Mbaruti ni nini?.(Mibaruti ni mimea ya aina gani) na umebeba ujumbe gani kiroho?.
Jibu: Turejee,
Mathayo 7:16 “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?”
Soma pia 2Wafalme 14:9, 2Nyakati 25:18 na Hosea 10:4.
Mbaruti/Mibaruti ni jamii ya mimea yenye maua, ambayo mara nyingi inajiotea maporini. (Mimea hii inatoa matunda ambayo ina miiba inayoizunguka pande zote, kuifanya kutolika na wanyama walao nyasi). Tazama picha juu..
Katika biblia Bwana YESU alinukuu mimea huu wa mbaruti katika swali lililowahusu manabii wa uongo.. Aliuliza je watu huchuma tini katika mibaruti?,.. Maana yake ni jambo lisilowezekana kupata matunda ya “Tini“ kutoka katika jamii ya mimea hiyo ya maua ya mibaruti.
Vile vile akasema haiwezekani kuchuma zabibu kutoka kwenye miti ya miiba…
Kuonyesha kuwa Manabii wa uongo wanatoa matunda yenye MIIBA MIIBA!!.yasiyofaa kwa kuliwa bali yanaumiza na kuchoma!.
Moja ya matunda wanayotoa ni tamaa za fedha, (wakizitamani na kuwafundisha watu hizo)..ambazo biblia inasema wanaozama huko wanajichoma kwa maumivu mengi..
1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.
Manabii wa uongo kamwe hawahubiri wala kufundisha Toba na Utakatifu, wala safari ya kwenda mbinguni hawaihubiri kwasababu huko hawaendi!.na wao si wasafiri wa kwenda huko, hivyo mioyo yao ipo hapa hapa duniani na wanahubiri vitu vya duniani, pasipo kuweka mambo katika uwiano.
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 7.20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua”
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?
Mungu amejifunua katika Ofisi kuu 3, (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu).
Lakini katika dhihirisho zote hizi tatu (3) Mungu anabaki kuwa mmoja na si watatu.
Sasa swali ni je kama ni mmoja kwanini ajifunua hivyo katika utatu?
Jibu rahisi ni kwamba, Mungu kajidhihirisha hivyo kwa lengo la kumkamilisha Mwanadamu na si kujitambulisha yeye. Na kwanini mwanadamu akamilishwe kupitia dhihirisho hizo tatu?..Ni kwasababu alikuwa amepotea na kujitenga mbali naye kwasababu ya dhambi.
(Dhambi zinatutenganisha sisi na Mungu) Kama maandiko yanavyosema…katika Isaya 59:2.
Mwanzo katika Edeni Mungu alikuwa karibu sana na MTU, aliweza kumwona, kumsikia, na hata kuzungumza naye (Mwanzo 3:8). Lakini baada ya dhambi kuingia ule ukaribu na Mungu ukapotea, Adamua akawa hawezi kumwona tena Mungu wala kumsikia kama alivyokuwa anamsikia mwanzo…Ile dhambi ikamtenga mbali na Mungu. (Isaya 59:2).
Na Mungu kwa upendo wake kwetu, akaanza mpango wa kuturejesha karibu naye tena. Tumwone tena, tuseme naye, tutembee naye na tumhisi ndani yetu kama mwanzo. Lakini matengenezo hayo si ya mara moja kama maharibifu. (kuharibu mahusiano ni mara moja, lakini kujenga inagharimu muda mrefu).
Na neno la ahadi ni kwamba siku moja MASKANI ya MUNGU itakuwa pamoja na wanadamu kuliko hata ilivyokuwa EDENI.
Ufunuo 21:3 “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, NAYE ATAFANYA MASKANI YAKE PAMOJA NAO, NAO WATAKUWA WATU WAKE. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao”.
Sasa mahusiano hayo yaliyoharibika Mungu alianza kuyatengeneza hatua kwa hatua..na sasa tupo katika hatua ya mwisho wa matengenezo hayo.. Hebu tuzitazame hizo hatua moja baada ya nyingine.
1.MUNGU JUU YETU. (Kama Baba)
Hii ni hatua ambayo Mungu alianza kuongea na watu kwa njia ya Maono na Ndoto, lakini akawa haonekani. Na alisema na watu wachache tu walioitwa manabii. Huu ni wakati ambao MUNGU alijidhihirisha kama NENO tu!.. (Maana yake MANENO YAKE ndiyo yaliyokuwa yanafahamika tu lakini yeye mwenyewe haonekani kwa macho).
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”.
2. MUNGU PAMOJA NASI (Kama Mwana).
Huu ni wakati ambao Mungu aliuvaa mwili, ili yale MANENO aliyokuwa anasema na watu kwa njia ya maono na ndoto basi ayaseme kwa mdomo wa damu na Nyama na kuyafafanua na kuyafundisha ili watu wamwone na kumwelewa.. Na mwili ambao aliuvaa ndio ukaitwa YESU.
Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.
Umeona?..Mungu anaanza kumsogelea tena mwanadamu kwa karibu.. Kwahiyo YESU ni Mungu aliyeuvaa mwili kwa lengo hilo la kuyasema yale maneno ya Mungu yaliyokuwa yanayosikika kwa ndoto na maono kupitia manabii..
Kuzidi kuuthibitisha uungu wa YESU basi soma mistari ifuatayo (Yohana 20:28, 1Yohana 1:1-2, Tito 2:13, Isaya 9:6 na 1Timotheo 3:16).
Lakini isingetosha tu Mungu aonekane katika mwili na kuyahubiri maneno yake kwa mdomo kama alivyokuwa anaongea na Adamu pale Edeni na huku bado mwanadamu hajui kanuni ya kuishi katika mapenzi ya Mungu…Hivyo akaongeza mpango wa pili juu yake wa kumfundisha mwanadamu njia na kanuni za kuishi kimatendo, kwahiyo ikambidi aishi kama mwanadamu ambaye anamcha Mungu.
Lengo si kutafuta ukamilifu yeye, bali ni kutufundisha sisi ukamilifu, ndio maana akaishi chini ya wazazi ili awafundishe watoto namna ya kuishi maisha ya kumcha Mungu, na tena akawa mtu mzima ili awafundishe watu wazima kanuni za kumcha Mungu, ndio maana akawa anaomba, akawa anafunga, akawa anamwambudu Mungu kana kwamba kuna Mungu juu n.k.
Hivyo maisha yake yakawa njia ili sisi tufahamu njia (soma Yohana 14:6). Lakini yeye hakuwa mtu, bali ni Mungu ndani ya mwili wa Mtu kwa lengo la kutufundisha njia..
Wafilipi 2:5 “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu”
Lakini pia isingetosha yeye ahubiri maneno yale kwa kinywa chake, na awe mwalimu wa kutufundisha sisi na ili hali bado tuna laana ya dhambi tuliyoirithi toka kwa wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa
Hivyo akaongeza mpango mwingine wa tatu (2) juu ya hiyo miwili, kwamba autoe mwili wake huo kuwa sadaka ya dhambi baada ya kumaliza huduma kazi hizo mbili.. Hiyo ndio sababu kwanini Kristo afe msalabani..Ni ili sisi tupate ondoleo la dhambi.
3. MUNGU NDANI YETU (Kama Roho Mtakatifu).
Baada ya kurejesha uhusiano namna hiyo, kwamba sasa tunamwona MUNGU na tumeondolewa dhambi na kile kizuizi kulichokuwa kinatutenga sisi na Mungu, na ile laana ya Adamu tuliyokuwa tunaibeba. Mungu aliongeza mpango mwingine wa Mwisho ambao kupitia huo tutakuwa karibu na Mungu moja kwa moja, kwamba tutamsikia na kumwona na kumwelewa sana.
Na mpango huo si mwingine Zaidi ya yeye kuingia ndani yetu, kama ROHO, ili atusaidie madhaifu yetu..Ni sawa na mchezaji aliye katika michezo anayepewa kinywaji cha kuongeza nguvu na kusisimua misuli ili ashinde katika mchezo ule.
Na Roho Mtakatifu ni MUNGU katika ROHO, ambaye anaingia ndani yetu na KUSISIMUA uwezo wetu wa kumwelewa MUNGU, UWEZO wetu wa KUSHINDA DHAMBI, uwezo wetu wa KUMCHA MUNGU, Uwezo wetu wa kukumbuka n.k (Yohana 14:26 na Yohana 16:12-13).
Sasa kuthibitisha kuwa Roho Matakatifu ndiye yule yule Mungu soma 2Wakorintho 3:17.
Hii ni zawadi kubwa na kipekee sana, na ya mwisho inayomsogeza Mtu karibu na Mungu kuliko zote.
Sasa swali la ziada ni hili; Kwanini KRISTO aondoke!
Sababu ya KRISTO kuondoka na kwenda juu mbinguni ni kwenda kutuandalia sisi makao (Yaani ile YERUSALEMU MPYA), Makao ya watakatifu. (soma Yohana 14:2, Ufunuo 3:12 na Ufunuo 21:2).
Na makao hayo anayokwenda kutuandalia ni ili wakati utakapofika tukae naye milele, katika mbingu mpya na nchi mpya. (Maskani yake iwe pamoja nasi)…Hapo yale yaliyoharibika Edeni yatakuwa yametengenezwa upya tena katika utukufu Mkuu kuliko ule wa kwanza.
Ufunuo 21:3 “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli”.
Je umeuona mpango wa Mungu??…na je umeyaona pia madhara ya dhambi??… Dhambi ilitutenga mbali na Mungu na mpaka sasa inatutenga mbali na Mungu..
Na kanuni pekee ya kumkaribia MUNGU ni kwa kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha (Mithali 28:13). Unapotubu kwa kumaanisha kuziacha unamkaribisha YESU maishani mwako ambaye humwoni kwa macho sasa, lakini siku moja utamwona… Lakini zawadi kubwa atakayokupa ambayo itakufanya ujihisi upo naye hata kama humwoni ni ROHO MTAKATIFU (ambaye kiuhalisia ni yeye mwenyewe katika mfumo wa Roho).
Na huyo Roho Mtakatifu atakulinda na ulimwengu, mpaka siku ya mwisho, ambayo BWANA YESU ATAKUJA na kutupa TAJI ZA UZIMA, na kukaa naye milele katika maisha ya furaha, yasiyo na mwisho, wala dhiki wala mateso, wala uchungu, wala vilio..kwasababu mambo ya kwanza yatakuwa yameshapita.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000
Kwa namna gani tumefanyika Makuhani na Ufalme?.(Ufunuo 1:6)
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
(Masomo maalumu yahusuyo matoleo na sadaka).
Karibu tujifunze bible, Neno la Mungu wetu lililo mwanga wa Njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zab. 119:105).
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa Sadaka katika agano jipya, na shetani anafanya kila awezalo kuwazuia watu wasitoe sadaka kwa Mungu, kwani anaijua Nguvu iliyopo katika sadaka kwa mkristo.
Na moja ya njia anayotumia kuwafanya watu wasimtolee Mungu, ni kuwanyanyua watu/watumishi wake ambao watalichafua eneo hilo kwa aidha kuwalazimisha watu, au kuwatapeli, au kutumia uongo kwa kivuli cha biblia.
Na mtu aliye dhaifu kiimani, akishaona kasoro hizo basi moja kwa moja anakata shauri au anaadhimia kutotoa kabisa sadaka mahali popote kwa kuamini kuwa ni utapeli tu ndio unaoendelea, hivyo adui anakuwa ameshinda juu ya huyo mtu katika eneo la utoaji.
Lakini jambo ni moja tu!.. SADAKA INA NGUVU, na kila MKRISTO (pasipo kujali wadhifa wake, iwe mchungaji au mwanafunzi) NI LAZIMA AJIFUNZE KUTOA SADAKA ili KUFUNGUA MILANGO YA BARAKA na KUONDOA VIKWAZO.
Sasa zipo faida nyingi za SADAKA, lakini leo nataka tuizungumzie hii moja, ambayo ni muhimu sana kuijua…Nayo si nyingine Zaidi ya “KUHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU”. Si kila madhabahu inaharibiwa kwa kuomba tu!, la! Nyingine ni lazima zihusishe matoleo/Sadaka.
Hebu tusome habari ya Gideoni kidogo.
Waamuzi 6:25 ”kawa usiku uo huo Bwana akamwambia, MTWAE NG’OMBE WA BABA YAKO, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI, aliyo nayo baba yako, UKAIKATE ASHERA ile iliyo karibu nayo;
26 UKAMJENGEE BWANA, MUNGU WAKO, MADHABAHU juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; UKAMTWAE YULE NG’OMBE WA PILI NA KUMTOA AWE SADAKA YA KUTEKETEZWA, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata”
Hapo kuna hatua 4 Gideoni alizoambiwa na Mungu azifanye, ambazo zimebeba funzo kubwa..
1.MTWAE NG’OMBE WA BABA
Kwanini Amtwae Ng’ombe wa Baba yake?.. Kwasababu madhabahu ile ya baali ilikuwa imemshika sana baba yake (ilikuwa na nguvu juu ya nyumba ya baba yake yote). Ikifunua kuwa na sisi tunapotaka kushughulika na madhabahu za mababa, ni lazima tutafute sadaka kwajili yao, tena zile zinazowagusa kama hiyo ya Gideoni.
2. UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI.
Baada ya Gideoni kumtwaa Ng’ombe wa baba yake, hatua iliyofuata ni kuangusha ile madhababu ya baali na ashera iliyomshika baba yake (kwa kuivunja vunja na kuiponda ponda). Na sisi baada ya kuandaa sadaka hatua inayofuata ni kuzivunja hizo madhabahu kwa damu ya YESU kwa njia ya maombi na kwa KUZIONDOA KABISA KIMWILI KAMA ZINAONEKANA..
Kama kuna miti fulani inatumika kiibada hapo ulipo unaikata, kama ni mazindiko yamewekwa juu ya dari unayaondoa, wala usiogope, na tena wakati mwingine usimwambie mtu..wewe yaondoe kimya kimya kama alivyofanya Gideoni..ukienda kutafuta ruhusa hawatakuruhusu..zaidi utanyanyua vita vikali..
Gideoni angeenda kumpa kwanza taarifa baba yake kwamba ile madhabahu ya baali anaenda kuivunja baba yake asingemwelewa kabisa, kwani zile roho zilikuwa zimemshika baba yake na alikuwa anaiogopa sana ile miungu.. Vile vile madhabahu za mababa/na mababu zimewashika na kuwaogopesha wanaoziabudu.
Hivyo wewe vaa ujasiri kuwasaidia, kwani baada ya hapo watamshukuru Mungu wako kwa mambo yatakayofanyika baada ya hapo.
3.UKAMJENGEE BWANA MADHABAHU.
Baada ya Gideoni kuvunja ile madhabahu akaijenga madhabahu ya BWANA pale pale. Na sisi baada ya maombi na kusafisha kila uchafu..tunalisimamisha jina la Bwana mahali pale, kwa kuanzisha ibada, au kanisa…Wengi baada ya maombi hakuna tena kinachoendele, jambo ambalo ni la hatari sana!..
Ni lazima jina la Bwana liendelee kutamkwa mahali pale, ili madhabahu ya adui isisimamishwe tena, kama ni nyumbani au kijijini. (Maombi ya asubuhi na jioni lazima yafanyike, vile vile nyakati za kujifunza Neno la Mungu lazima ziendelee, na watu waendelee kumtafuta Mungu).. Sio kuomba tu na kuacha!.
4. UKAMTOE NG’OMBE KUWA SADAKA.
Baada ya Gideoni kujenga madhabahu akamtoa yule Ng’ombe wa baba yake awe sadaka na hapo ndipo ukawa mwisho wa Nguvu ya ile madhabahu ya baali kutenda kazi…ikamwachia baba yake moja kwa moja, hata alipokuja na kusikia kuwa ile madhabahu ya ashera imevunjwa na mwanae wala hakuogopa kwani tayari vifungo vya uoga vilikuwa vimeshamwachia…. na hata yeye (Gideoni) naye pia alifunguliwa kwa ujumla.. Na hapo ndio ukawa mwanzo wa ushujaa wa Gideoni!.
Vile vile na sisi tunapomaliza maombi na kuhitimisha kuvunja madhabahu…Ile sadaka inapaswa itumike kujenga kanisa la pale, au kuimarisha ibada za pale, ikiwa na maana kwamba kama fedha basi zitumike kununua biblia, au vitabu vya nyimbo, au kama ni kiwanja kimetolewa kama sadaka basi kitumike kujenga kanisa ili watu wa Mungu waendelee kumwabudu Mungu wa kweli pale.
Lakini ikiwa hakuna namna ya wewe kufika mahali pale ambapo madhabahi hizo zimesimamishwa, aidha kutokana na umbali.. basi baada ya maombi toa sadaka katika madhabahu nyingine yoyote ya Mungu aliye hai na italeta matokeo yale yale. Lakini kumbuka USIOMBE TU, BILA KUTOA!..TOA TOA TOA!!!!!
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Manabii Wanaume katika biblia walikuwa wengi kiidadi kuliko manabii wanawake.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA JEDWALI:
Kutazama Jadwali zima, basi Slide kuelekea upande wa kushoto.
N/A | JINA | WAFALME WALIOTAWALA ENZI ZAKE | MIJI/MATAIFA ALIYOYATOLEA UNABII | MAJIRA ALIYOTOA UNABII |
---|---|---|---|---|
1. | ELIYA | Ahabu, Ahazia na Yoramu | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
2. | ELISHA | Yoramu, Yehu na Yehoahazi | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
3. | YONA | Yeroboamu wa Pili | NINAWI (Ashuru) | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
4. | NAHUMU | Manase, Amosi na Yosia | NINAWI (Ashuru) | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
5. | OBADIA | Sedekia | EDOMU | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
6. | HOSEA | Yeroboamu wa Pili, Zekaria, Shalumu, Menahemu, Pekahia,Peka na Hoshea | ISRAELI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
7. | AMOSI | Yeroboamu wa Pili | ISREALI | Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru |
8. | ISAYA | uzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
9. | YEREMIA | Yosia, Yehoahazi,Yehohakimu, Yekonia na Sedekia. | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
10. | YOELI | Yoashi | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
11. | MIKA | Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase. | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
12. | HABAKUKI | Yehoyakimu na Yekonia | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
13. | SEFANIA | Amoni na Yosia | YUDA | Kabla YUDA haijapelekwa Babeli |
14. | EZEKIELI | Yekonia na Sedekia | YUDA (Ikiwa utumwani Babeli) | Wakati YUDA Ikipelekwa utumwani Babeli |
15. | DANIELI | Yehohakimu, Yekonia na Sedekia. | YUDA (Ikiwa utumwani Babeli) | Wakati YUDA ikiwa utumwani Babeli |
16. | HAGAI | Liwali ZERUBABELI | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
17. | ZEKARIA | Liwali ZERUBABELI | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
18. | MALAKI | Liwali NEHEMIA | YUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani) | Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli |
Mbali na hawa walioorodheshwa katika Jedwali hilo hapo juu, walikuwepo pia Manabii wengine ambao hawakuonekana wakitajwa katika kutoa Nabii za Nchi au Taifa.. Mfano wa hao tunawaona katika Jedwali lifuatalo.
N/A | JINA | MFALME ALIYETAWALA WAKATI WAKE | HALI KIROHO | MAREJEO |
---|---|---|---|---|
1. | MUSA | Isreli wakiwa Misri na Jangwani | WA KWELI | Kutoka, M/Walawi, Kumbukumbu na Hesabu |
2. | MIKAYA | Ahabu | WA KWELI | 1Wafalme 22:13 |
3. | AHIYA | Yeroboamu | WA KWELI | 1Wafalme 1:45 |
4. | NATHANI | Sauli | WA KWELI | 2Samweli 7:2 |
5. | Nabii wa Yuda (Asiyetajwa jina) | Yeroboamu wa Kwanza | WA KWELI | 1Wafalme 13:1-9 |
6. | Nabii MZEE (Asiyetajwa jina) | Yeroboamu wa kwanza | MCHANGANYIKO | 1Wafalme 13:11-14 |
7. | HANANIA | Yekonia na Sedekia | WA UONGO | Yeremia 28:15-17 |
8. | Manabii 400 (wasiotajwa majina) | Ahabu | WA UONGO | 1Wafalme 22:6 |
9. | BALAAMU | Israeli wakiwa Jangwani | WA UONGO (Mchawi) | Yoshua 13:22 |
10. | BAR-YESU | Nyakati za kanisa la Kwanza | WA UONGO (Mchawi) | Matendo 13:9 |
11. | AGABO | Nyakati za kanisa la Kwanza | WA KWELI | Matendo 11:28 na Matendo 21:10 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU
Orodha ya Manabii wa kike katika biblia.
Jumla ya Manabii wa kike (wanawake) waliotajwa katika biblia ni 11, Kati ya hao manabii Tisa (9) walikuwa wa KWELI na Wawili (2) walikuwa wa UONGO.
LIFUATALO NI JEDWALI LA UFUPISHO..
Kulitazama jedwali zima, basi ‘SLIDE’ kuelekea kushoto.
N/A | JINA | URAIA | HALI ZA KIMWILI | HALI YA KIROHO | MAREJEO |
---|---|---|---|---|---|
1. | MIRIAMU | ISRAELI | Dada wa Musa na Haruni | WA KWELI | Kutoka 15:20 |
2. | DEBORA | ISRAELI | Haijatajwa katika Biblia | WA KWELI | Waamuzi 4:4 |
3. | HULDA | ISRAELI | Mke wa Shalumu | WA KWELI | 2Wafalme 22:14, 2Nyakati 34:22 |
4. | MKE WA ISAYA | ISRAELI | Mke wa Isaya | WA KWELI | Isaya 8:3 |
5. | ANA | ISRAELI | Mjane | WA KWELI | Luka 2:36 |
6. | BINTI WA FILIPO | ISRAELI | Binti wa Filipo | WA KWELI | Matendo 21:8-9 |
7. | BINTI WA FILIPO | ISRAELI | Binti wa Filipo | WA KWELI | Matendo 21:8-9 |
8. | BINTI WA FILIPO | ISRAELI | Binti wa Filipo | WA KWELI | Matendo 21:8-9 |
9. | BINTI WA FILIPO | ISRAELI | Binti wa Filipo | WA KWELI | Matendo 21:8-9 |
10. | NOADIA | ISRAELI (Mlawi) | Haijatajwa | WA UONGO | Nehemia 6:14, Ezra 8:33 |
11. | YEZEBELI | TIRO (LEBANONI) | Mke wa Mfalme Ahabu | WA UONGO (Mchawi) | Ufunuo 2:20 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.
Nini maana ya Mithali 11:17 inaposema;
Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
JIBU: Mwenye rehema ni mtu wa huruma, mwenye kusamehe, mwenye kuachilia hata kama tendo alilofanyiwa linastahili adhabu kwa yule mwingine.
Biblia inasema mtu kama huyo huipa faida nafsi yake. Huitendea mema nafsi yake. Ambayo huipata kwanza hapa hapa duniani, kwasababu Bwana alisema kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa na watu.
Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Maana yake ni anajijengea wigo mpana wa yeye naye kukutana na rehema nyingi mbeleni.
Vilevile anapata faida katika ulimwengu ujao, Bwana alisema..
Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Lakini anasema pia, mtu mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mkali ni kinyume cha mtu mwenye rehema, ni mtu asiye na huruma, mwenye visasi, asiyejali, mkorofi, akiudhiwa anarudisha Maudhi, akikosewa kidogo, analipiza mara mbili, maneno yake hayana staha, kugombeza wengine kwake ni jambo la kawaida n.k.
Sasa matokeo ya mtu wa namna hii ni kuadhibiwa na Mungu, aidha hapa hapa duniani, au kule aendapo.
Bwana alisema…auaye kwa upanga, atauwawa kwa upanga, ukimtendea mtu kwa ukali na wewe ukali utakurudia, ukimpiga mwingine kwasababu kakuudhi kidogo, na wewe utapigwa mahali fulani kwasababu ulimuudhi mwingine.. (hicho huitwa kisasi cha Mungu).
Hivyo tendea mema nafsi yako, lakini pia mwili wako, kwa kumpenda Bwana. Na kuwa mwema.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.(Opens in a new browser tab)
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
(Opens in a new browser tab)NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.(Opens in a new browser tab)
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?(Opens in a new browser tab)
SWALI: Nini maana ya Mithali 20:11 inaposema;
Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
JIBU: Mwandishi anatuonyesha kuwa tabia ya mwanadamu yoyote, huwa haijifichi kufuatana na umri wake, kwamba yaweza kukaa ndani tu kipindi cha utotoni isionekane ikaja kudhihirika ghafla ukubwani. Hapana, anasema “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili”.
Ikiwa na maana katika utoto ule ule unaweza kuuchunguza mwenendo wa mtoto, ukautambua. Na hiyo itakupa fursa ya kuurekebisha ukiwa ni mbaya, au kuuimarisha ukiwa ni mzuri, akiwa katika vipindi kile kile. Usione mwanao anayotabia ya udokozi, ukasema huyu ni mtoto tu, haelewi anachokifanya. Hapana unapaswa umrekebishe mapema, kwasababu hicho kitu kipo ndani yake, Ukiona mtoto anapenda kutazama biblia, anapenda kukaa kanisani, anapenda kusikiliza nyimbo za injili. Usiseme, huyu ni mtoto, ukampuuzia tu, kwa kuishia kusema ‘ubarikiwe mwanangu’ kinyume chake, mwendelezee mazingira hayo, kwasababu mwelekeo wa maisha yake, ni huko.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tabia zake zilianza kuonekana tangu utotoni, wazazi wake walimstaajabia, kumwona katika umri ule mdogo, yupo hekaluni, amekaa na waalimu na wakuu wa dini akiwauliza maswali, Kinyume chake wazazi wake hawakumkemea, bali waliyaweka yote mioyoni mwao, na kukubali kuutambua mwelekeo wa mtoto wao.
Hii ni kufundisha nini?
Lipo funzo la rohoni, lakini pia la mwilini.
La mwilini ni kuwa yatupaswa tuwatazame watoto, bila kupuuzia kitendo chochote wanachokidhihirisha katika umri ule wa chini. Ikiwa ni chema tukipalilie, ikiwa ni kibaya, tukikemee, na kushughulika nacho kwelikweli kabla hakijaweka mizizi. Hivyo hakuna mzazi au mlezi anaweza kusema, huyu mwanangu kabadilika tu ghafla. Ukweli ni kwamba mabadiliko yalianza kuwepo tangu zamani, isipokuwa kwa namna moja au nyingine tulipuuzia, tulipoyaona ndani yao tukadhani ni tabia za utoto tu. Wazazi wanaowajenga wanao katika maadili na vipawa tangu utotoni, ukiwatazama watoto wao wanapokuwa watu wazima, huwa wanakuwa na ufanisi na ujuzi wa hali ya juu sana, zaidi ya wale ambao watajijengea wenyewe wanapokuwa watu wazima. Hivyo mzazi jali maisha ya kiroho ya mwanao.
Vilevile rohoni, wapo ambao ni wachanga kiroho. Ikiwa na maana katika kanisa ni wale ambao wameokoka hivi karibuni. Halikadhalika hawa nao utaweza kutambua karama zao, sio mpaka wawe wakomavu kiroho. Aliye Mwinjilisti, utaona anapenda kushuhudia, lakini pia anauwezo wa kuwavuta wengine kwa Bwana. Aliye mwalimu, utaona anapenda sana kujifunza, aliye nabii, utaona karama za maono, ndoto, huwa zinamjia mara kwa mara, hata kwa namna ambazo hazielewi elewi, mwimbaji atapenda wakati mwingi kujifunza kuimba hata kama hawezi. Hivyo, kila mmoja wetu, kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake, hujidhihirisha mapema sana pindi ameokoka. Sio mpaka awe amekomaa sana kiroho kama wengi wanavyodhani.
Pindi unapookoka, kipindi hicho hicho karama yako inaanza kufanya kazi, unapachopaswa tu, ni kujishughulisha na utumishi wa Bwana, ndivyo utakavyoruhusu mambo hayo kutokea kwa wepesi na urahisi zaidi?
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
(TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.(Opens in a new browser tab)
Mitume wa BWANA YESU walikuwa 12, ambapo baadaye walisalia 11 baada ya YUDA ISKARIOTE, aliyemsaliti BWANA kufa kwa kujinyonga!.. Nafasi yake ilichukuliwa na MATHIYA, na hivyo kukamilisha idadi ya Mitume 12
IFUATAZO NI TAKWIMU YA MITUME WA BWANA.
Kutazama column za ziada slide jedwali lifuatalo kuelekea upande wa kushoto.
N/A | JINA | Majina Mengine | Jina la Mzazi | Mji aliotokea | kazi aliyokuwa anafanya | Vitabu vya biblia alivyoandika | Alivyokufa |
---|---|---|---|---|---|---|---|
1. | SIMONI | - Kefa/jiwe/Petro | Yona (Mathayo 16:17) | Bethsaida ya Galilaya | MVUVI | 2 (1Petro na 2Petro) | -Kwa Kusulibiwa kichwa chini miguu juu |
2. | ANDREA | Hakuna | Yona | Bethsaida ya Galilaya | MVUVI | Hakuna | - Kwa kusulibiwa |
3. | YAKOBO | -Boanerge | Zebedayo na Salome | Bethaida ya Galilaya | MVUVI | Hakuna | -Kwa kukatwa kichwa na Herode (Matendo 12:1-2) |
4. | YOHANA | -Boanerge | Zebedayo na Salome | Bethsaida ya Galilaya | MVUVI | 5 (Yohana, Waraka wa Yohana na Ufunuo) | - Katika uzee |
5. | MATHAYO | -Lawi | Alfayo (Marko 2:14) | Galilaya | MTOZA USHURU | 1 (Mathayo) | -Kwa kuchomwa Mkuki Ethiopia |
6. | BARTHOLOMAYO | - Nathanaeli | Halijatajwa katika Biblia | Galilaya | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | - Kwa kusulibiwa |
7. | TOMASO | - Pacha | Halijatajwa katika Biblia | Galilaya | MVUVI | Hakuna | -Kwa kuchomwa Mkuki, India |
8. | FILIPO | Hakuna | Halijatajwa katika Biblia | Galilaya | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | - Kwa kusulibiwa |
9. | YAKOBO | - Yakobo mdogo | Alfayo | Galilaya | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | -Kwa kupigwa Mawe |
10 | SIMONI | - Zelote | Halijatajwa katika Biblia | Kana ya Galilaya | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | - Kwa kusulibishwa |
11. | THADAYO | - Yuda | Yakobo | Galilaya | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | -Kwa kupigwa Mawe |
12. | YUDA | -Iskariote | Simoni | Keriothi | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | - Kwa kujinyonga |
13. | MATHIYA | Hakuna | Halijatajwa katika Biblia | Haujatajwa | Haijatajwa katika Biblia | Hakuna | -Kwa kukatwa kichwa |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Rudi nyumbani
Wafalme waliotawala ISRAELI, ukiwatoa wale watatu wa Mwanzo (Yaani Sauli, Daudi na Sulemani) walikuwa ni Wafalme 19 tu, na hakukuwa na Malkia aliyetawala Israeli kama ilivyokuwa kwa YUDA.
Kati ya Wafalme hao 19 waliotawala Israeli, hakuna hata mmoja aliyekuwa Mkamilifu mbele za MUNGU katika ukamilifu wote kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Wafalme waliotawala YUDA. Isipokuwa Mfalme mmoja tu aliyeitwa YEHU ndiye angalau alionekana kufanya Mema lakini pia alifanya na Mabaya.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.
JINA | MIAKA ALIYOTAWALA | MATENDO | MAREJEO | |
---|---|---|---|---|
1. | YEROBOAMU | 22 | MABAYA | 1Wafalme 12:25-33 |
2. | NADABU | 2 | MABAYA | 1Wafalme 15:25-31 |
3. | BAASHA | 24 | MABAYA | 1Wafalme 15:33-16:7 |
4. | ELA | 2 | MABAYA | 1Wafalme 16:8-14 |
5. | ZIMRI | 7 | MABAYA | 1Wafalme 16:15-20 |
6. | OMRI | 12 | MABAYA | 1Wafalme 16:21-27 |
7. | AHABU | 22 | MABAYA | 1Wafalme 16:29-33 |
8. | AHAZIA | 2 | MABAYA | 1Wafalme 22:51-53 |
9. | YORAMU | 12 | MABAYA | 2 Wafalme 1:17, 3:1-3 |
10. | YEHU | 28 | Nusu Mema- Nusu Mabaya | 2 Wafalme 9:30, 10:36 |
11. | YEHOAHAZI | 17 | MABAYA | 2 Wafalme 13:1-9 |
12. | YEHOASHI | 16 | MABAYA | 2 Wafalme 13: 10-25 |
13. | YEROBOAMU II | 41 | MABAYA | 2 Wafalme 14:23-29 |
14. | ZEKARIA | 6 | MABAYA | 2 Wafalme 15:8-12 |
15. | SHALUMU | Mwezi 1 | MABAYA | 2 Wafalme 15:13-16 |
16. | MENAHEMU | 10 | MABAYA | 2 Wafalme 15:17-22 |
17. | PEKAHIA | 2 | MABAYA | 2 Wafalme 15:23-26 |
18. | PEKA | 20 | MABAYA | 2 Wafalme 15:27-31 |
19. | HOSHEA | 9 | MABAYA | 2 Wafalme 17:1-7 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Wafalme waliotawala YUDA ni 19, na Malkia aliyetawala YUDA ni Mmoja (1), hivyo kufanya jumla ya Watawala 20 kupita katika Taifa la Yuda.
Kati ya hao Wafalme 19; waliofanya MEMA ni Wafalme saba (7) tu, wengine 12 waliosalia walifanya Mabaya. Na Malkia Mmoja aliyetawala naye pia alifanya Mabaya, hivyo kufanya jumla ya watawala 13 waliofanya mabaya.
UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.
Tafuta jina la Mfalme hapa >>
N/A | JINA | JINSIA | MIAKA ALIYOTAWALA | MATENDO | MAREJEO |
---|---|---|---|---|---|
1. | REHOBOAMU | M | 17 | MABAYA | 1Wafalme 11:42 |
2. | ABIYA | M | 3 | MABAYA | 1Wafalme 14:31-15:8 |
3. | ASA | M | 41 | MEMA | 1Wafalme 15:8-24 |
4. | YEHOSHAFATI | M | 25 | MEMA | 1Wafalme 22:41-51 |
5. | YEHORAMU | M | 8 | MABAYA | 2Wafalme 8:16-24 |
6. | AHAZIA | M | 1 | MABAYA | 2Wafalme 8:24-29 |
7. | ATHALIA | K | 6 | MABAYA | 2Wafalme 8:26, 11:1-20 |
8. | YOASHI | M | 40 | MEMA | 2Wafalme 11:21,12:1-21 |
9. | AMAZIA | M | 29 | MEMA | 2Wafalme 14:1-22 |
10. | UZIA | M | 52 | Mwanzo Mema-Mwisho-Mabaya | 2Wafalme 15:1-7 |
11. | YOTHAMU | M | 16 | MEMA | 2Wafalme 15:32-38 |
12. | AHAZI | M | 16 | MABAYA | 2Wafalme 15:38-16:20 |
13. | HEZEKIA | M | 29 | MEMA | 2Wafalme 18:1-20 |
14. | MANASE | M | 55 | MABAYA | 2Wafalme 21:1-18 |
15. | AMONI | M | 2 | MABAYA | 2Wafalme 21:18-26 |
16. | YOSIA | M | 31 | MEMA | 2Wafalme 21:26-23:30 |
17. | YEHOAHAZI | M | Miezi 3 | MABAYA | 2Wafalme 23:30-34 |
18. | YEHOYAKIMU | M | 11 | MABAYA | 2Wafalme 23:34- 24:6 |
19. | YEKONIA/ YEHOYAKINI | M | Miezi 3 | MABAYA | 2Wafalme 24:6-17 |
20. | SEDEKIA | M | 11 | MABAYA | 2Wafalme 15:24:17-25:30 |
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengineyo: