Moja kwa moja ndoto kama hii inatoka kwa Yule mwovu, kukimbizwa kwa namna yoyote ile maadamu ni kukimbizwa basi ni kutoka kwa yule mwovu, iwe ni kuota unakimbizwa na watu au kuota unakimbizwa na nyoka au kuota unakimbizwa na ng’ombe, au kuota unakimbizwa na simba, au kuota unakimbizwa na tembo au kuota unakimbizwa na nyuki, au kuota unakimbizwa na kichaa, ni ndoto kutoka kwa mwovu…Sikuzote kitu kinachokimbizwa ni kitu kilicho dhaifu, cha kuwindwa ili kiliwe, swala anakimbizwa na simba, ni kwasababu yeye ni dhaifu, lakini kitu chenye ujasiri kamwe hakikimbizwi.
Ukijiona unakimbizwa fahamu kabisa moja kwa moja kuwa wewe ni dhaifu rohoni, na hiyo ni kutokana na kuwa upo nje ya Kristo au kama upo basi hauijatambua mamlaka uliyonayo ndani ya Kristo kwa uchanga wako wa kiroho au kwa uzembe wako wa kutokujishughulisha na mambo ya Mungu..
Mithali 28:1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
Hivyo mrudie Mungu wako kama bado haujaokoka, Tubu ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe kwa Jina la Yesu Kristo, ili upate ondoleo la dhambi zake. Au kama tayari ulikuwa ndani ya Kristo na ulikuwa unayumba yumba huu ni wakati wako sasa kusimama imara.
Kisha anza kujifunza biblia kwa bidii, na pia tafuta kanisa la kiroho la kwenda kujifunzia Neno la Mungu, ili likae kwa wingi ndani yako, upate kujua nafasi uliyonayo katika Kristo. Mpaka siku moja na wewe uote unamkimbiza shetani.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”
Usipuuzie ndoto hizo, kwasababu shetani kweli anakuwinda akumeze…Fanya uamuzi wa busara kumgeukia Mungu.
Ubarikiwe.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
MTETEZI WAKO NI NANI?
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Hii ni moja ya ndoto ambayo inaotwa na watu wengi sana, na hii huwa inachukua maumbile tofauti tofauti, wengine utakuta wanaota wanafanya mitihani na hawajajiandaa, wanachoshtukia tu ni wakati wa mtihani umefika, na hakuna chochote walichofanya wanajiuliza siku zote alikuwa wapi…wengine wanaota wanafanya mtihani mgumu sana lakini wenzao wanaonekana wanafahamu cha kujaza yeye hajui,
wengine wanaota kama walikatisha masomo wakaondoka, baadaye waliporudi muda umeshapita mitihani ya mwisho imekaribia, wengine wanaota wamerudia madarasa ya nyuma ambayo tayari wameshayavuka siku nyingi na ni lazima wayavuke ili waendelee na madarasa ya mbele, wengine wanaota wapo wanafundishwa, wengine wanapewa adhabu, wengine wapo tu n.k.…Kwa ufupi ndoto unazoota upo katika mazingira ya shule, zote zina maudhui moja.
Na ndoto hizi huwa zinatesa sana, zinaweza kujirudia hata kila baada ya wiki au mwezi, au miezi kadhaa, inategemea na mtu na mtu, lakini ni ndoto ambazo haziachi kuja.
Biblia inasema..
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”
Mungu siku zote huwa anapenda kutumia vitu vinavyotuzunguka kutufikishia sisi ujumbe fulani , na ndio maana utaona Bwana Yesu alipokuwa anafundisha mifano yake yote alikuwa anatumia mambo ya kawaida tu yanatozunguka sikuzote ili kutufikishia sisi ujumbe na tuulewe utaona wakati mwingine alitumia mifano ya ndege, wafanyabiashara, wafalme, harusi n.k…
Hivyo na Mungu ili kukufikisha ujumbe wake wa wokovu huwa anapenda kutumia mfano wa kitu ambacho kimetukuka sana mbele yako, kitu chenye maana sana kwako ambacho ukikikosa anajua kabisa umekosa maisha na hicho si kingine zaidi ya ELIMU.
Kufunua kuwa Ipo elimu iliyokuu ambayo inayo ufunguo sio tu wa maisha ya hapa bali pia wa maisha ya ulimwengu unaokuja, na hiyo si nyingine zaidi ya Elimu ya Ufalme wa Mbinguni..Mungu anakuonyesha hali yako ya kiroho ilivyo kupitia maisha yako ya shuleni, kama unavyojiona upo shuleni hujajiandaa, au mtihani ni mgumu basi katika roho ndivyo hivyo ulivyo.. kuwa upo nyuma, na unapaswa ushinde, yapo madarasa haujayavuka bado, upo pale pale kiroho umekwama, unatamani uendelee mbele unashindwa au unaona ni ngumu kwasababu bado hujayamaliza madarasa ya nyuma Mungu aliyokupa.
Hivyo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ili ufike pale Mungu anapotaka kufika, ongeza kiwango chako cha maombi, jifunze Neno la Mungu sana, ishi maisha yanayompendeza Mungu, punguza muda wa kuihangaikia dunia, na ongeza muda wako wa kumtafuta Mungu, kwasababu yeye ndio ufunguo wa kweli wa maisha yako ndugu. Ukimpata Mungu umepata vyote.
Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
Hivyo ukiwa na bidii na Mungu akaridhika na wewe basi atakuvusha na kukupeleka katika kiwango kingine cha kiroho na kiufahamu. Kumbuka Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo, Hivyo usipuuzie ungeza bidii yako kwake.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
TABIA ZA ROHONI.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu YESU KRISTO, Suala la upambanuzi wa ndoto ni moja ya mambo ambayo yanawasumbua wengi, lakini kwa bahati mbaya watu wengi wamekosa kujua tafsiri ya ndoto zao, kulingana na maandiko…
Hivyo kabla ya mtu hukimbilia kupewa au kutafuta tafsiri ya ndoto yake ni vizuri kwanza akafahamu kuwa ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu, kundi la kwanza ni zile ndoto zinazotokana na Mungu, kundi la pili ni zile zinazotokana na shetani na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe, na hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya ndoto tunazoziota karibu kila siku, na aina hii ya tatu huwa inakuja kutokana na shughuli zetu tunazozifanya kila siku au mazingira yanayotuzunguka kila siku..
Ndoto za namna hii huwa hazibebi ujumbe wowote, hivyo hazihitaji kutafsiriwa, mara nyingi zinapaswa zipuuziwe..ikiwa hujafahamu vizuri namna ya kuitambua ndoto yako kulingana na makundi haya basi bofya somo hii ulipitie kisha ukishamaliza tuendelee…>> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?
Watu wengi wamekuwa wakiniuliza tafsiri ya ndoto hii ya kuota nyoka, sasa ikiwa ni ndoto ambayo inajirudia rudia, basi izingatie sana..kumbuka Nyoka katika maandiko tangu mwanzo anasimama kama ishara mbaya,
Na nyoka amebeba tabia kuu tatu, ya kwanza ni kudanganya kama tunavyomsoma pale Edeni alivyomdanganya Hawa (Mwanzo 3:1-5), tabia ya Pili ni kuuma kama biblia inavyotuambia atakugonga kisigino (Mwanzo 3:15), na ya tatu ni kumeza, kama tunavyosoma katika kitabu cha Ufunuo 12:4), pale alipotaka kummeza mtoto yule alipotaka kuzaliwa,..Na tabia hizi zote Shetani anazo na ndio maana kila mahali alifananishwa na joka, na sio kiumbe kingine chochote kama vile kondoo au njiwa.
Hivyo ndoto za namna hii nyingi zinatoka kwa shetani, na chache sana zinakuja kutoka kwa Mungu, lakini tukianza kuchambua upande mmoja mmoja hatutamaliza, wengine wanaota wanakimbizwa na nyoka, wengine wanaota wanaumwa na nyoka, wengine wanaota wameviringishwa na nyoka, wengine wanaota wapo karibu na ziwa au bahari na lijoka likubwa linatoka huko, wengine wanaota wanamezwa na joka, wengine wanaongea nayo n.k. n.k. vyovyote vile chamsingi ambacho mtu anapaswa kufahamu hapo ni kuwa ziwe zinatoka upande wa Mungu au upande wa shetani,..Ni kwamba ADUI YUPO MBELE YAKO.
Hapo Shetani yupo karibu na wewe kutimiza kazi hizo tatu au aidha mojawapo,
Jambo la kwanza ni kukudanganya au tayari ameshakudanganya: Sasa Ikiwa upo nje ya Kristo yaani hujaokoka basi fahamu kuwa upo chini ya udanganyifu wa shetani tayari, hivyo hapo unaonyeshwa hali yako ilivyo rohoni, Jambo unalopaswa kufanya ni kurudi kwa Kristo haraka sana kabla udanganyifu haujawa mkubwa zaidi ukakuzalia matunda ya mauti, hapo ulipo tayari umepofushwa macho pasipo hata wewe kujijua. Hivyo tubu umgeukie Mungu haraka sana, maadamu muda bado upo.
Au kwa namna nyingine shetani anakaribia kukushawishi kuingia katika kosa au dhambi ambayo itakugharimu sana, hata maisha yako, hivyo angalia njia zako, uchukue tahadhari, funga milango yote ambayo unaona itakupeleka mbali na Kristo, acha kufanya vitu ambavyo sasa hivi unavifanya unaona kabisa havimpendezi Mungu, acha haraka sana, upo mtego wa shetani nyuma yake.
Pili shetani anakutegea mtego au anataka kukuletea madhara aidha katika huduma yako, au afya yako,au familia yako au shughuli yako, anataka kukugonga kisigino chako usisonge mbele, hapo unapaswa uongeze kiwango chako cha maombi kama Bwana Yesu alivyosema ombeni msije mkaingia majaribuni..Hivyo ili kumshinda silaha uliyonayo ni kuomba sana.
Tatu shetani anataka kukimeza kile ambacho Mungu amekipanda ndani yako:
Na jambo la kwanza huwa anakimbilia ni NENO LA MUNGU hilo ndilo huwa anafanya bidii sana kupambana nalo kwasababu anajua likishakuwa ndani ya mtu litakwenda kuleta madhara makubwa sana katika ufalme wake hivyo anasimama hapo karibu na wewe ili akimeze kile ulichokisikia.. inafananishwa na zile mbegu ambazo zilingukia njiani ndege wakaja kuzila,
Mathayo 13:18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. 13.19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Mathayo 13:18 “Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi.
13.19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Hivyo kwa ufupi ikiwa upo nje ya Kristo fanya hima uingie ndani, na ikiwa upo ndani ya Kristo chukua tahadhari uimarishe uhusiano wako na Kristo kwasababu shetani yupo karibu na wewe kushindana nawe kwa kila hali..
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU.
JE! WEWE NI MWANA WA IBRAHIMU?
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
UZAO WA NYOKA.
Mtu anayeuliza swali hili ninaamini kabisa anauliza kutoka katika dhana hii “Kama Mungu ni tajiri, kwanini basi na watu wake wasiwe matajiri kama yeye”…Na ndio maana swali kama hili la kwanini wakristo wengi ni maskini linajengeneza kichwani mwake…Lakini laiti kama angejiuliza kwa kulinganisha wakristo na watu wengine, au kuulinganisha ukristo na dini nyingine basi swali hili ninauhakika lingeshajijibu lenyewe kichwani mwake..
Kwani bila shaka hakuna asiyejua idadi ya matajari na maskini duniani haiwezi kuwa sawa na wala haitakaa ikaribiane daima, karibu katika kila Nyanja na kila eneo na kila sekta, utakuta maskini au watu wenye uchumi wa kati ni wengi kuliko matajiri, hata ukienda katika mataifa yanayojiona kuwa ni matajiri, hata ukirudi mataifa maskini, hata ukienda katika dini zote, sio tu katika ukristo, ukienda pia kwa waislamu utakuta waislamu wengi ni maskini kuliko matajiri, ukienda kwa wahindu utakuta hivyo hivyo, ukienda kwa wasio na Mungu jambo ni lile lile kwahiyo ukitazama kwa jicho hilo utagundua kuwa hilo sio jambo la kushangaza sana.
Lakini kwasababu tunataka kuwalinganisha sawasawa na Mungu wao wanayemtumikia, naomba ubofye somo hili ulipitie taratibu naamini utapata majibu yote yaliyojibiwa kulingana na maandiko..…>>> JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
BIBLIA INAPOSEMA “HERI WALIO MASKINI WA ROHO MAANA UFALME WA MBINGUNI NI WAO”JE HATUNA RUHUSA YA KUWA MATAJIRI KATIKA ROHO?.
Kulingana na Biblia, Wakatoliki ni kweli wanaabudu sanamu…
Biblia inasema, katika
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”,
Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”,
Sasa tatizo sio kutengeneza sanamu, wala kuning’iniza picha manyumbani mwetu za watakatifu au za wanafamilia wetu, bali tatizo ni “kuzisujudia” na “kuzitumikia”…Hivyo vitu viwili ndio tatizo.
Sasa Kanisa katoliki linafundisha watu kusujudia sanamu pamoja na kutumikia sanamu. Na kumbuka sanamu haimaanishi tu lisanamu likubwa kama lile la Nebkadneza, bali sanamu hata ndogo tu kama punje ya harage pia ni sanamu…mbele za Mungu zote ni sawa!
Sasa Waumini wa kanisa katoliki wanafundishwa kuzipa hizi sanamu heshima fulani kana kwamba zimebeba kitu cha kiungu ndani yake..Kitendo tu cha kuzipa heshima fulani, kama kwamba ni kitu cha Kiungu hiyo tayari ni Ibada ndani ya moyo wa Mtu, na ndio kitu kinachomchukiza Mungu..
Kadhalika, kutumikia maana yake ni kukiwekea hicho kitu utaratibu fulani ambao ni kama sheria fulani inayokufanya wewe kuwa mtumwa wa hicho kitu…Kwamfano kusali rozari kila siku asubuhi, mchana na jioni na kuogopa hata kuikanyaga kwa bahati mbaya hiyo ni kuitumikia rozari….ambapo kwako inakufanya kuwa mtumwa..Jambo hilo ni machukizo mbele za Mungu.
Sasa si wakatoliki wote wanajua hilo, na si wakatoliki wote wana nia mbaya katika kwenda kuabudu katika kanisa hilo, wengi wana nia ya kweli ya kwenda kumtafuta Mungu, isipokuwa Mfumo wa Udini umewafunga hata hawawezi kuiona kweli tena!..Lakini wale Bwana aliowachagua wakati ukifika wanapokutana na Ukweli wanafunguka macho na kurekebisha njia zao, kwa kutoka katika mifumo ya kanisa hilo na kugeukia kumwabudu Mungu katika roho na Kweli.
JE BIKIRA MARIAMU ALIKUFA?
JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?
JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
WhatsApp
Mtume Paulo, hapo kwanza alikuwa akiitwa SAULI, Alikuja kuitwa Paulo baada ya kukutana na Bwana Yesu, na kubadilishwa….Alizaliwa mahali panapoitwa Tarso, huko Kilikia,…Kwasasa ni eneo la nchi ya UTURUKI.
Matendo 21:39 “Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge”.
Kwa asili Paulo alikuwa ni Myahudi (yaani Muisraeli) alikuwa ni wa kabila la Benyamini na alikuwa ni Farisayo.
(Wafilipi 3.5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,)
Mtume Paulo hakuoa mke, Alijizuia kuoa ili aihubiri Injili pasipo kuvutwa na mambo mawili, yaani mambo ya kumpendezesha mke na kumpendezesha Mungu..
1Wakorintho 7 :32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana; 33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”.
1Wakorintho 7 :32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”.
kama alivyokuwa Yohana Mbatizaji na Eliya Nabii hao pia hawakuoa. Na hivyo kuwafanya Injili yao kuwa na matunda mengi kuliko wengine wote.
Biblia inasema hakuna Nabii aliyetokea aliye Mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, kadhalika Eliya ni nabii pekee ambaye hakuonja mauti..Na Mtume Paulo ni Mtume pekee ambaye alifanya kazi kuliko wote waliomtangulia.
YOHANA MBATIZAJI NI NANI?
YESU NI NANI?
SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.
Napendelea kabla mtu hajakimbilia kutafuta tafsiri ya ndoto yake, ni vizuri kwanza apate elimu juu ya aina za ndoto, hiyo itamsaidia kujua ndoto yake inaangukia katika kundi la aina gani, hivyo atapata wepesi wa kuweza yeye mwenyewe kuzitafsiri ndoto pasipo hata kutegemea msaada wa mtu mwingine.
Ikiwa utapenda kujua aina hizi za ndoto bofya hapa >> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI? ukishamaliza kusoma kisha tuendelee…
Sasa kama ndoto yako sio ile inayotokana na shughuli za kila siku au mazingira yanayokuzunguka na unaiota mara kwa mara, basi fahamu kuwa kuna jambo Mungu anazungumza na wewe hapo zingatia sana..Biblia inasema..
Ayubu 33:14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,”
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,”
Mungu anakukumbusha kuwa upo safarini hapa duniani, kwamba kila jambo unalolifanya ukumbuke kuwa upo safarini hakuna na chochote utashikamana nacho hapa duniani milele,..
Na kama tunavyojua safarini, hata mkishuka kupumzika pengine kula au kujisaidia basi ni dakika chache tu 10 au 15 basi safari inaendelea, hakuna muda wa kuzurura zurura au kuanza kujihangaisha na mambo ya hapo mlipokuwa mnapita, utakuwa ni mjinga kama utawaza kuwekeza eneo hilo, au kwenda kufanya shughuli hapo, gari litaondoka na kukuacha, na mwisho wa siku kule ulipokuwa unatazamia kwenda hutafika..
Hivyo Mungu kukuonyesha hivyo ni kukuonya usiangalie sana mambo ya ulimwengu huu yanayopita bali angalia vya kule mbele vinavyodumu na ukumbuke kuwa upo safarini, inamaanisha kuwa kwa namna moja au nyingine ulishawahi kuyatazama mambo ya kule, ishi kama maisha ya mpitaji, kwasababu watu wote wa Mungu ndivyo wanavyoishi..
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.”
Hivyo angalia ni vitu gani vinavyokusonga katika maisha yako, Je! Ni shughuli za ulimwengu huu mpaka hauna muda na Mungu? Je! Ni tamaa ya mambo ya ulimwenguni huu, Je ni anasa? Biblia inasema:
1Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.”
1Petro 2:11 “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.”
Hivyo Fahamu kuwa Mungu anakupenda na ndio maana amekuonyesha ndoto za namna hiyo, basi usipuuzie sauti yake, anza sasa kumtazama YESU ikiwa bado upo mbali naye, Unachopaswa kufanya ni kutubu sasa mkabidhi yeye maisha yako upya, nenda kabatizwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, kisha yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu…nawe utakuwa na uhakika wa kuwa salama katika safari yako fupi iliyobakia hapa duniani… Aidha kama utakuwa upo tayari ndani ya Kristo na unajihisi huna kando lolote basi fahamu kuwa Mungu anataka uzidi kuiangalia safari yako zaidi kuliko kitu kingine chochote, kwasababu ipo thawabu kubwa amekuandalia mbele.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
MFALME ANAKUJA.
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.
CHANZO CHA MAMBO.
UNYAKUO.
SIKU YA HUKUMU ITAKUWAJE?
Usipokuwa na uelewa wa kutosha juu ya ndoto, unaweza ukajikuta unatoka nje ya kusudi la Mungu ambalo amekukusudia wewe uishi kwalo hapa duniani..
Na hiyo imewafanya watu wengi wazunguke huko na huko, kutafuta tafsiri ya ndoto zao..Lakini jambo la kwanza na la msingi sana kufahamu ni kuwa, tunapaswa kujua kuwa ndoto yoyote ni lazima iwepo katika mojawapo ya makundi haya matatu:
> Kundi la kwanza ni ndoto zinazotokana na Mungu,
> Kundi la Pili ni ndoto zinazotokana na shetani,
> na kundi la tatu ni ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe.
Sasa ndoto hizi zinazotokana na mtu mwenyewe huwa zinaathiriwa sana na mambo mbalimbali aidha kutokana na mazingira ya mtu yanayomzunguka au shughuli anazozifanya mara kwa mara, au mambo anayoyawaza kila wakati..Na aina hii ya ndoto ndiyo inayochukua asilimia kubwa sana ya ndoto watu tunazoziota kila siku, naweza kusema hata asilimia 95 ya ndoto tunazoziota kila siku na hizi huwa hazina maana sana, lakini watu kwa kukosa ufahamu imefanya wahangaike kutwa kuchwa kutafuta tafsiri ya kila ndoto yanazoziota mpaka inawafanya kuwa watumwa wa ndoto…Kumbe kiuhalisia sio kila ndoto ina ujumbe wa kutufaa..
Hivyo mtu akishakuwa na uelewa wa namna ya kuzigawanya ndoto hizi katika makundi haya hatapata shida kuitafsiri ndoto yake..Hivyo nakuashuri pitia kwanza somo hili kisha ndio tuendelee. >> NITAJUAJE KAMA NDOTO NI YA MUNGU AU YA SHETANI?
Sasa ukiota una mimba: Ikiwa ndoto hiyo haitokani na shughuli zako mwenyewe au mazingira yanayokuzunguka, au mawazo unayoyawaza kila mara, kwasababu kumbuka ndoto kama hizi huwa zinawatokea mara nyingi wanawake, kwahiyo uwezekano wa kuangukia katika kundi hilo la tatu la ndoto ni mkubwa kwasababu wanawake maisha yao tangu wakiwa watoto wanawaza siku moja ni kuwa na mtoto kwahiyo kuota wamebeba mimba si jambo la kushangaza, au utakuta mwingine maisha yake yote anatamani sana kuwa na mtoto, hana watoto, moja kwa moja mtu kama huyo ni rahisi kuota ni mjamzito au mwingine utakuta anaishi na mwanamke mjamzito karibu na mazingira yake au jana amemwona mwanamke mmoja barabarani akipita akiwa mjamzito akajikuta usiku anaota kabeba mimba akadhani kuwa ndoto hiyo inamaana sana kwake..,
Ikiwa ni hivyo, basi zipuuzie tu, ni ndoto zinazokuja kutokana na mawazo yako. Hizo hazibebi ujumbe wowote kwako.
Lakini hapa tunadhania kuwa ndoto hiyo haijatoka katika vyanzo vya namna hiyo,
Sasa fahamu kuwa tendo lolote kuchukua mimba liwe ni jema au liwe ni baya, liwe limekuja kwa njia ya uzinzi au kwa njia ya haki ni lazima tu kiumbe kipya kije duniani mwisho wa siku hakuna namna!..Na kabla hakijaja lazima dalili Fulani zionekane…Hivyo kama ndoto yako imekuwa ni ya kujirudia rudia basi itilie maanani zaidi kwasababu inaweza kuwa imebeba ujumbe kutoka kwa Mungu,..
Utakumbuka Farao alipoota ndoto ile ihusuyo miaka saba na njaa na miaka saba ya neema, ilikuja mara mbili, hata kama ilichukua taswira nyingine lakini ujumbe ulikuwa ni mmoja..ndipo akawa na uhakika wa kuwa ndoto ile ni ya kuizingatia..Vivyo hivyo na wewe ikiwa unaota mara kwa mara una mimba, ni mjamzito izingatie sana ndoto hiyo.
Kwahiyo jambo unalopaswa kufanya hapo kwa kuwa wewe ndiye unayeyafahamu maisha yako zaidi kuliko mtu mwingine yeyote , kaa chini kwa utulivu mwingi utafakari maisha yako na njia yako unayoiendea sasa hivi..iwe ni katika huduma yako, iwe ni katika familia yako, iwe ni katika shughuli yako unayoifanya sasa, kuna uamuzi uliuchua, au kuna jambo ulilifanya ambalo hivi karibuni utakwenda kuona matokeo yake..
Hivyo kama ulimwomba Mungu juu ya kitu Fulani, kwa muda mrefu akupatie basi kaa katika matarijio ya kukipata, au kama ulijitaabisha katika kitu ambacho kwasasa faida yake haionekana kaa katika matarajio ya kukipata muda si mrefu..
Sara alikuwa katika matarajio ya kupata mtoto kwa muda mrefu, lakini wakati ulipofika malaika alimjia na kumwambia panapo wakati kama huu mwakani utalea mtoto..VIvyo hivyo na wewe kama upo katika mstari ulionyooka na Mungu wako basi tarajia Mungu kukupa kile ulichokuwa unakitafuta. Kwasababu mimba sikuzote ni matokeo ya ile mbegu iliyoingia ndani yako..Kama ni mbegu njema uliipanda basi utavuna kilicho chema.
Vile vile kama ulikuwa ni mwovu unafanya mambo yasiyompendeza Mungu nawe pia kaa katika matarajio ya kukipata hicho ulichokuwa unakifanya, ikiwa ulikuwa mchawi jiandae kuvuna matunda ya uchawi wako, ikiwa ulikuwa ni tapeli au mla rushwa jiandae kukumbana na ulichokihangaikia, kama ulikuwa ni mrushi vile vile jiandae kukutana na malipo yake hivi karibuni…
Usishangae kukutana na mabaya, kwasababu biblia inasema dhambi nayo huwa inapitia hatua hizo hizo mpaka kufikia mauti.
Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”
Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.”
Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.”
Isaya 59:3 “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya.4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.”
Isaya 59:3 “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya.
4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.”
Hivyo kama unatenda maovu sasa, acha mara moja, Tubu dhambi zako, umegukie muumba wako YESU KRISTO kabla huo wakati wa mabaya haujafika, lakini kama unajijua upo katika njia iliyonyooka na umekuwa katika dua ya kumwomba Mungu kwa ajili ya kitu Fulani chema..Basi kuwa katika matarajio ya kukipata siku za hivi karibuni.
USHUHUDA WA RICKY:
KUOTA UNAPEWA PESA.
Warumi 3: 23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.
JEHANAMU NI NINI?
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
NJAA ILIYOPO SASA.
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele”.
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
SANDUKU LA AGANO LILIKUWA LINAWAKILISHA NINI KATIKA AGANO JIPYA?
BWANA YESU ALIKUWA NA MAANA GANI KUSEMA CHAKULA CHA WATOTO USIWAPE MBWA KATIKA MATHAYO 15:21-28?