu ya kuukosa unyakuo, na wakabaki kuipokea ile chapa ya mnyama, baadhi yao watakufa katika ile hukumu ya mataifa, na wachache watakaosalia basi watamwona BWANA YESU mawinguni akija kwa nguvu nyingi, na utukufu mwingi, kama umeme wa radi, na wataangamia kwa mwako wake. Na Lengo la KRISTO kuja ni kwaajili ya ule utawala wa miaka elfu unaotajwa katika Ufunuo 20.

> Sasa ZIPO ISHARA ZILIZOTANGULIA KUJA KWA KWANZA KWA KRISTO (yaani kipindi Bwana YESU anazaliwa).

> Na pia ZIPO ISHARA ZINAZOTANGULIA KUJA KWA PILI KWA KRISTO (yaani kipindi cha unyakuo wa kanisa).

> Na pia ZIPO ISHARA ZINAZOTANGULIA KUJA KWA TATU WA KRISTO (yaani kipindi cha utawala wa miaka Elfu, ambapo kila jicho la watakaokuwepo duniani litamwona.)

Kwa ufupi sana tuzitazame ishara hizo au dalili hizo.

1. Ishara za kuja kwa kwanza: Kuzaliwa kwa Bwana.

Ishara kuu ya kuja kwa kwanza, au kukaribia kutokea kwa Bwana duniani ni UJIO WA ELIYA, kwani maandiko yalitabiri kwamba kabla ya kuzaliwa kwa Masihi basi Bwana Mungu atamtuma kwanza mjumbe atakayetangulia kumtengenezea njia, ambaye huyo atakuwa na roho ya Eliya ndani yake, na huyo hakuwa mwingine Zaidi ya Yohana Mbatizaji.

Luka 1:13 “Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.

14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.

15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.

16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.

17 NAYE ATATANGULIA MBELE ZAKE KATIKA ROHO YA ELIYA, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa”

Soma pia Mathayo 11:10 na Mathayo 17:10-13, utaona ishara ya ujio wa Yohana mbatizaji kama Eliya.

Hivyo Yohana Mbatizaji alikuwa ni ishara ya kuja kwa Bwana dunia kwa mara ya kwanza kupitia kuzaliwa katika tumbo la bikira.

Na wote walioweza kumwelewa Yohana kiufunuo, walijua kuwa Masihi amekaribia kutokea au hata tayari kashatokea yupo duniani.

2. Ishara ya kuja kwa Pili: Yaani Unyakuo wa kanisa.

Kabla ya kanisa kunyakuliwa yapo mambo yatakayotangulia kutokea yatakayotambulisha kuwa ule wakati umekaribia au umeshafika, na mambo hayo ni baadhi ya yale yaliyotajwa katika Mathayo 24, na Luka 21 na Marko 13, ambayo ni Tetesi za vita, upendo wa wengi kupoa, maasi kuongezeka na kuzuka kwa manabii wa uongo, ambao watadanganya hata yamkini walio wateule.

Mathayo 24:4 “Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu”.

Ishara hizi hata sasa zimeshatokea, hivyo tumeukaribia sana unyakuo.

Hivyo kwa walio na macho ya rohoni, wakiziona hizo wanatambua kuwa wapo katika siku za kurudi kwa YESU kwa pili na wakati wowote unyakuo unatokea.

3. Ishara ya kutokea kwa tatu kwa Bwana: Kila jicho litamwona.

Huu ni wakati ambao kanisa limeshanyakuliwa, na dhiki kuu imepita, na KRISTO anarejea kwaajili ya utawala wa miaka elfu (na atarejea pamoja na watakatifu walionyakuliwa) sawasawa na ufunuo wa Yuda 1:14.

Na atakaporudi basi wale waliomchoma mkuki ubavuni (wakiwakilisha wale wote waliomkataa, waliopo duniani) wataomboleza na kulia, na wataharibiwa kwa mwako wa ujio wake.

Sasa zipo ishara zitakazotangulia kabla ya yeye kutokea mawinguni, na hizi kanisa hawataziona kwani tayari walishanyakuliwa, bali watakaoziona ni wale watakaokuwa wamesalia dunia na kuipokea chapa ya mnyama.

Luka 21:25 “ Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;

26 watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.

27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi”.

Na moja ya ishara hizo, zitakazotangulia ambazo zitawafanya watu wa mataifa wavunjike mioyo na kuwaza ni nini kitaukumba dunia, ni jua kuzima (kuwa jeusi) pamoja na mwezi kuwa damu na nyota kuanguka.

Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;

30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu”.

Soma pia Isaya 13:9-12 na Ufunuo 6:12-17 utaona unabii wa ishara hiyo na hofu ya mataifa.

Kumbuka tena: Kanisa litakalokwenda kwenye unyakuo halitaona ishara hii ya jua kutiwa giza, na mwezi kuwa damu na nyota kuanguka, kwani ishara hizi zitatokea baada ya dhiki kuu, ambapo kanisa litakuwa halipo, limeenda kwenye unyakuo.

Ndio zaweza kuonekana ishara chache chache mfano wa hizo kama ile iliyotokea katika sehemu za Ulaya mwaka 1780, ambapo giza lilionekana katika sehemu za uingereza, lakini kwa habari ya jua lote kuwa giza, na nyota kuanguka, ni jambo ambao kanisa halitalishuhudia.

Je umempokea YESU na unao uhakika kwamba akirudi leo utaenda naye kwenye unyakuo?.. Kama huna uhakika huo, basi utafute kwa bidii sana.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU KURUDI KWA YESU KUKO KWA NAMNA NGAPI?

MFANYE BWANA YESU MWENYEJI MAISHANI MWAKO.

Je kuwashwa mkono ni ishara ya kupata pesa?

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

Rudi Nyumbani

Print this post

Neno “Msiche” maana yake nini? (Kumbukumbu 1:17)

Jibu: Msiche linatokana na Neno “kucha/kumcha”.. Na maana ya Neno “Kucha” ni “kuhofu”.

Hivyo mtu anapomwofu “mtu”, maana yake anamcha huyo mtu, na pia anapomhofu MUNGU maana yake anamcha Mungu, na matokeo ya kumcha MUNGU ni kumheshimu, kumtumikia, na kufanya mapenzi yake. Lakini mtu asiyemcha MUNGU basi hawezi kufanya hayo yote.

Vile vile mtu anayemcha mwanadamu mwenzake, tafsiri yake ni kwamba anamtumikia, anamheshimu, anamtii na kufanya yale yote mtu huyo anayomwagiza.

Vile vile mtu anayeicha miungu mingine tofauti na MUNGU wa mbingu na nchi, tafsiri yake ni kwamba anaitumikia ile miungu, na kuihofu na kuitii na kuiheshimu.

Hivyo Neno “msiche” ni kinyume cha “kucha/kumcha” na tafsiri yake ni “kutohofu”

1. Mfano wa mistari unayokataza uchaji wa mtu (kumcha mtu)

Kumbukumbu 1:17 “Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; MSICHE USO WA MTU AWAYE YOTE; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza”.

Hapo Bwana MUNGU anakataza watu kuhofu wanadamu wenzao.. Na mistari mingine ni pamoja na Yoshua 10:25.

2. Mfano wa mistari inayotaja kuicha miungu mingine.

2Wafalme 17:35 “hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, MSICHE miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka

37 na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.

38 Na hilo agano nililofanya nanyi, msilisahau; wala MSICHE miungu mingine”

3. Mistari inayotaja uchaji wa MUNGU wa mbingu na nchi. (yaani kumcha MUNGU wa mbingu na Nchi).

Yoshua 24:14 “Basi sasa MCHENI BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana.”

Soma pia Kumbukumbu 13:4, 1Samweli 12:24, Zaburi 22:23, Zaburi 34:9, 1Petro 2:17, na Ufunuo 14:7.

Kwa hitimisho ni kwamba biblia imetukataza TUSICHE miungu yoyote wala mwanadamu yoyote, bali TUMCHE BWANA MUNGU MWETU, aliyetuumba.

Ufunuo 14:7 “akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji”

Je umeokoka?, Je una uhakika BWANA akirudi leo unakwenda naye??… Je huna uhakika huo basi tayari huo ni uthibitisho kuwa akija hutakwenda naye, ni heri ukampokea BWANA YESU LEO, akutakase na kukupa uhakika wa uzima wa milele.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

Kuna Mbingu ngapi?

Mbinguni ni sehemu gani?

Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).

FAHAMU SEHEMU NNE (4)  APANDWAPO MWAMINI.

Rudi Nyumbani

Print this post

PIGO LA KUFA KWA WAZALIWA WA KWANZA

Jina tukufu la Bwana YESU KRISTO libarikiwe.

Je umewahi kutafakari kwanini mapigo yote tisa (9) aliyopigwa Farao bado moyo wake ulikuwa mgumu? Na kwanini lile pigo moja la mwisho la kufa wazaliwa wa kwanza ndipo akawaruhusu wana wa Israeli?.

Sasa hakuna mahali popote maandiko yanasema kuwa “Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mlaini”.

Maana yake Farao aliendelea kuwa na moyo mgumu mpaka alipoingia kwenye ile bahari ya Shamu, na hapo ndio ikawa mwisho wake.

Sasa ni nini kilitokea mpaka Farao akawaachia wana wa Israeli?… Si kingine bali ni ule msiba alioupata,

Na huku bado moyo wake ukiendelea kuwa mgumu, alivunja sheria ya moyo wake na kuwafukuza wana wa Israeli kwa muda. (Lakini moyo wake bado ulikuwa mgumu tu).

Kutoka 11:1 “BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa”

Sasa ni siri gani iliyokuwepo ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri hata kumfanya Farao awafukuze wana wa Israeli?…Kwani ni wazi kuwa hata Farao angepigwa kwa mapigo gani ya asili asingewaachia wana wa Israeli.

Ila ni nini kilikuwa kwa wazaliwa wa kwanza wa kiMisri?

Kilichokuwa ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri, ikiwemo mwana wa Farao si kingine zaidi ya “miungu ya kimisri”..

Hivyo kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa ni hukumu kubwa kwa miungu yao pamoja kudhalilika kwa miungu yao ambao waliamini ina nguvu nyingi.

Ndio maana MUNGU aliposhuka kuwaharibu wazaliwa wa kwanza pia alisema ataiharibu na miungu yao (ambayo kiuhalisia ilikuwa inaishi ndani ya hao wazaliwa wa kwanza).

Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, namij nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.”

Zamani katika nchi ya Misri na hata katika mataifa mengine ya dunia, wazaliwa wa kwanza wa kiume waliaminika kama miungu ya familia na ya nchi.

Na wanyama wa kwanza kuzaliwa, ndio waliotumika kwa kafara za miungu yao.

Hivyo watoto wote wa kwanza wa kiume walikuwa wanabeba ukuhani wa miungu, na roho zote za miungu zilikuwa zinakaa ndani yao.

Kwahiyo kilichomwumiza zaidi Farao si msiba wa mtoto, bali ni kuhukumiwa kwa miungu yao iliyokuwepo ndani ya wale watoto!!..

Kwaufupi Farao alichanganyikiwa kidogo, hakuelewa ni nini kimetokea katika eneo lake la imani.

Na hata waMisri wote walichanganyikiwa vivyo hivyo, hakuna ambaye hakulia..wote walilia na kuhofu na kutoelewa ni nini cha kufanya, waliyeyuka mpaka kufikia hatua ya wana wa Israeli kuwateka nyara.

Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.

34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.

35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.

36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara”

Ni ujumbe gani tunapata hapo?..au ni kitu gani kilichokuwa kimewafunga wana wa Israeli?

Si utajiri wala hazina zilizoko Misri kwamaana Bwana aliuharibu utajiri wake wote kwa zile mvua za mawe na nzige, vile vile si uzuri wa Misri, kwasababu Bwana aliharibu uzuri wake kwa zile mvua za mawe lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.

Wala si ushujaa wa waMisri kwasababu Bwana aliwapiga kwa chawa, na majipu na aliwanyima maji ya kunywa kwa siku saba, hivyo walikuwa dhaifu..lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.

Ni nini kilichokuwa kimewashikilia wana wa Israeli???…..jibu ni “miungu ya kimisri” iliyokuwa inaabudiwa ndani ya watu.

Hiyo ilipopigwa pamoja na makuhani wake (ambao ndio wazaliwa wa kwanza)..vifungo vikalegea, wana wa Israeli wakaachiwa.

Laiti Bwana Mungu angelileta hilo pigo mwanzoni kabla ya yote, Farao angeshaawaachia Israeli kitambo sana pamoja na moyo wake kuwa mgumu, lakini Mungu aliliruhusu liwe mwisho wa kusudi lake maalumu.

Na ukiendelea kusoma mbele utaona Bwana anawapa amri wana wa Israeli wawatakase wazaliwa wa kwanza na kwamba kila mzaliwa wa kwanza atakuwa ni wa Bwana, maana yake atakuwa kuhani wa Bwana kwa lazima (kwasababu kulikuwa na kitu katika wazaliwa wa kwanza).

Maana yake kila mzaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli alipaswa kutolewa kwa Bwana kama Hana alivyomtoa Samweli kwa Bwana (hiyo ilikuwa ni amri).

Lakini sheria hiyo ilikuja kubadilika, na ukuhani wa wazaliwa wa kwanza likapewa kabila la Lawi.

Hesabu 3:12 “Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu;

13 kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA”.

Hivyo wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wanaozaliwa ilikuwa ni sharti wakombolewe kwa sadaka ili watokane na kiapo hiko cha Bwana cha kuwa makuhani.

Na maana ya kukombolewa si kutolewa katika vifungo vya laana, kama mafundisho ya siku hizi za mwisho yanavyofundisha.

Bali ukombozi ilikiwa ni ile hali ya mtoto kutolewa katika nafasi ya kikuhani ambayo angepaswa kuitumikia maisha yake yote.

Hivyo anapokombolewa anakuwa huru kama watu wengine wasio na utumishi wa kikuhani (kwa ufupi anafunguliwa kutoka katika vifungo vya ukuhani)

Na mtoto wa kwanza asipokombolewa anabaki katika kifungo cha dhambi ya nafasi ya kikuhani.

Sasa swali je hata sasa katika agano jipya tunasheria hizo za kukomboa mzaliwa wa kwanza?.

Jibu ni la!..katika agano jipya hatuna sheria za kumkomboa mzaliwa wa kwanza au wa mwisho, kwasababu sote tuliomwamini Bwana YESU na kutakaswa kwa damu yake tunafanyika kuwa makuhani wa Bwana.

Ufunuo wa Yohana 1:6 “na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.

Hivyo sote tunayo huduma ya kikuhani na mbele za Mungu, na ukishakuwa tu kuhani tayari ni mzaliwa wa kwanza pasipo kujali rika…Hivyo kanisa la Kristo ni wazaliwa wa kwanza.

Waebrania 12:23 “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika”.

Kwahiyo hakuna sadaka yoyote ya ukombozi kwa wazaliwa wa kwanza kwa jinsi ya mwili.

Mafundisho na maombi ya kukombolewa kwa wazaliwa wa kwanza si ya kiMungu, bali ni ya ibilisi.

Ndio tunaweza kuwaombea wazaliwa wetu wa kwanza na kuwaweka wakfu kwa Bwana, dhidi ya roho zinazofuatilia, lakini si kuwakomboa….uwakomboe na nini?…je uwakomboe uwatoe katika ukuhani?…maana ndio lengo la ukombozi hilo kibiblia lililokuwepo juu ya wana wa Israeli juu ya wazaliwa wa kwanza.

Zaidi sana watoto wetu wa kwanza wanapaswa wawe wazaliwa wa kwanza kiroho kwa kumwamini YESU na kutakaswa ndipo wanapofanyika makuhani kama wengine wote waliomwamini YESU.

Mwisho, fahamu kuwa kilichowafuga wana wa Israeli ni miungu ya misri, iliyokuwa inaabimudiwa ndani ya kila kiumbe kilichokuwa cha kwanza.

Hali kadhalika vile vitu vinavyojiinua katika maisha yetu vilivyo vya kwanza ndivyo ni lazima tuwe navyo makini kwani hivyo ibilisi anaweza kuvitumia kama mlango wa kutufunga.

Je cha kwanza kwako ni nini?…je ni kazi uliyonayo?…au ni cheo ulicho nacho?..au ni uzuri au ni Bwana YESU?..

Ni heri BWANA YESU akawa wa kwanza kwako, kwani yeye ndiye njia, kweli na Uzima.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

 UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.

USIMWABUDU SHETANI!

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je! ndoa ni lazima ifungwe kanisani? kama ndio, imeandikwa wapi?

SWALI: Je! tunalisoma wapi kwenye maandiko panasema ndoa inapaswa ifungwe kanisani. Utaratibu huo upoje?


JIBU: Ili kujibu swali hili tuanzie mbali kidogo.

kufahamu ndoa ni nini? aina za ndoa, kisha mahali sahihi pa kufungia ndoa ni wapi?.

Ndoa ni nini?

Ndoa ni muunganiko kati ya watu wawili(mwanaume na mwanamke ) unaotambulika na kuheshika kijamii, au kisheria.

Pale mwanaume anapomwona mwanamke na kupatana naye waishi pamoja kama mume na mke, kwa kufuata taratibu husika za kijamii, labda kukutanishwa kwanza wazazi, au walezi, wazee wa ukoo, kupokea mahari, kisha kuidhinisha jambo hilo, au serikali kuidhinisha, hiyo tayari inaitwa ndoa.

Aina mbili za ndoa.

  1. Ndoa za wapagani
  2. Ndoa za kikristo.

Ndoa za wapagani. Hizi ni ndoa lakini hazijadhibitiwa na kanuni timilifu za Mungu. Mfano wa hizi, ndio hizo kama za kijamii, na kiserikali, au za dini nyingine zote mfano wa ki-hindu, kiislamu, ki-budha n.k. zote hizi ni ndoa za wapagani.

Zingatia: (Hapa hatumaanishi zile za mashetani, kama za jinsia moja, au za wanadamu na wanyama hapana kwasababu hizo sio ndoa, bali tunazungumzia hizi za kawaida kabisa za asili).

Kiuhalisia mtu anaweza akawa katika mojawapo ya ndoa hizi, na asihesabike kuwa ni mkosaji kwasababu ndoa hasa ni jambo la kiutamaduni, ambalo huusisha wanadamu wote, bila kuchagua dini, rangi, au kabila.

Hivyo si sawa kudhani kuwa kwasababu watu fulani hawajafungishwa ndoa kikristo(kanisani) basi, zote hizo sio ndoa kwamba ni sawa tu hata kwenda kuoa tena hapo, au kuivuruga, wasiishi pamoja. Ukifanya hivyo Mungu atakuwajibisha kwa kuzivuruga ndoa za watu wengine. 

Aina ya pili ya ndoa ni ndoa ya kikristo.

Hii ni ndoa inayofungwa katika kanuni timilifu za Mungu alizozikusudia tangu mwanzo.

Kanuni zenyewe ni hizi

    i) Wote wawe waamini.

(1Wakorintho 7:39, 1Wakorintho 9:5, 2Wakorintho 6:14 – 16)

Kuamini si lazima muwe katika viwango sawa kiroho, lakini wote muwe upande mmoja wa Kristo, (Kwasababu hayo mengine yanaweza rekebika). Lakini mmoja ni mganga wa kienyeji, mwingine mkristo,.au mmoja ni muislamu mwingine mkristo. Hilo si sawa ni sharti wote wawe wakristo. Kwasababu hakuna ushirika wowote kati ya nuru na giza.

Kwasababu Ndoa ya kikristo ni lazima iwe katika jina la Bwana, vinginevyo, itaangukia katika lile kundi lingine.

      ii) Mume mmoja, mke mmoja.

Tofauti na ndoa za wapagani. Ambazo kwao unaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini mtu anayetaka ndoa yake itimilike mbele za Kristo, basi mume/mke atambue kuwa hana ruhusa ya kuongoza mwenza mwingine. 

Mathayo 19:4-5

[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 

[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? a

      iii) Malazi yawe safi:

Waebrania 13:4

[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. 

Malazi kuwa safi maana yake ni nidhamu ya kiasi, katika kukutana kimwili. Mkristo hapaswi kuwa mtu wa hulka ambaye wakati wote anawaza zinaa, mpaka anakosa muda wa kujishughulisha na mambo ya rohoni.

1 Wakorintho 7:5

[5]Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 

Vilevile viitendo kama kuingiliana kinyume na maumbile haviruhusiwi ndani ya ndoa (1Wakorintho 6:9).

      iv) Hakuna talaka. 

Tofauti na ndoa za wapagani, mtu anaweza kuacha/kuachwa kwa sababu yoyote, labda mfano wamechokana, au wameudhiana, lakini katika ukristo hilo jambo halipo mtaendelea kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha. 

Bwana alitoa ruhusa hiyo katika eneo la uasherati tu lakini ukumbuke, alisema pia ‘samehe mara saba sabini’. Hivyo kwa kauli hiyo hakuna popote tunaona wigo wa wanandoa kuachana kwa sababu yoyote ile.(1Wakorintho 7:39-40)

      V) Mume ni sharti ampende mkewe. 

Mume kumpenda mkewe ni amri ya kindoa, anawajibu wa kumtunza na kumuhudumia na kujitoa kwa ajili yake, kama Kristo alivyolipenda kanisa.(Waefeso 5:25-31)

     Vi) Mke ni sharti amtii mumewe.

Ni amri mke amtii mumewe kwa agizo atakaloambiwa/ elekezwa. Tofauti na ndoa za wapagani ambazo hili linaweza lisiwe la muhimu. Kwenye ukristo, ni lazima utii wa mwanamke uonekane kwa mumewe.

Waefeso 5:22

[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 

Sasa vigezo hivi wakivikidhi hawa wakristo ambao wameokoka na wanatarajia kuishi kama mke na mume. Basi hiyo huitwa  ndoa ya Kikristo iliyokidhi vigezo vitimilifu vya Mungu,.haijalishi imefungwa kanisani au kwenye familia, .

Swali ni je? kwanini watu wafungie kanisani? Na  Je ni takwa? 

Mkristo ambaye anathamini ukamilifu wote wa ki-Mungu, katika maeneo yake yote ya kiroho na kimwili, kufungia ndoa yake kanisani itakuwa ndio chaguo lake bora. Kwanini iwe hivyo?

Hizi ndio faida za ndoa kufungiwa kanisani

  1.  Kanisa ni mahakama ya wakristo

Biblia inatueleza mashtaka yetu, hayapaswi kutatuliwa na watu wa ulimwengu, bali ndani ya kanisa. Kwasababu kanisa ni zaidi ya mahakama yoyote, ambayo Mungu ameiheshimu mpaka akaamua malaika zake wahukumiwe katika hiyo.

Hivyo endapo kuna migogoro, au kutoelewana, au kupatiwa misaada, au mashauri, au maonyo, au maongozi,  basi kanisa, limewekwa na Mungu kwa ajili yako kukusaidia katika hayo yote. 

Lakini ikiwa hukuifungia ndoa yako kanisani. Fahamu kuna mambo kama hayo yatakupita, au yatakuwa magumu kwetu kutatulika.

1 Wakorintho 6:1-3

[1]Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 

[2]Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 

[3]Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? 

    2) Ushuhuda mwema.

Mungu anapenda mambo mema atufanyiayo tumtukuze mbele ya kusanyiko la watakatifu. Tunajua Ndoa ni kitu chema, hivyo tunapoweka wazi mbele za Bwana,  na mbele ya kanisa lake, yeye hutukuzwa lakini pia tunapokea baraka za kanisa, Ikiwa tunapoumwa na kuponywa hatuoni sawa kukaa na shuhuda zetu ndani, tunakwenda kushuhudia mbele ya kanisa, si zaidi ndoa zetu?, ni ushuhuda mkubwa, ambao utawafariji wengine, lakini pia utaihubiri injili ya Kristo.

Zaburi 35:18

[18]Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; 

Nitakusifu kati ya watu wengi. 

Hivyo, kwa maelezo hayo tunaweza kusema hakuna sababu ya Mkristo yoyote kuifungia ndoa yake, mbali na kanisa. 

Lakini hiyo haimaanishi kuwa usipofungia kanisani, ndoa yake haitambuliwi na Mungu. Maadamu umekidhi vigezo “mama”, tulivyoviorodhesha juu. Hiyo ni ndoa.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAFUNDISHO YA NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je wakati Bwana YESU anazaliwa shetani alikuwa amefungwa?

Swali: Je Bwana YESU alikuwa amemfunga shetani wakati wa kuzaliwa kwake Kulingana na Mathayo 12:29?


Jibu: Turejee.

Mathayo 12:29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.

Jibu ni kwamba shetani hakuwa amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana YESU, na hata sasa shetani hajafungwa!, kwani Ingekuwa shetani amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana, basi Herode asingetafuta kumwua mtoto..

Mathayo 2:13 “Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize”.

Tukio hilo linaeleweka vizuri katika Ufunuo 12:1-6.

Vile vile Ibilisi asingesimama kumjaribu Bwana kule jangwani..

Mathayo 4:1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ILI AJARIBIWE NA IBILISI.

2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate”

Na ikiwa shetani amefungwa leo, maasi yasingeendelea kuwepo na maandiko yasingetuonya kuwa tusimpe nafasi..

Waefeso 4:28 “wala msimpe Ibilisi nafasi.

28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji”.

Maandiko yametabiri shetani kuja kufungwa katika ule utawala wa miaka elfu wa Bwana wetu YESU hapa duniani. Na utawala huo utaanza baada ya dhiki kuu kuisha, na hukumu ya Mungu kwa mataifa kupita (Ufunuo 16), hapo ndipo utawala wa miaka elfu moja utakapoanza na shetani (pamoja na majeshi yake) kufungwa kwa kipindi hiko.

Ufunuo 20:1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.

2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;

3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.

Kwahiyo shetani kwasasa yupo na hakuwahi kufungwa wakati wowote huko nyuma, lakini atakuja kufungwa baada ya hukumu ya Mungu kwa mataifa inayotajwa katika Ufunuo 16.

Sasa swali kama ni hivyo je! Maandiko hayo katika Mathayo 12:29 yana maana gani?….

Turejee tena..

Mathayo 12:29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.

Haya ni maneno ambayo Bwana YESU aliyasema, akifundisha nguvu iliyo kuu/kubwa inapoingia mahali basi inateka au inafunga ile nguvu iliyo dhaifu.

Na ukisoma kuanzia juu kidogo utaona ni wakati ambapo Mafarisayo walimwona akitoa pepo kwa uweza wa Mungu, lakini wakasema yeye hatoi kwa uweza wa Mungu bali kwa uwezo wa Pepo mkuu aitwaye Beelzebuli, ambaye ni shetani mwenyewe.

Na Bwana akawahoji, akiwauliza yawezekanaje Shetani amtoe shetani mwenzake?..jambo ambalo haliwezekani!, vinginevyo ufalme wa giza hauwezi kusimama, lakini kama wakiona pepo katolewa maana yake katolewa kwa uweza wa Mungu, kwasababu kamwe shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake.

Na ili kulifanya hilo lizidi kueleweka vizuri ndipo akatoa mfano mwingine kwamba… “Awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”

Ikifunua kuwa Bwana anapotoa pepo, kwanza anauteka ule ufalme wa giza (maana yake wote unakuwa chini ya amri yake) halafu ndipo anaamrisha pepo zitoke na kwenda atakako yeye soma Mathayo 8:28-32.

Sasa kitendo cha Bwana YESU kusimama na kuamrisha, maana yake mamlaka yake ni KUU inayoteka, na kufunga, na kuhamisha.. Na mamlaka hiyo hajabaki kwake tu peke yake, bali pia amewapa na wale wote wanaomwamini na kufanya mapenzi yake, kwamba kwa jina lake wanateka, na wanafunga na kuhamisha kila falme za giza.

2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO;

6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.

Kwahiyo mantiki ya Bwana YESU hapo ya KUFUNGA, haikuwa ya kumfunga shetani asiwepo duniani, bali katika kuzifunga kazi za ibilisi na majeshi yake zisisimame mbele yetu. (lakini shetani yupo, na ataendelea kuwepo na kuwasumbua wale wote wasiomwamini na kumfuata Bwana YESU), lakini walio na Bwana shetani hana nguvu juu yao.

Mathayo 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni”.

Je umeokoka??..Hizi ni siku za hatari na BWANA anarudi. Na shetani anajua wakati wake uliobaki ni mchache sana, hivyo anafanya kazi kwa kasi sana kusudi asiende kwenye lile ziwa la moto peke yake.

Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”

Je bado wewe ni rafiki wa dunia?, bado ni mshabiki wa mipira, bado unacheza Kamari, bado unavaa kidunia na kuupenda ulimwengu?

1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je YUDA alikuwa ni shetani kulingana na Yohana 6:70?

NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?

Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?

Nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.

Kusujudu ni nini, na je tuna sharti la kusujudu kwa Mungu?

Rudi Nyumbani

Print this post