Je! mtu anayetungisha mimba kwenye chupa mahabara, anahatia mbele za Mungu?

Je! mtu anayetungisha mimba kwenye chupa mahabara, anahatia mbele za Mungu?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu nini maana ya watoto wa kwenye chupa…ikitokea mama anakuwa ana mayai lakini anapata shida kushika mimba huwa kuna uwezekano wa kuyatoa mayai yake kutoka kwenye uzazi na kuyaweka kwenye kifaa maalum kinachoitwa test tube au kwa kiswahili chupa, sasa wakishaliweka hilo yai la mwanamke mule huwa wanachukua mbegu za mwanamume na kuziweka kule kitaalamu ili kurahisisha lile yai kurutubishwa kirahisi…na baada ya lile yai kurutubishwa ndani ya ile chupa wanalichukua lile yai na kulirudisha kwenye tumbo la yule mama na kuendelea na hatua nyingine za ukuaji wa yule mtoto kwenye tumbo la mama yake…hiyo ndio maana ya mtoto wa kwenye chupa, sio kwamba yule mtoto anawekwa kwenye chupa maisha yake yote hapana….ni yai tu ndio linalorutubishiwa kule na kurudishwa mahali husika…

kwahiyo hakuna mazingira yoyote nje na tumbo la mama mtoto anaweza kukua..wanadamu hawajafikia huo uwezo. Tumbo la mama ndio sehemu pekee mtoto anaweza kukua mpaka kufikia hatua ya kuzaliwa.Sasa tukirudi kwenye swali je! ni dhambi yai kurutubishiwa kwenye chombo hicho maalumu nje na tumbo la mama??J

ibu ni kwamba Mungu anaangalia nia ya mtu kufanya vile ni ipi, wengi wanaofanya hivyo unakuta wana matatizo ya kutokushika mimba, kwahiyo njia rahisi wanayoshauriwa na madaktari ni kutumia hiyo njia, hivyo sio dhambi kwasababu nia yao ni kutafuta mtoto sio kuua mtoto. Na hatua hiyo ya kurutubisha yai kwenye chupa ni hatua ya awali kabisa hata mtoto hajaanza kutengenezwa. Ingekuwa kufanya hivyo ni dhambi basi pia kuzaa kwa operation ingekuwa ni dhambi kwasababu sio njia ya asili Mungu aliyoiumba kwa kuzalia watoto. Kwahiyo inategemea na sababu ya mtu kufanya hivyo ni nini?, kama mtu anafanya kwa nia nyingine tofauti na hiyo basi ni dhambi, Lakini ingekuwa ni vizuri zaidi kumtegemea Mungu kuliko madaktari yaani kumwamini Mungu kuliko kutafuta njia mbadala, lakini pia hatuna imani zinazofanana…wako wenye imani kuwa Mungu atawapa watoto pasipo njia hizo na wapo wasio na imani hiyo…Lakini mtu akitumia hiyo njia hafanyi dhambi endapo tu atakuwa na nia njema.


Warumi 14:5…”Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
Ukiwa na swali, lolote unaweza ukatutumia, kwa neema za Bwana tutakujibu na kukutumia kwa njia ile iliyo rahisi kwako (inbox, e-mail, au whatsapp)Weka jina lako, na swali lako”.

Ubarikiwe!


 

Mada Nyinginezo:

JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO,IKIWAMO MIPIRA?

JE! MUNGU ANAUPENDELEO KWA WANAUME ZAIDI YA WANAWAKE?

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Yes
Yes
11 months ago

Mbarikiwe

Andrew edwin
Andrew edwin
3 years ago

Mafundisho yako ni mazuri mnoo.Barikiwe sana