Ni muhimu kujua kanuni za kuomba, ili tusije tukajikuta tunapiga mbio bure, kwa kuomba maombi yasiyokuwa na majibu. Kwanza ni muhimu kumjua unayemwomba ni Mungu wa namna gani.. Usipozijua tabia za unayemwomba, na ukienda kumwomba..unaweza ukamchukiza badala ya kumpendeza.
Sasa zipo hoja nyingi, ambazo ni harufu mbaya mbele za MUNGU wetu, lakini leo tutajifunza hoja moja ambayo ni hoja inayoonekana kama Nzito, machoni petu, lakini mbele za Mungu wetu ni harufu mbaya..
Na hoja yenyewe ni ya KUWASHITAKI WALE TUNAOWAONA KUWA MAADUI ZETU, MBELE ZA MUNGU.
Hebu tusome kisa kifuatacho, kisha tujifunze tabia ya Bwana Yesu ambayo shetani katupiga upofu tusiijue…
Luka 12:13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, MWAMBIE NDUGU YANGU ANIGAWIE URITHI WETU. 14 Akamwambia, MTU WEWE, NI NANI ALIYENIWEKA MIMI KUWA MWAMUZI AU MGAWANYI JUU YENU?”
Luka 12:13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, MWAMBIE NDUGU YANGU ANIGAWIE URITHI WETU.
14 Akamwambia, MTU WEWE, NI NANI ALIYENIWEKA MIMI KUWA MWAMUZI AU MGAWANYI JUU YENU?”
Kikawaida hata mimi nilitegemea Bwana Yesu, angesuluhisha hii KESI!, Kwa kuwaweka mezani na kuzungumza na pande zote mbili, ili yule anayestahili HAKI apewe, na yule asiyestahili AONYWE!!.. Lakini ilikuwa kinyume chake!… Bwana Yesu anaanza kushughulika kwanza na huyu aliyeleta Mashitaka!… na kumwuliza..NI NANI ALIYEMWEKA YEYE AWE MWAMUZI JUU YAO, AU MGAWANYI!!!.. Ni kama vile Bwana anazikataa hizo mada!, ni kama vile havutiwi nazo, ni kama vile zinampotezea muda!!!. Ndio maana hata mashitaka ya Martha juu ya ndugu yake Miriamu hayakuwa kama alivyotegemea. (Luka 10:40-42).
Sasa maandiko yanasema Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele, hajabadilika, na hatabadilika (Waebrania 13:8)… kama aliyakataa mashitaka ya huyu mtu hadharani, dhidi ya adui yake, basi atakayataa hata na mashitaka yetu katika SALA!!!.. Kwasababu ni yeye yule, habadiliki.
Ni kweli umedhulumiwa kiwanja chako!, ni kweli umeonewa, ni kweli umestahili haki…Ila unapokwenda kwenye maombi, kamwe usimshitaki huyo unayemwona kama adui yako, kwasababu hutaambulia chochote!…maombi yako ni kama kichefuchefu tu kwa Bwana!..
Ni vizuri kumjua unayemwomba ana tabia gani kabla ya kumwomba!.. hii ndio shida kubwa inayosababisha watu wengi kutojibiwa maombi yao, na hawajui ni kwanini. Tatizo ni kwamba hawamjui wanayemwomba ana tabia gani.. Ndugu, Bwana Yesu hana tabia kama uliyonayo wewe, au niliyo nayo mimi na wala hutuwezi kumfundisha tabia zetu..na kamwe hawezi kufuata tabia zetu..na wala hana cha kujifunza kutoka kwetu.. sisi ndio tuna cha kujifunza kutoka kwake, na tunapaswa tuige tabia yake ili tufanikiwe.
Sasa tabia yake ni hii..
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lakini mimi nawaambia, MSISHINDANE NA MTU MWOVU; LAKINI MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI. 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, MSISHINDANE NA MTU MWOVU; LAKINI MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Maana yake ni kwamba kama mtu Kakupiga shavu moja bila kosa lolote, badala ya kwenda KUPIGA MAGOTI KUMSHITAKI KWA BWANA!.. wewe Mpe shavu la pili, alipige na hilo halafu nenda kapige magoti! Mshukuru Mungu kwakuwa umefanikiwa kumpa na shavu la pili alipige…Utakuwa umeyatenda mapenzi ya Mungu…na umeomba maombi yenye hoja… HALAFU SASA SUBIRIA MAJIBU YAKE!!!.
Mtu kakudhulumu kipande kidogo cha ardhi, mwongeze na mita kadhaa..halafu mshukuru Mungu..Hapo utakuwa umeukosha moyo wa Bwana Yesu kuliko unavyodhani!!!… Na utaona matokeo yake.. Ndani ya kipindi kifupi, utaona jinsi Bwana atakavyomtengeneza yule mtu, kwasababu atamgusa moyo na atajiona ni mkosaji, na utashangaa anakurudishia ile sehemu ya ardhi aliyokudhulumu, ndivyo maandiko yanavyosema.. kuwa Njia za mtu zikimpendeza Bwana, humpatanisha na maadui zake..
Mithali 16:7 “Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye”.
Kwasababu Bwana anataka Nuru yetu iangaze…kwamba watu wanapoyatazama matendo yetu mema, jinsi gani tulivyo wema..ndipo wapokee neema ya wokovu..lakini tukiwa watu wakaidi, wakushindana wa kutupiana maneno, wakushitakiana mchana kutwa na usiku kucha..bila shaka sisi hatutakuwa na utofauti wowote na shetani… maana tafsiri ya jina shetani ni MSHITAKI, AU MCHONGEZI. Usiku na mchana anatushitaki mbele za Mungu (Soma 1Petro 5:8 na Ufunuo 12:10). Sasa na sisi tusiwe mashetani wengine!!..kwa kupeleka mashitaka mbele za Mungu.
Ndugu, ukitaka baraka basi mwabudu na msikilize Bwana Yesu Kristo wa kwenye biblia, ambaye yupo hai sasahivi..na Bwana Yesu wa kwenye biblia ni huyu mwenye maneno yafuatayo..
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Na watumishi wake pia watakuwa na maneno hayo hayo…lakini pia yupo yesu mwingine asiyekuwa wa kwenye biblia, huyo anakuambia Mpige adui yako mchukie adui yako, ukimfuata huyo au ukiwafuata watumishi wake basi jua unaenda kuzimu.
2Wakorintho 11:4 “Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
VITA DHIDI YA MAADUI
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
Rudi nyumbani
Print this post
Utukufu kwa Mungu,kwa kweli nimebarikiwa sana na somo hili hakika haya ndiyo yalikuwa mafundisho ya YESU hasa na mitume.Barikiwa sana mwalimu.
Nini !ubatizo