Jibu: Turejee…
Isaya 13:10 “Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze
“Matangamano” ni “Mkusanyiko wa nyota” unaoonekana na kutengeneza umbile Fulani. Wanajimu baadhi wameyataja matangamano hayo kwa maumbile ya wanyama mbali mbali, kwamfano lipo kundi moja wamelitaja kuwa na umbile kama la N’ge, lingine kama Dubu, lingine kama Simba, lingine mapacha n.k
Kwamfano kundi la nyota lenye umbile kama la Ng’e jinsi linavyoonekana mbinguni kwa macho ya damu na nyama ni kama linavyoonekana kwenye picha hapo juu.. Lakini kwa jinsi lilivyounganishwa na wanajibu mpaka kuleta umbo kama la Ng’e ni kama inavyoonekana hapa chini..
Na makundi haya ya nyota, sasa yanatumika kwa unajibu (ambayo ni elimu ya shetani asilimia mia) kwaajili ya utambuzi wa majira na nyakati za watu, Elimu hii kwa jina lingine inaitwa FALAKI, Fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).
Elimu hii wanajimu wanaitumia kutabiri mambo yajayo juu ya mtu, ndio hapo mtu anaenda kusomewa nyota yake na kufanyiwa utabiri, jambo ambalo kiuhalisia ni elimu ya giza, mtu yule anakuwa haambiwi mambo yajayo bali anapangiwa mambo yajayo na ibilisi, akidhani ndio katabiriwa.
Sasa Elimu hizi za Falaki pamoja na ibada zote za jua na mwezi na sayari, Bwana Mungu kazilaani, na siku za mwisho Jua, na mwezi vitatiwa giza, na Nyota zote za mbinguni zitaanguka na Matangamano yote yatazima.. kuonyesha kuwa mambo hayo yaliyotukuka kwa wanadamu si kitu mbele za Mungu, na Bwana atawaadhibu waovu pamoja na ulimwengu, ndivyo maandiko yasemavyo.
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. 10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. 11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.
Kuhusiana na unabii wa kufutwa kwa Mwezi, nyota na sayari zote siku za mwisho pitia maandiko haya Yoeli 3:15, Marko 13:24, Mathayo 24:29, na Ufunuo 6:12.
Kwahiyo ndugu usiende kusoma gazeti kwa lengo la kutafuta utabiri wa nyota, ni machukizo kwa Bwana, usiende kwa waganga ili wakakusafishie nyota, kinyume chake ndio unaenda kuharibu maisha yako, badala yake mfuate Bwana YESU naye atayasafisha maisha yako.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MKUU WA GIZA.
UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?
Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?
AGIZO LA UTUME.
Rudi Nyumbani
Print this post
Mathayo 10:33 “Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni”
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia.
Hebu tulitafakari kwa upana kidogo hili neno “kukanwa”.
Kukanwa ni ile hali ya kukataliwa na mtu unayemjua, unayetembea naye daima, uliyeweka matumaini yako kwake, mnayekubaliana au uliye na mahusiano naye ya karibu”
Na ipo tofauti ya “kukana na kusaliti”…kwa urefu juu ya tofauti ya maneno haya mawili fungua hapa 》》Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?
Sasa Bwana YESU anasema kuwa tukimkana mbele ya watu naye atatukana mbele ya Baba yake kule mbinguni.
Hebu tengeneza unafika kule, halafu unakanwa na yule ambaye ulikuwa unaona anatembea na wewe kila siku, anakuponya, anakulinda, ukiliita jina lake maajabu yanatokea, pepo zinatoka na miujiza mingi inafanyika.
Halafu huyu huyu ambaye ulipokuwa duniani alikuwa haonyeshi dalili ya kukukataa lakini unafika kule anakukana anasema hakujui!..ni jambo gumu sana kuamini!.
Lakini ndivyo itakavyokuwa siku ile..
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”
Hatuna budi kukaza mwendo daima na kila siku tukihakiki ni lipi limpendezalo Bwana (Waefeso 5:10).
Mtume Paulo ijapokuwa alikuwa na wingi wa mafunuo lakini alisema maneno haya..
1 Wakorintho 9:26 “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
1 Wakorintho 9:26 “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa”.
Na pia alisema…
Wafilipi 3:12 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.
Wafilipi 3:12 “Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu”.
Bwana atusaidie.
MFALME ANAKUJA.
JINA LAKO NI LA NANI?
UWEZA WA MUNGU NJE YA WAKATI.
Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)
JE UNAMHUBIRI KRISTO KATIKA KWELI YOTE?.
Swali: Maandiko yanasema KRISTO ameketi kutuombea, hata tufanyapo dhambi?
Jibu: Tafadhali soma taratibu na kwa umakini…
Warumi 8:34 “Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; TENA NDIYE ANAYETUOMBEA”.
Ni kweli Neno la Mungu linasema BWANA WETU YESU KRISTO, katika mstari huo na linazidi kututhibitishia tena katika 1Yohana 2:1.
1Yohana 2:1 “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi TUNAYE MWOMBEZI KWA BABA, Yesu Kristo mwenye haki”
Lakini ni vizuri kuzijua lugha za kiroho na namna ya kuzitafsiri, vinginevyo itatuwia vigumu sana kuielewa biblia na hata wakati mwingine kujikuta tunaabudu sanamu kwa kushindwa kuzipambanua lugha za kiroho,
Kwamfano kuna mahali Bwana YESU alisema Mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake (soma Yohana 6:53), sasa tukiuchukua huo mstari kama ulivyo na kwenda kutafuta mwili wa Bwana kama nyama, na Damu yake kama ilivyo na kuinywa, tutakuwa tumeshindwa kutafsiri vyema lugha ya biblia, na hivyo tutakuwa tumefanana na waganga na wachawi walao nyama na kunywa damu!.
Lakini kama tukiweza kuelewa maana ya mwili wake Bwana Yesu na damu yake kuwa ni ule mkate na kile kikombe, sawasawa na (Mathayo 26:26-27) tutakuwa tumeenda sawasawa na Neno la Mungu.
SASA KWA MSINGI HUU, TUTAKUWA TAYARI KUJIFUNZA NI KWA NAMNA GANI KRISTO ANATUOMBEA KWA BABA.
Katika hiko kitabu cha Warumi mlango wa 8:34 tuliposoma kuwa KRISTO ndiye anayetuombea, hebu turudi mistari kadhaa nyuma mpaka ule mstari wa 26, tuone jambo..
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA kuugua kusikoweza kutamkwa. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”
Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”
Angalia hapa; Katika ule mstari wa 34 tumesoma kuwa ni BWANA YESU ndiye anayetuombea, lakini tena katika mstari wa 26 ndani ya sura hiyo hiyo, tunasoma kuwa ni ROHO MTAKATIFU ndiye anayetuombea.. Sasa swali ni yupi kati ya hawa wawili anayetuombea kwa Baba?… ni Roho Mtakatifu au ni Bwana YESU??.
Sasa jibu la swali hili ni rahisi sana na ndio tunaelekea katika kiini cha mada hii.
Jibu la swali hili tunalipata katika kitabu kile cha 2Wakorintho 3:17, sikiliza Neno la Mungu linavyosema…
2Wakorintho 3:17 “Basi Bwana ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru”.
Hapo anasema lakini “Bwana” (yaani YESU)..ndiye “Roho”(yaani Roho Mtakatifu).. kumbuka hapo Roho imeanza kwa herufi kubwa kuwakilisha Roho Mtakatifu. (Popote pale Roho inapoanza kwa herufi kubwa inamaanisha Roho wa Mungu).
Hivyo kulingana na hayo maandiko, ni sahihi kabisa kusema BWANA YESU ndiye ROHO MTAKATIFU, na Roho mtakatifu ndiye Bwana YESU.. Kwahiyo mahali popote asemapo Roho Mtakatifu ni Bwana YESU ndiye kasema..
Ndio maana utaona katika kile kitabu cha Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3 katika jumbe za yale makanisa saba, utaona ujumbe unaanza YESU ANASEMA, na unamaliza ROHO AYAAMBIA MAKANISA, ikiwa na maana kuwa Roho ndiye huyo huyo Bwana.
Vile vile Roho Mtakatifu akiomba ni Bwana ameomba.
Sasa swali la mwisho ambalo litahitimisha Mada hii, ni je!, Kama Bwana YESU ndiye Roho Mtakatifu, je huyo Roho Mtakatifu anatuombeaje sawasawa na huo mstari wa 26?
Roho Mtakatifu (ambaye ndiye Bwana mwenyewe) hatuombei kama sisi tunavyoombeana!.. La! Yeye anaomba ndani yetu.. Maana yake tuombapo sisi, basi yale maombi yetu anayachukua na kuyapeleka mbele za Baba katika lugha nzuri Zaidi, katika maelezo mazuri Zaidi.
Lakini si kwamba tumelala au tunacheza, au tunafanya mambo yetu mengine basi wakati huo huo yeye kule anatuombea, hapana! Hiyo si tafsiri yake kabia..
Kwa urefu jinsi Roho Mtakatifu anavyotuombea fungua hapa utapata kuelewa vizuri sana >>ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba jinsi Bwana YESU anavyotuombea ni kwajinsi ya Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu anachukua yale maombi yetu na kuyapeleka kwa Baba kwa lugha kamilifu Zaidi.. Hivyo kamwe usiwaze kuwa Bwana YESU yupo mbinguni mbele za Baba, akisali kwaajili yetu, bali ni kwa njia ya Roho wake mtakatifu ndani yetu, ndipo anapotuombea.
Kwanini tunajifunza haya?.
Ni kwasababu zipo Imani zilizoanzishwa na ibilisi mwenyewe zisemazo kuwa “hatuna haja ya kuomba, kwasababu Bwana YESU yupo mbinguni anatuombea usiku na mchana”…
Kamwe usidanganyike na hayo mafundisho kwani ni mafundisho ya Adui, ibilisi… Tusipoomba na Roho Mtakatifu hawezi kuomba, na Roho Mtakatifu asipoomba ni Bwana hajaomba.. Lakini tuombapo, Roho Mtakatifu ni kipaza sauti chetu kwa Baba..kwahiyo maombi ni lazima… (Pitia tafadhali somo la jinsi Roho Mtakatifu anavyotuombea).
Na mwisho kabisa, hakuna mtakatifu yoyote aliyekufa au aliyenyakuliwa anayetuombea… NI YESU TU PEKE YAKE, kwa NJIA YA ROHO WAKE MTAKATIFU, ndiye anayetuombea.. Hivyo Mtakatifu Mariamu, hawezi kutuombea, wala Eliya, wala Musa, wala Henoko, wala mtu mwingine yoyote aliye hai wala aliyekufa…(Hawana na hatuna hivyo vigezo).
Kwahiyo lililo kubwa na la msingi sana, ni kutafuta Roho Mtakatifu kwasababu kwa kupitia huyo ndio maombi yetu yatafika na kukubaliwa, na tena mtu asiyekuwa na Roho Mtakatifu huyo si wake kulingana na biblia (Warumi 8:9)
Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)
NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.
Roho Mtakatifu ni nani?.
Kwanza ni vema kufahamu uzazi wa mpango ni nini na kama ni dhambi au la!.
Uzazi wa mpango ni kuzaa kwa mpangilio ulioutaka wewe, kwamfano ukijiwekea malengo ya kuzaa watoto 30, huo ni uzazi wa mpango maadamu yalikuwa ni malengo yako, au ukijiwekea malengo ya kuzaa mmoja maisha yako yote huo pia ni uzazi wa mpango. Kinyume chake uzao usio wa mpango, ni ule wa kutojali idadi ya watoto utakaouzaa, wala kutojali muda wa uzaaji wako.
Ukweli ni kwamba uzazi wa mpango si dhambi. Kwasababu gani?
Licha ya kwamba Mungu ameweka maagizo yake kupitia biblia takatifu, lakini pia, ameweka hekima yake kupitia mambo ya asili (1Wakorintho 11:14, Warumi 1:20), Hivyo mambo ya asili yanatufundisha pia agizo la Mungu .
Si kila wakati mama atashika ujauzito, bali upo wakati wa hatari na wakati usio wa hatari. Sasa kwa hekima huo tayari ni utaratibu Mungu kamwekea mtu, atambue majira yake, achukue tahadhari. Umeona? Kwa namna nyingine Mungu anasema, kuna majira utapata mtoto, na kuna majira hutapata mtoto. Hivyo uamuzi ni wako, ukitaka kuzingatia mazunguko huo, ni wewe, usipojali pia ni wewe.
Sasa mtu ambaye anayechagua kuzingatia mzunguko huo wa asili wa Mungu, huyo tayari yupo katika uzazi wa mpango. Na pia ni agizo la Mungu tuwe na uwezo wa kuwatunza wale wa nyumbani kwetu (1Timotheo 5:8)
Lakini je! Vipi ambao wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango je na wao wapo sawa?
Tukisema njia za kisasa, ni kama zile za kutumia vidonge, kutumia sindano, kutumia vizuizi kama mipira (kwa wanaume na wanawake), kuweka kitanzi, na kuweka vipandiki/vijiti. Zote hizi ni njia za kisasa.
Hapa ni lazima tufahamu pia lengo ni nini?. Bila shaka lengo ni lile lile moja la uzazi wa mpango kwa wanandoa, na si vinginevyo. Lakini mwanadamu ameamua kutumia njia zake za kisasa, ili kufanikisha hilo?
Je! Ni kosa?
Ili kujibu swali hilo, tufikirie pia mambo mengine ya kisasa, leo hii tuna vitu vingi vya kisasa vimebuniwa na wanadamu, kwamfano kuna kuku wa kienyeji lakini pia wapo wa kisasa, kuna mchicha wa kienyeji lakini pia ipo ya kisasa, kuna matunda ya kienyeji lakini pia yapo ya kisasa. Je! Ni dhambi kutumia vitu hivyo, kwasababu vimebuniwa na mwanadamu?
Jibu ni hapana.
Lakini vinaweza kuwa na madhara yake, kwasababu mwanadamu hawezi kuumba kitu kiukamilifu. Ndio maana asilimia kubwa ya vitu hivi vya kisasa, huwa si vizuri kiafya. Vivyo hivyo katika matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Yaweza isiwe dhambi kwako kutumia. Lakini madhara ya kiafya, pia waweza kukumbana nayo. Wengine hupata shida ya vizazi, wengine ugumba kabisa kulingana na njia iliyotumika, lakini wengine hawapatwi na madhara. Hivyo amani ya Kristo iamue ndani yako.
Lakini ile y asili ni bora zaidi. Ukitumia njia ya kalenda, ni salama lakini pia Mungu ametubunia hiyo, ukijizoesha kuifuatilia utaweza tu kupangilia uzazi wako.
Lakini fahamu pia uzazi wa mpango, maadamu amani ya Kristo imeamua moyoni mwako, si dhambi mbele za Mungu.
Je ni halali kwa mkristo kufanya biashara ya Forex?
JE! KUBET NI DHAMBI?
Je Kutoa Mimba ni dhambi?
Mungu anaweza kuahidi, lakini kama hujui kanuni za kusubiria ahadi za Mungu unaweza usipokee lolote. Kila mmoja wetu amestahili kupokea lolote analo mwomba Mungu endapo ameomba sawasawa na mapenzi yake (yaani sio kwa matumizi mabaya). Yawezekana wewe umeomba Bwana akupe kazi, akupe mke/mume bora, akuponye ugonjwa wako, aikuze karama yako n.k.
Sasa mahitaji kama hayo na mengine yoyote. Mungu alisema kwenye Neno lake, atatupatia (1Yohana 5:14). Na hivyo inakuwa kwake ni ahadi ambayo lazima aitimize. Kwahiyo wewe unachopaswa kufanya ni kusubiri tu. Kuzingojea hizo ahadi za Mungu kwasababu ni lazima zije. Jifunze tu kungojea.
Maombolezo 3:25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. 26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu
Sasa unazingojea katika mazingira gani?. Hapo ndipo unapopaswa ujue.
Embu tuangalie kwa mtu mmoja ambaye aliahidiwa jambo na Mungu. Na hivyo alikuwa katika mazingira gani, mpaka akalipokea. Mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simeoni.
Tusome.
Luka 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, 31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
Luka 2:25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
Wengi wetu tukimtafakari Simeoni, tunatengeneza picha ya mtu Fulani, mzee aliyekuwa anamngoja Mungu tangu ujana wake hadi uzee atimiziwe ahadi yake. Lakini biblia haituelezi katika picha hiyo, inatueleza alikuwa ni “mtu mwenye haki mcha Mungu”. Na tazamio lake lilikuwa ni kuona mkombozi anakuja duniani, Mungu akasikia kiu yake, ndipo akamwambia utamwona.
Ni jambo gani unapaswa ujue?
Kungojea ahadi za Mungu sio tu kusema ‘Bwana naomba hiki au kile’. Hapana, ni pamoja na kutembea katika haki na kumcha Mungu. Simoni alikuwa hivyo, hakuwa mtu anayetarajia jibu lake, huku anaendelea na udunia kama wengine, huku anaendelea na anasa kama wanadamu wengine, huku anaendelea na uzinzi kama wapagani.
Alidumu muda wote, kuyalea maono aliyoonyeshwa na Mungu, katika hofu ya Kristo. Ndipo wakati ulipofika akaona alichokuwa akikitarajia.
Palilia maono yako uliyomwomba Mungu akutimizie/ au aliyokuonyesha, kwa kutembea ndani ya Kristo. Mche Mungu, kuwa mtu wa rohoni uliyejazwa Roho kama Simoni, tembea katika usafi wa Kristo, kataa udunia, na maisha ya kipagani, kuwa mwombaji.
Ni hakika hilo ulilomwomba Bwana utaliona tu, baada ya wakati Fulani, haijalishi ni gumu/zito kiasi gani, au limepitiliza muda kiasi gani. Utalipokea tu, katika ubora ambao hukuutegemea.
PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.
ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.
KANUNI JUU YA KANUNI.
Jibu: Miti ya Misunobari tunaisoma katika kitabu cha Isaya 55:13 na sehemu nyingine baadhi katika biblia.
Isaya 55:13 “Badala ya michongoma utamea MSUNOBARI, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali”
“Misonubari” ni jamii moja na miti ya “Mierezi”. Tofauti ya Msonubari na mwerezi ni kwamba Misonubari yenyewe haiwi mirefu kama mierezi, na pia ina matawi myembamba kuliko mierezi, lakini kwa sehemu kubwa inafanana kimatumizi na mierezi, ndio maana sehemu karibia zote panapotajwa miti ya Mierezi basi na Misunobari pia inatajwa..
Zekaria 11:2 “Piga yowe, MSUNOBARI, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia”.
Soma pia 2Wafalme 19:23, Isaya 14:8, Isaya 37:24, Ezekieli 27:5 na Ezekieli 31:8.
Miti ya Misonubari na Mierezi ilitumika katika ujenzi wa nyumba za thamani na ilipatikana sana katika nchi ya Lebanoni..
Sasa kwa urefu kuhusu miti ya Mierezi na matumizi yake fungua hapa >>>Mwerezi ni nini?
NI LAZIMA KUISHIKILIA IMANI MPAKA MWISHO.
Sala ya baraka (Hesabu 6:24-26).
Fahamu maana ya Mhubiri 10:9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;
FAHAMU SEHEMU NNE (4) APANDWAPO MWAMINI.
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.
Usingizi unaozidi unachelewesha utekelezaji wa majukumu ya muhimu. Kwamfano Mwanafunzi anayelala kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa shule, vilevile mfanyakazi alalaye kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa kazini, mfanya biashara anayelala kupita kiasi ni lazima atachelewa kuanza biashara yake.
Upo usemi usemao “biashara ni asubuhi” maana yake kwa mtu anayefanya biashara labda ya kuuza duka, asubuhi ndio wakati wa kufungua bishara maana watu wengi wanawahi kutafuta bidhaa asubuhi Zaidi ya mchana, hivyo alalapo sana hatapata zile faida za asubuhi, na hivyo yupo hatarini kufilisika.
Atapanga kweli kuwahi kuamka mapema kesho, lakini ifikapo asubuhi kitanda kinakuwa na nguvu kuliko maamuzi yake, atajiongezea muda wa kulala, na mwisho wa siku atashtukia kumeshapambazuka na jua linawaka..na hayo ni matokeo ya kusema “bado kulala kidogo”.
Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? 10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?
10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Sasa biblia ni kitabu kilichojaa hekima ya kumwongoza mtu hata katika maisha ya kawaida Zaidi ya yale ya rohoni…. ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mema yahusuyo kanuni za kimaisha na kitabu cha Mithali kimejaa mafunzo hayo.
Hivyo biblia inatufundisha wakristo tuwe na kiasi katika kulala, kwani usingizi unaozidi una matokeo mabaya.. Si kila changamoto inasababishwa na “wachawi”….. nyingine zinatokana na tabia zetu wenyewe.., na hivyo biblia inatufundisha jinsi ya kuepukana nazo, kwamba ni kubadili tu mienendo.
Maana yake ni kwamba, tukitaka kuepukana na “umasikini” kanuni sio tu “kufunga na kuomba” bali pia ni KUTOUPENDA USINGIZI!. Ukifunga na kuomba na huku unaendekeza usingizi kupita kiasi hakuna matokeo yoyote utakayoyaona.
Maana yake kama ni mfanyakazi basi usiwe mtu wa kupenda kulala mno..Ni kweli hatuwezi kuacha kulala kabisa, lakini kusizidi mipaka, kwani usingizi uliozidi ni zao la ibilisi.
Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”
Lakini pia kiroho hatupaswi kulala kabisa, kwani usingizi wa kiroho matokeo yake ni mabaya kuliko ule wa kimwili.. Matendo yote ya giza mtu ayafanyayo ni matokeo ya usingizi wa kiroho..
Mtu anayefanya uzinzi, uasherati, anayelewa pombe, anayeiba, anayetukana, anayesengenya…huyo macho yake yamefumba kwa usingizi mzito.
Je na wewe umo miongoni mwa waliolala kiroho? Basi huu si wakati wa kuendelea kulala, bali wa kuamka na kuyaacha matendo ya giza.
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
12 USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”
Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.
Bwana atubariki.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
NYOTA YA ASUBUHI.
Nini maana ya usijiongezee hekima mno? (Mhubiri 7:16b)
Masomo maalumu kwa wahubiri.
Isaya 29:16 “NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?”
Kama Mtumishi/Mhubiri jihadhari na MAPINDUZI yasiyo na msingi!.
USIIPINDUE INJILI YA KRISTO KWASABABU YA TAMAA YA FEDHA.
Unapoanza kuwadanganya watu wa wenye nia ya kumtafuta Mungu, ili tu upate fedha kutoka kwao!.. unapoanza kuwatumainisha watu wa Mungu mambo ya uongo ili tu uwatoe fedha!.. Hiyo ni ishara mbaya na hatari kubwa sana kwako!. Bwana ataenda kukupindua nawe pia!.
Tito 1:11 “Hao WANAPINDUA watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu”.
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kufanya biashara katika nyumba ya Mungu (ambayo ni wewe mwili wako sawasawa na 1Wakorintho 3:16) kwa kuanza kufanya uasherati na uzinzi na ukahaba fahamu kuwa Bwana naye atakupindua (Soma 1Wakoritho 6:19).
Ukilipindua Neno la Mungu kwa kuiharibu nyumba yake (kama jengo) kwa kuanza kufanya biashara ndani yake na kufanya yasiyofaa Bwana YESU atazipindua meza zako (soma Mathayo 21:12)
Ukilipindua Neno la Mungu juu ya utakatifu wa mwilini na rohoni (sawasawa na 1Wathesalonike 5:23) na kuanza kufundisha/ kuhubiri kuwa Mungu haangalii mwili bali anaangalia roho tu peke yake ni kupindua maandiko ambako matokeo yake ni Mungu kuyapindua maneno yako na wewe kwa ujumla.
Mithali 22: 12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali HUYAPINDUA MANENO YA MTU HAINI”
Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kuhubiri kuwa YESU KRISTO bado sana arudi, au kwamba hakuna mwisho wa dunia, huko ni kupindua mambo ambako matokeo yake ni mabaya kama ya Fileto na Himenayo.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, 18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.
Kama Mhubiri Ni heri KUPINDUA ulimwengu kwa mambo ya kweli ya INJILI kama walivyofanya Mitume wa kanisa la kwanza kuliko kuigeuza/kuipindua injili kwa faida zetu wenyewe.
Matendo 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA huku nako”
Siku ya Mapinduzi makuu inakuja, ambapo Bwana ataipindua dunia yote kama alivyoipindua miji ya Sodoma na Gomora (soma Kumbukumbu 29:23) na kipindi cha gharika ya Nuhu (Soma Ayubu 12:15).
Ezekieli 21:27 “NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa”
Hegai 2:22 “nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake”.
Usipindue Mambo yaliyonyooka, bali pindua yale yaliyopotoka.
VIJANA NA MAHUSIANO.
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
IMANI “MAMA” NI IPI?
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
SWALI: Nini tafsiri ya Mithali 27:22
Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.
JIBU: Kama tunavyojua mtwangio na kinu ni vyombo vinavyotumika kuponda-ponda nafaka ngumu kuwa unga, au wakati mwingine mimea migumu kuwa milaini. Mfano wa kisamvu ambacho ili kiweze kulika, majani yake huwezi yapika hivyo hivyo huna budi kuyatwanga twanga kidogo, yalainike ndipo upike ule.
Na vivyo hivyo, nafaka kama mahindi, au ngano, ili viweze kulika zamani vilikuwa vinatwangwa kwenye vinu ,tofauti na sasa vinasagwa na mashine.
Sasa katika mithali hiyo, Mungu anatoa, asili ya mtu mpumbavu, kwamba hata akitwangwa, mfano wa ngano kinuni, huo upumbavu hauwezi kumtoka. Yaani njia gani ya lazima itumike bado hawezi kuacha upumbavu.
Sasa ni vizuri kufahamu, mpumbavu ni nani?
Mpumbavu kibiblia sio mtu Fulani mjinga tu hapana, bali ni Neno pana, linalolenga kuanzia
mtu anayesema hakuna Mungu (zaburi 14:1)
Mtu mgomvi (Mithali 9:13),
Mtenda maovu (Mithali 10:23)
Anayejiona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)
Mwenye kiburi (Mithali 14:3)
Mwenye dharau (Mithali 15:5)
Yaani kwa kifupi mpumbavu ni mtu ambaye hana Mungu ndani yake. Kwasababu dhambi ndani ya mtu ndio chanzo cha Upumbavu wote.
Sasa mtu kama huyu, hakuna kitu kinachoweza kuutoa upumbavu huo ndani yake, waweza kusema elimu, lakini ni watu wangapi wameelimika, lakini walevi, watukanaji, mashoga. Hata atwangwe vipi kinuni hawezi lainika, ikiwa hajui ni kipi sahihi kinachoweza kutoa upumbavu huo.
Kumfunga mwizi, hakumfanyi wizi au tamaa ya kuiba itoke ndani yake, mara ngapi unasikia mwizi katoka jela, karudia wizi wake, au ni kiongozi ambaye anaaminiwa awe kielelezo cha kupambana na ufisadi, lakini yeye ndio anakamatwa katika ufisadi, au teja ametolewa hospitalini karudia, tena madawa la kulevya. Ndio maana jamii ijapojaribu kudhibiti vitendo viovu, bado haviishi, bali hubadilika tu maumbile. Kwasababu mpumbavu hata atwangwe kinuni, hawezi geuka, hakuna nidhamu inayoweza mbadilisha. Huwezi acha mwenendo wake mbovu kwa semina za kijamii, au kuwekewa sheria
Je! Ni kipi kinachoweza kumgeuza?
Ni Yesu Kristo tu. Yeye ndiye aliyetiwa mafuta, na Mungu kuwaokoa watu wa Mungu na kuwafungua. Amwaminiye na kudhamiria moyoni mwake kumfuata, basi atageuzwa moja kwa moja na kuwa mtu mwingine, huo ni uhakika.
Alisema.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Ni ahadi yake kuwa Ukimwamini jambo la kwanza ni kukusamehe dhambi zako, kwasababu ndio jambo lililomfanya aende msalabani kwa ajili yako miaka elfu mbili iliyopita,. Unakuwa huhesabiwi dhambi tena, unahesabiwa haki bure kwa neema yake. Lakini sambamba na hilo anakupa UWEZO wa kuwa kama yeye kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu atakayemwachia ndani yako, pindi tu unapoamini.
Na baada ya hapo utashangaa tu unavyoanza kubadilika moyoni mwako.
Zingatia tu toba ya kweli, pamoja na ubatizo sahihi (kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo). Na kumtii yeye.
Upumbavu utakutoka.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!
Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?
SWALI: Nini maana ya Mithali 26:2
Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
JIBU: Mungu anafananisha laana isiyo na sababu na ndege wanaotanga-tanga angani.
Kama tunavyojua ndege hawa aina ya shomoro na mbayuwayu, kila siku tunawaona wanaruka angani, kila siku tunawaona wapo hari-hari, wanaonekana kama wapo buzy, lakini katika kazi zao zote, na juhudi zao zote, na mikakati yao yote, kamwe huwezi ona yanaleta madhara yoyote kwa mwanadamu. Hata kama utawaharibia viota vyao, hata kama watakauwa na hasira na wewe, huwezi ona wanamshambulia mwanadamu, kwasababu uwezo huo hawana. Huwezi wafikiria na kila wanapokuona wanakimbia. Wewe mwenyewe ukiwaona huwezi kuwaogopa, tofauti na ukimwona nyoka, utajidhatiti asikuume. Lakini ndege huvai ‘chapeo’ kichwani kujilinda naye asikuume, kwasababu hana madhara.
Ndivyo Mungu anavyotufundisha, laana zisizo na sababu, haziwezi kukupata ni kama ndege tu angani, zitapita, na kuendelea na shughuli zake, kamwe haziwezi kukupata ikiwa wewe ni mtakatifu, Hii ni kutufundisha kuwa hatupaswi kuwa waoga wa maneno ya watu (laana) ambayo hayana sababu.
Ukiona laana imekupata basi ujue kulikuwa na sababu nyuma yake, (lakini sio tu maneno matupu mtu anayoyatoa), mfano wa laana hizi ni ile ya Elisha aliyowalaani wale vijana 42, walioraruliwa na dubu. Kwasababu walimdhihaki. (2Wafalme 2:22-25)
Lakini mfano wa laana zisizo na sababu, ni ile Goliathi aliyomlaani Daudi kwa miungu yake, ambayo ilikuwa ni kazi bure..
1Samweli 17:42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake
Ni mfano mwingine ni ile Balaamu mchawi alivyojaribu kuwalaani Israeli ikashindakana, kwasababu huwezi laani vilivyobarikiwa. (Hesabu 23)
Hata leo, ikiwa wewe umeokoka, hupaswi kuogopa, maneno yoyote iwe ya waganga au wanadamu. Kwasababu wewe tayari ni mbarikiwa. Ni ajabu sana kuona mkristo, analia na kutetemeka, eti! Mchawi kamwambia mwaka huu hautaisha atakuwa watoto wake wote watakuwa wamekufa!!. Mzee wa mila kamwambia atapata ajali kwasababu hakutambika kijijini mwaka huu.
Mwingine anawaza, mzazi kamwambia hatafanikiwa kwasababu kaamua kuokoka. Haa! Unaogopa nini hapo?. Hizo ni laana zisizo na sababu. Ishi kwa amani zione tu kama ndege wa angani ambao hukai kuwafikiria kama watakushambulia siku moja.
Ukiokolewa na Kristo umebarikiwa, wewe sio wa kunenewa maneno ovyo ovyo tu, na yakatokea. Wewe ni uzao wa kifalme usiotetemeshwa, ngome imara isiyoangushwa. Mwamba mgumu usiogharikishwa. Yatambue mamlaka na nguvu ulizopewa ndani ya Kristo. Usiogope!
Elewa maana ya Mithali 26:2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake,
Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,
Maana yake nini, Mwe na hofu wala msitende dhambi? (Zaburi 4:4)
NUHU WA SASA.