Moja ya kazi kubwa PIA shetani anayoifanya ni kuhakikisha watu hawaelewi dhambi ni nini?…Na hivyo anatumia nguvu kubwa kuwafanya watu waamini kuwa chanzo cha matatizo yote ni yeye!…hata mtu akifanya uasherati ni shetani! Mtu akiua ni shetani! Mtu akiiba ni shetani!…Lakini wengi hawajui kuwa shetani naye pia hakudanganywa na mtu, hakukuwa na mtu juu yake wa kumdanganya…alijidanganya mwenyewe (moyo wake ulimpoteza mwenyewe Yeremia 17:9).
Sababu ya kutenda dhambi watu wengi ambao hawaelewi huwa wanamtupia shetani…lakini kumbe ni wao..Shetani, anachokifanya yeye ni kupalilia UOVU tu duniani…lakini yeye sio aliyeuumba uovu, Uovu upo katikati yetu uliumbwa na Mungu, kwa makusudi maalumu ya kutambua wema, kwamfano uovu usingekuwepo basi hata wema usingekuwepo, ili kutambua kitu hiki ni kitamu lazima kiwepo kichungu, lakini kama hakuna kichungu, umejuaje kuwa kile ni kitamu?. (Vivyo hivyo na sisi tumeumbiwa tayari mema na mabaya ni sisi kuchagua)…..Na malaika nao waliumbiwa hicho kitu ilikuwa ni kitendo tu cha wao kuchagua…Na shetani na malaika zake wakachagua mabaya (na huko ndiko kuasi), na matokeo yake wakatupwa duniani…
Na huku duniani tayari kulikuwa kuna mti wa mema na mabaya pale Edeni…Kiasi kwamba hata kama shetani asingekuwepo bado Hawa alikuwa anao uwezo wa kuchagua mabaya, kama angetaka……kwahiyo asili ya uovu sio shetani! Uovu ulikuwepo tangu asili, ni kitendo cha watu kuchagua..(pale Edeni shetani alikuwa ni kama dalali tu! Wa kumvutia na kumshawishi mwanadamu achague uovu). Kwahiyo shetani anachofanya sasahivi yeye na malaika zake ni kuipalilia tu ile njia ya ouvu izidi kuwa pana kwa watu….Ukilijua hilo litakufanya kuwa makini kutokufikiria kila kitu chanzo ni shetani.
Kwahiyo mtu anayekwenda kufanya uasherati leo, ni yeye mwenyewe amechagua uovu kwa ushawishi wa nguvu za shetani…zingati hili (Ni huyo mtu kafanya na sio shetani kafanya kwa niaba yake)…Kwahiyo hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza ni huyo mtu, kwasababu kachagua kufanya mabaya…
Ni sawa leo uende sokoni kununua nguo, ukute maduka mawili mbele yako, moja linauza nguo nyeupe lingine nyeusi…na ndani kila mmoja anakushawishi ununue kwenye duka lake…maamuzi ya mwisho yanatoka kwako wewe, na sio kwa mwenye duka…hapo kama utachagua nyeusi au nyeupe na kwenda nyumbani kukuta kasoro, hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza sio muuzaji bali ni wewe ambaye ulikwenda kuchagua…ulipaswa ukague nguo yote kwa makini kabla ya kuinunua, sio kusikiliza tu maneno ya wauzaji na kuamini!
Na ndivyo ilivyo sasa hivi duniani kuna maduka mawili, moja linauza mavazi meupe(ya uzima wa milele), na lingine meusi ni jukumu lako wewe kuchagua lipi linakufaa…kila moja lina watu ndani yake wanaokushawishi na kukuvutia, maamuzi ya mwisho unatoa wewe..sio muuzaji!…Muuzaji anakazi tu ya kukudalalia basi! Mambo mengine unafanya wewe, uchaguzi unafanya wewe na gharama unaingia wewe.
Leo utasikia mtu anakwenda kuzini, halafu anakwambia ni shetani kafanya vile, atakuambia shetani kanipitia tu!… hajakupitia ndugu ni wewe umechagua mwenyewe uovu, kwa kukubali ushawishi wake…Kama ingekuwa ni shetani, basi Mungu asingesema “siku ile kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu kutoa hesabu ya mambo yake”…asingesema hivyo, badala yake angesema “shetani atasimama kueleza ni kwanini kawaingia watu na kuwalazimisha wafanye dhambi”…Lakini siku ile kila mtu atahukumiwa kwa aliyoyatenda…kwanini? kwasababu si shetani aliwalazimisha watu kutenda, bali ni watu kwa uchaguzi wao wenyewe walichagua uasi…
Yohana 3: 19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Kwahiyo mtu yeyote anayetenda dhambi, ni katenda dhambi kwa idhini yake mwenyewe baada ya kuzidiwa na ushawishi wa shetani kufanya hilo jambo. Hivyo hapo shetani ni mtu wa pili kulaumiwa baada yake yeye…wa kwanza kabisa kulaumiwa ni yeye na ndio afuate shetani.
Hebu tafakari juu ya hili ili upate kuelewa kuwa kuna upofu Fulani unaendelea…..Mtu atakapotenda jambo fulani jema, labda amsaidie maskini hatasema ni Mungu kafanya lile jambo…atasema ni yeye kafanya…ukimwuliza imekuaje umefanya hivyo, atakwambia nimeguswa tu kufanya hilo jambo! Na tena ukimwuliza ni wewe au Mungu ndio kafanya hilo jambo atakwambia ni yeye ndiye aliyefanya 100%….. Mungu ni kama kamsaidia tu…na tena ataamini kuwa anastahili baraka kutoka kwa Mungu kwa alichokifanya lakini huyo huyo mtu hebu afanye uasherati utasikia anasema ni shetani huyo!..sio mimi ni shetani, utaona malaumu yote na sababu zote anamtupiwa shetani na kuanza kumlalamikia Mungu kwanini hakumwua shetani…lakini alipotenda mema hakusema ni Mungu kafanya bali alisema ni yeye, tena alipokea utukufu kutoka kwa watu kuwa yeye ndiye aliyefanya ule wema!.
Ndugu kama ni haki yako kupata baraka kutoka kwa Mungu kwa kutenda mema…jua pia ni haki yako kupata laana kutoka kwa Mungu kwa uovu unaoufanya!..Uovu unaoufanya, Mungu wala shetani hawahusiki, ni wewe ndio unaoamua kuufanya..wao ni kama washauri tu!..Ndio maana Mungu pia atawapa thawabu watakatifu wake watakaoshinda mbinguni, siku ile hatajipa yeye thawabu, atawapa watakatifu kwasababu ni wao ndio walioamua kufanya mema, sio Mungu.
Kumbuka pia unapotenda mema ni Mungu ndiye atakubariki, na unapotenda mabaya ni Mungu ndiye atakulaani na sio shetani, kwasababu sio shetani aliyeuumba uovu, ndio maana unaona pale Edeni baada ya Adamu na Hawa kuasi ni Mungu ndiye aliyewalaani na sio shetani!…aliyesema tutakula kwa jasho sio shetani ni Mungu!…aliyesema tutazaa kwa uchungu sio shetani ni Mungu! Aliyeilaani ardhi sio shetani ni Mungu!. Kwahiyo ukitenda uovu leo hii ni umeuchagua kwa hiyari yako mwenyewe na hivyo utakuwa unaishi katika laana kutoka kwa Mungu. Shetani hahusiki hapo!.
Wengi wanawalaumu pia Adamu na Hawa kuwa ndio sababu ya mambo yote..Ni kweli wao walichangia kuifanya njia ya upotevu iwe pana Zaidi lakini ni vyema ukafahamu kitu kimoja…hata kama Adamu na Hawa wasingekula lile tunda, kusingemzia shetani kuwajaribu Watoto wao, na hata kama watoto wao pia wasingekula tunda kwa kukataa ushawishi wa shetani pia isingemzua shetani kuwajaribu wajukuu wao na vitukuu vyao…na ingeendelea hivyo hivyo mpaka mwisho wa vizazi vyote, shetani angekuwa anandelea kuwajaribu tu wanadamu….hata siku wewe unazaliwa ungemkuta shetani naye pia asingeacha kukujaribu kula tunda hata kama vizazi vyako vya nyuma vyote vimeshinda…Kwahiyo hata kama Adamu na Hawa wasingenaswa pengine ungeweza kunaswa wewe!…uthibitisho ni hizo dhambi za makusudi unazozifanya sasa….
Ndio maana huoni mahali popote kwenye Biblia Mungu akiwalaumu Adamu na Hawa, baada ya kutoka pale Edeni..kwasababu wote tumefanya dhambi… Hivyo geuza mtazamo wako wa kuwasingizia baadhi ya watu na shetani kuwa ndio chanzo cha matatizo Fulani, ni kweli wanaweza kuwa wamehusika kwa sehemu Fulani…lakini sehemu kubwa ya maamuzi ipo kwako!!.
Kristo leo anagonga moyoni mwako umegeukie kumbuka shetani anapenda umsingizie yeye ili siku ile ya hukumu ujute! Useme laiti ningepata huu ufahamu angali nipo duniani nisingekuwa mtu wa visingizio…Chagua mema leo usichague mabaya yaletayo laana. Ni rahisi kuchagua mema, yupo mmoja ambaye aliweza kuchagua mema, yeye ndiye anayeweza kutufundisha na sisi namna ya kuchagua mema…na huyo si mwingine Zaidi ya YESU KRISTO, aliyemzungumziwa mahali Fulani hivi…
Isaya 7: 14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. 15 Siagi na asali atakula, WAKATI AJUAPO KUYAKATAA MABAYA NA KUYACHAGUA MEMA”.
Isaya 7: 14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
15 Siagi na asali atakula, WAKATI AJUAPO KUYAKATAA MABAYA NA KUYACHAGUA MEMA”.
Huyu ndio Mkuu wa Uzima, aliyebeba wokovu, hakuna aliyemfuata yeye akajuta, alituambia maneno haya..
Mathayo 11: 27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11: 27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Hivyo tunamtii na kumfuata kama tulivyo, na mizigo yetu.. kama ni mwasherati unaenda kama ulivyo, kama ni mtazamaji wa pornography unaenda kama ulivyo, kama ni msengenyaji vivyo hivyo, kama ni mlawiti, shoga, mlevi, mtoaji mimba, mwizi,muuaji, mla rushwa, mcheza kamari, mwenye huzuni, mwenye msongo wa mawazo, uliyefungwa na nguvu za giza,..msogelee leo, utue mzigo wako pale… hapo ulipo Tubu kwa kumaanisha kuacha kabisa kufanya hayo mambo, na yeye ni mwaminifu atakusamehe…
Na baada ya kufanya hivyo ili ukamilishe toba yako nenda katafuta ubatizo sahihi wa kuzama mwili wote katika maji na kwa jina la YESU KRISTO, kwaajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na Matendo 2:38, dhambi zinakamilika kuondolewa kwa ubatizo sahihi…na baada ya Hapo Roho mwenyewe ataingia ndani yako na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia na kukusaidia katika kuchagua yaliyo mema na kukataa mabaya..na utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.
Kumbuka tunaishi siku za mwisho, siku yoyote Parapanda inalia, na watakatifu watanyakuliwa kwenda juu mbinguni, tujitahidi mimi na wewe tuwe miongoni mwao walioalikwa Karamuni.
Bwana akubariki sana, Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu.
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAP
Mada Zinazoendana:
SHETANI NI NANI?
‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI
MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
Rudi Nyumbani
Print this post
Yeremia 30:7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Biblia inasema ni siku ambayo haiwezi kufananishwa na siku yoyote katika historia ya siku zote za dunia ambazo zilishawahi kuwepo mambo ambayo yataenda kulikuta Taifa la Israeli, Hicho ndio kipindi cha taabu kuu ambacho Danieli alionyeshwa;
Danieli 12: 1 “ Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile”.
Na Bwana wetu Yesu Kristo alikuzingumzia pia, kuweka msisitizo wa uzito wa dhiki hiyo ..
Mathayo 24:21 “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”
Mathayo 24:21 “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”
Na cha kuzingatia ziadi ni kuwa dhiki hii haitakuja wakati wowote isipokuwa wakati ambapo Israeli imesharudi na kuwa kitu kimoja kama zamani za kale za mfalme Daudi na Sulemani.
Yeremia 30:1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, 2 Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia. 3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki………… 7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Yeremia 30:1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,
2 Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.
3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki…………
7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Na jambo hilo lilitimia mwaka 1948, baada ya kukaa zaidi ya miaka 2500 bila kuwa taifa huru, Israeli sasa ni taifa huru, na sisi ni mashahidi kuwa tumeshaanza kuona mwanzo wa utungu wa mambo hayo, kipindi cha vita ya pili vya dunia jinsi wayahudi walivyouliwa kikatili na Dikteta wa kijerumani Adolf Hitler bila sababu yoyote, tafakari jinsi wanawake na watoto walivyokuwa wanachukuliwa uchi, na kudanganywa kuwa wanaenda kuogeshwa kumbe wanafungiwa kwenye mabafu ya gesi za sumu (Gas chambers), na huko ndani kwenye vyumba hivyo, vya giza inatupwa gesi moja kali ijulikanayo kama Zyklon B, inawaua watu kama kuku waliochinjwa, huku damu zikitoka midomoni na puani, ndani ya dakika 4 tu zinakuwa ni maiti zilizolala chini. Na mauaji mengine ya kikatili ukifuatilia katika historia utayaona. Wayahudi zaidi ya milioni 6 waliuliwa kwa namna kama hizo kikatili.
Sasa huo ni mfano mdogo sana,(mwanzo wa utungu) kwa hiyo dhiki itakayokuja huko mbeleni. Mambo yatakuwa mabaya zaidi, kutakuwa kuna mateso ya ajabu ambayo hayajawahi kufanyika popote, kama tu wakati wa Hitler watu walikuwa wanachukuliwa kwa marika tofautitofauti na wanawekwa kwenye barafu wakiwa uchi na wanaangaliwa mpaka wafe, huku wengine wakichukua data, kuchunguza ni rika lipi linawahi kufa katika hali ya ubaridi (na hiyo biblia inaiita tu ni mwanzo wa utungu)…unadhani itakuaje utungu wenyewe ukianza?….pengine watu watalishwa nyama za miili yao wenyewe wangali wakiwa hai….Dhiki hii Mungu atairuhusu kwa watu wake Israeli, na watu wa mataifa wachache ambao walibaki kwenye unyakuo….na hiyo yote Mungu ameruhusu kwa makosa ya Israeli ukiendelea kusoma mistari inayofuata ya hiyo Yeremia 30 utaona, na atakayetekeleza hilo zoezi ni mpinga-Kristo, Wayahudi (Waisraeli) wataadhibiwa hivyo lakini baadaye Mungu atawaokoa..
Lakini mpaka hayo yote yatokee, Kanisa la Kristo litakuwa limeshanyakuliwa, mbinguni, Bibi-Arusi sikuzote haandaliwi kupitia dhiki bali anaandaliwa kwa ajili ya sherehe, na ndivyo itakavyokuwa kwa Bibi-arusi wa Kristo, wakati wote huu ambao yupo duniani sasa anaandaliwa kwa ajali ya karamu ya mwana-kondoo, ambayo Kristo amekuwa akituandalia mbinguni kwa miaka 2000 sasa, Siku watakapoisikia paraparanda ya Mungu ikiwaita, muda huo huo watageuzwa kufumba na kufumbua na kuwa na miili ya utukufu ya kimbinguni, wataungana na wale watakatifu waliolala, kisha kwa pamoja watapaa zao mbinguni, kumfurahia Bwana wao. Hivyo watakaopitia hii dhiki ni wale wanawali wapumbavu, ambao hawakujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana wao akiwa hapa duniani….Hao ndio watakaojumuika na wayahudi,
Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Utajisikiaje, siku ile unaona wenzako wapo juu mbinguni karamuni, halafu wewe umeachwa?, umetengwa na uso wa Mungu milele, Ikiwa neema unaichezea leo, usidhani itakuwepo kipindi kile, wakati huo neema ya Mungu itakuwa kwa wayahudi watu wake, kupigwa kwao upofu leo ni ili wewe na mimi tutubu tumgeukie Mungu, (soma Warumi 11:8-36 )wakati ule ukifika Mungu hatakuwa na habari tena na wewe, au mtu yoyote wa mataifa, bali watu wake, wateule wake wayahudi. Na hao ndio Bwana atakaowakoa.
Hizi ni nyakati za mwisho ndugu, usipumbazwe na huu ulimwengu unaopita, angalia ni faida gani unakuahidia maisha baada ya hapa?, majira yanabadilika haya, matukio yanayotokea duniani, ni kuonyesha kuwa dunia imeshafika OMEGA. Acha kusuasua kwenye njia mbili, huu sio wakati wa kuhubiriwa injili ya kubembelezwa tena, mkabidhi Kristo maisha yako leo, tubu kabisa na umaanishe kumfuata, na yeye ni mwaminifu na mwenye huruma, hata kama dhambi zako ni nyingi kiasi gani ataziweka mbali na wewe. Tubu ukabatizwe, Upokee Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?.
WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA.
ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?
Ili kujua kama ku-BET ni dhambi au la! Ni vizuri kwanza kufahamu mapenzi ya Mungu ni yapi?…Huwezi kujua kipi kisichompendeza Mungu kama hujui kipi kinachompendeza…Sasa Mungu alivyotuumba watu wake na viumbe vyake vyote hata Wanyama, alituwekea kitu kinachoitwa dhamira ndani yetu…Hii dhamira kazi yake ni kutulinda sisi tusiende kinyume na mapenzi ya Mungu tunapoishi…Na ipo kwa viumbe vyote (wanadamu na wanyama)..Ndani ya hii dhamira kumefungiwa sheria za Mungu. Kwahiyo pasipo hata Mungu mwenyewe kuzungumza na mtu juu ya jambo Fulani tayari ile dhamira iliyopo ndani yake ina uwezo wa kukamata na kuhisi jambo ambalo sio sawa.
Kwamfano utaona, Simba anauwezo wa kula swala na kumrarua kikatili, lakini simba huyo huyo hamli mtoto wake…ni kwanini? Ni kwasababu dhamira iliyopo ndani yake inamshuhudia kuwa jambo hilo sio sawa…simba hajapewa sheria yoyote na Mungu, lakini ndani ya moyo wake kumefungiwa sheria, kwa kupitia dhamira aliyo nayo. Kadhalika huwezi kuona mbwa au mnyama yoyote analala na mnyama wa jinsia moja naye…
Ni kwanini? ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yao..inayowashuhudia kuwa jambo Fulani sio sahihi, sio kwamba hawana hisia! Wanazo hisia lakini hawawezi wakavuka hiyo mipaka.
Na wanadamu ni hivyo hivyo, kuna kitu kinaitwa dhamira ambayo hiyo imebeba sheria za Mungu ndani yake, kiasi kwamba mtu anaweza asizijue kabisa amri za Mungu, lakini bado akazitimiza vile vile..
Haihitaji biblia kujua kuwa uuaji ni mbaya, au kuwatesa Watoto wako ni vibaya…Hiyo sheria tayari mtu anazaliwa nayo moyoni mwake…ndo maana hata wanyama pamoja na ukatili wao wote hawayafanyi hayo, hawasomi biblia lakini wanazitimiza sheria za Mungu….Haihitaji biblia kujua kuwa utoaji mimba ni vibaya, au kumdhulumu mtu ni vibaya, hiyo tayari mtu angejua hata kama hajawahi kusikia habari za Mungu. Haihitaji sheria kufahamu kumuoa dada yako/kaka yako wa damu ni makosa, hiyo tayari ipo ndani yako, hata hizo hisia zenyewe hazipo licha tu ya dhamira kukushuhudia.
Sheria ilipokuja, kazi yake ni kuitoa hiyo hiyo sheria kutoka katika roho na kuileta katika maandishi..Na hiyo ni kutokana na ugumu wa mioyo yetu, unajua hata watoto wanapotumwa dukani, na wanaonekana ni wazito kidogo kuelewa au wanasahausahu sahau, basi wazazi wanaamua kuwaandikia kikaratasi kidogo cha maelekezo ili wasisahau. Na sheria ilikuja kwa namna hiyo hiyo. Ililetwa kutufanya tuyakumbuke yale tuliyokuwa tumeyasahau katika roho zetu na dhamira zetu..
Sasa Watu waliokuwa wanaishi wakati wa Nuhu, walikuwa hawana sheria yoyote, Maana sheria ililetwa na Musa miaka mingi sana baada ya gharika?..Sasa unaweza kuuliza kama kulikuwa hakuna sheria, wale watu walihukumiwa kwanini?…Walihukumiwa kwa dhamira iliyokuwepo ndani yao…walikuwa wanafanya mambo ambayo ndani ya dhamira zao walikuwa wanajua kabisa sio sawa…lakini waliendelea kuyafanya! Hivyo ikawa dhambi kwao,(Warumi 1:17-30) Na Mungu akawaangamiza wote kwa gharika. Kwahiyo sheria hii ambayo tayari ipo ndani ya dhamira zetu ndio inayojulikana kama INJILI YA MILELE (Ufunuo 14:6). Kwa maelezo marefu juu ya injili hii ya milele Bofya hapa >> INJILI YA MILELE
Sasa mpaka sasahivi hii INJILI YA MILELE ipo, Kuna vitu ambavyo havijazungumziwa hata kwenye Biblia takatifu lakini mtu akiona tu! Anajua hiyo sio sawa machoni pa Mungu..Mfano wa vitu hivyo ni Uvutaji wa sigara, utoaji mimba, mtu anayetoa mimba anajua kabisa ndani ya moyo wake anaua na anafanya jambo lisilo sahihi…ingawa ukitafuta mahali popote kwenye biblia palipoandikwa utoaji mimba ni dhambi huwezi kupata…Lakini mtu anayefanya hivyo anajua kabisa na anauhakika ndani ya moyo wake anamkosea Mungu, na ndivyo ilivyo…au mtu anayetumia madawa ya kulevya…anajua kabisa jambo afanyalo sio jema…
Jambo lingine ni mtu anayefanya masturbation, ukienda kumwuliza mtu anayefanya masturbation unajua ni kosa kufanya hivyo, wala hatakubishia Zaidi ataogopa na atakuuliza namna ya kuacha!…lakini ukienda kwenye maandiko ukitafuta mahali popote pamezungumzia suala la masturbation kuwa ni dhambi hutapaona!…lakini kwanini yule mtu ndani ya moyo wake anauhakika kuwa anachokifanya sio sahihi?..
Ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yake! (Sheria ambayo Mungu alishaiweka ndani ya moyo wake) inayomshuhudia jambo sahihi na lisilo sahihi…Au leo hii ukimfuata mtu anayeangalia pornography, atakwambia kabisa mimi nafanya makosa, wala hatakubishia wala kukuuliza ni wapi pameandikwa hivyo kwenye biblia?…wala hatataka kujua, yeye anachojua kuwa anafanya dhambi, jambo lisilompendeza Mungu, hilo tu!…Au mtu anayecheza kamari, anajua kabisa jambo afanyalo sio sawa, na anajua kabisa huo mchezo ni wa kishetani, anajua kabisa ni mchezo wa dhuluma ambao wakati mwingine unaweza kuhatarisha, uchumi wake, na usalama wake, anajua kabisa Mungu hayupo katikati ya huo mchezo, Na dhambi nyingine nyingi zinazofanywa na wanadamu ndio hivyo hivyo, hazihitaji biblia kuzihakiki, tayari zimeshajihakiki zenyewe ndani yetu.
Sasa tukirudi kwenye suala la KU-BET na lenyewe ni hivyo hivyo, Kubet ni kamari, isipokuwa iliyohalalishwa na nchi.
Hakuna mahali popote katika biblia imezungumzia habari za kubet…Lakini ipo INJILI YA MILELE ndani ya kila mtu…Inayokushuhudia kuwa hichi kitu sio sahihi.
Kama ukichunguza kwa makini mtu anayebet kabla hajaanza kufanya hicho kitu kina kitu ndani yake kinamshtua kwanza, anaanza kukosa amani na anakuwa na mashaka mashaka na huo mchezo, ndio hapo ataanza kujiuliza, hivi kweli huu mchezo ni wa KiMungu? Hayo ndio maswali ya kwanza mtu anayoanza kujiuliza kabla ya kuingia…Na anapoikataa hiyo sauti na kuingia huko, baadaye haisikii tena ndio anaanza kuona ni mchezo wa kawaida tu usio na madhara yoyote, lakini siku za kwanza kwanza atakwenda mpaka kuuliza watu kama ni sawa kuucheza au la?..Ukishaona hali kama hiyo jua kabisa kuna kitu cha hatari unakiendea..
Na ni kwanini unaanza kusikia hivyo viashiria kabla hata hujajiingiza kwenye huo mchezo? Ni kwasababu mchezo huo ni wa kishetani, na unamwingiza mtu kwenye roho moja kwa moja..Mashirika yote ya betting ulimwenguni yanafanya kazi ya shetani kama ulikuwa hulijui hilo ndugu yangu.., yanafanya mambo mengi ya siri ambayo shetani hawezi kuruhusu watu wayajue, ndio mashirika yanayokusanya utajiri mkubwa kwa shetani..Na hayo ndiyo yatakuja kushirikiana na mpinga-Kristo katika kumpa nguvu.
Mashirika hayo mengi yanamilikiwa na vikundi vya kichawi vikubwa duniani kama freemason, brotherhood, yana kivuli cha kulipa kodi, lakini yana agenda nyingine za siri nyuma ya pazia, yanapokea maagizo kutoka kwa lusifa mwenyewe kufadhili mikutano ya hadhara ya ushoga ili kuipalilia roho ya ushoga duniani,..kufadhili haki za mashoga na wasagaji, kufadhili agenda za utoaji mimba n.k kwa nje yanaonekana ni mazuri, lakini wamiliki wa mashirika hayo ni mawakala wa shetani mwenyewe waliowekwa na shetani kwa kazi hiyo.
Na baadhi ya mashirika hayo pia yanafadhili ugaidi kwa siri, ili kuihimiza dunia ilete ustaarabu mpya wa ulimwengu, na pia yanatumia fedha nyingi kuyanyanyua mashirika mengine madogo madogo yanayofanya kazi kama hizo za kuiharibu dunia.…Shetani anafanya kazi kubwa kuachilia mapepo ambayo yatahakikisha watu wengi wanakwenda kubet na kuhakikisha wanakosa, ili aongeze fedha nyingi katika ufalme wake kwaajili ya kumwekea njia mpinga-Kristo. Biblia inasema shetani anampa aliyewake jinsi apendavyo, yeye ndiye anayechagua ni nani apate na ni nani akose, na kumbuka anawapa walio wake, hawezi kumpa ambaye anajua hamsujudii wala haongezi chochote katika ufalme wake..
Mtu anayekwenda kubet kuna pepo Fulani linamvaa, ambalo litamfanya Kesho arudi tena kufanya hivyo hata kama atakosa mara ngapi lakini hatachoka kubet…Mwisho wa siku unakuwa fukara, na bado taabu yako umempa shetani aitumie.
Kwahiyo Biblia inatuambia tutoke huko? (2 Wakoritho 6:15-18)..tutatokaje! Ni kwa kutubu na kudhamiria kuacha hivyo vitu…Biblia inasema shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, unapotamani kupata fedha za ghafla, tambua ni kama mtu aliyewasha WIFI kwenye simu yake, mtu aliyekaribu na yeye anaweza kuupata mtandao wake, na kadhalika mtu anayependa au kutaka kupata fedha za ghafla, anakuwa ni rahisi sana kuonekana kwenye mitandao ya mashetani na kuvaliwa na maroho…
1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. 10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.
1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.
Hivyo tunaonywa tusipende fedha za ghafla! huo ni mtego mkubwa sana shetani anaoutumia…Tembea huko barabarani kwenye nguzo za umeme uone vibao vya waganga,..wote kitu cha kwanza watakwambia…njoo upate utajiri!..Mpango wa Mungu ni kuchuma kidogo kidogo…Sio kwamba hapendi tupate kingi hapana! Ndio mpango wake tuwe na vingi Lakini tukusanye kidogo kidogo…….Tukusanye shilingi mia, mia, kuanzia asubuhi hadi jioni na kupata milioni kumi hiyo ni sawa!….lakini kupata milioni kumi ndani ya dakika moja ogopa sana hizo njia!..Vingi vya hivyo ni mitego ya shetani, Na ndio betting inachofanya.
Mithali 13: 11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.
Bwana akubariki sana.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
INJILI YA MILELE.
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
Licha ya kulinda, jukumu lingine kuu mlinzi alilonayo ni kuhisi hatari kutoka mbali, Na ndio maana utaona mnyama ambaye Mungu alimuumba kutulinda sisi (Mbwa), licha tu ya kupewa ukali, lakini pia amepewa uwezo wa kunusa mbali, na kusikia, na ndio maana wakati wa usiku utaona mbwa wanabweka sana, hiyo ni kutokana na kuwasikia na kunusa vitu vilivyo mbali sana visivyo vya kawaida, ambavyo hata wewe huwezi kuvihisi au kuvisikia, ule wakati ambao unauona ni wa utulivu na salama lakini kwa Mbwa ni machafuko.
Vivyo hivyo na mlinzi yoyote, hana jukumu la kulinda tu pale adui anapokuja, bali pia anajukumu la kuhisi hatari, na hiyo inakuja kwa kupepeleza, kuchunguza, kutafiti na kutazama, na wakati mwingine kufanya doria, itakayomsaidia kuhisi tatizo kabla halijatokea.. na thamani ya mlinzi sikuzote ipo usiku n.k…
Isaya 21:11 “Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? 12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.”
Isaya 21:11 “Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?
12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.”
Ukisoma hata katika agano la kale utaona walinzi wa miji walikuwa wanakaa katika minara mirefu, ili kuwasaidia kuona kitu kinachokuja kutoka mbali, na wakiona hatari basi bila kuchelewa tarumbeta lilikuwa linapigwa na mji wote kujiweka tayari kwa vita.
Ezekieli 33:1 “Neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, Hapo nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka AWE MLINZI WAO; 3 ikiwa, aonapo upanga unakuja juu ya nchi hiyo, apiga tarumbeta na kuwaonya watu; 4 basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. 5 Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake.”
Ezekieli 33:1 “Neno la Bwana likanijia, kusema,
2 Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, Hapo nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka AWE MLINZI WAO;
3 ikiwa, aonapo upanga unakuja juu ya nchi hiyo, apiga tarumbeta na kuwaonya watu;
4 basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.
5 Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake.”
Lakini kama mji utakosa walinzi, au watazamaji, ni dhahiri kuwa utakuwa katika hatari ya kuvamiwa na maadui wakati wowote, na siku maadui watakapokuja watakuja ghafla wenyeji hawatajua chochote kwasababu hawakuwa na waonaji wanaoona mbele yao.
Ndivyo Bwana alivyotabiri jinsi itakavyokuwa katika hizi siku za mwisho, kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, kama mwivi usiku wa manane.
(Ufunuo 16:15 “Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake”.)
vile vile mwisho wa dunia utawajia watu kwa ghafla,
(2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea”.)
na hiyo yote ni kwasababu wamekosa MLINZI katika mioyo yao.
Na ndio maana jambo kuu na la muhimu sana ambalo Bwana Yesu alituachia siku ile aliyokuwa anaondoka, alikuwa ni ROHO MTAKATIFU, akamwita ni msaidizi wetu, kwa namna nyingine ni mlinzi wetu, alijua kabisa, wakati wa giza utapita duniani, na sikuzote giza linaleta usingizi, hivyo kama hatakuwepo mtu wa kuwasaidia kukesha nao, watasinzia na uharibifu utawapata kwa ghafla…
Hivyo akatugawia Roho Mtakatifu, ambaye ndio tupo naye sasa, wote waliompokea kila siku anawashuhudia ndani ya mioyo yao hatari iliyopo duniani sasahivi na jinsi ya kuwa waangalifu. Anawataarifu kila iitwapo leo habari za mwisho wa dunia na kuja kwa Kristo. Na hawa ndio wale hata siku ile ya unyakuo itakapokaribia sana kufika wataifahamu, kwasababu mlinzi wa kuwapasha habari yupo mioyoni mwao.
1 Wathesalonike 5 :1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi”.
1 Wathesalonike 5 :1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi”.
Unaona, wale waliojazwa Roho Mtakatifu ndio siku hiyo hatawapa kama mwivi kwasababu, atakuwepo kuwapasha habari juu ya mambo yote yanayokuja. Watajua kabisa wakati wa kuondoka umefika, kama wanavyoshuhudiwa hata sasa, itakapofika kipindi kifupi sana kabla ya unyakuo, mlio wa kengele utazidi kuongezeka ndani ya mioyo yao.
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, NA MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA HABARI YAKE”.
Lakini wale wengine, ambao hawana ROHO MTAKATIFU sasa, ndio wale hata wakisikia kuwa tunaishi siku za mwisho hawashtuki, mioyoni mwao hakuna mabadiliko yoyote, macho yao yamefumbwa, ukiwaambia Yesu Kristo yupo mlangoni kurudi, wanakudhihaki, Na wengine tayari walishampa Bwana maisha yao, zamani walikuwa wanaishi kama wana wa mbinguni lakini baada ya muda na wao wamegueka wakafanana na watu wengine wa kidunia, hao ndio wale ambao wamemzimisha ROHO MTAKATIFU ndani yao, Yule mlinzi anayewalinda amelala, na hivyo hawezi tena kuwapasha habari ya mambo yanayokuja na hatari iliyopo mbele yake.
Mtunzi wa Zaburi aliandika hivi, kwa wachao Mungu..
Zaburi 121:3 “Asiuache mguu wako usogezwe; ASISINZIE AKULINDAYE; 4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 5 BWANA NDIYE MLINZI WAKO; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.”
Zaburi 121:3 “Asiuache mguu wako usogezwe; ASISINZIE AKULINDAYE;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA NDIYE MLINZI WAKO; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.”
Wapo ambao, awalindaye amesinzia, na hao ndio wale wanawali wapumbavu wanaozungumziwa katika Mathayo 25. Ambao kwa pamoja na wenzako (wale wanawali werevu) walikuwa wanamngoja Bwana wao, lakini kwasababu hawa hawakuwa na mafuta ya ziada katika chupa zao, wakarudi baadaye wakakuta mlango umeshafungwa, kule kuishiwa na mafuta ndio kumzimisha Roho..Kwasababu mwanzoni walikuwa nayo lakini baadaye yaliwaishia..Na mafuta siku zote katika biblia yanamwakilisha ROHO MTAKATIFU.
Ndugu yangu nataka nikuambue tunaishi katika siku za mwisho, hakuna mtu asiyejua kuwa Dalili zote zimeshatimia, Jiulize Kristo akirudi leo kulichukua kanisa lake, utaufichia wapi uso wako wewe ambaye bado unasuasua, kwa injili ulizokuwa unahubiriwa kila kukicha lakini bado hutaki kugeuka?. Roho Mtakatifu kila siku anagonga katika mlango wa moyo wako lakini hutaki kufungua. Biblia ipo wazi inasema na mtu yoyote asiyekuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake (Warumi 8:9).
Ni maombi yangu utamruhusu huyu mlinzi ayaongoze maisha yako kuanzia sasa katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho kabla ya hii dunia kuisha..Kama ulikuwa umepoa, au umemzimisha Roho Mtakatifu ndani yako, ni wakati wa kutengeneza mambo yako upya sasa. Na kama hujamkabidhi Bwana maisha yako, unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi, kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na ukishatii maagizo hayo mepesi Bwana mwenyewe atamshusha Roho wake Mtakatifu ndani yako, kuanzia huo wakati na kuendelea naye atakuongoza na kukupasha habari ya mambo yote yahusiyo saa tunayoishi na siku za mwisho, na hatimaye siku ile haijakujia kama mwivi.
Pia Kwa Maombezi/Ushauri/Ratiba za Ibada Wasiliana nasi Kwa namba
+225683036618/+225789001312
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Kitabu cha Jeografia, hawajaandikiwa watu ambao sio wanafunzi, kadhalika kitabu cha Fizikia na Baolojia…Vitabu vyote hivi wameandikiwa watu husika…yaani wanafunzi wa masomo hayo..Mtu mwingine yeyote akisoma hataelewa au hakitamsaidia sana…Na maudhui ya vitabu hivyo havijaandikwa kwa lengo la kusomwa tu, bali kujifunza…lengo la mwanafunzi kujifunza mambo yaliyoandikwa ndani ya kitabu kile ni ili kumpa maarifa ambayo yatamsaidia katika maisha yake na pia yatakayomsaidia kufaulu mitihani…asipokielewa kitabu hicho na kukisoma tu kama gazeti, anaweza kweli kukisoma chote ndani ya siku moja lakini utakapokuja mtihani atafeli…Kwasababu waandishi wa vitabu hivyo, lengo lao sio mwanafunzi asome ndani ya siku moja, bali ajifunze kidogo kidogo mambo yaliyopo kule na ayafanyie mazoezi na alinganishe mambo kutoka vitabu vingine, na ndio maana mpaka atakapohitimu inaweza kumchukua hata miaka 4 na zaidi.
Kadhalika na Biblia, NI KITABU CHA MAISHA. Kitabu hichi, hakimuhusu kila mtu, bali kinawahusu wanafunzi tu! Wengine watakisoma kama gazeti na hakitawasaidia chochote, lakini wanafunzi wanakisoma kama ni sehemu ya Maisha yao, future yao ipo hapo, Ndio ufunguo wa Maisha yao…Ndio maana biblia iliposema “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.(Mithali 4:13)”…Mstari huo haukulenga Elimu ya darasani…hapana! Bali ulilenga Elimu ya Mungu (Elimu ya ufalme wa mbinguni) Mathayo 13:52..maana huo ndio uzima wetu…wengi wanaupeleka mstari huu moja kwa moja kwenye Elimu ya duniani, lakini hiyo si kweli.. “hiyo ni maana ya pili ya mstari huo lakini maana ya kwanza Kabisa Sulemani aliyomaanisha hapo ni ELIMU YA UFALME WA MBINGUNI”.
Na unapozungumzia Elimu huachi kuzungumzia, Shule, huwezi kuacha kuzungumzia,Waalimu, huwezi kuacha kuzungumzia wanafunzi, wala huwezi kuacha kuzungumzia Mtaala (ambao upo ndani ya vitabu husika).
Na kadhalika Maisha mapya katika Kristo ndio shule yetu, Roho Mtakatifu ndio Mwalimu Mkuu wetu, Biblia ndio Mtaala wetu (Kitabu husika)..na wote waliomwamini Yesu Kristo kwa kuzaliwa mara ya pili, kwa kudhamiria kabisa kumfuata kwa kujikana nafsi zao ndio wanafunzi wake…Utasema hilo linapatikana wapi kwenye maandiko…soma
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Sasa mwanafunzi kabla hajajiunga na shule yoyote ya kidunia, anakubali kuachana na wazazi wake, na ndugu zake, na hata marafiki zake, anakwenda kujiunga na shule ya Bweni…Huko shuleni hataishia tu kukaa mbali na wazazi wake kwa kipindi kirefu, bali atalazimika kuvikataa pia vile vitu vizuri alivyokuwa anavipenda akiwa nyumbani kama Tv, simu, uhuru, nk..anakwenda mahali ambapo hapana uhuru aliokuwa anautaka, mahali ambapo pengine atakutana na changamoto za chakula kibovu, na malazi mabaya.…Na katika Ukristo ndio hivyo hivyo unapoamua kumfuata Kristo ni sawa na umejiunga na shule mpya, Maisha yako ya kale unayakataa, pamoja na mapenzi ya wazazi wako…kwasababu unakwenda kutafuta Uzima wako wa baadaye (future). Na Ukristo sio mteremko kama wengi wanavyofikiri, ukiamua kumfuata Kristo kupungukiwa wakati mwingine kunakuwepo na pia kuna kupitia dhiki nyingi..tofauti na wale watu wanaowahidia watu uongo kuwa watafanikiwa siku zote.
Vivyo hivyo unapoingia shuleni, unakutana na sheria za shule na moja ya sheria hizo ni mavazi, na mwiko kutoka nje ya uzio wa shule.…shuleni huwezi kujivalia utakavyo, kunakuwa na UNIFORM maalumu…na wote mnafanana…na huwezi kuingia na kujitokea kama unavyotaka, ukitoka bila sababu maalumu ndio umejifukuzisha hivyo…..kadhalika Unapozaliwa mara ya pili, mavazi yako na mwonekano wako ni lazima ubadilike, ulikuwa unavaa vimini ni sharti uache, ulikuwa unavaa suruali wewe mwanamke ni sharti uache, ulikuwa unanyoa kiduku na kuvaa nguo zinazobana na milegezo wewe mwanamume sharti uache, ulikuwa unapenda kusikiliza miziki ya kidunia, na movie zisizo na maana na fashion za ulimwengu, na kuzurura huku na huko vyote hivyo unaacha!…Na pia Ukristo sio kuingia na kutoka…Ukiingia umeingia! Na ukitoka umetoka…Mwalimu Mkuu huwa hawi mkali kwa Watoto wa mitaani, huwa anakuwa mkali kwa Watoto walioko shuleni kwake, vivyo hivyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha watu waliozaliwa mara ya pili ni tofauti na ambao wapo nje.
Baada ya kukubaliana navyo hivyo vigezo, ndipo unapewa MTAALA MAALUMU pamoja na Waalimu wa kukufundisha, na wewe mwenyewe unaongeza bidii zako binafsi kujisomea…Ukisubiri tu kila siku kufundishwa darasani na wewe mwenyewe hutaki kutafuta, utafeli mtihani wa Mwisho, na Katika Ukristo ni hivyo hivyo, umezaliwa mara ya pili, wewe kila siku unapenda tu kufundishwa Biblia, muda wa kujisomea mwenyewe huna, utafeli majaribu na hutaendelea mbele kila siku utakuwa unarudi darasa lile lile, miaka yote wakati wenzako wanaenda mbele..
Na jambo lingine baada ya kujiunga na shule za kidunia ni kwamba utakaa shuleni katika hayo mazingira ya kuteseka kwa muda mrefu kidogo inaweza kuchukua hata miaka kadhaa, lakini siku utakapokuja kufanya mtihani wa mwisho na kufaulu utapokea cheti, ambacho hicho kitaonyesha tofauti yako wewe uliyekwenda shule na yule ambaye hajakwenda…kuvumilia viboko vya shule na kula chakula kibovu na wakati mwingine kulala vitanda vyenye kunguni sio bure!…siku utakapohitimu na kupata cheti heshima yako ndio itakapoonekana kuwa hukuwa mjinga kujikana nafsi yako.
Kadhalika Roho Mtakatifu akishakupitisha katika madarasa yake na kuyahitimu vizuri faida zake utakuja kuziona hapa hapa duniani pamoja na katika ulimwengu ujao…lakini sana utakuja kuziona katika ulimwengu ujao kwasababu vitu vya hapa duniani havidumu, vinapita lakini vya huko mbinguni ni vya milele…Siku zile wateule walioshinda watang’aa kama jua mbele za malaika wa mbinguni…
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?. 28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. 29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?.
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele”.
Umeona Umuhimu wa kuitafuta Elimu ya ufalme wa mbinguni sasa?..Elimu ya dunia hii inafunua elimu ya ufalme wa mbinguni, Kristo anapokuambia leo utubu na kuacha dhambi, na ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake na uache ulimwengu na mambo yake yote, na kisha umfuate sio kwamba anataka atutese, hapana ni kwasababu anataka atusajili kwenye shule yake ambayo baadaye itatupa cheti kilicho bora! Zaidi kuliko vyeti vyote.. Na heshima! Zaidi kuliko heshima zote….na kumbuka hakuna shule yoyote isiyokuwa na sheria ndio maana anakuambia ewe mwanamke jikane nafsi!! acha mavazi yako ya kikahaba, acha mawigi, acha kupaka wanja, acha mavipodozi baki katika hali yako ya asili…kama unapenda kujipamba subiri tukifika mbingu za mbingu utajipamba utakavyo kama kutakuwepo na kujipamba….lakini kwasasa upo shule!..fanya kile Mwalimu Mkuu anachokuagiza ukifanye kwa faida yako…
Ulipokuwa katika shule za kidunia ulipoambiwa uvae sketi za marinda ulitii na usisuke nywele ulitii bila shuruti lakini unapoitafuta elimu ya Roho Mtakatifu hutaki kutiii…nataka nikuambie ukweli bado hujaanza madarasa ya Roho Mtakatifu, bado upo nyumbani wala mtu asikudanganye kuwa upo sawa na Mungu bado haupo sawa, usidanganywe pia Mungu haangalii mavazi anaangalia Roho, ni kweli kabisa anaangalia roho lakini roho inamahusiano makubwa na mwili ndio maana ipo ndani ya mwili, kama vile elimu ya kidunia ilivyo na uvaaji wa wanafunzi wake..Elimu ni ufunguo wa Maisha, yaangalie Maisha yako ya baadaye yatakavyokuwa usijiangalie leo…dhambi za kitambo zisije kukuponza ukaja kujuta milele huko baadaye..Fanyika mwanafunzi wa Kristo leo.
+225693036618/+225789001312
NJIA YA MSALABA
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
MJUE SANA YESU KRISTO.
1 Wakorintho 6: 19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;”
Ukilijua Neno hili utauheshimu mwili wako, kuliko hapo kwanza. Kitu kikubwa kisichofahamika na wengi ni kuwa Miili hii tuliyonayo sio mali yetu..hatujapewa dhamana ya kuitawala asilimia 100. Kama ingekuwa ni mali yetu asilimia mia moja, tungekuwa na uwezo wa kuzisimamisha nywele zetu zisiote kwa amri zetu, tungekuwa tunaweza kuiambia mioyo yetu isimame kusukuma damu na ingetutii kama tu vile tunavyoamua kusimama au kukaa…
Kwahiyo unaweza kuona miili hii, tunamamlaka nayo sehemu ndogo sana, tena sana….huwezi kukiongoza chakula tumboni, kinajiongoza chenyewe, huwezi kuuongoza mwili wako utoe jasho unajitoa wenyewe, au kucha kukua…mwanamke hawezi kutengeneza kiumbe ndani ya tumbo lake, kiumbe kinajitengeneza chenyewe ndani kwa ndani, anajikuta tu, uchungu umemfikia na anajifungua mtoto… kadhalika hatuwezi kujifanya tukue..tangu tulipokuwa Watoto tunajikuta tu tunaongezeka kimo na ukubwa bila idhini yetu, vitu kama ini, figo, kongosho, seli zinafanya kazi pasipo hiyari zetu nk…chunguza utagundua kuwa hii miili yetu, tuna mamlaka nayo sehemu ndogo sana, karibia kila kitu kinaongozwa na nguvu nyingine..
Mamlaka tuliyopewa sisi ni uwezo wa kusogeza viungo vyetu vya nje kama miguu, mikono, macho, na uwezo wa kujisogeza kutoka sehemu moja hadi nyingine..basi hakuna kingine cha ziada…Hii yote ni kuonyesha kuwa HII MIILI SI MALI YETU NI MALI YA MWINGINE.
Ni kama tu mtu unapofungua account ya Facebook au ya Bank au anapoisajili laini ya simu…Unapofungua account ya facebook kwa mfano, account hiyo inakuwa ni ya kwako ina jina lako na password yako, kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kujua kinachoendelea ndani ya account hiyo, isipokuwa wewe umwonyeshe… kila kitu unaweza ukakifanya private mtu yeyote asijue unafanya nini, na unaweza kuitumia utakavyo…lakini pamoja na kwamba unao uwezo wa kuitumia utakavyo, bado kuna vitu utakuwa huwezi kufanya…kwamfano ukikiuka sheria za wamiliki wa facebook wanakunyanganya hiyo account, aidha wanakufuta kabisa au wanakublock kwa muda…na huwezi kuirudisha kwa namna yoyote ile,
Hiyo yote ni kuonyesha kwamba hiyo account si yako bali ni yao. Hata kama unauwezo wa kuweka password ngumu kiasi gani, lakini wenyewe wakitaka kujua kinachoendelea ndani ya account hiyo huwezi kuwazuia, wakitaka kukupokonya vile vile huwezi kuwazuia.
Na Zaidi ya yote, jinsi account za facebook na nyinginezo zinavyofanyiwa marekebisho, huwa mwenye account hahusiki, anajikuta tu kuna kitu Fulani kimeongezeka kipya, au kuna kitu Fulani kimeondolewa..Hiyo yote ni kuonyesha kuwa hiyo account ni ya kwako lakini bado sio ya kwako. Ni watu Fulani walikupa tu..
Na hii miili tuliyopewa ni hivyo hivyo, ni Mali ya Mungu…Si mali yetu kabisa, na ilivyowekwa hapa duniani na aliyeiweka (yaani Mungu) kaiwekea sheria na utaratibu wake, namna inavyopaswa iwe…Hakutupa kwa lengo la kuigeuza bango la matangazo, au chombo cha kuharibu wengine, au kituo cha roho nyingine chafu zinazoharibu kukaa…Mwili unaofanya hivyo utafungiwa haki ya kuishi (maana yake utakufa).
Ndio maana kuna umuhimu sana wa kuitunza hii miili tuliyopewa, na kuelewa kwa undani masomo kuhusu NAFSI, MWILI na ROHO.. kwasababu si MALI YETU WENYEWE…Ukiuchora mwili wako tattoo isingekuwa shida endapo ingekuwa ni mali yako…lakini kwasababu si mali yako ni ya mwingine usifanye hivyo, utajitafutia mabaya badala ya mazuri….Ni sawa sasahivi uanze kutumia hiyo account ya facebook vibaya, ukaanza kuitumia kuweka picha chafu na zisizofaa na kuharibu jamii, na kufanya uhalifu, wamiliki wakiligundua hilo unafungiwa mara moja na wala hutapata nafasi ya kuongea nao..kwasababu hata hawajawahi kuzungumza na wewe hapo kabla…password haimaanishi kuwa ndio umepata uhalali wa kuimiliki hiyo account asilimia 100. Kadhalika sio kwasababu unauwezo wa kusitiri siri ndani ya mwili wako kiasi kwamba hakuna mtu awezaye kujua kinachoendelea ndani mwako, na una uwezo wa kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kama utakavyo, ndio iwe sababu ya kusema huo ni mwili wako…Huo sio wako ni mali ya Mungu, akiutaka anauchukua siku yoyote, na huwezi kumwuliza kwanini.
Hivyo ili tuweze kuishi ndani ya hii miili kwa muda mrefu na kwa kheri hatuna budi kuishi kwa kuzifuata sheria zake, Neno lake linasema…mwanamke avae mavazi ya kujisitiri (1 Timotheo 2:9) basi ni vizuri kutii…usiseme una uhuru juu ya mwili wako, na kuvaa utakavyo, kumbuka huo si wako…
Biblia inasema usichanje chale wala usichore alama (tattoo) katika mwili wako ni machukizo, basi usijifanye wewe ni mgunduzi wa huo mwili, yupo mwenye huo mwili ambaye akiutaka anao uwezo wa kuutahifisha muda wowote.
Walawi 19: 28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana”.
Biblia inasema uashareti hata usitamkwe kamwe kwenu (Waefeso 5:3)…Usiseme mwili wangu, nina uhuru wa kufanya nitakalo, Hivyo Mungu hawezi kunihukumu kwa kitu ambacho ni mali yangu…Ndugu huo sio mali yako, ingekuwa hii miili ni mali yetu katupa moja kwa moja, wala asingetusumbua kutuwekea sheria sheria,… tungekuwa na uhuru wa kila mtu kufanya atakalo…mtu angeamua kujirefusha kuwa kama mlingoti, ni sawa, mwingine angetaka kujifanya kuwa tembo pia ni sawa…lakini kwasababu ni mali yake, wote anatuweka kwenye kimo Fulani karibia kinachofanana na maumbile yanayofanana, kutimiza kusudi lake yeye na si la kwetu…Kwahiyo Uasherati ni moja ya dhambi mbaya sana ambayo inaweza kusababisha kifo cha ghafla kuliko dhambi nyingine zote..
1 Wakorintho 6: 18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Na dhambi nyingine ambazo ni mbaya zinazopelekea kuharibu mwili ni Ulevi, uvutaji sigara, matumizi ya madawa ya kulevya na matumizi ya vipodozi na utoboaji mwili.
Kama uliyafanya hayo pasipo kujua, na ulikuwa hujui kuwa mwili huo ulionao sio mali yako, basi hii ndio nafasi yako ya kutubu, unatubu na kumwambia Bwana hutaki tena hayo mambo na hivyo unataka kutimiza kusudi lake alilolikusudia juu ya mwili wako, baada ya kutubu katafute ubatizo sahihi popote pale, kama hujafanya hivyo, ubatizo sahihi ni wa umuhimu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako (Matendo 2:38) na ubatizo sahihi ni wa kuzama mwili wote katika maji na kwa jina la Yesu, na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa Roho Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia. Hakuna mtu awezaye kushinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe, wote tunamtegemea Roho Mtakatifu kutuwezesha, hivyo Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana baada tu ya kumwamini na kubatizwa, maana yeye ndio Muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30)
Bwana akubariki.
WEWE NI HEKALU LA MUNGU.
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
Rudi Nyumbani:
Moja ya Wafalme 19 waliopitia Yuda, na Wafalme 20 waliopita Israeli, enzi zile wafalme, tukiachilia wale wafalme watatu ambao waliitawala Israeli kabla ya kugawanyika yaani (Sauli, Daudi, na Sulemani)..Ni mfalme mmoja tu ambaye kuzaliwa kwakwe kulitabiriwa kwa namna ya ajabu sana, na mfalme huyu alijulikana kama mfalme Yosia,.
Mwanzoni kabisa wa ufalme kugawanyika, ambao tunajua ulisababishwa na kosa la Sulemani, la kuweka miungu migeni Israeli, Mungu alikasirishwa hadi kufikia hatua ya kutaka kumnyang’anya ufalme wote lakini kwasababu ya viapo ambavyo Mungu alimwahidia Daudi baba yake kuwa hatakosa mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli milele(2Nyakati 6:16),hivyo Mungu akambakishia Daudi kabila moja , yaani kabila la Yuda, na la Benyamini kama msindikizaji wake.
Lakini mengine yote kumi, alimgawia mtu mwingine ambaye alikuwa ni mtumwa wa Sulemani aliyeitwa Yeroboamu, ikiwa hujapata uchambizi wa vitabu vya wafalme, bofya hapa..⏩Vitabu vya biblia
Sasa siku ile Yeroboamu anaahidiwa ufalme huo Mungu alimwambia maneno haya:
1Wafalme 11:38 “Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli. 39 Tena nitawatesa wazao wa Daudi kwa sababu hii, lakini si daima”.
1Wafalme 11:38 “Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli.
39 Tena nitawatesa wazao wa Daudi kwa sababu hii, lakini si daima”.
Lakini kama tunavyosoma, huyu mfalme japo alijua kuwa ufalme umekuja kwake kwa kosa la Sanamu za Sulemani, yeye hakulitia hilo moyoni mwake badala yake, akawa mbaya kuliko hata Sulemani, na kiongozi yoyote ambaye alishawahi kutokea Israeli, alileta giza kubwa Israeli ambalo kuondoka kwake iligharimu miaka zaidi ya 400, ni huyu Yeroboamu…yeye alijenga madhabahu za ng’ombe kaskazini na kusini mwa ufalme wake, ili kuzuia watu wasiende kuabudu Yerusalemu kwenye Hekalu la Sulemani, mahali ambapo Mungu alipachagua mambo ya ibada yafanyike, hakuishia kuwazuia tu watu wasiende kuabudu bali akatunga mpaka na sikukuu zake mwenyewe za miezi yake mwenyewe ya kuabudu, hivyo kwasababu yeye ndiye aliyekuwa mfalme basi watu wote walimtii na kumfuata..
Sasa sikumoja wakati amekaa katika dhabihu ya jioni, anaifukuzia uvumba miungu yake, Nabii wa Mungu alitokea palepale kama tunavyosoma katika kitabu cha 1 Wafalme..
1 WAFALME: MLANGO 13
1 “Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. 2 Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, JINA LAKE YOSIA; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. 3 Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika. 4 Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. 5 Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana”.
1 “Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.
2 Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, JINA LAKE YOSIA; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
3 Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.
4 Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena.
5 Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana”.
Huyu nabii alipomaliza kutoa Ishara ile akaondoka zake,..Lakini maneno yale yalisikiwa sio tu na wale waliokuwa pale, bali pia habari ile ilivuma Israeli yote, kwamba kuna mtoto atazaliwa naye ataitwa YOSIA ndiye atakayekuwa na ujasiri wa kuja kuibomoa madhabahu hiyo ya ndama iliyopo Betheli karibu na Yerusalemu, na nyingine zote, ziliyosimamishwa na Yeroboamu,..Na hatazaliwa katika Israeli ufalme wake, bali atazaliwa katika YUDA ufalme wa Daudi..
Basi pengine ilidhaniwa jambo hilo lingetokea kwa mzao aliyefuata wa mfalme wa Yuda aliyekuwa anatawala kipindi hicho, aliyeitwa Rehoboamu, lakini hakuwa huyo, wakatazamia pengine mjukuu wake, bado hakuwa huyo, wakatazamia pengine atakayefuata baada ya huyo bado haikuwa hivyo. Leo hii tukiona unabii wa Mungu unachelewa ni rahisi kusema mtu huyu si wa Mungu, hata kama Mungu alilithibitisha hilo kwa ishara kubwa kiasi gani, kitendo tu cha unabii kuchelewa basi tayari tunahitimisha kuwa yule ni nabii wa uongo….
Siku zikapita hivyo hivyo mpaka kikanyanyuka kizazi kingine kisichowajua manabii hao, Na siku zilivyokuwa zinazidi kwenda ndivyo uovu ulivyokuwa unashamiri katika Taifa ya Israeli na Yuda, mpaka enzi za mfalme Ahabu, lakini bado huyo Yosia hajulikani,..Watu wa kejeli walikuwepo, kama tu walivyo wengi sasa hivi, wanaosema huyo YESU aliyesema anarudi yupo wapi?. Wafalme 20 ishirini walipita juu ya Israeli, Yosia bado hajazaliwa…Mpaka taifa nzima linaondolewa na kuchukuliwa utumwani Ashuru, bado Yosia hajazaliwa, hapo ndipo unabii wa namna hiyo unathibitika kuwa ni batili, kwani mpaka taifa halipo tena hakuna chochote kinachoweza kutokea, hata akizaliwa leo atakuwa na faida gani…Lakini siku zilizidi kuendelea..
Miaka kama 300 baadaye tangu unabii ulipotolewa, wakati taifa la Yuda peke ndio liliobakia Israeli, mfalme mmoja aliyejulikana kama mfalme Amoni, akamzaa mtoto akamwita jina lake Yosia, mtoto huyu katika umri wa miaka 15 alianza kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii sana, na alipofika umri wa miaka 19, alianza kusafisha, madhabahu zote za mabaali na maashera na mahali pa juu, ambazo baba zake walishindwa kufanya,.kwa muda miaka yote hiyo, alizifanya kuwa vumbi, yaani hakuacha sanamu yoyote katika Yuda, isitoshe hakuishia hapo alipanda mpaka kule Israeli ambapo sio hiyama yake, akasafisha kila madhabahu ya mabaali aliyokutana nayo njiani, aliipondoponda na kuiichoma, na alikuwa haondoki mpaka ahakikishe imekuwa jivu, akawaua wapunga pepo wote, na makuhani wao, vile vile akafukua makaburi ya makuhani wao waliokuwa wanaifukizia uvumba zamani, moja baada ya lingine, na kutoa mifupa yao, na kuisagasaga
Mpaka alipofikia kwenye kaburi moja lililokuwa kando-kando ya madhabahu zile, akaliona limekewa kumbukumbu juu yake, akaisoma, akasema hii ni kumbukumbu ya nani?..ndipo akaambiwa, hebu tusome ili tuelewe vizuri..
2 Wafalme 23:17 “Kisha akasema, Ni kumbukumbu la nani, hili ninaloliona? Na watu wa mji wakamwambia, Ni kaburi la yule mtu wa Mungu, aliyetoka Yuda, akayanena mambo hayo uliyoyatenda wewe juu ya madhabahu ya Betheli. 18 Akasema, Mwacheni; mtu awaye yote asiiondoe mifupa yake. Basi wakaiacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya yule nabii aliyetoka Samaria.”
2 Wafalme 23:17 “Kisha akasema, Ni kumbukumbu la nani, hili ninaloliona? Na watu wa mji wakamwambia, Ni kaburi la yule mtu wa Mungu, aliyetoka Yuda, akayanena mambo hayo uliyoyatenda wewe juu ya madhabahu ya Betheli.
18 Akasema, Mwacheni; mtu awaye yote asiiondoe mifupa yake. Basi wakaiacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya yule nabii aliyetoka Samaria.”
Ndipo hapo Israeli yote ikajua kumbe huyu ndiye aliyetabiriwa vile vile zamani, na Yosia akagundua kumbe Mungu alishauona wema wake tangu zamani, na kumwekea kumbukumbuku lake. Haleluya. Maandiko yanatuambia hakukuwa na mfalme aliyemwelekea Mungu kwa moyo wake wote kama ilivyokuwa kwa Yosia, Alimfanyia Mungu sherehe kubwa ambayo haikuwahi kufanywa Israeli tangu enzi za wafalme, isitoshe alikwenda kulikarabati hekalu la Mungu ambalo lilikuwa limechakazwa na wafalme waliotangulia.
2Wafalme 23:25 “Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.”
Ndugu kanuni ya Mungu ni ile ile wala hana upendeleo biblia inasema, Mungu huwapa thawabu wale wote wamtafutao kwa bidii,(Waebrania 11:6), Na wewe pia unaweza ukawa YOSIA ya KRISTO leo, ikiwa tu utataka kumwelekea Mungu kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote bila kujali dini yako inaamini hiki au uamini hiki, ndugu zako wanasema hivi au hawasemi hivi. Ukianza leo hakika kumbukumbu lako Bwana alishaliweka, kama hutalifahamu leo hii basi utafahamu siku ile unayomalizia mwendo kama vile YOSIA. Utakuja kugundua kuwa Mungu alishaziandika thawabu zako kabla hata hujazaliwa, kama ilivyo kwa Yosia, Hivyo habari ya Yosia ni habari ya kutupa moyo kukaza mwendo kwasababu Mungu anaijua hatima yetu na kazi zetu na bidi zetu kabla hata hatujazaliwa..
Na pia habari hii inatufundisha kuwa unabii wa Mungu alioutoa ni lazima uje kutimia haijalishi utachukua miaka mingapi, lakini ni lazima uje kutimia, hapa ulitolewa lakini ulikuja kutimia baada ya miaka 300, wakati ambao watu hawatazamii kama ungekuja kutimia, kadhalika Yesu alisema atarudi…hakika atarudi, na wala hadanganyi…Unabii huo upo karibuni sana kutimia, inaweza ikawa ni leo. Je! Umeokolewa? Wewe utakuwa ni miongoni mwa watakaoenda naye?
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
LAANA YA YERIKO.
MFALME ANAKUJA.
NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).
NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:
Tukisoma katika biblia mahali pengine Bwana alijitambulisha kama ALFA na OMEGA.
Ufunuo 22: 12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Hapo kuna vitu vitatu…1) Yeye ni Alfa na Omega…2) Yeye ni mwanzo na mwisho….3) Yeye ni wa kwanza na wa mwisho.
Hizo ni sentensi tatu zinazoelezea maumbile ya Mungu. Hebu tuzitame kwa ufupi moja baada ya nyingine.
ALFA NA OMEGA:
Tafsiri ya Alfa na Omega sio mwanzo na mwisho, kama inavyofahamika na wengi…ingekuwa ndiyo tafsiri yake hiyo, visingetenganishwa vitu vitatu hapo juu…Sasa Afla ni herufi ya kwanza kwenye alfabeti za Kingiriki..yenye alama hii (α) Na Omega ni herufi ya mwisho ya kwenye alfabeti za lugha ya kigiriki yenye alama hii (ω)…Kwenye alfabeti zetu sisi herufi ya kwanza ni (A) na ya mwisho ni (Z)….kwa kigiriki ya kwanza ndiyo hiyo alfa na ya mwisho ni omega.
Kwahiyo katika mstari huo aliposema yeye ni alfa na omega, alikuwa anajitambulisha uungu wake katika umbo la NENO. (Kumbuka hapo mwanzo kulikuwako Neno….naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa ni Mungu,…Vitu vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakuna chochote kilichofanyika Yohana 1:1).
Kwahiyo akiwa katika Neno, yeye ndiye Neno la Kwanza na ndiye Neno la Mwisho, kwahiyo ili lijitambulishe lazima litumie Herufi kujitambulisha, (herufi ya kwanza na ya mwisho, alfa na Omega)… Kwanini hakutumia herufi ya A na Z?..ni kwasababu lugha zinazotumia alfabeti hizi kama vile kiingereza zilikuwa hazijazaliwa bado, na hata kama zingekuwa zimeshazaliwa bado zilikuwa ni lugha changa, kwani wakati Yohana anapewa haya maono lugha iliyokuwa kuu na uliyozungumzwa sehemu kubwa ya dunia ilikuwa ni kigiriki, hata lugha iliyotumika kuandika vitabu vingi vya agano jipya ni lugha hii, ndio maana yakatumika maneno ya kigiriki.
Yeye ni MWANZO NA MWISHO:
Sifa ya pili, Hapa Mungu anajitambulisha kwa umbo la MUDA….
Kama alivyosema mahali Fulani yeye ni UPENDO, na sio yeye ana upendo…kadhalika hapa, anajitambulisha kuwa yeye ni MWANZO na sio yeye ana mwanzo!..halikadhalika yeye ndiye MWISHO, na sio yeye mwenye mwisho…yeye hana mwanzo na wala hana mwisho, kwasababu yeye ndio mwanzo wenyewe na ndio mwisho wenyewe.
Ili uelewe vizuri hebu tafakari jambo hili: umewahi kuchunguza mwanzo wa magharibi ni upi? Au mwisho wa magharibi ni upi?…au mwanzo wa mashariki ni upi na mwisho wake ni upi?..utakuja kugundua kuwa mashariki haina mwanzo wake wala mwisho wake, vivyo hivyo na magharibi haina mwanzo wala haina mwisho, kwasababu mahali ulipo tayari panaweza kuwa ni mashariki ya mbali sana kwa sehemu nyingine halikadhalika panaweza kuwa ni magharibi ya mbali sana kutoka sehemu nyingine…kwahiyo hapo ulipo tayari ni mwanzo na mwisho wa magharibi na mashariki. Kuna mstari wanaouita kitaalamu IDL huo ndio wanasema umetenganisha mashariki na magharibi lakini kiuhalisia hakuna mstari pale…Wamebuni tu, ili kuwarahisishia kutimiza matakwa yao ya kijeografia, lakini hakuna mwanzo wa mashariki wala magharibi, ingawa kuna mashariki na magharibi..
Na ndio Mungu yupo hivyo hivyo, ingawa kuna kitu kinaitwa MWANZO na Mwisho, lakini yeye hana mwanzo, wala hana mwisho……kwasababu yeye pale alipo ndio mwanzo na ndio mwisho….Na kama vile tunavyozidi kuelekea sana mwisho wa mashariki ndivyo tunavyojikuta tunatokea mwanzo wa mashariki hiyo hiyo…kadhalika na Mungu…tunapodhani tunamjua sana na hivyo tumefika karibia na mwisho wa kumjua yeye…kumbe ndio tupo mwanzo wa kumjua yeye….Na pale tunapodhani yupo mbali sana na sisi kumbe ndio yupo karibu sana na sisi, na pale tudhaniapo kuwa tumemkaribia sana, kumbe bado sana tumfikie..Kwasababu yeye ndio mwanzo na ndio mwisho, akili zake hazichunguziki, wala hakuna mtu anayeweza kumwelezea asilimia mia na kusema sasa nimemjua Mungu.
Isaya 40:28 “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.”
Yeye ni WA KWANZA NA WA MWISHO:
Sifa ya tatu na ya mwisho, Hapa Mungu anajifunua na kujitambulisha katika umbo la mtu…Lile Neno lililojitambulisha kwa herufi alfa na Omega, sasa linavaa mwili na kujitambulisha kama Mtu, na kusema Yeye ni wa Kwanza na wa Mwisho.
Hapa anaelezea Uungu wake kabla ya vitu vyote..Yeye alikuwepo kabla ya kiumbe chochote kile…kabla ya Malaika na kitu kingine chochote…ndiye wa Kwanza, akaitoa sehemu ya roho yake akatuumba sisi wanadamu na malaika…Na hivyo sisi wote tumetoka kwake…Na mwisho wa siku tutarudi kwake..kwasababu yote yametoka kwake..
Mungu wetu hakuna linalomshinda, wala hakuna asilolijua, utasemaje leo hakujui, wala hajui unayopitia?..huyu mwanzo na mwisho utasemaje kakusahau?..hajakusahau alisema “hata nywele za vichwa vyetu zimehesabiwa zote (Luka 12:7)”….kama anajishughulisha na mambo madogo sana ya nywele zetu atashindwaje kujishughulisha na mambo makubwa ya Maisha yetu, Hivyo kuna baraka nyingi sana katika kumwamini huyu Mungu.
Lakini pia huyu Mungu ni alfa na Omega, maneno yake ndio mwanzo na mwisho, akisema Neno lake ni lazima litimie, na halirekebishwi wala halina marekebisho…limehakikiwa na limejitosheleza, akisema roho itendayo dhambi itakufa…ni kweli itakufa, akisema mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuurithi ufalme wa mbinguni…maneno yake hayo ni alfa na Omega..yatatimia kama yalivyo, akisema atakuja ni kweli atakuja..
Hivyo mpaka sasa bado anawaalika watu karamuni, je! Wewe ni mmoja wao wa walioalikwa?..kama bado unasubiri nini, usigeuke leo na kutubu? Siku ile utakuwa mgeni wa nani utakapojikuta upo kuzimu?..kumbuka hakuna nafasi ya pili kwa mtu yeyote atakayekufa katika dhambi leo,..wengi wanajifariji kuwa mbele ya kiti cha hukumu watakuwa na hoja za kujitetea, nataka nikuambie siku ile kutakuwa hakuna kujitetea…Kwasababu hakuna yeyote awezaye kumtega wala kumkamata Mungu kwa maneno.
Pia kwa Mawasiliano, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa +225693036618/ +225789001312
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
Kutoka 34:29 “Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling’aa kwa sababu amesema naye. 30 Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling’aa; nao wakaogopa kumkaribia. 31 Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao. 32 Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo Bwana amemwambia katika mlima Sinai. 33 Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake. 34 Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za Bwana kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa. 35 Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling’aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.”.
Kutoka 34:29 “Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling’aa kwa sababu amesema naye.
30 Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling’aa; nao wakaogopa kumkaribia.
31 Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao.
32 Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo Bwana amemwambia katika mlima Sinai.
33 Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake.
34 Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za Bwana kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa.
35 Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling’aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.”.
Itakuwa hata wewe ulishawahi kugundua kitu hichi mfano ukikaa karibu na mtu ambaye amejipulizia marashi makali kwa muda mrefu, halafu ukaondoka utagundua kuwa vimelea vya yale marashi kwa sehemu Fulani vimebaki kwenye mwili wako,..Na ndivyo ilivyokuwa kuwa kwa Musa, baada ya kukaa uweponi mwa Mungu kwa muda wa siku nyingi, siku zaidi ya 80, ukijumlisha na zile 40 za Kwanza, alizokwenda kupewa amri na hukumu na zile mbao 2 za mawe, kwa wakati huo wote alipokuwa uweponi mwa Mungu kumbe kidogo kidogo utukufu wa Mungu ulikuwa unajiambukiza ndani yake pasipo yeye kujijua..Hadi siku aliposhuka chini na kuona watu wanamwogopa ndipo alipogundua kuwa Uso wake uling’aa sana kwa kule kumtazama Mungu.
Japo biblia haituambii ulikuwa unang’aa kwa namna gani hadi watu kumwogopa, lakini tunajua uling’aa kwa utukufu wa Mungu, pengine ulikuwa unameta meta kama almasi, mpaka watu wakaona huyu anaweza akawa asiwe mtu wa kawaida, pengine tukimgusa tunaweza tukafa..Ndipo Musa alipoona hivyo, akachukua utaji akaufunika uso wake, kupunguza makali ya utukufu ule, ili aweze kusimama mbele ya watu na kungumza nao.
Lakini japo uso wake uling’aa sana kwa namna ile, bado utukufu ule ulikuwa sio wa kudumu, kwasababu ulikuwa na wa kuhakisi tu, na sio kitu kilichotoka ndani yake, hivyo alipoondoka katika uwepo wa Mungu, kidogo kidogo ulikuwa unapungua hadi mwishowe ukatoweka kabisa…Japo biblia haituambii ni kwa kipindi gani utukufu huo ulidumu kwenye uso wake, pengine ulichukua siku, au wiki, au mwezi, au miezi, hatujui, lakini tunachojua ni kuwa ulikuwa ni utukufu usiodumu…Ulihitaji kuu-chaji, Na ndio maana ukisoma hapo juu utaona kila wakati Musa alipotoka kuzungumza na Mungu aliuvaa utaji ule, kwasababu utukufu wa Mungu ulijiakisi kwenye uso wake tena kwa wakati huo.
Hivyo ule utaji uliwazuia wana wa Israeli kuona hatma ya ule utukufu jinsi unavyokwisha, kwasababu Musa alikuwa anavaa utaji muda wote, Na ndio maana mtume Paulo, aliandika katika 2Wakorintho 3:13-16, kuwa hata leo hii wana wa Israeli utaji huo upo mbele yao, kwamba hawawezi kuona jinsi utukufu wake Torati ya Musa usivyokuwa wa kudumu..
“13 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; 14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; 15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. 16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.”
“13 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;
14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo;
15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.
16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.”
Swali linakuja je! mwanadamu afanye nini ili awe na utukufu usio batilika kutoka kwa Mungu? Apate Utukufu unaodumu wakati wote?.
Jibu lipo pale pale juu, tunapaswa tusiuakisi utukufu wa Mungu, bali tugeuzwe tuwe kama yeye. Hiyo ndio dawa pekee. Kwa kuelewa zaidi angalia mfano wa mwezi na nyota, utagundua kuwa nyota siku zote zinaangaza tu, huwezi kuta zinaonekana nusu, lakini mwezi, leo utauona unaonekana wote, kesho nusu, kesho kutwa theluthi, ni kwasababu gani?, ni kwasababu wenyewe unategemea mwanga wa jua kuangaza, unalihakisi jua, lakini nyota hazihakishi chochote kutoka katika jua kwani watafiti wanasema Nyota ni ma-jua mengine, isipokuwa tu yapo mbali na dunia na ndio maana kuangaza kwa nyota hakubadiliki badiliki.
Vivyo hivyo, ili sisi tuangaze utukufu kamili wa Mungu, tunapaswa tuguezwe tuwe miungu duniani, na anayeweza kufanya hii kazi si mwingine zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe.
Pale tunapoiamini injili kweli kweli kwa kudhamiria kumwishia Mungu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi, tunapotubu dhambi zetu, kuanzia hapo Kristo anachofanya ni kutubadilisha asili zetu, na kuwa kama Mungu,..kuanzia huo wakati utukufu wa Mungu unakuwa unamulika ndani yetu milele NON-STOP..Kazi yako itakuwa ni kujiweka mbele zake katika hali ya utakatifu na usafi zaidi, na kulitii Neno lake, ili uzidi kuangaza kwa utukufu mwingi zaidi, hapo ndipo unapokuwa kutoka utukufu hadi utukufu, kwasababu kumbuka hata nyota zinatofautiana utukufu(1Wakorintho 15:41)..Isipokuwa tu utukufu wa zote hauwezi kuisha kabisa kama mwezi, kwasababu tayari ndani yao kuna Nuru ya jua, lakini ni wajibu wa kila mwaminio, atoke utukufu hadi utukufu.
2 Wakorintho 3:7 “Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika; 8 je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? 9 Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 10 Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. 11 Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu. 12 Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; 13 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; 14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; 15 ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. 16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. 17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, TUNABADILISHWA TUFANANE NA MFANO UO HUO, TOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho”.
2 Wakorintho 3:7 “Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;
8 je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?
9 Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi.
10 Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana.
11 Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.
12 Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;
13 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika;
16 Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.
17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, TUNABADILISHWA TUFANANE NA MFANO UO HUO, TOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho”.
Unaona ni faida gani, mtu aliyonayo aliyedhamiria kweli kumwamini Kristo, na sio kigeugeu,? Mtu wa namna hii hata katika ulimwengu wa roho mashetani na mapepo wanachokiona ni miale ya moto tu inapita, uchawi utampatae mtu kama huyo? Au LAANA?. Na ndio maana Shetani anachofanya sasa katika hichi kipindi cha mwisho ni kupofusha tu fikra za watu wapuuzie mambo haya ya msingi:
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, ISIWAZUKIE NURU YA INJILI YA UTUKUFU WAKE KRISTO ALIYE SURA YAKE MUNGU.”
2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, ISIWAZUKIE NURU YA INJILI YA UTUKUFU WAKE KRISTO ALIYE SURA YAKE MUNGU.”
Mfikirie Kristo kwa jicho lingine, Yule huwa akimbadilisha mtu, anambadilisha kweli kweli, hasemi uongo kama sisi wanadamu tulivyo, Hakuja kufanya kazi ya kubahatisha duniani, kazi yake ni thabiti kabisa.
Kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +255789001312
DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.
MADHAIFU
WATU WASIOJIZUIA.
UNAFANYA NINI HAPO?
Karibu katika mwendelezo wa vitabu vya Biblia, leo tutaendele na vitabu 4 vya mbele, yaani Wafalme wa kwanza (1Wafalme), na Wafalme wa Pili (2Wafalme), Mambo ya nyakati wa kwanza (1Nyakati) na Mambo ya nyakati wa pili(2 Nyakati).. Tumekwisha pitia vitabu 10 vya kwanza, hivyo ni vizuri kama hujapitia maelezo ya vitabu vilivyopita, ukavipitia kwanza ili tuende pamoja katika hivi vitabu vinavyofuata.
Kitabu cha Wafalme wa kwanza na Wafalme wa Pili, kilikuwa ni kitabu kimoja, isipokuwa kiligawanywa katika sehemu mbili…Na mwandishi wa kitabu hichi alikuwa ni Nabii Yeremia. Ingawa Nabii Yeremia alizaliwa mwishoni kabisa mwa enzi za Wafalme lakini aliweza kukusanya rekodi zote za habari za Wafalme, kwani habari za kila mfalme na matendo yake zilikuwa zinarekodiwa na kuhifadhiwa kwenye vitabu maalumu vinavyojulikana kama vitabu vya Tarehe.
Lakini kwa ufupi Kitabu hivi viwili vya wafalme kama jina lake lilivyo, vinazungumzia Utawala wa wafalme wa Israeli, Na vitabu viwili vinavyofuata vya (1 Nyakati na 2 Nyakati) Ni marudio ya habari hizo hizo za Wafalme isipokuwa yana habari chache chache sana ambazo hazikurekodiwa katika kitabu cha wafalme…Ni sawa na injili iliyoandikwa na Mathayo na Luka ni vitabu viwili vilivyoandikwa na waandishi wawili tofauti lakini vyote vinazungumzia habari moja..ndivyo ilivyo kitabu cha Wafalme na Mambo ya nyakati, vyote vinaelezea habari moja za Wafalme wa Israeli…isipokuwa hichi cha mambo ya nyakati kimeanzia nyuma kidogo, kwa mfalme Daudi. Na mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati alikuwa ni EZRA..ambaye ndiye aliyekiandika kitabu cha Ezra pia..Huyu alikuwa ni mwandishi..ambaye habari zake tutakuja kuziona tutakapofika katika kitabu cha Ezra..
Sasa tukirudi katika habari za Wafalme..kumbuka haukuwa mpango wa Mungu, Israeli wawe na Mfalme juu yao tangu mwanzo, lakini kwasababu ndio ilikuwa nia yao kukataa uongozi wa Mungu, usiohusisha mwanadamu, Mungu akawapa haja ya mioyo yao, lakini pamoja na hayo hakuwaacha…tofauti na sisi wanadamu, mtu asipofanya tunavyotaka tunamtupa moja kwa moja, hatutaki hata kumsikia tena, lakini kwa Mungu haipo hivyo, hakuwatupa Israeli watu wake moja kwa moja ingawa walimuasi…Hivyo Mungu akatengeneza njia ya kuwaokoa kwa kupitia hao hao wafalme waliowataka…
Kwahiyo kitabu cha Wafalme wa Kwanza, kinaanza na Mfalme Sulemani, ambaye alikuwa ni mfalme wa tatu wa Israeli akitanguliwa na Sauli na Daudi ambao habari zao utazipata katika vitabu vya Samweli. Sulemani alikuwa ni mwana wa Daudi, na mama yake alikuwa ni yule mke wa Uria, ambaye Daudi aliyemtamani..Hivyo baadaye Mungu alikuja kumfanyia wema mwanamke yule na kumfanya mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli, Sulemani alitawala miaka 40 katika Israeli, alianza vizuri lakini hakumaliza vizuri, kwani pamoja na Hekima yote na ufahari wote aliopewa na Mungu alikuja kukengeuka dakika za mwisho, na kwenda kuoa wanawake wa kigeni, ambao Mungu alimkataza asioe, (Nehemia 13:25-26 )na hao wanawake wakamgeuza moyo akaenda kutengenezea maashera hiyo miungu migeni, ambayo ni machafuko makubwa sana mbele za Mungu, Ingawa alikuja kutubu dakika za mwisho, na Bwana alimsamehe lakini tayari alikuwa ameshaisababishia Israeli madhara makubwa sana..
Sasa kabla ya kwenda kwenye madhara aliyoisababishia Israeli, tutazame jambo moja jema na kuu alilolifanya.; Tunaona baada ya kufa baba yake, yeye ndiye aliyekuwa na dhamana ya kumtengenezea Mungu nyumba, biblia inasema Mungu hakai kwenye nyumba zilizotengenezwa na mikono, lakini pamoja na Daudi kulifahamu hilo bado alilazimisha kumjengea Mungu nyumba hivyo hivyo, na Mungu akaliona hilo akapendezwa naye na kumbariki, na kuuchagua mji wake na kabila lake kuwa makao makuu ya kuweka jina lake, japo Mungu alimzuia Daudi asimjengee kwasababu alimwaga damu nyingi, hivyo mwanawe ambaye ni Sulemani ndiye atakayejenga HEKALU kwa niaba yake. Na wakati ulipowadia Sulemani alimjengea Mungu hekalu, alitumia akili nyingi, na hekima nyingi kuijenga ile nyumba…
Alikwenda kutafuta miti maalum na ya thamani kutoka nchi za mbali, na vito maalumu kutoka kila kona ya dunia, na kuileta Israeli, Zaidi alikwenda kutafuta watu wenye akili nyingi, kutoka mataifa mengine kusaidia kuongeza ujuzi katika ujenzi, kwahiyo Hekalu lilijengwa kwa gharama kubwa na kwa ujuzi wa hali ya juu, kulikuwa hakuna mfano wake duniani kote. Na lilitengenezwa Yerusalemu, katika mji wa kabila la Yuda, hakukusikika kelele yoyote wakati wa ujenzi, hivyo ilipunguza hata kasi ya maadui, kuvamia kwasababu hakuna mtu aliyekuwa anaelewa kitu kinachoendelea ndani..wengi walidhani kazi imesimama tu!..lakini ilikuwa inaendelea ndani kwa ndani…ghafla wanakuja kushangaa nyumba hii hapa imekamilika!..Sasa inawekwa wakfu kwa Mungu.
Mungu akalibariki Taifa la Israeli na Mfalme, kwa jambo hilo, na kukawa na amani kwa Zaidi ya miaka 40, lakini Sulemani alipokuwa mzee akakengeuka, na hivyo Mungu hakupendezwa naye tena, hakumwua lakini alimnyang’anya sehemu ya Ufalme wake, kwani hapo kwanza alikuwa anatawala makabila yote 12, kama Sauli na Daudi walivyokuwa wanatawala, lakini matokeo yake akapokonywa 10 akabakiwa na mawili tu, yaani kabila la Benyamini pamoja na kabila lake mwenyewe Yuda…lakini hakunyakang’anywa kwenye utawala wake bali wa mwanae.
1 Wafalme 11:1 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, 10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana. 11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. 12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. 13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua”
1 Wafalme 11:1 “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.
4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.
8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.
9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,
10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.
11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.
12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.
13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua”
Hivyo hayo yote yalitokea wakati wa utawala wa mtoto wake Rehoboamu, na kuanzia huo wakati Israeli ikagawanyika sehemu mbili, kaskazini na kusini, upande wa kusini ndio huo uliokuwa na makabila mawaili (yaani Yuda na Benyamini) na upande wa kaskazini (makabila 10 yaliyosalia). Hivyo kaskazini wakawa na mfalme wao na Kusini wakawa na Mfalme wao…
Kaskazini PAKAITWA ISRAELI na kusini PAKAITWA YUDA. Hivyo Israeli ambayo hapo kwanza ilikuwa ni taifa moja ikagawanyika na kuwa mataifa mawili ndani ya Taifa moja…kutokana na dhambi ya Sulemani.
Hayo ndio madhara ya dhambi aliyoyaleta Sulemani, na ndio madhara ya dhambi, unaweza ukasema nikitenda dhambi fulani itaniathiri mimi peke yangu, haitawahusu wengine, nataka nikuambie ndugu, ukiwa mwamini ukifanya dhambi yoyote ya makusudi haitakuathiri wewe peke yako bali itaathiri na wengine na Zaidi ya yote itaathiri kazi ya Mungu, kwasababu jina la Mungu litatukanwa kwa ajili yako.
Baada tu ya Israeli kugawanyika katika sehemu hizo mbili, hapo ndio ikawa sehemu nyingine ya chanzo cha machafuko, watu waliokuwa wanakaa kaskazini (yaani yale makabila 10) yakaacha kabisa kumcha Mungu wa Israeli kama hapo kwanza kwasababu mfalme wao wa kwanza anayeitwa Yeroboamu aliwatengenezea sanamu ya ndama, waiabudu kama Mungu wao badala ya Mungu wa Israeli..hivyo ikawa ni machafuko makubwa zaidi, wakawa hawana tofauti na watu wa Mataifa.
Na yale makabila mawili yaliyosalia ambayo yalikuwa kusini angalau kidogo watu waliokuwa wanakaa kule walikuwa wanamwogopa Mungu ingawa si sana, na walikuwa wanamcha Mungu kwasababu tu Hekalu la Mungu lilikuwa huko nchini kwao Yuda, hiyo kidogo ikawafanya wawe na hofu ya Mungu. Lakini na wao pia wakaja kukengeuka baadaye…Hivyo mataifa haya mawili ndani Taifa moja yakawa na kila moja na mfalme wake, na itikadi zake, ingawa walikuwa wanatambuana kama ndugu, na hakukuwa na Mfalme mmoja kwa mataifa yote mawili, hapana kila moja lilikuwa na mfalme wake kuanzia huo wakati na kuendelea.
Walipita Wafalme karibia 20 katika Israeli ( yaani upande wa kaskazini)…lakini wote walifanya machukizo mbele za Mungu, kila aliyekuja alikuwa anafanya mabaya kuliko aliyemtangulia…Na miongoni mwa wafalme waliofanya mabaya sana ni Mfalme Ahabu ambaye alikuwa na mke wake aliyemtoa nchi za mataifa, ambaye alikuwa ni mchawi, aliyeitwa Yezebeli, hawa waliichafua Israelli kwa kiwango cha juu sana…Mpaka ikafika kipindi Bwana akaileta huduma ya Eliya duniani, na lengo la huduma ya Eliya ilikuwa ni KUWAREJESHA WANA WA ISRAELI WAMRUDIE MUNGU WAO. Mungu alitumia ishara nyingi katika huduma ya Eliya ili kuwarejesha wamgeukie yeye…(kwa maelezo marefu juu ya huduma hii ya Eliya tutumie ujumbe inbox tukutumie )…wachache wakawa wanatii na kugeuka lakini wengi wakawa hawatii..
Na katika Yuda pia walikuwa wanatumiwa manabii wengi, lakini angalau Yuda kidogo watu walikuwa si wagumu kama Israeli..Kwani kulikuwa kuna Wafalme katika Yuda ambao walikuwa wanamtii Mungu na kumheshimu kama alivyofanya Daudi, mfano wa wafalme hao alikuwepo mfalme Hezekia, na Mfalme Yosia hawa walikwenda katika njia za Mungu katika ukamilifu wote, hivyo katika vipindi vya utawala wao Mungu aliwabariki na kuwaepushia madhara,… Manabii wote tunaowasoma katika Biblia, kuanzia Eliya, Elisha, Habakuki, Isaya, Hosea, Nahumu, Yona, Amosi, Yeremia, Obadia, Habakuki, Mika n.k wote hawa walitokea kipindi hichi cha Wafalme kasoro nabii Danieli, Hegai, zekaria pamoja na Malaki hawa walitokea baada ya Isreali kutawanyishwa…
lakini hao wengine Walikuwa wanatumwa kuwaonya wana wa Israeli na wana wa Yuda pamoja na wafalme wao wamgeukie Mungu…Unapopitia kitabu hichi ili upate picha vizuri, ni vyema ukapitia pia vitabu vya manabii, uone Bwana alivyokuwa anawaonya Israeli kwa nguvu, na jinsi gani alivyokuwa anawatabiria kuwa watakwenda utumwani Babeli wasipotubu..Kwa muda wako soma kitabu cha Yeremia, Hosea, Nahumu, Isaya utayaona mambo hayo kwa urefu, …
Kwa miaka mingi Zaidi ya 400, walikuwa wanatumiwa manabii wa kuwarejesha lakini ni wachache tu ndio waliokuwa wanatii na kugeuka, hivyo uvumilivu wa Mungu ukafika kikomo, kukawa hakuna tena msamaha, Mungu akaamua kuwatoa Waisraeli wote kutoka katika nchi yao waliyopewa na Mungu, waliokuwa wanakaa upande wa kaskazini, yaani Israeli (yale makabila 10)..yalichukuliwa utumwani kwenda nchi inayoitwa ASHURU, na wale waliokuwa wanakaa kusini (yaani Yuda) baada ya miaka 125 mbeleni nao pia walichukuliwa na kupelekwa utumwani BABELI,..wao hawakuchukuliwa kipindi kimoja na Israeli kwasababu angalau kwao kulikuwa na hofu ya Mungu kuliko Israeli, lakini baadaye nao pia wakakengeuka kama Israeli na kuchukuliwa mpaka Babeli…Nchi ya Ahadi ikabaki nyeupe!! Wakaletwa makafiri wakaishi huko kwa niaba yao, nchi ya Israeli ikakaliwa na makafiri. Yuda Wakapelekwa utumwani miaka 70..
2 Nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu. 15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu ALIWAHURUMIA WATU WAKE, NA MAKAO YAKE; 16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA. 17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake. 18 Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli. 19 Wakaiteketeza nyumba ya Mungu, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani. 20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi; 21 ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.”
2 Nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu.
15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu ALIWAHURUMIA WATU WAKE, NA MAKAO YAKE;
16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA.
17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake.
18 Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
19 Wakaiteketeza nyumba ya Mungu, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, wakaviharibu vyombo vyake vyote vya thamani.
20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;
21 ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.”
Mstari wa 16, unasema “lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA”.
Ndugu katika vitabu hivi tunajifunza kuwa..kuna wakati unafika ghadhabu ya Mungu, itajaa hata kusiwe na kuponya, wewe unayesema Mungu anakawia, wewe unayedharau na kuidhihaki na kuicheka injili leo, na kuwacheka na kuwafanyia mizaha watu wa Mungu, siku inakuja ambapo utalia na kutakuwa hakuna msaada, siku ya ghadhabu ya Mungu inakuja! Usidanganywe na watu wanaosema kuwa Mungu hawezi kuangamiza dunia, au hakuna mwisho wa dunia, ndugu watu wa kipindi cha Nuhu ndio walikuwa wanasema hivyo hivyo…lakini ghafla tu walishangaa siku moja mbingu zimefunga, zimekuwa nyuesi……Jiepushe na ghadhabu ya Mungu, Uvumilivu wa Mungu ni kukufanya wewe utubu, umgeukie Mungu, tubia uasherati wako, rushwa zako, utukanaji wako, usengenyaji wako, na kutokusamehe kwako…Wema wa Mungu unakuvuta leo kwasababu hataki upotee soma tena mstari wa 15 unasema…
“15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu ALIWAHURUMIA WATU WAKE, NA MAKAO YAKE; ”
Ni mara ngapi asubuhi na mapema umekutana na mahubiri, kwenye redio, kwenye Tv, mitandaoni, mitaani au hata sehemu zako za kazi?..Usipuuze unaposikia injili unayopewa bure pasipo hata kulipia hata sh. Moja..siku ile utakosa cha kujitetea..
Kuna wakati mlango wa rehema utafungwa, ambapo utatamani kutubu utashindwa: Wana wa Israeli walilia na kuomboleza, siku ile wanapochukuliwa mateka, lakini Mungu hakusikia chochote. Ndivyo itakavyokuwa kwa wale wanaochezea neema sasa.
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.”
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno,
mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.”
Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu hapo ulipo kwa kudhamiria kuacha dhambi zako, na kwenda kutafuta ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa mwili wote na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Hakikisha unakisoma vitabu hivi mwenyewe, usiache kipengele hata kimoja, kwasababu ni habari zinazoeleweka na zimewekwa katika mfumo mrahisi wa kueleweka, haihitaji ufafanuzi sana kukielewa. Hapa tunajaribu kukupa picha tu, ili kukusaidia wewe mwenyewe kuvisoma vitabu hivyo kiurahisi, Hivyo tumia muda wako mwingi kuvisoma peke yako, Na Mungu atakufunulia mengi zaidi…
Usikose mwendelezo, na Pia washirikishe wengine habari njema..
Kwa mwendelezo >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
BIDII YA MFALME YOSIA.
KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?
NABII ELISHA ALIKUWA ANA MAANA GANI KULIA NA KUSEMA”GARI LA ISRAELI NA WAPANDA FARASI WAKE”?
ROHO YA ELIYA KATIKA AGANO JIPYA INATENDAJE KAZI?
SAUTI NYUMA YA ISHARA.
KANUNI JUU YA KANUNI.