Je ile habari ya mtini kunyauka inajichanganya?

Je ile habari ya mtini kunyauka inajichanganya?

Swali: Mathayo 21:19 inasema “mtini ulinyauka mara (maana yake muda ule ule uliolaaniwa)”.. lakini katika Marko 11:20 biblia inasema “mtini ulinyauka kesho yake, na sio siku ile ile ulipolaaniwa”.. Je mwandishi yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa biblia haijichanganyi mahali popote na wala haijawahi kujichanganya mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, fahamu zetu na tafakari zetu ndizo zinazojichanganya pale tunaposoma pasipo kutafakari kwa kina.

Sasa turejee habari hizo moja moja na kisha tuzitafakari tena..

Mathayo 21:18 “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.

19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. MTINI UKANYAUKA MARA.

20 WANAFUNZI WALIPOONA, WALISTAAJABU, WAKISEMA, JINSI GANI MTINI UMENYAUKA MARA?

21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka”.

Hapa tunaona mtini ulinyauka “Mara”.. Lakini turejea kitabu cha Marko ni kama tunasoma habari tofauti…

Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

13  Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

14  Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”

Turuke mpaka mstari wa 19-23..

“19  Na kulipokuwa jioni alitoka mjini.

20  NA ASUBUHI WALIPOKUWA WAKIPITA, WALIUONA ULE MTINI UMENYAUKA TOKA SHINANI.

21  PETRO AKAKUMBUKA HABARI YAKE, AKAMWAMBIA, RABI, TAZAMA, MTINI ULIOULAANI UMENYAUKA.

22  Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.

23  Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake”

Hapa tunasoma “MTINI ULINYAUKA SIKU INAYOFUATA na si muda ule ule”.. Sasa swali? habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?

Jibu ni kwamba habari zote ni sahihi, waandishi wote wote wapo sahihi, hakuna hata mmoja aliye mwongo..…

Sasa kwa ufupi ni kwamba mtini haukunyauka muda ule ule Bwana alipoulaani, bali mpaka kufikia kesho yake ndio ulikuwa umekwisha nyauka kabisa..…Sasa swali, kama ni hivyo kwanini Mathayo aseme ulinyauka MARA?…

Jibu la swali hili ni kwamba…si kila mahali panapotumika neno “Mara” panamaanisha “dakika ile ile, au sekunde ile ile, au muda ule”… Hapana!.. Bali neno “Mara” linaweza kumaanisha kipindi fulani cha muda/wakati… ili tuelewe vizuri, tusome habari ifuatayo..

Marko 1:26 “Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.

27  Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!

28  Habari zake ZIKAENEA MARA KOTEKOTE KATIKA NCHI ZOTE kandokando ya Galilaya”

Hapo biblia inasema habari za Bwana YESU zikaenena “MARA KOTE KOTE KATIKA NCHI ZOTE”… Sasa swali??…Je zilienea sekunde ile ile, au muda ule ule, aliotoa Pepo?..Jibu ni la!...bali ni baada ya kipindi Fulani cha wakati labda masaa kadhaa mbele au siku moja mbele au siku kadhaa???… Kwani isingewezekana ndani ya sekunde ile ile muujiza ulipotokea, habari zifike Galilaya yote ambayo ilikuwa na vimiji vidogo vidogo Zaidi ya 400 kulingana na historia na miji hiyo ikiwemo Nazareti, Kapernaumu, korazini na Bethasaida, Na tena si Galilaya tu!, na hata nje ya Galilaya, maana hapo anasema taarifa zilifika miji yote ya kandokando ya Galilaya (maana yake nje ya Galilaya).

Kwa mantiki hiyo basi tutakuwa tumeelewa kuwa Mathayo alipotumia neno “kunyauka Mara” hakumaanisha sekunde ile ile, bali alimaanisha kuwa ni kwa kipindi Fulani cha masaa kadhaa, (haraka sana, ambako sio kwa kawaida kwa desturi ya miti kunyauka)… kwa maana kikawaida mpaka mti unyauke unachukua siku kadhaa, na huo ni kama umekatwa…sasa ule haukuonekana kama umekatwa, lakini ulinyauka kabisa (Hivyo ni muujiza).

Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa mtini mpaka kufikia asubuhi ndio ulionyesha kunyauka na wanafunzi walishagaa hiyo asuhubi hivyo biblia haijichanganyi mahali popote..

Je unaliamini Neno la Mungu?.. Na je umeokoka?…Kama bado ni nini kinachokusubirisha usimpokee Bwana YESU??.. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na YESU yu mlangoni.. hivyo usiyachezee maisha yako wala mtu mwingine yoyote asiyachezee..

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MTINI, WENYE MAJANI.

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments