Tunaona kuna baadhi ya watu ambao majina yao yameongezwa vionjo kwa mbele, kwa mfano Simoni Petro, Yuda Iskariote, Tomaso pacha, Simoni mkananayo, Yohana Mbatizaji n.k
Watu hawa ambao majina yao yanaonekana kuongezewa vionjo mbele yake ni kwa lengo la kuwatofautisha na watu wengine wenye majina kama ya kwao. Na vionjo hivyo vilivyokuwa vinawekwa ni aidha kulingana na mahali (miji) wanayotokea, au majina ya wazazi wao, au matendo/huduma wanazozifanya.
Wafuatao ni baadhi ya majina ya watu yaliyoongezewa vionjo kulingana na Matendo waliyokuwa wanayafanya;
Kulingana na Mahali walipotokea;
Kwahiyo ili kumtofautisha na Simoni Petro au Simoni mwingine yeyote, ndipo huyu akaitwa Simoni Mkananayo au Simoni Zelote.
Kulingana na majina ya Wazazi/ Ndugu
1 .Yakobo wa Alfayo: Yakobo alikuwa ni mtoto wa Mtu aliyeitwa Alfayo, Aliitwa hivyo ili kumtofautisha na akina Yakobo wana wa Zebdayo na wengine waliokuwepo kwa wakati huo.(Marko 3:18).
2. Yuda mwana wa Yakobo: Huyu alikuwa ni mwanafunzi wa Bwana Yesu ambaye pia aliitwa kwa jina lingine “Thadayo”(Marko 3:18). Ili kumtofautisha na Yuda aliyemsaliti Bwana Yesu, ndipo kwa jina lingine akajulikana hivyo kama Yuda wa Yakobo au Thadayo.
3. Tomaso aitwaye Pacha (Yohana 20:2)– Ni kuonyesha Tomaso kuwa alikuwa na Pacha lakini hakutajwa katika maandiko huyo pacha wake alikuwa ni nani, ila aliitwa hivyo ili kumtofautisha na wakina Tomaso wengine waliokuwepo pale.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Je jina lako ni nani? Na linabeba ujumbe gani?… >>JINA LAKO NI LA NANI?
Maran atha
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
MAANA YA MAJINA NA TAFSIRI ZAKE.
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Tukimtafakari Yesu, jinsi alivyopendwa na Mungu kiasi cha kukabidhiwa vyote na Baba, jinsi alivyojaliwa kutenda miujiza mikubwa ambayo hata vitabu vyote duniani vingeandika habari zake visingetosha kueleza biblia inasema hivyo, tunatamani sana kuwa kama yeye. Yesu ni mtu pekee ambaye alikuwa akimwomba Mungu kitu chochote anapewa saa hiyo hiyo, Lakini mwisho wa siku anakuja kutoa siri ya kukubaliwa kwake..Siri ambazo anasema manabii wengi na wafalme walitamani kuyafahamu hayo wasiyafahamu(Luka 24:10). Lakini mimi na wewe tunazifahamu.
Na siri mojawapo ni hii inayohusiana na namna ya kudili na maadui zetu na wale wanaotuudhi. Alisema hivi,
Mathayo 5:44 “lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi”,
Mwanzoni nilipokuwa nasoma huu mstari nilidhani nimeulewa vizuri, lakini baadaye nilikuja kujua kimatendo kuwa nipo mbali sana nao, nilipotafakari matukio ambayo niliudhiwa na watu, Na muda niliotenga kuwaombea hao watu walioniudhi na kunichukia.. Nikagundua kuwa sijawahi kufanya hivyo.
Ni kweli nilisamehe, lakini kusamehe kwangu kuliishia tu katika ‘kusamehe’ na baada ya hapo ikawa ni kujiepusha naye ili asiniudhi tena. Lakini kwa Mungu huo bado sio ukamilifu, Ukamilifu ni kumwombea huyo anayekuudhi.. Na Zaidi sana kumpenda yule ambaye unahisi ni adui kwako.
Bwana wetu Yesu Kristo ni mtu aliweza kuishi kile alichokisema, Vinginevyo angekuwa ni mnafki.. Yeye ni mtu ambaye aliweza kuishi na mmoja wa maadui zake hatari sana. Adui aliyemuuza mbele ya macho yake. Na huyo si mwingine Zaidi ya Yuda. Yesu alimjua tangu mwanzo kuwa ndiye atakayemsaliti, Lakini hakuwahi kumfukuza, hakuwahi kumnenea mabaya, Zaidi sana alimwita RAFIKI, na pale alipokula chakula kizuri alimchagua Yuda kula naye(Yohana 13:18).. Na tunajua Yesu si mnafki, alipomwita Yuda rafiki(Mathayo 26:50), alimaanisha kweli, kwamba yule alikuwa ni rafiki yake tena hata Zaidi ya mitume wengine.
Tengeneza picha Japo Yesu alijua unafiki wake, lakini ndani yake hakukuwa na sababu ya kutomwona kama yeye ni rafiki tu. Aliweza kuishi naye miaka yake yote ya kiutumishi, akamwongezea na neema juu ya kutoa Pepo na kufanya miujiza. Alipopanda kuwaombea wanafunzi wake, alimwombea na Yuda pia, japokuwa alijua kuwa huyo ndiye msaliti wake. Yuda hakuwahi kumrudishia fadhili Yesu wakati wowote, hata kipindi kile yule mwanamke anamwagia marahamu, yeye bado alipinga. Lakini Yesu alimpenda.
Tujiulize na sisi tuliookoka tunaweza kuwa kama mwana wa Mungu Yesu Kristo. Kuishi na maadui zetu tunaojua wanakwenda kutuchinja na Zaidi sana tunawaombea na kuwabariki? Huo ndio ukamilifu ambao Mungu anataka kuuona kwetu.
Hii ndio sababu kwanini Yesu anasema tuwe watu wa namna hiyo na si vinginevyo anasema..
Mathayo 5:45 “ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Umeona? Kwasababu tabia ya Mungu ndio hiyo, anawarehemu watu wote, wanaomshukuru na wasiomshukuru, hata maadui zake, anawapa chakula. Kwasababu anajua huwenda siku moja watatubu. Hata sisi pia kabla ya kuokolewa, tulikuwa katika dhambi, tulimkosea sana yeye, lakini hakututendea jambo lolote baya, akatusamehe,. Vivyo hivyo anataka na sisi tufanye kwa maadui zetu, na kwa wale wanaotuchukia.
Ikiwa ni mfanyakazi wako anakuudhi, chukuliana naye tu..Hamna namna, mwombee, mbariki, usiwe mwepesi kumfukuza kazi. Ikiwa ni mpendwa mwenzako anakukwaza mara kwa mara, hupaswi kumsamehe tu na kujiepusha naye mbali, bali umwombee, na Zaidi umwite rafiki yako.
Tabia kama hii, haitokani na sisi wanadamu bali na Mungu, kwa nguvu zetu hatutaweza, lakini tukiwa na Neno la Mungu sana mioyoni mwetu, atatusaidia kuidhihirisha tabii yake hii ya kiMungu. Na kama tukifaulu kushinda, Basi tujue ndivyo Baba atakavyotukaribia, na kujifunua kwetu. Kwasababu tunafanya yanayompendeza.
Hivyo, tumwombe Bwana atusaidie, na sisi tuonyeshi bidii katika kudhihirisha jambo hilo, ili tuwe wakamilifu kama yeye alivyomkamilifu.
Tahadhari:
Epuka mahubiri, unayoambiwa walete maadui zako hapa tuwapige kwa moto wa Roho Mtakatifu wafe. Epuka sana, hayo hayakusaidii kitu Zaidi sana yanakuongezea chuki na visasi moyoni mwako. Ambayo ni zao la shetani na sio Roho Mtakatifu. Bali penda ushauri wa Bwana Yesu, kisha uutende hata kama ni mgumu, lakini ndio njia yenyewe ya kumfikia Mungu, hakuna nyingine.. Wapende maadui zako, kisha waombee
Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
USIMPELEKEE BWANA MASHITAKA, YA MAADUI ZAKO.
YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.
BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?
Jibu: Iskariote sio jina la mtu fulani, au la mzazi wa Yuda, bali ni jina lenye maana ya “Mtu wa Keriothi/ Kariote”…
Neno Iskariote ni neno la kigiriki lililoungwa na maneno mawili: “Is” ambalo maana yake ni “mwana wa” na la pili ni “Kariote”..likimaanisha mji wa Kariote au Keriothi
Kwahiyo ukiunganisha maneno hayo mawili maana yake ni “Mwana wa Keriothi”
Na Keriothi ni mji uliokuwepo katika Nchi la Moabu, ambayo kwasasa ni maeneo ya nchi ya Jordani.
Na Wamaobu walikuwa ni watu wa mataifa, hawakuwa waIsraeli, kwa urefu kuhusu Taifa hili unaweza kufungua hapa >>> MOABU NI WAPI
Sasa swali ni je! Kwanini Yuda aitwe hivyo, na asiitwe tu Yuda! Kwanini atambulike kama Mwana wa Keriothi(Iskariote)?… kulikuwa na umuhimu gani yeye kutajwa kwa jina hilo?.
Jibu rahisi ni kwamba, alitajwa vile ili kumtofautisha na wakina Yuda wengine, kwasababu kulikuwa na watu wengi wanaoitwa Yuda ambao pia walikuwa wanafuatana na Yesu. Na Kuna mwingine alikuwa mdogo wake Yesu.
Kwa mfano utaona kuna wanafunzi wawili wa Bwana Yesu waliokuwa na majina yanayofanana..wote walikuwa wanaitwa Simoni, sasa ili kuwatofautisha ndio mmoja akajulikana kama Simoni Petro na mwingine Simoni Mkananayo. (Mathayo 10:2-4).
Vile vile kulikuwa na wanawake wengi waliomfuata Bwana walioitwa Mariamu, sasa ili kuwatofautisha hao akina Mariamu, ndipo hapo wengine wakatajwa kulingana na miji waliyotokea mfano Mariamu aliyetolewa pepo saba alijulikana kama Mariamu Magdalene, kufuatia mji aliotokea ujulikanao kama Magdalene. (Luka 8:2).
Na Yuda Iskariote aliitwa hivyo kufiatia mji ambao Baba yake alitokea (Keriothi).
Yohana 6:71 “Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.
Soma pia Yohana 13:2, na Yohana 13:26, huenda baba yake Yuda alikuwa ni myahudi lakini mwenyeji wa Kerioth pamoja na Yuda mwanae.
Kuhusiana na mji wa Keriothi au Kariote, pitia mistari ifuatayo; Amosi 2:2, Yeremia 48:24, na Yoshua 15:25.
Na sisi Bwana anatujua majina yetu kulingana na tabia zetu.
Kutoka 33:17 “BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako”
Mbele za Mungu kila mtu anajulikana kwa tabia yake…fulani mcha Mungu, fulani mwombaji, fulani mkaribishaji, fulani mwizi, fulani mzinzi, fulani msengenyaji.
Bwana atujalie tujulikane kwa majina mazuri na mema mbele zake ili tupate neema.
Kutoka 33:17 “BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako”
Maran atha
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.
Jibu: Kulikuwa na tukio zaidi ya moja la Bwana Yesu kupakwa mafuta…Tukio la kwanza ni hilo tunalolisoma katika injili tatu, (Mathayo 26:6-13 na Marko 14:3-8 na Yohana 12:1-3), ambapo biblia inaonyesha moja kwa moja kuwa ni Mariamu ndugu yake Lazaro, ndiye aliyempaka Bwana Marhamu siku sita kabla ya pasaka.
Tusome,
Yohana 12:1 “Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
2 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye.
3 Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu”.
Lakini tukirudi katika Injili ya Luka, tunasoma tukio lingine ambalo linakaribia sana kufanana na hili la Bethania, ambapo biblia inasema alitokea mwanamke mmoja mwenye dhambi na kuanguka miguuni pake na kulia huku akimpaka mafuta.
Jibu: Turejee..
Luka 7:36 “Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
37 Na tazama, mwanamke MMOJA WA MJI ULE, ALIYEKUWA MWENYE DHAMBI, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.”
Sasa ni viashiria gani vinatuthibitishia kuwa yale yalikuwa ni matukio mawili tofauti?
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa haya ni matukio mawili tofauti, yaliyotokea kukaribiana na biblia haikumtaja Yule mwanamke wa Galilaya alikuwa ni nani?.. labda huenda alikuwa ni Yule Yule Mariamu alimpaka mara mbili, au ni mwanamke mwingine ambaye biblia haijamtaja jina lake.
Lakini hayo yote si ya muhimu sana kuyajua, (kwamba ni nani, au ni matukio mangapi) lililo la muhimu kulijua ni tendo hilo la kiimani wanawake hawa waliloyoyafanya.. sasa kujua kwa undani Siri iliyokuwepo katika kumpaka Bwana mafuta fungua hapa >>> AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.
Bwana atubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani? Ni mpangalio wake upoje kulingana na mwandishi?
JIBU: Kitabu Cha Zaburi hakikuandikwa na mtu mmoja, Bali ni mjumuisho wa waandishi mbalimbali. Kitabu hiki ndio kilichoandikwa na waandishi wengi kuliko vyote kwenye biblia.
Kiliandikwa katika nyakati mbalimbali Kwa kipindi Cha miaka elfu moja na zaidi..kitabu hiki kimebeba mashahiri, maombolezo, nyimbo na maombi.
Mfalme Daudi ndiye aliyeandika Kwa sehemu kubwa kitabu hichi;
Jumla Zaburi zilizojuliakana kuwa zimeandikwa na Daudi ni 73. Lakini pia zipo nyingine 2 ambazo hazikutajwa moja Kwa moja lakini waandishi wengine katika nyaraka zao walinukuu baadhi ya maneno kwenye Zaburi, na kusema ni ya Daudi.
Ambazo ni Zaburi 2 ambayo sehemu ya maandishi hayo yanatajwa katika Matendo 4:25,
Na Zaburi 95 Waebrania 4:7
Hivyo kudhaniwa kuwa Daudi aliandika Zaburi 75;
Hizi ndio orodha ya hizo Zaburi 73 alizoziandika yeye;
3-9
11-32
34-41
51-65
68-70
86
101
103,
108-110
122
124
131
133
138-145
2. SULEMANI
Mwandishi mwingine ni Sulemani yeye aliandika Zaburi mbili tu..ambazo ni Zaburi 72 na Zaburi 127″
3. ETHANI na HEMANI
Nyingine zimeandikwa na Ethani na Hemani, Hawa ni watu ambao waliokuwa na hekima nyingi mfano wa Mfalme Sulemani, wanatajwa katika vifungu hivi;
1 Wafalme 4:30-31
30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
Ethani aliandika Zaburi moja tu nayo ni Zaburi 89
Hemani pia aliandika Zaburi moja ambayo ni Zaburi 88
4. MUSA
Mwandishi mwingine alikuwa ni Musa yeye pia aliandika Zaburi 1 ambayo ni ya 90.
5. ASAFU
Zaburi nyingine 12 ziliandikwa na Asafu na familia yake.
Ambazo ni
50, 73-83
6. WANA WA KORA
Wana wa Kora, waliandika Zaburi 11
42, 44-49,84-85, 87-88
7. WASIOTAMBULIKA
Na Zaburi nyingine 48, zilizobakia hazijulikani waandishi wake.
Hivyo Kwa ufupisho ni kwamba Daudi aliandika Zaburi 73, Sulemani 2, Musa 1, Ethani 1, Hemani 1, Asafu 12, Wana wa Kora 11, wasiotambulika ni 48.
Bwana akubariki.
Ikiwa utapenda kupata uchauzi zaidi ya kitabu Cha Zaburi pitia link hii >> https://wingulamashahidi.org/2020/11/27/vitabu-vya-biblia-sehemu-ya-9-kitabu-cha-zaburi/
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
(Masomo maalumu kwa Wakristo, Je! Unajijua nafasi yako?.. je unajijua kuwa wewe ni manukato yanayokubalika na pia yasiyokubalika kwa upande mwingine?).
Manukato ni neno lingine la “Marashi”.. Na kazi ya manukato/Marashi ni kukifanya kitu kivutie, hakuna mtu anayejipaka marashi ili mtu amkimbie. Lakini changamoto ni kwamba haijalishi marashi yatakuwa ni mazuri kiasi gani, ni lazima kwa upande mwingine kuna mtu yatamtia kichefuchefu tu. (Si kila marashi yaliyo mazuri kwa mtu, yatakuwa mazuri kwa watu wote).. ni lazima upande mmoja utayakosoa tu.
Na siku zote, marashi yaliyokosolewa huwa yanatia kichefuchefu na hata wakati mwingine kumuumiza Yule anayeyasikia..
Kadhalika biblia inasema kuwa sisi ni Manukato ya Kristo. Na kama ni manukato ni lazima upande mmoja yatakubalika na upande mwingine yatakatalika.. Na siri ya manukato ya Kristo ni kwamba wengi wanayachukia zaidi ya wale wanayoyapenda..
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
15 KWA MAANA SISI TU MANUKATO YA KRISTO, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?
17 Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo”.
Wakristo wengi wanadhani kuwa wanapookoka bali wataanza kupendwa, na kukubalika na kupokea kibali kila mahali. Ni kweli hayo yanaweza kutokea kwasababu kwa Mungu yote yanawezekana.. Lakini fahamu kuwa wewe ni marashi mazuri lakini yenye kuleta harufu mbaya kwa wanaopotea..
Maisha ya usafi na ukamilifu unayoishi ni harufu nzuri kwa wanaookolewa, (Maana yake ni mfano mzuri wa kuigwa, kwa waongofu wapya na waaliookoka), kuomba kwako na kufunga kwako na kuhubiri kwako ni harufu nzuri kwa waliookoka kama wewe.
Lakini kwa wale ambao hawamtaki Yesu, fahamu kuwa maisha yako ni kichefuchefu kwao….ni lazima watakupinga tu, ni lazima watakuletea vita tu, ni lazima watakukosa tu, ni lazima watakurushia mishale tu..Kwasababu kwao wewe ni manukato yenye harufu mbaya, tena harufu inayoleta mauti kabisa…yaani maisha yako yanawahukumu..
Hili ni jambo la kufahamu wewe uliyempokea Kristo na kuokoka!.. Kamwe usifikiri kuwa utaendelea furaha yako ndani ya Kristo ni jambo linalovutia machoni pa wengine… Ukristo ni vita, unapoamua kuwa mkristo ni kama mtu aliyevaa kombati na kuingia vitani.. Kwahiyo tegemea kukumbana na maadui wa imani, watakaokukosoa na kukutatisha tamaa..
Yohana 15:18 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?
USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)