Title July 2018

JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?

Jibu ni ndio kwasababu biblia inasema pasipo kumwagika damu ya Yesu hakuna ondoleo, ukisoma waebrania 9:22 “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. ”

Hii ndio njia pekee ambayo Mungu aliichagua tangu awali kwamba, ili tendo lolote la rohoni lifanyike na kufanikiwa ni lazima damu ihusishwe, na ndio maana tunaona katika agano la kale ilikuwa kwamba ili mtu apate kibali mbele za Mungu ni lazima aende na sadaka, ambapo mnyama alisiyekuwa na mawaa anachinjwa ili kufanya upatanisho, na mambo yote yanaliyohusishwa na dhambi yalikuwa yanatakaswa kwa damu, hiyo ilikuwa ni kanuni.

Kwahiyo tunaona damu ina mahusiano makubwa kuwa  kama kiunganishi kati ya ulimwengu wa mwilini na wa rohoni, na ndio maana hata shetani kwa kulijua hilo anapenda kutumia damu ili kufanikisha mambo yake maovu katika ulimwengu huu,

Kwamfano mara nyingi wachawi wanawaambia watu wapeleke damu za mnyama fulani ili kufanikisha mambo yao ya kishirikina pamoja na  haja za hao watu, na ukitazama kwa makini utaona kuwa wanapendelea zaidi damu za wanadamu kuliko za wanyama kwasababu wanajua hizo zina mlango mkubwa zaidi wa kuunganisha mambo ya rohoni na ya mwilini kiurahisi. Na ndio maana hao wanaotoa damu za watu utakuta matokeo yao ya kiroho(kichawi) yanakuwa ni makubwa zaidi kuliko wale wanaotoa za wanyama.

Kuna kitu kikubwa sana ndani ya DAMU ambacho mkristo akikitambua hakuna chochote kitakachomsumbua na hakika ataweza kufanya mambo yote, ataweza kufanya yote ya mwilini na ya rohoni, na kama tunavyojua  hiyo damu ili iwe na nguvu ni lazima iwe ya mwanadamu na sio mnyama, tena inatakiwa ipatikane ya mwanadamu asiyekuwa na hila wala mawaa, hakika ikipatikana hiyo ni zaidi ya tambiko lolote ambalo lilishawahi kufanyika duniani!!!

Kumbuka mambo yote yanatoka rohoni, ni ngumu kushindana na watumishi wa shetani ambao wamepata nguvu nyingi za kumkaribia shetani kwa sadaka zao za damu za watu wasio na hatia,halafu  na wewe unataka kwenda kushindana nao pasipo damu yoyote, hapo ni lazima ushindwe tu! ni lazima ujue mbinu za kumshinda adui yako, mambo ya rohoni yana kanuni zake.

Lakini habari njema ni kwamba hii damu yenye nguvu ipitayo damu zote isiyoharibika ambayo inaweza ikashinda mambo yote ipo na inajulikana, na hii si nyingine zaidi ya DAMU YA YESU ambayo haikuwa na hila wala mawaa yoyote. lakini wengi wanashindwa kuielewa matumizi yake, na ndio maana shetani anaendelea kupata nguvu juu yao, 

Jambo shetani analotaka ni waifahamu tu lakini wasiielewe matumizi yake, kila mtu anaifahamu damu ya mwanakondoo lakini ni wachache wanayoielewa, siku utakapoielewa kisawasawa utamshinda shetani kwa kila nyanja.

ukisoma;

Ufunuo 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

11 NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANAKONDOO, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “

Unaona hapo? ni Damu tu ya mwana-kondoo inayoweza kumshinda yule joka ( shetani ) na hakuna kingine chochote. Lakini wengi wanadhani utamshinda kwa  kutamka tu  “nakukemea kwa damu ya Yesu”……akidhani hapo amempata shetani, kumbe hajui hapo hajafanya lolote kama hajaingia ndani ya hilo Agano kwanza. Ni lazima uingie kwanza.

JINSI YA KUINGIA KATIKA HILI AGANO LA DAMU YA YESU.

Kumbuka katika agano la kale kuhani mkuu alipokuwa akienda kila mwaka kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa njia ya damu za wanyama, hakuwa anafanya kwa watu wote wa ulimwengu mzima bali tu kwa wale waliokuwa katika hilo agano yaani wana wa Israeli pekee. Na ndio waliokuwa wanafunikwa dhambi zao na kushiriki baraka zote za rohoni na sio watu  wa ulimwengu mzima.

Vivyo hivyo katika Agano jipya ili maombi yako yasikiwe, ili sadaka zako zikubaliwe, ili dhambi zako zisamehewe, ili uweze kumshinda shetani na magonjwa yake yote na laana ni lazima uingie katika hili Agano jipya la DAMU YA YESU KRISTO. na hauingiii kwa kuzaliwa katika familia ya kikristo, wala hauingii kwa kujiunga na dhehebu fulani, wala hauingii kwa njia nyingine yoyote isipokuwa KWA KUTUBU kwanza, NA KUMWAMINI YESU KRISTO, NA KUBATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kisha upokee ROHO MTAKATIFU hapo ndipo umezaliwa mara ya pili na umeingia katika hili AGANO HILI KUU.

Sasa kuanzia hapo na kuendelea ile damu inaanza kunena kwa ajili yako mbele za Mungu, shetani hana la kukushinda kwa lolote, wala la kukushitaki, kwasababu damu isiyoharibika tayari ipo kunena kwa ajili yako, hauhitaji kupigana na wachawi, wala waganga, wala kuogopa magonjwa au shida, ipo hiyo damu tayari inafanya kazi kuliko tambiko lolote lililowahi kufanyika tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.

Kumbuka shetani anapotaka kuleta laana juu yako jambo la kwanza analoangalia ni je! upo chini ya damu? shetani hawezi kulaani kilichobarikiwa kama vile Balaamu alivyoshindwa kuwalaani wana wa Israeli.

Kwahiyo ndugu hakuna njia nyingine yoyote katika hii dunia unaweza ukamshinda shetani isipokuwa kwanza kutubu, na kumruhusu Yesu Kristo ayasafishe maisha yako kwa damu yake, uchukua uamuzi wa kubatizwa leo kwa ubatizo ulio sahihi wa kuzamishwa na sio wa kunyunyuziwa na iwe ni  kwa jina la YESU KRISTO kulingana na maandiko ( matendo 2:38.), kisha Bwana atakupa Roho Mtakatifu hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuingia katika lile AGANO KUU LA DAMU YA YESU, kwa uhakika wa maisha yako ya sasa na ya baadae, kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wachanga, kama ulifanyiwa hivyo hapo hujabatizwa unapaswa ukabatizwe tena.

Nakukumbusha tena ndugu yangu hauwezi ukamshinda shetani kwa njia nyingine yoyote ile, sio kwa matendo, wala kwa juhudi yako bali kwa damu ya mwana-kondoo pekee. 

Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. “. tubu, kabatizwe na upokee Roho Mtakatifu.

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.

JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?

UBATIZO WA MOTO NI UPI?

JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.


Rudi Nyumbani

Print this post

NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?

Kazi kubwa shetani anayoifanya kwa mkristo kila siku ni kutaka kumwangusha katika imani yake hivyo anatumia njia ya majaribu kumwangamiza, majaribu ni vikwazo, na kuna vikwazo vya aina nyingi katika safari ya ukristo ambavyo shetani lazima avilete na sio kila mtu atakutana navyo bali ni mkristo tu aliyeamua kujitoa kikamilifu na kumfuata YESU KRISTO kwa moyo wake wote.

kwahiyo shetani akishajua umechagua njia hiyo ndipo atakapoanza kuamua kukupepeta kwa njia zozote zile; anaweza akaja aidha kwa njia ya magonjwa, shida, mafarakano baina yako na watu wanaokuzunguka ili tu kuikana imani yako, au vikwazo vya nguvu za giza, mabalaa, ajali, mikosi, na vishawishi vya kukufanya utende dhambi zisizo za kukusudia, n.k.. haya yote shetani anayaleta kwa dhumuni tu la kukufanya wewe ulegee katika imani, au umkane Mungu, au uteseke na pengine ufe kabla hata hujamaliza kusudi lako uliloitiwa duniani, kumbuka mambo haya shetani anayalengesha kwa mkristo tu aliyeamua kusimama,

Tunaona Bwana YESU aliwaonya wanafunzi wake akiwaambia “makwazo hayana budi kuja”. Lakini pamoja na hayo alitoa njia ya kuweza kuyadhibiti, na ni kwa njia moja tu nayo ni kwa “KUOMBA”.

Tufuatilie mahali pengine alichowaambia wanafunzi wake:

Mathayo 26:40 ” Akawajia wale wanafunzi wake, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, je! hamkuweza kukesha pamoja nami hata SAA MOJA?.

41Kesheni, MWOMBE, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Tunaona hapo Bwana YESU aliwasisitiza wanafunzi wake waombe kwasababu majaribu mazito yalikuwa yanawangojea mbeleni, na ndio maana Bwana angali akiyaona hayo ya kwenda kupata mateso alimwomba Mungu amwepushe na kile kikombe cha majaribu, hivyo kwa kufanya vile japo lile jaribu halikuondolewa lakini alipewa nguvu ya kulishinda na ndio maana malaika walimtokea na kumtia nguvu, lakini kwa wale wengine (wanafunzi wake) ambao nao majaribu mazito yalikuwa yanawangojea walila wakidhani kuwa adui yao(shetani) na yeye alilala?. Lakini tunafahamu kitu gani kilichowatokea dakika chache baadaye, tunaona shetani alipomjaribu Petro alimkana KRISTO pale pale na wengine wote walikimbia na kujitenga na Bwana.

Lakini je! mfano wangekesha na BWANA kuomba wasiingizwe majaribuni, unadhani yale yote yangewatokea? La! Hakika Mungu angewaepushia pengine malaika angewaonya waondoke maeneo yale, au mazingira ya wanafunzi kushikwa na wale askari au mazingira ya Petro kutaka kumkana Bwana yasingekuwepo, na kama wangekaa kuomba na YESU wasiingie majaribuni hata kama wangeingia majaribu Mungu angewapa wepesi wa kushinda kama Bwana alivyopewa ule wepesi wa kushinda.

Na jambo hili hili linajirudia hata sasa hivi, kwa mkristo yoyote aliyesimama, wakati wewe umelala fahamu kuwa adui yako hajalala yupo nje anaandaa majeshi ya kukuangamiza wewe, unadhani kama yalimpata BWANA kwanini yasikupate na wewe?, kama alimwomba BABA amwepushe na majaribu inakupasaje wewe?. Na ndio maana hata tunaona pale alipowafundisha wanafunzi wake kusali aliwaambia hivi ” ..USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUEPUSHE NA YULE MWOVU..” . Haya maombi ni muhimu sana katika maisha ya kila mkristo.

Na ukiwa kama mkristo ni muhimu kufahamu maeneo ambayo adui anapenda sana kutumia kukushambulia na hapo ndipo unapotakiwa kutilia mkazo katika kuomba Mungu atoweshe majeshi ya mwovu katika eneo hilo, yapo maeneo mengi mfano, mara nyingine shetani anaweza kutumia marafiki zako wa karibu au ndugu zako kudhoofisha imani yako unashindwa aidha kusoma NENO, au kuwa huru na imani yako au kusali, na unaona unaishi katika mazingira ambayo hayaepukiki kuwa na hao watu, hapo sasa unatakiwa umwombe BWANA awalinde ndugu zako dhidi ya yule mwovu asipate nafasi ya kuwatumia kuidhoofisha imani yako.

Au mara nyingine shetani anaweza kutumia wafanyakazi wenzako au maboss wako kukuharibu wewe uiache au uikosee imani yako, pengine hata kuikana, maeneo kama hayo ni vema ukeshe katika kuomba BWANA awafunike wafanyakazi wenzako shetani asiwatumie wao kama vyombo kwa kukujaribu wewe. Kwa kufanya hivyo utajikuta imani yako haisumbuliwi hata kama upo katikati ya watu wasioamini kiasi gani na hata kama ikitokea shetani akiruhusiwa kuwatumia kukujaribu wewe Mungu atakupa nguvu ya kuyashinda kama alivyompa Danieli hutaweza kumkana Mungu hata kama utatupwa katika tundu la simba, utashinda kama Bwana YESU hata kama ni kuwekwa msalabani, lakini ni kwanini ? ni kwasababu ULIMWOMBA BWANA AKUEPUSHE NA MAJARIBU.

Lakini usipokuwa mwombaji ndugu, hutaweza kumshinda shetani utabakia tu kutamka ushindi wa mdomoni lakini mwisho utaishia kuikana imani kama vile tu Petro, Kumbuka nia ya Petro ilikuwa kweli sio kumkana BWANA lakini kwasababu alikuwa hana nguvu ya kushinda majaribu alijikuta ameingia katika matatizo makubwa, na nguvu hii ingepatikana kwa njia ya MAOMBI TU!.

Na ndio maana Bwana alisema tuombe walau hata “SAA MOJA” kwa siku. Ni hatari sana kama wewe ni mkristo hata dakika 10 husali, si ajabu unaona ukristo ni mgumu kuuishi, mitego ya adui chungu nzima imetuzunguka, pasipo maombi tutawezaje kuishinda?. Wachawi hawalali wanakesha kila siku kuloga na kuilaani siku yako kwa BWANA, wewe unatakiwa uamke uibariki siku yako.

Utawezaje kushinda tamaa za uasherati, kama Yusufu kwenye maeneo yako ya kazi, au shule, au makazi unayoishi,? katika kizazi hichi cha uzinzi kama sio mwombaji?..NI WEWE AMBAYE UNASEMA KUWA NI MKRISTO.

Yakobo 4: 1″ Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?.

2Mwatamani wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu KWA KUWA HAMWOMBI.

Hivyo ndugu ni muhimu kutenga walau SAA MOJA kila siku kuomba, kuibariki siku yako, yapo mambo mengi ya kuombea ipo familia yako,ukoo wako, jamaa zako na marafiki zako mwombe Mungu awalinde wasiwe vyombo vya shetani kukuangamiza Katika UKRISTO wako, ombea wakristo wenzako na watumishi wa Mungu shetani asipate nafasi ya kuliharibu kanisa, ombea taifa unaloishi pamoja na viongozi wake ili uishi kwa amani, wasikuingize majaribuni kumbuka usipofanya hivyo wanaweza hata kuibua sheria zilizotungwa kuzimu ushindwe kumwabudu Mungu wako kwa uhuru, ombea kazi yako, vyombo vyako vya usafiri, shule yako, n.k. shetani asivitumie kuharibu imani yako au uhusiano wako na Mungu.,

Wakati mwingine unajikuta muda wote upo buzy hujamaliza hili linazuka lingine, na hali hiyo inaendelea kila siku mpaka inasonga imani yako na uhusiano wako na Mungu, hayo ni majaribu unapaswa UOMBE Mungu ayaepushie mbali hayo majaribu ili shughuli za kidunia zisizoisha ziondoke mbele yako na upate Muda mwingi binafsi na Mungu wako.

Usipofanya hivyo ndugu shetani atakuwa amekushinda utafananishwa na ile mbegu iliyotupwa kwenye miiba, ilipomea shughuli,udanganyifu wa mali na masumbufu ya maisha hayo yakaisonga ikawa haizai(mathayo 13:22). Kwa nyanja zote hizi ukiomba hakika hautashindwa kumaliza saa moja.

Hivyo kwa wewe mkristo ni muhimu sana kumwomba Mungu akuepushe na Majaribu maadamu upo safarini, vikwazo na majaribu Bwana alituonya hatuna budi kukutana navyo na ni kwa MAOMBI tu! tunaweza kudhibiti.

OMBA WALAU SAA MOJA KILA SIKU.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA

FAIDA ZA MAOMBI.

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

KWANINI MUNGU HAKUMUUA NYOKA MPAKA AKARUHUSU AJARIBIWE PALE BUSTANI NA EDENI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

Waefeso 1 : 4 ” Kama vile alivyotuchagua katika yeye KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na urathi wa mapenzi yake.”

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

Mambo yote tunayoyaona sasa katika ulimwengu yalikuwa yameshakusudiwa yawepo kabla hata ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, hakuna lolote linalotokea kwa bahati mbaya ambalo Mungu hakulijua, Kuna swali watu wengi wanauliza je! Mungu anafahamu mtu kabla hajazaliwa kwamba atakuja kwenda mbinguni au kuzimu?? Jibu ni ndiyo anafahamu!..

Ni lazima ajue hayo yote ili awe Mungu..na kuna wengine wanauliza kama ni hivyo basi kwanini aumbe wengine angali anajua mwisho wao utakuwa ni kuzimu?? Jibu ni kwamba ewe mwanadamu wewe ni nani umuulize Muumba wako, kwanini chombo hichi unakifanya hivi na kile unakifanya vile? Hatuwezi kushindana na kusudi la Mungu Akili za Mungu hazichunguziki wala njia zake hazitafutikani.

Mtume Paulo alisema katika warumi 9:20 kwamba vipo vyombo Mungu aliviumba vya ghadhabu kwa ajili ya uharibifu tunaona kama vile Farao,Yezebeli,Balaamu,n.k. na vipo vingine aliviumba kwa ajili ya heshima mfano Musa, Ayubu,Ibrahimu n.k.

Hivyo basi tukivitazama hivi vyombo vya heshima Mungu alivyovichagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu na kuvitengenezea njia ya kupitia mpaka vitakapofikia ule utukufu wa Mungu alioukusudia juu yao. Na ndio maana alisema katika..

Warumi 8:28-30” Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, WALE WALIOITWA KWA KUSUDI LAKE.

29. MAANA WALE ALIOWAJUA TANGU ASILI, ALIWACHAGUA TANGU ASILI WAFANANISHWE NA MFANO WA MWANA WAKE, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

30. Na wale aliowachagua tangu asili hao AKAWAITA, na wale aliowaita, hao AKAWAHESABIA HAKI; na wale aliowahesabia haki, hao AKAWATUKUZA.

Unaona hapo kuna hatua za kufuata kwa kile chombo cha heshima kilichoteuliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili kifikie utukufu wake uliokusudiwa. Sasa Baada ya kuchaguliwa tangu asili zipo hatua TATU za kufuata 1) KUITWA, 2) KUHESABIWA HAKI, 3) KUTUKUZWA. Embu tuzitazame kwa ufupi hizi hatua.

1) KUITWA:

Waliochaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ni lazima waisikie sauti ya Mungu inapolia masikioni mwao.Kumbuka na sio watu wote wataisikia hiyo sauti, bali ni wale tu Mungu aliowachagua tangu asili,. Bwana Yesu aliwaambia makutano hivi wale waliomtilia shaka kwamba yeye hajatumwa na Mungu kuwaokoa wanadamu alisema hivi..

Yohana 6:43″ …Msinung’unike ninyi kwa ninyi. HAKUNA MTU AWEZAYE KUJA KWANGU, ASIPOVUTWA NA BABA ALIYENIPELEKA; nami nitamfufua siku ya mwisho” kwahiyo unaona ni lazima uvutwe kwanza.

Mahali pengine Yesu aliwaambia hao hao mafarisayo alisema..Yohana 10:26″ Lakini ninyi hamsadiki, kwasababu HAMMO miongoni mwa kondoo wangu. KONDOO WANGU WAISIKIA SAUTI YANGU; NAMI NAWAJUA NAO WANIFUATA. NAMI NAWAPA UZIMA WA MILELE; WALA HAWATAPOTEA KAMWE.

Umeona hapo tena walio wa Kristo wataisikia sauti yake tu!, haihitaji kuwa bembeleza sana, kwani ile mbegu ya nuru Mungu alishaiweka ndani yao tangu asili, wakisikia tu, saa hiyo hiyo wanabadilika na kumfuata Kristo katika hali zote.

Jiulize ni kwasababu gani mafarisayo na masadukayo pamoja na dini zao zote walishindwa kumwamini YESU KRISTO jibu ni rahisi kwasababu hawakuwa miongoni mwa kondoo wake aliowachagua tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, lakini tunaona wale watu wasiokuwa na elimu, wavuvi, wakina Petro walimkubali YESU pasipo maswali mengi au shuku shuku nyingi ni kwasababu gani? ni kwasababu walikuwa ni miongoni mwa wale aliowachaguliwa tangu asili.

2) KUHESABIWA HAKI.

Mtu anahesabiwa haki kwa kumwamini YESU KRISTO katika uweza wa Damu yake inayoondoa dhambi, kumbuka wale wote walio wake baada ya kuitikia wito wao wenyewe watataka kuuliza tufanyeje?? Hapo ndipo Bwana atakapowaongoza katika hatua inayofuata ya kuufanya imara WITO wao na UTEULE wao (2Petro 1:10). Hapo ndipo mtu anapoutafuta ubatizo wa MAJI na wa ROHO MTAKATIFU..

Tunaona ile siku ya Pentekoste Petro baada ya kuwashuhudia wale makutano walio kusanyika waliamini ..tusome

 Matendo 2:37-38″ Waliposikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI, MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote WATAKAOITWA, na Bwana Mungu wetu WAMJIE.”

Kwahiyo unaona hapo? ili uhesabiwe haki lazima ukabatizwe katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. kumbuka hakuna ubatizo wa watoto wadogo, wala hakuna ubatizo wa kunyunyuziwa maji, unapaswa UKAZAMISHWE, na ubatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO kulingana na maandiko, hata mimi nilinyunyuziwa nilipokuwa mchanga lakini baada ya kufahamu ubatizo sahihi kulingana na maandiko ilinipasa nikarudie tena. Kisha baada ya hilo una AHADI YA ROHO MTAKATIFU, na ni vizuri kujua kuwa ahadi hii si kwa ajili ya kila mtu(hata kafiri) bali ni kwa wale watakaoitwa na Bwana wamjie. Naamini nawewe ni mmoja wapo wa walioitwa.

3) KUTUKUZWA.

Baada ya kupokea Roho Mtakatifu ambao ndio muhuri wa Mungu (Efeso 4:30). Kitu kilichotiwa muhuri maana yake ni kimehakikiwa na kuonekana kimekamilika. Hivyo mtu anapopokea Roho Mtakatifu anakuwa ametiwa muhuri na Mungu mpaka ile siku ya ukombozi. Kumbuka Kupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zaidi ya kunena kwa lugha, kunena kwa lugha ni karama sio watu wote wanaweza wakanena, ni kama vile sio watu wote wanaweza wakawa manabii, au wainjilisti, vivyo hivyo mtu anaweza akapokea Roho Mtakatifu na asinene kwa lugha, bali karama nyingine ikajidhihirisha, na pia wapo ambao wananena kwa lugha na hawajapokea Roho Mtakatifu. Kwahiyo kipimo cha kwamba umepokea Roho Mtakatifu sio karama uliyonayo bali ni maisha matakatifu unayoishi baada ya kumpokea Roho.

Hivyo baada ya kukamilishwa kwa kubatizwa na Roho Mtakatifu tunasubiria siku ya ukombozi wetu( yaani siku ya kutukuzwa) kwenda mbinguni, siku tutakapovaa miili ya utukufu na kuwa kama BWANA YESU KRISTO alivyo sasa.

Kwahiyo ndugu tathimini maisha yako, je! unavyoishi leo hii ni miongoni mwa wale kondoo wake aliowachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu? au vile vyombo vya ghadhabu vilivyowekwa kwa ajili ya uharibifu??..

Kumbuka kuna makundi mawili tu, ni aidha kondoo au mbuzi, umeitikia wito au hujaitikia wito, umechaguliwa au haujachaguliwa, ni wa mbinguni au ni wa kuzimu? jibu lipo moyoni mwako. Je! upo katika hizo hatua? kwamaana biblia inasema wale wote wasio na Roho wa Kristo hao sio wake (warumi 8:9).

2 Timotheo 2:19 ” Lakini msingi wa Mungu ulioimara umesimama, wenye MUHURI HII, BWANA ANAWAJUA WALIO WAKE. NA TENA, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AACHE UOVU.

20 Basi katika nyumba nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina.

21 Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima kilichosafishwa, kimfaacho BWANA, KIMETENGENEZWA KWA KILA KAZI ILIYO NJEMA.

AMEN!

Maombi yangu ndugu ni uchague kufanyika chombo cha heshima. Muda umeenda kuliko unavyodhani Bwana yupo mlangoni kurudi.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

JE! WEWE NI MBEGU HALISI?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

ILI TUONEKANE WAKAMILIFU MBELE ZA MUNGU.

MSTARI HUU UNAMAANA GANI? ″WALAKINI HAUTAPOTEA HATA UNYWELE MMOJA WA VICHWA VYENU? (LUKA21:18).


Rudi Nyumbani

Print this post

GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.

Kuna gharama kubwa sana katika kuupata ufalme wa mbinguni kama Bwana Yesu alivyotangulia kusema kwenye Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. ” Hii ikiwa na maana kuwa ufalme wa mbinguni ni kitu kinachogombaniwa kwa nguvu na watakaokipata ni wachache. Na kumbuka NGUVU zinazozungumziwa hapo sio nguvu za kimwilini, Tukisoma..

Mathayo 13:44-46 “

44 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akalinunua shamba lile.

45 Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;

46 naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akainunua. “

gharama ya ufalme wa mbinguni..Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri;  46 naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda AKAUZA ALIVYO NAVYO VYOTE, akainunua. "

Bwana Yesu alifananisha ufalme wa mbinguni na maisha yetu tunayoishi kila siku, kama tukisoma hiyo mifano hapo juu tunaona kuna mfanya biashara aliyekuwa anatafuta lulu nzuri ya thamani kubwa, na alipoiona akaipenda sana, pengine hakuwa na fedha za kutosha, kuinunua kutokana na gharama ya LULU hiyo ilivyokuwa na thamani kubwa, lakini kwasababu ni mfanya biashara, alitafakari sana, kwamba japo inauzwa kwa thamani nyingi, lakini akiipata ataweza kuiuza mahali pengine kwa gharama kubwa zaidi, Hivyo atarudisha fedha aliyoinunulia pamoja na faida nyingi juu yake.

Kwasababu hiyo basi ilimpasa aende kuuza kila kitu alichokuwa nacho pengine hata nyumba yake, na miradi yake yote, ilimradi tu afikie kiwango kile cha pesa akainunue lulu ile yenye thamani kubwa.

Labda pengine alivyodhamiria kufanya hivyo, alionekana mwendawazimu mbele za watu kuuza mali alizozitaabikia kwa muda mrefu, lakini kwasababu ni mfanya biashara alifahamu ni kitu gani anafanya.

Vivyo hivyo na yule mwingine aliyeona hazina iliyositirika katika shamba na kwenda kuuza vyote alivyonavyo hakuwa mwendawazimu, pengine aliiona ALMASI imejichimbia katika kiwanja cha jirani yake, hivyo ili aweze kuipata ni sharti kile kiwanja kiwe chake, ili awe na ruksa ya kuifukua,

Sasa kwa ujanja, akaenda kumshawishi mwenye kiwanja amuuzie hata kwa bei mara 10 ya bei halisi ya kiwanja kile ili aweze kukipata kwa haraka na bila ya usumbufu , kwa kuwa mtu huyo anajua ni kitu gani anachokifanya, akaamua akauze kila kitu alichokuwa nacho, pengine mifugo yake, au majumba yake, au magari yake, na kama fedha isingetosha angeweza hata kwenda kukopa ili atimize lengo lake la kupata kiwanja kile.

Lakini kwa namna ya kawaida watu wangemuona kama amelogwa, au amerukwa na akili, kugharimikia kitu kisichokuwa na faida, lakini yeye hakuona tu kiwanja, bali aliuona UTAJIRI mkubwa zaidi ya kile kiwanja.

Mifano hiyo hiyo inatufundisha sisi kama wanadamu, HATUTAWEZA KUUPATA UFALME WA MBINGUNI, KAMA BADO HATUJAJUA THAMANI YAKE. Kumbuka yule mfanyabiasha hakuona tu lulu bali aliona thamani kubwa iliyopo ndani ya lulu, ndiyo ikamgharimu kuuza kila kitu, vivyo hivyo na yule aliyenunua shamba, hakuona tu shamba, bali aliona thamani ya kitu kilichokuwa kimejificha ndani ya lile shamba na ndipo gharama za kukipata hicho kitu zinajitokeza.

Na katika ufalme wa mbinguni, usiuone tu ufalme wa mbinguni halafu basi, bali tazama thamani na utajiri ulioko ndani ya huo ufalme, ukishalifahamu hilo au kupata ufunuo huo utakuwa na nguvu za kuchukuliana na gharama zozote utakazokumbana nazo kwa furaha zote.

Tukirudi kwa kijana mmoja aliyeitwa Musa, tunaona alizaliwa katika makasri ya kifalme ya FARAO, aliyekuwa msomi, na mtawala mwenye cheo, pamoja na mali nyingi, lakini ilifika wakati neema za Mungu ilifunguliwa machoni pake,na kuuona uzuri ulio katika ufalme wa mbinguni, hivyo kwa furaha yote aliamua kuuza kila kitu alichokuwa nacho ili aupate ,alidharau elimu yake ya kipagani, alidharau cheo chake kama mfalme mrithi, alidharau anasa na fahari alizokuwa anazipata katika jumba la kifalme, ili tu aupate ufalme usioharibika wa mbinguni..

Mtume Paulo aliandika katika.Wabrania 11:24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

26 AKIHESABU YA KUWA KUSHUTUMIWA KWAKE KRISTO NI UTAJIRI MKUU KULIKO HAZINA ZA MISRI; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. “

Tunaona hapo Musa alihesabu kushutumiwa kwake Kristo ni Utajiri mkuu kuliko hazina zote za Misri, ilimpasa AUZE baadhi ya mambo, ili aweze KUUNUNUA ufalme wa mbinguni, aliuona utajiri mkubwa huko mbeleni kuliko hazina zote za Misri, Ilimpasa auze umaarufu wake, ilimpasa auze anasa zake, ilimpasa auze ujana wake, ilimpasa auze kiburi chake, ilimpasa auze fashion zake, ilimpasa auze majigambo yake na ujuzi wake, ilimpasa auze dhuluma yake, ili aweze kufikia viwango vya kuununua ule UFALME WA MBINGUNI.

Vivyo hivyo na mtume Paulo mwenyewe aliingia gharama hizo hizo..ukisoma Wafilipi 3:7-8 inasema..

” Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama “MAVI” ili nipate Kristo; “

Paulo ambaye alikuwa ni msomi mwenye cheo na kiburi alihesabu mambo yote kuwa kama mavi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, kumbuka kilichomfanya achukue uamuzi huo sio tu kwasababu ni neno “ufalme wa mbinguni” , hapana bali ni UTAJIRI aliouna angeupata katika huo ufalme.Na kwa kufunuliwa na Roho Paulo alifika wakati na kusema

 Warumi 8:18-19

18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama UTUKUFU ULE UTAKAOFUNULIWA KWETU.

19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.

Hivyo ndugu fungua macho yako uone thamani na utajiri mkubwa ulio katika huo ufalme, ndipo utakapoona sababu ya kuacha kila kitu kisichompendeza Mungu kwa furaha zote na kumwandamia Mungu kwa hali zote,. Kumbuka thawabu za UFALME WA MBINGUNI, zitakazokuja huko ni mambo mazuri ambayo biblia inasema katika..1Wakoritho 2:9 “lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)

Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. “, pia usisahau, kutakuwa na wafalme na wenye mamlaka kubwa, pamoja na makuhani wa Mungu hawa watakaa pamoja na Kristo na kuhudumu pamoja naye, na huko watakuwepo pia watu wa kawaida tu, thawabu zitatofautiana sana, na ni milele, ikiwa na maana kuwa kama wewe ni mdogo kule utabaki hivyo hivyo milele, na kama wewe ni mfalme kule utadumu mfalme milele, na Bwana wetu YESU KRISTO akiwa kama MFALME WA WAFALME.  

Jina la BWANA YESU LIBARIKIWE.

Kuna wakati mitume walimuuliza Bwana..

Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?

28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. “

Hivyo wale watakaoketi karibu na Bwana ni wale tu, walioona thamani na kuingia gharama za kuununua ufalme wa mbinguni, je! ufalme huu unathamani gani kwako? , wewe mwanamke hauwezi ukaacha fashion na kuvaa hivyo vimini na suruali, kwasababu hauoni faida yoyote ya kuacha kufanya hivyo, mwanamume hauwezi kuacha pombe na sigara kwasababu kwako ni sawasawa ni biashara isiyo na faida, hauwezi kuacha uasherati, wizi kwasababu faida ya ile LULU(UFALME WA MBINGUNI) haijafunuliwa machoni pako. Laiti ungeifahamu thamani ya LULU usingefanya hivyo.

Lakini kumbuka wana wa Mungu, sio wajinga kuwaona wanauza mambo ya ulimwengu huu sasa ivi ili wanunue mambo ya ulimwengu unaokuja, ni kwasababu wanaona mbele, na kujipenda na wanapenda maisha ndio maana wanatafuta maisha ya milele yanayodumu, na wanapenda furaha zaidi hata ya wewe unayejiona unajistarehesha katika anasa za ulimwengu huu.

Kanisa tunaloishi ndilo la mwisho linalojulikana kama LAODIKIA kulingana na Kalenda ya Mungu, na ujumbe wetu tuliopewa umeandikwa katika kitabu cha Ufunuo 3:14 unasomeka hivi..

“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, UNUNUE KWANGU DHAHABU ILIYOSAFISHWA KWA MOTO, UPATE KUWA TAJIRI, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “

Bwana ametupa shauri tukanunue dhahabu kwake tupate kuwa matajiri, kumbuka ili KUNUNUA lazima TUUZE yote maovu tulionayo ili tuweze kukidhi viwango vya kuupata ufalme wa mbinguni. Maombi yangu ni Bwana akupe neema ya kuona THAMANI YA UFALME WA MBINGUNI kwasababu UFALME WA MBINGUNI unapatikana kwa nguvu, na wenye nguvu ndio wanaouteka.

Print this post

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.

Kama tunavyofahamu wakati wa usiku kabla hatujalala, huwa ni lazima tufunge milango yetu yote, kwa makufuli na makomeo, na hii sio kwasababu tunapenda kujifungia tu hapana! bali ni kujiweka katika hali ya usalama dhidi ya WEZI usiku, Kwasababu hatujui ni wakati gani wataingia na kuleta madhara. Hii ni desturi kwa kila mtu,hakuna mtu asiyefahamu kuwa anapaswa kufunga milango yake wakati wa usiku.

Lakini pamoja na hayo kufunga mlango tu na kwenda kulala haitoshi, kwasababu mwizi anajua kabisa akienda atakutana na changamoto ya milango kufungwa hivyo atakuwa amekwisha jipanga kwa njia mbadala ili kuhakikisha kuwa zoezi lake la kuiba linafanikiwa kikamilifu, hivyo ni dhahiri kuwa atakuwa na vifaa husika vya kuvunjia nyumba.

Kwahiyo ili mwenye nyumba aweze kunusuru mali zake au roho yake sio tu KUBANA MILANGO yake bali anapaswa pia AKESHE, Kwasababu mwizi hawezi kuharibu kama mwenye nyumba yupo macho. Hivyo dawa pekee ya kudhibiti wizi usiku ni kubana milango pamoja na KUKESHA.

Ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Bwana Yesu Kristo,akifananisha kuja kwake na kama ujio wa mwizi wakati wa usiku alisema …

Mathayo 24:40-44″ Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

43 Lakini fahamuni neno hili; KAMA MWENYE NYUMBA ANGALIIJUA ILE ZAMU MWIVI ATAKAYOKUJA, ANGALIKESHA, wala asingaliiacha nyumba yake KUVUNJWA. 

44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa damu yuaja.

43 Lakini fahamuni neno hili; KAMA MWENYE NYUMBA ANGALIIJUA ILE ZAMU MWIVI ATAKAYOKUJA, ANGALIKESHA, wala asingaliiacha nyumba yake KUVUNJWA.

Tukisoma pia katika 

Marko 13:32 Bwana Yesu alisema maneno haya: Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.

33 Angalieni, KESHENI, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.

34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.

35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, KWAMBA NI JIONI, AU KWAMBA NI USIKU WA MANANE,au AWIKAPO JIMBI, au ASUBUHI;

36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.

37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, KESHENI.”

Kumbuka hapo Bwana Yesu hakusema “fungeni milango” bali alisema “kesheni” kwasababu inajulikana ni wajibu wa kila mtu kufunga milango yake, na kufunga milango ina maana kujiona umeokoka lakini maisha yako hayaendani na ukristo,umebatizwa na unaenda kanisani lakini umelala katika roho(vuguvugu), nje milango imefungwa lakini ndani umelala kwasababu hiyo basi mwizi atakapokuja hautajua lolote.

Mkristo aliyeridhika na dhehebu lake au mapokeo yake lakini hazingatii mambo ya muhimu yanayohusiana na wokovu wake na maisha yake ya umilele ni sawa na mtu aliyejifungia na kulala usingizi.

Dunia sasa hivi ipo katika GIZA NENE SANA ikiashiria kwamba huu ni wakati wa USIKU na ndio wakati uliokaribia wa BWANA kurudi tena, kuongezeka kwa maovu ulimwenguni kama vile anasa,ulevi,uasherati uliokithiri hususani katika ulimwengu huu wa sasa wa utandawazi,mauaji,uchawi,rushwa,dhuluma, kupenda ulimwengu zaidi ya Mungu,n.k. vinawafanya watu wazidi KULALA usingizi wa mauti, na jinsi giza linavyozidi kuongezeka ndivyo wakristo nao wanavyozidi kushawishika kulala.

Sasa katikati ya kilele hichi cha maovu hapo ndipo Kristo atakaporudi, alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu watu walikuwa wakila na kunywa(ikiashiria kufanya anasa),walikuwa wakipanda na kujenga, hata siku ile ikawajilia kama ghafla, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.

1Thesalonike 5:1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. “

Bwana Yesu pia alisema..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) “.

MAANA YA KUKESHA NI NINI?

Kukesha kunakozungumziwa ni KUKESHA KATIKA ROHO, kutokulala katika roho, kudumu katika utakatifu,huku matunda ya roho yakijidhihirisha upole,kiasi,upendo,uvumilivu,n.k pamoja na kuishi maisha ya kama mtu anayemngojea Bwana wake, kama msafiri duniani, asiyefanana na watu wa ulimwengu huu waliousingizini, huku macho yake yakitazama mambo ya mbinguni yanayokuja,

Utajisikiaje siku hiyo utakapoona wenzako wamekwenda kwenye unyakuo na wewe umebaki? ni uchungu usioneneka, mara nyingine Mungu anawaotesha watu ndoto kwamba unyakuo umepita na wenyewe wamebaki, hapo ni Mungu anajaribu kuwakumbusha watu kwamba maisha yao hayajakidhi vigezo vya kwenda mbinguni.Huu ni wakati wa kuamka usingizini biblia inasema..katika Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.”

Amka ndugu utoke katika usingizi wa wafu wa ulimwengu huu, uasherati ni usingizi,kiburi cha uzima ni usingizi,ulevi,sigara,anasa,fashion,ushirikina,usengenyaji,rushwa,ulawiti,utoaji mimba,wizi,utukanaji vyote hivi ni usingizi wa kiroho, na kumbuka siku Kristo atakapokuja kulichukua kanisa lake hawa hawatajua lolote badala yake watabaki hapa wakingojea ile SIKU KUU YA BWANA inayowaka kama tanuru ndivyo biblia inavyosema,

2 Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana ITAKUJA KAMA MWIVI; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo,IMEWAPASA NINYI KUWA WATU WA TABIA GANI KATIKA MWENENDO WENU MTAKATIFU NA UTAUWA,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? “.

Kwa kuwa sisi sote hatujui ni saa gani Bwana atakayokuja , ni wajibu wa kila mtu aliye mkristo kukesha kwa kuishi maisha ya uangalifu katika giza hili nene lililopo dunian sasa.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?


Rudi Nyumbani

Print this post

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

Bwana alituweka duniani kila mmoja wetu tumzalie matunda, na kuna matunda ya aina mbili

1) Matunda ya Haki: (Wafilipi 1:11, wagalatia 5:22) nayo ni upendo, furaha, utu wema, kiasi, uvumilivu, upole, amani, fadhili, n.k. ambayo kwa ujumla tunaita ni UTAKATIFU.

2) Matunda ya kazi ya Mungu: Ambayo ni kuwavuta watu wa Kristo, kwa njia mbalimbali za kuhubiri, kufundisha, na kuhudumu, nk.

Biblia mahali pengine imefananisha matunda haya yote kama “TALANTA”. Tukisoma mfano Bwana Yesu aliowapa wanafunzi wake kwenye

Mathayo 25:14-30″

14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.

15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.

16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.

17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.

18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.

19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.

21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.

23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29 KWA MAANA KILA MWENYE KITU ATAPEWA, NA KUONGEZEWA TELE; LAKINI ASIYE NA KITU, HATA KILE ALICHO NACHO ATANYANG’ANYWA.

30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”

Bwana alituweka duniani kila mmoja wetu tumzalie matunda, na kuna matunda ya aina mbili

Mfano huu ni dhahiri unajulikana kuwa moja kwa moja unalenga katika kuifanya kazi ya Mungu kwa karama mtu aliyopewa, kama amepewa karama ya aulimu, au amepewa karama ya kichungaji, au karama ya kinabii au uinjilisti au nyingine yoyote ni jukumu lake kuitumia kuwavuta watu kwa Kristo ili siku ile Bwana atakapokuja na kumuuliza mtu huyo umemzalishia vingapi aweze kumpa vya kwake na vya ziada.

Lakini pia tafsiri kuu ya mfano huu, TALANTA haimaanishi karama peke yake, bali pia hata KILE MTU ANACHOSIKIA ni talanta. Unapohubiriwa NENO la Mungu hiyo ni talanta imepandwa moyoni mwako na Bwana ataihitaji ya kwake pamoja na ya ziada katika siku ile ya hukumu kwa yote uliyoyasikia.

Kama ukisoma kwa makini mstari wa 29 unasema “Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.”

Mstari huu huu umejieleza zaidi kwenye 

Mathayo 13:2-13″ unasema…”Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.

3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.

4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;

5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;

6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.

7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;

8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.

9 Mwenye masikio na asikie.

10 Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?

11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.

12 KWA MAANA YE YOTE MWENYE KITU ATAPEWA, NAYE ATAZIDISHIWA TELE; LAKINI YE YOTE ASIYE NA KITU, HATA KILE ALICHONACHO ATANYANG’ANYWA.

13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. “

Bwana Yesu mara nyingi alipokuwa akiwafundisha makutano, hakuzungumza nao moja kwa moja, kwa kufafanua mambo, bali kama kwa njia ya mafumbo, hivyo wengi walikuwa wakitoka na maswali mengi kichwani, au wengine hawakumuelewa kabisa, na wengine walimwona kama vile mtunga hadhithi tu zisizo na maana, lakini alifanya hivyo kwa makusudi ili ajue ni wangapi walio tayari kujifunza , na ndio maana tunaona baada ya kumaliza ile mifano ni kikundi cha watu wachache tu(wanafunzi wake) kati ya maelfu kilichoenda kumuuliza tafsiri ya ile mifano yote aliyokuwa anazungumza,

Na ndipo hapo anapowafunua macho yao na kuwaelewesha tafsiri ya mifano ile na kuponyeka roho zao, bali wale wengine waliosalia ambao hawakutaka kujifunza zaidi kwao ilikuwa ni kama hadhithi tu. Na mahali popote Bwana alipokuwa akifundisha kwenye makutano mengi hiyo ndiyo ilikuwa desturi yake. Na ndivyo anavyofanya hata sasa.

Jambo la kujifunza ni kwamba hawa wanafunzi walipopewa talanta za Neno la Mungu mikononi mwao kwa ile mifano, hawakuenda kuichimbia chini(yaani kuridhika na mifano ile), badala yake walikwenda kuifanyia biashara ili wanufaike, pale walipokwenda kumuuliza Bwana tafsiri ya mifano ile.

Na hao ndio pekee waliozidi kuimarika na kukua kiroho siku baada ya siku kwa kuzijua siri za Mungu, wakifananishwa na mbegu zile zilizotupwa katika udongo mzuri, zilizozaa moja 30, nyingine 60 na nyingine 100, lakini wale wengine walifananishwa na zile mbegu zilizoangukia njiani, na kwenye miamba na kwenye miiba ndege walipopita wakazila, jua lilipokuwa kali zikaungua, na mwamba ulipokuwa mgumu zikasinyaa kwa kukosa mizizi hawakuzalisha chochote.

Hawa ni mfano ya watu wasiotumia talanta zao vizuri (yaani kusikia NENO la Mungu), wale wa kwenye njia ndio wale wanaosikia Neno la Mungu kila siku likihubiriwa lakini wanalizembea kulitendea kazi au pengine hawajalielewa vizuri, kwao limekuja tu kama fumbo badala waendelee kutafuta kujua zaidi wao wanaliacha ,

Maana biblia inasema “kila atafutaye ataona” kama ulivyo mfano wa wale makutano ambao mwisho wa siku shetani anapata nafasi ya kulichukua mioyoni mwao na kulisahau, ni mara ngapi umesikia ukihubiriwa Neno la Mungu ubadilike lakini haubadiliki?, umefundishwa usivae vimini, hata kama haujalielewa au linakuchanganya je! ulishawahi kukaa na kumuuliza Mungu una maana gani kukataza mwanamke kuvaa suruali au kuweka make-up na kuvaa vimini??. Hiyo TALANTA uliyopewa na Mungu kwa kuhubiriwa umeitumiaje??..Ni dhahiri kuwa umeifukia chini na katika siku ile ya Hukumu utatoa hesabu yake.

Umehubiriwa mara nyingi uache uasherati, ulevi, usengenyaji, ushirikina, lakini huachi ulishawahi kukaa na kwenda kukufanyia kazi hicho ulichoambiwa? kumbuka hiyo ni talanta uliyopewa kwa kuhubiriwa Injili itatakwa na ya ziada siku ile ya hukumu.

Umefundishwa utukanaji, wizi, uvutaji sigara, utoaji mimba,usagaji, kutazama pornoghaphy, musterbation ni dhambi, talanta hizi zote zilipandwa ndani ya moyo wako kwa mafundisho mbalimbali uliyoyasikia ya Neno la Mungu, pengine mengi yalikuacha njia panda lakini je! ulishawahi kutenga muda na kwenda kumuuliza Mungu au kutaka kujua zaidi kama ni kweli au sio kweli, lakini umepuuzia kama yale makutano yalivyofanya. TALANTA hiyo itatakwa siku ile ya Hukumu.

Umesikia Neno la Mungu limepiga kelele masikioni mwako kwamba kuabudu sanamu, kusali rozari, mafundisho ya kwenda toharani na ibada za wafu ni mafundisho potofu yanayawapeleka mamilioni kuzimu, pengine uliposikia mara ya kwanza kwako ilikuwa kama ni kitendawili lakini je! ulishawahi kutenga Muda na kumuuliza Mungu je! mambo hayo ni kweli kuliko kupuuzia au kubisha, Kumbuka hiyo ni TALANTA ambayo Bwana alikupa moyoni mwako na usipoizalisha utaulizwa katika ile siku ya Hukumu.

Lakini kama ungependa kujifunza na kuyatendea kazi yale unayohubiriwa au kufundishwa..Bwana anasema: “KWA MAANA YE YOTE MWENYE KITU ATAPEWA, NAYE ATAZIDISHIWA TELE;”. Hivyo ungejikuta hata yale uliyokuwa huyajui Bwana anakuongezea na mengine mengi, Neno la Mungu linajifunua kwako , na kujikuta unaimarika kiroho siku baada ya siku.

Kwahiyo cha muhimu sana ni kuzingatia “kile unachokisikia” na kukifanyia kazi kwa bidii adui asije akakichukua hata hicho kidogo Mungu alichokupa neema ya kukisikia kikapotea moyoni mwako. Kwasababu alisema…

Marko 4:24 … ANGALIENI MSIKIALO; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

25 Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. “

Maombi yangu ni uanze kukitendea kazi kile ulichokisikia tangu zamani, ili atakapokuja aone matunda ya kusikia kwako Neno lake.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

MVUTO WA TATU!

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

FUVU LA KICHWA.

Luka 23:32 “Wakapelekwa na wawili wengine, wahalifu, wauawe pamoja naye.

33 Na walipofika mahali paitwapo FUVU LA KICHWA, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. “

3 Na walipofika mahali paitwapo FUVU LA KICHWA, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. "

Zamani zile tunafahamu utawala wa kikatili wa kirumi, uliua watu wengi kwa kuwatundika katika miti na misalaba, uliosambaa karibia ulimwenguni kote, na Israeli pia, Lakini tunaona wakati wa kumsulibisha Bwana wetu Yesu Kristo walimchukua na kumpeleka mahali panapoitwa FUVU LA KICHWA, Lakini swali la kujiuliza ni kwanini asipelekwe mahali pengine kama vile bethania, au Emau, badala yake walimpeleka mahali panapoitwa FUVU LA KICHWA.?

Vitu hivi vinafunua mambo ya rohoni, kuashiria kwamba kabla Kristo hajapandishwa msalabani tayari walishamsulibisha katika VICHWA vyao,Kupandishwa msalabani ni matokeo tu ya kitu kilichokuwa ndani , walishamkataa tangu siku nyingi na ndio maana biblia inasema Yohana 3:19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. “

Unaona hapo NURU ilikuja lakini waliipinga. Bwana alikataliwa tangu kuzaliwa kwake kama tunavyosoma katika maandiko habari hizo zilimfadhahisha Herode pamoja na Israeli yote. Alipingwa na viongozi wa dini pamoja na jamaa zake wakaribu, huko ndiko kumsulibisha Kristo katika vichwa vyao.

 Isaya 53:3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

Ni rahisi kusema ningekuwepo kipindi kile cha Bwana Yesu kamwe nisingeshirikiana nao kumsulibisha Bwana, Lakini ukweli ni kwamba Kristo anasulibishwa mpaka leo, na jambo hili linaanzia katika VICHWA VYA WATU.

huwezi kusema moja kwa moja unamsulibisha Kristo lakini ulishamsulibisha Katika KICHWA CHAKO, kwa kulikataa Neno La Mungu lilipokuwa linalia ndani ya moyo wako, Kutoa maneno ya kijeli na mizaha juu ya jina la Bwana( maneno kama ” eti unakuja umekuwa Yesu?), ni kumsulibisha Kristo, unapoambiwa ukweli na moyoni unajua kabisa ni kweli lakini unapinga kama wale mafarisayo ni sawa na kumsulibisha Kristo huna tofauti na watu wa kipindi kile, n.k.

Huu ni wakati wa kufungua moyo wako, Kristo ayafanye maisha yako kuwa mapya, badilisha fikra zilizo ndani ya fuvu la kichwa chako, kwa kulitii NENO la Mungu uokolewe uishie maisha ya yakumpendeza yeye, ili jambo lile lisikutokee kama lilivyowatokea wale watu wa wakati ule.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

NJIA YA MSALABA

NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?

KWANINI BWANA YESU ALISEMA PALE MSALABANI NAONA KIU?

BIBLIA INAMAANA GANI KUSEMA “VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI”?


Rudi Nyumbani

Print this post

NJIA MUNGU ALIYOIWEKA KWA KILA JAMBO.

Kuna NJIA za kufikia kila jambo, ambayo Mungu tayari alishaziweka tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, kwa mfano ili mwanadamu amfikie Mungu, tayari njia ilishaandaliwa, nayo ni YESU KRISTO, (Yohana 14:6″ Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”. ), watu wengi wanapotea wakidhani au wakijifariji kuwa zipo njia nyingi mbalimbali za kumfikia Mungu na zote zinaishia sehemu moja, kwamba unaweza ukawa muhindu, au m-muhamedi au m-budha n.k. na bado ukafika kwa Mungu. Huo ni uongo NJIA ni moja tu (nayo ni YESU KRISTO) na Mungu alishaitengeneza na hakuna mikato. Hivyo kama unataka kumfikia Mungu ni sharti upitie hiyo, nyingine zote zinapotosha.

Vivyo hivyo pia katika kufikia BARAKA fulani za MAISHA, Kuna njia ambazo Mungu alishaziweka zifuatwe hapa duniani, kwamfano ili kupata afya, ili kupata maisha marefu, ili kupata mafanikio, ili kupata cheo, ili kupata amani,n.k. ni lazima uzingatie njia hizo ambazo Mungu alishaziweka vinginevyo utajikuta unakosa shabaha na kuona kama Mungu hana msaada wowote kwako kwasababu tu ulikosa kujua njia sahihi ya kupita ili kufikia malengo yako ni ipi?

Kwa mfano Njia ambayo Mungu aliiweka kwa mtu apate kuishi maisha marefu na ya kheri biblia inasema katika 

Mithali 10:27″Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa. Na pia ukisoma..”

Waefeso 6:2-3 inasema ” Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.”

Kwahiyo kama ungependa uwe na maisha marefu hapa duniani kwanza ni UMCHE BWANA, na lingine ni kuwaheshimu wazazi, lakini njia nyingine zinazoonekana kuwa ni sawa kama vile kuzingatia MLO KAMILI, kuzingatia MAZOEZI, au Kupata muda mrefu wa kupumzika, au kuzingatia vyakula vya asili, vyote hivyo ni sawa lakini Havikuongezei maisha marefu na ya Kheri duniani. Kumbuka kosa la kwanza lilofanya maisha ya wanadamu kupunguzwa kutoka miaka 1000 mpaka miaka 120 ilikuwa sio kutokuzingatia mlo kamili bali ni kwasababu ya kutokushika maagizo ya Mungu. Hivyo kama unalegalega na njia zako hazimpendezi Mungu badilika sasa ishi maisha ya kumpendeza Mungu kama Mkristo na zingatia pia kuwaheshimu wazazi Mungu aliokupa hapa duniani. Kwa kufanya hivyo Mungu atakuongezea maisha marefu na sio tu marefu bali pia na ya Kheri.

Vivyo hivyo ili kupata afya, ni vizuri ukafahamu njia ya Mungu ni ipi aliyoiweka yeye, 

Mithali 3:7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; MCHE Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa AFYA MWILINI PAKO, Na mafuta mifupani mwako. ” 

Ukisoma pia.

Kutoka 15:26 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. “.

NJIA MUNGU ALIYOIWEKA KWA KILA JAMBO.

Mara nyingi tunajiuliza kwanini kila kukicha magonjwa yanatuandama, nimezunguka kutoka kwa mtumishi huyu hadi mtumishi huyu, nimeombewa na kila mtu lakini hali inazidi kuwa mbaya unaona kama vile Mungu hayupo pamoja nawe, Lakini hujui kuwa wewe ndio umemwacha Mungu na shetani ndipo anapopata nafasi ya kukutesa kwasababu umeiacha njia ambayo Mungu aliiweka tangu mwanzo tuiendee na kuwa na afya zetu, huwezi ukawa mwasherati, mlevi, mvutaji sigara, msengenyaji, fisadi, mwizi, au mtukanaji n.k halafu hayo yote yasikupate. Kumbuka biblia inasema KUMCHA BWANA ni KUCHUKIA UOVU (Mithali 8:13).

Jifungue mwenyewe kwanza katika hivyo vifungo vya uovu kwa kuacha kutenda dhambi, kumpoke Yesu Kristo, ndipo Bwana akulinde na maradhi kwasababu yeye anasema “ndiye Bwana akuponyaye”, Kwahiyo hauhitaji nguvu nyingi kujinyima kula vyakula vya aina fulani, au kuzunguka kwenda kuombewa na watumishi wakati wewe mwenyewe unaweza kujifungua..KUMCHA BWANA ndio msingi wa kila kitu!!

Vivyo hivyo ili kupata mafanikio ya kimwili ipo njia ambayo Mungu alishaiweka ukiikosa hiyo utaona kama vile Mungu kakuacha kwasababu Mungu siku zote anatembea katika kanuni zake na si katika kanuni zetu sisi tunazotaka yeye azitembelee. Tumekuwa tukimkumbusha Mungu kila siku tukisema “Mungu umesema; Utatubariki mijini, utatubariki mashambani, utatubariki tuingiapo utatubariki tutokapo, utatubariki kapu letu, na vyombo vyetu vya kukandia unga, atatufanya kuwa vichwa wala si mikia, atatubariki mifugo yetu na uzao wa matumbo yetu n.k.”

Ni wimbo ambao tumekuwa tukiuimba pengine pasipo kuona matokeo yoyote, na kufanya watu waishie kuzunguka kutoka kwa nabii huyu hadi nabii huyu,.Nataka nikuambie tu ndugu yangu mtu anayekutamkia kwamba “pokea baraka mwaka huu”, ki-uhalisia ni kwamba huyo mtu hajakubariki bali “AMEKUTAKIA TU KHERI”..kama vile tu mtu anavyokutakia Kheri ya mwaka mpya, au kheri ya maisha marefu.

BARAKA HALISI INATOKA WAPI?

Tumesahau Neno moja katika hiyo mistari ambalo ni la muhimu sana nalo ni “IKIWA”..”IKIWA UTAKAPOSIKIA SAUTI YA BWANA MUNGU WAKO”

Kumbukumbu 28:1 inasema; ITAKUWA UTAKAPOSIKIA SAUTI YA BWANA, MUNGU WAKO, KWA BIDII, KUTUNZA KUYAFANYA MAAGIZO YAKE YOTE NIKUAGIZAYO LEO, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.

5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.

6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo….”

Kwahiyo unaona hapo NJIA Mungu aliyoiweka ili kupokea hizo baraka, ni KWA KUYATUNZA NA KUYAFANYA MAAGIZO YOTE YA MUNGU, ambayo ki uhalisia ni wachache wanafanya hivyo, utakuta mtu ni fisadi au mla rushwa bado anakwenda mbele za Mungu na kumwomba baraka, utakuta mtu anaishi maisha ya anasa halafu anamfuata mtumishi amwombee abarikiwe, utakuta mtu hata hana mpango na Mungu na yeye pia anakimbilia kwenda kununua mafuta ya upako, hiyo ni sawa na uganga wa kienyeji tu, ni vyema ukaacha na kutubu.

Njia pekee Mungu aliyoiweka ni KUMCHA yeye na kuyashika aliyokuagiza, kwa kuzingatia hivyo hautahitaji kwenda kwa mtumishi yoyote akuombee, au kukesha kuomba, au kutumia mafuta au chumvi vinavyoitwa vya upako, ili kufanya mambo yabadilike, Mungu mwenyewe atakutengenezea njia, kwa wakati wake, kwasababu anasema yeye mwenyewe anajua kuwa tunahaja na hayo yote.

Na ndio maana biblia inasema..

Mathayo 6:32-33 “…kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

Usihangaike huku na huko, hakutakusaidia chochote MCHE MUNGU.

Vivyo hivyo ukitaka CHEO (ukubwa mahali popote), njia ipo nayo ni “kuwa mdogo kuliko wote” jinyenyekeze kwa maana ajishushaye atakwezwa na ajikwezaye atashushwa,usitumie njia za kujipendekeza kwa watu ili upate kibali wewe jishushe kuwa mnyenyekevu hakuna mtu yeyote asiyependa mtu mnyenyekevu..hizo ndio NJIA zilizowekwa na Mungu, ukitaka kupokea vitu kutoka kwa watu, Bwana Yesu alisema.. katika 

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa. ” 

Hata siku zote ili bomba litoe maji ya kujaza vyombo vingi ni sharti lifunguliwe, lakini likifungwa litabakia na maji yake ya ndani tu..vivyo hivyo ukitaka upokee “favour” inakupasa utoe kwa wengine na kwa Mungu.

Ukitaka furaha, amani na watu, mche Bwana kwa kuzishika amri zake,Mithali 16:7 ” Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.”

Sulemani mtu aliyekuwa na mafanikio na mwenye utajiri mwingi kuliko watu wote waliomtangalia na waliokuja baada yake, japo katika ufahari wake wote alihitimisha na kusema..

Mhubiri 12:13-14″ Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. “

Sisi ni akina nani tusimche Bwana?.

Ubarikiwe sana na Bwana wetu YESU KRISTO.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

MCHE MWORORO.

FANYA KAMA UONAVYO VEMA.

TUKAZE MWENDO KWA TULIYOANDALIWA.

KANUNI JUU YA KANUNI

ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

Daudi aliyekuwa mfalme wa Israeli, mwenye sifa ya kuupendeza moyo wa Mungu na ushujaa mwingi, lakini chanzo cha kunyanyuka kwake kilikuwa cha kipekee sana, habari hii tunaisoma katika 1 Samweli 17, Tunaona pale ambapo Daudi alitoka kama mtu asiyejua wala kuwa na uzoefu wowote wa vita na kumuua mtu ambaye alikuwa jemedari wa vita wa jeshi la wafilisti(Goliathi).

Kumbuka Daudi alikuwa ni kijana mdogo tu na mchungaji aliyekuwa anakaa maporini akichunga kondoo wa baba yake, hii ni shughuli isiyokuwa na mahusiano yoyote na vita, tunasoma na ilipofika wakati vita kutokea wafilisti kupigana na waisraeli ndipo wafilisti wakamnyanyua Goliathi aliyekuwa hodari wa vita, kwa ukubwa wake na uzoefu wake wa vita, hakuna shujaa yoyote wa Israeli aliyeweza kumkaribia kupigana naye kwa hofu. 

Tunasoma kijana mmoja mdogo Daudi asiyekuwa miongoni mwa wale mashujaa wa Israeli waliokuwa na ujuzi wa vita kwa miaka mingi, aliweza kunyanyuka na kumwangusha yule simba wa wafilisti.

Lakini siri ya Daudi kushinda na kuwa jemedari ni ipi?

Tukisoma …

1 Samweli 17:31 “Na maneno hayo aliyosema Daudi yaliposikiwa, watu wakamweleza Sauli; naye akatuma mtu kwenda kumwita.

32 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.

33 Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.

34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,

35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.

36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

37 Daudi akasema, BWANA ALIYENIOKOA NA MAKUCHA YA SIMBA,NA MAKUCHA YA DUBU, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe. “

Hapa katika habari hii tunaona Daudi akitoa ushuhuda wa matendo makuu ya Bwana aliyomtendea, katika nafasi yake ya udogo aliyokuwa nayo, jinsi alivyoweza kuwaua dubu na simba alipokuwa akichunga kondoo wa baba yake, AKAHESABU kuwa kama Mungu aliweza kumshindania katika makucha ya maadui wa mifugo yake, hatashindwa pia kumwokoa kutoka katika makucha ya maadui wa ndugu zake na Taifa lake Israeli.

Pengine Sauli alitegemea kusikia kutoka kwa Daudi ushuhuda wa madaraja mangapi ya uluteni amepitia, au mafunzo mangapi ya kijeshi amepitia, alitegemea kusikia aidha kama alishawahi kupitia mafunzo ya ukomandoo, lakini badala yake aliishia kusikia shuhuda za mbuzi na kondoo zaidi ya yote alionekana ni kijana laini hata mkuki hawezi kubeba vizuri, hivyo kwakuwa hawakuona jemedari mwingine kwa kujitokeza kupambana wakaona wamwache aende tu kama vile kwa shingo upande.

Lakini hawakujua kuwa Daudi anao UFUNUO wa Mungu ni nani kwake, ALIMUHESABIA MUNGU kuwa ni muweza wa yote. Hivyo hakutumia njia zao walizozizoea kumkabili adui yake, hakwenda na chepeo na dirii bali alikwenda na JINA LA BWANA WA MAJESHI (YESU KRISTO)

1 Samweli 17:45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.

46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya aWafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. “

Amina.

Tunaposoma habari hii tunajifunza nini?

Kumbuka katika safari ya kuwa askari wa Mungu kwenye shamba lake, jua tu utakumbana na changamoto nyingi ikiwemo kukatishwa tamaa, na kibaya zaidi watakao kukatisha tamaa sio watu wengine bali ni hao askari wenzako waliokutangulia katika hilo shamba, kama vile tu Daudi alivyokatishwa tamaa na wale ndugu zake, walimwambia ana kiburi, na wakataka kumfukuza arudi kuchunga mbuzi za baba yake, lakini Daudi alipuuzia.

Vivyo hivyo inawezekana umesikia wito wa kumtumikia Mungu, watu wa kwanza utakaokutana nao na kukuvunja moyo hawatakuwa watu wasiomjua Mungu bali ujue tu watakuwa ni hao waliokutangulia katika kazi ya Bwana, sio kana kwamba ni watumishi wa shetani la! lakini ndivyo ilivyo, pale utakaposema tu nataka kumtumikia Mungu utasikia “ni chuo gani cha biblia umepitia wewe? “…utaulizwa “umepitia kwanza chini ya huduma ya nani mpaka wewe utake kumtumikia Mungu”..

Utasikia wenye ujuzi wameshindwa wewe ni kama nani, hata biblia huijui vizuri, kwanza ndio umeokoka juzi tu, mchanga wa kiroho, walau hata ungekuwa umepitia kwanza mafunzo fulani ndio uanze..na vitu vinavyofanana na hivyo vya kukatishwa tamaa vingi vitakuja, lakini fahamu kuwa huyo ni shetani akitaka kukatisha tamaa usisonge mbele, kama vile Daudi hakutumia uzoefu unaofanana na wao kumuua Goliathi bali alitumia uzoefu Mungu aliomshindania katika maisha yake aliyokuwa anapitia katika ufugaji wake..na kwa kufanya vile aliweza hata kuwa shujaa, kushinda hata wale askari waliokuwa wanajiona wenye uzoefu mwingi na kupitia mafunzo mengi ya vita kabla yake.

Inawezekana una wito fulani wa kumtumikia Mungu, lakini kulingana na mazingira ya watu waliokutangulia katika huduma yanakufanya ujione kama haustahili, kwasababu haujapitia chuo cha biblia, au hujaenda shule, au hujakaa chini ya mtumishi yeyote unajiona hauwezi, fahamu jambo moja kuwa “UNAWEZA katika yeye akutiye nguvu“..Kwamba unasikia wito wa Mungu ndani yako, kaza mwendo, uendee na Mungu atakuwa na wewe

Kumbuka kama Daudi alivyotumia ujuzi wa mambo yaliyopita ya maisha yake na kumhesabia Mungu kuwa anaweza kumpigania hata sasa na wewe vivyo hivyo kumbuka mambo yote ambayo uliona kabisa Mungu alikupigania kama sio yeye ungekwama, au kama sio yeye usingukuwepo leo, tumia huo huo uzoefu Mungu aliokuonekania katika maisha yako uulete katika kazi ya Mungu. Mungu yule yule aliyekupigania kule ndio huyo huyo atakayekupigania kwenye kazi yake.

Watakao mwangusha Goliathi(shetani) kwenye kanisa hili la mwisho hawatakuwa wanaodhaniwa kuwa wamekuwa katika huduma kwa muda mrefu, bali watakuwa ni vijana(wa kiroho) kama wakina Daudi wenye ufunuo, ambao watamwamini Mungu katika utimilifu wake wote. Hao wengine wataua wafilisti tu lakini Goliathi ni kwa Daudi.Kwa maana Bwana Yesu alisema,

 Mathayo 11:25-26 ” Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. 

Na pia alisema..Mathayo 20:16 “Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho. “

Hivyo ndugu ni wajibu wetu kusonga mbele pasipo kukwazwa na jambo lolote, usitazame mpaka upate kitu fulani ndio ufanye kitu kwa ajili ya Mungu. 2Wakorintho 6:2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

Ni maombi yangu Bwana atupe neema hiyo ya kuwa mashujaa wake kama Daudi.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

UNAFANYA NINI HAPO?

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU

KULINGANA NA 1WAKORINTHO 3:10-15, KAMA INAVYOSEMA..NI KWA NAMNA GANI KAZI YA MTU ITATEKETEA, NA KUPIMWA KWA MOTO?

SHETANI KWA SASA NI MZURI WA UMBO KAMA MALAIKA WATAKATIFU AU NI MWENYE MAPEMBE NA MAKWATO NA MAKUCHA MAREFU?


Rudi Nyumbani

Print this post

UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?

Kuna namna nyingi watu wanavyompokea YESU katika maisha yao, lakini sio namna zote zina manufaa kwa ajili ya uzima wa mtu. Ni muhimu sana kufahamu kusudi la msingi la Bwana Yesu lililomfanya aje duniani vinginevyo utadhani kwamba unatembea na Mungu kumbe Hayupo na wewe.

Tunaweza tukajifunza baadhi ya mifano katika biblia: Mahali fulani Petro alipokuwa anavua samaki, katika kuhangaika kwake usiku kucha bila kuwa na matumaini ya kupata chochote alimuona mtu anakuja asiyemfahamu na kuanza kufundisha watu kando kando ya Habari pembezoni mwa chombo chake, kisha alipomaliza akamwambia Petro tweka ukavue samaki vilindini, pengine Petro alimuona kuwa ni mtu wa Mungu hivyo akaona ayatii yale maagizo, lakini walipofika hata sio mbali, walipata samaki wengi sana kimiujiza kiasi cha nyavu kuweza kukatika, mpaka iliwabidi waombe msaada kwa wavuvi wenzao waliokuwa kando kando yao, nao pia wakajaza vyombo vyao kwa wingi wa samaki wale.

Lakini je! jambo gani lilitokea baada ya hapo?

Tunasoma;

Luka 5:4″ Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;

7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama.

8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, ONDOKA KWANGU, KWA KUWA MIMI NI MTU MWENYE DHAMBI, BWANA.

9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;

10 na kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu.

11 Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, WAKAACHA VYOTE WAKAMFUATA.

UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?

Hapo ni jambo gani tunajifunza? Petro baada ya kuona ule muujiza wa samaki saa hiyo hiyo alijisalimisha kwa Bwana na kumwambia, ondoka kwangu mimi ni mwenye dhambi!!..muujiza ule ulimfanya ajihukumu maisha yake akijua kuwa ni Mungu amesimama mbele yake na kusema naye, na zaidi ya yote aliacha hata ile kazi aliyokuwa anaifanya pamoja na wale samaki aliowapata na kumfuata YESU , Lakini kwa mtu mwingine asiyekuwa na ufahamu angechukulia lile tendo kuwa ndio FURSA ya kumtumia YESU kama chombo cha baraka katika kazi zake za uvuvi, kama wanavyofanya watu wengi leo.

Mtu angesema Mungu kaona mateso yangu ya kuteseka kwangu usiku kucha na leo hii kanikumbuka na kunibariki..Angesema leo hii Mungu kajifunua kwangu nimemuona biashara yangu inafanikiwa, Bwana kanipa utajiri jana tu nilikuwa maskini leo nimekuwa tajiri, Bwana kawaaibisha maadui zangu,

Nimeuona mkono wa Mungu katika maisha yangu mtaji wangu umeongezeka… Lakini kumbuka kwa PETRO haikuwa hivyo, hakuona hayo mambo kwa BWANA, alijua kuwa ile ishara sio kwa ajili ya tumbo lake bali ilikuwa kwake kama chachu ya yeye KUMTAZAMA KRISTO. Na ndio maana tunaona baada ya hapo alifikia mpaka hatua ya kuacha vyote na kumfuata YESU.

Lakini tunaweza tukajifunza pia katika kundi lingine la watu, na hili tunasoma habari zake katika kitabu cha Yohana 6:1-32. Watu hawa walitendewa muujiza unaofanana na ule wa Petro isipokuwa hawa Bwana aliwagawanyishia mikate 5 na samaki 2 kwa maelfu yao,

Lakini walipoona ile ishara walitaka kwenda kumshika wamfanye mfalme, sio kwasababu awe mfalme kwao ili waokolewe bali kwasababu waliona kama akiwa mfalme wao atawasaidia katika vipindi vya njaa na vigumu kwa kuwashushia chakula kimujiza kama vile Musa jangwani. Ni sawa tu na sasa hivi watu wanamtafuta Bwana Yesu ili awavushe tu katika vipindi vyao vigumu na si zaidi ..Tunasoma

Yohana 6:24-27″

24 Basi mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.

25 Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa?

26 Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ISHARA, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

27 Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. “

Hiyo ndio sababu YESU aliwakimbia, hakuambatana nao, kwasababu walikuwa wanaangalia TUMBO na sio BWANA. Walimchukulia kama yeye ni fursa ya kuwafanikisha katika mambo yao lakini mambo mengine zaidi ya hapo hawakutaka,

Lakini tunaona wakati mwingine Bwana alimponya kipofu mmoja aliyekuwa vile tangu kuzaliwa kwake, na baada ya kuponywa alijua tu ni YESU amemponya ila hakumwona, lakini kwa kuzidi kutaka kumjua na kuushikilia ushuhuda wake mpaka walipomfukuza nje ya sinagogi kwasababu ya kiu yake kwa YESU, ndipo YESU akamjia na kujifunua kwake na kumjua, lakini hapo kabla alikuwa hamjui japo aliponywa na yeye(Yohana 9).

Vivyo hivyo katika maisha ya sasa, Bwana anawatendea miujiza watu wengi lakini hawatambui kwanini Mungu anawatendea hiyo miujiza, wanadhani kwa kuwatendea hivyo ni Mungu kajifunua kwao! Hapana, miujiza ni kitu(chambo) cha kuwafanya watu wamgeukie yeye, hivyo kusudi kubwa la yeye kufanya hivyo ni kuwafanya watu watubu, au wazidi kumsogelea karibu na sio kuwarahisishia mambo tu.

Mungu anapokuponya ugonjwa wako, hapo Bado haujamwona Mungu, Mungu kukufanikisha katika kazi za mikono yako, hapo bado haujamwona Mungu, ni sawa na wale waliovunjiwa mikate nyikani, wakala wakashiba na kuishia hapo hapo, Bwana kukufaulisha katika mambo yako hapo bado haujampata yeye, mpaka pale utapotambua maana ya yeye kukunyooshea mkono wake ni ipi?.

Siku utakapotambua UTATUBU na KUJINYENYEKEZA MBELE ZA BWANA..utafikia mahali na kusema kama Petro alivyosema..ONDOKA KWANGU MIMI NI MWENYE DHAMBI, kuonyesha kuwa haustahili mbele zake..Ukilijua hilo hautatamani hata vile vitu alivyokubariki navyo bali yeye tu wala hautamchukulia Bwana kwa jinsi unavyomchukulia leo.

Bwana aliyesema fedha na dhahabu ni mali yangu, ndiye huyo huyo alisema “ITAKUFAIDIA NINI UUPATE ULIMWENGU MZIMA NA KUPATA HASARA YA NAFSI YAKO?”. Kumbuka kusudi la msingi kabisa la Bwana Yesu kuja hapa duniani sio kutufanya sisi kuwa mabilionea, au kutuponya magonjwa yetu, au kutufanikisha katika mambo yetu, hapana bali ni KUTUOKOA sisi kutoka katika dhambi, kama tafsiri ya jina lake lilivyo {YESU= YEHOVA MWOKOZI}, ndipo mambo mengine yafuate.

Hivyo ndugu ishara na miujiza yote Mungu anayokutendea leo, ni kukufanya wewe utubu, akuponye roho yako, kumbuka Bwana ataanza tu KUJIFUNUA KWAKO pale utakapoamua kumruhusu afanye kazi katika maisha yako, lakini ukiangalia KIGANJA CHAKE tu atakupa nini! atakukimbia kama alivyowakimbia wale wasamaria hivyo ule wokovu hautafunuliwa kwako ambacho ndio kiini cha maisha ya kila mwanadamu…Siku ile atakuambia ulinifuata mimi si kwasababu ulitaka kuokolewa bali kwasababu ulitaka gari, ulitaka pesa, ulitaka mtoto, ulitaka kuolewa. Na kundi la namna hii ndilo kubwa kabisa katika kanisa hili tulilopo la siku za mwisho.

Maombi yangu ni utafakari mambo yote makuu Mungu aliyokutendea ujue kuwa hayo ni kukutaka utubu kabla wakati haujaisha, utubie uasherati wako, ulevi wako, wizi wako, ufisadi wako, usengenyaji wako, utukanaji wako, ibada zako za sanamu n.k.

hii ndio sababu ya Mungu “kuruhusu” miujiza na ishara nyingi kupita kiasi zitendeke KILA MAHALI katika kizazi chetu hichi tunachoishi, kila kitu unachomwomba Mungu hata kama ni mwenye dhambi anakupa, unaumwa anakuponya, sio kwasababu anafurahishwa na wewe, bali anataka utubu, lakini usipotubu alisema maneno haya:

Mathayo 11:20-24 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu HAIKUTUBU.

21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.

22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.

24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe. “

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/Ushauri/Ubatizo/ Whatsapp. Tupigie namba hizi: +255693036618


Mada Nyinginezo:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?

KATIKA KITABU CHA UFUNUO 16:5, TUNAONA AKITAJWA MALAIKA WA MAJI SWALI HUYU MALAIKA WA MAJI NI NANI? NAJE! KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?

HABARI ILE YA PILATO KUCHANGANYA ZILE DAMU ZA WAYAHUDI NA PAMOJA NA DHABIHU ZAO,(LUKA 13) ILIHUSU NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post