Je unajua kwamba kuikaribia dhambi ni “DHAMBI”, Hata tu kabla ya kuifanya?.
Mungu hakumpa tu Adamu maagizo ya kutokula yale matunda ya mti wa katikati…bali pia alimwambia “Asiyaguse yale matunda”..asije akafa. Wengi wetu tunaona tu habari ya “kula” kama kosa, lakini hatujui kuwa Mungu aliwaagiza kwamba hata kuyagusa wasiyaguse, (maana yake wakae mbali nayo).
Mwanzo 3:2 “Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala MSIYAGUSE, msije mkafa”.
Kumbe hata wangeyagusa tu yale matunda bila hata ya kuyala, bado Wangekufa!!.
Hii ni hatari sana..na inatupa fundisho kubwa sana..
Kwanini Mungu akataze wasiyaguse?..Je kuna ubaya wowote katika kuyagusa???… Jibu ni ndio!… kwasababu chanzo cha dhambi ya kula tunda ni kulishika lile tunda kwanza, (Hawa asingeweza kulipeleka mdomoni kabla ya kulishika) kabla ya kulichunguza chunguza kwanza, kabla ya kulidadisi dadisi, ndipo akaangukia katika ushawishi wa kulila.
Hivyo Mungu aliona chanzo cha dhambi kuwa ni “kushika” ndipo akatoa maagizo kwamba WASIYAGUSE!! Wasije wakafa… lakini wenyewe (Waligusa, na tena wakala) Hivyo ikawa ni makosa mawili yaliyozaa Mauti kamilifu.
Na hata leo Bwana anatuonya tukae mbali na dhambi, tusiikaribie kabisa dhambi, tusiiguse dhambi licha ya kuitenda!!..
Tukae mbali na Wizi kama ya wizi wenyewe kutendeka,…tukae mbali na Ulevi kabla ya ulevi wenyewe kutendeka… tukae mbali na Utukanaji, Uadui, Kiburi, Uasherati, kabla ya kufanya mambo hayo (Wagalatia 5:19-20)… Tusizikaribie kabisa hizi dhambi!!.. tukae nazo mbali maili nyingi sana, kwasababu kitendo cha kuzikaribia tu tayari ni kosa..
leo hii utaona mtu anasema hazini, wala hafanyi uasherati lakini katika simu yake kumejaa picha zinazochochea mambo hayo, kumejaa miziki inayochochoea mambo hayo, kumejaa filamu zi kidunia zenye maudhui hayo ya kiasherati, simu yake imejaa magroup ya mizaha, na uhuni, unaochochea mambo hayo…pasipo kujua kuwa anafanya makosa makubwa kuisogelea dhambi kwa namna hiyo..
Neno la Mungu linasema kwamba tuikimbie zinaa, sio tuishi nayo, au tuikemee!..bali tuikimbie (Soma 1Wakorintho 6:18 )...kama vile Yusufu alivyoikimbia mbele ya mke wa Potifa, na sisi tunapaswa tuikimbia hivyo hivyo Yusufu hata hakukubali kuzungumza na Yule mwanamke..
Lakini ni kinyume chake katika siku hizi za mwisho, utaona binti anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno na mwanaume anayemtaka, kijana anayekiri kumpokea Yesu anapiga maneno ya kidunia na binti anayemtamani, na hata kufanya naye mizaha..Hii ni hatari kubwa!, kumbuka ushawishi wa Hawa kula tunda haukuanzia mdomoni bali mkononi!..baada ya kulishika ndipo ushawishi ukamwingia..
Na sisi tukijishikamanisha na dhambi, basi ni lazima tutazitenda tu!, haijalishi itachukua muda gani ni lazima tutazitenda tu!…Hauwezi kusema umeacha utukanaji, lakini kila kukicha kampani zako ni za watu wanaotukana…ni lazima tu na wewe utatukana, haijalishi itakuchukua muda gani kudumu bila kutukana lakini mwisho wa siku utaishia kurudia matukano tu.
Hauwezi kukaa unasikiliza usengenyaji na wewe usiwe msengenyaji..ni suala la muda tu!, utajikuta na wewe upo kama wao.. Kumbuka Adamu na Hawa waliambiwa “wasiukaribie kabisa ule mti, na hata kuugusa”.. Vile vile na sisi leo hii tunapaswa tusiikaribie miti ya dhambi…wala tusiguse mashina yake wala matawi yake.. maana kugusa ndio chanzo cha kula..
Bwana atusaidie na kutuwezesha katika yote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MUME / MKE BORA KUTOKA KWA BWANA UTAMWONA UKIWA KATIKA MAZINGIRA GANI?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
Tofauti na Kalenda ya Kirumi ambayo ndiyo tunayoitumia sasa yenye miezi 12, Kalenda ya kiyahudi yenyewe inakuwa na miezi 13 kwa mara saba kila baada ya miaka 19. (Yaani katika kipindi cha miaka 19, miaka 7 inakuwa na miezi 13, na miaka 12 iliyosalia inakuwa na miezi 12 kama kawaida), Na miaka yenye miezi 13 ni inakuwa ni mwaka wa 3, 6,8,11,14, 17 na 19 na mzunguko wa miaka 19, unapoisha na unapoanza mzunguko mwingine, basi mgawanyo wa miezi unakuwa ni huo huo, wa baadhi ya miaka kuwa na miezi 13 na mingine 12.
Sasa mwezi wa 13, unaoongezeka juu ya miezi 12 ya kiyahudi ni mwezi ujulikanao kama Adari II, Sasa kabla ya kwenda kuutazama huu mwezi wa 13 wa Adari, hebu tuitazame miezi 12, na rejea zao katika biblia.
Mwezi wa 1: Abibu au Nisani.
Mwezi wa Abibu au Nisani ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiyahudi, mwezi huu unaanza katika mwezi Machi katikati na kuisha mwezi Aprili katikati katika kalenda yetu ya kirumi tunayoitumia..
Mwezi wa Abibu ndio mwezi ambao wana wa Israeli walitoka Misri..
kutoka 13:3 Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa Bwana aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
4 Ninyi mwatoka leo katika MWEZI WA ABIBU.
Na wakati ambapo Hamani ananyanyuka kutaka kuwaangamiza Israeli yote katika ufalme wote wa Ahasuero, tunasoma wazo hili lilimjia katika Mwezi wa Nisani/ Abibu..
Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio MWEZI WA NISANI, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.
Na pia tunausoma huu mwezi ukitajwa wakati Nehemia alipoingiwa na wazo la kwenda kuujenga Yerusalemu..
Nehemia 2:1 “Ikawa katika MWEZI WA NISANI, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote.”.
Mwezi wa 2: Zivu au Ayari
Mwezi huu unaangukia kati ya mwezi Aprili na mwezi May kwa kalenda yetu tunayoitumia, na ni mwezi wa pili katika kalenda ya kiyahudi.
Mwezi huu ndio mwezi ambao Mfalme Sulemani alianza kulijenga Hekalu la Mungu katika Yerusalemu..
1Wafalme 6:1 “Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika MWEZI WA ZIVU, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana.
2 Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini”.
Mwezi wa 3: Siwani
Huu ni mwezi wa tatu kwa kalenda ya kiyahudi, lakini kwa kalenda yetu ni mwezi unaoangukia kati ya mwezi Mei na mwezi Juni.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Mfalme Ahasuero, enzi za malkia Esta alitoa ruksa kwa wayahudi kujilipizia kisasi juu ya adui zao.
Esta 8:9 “Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio MWEZI WA SIWANI; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao”.
Mwezi wa 4: Tamuzi
Huu ni mwezi wa Nne katika kalenda ya kiyahudi, lakini kwetu sisi unaanguka katika ya mwezi Juni na mwezi Juni na mwezi Julai.
Mwezi huu katika bibli unaonekana kutajwa mara moja tu katika kitabu cha Ezekieli.
Ezekieli 8:14 “Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia TAMUZI”.
Mwezi huu wa nne umetajwa sehemu nyingine kama kwa namba na si kwa jina (Soma Yeremia 39:1-2, na Yeremia 52:6-7).
Mwezi wa 5: Avu
Huu ni mwezi wa tano kwa wayahudi na kwetu sisi unaangukia kati ya mwezi wa Julai na Mwezi Agosti.. Mwezi huu katika biblia haijatajwa kwa jina bali kwa namba..
Kwamfano tunasoma Ezra aliwasili Yerusalemu katika mwezi wa 5
Ezra 7:8 “Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme”
Na pia katika (2 Wafalme 25:8-10, Yeremia 1:3 na Yeremia 52:12-30)
Mwezi wa 6: Eluli
Huu ni mwezi wa 6 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi wa Agosti na Septemba katika kalenda yetu.
Katika biblia mwezi huu ndio mwezi ambao Nehemia alimaliza kati ya kuukarabati ukuta Yerusalemu..
Nehemia 6:15 “Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa ELULI, katika muda wa siku hamsini na mbili”
Mwezi huu pia umetajwa kwa namba katika kitabu cha Hegai 1:14-15.
Mwezi wa 7: Ethanimu
Huu ni mwezi wa 7 kwa kalenda ya kiyahudi na kwa kalenda yetu unaangukia katika ya mwezi wa Septemba na Oktoba.
Hekalu la Sulemani liliwekwa wakfu katika mwezi huu wa Ethanimu
1Wafalme 8:1 “Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.
2 Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika MWEZI WA ETHANIMU, ndio mwezi wa saba. 3 Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku”
Unaweza kuusoma pia mwezi huu katika..(1Wafalme 8:2, Walawi 23:24, Nehemia 8:13-15).
Mwezi wa 8: Buli.
Mwezi huu ni mwezi wa 8 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi Octoba na mwezi mwezi Novemba katika kalenda yetu ya kirumi.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Sulemani alimaliza kuijenga nyumba ya Mungu (Hekalu).
1Wafalme 6:38 “Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika MWEZI WA BULI, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Unaweza kusoma pia habari za mwezi huu katika (1Wafalme 12:32-33, 1Nyakati 27:11).
Mwezi wa 9: Kisleu
Huu ni mwezi wa 9 kwa kalenda ya kiyahudi na unaangukia kati ya mwezi wa Novemba na Disemba katika kalenda yetu ya sasa ya kirumi.
Katika mwezi huu Nabii Zekaria alioneshwa maono juu ya Yuda na Israeli.
Zekaria 7:1 “Ikawa katika mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi wa kenda, yaani, KISLEU”
Mwezi wa 10: Tebethi
Huu ni mwezi wa 10 kwa Wayahudi na kwa kalenda ya kirumi unaangukia kati ya mwezi Disemba na January.
Katika biblia mwezi huu ndio mwezi ambao Esta aliingizwa katika nyumba ya kifalme..
Esta 2:16 “Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.
17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti”.
Na ndio mwezi ambao Nebukadreza aliuhusuru Yerusalemu (2Wafalme 25:1, Yeremia 52:4).
Mwezi wa 11: Shebati
Mwezi huu unaangukia kati ya mwezi Januari na mwezi Februari kwa kalenda ya kirumi na katika kalenda ya kiyahudi ni mwezi wa 11.
Katika mwezi huu ndio mwezi ambao Zekaria aliona maono tena juu ya Yerusalemu..
Zekaria 1:7 “Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani, mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, mwana wa Berekia, mwana wa Ido, nabii, kusema,
8 Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe”.
Mwezi wa 12: Adari I.
Huu ni mwezi wa 12 na wa mwisho kwa kalenda za kiyahudi, ambapo kwa kalenda ya kirumi unaangukia kati ya Mwezi Februari na mwezi Machi.
Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.
Kutokana na kuwepo na miaka mirefu na mifupi, Marabi wa kiyahudi katika karne ya 4, wakiongozwa na Rabbi Hillel II, waliongeza mwezi mmoja wa 13, katika kalenda ya kiyahudi ambao waliuita mwezi ADARI II (Adari wa pili).
Lengo la kuongeza mwezi huu ni ili kuziweka sikukuu za kiyahudi katika majira halisia, vinginevyo sikukuu za kiyahudi zingeangukia misimu ambayo sio, kwamfano sikukuu ya pasaka ambayo kwa wayahudi inaseherekewa katika mwezi wa March au April kwa kalenda yetu, kama kusingekuwepo huu mwezi wa 13, basi huenda miaka mingine sikukuu hii ingeangukia mwezi wa 8 kwa kalenda yetu, jambo ambalo lingekuwa halina uhalisia hata kidogo.
Lakini swali ni je!, sisi wakristo tunapaswa kuifuata kalenda ipi?, ya kiyahudi au hii inayotumika sasa ya kirumi?
Jibu ni kuwa Kalenda hazitusogezi karibu na Mungu wala hazipeleki mbali na Mungu, tukitumia kalenda ya kiyahudi, au ya kirumi au ya kichina au hata ya kichaga haituongezei chochote, kilicho cha muhimu ni kuishi kwa kuukomboa wakati kama biblia inavyosema katika..
Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”
Na tunaukomboa wakati kwa kufanya yale yanayotupasa kufanya, ikiwemo Kujitakasa, kufanya ibada, kuomba, kusoma Neno, kuifanya kazi ya Mungu kupitia karama iliyo ndani yako kabla ya ule mwisho kufika na mambo mengine yote yanayohusiana na hayo.
Bwana akubariki.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?
2Timotheo 1:6 “Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu”.
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.
Neno la Mungu linatufundisha kuzichochea KARAMA tulizopewa,.. Ikiwa na maana kuwa “Kuwa na karamaa pekee haitoshi kuifanya kazi ya Mungu vizuri”..bali inahitajika Karama iliyochochewa. Na anayeichochoea si Mungu, bali ni sisi ndio tunaoichochea.
Mtu anapomgeukia Kristo na kuokoka, tayari Mungu anakuwa ameiweka karama ndani yake, kama mbegu ndogo sana.. Lakini karama ile isipochochewa inaweza kufa ndani ya mtu, na hatimaye mtu yule akabaki kama mtu asiye na karama kabisa.
Hata wanaoshiriki michezo ya kidunia, ijapokuwa wanavyo vipaji vya michezo hiyo, lakini wasipovifanya mazoezi ya kutosha, haijalishi wana vipaji vikubwa kiasi gani, bado vipaji vyao hivyo vitakuwa si kitu. Na vipaji vina muda wake, mwanamichezo akifikia umri Fulani kama hajakitumia vizuri kipaji chake, basi kinapungua nguvu chenyewe, kwasababu tayari umri umeshaenda!.
Na karama za rohoni au vipaji vya rohoni ni ivyo hivyo.. visipochochewa vinakufa na visipotumika katika muda fulani, vinaisha thamani nguvu ndani yake..Ndio maana maandiko yanasema..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua”
Na pia inasema..
1Yohana 2:14 “…..Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”
Sasa maandiko yanasema Bwana alitoa wengine kuwa mitume, wengine manabii, wachungaji, waalimu, wainjilisti, karama za kuponya, matendo ya miujiza, karama za lugha, karama za masaidiano, imani, hekima, maarifa n.k (kasome Waefeso 4:11-12, 1Wakorintho 12). Lakini wengi hawajijui kama wanazo hizo karama.. kwasababu wanadhani zinaanza katika ukubwa wanaotugemea wao.
Wengi sana leo hii ni wainjilisti tangu siku ile wanapookoka, lakini kwasababu hawajijui kama wao ni wainjlisti, pale wanapojiona kuwa hawafanani na mwinjilisti mmoja maarufu, basi moto unazima ndani yao, pasipo kujua kama wanamzimisha roho, wengi ni waalimu tangu siku ile wanapookoka, lakini kwasababu hawajui namna ya kuzitumia karama zao na wanapoona wao si kama waalimu Fulani maarufu wanaowajua basi moto unazima ndani yao, wanabaki kusubiria muujiza siku moja wajikute wamekuwa wahubiri wenye uwezo wa kuhubiri kama watu Fulani maarufu.
Wengi wamepewa karama za kumwimbia Mungu, tangu siku walipookoka lakini kwasababu wanajiona kama sauti zao bado zinakwaruza, kwa kujilinganisha na wengine ambao tayari wanamwimbia Mungu kwa muda mrefu, basi wanatulia huku wakisubiri muujiza mwingine uwashukie utakaowafanya wawe kama hao wengine.
Kungoja huko ndiko kunakuua karama za watu wengi ndani yao.
Leo tutatazama njia 3, za namna ya kuzichochea karama zetu ili zifanye kazi katika viwango ambavyo Mungu amevikusudia.
1.KUJIFUNZA NENO.
Msingi wa karama zote ni Neno la Mungu, mtu aliyepungukiwa Neno la Mungu ndani yake, tayari karama yake inazima yenyewe tu ndani yake.. Kwanini Neno la Mungu??… kwasababu Neno la Mungu linatia hamasa, linatia moyo, linatupa sababu ya kuzitumia karama zetu, linafundisha jinsi ya kuzitumia kupitia mifano mbali mbali ya watumishi wa Mungu ndani ya biblia, na pia linatuonya madhara ya kutozitumia karama zetu. Hivyo Mtu mwenye Neno la Mungu la kutosha ni lazima tu karama yake itanyanyuka.
2. MAOMBI.
Hii ni njia ya pili ya kuchochoe karama zetu, Maandiko yanasesema tuombe bila kukoma (1Wathesalonike 5:17), Na kuomba kunajumuisha pia na kufunga, vitu hivi viwili vinaenda pamoja..tunapoomba Bwana anatuongezea uwezo na upako katika karama zetu.
Mathayo 17:21 “Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.”
3. MAZOEZI.
Hii ni njia ya tatu na ya muhimu sana, chochote kisichofanyiwa mazoezi hakiwezi kuwa bora.. hata karama isipofanyiwa mazoezi haiwezi kuwa bora, maana yake ni kwamba kama wewe una karama ya kuimba, kamwe usitegemee utakuwa bora, bila kuifanyia mazoezi karama hiyo, ni lazima uwe na vipindi vya kuinoa sauti yako, kutafuta na kujifunza jinsi ya kuzipangilia sauti kupitia waliokutangulia au waalimu, huku wewe mwenyewe ukifanya mazoezi ya kurudia rudia mara kadhaa… hivyo ndivyo karama yako itakavyoongezeka nguvu, lakini ukiiacha tu na kujiona tayari unajua kila kitu, basi hutaweza kupiga hatua..
Vile vile kama umepewa karama ya kiualimu, au kiinjiilisti..kama utaketi tu kusubiri kufundishwa, basi kamwe hutaweza kufundisha wengine..unapaswa utenge muda wa wewe kwenda kufundisha wengine, hata kama bado hujui vitu vingi,.. wewe kafundishe hivyo hivyo, Bwana atakufundisha huko mbele ya safari, makosa utakayoyafanya ndiyo yatakuwa darasa lako la kufanya vizuri katika matukio ya mbele..hivyo usiogope, nenda kahubiri..
Vile vile kama umepewa karama ya matendo ya imani, au karama za kuponya, usingoje ngoje.. nenda mahospitalini, nenda sehemu mbali mbali kafanye maombezi huku ukiwahubiria habari za njema za wokovu, usiogope wala kuvunjika moyo, unapoona umeombea watu 10, na hakuna aliyepona hata mmoja.. wewe endelea mbele, hizo ni hatua za awali, katika matukio yanayokuja Bwana atakutumia kwa maajabu mengi.
Na karama nyingine zote ni hivyo hivyo, ni lazima UZICHOCHEE!!..kama vile moto unavyochochewa.
Na ulingo mzuri wa kuiona karama yako ikifanya kazi ni ndani ya KANISA, yaani unapokuwa katika kusanyiko la Kristo ni kipindi kizuri cha kuiona karama yako kuliko unapokuwa nje ya kusanyiko, kwasababu Biblia inasema karama hizi lengo lake la kwanza ni kuujenga mwili wa Kristo, maana yake kulijenga kanisa (Waefeso 4:11).
Ichochee karama yako!
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nini tofauti kati ya Kipawa na Karama?
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
Kiburi ni nini?
Kulingana na biblia kiburi “ni hali ya mtu kujiinua kifikra, na kuamini kuwa hahitaji msaada wowote kutoka kwingine”. Hali hii inaambatana na kudhihirisha tabia nyingine ndogo ndogo kama majivuno, matukano, au kuwadharau wengine, au kuwa na ujasiri kupitiliza na hata kukufuru.
Viburi vimegawanyika katika sehemu mbili (2);KIBURI BINAFSI, na KIBURI CHA UZIMA.
KIBURI BINAFSI:
Kiburi binafsi ni kile kinachomfanya mtu aamini kuwa Mawazo yake, au maamuzi yake, au msimamo wake ni thabiti na hauwezi kubadilishwa na yeyote. Mtu mwenye kiburi binafsi hata aambiwe ukweli kiasi gani, au athibitishiwe jambo kiasi gani bado huwa habadiliki. Tayari anachokiamini, au alichokiamua amekiamua!. Mtu mwenye aina hii ya kiburi anakuwa pia ni mbishi na mtu wa mashindano, na anakuwa anajiona yeye ni bora kuliko wengine wote..
Mithali 13:10 “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana”.
Kiburi binafsi kipo kwa Wakristo na kwa wasio waKristo..
Kwa wakristo ni pale ambapo mtu hataki kuambiwa jambo wala kuelekezwa ndani ya kanisa…yeye mawazo yake ndio bora siku zote, au njia zake ndio bora, na zaidi ya yote anakuwa anapenda kuwa juu ya wote, na anawadharau wengine wote…
WaKristo wenye kiburi cha namna hii Bwana amesema anapingana nao…
1Petro 5: 5 “..ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa SABABU MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, lakini huwapa wanyenyekevu neema”.
Mithali 29:23 “Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa”.
Kwa wasio wakristo ni pale ambapo mtu hashauriwi na yeyote, juu ya jambo lolote, hata aambiwe vipi anakuwa yupo vile vile, yeye ni wa kuelekeza tu na sio wa kuelekezwa.
KIBURI CHA UZIMA:
Kiburi cha uzima ni kile kinachozungumziwa katika.. 1 Yohana 2:16
“Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na KIBURI CHA UZIMA, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.”
Kiburi cha Uzima ni kiburi kinachompata mtu kutokana na Vitu alivyonavyo, au anavyotegemea kuwa navyo..
Watu wengi wenye mali wanakuwa na hiki kiburi(japokuwa si wote, bali asilimia kubwa).. Wanaona mtu asiyekuwa na mali kama wao hawezi kuwaambia chochote,..kiburi hiki cha mali kinamfanya mtu aone hata Mungu hana maana, Neno la Mungu kwake ni kama habari zilizopitwa na wakati.
Kulifanyia mizaha Neno la Mungu, ni habari ya kawaida kwao…hata wasikie maonyo ya Mungu kiasi gani, kwao ni habari tu upuuzi.. Mioyo yao imeinuka kutokana na Mali au vitu walivyonavyo, wanaona wanaweza kula hata pasipo kumwomba Mungu, wanaweza kuendeleza maisha yao hata pasipo kupiga magoti.. hivyo hawamhitaji Mungu tena..
Kiburi hiki ndio kibaya kuliko vyote, na ndicho kilichozungumziwa sehemu nyingi katika biblia.. naa watu wote wenye hiki kiburi, biblia imeandika hatima yao..
Isaya 2:12 “Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote WENYE KIBURI NA MAJIVUNO, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.”
Mithali 16:5 “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu”.
Mithali 8:13 “Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.”’
Ayubu 40:12 “Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo”.
Zaburi 119:21 “Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako”.
Soma pia Mithali 21:4, Mithali 16:18, Zaburi 31:18, Zaburi 119:51, Mithali 11:2, na Malaki 4:1 biblia imeelezea zaidi juu ya kiburi na madhara yake..
Tujiepushe na kiburi, tunyenyekee chini ya mkono wa Mungu ulio hodari
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu, lililo Taa ya miguu yetu na Mwanga wa njia yetu.
Kuna jambo la muhimu la kujifunza juu ya safari ya Wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kaanani. Maandiko yanaonesha kuwa wana wa Israeli hawakutoka wenyewe Misri, bali walitoka na Kundi lingine lililochanganyikana.
Hebu tusome..
Kutoka 12:35 “Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto.
38 NA KUNDI KUBWA LA WATU WALIOCHANGAMANA MNO WAKAKWEA PAMOJA NAO; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana”
Umeona hapo?.. Kulikuwa na watu wengine tofauti na Waisraeli walioondoka Misri pamoja na wana wa Israeli.
Sasa swali ni je! kundi hilo lilikuwa ni kundi gani?.
Kundi hilo lilijumuisha baadhi ya Wamisri ambao huenda walikuwa hawataki kuendelea kuishi Misri, labda kutokana na aina ya Maisha ya Misri, pamoja na Wamisri ambao walioana na Waisraeli, maana yake huenda (mwanamke wa kimisri aliolewa na Mwisraeli) hivyo ni lazima aondoke na mumewe, au mwanamke wa kiisraeli aliolewa na Mmisri, na hivyo huyo Mmisri, hataki kumwacha mke wake huyo na akawa radhi kuondoka naye, na kwenda na wana wa Israeli. Hivyo lilikuwa ni kundi kubwa sana!!..
Sehemu nyingine iliyotaja kundi hili lililochanganyikana ni mchanganyiko katika kile kitabu cha Mambo ya Walawi 24:10-16. (Kisa cha Yule mwana wa kiMisri, aliyechanganyikana).
Walawi 24:10 “Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago;
11 kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani.
12 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa Bwana.
13 Na Bwana akasema na Musa, na kumwambia,
14 Mtoe huyo aliyeapiza nje ya marago; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe.
15 Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake.
16 Na yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa”.
Sasa tukirudi katika habari ya Huu Mkutano uliochanganyika, huenda mkutano huu ukaonekana kama ulikuwa ni mwema, lakini kinyume chake ulikuja kuwa mwiba mkubwa kwa wana wa Israeli, kwani uliwakosesha sana mbele za Mungu wao.
Katika biblia tunasoma kwamba sio wana wa Israeli walioanza kumlalamikia Mungu kuhusu kutaka Nyama jangwani, bali tunasoma ni hili kundi lililochanganyikana ndilo lililoanza kunung’unika na hatimaye kushawishi mkutano mzima hadi wa wana wa Israeli kunung’unika, na kusababisha kuwa dhambi kubwa sana kwa wana wa Israeli.. Hebu tusome habari hiyo…
Hesabu 11:4 “Kisha MKUTANO WA WAFUASI WALIOKUWA KATI YAO, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule?
5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu”
Umeona tena hapo?.. maandiko yanasema “MKUTANO WA WAFUATI WALIOKUWA KATI YAO” ndio walioanza kushikwa na tamaa..wakata nyama..na ndipo Israeli wote nao wakaingiwa na tamaa.
Maandiko yanasema, agano la kale ni kivuli cha agano jipya..Safari ya wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kaanani , inafananishwa na safari yetu ya kutoka katika utumwa wa dhambi, hapa duniani na kuelekea mbinguni.. Hivyo basi tunapokuwa katika safari hii, hatuna budi kujihadhari na watu waliochanganyikana, (yaani watu waliovuguvugu katika imani), kwasababu kwa nje wanaweza kuonekana hawana madhara yoyote, lakini tukijifunga Nira nao, na kutembea nao huko mbeleni watatukosesha na Mungu wetu na kuturudisha nyuma pakubwa sana, kama hawa walivyowakosesha wana wa Israeli.. Ndivyo maandiko yanavyosema..
2 Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike”
Unapoanza safari ya Wokovu, ni Mungu kakuita wewe, na si wewe pamoja na rafiki yako au mfanyakazi mwenzako.. kama bado yeye hajaokoka hupaswi kujifunganisha naye Nira, maana yake ni kwamba kama mlikuwa mmezoea kwenda bar pamoja unaacha!, (wewe unapaswa umhubirie wokovu kuanzia huo wakati na kuendelea na si kujishikamanisha naye tena), kama mlikuwa mnaketi kuwasengenya watu, unaacha!, unajitenga naye katika hilo eneo.. Na mambo mengine yote mabaya hupaswi kuambatana naye, mpaka na yeye atakapobadilika na kuwa kama wewe.
Lakini usipoamua kujiachanisha naye katika utu wenu wa kale..basi tambua kuwa atakuja kuwa kikwazo kwako kumaliza safari yako salama ya Imani, (atakuwa ni lango la shetani kumtumia kukurudisha wewe nyuma) kama alivyolitumia lile kundi liliochanganyikana kuwarudisha Israeli nyuma kiimani.
Bwana atusaidie katika safari yetu ya Imani.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.
KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.
Sala ya Bwana ni sala ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake, kabla ya kuondoka kwake. Na kwa kupita sala ile, hakuwafundisha tu wanafunzi wake bali alitufundisha na sisi pia, maana yake ni kwamba, nasi pia tunapaswa tuombe kama vile Bwana alivyowaelekeza wanafunzi wake.
Lakini ni muhimu kuielewa sala hii kwa mapana, ili kusudi tuisikose shabaha tunapoomba.. Kwa maana tusipoielewa vizuri basi tutajikuta tunaifanya kama Mashairi (kwa kuirudia rudia kama watu wa mataifa, wanavyofanya wanapoiomba miungu yao).. Sisi biblia imetuambia tusifanane na hao.(Mathayo 6:7).
Sasa sala ya Bwana Imegawanyika katika vipengele vikuu nane (8).. Na vipengele hivyo sio sala yenyewe bali ni kama “maelekezo ya sala”. Sala yenyewe hatuwezi kuandikiwa, bali tunaomba kila mtu kulingana na anavyoongozwa au kujaliwa na Roho Mtakatifu.
Ni sawa mtu akupe vipengele saba vya kuombea, akakuambia ombea Familia, ombea Taifa, ombea Kanisa, ombea Marafiki.. Sasa kwa kukwambia hivyo huwezi kwenda kupiga magoti na kusema naombea Taifa, kanisa, ndugu na marafiki halafu basi uwe umemaliza!, Huwezi kufanya hivyo.. bali utakachofanya ni kuzama ndani kwa kila kipengele kukiombea..
Kwamfano Katika kipengele cha kuombea Taifa utaombea Viongozi wote na Hali, na hali ya Taifa, na ya Imani kwa ujumla katika Taifa zima, jambo ambalo linaweza kuchukua dakika kadhaa au masaa kadhaa, vile vile katika Familia, na katika kanisa utafanya hivyo hivyo..zitahitajika dakika nyingi kwasababu kuna watu wengi katika familia, na kuna matatizo mengi ambayo ukianza kuyataja mbele za Mungu, huenda yakachukua dakika nyingi au masaa mengi.. Hivyo kwa vipengele tu hivyo vichache unaweza kujikuta unasali hata masaa 6.
Vile vile katika sala ya Bwana, ni hivyo hivyo, vile alivyoviorodhesha Bwana ni vipengele tu, na sio sala yenyewe, maana yake Mitume hawakuchukua hiyo sala na kuikariri kama shairi na kisha kuirudia rudia kila wakati kabla na baada ya kulala, kama inavyozoeleka leo kufanyika hivyo.
Sasa hebu tuisome sala yenyewe na kisha tutazame kipengele kimoja baada ya kingine.
Mathayo 6:7 “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana BABA YENU ANAJUA MNAYOHITAJI KABLA NINYI HAMJAMWOMBA.
9 BASI NINYI SALINI HIVI; BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE,
10 MAPENZI YAKO YATIMIZWE, HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI.
11 UTUPE LEO RIZIKI YETU.
12 UTUSAMEHE DENI ZETU, KAMA SISI NASI TUWASAMEHEVYO WADENI WETU.
13 NA USITUTIE MAJARIBUNI, LAKINI UTUOKOE NA YULE MWOVU. [KWA KUWA UFALME NI WAKO, NA NGUVU, NA UTUKUFU, HATA MILELE. AMINA.]”
1.BABA YETU ULIYE MBINGUNI
Hiki ni kipengele cha kwanza, ambacho Bwana anatuelekeza tuanze nacho katika sala zetu. Kwamba maombi yetu tuyaelekeze kwa Baba aliye mbinguni, kwamba tumwite Baba asikie maombi yetu na haja zetu, na yeye ni mwaminifu atatupa kama tutakavyomwomba, ikiwa tutaomba sawasawa na mapenzi yake.
Na jambo la kuzingatia hapo ni kwamba Bwana Yesu anatufundisha kuomba kwa “Baba” na sio kwa “Mungu”. Sasa Baba ndio huyo huyo Mungu, lakini cheo cha ubaba kinahubiri mahusiano mazuri zaidi kwetu na aliyetuumba kuliko cheo cha UMUNGU. Viumbe vyote vinamwona muumba kama Mungu, lakini kwetu sisi wanadamu tumepewa heshima ya kipekee kwamba tumwite Mungu, Baba yetu (1Yohana 3:1).
Kwahiyo tunapoingia kwenye sala/ maombi ni vizuri sana kuomba kwa kumwita muumba wako Baba kuliko Mungu, kwasababu wewe ni zaidi ya kiumbe chake bali ni mtoto wake.
Luka 11:11 “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
2. JINA LAKO LITAKASWE/ LITUKUZWE
Baada ya kumwita Baba aliye mbinguni kwamba atege sikio lake na kusikia maombi yetu sisi watoto wake, Hoja ya kwanza tunayopaswa tumpelekee ni kwamba JINA LAKE LITAKASWE au LITUKUZWE. Wengi hawajui kuwa jina la Mungu linachafuliwa kila siku kutokana na maovu watu wa Mungu wanayoyafanya..
Warumi 2:22 “Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?
23 Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?
24 KWA MAANA JINA LA MUNGU LATUKANWA KATIKA MATAIFA KWA AJILI YENU, kama ilivyoandikwa”.
Madhara ya jina la Mungu kutukanwa katika mataifa, ni watu wengi kupotea na kuifanya thamani ya msalaba isionekane.. Hivyo basi mwenye uwezo wa kulitakasa jina lake ni Mungu tu, (yeye mwenye jina), hivyo tunapochukua nafasi hiyo ya kuomba kwamba Bwana alitakase jina lake, maana yake tunaomba Mungu alete utukufu katika Injili yake.. Kwamba Bwana ajalie watu kuliogopa jina lake, kwa kuonyesha matendo makuu na ya ajabu, na hivyo wengi kutubu na kumrudishia yeye utukufu.
Kwahiyo hii inapaswa iwe sehemu ya sala kwa kila mkristo kila mahali..
3. UFALME WAKO UJE.
Siku ambayo Ufalme wa Mungu utakuja duniani ni siku ambayo Mateso yatakuwa yameisha, tabu zitakuwa zimeisha, huzuni zitakuwa zimeisha, na maumivu yatakuwa yameisha.. (hakika huo ni wakati mzuri sana). Dunia ya sasa imejaa tabu na mahangaiko na majaribu mengi.. hivyo kila siku hatuna budi kuomba kwa Baba kwamba aharakishe kuileta ile siku ambayo tutapata pumziko la hakika, dhidi ya haya majaribu mengi ya ulimwengu.
Kwa mtu ambaye anatamani kuondokana na haya maisha na kutamani kukaa na Mungu milele, basi atatumia muda wa kutosha kumwomba Bwana aulete ufalme wake. Na kwa kuomba hivi maana yake, tunaomba pia watu wengi waokolewe, kwasababu ile siku haitakuja mpaka kondoo wa mwisho aliyekusudiwa uzima wa milele, aingie ndani ya zizi.. Hivyo basi kwa kuomba ufalme wake uje basi moja kwa moja pia tutakuwa tumeomba Bwana aharakishe kuwavuta watu wake ndani ya Neema.
4. MAPENZI YAKO YATIMIZWE.
Baada ya kuomba kwamba ufalme wake uje, basi hatua inayofuata ni kuomba kwamba Mapenzi yake yatimizwe.. Tunayo mapenzi yetu (yaani matakwa yetu), lakini pia yapo mapenzi ya Mungu ambayo huwenda sisi hatuyafahamu.. Bwana Yesu kabla ya kuteswa alimwomba Baba na kusema, “kikombe hiki kiniepuka lakini si kama nitakavyo mimi bali utakavyo wewe soma Mathayo 6:39.
Na sisi hatuna budi kuomba kuwa mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani, katika shughuli zetu, katika utendaji kazi wetu, na katika mambo yote yanayoendelea, mapenzi yake yakatimizwe kama yanavyotimizwa huko mbinguni, mahali malaika walipo..
5. UTUPE LEO RIZIKI ZETU.
Baada ya kuomba mapenzi yake yatimizwe, sasa ni wakati wa sisi kupeleka haja zetu, kama chakula, mavazi, makazi, fedha, na mambo yote tunayoyahitaji katika mwili na katika roho, Baba akatupatie.. Na Mungu anayesikia maombi atatupa kama ni fedha, au chakula au makazi au malazi, vile vile katika kipengele hiki ndicho kipengele pia cha kuwaombea wengine Bwana awape pia riziki, hivyo kinaweza kuchukua muda mrefu, kulingana na haja mtu alizonazo.
6. UTUSAMEHE DENI ZETU.
Ipo tofauti ya Deni na dhambi, Mtu anaweza kusamehewa dhambi lakini Deni la adhabu lipo palepale, Daudi alisamehewa dhambi yake ya kumtwaa mke wa Uria, lakini deni la kuadhibiwa yeye na mtoto wake halikuondoka, na hapa sala ya Bwana inatuelekeza kwamba tumwombe Bwana atusamehe Deni zetu, huenda tumemkosa Mungu na tukamwomba msamaha na yeye akatusamehe lakini adhabu bado hajaiondoa.. hivyo hatuna budi kumwomba Mungu kwa kuugua sana kwamba atuondolee dhambi zetu pamoja na madeni yetu,
Hapa mtu anaweza kutumia muda mrefu, kujiombea mwenyewe na kuwaombea wengine. Lakini tunapoomba tusamehewe madeni ni sharti kwamba na sisi tuwasamehe wadeni wetu, tusipowasamehe wadeni wetu na Baba yetu aliye mbinguni hatatusamehe sisi.
7. USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU.
Shetani anatutafuta usiku na mchana ili atuingize katika kukosa, sasa hila zote za shetani ili kutuangusha sisi ndio “majaribu yanayozungumziwa hapo”
Bwana anatufundisha kumwomba Baba, atuepushe na mitego hiyo ya mwovu, ambayo kaiweka kila mahali ili kutuangusha, na mitego hiyo shetani kaiweka makanisani, mashuleni, makazini na kila mahali.. hivyo lazima kuomba kwa muda mrefu kwaajili ya mahali ulipo, au unapokwenda ili kusudi usianguke katika mitego ya ibilisi. Na pia unapaswa uwaombee na wengine. (Wagalatia 6:2).
8. KWA KUWA UFALME NI WAKO, na Nguvu na Utukufu
Hii ni hatua ya mwisho ya kumtukuza Mungu na kumwadhimisha, na kumshukuru..hapa mtu anaweza kupaza Sauti yake kama Daudi kwa nyimbo au kwa kinywa na kusema Bwana ni mwenye Nguvu, asikiaye maombi , ajibuye maombi..Bwana ni mwenye haki, Bwana ni mwenye enzi na mamlaka..utukufu una yeye milele na milele.
Tukisali kwa namna hiyo, au kwa ufunuo huo basi tutakuwa tumeomba sawa sawa na mapenzi yake.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kuna tofauti gani kati ya SALA na DUA?
SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.
NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.
(Masomo maalumu kwa wanawake)
Wanawake waombolezaji maana yake nini?, Na je hadi leo wapo?, au wanapaswa kuwepo?.
Kabla ya kuingia ndani kuhusiana na wanawake waombolezaji, hebu tujue kwanza maana ya neno kuomboleza.
Kuomboleza maana yake “ni kuingia katika sikitiko kuu, kutokana na tukio ambalo limetokea au litakalotokea!”.. Sikitiko hili linaambatana na Toba, na Majuto.
Kwamfano mtu anayeomboleza kutokana na msiba alioupata anakuwa katika hali ya huzuni kuu, akitafakari kwa undani tukio lililotokea huku akiomba rehema na msamaha kwa Mungu, na huku akiomba Mungu amponye majeraha yake na pia akiomba jambo kama hilo lisijirudie tena, (huyo ndio mtu anayeomboleza kibiblia kutokana na tukio lililotokea).Na mtu anayeomboleza kwajili ya tukio lijalo pia anakuwa katika hali hiyohiyo.
Hebu tuangalie mifano ya watu walioomboleza kabla ya tukio Fulani/msiba Fulani kutokea na watu walioomboleza baada ya Tukio kutokea.
1.KABLA YA TUKIO.
Mfano wa watu waolioomboleza kabla ya Msiba kutokea ni wana wa Israeli kipindi cha Malkia Esta, wakati ambapo waraka wa kuuawa wayahudi uliposomwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahasuero, ambapo uliasisiwa na Hamani, aliyekuwa adui wa wayahudi.
Lakini tunasoma mara baada tu ya waraka ule kutolewa, Wayahudi wote wakiongozwa na Mordekai walifunga, kwa kulia na kuomboleza.
Esta 4:1 “Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
2 Pia akafika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia.
3 Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, PALIKUWAKO MSIBA MKUU KWA WAYAHUDI, NA KUFUNGA, NA KULIA, NA KUOMBOLEZA; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu”
Na matokeo ya maombolezo haya ni USHINDI KWA WAYAHUDI, na Mauti kwa maadui zao.
2. BAADA YA TUKIO.
Mfano wa maombolezo ambayo yalifanyika baada ya tukio Fulani/msiba Fulani kutokea ni yale ya NABII YEREMIA.
Baada ya wana wa Israeli, kuuawa kikatili na Mfalme Nebukadreza na baadhi yao kuchukuliwa mateka mpaka Babeli, tukio hilo lilikuwa ni tukio baya ambalo halikuwahi kutokea kama hilo katika Israeli, kwani wanawake wajawazito walipasuliwa matumbo yao, na vijana na wazee walichichwa kikatili pale Yerusalemu, na zaidi sana kundi dogo lililosalia lilipelekwa utumwani kwa aibu, kwani walikuwa uchi kabisa na wengine nusu uchi. Na wachache sana ambao walikuwa ni maskini na walemavu ndio waliobakishwa Israeli ili wayatunze mashamba.
Sasa miongoni mwa waliobaki alikuwa ni Yeremia, yeye hakuwa maskini wala mlemavu, lakini Mungu alimlinda na maangamizi hayo kwasababu alikuwa anamcha yeye, Kwasababu hiyo basi YEREMIA, baada ya kulishuhudia tukio hilo, alilia kwa machozi mengi na kuomboleza siku nyingi.. (na ndio akaandika maombolezo yake katika kitabu, ambacho ndio sisi leo tunakisoma kama kitabu cha Maombolezo).
Maombolezo 3:47 “Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu.
48 Jicho langu lachuruzika mito ya maji Kwa ajili ya uvunjifu wa binti ya watu wangu.
49 Jicho langu latoka machozi lisikome, Wala haliachi;
50 Hata Bwana atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni.
51 Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa sababu ya binti zote za mji wangu.
52 Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege”
Sasa ni Maombolezo gani kati ya hayo mawili, Mungu anayotaka sisi tuyafanye??
Jibu ni “Maombolezo ya kabla ya tukio”. Mungu hataki tuomboleze baada ya tukio, bali anataka tuomboleze kabla ya tukio..
Leo hii dunia tayari imeshatamkiwa hukumu na Mungu, huenda Taifa lako limeshatamkiwa hukumu, huenda familia yako imeshatamkiwa hukumu na Mungu, huenda Nyumba yako imeshaandikiwa hukumu na Mungu, kutokana na mambo yanayoendelea humo yasiyompendeza yeye.
Huenda Kanisa lako limeshaandikiwa hukumu, washirika wenzako wameshaandikiwa hukumu, mchungaji wako kashaandikiwa na kashakusudiwa kuadhibiwa na Mungu hapa hapa duniani kabla hata hajaondoka..Hivyo kabla hukumu hizo hazitimia, Bwana Mungu anataka tuwe na jicho la kuona na KULIA NA KUOMBOLEZA KWA TOBA NA MSAMAHA, NA KWA KUTAKA REHEMA kwa Mungu ili Mabaya haya yasitokee, Kama Akina Esta, Mordekai na Wayahudi wote walivyofanya kipindi cha Hamani.
Sasa pamoja na hayo, lipo kundi moja la Watu, ambalo ni rahisi kuzama katika Maombolezo na hata kuvuta rehema za Mungu, na fadhili za Mungu upesi.
Na kundi hilo si lingine zaidi ya kundi la Wanawake.. Mwanamke anapoomba kwa hisia (iliyo ya kiMungu), basi ni rahisi maombi yake kufika kwa Baba mbinguni zaidi ya wanaume.. Hivyo biblia imewataja wanawake kama viungo vifaavyo kusimama katika hii nafasi ya kuomboleza.
Hebu tulithibitishe hili kimaandiko…
Yeremia 9:17 “Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;
18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu”.
Umeona Nafasi yako wewe mwanamke?..Wewe umewekwa na Mungu katika hilo kanisa ili ulie na kuomboleza kwaajili ya Uovu, ili Bwana akumbuke rehema, wewe umewekwa katika hilo Taifa ili ulie na kuomboleza Bwana aachilie neema na rehema.. Hiyo ndio nafasi yako ambapo usipoitumia siku ile utakwenda kuulizwa!!.
Biblia haijashindwa kuwaweka hapo wanaume, na kusema wao ndio waomboleze!!.. lakini imewaweka pembeni na kuwapa vipaumbele wanawake!..Sasa sio kwamba ina upendeleo haina upendeleo..bali ni kutokana na jinsi wanawake walivyoumbwa!.. Kadhalika mwanamke usikimbilie kuwa mchungaji, hiyo ni nafasi ya wanaume..(kasome 1Wakorintho 14:34). Kwahiyo biblia imetoa majukumu kwa kila jinsia..
Je umewahi kulia na kuomboleza kwaajili ya Nyumba yako, au kanisa lako au Taifa lako? Kama bado halafu wewe ni mwanamke unayesema umeokoka, basi badilika leo.. Litii Neno na lifuate hilo, usijiamulie utumishi au usijitwike wito ambao hujawekewa juu yako.. kaa katika nafasi yako hiyo na Mungu atakutumia.
Na baada ya kujua nafasi yako hii basi wafundishe na wanawake wengine kuwa kama wewe (mwombolezaji)..ndivyo biblia inavyoelekeza..
Yeremia 9:20 “Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.
21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu”.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
Karibu tujifunze biblia..
Daudi anasema..
Zaburi 39:4 “Bwana, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani……..”
Hapa si kwamba Daudi anataka aijue siku ya kufa kwake!, Hapana!, Mungu hajawahi kumwahidia mwanadamu hayo maarifa..(Hakuna maombi ya mtu kufunuliwa siku yake ya kufa). Bali hapo Daudi anaomba Mungu ampe KUZIJUA SIKU ZAKE DUNIANI KWAMBA SI NYINGI, Kwamba siku za mwanadamu ni kama maua! Si wa kudumu (Zaburi 103:15).
Hivyo Daudi alijua Mungu akimpa moyo wa kuelewa kuwa “Yeye ni kama mpitaji tu hapa duniani, na siku zake si nyingi”.. basi atakuwa mnyenyekevu zaidi, na ataishi maisha ya kumtafuta Mungu, kumcha Mungu na kuishi kwa hekima duniani..
Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”.
Na sio tu yeye aliyepaswa kuomba maombi kama haya, bali hata sisi pia watu wa siku za Mwisho, ni lazima tumwombe Mungu atujulishe siku zetu! (Yaani atupe mioyo ya hekima kujua kuwa sisi ni wapitaji tu, na siku zetu za kuishi si nyingi).
Faida ya kuomba Moyo huu kutoka kwa Mungu, ni kwamba tutakuwa watu wa kutazama maisha yajayo zaidi kuliko maisha haya ya hapa duniani ya kitambo!.. Kwasababu ndani ya akili zetu tutajua kuwa siku zetu si nyingi!..kwamba siku yoyote safari ya maisha yetu itafikia mwisho.
Watu wengi wenye huu moyo, utaona ndio watu wenye mioyo ya kumtafuta Mungu kwa kujikana nafsi kwelikweli…ndio watu wenye mioyo ya kusaidia wengine, ndio watu wenye mioyo ya kuwahubiria wengine mwisho wa maisha haya.
Na watu kama hawa, hata kama wakiambiwa kuwa watapewa miaka elfu moja ya kuishi duniani, bado tu!, watajiona kuwa siku zao ni chache, kwasababu tayari ndani yao wamepewa mioyo ya “kuzihesabu siku zao na kujijua kuwa wao si kitu, ni kama maua tu, yaliyopo leo na kesho kutupwa kwenye tanuru” hivyo maisha yao yatakuwa ni yale yale siku zote ya kutafuta kutengeneza maisha yajayo ya umilele.
Shetani hapendi watu wawe na moyo huu, anataka watu wawe na moyo wa kufikiri kwamba wataishi milele katika hii dunia, hataki watu wajue kwamba siku yoyote safari ya maisha yao itafikia ukingoni, kwasababu anajua watu wakilijua hilo, basi watatengeneza maisha yao hapa kwaajili ya huko waendako, na hivyo atawapoteza wengi. Na yeye (shetani) hataki kumpoteza mtu hata mmoja, anataka wote waende katika ziwa la moto kama yeye!!.
Kwahiyo kila siku ni muhimu sana kuomba Bwana atupe huu moyo.. “Atujulishe miisho yetu, na siku zetu za kuishi” ili tufahamu kuwa “sisi ni wapitaji tu”.
Moyo huu utaupata kwa kufanya mambo yafuatayo matatu (3)
1.Kwa kuomba
Majibu ya mambo yote tunayapata katika maombi, kama vile Sulemani alivyoomba kwa Mungu apewe moyo wa hekima na Mungu akamsikia, vile vile pia Moyo wa kujua kuwa wewe ni mpitaji tu, unatoka kwa Bwana, ndio maana hata hapo Daudi anaonekana kama anaomba.. “Bwana nijulishe”..Na wewe siku zote sema “Bwana nijulishe”
2. Kwa kutafakari matukio ya vifo yanayotokea.
Unapotenga muda wa kutafakari matukio ya Ajali yanayotokea, au unapotazama wagonjwa mahututi, au unapokwenda kwenye nyumba za misiba..sehemu hizo ni sehemu ambazo Mungu anaitengeneza mioyo ya wengi.. Hivyo na wewe huna budi kuhudhuria misiba, au kufuatilia matukio (Wengi hawapendi kufuatilia haya), kwasababu hawataki kuumia moyo, lakini ndani ya mioyo yao wana viburi vya maisha, wanajiona kama wao wataishi milele.. Biblia inatufundisha pia tuhudhurie sehemu za Misiba, sio kwenye karamu tu, ili tukajifunze huko..
Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.
3. Kwa kusoma Neno.
Unaposoma Biblia, huko ndiko utakapopata Maarifa kamili ya Neno la Mungu, na maneno ya kuunyenyekeza moyo wako, biblia ndio kioo kamili cha kujijua wewe ni nani?.. ukitaka kujijua wewe ni mtu wa namna gani, basi soma Biblia.
Bwana atubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
Yakobo 1:13 “Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu”
Hapo Neno linasema kuwa Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, kinyume chake ni kweli kwamba yeye anajaribiwa na MEMA tu!. Maana yake tunapofanya mema hapo tunakuwa tunamweka Mungu kwenye jaribu la kutubariki.. Na hivyo ni lazima aachie baraka kwetu.
Lakini tukienda kinyume na Neno lake na huku tunataka atubariki, hapo maana yake tunamjaribu yeye kwa Maovu.. Mfano wa watu waliomjaribu Mungu kwa maovu ni Wana wa Israeli kipindi wapo jangwani, Walitaka Bwana awashushie chakula kile cha kimiujiza, huku mioyoni mwao wamemwacha Mungu, ni watu wenye viburi, ni watu wa kunung’unika, ni watu wasio na heshima wala staha kwa Mungu na mwishowe wakaangukia hukumu.
Waebrania 3:7 “Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu”.
Na maandiko yanasema Mungu ni yeye Yule jana na leo na hata milele, alilolikataza miaka elfu 2 iliyopita analitakata hata leo.. Akisema “yeye hajaribiwi na Movu, ni kweli hajaribiwi na hayo”.. Lakini kinyume chake anajaribiwa na Mema yaliyoandikwa katika Neno lake.
Kwamfano unapomtolea Mungu sadaka isiyo na kasoro (Maana yake iliyo sawasawa na Neno lake, na kwa nia njema) Hilo ni jaribu kwa Mungu kukubariki wewe, na hapo utakuwa umemjaribu kwa Mema.
Malaki 3:8 “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi”.
Na mambo mengine yote mema, ambayo tunayafanya yaliyo sawasawa na Neno la Mungu, mambo hayo ni TANZI kwa Mungu, kutumwagia Baraka zake, au kuzungumza na sisi.
Lakini kama moyoni mwako umemwacha Bwana, halafu unatafuta kuisikia sauti yake, unaenda kwa nabii ili usikie Mungu anasema nini kuhusu wewe, hapo unamjaribu Mungu kwa mabaya na hivyo unajitafutia laana badala ya Baraka.
Ezekieli 14:4 “Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;
5 ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao.
6 Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.
7 Kwa maana kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, kisha kumwendea nabii, na kuniuliza neno kwa ajili ya nafsi yake; mimi, Bwana, nitamjibu, mimi mwenyewe
8 nami nitaukaza uso wangu juu ya mtu yule, na kumfanya kuwa ajabu, awe ishara na mithali, nami nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”
Bwana Yesu atusaidie.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je Adamu na Hawa, walikuwa hawafanyi mema kabla ya kula tunda?
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
Jina la Bwana na Mwokozi, Mkuu wa Uzima, Yesu Kristo lihimidiwe!..karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu.
Upo wakati ambao TAA ya Mungu itazima!.. Tuitikie wito wa Mungu, kabla ya huo wakati kufika..
1Samweli 3:2 “Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),
3 NA TAA YA MUNGU ILIKUWA HAIJAZIMIKA BADO, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;
4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.”
Sasa ili kuelewa vizuri Taa ya Mungu ni kitu gani, na ilikuwa inazimika wakati gani..hebu turejee ile Hema ambayo Musa aliagizwa aitengeneze, tunasoma Ilikuwa imegawanyika katika Sehemu kuu tatu, Ua wa Ndani, Patakatifu na Patakatifu pa patakatifu.
Na ndani katika Patakatifu, palikuwa na madhabahu ya uvumba, Meza ya mikate ya wonyesho pamoja na KINARA CHA TAA, ambacho kilikuwa na Mirija saba. (Tazama picha juu).
Hiki kinara cha Taa kazi yake ilikuwa ni kutia Nuru ile hema wakati wa USIKU. Kwamba Nyakati zote za usiku ni sharti ndani ya Hema kuwe na Nuru, na amri hiyo ilikuwa ni ya Daima, maana yake ya kila siku!.. haikupaswa hata Usiku mmoja upite bila Kinara hicho kuwashwa ndani ya Hema.
Kutoka 27: 20 “Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
21 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza TANGU JIONI HATA ASUBUHI MBELE YA BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israel”
Tusome tena..
Walawi 24:1 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima.
3 Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza TANGU JIONI HATA ASUBUHI MBELE ZA BWANA DAIMA; ni amri ya milele katika vizazi vyenu”
Hapo mstari wa 3, unasema ataitengeneza “tangu jioni hata asubuhi” maana yake wataiwasha tangu jioni mpaka asubuhi, na kukiisha pambazuka basi taa ile inazimwa, kwasababu kulikuwa na Nuru ya mwanga wa Nje wa jua iliyokuwa inaingia ndani ya Hema.
Sasa tukirudi katika habari hiyo ya Samweli, maandiko yanasema Samweli alikuwa analala katika Hema karibu na sanduku la BWANA, na wakati ambapo Taa ya Mungu bado haijazimika..Maana yake bado hakujapambazuka, (kwasababu kukisha pambazuka tu, tayari ile taa ilikuwa inazimwa).
Wakati huo ndipo Samweli aliisikia Sauti ya Mungu ikimwita mara 4, na Samweli akaitikia wito wa Mungu.
Lakini ni nini tunajifunza katika hiyo habari?
Upo wakati ambao sauti ya Mungu inaita juu ya Mtu..na wakati huo ni wakati wa giza Nene juu ya maisha ya mtu.. Huo ndio wakati ambapo Mungu anamwita mtu, na anamwita kwa sauti ambayo inakuwa inayofanana na ya watu wa Mungu.. kiasi kwamba mtu anaweza kudhani ni mtu anayemwita/kumshawishi kumbe ni Mungu, ndio maana Samweli alipoitwa alikimbilia kwa Eli akidhani ni Eli anayemwita kumbe ni MUNGU.
Vile vile Mungu anawaita leo watu kutoka katika dhambi, na uvuguvugu lakini watu wanadhani ni wachungaji wao ndio wanaowaita, wengine wanadhani ni wahubiri ndio wanaowatafuta wawe washirika wao, pasipo kujua kuwa ni sauti ya Mungu ndio inayowaita na si watu.
Sasa endapo Samweli asingeitikia ule wito wakati ule ambapo TAA BADO HAIJAZIMIKA, huenda ile sauti ya Mungu asingeisikia tena kwa wakati ule mpaka labda kipindi kingine ambapo Taa hiyo itakuwa inawaka.
Ndugu TAA ya Mungu leo ni NEEMA, Hii Neema kuna wakati itasimama!, na hakutakuwa tena na nafasi ya kumkaribia Mungu, wakati ambao unyakuo wa kanisa utapita, ndio wakati ambao TAA itakuwa imezima, vile vile wakati ambao utaondoka katika haya maisha huo ndio wakati ambao Taa ya Mungu itakuwa imezimika juu yako.
Je umemkabidhi Yesu maisha yako?.. Umebatizwa katika ubatizo sahihi? Umeokoka?.. Kama bado ni vyema ukafanya hivyo sasa kabla Taa haijazimika.
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Maran atha!
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
Kiango na Pishi ni nini (Mathayo 5:15)?
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.