Title 2019

Je! Mbinguni Kutakuwa na kula na kunywa?.

JIBU: Biblia haijaeleza kwa mapana na marefu mambo yatakayokuwa yanaendelea mbinguni baada ya unyakuo kupita, na ndio maana mtume Paulo anasema katika 1Wakorintho 13:9 “Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;..”

Hivyo kuhusu kama watakatifu watakula au hawatakula na kunywa biblia haijatoa jibu la moja kwa moja lakini tunaweza kutazama baadhi ya mistari inaweza kutusaidia kupata picha fulani. Tukisoma:

Marko 14.23 “Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.

24 Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.

25 Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.

26 Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni”. 

Tunaona katika habari hiyo hapo, Yesu akiwaagiza mitume wake kwa habari ya kunywa katika ufalme wa mbinguni, Lakini pia tukimtazama Bwana baada ya kufufuka kwake alikuwa na mwili wa umilele wa utukufu usioweza kufa tena, wala kuugua, mwili ambao uliweza kufanya mambo makubwa zaidi yasiyoweza kufanywa na mwili wowote wa asili, ule mwili uliweza kupotea na kutokea mahali popote, uliweza kuchukua sura tofauti tofauti, uliweza kupaa, na mpaka sasa unaishi n.k. Na kumbuka pia biblia inatuambia “siku atakapodhihirishwa tutafanana naye (1Yohana 3:2)”..Sasa jambo ambalo utaliona pale alipowatokea mitume wake baada ya kufufuka kwake aliwaambia wampe chakula chochote ale.

Luka 24.41 “Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?

42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.43 Akakitwaa, akala mbele yao”. 

Hiyo inatupa picha kwa sehemu jinsi miili hii ya utukufu itakavyokuwa, haitakuwa na mipaka Fulani kwamba kwasababu ni ya umilele haitaweza kula wala kunywa. Ni kweli kabisa uzima wa hiyo miili hautakuwa tena katika vyakula, inaweza kuendelea kuishi bila ya njaa wala chakula wala kutegemea chochote kile,kwasababu asili yake ni ya kimbinguni lakini hiyo haimaanishi kuwa haitaweza kunywa wala kula. Pia kumbuka Adamu kwa asili kabla ya kuasi alikuwa mtu wa umilele, asiyeweza kufa, wala kuugua, wala kuzeeka, lakini pamoja na ukamilifu wake Mungu bado alimuumbia ndani yake kula na kunywa katika ile bustani ya Edeni. Hivyo tusubiri tuone, tukifika huko tutajua zaidi, kikubwa tu tunachopaswa kufanya sasahivi ni kujitahidi kuishi maisha ya ushindi yampendezayo Mungu ili siku ile itakapofika tusikose kuyaonja hayo mambo mazuri Mungu aliyotuandalia ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.

UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

SWALI: Maana unanipa utata je! Ni kwamba Nisiwabariki watu asubuhi?.


JIBU: Kumbuka Neno kubariki katika biblia ni Neno pana, licha tu ya kuwa na maana ya kutoa Baraka kwa mtu lakini pia linaweza kumaanisha kushukuru, kutukuza, kusifia, kusujudia, au kuhimidi..inategemea na mahali lilipotumika.   Kwamfano mstari kama huu

Zaburi 96:2 “Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku”

Haimaanishi tu tulibariki (kwa kulitakia mema jina lake), hapana bali pia linamaanisha litukuzeni, lihimidini jina lake takatifu.   Sasa tukirudi kwenye huo mstari hapo juu, Tunaweza kuona kuna mambo mawili ambayo yamesababisha Baraka za huyu mtu zibadilishwa na kuwa laana. Jambo la kwanza ni kitendo cha yeye kumbariki mwenzake kwa SAUTI KUU. Na jambo la pili ni kufanya hilo tukio ASUBUHI NA MAPEMA.

  Mpaka mtu amsifie mwenzake kwa sauti kuu, kumbuka sio sauti tu ya kawaida hapana bali kwa sauti KUU ni wazi kuwa mtu huyo lengo lake ni asikiwe au aonekane na watu kitu anachokifanya na siku zote sifa za namna hiyo huwa zinakuwa si za kweli bali ni za kinafki. Na ndio hapo zinageuzwa na kuwa laana, mfano wake ndio ule Bwana Yesu alioutoa katika..  

Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”

Unaona mtu huyu, kama angekuwa na nia kweli ya kubariki angemwombea yeye mwenyewe kwa siri au kwenda kuzungumza naye kawaida tu, na sio mpaka apige panda mbele.  

Pili kitendo cha mtu huyu kufanya hivyo asubuhi na mpema katika roho kuna maana kubwa sana. Sikuzote asubuhi na mapema ni wakati mtulivu ndio mwanzo wa siku, ambao mtu analazima kukatiza usingizi wake kwa ajili ya mambo ya muhimu sana. Na jambo la kwanza kabisa mtu akiamka asubuhi anachopaswa kufanya ni Kumbariki Mungu wake (kwa kumshukuru, kumwimbia na kumsifu). Ndege wakiamka asubuhi jambo la kwanza wanalolifanya ni kumsifu Mungu kwa sauti kuu ya shangwe, utawasikia kila mahali kwenye viota vyao kabla hata hawajaenda popote huko ndani wanamsifu Mungu.   Daudi aliamka ALFAJIRI na kumbariki Mungu kwa vinanda na vinubi kwa sauti Kuu sana.  

Zaburi 57:7 “Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti. Nitaimba, nitaimba zaburi, 8 Amka, utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, NITAAMKA ALFAJIRI. 9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. 10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. 11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako”.  

Halikadhalika Mungu aliwaamsha Manabii wake, asubuhi na mapema wawpeleke habari njema za wokovu kwa watu wake(Yeremia 44:4)

Unaona Alfajiri siku zote ni ya Mungu..Ukiamka na Bwana, basi siku yako yote itakuwa ni ya Baraka.   Lakini huyu anaamka asubuhi na mpema jambo la kwanza ni kumpa mwanadamu utukufu, tena kwa sauti kubwa kana kwamba yeye ndio aliyemfanya aamke asubuhi. Hivyo mbele za Mungu kwake inakuwa ni laana. Mambo kama hayo yanajirudia hata sasa hivi ikiwa utamka asubuhi jambo la kwanza ni kukimbila SMARTPHONE yako uangalie message zote jana zilizotumwa whatsapp na facebook. Jambo la kwanza ni kuchati na kupiga simu za biashara zako, jambo la kwanza ni kuamka na kuwatukuza wanadamu badala ya muumba wake, Jambo la kwanza ni kuongea na mpenzi wako ambaye hata si mke wako/mume wako.Basi fahamu kuwa hata siku yako nzima umeiharibu mwenyewe.

Mika 1: 1 “Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao”.  

Isaya 5:11 “Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!”.

Hivyo Ujumbe mkuu hapo tuopaswa kuufahamu ni kuwa kitendo cha kusumbukia kitu kingine asubuhi na mapema tena kwa sauti kubwa kabisa, basi hicho kitu ni wazi kabisa kimekuwa ni KINGA yako, na biblia imeweka wazi kuwa amelaaniwa mtu Yule amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake. (Yeremia 17:5).   Alfajiri ikiwa ni ya Bwana, basi yaliyosalia nayo yatabarikiwa.

Warumi 11:16 “Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika”

Ubarikiwe.

Print this post

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

SWALI: 2 Samweli1:17-18. Inasema: Daudi akamwomboleza Sauli,na Yonathani, mwanawe,…”(Kama ilivyoandikwa katika KITABU CHA YASHARI’).Hicho kitabu cha Yashari ni kipi?


JIBU: Kumbuka Biblia sio kitabu cha kinabii tu kutabiri mambo yajayo peke yake, hapana bali pia ni kitabu kilichorekodi historia ya mambo yaliyopita, Na hiyo yote ni ili kutufundisha na kutuonya sisi kwa mifano iliyo hai ambayo ilishawahi kutokea huko nyuma,tuamini na kugeuka,

Hivyo sikuzote ili historia iweze kukubalika kuwa ni kweli ipo wazi kuwa ni lazima iwe imetibitishwa kwa ushahidi zaidi ya mmoja,   Kwa mfano haiwezekani historia ya vita vya Kagera ijulikane na watanzania tu peke yao watu wengine duniani wasiifahamu, yaani tujitangaze duniani kote sisi tulipigana vita na Uganda, lakini hakuna taifa hata moja lililoona hilo na kuthibitisha habari hiyo, kwa namna moja au nyingine zinaweza zikawa ni habari za kuzusha tu, lakini kama jirani zetu wakenya walishuhudia ni kweli, waganda walishuhudia ni kweli tulipigana nao, na Waafrika wote waliokuwepo kipindi kile watashuhudia jinsi walivyoshirikiana na sisi katika vita vile, basi hiyo vita kwa asilimia zote itakuwa ni ya ukweli na ilishawahi kupiganwa na hata kwa vizazi 100 vijavyo havitaweza kukana kwa ushahidi huo.  

Vivyo hivyo biblia nayo, ilivyoandika habari, kwa kuwathibitishia watu kuwa hayo yote ni kweli ikiwa kama mtu atatokea hatoamini kilichoandikwa, basi vipo vitabu vingine ambavyo vimerekodi habari za matukio hayo hayo biblia iliyoyarekodi, na mojawapo ndio hichi kitabu cha YASHARI ambacho tunaona kimeandika maombolezo ya mashujaa na sehemu nyingine matendo makuu yaliyofanywa na mashujaa wa Israeli.   Sasa tafsiri ya hilo Neno Yashari “NI MTU MWEMA AU MTU MTU WA HAKI”, hili ni Neno la Kiyahudi, hivyo kitabu cha Yashari ni kitabu cha mtu mwema, au mtu wa haki, na kitabu hichi katika biblia hakijazungumziwa hapa tu tunakisoma pia katika kitabu cha Yoshua :

Yoshua 10:12 “Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo, Je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha YASHARI? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima”.


Unaona, vipo pia vitabu vingine vinatajwa mbali na hii biblia yetu, ukisoma Hesabu 21:14, utaona kimoja kinaitwa kitabu cha VITA VYA BWANA. Ukisoma pia (1Nyakati 29:29), Utaona kulikuwa na kitabu kinachojulikana kama KITABU CHA TAREHE CHA SAMWELI MWONAJI, kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Nathani nabii, na pia kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Gadi mwonaji; Pia kulikuwa na kitabu cha tarehe cha wafalme wa Yuda, ukisoma (1Wafalme 14:29), utaliona hilo:..

1Wafalme 14:29 “Na mambo yake Rehoboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?”

Unaona vyote hivyo vilinakili matukio ambayo biblia ilirekodi pia. Lakini sasa hiyo haimaanishi kuwa ni vitabu vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu kwamba vitumike kuwa mbadala wa Biblia hapana, Hivyo vipo kuithitisha kuwa Biblia ni kweli na sio biblia kuthibitisha kuwa vitabu hivyo ni kweli.   Halikadhalika leo hii, utasema mimi siiamini kuwa biblia ina habari za ukweli, wala siamini kama YESU alizaliwa na bikiria kwa uweza wa Roho Mtakatifu, wala siamini kama alipaa, hizo ni hadithi za kutunga tu, zilibuniwa tu na watu Fulani Rumi, lakini nataka nikuambie vipo vitabu vingi vya historia na vya kidini mbali na hiyo biblia unayoitilia mashaka na vyote vinathibitisha ujio wa kwanza wa Yesu Kristo kuwa ni yeye pekee ndiye aliyezaliwa na bikiria kadhalika vinathibitisha ujio wake wa pili duniani kuwa atakuja kuuhukumu ulimwengu wote. na mojawapo wa vitabu hivyo ni QURAN!..

Sasa sio kwamba Qurani ni kitabu cha kweli cha Mungu hapana, kina mambo mengi sana yasiyo ya ukweli, lakini ndani yake kibebea chembechembe ndogo za ukweli kwamba ni kweli alishawahi kutokea Mtu wa kipekee aliyezaliwa bila dhambi na kuishi duniani anayeitwa YESU, na huyo atarudi tena mara ya Pili.   JE! Mambo yote Yesu aliyoyafanya tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake, na kurudi kwake hayakuandikwa katika kitabu cha waislamu Quran?. Ni uthitisho gani tena unahitaji?   Utakwenda wapi uukimbie uso wa Mungu, na ukweli uliopo katika Kristo Yesu?. Tubu leo YESU ndiye Njia kweli na uzima, NA YUPO MLANGONI KURUDI TENA, Hakuna tumaini nje ya yeye. Wala siku ile hakutakuwa na cha kujitetea.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?

VITABU VYA BIBLIA: SEHEMU YA 1

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)

SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?

WITO WA MUNGU

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! tunaruhusiwa kumuombea mtu ambaye haweki bayana kile anachohitaji kuombewa?

SWALI: Je! Kwetu SISI WATAKATIFU mtu akikuambia umuombee anaTATIZO halafu ukimuuliza ni tatizo gani asikuambie tatizo(Anasema hilo ni siri yake moyoni)-Huyo Tumuombee hilo tatizo lake la siri yake moyoni au?? Karibuni wapendwa..


JIBU: Kuna maombi ya kuombeana sisi kwa sisi ambayo hayahitaji mtu kumuhadithia mwingine ili amwombee, kwamfano kumwombea ndugu yako, Mungu amlinde na Yule mwovu, Mungu asimsahau katika ufalme wake, Mungu ampe kuokoa, Mungu ampe afya njema, Mungu amsaidie asimame katika imani asitetereke, Mungu ampe Amani na Upendo, mafanikio n.k..hayo ni maombi ambayo kila siku tunatakiwa tuyatamke kwa ndugu zetu wote wa mwilini na rohoni, Ndio jambo ambalo Mtume Paulo pia alikuwa analifanya:

Wakolosai 1:9 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, HATUACHI KUFANYA MAOMBI NA DUA KWA AJILI YENU, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;’’ 

Lakini yapo mahitaji mengine ambayo ni LAZIMA mtu AYANENE kwa faida yake mwenyewe, kama amedhamiria kuhitaji msaada kutoka kwa wengine. Kama mtu anayehitaji kuombewa tatizo Fulani linalomsumbua halafu haweki bayana hitaji hilo, nguvu ya kuombewa itatoka wapi, ni wazi kuwa anajizuilia Baraka zake yeye mwenyewe.

Biblia inaposema tuchukuliane mizigo, inamaanisha kuwa tusaidiane kwa kuitambua mizigo ya wenzetu, ukubwa wake, na uzito wake, ili mtu ajue ni jinsi gani kwa sehemu ya neema aliyopewa atamsaidia kuubeba, lakini kama mzigo kauficha mwenyewe ndani yake, wale wengine hata wakimwombea hawataomba ipasavyo, kwasababu hawatajua ukubwa au uzito wa tatizo lenyewe. 

Jaribu kufikiria labda mtu ana ugonjwa ambao unamsumbua kwa muda mrefu, halafu hataki kuwaambia watu wanaomwombea kuwa anaumwa yeye anasema niombeeni tu..wale watu kweli wataomba pamoja naye lakini hiyo itaishia pale pale, lakini kama mfano kama angeweka bayana kuwa anasumbuliwa na ugonjwa Fulani (akautaja jina) na ameshahangaika muda mrefu bila matumaini yoyote, sasa kwa kuzungumza tu vile tayari katika roho anauchukua ule mzigo wake na kuwapa wengine, ndio hapo inatokea wale wenzake wanaguswa sana na shida yake, huruma zinawajaa ndani, wanaamua hata kutenga muda wao kufunga na kuomba kwa ajili ya shida yake, wengine wanampa maneno ya faraja ya kimaandiko, wanakuwa karibu naye kila siku, wengine wanaguswa wanamsaidia katika mahitaji machache ya mwilini kama kuna ulazima, na mwisho wa siku Yule mtu uponyaji wake unamfikia kwa haraka zaidi kwasababu walikuwepo wengine kuuchukua mzigo pamoja naye..

 Hivyo ni lazima tujue kuwa kuna aina ya mahitaji ambayo mtu anaweza kukuombea bila hata ya kueleza siri ya moyo wako, lakini kuna mahitaji mengine kwa faida yako mwenyewe, unapaswa uwaambie ndugu wengine waaminifu, kumbuka pia sisemi kuwa kila jambo umweleze mtu, hapana, yapo mengine hayapaswi kuwekwa hadharani bali kwa watu uliowathibitisha kuwa ni waaminifu kwa Mungu. Kuna vitu vitu kama ukimwi, kesi za mauaji, n.k. hizo tafuta tu watumishi waaminifu wa Mungu, lakini vitu vingine kama magonjwa ya kawaida, ndoa, migongano, uzinzi n.k. Zungumza kwa ndugu wengine.

Lakini usikae na tatizo lako moyoni ikiwa unahitaji kweli kuombewa na wengine. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

KWANINI KUNA WATU WANAFANYIWA DELIVERANCE LAKINI BAADA YA MUDA WANARUDIWA TENA NA HALI ILE ILE?

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Samweli aliruhusuiwa kuhudumu hekaluni kama vile Walawi wakati yeye ni mu-Efraimu?

SWALI: Katika Biblia tunaona, ni Makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kuhudumu katika Hema ya Mungu, na ndio walioruhusiwa kuingia ndani ya nyumba ya Mungu,ambao walikuwa ni wa kabila la LAWI mwingine yeyote akiingia kule anakufa, lakini katika biblia hiyo hiyo tunamwona mtoto Samweli ambaye hakuwa Mlawi aliwekwa ndani ya ile hema mbele ya lile sanduku la agano, na hakufa na tunasoma Baba yake aliyeitwa ELKANA alikuwa anatokea katika kabila la EFRAIMU, ukisoma 1 Samweli 1 utaona jambo hilo. Hapo nahitaji ufafanuzi kidogo.


JIBU: Tukisoma

1Samweli 1:1 inasema

“ Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, MWEFRAIMU”.  

Ni kweli kabisa kwa sentensi hiyo inaonyesha dhahiri kuwa Baba yake Samweli alikuwa ni Mwefraimu, lakini ukijifunza maandiko kwa undani! Utagundua kuwa Elkana Baba yake Samweli hakuwa Mwefraimu bali alikuwa Mlawi. Kumbuka wakati wa agano la kale, Kipindi ambacho Yoshua anaigawanya nchi ya Kaanani kwa makabila yote ya Israeli, Kabila la LAWI halikuwa na urithi wowote, Mungu aliwaweka wawe wakfu kwake kwa ajili ya shughuli ya madhabahuni tu, hivyo walipovuka Yordani walitawanywa na kukaa katikati ya makabila yote kuwahudumia watu katika masuala ya Torati na Ibada,..

Hivyo walawi waliokuwa wanakaa Dani, waliitwa wanadani, walawi waliokuwa Rubeni waliitwa warubeni, vivyo hivyo walawi waliokuwa wanakaa Efraimu waliitwa waefraimu.

Kumbukumbu 18:1 “Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake.

2 Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia”  

Sasa kuthibitisha jambo hilo kuwa Samweli alikuwa ni mlawi, turudi katika kitabu cha Mambo ya Nyakati..Tusome.

1 Nyakati 6:33 “Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, MWANA WA SAMWELI;

34 MWANA WA ELKANA, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;

36 mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;

37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;

38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

39 Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;

41 mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;

42 mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;

43 mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;

45 mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;

46 mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;

47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, MWANA WA LAWI.

48 Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu”.  

Unaona hapo? Ukiufuatilia huo uzao wa Elkana baba yake Samweli utaona unakuja kuishia kwa LAWI. Kwahiyo ni wazi kuwa Baba yake Samweli, Elkana hakuwa Mwefraimu bali Mlawi..Mungu asingeweza kuruhusu mtu yeyote asiyekuwa mlawi kuhudumu katika nyumba yake au hema yake.   Kwahiyo Samweli alikuwa ni Mlawi, Mlawi mwenye asili ya Efraimu   Ni sawa na leo Mchaga aliyezaliwa Kenya aje kuishi Tanzania, moja kwa moja atajulikana kama ni Mkenya..kwasababu amezaliwa Kenya na si Tanzania, ingawa asili yake na kabila lake ni Tanzania.   Kwahiyo hiyo ndio sababu Elkana baba yake Samweli aliitwa Mwefraimu, ni kutokana na mahali alipotokea na sio kutokana na kabila lake.  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

YONA: MLANGO 1

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

CHAPA YA MNYAMA

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

PENTEKOSTE NI NINI?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia ituambia tusalimiane kwa busu takatifu. Hili busu ndio lipi?

SWALI: 1 Petro 5:14 Biblia inasema …“Salimianeni kwa BUSU LA UPENDO. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. ”….Hapo ana maana gani? Mfano Binti mtakatifu akikutana nami anibusu shavuni kisha anisalimu au Mimi nikionana na Mke wako barabarani kwa kuwa ni mtakatifu kama mimi nimbusu kisha nimsalimu SHALOM?..


JIBU: Ukisoma mstari huo kwa makini utaona biblia inasema ‘BUSU LA UPENDO’ Sehemu nyingine biblia inataja kama BUSU TAKATIFU..Unaweza kusoma hiyo katika Warumi..Warumi 16: 16 “Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.”.. Na Pia katika 1Wakorintho16:20 inasema: “Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.”…Na mistari mingine utakayoweza kukutana na hilo neno ni 2 Wakorintho 13:11, na 1 Wathesalonike 5: 24…Mistari yote hiyo inathibitisha kuwa kuna kitu kinaitwa Busu Takatifu. Sasa zamani kipindi cha Bwana wetu Yesu Kristo, na hata kabla ya hapo, kulikuwa na utaratibu wa kubusiana kama ishara ya salamu ya heshima kidogo, salamu ya kubusiana ndio ilikuwa salamu ya msingi kabisa kwa wakati huo, kama sasahivi ilivyo salamu ya kupeana mkono…kwahiyo watu walikuwa wakikutana walikuwa wanabusiana kwa nia ya kuonyesha upendo,shukrani, uthamani wa mtu n.k…Na kumbuka haikuwa busu la mdomo kwa mdomo hapana! Bali busu la mdomo kwa shavu au ubavu wa shavu. Na sasa tukirudi kwenye biblia inasema kuwa tusalimiane kwa BUSU TAKATIFU, ikiwa na maana kuwa sio Busu la mapenzi, wala sio busu la ubaya kama lile Yuda alilomsaliti nalo Bwana katika.. 

Mathayo 26: 48 “Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu”. 

Bali busu linalotajwa hapo ni BUSU LA HERI, NA BARAKA na UPENDO..Yaani mtu anambusu ndugu yake katika Kristo kwa nia ya kumtakia heri na Baraka kutoka kwa Mungu, kama mwamini. Lakini huo ulikuwa ni utamaduni wa zamani za wakati huo, ambapo Busu lilikuwa halina tafsiri nyingi tofauti tofauti kama ilivyo leo…Lakini leo hatuna utaratibu huo wa kubusiana..tuna utaratibu wa kupeana mikono…ambao huo unaweza kubeba maana kubwa zaidi au pengine hata sawa na kubusiana…Leo hii mwanamume akikutana na mwanamume mwenzake na kumbusu mbele za jamii haileti hiyo tafsiri Mtume Paulo aliyokuwa anaizungumzia hapo ya BUSU TAKATIFU, bali inaleta tafsiri nyingine…

Ingekuwa ni kwa kipindi cha wakati wake ingeweza kueleweka..Kwa wakati huu Busu takatifu linalokubalika katikati ya kanisa ni Busu kati ya dada na dada, au kati ya mzazi na mtoto na si kati ya kaka na dada ambao si ndugu, au kaka na kaka…Busu kati ya kaka na kaka inaleta tafsiri nyingine na maswali mengi,… 

Kwahiyo hapo ni muhimu kutofautisha tu salamu zinazotumika kulingana na nyakati..Mtume Paulo hakusema kuwa hilo ni agizo toka kwa Mungu, kwamba ni lazima kila tukutanapo tusalimiane kwa kubusiana..hapana! kwasababu salamu zinabadilika kulingana na nyakati…angekuwepo katika wakati huu ambao tunapeana mikono au kukumbatiana kama salamu badala ya kubusia, angeshauri tusalimiane kwa kupeana mikono ya Utakatifu, nk. Kwahiyo ukikutana na mwamini mwanamke, msalimie tu kwa kumpa mkono hiyo ni sawa na kumsalimia kwa busu takatifu haileti tofauti yoyote. 

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA MSTARI HUU: (MTU AMBARIKIYE MWENZAKE KWA SAUTI KUU ASUBUHI NA MAPEMA; ITAHESABIWA KUWA NI LAANA KWAKE.MITHALI 27:14 )?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

UZAO WA NYOKA.

FASHION! NI DHAMBI KWA BINTI ZA MUNGU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia inaposema kwamba “kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo lakini utauwa wafaa kwa mambo yote..inamaana gani”? (1Timotheo 4:8).

JIBU: Kama ukisoma vifungu vya juu katika hiyo habari utaona, ni kuwa kulikuwa na baadhi ya watu wanawashurutisha watu kwa kuwaambia kushika mambo ya mwilini ndio bora na kunafaa kwa uzima wa mtu, kwa mfano kuzingatia aina Fulani ya vyakula, kwamba usile kambale, au usile nguruwe, au ni lazima utahiriwe unapozaliwa, au ni lazima unawe mikono pale unapokula, au kutawadha, au ni lazima mtu afanye mazoezi ya mwili, au mtu ili awe mtakatifu ni lazima mtu asioe,… n.k…   Na huku wamesahau au wamepuuzia kabisa mambo ya muhimu ya rohoni yaani kumcha MUNGU na utakatifu wa roho zao….  

Na ndio hapa Paulo anamwambia Timotheo Ni kweli kwa namna moja au nyingine vinaweza vikampa mtu uzima wa mwili wake, na afya njema, hapa duniani lakini haviwezi kumpa uzima huko anapokwenda…Vitu kama hivyo haviwezi kumpa mtu daraja la moja kwa moja kwenda mbinguni, haviwezi kuzuia vitu kama tamaa za mwili n.k.

Wakolosai 2:20 “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21 Msishike, msionje, msiguse;

22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; LAKINI HAYAFAI KITU KWA KUZIZUIA TAMAA ZA MWILI”.  

Unaona?. Na ndio maana Paulo anamshauri Timotheo jambo jema la kuchagua…Nalo ni Utauwa, (Utakatifu), kuwa mtu wa rohoni, au kwa namna nyingine ni KUWA NA HOFU YA MUNGU ambalo hilo tu ndio linaweza kuyadhibiti mambo yote ya mwilini na rohoni….Ukiwa na hofu ya Mungu, ukimcha Mungu hata usipozingatia mlo kamili, bado Mungu atakulinda tu na kukupa afya, na bado juu yake utakuwa na ahadi ya uzima wa milele..Tofauti na Yule mtu anayezingatia lishe bora na huku maisha yake ya rohoni yapo chini, anaweza kweli akapata afya njema, na mwonekano mzurimkwa kitambo tu lakini siku akifa atakuwa wapi kama moyo wake ni mchafu..  

Unaweza ukawa umehangaika kujipatia mali ili uwe na maisha bora hapa duniani, ni kweli hapo ni sawa na umejipatia nguvu za mwilini, kwani mali ni ulinzi, zinaweza kukulinda kwa sehemu Fulani, lakini roho yako haiwezi kulindwa na mali…lakini ukiwa ni mtu wa rohoni, mtauwa, mtakatifu, unayemcha Mungu, unayeyajua maandiko, anayezijua ahadi za Mungu, analisimama imara katika Imani,..Mali ameahidiwa kuzipata halikadhalika uhakika kwa maisha ya milele upo. Sasa Kwanini na sisi tusichague fungu hilo?

1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.

Hivyo tusipoteze muda mwingi kwa vitu vya muda tu, bali tujishuhulishe zaidi na vile vitakavyotusaidia kwa mambo yote..Hiyo ni hesabu rahisi sana na inayoeleweka.

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

MIISHO YA ZAMANI.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! ni kweli kuna viumbe vinavyoishi sayari nyingine (ALIENS)?

SWALI: Bwana akubariki ndugu yangu wa thamani . Naomba kujua kwa namna Bwana alivyokujalia kujua juu ya hawa viumbe kutoka katika sayari ya Mars kama sikosei wanaiotwa ALIENS je ni kweli wapo ?au ni elimu ya dunia (sayansi ) inayoidanganya ulimwengu?.

JIBU: Ubarikiwe sana kwa swali zuri ndugu, Ukweli ni kwamba hakuna viumbe vingine vinavyoishi katika ulimwengu (Universe) zaidi ya wanadamu, Biblia haijasema kama kuna viumbe wengine tofauti na wanadamu na wanyama. Hadithi ya huu ulimwengu inamuhusu Mwanadamu na Muumba wake basii!! Inahusu ni jinsi gani Mungu alivyomuumba Mwanadamu na kumpa mamlaka juu ya vitu vyote chini yake, vilivyopo ulimwenguni…

Kwahiyo hakuna kiumbe kingine chochote kilicho na akili zaidi ya mwadamu kinachoishi ulimwenguni wa mbali, kumbuka tunapozungumzia ulimwengu hatuzungumzii tu dunia tunayoishi peke yake hapana bali tunazungumzia sayari zote na magimba yote yaliyopo angani, na kila mahali ambapo upeo wa mwanadamu unaweza kufika kote huko ni ulimwenguni, na hakuna kiumbe kingine chochote kinachoishi katika ulimwengu chenye kumzidi mwanadamu akili…

Zaburi 8: 3 “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;

8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.

9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!” 

Sasa utauliza kama hakuna viumbe wengine wenye akili kuliko mwanadamu wanaoishi huko angani na kwenye masayari mengine…ni nini basi viumbe hivi wanasayansi wanavyoviona na kuvipiga picha huko angani vinavyofanana na watu?.

 Ni ukweli usiopingika kwamba wana-sayansi kuna vitu wanaviona angani, na wakati mwingine wanafanikiwa kuvipiga picha, na wakati mwingine wanaona vinawapa ujumbe Fulani kwa ishara, na wakati mwingine vinatokea tu kwa mfano wa mwanga Fulani na kutoweka, na kuwabakisha katika maswali mengi. Na kwasababu Sayansi kwa sehemu kubwa haiamini kama kuna Mungu hivyo wana-sayansi hawa wanaishia kutafuta kujua ni nini hasa wanavyoviona au kuvipiga picha. 

Sasa hivi viumbe (Ambavyo wana-sayansi wanaviiita ALIENS) ni wakina nani?..Jibu la swali hilo tunaweza kulipata katika mstari ufuatao.

Ufunuo 12: 7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.

Kwahiyo viumbe hawa wanasayansi wanaoviona huko angani ni shetani na majeshi yake (mapepo).Na kwasababu shetani naye ana akili, kama biblia inasema ana uwezo wa kujigeuza na kuwa mfano wa malaika wa Nuru, hivyo anachokifanya yeye na malaika wake walioasi (yaani mapepo) ni kujigeuza na kujifanya kuwa ni viumbe wengine wenye akili sana wanaotokea sayari za mbali, na wanawatokea baadhi ya watu tu! Wale wenye kuamini mambo hayo, na lengo lake Shetani ni lile lile KUDANGANYA WANADAMU. Kuwatoa wanadamu katika kuamini kuwa kuna Mungu na kuwafanya waamini kuna viumbe wengine wanaoishi sayari za mbali wenye akili nyingi zinazowazidi wao…Hivyo wanaweza kuwatumainia wao kuwaletea msaada na utatuzi wa mambo yao ya kiteknolojia na kijamii…

Ni kama vile MASIHI wao wanamngojea. Kumbuka shetani ana vitengo vingi vya kuwapotosha wanadamu, anatumia uchawi kuwapotosha wale watu wanaoamini kuna uchawi, anatumia manabii wa uongo na waalimu wauongo kuwapotosha wale wanaokwenda kanisani wasioamini katika uchawi bali Mungu…na anatumia uongo wa Ma-ALLIENS Kuwadanganya wale watu wasioamini kuwa kuna Mungu, ili waendelee kuamini hivyo hivyo kuwa hakuna Mungu bali kuna viumbe wengine huko angani. Kazi yake ni kuwa akishagundua unapenda nini na upo wapi, anakutafutia upotoshaji katika hicho hicho kitu unachokipenda. 

Nimewahi kusoma ushuhuda mmoja, mwanamke mmoja ambaye alikuwa ndio amempa Kristo maisha yake ila hajasimama vizuri, anasema alikuwa anapenda sana kusoma habari za ma-Alliens, na moyoni mwake alikuwa ameshaanza kuamini na kushawishika kuwa kwa namna moja au nyingine ni lazima kutakuwepo na viumbe wengine tofauti na wanadamu wanaoishi mojawapo ya zile sayari kule juu, sasa wakati akiwa katika uchunguzi wake akitamani sana siku moja awaone..maana alisikia shuhuda nyingi mbali mbali kuwa watu wamewaona na wengine wametokewa…anasema siku moja wakati anaendesha gari lake usiku wakati yupo njiani anarejea nyumbani..ghafla mbele ya barabara mbali kidogo akaona kitu kama mwanga Fulani mzuri sana alivyozidi kutazama aliona kile kitu kikakaribia mpaka pale gari lake lilipo na akafunga breki anasema hicho kitu kilikuwa kama ndege Fulani mfano wa kisahani hivi (spaceship).

Na alipokiona ni kama kilikuwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, ambayo duniani kwasasa haipo. Na vile viumbe vilivyomo mule ndani hakuviona isipokuwa alisikia tu sauti ikizungumza na yeye ndani yake ikimwambia wao ni viumbe kutoka sayari ya mbali wamekuja kuusaidia ulimwengu..Huyo dada anasema ndani ya moyo wake akafurahi sana akahisi kama ndoto yake imetimia ya kuwaona Ma-Aliens…Lakini kipindi kifupi nyuma alisikia injili na kuamua kumfuata Bwana Yesu, lakini alikuwa mguu mmoja nje mwingine ndani..

Hivyo akajikuta tu anawauliza swali hao viumbe..akawauliza “huko mlipo mnamwabudu Yesu?”..havikujibu, alipozidi kuviuliza hilo swali ndipo vikamjibu na kumwambia “sisi hatumwabudu Yesu nyinyi wanadamu ndio mnaomwabudu, sisi sio wanadamu”..wakati anaendelea kuwauliza wao wanamwabudu nani hicho chombo chao kikaondoka mbele yake..Baadaye, anasema kutoka na mwanga ule aliouna ulianza kumletea shida kila alipokuwa anasoma biblia alikuwa anaona mwanga tu, haoni chochote, lakini siku alipokuja kuombewa na hizo roho kumtoka ndipo akaja kufahamu kuwa alichokiona sio ma Aliens kama alivyokuwa anafikiri bali ni mapepo yaliyojigeuza na kujifanya kuwa ni ma aliens. Kwahiyo kwa kuhitimisha, elimu ya ma-ALIENS ni elimu ya shetani kabisa, iliyotengenezwa kuzimu kwa lengo na nia ya kuwapoteza watu wasiamini kuhusu Mungu bali waamini utafiti wa kisayansi juu ya uwepo wa viumbe wengine zaidi ya wanadamu. Na jambo hili limewaathiri sana watu wa Ulaya, huku kwetu ndio nalo linaanza kukita mizizi. 

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

MIHURI SABA

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

HUDUMA YA UPATANISHO.

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO.

MVUTO WA TATU!


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Nabii Elisha alikuwa ana maana gani kulia na kusema”Gari la Israeli na wapanda farasi wake”?

SWALI: 2 Wafalme2:12; `Naye Elisha akaona,akalia,Baba yangu,baba yangu,GARI LA ISRAELI NA WAPANDA FARASI WAKE! Asimwone tena kabisa;’ ” Hapo anaposema “Gari la Israeli na wapanda farasi wake!-Anamaana gani?”


JIBU: Hilo ni swali la kujiuliza ni kwanini mwisho wa safari ya Eliya linatokea gari kutoka mbinguni na wapanda farasi wake, na si isiwe kitu kingine labda ngazi, au upepo au aishie kutoweka tu asionekane mpaka litokee gari la vita?, Hizi ishara zinazotokea mwisho za washindania Imani, zinakuwa na maana kubwa sana kwetu, ni sawa na Bwana wetu Yesu alivyoondoka tujiulize ni kwanini WINGU lilimpokea na si gari au malaika..lipo jambo Mungu anatuonyesha katika haya matukio.

 Lakini tukirudi kwenye tukio la Eliya, Kulitokea gari la Vita, Elisha ndio alivyoliona, hii kuonyesha kuwa Eliya alikuwa vitani Duniani anapigana, na sasa mwisho wa vita vyake umefika, Ushindi ameshaupa, vita kavipiga, mwendo kaumaliza, Umefika wakati wa kuondoka, Hivyo ni wajibu lile jeshi lililokuwa linapigana naye yeye kama Jemedari wao siku zote za maisha yake, lije kumchukua na kumpeleka nyumbani kwa vishindo vikuu vya ushindi. Vivyo hivyo hata leo kwa mtakatifu yoyote atakayemaliza kazi yake duniani kwa ushindi , siku ile anayokufa, katika Ulimwengu wa Roho lile Gari la Israeli [yaani Jeshi la ki-mbinguni] ambalo siku zote za maisha yake amekuwa akitembea nalo kupigana vita litamchukua moja kwa moja mpaka Paradiso kule watakatifu wengine walipo. Lakini hiyo ni mpaka mtu apigane na ashinde, asiposhinda hakuna atakayekuja kumchukua, huyo atabakia kaburini, Na ndio maana Mtume Paulo mwisho wa safari yake aliandika hivi: 

2Timotheo 4:6 “Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.

7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”. 

Hivyo na sisi pia tujitahidi tukaze mwendo, siku ile tuondoke na ushindi mnono duniani. Kwasababu yapo mema mazuri Mungu ametuandalia huko tuendako.

 Ubarikiwe.


ROHO YA ELIYA KATIKA AGANO JIPYA INATENDAJE KAZI?

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

SWALI : Pale Bwana Yesu aliposema “Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.(Mathayo 5:32)” Alimaanisha nini?.


JIBU: Neno usherati kama linavyoonekana kwenye kamusi, tafsiri yake ni “kufanya kitendo cha ngono na mtu ambaye bado haujaoana naye”..hii ikimaanisha kuwa inaweza ikawa mtu yupo ndani ya ndoa au nje ya ndoa, tofauti na Neno UZINZI, ambao huo unakuja pale mtu anapofanya kitendo cha ngono na mtu ambaye si mwanandoa mwenzake (yaani kitendo cha kutoka nje ya ndoa na kwenda kufanya ngono). Hivyo tunaweza kusema Neno Usherati ni Neno la ujumla likimaanisha kitendo chochote cha zinaa kinachofanywa na mtu isivyopaswa yaani nje ya ndoa halali. Kwahiyo Bwana Yesu aliposema pale katika Mathayo 5:32 na Mathayo 19:9, kwamba lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi;.. kitendo kile alikilenga hasa kwa wanandoa, kwasababu habari iliyokuwa inazungumziwa pale ni ya watu ambao wapo katika mahusiano ya mke na mume. 

Pia kwa kuongezea hapo, ukisoma sehemu nyingi katika maandiko kwenye agano la kale na jipya, utaona Mungu alilitumia hilo neno Uasherati, kumaanisha uzinzi ambao watu wake walikuwa wanafanya katika roho, soma 〈2 Nyakati 21:10-14,〉 〈Ezekieli 16:27, 43, 58,〉 Ezekieli 22:11, 〈Ufunuo 17:1-5, 19:2 〉n.k. vipo vifungu vingi sana na vyote hivyo vinautaja uzinzi kama uasherati, ambao watu wa Mungu wameufanya na sanamu na machukizo yao…Uasherati ni Neno la Ujumla, ukitaka kushikilia tu Uasherati katika biblia unamaanisha kitendo cha ngono nje ya ndoa takatifu, basi biblia itakuwa haina maana sehemu nyingi, ikiwemo katika hivyo vifungu nilivyovitoa hapo juu. 

Hivyo biblia inaposema Ndoa na iheshimiwe na watu wote, ilimaanisha kweli kweli. huwezi kuingia tu kwenye ndoa halafu ukajifanyia tu mambo unayotaka ukaamua kwenda kuzini ukijifariji kuwa hiyo ndoa tayari imeshafungwa haiwezi kuvunjika..Ndugu nataka nikuambie Inaweza kuvunjika kwa kitendo hicho na isiwe makosa mbele za Mungu kwenda kuoa/kuolewa na mwingine.

 Lakini ifahamikie pia hilo halikuwa agizo kwamba kila kitendo cha kukosa uaminifu katika ndoa iwe sababu ya mtu kumwacha mkewe na kwenda kuoa mwingine hapana.. Mungu hapendi kuachana biblia imesisitiza hilo, na zaidi ya yote tumefundishwa kusamehe, kwani hata na sisi tunamkosea Mungu kwa mengi. Hivyo kusamehe ni msingi mkubwa sana wa ndoa kusimama. Na zaidi ya yote ni uaminifu na kuwa na hofu kwa Mungu, tukijua kuwa ndiye Mungu aliyeiunganisha, tusigeuke kuwa VIFO katikati yetu. mwanandoa aliweke hilo kichwani kuwa akienda kuzini amestahili kuachwa kibiblia na kusiwe na hatia zozote mbele za Mungu. 

Shalom.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI

USIWE SABABU YA WATU KUMKUFURU MUNGU.

KITABU CHA UZIMA

MPINGA-KRISTO

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!


Rudi Nyumbani:

 

 

 

 

Print this post