Title 2018

DANIELI: Mlango wa 10

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe.

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli, leo tukitazama ile sura ya 10, Kama tukiangalia kwa undani kitabu hichi tutaona kuwa sehemu kubwa ya Unabii Danieli aliopewa ulikuwa unahusu zile FALME 4 zitakazotawala mpaka mwisho wa dunia, ambazo ni 1) BABELI 2) UMEDI na UAJEMI 3) UYUNANI na 4) RUMI.

Lakini kama ukichunguza ile sura ya pili, utaona Danieli alifunuliwa kwa juu juu picha inayohusu falme hizo, kwa kupitia ndoto ya mfalme Nebukadneza aliyoiota juu ya ile sanamu, tunaona pale hakupewa maelezo yoyote marefu kuhusu hizo falme, alionyeshwa tu utaanza ufalme wa kwanza ambao ni wa dhahabu, kisha fedha, halafu shaba na mwisho chuma, hakupewa hata majina ya falme hizo zitakazokuja kutawala baadaye isipokuwa Babeli tu.

Lakini pamoja na hayo Danieli hakuridhika aliendelea kumsihi Mungu amfunulie undani wa mambo hayo na ndio maana tunaweza kuona katika sura ya 7, akionyeshwa maono yanayohusu jambo lilelile isipokuwa hapa yameingia kwa undani zaidi tofauti na alivyoonyeshwa kule kwanza.

Tunasoma aliona wanyama 4 wakitoka baharini ambao ndio zile zile falme 4 zenyewe. Mnyama wa kwanza ndio yule kama simba(Babeli), wa pili alikuwa kama dubu na mifupa mitatu ya mbavu mdomoni mwake ambayo tulishaona tafsiri yake ni nini, wa nne alikuwa mfano wa chui mwenye vichwa vinne, na tunaona Danieli alipewa tafsiri juu ya vichwa vile akaelezwa kuwa watakuwa ni wafalme 4 watakaonyanyuka katika huo utawala wa tatu ambao ni wa uyunani, pia akaonyeshwa mnyama mwingine wa mwisho wa 4 ambaye alikuwa mbali sana na wale wengine kimaumbile.

Pamoja na hayo Danieli katika maono haya alitajiwa na majina ya falme hizi 2 zitakazofuata, tofauti na maono yale ya kwanza hapa alifunuliwa kuwa ufalme wa pili utakuwa ni UMEDI NA UAJEMI, na watatu utakuwa ni ufalme wa UYUNANI. Kwa undani wa maelezo haya unaweza ukasoma mlango wa 7 tuliokwisha kuupitia.

Lakini bado tunaona Danieli baada ya kuona hayo picha bado haikuwa dhahiri kwake hivyo alikuwa na shauku ya kuzidi kufahamu juu ya mambo hayo yataishiaje, na ndio tunaona katika ile sura ya 8 Mungu aliendelea kumfunulia juu matukio yatakayokuwa yanatendeka ndani ya hizo falme, hapa tunaona akionyeshwa yule kondoo mwenye pembe mbili na Beberu, ambapo yule Beberu alikuja kumshambulia yule kondoo na kumuua kwa ile pembe moja aliyokuwa nayo, ambayo baadaye ilikuja ikavunjika na kuzuka pembe nyingine nne.

Sasa Danieli alizidi kuonyeshwa kwa ufafanuzi zaidi mambo yatakayokuja kutokea katikati ya hizi falme, kwamba yule kondoo mwenye pembe mbili ni ufalme wa Umedi na Uajemi, na yule beberu ni ufalme wa uyunani, na ile pembe moja ni mfalme wa kwanza wa uyunani ambaye atanyanyuka na kuuvunja ufalme wa Uajemi, kumbuka mambo hayo yote Danieli hakuonyeshwa katika maono mengine yaliyotangulia, hivyo unaweza ukaona ni mambo yale yale isipokuwa Danieli anafunuliwa kwa undani zaidi, ukiendelea kusoma utaona alionyeshwa pia kutakuwa na pembe nyingine ndogo itakayozuka katikati ya zile pembe 4, itakayojitukuza mbele za Mungu na huyu si mwingine zaidi ya ANTIOKIA EPIFANE 1V. wa uyunani kama historia inavyoonyesha.

Kumbuka Danieli wakati anaonyeshwa juu ya Falme hizi ukisoma katika ile sura ya 7 aliona pembe ndogo(mpinga-kristo) ikizuka katika ufalme wa mwisho wa 4 ambao tunafahamu ni Rumi, lakini hakuonyeshwa pembe nyingine ndogo itakayozuka katika Ufalme wa 3 wa uyunani, lakini hapa tunaona ameonyeshwa pembe hii katika sura hii ya 8. Hivyo tunaona ni mwendelezo wa maono yale yale isipokuwa kwa undani zaidi.

Vivyo hivyo ukiendelea sura ya 10, 11 na ya 12, utaona jinsi Danieli akifunuliwa maono yale yale kwa uchambuzi zaidi, tukio baada ya tukio, mpaka maono yale yakawa dhahiri kwake.

Kwenye Sura hii ya 10 tunaona Danieli akijisogeza mbele za Mungu kwa unyenyekevu akimsihi Mungu ampe ufahamu zaidi juu maono hayo aliyokuwa anafunuliwa na ndio maana utaona baada ya kufunuliwa biblia inasema “alifahamu na kuelewa maono yale”, ikiwa na maana hapo mwanzo mambo yale hayakuelewa vizuri kwake.

Tukisoma..

Mlango 10:1-21”

1 Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni VITA VIKUBWA; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.

2 Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.

3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.

4 Na siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli;

5 naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi;

6 mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.

7 Nami, Danielii, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia ili kujificha.

8 Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.

9 Walakini naliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.

10 Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu.

11 Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.

12 Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.

13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

14 Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.umed

15 Na alipokwisha kusema nami maneno hayo, nikauelekeza uso wangu chini, nikawa bubu.

16 Na kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena, nikamwambia yeye aliyesimama karibu nami, Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata asikusaziwa nguvu.

17 Maana, mtumishi wa Bwana wangu huyu atawezaje kusema na Bwana wangu huyu? Kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.

18 Kisha mmoja mfano wa mwanadamu akanigusa tena, akanitia nguvu.

19 Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu.

20 Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.

21 Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.

Kumbuka sura hii inaeleza jinsi Gabrieli alivyomtembelea Danieli, akimweleza sababu ya kukawia kwake, kwamaana hata baada ya Danieli kumaliza kufunga na kuomboleza majibu yalikuwa hayajafika bado, Lakini ujumbe kamili Gabrieli aliomletea ulikuwa unahusu maelezo ya ndani kabisa yahusuyo zile falme na sio kitu kingine, ambayo tutakuja kuona katika sura ya 11 na 12.

Lakini katika sura hii tutaona SIRI zilizopelekea Danieli kupokea mafunuo makubwa kama yale, Awali ya yote Danieli alisema NI VITA VIKUBWA, ikiwa na maana kuwa kuna upinzani mkubwa katika kuyapata mambo hayo, Tunaweza kusoma pale Gabrieli alimwambia “Tangu siku ile ya kwanza alipoutia moyo wake ufahamu maombi yake yalisikiwa Lakini mkuu wa ufalme wa uajemi alimpinga siku 21…”

Tunajifunza nini hapo? Mungu huwa hamjibu mtu maombi yake baada ya kufunga na kuomba, hapana bali huwa anamjibu mtu maombi yake pale tu anapotia moyo wake ufahamu, na ndipo maagizo yanatolewa papo hapo na ndio maana Bwana Yesu alisema (Mathayo 6:8) “Baba yetu anajua tunachohitaji kabla hata hatujamwomba” unaona?.. Lakini sasa adui yupo huyo ndiye anayehakikisha majibu hayafiki kwa muhusika, hivyo inahitaji kupigana vita kumshinda.

VITA KATIKA ANGA.

Kama ukisoma hapo juu utaona kuwa mkuu wa ufalme wa uajemi alimpinga Gabrieli, pia ukiendelea kusoma utaona alisema “atakapotoka huko kupigana na mkuu wa uajemi, mkuu mwingine w a Uyunani atakuja”. Sasa kumbuka hawa wakuu wa uajemi na uyunani sio wafalme wa dunia, bali ni roho za mashetani zilizokuwa zinaendesha hizo falme 4 za dunia, kumbuka wakati Danieli anafunuliwa maono haya alikuwa katika Ufalme wa Uajemi, Babeli ilikuwa imeshaanguka, Hivyo mkuu wa ufalme wa Babeli (PEPO) alikuwa ameshaondoka, lililopo hapo ni la uajemi, kisha litakuja PEPO la Uyunani na mwisho litakuja la RUMI, ambalo ndio lipo sasahivi likitenda kazi.

Lakini kumbuka kama biblia inavyosema Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME na mamlaka, juu ya WAKUU WA GIZA HILI, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. “

Neno hilo likiwa na maana kuwa hatutumia njia za kibinadamu kushinda na hizi FALME za giza, Kushindana kwetu sio kusema ninatuma kombora, au moto, kuzimu, au maombi ya kuteketeza anga na wakuu wa anga, hapana Danieli hakufanya hivyo, njia hiyo ni kwa namna ya damu na nyama na haiwezi kumshinda shetani hata kidogo, bali biblia inaendelea kusema..

Waefeso 6: 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

14 Basi simameni, hali mmejifunga KWELI viunoni, na kuvaa dirii ya HAKI kifuani,

15 na kufungiwa miguu UTAYARI tupatao kwa Injili ya amani;

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya IMANI, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya WOKOVU, na upanga wa ROHO ambao ni NENO LA MUNGU;

Hivyo malaika kabla ya kuwasilisha maombi ya mtu kwanza huwa anakutana na MSHITAKI HAPO JUU (mkuu wa giza na mapepo yake), ambaye anatushitaki sisi mbele za Mungu (Ufunuo 12:10)kwa kuonyesha kwamba hatustahili kukipokea kitu tunachokiomba, na hoja yake ikiwa na nguvu, majibu hayatufikii anayazuia kwa kuwa ana hati miliki yako, (kwamfano, mtu anaomba jambo fulani kwa Mungu halafu bado anamashaka mashaka kama kweli atajibiwa maombi yake au la!. biblia inasema lolote muombalo aminini ya kwamba mmepokea nalo litakuwa lenu. Sasa mwovu, akikuangalia na kuona kuwa hauna Imani ya kupokea jambo hilo mitikisiko fulani inakutokea unakataa tamaa, yeye anatumia hiyo nafasi kukushitaki mbele za Mungu kuwa huyu mtu hana uhakika na anayemwomba hivyo hastahili kupokea hicho kitu, hapo shetani anakuwa ameshinda vita, hivi ndio vita vinavyopiganwa. Na ndio maana biblia inasema Imani ni ngao itakayoweza kuzima mishale yote ya moto ya yule mwovu.

Yakobo 1:5-8″ Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. “

Mfano mwingine mtu anaomba Neno fulani kwa Mungu, halafu hajakoloewa, tatizo sio kwamba maombi yake hayajasikiwa, hapana bali MKUU WA GIZA yupo hapo juu akipeleka hoja juu ya maisha yako mbele za Mungu, kwamba Neno linasema ” Mtu yeyote asiye na Roho wa Kristo huyo sio wake (Warumi 8:9)” Hivyo yule malaika aliyetumwa kukuletea majibu akikutana na hoja zenye nguvu kama hizo atakwama, maana yule mshitaki atamwambia, Mtu huyu ni mali yangu kwasababu hana Roho wa Mungu, hivyo haya majibu hayamuhusu. Sasa mtu wa namna hii kakosa CHEPEO YA WOKOVU na UPANGA WA ROHO. hivyo lazima vita hivi vimshinde tu na akose anachokitafuta.

Mfano mwingine mtu anayeabudu sanamu (sanamu za bikira Maria, na watakatifu, pamoja na kusali rozari), halafu bado unakwenda kumwomba Mungu, mkuu wa giza atapeleka hoja, za kimaandiko “Kutoka 20:4 inasema Mungu atawapatiliza maovu yao hao wote wanaoabudu sanamu kwa wivu wake”, Hivyo badala ya kupokea baraka, yanageuka kuwa laana kwa mtu huyo.

Neno la Bwana linasema..

Ezekieli 14: 3, & 7-8 “Mwanadamu, watu hawa wametwaa VINYAGO vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu NIULIZWE na wao katika neno lo lote?

…….7 Kwa maana kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na KULIWEKA KWAZO LA UOVU MBELE YA USO WAKE, kisha kumwendea nabii, na kuniuliza neno kwa ajili ya nafsi yake; mimi, Bwana, nitamjibu, mimi mwenyewe;

8 nami nitaukaza uso wangu juu ya mtu yule, na kumfanya kuwa ajabu, awe ishara na mithali, nami nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. “

Kwahiyo kwa Danieli mpaka majibu kama hayo kumfikia, aliweza kumshinda (mkuu wa uajemi) katika nyanja zote katika ulimwengu wa roho, hivyo shetani alishindwa kwasababu hakuwa na hoja yoyote ya kumshitaki mbele za Mungu yamfanye asipokee majibu yake.

Na faida aliyoipata Danieli baada ya kushinda tunaweza kuiona katika sura zinazofuata, Mungu aliweza kumfunulia agenda na mpango mzima wa mambo yanayokuja mbeleni juu ya ufalme aliokuwepo na unaokuja wa Uyunani pamoja na ule wa mwisho. hatua kwa hatua tofauti na maono aliyokuwa anayaona mwanzo, mambo hayo utayaona katika sura ya 11 na 12.

Kwahiyo kwa ujumla tunaweza kujifunza katika sura hii Danieli ni mtu aliyekuwa anahama kutoka utukutu hata utuktufu, ono moja halikumfanya aridhike na hali aliyopo aliendelea kutafuta kwa kusoma vitabu na kuomba mpaka mambo yote ya mbeleni yakawa wazi kwake, na sisi vivyo hivyo tunahitaji kusoma sana maandiko na kuomba, mpaka mambo yatakayotukabili huko mbeleni yawe wazi kwetu, hatupaswi kuridhika tu katika hali tulizopo angali tukijua hatufahamu yanayokuja mbeleni.

Biblia inasema Bwana Yesu alikuwa akiongezeka KIMO na HEKIMA, kumbuka sio KIMO cha urefu bali Kimo cha kumjua Mungu, na aliongezeka hekima pia ya kuyajua mapenzi ya Mungu, ikiwa na maana kuwa alipozaliwa sio kwamba alikuwa anajua kila kitu kama ndio hivyo alipokuwa na miaka 12 asingekuwa anawasikiliza na kuwauliza maswali marabi, Hii inaonyesha kuwa alikuwa anakua kwa hekima. Sasa kama yeye ambaye ni Bwana wetu alifanya hivyo inatupasaje sisi?. Tunapaswa tukue tufikie cheo cha kimo cha utimilifu wake (Waefeso 4:13).

Kumbuka pia mkuu wa giza tulilopo sio tena wa uyunani au uajemi bali ni RUMI, na ni roho inayowapofusha watu wasione mbele, wala wasitake kufahamu mambo ya mbele kama wale wengine walivyomzuia Danieli asione mambo ya mbeleni, kwahiyo fahamu kuwa vita vilivyopo sasahivi ni vikubwa kuliko vile vya Danieli. Si ajabu watu wamepoteza hamu ya kufahamu mambo ya mbeleni na mbinguni, injili wanazopenda kuzisikia ni za mafanikio tu, na mambo ya ulimwengu huu yanayopita, ni dhahiri kabisa mkuu wa giza hili amewapofusha macho.

Hivyo ndugu kama unaabudu sanamu, kama hujaokolewa, kama unaishi katika dhambi, kama Huliamini Neno la Mungu, una mashaka upo vuguvugu, fahamu upo chini ya mamlaka ya mkuu wa anga hili, na yeye ndiye mshitaki wako mbele za Mungu usiku na mchana ili usione mambo ya mbeleni au usipokee baraka za Mungu na mwisho kabisa usiione mbingu.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mwendelezo >>> Mlango wa 11

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Nyinginezo:

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI.

MKUU WA GIZA.

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

VITA BADO VINAENDELEA.

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 9

Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe;

Katika sura hii tunaona Danieli kwa shauku ya kutaka kujua hatma ya Taifa lake Israeli na watu wake,hata lini wataendelea kukaa katika nchi ya ugenini,aliazimu kutafuta kwa bidii, kwa njia nyingi ikiwemo kwa kusoma VITABU, na kufunga na kuomba juu ya jambo hilo mpaka akasikiwa. Kama tunavyosoma;

Danieli 9:1-2 ” Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;

2 katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, KWA KUVISOMA VITABU, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, MIAKA SABINI.

Tukisoma habari hii (Danieli 9:–2) tunaona Danieli alikwenda kusoma VITABU, na sio KITABU, ikiwa na maana kuwa alisoma kitabu zaidi ya kimoja, na moja ya hicho kilikuwa ni kitabu cha Yeremia Nabii. Na katika kuchunguza kwake alikutana na maandiko yanayosema hivi.

Yeremia 29:1-10″ Maneno haya ndiyo maneno ya waraka, ambao nabii Yeremia aliupeleka toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadreza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hata Babeli.

2 (hapo walipokwisha kutoka Yerusalemu Yekonia mfalme, na mama yake mfalme, na matowashi, na wakuu wa Yuda na Yerusalemu, na mafundi, na wahunzi;)

3 kwa mkono wa Elasa, mwana wa Shafani, na Gemaria, mwana wa Hilkia, (ambao Sedekia, mfalme wa Yuda, aliwatuma hata Babeli, kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli), kusema,

4 Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, AWAAMBIA HIVI WATU WOTE WALIOCHUKULIWA MATEKA, NILIOWAFANYA WACHUKULIWE TOKA YERUSALEMU MPAKA BABELI;

5 Jengeni nyumba, mkakae ndani yake, kapandeni bustani, mkale matunda yake;

6 oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.

7 Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani.

8 Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Manabii walio kati yenu, na wabashiri wenu, wasiwadanganye ninyi, wala msisikilize ndoto zenu, mnazootesha.

9 Kwa maana kwa jina langu hutabiri maneno ya uongo kwenu; mimi sikuwatuma, asema Bwana.

10 Maana Bwana asema hivi, BABELI UTAKAPOTIMIZIWA MIAKA SABINI, NITAWAJILIA NINYI, NA KULITIMIZA NENO LANGU JEMA KWENU, KWA KUWARUDISHA MAHALI HAPA.”

Unabii huu Bwana aliwaambia watu wa Yuda kwa kinywa cha Yeremia kutokana na maasi yao na uovu wao kwamba watachukuliwa mateka na watu wa Babeli nao watakaa huko kwa muda wa miaka 70 kisha Bwana atawajilia tena na kuwarudisha katika nchi yao. Kumbuka wakati wayahudi wote wakiwa wamelala licha ya kuwa katika hali yao ya utumwa Danieli aliazimu binafsi kutafuta kufahamu majira na nyakati anazoishi, kwa maana Bwana Yesu alisema katika Mathayo 7, tafuteni nanyi mtaona, kwa maana kila atafutaye huona. Hivyo Danieli kwa kufanya hivyo kutafuta kwa bidii, Mungu alimjalia kuona kuwa imebakia miaka miwili tu, mpaka wao kutoka Babeli yaani walikuwa wameshamaliza miaka 68 kati ya ile 70 ya wao kukaa utumwani. Na ndio maana Biblia imemwita Danieli kama mtu mwenye Hekima, na mtu apendwaye sana.kwasababu ni mtu aliyependa kutafuta kujua majira na saa anayoishi.

Vivyo hivyo na kizazi chetu cha mwisho tulichopo, Mungu ameshaweka majira ya watoto wake kwenda kwenye unyakuo na siku ambayo hii Babeli ya rohoni itakapo hukumiwa, Kumbuka Mungu hana desturi ya kumlazimisha mtu kufahamu agenda yake ya ukombozi bali wale waliotayari na wanaotafuta kujifunza na kutuka kujua ndio watakaofahamu, na Mungu atawaongoza katika Kusoma, na ndio maana kuna umuhimu sana wa KUJIFUNZA na KUYACHUNGUZA MAANDIKO kila Siku, kwasababu SIRI nyingine hazitafahamika isipokuwa kwa kujifunza sana NENO LA MUNGU kwa mfano wa Danieli.

Hauoni hata katika majira tunayoishi, ile roho ya mpinga-kristo inatenda kazi, na inatenda kazi ndani ya kanisa lakini ni wachache tu ndio wanaweza kuliona ni kwasababu Biblia inasema ni wenye hekima tu, ndio watakaojua, na Hekima hii huja kwa kusoma, na kujifunza chini ya uongozo wa Roho Mtakatifu, Kumbuka hata jina la yule mnyama, inahitaji hekima kulijua, kwamba ukihesabu jina lake ndio ilete jumla ya 666. (VICARIVS FILII DEI).

Ufunuo 13:17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na AIHESABU HESABU YA MNYAMA HUYO; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.

Vivyo hivyo Bwana Yesu alisema katika Luka 12:54 Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.

55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?”

Hivyo ni vema kufahamu MAJIRA unayoishi, kwamba dalili zote zinaonyesha unyakuo umekaribia, kwamfano kulingana na biblia, yale makanisa 7 yanayozungumziwa katika ufunuo 2&3, sita kati ya hayo yameshapita na wajumbe wake wameshapita na sasa ndio tupo katika kanisa la saba na la mwisho liitwalo LAODIKIA na mjumbe wake alishapita, hili ndio kanisa la mwisho litakaloshuhudia kuja kwa pili kwa Kristo, lakini cha kusikitisha watu wengi hawalijui hilo kwasababu hawataki kusoma na kujifunza NENO la Mungu kwa undani.

Ishara nyingine inayoonyesha kuwa tunaishi katika kizazi ambacho kinaweza kushuhudia kuja kwa pili kwa Kristo ni kunyanyuka kwa taifa la Israeli, kumbuka kwa muda wa miaka zaidi ya 2000 taifa la Israeli lilikuwa limetawanyika kwenye mataifa mbalimbali duniani, lakini mwaka 1948 Mungu alilirejesha tena na kuwa taifa huru, na sasa hivi limetimiza miaka 70, na Bwana alisema kwa MTINI jifunzeni mfano mtakapoanza kuona unachipua tena, basi mjue wakati wa mavuno umekaribia,” Kumbuka Mtini unafananishwa na Taifa la Israeli (Yeremia 24)

Hivyo tukiona Israeli inachipuka tena basi tujue wakati wa Bwana Kurudi umekaribia..Lakini Bwana alizidi kusema ..Amin! Amin! nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia”. Kwahiyo kizazi kinachozungumziwa hapo ni kizazi kilichoshuhudia Taifa la Israeli kuchipuka tena, na ndio hichi kizazi tunachoishi mimi na wewe. Hizi ni baadhi tu ya ishara nyeti ambazo zinatuonyesha kuwa hatuna muda mwingi tena hapa duniani. Ukombozi wetu upo karibu.

Tukirejea katika kitabu cha Danieli tunafahamu hakuishia tu kusoma kitabu cha Yeremia bali hata vingine kwamfano kitabu cha Isaya, kilishatabiri mambo kama hayo hayo (Soma Isaya 13 & 14).

Hivyo baada ya kuyajua hayo ndipo Danieli akamgeukia Mungu wake kumwomba dua na kumsihi sana juu ya dhambi zake na za watu wake Israeli.

MAOMBI YA DANIELI:

Tunasoma..

Danieli 9:2-23 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.

4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;

5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;

6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.

7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.

8 Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi.

9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi;

10 wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.

11 Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi.

12 Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.

13 Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba Bwana, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake.

14 Basi Bwana ameyavizia mabaya hayo, akatuletea; maana Bwana, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake.

15 Na sasa, Ee Bwana Mungu wetu, uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia sifa, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu.

16 Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.

17 Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.

18 Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.

19 Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.

20 Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;

21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.

22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danielii, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.

23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya. “

Jambo la kujifunza hapo tunaweza kuuona unyenyekevu wa Danieli mbele za Mungu, ijapokuwa alikuwa ni mtu mkamilifu aliyependwa na Mungu lakini alijihesabia kuwa ni mwenye makosa pamoja na watu wake, alitubu kwa kufunga na kuugua, Vivyo hivyo na Bwana wetu YESU KRISTO, ingawa alikuwa ni mkamilifu hakutenda dhambi hata moja, lakini alitubu kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili yetu kwa kufunga na kuomba kwa dua nyingi pamoja na machozi.

Waebrania 5:7-10″ Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

8 na, ingawa ni MWANA, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;

9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. “

Lakini wengi wetu inapotokea Bwana ametupa kibali fulani mbele zake, ndio wakati wa kujiinua na kujiona bora kuliko wengine wote, pengine kwasababu Mungu amekupa karama fulani aidha ya uchungaji, au unabii, au uponyaji, au lugha, au maono, au miujiza ukaanza kujiona bora mbele za Mungu kuliko wengine, lakini kwa Danieli haikuwa hivyo, licha ya kwamba alikuwa na vipawa vyote hivyo, lakini alijinyenyekeza.

Vivyo hivyo tunamwona na Bwana wetu YESU KRISTO pamoja na kwamba alikuwa ni Mungu mwenyewe katika mwili lakini alijishusha kiasi cha kufikia kuosha miguu ya wavuvi(mitume). Kama wao walifanya hivyo inatupasaje sisi tunaojiita watu wa Mungu, .??

Tukiendelea kusoma tunaona Malaika Gabrieli alimjia Danieli kumtia moyo na kumpa vitu vingine vya ziada kuliko hata vile alivyokuwa anavitazamia, licha tu ya kuonyeshwa mambo yahusuyo kutoka Babeli alioonyeshwa pia mambo yatakayokuja kutokea mpaka mwisho wa Dunia kwa watu wake.

MAJUMA 70:

Tukisoma..

Danieli 9:23-27″ Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.

24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili KUKOMESHA MAKOSA, na KUISHILIZA DHAMBI, na KUFANYA UPATANISHO KWA AJILI YA UOVU, na KULETA HAKI YA MILELE, na KUTIA MUHURI MAONO NA UNABII, na KUMTIA MAFUTA YEYE ALIYE MTAKATIFU.

25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.

26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.

27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu. “

Kama tunavyosoma hapo kutakuwa na majuma 70 yaliyoamuriwa juu ya watu wake Danieli (Yaani wayahudi pekee). Kibiblia juma moja, linasimama kama miaka 7, hivyo majuma 70, ni sawasawa na miaka (7×70 = 490), Hivyo kutakuwa na miaka 490 kwa wayahudi mpaka mwisho wa mambo yote utakapofika(yaani mwisho wa dunia).

Tukisoma pia tunaona “tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu”. kutakuwa na majuma 7 na 62 ambayo ni sawasawa na majuma 69, Kumbuka miaka hii ilianza kuhesabiwa pale tu amri ya kuujenga upya Yerusalemu ilipotolewa, na jambo hili lilitimizwa na Mfalme Koreshi wa Uajemi, aliyetabiriwa na Bwana tangu zamani za nabii Isaya kwamba ataujenga upya Yerusalemu.

Tukisoma Isaya 44:26-28 ” nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, UTAKALIWA NA WATU, nayo miji ya YUDA, ITAJENGWA, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;

27 niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;

28 nimwambiaye KORESHI, MCHUNGAJI WANGU, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa. “

Pia ukisoma Isaya 45:1, 45:13, utaona jambo hilo, Kuwa Mungu alishamtabiri Koreshi amjengee nyumba kule Yerusalemu. Na amri ya kujenga tena Yerusalemu ilikuja kutoka mwaka 454 KK.

Hivyo ndani ya haya majuma 69 ya kwanza, yaani miaka 483 Jerusalemu ulijengwa tena na njia kuu zake na handaki zake katika nyakati za taabu kama biblia inavyosema.

Tukiendelea mstari wa 26 unasema “Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu(Danieli 9:26)”. Kwahiyo tunaona hapo mara baada ya yale majuma 69 kuisha (yaani 62+7) MASIHI atakatiliwa mbali. Jambo hili lilitimia mwaka 30WK, wakati Bwana YESU aliposulibiwa, hivyo kukamilisha miaka 483 tangu agizo kutolewa na Mfalme Koreshi kuujenga upya Yerusalemu.

Na kama tunavyoendelea kusoma “watu wa mkuu atakayekuja wataungamiza mji (Danieli 9:26)”. Huyu mkuu anayezungumziwa hapa ni Mpinga-kristo ambaye atakuja siku za mwisho, naye atatokea RUMI, kwasababu biblia inasema watu wake ndio watakaouteketeza mji, na hii ilitimia mwaka 70WK pale jeshi la Rumi lilipouzunguka mji wa Yerusalemu na kuuteketeza kwa moto ili kutimiza ule unabii wa Bwana Yesu aliousema juu ya mji wa Yerusalemu (ukisoma katika Luka 19:41-44).

Kwahiyo mpaka hapo litakuwa limesalia Juma moja yaani miaka 7 kutimiza yale majuma 70. Lakini ukitazama utaona wayahudi baada ya kumkataa MASIHI wao muda wao ulisimamishwa (Luka 13:34-35) na Mungu akaacha kushughulika nao, hivyo neema ikahamia kwa mataifa, na ndiyo iliyopo mpaka sasa hivi, takribani miaka zaidi ya 2000, lakini haitadumu huku siku zote, wakati utafika nao umeshakaribia na neema itarudi tena Isreali kwa muda mfupi kumalizia juma lao moja la mwisho yaani miaka 7, na kumbuka wakati wa mataifa utaisha pale tu kanisa litakaponyakuliwa.

(Warumi 11:25″ Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. )

Tukiendelea mstari wa 27 tunasoma..” Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu (Danieli 9:27).”

Sasa kumbuka huyu anayezungumziwa hapa ni mpinga-kristo (ambaye ndie yule mkuu wa watu atakayekuja), atafanya agano thabiti na watu wengi kwa juma moja, na katika nusu ya juma, yaani miaka mitatu na nusu ya kwanza atalivunja,

Hii itatokea baada ya unyakuo kupita pale mpinga-kristo (PAPA) atakapoingia agano la amani na wayahudi kwa muda wa juma moja wakati huo Hekalu la tatu YERUSALEMU litakuwa limeshajengwa na sadaka za kuteketezwa za daima zitakuwa zinaendelea, lakini katikati ya Juma hilo moja atalivunja hilo Agano, na kuzuia sadaka zote na dhabihu zisitolewe katika nyumba ya Mungu. Zaidi ya yote atataka yeye aabudiwe kama Mungu (2Wathesalonike 2:2), hilo ndilo chukizo la uharibifu. Na katika hiyo miaka mitatu na nusu ya mwisho atawaua watu wote watakaokataa kumsujudia yule mnyama au kupokea chapa yake katika kipindi kinachojulikana kama kipindi cha DHIKI KUU.

Kumbuka dhiki hii ilikusudiwa kwa wayahudi tu lakini na kwa watakaobaki (watu wa mataifa ) wasiokwenda kwenye unyakuo nao pia wataipitia. Lakini mwisho wake(mpinga-kristo) utafika ghafla, na makao yake yataharibiwa na kuangamizwa kabisa.

Kisha baada ya hapo utakuja utawala mpya wa miaka 1000 usio na uharibifu wa BWANA wetu YESU KRISTO, naye atatawala na watakatifu wake MILELE na MILELE.

Tukiyajua haya kuwa wakati tulionao ni mfupi tunapaswa kila siku tuufanye imara WITO WETU, NA UTEULE WETU (2Petro 1:10). Kwa maana ..1Wakoritho 6:9-10″ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.”

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 10

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


 

Mada Nyinginezo:

JUMA LA 70 LA DANIELI.

NGURUMO SABA.

MIHURI SABA

“WALA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI”..HAPO BWANA WETU YESU ANAMAANISHA NINI KUSEMA HIVYO?

BIDII YA MFALME YOSIA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 8

Jina la YESU KRISTO, BWANA wetu libarikiwe.

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli, Kama tulivyoona katika sura iliyotangulia Danieli akionyeshwa wale wanyama 4 waliotoka baharini, wa kwanza mwenye mfano wa simba, wa pili kama Dubu, watatu kama Chui na wanne alionekana kuwa mbali sana na wale wengine kwa muonekano wake ikiashiria utendaji wake ulikuwa ni wa tofauti, na tuliona wanyama wale waliwakilisha zile FALME 4 zitakazotawala mpaka mwisho wa Dunia, wa kwanza ukiwa ni Babeli, wapili, Umedi & uajemi, watatu Uyunani na wanne ambao ni wa mwisho ni RUMI.

Lakini tukiendelea na mlango huu wa 8, tunaona Danieli akionyeshwa maono mengine ya kipekee yanayohusiana na mambo yatakayokuja kutokea huko mbeleni kuhusiana na hizo falme kama Danieli 8:19 inavyosema..” Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa. “

Tusome.

Danieli 8:1-4″

1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya hayo yaliyonitokea hapo kwanza.

2 Nami naliona katika maono; ilitukia, nilipoona, nalikuwako huko Shushani ngomeni, katika wilaya ya Elamu; nikaona katika maono, nami nalikuwa karibu na mto Ulai.

3 Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.

4 Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.

Danieli katika maono haya alimwona kondoo mume mwenye pembe mbili, kumbuka ukiendelea mbele kwenye mstari wa 20 utaona tafsiri yake kuwa huyo kondoo anawakilisha ufalme wa UMEDI & UAJEMI,..

“Danieli 8:20 Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.

Na kama tunavyosoma hapo pembe moja ilikuwa ndefu kuliko nyingine na ndio iliyozuka mwishoni hii ikiwa na maana kuwa mfalme mmoja atakuwa na nguvu kuliko mwingine na huyu sio mwingine zaidi ya Koreshi mfalme wa UAJEMI ambaye tunaona alinyanyuka mwishoni baada ya Dario ambaye alikuwa ndugu yake mfalme wa Umedi kufa, Hivyo Ufalme wa Uajemi chini ya Koreshi uliimarika sana, mpaka ulipofikia wakati wa utawala wa Mfalme Ahasuero aliyemtwaa Esta kuwa malkia.

Na pia tunaona kondoo huyu akisukumu pande zote nne za nchi ikiashiria kuwa alifanikiwa kuteka sehemu kubwa ya dunia na mataifa makubwa, kuanzia India mpaka Ethiopia, jambo hili tunaweza tukalisoma katika kitabu cha Esta 1:1…” Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba; “

Alionekana pia akijitukuza nafsi yake, ni dhahiri kuwa milki kubwa aliyokuwa nayo ni rahisi kujinyanyua moyo hivyo pengine alifikiri kuwa hakuna taifa lolote lingeweza kumwangusha. lakini kama tunavyoendelea

Mstari wa 5-8″ unasema…

Danieli 8:5 Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, BEBERU akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.

6 Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake.

7 Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake.

8 Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.

Vivyo hivyo ukienda mbele kusoma mstari wa 21-22 utaona tafsiri ya yule beberu kuwa ni Ufalme wa UYUNANI, ambao ndio ulioungusha ufalme wa Umedi na Uajemi,…{“21 Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.22 Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake. (Danieli 8:21-22)”}

Kumbuka kama tulivyosoma katika milango iliyopita, ufalme wa tatu uliokuja kutawala dunia ulikuwa ni UYUNANI na ndio unawakilishwa na yule chui mwenye vichwa 4 katika Danieli sura ya 7,

Hivyo Danieli anaonyeshwa tena jambo lile lile katika ono tofauti lakini kwa undani zaidi, na Beberu huyu anaonekana akija akiwa na PEMBE MOJA MASHUHURI katikati ya macho yake naye akaenda kumvamia yule kondoo mwenye pembe mbili na kumwangamiza kabisa.

“Alexanda Mkuu” ndio ile pembe mashuhuri iliyozuka, Historia inasema mtu huyu alifanikiwa kuteka falme nyingi kwa kipindi cha muda mfupi sana, ndani ya miaka 12 alikuwa ameshaitiisha sehemu kubwa ya dunia kuanzia makedonia, India, hadi Misri na ilipofika 331 KK aliidondosha ngome ya Umedi na Uajemi (ndio yule kondoo) na kuiangamiza kabisa.

Na kama tunavyosoma mstari wa 8, tunaona ile pembe ilipokuwa na nguvu ilivunjika ghafla, na badala yake zikazuka pembe nyingine 4 mashuhuri. Historia inaonyesha Alexandra Mkuu, ambaye ndio ile pembe, alikufa ghafla na ugonjwa akiwa bado kijana wa miaka 31, Hivyo baada ya kufa hakuonekana wa kumrithi, hivyo wale majenerali wake 36 waliokuwa chini yake walianza kuupigania ufalme, hakuonekana aliyekuwa na nguvu kama za Alexanda hivyo mwishoni walikuja kuishia wanne tu, na kuugawanya ufalme katika pande nne sawasawa na biblia ilivyotabiri. Na majenerali hao walikuwa ni:

1)CassanderAlitawala pande za magharibi ambazo ni Makedonia na Ugiriki

2)LysimachusAlitawala pande za kaskazini ambazo ni Bulgaria na maeneo ya Asia ndogo

3)PtolemyAlitawala pande za kusini ambayo ni Misri

4)SeleucusAlitawala pande za Mashariki ambazo zilikuwa Israeli, Syria na mashariki yake.

Kumbuka hizi Pembe NNE ndio vile Vichwa vinne Danieli alivyoonyeshwa katika yule mnyama wa tatu, aliyefanana na CHUI katika Danieli sura ya 7.

Lakini tukiendelea kusoma kuanzia ule mstari wa 9 hadi wa 14 tunaona PEMBE nyingine NDOGO, ikizuka katikati ya moja ya zile pembe nne.

Tusome..

“Danieli 8:9 Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.

10 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.

11 Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.

12 Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.

13 Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?

14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. “

PEMBE NDOGO

Hii Pembe ndogo iliyozuka kati ya zile nne, historia inaonyesha ni mtawala aliyezuka katika ufalme wa Seleucus mmoja wa wale watawala wanne ambaye alikuwa wa mashariki, na tunaona ilizidi kujiimarisha mpaka kufikia NCHI YA UZURI (AMBAYO NI ISRAELI), Na mtawala huyu si mwingine zaidi ya ANTIOKIA IV, EPIFANE. Aliyetawala kuanzia 175-164 KK ..alijiita EPIFANE, akiwa na maana kuwa yeye ni “MUNGU ALIYEDHIHIRIKA”, huu ni mfano wa kile kile cheo cha mpinga-kristo atakayenyanyuka siku za mwisho. Kumbuka mambo yanayoandikwa, au yaliyotokea katika historia ni kivuli cha mambo yatakayokuja kutokea siku za mwisho.

Lakini tukisoma mstari wa 10 tunaona “Nayo ikakua{PEMBE}, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.

Kumbuka nyota za mbinguni zinafananishwa na makuhani wa Mungu, au viongozi wa watakatifu wa Mungu, ukisoma (Danieli 12:3., na ufunuo 2 & 3)utaona hilo jambo. Hivyo historia inaeleza huyu mtawala katili ANTIOKIA alishuka Yerusalemu na kuanza kuua wakuhani wa Mungu walokuwa wanahudumu katika nyumba ya Mungu na kuzuia watu wasitoe dhabihu katika nyumba ya Mungu( Hekaluni) na ndio maana ukisoma mstari wa 11 unasema ” Naam, ikajitukuza{hiyo pembe} hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, IKAMWONDOLEA SADAKA YA KUTEKETEZWA YA DAIMA, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini”.

Hivyo kuanzia huo wakati wayahudi wote walikatazwa kufanya ibada yoyote katika nyumba ya Mungu, badala yake Antiokia akawalazimisha wayahudi wafuate tamaduni za kipagani za kigiriki badala ya sheria ya Musa.

Alizidi hata kufikia hatua ya kuiba vyombo vya hekaluni na kutengeneza madhabahu ya mungu wake wa kipagani-ZEU ndani ya HEKALU la Mungu, Hilo ni chukizo kubwa sana kwa Mungu na kwa Wayahudi, aliendelea kwa kuchinja vitu haramu kama nguruwe na kunyunyiza damu juu ya madhabahu ndani ya hekalu la Mungu. Na wayahudi walipojaribu kwenda kinyume naye juu ya kulichafua hekalu la Mungu aliwaua wengi kikatili na wengine kuwauza utumwani, alikataza wayahudi kutahiriwa, yeyote atakayekiuka adhabu yake ilikuwa ni kifo, wayahudi walilazimishwa kula nyama za nguruwe na kutolea dhabihu miungu migeni ya kigiriki mambo ambayo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu. Lakini kumbuka haya yote yaliwapata wayahudi kwasababu ya MAKOSA YAO, kama mstari wa 12 unavyoeleza….”12 Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, KWASABABU YA MAKOSA; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. “

Wayahudi walimsahau Mungu na kuacha kuzishika sheria zake hivyo Mungu akaruhusu kiongozi mbaya na mkatili kama huyu anyanyuke dhidi yao. Lakini baadaye Mungu alikuja kumuhukumu na kufa ghafla.

Kumbuka Antiokia ni kivuli cha mpinga-kristo atakayekuja, biblia inasema atajiinua nafsi yake na kutaka kuabudiwa kama Mungu tunasoma.1Wathesalonike 2:3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU, AMA ; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. “

Na kama vile Antiokia aliwalazimisha wayahudi waikane imani yao na kuabudu miungu ya kipagani, vivyo hivyo na mpinga-kristo (PAPA) atawalazimisha watu wa ulimwengu mzima kupokea dini yake inayotambulishwa na ile chapa, na yeyote atakayepinga adhabu yake itakuwa ni kifo cha mateso kama ilivyokuwa kwa Antiokia kumbuka wakati hayo yanatokea kanisa litakuwa limeshanyakuliwa.

Tukiendelea mstari wa 13-14 inasema..

Danieli 8:13 “Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?

14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi ELFU MBILI NA MIA TATU (2300); ndipo patakatifu patakapotakaswa. “

Hizi siku 2300 ni sawa na miaka sita na theluthi moja hivi, ndipo uovu wote utaondolewa katika hekalu la Mungu, na Historia inaonyesha tangu kipindi Antiokia kuzuia sadaka za kuteketezwa mpaka siku ziliporejeshwa tena, ilikuwa ni siku 2300 kamili kama unabii ulivyotabiri.

Hii ilitokea pale baadhi ya wayahudi kutokuvumiliana na vitendo vya Antiokia na kuamua kuasi kwa kuingia vitani hivyo wakanyanyuka wana wa Matthatias mmoja wao akiwa YUDA MAKABAYO, na kwenda porini kumpinga Antiokia siku zote za utawala wake, walifanikiwa kumshinda na kuichukua tena YERUSALEMU na KULIWEKA TENA WAKFU Hekalu la Mungu baada ya kuchafuliwa kwa muda mrefu, hivyo wakatimiza unabii wa siku 2300 hii ilikuwa ni mwaka 164 KK. Siku hiyo wayahudi wakaanza tena kutoa sadaka za kuteketezwa, Na ndipo ile sikukuu ya KUTABARUKU ilianzia hapo {KUTABARUKU ni kuweka wakfu} (Yohana 10:22).

Kumbuka Danieli alionyeshwa mambo hayo kwa ajili ya SIKU ZA MWISHO, kwa sehemu yametimia kama KIVULI TU, lakini matukio halisi yenyewe yatakuja katika vizazi hivi vya siku za mwisho siku mpinga-kristo atakaposimama na kuwakosesha watu wengi.

Hivyo ndugu biblia inasema 2 Thesalonike 2:

7 Maana ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

Biblia inasema ni SIRI, hivyo inahitaji hekima kuigundua, utendaji kazi wake ni katika SIRI, na JINA lake pia lipo katika SIRI, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI! (Ufunuo 17:5). ni roho ile ile iliyokuwa kwa Antiokia, ndio ipo mpaka sasa hivi, IBADA ZA SANAMU katika nyumba ya Mungu(KANISA), pombe kanisani, uasherati kanisani, ushoga kanisani, vimini kanisani, burudani kanisani, sanaa & siasa kanisani, mizaha kanisani, biashara kanisani n.k. haya yote ni machukizo kama aliyofanya Antiokia na Belshaza juu ya nyumba ya Mungu. Ni roho ile ile.

2Wakoritho 6:15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16 Tena pana mapatano gani kati ya HEKALU LA MUNGU NA SANAMU? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, “

EPUKA ROHO YA UDHEHEBU NA DINI ZA UONGO MGEUKIE KRISTO AYASAFISHE MAISHA YAKO KWA NENO LAKE NA UZALIWE MARA YA PILI ILI UWE MTAKATIFU. Kwasababu biblia inasema pasipo huo UTAKATIFU hakuna mtu atakayemwona Mungu(Waebrania 12:14).

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 9

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.


Mada Nyinginezo:

UFUNUO: MLANGO WA 13

UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.

NGUVU YA UPOTEVU.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “HERI WALIOTASA, NA MATUMBO YASIYOZAA, NA MAZIWA YASIYONYONYESHA”?

MAFUMBO YA MUNGU.

JE! MTU ANAYETUNGISHA MIMBA KWENYE CHUPA MAHABARA, ANAHATIA MBELE ZA MUNGU?

KUJIPAMBA NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 7

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe.

Katika sura zilizotangulia (yaani ya 1-6), tuliona zikielezea sana sana historia za maisha ya watakatifu waliyopitia zaidi kuliko unabii lakini kuanzia Mlango huu wa 7 na kuendelea tunaona Danieli akionyeshwa maono ya mambo yatakayokuja kutokea katika siku za mwisho. Tukisoma..

Danieli 7:1-8″ Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.

2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.

3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.

4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.

5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.

6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.

7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.

Tukirejea kwenye ile sura ya pili tunaona jinsi Mfalme Nebudreza akionyeshwa katika ndoto Falme nne zitakazotawala dunia mpaka hapo ALIYE JUU(YESU KRISTO) atakapochukua Falme zote za dunia, hivyo Danieli alimpa tafsiri yake, Ufalme wa kwanza ukiwa ni Babeli, wa pili ukiwa ni Umedi na uajemi, wa tatu ukiwa ni ufalme wa uyunani na wa nne ni Rumi. Jambo hili hili tunaona linajirudia tena katika sura hii ya 7, Danieli akifunuliwa zile zile Falme 4 zitakazotawala ulimwengu wote mpaka mwisho wa dunia isipokuwa hapa anaonyeshwa kwa undani zaidi.

Hapa aliona wanyama 4, wakitoka baharini, kumbuka bahari inawakilisha mikusanyiko ya watu wengi(makutano){ufunuo 17:15, } hivyo hizi falme zitanyanyuka kutoka katikakati ya watu.Kumbuka wanyama hawa 4 Danieli aliowaona ndio yule yule mnyama Yohana alioonyeshwa akitoka Baharini mwenye vichwa 7 na pembe 10, wa kwenye Ufunuo 13 isipokuwa hawa wameunganishwa wote pamoja..

“ufunuo 13:1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa MFANO WA CHUI, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya DUBU, na kinywa chake kama kinywa cha SIMBA, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. “

Tutazame wanyama hawa.

MNYAMA WA KWANZA:

Kama tunavyosoma yule mnyama wa kwanza alionekana kama mfano wa SIMBA na akiwa na mabawa ya tai, kumbuka utawala wa kwanza Babeli ndio uliohusika kuwapeleka wana wa Israeli utumwani, ulifananishwa na simba ukisoma Yeremia 4:5-6 inaelezea kuwa watu walioichukua Israeli mateka na kuwapeleka Babeli walifananishwa na kama simba aangamizaye mataifa. Na pia kama anavyoonekana na mabawa ya tai hii inaashiria uharaka wake katika kuteka, kitu kinachopaa siku zote kina kasi kuliko vinavyokwenda kwa miguu hivyo Babeli ulikuwa mwepesi wa kuteka.

Habakuki 1:6″ Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo {wakaldayo ni wa-babeli}, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.”

7 Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.

8 Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; HURUKA KAMA TAI AFANYAYE HARAKA ALE. “

Kwahiyo tunaona hapo yule mnyama wa kwanza ni ufalme wa Babeli ambao ulikuja kuanguka baadaye na kunyanyuka mwingine wenye nguvu kushinda huo.

MNYAMA WA PILI:

Mnyama huyu anaonekana akifanana na Dubu, na pia anaonekana kama ameinuliwa upande mmoja ikiwa na maana kuwa anazo pande mbili na upande mmoja imezidi mwingine, na tunafahamu utawala huu si mwingine zaidi ya ufalme wa UMEDI na UAJEMI, na historia inaonyesha ufalme wa Uajemi ulikuwa na nguvu zaidi kuliko Umedi , hivyo zilipoungana zikaja kuundoa ufalme wa Babeli katika mamlaka yake na kuimiliki dunia upya, na pia yule Dubu anaonekana akiwa na MIFUPA MITATU ya mbavu kinywani mwake hizi ni ngome tatu walizoziangusha hawa wafalme wa Umedi na Uajemi, nazo ni Lidya, Misri na Babeli.

Ukisoma Isaya 13:15 ilishatabiri ukatili wake hata kabla ya utawala huo kunyanyuka.inasema ..

“15 Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.

 16 Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri.

17 Tazama, nitawaamsha WAAMEDI juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.

18 Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.

19 Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.”

ukizidi kusoma utaona huyu mnyama anaambiwa “ainuke ale nyama tele” ikiwa na maana kuwa atapewa uwezo wa kuteka mataifa mengi, na ndivyo ilivyokuja kuwa, katika historia inaonyesha Umedi na Uajemi uliteka na kutawala mataifa mengi Kuanzia India mpaka Ethiopia majimbo 127 (Esta 1:1) inaelezea vizuri.

MNYAMA WA TATU:

Mnyama huyu wa tatu Danieli alimwona akiwa mfano wa chui mwenye vichwa vinne, tukisoma..“6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Huu ni utawala wa UYUNANI (UGIRIKI) ambao ulikuja kunyanyuka baada ya mtawala wa Uyunani “Alexander the great” kuiangusha ngome ya Umedi na Uajemi, ni mtawala aliyekuwa na nguvu sana, kama chui alivyo mwepesi wa kushika mawindo yake, ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mtawala mdogo, kila alipokwenda kupigana na maadui zake alifanikiwa, kwa muda wa miaka 12 tu alikuwa tayari amekwishafanikiwa kuiteka dunia nzima. Lakini naye pia hakudumu sana katika utawala wake, alipokuwa na miaka 31 alipata ugonjwa na kufa, hivyo hakuacha mtu wa kumrithi baada yake, Hivyo ikasabisha wale majemedari waliokuwa chini yake kupigania ufalme lakini hakufanikiwa kutokea mwenye nguvu kama za Alexander hivyo ufalme ule ukagawanyika katika pande NNE, Ambavyo ndio vile vichwa vinne vya yule mnyama; Cassander, Lysimachus ,Ptolemy na Seleucus

MNYAMA WA NNE:

 Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

Mnyama huyu ni utawala wa RUMI, ndio ile miguu ya chuma kwenye yale maono aliyoyaona Mfalme Nebukadreza kwenye Danieli 2, na mnyama huyu hapa anaonekana akiwa na meno ya chuma, ikiashiria ana nguvu nyingi za kuharibu na kusagasaga, na pia hapa anaonekana na pembe 10, ambavyo ndio vile vidole 10 vya kwenye ile sanamu ya Nebukadreza. Kumbuka utawala huu ndio uliokuwa utawala katili kuliko yote iliyotangulia, na ndio unaotawala hata sasa katika roho,Lakini Katika historia, utawala wa Rumi ya magharibi ulikuja kugawanyika katika mataifa 10 yanayojitegemea AD 476, ambayo ni

1) Alemanni– kwa sasa ni Ujerumani

2) Franks – kwa sasa ni Ufaransa

3) Burgundians-Kwa sasa ni uswizi

4) Visigoths -Hispania

5) Lombards-Italia

6) Anglo-Saxons– Uingereza

7) Suevi- Ureno

8) Vandals -iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

9) Ostrogoths-ilingom’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

10) Heruli– iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

Lakini tukiendelea kusoma mstari wa 8 tunaona kuna PEMBE nyingine ndogo ikizuka

“Danieli 7:8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake PEMBE TATU katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.

Hivyo baada ya Danieli kuona haya alitamani kufahamu ile pembe ndogo maana yake ni nini??, Kama tunavyosoma Danieli 7:19 Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;

20 na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.

Kumbuka Pembe zinawakilisha ufalme au mfalme, Hivyo zile pembe 10 zinasimama kama wafalme wenye falme, vivyo hivyo na ile pembe ndogo ya 11 iliyoonekana kuzuka na kung’oa pembe nyingine tatu ni mfalme atakayenyanyuka na kuangusha wafalme wengine watatu. Historia inaonyesha mara baada ya utawala wa RUMI kugawanyika katika zile Falme 10, utawala wa KIPAPA ulizuka na kungusha tatu ya hizo ngome 10, pale zilipotaka kushindana na utawala wa PAPA aliziharibu kabisa na kuzishinda na hizo si nyingine zaidi ya Vandals, Ostrogoths na Heruli.

Na kama tunavyosoma pembe hiyo ilijitukuza sana na kunena maneno makuu ya makufuru, tunafahamu cheo pekee kinachosimama kama Mungu duniani ni cheo cha UPAPA, leo hii katika enzi yake yeye anasimama kama ” badala ya Kristo duniani”, anao uwezo wa kusamehe dhambi, anafahamika kama mtawala wa mbinguni, duniani, na chini ya nchi, N.K. hayo yote ni maneno ya makufuru mbele za Mungu. watu wanamtazama duniani yeye kama Mungu.

Lakini Mstari wa 21 unasema. ” Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; “ hakuishia tu katika kujitukuza lakini aliendelea hata kufanya vita na watakatifu Hili ni jambo limekuwa likijirudia katika historia tangu utawala wa KIPAPA chini ya Kanisa Katoliki uanze, wakristo wengi wamekuwa wakiuliwa kikatili pindi tu pale walipoonekana wanaenda kinyume na Dini hiyo. Wakristo zaidi ya milioni 68 waliuawa kikatili walipoonekana tu wanalishika Neno na kupinga mafundisho ya uongo ya kanisa hilo. Kumbuka wakatoliki sio wapinga-kristo isipokuwa ule mfumo wa lile kanisa na kile cheo anachokikalia kiongozi wa lile kanisa ndio cha MPINGA-KRISTO MWENYEWE.

Mstari wa 25 unasema Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI (Danieli 7:25)”. Hii inafunua siku mpinga-Kristo yule PAPA wa mwisho atakaposimama kutenda kazi.

Kumbuka hawa PAPA waliopo sasa hivi na waliopita wamekaa katika viti vya mpinga-kristo lakini yupo MMOJA atakayesimama na kubadilisha majira, na sheria, biblia inasema

( 1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba MPINGA KRISTO YUAJA , hata sasa WAPINGA KRISTO WENGI wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho).

Na siku sio nyingi atasimama atawale na kuitesa dunia kwa nyakati na nyakati mbili na nusu wakati, ambayo ni miaka mitatu na nusu, kwasababu kibiblia nyakati moja ni mwaka mmoja.

Hivyo hiyo itakuwa ni miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu,. labda anaweza akawa ndio huyu PAPA aliyepo sasa au mwingine muda utaeleza yote.. Huu ni wakati wa kujiweka tayari muda wowote mambo yanabadilika, Hauoni sasa hivi anavyozunguka kuleta DINI zote pamoja, akiwa kama mtu mwenye wafuasi wengi kuliko wote duniani. Kilio chake ni AMANI! AMANI! kwa kivuli hicho anatafuta ufalme ili baadaye aje kupambana na uzao wa Mungu.

Biblia inasema..1Wathesalonike 5:1-3″ Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.Wakati wasemapo, KUNA AMANI NA SALAMA, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. “

Ndugu wakati umeisha usidanganyike na watu wanaosema dunia haishi leo wala kesho, geuka weka mambo yako sawasawa yahusuyo wokovu.Huu ulimwengu unapita na mambo yake yote.

Mstari wa 9-10. unasema…” Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na VITABU VIKAFUNULIWA.

Hapa tunaona mwisho wa yote vitabu vitafunguliwa vihusuvyo maisha yetu, kila mtu na kitabu chake na utahukumiwa katika hicho, je! kitabu chako unakiandikaje? Biblia inasema sisi ni barua, na kila siku tunafungua kurasa mpya wa vitabu vyetu, na siku ile utakapokufa kitafungwa kikingojea kufunguliwa tena katika siku ile ya HUKUMU.

Hivyo tukiona mambo haya tunajua kabisa ule mwisho umekaribia UTAWALA USIOWEZA KUHARIBIKA wa mwokozi wetu ,hivi karibuni utakuja hapa ulimwenguni,.BWANA wetu YESU KRISTO MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA, atamiliki pamoja na watakatifu wake milele tunasoma..

Danieli 7:27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; UFALME WAKE NI UFALME WA MILELE, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

2Petro 1:10” Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

AMEN!

Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 8


Mada Nyinginezo:

UFUNUO: MLANGO WA 13

UFUNUO: MLANGO WA 17

JE! KUSHIRIKI AU KUJIHUSISHA KWENYE MICHEZO NI DHAMBI?

   WAPUNGA PEPO WANAOZUNGUMZIWA KWENYE BIBLIA NI WATU WA NAMNA GANI?

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 7

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe.

Katika sura zilizotangulia (yaani ya 1-6), tuliona zikielezea sana sana historia za maisha ya watakatifu waliyopitia zaidi kuliko unabii lakini kuanzia Mlango huu wa 7 na kuendelea tunaona Danieli akionyeshwa maono ya mambo yatakayokuja kutokea katika siku za mwisho. Tukisoma..

Danieli 7:1-8” Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.

2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.

3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.

4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.

5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.

6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.

7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.

Tukirejea kwenye ile sura ya pili tunaona jinsi Mfalme Nebudreza akionyeshwa katika ndoto Falme nne zitakazotawala dunia mpaka hapo ALIYE JUU(YESU KRISTO) atakapochukua Falme zote za dunia, hivyo Danieli alimpa tafsiri yake, Ufalme wa kwanza ukiwa ni Babeli, wa pili ukiwa ni Umedi na uajemi, wa tatu ukiwa ni ufalme wa uyunani na wa nne ni Rumi. Jambo hili hili tunaona linajirudia tena katika sura hii ya 7, Danieli akifunuliwa zile zile Falme 4 zitakazotawala ulimwengu wote mpaka mwisho wa dunia isipokuwa hapa anaonyeshwa kwa undani zaidi.

Hapa aliona wanyama 4, wakitoka baharini, kumbuka bahari inawakilisha mikusanyiko ya watu wengi(makutano){ufunuo 17:15, } hivyo hizi falme zitanyanyuka kutoka katikakati ya watu.Kumbuka wanyama hawa 4 Danieli aliowaona ndio yule yule mnyama Yohana alioonyeshwa akitoka Baharini mwenye vichwa 7 na pembe 10, wa kwenye Ufunuo 13 isipokuwa hawa wameunganishwa wote pamoja..

“ufunuo 13:1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa MFANO WA CHUI, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya DUBU, na kinywa chake kama kinywa cha SIMBA, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. “

Tutazame wanyama hawa.

 

MNYAMA WA KWANZA:

Kama tunavyosoma yule mnyama wa kwanza alionekana kama mfano wa SIMBA na akiwa na mabawa ya tai, kumbuka utawala wa kwanza Babeli ndio uliohusika kuwapeleka wana wa Israeli utumwani, ulifananishwa na simba ukisoma Yeremia 4:5-6 inaelezea kuwa watu walioichukua Israeli mateka na kuwapeleka Babeli walifananishwa na kama simba aangamizaye mataifa. Na pia kama anavyoonekana na mabawa ya tai hii inaashiria uharaka wake katika kuteka, kitu kinachopaa siku zote kina kasi kuliko vinavyokwenda kwa miguu hivyo Babeli ulikuwa mwepesi wa kuteka.

Habakuki 1:6″ Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo {wakaldayo ni wa-babeli}, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.”

7 Hao ni watu wa kutisha sana, wa kuogofya sana; hukumu yao na ukuu wao hutoka katika nafsi zao wenyewe.

8 Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; HURUKA KAMA TAI AFANYAYE HARAKA ALE. ”

Kwahiyo tunaona hapo yule mnyama wa kwanza ni ufalme wa Babeli ambao ulikuja kuanguka baadaye na kunyanyuka mwingine wenye nguvu kushinda huo.

MNYAMA WA PILI:

Mnyama huyu anaonekana akifanana na Dubu, na pia anaonekana kama ameinuliwa upande mmoja ikiwa na maana kuwa anazo pande mbili na upande mmoja imezidi mwingine, na tunafahamu utawala huu si mwingine zaidi ya ufalme wa UMEDI na UAJEMI, na historia inaonyesha ufalme wa Uajemi ulikuwa na nguvu zaidi kuliko Umedi , hivyo zilipoungana zikaja kuundoa ufalme wa Babeli katika mamlaka yake na kuimiliki dunia upya, na pia yule Dubu anaonekana akiwa na MIFUPA MITATU ya mbavu kinywani mwake hizi ni ngome tatu walizoziangusha hawa wafalme wa Umedi na Uajemi, nazo ni Lidya, Misri na Babeli.

Ukisoma Isaya 13:15 ilishatabiri ukatili wake hata kabla ya utawala huo kunyanyuka.inasema ..

“15 Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.

 16 Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri.

17 Tazama, nitawaamsha WAAMEDI juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu.

18 Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.

19 Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.”

ukizidi kusoma utaona huyu mnyama anaambiwa “ainuke ale nyama tele” ikiwa na maana kuwa atapewa uwezo wa kuteka mataifa mengi, na ndivyo ilivyokuja kuwa, katika historia inaonyesha Umedi na Uajemi uliteka na kutawala mataifa mengi Kuanzia India mpaka Ethiopia majimbo 127 (Esta 1:1) inaelezea vizuri.

MNYAMA WA TATU:

Mnyama huyu wa tatu Danieli alimwona akiwa mfano wa chui mwenye vichwa vinne, tukisoma..”6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

Huu ni utawala wa UYUNANI (UGIRIKI) ambao ulikuja kunyanyuka baada ya mtawala wa Uyunani “Alexander the great” kuiangusha ngome ya Umedi na Uajemi, ni mtawala aliyekuwa na nguvu sana, kama chui alivyo mwepesi wa kushika mawindo yake, ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mtawala mdogo, kila alipokwenda kupigana na maadui zake alifanikiwa, kwa muda wa miaka 12 tu alikuwa tayari amekwishafanikiwa kuiteka dunia nzima. Lakini naye pia hakudumu sana katika utawala wake, alipokuwa na miaka 31 alipata ugonjwa na kufa, hivyo hakuacha mtu wa kumrithi baada yake, Hivyo ikasabisha wale majemedari waliokuwa chini yake kupigania ufalme lakini hakufanikiwa kutokea mwenye nguvu kama za Alexander hivyo ufalme ule ukagawanyika katika pande NNE, Ambavyo ndio vile vichwa vinne vya yule mnyama; Cassander, Lysimachus ,Ptolemy na Seleucus

 

 

MNYAMA WA NNE:

“7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

Mnyama huyu ni utawala wa RUMI, ndio ile miguu ya chuma kwenye yale maono aliyoyaona Mfalme Nebukadreza kwenye Danieli 2, na mnyama huyu hapa anaonekana akiwa na meno ya chuma, ikiashiria ana nguvu nyingi za kuharibu na kusagasaga, na pia hapa anaonekana na pembe 10, ambavyo ndio vile vidole 10 vya kwenye ile sanamu ya Nebukadreza. Kumbuka utawala huu ndio uliokuwa utawala katili kuliko yote iliyotangulia, na ndio unaotawala hata sasa katika roho,Lakini Katika historia, utawala wa Rumi ya magharibi ulikuja kugawanyika katika mataifa 10 yanayojitegemea AD 476, ambayo ni

1) Alemanni– kwa sasa ni Ujerumani

2) Franks – kwa sasa ni Ufaransa

3) Burgundians-Kwa sasa ni uswizi

4) Visigoths -Hispania

5) Lombards-Italia

6) Anglo-Saxons– Uingereza

7) Suevi- Ureno

8) Vandals -iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

9) Ostrogoths-ilingom’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

10) Heruli– iling’ofolewa na ile pembe ndogo iliyozuka

Lakini tukiendelea kusoma mstari wa 8 tunaona kuna PEMBE nyingine ndogo ikizuka

“8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake PEMBE TATU katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.

Hivyo baada ya Danieli kuona haya alitamani kufahamu ile pembe ndogo maana yake ni nini??, Kama tunavyosoma Danieli 7:19 Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;

20 na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake.

Kumbuka Pembe zinawakilisha ufalme au mfalme, Hivyo zile pembe 10 zinasimama kama wafalme wenye falme, vivyo hivyo na ile pembe ndogo ya 11 iliyoonekana kuzuka na kung’oa pembe nyingine tatu ni mfalme atakayenyanyuka na kuangusha wafalme wengine watatu. Historia inaonyesha mara baada ya utawala wa RUMI kugawanyika katika zile Falme 10, utawala wa KIPAPA ulizuka na kungusha tatu ya hizo ngome 10, pale zilipotaka kushindana na utawala wa PAPA aliziharibu kabisa na kuzishinda na hizo si nyingine zaidi ya Vandals, Ostrogoths na Heruli.

Na kama tunavyosoma pembe hiyo ilijitukuza sana na kunena maneno makuu ya makufuru, tunafahamu cheo pekee kinachosimama kama Mungu duniani ni cheo cha UPAPA, leo hii katika enzi yake yeye anasimama kama ” badala ya Kristo duniani”, anao uwezo wa kusamehe dhambi, anafahamika kama mtawala wa mbinguni, duniani, na chini ya nchi, N.K. hayo yote ni maneno ya makufuru mbele za Mungu. watu wanamtazama duniani yeye kama Mungu.

Lakini Mstari wa 21 unasema. ” Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; “ hakuishia tu katika kujitukuza lakini aliendelea hata kufanya vita na watakatifu Hili ni jambo limekuwa likijirudia katika historia tangu utawala wa KIPAPA chini ya Kanisa Katoliki uanze, wakristo wengi wamekuwa wakiuliwa kikatili pindi tu pale walipoonekana wanaenda kinyume na Dini hiyo. Wakristo zaidi ya milioni 68 waliuawa kikatili walipoonekana tu wanalishika Neno na kupinga mafundisho ya uongo ya kanisa hilo. Kumbuka wakatoliki sio wapinga-kristo isipokuwa ule mfumo wa lile kanisa na kile cheo anachokikalia kiongozi wa lile kanisa ndio cha MPINGA-KRISTO MWENYEWE.

Mstari wa 25 unasema ” Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa WAKATI, NA NYAKATI MBILI, NA NUSU WAKATI. Hii inafunua siku mpinga-Kristo yule PAPA wa mwisho atakaposimama kutenda kazi.

Kumbuka hawa PAPA waliopo sasa hivi na waliopita wamekaa katika viti vya mpinga-kristo lakini yupo MMOJA atakayesimama na kubadilisha majira, na sheria, biblia inasema

( 1Yohana 2:18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba MPINGA KRISTO YUAJA , hata sasa WAPINGA KRISTO WENGI wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho).

Na siku sio nyingi atasimama atawale na kuitesa dunia kwa nyakati na nyakati mbili na nusu wakati, ambayo ni miaka mitatu na nusu, kwasababu kibiblia nyakati moja ni mwaka mmoja.

Hivyo hiyo itakuwa ni miaka mitatu na nusu ya dhiki kuu,. labda anaweza akawa ndio huyu PAPA aliyepo sasa au mwingine muda utaeleza yote.. Huu ni wakati wa kujiweka tayari muda wowote mambo yanabadilika, Hauoni sasa hivi anavyozunguka kuleta DINI zote pamoja, akiwa kama mtu mwenye wafuasi wengi kuliko wote duniani. Kilio chake ni AMANI! AMANI! kwa kivuli hicho anatafuta ufalme ili baadaye aje kupambana na uzao wa Mungu.

Biblia inasema..1Wathesalonike 5:1-3″ Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.Wakati wasemapo, KUNA AMANI NA SALAMA, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. “

 

Ndugu wakati umeisha usidanganyike na watu wanaosema dunia haishi leo wala kesho, geuka weka mambo yako sawasawa yahusuyo wokovu.Huu ulimwengu unapita na mambo yake yote.

Mstari wa 9-10. unasema…” Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na VITABU VIKAFUNULIWA.

Hapa tunaona mwisho wa yote vitabu vitafunguliwa vihusuvyo maisha yetu, kila mtu na kitabu chake na utahukumiwa katika hicho, je! kitabu chako unakiandikaje? Biblia inasema sisi ni barua, na kila siku tunafungua kurasa mpya wa vitabu vyetu, na siku ile utakapokufa kitafungwa kikingojea kufunguliwa tena katika siku ile ya HUKUMU.

Hivyo tukiona mambo haya tunajua kabisa ule mwisho umekaribia UTAWALA USIOWEZA KUHARIBIKA wa mwokozi wetu ,hivi karibuni utakuja hapa ulimwenguni,.BWANA wetu YESU KRISTO MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA, atamiliki pamoja na watakatifu wake milele tunasoma..

27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; UFALME WAKE NI UFALME WA MILELE, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

2Petro 1:10” Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”

AMEN!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.

Print this post

DANIELI: Mlango wa 6

Jina KUU la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe.

Ndugu mpenzi karibu tujifunze Neno la Mungu na leo tukiwa katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli, kama Biblia inavyosema, katika 2 Timotheo 3:16″ Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa MAFUNDISHO, na kwa kuwaonya watu makosa yao, NA KWA KUWAONGOZA, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.”

Hivyo kila habari tunayoisoma katika biblia kwa namna moja au nyingine ina mafunzo tosha ya kutufanya sisi tuenende kiukamilifu katika safari yetu hapa duniani pasipo kukwazwa na majaribu ya aina yoyote ya shetani, na ndio maana maandiko yanasema ” Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (1Wakoritho 10:11) . Kwahiyo mambo yote waliyoyapitia watakatifu wa kale ni kwa ajili ya kutuonyesha sisi njia ya kupita tunapokumbwa na majaribu kama ya kwao.

Katika sura hii ya sita Danieli licha ya kwenda katika ukamilifu wake wote lakini bado tunaona akiingizwa katika majaribu mazito, kama tunavyoweza kusoma habari hii:

Danieli 6:1-18″

1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;

2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.

3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, TUSIPOIPATA KATIKA MAMBO YA SHERIA YA MUNGU WAKE.

6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.

7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.

8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.

9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.

10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

11 Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.

12 Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.

13 Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danieli, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.

14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.

15 Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.

16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.

17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.

18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.

Kama tukifuatilia habari hii tunaona Danieli alitumika kikamilifu katika kazi zote za uliwali pasipo dosari yoyote, alikuwa mwaminifu, hakuruhusu jambo lolote ovu limkoseshe katika kazi zake za uliwali siku zote za maisha yake, hakuwa anakula rushwa, wala kuwa na matumizi mabaya ya fedha za ufalme katika mamlaka aliyopewa, na ndio maana mfalme ilibidi atafute watu watatu waaminifu ambao wataweza kuzisimamia hizo hazina kubwa za fedha ili mfalme asipate hasara katika mahesabu yake na mmojawao alikuwa ni Danieli.

Lakini haikuwa hivyo kwa wale wakuu wenzake waliokuwa na Danieli, wao walikuwa wanatafuta faida zao wenyewe, mambo kama ufisadi, rushwa, na ubadhilifu wa fedha vilikuwa ni sehemu ya maisha yao, Hivyo mtu kama Danieli alikuwa ni kikwazo kikubwa kwao. Pengine walipojaribu kuhujumu fedha za nchi Danieli aliwakemea na kuwashitaki kuwa wanachokifanya sio sawa, Hivyo ikawapelekea kumchukia Danieli sana na kuanza kumuundia visa, kwasababu nuru na giza haviwezi kuchangamana.

Kumbuka huo ulikuwa ni mpango wa shetani ndani ya watu, alipoona kuwa Danieli ni mkamilifu na hawezi kuuacha ukamilifu wake, akaamua kubadilisha kinyago chake na kuja na mbinu mpya, isipokuwa hii ni katika IMANI YAKE. Na hapo ndipo vita vinapokuwa vikali, pale unapolazimika kuchukua maamuzi ya NDIO AU HAPANA juu ya IMANI yako.

Na ndio maana ukisoma pale kwenye ule mstari wa 5 “Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, TUSIPOIPATA KATIKA MAMBO YA SHERIA YA MUNGU WAKE”.(Danieli 6:5)

Kwahiyo wale wakuu tunaona waliunda SHERIA moja madhubuti ihusuyo IMANI katika DUNIA YOTE ili tu kumnasa mtu mmoja wapate kumuangamiza. Lakini Danieli alipoona kuwa ile amri imeshapitishwa hakuacha msimamo wake zaidi ya yote alifungua madirisha yake kuelekea YERUSALEMU na kuendelea kusali kutwa mara tatu kama ilivyokuwa desturi yake, alichukua uamuzi wa kukubali kufa kwa ajili ya imani yake, na walipomwona bado anashikilia uamuzi wake wakamtupa katika Tundu la Simba, lakini tunaona Bwana ni mwaminifu alikuja kumwokoa.

Vivyo hivyo mambo hayo waliyoyakuta akina Danieli na sisi pia yatatukuta kwa namna moja au nyingine, Kama hao walikuwa ni watoto wa Mungu waliopendwa wameyapitia hayo vivyo na sisi pia tutayapitia kama hayo. Kumbuka ikiwa wewe ni mkristo na unajiona umesimama katika imani yako, fahamu kuwa shetani anakuchunguza maisha yako kila siku, ni kweli unaweza ukawa hauli rushwa kazini kwako, au haufanyi uasherati, au haunywi pombe, au hauvai mavazi ya kikahaba au hauabudu sanamu au haukosi kwenda ibadani au kusali n.k. Hivyo vyote shetani anaviangalia na atakapokujaribu kwa ushawishi wa muda mrefu ili uache msimamo wako na kuona unazidi tu kuvishinda, atatafuta njia mbadala ambayo moja kwa moja itaathiri UHUSIANO wako wewe na Mungu, aidha ukiache uishi au uendelee nacho uangukie MATATIZO MAKUBWA.

Kwamfano umekuwa mwaminifu kwa bosi wako kazini kwa muda mrefu na anafahamu kuwa wewe ni mkristo, lakini hapa ghafla anakuletea ripoti ya kukulazimisha usaini mapatano ya rushwa, kumbuka yule ni bosi wako na ukimkatalia utafukuzwa kazi,mkumbuke Danieli,

Au wewe wewe desturi yako ni kujisitiri lakini ghafla sheria mpya inakuja ofisini ni lazima kuvaa suruali au vimini, na usipofanya hivyo ni kuhatarisha kazi yako, sasa hilo ni jaribu shetani anakuletea la kutumia nguvu ili umtendee Mungu wako dhambi kwamaana ameona kwa utaratibu huwezi, hivyo anakuja kwa nguvu.

Au pengine kiongozi/mwalimu wako anakulazimisha ufanye naye uasherati usipokubali anakufelisha mitihani, au anakuzushia mabaya yatakayokupelekea hata pengine kufungwa. Katika mazingira kama hayo mkumbuke Yusufu, Kimbia! ni heri upoteze kila kitu kuliko kuipoteza nafsi yako.

Au wewe ni mwombaji mzuri, unasoma Neno, unafunga lakini unashangaa ghafla mzazi anatoa sheria nyumbani hakuna kuomba muda mrefu tena, hakuna kufunga, au hakuna kusoma NENO, unalazimishwa kurudia ibada za sanamu ambazo hapo mwanzo ulishaziacha, na ukijaribu kukataa tu, unatengwa na wazazi au unafukuzwa nyumbani. Usiogope kufukuzwa wala kutengwa hayo ni mapito ya muda tu! Bwana anakuwazia yaliyo mema.

Fahamu tu yatakapokutokea hayo yote usione kama Mungu amekuacha, wewe mkumbuke Danieli, mkumbuke Yusufu, mkumbuke Shedraka, Meshaki na Abednego, mkumbuke na Ayubu, mkumbuke Mordekai, hawa wote baada ya kuonekana wamesimama katika imani yao, shetani aliwaletea SHERIA ZA MASHARTI YA NGUVU. aidha ukubali kuabudu sanamu au ufe, aidha ukubali kuzini au uende gerezani, aidha ukuendelee kumtumikia Mungu wako kwa dua na sala au uishie kwenye matundu ya simba na moto. Lakini kumbuka mwisho wao hawa wote ulikuwa ni wa faraja, badala ya kuangamia kabisa walinyanyuliwa mara dufu. Hivyo usiogope yatakapokupata.

Na mambo hayo hayatamkuta kila mtu isipokuwa ni wale tu watoto wa Mungu waliosimama imara katika Imani ya YESU KRISTO, haya hayana budi kuja na ndio maana Bwana Yesu mwenyewe alisema.

Yohana 16:1-4 ” Maneno hayo nimewaambia, MSIJE MKACHUKIZWA.

2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.

3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi.

Unaona hapo, shetani hatoweza kuvumulia kumuona mtoto wa Mungu anadumu katika utakatifu wakati wote hivyo ni lazima ameletee majaribu yatakayohusu imani yake na wakati mwingine Mungu anaruhusu kama vile Ayubu kwasababu biblia inasema. Wafilipi1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; “

Na pia inasema kwenye 2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.”

Kumbuka pia jambo kama hili hili litajitokeza tena wakati wa kipindi cha dhiki kuu pale mpinga-kristo atakaponyanyuka na kuunda SHERIA MOJA YA SHARTI inayohusu IMANI, na shabaha yake itakuwa sio kila mtu aliye duniani bali ni kwa wale waliobaki (wasiokwenda kwenye unyakuo) wakristo vuguvugu wanawali-wapumbavu ambao watajaribu kutoshirikiana naye hao ndio watakaopitia dhiki kuu kwa kuteswa kwa mateso ambayo hayajawahi kuwako tangu ulimwengu kuumbwa. Na sheria itakuwa ni moja tu aidha uisujudie sanamu yake na kupokea chapa yake, ili uendelee kuisha au ukatae kuisujudia na kuteswa na kuuawa kikatili.

Kumbuka lile neno : Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (1Wakoritho 10:11) . Mambo ya kale ni kivuli cha mambo yanayokuja.

Hivyo ndugu kuna wakati unakuja mbeleni ulio mgumu sana, wa ulimwengu mzima kujaribiwa na yule mwovu shetani( katika dhiki kuu), Na huu ndio wakati wa kuziweka taa zetu sawa kwa kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu ili Bwana atuepushe na hiyo saa itakapofika (kwa kutunyakua). Kwasababu muda umeisha na wakati wowote Bwana anakuja kulichukua kanisa lake. NI WATAKATIFU TU! NDIO WATAKAOEPUKA HIYO DHIKI KAMA BWANA ALIVYOSEMA..

Ufunuo 3:10-11″ Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, UTOKE KATIKA SAA YA KUHARIBIWA ILIYO TAYARI KUUJILIA ULIMWENGU WOTE, KUWAJARIBU WAKAAO JUU YA NCHI. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”

Kama bado haujatubu ndugu, ni vema ukafanya hivyo leo angali muda upo.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 7


Mada Nyinginezo:

MPINGA-KRISTO

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO.

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.

NGURUMO SABA


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 5

DANIELI 5: KUANGUKA KWA BABELI:

Tukisoma katika Historia na kwenye biblia tunapata picha jinsi mji wa Babeli ulivyokuwa mkubwa, wenye maboma yenye nguvu, na ngome Imara iliyokuwa imezungukwa na kuta ndefu zenye njia katikati pande zote, mpaka kufikia wenyeji wa mji ule kusema kuwa ni “mji udumuo milele”,

Lakini tunaona wakati mmoja Mfalme wa Taifa hilo (BELSHAZA) alipokuwa amestarehe na kujifurahisha kwa anasa katika fahari yake tunaona uharibifu ulimkuta kwa ghafla, habari hii tunaisoma katika kitabu cha Danieli mlango wa 5, pale ambapo kiganja cha mkono kilipotokea na kusimama ukutani na kundika maneno yale magumu ambayo hakuna mchawi, wala mwenye hekima aliyeweza kuyasoma na kuyatafsiri maneno yale isipokuwa Danieli peke yake kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.

Danieli 5:1-8″ Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao.

2 Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile VYOMBO VYA DHAHABU NA FEDHA, ambavyo baba yake, Nebukadreza, ALIVITOA KATIKA HEKALU LILILOKUWAKO YERUSALEMU; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.

3 Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.

4 Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.

5 Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika.

6 Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.

7 Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.

8 Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake.”

Kama tunavyosoma hapo Mfalme Belshaza aliona haitoshi kujifurahisha katika anasa pamoja na masuria wake tu, lakini aliongezea kwenda kuchukua vyombo vya nyumba ya Mungu ambavyo baba yake (Nebukadreza) aliona vema kuvitunza visitumiwe kwa namna yoyote kwasababu viliwekwa wakfu kwa Bwana mpaka wana wa Israeli watarejea katika nchi yao, ni vyombo vilivyotumiwa na makuhani tu katika nyumba ya Mungu kwa ajili ya ibada. Lakini ijapokuwa Belshaza ALIYAFAHAMU HAYO YOTE, na kwamba vitu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa Israeli havipaswi kutumiwa kwa namna yoyote. Lakini kwa kiburi chake cha kufanya moyo wake kuwa mgumu kwa kutokujali na kumdharau Mungu, alikwenda kuvitumia kwa anasa zake, tukiendelea kusoma..

Danieli 5:9-31″

9 Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa.

10 Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.

11 Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;

12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danielii huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri.

13 Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?

14 Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako.

15 Basi sasa, watu wenye hekima na wachawi wameletwa mbele yangu, wapate kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake; lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri ya jambo hili.

16 Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.

17 Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.

18 Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;

19 na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.

20 Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.

21 Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.

22 Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote.

23 Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.

24 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.

25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE MENE TEKELI, NA PERESI.

26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.

30 Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, AKAUAWA.

31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.

Amen.

DANIELI: Mlango wa 5, mene, tekeli, peresi

Habari hiyo imejifafanua yenyewe, huo ndio ulikuwa mwisho wa Babeli, historia inasema usiku ule ule Danieli alipokuwa anawapa tafsiri ya maneno yale, kumbe jeshi la waamedi na waajemi lilikuwa limeshauzingira mji kwa mbali, hao hawakujua lolote kwasababu walishajitumainisha katika ulinzi wa kuta zao ndefu zinazouzunguka mji huku geti kubwa la kuingilia njia za miji ukiwa umefungwa,

Hivyo walijua hakuna namna yoyote taifa lolote lingeweza kuwavamia kwa njia yoyote ile, lakini hawakufahamu jambo moja, kwamba kwa Mungu hakuna lolote linaloshindikana, akisema mji huu utaanguka, ni kweli utaanguka! Hivyo Danieli alipomwambia maneno yale: “ufalme wako umeanguka na wamepewa waamedi na wajemi”, Mfalme alichukulia kama ni jambo ambalo ni gumu kutokea kwa wakati ule hivyo pengine ifikiria kichwani kwake kwamba kuta zake ndefu na majeshi yake imara yanayokesha usiku kucha kuulinda mji hayawezi kuvamiwa, na hakuna taifa lolote duniani lingeweza kupigana nalo , hivyo akastarehe tena na kutaka kumtukuza Danieli pasipo kujali maneno yale kwa kuanguka na kutubu saa ile ile.

Pia tazama..

1 Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
2 Jehanamu ni nini?
3 Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?.
4 Kabila la Benyamini.
5 Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
6 Moabu ni nchi gani kwasasa?
7 VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
8 Ashuru ni nchi gani kwa sasa?
9 Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
10 Umedi na uajemi, zilitawalaje?

Lakini hakujua maabaya yatakayomkuta muda mfupi baadaye, kulikuwa na mto mkubwa uliokuwa unaingiza maji katika mji ule, na tunafahamu siku zote hauwezi kuziba njia ya maji kupita, lazima kuachwe tundu kuruhusu maji kupita yaingie mjini, na ndivyo ilivyokuwa Babeli.

Palikuwa na mto mkubwa (FRATI) uliokatiza mji ule hivyo maadui zao walipokuja (Waamedi na waajemi) hawakupita kwa njia ya mageti au kubomoa kuta za miji, kwasababu kule zilikuwa zinalindwa na maaskari wengi waliomakini, Hivyo njia waliyoitumia waamedi na wajemi ni kwenda kukausha maji ya ule mto kwa kuyaundia mchipuko mwingine, hivyo yakaanza kupungua kidogo kidogo pasipo wao kujua, na mwisho kufikia kiwango cha watu kuweza kupita kwa miguu, jeshi kubwa la waamedi na wajemi liliweza kuingia kiurahisi kuuteka mji, na usiku ule ule Mfalme Belshaza aliuliwa bila kujua watu wameingilia wapi? na ufalme wake ukachukuliwa. Na Babeli kuishia hapo.

Wengi wanasema unabii wa Mungu huwa unachelewa kutimia, lakini si kweli ukichelewa ni kukufanya wewe utubu, kumbuka hapa tunaona mara tu baada ya Danieli kumtabiria Belshaza kuanguka kwake pengine alidhani ingekuwa kama ya Baba yake, kwamba yatatimia baada ya miezi au miaka kadhaa, lakini haikuwa hivyo kwake yeye ilitimia usiku ule ule.

Vivyo hivyo na BABELI ya rohoni (Utawala wa dini ya RUMI -UKATOLIKI ) iliyopo sasa, ambayo inapeleka mamilioni ya watu kuzimu, kama biblia inavyomwita katika

Ufunuo 17,“BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI”. NAYO PIA uharibifu wake utakuja ndani ya siku moja Biblia inasema 

Ufunuo 18:6-8″ Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.

7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

8 KWASABABU HIYO MAPIGO YAKE YATAKUJA KATIKA SIKU MOJA, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. ” AMEN.

Kumbuka pia jambo lingine lilolosababisha Mungu kuihukumu Babeli ni pale VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU vilipochanganywa na SANAMU na kusababisha CHUKIZO kubwa lililoleta UHARIBIFU, Vivyo hivyo pia katika Babeli ya rohoni itakuja pale yule mtawala wake yaani mpinga-kristo (PAPA wa wakati huo) atakapojiinua na kuingia katika hekalu la Mungu kule YERUSALEMU na kutaka kuabudiwa kama Mungu, litakuwa ni chukizo kubwa kwa Mungu ambalo litapelekea uharibifu wake moja kwa moja hilo ndilo CHUKIZO LA UHARIBIFU.

Habari zake zinazungumziwa hapa na mtume Paulo;

2 Wathesalonike 2:1-4″ Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,

2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa YULE MTU WA KUASI, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”

Vivyo hivyo kuutumia MWILI wako kwa uasherati, au fashion (vimini, suruali, hereni, wigy,) au ulevi, au wizi, au anasa, au rushwa,ulanguzi, NI SAWA NA KUVICHUKUA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU NA KWENDA KUVITUMIA KWA ANASA, haya yote ni machukizo yatakayokuletea uharibifu wa ghafla, Kwasababu Bwana alisema katika 1Wakoritho 6 kuwa “mwili ni kwa BWANA na BWANA ni kwa mwili na atakayeliharibu hekalu la hilo, Mungu atamuharibu mtu huyo.”

Au unapotumia Karama za Mungu kwa ajili ya faida zako mwenyewe, kwamfano unajiita mchungaji/nabii/mwinjilisti na bado ni unazini na washirika wako, au unatumia karama/vipawa hivyo kuwachukulia watu fedha,au kuwalaghai, huko ni SAWA NA KUVICHUKUA NA KUVITUMIA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU KWA ANASA, kama alivyofanya Belshaza hayo yote ni machukizo makubwa ambayo yatakupelekea kuanguka kwako haraka sana.

Hivyo ujumbe tulionao kwa kizaazi hiki cha mwisho ni huu:

2 Wakorintho 6:14 -18″ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16 TENA PANA MAPATANO GANI KATI YA HEKALU LA MUNGU NA SANAMU? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, MKATENGWE NAO, ASEMA BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

Ukisoma tena Ufunuo 18:4 inasema;

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Hivyo Jitenge na DINI za uongo, na pia jitenge na mienendo ya watu watendao dhambi.

Ubarikiwe na Bwana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Kwa mwendelezo >>> Mlango wa 6


Mada Nyinginezo:

MNARA WA BABELI.

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 4

Danieli 4:

JINA LA BWANA wetu YESU KRISTO, Mkuu wa milki zote za dunia lihimidiwe.

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli;

Sura hii inaelezea Maono Mfalme Nebukadreza aliyoyaona na kumpelekea kubadili fikra zake na kuwa mtu mkamilifu mbele za Mungu, aliandika barua hii..

Danieli 4:1 Mfalme Nebukadreza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.

2 Mimi nimeona vema kutangaza habari za ISHARA NA MAAJABU, aliyonitendea Mungu aliye juu.

3 Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.

Hapa tunaona Nebukadreza anaanza kwa kushuhudia ISHARA na MAAJABU Mungu aliyomtendea alipokuwa amestarehe katika ufalme wake, tunajua siku zote jambo fulani Baya Mungu akitaka kulileta kwa mtu/watu kabla ya kulileta jambo hilo huwa anatanguliza ishara kwanza kama onyo, na kazi ya ishara ni kumfanya mtu atubu, kwamfano tunaona wakati wa kipindi cha Yona,

Kabla ya Mungu kuiangamiza Ninawi ndani ya siku 40, Mungu alitangulia kuwapa ishara kwanza ya Yona kukaa ndani ya tumbo la samaki siku tatu, ili watakapoiona ishara kama hiyo watubu,na wasipotubu wataangamizwa, lakini tunaona walitii na kutubu na Mungu akaghahiri kuleta ubaya ule.

Vivyo hivyo na kwa Nebukadreza katika utawala wake Mungu alishatangulia kumpa ISHARA nyingi ili aache uovu wake lakini hakutubu, Kwamfano ile ndoto aliyoota ya kwanza “ya sanamu KUBWA” ilikuwa ni ishara kuwa ufalme wake siku moja utaangushwa, hivyo amgeukie Mungu lakini hakufanya hivyo, na Mwishoni pia Mungu alimpa ISHARA nyingine ya ndoto juu ya ule mti mrefu sana, uliokatwa na kuachwa kisiki tu, ambao ulimuhusu yeye moja kwa moja ili atubu aache maovu yake lakini hakutubu..Na ndio maana hapa tunaona anashuhudia na kusema ISHARA ZAKE NI KUBWA KAMA NINI!!.

Pia tazama..

1 Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
2 Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
3 DANIELI: Mlango wa 1
4 Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)
5 Unyenyekevu ni nini?
6 Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? (Danieli 10:12)
7 Kwanini awe Ayubu, Nuhu na Danieli tu?
8 Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
9 Je suruali ni vazi la kiume tu?
10 Tabia zitakazomtambulisha mpinga-Kristo ajaye

Licha ya Ishara alionyeshwa pia na maajabu, ambayo ni miujiza mfano wa ya akina Shedraka, Meshaki na Abednego ya kukaa katika moto mkali pasipo kuteketea, mambo ambayo hakuwahi kuyaona hata kwa wachawi wake aliokuwa nao Babeli na ndio maana alisema anaona vizuri kuandika maajabu Mungu aliyomtendea, yenye UWEZA MKUBWA.

Vivyo hivyo hata kwa mtu yeyote kabla ya Mungu kufanya jambo huwa anatanguliza kwanza ISHARA NA MAAJABU kama ONYO kumfanya mtu huyo atubu, lakini asipotubu mambo mabaya yatamkuta kama yalivyomkuta Mfalme Nebukadreza. Na kizazi tunachoishi sasa hivi kilishapewa ISHARA kama ya NINAWI ili kitubu na ishara hiyo si nyingine zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe Ukisoma..

Mathayo 12:38-42″ Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.

39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ISHARA YA NABII YONA.

40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.

41 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao WALITUBU kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

42 Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. “

Na MAAJABU pia Mungu anatutenda, tunayaona kila siku katika maisha yetu, wafu wanafufuliwa, viwete wanatembea, vipofu wanaona, watu wanaponywa magonjwa yao, wenye UKIMWI, Cancer, magonjwa yasiyotibika yote yanapona, n.k. Hivi vyote Mungu anavifanya ili watu watubu na kumgeukia yeye, lakini wengi wanakimbilia kwa Mungu ili watendewe miujiza tu na sio kwa ajili ya TOBA, Lakini Bwana alisema…

Mathayo 11:20 -24 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu HAIKUTUBU.

21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.

22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama MIUJIZA iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.

24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. “

Kwahiyo dhumuni KUBWA la Mungu Kuruhusu ishara na maajabu sio kututimizia mahitaji yetu pekee, bali ni KUTUONYA na kutufanya TUTUBU, ili tusije tukaangukia hukumu, jiulize, Mungu amekufanyia Ishara na Maajabu mara ngapi katika maisha yako? na Je! yalikufanya wewe utubu na kuacha dhambi au umkaribie Mungu zaidi? Kama sivyo jitathimini tena.

Tukirejea kwenye ule mstari wa nne tunaona Nebukadreza aliendelea na kusema:

Danieli 4:4-17″

4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi.

5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.

6 Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.

7 Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake.

8 Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,

9 Ee Belteshaza, mkuu wa waganga, kwa sababu ninajua ya kuwa roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako, na ya kuwa hapana neno la siri likushindalo, niambie njozi za ndoto yangu niliyoiona, na tafsiri yake.

10 Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana.

11 Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia.

12 Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.

13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, “MLINZI”, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni.

14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake.

15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;

16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.

17 Hukumu hii imekuja kwa AGIZO LA WALINZI, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge. “

Baada ya Mfalme Nebukadreza kumsimulia Danieli ndoto hii, ndipo tunasoma Danieli mkuu wa waganga alimpa tafsiri yake na kumwambia ule mti mkubwa wenye nguvu ambao wanyama wote wa kondeni walipata uvuli chini yake, unamwakilisha yeye, na kwamba ulionekana umekatwa kwa agizo la WALINZI, ikiwa na maana kuwa ataondolewa katika enzi yake ya kifalme, naye atakaa mwituni na kula majani kama ng’ombe mpaka nyakati saba zitakapotimia ( yaani miaka 7), hadi hapo atakapofahamu kuwa aliye juu ndiye anayetawala falme zote za dunia.

Lakini tunaona pamoja na kupewa ISHARA hii na Danieli kumshauri ATUBU aache njia zake mbaya kwa kuwahurumia MASKINI, Hakutubu aliendelea kuwa na kiburi, kuwanyanyasa maskini na kutokuwa na huruma kwa watu, mpaka kiwango cha maovu yake kilipofikia kilele, tunasoma baada ya miezi 12 jambo hilo lilimtokea kama lilivyo.

Danieli 4:28-30″

28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.

29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.

30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?

31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.

32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.

33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.

AGIZO LA WALINZI:

Kama tunavyosoma habari hii kuwa kulikuwa na WALINZI mbinguni waliokuwa wanatazama mienendo yote Ufalme wa Nebukadreza, mema yake yote na mabaya yake yote aliyoyafanya, Kumbuka Hawa ni MALAIKA WATAKATIFU walioko mbinguni, wanaotazama kila cheo, nafasi au mamlaka mtu aliyonayo, je! anavitumiaje?. Kama mtu anatenda mema Mungu kwa mkono wa hao walinzi anakulipa, lakini kama unatenda maovu au unaitumia vibaya nafasi yako uliyopewa, Mungu kwa mkono wa hao walinzi utapokea HUKUMU. Na mambo hayo ni hapa hapa duniani kabla ya hukumu kuu ya siku ya mwisho.

Kama wewe ni Raisi fahamu tu kuna WALINZI mbinguni wanakutazama kama vile wale waliokuwa wanamtazama Mfalme Nebukadreza, kama wewe ni waziri,mbunge, mkuu wa mkoa, balozi, diwani, m/kijiji, mjumbe, n.k. fahamu tu wapo walinzi juu wanakutazama mienendo yako kama je unaenenda katika haki au la!..Kama wewe ni mchungaji, mwinjilisti, Nabii, mwalimu, shemasi, mwimba kwaya, mfanya usafi kanisani, mwandishi, n.k. fahamu tu wapo walinzi mbinguni wanakutazama kama je! unasimama katika njia ya haki au la!, Kama wewe ni baba, au mama, au mlezi au boss, jua tu kuna walinzi watakatifu mbinguni wakifuatilia nyendo zako kama kweli hao unaowalea unawatendea haki au la!….n.k.

Kwahiyo katika nafasi yoyote uliyopewa na Mungu ni muhimu kuendana nayo kwa umakini ukijua kuwa, hakuna mamlaka iliyojiweka yenyewe (Warumi 1:1 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana HAKUNA MAMLAKA ISIYOTOKA KWA MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.). Mfalme Nebukadreza alipuuzia hilo na kusahau kuwa anatazamwa juu na kwamba Bwana ndiye anayetoa mamlaka yote, matokeo yake thamani yake ikashushwa kuliko hata mnyama wa porini kwa muda wa miaka 7, lakini alipogundua kosa lake, alitubu na kuwa mnyenyekevu hivyo Mungu akamrehemu na kumrejeshea vyote na enzi kupita kiasi. Sasa huyu alifanyika kama mfano,neema hiyo inaweza isiwepo kwako, kama utatumia vibaya nafasi uliyopewa.

Ndipo Mfalme Nebukadreza alimalizia na kusema:

Danieli 4:34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;

35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?

36 Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.

37 Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.

Kwahiyo ndugu kumbuka ishara na maajabu(ndoto, Maono, mafanikio, uponyaji, kuepushwa na mabaya, kutendewa miujiza Mungu anayokuonyesha ni kukutaka ufikie toba, utubie uasherati wako, ulevi wako, sanamu zako, vimini vyako, makeup zako na usengenyaji wako n.k. Pia usisahau katika nafasi uliyopewa wapo walinzi juu wanakutazama.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Kwa Mwendelezo >>> MLANGO WA TANO:


Mada Nyinginezo:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 3

Danieli 3:

Jina la Bwana wetu na Mkuu wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli. Leo tukiutazama ule mlango wa tatu, Tunasoma baada ya Mfalme Nebukadreza kuota ile ndoto ya kwanza, inayohusu zile falme 4 zitakazotawala mpaka mwisho wa dunia,lakini hapa kwenye sura hii tunaona akitimiza maono yake kwa kunyanyua SANAMU kubwa ya dhahabu, na kulazimisha watu wa dunia yote waiabudu, Na mtu yeyote atayeonekana amekaidi adhabu yake ni kwenda kutupwa katika tanuru la Moto. Kama tunavyosoma.

Danieli 3:1-6″ Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.

2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.

3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.

4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,

5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.

6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.

Lakini pamoja na hayo walionekana watu baadhi waliokaidi amri ya mfalme nao ni Shedraka Meshaki na Abednego. watu hawa tunasoma walikuwa ni wacha Mungu tangu awali, tunaona walikataa kula vyakula najisi vya mfalme, na hapa pia wanakataa kuabudu sanamu ambayo ni kinyume na sheria ya Mungu aliyowapa, kwa mkono wa Musa kule jangwani ikisema..

Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Hivyo Mfalme aliposikia habari yao alighadhibika na kuwatupa katika tanuru la Moto, lakini tunaona Bwana aliwaokoa na ukali wa moto ule.

Kumbuka Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya, (wakolosai 2:17) yaliyotokea katika mwili agano la kale, yatakuja kutokea katika roho kwenye agano jipya, na ndio maana tunaona hapa inatajwa BABELI ya NJE, lakini tukisoma katika kitabu cha Ufunuo 17 &18 Tunaona inatajwa BABELI nyingine itakayokuja kunyanyuka nayo ni ya rohoni. Hivyo tabia inayojitokeza kwenye hiyo ya mwilini itafanana na hiyo ya rohoni.

Na kama Babeli ile ya kwanza ilivyounda sanamu na kulazimisha watu wa dunia nzima waiabudu na yeyote asiyeabudu atatupwa katika tanuru kali la moto vivyo hivyo na hii ya rohoni itaunda SANAMU yake na mtu yeyote atakayekaidi kuiabudu, adhabu yake itakuwa ni mateso ambayo biblia inasema hayajawahi kuwepo tangu dunia kuumbwa (DHIKI KUU)..Habari hii tunaweza kuisoma katika…

Ufunuo 13:15 Akapewa kutia pumzi katika ile SANAMU YA MNYAMA, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao WOTE WASIOISUJUDIA SANAMU YA MNYAMA WAUAWE.

16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao:

17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.

Kumbuka Mnyama huyu ni RUMI na dini yake ni KATOLIKI, ndio BABELI ya rohoni iliyopo sasa. Itafika kipindi itapata nguvu kwa kuunganisha DINI zote na Madhehebu yote ulimwenguni ili kuunda DINI moja (ambayo ndio SANAMU YA MNYAMA), ambayo pasipo hiyo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa, na yeyote atakayeonekana hana chapa(utambulisho) wake, adhabu yake itakuwa ni mateso makali na vifo. Kama vile amri ya Mfalme ilivyokuwa kali juu ya akina Shedraka mpaka moto ukachochewa mara saba, ndivyo mateso yao yatakavyokuwa makali kwa wale wote watakaokataa kusujudia ile SANAMU ya Mnyama au kupokea CHAPA YAKE.

Pia tazama..

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
DANIELI: Mlango wa 1
Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)
Unyenyekevu ni nini?
Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? (Danieli 10:12)
Kwanini awe Ayubu, Nuhu na Danieli tu?
Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
Je suruali ni vazi la kiume tu?
Tabia zitakazomtambulisha mpinga-Kristo ajaye

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa Historia utaona mateso waliopitia wayahudi wakati wa utawala wa kimabavu wa Adolf Hitler, jinsi wayahudi walivyouawa kikatili kwenye magereza maalumu (CONCENTRATION CAMPS), walivuliwa nguo uchi wa mnyama na kuingizwa katika matanuru ya Gesi, wengine walikuwa wanapasuliwa wazima kama kuku kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara mifupa na msuli inachomolewa pasipo ganzi na kuwekwa kwa mwingine,

wengine walitiliwa sumu machoni, wengine wanadondoshwa kwenye ndege maili nyingi kutoka hewani( zote hizi ni kwaajili ya utafiti wa kijeshi na kibaolojia), wengine wanafungiwa kwenye mashehena yenye kemikali kwa muda mrefu ili tu wafe taratibu kwa maumivu makali, wengine walikuwa wanaachwa kwenye barafu uchi, wengine wanafanyishwa kazi ngumu kwa muda mrefu bila chakula mpaka wafe, wengine wanaachwa na kiu kwa muda mrefu na kupewa maji ya chumvi tu kuchunguza kama mtu anaweza kuishi kwa maji ya chumvi kwa muda gani?, watoto wanafungwa na kugongwa nyundo kichwani kidogo kidogo kwa muda mrefu mpaka kufa, au ukichaa ili tu kuchunguzwa ni kwa muda gani mwanadamu anaweza akavumilia maumivu n.k. embu fikiria ni mateso ya aina gani hayo?, tazama picha hapo chini..

DANIELI: Mlango wa 3

Kumbuka Adolf Hitler aliwafanyia hivyo kwasababu tu ni wayahudi, kwasababu wao ni taifa teule la Mungu, na si vingine, sasa hayo yote ni kivuli cha yatakayokuja huko mbeleni, huo ni mfano mdogo sana, Biblia inasema kutakuwepo na dhiki ambayo haijawahi kutokea na wala haitakuja kutokea tena baada ya hapo, Hivyo hawa wa mwisho watakuja kuuliwa kwasababu wanashikilia ushuhuda wa Kristo kwa kukataa kuisujudia SANAMU ya yule mnyama na kupokea chapa yake.

Ni mambo ya kutisha yanakuja huko mbele usitamani uwepo, anza kuweka sawa mambo yako yahusuyo wokovu leo kabla wakati haujaisha.

Lakini jambo lingine tunaweza kulisoma katika hii habari, Ni kwamba DANIELI haonekani kuwepo wakati sanamu ile inasimamishwa na watu walipolazimishwa kuiabudu. je! hii inafunua nini??.

Kama vile tulivyoona agano la Kale ni kivuli cha Agano jipya. Danieli ni mfano wa BIBI-ARUSI wa Kristo aliyekwisha jiweka tayari na kwenda kwenye UNYAKUO. Na ndio maana hatumwoni Danieli miongoni mwa wakina Shedraka, Meshaki na Abednego,.

Hivyo kabla ya hii DHIKI KUU kuanza kuna kundi dogo sana(BIBI-ARUSI wa KRISTO) watakuwa wameshanyakuliwa kwenye utukufu , watu hawa ni wale waliokuwa wamejiweka tayari, kwa UTAKATIFU, na Kudumu katia NENO na UFUNUO wa Roho Mtakatifu, ni watu walioshi kama vile wapitaji duniani wanaomngojea Bwana wao, Hawaabudu sanamu, sio walevi, sio wavutaji sigara, sio waenda disco na wasikilizaji wa miziki ya dunia hii, wasengenyaji, sio wezi wala walarushwa, sio wazinzi, sio watukanaji, n.k.

Kumbuka ndugu huyu mnyama anafanya kazi ndani ya DINI YA KATOLIKI, na atakayeisimamisha SANAMU yake atakuwa ni mpinga-kristo(katika kiti cha UPAPA)..na sanamu yake itakuwa ni “Muungano wa dini zote na madhehebu yote duniani (Ekumene)” .Na sanamu hii ilishaanza kuundwa tangu miaka ya 1900. kilichobaki ni “KUSIMAMISHWA TU” ili watu waiabudu.Na hivi karibuni itasimamishwa, lakini kinachohuzunisha zaidi ni watu wameshaanza kuiabudu hata kama haijasimamishwa, na ndio maana Bwana anasema tokeni kwake enyi watu wangu..(Ufunuo 18:4) kwa ufahamu jinsi gani chapa ya mnyama itatenda kazi fungua hapa >> Chapa ya Mnyama

Unaweza ukaona ni jinsi gani siku zilivyokwisha, matunda ya nchi yamekwisha iva, Tunapoona vikundi vya kigaidi vinakirithiri, vikundi kama ISIS, Boko Haramu, Alshabaab, n.k. migogoro ya kidini kati ya taifa na taifa, Israeli na wapalestina, wabudha & waislamu, wakristo & waislamu n.k. yote haya yanazidi kumfungulia njia mpinga-kristo kuleta muafaka wa AMANI-FEKI, Juu ya masuala ya dini ambao wanasiasa wa dunia nzima wameshindwa kuyatatua. Kwa jinsi yanavyoendelea kuongezeka mpinga-kristo (PAPA wa wakati huo) atapewa nguvu na mataifa ya dunia yote, ndipo atakapoleta utaratibu mpya (NEW WORLD ORDER) ambao katika huo watu wote watalazimika kuufuata na mtu yeyote atakayekaidi, ni mateso yasiyoelezeka yatamkumba.

Hivyo NENO la Mungu linasema 

1Wakorintho 7:29 Lakini, ndugu, nasema hivi, MUDA UBAKIO SIO MWINGI; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;

30 na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu.

31 Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.

Tujiweka tayari kwasababu siku ya Bwana itakuja kama mwivi..

1Wathesalonike 5:1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, KUNA AMANI NA SALAMA, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi”. 

Uzidi kubarikiwa na BWANA YESU.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Kwa Mwendelezo >>> Mlango wa 4


Mada Nyinginezo:

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU.

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.

SIFA TATU ZA MUNGU.

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

DANIELI: Mlango wa 2

Kulikuwa na sababu kwanini Mungu aliinyanyua Babeli kuwa taifa lenye nguvu kuliko yote duniani na kutawala falme zote za dunia kwa wakati ule, hata kudhubutu kulichukua taifa teule la Mungu Israeli kulipeleka utumwani, pamoja na kuteketeza mji na Hekalu la Mungu..Aliruhusu kwasababu alitaka kuonyesha kuwa ijapokuwa ni mji uliokuwa umetukuka sana, lakini siku moja kwa wakati ulioamriwa mji huo utaanguka na kuwa makao ya mbuni, na hayawani wote wa mwituni usioweza kukalika na watu . Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia kwa BABELI YA ROHONI iliyopo leo ijapokuwa imetukuka sana, biblia inasema kwenye ufunuo 18 itaanguka na kuwa ukiwa na watu wote watauomboleza kwa kuanguka kwake.

Tunasoma miaka kadhaa kabla ya kuanguka kwake Mungu alishaanza kutoa maonyo kwa watawala wa Taifa hilo, na ndio maana tunaona ndoto zote na maono waliyoyaona yaliwafadhaisha sana, kwasababu walikuwa wanafahamu kwa namna moja au nyingine zinawahusu wao na utawala wao. Na kibaya zaidi ni kuona jinsi yale maono yalivyokuwa yanaishia.

Kama tunavyosoma katika sura hii ya pili Mfalme Nebukadneza aliota ndoto, ambayo ilimhuzunisha sana mpaka kufikia kwenda kuwaita waganga, na wachawi pamoja na watu wote wenye hekima waliokuwa Babeli wampe tafsiri ya ndoto ile, lakini hakuonekana hata mmoja ambaye angeweza kutoa tafsiri, waganga wote na wachawi walikiri kuwa hakuna awezaye kuingia katika vyumba vya ndani vya moyo wa mwanadamu isipokuwa Mungu peke yake. Na ni kweli ndivyo ilivyo shetani hana uwezo wa kuingia ndani ya mtu na kuyafahamu mawazo yake, ndio anaweza kutuma mawazo mabaya lakini hawezi kutambua fikra za mtu zikoje, mwenye uwezo huo ni Mungu tu,

Waebrania 4:12-13″ Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. “

Kwahiyo Mfalme alipoona hakuna mtu wa kumtafsiria ndoto yake, akakusudia kuwaangamiza waganga na wenye hekima wote wa Babeli lakini Mungu akamjalia Danieli na wenzake neema ya kufahamu tafsiri ya ile ndoto, na kuipeleka kwa mfalme. Tunasoma..

Danieli 2:26″ Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake.

27 Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;

28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;

29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.

30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.

31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.

32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;

33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.

34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.

37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;

38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.

39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.

40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.

41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.

42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.

43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.

45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.

46 Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danielii, akatoa amri wamtolee Danielii sadaka na uvumba.

47 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.

48 Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.

49 Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme.

Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.

Katika ndoto hii tunaona Danieli akifunuliwa na Mungu Falme 4 zitakazokuja kutawala mpaka mwisho wa dunia, Kumbuka hakutakuwa na falme nyingine zaidi ya hizo, na ule wa tano ambao ndio uleule wa nne isipokuwa umechanganyikana na udongo ndio utakuwa wa mwisho kabla ya lile jiwe lilolochongwa mlimani pasipo kazi ya mikono kuupiga na kuuharibu kabisa.

Kama Danieli alivyomtafsiria mfalme kwamba kile kichwa cha dhahabu kinamwakilisha yeye(yaani ufalme wake wa Babeli),ambao kulingana na Historia ulidumu kuanzia mwaka 605BC hadi mwaka 539BC, Hichi ni kipindi cha miaka 66 , na baada ya hapo ukaanguka kama kitabu cha Danieli sura ya tano kinavyoelezea pale Mfalme Belshaza alipokuwa anafanyia anasa vyombo vya hekalu la Mungu kukatokea kiganja na kutoa hukumu juu ya kuanguka kwa ufalme wake, tunasoma katika usiku huo huo ufalme wake ulianguka.

Kisha ukanyanyuka utawala mwingine baada yake, tukisoma katika biblia ulikuwa ni utawala wa (Umedi na Uajemi) ambao ndio unawakilishwa na kile kifua na mikono ya fedha, Huu ulianza kutawala pindi tu Babeli ilipoanguka kuanzia mwaka 539BC hadi 331 BC. Nao ulienda kwa kipindi cha miaka 208, Pia kumbuka mwanzoni mwa utawala huu ndio Taifa la Israeli lilipokea Uhuru wake ili kutimiza unabii wa miaka 70 ya kukaa kwake utamwani kama Yeremia alivyotabiri, na kurejea tena katika nchi yake, ili kuijenga nyumba ya Bwana aliyokuwa imeharibiwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli.

Agizo hilo la kurejea na kuijenga tena nyumba ya Mungu, liliasisiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi. Tunasoma..

Ezra 1:1 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,

2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;

3 Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.

4 Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. “

Lakini baadaye mwishoni historia inaonyesha ulikuja ukaanguka.

kisha baada ya huo ulikuja Utawala mwingine wa tatu chini ya Mfalme “Alexander the great” aliyekuwa mfalme mwenye nguvu, tunasoma katika historia na katika biblia ulikuwa ni utawala wa Uyunani ambao unawakilishwa na kile kiuno na shaba, Huu ulianza kutawala kuanzia mwaka 331 BC hadi 168 BC, Ni kipindi cha miaka 163,

Na baada ya huu ufalme wa Uyunani kuanguka ulinyanyuka utawala mwingine uliokuwa na nguvu kama za chuma, uliowakilishwa na ile miguu ya chuma, na huu haukuwa mwingine zaidi ya utawala wa RUMI ya kipagani.Utawala huu ulidumu tangu kipindi cha 168 BC hadi kipindi cha 476 AD, ni zaidi ya miaka 644 na huu ndio utawala uliomsulibisha Bwana Yesu, uliwaua watu wengi kikatili kwa kuwasulibisha misalabani, wengine kwa kuchomwa moto n.k. na ndio maana biblia inasema ulikuwa ni mgumu kama CHUMA.

Tukiendelea tunasoma utawala mwingine wa tano na wa mwisho ulifuatia ambao ni chuma kilichochanganyikana na udongo, huu ni utawala ule ule wa nne isipokuwa hapa unaonekana kama umechanganyikana na udongo, Hivyo ni ule ule wa Rumi lakini umechanganyikana ndio unaowakilishwa na zile nyayo na vidole vya miguu ..

JE! huu udongo uliochanganyikana na chuma ni nini?. 

Mstari wa 43 unasema..

43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

Kumbuka hapo kabla, Taifa la Rumi lilikuwa haliingiliani na Taifa la Mungu kiimani kwa kipindi chote lilipokuwa linatawala dunia kama chuma, wakati huo lilikuwa lipo kisiasa na kiuchumi zaidi, lakini lilikuja kubadilika baadaye na kubadili tasira yake kwa kupitia DINI ili kujiingiza katikati ya taifa la Mungu (wakristo na wayahudi) 

1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, TAIFA TAKATIFU, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, BALI SASA NI TAIFA LA MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Kumbuka hii ilikuwa ni agenda ya shetani alipoona mambo yamehamia Rohoni na yeye akahamia rohoni.

Kwahiyo ule UDONGO unawakilisha WATU WA MUNGU au TAIFA LA MUNGU, na ndio zile mbegu za wanadamu.

Hivyo taswira hii ya kujigeuza ilianza kujidhihisha wakati wa utawala wa Costantine, pale upagani wa kirumi ulipoingizwa rasmi katika Ukristo, hapo ndipo mafundisho ya kweli ya NENO la Mungu yalipoanza kuchanganywa na mafundisho ya kipagani ya kirumi ili tu kuwafanya watu wabebe taswira ya ufalme wa Rumi na wakati huo huo bado wabebe taswira ya Ufalme wa Mungu (Ukristo), Na ndio maana leo mtu akiulizwa wewe ni nani? atakuambia mimi ni MROMA, badala ya kuwa na utambulisho wa taifa lake la mbinguni (yaani kuitwa mkristo), atakuambia ndio mimi ni mkristo na pia ni Mroma, unaona hapo tayari ameshachanganyikana na ule ufalme wa chuma (ambao ndio Babeli ya rohoni ya sasa), na ndio wenye watu wengi duniani leo.

Kumbuka huu utawala ndio wa mwisho na hakutakuwa na mwingine baada ya huo (BABELI YA ROHONI) inayozungumziwa katika Ufunuo 17 & 18, Hivyo hii Rumi iliyochanganyikana na udongo ni UKATOLIKI. DINI hii imechukua desturi za Roma za kipagani ikazileta katikati ya watu wa Mungu, kwamfano ibada za sanamu ambazo Mungu alizikemea akilionya taifa lake lisifanye mambo kama hayo ni machukizo (Kutoka 20) lakini hili limeyaleta katikakati ya watu wa Mungu, ibada kama kusali rozari na kuomba kwa wafu, mafundisho ya kwenda toharani, kukataa uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuua karama za Roho na kuweka vyeo vya uongozi wa kibinadamu badala yake, n.k. Haya yote yalipenyezwa katika NENO la Mungu na kuleta mchanganyiko mkubwa sana katika Kanisa la Kristo.

Lakini mwisho wa lile ONO lilionekana JIWE likiwa limechongwa Mlimani na kushuka, tukisoma..

34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Na jiwe hili si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, yeye ndiye atakayebatilisha hizi falme zote mbovu kwa kuupiga ule ufalme wa mwisho kuleta utawala mpya Duniani ambao huo utadumu milele. Kwasababu yeye ni BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME. Haleluya!!..Na jiwe lile lilionekana likiwa milima mikubwa ikishiria kuwa Kristo atatawala duniani kote pamoja na wafalme wengi(wateule wake) milele na milele.

Mstari wa 44 unasema..

” Danieli 2:44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”

Hivyo ndugu kama tunavyosoma hakitasalia chochote katika ile sanamu?, na wewe je! upo kwenye ile sanamu kumbuka utawala wa shetani uliopo leo ndio ule wa tano uliojichanganyika yaani chuma na udongo(shetani ni mdanganyifu, haji kwako moja kwa moja,)..Udongo ni wewe unayejiita mkristo, na chuma ni ROMA, chini ya mwamvuli wa dini ya katoliki, je na wewe umejichanganya humo? kumbuka lile jiwe lilisaga saga chuma na udongo vyote kwa pamoja, hivyo kama na wewe umejichanganya naye utasagwasagwa kama yeye hakitasalia kitu.

Kumbuka yule mnyama anayezungumziwa kwenye Ufunuo 13 & 17 ni dola ya Rumi inayounda ile chapa ya mnyama, na yule mwanamke aliyeketi juu ya yule mnyama ni Kanisa Katoliki, na anafahamika kama mama wa makahaba, ikiwa na maana kuwa anao mabinti wenye tabia kama za kwake za kikahaba, na hawa mabinti si wengine zaidi ya madhehebu mengine yote yaliyoacha uongozi wa Roho wa mtakatifu na kufuata desturi zisizoendana na NENO LA MUNGU.

Na ndio maana NENO LA MUNGU linasema Ufunuo 18:4″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Kanisa tulilopo ni la mwisho linaloitwa LAODIKIA, na Bwana alilikemea kuwa ni kanisa vuguvugu (lililochanganyikana), na Bwana amesema atalitapika kama lisipotubu,

Ufunuo 3:14-20″14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “

Huu ni wakati wa kuwa bibi-arusi safi wa Bwana asiwe na mawaa, kwa kujitenga na mafundisho ya uongo pamoja na kuishi maisha matakatifu( waebrania 12:14″ Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;” ) ili BWANA atakapokuja tuwe tayari kwenda naye katika unyakuo.

Print this post