Je biblia inajichanganya katika ile habari ya binti wa Yairo?

Je biblia inajichanganya katika ile habari ya binti wa Yairo?

Swali: Je biblia takatifu inajichanganya katika habari ile ya binti wa Yairo?.. kwamaana katika Marko na Luka inaonyesha kuwa Binti alikuwa katika kufa! (Marko 5:23) Lakini katika Mathayo 9:18 inasema binti alikuwa amekwishakufa, sasa habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa biblia haijichanganyi mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, na tafakari zetu ndizo zinazochanganyikiwa. Sasa ili tuelewe vizuri, turejee mistari hiyo..

Marko 5:21  “Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.

22  Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,

23  akimsihi sana, akisema, BINTI YANGU MDOGO YU KATIKA KUFA; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi

24  Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.”…..

Turuke mpaka mstari ule wa 35 na 36 ili tuimalizie habari hii kama ilivyoelezewa na Marko..

35  Hata alipokuwa katika kunena, WAKAJA WATU KUTOKA kwa yule mkuu wa sinagogi, WAKISEMA, BINTI YAKO AMEKWISHA KUFA; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?

36  Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu”

Katika kisa hiki ni kweli tunaona taarifa zinaanza na binti kuwa katika HALI YA KUFA, na zinaishia na BINTI KUFA.. Lakini tukirejea katika kitabu cha Mathayo tunaona habari nyingine ambayo inaonekana kama ni tofauti kidogo..

Turejee…

Mathayo 9:18  “Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, BINTI YANGU SASA HIVI AMEKUFA; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.

19  Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake”……….

Hapa tunasoma kuwa Jumbe-Yairo anamwambia Bwana kuwa Binti yake amekwisha kufa, na si yu katika kufa!, hivyo aende kumwekea mikono afufuke.. sasa swali je! Biblia inajichanganya?

Jibu ni la!.. kama tulivyosema, biblia haijichanganyi, isipokuwa ni pambanuzi zetu.

Sasa ili tukiweke hiki kisa vizuri; ni kwamba Yairo alipotoka nyumbani mwake kumfuata Bwana YESU, binti yake alikuwa hajafa bado!, ila alikuwa katika hali ya kufa,..na alipokutana na Bwana akamwomba aende amwekee mikono ili apone, sawasawa na Marko alivyorekodi hapo katika Marko 5:23, tukio ambalo halijarekodiwa na Mathayo..

Lakini alipokuwa katika kumsihi Bwana kuna watu baadhi waliotokea nyumbani kwake na kumpa taarifa kuwa binti yake amekwisha kufa!…Sasa Yairo aliposikia kuwa mwanae kafariki hakukata tamaa, bali aliendelea kumsihi Bwana kuwa aende kumwekea mikono ili afufuke hata kama amekwisha kufa!, Na Bwana YESU aliposikia hayo akaahidi kwenda naye.

Lakini alipokuja mtu mwingine kutoka nyumbani mwake kumpa hizo hizo taarifa kuwa binti yake kashafariki hivyo asizidi kumsumbua mwalimu… (maana yake alikuwa anarudia rudia kumwambia, sasa hiyo kauli ya asizidi kumsumbua Marko 5:35) ndio iliyomfanya Bwana YESU amwambie ASIOGOPE!, kwani ndiyo inayokatisha tamaa, na yenye kuua Imani ya Jumbe (Marko 5:36).

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa Mwandishi wa kitabu cha Marko alianzia kuelekezea tukio kuanzia mwanzo kabla ya binti kufa, na kutaja kuwa watu walikuwepo Zaidi ya mmoja waliokuja kumpa taarifa Yairo za kifo cha mwanae (Marko 5:35),

Lakini mwandishi wa kitabu cha Mathayo alianzia kuelezea tukio katikati wakati ambao tayari binti amekwishakufa na hakuelezea kabla ya kufa kwake…..Hivyo hakuna mkanganyiko wowote hapo, na wala mahali pengine popote katika biblia.

Je umeokoka?.. Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya siku za mwisho?, na Kristo yupo mlangoni?. Kama bado hujampokea unangoja nini?.. Mpokee leo na ubatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

USIFE NA DHAMBI ZAKO!

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)

Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mch Elisha samweli
Mch Elisha samweli
4 months ago

Mimi swali langu ni kutoka kitabu hiki Cha mathayo
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”
— Mathayo 28:19

Naomba kusaidiwa kufahamu jambo Hilo vyema Magizo ya YESU aliwagiza wanafunzi kutumia majina hayo kama nukuu ya andiko lilivyo au alimanisha watumie jina la baba jina la mwana jina la Roho mtakatifu ambalo ni YESU Asante

Mch Elisha samweli
Mch Elisha samweli
4 months ago

Bwana awape nguvu ndani ya mifupa yenu mzidi kutulisha chakula Cha kiroho