Title June 2024

JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA? 

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu katika kujifunza Neno la uzima.

Ni vizuri kufahamu mana waliyopewa wana wa Israeli jangwani, ijapokuwa ilikuwa ni ileile lakini haikuwa na ubora sawa. Utajiuliza kwa namna gani?

  1. Ipo mana iliyodumu kwa siku moja (1): Ndio ile waliyokuwa wanaiokota kila siku asubuhi, na kuipika, jua lilipozuka iliyeyuka, lakini pia iliposazwa siku ya pili yake ilivunda.
  2. Mana ya pili ni ile iliyodumu kwa siku mbili(2). Mungu aliwaangiza siku moja kabla ya sabato waokote mana ile, ambayo wataila, mpaka siku ya sabato, na itakuwa sawa. Lakini ikisazwa hadi siku ya tatu, inavunda.
  3. Mana ya tatu, ilidumu daima: Hii haikuharibika kwa vizazi vyote. Ni ile aliyoambiwa Musa aichukue na kuihifadhi ndani ya sanduku la agano. Iwe kumbukumbu kwa vizazi vyote vijavyo.

Habari hiyo utaisoma kwenye Kutoka 16:19-36

Je hili hufunua nini katika agano jipya?

Mana ya kwanza:

Kama vile tunavyojua mana ni chakula walichopewa na Mungu wakile na kuishi, katika mazingira magumu (ya jangwani).Na katika hiyo hawakuugua, wala miguu yao kupasuka.

Vivyo hivyo kwa sasa Mana ni chakula cha rohoni ambacho tumepewa tukile sisi tuliookoka, katika huu ulimwengu wa upotovu, ili katika hicho tusiathiriwe na dhambi au mauti, mpaka siku ya ukombozi wetu.

na chakula chenyewe ni “ufunuo wa Yesu Kristo” au kwa lugha nyingine ni “Neno la Mungu lililofunuliwa”(Yohana 6: 30-35)

Mtu yeyote anayeokoka, lazima ajue hapaswi kukaa tu, na kusema imekwisha, Yesu aliyamaliza yote. hapana vinginevyo atakufa kiroho. Bali anapaswa aanze kula NENO (ndiyo mana) ili aukulie wokovu, kama Israeli walivyokula jangwani. Na hiyo huchangiwa na kufundishwa injili ya kweli kutoka kwa walimu sahihi, huku na yeye mwenyewe akionyesha bidii katika kutamani kufundishwa pamoja na kusoma Biblia kila siku.

Sasa mtu kama huyu rohoni akifanya hivyo anaonekana anakula mana lakini sasa mana yake kwa mwanzoni, humtia nguvu ya kitambo kidogo, ni sawa na mtu anayekunywa maziwa na yule anayekula ugali ipo tofauti, ni kweli vyote vinafaa mwilini lakini vyote vina nguvu tofauti.

Ndivyo ilivyo kwa mtu aliye mchanga kiroho, hufunuliwa  lile neno la awali (Maziwa).

Hivyo fadhili za Mungu zitamlinda mtu huyu, siku kwa siku kwa jinsi anavyozidi kufundishwa na kujisomea, ndio maana Mtu aliyemchanga kiroho akikosa Neno au fundisho kwa muda mrefu, ni rahisi sana kufa, Haiwezekani mtu akasema nimeokoka halafu hana habari na kufundishwa. Kujipima kama wewe ni hai au umekufa angalia usomaji wako/kujifunza kwako Neno.

Mana ya pili:

Lakini kwa jinsi mtu huyu anavyojenga uhusiano wa karibu na Mungu wake siku baada ya siku, basi Neno lile linapokea nguvu, ya kumuhifadhi kwa kipindi kirefu kidogo,. Wana wa Israeli kwasababu walikuwa wanaingia  katika sabato kwa Mungu wao,ili kumwabudu na kumsifu, ile mana ilipokea nguvu kwa hiyo siku yao ya sabato haikuharibika.

Halikadhalika na mtu awapo katika kujibidiisha na kazi ya Mungu, utumishi wa Mungu, huduma ya Mungu. Lile Neno linapokea nguvu ya kumuhifadhi wakati wote huo ahudumupo. Maana yake uwezo wa kuhifadhiwa na Mungu unakuwa mkubwa. Huyu mtu anayejibiisha na Mungu, hawi mwepesi kuanguka dhambini, hawi mwepesi kurudi nyuma ovyo, hawi mwepesi kushambuliwa na mwovu hata kukosa shabaha kabisa, hawi mwepesi kupungukiwa kabisa.

Fadhili za Mungu hukaa juu yake, huyu mtu kwa wakati wote amtumikapo Mungu kwa moyo wa dhati, au azingatiapo ibada nyingi. Mungu humuhudumia yeye. Lakini kwamfano akianza kupoa, na kulegea, ataanza kuona tu nguvu za Mungu zinaisha ndani yake ukame unatokea, uzito unakuja, ugumu unaamka tena ndani yake. Hufananishwa na kile chakula alichopewa Eliya na malaika, akaweza kuenda na nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini. Hiyo ndio mana ya pili ambayo Bwana atakulisha wewe utumikaye mbele zake.

Mana ya Tatu:

Lakini ile mana ambayo hudumu milele. Utakumbuka kuwa sharti yake ni ikae ndani ya sanduku. Na sanduku letu ni Kristo, ambaye ndani yake hazina zote za hekima na maarifa  zimesitika (Wakolosai 2:3).

Kwa jinsi mtu unavyoendelea kudumu ndani ya Kristo, kwa uaminifu, kwa wakati fulani mrefu, Bwana hujifunua kikamilifu kwao. Na hapo fadhili za Mungu hazikomi, wala kupungua juu yao milele. kwasababu wameufikia ule utukufu halisi wa Mana iliyofichwa, ambayo si kila mtu anaifikia. Hatua hii, humfanya huyo mtu wakati wote kuwa chini ya fadhili nyingi za Mungu, neema nyingi zinakuwa juu yake, sikuzote ni kwenda mbele tu hakuna kurudi nyuma, wala kupoa, wala hakuna siku atapoa ki-upendo kwa Mungu, Mungu atajifunua kwake kwa namna yake mwenyewe.

ndio maana alitoa ahadi hiyo kwa kanisa la Pergamo akasema..

Ufunuo 2:17

[17]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. YEYE ASHINDAYE NITAMPA BAADHI YA ILE MANA ILIYOFICHWA, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

Kushinda nini?

Ukianzia juu (Ufunuo 2:12-17) utaona anasisitiza,

kutoikana imani na kuendelea kuwa mwaminifu, kwa kutojichanganya na mafundisho ya uongo, ambayo yanakufanya usiwe mtakatifu Rohoni. Mafundisho hayo yalifananishwa na yule Balaamu aliyewaletea Israeli wanawake wa kimataifa ili wawaoe  kisha wafundishwe kuabudu miungu, ili wamkosee Mungu. Ndugu epuka mafundisho ya kidunia, baki kwenye Neno likufanyalo kuwa mtakatifu, tembea katika huo. Fahamu tu Mana hiyo ipo sandukuni imefichwa, si kila mtu anaweza kuifikia hivyo huna budi na wewe kuingia humo, kwa kuishi maisha ya kumtii Kristo. Fikia utukufu huo wa mana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.

MNGOJEE BWANA

CHAKULA CHA ROHONI.

(Opens in a new browser tabUSIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Mchuuzi ni nani? (Hosea 12:7).

Swali: Mchuuzi maana yake nini kama tunavyosoma katika Hosea 12:7? na je tunaruhusiwa kuwa wachuuzi?


Jibu: Turejee.

Hosea 12: 7 “Ni MCHUUZI, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu”

Mchuuzi ni mtu anayefanya biashara ya kununua bidhaa na kuzisafirisha kwenda kuziuza mahali pengine hususani nje ya nchi yake.

Utalisoma neno hili tena katika kitabu cha Wimbo ulio bora 3:6, Ezekieli 27:3,  Ezekieli 27:20-22 na Isaya 23:8.

Swali ni je biblia inaturuhusu wakristo kuwa Wachuuzi (yaani biashara ya kutoka nchi moja kwenda nyingine)?

Jibu ni ndio inaruhusu!, isipokuwa katika biashara yoyote ile ni muhimu kuzingatia viwango vya utakatifu na ukamilifu, Uchuuzi wowote ukihusisha rushwa au biashara haramu ni kosa kibiblia, na pia ni hatari kama maandiko yanavyosema katika Ezekieli 28:18.

Ezekieli 28:18 “Kwa wingi wa maovu yako, KATIKA UOVU WA UCHUUZI WAKO, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).

Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).

Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipo hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)

Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Rudi Nyumbani

Print this post

KUWA NA JUHUDI KATIKA ROHO.

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo Mwanga wa njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zaburi 119:105).

Wengi tuna juhudi katika “mwili” lakini hatuna juhudi katika “roho”. Juhudi katika mwili ni nzuri na inafaa lakini ile ya roho ni bora Zaidi na inafaa sana. Kwasababu biblia inasema Roho ndiyo inayoutia uzima (Yohana 6:63).

Sasa Neno la Mungu linasema..

Warumi 12:11 “kwa bidii, si walegevu; MKIWA NA JUHUDI KATIKA ROHO ZENU; mkimtumikia Bwana”.

Sasa hizi juhudi katika roho ni zipi?..

   1. JUHUDI KATIKA MEMA.

1Petro 3:13 “Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema”.

Matendo mema ni pamoja na kuwasaidia wanyonge (masikini, wayatima na wajane), kusamehe na mengineyo..

    2. JUHUDI KATIKA KUPENDANA.

1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

9  Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika”

Mtu mwenye juhudi katika roho ni yule pia mwenye juhudi katika kuutafuta upendo.

    3. JUHUDI KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU.

Kazi ya Mungu si lazima iwe ule ya kusimama mimbarini na kuhubiri/kufundisha.. Lakini pia ile ya kusafisha nyumba ya Mungu, ni kazi yenye thawabu kubwa na heshima kubwa kwa Mungu… Ukiwa na juhudi katika kumtumikia Mungu kwa njia hiyo pasipo kusukumwa au kukumbushwa kumbushwa bali unajituma wewe mwenyewe, basi hapo unaonyesha juhudu uliyonayo katika roho, na ukomavu wako kiroho.

   4. JUHUDI KATIKA KUOMBA.

Ikiwa utaweza kuomba kila siku kwa muda usiopungua lisaa limoja, hiyo ni ishara kubwa ya kuwa una juhudi katika roho, lakini kama kuomba kwako ni mpaka jumapili kwa jumapili, basi kuna ulegevu ulio ndani yako.

   5. JUHUDI KATIKA KUSOMA NENO.

Mtu mwenye kutia bidii katika kujua mafunuo yaliyo ndani ya biblia kwa njia ya kujifunza na kutafiti na kurudia rudia kutafakari yale aliyoyasoma na kujifunza, mtu wa namna hiyo kibiblia ni mwenye juhudi katika roho na si mlegevu.

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.

   6. JUHUDI KATIKA KUMTOLEA MUNGU.

Sadaka inakamilisha ibada kwa mkristo yoyote yule (ikiwemo mchungaji, mwalimu, nabii, mwinjilisti au mtumishi mwingine yoyote). Na mtu mwenye bidii nyingi katika kumtolea Mungu, mtu huyo kulingana na biblia ni mwenye juhudi katika roho.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwa namna gani mauti ya wacha Mungu ina thamani machoni pake? (Zaburi 116:15).

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

IKIWA MWENYE HAKI AKIOKOKA KWA SHIDA, MWENYE DHAMBI ATAONEKANA WAPI?

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).

Rudi Nyumbani

Print this post

Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini? (Mwanzo 4:15)

SWALI:Ni alama gani Mungu aliyomtia Kaini mwilini?


Tunaona Kaini baada ya kumuua ndugu yake Habili, Mungu alimpa adhabu kwa kumwambia maneno haya;

Mwanzo 4: 9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

Lakini tukiendelea kusoma tunaona, Kaini anamlilia Mungu na kumwambia adhabu yangu ni kali sana, haichukuliki, kila mahali nitakapoenda nitakuwa mtu wa kuuliwa, ndipo Mungu akamuhakikisha ulinzi kwa kumwekea alama. Kama tunavyosoma kwenye vifungu vinavyofuata;

13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.

14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga

Swali linakuja hii alama ni ipi?

Lakini kabla ya kufahamu alama yenyewe ni nini ni vizuri ukaelewa maana ya adhabu aliyopewa ya kuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. Fungua hapa ufahamu tafsiri yake >>>> UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.

Hivyo tukirudi kwenye swali alama ni ipi?

Zipo nadharia nyingi, lakini tujifunze kwanza baadhi ya mambo.  Kumbuka kuwa adhabu ile Kaini aliitambua kabisa ilihusu kutengwa na fadhili na uso wa Mungu kabisa. Na mahali popote pasipo na mkono wa Mungu hapana usalama wowote, ni sawa na mwili unaokosa kinga, kila kila ugonjwa unaopita pale utaushambulia, haya yale madhaifu kabisa,. Ndicho alichokigundua Kaini alijua pasipo Mungu duniani hata kwa sehemu ndogo, haiwezekaniki  kuishi kila mwenye uhai atakuweza tu, wanyama watakuweza, mapepo yatakuweza. Ndio maana ya kauli yake hiyo ‘kila anionaye ataniua’.

Lakini Mungu akamuhakikishia usalama, kwa kumwekea alama, ili yoyote akimwona asimuue Kaini. Sasa kufikiri alama hiyo ni mchoro(tattoo) Fulani mwilini, si rahisi kumfanya mtu asidiriki kumuua, kwani mchoro hauzuii mtu kuangamizwa.

Lakini kufikiri alama iliwekwa katika eneo la ki-mwonekano (ukubwa), au eneo la kuongezewa sifa/ufanisi Fulani ulitofauti na wengine yaweza kuwa jambo la kweli.

Kwanini?

Tunaweza kuona baada ya pale sifa za uzao wa Kaini jinsi zilivyokuwa, walikuwa ni watu wavumbuzi, watu wa elimu (Mwanzo 4:20-22) lakini pia Hodari na wengine wao wenye maumbo makubwa (Mwanzo 6:4),.  Kwahiyo sikuzote tunafahamu hata sasa walio na uwezo mkubwa wa kielimu na kiteknolojia si rahisi kuwaweza kivita, hata iweje. Tofauti na uzao wa Adamu kwa Sethi, walikuwa ni wakulima tu na wafugaji. Hawakuwa na ujuzi mwingi ijapokuwa walikuwa ni uzao wa Mungu.

Kwahiyo wana wa Kaini, waliitawala dunia, hawakuwa watu dhaifu dhaifu, na yoyote ambaye angejaribu kumuua mmojawapo, kisasi kingemrudia mara saba, kwa nguvu tu walizokuwa nazo, ijapokuwa hawakuwa na Mungu maishani mwao.

Ni kutufundisha nini?

Si jambo la ajabu Mungu kumuhakikisha ulinzi mtu mwovu, leo hii wengi watasema Bwana mbona wenye dhambi ndio wanaofanikiwa, mbona waovu ndio wenye nguvu duniani, wapo salama, ndio wenye mavumbuzi makubwa. Fahamu kuwa hiyo ni alama yao. Ambayo ilianzia tokea mbali kwa Kaini. Kwasababu wangekuwa waovu, halafu pia wanyonge, wangeishije kwenye hii dunia.

Kamwe usiitamani alama ya Kaini, usitamani kulindwa ndani ya uovu, kwasababu utadumu kwa kitambo tu, baadaye utaangamizwa kama ilivyokuwa kwa hawa, katika gharika. Yesu alitoa mfano wa magugu na ngano katika shamba, kama tunavyoifahamu ile habari, wale wakulima walitaka kwenda kuyang’oa magugu shambani ili waziache ngano. Lakini mwenye shamba akasema waache vyote vikue pamoja mpaka siku ya mavuno, ndipo yatakusanywa na kutupwa motoni.

Na tafsiri ya mfano ya ule mfano akasema shamba ni ulimwengu, na ngano ni wana wa ufalme, lakini magugu ni wana wa ibilisi, na wavunaji ni malaika. Kuonyesha duniani yapo mapando ya aina mbili, na yote yatashiriki mbolea, maji, matunzo yote kutoka kwa Mungu, na kimsingi magugu huwa ndio mepesi kustawi kwa haraka kuliko ngano.

Jiulize na wewe ambaye unastarehe katika dhambi na hauoni madhara yoyote, unaelekea wapi? Hujui umetiwa alama kwa muda, nguvu zako, utajiri wako, mafanikio yako, zaidi ya watu wa Mungu, usidhani ndio umebarikiwa unathamini na Mungu.  lakini wakati utafika kuzimu utaiona.  Embu kubali sasa kuwa mwana wa ufalme, kwa kumaanisha kutubu dhambi, na kumfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili akuondolee deni la dhambi uwe mtakatifu mbele zake kwa damu yake, akuepushe na hukumu inayokuja .

Ikiwa upo tayari kuokoka leo. Fungua hapa >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

Nitamjuaje nabii wa Uongo?

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Fahamu ni nani aliye mwandishi wa kitabu cha Mathayo.

SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Mathayo ni nani?


Kama jina la kitabu linavyojieleza “INJILI KAMA ALIVYOIANDIKA MATHAYO MTAKATIFU”. Maana yake ni kuwa kitabu hiki kiliandikwa na Mathayo. Lakini utata unakuja ni Mathayo yupi?

Ijapokuwa biblia haielezi ni Mathayo yupi lakini wanazuoni wengi na watafiti wa historia kibiblia, wanahitimisha kusema ni Mathayo mtume wa Yesu Kristo Yule mtoza ushuru, ambaye alijulikana pia kwa jina la Lawi (Marko 2:14) ndiye aliyekiandika kitabu hicho.

Kitabu hiki kinaeleza Mwanzo wa kutokea mwokozi duniani, mpaka Kifo chake na kufufuka kwake. Ndani yake kuna historia ya mwokozi, mafundisho na matendo ya miujiza aliyoyafanya. Katika kitabu hiki zipo hotuba kuu tano ambazo Yesu alizisema;

  1. Hotuba ya mlimani (Mathayo 5-7)
  2. Hotuba ya utume (Mathayo 10)
  3. Hotuba ya ufalme wa mbinguni (Mathayo 13)
  4. Hotuba ya kanisa (Mathayo 18)
  5. Hotuba ya Siku za mwisho (Mathayo 24)

Kwa upana wa hotuba hizi na uchambuzi wa kitabu hiki, fungua hapa, >> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA MATHAYO.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?

Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Wafalme(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Nini maana ya  “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)

Rudi Nyumbani

Print this post

Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?

SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Mithali alikuwa nani?


Sulemani mwana wa Daudi, anajitaja mwenyewe kama mwandishi, katika mwanzo kabisa wa kitabu hiki

Mithali 1:1 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.2 Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu

Kitabu hichi kinakadiriwa kuandikwa miaka mia tisa (900) kabla ya Kristo.Ni kitabu kilichojaa maneno ya hekima na kanuni, maagizo ya rohoni, vilevile maonyo mbalimbali yanayohusiana na maisha ya kawaida,  pamoja na maarifa na mafunzo yaliyo katika vitu vya asili.

Migawanyo yake:

Mithali 1-22:16, Iliandikwa na Sulemani mwenyewe.

Kuanzia Mithali 22:17-24:34, zilizojulikana kama kitabu cha Tatu, huwenda ziliandikwa na wengine lakini zikakusanywa na Sulemani mwenyewe.

Lakini Kuanzia Mithali 25-29, biblia inatuambia ziliandikwa na Sulemani, lakini watu wa mfalme Hezekia ndio waliozirekodi.

Na Mithali 30, Ambacho hujulikana kama kitabu cha Tano. Kiliandikwa na Aguri bin Yake.

Lakini Mithali 31 ambacho ni cha mwisho, kiliandikwa na mfalme Lemueli.

Japo wanazuoni wengine husema Aguri bin yake na Lemueli, yalikuwa  ni majina mengine ya Sulemani.

Kwa vyovyote, kitabu hichi kwa sehemu kubwa kimeandikwa na Sulemani. Ndio maana hujulikana kama kitabu cha Sulemani. Lakini pia hatuna uhakika asilimia zote  hekima zote ziliandikwa na yeye mwenyewe, kufuata na hao watu wawili wa mwisho wasiojulikana.

Kwa urefu wa chambuzi wa kitabu hichi fungua link hii >> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)

Hizi ni baadhi ya fafanuzi ya hekima tuzisomazo katika kitabu hicho

Maana ya Mithali 21:17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;

Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; 

Fahamu maana ya Mithali 25:13 Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; 

Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?

Nini maana ya  Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je! Sulemani alienda mbinguni?

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.

Print this post

Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Wafalme

SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Wafalme alikuwa nani?


Biblia haijaweka bayana aliyekuwa mwandishi wa kitabu hiki, lakini kufuatana na hadithi za kiyahudi huaminika kuwa nabii Yeremia ndiye alikuwa mwandishi wa vitabu hivi viwili vya wafalme.

Kitabu hichi kinaeleza kwa kina tawala za kifalme Kuanzia Mfalme Sulemani, na kugawanyika kwa  taifa la Israeli pande mbili, hadi kuanguka kabisa kwa taifa lote la Israeli  kwa kuchukuliwa  utumwani Ashuru na Babeli. Miongoni mwa Wafalme wapo waliosimama vema, lakini pia wapo wengi waliolikosesha taifa la Israeli, Wa kwanza alikuwa  ni Yeroboamu ambaye ndiye aliyeupokea ufalme uliogawanyika yeye aliunda  sanamu na kuzisimamisha kaskazini na kusini mwa Israeli, ili waisraeli wakamwabudu Mungu huko. Machukizo ambayo yaliendelea hivyo kwa muda mrefu, ijapokuwa zilikuja kuondolewa hizo sanamu na mfalme aliyeitwa Yosia, lakini bado hasira ya Mungu haikupoa kwa mambo mengi mabaya waliyokuwa wanayatenda wana wa Israeli, Hadi walipofikia hatua ya kuhamishwa.

Kwa urefu wa uchambuzi wa vitabu hivi waweza fungua hapa upate kujisomea  >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5

Bwana akubariki.

Je! Wewe umepokea wokovu wa Roho yako kwa Kristo Yesu? Kama ni la! Basi wakati ndio huu wa kufanya geuko la dhati, moyoni mwako. Ikiwa upo tayari basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.

Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)

Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

Mwandishi wa kitabu cha Filemoni ni nani?

Mwandishi wa kitabu cha Filemoni

Kitabu cha Filemoni ni moja ya nyaraka ambazo mtume Paulo aliziandika akiwa kifungoni Rumi.  Waraka huu alimuandikia Filemoni mtu ambaye alimgeuza yeye mwenyewe katika injili yake. Baadaye akawa mtendakazi katika utumishi wa Bwana, katika nyumba yake mwenyewe. Na kuwa Baraka kwa watakatifu wengi huko Kolosai.

Filemoni 1:2 “na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako”

Kilichomsukuma hasaa mtume Paulo kuandika waraka huo ilikuwa ni kwa mtendakazi wake mpya aliyemzaa katika Kristo aliyeitwa Onesmo ambaye hapo mwanzo alikuwa ni mtumwa wa Filemoni aliyemwibia vitu vyake na kukimbia. Kwamba sasa ampokee na kumchukulia kama mtendakazi mwenzao, kwasababu ametubu na anafaa kwa utumishi. Kwa urefu wa mafunzo yaliyo ndani ya kitabu hichi cha Filemoni, Fungua hapa, ujifunze kwa kina >>>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.

Je! Umempokea Kristo maishani mwako?

Kama ni la! Basi wakati ndio huu, bofya hapa kwa mwongozo wa namna ya kumpokea Kristo maishani mwako. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>   https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.

Shalom.

Usiishie kutafuta tu utakaso wa roho, bali tafuta pia UTAKASO WA MWILI, kwamaana vitu hivi viwili vinaenda sambamba, kwasababu vitu hivi vikichafuka vinaiharibu pia nafsi ya mtu.

2Wakorintho 7:1“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.

Upo usemi kuwa Mungu wetu hatazami sana Mwili, lakini anatazama Zaidi Roho ya Mtu. (Hatuna budi kuwa makini na kauli hii!!)

Kutokana na kwamba asilimia kubwa ya maombi yetu yanalenga MAHITAJI YA MWILINI, basi ni wazi kuwa Mungu anaitazama pia miili yetu. Kwasababu kama mtu atamwomba Mungu Baba ampe fedha, au chakula, au makazi hayo yote si kwasababu ya “roho” kwasababu roho haili chakula, wala haivai nguo, wala haiishi kwa fedha.. bali mwili ndio unaohitaji hayo yote.

Sasa kama tutamlazimisha Mungu Baba aangalie miili yetu kwa mahitaji yetu, halafu wakati huo huo tunasema Mungu haangalii mwili, tutakuwa WANAFIKI!!.

Sasa ikiwa asilimia Zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yetu, yanalenga MIILI YETU, Basi ni wazi kuwa Mungu anaangalia Miili yetu na anajishughulisha nayo sana….

Ni lazima kulijua hili ili tusipotee na elimu ya uongo ya shetani,.. Ni lazima pia tujishughulishe kutafakari namna ya kuyafanya mapenzi ya Mungu katika miili yetu kama tu vile tunavyojishughulisha katika kumwomba mahitaji ya mwili..

1Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU mhifadhiwe MWE KAMILI, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Katika mstari huo biblia imetaja mambo yote matatu; Nafsi, mwili na roho. (yanapaswa yawe makamilifu, bila lawama mpaka wakati wa kuja kwake Bwana YESU).

Hivyo zingatia yafuatayo:

  1. NI NINI UNAFANYA KUPITIA MWILI WAKO.

Jipime ni nini unakifanya katika mwili,.. je shughuli au matendo unayoyafanya kupitia mwili wako ni kulingana na mapenzi ya Mungu??.. Kama unafanya kazi haramu (mfano ukahaba, au kazi ya kuuza vitu haramu kama pombe, sigara, na mengineyo), basi kazi hiyo unaifanya kupitia mwili wako hivyo ibadili ili isikupeleke jehanamu ya moto.

Kama matendo unayoyafanya katika mwili ni  haramu mfano uzinzi (1Wakorintho 6:18), wizi, au mauaji n.k geuka leo yasije yakawa sababu ya kukupeleka hukumuni.

   2. NINI UNAKIAMBATANISHA NA MWILI WAKO

Angalia ni nini unakiambatanisha/unakishikamanisha na mwili wako.. Hapa nazungumzia aina ya mavazi na urembo na michoro (tattoo). Je mavazi uvaayo ni sawasawa na Neno la Mungu?.. Je yanaipasa jinsia yako sawasawa na Kumbukumbu 22:5.

Je mavazi unayovaa ni ya kujisitiri?, kuzuia tamaa kwa upande mwingine na kutunza heshima yako? (1Timotheo 2:9 na Mathayo 5:28)

Je michoro uichorayo na rangi yako ya asili uiondoayo ni mapenzi ya Mungu? (Walawi 19:28)

Angalia ni nini kinanin’ginia mwilini mwako.. Je hizo cheni, hereni, mikufu, bangili, vikuku n.k ni mapenzi ya Mungu?? Je si ishara ya utumwa?? (hebu soma Kutoka 21:5-6 na Kumbukumbu 15:16-17).

   3. NI NINI KINAINGIA MWILINI MWAKO.

Angalia ni kitu gani unakiingiza mwilini mwako.. Je Mungu amekusudia moshi uingia katika mapafu yako ambayo yanapaswa yavute hewa safi ili kutimiza miaka uliyopewa yakuishi duniani?..

Je Mungu amekusudia uingize vilevi na madawa ya kulevya ndani ya mwili wako na kukutoa ufahamu wako kwa muda?.. Jiulize kama si ruhusu kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa umelewa/umekunywa pombe.. vipi kuuendesha huo mwili ukiwa umelewa??.. Huoni kama huo ni uvunjaji wa sheria kubwa Zaidi, kwasababu mwili ni bora kuliko gari au chombo kingine chochote cha usafiri.

2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

KIJITO CHA UTAKASO.

Nini Maana ya Adamu?

WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Rudi Nyumbani

Print this post

Maana ya Mhubiri 1:9 “wala jambo jipya hakuna chini ya jua”. 

SWALI: Mhubiri anamaana gani anaposema “Wala jambo jipya hakuna chini ya jua” na angali tukiangalia tunaona kila siku mambo mapya yanavumbiliwa mfano wa AI (artificial inteligence)? ambayo hayakuwepo zamani?.


JIBU: Kuelewa vizuri alimaanisha nini kwa kusema hivyo tuanzie vifungu vya  juu kuitazama habari yote ililenga eneo lipi.

Mhubiri 1:2-11

[2]Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.

[3]Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?

[4]Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.

[5]Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.

[6]Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.

[7]Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.

[8]Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.

[9]Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.

[10]Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.

[11]Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.

Ukichunguza hapo halengi uvumbuzi na maendeleo ya kibinadamu, kwasababu hata wakati wake Sulemani kulikuwa na mavumbuzi mengi tu yeye mwenyewe alisema;

Mhubiri 7:29

[29]Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.

Lakini alikuwa analenga ‘kazi ya Mungu aliyoifanya chini ya jua’ na ‘misingi ya mifumo ya kiulimwengu’ kwa ujumla, katika hayo hakuna jipya. ndio maana anasema jua huchomoza jua huzama, tangu zamani jua ni lile lie, ijapokuwa sayansi inakuwa, kamwe haliwezi siku moja nikachomoza la kijani, upepo ni ule ule unafuata mkondo wake, kamwe hauwezi tokea ardhini, kizazi kinakuja, kizazi kinakwenda hakuna jipya, mito ni ile ile inatiririka kamwe maji hayewezi kubadilika na kuongea,  Yaani mwanadamu hata hajitahidi vipi, katika ujumla wake wa maisha atazunguka tu mulemule watu wa kale walipozunguka. Watu watazaliwa, watu watakufa.

Vilevile katika mifumo ya kiulimwengu, wafanyabiashara walikuwepo, watakuwepo, wajenzi walikwepo watakuwepo, maudhui ya maisha ni ile ile, ni mwonekano tu unabadilika, ni sawa na mtu aliyevaa leo suti, kesho kanzu, haviwezi kumbadili mtu na kumfanya malaika. Au unga wa ngano, leo utatengenezea chapati, kesho mkate, kesho kutwa maandazi, bado ngano ni ileile hakuna jipya ndani yake tukaona inazaa pilau.

Ndio maana maandiko yanatufundisha ni nini jambo sahihi la kufanya tuwapo duniani tusije kuta tunapoteza muda kudhani tunaweza leta jambo jipya duniani. Lakini tunafundishwa tumche Bwana, ndio jambo lenye maana linaloleta jambo jipya moyoni mwa mwanadamu, ambalo ni uzima wa milele.

Mhubiri anamalizia kwa kusema…

Mhubiri 12:13

[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;  Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Je! Umeupokea wokovu wa Bwana Yesu? Kama ni La! Huu ndio wakati sahihi wa kupokea msamaha wa dhambi zako na uzima. Tubu ukabatizwe katika jina la Yesu Kristo, upokee ondoleo la dhambi zako na kipawa cha Roho Mtakatifu, atakayekusaidia kuishi maisha matakatifu. Ikiwa utapenda mwongozo huo basi fungua hapa kwa msaada huo.. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MJUMBE WA AGANO.

NI KIZAZI KIPI WEWE UPO?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

SAUTI NYUMA YA ISHARA.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post