Title July 2025

Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo.

SWALI: Tukisoma Kitabu cha Waebrania tunaona mwandishi akitaja vitu viwili vya Mungu visivyoweza Kubadilika ambavyo tumepewa viwe kama nanga ya Roho, je ni vipi hivyo? Au Maana yake ni nini?

Waebrania 6:17-19

[17]Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;

[18]ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

[19]tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,


JIBU: Ukisoma hiyo habari vifungu vya juu na vile vinavyoendelea mbele yake. Habari inayozungumziwa pale ni ya Ibrahimu na jinsi Mungu alivyompa ahadi ya mbaraka pamoja na uzao wake. Na jinsi alivyokuja kuitimiza

Lakini tunaonyeshwa ahadi ile pekee aliyopewa, haikutosha kumfanya Ibrahimu, aamini bali Mungu Ili kumthibitishia kuwa atavipokea kweli kweli basi aliongezea Na kiapo.

Mwanzo 22:15-17

[15]Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

[16]akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

[17]katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Kwasababu kiapo ni kifungo cha mwisho ambacho Mtu humaliza shuku zote, mashaka yote mijadala yote..

Ilimbidi Mungu aweke kiapo ijapokuwa angetimiza Ahadi zake bila kiapo. Lakini ilimbidi afanye vile ili kumpa uthabiti Ibrahimu juu ya maadhimio yake.

Hivyo mambo hayo mawili yasiyoweza Kubadilika ya Mungu ni;

1)Neno lake(ambalo lilikuja kama ahadi),

2) lakini pia Kiapo, ambacho hukata maneno yote.

Na kweli tunakuja kuona yote Mungu aliyomuahidi Ibrahimu yalitokea kama yalivyo..

Lakini Ahadi hiyo haikuishia kwa Ibrahimu, bali ilitimilizwa yote na Bwana wetu Yesu Kristo.

Ambao sisi tuliomwamini, tunaingizwa Katika ahadi hizo..alizozithibitisha Kwa kiapo kupitia Bwana wetu Yesu Kristo. Ambaye Mungu alimthibitisha kama kuhani mkuu wa milele mfano wa Melkizedeki kuhani Wa Ibrahimu (rohoni)..

Waebrania 7:21-25

[21](maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;)

[22]basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

[23]Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;

[24]bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.

[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Hivyo sisi tuna Neno la ahadi..kwamba tunaomwamini tunapokea uzima wa milele kama yeye.. Lakini pia jambo Hilo amelikolezea Kwa kiapo kuwa hatalibatilisha..Ni hakikisho kubwa sana..Haleluya!

Hivyo ni wajibu wetu kuendelea mbele kwaujasiri na bidiii katika imani na kumtumikia yeye kwasababu yupo pamoja nasi, wala kamwe hawezi kutuacha hata Iweje.

Kwasababu Neno lake ni hakika, alilotuahikikishia Na kiapo juu.

Je umempokea Bwana Yesu kwenye Maisha yako?. Fahamu kuwa hakuna tumaini lolote nje ya Kristo. Okoka leo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

Je mkristo anaruhusiwa kuoa mke wa ndugu yake aliyefariki?

Katika agano la lake, iliruhusiwa Kufanya hivyo, ikiwa mtu amefiwa na ndugu yake na hana mtoto, aliruhusiwa kwenda kumwoa mke wa ndugu yake ili amwinulie uzao, lakini halikuwa kwa lengo la kimahisiano ya kindoa kana kwamba ni wapenzi. Bali kwa kusudi tu la kumwinulia uzao.

Kumbukumbu la Torati 25:5-10

[5]Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 

[6]Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. 

[7]Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. 

[8]Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, 

[9]ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. 

[10]Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu. 

Halikadhalika tunapokuja kwenye agano jipya hatuoni pia agizo lolote la moja kwa moja linalokatazama ndugu kuoa mke wa ndugu yake aliyekufa…

Zaidi inasema mwanamke Yeyote anapokuwa mjane yupo huru kuolewa na ‘Yeyote’ amtakaye katika Bwana.. 

1 Wakorintho 7:39

[39]Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu. 

Warumi 7:3

[3]Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine. 

Hiyo ikimaanisha kuwa anaweza akawa huru kuolewa hata na ndugu wa kaka yake (aliyefariki)…

Lakini lazima tufahamu kuwa si kila jambo linalohalalishwa kibiblia linaweza likafaa katika mazingira yote au majira yote, yapo mambo mengine ya kuzingatia, mfano utamaduni wa mahali fulani..

Kwasababu Biblia bado inatuambia…

1 Wakorintho 10:23

[23]Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. 

Kwa mfano kwa wayahudi ilikuwa ni tamaduni Watu kusalimiana kwa ‘busu’ la upendo. Lakini katika mazingira ya jamii zetu jambo kama hilo huleta ukakasi, au kutoa tafsiri nyingine hata kama nia sio mbaya..ndio maana tunaishia kipeana mikono, na ikizidi sana kukumbatiana kwa jinsia tu zinazofanana.

 

Vivyo hivyo katika jambo hili, kuoa mke wa ndugu yako aliyefariki, kijamii halina munyu ndani yake.

 

Hivyo twaweza sema kijamii halikubaliki, lakini kibiblia halijakatazwa..ukiniomba mimi ushauri nitakuambia usifanye hivyo..kaoe pengine..lakini ukimwoa mke wa ndugu yako aliyekufa pia hujafanya dhambi ikiwa tu, pana makubaliano kamili katika pande zote mbili, lakini pia wewe mwenye uwe haupo katika ndoa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> 

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.

Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?

https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/bwana-yesu-alikuwa-anamaanisha-nini-kusema-marko-219%e2%80%b3walioalikwa-harusini-wawezaje-kufunga-maada

Print this post

Umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu

SWALI: Yule tajiri alimaanisha nini kumwambia Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini uuburudishe ulimi wake?

Luka 16:24

[24]Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

JIBU:

Habari hiyo la Tajiri na Lazaro, Bwana Yesu aliieleza kufunua uhalisia wa jehanamu jinsi ulivyo… Na mambo ambayo mtu aliyeukataa wokovu atakutana nayo baada ya kifo.

Anaeleza jinsi yule tajiri alivyokufa katika hali ya dhambi..na hatimaye akajikuta mahali pale pa mateso, ambapo hakutana hata ndugu zake wafike, tunaona hata alipoomba mtu atokaye kwa wafu aende kuwahubiria ndugu zake akaambiwa hawatashawishwa…Ni kuonyesha kuwa mahali pale palikuwa pa mateso Sana, kiasi cha kutaka mwingine yeyote kufika.

Lakini tukio lingine tunaonyeshwa akimwomba Ibrahimu Amruhusu Lazaro achovye ncha ya kidole Chake majini amburudishe ulimi wake, nalo pia akaambiwa haiwezekaia kwasababu kuna kizuizi kikubwa Sana katikati yao.

Sasa swali linakuja tukio lile linamaana gani Je kiu kile ni halisi au ni ufunuo?.

Bwana Yesu alipokuja duniani.. aliona Dunia nzima ina Kiu kikubwa sana.. na hivyo inahitaji maji ya kuweza iponya.

Sasa maji inayohitaji sio haya ya mtoni..bali maji ya rohoni ambayo ni ya uzima, na mtu pekee awezayo kutoa hayo ni yeye mwenyewe..hakuwahi kutokea mtu aliyeweza kuyatoa.

Kama tunavyojua mwili ukikosa maji, mwishowe utakufa..Ndivyo ilivyokuwa sisi sote, hapo mwanzo kabla ya Kristo, Wote tulikuwa wafu kiroho..

Utauliza vipi kwa watakatifu wa kale kama akina Musa na Eliya?…Wale walikuwa wanaishi kwa ahadi ya Kristo, Hivyo walitii madhihirisho yake aliyokuwa akijifunua kwao kwa namna mbalimbali huku wakiiongejea ahadi kamili ya ukombozi ambayo alikuja kuikamilisha yeye mwenyewe (Yesu Kristo) alipofufuka Katika wafu..(waebrania 11)

Yeye mwenyewe Alisema..

Yohana 7:37-39

[37]Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

[38]Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

[39]Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

Sasa kiu hii ni ya nini?

Ya maisha….

Tangu zamani mwanadamu amekuwa akitafuta ‘maisha’ ambayo hata sasa hajayapata…ndio maana wengi wanakimbilia kutafuta elimu, fedha na utajiri wakidhani kuwa ndio wamepata maisha, lakini hivyo vipo mbali sana na maisha …vitakufanya ule vizuri tu, unywe vizuri, ulale vizuri kama maandalizi ya heri ya kifo chako baadaye..kwasababu Haviwezi kukudumishia maisha.. vinapooza tu kiu..lakini haviondoi kiu.

Yesu amekuja kuondoa kiu.

Sasa watu Ambao watapuuzia kuyapokea maji hayo ambayo Yesu anatupa…wakifa Katika hali hiyo hiyo huko waendapo ni majuto makubwa.

Kwasababu watataka hata tone dogo la maji hawatapata…yaani kiwango kidogo tu cha neema ya uzima hawatapata…

Leo Yesu hatupi maji tu, kwa kipimo fulani bali anapanda kabisa chemchemi za maji ndani yetu Ambazo zinabubujika uzima wa milele.

Yohana 4:14

[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Madhara ya kukosa maji ya uzima si tu baada ya kufa…hata hapa Hapa duniani.. mtu ambaye hana Kristo rohoni anajulikana kama nchi kamena matokeo yake ni kuwa makao ya mapepo yanakuwa Ndani yake hata kama hujui..

Angalia Yesu alichokisema juu ya hilo.

Mathayo 12:43-45

[43]Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

[44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

[45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.

Yanakwenda mahali pasipo na maji…yaani moyo ambao hauna Kristo ndani yake.

Ndugu…umeona hatari waliyonao wenye dhambi, hapa duniani na baada ya kifo?

Shetani asikupumbaze, tubu leo kwa kumpokea Bwana Yesu katika maisha yako ili upate ondoleo la dhambi zako haraka sana.

Hizi ni siku za mwisho, dunia hii inakwisha…vilevile hujui ni siku Gani utakufa…Acha kuchezea maisha yako, ukafanana na yule tajiri aliyekosa maji ya uzima angali akiwa hai.

Okoka leo..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Jehanamu ni nini?

MILANGO YA KUZIMU.

ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.

Print this post

WALIKUWA WAKINUNUA NA KUUZA, WAKIOA NA KUOLEWA KAMA ISHARA YA KANISA !

Bwana Yesu alitutahadharisha kuwa karibia na kurudi kwake, tabia za watu zitabadilika na kukaribia kufanana na zile za watu wa Nuhu na Lutu.

Luka 17:26 “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.

27 Walikuwa WAKILA NA KUNYWA, walikuwa WAKIOA NA KUOLEWA, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa WAKILA NA KUNYWA, walikuwa WAKINUNUA NA KUUZA, wakipanda na kujenga;

29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.

30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu”.

Sasa ishara hii ya watu kununua na kuuza,  kuoa  na kuolewa na kula na kunywa ilikuwa inalenga makundi mawili, kundi la kwanza ni WATU WASIOMJUA MUNGU, na kundi la pili ni WATU WANAOMJUA MUNGU, hetu tuanze tathmini ya kundi moja baada ya lingine.

       1. WATU WASIOMJUA MUNGU.

Kipindi cha Nuhu na Sodoma na Gomora walikuwa wakila kwa anasa, na kunywa kwa kulewa, na wakamsahau Mungu, lakini pia walikuwa wakioa na kuolewa kwa ndoa haramu (maana yake za watu waliocha waume zao au wake zao, au wa jinsia moja) vile vile walikuwa wakinunua vitu haramu na kuuza vitu haramu kwa njia zisizo halali, ikiwemo dhuluma na rushwa, na utapeli na wakamsahau Mungu, hivyo gharika ikawachukua wote.

Ndicho kinachoendelea sasa kwa watu wengi walio nje ya wokovu, rushwa ni kitu cha kawaida kwao, kuoana kiholela ni kitu cha kawaida, (yaani mtu kuoa/kuolewa leo na kesho kuachana na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine ni jambo la kawaida), hali kadhalika kuhudhuria kwenye karamu za ulafi na kula bila kiasi pamoja na kulewa ni mambo ya kawaida kila mahali, ndio maana utaona Bar ni nyingi kila kona.

Lakini hiyo ni ishara kwa watu wasiomjua Mungu, ambayo kiuhalisia pia inatangaza kwamba tunaishi katika siku za mwisho, lakini hebu tuangalie kwa upande mwingine kwa watu wa Mungu (kanisa.)

     2. WATU WANAOMJUA MUNGU (Kanisa)

Utauliza je! Watu wanaomjua Mungu pia wanaangukia katika hili kundi la kula na kunywa, kuoa na kuolewa, kununua na kuuza?.. Jibu ni ndio!.. sasa labda utauliza ni kwa namna gani?.. hebu tusome maandiko yafuatayo..

Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,

17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.

18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, NIMENUNUA SHAMBA, SHARTI NIENDE NIKALITAZAME; tafadhali unisamehe.

19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.

20 Mwingine akasema, NIMEOA MKE, na kwa sababu hiyo siwezi kuja”

Nataka tuone huo udhuru hao watu walioutoa!.. Kumbuka hao ni waalikwa, maana yake watu wenye mahusiano na mwenye harusi, na huo ni mfano ambao Bwana aliutoa kuhusu karamu ya mwanakondoo itakayofanyika mbinguni baada ya unyakuo,

 Kwamba sasa anawaaalika watu, lakini waalikwa (yaani watu wanaomjua Mungu) wanatoa udhuru!, kwamba Nimeoa Mke, wengine nimenunua shamba sharti nikalitazame!.. Je huoni haya ndio yale yale Bwana aliyoyasema kwamba siku za mwisho watu watakuwa wakioa na kuolewa, na kununua na kuuza?

Kumbe ishara hii pia inatimia kwa watu wa Mungu!.. watu wasiomjua Mungu wao wataoana ndoa haramu, watanunua vitu haramu na kuuza kwa njia haramu.. lakini watu wa Mungu wataoa kihalali, na kununua na kuuza kihalali lakini watavifanya hivyo kuwa udhuru utakaowazuia kumsogelea MUNGU zaidi.

Hii ni hali halisi kabisa ya kanisa la leo!.. Asilimia kubwa ya tunaojiita wakristo, shughuli zimetusonga kiasi cha kuupunja muda wa Mungu, hatuombi tena kwasababu ya wingi wa kazi, hatuifanyi tena kazi ya Mungu kwasababu ya majukumu ya kifamilia na ndoa!, hatukusanyiki tena pamoja na wengine kwasababu ya mialiko mingi tuliyonayo ya kula na kunywa!..

Je unajua matokeo yake ni nini?.. Hebu tuendelee na mistari ile..

“20 Mwingine akasema, NIMEOA MKE, na kwa sababu hiyo siwezi kuja,

21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.

22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.

23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.

24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.

Matokeo yake ni kwamba Neema tuliyoipewa watapewa watu wengine , wote wenye kuwa na udhuru mwingi kwa Bwana wapo katika hatari ya kukosa kuingia mbinguni, wapo katika hatari ya kukumbana na gharika ya mwisho ya moto kulingana na Biblia.

Je wewe upo kundi gani?..  Unakula na kunywa kwa anasa au kihalali?, na kama kihalali je hiyo kwako ni udhuru wa kumtafuta Mungu?.. je wewe unanunua na kuuza kiharamu au kihalali?.. na kama ni kihalali je hiyo kwako ndio udhuru wa kutojitoa kwa Mungu?.. majibu yapo kwako na kwangu.

Bwana atusaidie tusiwe watu wa udhuru, bali tumtumikie Bwana kwa moyo wote, kwani hiyo ni amri tuliyopewa.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ISHARA YA KANISA LA LAODIKIA

Je mtu anaweza kubatizwa mara mbili?

Je tumepewa kujua nyakati na majira ya kurudi kwa Bwana au la?.

KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.

MGAWANYIKO WA ISHARA ZA UJIO WA BWANA YESU KRISTO.

Print this post