Shalom, Mwana wa Mungu karibu tujifunze maandiko…Leo tutajifunza kwa Neema za Bwana namna ya kuokoa roho.
Bwana Yesu alisema “sikuja kuziangamiza roho bali kuziokoa (Luka 9:56)” sentensi hiyo aliisema baada ya wanafunzi wake kumwomba ashushe moto uwaangamiza wale watu wa Samaria waliokataa kumpokea…Lakini kwanini alisema vile kuwa hakuja kuziangamiza bali kuziokoa?…ni kwasababu alikuwa na uwezo wa kuziangamiza lakini hakutaka kufanya vile..kinyume chake alitafuta namna ya kuwafikishia wokovu na sio kuwaua.
Wakati mwingine tunaweza tukawa na silaha mikononi mwetu au midomoni mwetu tulizopewa na Mungu kihalali kabisa za kujeruhi na kuangusha watu wote wanaokwenda kinyume na sisi..lakini tukikosa hekima kama aliyokuwa nayo Bwana tutajikuta tunaangamiza roho badala ya kuokoa.
Hebu mtafakari Musa, wakati wana wa Israeli wanamkosea Mungu kule jangwani…Mungu alimwambia Musa ajitenge na wale watu ili apate kuwaangamiza…na atamfanya Musa kuwa Taifa kubwa, atampa uzao utakaoirithi nchi….ingekuwa ni mmojawapo wa sisi tungesema asante Mungu, kwa kuwa umeteta nao wanaoteta nami, lakini tunaona Musa, alilipindua wazo la Mungu na kuanza kuwaombea msamaha ndugu zake na kuwatafutia upatanisho na Mungu, na Mungu akalisikiliza ushauri wa Musa na kughairi mawazo yake…
Sasa tuchukulie mfano Musa, angekubali kujitenga nao, unadhani, kulikuwa kuna kosa lolote pale? hapana Mungu kweli angewaangamiza wale watu na angeenda kumfanya Musa kuwa Taifa kubwa kama alivyomwahidia..Lakini Musa angekuwa hajatenda kwa busara mashauri yale yalitoka kweli kwa Mungu, angekuwa hajastahili kuwa kiongozi bora kwasababu hakuizuia ghadhabu ya Mungu juu ya watu wake. Kwahiyo pengine hata Mungu asingemtukuza Musa kwa kiwango hichi alichomtukuza sasa.
Kutoka 32:9 “Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu 10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. 11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. 13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. 14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake”.
Kutoka 32:9 “Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu
10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.
14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake”.
Kwahiyo hiyo inatufundisha kuwa siyo kila fursa au mamlaka tunayopewa na Mungu, tuyatumie tu bila kutafakari vizuri..Mungu wetu hajatuumba kama maroboti kwamba yeye ni wa kusema na sisi ni wakufuata tu pasipo kutafakari..hapana! huo ni utumwa na sisi sio watumwa sisi ni wana, tunazungumza na Baba yetu na kushauriana naye…ametuumba tuzungumze naye, tusemezane naye, tupeane naye mashauri.
Isaya 1: 18 “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”.
Ndio maana Musa alisemezana na Bwana na akasafisha dhambi za wana wa Israeli zilizokuwa nyekundu kama bendera, na akazifanya kuwa nyeupe kama sufu. Haleluya!
Mungu anaweza kumweka mtu anayekuchukia, au anayekupiga vita mikononi mwako, au mtu ambaye alikufanyia visa Fulani, ukapata madhara fulani…Mungu anaweza kumweka mikononi mwako kiasi kwamba ukisema tu neno moja umemmaliza, au ukifanya jambo Fulani tu, habari yake imekwisha ikawa ni kweli Mungu kamtia mikononi mwako ili kumlipizia kisasi, kwa ubaya aliokufanyia….kama vile Mungu alivyomtia Sauli mikononi mwa Daudi..akajua kabisa hii ni fursa ya kummaliza lakini hakufanya hivyo…nasi pia huo usiwe wakati wa kummaliza, badala yake uitumie fursa hiyo kumgeuza kwa Kristo, huo ndio wakati wa kusemezana na Bwana juu ya dhambi zake zote, na kumwombea Msamaha…hakika ukifanya hivyo na kuigeuza hasira ya Bwana, Bwana atakupenda zaidi ya anavyokupenda sasa…atakutukuza zaidi ya anavyokutukuza sasa…
Utasema hiyo habari ya Musa na Daudi ilikuwa ni ya agano la kale, vipi kuhusu agano jipya, je! Kuna mtu yeyote alishawahi kufanya hivyo..Jibu ni ndio! Hata katika agano jipya tunayo hiyo mifano.
Tunasoma habari za Paulo na wenzake, wakati mmoja walipokwenda Makedonia kuhubiri, walikutana na mtu mwenye pepo na walipomtoa Yule pepo, ndipo wakuu wa mji wakawakamata na kuwachapa bakora na kisha kuwatupa gerezani.
Sasa lile jambo halikumpendeza sana Mungu, na hivyo Bwana akawatengenezea njia ya kutoka mule gerezani, akamtuma malaika wake usiku ule wakati Paulo na Sila walipokuwa wanamsifu Mungu, ghafla vifungo vikalegea na milango ya gereza ikafunguka…sasa Lengo la Yule malaika kufungua milango ya gereza haikuwa tu kuwafurahisha wale watu , hapana ilikuwa ni ili Paulo na Sila watoke!!, waondoke mule gerezani,..Kama vile Yule malaika alivyomtoa Petro gerezani wakati Fulani alipokuwa amefungwa.
Lakini tunasoma Paulo na Sila walilitengua agizo la Bwana, badala ya kutoka na kwenda zao, waliendelea kukaa mule gerezani japokuwa Mungu aliwafungulia mlango wa kutoka…lakini walitafakari mara mbili mbili, endapo tukitoka na kwenda zetu tutakuwa kweli hatujatenda dhambi lakini tutaacha madhara makubwa huku nyuma, tutasababisha kifo badala ya kuokoa roho, na zamani zile utawala wa Rumi, mfungwa yoyote akitoroka kinachobakia kwake ni kifo tu, na ndio maana Yule askari ilikuwa nusu ajiue, lakini Paulo na Sila wakamzuia.
kwahiyo wakaitumia ile nafasi sio kwa faida yao bali kwa faida ya wengine, ndio tunaona wakaenda kumwuhubiria Yule askari injili pamoja na familia yake wote wakaokoka, na mwisho wa siku kesho yake asubuhi wakatolewa gerezani, kwahiyo ikawa faida kwao mara mbili.
Matendo 16: 22 “Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. 23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana. 24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale. 25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26 GHAFULA PAKAWA TETEMEKO KUU LA NCHI, HATA MISINGI YA GEREZA IKATIKISIKA, NA MARA HIYO MILANGO IKAFUNGUKA, VIFUNGO VYA WOTE VIKALEGEZWA. 27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia 28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa. 29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila; 30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo. 34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu. 35 Kulipopambauka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao. 36 Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Makadhi wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani”.
Matendo 16: 22 “Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
24 Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mkatale.
25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
26 GHAFULA PAKAWA TETEMEKO KUU LA NCHI, HATA MISINGI YA GEREZA IKATIKISIKA, NA MARA HIYO MILANGO IKAFUNGUKA, VIFUNGO VYA WOTE VIKALEGEZWA.
27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia
28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.
29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;
30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.
33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.
34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.
35 Kulipopambauka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.
36 Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paulo maneno haya akisema, Makadhi wametuma watu ili mfunguliwe; basi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani”.
Sasa hebu fikiri endapo Paulo na Sila wangeondoka usiku ule mule gerezani, na kusema safi sana! Mungu katupigania! Kawaaibisha maadui zetu!…. ni wazi kuwa wangeshampoteza Askari na kusudi la wao kwenda makedonia lingekuwa ni sifuri kwa maana wenyewe walikwenda kwa nia ya kuhubiri injili, na sasa hapa ni sawa na wamemsababishia wengine mauti.
Kwahiyo ndugu tunajifunza, sio kila fursa ya kumpiga adui yako ni mapenzi kamili ya Mungu, sio kila mlango Mungu anaokufungulia ni wa kuutumia pasipo kutafakari, aliyekutukana, aliyekuaibisha, aliyekupiga, aliyekunyima kazi wakati Fulani tena akakufanyia na visa juu, aliyekurusha, aliyekuharibia mipango yako na maisha yako, sasa Mungu kamleta mikononi mwako..huo sio wakati wa kuitumia hiyo fursa Mungu aliyokuwekea mbele yako pasipo hekima!! Itumie hiyo KUOKOA ROHO, BADALA YA KUANGAMIZA. Hicho ndio kitu Mungu anachotaka kuona kwetu!.
Kuna muhubiri mmoja, ambaye alikuwa ni Nabii, siku moja wakati anahubiri kanisani kwake malaika wa Bwana alimwambia atazame mwisho kabisa wa kanisa, na alipotazama akaona watu wawili kwa mbali mwanamume na mwanamke wanafanya kitendo kichafu cha kunyonyana ndimi na hiyo ilikuwa ni katikati ya ibada…Yule muhubiri akakasirika sana, akawa anawaendea…wakati yupo njiani anawaendea Yule malaika aliyemwambia atazame nyuma ya kanisa, huyo huyo akamwambia sema Neno lolote na mimi nitalitimiza hilo neno saa hivi hivi kama ulivyosema…yaani maana yake angesema “Bwana naomba waanguke sasa hivi wafe, wangekufa saa ile ile”..na alipofika pale Yule muhubiri..kitu fulani kikamwingia ndani yake, kama huruma Fulani hivi… akasema “nimewasamehe”…Baadaye alivyomaliza ibada, sauti ikazungumza ndani ya moyo wake na kumwambia..”hicho ndio nilichokuwa nataka kusikia kutoka kwako”…msamaha…
Ni wazi kuwa hao watu kwa msamaha huo, baadaye walitubu na kumgeukia Mungu kwa kumaanisha.
Umeona? Epuka injili unazohubiriwa kila wakati piga adui yako, usiposamehe kuna wakati nawe utafika utamkosea Mungu, naye Mungu hatakusamehe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Mada Zinazoendana:
VITA DHIDI YA MAADUI
KISASI NI JUU YA BWANA.
NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
Rudi Nyumbani
Print this post
Kutoka 20:7 “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure..”
Hii ni moja ya amri tulioizoea sana, Na tumekuwa tukidhani kulitaja jina la Mungu bure ni pale tu tunapo muhusisha na mambo yasiyo na maana, au pale tunapo apa, lakini hiyo ni sehemu mojawapo ya kulitaja bure jina la Mungu, ipo sehemu nyingine ambayo ni kuu zaidi, na inamuudhi Mungu sana, pengine na wewe ulishawahi kuifanya bila kujua na pengine ndio imekuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio ya roho yako.
Pale unaposema leo nimeamua kuwa Mkristo nimeamua kumfuata Mungu kwa moyo wangu wote, pale unaposema maisha yangu ya kale basi, hapo ni sawa na umemwita Mungu aje kuyaongoza maisha yako kuanzia huo wakati na kuendelea, au kwa lugha ki-kibiblia tunasema umeliitia jina la Mungu lije kukuokoa, lakini pale unaposema Nimeokoka, mimi ni mkristo halafu, unaendelea kuyafanya yale yale uliyoyaacha kule nyuma, unaendelea kuiba,unazidi kuzini, unatazama pornography, unasengenya n.k. Hapo ni sawa kabisa na umemdhahaki Mungu kwamba ulimwita akuokoe na kumbe haupo tayari kuokolewa, Hapo umelitaja JINA LA MUNGU wako bure!.. Ni heri usingedhubutu kuujaribu wokovu kabisa maishani mwako ..
Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo utaona watu walioanza kumtafuta Mungu, biblia imetafsiri kama “waliliita au wanalitaja Jina la Mungu”
Mwanzo 4: 25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua. 26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA”.
Mwanzo 4: 25 “Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA”.
Utaona pia katika maandiko BWANA akitangaza jina lake yeye mwenyewe…utaona halitaji jina lake kama YEHOVA, bali analitaja jina lake kama TABIA..Tunalisoma hilo katika kitabu cha Kutoka.
Kutoka 34: 5 “Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, AKALITANGAZA JINA LA BWANA. 6 Bwana akapita mbele yake, AKATANGAZA, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; WALA SI MWENYE KUMHESABIA MTU MWOVU KUWA HANA HATIA KAMWE; MWENYE KUWAPATILIZA WATOTO UOVU WA BABA ZAO, NA WANA WA WANA WAO PIA, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE”.
Kutoka 34: 5 “Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, AKALITANGAZA JINA LA BWANA.
6 Bwana akapita mbele yake, AKATANGAZA, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; WALA SI MWENYE KUMHESABIA MTU MWOVU KUWA HANA HATIA KAMWE; MWENYE KUWAPATILIZA WATOTO UOVU WA BABA ZAO, NA WANA WA WANA WAO PIA, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE”.
Unaona mstari wa saba hapo?…tafsiri ya jina lake sio tu Mungu mwenye huruma bali pia ni MUNGU asiyeacha kumwesabia mtu mwovu kuwa hana makosa kamwe. Kwahiyo unapompokea Kristo maishani mwako halafu maisha yako yapo vilevile hayabadiliki…Hapo ni sawa na umelitaja jina Bwana Mungu wako Bure na atakuhesabia kuwa na hatia kwa hilo.
Embu tafakari mfano huu halafu wewe uhukumu, ni sawa na leo mtu ameagiza gari nje ya nchi labda tuseme Japan kwa makubaliano ya kuwa siku litakapofika ndipo atalilipa..Lakini siku linafika ili akabidhiwe gari lake afanye malipo biashara iishe, anageuka na kusema mimi sina haja na hilo gari kwanza nilikuwa ninawatania tu, labda siku nyingine nikiwa tayari.
Wewe unadhani, wale watu watamfanyaje?. Ni dhahiri kuwa hawawezi kumwacha hivi hivi waingie hasara kwa ajili ya uzembe wake, hivyo hapo kama hatatozwa faini, basi atafunguliwa mashtaka mahakani, na mwisho wa siku lazima atajikuta analipa mpaka senti ya mwisho kwa njia yoyote ile,…Na ndivyo ilivyo kwa Mungu, tunapolitaja jina lake, (JINA LA YESU ambalo hakuna jingine zaidi ya hilo ambalo litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo 4:12) lije lituokoe, tuonyeshe kweli kweli kutaka kuokolewa vinginevyo , Bwana hatutacha hivi hivi bila kutuhesabia kuwa wenye hatia..wakati mwingine mapigo au vifo vinatukuta kwa sababu hiyo.
Na ndio maana mtunzi wa Mithali alisema.. 30:8 “Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. 9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana NIKAIBA, NA KULITAJA BURE JINA LA MUNGU WANGU”.
Unaona huyu mtu alijua kabisa dhambi za wizi ni sawa na kulitaja jina la Mungu wake bure.
Na sisi pia kama tunalitaja jina la YESU mwokozi wetu kuwa ndio jina pekee linalotusababisha kuwa hivi tulivyo leo ndani ya wokovu basi na tuuweke ulimwengu mbali na sisi tumfuate Mungu wetu kweli kweli kwa kumaanisha..ili tujiepushe na laana, Kwasababu maandiko ndivyo yanavyotuonya.
2Timotheo 2:19 “..KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU”.
Jina la Kristo lisitamkwe kinywani mwako kama haupo tayari kuuacha ouvu..Na unaacha uovu kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutokuzifanya tena, na kisha kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO na lihimidiwe daima..
Amen.
Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
JINA LA MUNGU NI LIPI?
JINA LAKO NI LA NANI?
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
KANUNI JUU YA KANUNI.
⭃Ukisoma kitabu cha Ayubu utagundua kuwa jaribu kubwa shetani alilomshambulia Ayubu halikuwa Kufiwa na wanawe au kupoteza mali zake zote ndani ya siku moja! Hayo kweli yalimuumiza sana…lakini utaona Ayubu hakuongea lolote kuhusu hayo…Alisema tu BWANA ALITOA na BWANA AMETWAA…Jina la Bwana libarikiwe. Basi akaishia hapo! Ndio maana unaona mpaka sura ya Pili habari ya Ayubu inakuwa imeshaisha…
Lakini kuanzia sura ya 3 hadi ya 42…utaona ni habari nyingine zinaanza kuzungumziwa hapo…utaona ni mazungumzo kati ya watu watatu mpaka wane…Ayubu, Sofari, Bildadi na Elifazi…akitoka huyu anaongea huyu, akitoka huyo sofari anaongea bildadi, akitoka bildadi anaongea Ayubu hivyo hivyo mpaka mpaka sura ya 40.
Sasa wengi wetu tunapenda kusoma tu ile sura ya kwanza na ya Pili tukidhani kuwa ndio lengo la kile kitabu cha Ayubu, lakini hiyo sio kweli..Ufunuo mkubwa wa kitabu cha Ayubu upo kuanzia ile sura ya 3 na kuendelea…kuanzia ile sura ya 3 na kuendelea ndio utaona jinsi gani shetani alivyokuwa anampepete Ayubu kwa kupitia vinywa vya wale marafiki zake watatu.
Utaona jinsi gani wale marafiki zake Ayubu, walivyokuwa wanatumia maandiko kuivunja imani ya Ayubu. Nakushauri ndugu kama hujakipitia kitabu cha Ayubu kuanzia hii sura ya 3 na kuendelea kafanya hivyo leo..Kuna mambo mengi sana Bwana atakuonyesha ambayo ulikuwa huyajui.
Shetani anakawaida ya kuwa..akishindwa kumjaribu mtu kwa njia ya kawaida ya nje! Huwa anabadilisha mbinu na kuja kwa njia nyingine ya kutumia maandiko, atawaingia hata wapendwa au hata wachungaji kukuhakikishia jambo Fulani ambalo sio sahihi, nia na madhumuni ni kukuangusha tu!. Ili kulielewa hili vizuri chukua mfano ufuatao.
Tuseme shetani anataka kumwangusha mtu anayeitwa Amelia aanguke kwenye dhambi ya uasherati. Atakachokifanya kama kawaida atatafuta kwanza kibali kutoka kwa Mungu, akishakipata ataanza kutikisa kwanza uchumi wake..ili amweke katika mazingira ya uhitaji wa fedha, wakati yupo katika hayo mazingira ya kuhitaji fedha anatokea mtu mwenye fedha nyingi kidogo na kumshawishi. Na atakaposhinda vile vishawishi na kumkataa Yule mtu…Shetani atamjaribu kwa njia nyingine, atamletea mpaka magonjwa ilimradi tu! Atafute njia mbadala ya kupata fedha kwa kuutoa mwili wake….Na endapo akimwona bado huyo mwanamke kasimama…atamjaribu kwa njia nyingine mbalimbali..Na mwishowe ataacha na kuingia kwenye mbinu yake ya mwisho na kuu kuliko zote ya kumwangusha.
Katika hiyo mbinu yake ya mwisho hatatumia tena watu wa nje kumshawishi, kwasababu anajua huyu dada Amelia amesimama hawezi kutikiswa na watu wasiomjua Mungu, atakachokifanya atamfuata kule kule kanisani kwasababu imani yake yote ipo katika nyumba ya Mungu na anawaamini watu wa Mungu.
Kwahiyo siku moja ataingia kanisani na kusikia mahubiri yafuatayo…. “kuna watu humu ndani wanachezea bahati, utakuta mtu anashida, Mungu anamfungulia mlango wa fedha anakataa, unakuta mtu ni mgonjwa, hana hela anakuja mtu anataka kumsaidia anakataa, kwa njia hiyo hata kuolewa hutaolewa..dada! na watu wote kanisani wanajibu Ameen!” Na huyo mtumishi atasoma mistari kadha kadhaa kwenye biblia kuthibitisha mahubiri yake.
Sasa kwa mahubiri kama hayo..huyu dada atatoka kanisani huku kuna kitu kinamuhukumu ndani,…anaanza kujitathimini pengine lile Neno lilikuwa linamhusu yeye…Ni watu wangapi wamekuja kumjaribu akawakataa…pengine kweli anachezea bahati! Akijiangalia ni kweli ana matatizo ya fedha, sasa Kidogo kidogo anaanza kushawishika na kuhisi alikuwa anafanya makosa kujiepusha na wale watu waliokuwa wanakuja kumjaribu, anaanza kufikiri pengine hata alikuwa anamkosea Mungu, hivyo baada ya siku kadhaa akitokea mwingine anaanza kumsikiliza na mwishowe kuanguka kwenye dhambi ya uasherati na kushindwa na shetani.
Hizo ndizo njia shetani anazozitumia kuwaangusha wengi waliosimama…Na ndio Ayubu naye yalimkuta hayo hayo…shetani alipoona hatetereki hata kwa msiba wa wanawe..akawaingia marafiki zake Ayubu watatu ambao nao pia walikuwa tunaweza kusema ni watumishi kama Ayubu, walikuwa wanamtafuta Mungu pamoja naye na kusali pamoja naye. Wakaanza kumwambia Ayubu, tatizo haliko kwa Mungu, tatizo lipo kwako, haiwezekani yakupate haya yote wewe tu na si mtu mwingine, lazima utakuwa umetenda dhambi kwahiyo nenda katubu! Ubadilishe na njia zako. Na walitumia maaandiko kumshawishi Ayubu ageuke aiache njia yake. Lakini tunaona Ayubu alisimama thabiti mpaka Mwisho na hatimaye Bwana akageuza uteka wake..
Sasa leo kwa Neema za Bwana hatutazungumzia sana juu ya huduma za hawa rafiki zake watatu Ayubu, kama utahitahi somo kwa urefu kuhusu huduma zao unaweza ukawasiliana na mimi inbox nikutumie somo hilo.
Lakini leo tutazungumzia ni kwa namna gani Bwana alimrejeshea Ayubu mali zake zote maradufu na familia yake. Kwa namna hiyo hiyo na sisi tunaweza kuzipata Baraka zetu maradufu endapo tukifanya kama Ayubu alivyofanya.
Ukisoma Mwishoni mwa kitabu cha Ayubu ile sura ya 42 tunasoma..
Ayubu 42: 7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu. 10 KISHA BWANA AKAUGEUZA UTEKA WA AYUBU, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; BWANA NAYE AKAMPA AYUBU MARA MBILI KULIKO HAYO ALIYOKUWA NAYO KWANZA. 11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. 12 Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. 13 Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu. 14 Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. 15 Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. 16 Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne. 17 Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku”. Nataka uuone huo mstari wa 10 unaosema.. “ kisha bwana akaugeuza uteka wa ayubu, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; Bwana naye akampa ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.
Ayubu 42: 7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu.
10 KISHA BWANA AKAUGEUZA UTEKA WA AYUBU, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; BWANA NAYE AKAMPA AYUBU MARA MBILI KULIKO HAYO ALIYOKUWA NAYO KWANZA.
11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.
12 Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu.
13 Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu.
14 Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu.
15 Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume.
16 Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne.
17 Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku”.
Nataka uuone huo mstari wa 10 unaosema.. “ kisha bwana akaugeuza uteka wa ayubu, HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE; Bwana naye akampa ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.
“HAPO ALIPOWAOMBEA RAFIKI ZAKE”…hilo ndilo Neno la Msingi la leo. Pamoja na kwamba shetani aliwatumia rafiki zake kumjaribu yeye, pamoja na kwamba rafiki zake walimchukiza sana Mungu, mpaka hasira za Bwana zikawaka juu yao, akataka kuwaua…Lakini Ayubu hakuwahukumu wala kuwachukia aliwahurumia…akaenda akapiga magoti akawaombea toba! Na msamaha! Akatubu kwa ajili yao kwa dhabihu na machozi…Akawaombea rafiki zake Baraka badala ya Laana, heri badala ya shari..Na Mungu akawasamehe.. Na Bwana akapendezwa sana na AYUBU kwasababu hiyo ya kuwaombea rafiki zake…ndipo UTEKA WAKE UKAGEUZWA.. Akapewa vile vitu mara mbili..Bwana akamrudishia vyote alivyopoteza HALELUYA!!
Tunajifunza nini hapo?…kuna watu watatumiwa na shetani kutujaribu, hususani wanaotumia biblia..pengine ni marafiki zetu au ndugu zetu, na kwasababu Neno la Mungu linakaa ndani yetu, tunazitambua fikra za shetani ndani yao..Na mambo wanayofanya ukaona kabisa yanamchukiza Mungu na Mungu kawakasirikia, sasa huo sio wakati wa kupiga maadui yako!! Sio wakati kusema walaaniwe maadui zangu, wafe maadui zangu, waanguke!! Hapana! Biblia haitufundishi hivyo hata kidogo…inatufundisha kwenda kwenye magoti kutubu kwa ajili yao, kuwaombea msamaha, kulia hata ikiwezekana kutoa sadaka kwa ajili yao…hivyo ndivyo Bwana naye atakavyogeuza UTEKA WETU! Ndugu jitenge na injili za kupiga maadui si za kimaandiko hata kidogo…ukifanya hivyo Mungu hatageuza uteka wako hata kidogo. Tujifunze kwa Ayubu hakuna mtu aliyeumizwa moyo kama Ayubu, kapata msiba na wakati huo huo rafiki zake wanamwambia ana dhambi nyingi…inaumiza kiasi gani, lakini hakuwalaani bali aliwaombea..
Biblia inasema katika Mithali 24: 17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.
Unaona! Ndio maana Bwana alisema “ombea adui yako”..kwasababu unavyomwombea ndivyo Bwana anavyogeuza uteka wako.
Bwana akubariki sana.
Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada, Wasiliana nasi kwa namba
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
MNGOJEE BWANA
AYUBU ALITESEKA KATIKA MAJARIBU KWA MIAKA MINGAPI?.
NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:
AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
Kwa ufupi tumeshapitia vitabu vinne vya kwanza yaani kitabu cha Mwanzo, kutoka,Mambo ya Walawi na Hesabu na leo Kwa Neema za Bwana tutasogea mbele na vitabu vingine vinne vinavyofuata.
5) KUMBUKUMBU LA TORATI:
Kitabu hichi cha kumbukumbu la torati kiliandikwa na Musa, katika hatua za mwisho kabisa karibia na wana wa Israeli kuingia nchi ya Ahadi, Musa alipewa maagizo na Mungu aandike kitabu hichi kwaajili ya ukumbusho wa Torati..Kama jina lake lilivyo “kumbukumbu la Torati”..kwahiyo ni wazi kuwa kilikuwa ni kitabu cha kumbukumbu ya vitu ambavyo walikuwa tayari walishapewa au kuagizwa.
Mungu aliruhusu kitabu hichi kiandikwe kwaajili ya kizazi kipya cha wana wa Israeli, waliozaliwa katikati ya safari. Kwasababu wengi wa waliotoka nchi ya Misri walikufa njiani, kutokana na manung’uniko yao kwa Mungu ndio wale waliyoyaona matendo yote makuu Mungu aliyowatendea kwa macho yao lakini hawakutaka kumwamini na hiyo ikapelekea Mungu kuchukizwa nao, Mpaka kuwaahidia kuwa hakuna hata mmoja aliyetoka nchi ya Misri atayaeiona nchi ya Ahadi isipokuwa Kalebu na Yoshua tu! Ndivyo ilivyokuja kutimia kama ilivyo, wote walikufa wakabaki watoto wao..na hawa watoto waliozaliwa jangwani walikuwa hawamjui Mungu wa Israeli vizuri, hawakuyaona matendo Mungu aliyoyafanya wakiwa kule Misri,
kwahiyo ililazimika Kitabu kiandikwe ili kuwakumbusha TORATI ya Mungu aliyowapa wakiwa jangwani…ili wasije wakakengeuka na kumkosea Mungu kama baba zao na mama zao walivyofanya.
Kumbukumbu la torati 6: 4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 NAWE UWAFUNDISHE WATOTO WAKO KWA BIDII, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo”.
Kumbukumbu la torati 6: 4 “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 NAWE UWAFUNDISHE WATOTO WAKO KWA BIDII, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo”.
Kwahiyo kwa maagizo ya kitabu hichi cha kumbukumbu la torati, watoto wote waliozaliwa katikati ya safari kiliwasaidia kuwakumbusha matendo ya Mungu yote aliyoyafanya tangu alipowatoa wana wa Israeli katika nyumba ya utumwa, Kwahiyo kilibeba kumbukumbu ya sheria na amri zote za Mungu kuanzia Amri kumi mpaka sheria za Makuhani (Walawi). Kwahiyo kwa ufupi tunaweza kusema ni kama kitabu cha marudio ya sheria, hukumu, na baraka..Mungu alizowawekea wana wa Israeli wakiwa njiani kuelekea Nchi ya Kaanani.(Ndio maana kikaitwa kumbukumbu la Torati)
6) KITABU CHA YOSHUA:
Kitabu cha Yoshua kiliandikwa na Yoshua mwenyewe, baada ya Musa kufa…Yoshua ndiye aliyekabidhiwa gurudumu na Mungu mwenyewe, kuwaongoza wana wa Israeli kuingia nchi ya Kaanani, baada ya kuzunguka miaka 40 jangwani..Kwahiyo Yoshua na Kalebu ndio waliosalia miongoni mwa waliotoka Misri, hawa wawili ndio waliobebeshwa jukumu kukiingiza kizazi kipya cha wana wa Israeli katika nchi ya ahadi.
Kusudi kubwa la kuandika hichi kitabu cha Yoshua ni kuonyesha jinsi Wana wa Israeli walivyoshindana katika kutwaa urithi wao walioahidiwa…Hatua kwa hatua, jinsi walivyopigana vita na kuyatoa yale mataifa saba yaliyoshikilia urithi wao..Ni kitabu cha Vita, chini ya amiri jeshi wao Yoshua, Bwana aliyemtia mafuta kwa kuwashindania Israeli.
Yoshua 1: 1 “Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, 2 Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. 3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. 4 Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu. 5 Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha”.
Yoshua 1: 1 “Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,
2 Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.
3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
4 Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.
5 Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha”.
Kwahiyo rekodi yote ya vita, iliandikwa ndani ya hichi kitabu cha yoshua, ni sawa kipindi kile Rais Nyerere amwagize aliyekuwa mkuu wa Majeshi, aandike kitabu cha jinsi walivyovamia majeshi ya Uganda na kuyaangusha, kwenye vita dhidi ya Idd Amin, hatua kwa hatua jinsi walivyoteka jimbo moja baada ya lingine, na hatimaye jinsi walivyofanikiwa kuiteka Uganda yote na kuuangusha utawala wa Idd Amini. Ndivyo kitabu cha Yoshua kilivyo kinaelezea hatua kwa hatua namna Israeli walivyoteka na kuyatwaa maeneo ambayo Mungu aliwaahidia yatakuwa urithi wao katika nchi ya Ahadi.
Na hichi kitabu cha yoshua pia kiliandikwa kwa dhumuni ya kuonyesha mipaka ya wana wa Israeli katika nchi mpya ya Kaanani waliyoiingia..kwamba kila Kabila liligawiwa sehemu yake..
Kumbuka vitabu hivi pia, havikuandikwa kama hadithi tu, kutufurahisha sisi tunaosoma wa vizazi hivi..hapana bali kila kitabu kimebeba maana kubwa sana na ujumbe mzito katika roho. Vitabu hivi vina maudhui makubwa sana katika kutufundisha sisi watu wa siku za mwisho. Hivyo nakushauri unaposoma vitabu hivi, omba Roho wa Mungu akusaidie kupata uelewa ya ujumbe kwa wakati wako husika. Na hakika utafurahia na kujifunza mengi sana.
7) KITABU CHA WAAMUZI:
Kitabu kinachofuata ni kitabu cha Waamuzi kitabu hichi kiliandikwa na nabii Samweli. Kama jina la kitabu lilivyo “waamuzi” maana yake ni kitabu kinachozungumzia watu fulani ambao wamewekwa kutoa “suluhisho la mwisho la mambo yahusuyo nchi” au kwa lugha rahisi tunaweza kuwaita mahakimu.
Sasa Nabii Samweli ndiye aliyeagizwa na Bwana akiandike hichi kitabu cha Waamuzi, miaka mingi sana baada ya waamuzi wote kupita…aliagizwa aandike mambo waliyoyafanya hawa waamuzi moja baada ya lingine, kwani matendo yao yamebeba ufunuo wa KiMungu mkubwa sana ambao ungekuja kueleweka na vizazi vya mbeleni..ambao ndio sisi tunaosoma sasa.
Waamuzi walikuwa ni watu waliokuwa wanatoa maamuzi ya mwisho katika Israeli, baada tu ya wana wa Israeli kuingia katika nchi ya Kaanani..Mungu hakuwahi kuweka muamuzi katika nchi, lakini kwasababu ya kukengeuka kwa wana wa Israeli na kuiacha sheria na maagizo yake, Ndipo Mungu aliwatupa kwenye mikono ya maadui zao wateswe lakini walipomlilia Mungu, ndipo Mungu akawatumia mwokozi ili awaokoe kutoka kwenye shida zao, na huyo mwokozi Bwana aliyewatumia baada ya kuwaokoa katika shida zao ndio anakuwa kama MWAMUZI wa Taifa hilo kwa wakati huo.
Kitabu cha Waamuzi 2: 8 “Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi. 9 Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi. 10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. 11 WANA WA ISRAELI WALIFANYA YALIYOKUWA NI MAOVU MBELE ZA MACHO YA BWANA, NAO WAKAWATUMIKIA MABAALI. 12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika. 13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. 14 HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA ISRAELI, NAYE AKAWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WALIOWATEKA NYARA, AKAWAUZA NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA ADUI ZAO PANDE ZOTE; HATA WASIWEZE TENA KUSIMAMA MBELE YA ADUI ZAO. 15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. 16 KISHA BWANA AKAWAINUA WAAMUZI, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara. 17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo. 18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. 19 Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi”.
Kitabu cha Waamuzi 2: 8 “Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi.
9 Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
11 WANA WA ISRAELI WALIFANYA YALIYOKUWA NI MAOVU MBELE ZA MACHO YA BWANA, NAO WAKAWATUMIKIA MABAALI.
12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.
13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
14 HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA ISRAELI, NAYE AKAWATIA KATIKA MIKONO YA WATU WALIOWATEKA NYARA, AKAWAUZA NA KUWATIA KATIKA MIKONO YA ADUI ZAO PANDE ZOTE; HATA WASIWEZE TENA KUSIMAMA MBELE YA ADUI ZAO.
15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.
16 KISHA BWANA AKAWAINUA WAAMUZI, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara.
17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo.
18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
19 Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi”.
Katika Israeli walipita waamuzi 16 Samsoni akiwa mmoja wao, na Gideoni na Debora, na Yefta n.k. Hawa wote waliiamua Israeli kwa vipindi tofauti tofauti walikuwa wana madaraka karibia yafanane na ya kifalme lakini hawakuwa wafalme..Na Samweli mwandishi wa kitabu hichi ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Mwisho katika Israeli, ni sharti mwamuzi wa Mwisho ndiye awe mwandishi kwasababu yeye ndiye atakayekuwa na rekodi ya matukio yote ya waamuzi waliomtangulia…Mwamuzi wa kwanza haiwezekani apewe jukumu la kuandika historia ya mbeleni, ni lazima yule wa mwisho ndio awe muhasisi….
Kwahiyo hichi kitabu cha WAAMUZI, unapokisoma kimebeba siri nyingi Mungu alizozificha ndani ya hawa waamuzi, ukimsoma Gideoni utaona ufunuo wa ajabu sana, Vivyo hivyo Samsoni, vivyo hivyo Debora, vivyo hivyo Yeftha na wengine wote.
8) KITABU CHA RUTHU:
Hichi kitabu cha Ruthu ni kitabu cha Nane katika Biblia..Kitabu hichi kiliandikwa na Nabii Samweli yule yule aliyekuwa mwamuzi wa Mwisho wa Israeli, na aliyeandika kitabu cha Waamuzi, Bwana alimwongoza Nabii Samweli akiandike kitabu hichi kwani kimebeba maudhui makubwa sana katika mwili na katika Roho kwa kanisa lake..katika siku za mbeleni.
Kama jina la kitabu lilivyo RUTHU, Ikimaanisha kuwa ni kitabu kinachomwelezea mtu anayeitwa Ruthu.
Kinaelezea maisha ya Ruthu, na kinaelezea jinsi Mungu alivyomlipaji wa thawabu kwa wote wenye haki, jinsi alivyomlipa Ruthu kwa uvumilivu wake na upendo wake..Mpaka kufanyika kuwa mama wa Bibi wa Mfalme Mkuu atakayekuja kutokea miaka michache mbeleni (yaani Mfalme Daudi)…
Mwana wa Mjukuu wa Ruthu ndiye Mfalme Daudi. Yaani katika uzao wa tumbo lake ukawa uzao wa kifalme. Jinsi gani Mungu anawapa thawabu hata watoto wa watoto wetu endapo sisi tukimcha yeye na kumpendeza na kuwa wavumilivu na wenye upendo kama wa Ruthu…Kumbuka Ruthu hakuwa hata mwisraeli alikuwa ni mtu wa mataifa lakini kwa upendo wake na uvumilivu wake…katika uzao wa tumbo lake akatoka Mfalme Mkuu Daudi, aliye Baba yake Suleimani…na katika Mnyororo huo ndio MFALME WA WAFALME, YESU KRISTO KATOKEA!! Ni Baraka kiasi gani…
Kwahiyo hichi kitabu cha Ruthu kimebeba maudhui makubwa sana ya kutufundisha sisi watu wa siku za mwisho, tukianza kuzungumzia jambo moja baada ya lingine na kulitolea ufafanuzi tutamaliza kurasa na kurasa hapa…lakini wewe mwenyewe chukua nafasi ya kukisoma hichi kitabu cha Ruthu na Bwana atakupa ufunuo wa kipekee..na pia kama utahitaji maelezo marefu juu ya kitabu hichi cha Ruthu unaweza kubofya hapa kwa uchambuzi zaidi >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
Bwana akubariki sana..
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Tutaendelea na sura zinazofuata Bofya hapa >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 3
Mada Nyinginezo:
BWANA ALIMPA FARAO MOYO MGUMU, ASIMTII, JE! HAPO BWANA ATAMHUKUMU KAMA MKOSAJI SIKU ILE?
KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?
RAHABU.
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)
SANDUKU LA AGANO LILIKUWA LINAWAKILISHA NINI KATIKA AGANO JIPYA?
YATAFUTE YALIYO JUU SIKU ZOTE.
Rudi Nyumbani:
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu…”
Hakika tukilifahamu Neno la Mungu kama mtu mmoja alivyosema, hata tukifungiwa katika chumba chenye giza tukapewa mshumaa na Biblia tu tutaweza kukuleza mambo yote yanayoendelea na kazi zote za shetani azifanyazo duniani bila hata kuhadithiwa na mtu yeyote,..Kumbe hatuhitaji shuhuda kutoka kuzimu ili kutusaidia sisi kufahamu utendaji kazi wa shetani, Biblia imeweka wazi mambo yote, na leo hii tutaziona hizo kazi kubwa shetani anazojishughulisha nazo kwa msaada wa Neno la Mungu:
1) KUSHITAKI WATAKATIFU:
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni,ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, YEYE AWASHITAKIYE mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni,ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, YEYE AWASHITAKIYE mbele za Mungu wetu, mchana na usiku..
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Leo umekuwa mtakatifu kwa kumwamini mwana wa Mungu, lakini fahamu kuwa shetani bado hajakata tamaa ya kukufutilia, nyendo zako, na akipata kosa tu kazi yake ni kulipeleka mbele za Mungu ili uhukumiwe, anapeleka mashtaka usiku na mchana, lakini ashukuruwe Mungu sisi tulio ndani ya Kristo, pale anapokwenda kutushitaki, hapo hapo ameketi mwombezi wetu Yesu Kristo, kututetea sisi. Hivyo ni jukumu letu kuziweka njia zetu katika mstari ulioonyooka ili adui akose la kutushitaki.
2) KUZUIA KAZI YA MUNGU: 1Wathesalonike 2.18 “Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia”.
Ni jambo la kawaida kukutana na shetani uso kwa uso unapojaribu kuieneza kazi ya Mungu, Hiyo ni moja ya huduma yake duniani, Paulo alizuiwa na jeshi la mapepo alipokuwa akienda kuhubiri Injili Thesalonike,.Hata sasa mambo hayo hayo anayafanya,.Hivyo nawe pia ukiwa umevaa zile silaha zote zinazozungumziwa katika Waefeso 6, usiogope, kusimama, kwasababu aliyesimama upande wetu ni mkuu kuliko aliyeupande wao..Utakutana na visa na mawimbi ya ajabu njiani lakini usiogope..Aliyekutuma atakuwa pembeni yako.
3) KULETA MAJARIBU: Hii pia ni kazi anayoifanya shetani kwa maaminio kila siku, ili kuwadondosha , na kuwafanya wauone ukristo kuwa ni mgumu na mwisho wa siku wakate tamaa, na waiache njia ya wokovu,Tunaona yalitokea kwa Ayubu, Yalitokea kwa Bwana wetu Yesu Kristo, yalitokea kwa mitume, na yatatokea na kwetu,
Waebrania 11: 36 “wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;”
Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye anatupa nguvu ya kuyashinda,.kwasababu biblia inaweka wazi kabisa mtu yeyote atakayeingia katika PENDO la Kristo, hakuna kitu chochote kitakachoweza kumtenganisha nalo.
Lakini kumbuka pia mtu yeyote aliye nje ya Kristo hajaribiwi, wala asijidanganye kusema anapitia majaribu, atajaribiwa na nini wakati yupo tayari kwenye dhambi?.kinyume chake yeye ndiye anafanyika chombo cha shetani kuwajaribu watu wa Mungu..
4) KULETA MAGONJWA: Luka 13:16 “Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?”
Huyu ni mwanamke aliyefunguliwa na Bwana Yesu ambapo Pepo la udhaifu lilimsababishia ulemavu wa kudumu wa mgongo (yaani kibiongo). Hii ni kutuonyesha kuwa sababu ya magonjwa mengi yanayowapata watu leo hii ni kazi ya shetani. Yeye ndiye anayehusika na magonjwa na matatizo yote, Lakini tumaini lipo na tiba na kinga vile vile ipo kwa yeyote amwaminiye Kristo leo, kwasababu maandiko yanasema (Isaya 53: 4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu;..Na kwa kupigwa kwake sisi tulipona)..HALELUYA!!
5) KUUA:
Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; ..”
Hii ni kazi nyingine kubwa ya shetani kuangamiza kotekote yaani mwilini na rohoni. Ndugu fahamu kuwa shetani hakupendi hata kidogo, ni Rehema za Mungu tu zinatushikilia wewe na mimi, zinakushikilia wewe ambaye bado upo kwenye dhambi, ungeshakufa siku nyingi biblia inasema shetani asili yake ni uuaji tangu mwanzo alikuwa hivyo, na ndio chanzo cha mauaji unayoyaona yanaendelea sasahivi duniani, na atakuja kutekeleza vizuri katika kipindi cha ile dhiki kuu, lakini yeye aliye ndani ya Kristo, amefichwa ndani ya ule mwamba imara wala mwovu hawezi kumgusa, na hata akimgusa basi ni kwa ajili ya kutimiza kusudi la Mungu kama Ayubu, na sio kuuliwa ovyo ovyo kama tu kuku.
6) KUDANGANYA:
Yohana 8:44“…..wala hakusimama katika kweli [shetani], kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.
Unaona?. Kazi ya upotoshaji ni kazi inayomletea shetani matunda makubwa sana, Anachofanya yeye, hakuzuii kumwabudu Mungu wala kwenda kanisani, bali anakuhubiria njia zake za uongo, ili umwabudu yeye pasipo wewe kujua ukidhani unamwabudu Mungu, au anakushawishi ufanye kitu Fulani ukidhani ni chema kumbe unamkosea Mungu, na mwisho wa siku unakufa unajikuta upo kuzimu, mpango wake umekamilika juu yako. Na ndio maana tumeonywa kila siku tuijue kweli ili tuwe huru, na KWELI ni NENO LA MAUNGU, katika zama tulizopo udanganyifu wa ibilisi umezidi kuongezeka, tuombe Mungu atusaidie, huku na sisi wenyewe tukionyesha bidii kumtafuta Mungu.
7) KUPOFUSHA:
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao MUNGU WA DUNIA HII AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO WASIOAMINI, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
4 ambao ndani yao MUNGU WA DUNIA HII AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO WASIOAMINI, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Leo hii unaweza ukajiuliza ni kwanini watu wengi wanasikia injili, wanaziona kazi za Mungu waziwazi akifanya ishara na miujiza, wanajua kabisa Mungu yupo lakini bado hawataki kubadilika,..ni kwasababu wametaka wenyewe kuwa chini ya shetani, hivyo na shetani naye akatumia fursa hiyo kuwapofusha fikira zao moja kwa moja wasiiamini Injili wakapona.. Na anafanya hayo akishirikiana na wakuu wake wa giza hili pamoja na mapepo yote,.Hivyo ndugu ikiwa wewe ni mmojawapo wa watu wasiosikia injili, jichunguze tena, na uamue kubadilika, Mgeukie Bwana akupake dawa kwenye macho yako upate kuona.
Bwana anasema katika
Ufunuo 3:17-20 “…Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, NA KIPOFU, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”
Ufunuo 3:17-20 “…Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, NA KIPOFU, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”
8) KUNYAKUA NENO LA MUNGU:
Mathayo 13:18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Hapa napo shetani amewekeza sana, na amefanikiwa pakubwa..Akishaona mtu Fulani anaonyesha uelekeo wa kutaka kuamini, alipohubiriwa injili, ilipomchoma, sasa yeye anachohakikisha ni kuwa anapambana kwa kila namna kuliondoa lile Neno ndani ya mtu yule, ndio hapo utakuta mtu anakosa Muda wa kutafari lile Neno alilofundishwa, badala yake shetani atamletea vitu mbadala vya kujishuhulisha navyo, kama vile movies, mpira, michezo, tv, kuchati, mihangaiko, miziki n.k..mwisho wa siku anasahau kile alichopandiwa ndani yake, na baadaye anarudia hali yake ya mwanzo na kuwa kama vile mtu ambaye hajawahi kusikia Neno la Mungu kabisa..
Hiyo ni njama kubwa sana shetani anayoitumia kuiondoa mbegu iliyopandwa ndani ya mtu, hata katika mambo ya dunia, mwanafunzi akitaka kuondoa kitu alichokipata darasani, aanze tu kungalia movie muda mrefu, au kuchat au kusikiliza miziki…mwanafunzi wa namna hiyo ndani ya muda mfupi sana, utakuta kashazika kila kitu katika akili yake kuhusu kitu alichojifunza muda mfupi au siku chache nyuma..Na shetani ndio anatumia vitu hivyo hivyo kuiba mbegu iliyopandwa ndani ya mtu.
Embu jiulize injili imehubiriwa kwako mara ngapi, na bado upo vilevile, Neno la Mungu lilivyo na nguvu ilipaswa usikie mara moja tu na kugeuka moja kwa moja, lakini kwasababu shetani umempa nafasi basi amekuwa akiifanya hii kazi ndani yako kila siku pasipo hata wewe kujijua, Hivyo chukua hatua ubadilike mara kwa kuitii Injili inapohubiriwa kwako weka mbali miziki ya kidunia, filamu, tamthilia, novels zisizokuwa na maana na mambo mengine yote yanayofanana na hayo.
9) KUJIGEUZA NA KUWA MFANO WA MALAIKA WA NURU:
2Wakorintho11:13 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
2Wakorintho11:13 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”
Ni tabia ya shetani kujigeuza na kujifanya malaika mtakatifu, hivyo anawarithisha na watoto wake kazi hiyo hiyo, na ndio maana katikati ya kanisa la Mungu leo hii utaona manabii wengi wa uongo na mitume na watumishi wa uongo humo humo. Hiyo ni kazi ya shetani ili kulikoroga kanisa la Mungu lisisimame. Lakini sasa wewe kama mkristo ni jukumu lako kuwatambua, kwasababu biblia inasema mtawatambua kwa matunda yao.. je! Wanayatenda mapenzi ya baba yao aliye mbinguni?..Hilo tu.
Unafundishwa Neno la Mungu na utakatifu? Au mambo mengine, je! Tangu uwepo mahali hapo maisha yako ya kiroho yalishawahi kubadilika au ndio yanazidi kuteterekea?. Unapata matumaini ya utajiri na mali lakini je! Juu ya hayo ulishapata matumaini ya uzima wa milele yanayopatikana kwa kuishi maisha ya utakatifu na kujitenga na dhambi?
10) KUFANYA ISHARA NA MIUJIZA YA UONGO:
Ufunuo 13:13 “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. 14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.”
Ufunuo 13:13 “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.”
Mambo haya haya yalifanyika wakati wa kipindi cha Musa, wakati wale Yane na Yambre, walipokuja na wao kutoa ishara zao mbele za Musa ili kuwachanganya watu wa Mungu,.hata sasa anafanya hayo hayo, kwa kutumia uchawi wake, anaowapa watumishi wake wa uongo.
Tunaweza kuona kulikuwa na mtu mwingine aliyeitwa Simoni kwenye Biblia, naye alikuwa vivyo hivyo.
Matendo 8:9 “Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. 10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake”.
Matendo 8:9 “Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.
10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake”.
Hivyo kwa kuyafahamu hayo tutaweza kujua ni jinsi gani shetani anavyotuwinda kuliko tunavyodhani, hofu ni kwako wewe uliye nje ya wokovu, nje ya YESU KRISTO utawezaji kuviruka viunzi vyote hivyo vya adui?. Upo katika hatari kubwa sana ya kuangamia na kuishia kuzimu. Kinga tulishapewa nayo ni YESU KRISTO, Amwaminiye yeye shetani kwake ni kama KIKARAGOSI!! Kisichoweza kumfanya lolote, wala kumdhuru. Lakini ukiwa nje ya Kristo shetani kwako ni mungu wako, atakufanya anachotaka.
Uamuzi ni wako, TUBU leo ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kimaandiko upate ondoleo la dhambi zako, uingie katika familia ya wana wa Mungu, furahani kwa Bwana, mahali ambapo chemchemi ya maji ya uzima inapobubujika. Mahali ambapo hakuna aliyemfuata akajuta. Tulikuwa na sisi katika dhambi kuliko wewe lakini sasa tunapata raha ndani ya Kristo Yesu, Ingia na wewe ujionee mwenyewe..
Ubarikiwe …
SHETANI NI NANI?
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
KAENI NDANI YANGU NAMI NDANI YENU.
WhatsApp
1 Timotheo 4 :1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”
Mwanzoni nilipokuwa ninausoma huu mstari nilidhani kuwa itafikia kipindi watu watauchukia ukristo na kugeukia imani nyingine, labda uislamu au kama sio hivyo basi watageuka na kuwa wapagani moja kwa moja, lakini nilipokuja kuuchunguza tena kwa makini Bwana akanipa kujua kuwa kumbe sio hivyo, badala yake ni kwamba watu wataendelea kubakia katika Ukristo lakini kumbe Imani zao siku nyingi tayari zilishabadilishwa na kuwa kitu kingine,..
Ni sawa na wanafunzi waliosajiliwa shuleni Tanzania lakini mwalimu wao anawafundisha sylabus ya Kenya, unaona haijalishi wataelimika kiasi gani, haijalishi watafahamu mambo mengi kiasi gani, siku ikifika ya mtihani wa mwisho wa taifa wanafunzi wale wote wanauwezekano mkubwa wa kufeli, kwani watakutana na mambo ambayo hawajawahi kufundishwa. Na mwisho wa siku itageuka na kuwa hasara kwao na sio hasara ya mwalimu.
Na ndivyo ilivyo katika siku hizi za mwisho, Biblia inasema wengine watajitenga na Imani, hii ikiwa na maana kuwa watakosa shabaha ya Imani halisi ya kikristo, wakidhani kuwa wapo katika njia sahihi kumbe walishapotea au walishapotezwa siku nyingi. Wameifuata Imani feki isiyotambulika mbinguni.
Ndugu jambo hili sio la kulichukulia juu juu tu, naomba usome mpaka mwisho inawezekana na wewe ulichukuliwa katika wimbi hilo pasipo kujijua, kwani shetani ni mjanja sana, usijione unafahamu kila kitu, wala tusijione kuwa tunafahamu mambo yote, tunakuwa na kujifunza kila siku.
Leo tutaona mambo mawili makuu yatakayopelekea wewe kujitenga na Imani ya kweli mwenyewe. Sasa tukirudi kwenye huo mstari hapo juu, tunaona unasema.. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na MAFUNDISHO YA MASHETANI;
Umeona sababu zenyewe hapo?, kitakachowasababishia kujitenga na Imani kwanza, ni kusikiliza roho zidanganyazo, na pili ni Kusikiliza mafundisho ya mashetani.
1) KUSIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO: Hizi roho zidanganyazo ni zipi,? biblia imeweka wazi kama tukindelea kusoma vifungu vinavyofuata tutapata picha yote ilivyo…Na roho hizi pia zimetajwa kugawanyika katika mafungu makuu mawili, moja ni Kuzuiwa kuoa, na pili ni kulazimishwa ujiepushe na vyakula…Tusome.
Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”. 4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba”.
Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”.
4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba”.
Angalia maneno hayo ndugu ukishaona unafika mahali unaambiwa ili ukubaliwe na Mungu au ili uwe mtumishi wa Mungu, ni lazima usioe kama Mtume Paulo alivyokuwa vinginevyo haustahili kuwa askofu, au mchungaji au mtumishi wa kanisa, basi fahamu kuwa hizo ni roho zidanganyazo na zinakutenga na Imani halisi inayotajwa kwenye biblia ya mitume..
Hali kadhalika ukiona, umefika mahali unaanza kuambiwa chakula hichi ule au hichi usile, hiki ni najisi hakifai, ukila hichi ni dhambi, kama vile wafanyavyo baadhi ya dini kama sabato, Ndugu fahamu kuwa upo katikati ya roho zidanganyazo, zitakazokupeleka mbali na Imani, Ni kwanini hayo mambo ni mabaya?…Ni kwasababu yanakutoa katika kuhesabiwa haki kwa Imani na kukuleta katika kuhesabiwa haki kwa vitu vya mwilini kama vyakula, na kuutiisha mwili kwa nguvu.. …Haihitaji ufunuo kuelewa hilo, na ndio maana hapo juu biblia inasema Roho ananewa wazi wazi, unaona ni mambo yaliyowazi kabisa,
Jitenge nazo haraka sana, kwasababu zilishatabiriwa katika siku za mwisho hizo ndizo zitakazowaongoza watu waikose mbingu, watu watakuwa wanakazana kuangalia namna ya kula kama ndio kitu kinachompendeza Mungu, na wanasahau mambo muhimu ya Imani kama upendo, utakatifu, amani n.k
Wakolosai 2:20 “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, 21 Msishike, msionje, msiguse; 22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? 23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili”.
Wakolosai 2:20 “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,
21 Msishike, msionje, msiguse;
22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili”.
2) MAFUNDISHO YA MASHETANI: Haya mafundisho ya mashetani ni yapi?, Biblia nayo imeendelea kuweka wazi katika vifungu vinavyofuata..
(4:7 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa..)
Unaona biblia inazitaja hadithi za kizee, ambazo hizo hata hazina vimelea vya dini ndani yake, haya ndio mafundisho ya mashetani yaliyobuniwa kuzimu ili kuwafanya watu wasiliamini tena Neno la Mungu hata kidogo na uweza ulio katika Kristo Yesu badala yake kuhamishia imani zao katika vitu visivyo na uhai. Na hapa ndipo wakristo wengi walipokamatiwa hususani wa makanisa ya kiroho,.Hizi zinaitwa hadithi za kizee, ni hadithi ambazo zimetungwa lakini zinahusishwa na imani, kwamfano utafika mahali unafundishwa usipande mti Fulani nyumbani kwako, unasababisha baba wa nyumba kufa, unasababisha mikosi kwenye nyumba, na magombano yasiyoisha, na wewe kama mkristo unakwenda kuung’oa huo mti, wewe hujui kuwa Imani yako imehamishwa kutoka katika kweli ya Mungu na kuamia katika ibada za sanamu, mambo ambayo hayana tofauti na yale yanayofanywa na waganga wa kienyeji.
Utakuta mwingine anakuambia, lipande ua hili au mti huu au fuga mnyama ndani ni viumbe rafiki vinaleta Baraka katika nyumba na kuondoa mikosi, na wewe kama mkristo unamsikiliza mtu huyo ambaye anajiita ni mtumishi wa Mungu bila kuhakiki jambo hilo linatoka wapi katika maandiko wewe unakwenda kufanya hivyo, hujuwi unamtia Mungu wivu kiasi gani unasahau kuwa Baraka za Mungu zinatoka katika chemchemi ya maji ya Uzima ndani Yesu Kristo peke yake,..unasahau kuwa utakatifu ndio nyenzo ya kuishi maisha ya amani hapa duniani lakini wewe unakwenda kutafuta njia mbadala kutoka katika viumbe na mimea, na mchanga, na vyakula, unasikiliza hadithi za kizee sizizo na dini, unajitenga na Imani ya Kristo Yesu wewe mwenyewe bila ya wewe kujijua, unamtia Mungu wivu kwa mambo hayo yasiyotokana na Imani ya Kristo Yesu.
Kaka/ndugu, Hizi ni siku za mwisho Roho amekwisha kunena wazi wazi tena leo hii bila kutuficha, Biblia Inaposema wengi watajitenga na Imani, haimaanishi watahama ukristo na kugeukia dini nyingine, hapana watabaki huku huku lakini kumbe siku nyingi walishahamishwa..Na ndio lengo la shetani hilo…Kudanganya, siku zote kudanganya..Maana ya kudanganya ni kudhani umeambiwa/unafanya kweli kumbe ni uongo.
Na ndio maana Paulo kwa uweza wa Roho alimsisitiza sana Timotheo kwenye vifungu hivyo vya maandiko na kumwambia.
4:6 “Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na MZOEVU WA MANENO YA IMANI, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata..”
Unaona, kama mtumishi wa Mungu alionywa kuwakumbusha watu mambo hayo na kufanya vile naye atakuwa “mzoefu wa maneno ya Imani”, hii ikiwa na maana kuwa asipokuwa makini kama mahubiri atakengeuka na kufundisha maneno mengine ambayo sio ya Imani.
Nasi tunakukumbusha leo hii na kukwambia, ONDOKA! Mahali unapozuiwa kuwa mchungaji kisa umeoa mke, kama kanisa Katoliki lifanyavyo, Vile vile mahali ambapo pia wanakuzuia kuwa mhudumu wa Kristo kisa hujaona, ondoka hilo eneo kwasababu katika maandiko hakuna mahali popote pameagiza hivyo.
Ondoka, mahali ambapo unaambiwa ili Mungu akukubali au ili uwe kwenye njia sahihi ni lazima usile kitu Fulani, ni lazima, ushike siku Fulani, ya jumamosi au jumapili, ni lazima ushike sabato, wanasisitiza mambo ya mwilini tu siku zote lakini Utakatifu wa ROHONI haugusiwi ondoka haraka eneo hilo kabla tatizo hilo halijawa donda ndugu kwako lisiloweza kupona tena, usije ukabakia kuwa mfuasi wa dini kushindana na kulumbana na watu kila mahali kama walivyokuwa wanafanya mafasayo na waandishi. Na uthibitisho wa roho hii, huwe inawapeleka watu kwenye malumbano na mashindano ya dini, ambayo biblia imetuonya tukae mbali nayo.
Ondoka pia mahali ambapo wanapenda njia mbadala za kutatua matatizo yako kwa kutegemea vitu vingine nje ya Neno la Mungu na uweza wa damu ya Yesu Kristo. Unaambiwa suluhisho la matatizo yako ni maji Fulani yaliyoombewa, au mafuta, au chumvi au udongo, na huambiwi kwasababu hapana tofauti na kwa mganga wa kienyeji, kwasababu huwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji hata siku moja ukakemewa tabia yako, yeye ukifika pale atakupa dawa ya matatizo yako kwa njia nyingine anayoijua yeye, lakini sio kwa kukutathamini tabia yako, hata siku moja hawezi kukwambia wewe ndio mbaya, atakwambia mtu Fulani ambaye ni adui yako ndio mbaya, kwahiyo hata kama wewe ndio mwenye makosa atakupa dawa ya kumshambulia Yule asiye na kosa, vivyo hiyo na mahali popote unapofika ambapo unatabiriwa tu kupigwa kwa maadui zako lakini hujawahi kuambiwa kuwa ile tabia yako ya uasherati ndio adui mkubwa wa maisha yako, ondoka hilo eneo kwa usalama wa maisha yako. Unafika tu na kuambiwa nunua maji haya yaliyoombewa baada ya siku kadhaa matatizo yako yote yataondoka..Ujue hizo ni hadithi za kizee za kujitenga nazo.
Hivyo Kwa kuzingatia vipengele hivyo vikubwa viwili basi utakuwa umenusurika pakubwa na undanganyifu ulipo duniani katika siku hizi za mwisho.
Ni jukumu la Kila mkristo kuilinda Imani yake na kuishindania, biblia inatuagiza hivyo.
Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU.
Ikiwa wewe ni mmoja wa waliokombolewa na Yesu basi Nikutakia heri na mafanikio yote katika safari yako njema ya kwenda mbinguni. Bwana akubariki sana.
HADITHI ZA KIZEE.
MAFUNDISHO YA MASHETANI
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!
INARUHUSIWA KULA NYAMA YA NGURUWE KWA MKRISTO WA KWELI?
TUZIJARIBU HIZI ROHO.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe! Karibu tujifunze Biblia. Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza juu ya “swali kuu la kujiuliza katika maisha yetu”.
Hebu jaribu kutengeneza picha labda kuna mtu, kakukamata halafu kakufunga macho na kisha akakusafirisha na kukupeleka labda tuseme nchi ya India, na ulipofika pale hakukwambia kama upo India, badala yake akakutelekeza kwenye moja ya mitaa ya India na kukimbia, na baadaye ulipofanikiwa kufungua kile kitambaa mbele yako ukaona mazingira ambayo hujawahi kuyaona, mitaa ambayo ni mipya kwako, watu ambao huwajui, lugha inayozungumzwa ni ngeni kwako, ulipotazama kulia ukaona kuna watu wanacheza mpira kiwanjani, ulipotazama kushoto ukaona kuna mgahawa wa chakula, watu wanakwenda pale kula, ulipotazama nyuma ukaona kuna watu wanakimbilia kupanda gari la usafiri, na pembeni mwa barabara ukaona kuna kama soko Fulani la mboga mboga na matunda na wafanyabiashara wengi, mbele yake kidogo unaona nyumba nzuri za kifahari na bustani nzuri za kumpumzika..
Jiweke katika hiyo nafasi halafu uniambie..ungekuwa ni wewe ungekimbilia kipi cha kwanza?..inawezekana ukasema ningekimbilia kucheza mpira, au kwenye mgahawa wa kula, au sokoni kula matunda. Lakini kama umefikiria mojawapo ya hivyo basi ni wazi kuwa utakuwa umefikiria jambo la kipumbavu la mtu asiyefikiri.
Kwanini ni jambo la kijinga?…Ni kwasababu baada ya kujikuta tu pale, swali la kwanza ambalo ungetakiwa kujiuliza HAPA NI WAPI? Na NI KWANINI NIPO HAPA?..Hilo ndio jambo la kwanza kabisa la kujiuliza kabla ya kufanya jambo lolote au kujiunga na kitu chochote kule..Utajiuliza kwa makini sana HAPA NI WAPI?..Niko wapi hapa?..na baada ya hilo swali kujiuliza litakalofuata ni NI KWANINI NIPO HAPA?.
Sasa majibu ya maswali haya utayapata kutoka kwenye vyanzo viwili tofauti…Swali la kwanza linalouliza HAPA NI WAPI au NIKO WAPI HAPA…Jibu lake utalipata kwa kwenda kuwauliza watu wanaokuzunguka, labda utaenda pale mgahawani na kumwuliza mtu mmoja na kuwambia “samahani eti hapa ni wapi?”…Pengine Yule mtu anaweza akashangaa kidogo kuulizwa swali kama lile anaweza akafikiri wewe ni kichaa lakini mwisho wa siku atakwambia hapa ni INDIA.
Na baada ya kujua kuwa upo INDIA, swali litakalofuata ni NANI aliyenileta hapa, na ni kwa dhumuni gani yeye kunileta hapa?..sasa jibu la hili swali huwezi kulipata kwa wale watu tena wanaokuzunguka, kwasababu ukienda kuwauliza watakuona umerukwa na akili…Hivyo itakugharimu kufanya uchunguzi wako kumjua aliyekupeleka pale na dhumuni lake, hapo ndipo itakugharimu uchunguzi kidogo Kumtafuta Na kama Yule aliyekuleta atapenda kujidhihirisha kwako, ili kukueleza sababu ya yeye kukuweka pale basi atakupa sababu zote, na dhumuni lake lote, kisha ukishatimiza mapenzi yake, yeye ndiye atakayekuonyesha njia ya kurudi katika nchi uliyotoka. Huo ni mfano tu!.
Sasa katika maisha tunayoishi ndio hivyo hivyo….Sisi wanadamu wote tumezaliwa katika hii dunia, TUMEJIKUTA TU! TUMETOKEA HAPA ULIMWENGUNI. Hatukukaa katika kikao cha makubaliano na yeye aliyetuleta hapa ulimwenguni. Tumejikuta tu! Tupo tayari ulimwenguni ni kama tumetekwa mateka na kuletwa mahali tusipopajua. Na wote tulipozaliwa tayari tumekuta kuna mambo yanaendelea duniani, tumekuta kuna michezo, kuna burudani, kuna shughuli hizi na zile, kuna kumbi za starehe na mambo mengi, kuna fursa nyingi kila mahali…Lakini swala ni lile lile litakuwa ni jambo la kipumbavu kujiunga na hayo mambo kabla ya kujiuliza baadhi ya maswali..KWAMBA MIMI NI NANI? NIMETOKA WAPI? NIPO WAPI? NA NI NANI ALIYENILETA HAPA? NA KWA DHUMUNI GANI?…Hayo ndiyo maswali ya kwanza ya muhimu ya kujiuliza ya mtu mwenye akili kabla ya kujiunga na taasisi yoyote ile, kabla ya kujiunga na chuo Fulani, kabla ya kujiunga na biashara Fulani, kabla ya kuanza kupanga mipango fulani ya maisha…hayo ndio maswali ya msingi ya kujiuliza.
Na baadhi ya majibu ya hayo maswali unaweza kuyapata kwa wanadamu wenzako lakini kuna ambayo huwezi kuyapata kutoka kwa wanadamu, kwamfano ukienda kumwuliza mtu hapa ni wapi? Atakuona mwendawazimu lakini mwisho wa siku atakupa jibu hapa ni duniani, na atakupa mpaka historia ya dunia ilipotokea n.k.
Na swali la kwamba ni nani aliyekuleta hapa duniani, unaweza ukajibiwa tu kirahisi kuwa ni MUNGU..Lakini dhumuni la yeye kukuleta hapa ni lipi? Hakuna atakayekujibu!..hapo itakugharimu wewe utafute, hakuna mtu anayeweza kukupa jibu la dhumuni la Mungu kukuleta hapa duniani?..Kwasababu kila mtu anakusudi lake la kutimiza hapa duniani tofauti na mwingine.
Sasa utajuaje kusudi la aliyekuleta hapa duniani (Yaani kusudi la Mungu)..juu yako?
1) Kwanza Ni lazima umpate huyo aliyekuleta duniani, na namna ya kumpata huyo ni kwa kupitia kitu kimoja kinachoitwa MSALABA..Kwa kupitia YESU KRISTO, Hakuna namna nyingine yoyote utakayoweza kumjua Mungu nje ya huyu YESU KRISTO, Huo ndio ukweli ndugu yangu, na huyu unampata tu kwa kumwamini na kwa kutubu dhambi zako na kumgeukia yeye kikweli kweli, na kwa kubatizwa na kwa kupokea Roho Mtakatifu. Hapo utakuwa umempata huyu aliyekuleta ulimwenguni.
2) Baada ya kumpata kwa kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, sasa moja kwa moja ataanza kuongea na wewe na kukuongoza katika lile kusudi alilokuitia duniani, hajakuleta hapa duniani bure bure tu! Wala hajakuleta hapa ili uwe mfanyabiashara, au uwe maarufu, au uwe milionea, hapana lipo kusudi lingine ambalo ndilo alilokuletea hapa, na hilo kusudi linafanya kazi kwa silaha alizoziweka ndani yako tayari (yaani karama aliyoiweka ndani yako), kwa kupitia huyu Roho wake Mtakatifu atakufunulia hilo kusudi, na ukishalijua hilo kusudi ndipo amani ya ajabu ya kuishi duniani itakujia, kwasababu umeshajua dhumuni la wewe kuletwa duniani. Na kusudi hilo ndilo litakalokufanya uishi kama mpitaji tu katika hii dunia, ukijua kuwa hapa duniani, sio kwako, ni kama umetekwa tu na umeletwa ili utimize kusudi Fulani, na huku ukijua kabisa aliyekuleta sio mjinga kwamba akulete humu duniani na kisha ashindwe kukuhudumia mahitaji yako ya mwilini, kwahiyo utakuwa unaishi kwa bajeti ya aliyekuleta, sio bajeti yako wewe, huku ukiangalia na kulitazama kusudi lake. Na lolote utakalolifanya ndani yake utafanikiwa.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, swali ni lile lile? UNAJUA UPO WAPI?…UNAJUA SABABU YA WEWE KUWEPO HAPA?...Ni jambo la kuhuzunisha kama unaishi katika hii dunia na unafanya anasa, unaendelea na shughuli zako za kiuchumi…lakini hujui sababu ya wewe kuishi duniani, ni sawa na Yule mtu aliyetweka na kufumbuliwa macho na pasipo hekima yoyote akaanza kukimbilia mgahawani kula chakula, pasipo hata kujiuliza yupo wapi…Hivyo ndiyo unavyoonekana mbele za Muumba wako wewe usiyetaka kuyatafakari msingi wa maisha yako?..unaonekana mpumbavu mbele zake kwa kutokutambua kusudi lako na uwepo wake na wako..wewe na mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo hamna tofauti.
Zaburi 14: 1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu….”;
Kama leo hii umeamua kufumbua macho yako na kutafuta kujua kusudi la Mungu juu ya maisha yako, hatua ni nyepesi za kufuata, ndio hizo hapo juu…kwanza tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutokuzitenda tena, kusudia moyoni kuacha uasherati, uzinzi, utazamaji wa pornography, masturbation, usengenyaji, ulevi, uvutaji wa sigara, rushwa, utoaji mimba, ulawiti,wizi, utukanaji na mengineyo..kisha ukishadhamiria kuacha hayo mambo…hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa, kumbuka ubatizo sahihi ni wa muhimu sana na ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji tele na kwa JINA LA YESU KRISTO, Ubatizo wa udogoni sio sahihi kulingana na maandiko, kama ulibatizwa hivyo, hukufanya dhambi kwasababu ulikuwa hujui, ulifanyiwa pasipo kujua lakini sasa umejua ukweli,nenda kabatizwe tena upya kwa Imani, kwasababu ni maagizo ya Bwana YESU mwenyewe. Kulingana na Matendo 2:38. Na baada ya kumaliza hatua hizo muhimu..Nguvu ya Ajabu ya Roho Mtakatifu itaingia ndani yako, hiyo itakuongoza katika kuijua kweli yote ya biblia na kukufunulia kusudi la Mungu juu ya maisha yako, na jinsi ya kulitimiza hilo kusudi hatua kwa hatua..Na huyo huyo Roho atakusaidia kulitimiliza mpaka mwisho wa siku zako.
Wafilipi 1: 6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu”;
Anza leo kazi njema, Timiza kusudi la aliyekuleta hapa ulimwenguni, na siku ile upokee Taji ya Uzima.
Bwana akubariki sana.Tafadhali “share” na wengine ujumbe huu.
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Inada Wasiliana nasi kwa namba
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
JE! UBATIZO SAHIHI NI UPI?
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze Maneno ya uzima, Leo hii ukimwuliza mtu yeyote aliye mkristo swali.. ‘chakula cha rohoni ni nini?’….atakujibu pasipo kusita sita kuwa ni NENO LA MUNGU. Na ndivyo ilivyo Neno la Mungu ndio chakula cha Roho zetu. Ni swali ambalo jibu lake linajulikana na watu wote.
Wapo wengi wanaofahamu umuhimu wa Neno la Mungu, lakini vile vile si wengi wanaofahamu kazi ya Neno la Mungu katika maisha yao ya hapa duniani na huko wanakokwenda.
Leo tutatazama kwa ufupi kazi ya Neno la Mungu juu ya maisha yetu ya kikristo.
Kwanza kabisa kama tunavyojua wengi wetu kuwa Neno la Mungu linafananishwa na chakula, na pia kama tunavyojua mtu hawezi kukua vizuri au kuongezeka kimo au unene pasipo kula vizuri..Moja ya kazi ya chakula ni kutufanya tukue kimwili na kuwa na afya njema.
Kadhalika katika roho, ili tusitawi katika roho vile ipasavyo ni lazima tule vizuri rohoni, na chakula hakiliwi mara moja kwa mwaka, vinginevyo utakufa, bali kinaliwa mara tatu kwa siku, angalau huo ndio tunaweza kusema ni mlo ulio sahihi.
Lakini licha ya faida mojawapo ya chakula ambayo ni ya kuukuza mwili, ipo pia faida nyingine ya muhimu sana ambayo wengi wetu hatuifahamu, au kama tunaifahamu basi hatuitilii maanani.
Na faida hiyo ni kuupa MWILI NGUVU.
Mtu anapokula chakula, kile chakula kinaingia tumboni, na kuchanganyikana na baadhi ya vimeng’enyo na kisha kuna baadhi ya hatua zinaendelea pale, kile chakula kinavunjwa vunjwa na hatimaye kunapatikana virutubisho ambavyo vinaweza kuupa mwili nguvu, ndio hapo mtu anapata nguvu ya kuweza kusimama, kutembea, kufanya kazi, kukimbia, kuongea, kuona n.k. kama alikuwa ni mtu wa mapambano vitani anapata nguvu ya kupambana vizuri zaidi na kushinda.
Na Neno la Mungu ni hivyo hivyo, halitusaidii tu kukua kiroho, kama wengi wetu tunavyojua, bali pia linatupa nguvu za kila siku zinazoweza kutusaidia kufanya kazi za kiroho, kusimama katika roho, kukimbia katika roho, kushindana katika roho na kushinda. Ndio maana mtu mwenye afya njema utakuta anakula mara tatu kwa siku na anakula mlo kamili. Na mtu wa namna hiyo ni ngumu kuwa mdhaifu au kushambuliwa na magonjwa.
Kadhalika ni wajibu wetu hata sisi kulitafakari Neno si mara moja tu kwa siku au kwa wiki, hapana hata ikiwezekana mara tatu au mara nne kwa siku, ili kujiweka katika hali ya kuwa na afya njema katika roho. Kwasababu nguvu za rohoni kila siku zinapungua na zinahitaji kuongezwa chaji kwa kula chakula kizuri cha roho…Mtu asikudanganye eti! Kuwa nguvu za rohoni, hazipungui au haziishi,!! Huo ni uongo ndugu!! Watu wote nguvu zao zinaisha kila siku kwasababu zinatumika katika roho kufanya shughuli nyingi..hivyo ni lazima kila siku ziongezwe na zinaongezwa kwa kula chakula cha rohoni (Neno la Mungu).
Ndio maana biblia inatuambie “yeye ajidhaniaye kuwa amesimama aangalie asianguke 1Wakorintho 10:12”..Ikiwa na maana kuwa tunajukumu kila siku la kujiongeza nguvu za rohoni. Hata vyombo vya elektroniki kama simu, hakuna kifaa kinachokaa na charge muda wote ni lazima kuna wakati kinakwenda kuongezewa nguvu kwa kuchajiwa…Watu tu wa imani nyingine katika mambo yao wanaweza kufanya dua mara tano kwa siku, lakini wakristo hatuwezi kufanya lolote.
Ni kwanini wakati mwingine mtu anashambuliwa na nguvu za giza?..Ni kwasababu nguvu zake za rohoni ni chache, kila kukicha wachawi wanakusumbua, na magonjwa ya ajabu ajabu yasiyofahamika chanzo chake..mengi ya hayo (ingawa sio yote) yanasababishwa na roho yako kutokula vyema. Mara ya mwisho ulikula wiki iliyopita unategemea vipi usiwe dhaifu?, usishambuliwe na wachawi?.
Nguvu za rohoni hazipatikani kwa kulisoma Neno siku moja na kwenda zako?, haiko hivyo kabisa, Tunahitaji kujifunza Maandiko kila siku ili tuishi. Hata kama tutarudia chakula kile kile kila siku ni afadhali kufanya hivyo kuliko kutokula kabisa.
Ni afadhali kurudia kile kile nilichojifunza jana na juzi kuliko kutoshika kabisa Biblia na kujifunza maandiko, ndugu zipo hatari nyingi sana za kutolitafakari Neno la Mungu.
Ili siku yako, mwezi wako, mwaka wako uende vizuri unahitaji Neno la Mungu rohoni mwako, ili roho yako iwe salama unahitaji kujifunza Neno la Mungu kila siku, ili ukue katika maarifa ya ki-Mungu na ili umjue yeye zaidi, Kujifunza Neno lake kila siku hakukwepeki. Hiyo ndio siri ya kuishi pasipo kusumbuliwa na shetani na kuendelea mbele, Ni kwa kula tu chakula kilicho sahihi.
Zaburi 119: 105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu”.
Sikiliza maneno haya ya YEHOVA…
Kumbukumbu 11:18 “Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. 19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; 21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi Bwana aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi”.
Kumbukumbu 11:18 “Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako;
21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi Bwana aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi”.
Wakolosai 3: 16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
Ubarikiwe!
+225693036613/ +225789001312
NJAA IPO!, USIACHE KULA ASALI.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
CHAKULA CHA ROHONI.
MAJI YA UZIMA.
Shalom! shalom!, karibu tuongeze maarifa katika mambo yetu yahusuyo wokovu wetu hapa duniani. Wengi wanadhani mtu akiingia tu katika wokovu basi, akili yake huwa inafutwa na kugeuzwa kuwa kitu kingine cha kimbinguni, Na hivyo vitu kama wivu, hasira, ghadhabu, visasi, vinyongo, chuki, huzuni, hofu, vinakuwa vimeondoka kabisa ndani ya huyo mtu, Na ikionekana kuwa havijaondoka basi huyo mtu bado hajafanyika kiumbe kipya.
Mimi hapo nyuma niliomuomba sana Mungu aniondolee hivyo vitu ndani yangu, kwasababu nilikuwa ninachukia ninapoona hasira inakuja ndani yangu na mimi ni mkristo, wakati mwingine hofu Fulani,.hayo yalinifanya nijione kama bado sijawa mkristo. Lakini baada ya kuona ninaomba sana viondoke bila ya kuona mafanikio yoyote, ndipo Mungu akanifumbua macho yangu ya ndani nikaona…
Nikaja kugundua kuwa nilikuwa ninamuomba Mungu aniondolee vitu ambavyo ameniumbia ndani yangu, na kama hiyo haitoshi, yeye mwenyewe anavyo…Nikafikiria nikasema ni kweli ukitafakari utaona Mungu anao wivu, amejitaja mwenyewe kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 20), amejitaja kuwa yeye ni Mungu mlipiza kisasi, amejitaja yeye ni Mungu mwenye hasira nyingi na ghadhabu, isitoshe amejionyesha sehemu nyingi kuwa anahuzunika wakati mwingine,..Sasa kama hivyo vitu vipo ndani yake kwanini mimi nimwombe aniondolee?..Na yeye katuumba sisi kwa mfano wake, biblia inasema hivyo.
Kiuhalisia vitu hivi Mungu hakuviumba kwa ubaya ndani yake na ndani ya watu wake, bali ni kwa nia njema kabisa na ya Upendo. Embu jaribu kufikiria kama mtu asingekuwa na wivu hata kidogo kwa mpenzi wake, inamaanisha kuwa hata angemwona mtu mwingine anam-baka mke wake, asingeshuhulika kufanya lolote angemwacha tu, kwasababu ndani yake hakuna chembe chembe za wivu, ambazo hizo zingemsaidia kumpigania mke wake asifanyiwe kitendo kama kile..
Jaribu pia kufikiria kama mtu asingekuwa na hofu ndani yake, angeweza hata kwenda kuchukua kisu na kumchoma mtu mwingine, au angeweza hata kwenda kusimama juu ya ghorofa refu na kujitupa chini, kwasababu ndani yake hakuna hofu ya kuogopa chochote, unadhani tungekuwa na madhara mengi na makubwa kiasi gani duniani?. Jamii zetu zingesimamaje?
Au fikiria ungekuwa hauna hasira hata kidogo ungekuwa wewe ni wa kuonewa au kuudhiwa tu kila saa, au unadhulumiwa haki yako, lakini kama mtu akiona umekasirika, ataogopa na kuacha kile alichokuwa anakifanya kwasababu anajua akiendelea madhara yoyote yanaweza kumtokea..Hivyo unaona hasira hapo inasimama kama ulinzi kwa mtu asionewe au asidhulumiwe au asiudhiwe.
Vivyo hivyo na vitu kama ukali, na vinginevyo. Ni mambo ambayo Mungu ametuumbia ndani yetu, ili yatumikie katika mahali papasapo,..Lakini leo hii ni kwanini tunaona , Wivu ni kitu kibaya, hasira ni kitu kibaya, kisasi ni kitu kibaya, chuki ni kitu kibaya, kinyongo ni kitu kibaya….Ni kwasababu tunavitumia mahali ambapo Mungu hakutaka vitumike na ndio hapo vinaonekana kuwa ni vitu vibaya visivyofaa kuonekana ndani ya mtu yeyote.
Embu tuangalie mfano wa wivu mzuri, Tuchukulie mfano wa Bwana wetu Yesu, yeye kuna wakati alishikwa na WIVU wa kushindwa kuvumilia mpaka kufikia hatua ya kuleta madhara na vurugu..Hayo yalitokea pale alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wanafanya biashara mahali ambapo pangepaswa pawe mahali pa Ibada…ndipo tuona akapindua mezi zile na kuwachapa wale waliokuwa wanafanya biashara mule ndani. ..Mpaka wanafunzi wake wakakumbuka kuwa iliandikwa hivyo (Yohana 2:17 ….Wivu wa nyumba yako utanila.).
Unaona huo ni mfano mzuri jinsi wivu ulivyotumika jinsi ipasavyo. Lakini tujiulize ingekuwa na sisi tupo pale na yeye je! Tungeshirikiana naye kufanya kile kitendo? Ni rahisi kusema ndio. Lakini ikiwa leo hii tunaona Injili ya YESU KRISTO Bwana wetu inageuzwa na kuwa taasisi za kibiashara, na hakuna chochote kinachotukuna ndani yetu?..Badala yake wivu wetu unajidhihirisha katika mambo mengine yasiyokuwa na umuhimu sana, pale tunapoona wafanyakazi wenzetu wanatuibia ofisini, ndio tunakuwa na wivu, pale tunapoona mafisadi wanaaiibia nchi, wanapitisha magendo, ndio tunazungumza mpaka mshipa ya shingo inatutoka, na kibaya zaidi pale tunapoona majirani zetu wanafanikiwa, ndipo tunatafuta namna zote juu chini za kuwashusha ili wasiendelee mbele …
Sasa kama wivu wa namna hii ndio Mungu kaukataa, kama upo ndani yetu basi tujue umetumika isipovyopasa na hivyo unahesabika kuwa ni dhambi mbele za Mungu..Nguvu hizo hizo unazotumia kuhakikisha adui yako hafanikiwi kwanini usizipeleke mbele za Mungu wako kuhakikisha adui yako MKUU shetani hafanikiwi na kazi zake mbovu?..Kwanini tunaona kazi ya Mungu inachezewa na sisi tunakaa kimya, wachekeshaji wameingia mpaka madhabahuni wanamfanyia Mungu dhihaka na sisi tunafurahi pamoja nao,..
Halikadhalika KISASI ni kitu chema ambacho kimeumbwa ndani yetu ili kitimize kusudi Fulani..Na kusudi hilo si lingine zaidi ya kumpiga shetani. Fikiria Ulipokuwa katika dhambi ulivyokuwa unateseka na magonjwa, ulivyokuwa unateswa na nguvu za giza au mapepo au wachawi au jinsi ulivyokuwa unakesha Disco na kupoteza muda mwingi na pesa nyingi, hata kwa wiki mara mbili ukimwabudu shetani kule..Lakini sasa umekuwa mkristo, kuna kitu Fulani ndani yako unapaswa ukihisi kitu kama kisasi kumlipizia shetani kukupotezea muda wako, na kukutesa na mambo mabaya, Hivyo sasa utahakikisha muda wako hata kwa wiki mara tatu unakesha katika kumsifu Mungu na na katika kuomba nakuziharibu kazi za shetani katika kuwavuta watu kwa Kristo..Hicho ndio kisasi Mungu anachokitafuta, ulikuwa unaimba nyimbo za kidunia, sasa umeokoka ni wakati wa kumwimbia na kumsifu Mungu kwa nguvu zaidi kulipiza kisasi kwa vile shetani alivyokutenda..
Ulikuwa ni msengenyaji na mmbea wa kupelekea taarifa za watu kwa watu wengine mpaka mtaa wa tatu sasa umeokoka ni wakati wa kutumia kipawa kilekile kumlipizia shetani kisasi kwa kusambaza habari za Yesu kwa nguvu wa watu wengine zaidi ya pale ili kumkomesha shetani. Hivyo ndio visasa ambavyo Mungu anavihitaji.
Vivyo hivyo tumeumbiwa hofu. Ulikuwa unamwogopa shetani na wachawi kiasi kwamba hata wewe mwenyewe ulikwenda huko huko kumwomba akupe hirizi kama kinga yako. Lakini sasa umeokoka, ile hofu imerudi mahali ipasapo, itumie hiyo kumwogopa Mungu wako na sio adui yako tena..kama Bwana Yesu alivyotuambia
Luka12:5 “Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.”
Hofu yako ikiwa kwa Mungu utaogopa kwenda kuzini, utaogopa kutukutana, utaogopa kusema uongo, utaogopa kufanya mambo maovu, kama haipo hautamjali Mungu n.k.
Chuki iliyopo ndani yako, ndugu hiyo Mungu hakukuumbia kwa ajili ya kuwachukia ndugu zako, ni wazi kuwa huwezi kumwekea chuki mdogo wako au kaka yako au mama yako aliyekuzaa, utakuwa na chuki sana na Yule ambaye uliyemwona akimchoma mdogo wako moto bila huruma., Vivyo hivyo chuki hasaa ya ki-Mungu ipo ndani yetu kumchukia SHETANI pamoja na mapepo yake yote, na kazi zake zote, na sio wanadamu wenzetu ambayo hayo ndiyo yamekuwa sababu ya ndugu zetu wengi mamilioni kuwepo kuzimu leo hii.. Na hivyo kama hiyo chuki itatumika ndani yetu kisawasawa leo hii tutaweka mikakati kabambe ya kumwangamiza shetani na kazi zake kwa KUHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO kwa watu wote.
Hivyo kwa kumalizia, ni maombi yangu kuwa vipawa vyote na tabia zote Mungu alizoziweka ndani yako, usiruhusu shetani azitumie vibaya kwa faida zake, bali badala yake, tuziteke zikaleta manufaa makubwa katika ufalme wa mbinguni. Leo hii usimwombe Mungu akuondolee hasira ndani yako, haitaondoka hiyo, ili uwe mfano wa Mungu lazima uwe nayo, badala yake pale inapokuja basi ukumbuke lile Neno kuwa je! Mahali ninapoiachilia ni mahali pafaapo, kama hapafai, moja kwa moja ikatae hiyo hali na yenyewe itatulia,. Lakini ikiwa ni sehemu ifaayo yaani ni sehemu yenye manufaa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni na kumkandamiza shetani..basi usiizuie kwani hiyo imevuviwa na Mungu kutimiza kusudi lake.
Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
KIFAA BORA CHA MATUMIZI.
Mhubiri 1:1 “Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu. 2 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. 3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6 Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. 7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. 8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. 9 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. 10 Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi”.
Mhubiri 1:1 “Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu.
2 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.
3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.
6 Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
9 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
10 Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi”.
Shalom karibu tujifunze Neno la Mungu, Sulemani alipewa na Bwana hekima kuliko watu wote wakati huo, alichunguza mambo mengi na kupata jawabu moja ya mambo hayo na kusema yote ni UBATILI.
Ubatili maana yake ni “kitu kisichokuwa na maana”…au “kitu ambacho kwa nje kinaonekana kina thamani kubwa lakini ndani yake hakina maana”..hiyo ndio maana ya Neno UBATILI.
Umewahi kujiuliza kwanini Sulemani aliishia kusema mambo yote ni Ubatili??…Hebu tujifunze kidogo ni kwanini alisema hivyo..
Ukisoma mstari wa 4, 5,6 na wa 7 hapo juu utapata picha ni kwanini Sulemani anasema mambo yote ni Ubatili. Utaona kuwa aliyajaribu kutafiti mambo kadhaa akidhani kuwa atapata jambo jipya ndani yake lakini kinyume chake akagundua kuwa mambo yote yanamrudisha kwenye jambo lile lile la kwanza, akachukia na kuhuzunika akasema sasa inafaida gani kujitaabisha na kitu ambacho hatma yake ni kule nilikotokea.
Alilitafakari jua, alilichunguza linapozama huwa linaenda wapi…pengine akatafakari labda linapotea na kutokea jua jingine jipya…lakini alipozidi kuchunguza akagundua jua ni lile lile moja, hakuna jua jipya, ni lile lile lipo kwenye mzunguko wake..
Akatafakari tena ni wapi maji masafi yanatengenezwa, akachunguza milimani ni sehemu gani hiyo inayoyatengeneza safi kila siku malita ya maji mapya yanayotiririka chini ya milima na kuishia baharini, alipochunguza sana akitazamia agundue jambo jipya, akaishia kugundua kuwa hata hakuna mahali maji mapya yanapotengenezwa, maji ni yale yale yanajisafisha na yapo kwenye mzunguko wake..yanaingia kwenye bahari yanarudi milimani na kutiririka tena, akaona tabu yote aliyoipata kuchunguza inamrudishia jibu lile lile kuwa hakuna jipya.
Hakuishia hapo, akaanza kuutafakari tena na upepo, akitafuta upepo, baada ya kumpuliza mtu unaenda wapi, akitazamia kugundua kuwa kuna mahali upepo mpya unajitengeneza kila siku na ule wa zamani kuna mahali unakwenda kuishia…Lakini Mwisho wa siku akagundua kuwa hakuna upepo mpya, upepo ni ule ule upo kwenye mzunguko wake. Akachukia kwasababu alitumia muda mwingi kuchunguza akitegemea kuvumbua kitu kipya ndani yake, kinyume chake alipata majibu madogo.
Ili kuuelewa vizuri uchungu wa kupoteza muda Hebu tafakari mfano huu: mtu mmoja asiyeijua Jeografia ya dunia aliamua kuanza safari ya kwenda mbali na makazi yake ili kuutafuta mwisho wa dunia, akitumaini kuwa pale upeo wa macho yake unapoishia ndio kutakuwa ni mwisho wa dunia, kwahiyo akaanza kufunga safari na kusafiri mamia ya maili huku kila siku anaongeza mamia ya maili katika safari yake, akajifariji kuwa kashafika mbali sana, hivyo akazidi kusafiri miezi na miezi na hatimaye miaka, akisema akilini mwake kuwa nataka nifike mwisho wa dunia, nitasafiri maisha yangu yote mpaka nifike mwisho wa dunia mahali atakapokuta kuna ukomo wa ardhi. Akavuka bahari na mito, na ghafla pengine baada ya miaka 50 ya safari yake anakuja kujikuta katokea tena pale pale alipoanzia safari yake….
Baadaye sana ndio anakuja kugundua kuwa dunia ni duara..utakapoanzia ndipo utakapomalizia..Unafikiri mtu huyo atajisikiaje?? Ni wazi kuwa atakasirika na kuchukia, kwasababu kapoteza miaka mingi kutafuta kitu kisichokuwa na maana, na pengine atajiona mjinga na kapoteza muda wake mwingi kwasababu alifikiri anavyozidi kusafiri ndipo anapokwenda mbali zaidi kumbe ndivyo anavyozidi kuukaribia mwanzo wake.
Ndio maana unaona katika kitabu hichi Mfalme Sulemani haanzi na salamu, wala maneno ya hekima kama alivyoanza katika mithali..badala yake anaanza kama mtu aliyeonja kitu na kukitema haraka na kusema hakifai!! hakifai!! Kimeoza!! Kimeoza kimeoza!!…na ndio tunaona anasema hapa ubatili!! Ubatili!! kila kitu ni ubatili!!…Hiyo ni sentensi ya kuwaonya wale watu ambao bado hawajaonja!! Kwamba wasijaribu kuonja! Kwasababu watakuta kitu ambacho hawajakitegemea, na mwisho wa siku watapata hasara.
Mhubiri 1: 12 “Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 13 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. 14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo”.
Mhubiri 1: 12 “Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.
13 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo”.
Anatuonya sisi tulio watoto, ndugu tusisubiri tufike mwisho ndio tugundue kuwa tulikuwa tunapoteza muda. Mfalme Sulemani anatosha kutufanyia utafiti na sisi tusiurudie tena huo utafiti ambao hauna matumaini yoyote mwisho wake.
Ndugu Mwanzo wa Mwanadamu ndio Mwisho wa mwanadamu. UMETOKA KWA MUUMBA WAKO UTARUDI KWA MUUMBA WAKO. Watu wengi ambao wapo katika dhambi hawalijui hilo…hawajui maisha ni DUARA kama vile DUNIA ilivyo duara..unapoanzia ndipo utakapoishia..haijalishi utajiona umepiga hatua kiasi gani kutoka katika mwanzo wako..lakini siku moja utaparudia tu pale ulipokuwa penda usipende, Na siku hiyo utajichukia na kujiona mjinga na umepoteza muda mwingi.
Ndio maana Sulemani huyu huyu sura za mbeleni anasema “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako Mhubiri 12” ..
kwasababu siku za uzee wako ndio siku za kuurudia mwanzo wako..Usiku unavyozidi sana ndipo asubuhi inavyokaribia…
Utajiona umefanikiwa katika mambo yako, kwahiyo huna haja ya kutubu wala kumkumbuka muumba wako, utajiona umekuwa na majukumu mengi hivyo huna haja ya kulisoma Neno lake na kulitafakari, utajiona umekwenda mbali sana kiteknolojia na kisayansi hivyo mambo madogo madogo yanayohusu Imani, na wokovu hayana maana tena kwako, utajiona una afya nyingi na ulinzi mkubwa hivyo hakuna haja ya kutafuta ulinzi wa maisha yangu ya milele…Siku zinazidi tu kwenda unajishughulisha na mambo tu yasiyokuwa na maana, Lakini nataka nikuambie HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA..ULIPOANZIA NDIPO UTAKAPOMALIZIA. Hujui kuwa Unakaribia kumaliza duara la maisha yako, kurejea mwanzoni, pasipo wewe kujijua na siku hiyo ndio utakayofahamu kuwa yote uliyokuwa unajitaabisha nayo hayana maana.
Sulemani anasema..Mkumbuke Muumba wako kabla roho yako haijamrudia yeye aliyoitoa..
Mhubiri 12: 6 “Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; ……… 7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA”.
⏩Anamalizia kwa kusema maneno haya..
Mhubiri 12: 8 “Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili! 9 Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi. 10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, YAANI, MANENO YA KWELI. 11 Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja. 12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. 13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Mhubiri 12: 8 “Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!
9 Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.
10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, YAANI, MANENO YA KWELI.
11 Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.
12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Jumla ya mambo yote ndio hiyo MCHE Mungu uzishike amri zake, je! Swali linakuja unazishika amri?, je wewe ni mlevi? Mwasherati? Mshirikina? Mtazamaji pornography?, mwizi? Msengenyaji? Je ni mfanyaji masturbation?..je ni mtukanaji? Je ni mtoaji mimba? Ni msagaji au shoga?..au ni mfanyaji wa dhambi kwa siri? Watu nje wanakuona uko sawa lakini ndani yako hakufai kumeoza?.
Usisubiri mwisho wako ufike, kwasababu wengi siku ile watatazamia wafike sehemu mpya, wengine watafikiri baada ya kufa kutakuwa hakuna maisha, lakini watajikuta wamerudi pale pale kwa mwokozi wao waliomkimbia mwanzo, leo wewe usiwe mmoja wao. Kristo yupo hai , na anawapokea wenye dhambi na wote wanaomkimbilia, unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kutenga dakika chache kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha sasa angali muda upo..unadhamiria kwa vitendo kuacha ulevi, sigara, pornography, utukanaji, usengenyaji, wizi n.k, na ndipo Mungu atakapokupa NGUVU ya kuvishinda ……hapo ulipo yeye yupo haihitaji mtu akuombee, kwa Imani amini yupo hapo anakusikia..Mwambie akuoshe dhambi zako zote na yeye ni mwaminifu na si mwongo atakupokea na kukufanya mpya na kukusamehe..
Kisha baada ya kutubu nenda katafute ubatizo sahihi kama hujafanya hivyo, mahali popote karibu na wewe kumbuka ubatizo ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji mengi na kwa Jina la YESU, na baada ya kubatizwa, Roho atafanya kazi ndani yako kwa namna isiyo ya kawaida na uwezo wa ajabu wa kushinda dhambi utashuka ndani yako, na uwezo mkubwa wa kuyaelewa maandiko utaingia ndani yako..Hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuwa na uhakika wa kuiona mbingu.
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?