SWALI: Maandiko yanaposema Habili ijapokuwa amekufa angali akinena, je! Ananenaje, wakati yeye ni marehemu. Je! Hiyo inamaana wazee wetu wa zamani wanaweza kunena na sisi?
Waebrani 11:4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena
JIBU: Kibiblia ni kweli kabisa watakatifu waliokufa kale hunena nasi. Lakini kunena kwao ni tofauti na huku kunakodhaniwa, kwamba mzimu unakutokea kwenye ndoto, au unasikia sauti ya petro makaburini ikizungumza na wewe, Hapana, ukiona hivyo ujue huzungumzi na huyo mtu, bali ni pepo.
Sasa watakatifu waliokufa wanazungumzaje na sisi?
Ni kwa ushuhuda waliouacha. Maisha yao na maagizo yao, ndio huzungumza nasi, sikuzote, kana kwamba tupo nao sasa, kwa mafundisho yao yaliyopo mpaka sasa kana kwamba tunawaona wenyewe kumbe wamekufa.
Ndio maana ile habari ya Yule tajiri wa Lazaro, tunaambiwa alipofika kule kuzimu akaomba mtu atolewe kwa wafu awahubirie injili, akakataliwa, kuonyesha kuwa hakuna mtu aliyekufa mwenye uwezo wa kuja tena kuzungumza na sisi, nafasi hiyo haipo kwao. Lakini waliambiwa WANAO MUSA NA MANABII, WAWASIKILIZE.
Luka 16:29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
Maana yake ni kuwa sio kwamba Musa kweli alikuwepo duniani, au manabii wa kale kama Isaya walikuwa duniani kwa wakati huo, anaambiwa hayo maneno. Lakini shuhuda zao na mahubiri yao, huwawakilisha wao. Tunaweza kusema “ijapokuwa wamekufa wangali wakinena”
Ndivyo ilivyo kwa Habili, ijapokuwa aliuliwa na ndugu yake, lakini IMANI yake inasema nasi mpaka leo. Mitume wa Kristo ijapokuwa hawapo duniani lakini sauti zao tunazisikia hadi sasa.
Lakini pia kuna mahali pengine biblia inasema damu ya Yesu hunena mema kuliko ya Habili (Waebrania 12:24). Kufahamu kwa kina damu ya mtakatifu hunenaje? Pitia somo hili. >>> DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.
ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.
Rudi Nyumbani
Print this post
Zifuatazo ni baadhi ya tabia za kuigwa walizokuwa nazo wanafunzi wa Bwana YESU ambazo nasi tunapaswa tuzionyeshe.
1. WALIJIKANA NAFSI ZAO.
Hii ni sifa ya kwanza waliyokuwa nayo wanafunzi wa YESU, Kwani mtu aliyekosa hii sifa hakuweza kuwa mwanafunzi wake.
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Halikadhalika na sisi kama wanafunzi wa Bwana ni sharti tujikane nafsi kila siku, na kubeba msalaba. (Zingatia hilo neno, “Kila siku”), na si siku moja tu..
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate”.
2. WALIKAA KUFUNDISHWA NA BWANA.
Maana ya kuwa mwanafunzi ni kuketi na kufundishwa mpaka kuhitimu. Na wanafunzi wa Bwana YESU walilijua hilo, hivyo walikuwa walijiunga na chuo hicho cha Bwana ili kupokea mafunzo.
Na leo ni hivyo hivyo, Mwalimu wetu ni ROHO MTAKATIFU na chuo chetu ni Biblia. Na kila mtu ni lazima apite chini ya chuo hicho, ili aweze kuwa mwanafunzi wa Bwana.
3. WALIMFUATA BWANA KILA ALIKOKWENDA.
Maisha ya Bwana YESU hayakuhusisha kukaa mahali pamoja, bali kuzunguka huku na kule, katika miji na vijiji kuhubiri injili.
Mathayo 9:35 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”.
Hata wanafunzi wasomao chuo, upo wakati wanaenda katika mafunzo kwa njia ya vitendo kabla ya kuhitimu (maarufu kama mafunzo ya field).
Na vivyo hivyo na sisi kama wanafunzi ni lazima tuifanye kazi ya Bwana kwa yale tuliyoyapokea hata kama hatujabobea katika hayo..
Lakini utaona leo, mtu hataki kuwahubiria wengine kwa hofu ya kwamba yeye hajui….Ni kweli usifundishe usichokijua lakini kile kidogo ambacho umeshakijua, usikifukie chini bali kawape wengine wasiokijua kabisa.
4. WALIMTII BWANA.
Tabia nyingine ya mwanafunzi Halisi ni UTII na NIDHAMU.
Wanafunzi wa Bwana YESU wale 11 walimtii Bwana kwakila jambo, kuanzia maagizo ya ubatizo, kuhubiri, meza ya Bwana na mengineyo.
Na wote walimwogopa Bwana (hakuna aliyedhubutu kuhojiana naye wala kushindana naye) Luka 9:45.
5. WALIMWAMINI BWANA.
Wanafunzi halisi wa Bwana YESU hawakuwa na mashaka mashaka na Bwana YESU…walimwamini moja kwa moja…
Yohana 2:11 “Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”
6. WALIMVUMILIA BWANA
Hata kama yalikuwepo mambo ambayo yalikuwa ni magumu kueleweka katika hali yao ya uchanga…lakini walivumilia wakiamini siku moja watakuja kuelewa vizuri..
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? 68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.”
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?
68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.”
Na sisi kama wanafunzi wa YESU hatupaswi kurudi nyuma, tunapokutana na mambo tusiyoyaelewa katika imani au maandiko..badala yake tunapaswa kuwa wavumilivu kwa matumaini mazuri yajayo.
Na kumbuka maana ya kuwa MRISTO ni kuwa MWANAFUNZI…Huwezi kusema ni mkristo na sio mwanafunzi.
Matendo ya Mitume 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo ANTIOKIA”.
BWANA ATUSAIDIE.
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
Ndoa za wake wengi ni za ibilisi!..ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!… ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!!. Hali kadhalika ndoa za waume wengi ni za ibilisi, kama tu zilivyo za jinsia moja (zote ni zao la ibilisi).
Zipo hoja kuwa kwasababu Daudi, Sulemani na manabii wengine wakale walioa wake wengi, basi hata leo ni halali kuoa wake wengi.. tena zipo hoja zifananishazo wanyama wa porini na wa kufugwa na uhalali wa kuoa wake wengi.
Hoja zote hizi ni za ibilisi… Ndugu, usiongeze wake, wala usiongezee waume.
Bwana YESU alipokutana na yule mwanamke Msamaria kisimani hakumwambia akawalete WAUME ZAKE!.. Ingawa alikuwa ana wanaume wengi (na Bwana alilijua hilo), lakini alimwambia nenda “kamlete mumeo”… ikimaanisha kuwa ndoa halali na takatifu ni ya mume mmoja na mke mmoja.
Sasa Kristo alikuwa anamjua Sulemani, na Daudi..
Yohana 4:15 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16 Yesu akamwambia, NENDA KAMWITE MUMEO, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli”.
Yohana 4:15 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.
16 Yesu akamwambia, NENDA KAMWITE MUMEO, uje naye hapa.
17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume;
18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli”.
Bwana YESU kabla ya kukutana na huyu mama, alikuwa anamjua Daudi pamoja na Sulemani na idadi ya wake waliooa!.. Lakini tunaona hakumwambia huyu mwanamke Msamaria, kwamba akawalete waume zake!!.. Bali alimwambia kamlete mumeo! (maana yake mmoja tu).. bado huoni tu, kuwa ndoa za mitara ni batili na za ibilisi!.
Na tena biblia inasema hapo Mwanzo Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke, na si mwanaume na wanawake, au mwanamke na wanaume (soma Mwanzo 1:27 na Mathayo 19:4).
Huoni kuwa ndoa hizo za wake wengi zitakukosesha maji ya uzima!.. Na pia fahamu kuwa ndoa za wake wengi sio zile tu zinazohusisha mtu kuwa na wake wengi katika boma moja kwa wakati mmoja…la! Hata zile za kuacha na kuoa mwingine ilihali yule wa kwanza bado yupo hai.. hiyo ni mitara! Ndicho kilichokuwa kwa huyu mwanamke Msamaria.
Huyu mwanamke msamaria alikuwa na wanaume watano kulingana na darubini ya kimbingu! Ingawa haishi nao, lakini alikuwa nao watano, na anayeishi naye ni wa 6, vile vile kuna watu leo hii wameacha wake zao na kuoa wengine, na kuacha tena na kuoa wengine, (hawa hawana tofauti na wale waliooa wake wawili na kuishi nao wote kwa pamoja).
Na madhara ya ndoa za mitara ni “KUKOSA MAJI YA UZIMA”..
Yapo maji ya Uzima tuyanywayo hapa Duniani, na yapo yale tutakayoyanywa katika mbingu mpya na nchi mpya.
Maji ya Uzima duniani ni YESU KRISTO, tumpatapo yeye tunapata uzima wa milele (Yohana 4:14), lakini ukijiunganisha na hizi ndoa za mitara hawezi kuingia ndani yako!.. vile vile maji ya uzima baada ya maisha haya tutayanywa kutoka katika ule mto wa maji ya Uzima katika mbingu mpya na nchi mpya.
Ufunuo 22:1 “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele”.
Ufunuo 22:1 “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;
4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.
5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele”.
Neema ya Bwana YESU itufunike.
MAFUNDISHO YA NDOA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.
NDOA NI NINI?
KUWA NA MAFUTA YOTE YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.
Jina la BWANA wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia neno la Mungu wetu ambalo ni Taa na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Hebu tuangalie uzito wa kuzaliwa mara ya pili kupitia maneno ya BWANA WETU YESU KRISTO.
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, TWAJUA YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE. 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, TWAJUA YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.
Hapa Nekodemo anataja vigezo vya Mtu kuwa na MUNGU kuwa ni “Ishara azifanyazo”…na anamthibitisha Bwana kwa ishara hizo, lakini Bwana anamrekebisha, kuwa “MTU asipozaliwa mara ya pili hawezi kuurithi ufalme wa Mungu (maana yake hawezi kuwa na MUNGU)”… Je! na sisi leo tunalijua hilo??????….Je unalijua hilo??? .
Nikodemo anaona ISHARA ni tiketi ya kuwa na MUNGU,… Bwana YESU anataja KUZALIWA MARA YA PILI ndio TIKETI.. Sasa tuchukue ya nani tuache ya nani?.. Bila Shaka maneno ya BWANA YESU ni hakika, na tena ndio uzima.
Ndugu haijalishi tutakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mingi na mikubwa kiasi gani, kama HATUJAZALIWA MARA YA PILI (Maana yake kwa maji na kwa Roho) hatuwezi kuwa na Mungu, kutembea naye wala hatutamwona siku ile.
Mtu anapozaliwa mara ya pili anakuwa kiumbe kipya, maana yake yale maisha ya kwanza ya dhambi yanakuwa hayapo tena maishani mwake.
Kuzaliwa kwa maji ni Ubatizo wa Maji mengi na kwa jina la Bwana YESU na kuzaliwa kwa Roho ni ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 2:37-38), mambo haya ndiyo yanamkamilisha mtu baada ya kutubu.
Na anayetuzaa mara ya si mtu bali ni Mungu mwenyewe, na Mungu ni Roho (sawasawa na Yohana 4:24), na tunapozaliwa na Roho, basi tunakuwa watu wa rohoni.
Yohana 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho”
Na kuwa mtu wa rohoni, si kuona maono, au mapepo, bali ni kuzaliwa katika Roho, na Maji. Na sifa kuu ya mtu wa rohoni ni kuushinda ulimwengu (dhambi na mambo mengine ya kidunia).
1Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.
Soma pia 1Yohana 3:9 na 1Yohana 5:18.
Hivyo ukiona tamaa za kidunia bado zinakusumbua kuna uwezekano kuwa bado hujazaliwa mara ya pili, kwasababu wote waliozaliwa mara ya pili wanayo nguvu ndani yao ya kuushinda ulimwengu na ndio watu wa rohoni.
Je ishara ni uthibitisho wa mtu kuwa na Mungu??..jibu ni ndio!, lakini si uthibitisho wa kwanza… bali uthibithsho wa kwanza wa mtu kuwa na Mungu ni KUZALIWA MARA YA PILI. Kwasababu wapo watakaotenda miujiza na kufanya ishara nyingi lakini wasimwone Bwana siku ile sawasawa na Mathayo 7:22.
Kwahiyo kilicho cha msingi kuliko vyote ni “KUZALIWA MARA YA PILI (kuwa kiumbe kipya)” na mengine ndio yafuate.
Wagalatia 6:15 “Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya“.
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
SWALI: Maana ya Mithali 27:18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake; Naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
JIBU: Mstari huo una vipengele viwili cha kwanza ni Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake
Na cha pili ni naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa.
Tukianzana na hicho cha kwanza. Tufahamu kuwa Mungu ameiandika injili yake sio tu kwenye kitabu chake, bali pia kwenye vitu vya asili, ndio maana Yesu alitumia mifano mingi ya namna hiyo, kuzungumza nao habari zake mwenyewe. Kuanzia wakulima, mimea, wanyama, wafanya biashara, wafalme n.k.
Sasa hapa anasema yeye atunzaye mtini atakula matunda yake. Kumbe kula matunda ni “kutunza”. Usipotunza huwezi pata chochote. Ili uone kazi yako, utaiwekea mbolea, utaipalilia, utaipiga dawa n.k. Na mwisho utakuwa mvumilivu aidha miaka mitatu/ minne ukisubiri mazao.
Halidhalika rohoni. Sisi kama watoto wa Mungu (tuliookolewa), kila mmoja wetu anao “mtini” moyoni mwake, na huo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo. Wengi wasichojua ni kwamba Kristo huanza kama kichanga, kisha huwa kijana mdogo, baadaye huwa mtu mzima, na mwisho huanza kutenda kazi zake. Kama tu alivyokuwa hapa duniani alivyoishi na Mariamu na Yusufu, hakuanza kufanya chochote pindi anazaliwa.
Hivyo usipomlea ipasavyo hutafaidi matunda yake vema. Ndio mfano wa mpanzi ambao Yesu mwenyewe aliutoa, akasema zile mbegu ziliporushwa nyingine zikaishia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri, moja ikazaa thelathini, nyingine sitini, nyingine mia. Akatoa ufafanuzi wake, kwamba zile zilizofanikiwa kuzaa, ni kwamba zilichangiwa na KUVUMILIA (Luka 8:15). Sasa kuvumilia nini? Kuvumilia hatua zote tatu za mwanzo, yaani dhiki kwa ajili ya Kristo, kujiepusha na anasa, udanganyifu wa mali, na uvivu wa kulitendea kazi Neno.
Ukuaji wa kiroho tafsiri yake ni ‘Kristo kukua ndani yako’. Ukiona upo ndani ya wokovu kwa miaka mingi, halafu huoni matunda yoyote ya wokovu wako, katika ufalme wa Mungu, tatizo linakuwa hapo, hukuwa na nafasi ya kuutunza mtini wako.
Ukiokoka, ni lazima bidii ya kusoma Neno iwe ndani yako kila siku, usiwe mvivu wa maombi, vilevile epuka maisha ya kidunia, na ubize uliopitiliza, ambao unakufanya hata nafasi ya Mungu wako unakosa. Ukizingatia hayo, baada ya kipindi Fulani utaona Kristo anavyojengeka nafsini mwako , na kukutumia.
Lakini pia sehemu ya pili inasema naye amhudumiaye bwana wake ataheshimiwa,. Ni hekima ya kawaida, ukiwa mfanyakazi mwema kwa bwana wako, hawezi kukuchikia kinyume chake atakupa heshima yako, lakini pia na watu wengine wote wa nyumbani kwake watafanya hivyo.
Si zaidi Mungu?
Heshima hasaa kwa Mungu wako, sio kumwambia “Shikamoo” au kuomba kwa sauti ya unyenyekevu, au kuinamisha kichwa uwapo ibadani. Heshima yake hasaa ni pale unapomtumikia, unapotii agizo lake la kuwaeleza wengine habari za injili, na pale naposimama katika nafasi yako kwenye mwili wa Kristo.
Tutafute kuheshimiwa na Bwana kwa kuwashuhudia wengine injili.
MTINI, WENYE MAJANI.
Biblia imemaanisha nini kusema Nyoka atakula mavumbi?(Opens in a new browser tab)
(Opens in a new browser tab)Je ile habari ya mtini kunyauka inajichanganya?(Opens in a new browser tab)
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.(Opens in a new browser tab)
Jibu: Turejee…
Isaya 13:10 “Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze
“Matangamano” ni “Mkusanyiko wa nyota” unaoonekana na kutengeneza umbile Fulani. Wanajimu baadhi wameyataja matangamano hayo kwa maumbile ya wanyama mbali mbali, kwamfano lipo kundi moja wamelitaja kuwa na umbile kama la N’ge, lingine kama Dubu, lingine kama Simba, lingine mapacha n.k
Kwamfano kundi la nyota lenye umbile kama la Ng’e jinsi linavyoonekana mbinguni kwa macho ya damu na nyama ni kama linavyoonekana kwenye picha hapo juu.. Lakini kwa jinsi lilivyounganishwa na wanajibu mpaka kuleta umbo kama la Ng’e ni kama inavyoonekana hapa chini..
Na makundi haya ya nyota, sasa yanatumika kwa unajibu (ambayo ni elimu ya shetani asilimia mia) kwaajili ya utambuzi wa majira na nyakati za watu, Elimu hii kwa jina lingine inaitwa FALAKI, Fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
Elimu hii wanajimu wanaitumia kutabiri mambo yajayo juu ya mtu, ndio hapo mtu anaenda kusomewa nyota yake na kufanyiwa utabiri, jambo ambalo kiuhalisia ni elimu ya giza, mtu yule anakuwa haambiwi mambo yajayo bali anapangiwa mambo yajayo na ibilisi, akidhani ndio katabiriwa.
Sasa Elimu hizi za Falaki pamoja na ibada zote za jua na mwezi na sayari, Bwana Mungu kazilaani, na siku za mwisho Jua, na mwezi vitatiwa giza, na Nyota zote za mbinguni zitaanguka na Matangamano yote yatazima.. kuonyesha kuwa mambo hayo yaliyotukuka kwa wanadamu si kitu mbele za Mungu, na Bwana atawaadhibu waovu pamoja na ulimwengu, ndivyo maandiko yasemavyo.
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. 10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. 11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.
Kuhusiana na unabii wa kufutwa kwa Mwezi, nyota na sayari zote siku za mwisho pitia maandiko haya Yoeli 3:15, Marko 13:24, Mathayo 24:29, na Ufunuo 6:12.
Kwahiyo ndugu usiende kusoma gazeti kwa lengo la kutafuta utabiri wa nyota, ni machukizo kwa Bwana, usiende kwa waganga ili wakakusafishie nyota, kinyume chake ndio unaenda kuharibu maisha yako, badala yake mfuate Bwana YESU naye atayasafisha maisha yako.
MKUU WA GIZA.
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?
AGIZO LA UTUME.
Mungu anaweza kuahidi, lakini kama hujui kanuni za kusubiria ahadi za Mungu unaweza usipokee lolote. Kila mmoja wetu amestahili kupokea lolote analo mwomba Mungu endapo ameomba sawasawa na mapenzi yake (yaani sio kwa matumizi mabaya). Yawezekana wewe umeomba Bwana akupe kazi, akupe mke/mume bora, akuponye ugonjwa wako, aikuze karama yako n.k.
Sasa mahitaji kama hayo na mengine yoyote. Mungu alisema kwenye Neno lake, atatupatia (1Yohana 5:14). Na hivyo inakuwa kwake ni ahadi ambayo lazima aitimize. Kwahiyo wewe unachopaswa kufanya ni kusubiri tu. Kuzingojea hizo ahadi za Mungu kwasababu ni lazima zije. Jifunze tu kungojea.
Maombolezo 3:25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. 26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu
Sasa unazingojea katika mazingira gani?. Hapo ndipo unapopaswa ujue.
Embu tuangalie kwa mtu mmoja ambaye aliahidiwa jambo na Mungu. Na hivyo alikuwa katika mazingira gani, mpaka akalipokea. Mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simeoni.
Tusome.
Luka 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, 31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
Luka 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
Wengi wetu tukimtafakari Simeoni, tunatengeneza picha ya mtu Fulani, mzee aliyekuwa anamngoja Mungu tangu ujana wake hadi uzee atimiziwe ahadi yake. Lakini biblia haituelezi katika picha hiyo, inatueleza alikuwa ni “mtu mwenye haki mcha Mungu”. Na tazamio lake lilikuwa ni kuona mkombozi anakuja duniani, Mungu akasikia kiu yake, ndipo akamwambia utamwona.
Ni jambo gani unapaswa ujue?
Kungojea ahadi za Mungu sio tu kusema ‘Bwana naomba hiki au kile’. Hapana, ni pamoja na kutembea katika haki na kumcha Mungu. Simoni alikuwa hivyo, hakuwa mtu anayetarajia jibu lake, huku anaendelea na udunia kama wengine, huku anaendelea na anasa kama wanadamu wengine, huku anaendelea na uzinzi kama wapagani.
Alidumu muda wote, kuyalea maono aliyoonyeshwa na Mungu, katika hofu ya Kristo. Ndipo wakati ulipofika akaona alichokuwa akikitarajia.
Palilia maono yako uliyomwomba Mungu akutimizie/ au aliyokuonyesha, kwa kutembea ndani ya Kristo. Mche Mungu, kuwa mtu wa rohoni uliyejazwa Roho kama Simoni, tembea katika usafi wa Kristo, kataa udunia, na maisha ya kipagani, kuwa mwombaji.
Ni hakika hilo ulilomwomba Bwana utaliona tu, baada ya wakati Fulani, haijalishi ni gumu/zito kiasi gani, au limepitiliza muda kiasi gani. Utalipokea tu, katika ubora ambao hukuutegemea.
PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.
ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.
KANUNI JUU YA KANUNI.
Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.
Usingizi unaozidi unachelewesha utekelezaji wa majukumu ya muhimu. Kwamfano Mwanafunzi anayelala kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa shule, vilevile mfanyakazi alalaye kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa kazini, mfanya biashara anayelala kupita kiasi ni lazima atachelewa kuanza biashara yake.
Upo usemi usemao “biashara ni asubuhi” maana yake kwa mtu anayefanya biashara labda ya kuuza duka, asubuhi ndio wakati wa kufungua bishara maana watu wengi wanawahi kutafuta bidhaa asubuhi Zaidi ya mchana, hivyo alalapo sana hatapata zile faida za asubuhi, na hivyo yupo hatarini kufilisika.
Atapanga kweli kuwahi kuamka mapema kesho, lakini ifikapo asubuhi kitanda kinakuwa na nguvu kuliko maamuzi yake, atajiongezea muda wa kulala, na mwisho wa siku atashtukia kumeshapambazuka na jua linawaka..na hayo ni matokeo ya kusema “bado kulala kidogo”.
Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? 10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Sasa biblia ni kitabu kilichojaa hekima ya kumwongoza mtu hata katika maisha ya kawaida Zaidi ya yale ya rohoni…. ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mema yahusuyo kanuni za kimaisha na kitabu cha Mithali kimejaa mafunzo hayo.
Hivyo biblia inatufundisha wakristo tuwe na kiasi katika kulala, kwani usingizi unaozidi una matokeo mabaya.. Si kila changamoto inasababishwa na “wachawi”….. nyingine zinatokana na tabia zetu wenyewe.., na hivyo biblia inatufundisha jinsi ya kuepukana nazo, kwamba ni kubadili tu mienendo.
Maana yake ni kwamba, tukitaka kuepukana na “umasikini” kanuni sio tu “kufunga na kuomba” bali pia ni KUTOUPENDA USINGIZI!. Ukifunga na kuomba na huku unaendekeza usingizi kupita kiasi hakuna matokeo yoyote utakayoyaona.
Maana yake kama ni mfanyakazi basi usiwe mtu wa kupenda kulala mno..Ni kweli hatuwezi kuacha kulala kabisa, lakini kusizidi mipaka, kwani usingizi uliozidi ni zao la ibilisi.
Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”
Lakini pia kiroho hatupaswi kulala kabisa, kwani usingizi wa kiroho matokeo yake ni mabaya kuliko ule wa kimwili.. Matendo yote ya giza mtu ayafanyayo ni matokeo ya usingizi wa kiroho..
Mtu anayefanya uzinzi, uasherati, anayelewa pombe, anayeiba, anayetukana, anayesengenya…huyo macho yake yamefumba kwa usingizi mzito.
Je na wewe umo miongoni mwa waliolala kiroho? Basi huu si wakati wa kuendelea kulala, bali wa kuamka na kuyaacha matendo ya giza.
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
12 USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”
Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Bwana atubariki.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
NYOTA YA ASUBUHI.
Nini maana ya usijiongezee hekima mno? (Mhubiri 7:16b)
Masomo maalumu kwa wahubiri.
Isaya 29:16 “NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?”
Kama Mtumishi/Mhubiri jihadhari na MAPINDUZI yasiyo na msingi!.
USIIPINDUE INJILI YA KRISTO KWASABABU YA TAMAA YA FEDHA.
Unapoanza kuwadanganya watu wa wenye nia ya kumtafuta Mungu, ili tu upate fedha kutoka kwao!.. unapoanza kuwatumainisha watu wa Mungu mambo ya uongo ili tu uwatoe fedha!.. Hiyo ni ishara mbaya na hatari kubwa sana kwako!. Bwana ataenda kukupindua nawe pia!.
Tito 1:11 “Hao WANAPINDUA watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu”.
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kufanya biashara katika nyumba ya Mungu (ambayo ni wewe mwili wako sawasawa na 1Wakorintho 3:16) kwa kuanza kufanya uasherati na uzinzi na ukahaba fahamu kuwa Bwana naye atakupindua (Soma 1Wakoritho 6:19).
Ukilipindua Neno la Mungu kwa kuiharibu nyumba yake (kama jengo) kwa kuanza kufanya biashara ndani yake na kufanya yasiyofaa Bwana YESU atazipindua meza zako (soma Mathayo 21:12)
Ukilipindua Neno la Mungu juu ya utakatifu wa mwilini na rohoni (sawasawa na 1Wathesalonike 5:23) na kuanza kufundisha/ kuhubiri kuwa Mungu haangalii mwili bali anaangalia roho tu peke yake ni kupindua maandiko ambako matokeo yake ni Mungu kuyapindua maneno yako na wewe kwa ujumla.
Mithali 22: 12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali HUYAPINDUA MANENO YA MTU HAINI”
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kuhubiri kuwa YESU KRISTO bado sana arudi, au kwamba hakuna mwisho wa dunia, huko ni kupindua mambo ambako matokeo yake ni mabaya kama ya Fileto na Himenayo.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, 18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
Kama Mhubiri Ni heri KUPINDUA ulimwengu kwa mambo ya kweli ya INJILI kama walivyofanya Mitume wa kanisa la kwanza kuliko kuigeuza/kuipindua injili kwa faida zetu wenyewe.
Matendo 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA huku nako”
Siku ya Mapinduzi makuu inakuja, ambapo Bwana ataipindua dunia yote kama alivyoipindua miji ya Sodoma na Gomora (soma Kumbukumbu 29:23) na kipindi cha gharika ya Nuhu (Soma Ayubu 12:15).
Ezekieli 21:27 “NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa”
Hegai 2:22 “nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake”.
Usipindue Mambo yaliyonyooka, bali pindua yale yaliyopotoka.
VIJANA NA MAHUSIANO.
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
IMANI “MAMA” NI IPI?
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
SWALI: Nini tafsiri ya Mithali 27:22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
JIBU: Kama tunavyojua mtwangio na kinu ni vyombo vinavyotumika kuponda-ponda nafaka ngumu kuwa unga, au wakati mwingine mimea migumu kuwa milaini. Mfano wa kisamvu ambacho ili kiweze kulika, majani yake huwezi yapika hivyo hivyo huna budi kuyatwanga twanga kidogo, yalainike ndipo upike ule.
Na vivyo hivyo, nafaka kama mahindi, au ngano, ili viweze kulika zamani vilikuwa vinatwangwa kwenye vinu ,tofauti na sasa vinasagwa na mashine.
Sasa katika mithali hiyo, Mungu anatoa, asili ya mtu mpumbavu, kwamba hata akitwangwa, mfano wa ngano kinuni, huo upumbavu hauwezi kumtoka. Yaani njia gani ya lazima itumike bado hawezi kuacha upumbavu.
Sasa ni vizuri kufahamu, mpumbavu ni nani?
Mpumbavu kibiblia sio mtu Fulani mjinga tu hapana, bali ni Neno pana, linalolenga kuanzia
mtu anayesema hakuna Mungu (zaburi 14:1)
Mtu mgomvi (Mithali 9:13),
Mtenda maovu (Mithali 10:23)
Anayejiona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)
Mwenye kiburi (Mithali 14:3)
Mwenye dharau (Mithali 15:5)
Yaani kwa kifupi mpumbavu ni mtu ambaye hana Mungu ndani yake. Kwasababu dhambi ndani ya mtu ndio chanzo cha Upumbavu wote.
Sasa mtu kama huyu, hakuna kitu kinachoweza kuutoa upumbavu huo ndani yake, waweza kusema elimu, lakini ni watu wangapi wameelimika, lakini walevi, watukanaji, mashoga. Hata atwangwe vipi kinuni hawezi lainika, ikiwa hajui ni kipi sahihi kinachoweza kutoa upumbavu huo.
Kumfunga mwizi, hakumfanyi wizi au tamaa ya kuiba itoke ndani yake, mara ngapi unasikia mwizi katoka jela, karudia wizi wake, au ni kiongozi ambaye anaaminiwa awe kielelezo cha kupambana na ufisadi, lakini yeye ndio anakamatwa katika ufisadi, au teja ametolewa hospitalini karudia, tena madawa la kulevya. Ndio maana jamii ijapojaribu kudhibiti vitendo viovu, bado haviishi, bali hubadilika tu maumbile. Kwasababu mpumbavu hata atwangwe kinuni, hawezi geuka, hakuna nidhamu inayoweza mbadilisha. Huwezi acha mwenendo wake mbovu kwa semina za kijamii, au kuwekewa sheria
Je! Ni kipi kinachoweza kumgeuza?
Ni Yesu Kristo tu. Yeye ndiye aliyetiwa mafuta, na Mungu kuwaokoa watu wa Mungu na kuwafungua. Amwaminiye na kudhamiria moyoni mwake kumfuata, basi atageuzwa moja kwa moja na kuwa mtu mwingine, huo ni uhakika.
Alisema.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Ni ahadi yake kuwa Ukimwamini jambo la kwanza ni kukusamehe dhambi zako, kwasababu ndio jambo lililomfanya aende msalabani kwa ajili yako miaka elfu mbili iliyopita,. Unakuwa huhesabiwi dhambi tena, unahesabiwa haki bure kwa neema yake. Lakini sambamba na hilo anakupa UWEZO wa kuwa kama yeye kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu atakayemwachia ndani yako, pindi tu unapoamini.
Na baada ya hapo utashangaa tu unavyoanza kubadilika moyoni mwako.
Zingatia tu toba ya kweli, pamoja na ubatizo sahihi (kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo). Na kumtii yeye.
Upumbavu utakutoka.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?