SWALI: Nini maana ya 2 Wakorintho 8:9
isemayo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.
2 Wakorintho 8:9
[9]Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
JIBU: Katika sura hii mtume Paulo anawaandikia wakorintho juu ya huduma ya utoaji kwa watakatifu walio maskini katika makanisa mengine, ya mbali
Na hapa anawasisitiza kukubali kutoa kwa kufuata kielelezo cha Kristo katika eneo la neema yake..Jinsi alivyokubali kuwa maskini, kwa kuacha enzi na utukufu na mamlaka juu mbinguni, na kuja duniani, katika hali ya chini sana (ijapokuwa hakuwa duni), ili tu atukomboe sisi tulio katika hali ya ufukara wa roho.
Kwasababu kama asingeweza kujishusha vile, na kukubali kuhesabiwa si kitu (ijapokuwa alikuwa na nguvu), matokeo yake ni kwamba asingekwenda msalabani kusulubiwa kwa ajili yetu tena uchi, na mwisho wake kusingekuwa na msamaha wa dhambi.
Isaya 53:3
[3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Lakini sasa tumepokea neema na utajiri wote wa rohoni kupitia yeye kujishusha kwake.
Waefeso 1:3
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Vivyo hivyo Mtume Paulo anawahimiza Wakorintho waige mfano huo huo, katika eneo la kuwahudumia watakatifu wengine. Akitumia mfano wa Wamakedonia ambao walikuwa ni maskini, na wenye dhiki lakini walikuwa tayari kutoa kwa moyo na furaha kwa watakatifu maskini waliokuwa Yerusalemu.
2 Wakorintho 8:1-3
[1]Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; [2]maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. [3]Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
[1]Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;
[2]maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.
[3]Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
Halikadhalika Bwana anataka na sisi tuhudumiane katika ufahamu wa Kristo, yaani kuwa tayari kuwasaidia watakatifu wengine hata katika hali zetu za dhiki.
Lakini mtazamo ambao si sahihi kuhusiana na vifungu hivi ni kudhani kwamba andiko hilo moja kwa moja linamaanisha lengo la Bwana Yesu kuwa maskini duniani ni ili sisi tuwe matajiri kifedha. Ni kweli kupitia Yesu, tunabarikiwa mwilini, lakini hicho sio kinachozungumziwa hapo. Bwana Yesu kuwa maskini ni kutupa utajiri wa roho zetu, pamoja na ule wa ulimwengu ujao.
Bwana akubariki.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
Kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi ( 1 Wakorintho 7:14)
Nini maana ya waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? (Matendo 11:23)
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Je! kulingana na mstari huu, watoto wa wapagani hawataokolewa?
1 Wakorintho 7:14
[14]Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
JIBU: Ukianzia juu utaona andiko hilo linazungumzia juu ya wandoa wanaoishi pamoja lakini mmojawapo hajaamini. Bwana anatoa agizo kwamba ikiwa bado huyo ambaye hajaamini anaona sawa kuendelea kuishi naye, basi yule aliyeamini asimwache.
Kwasababu kwa kupitia njia hiyo, yule asiyeamini hutakaswa na yule aliyeamini Pamoja na watoto wake pia.
Lakini je mstari huo unamaanisha kuwa mwanandoa mmoja katika familia akiokoka, basi ameiponya familia yote mpaka watoto wake?
Jibu ni la! andiko hilo halikumaanisha hivyo.
Bali linamaanisha kuwa, kwa kupitia yeye, ni rahisi wao kuambukizwa imani na hatimaye kufanya uamuzi wa kuokoka.
Wokovu hauji kwa kurithishana au kwa ‘niaba-ya’ bali kwa mtu mwenyewe kufanya maamuzi binafsi mara baada ya kushawishwa na injili.
Hata sasa tumeona shuhuda nyingi watu wakiwavuta ndugu zao kwa Kristo, aidha kwa injili au mienendo yao, na hatimaye wote kugeuka.
1 Petro 3:1-2
[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; [2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
[2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
Hivyo kwa hitimisho, watu wote, haijalishi wakubwa au wadogo, aidha wa waamini au wapagani, wote wanahitaji kumwamini Yesu ndipo waokolewe dhambi zao. Lakini hiyo huja kwa ushawishi wetu, kwa jinsi tunavyosema nao, tunavyoenenda katika mwenendo wetu mzuri, tunapozifanya nyumba zetu kuwa makao ya ibada, ni njia rahisi ya kuwashawishi.
Washirikishena akubariki.
je! Paulo aliwalaani Wagalatia na Wakorintho?
UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?
Matasa ni nini? (1Nyakati 28:17)
SWALI: Ni kipawa kipi hicho tusichoweza kukisifu jinsi ipasavyo?
2 Wakorintho 9:15
[15]Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
JIBU: Mungu alitupa mwana wake (Yesu Kristo), kama zawadi kwetu, ambaye anakaa ndani yetu kwa Roho wake Mtakatifu.
Warumi 5:17
[17]Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
Yesu (kupitia Roho Mtakatifu), ni kipawa kikubwa ambacho hatuwezi kukielezea uzuri wakev(kukisifu), jinsi ipasavyo.
Ndani ya Yesu ni hakika tunapata vitu vyote (vya rohoni na mwilini)
Hivyo kulingana na vifungu hivyo ukianzia tokea juu katika sura hiyo ya tisa (9), anaegemea hasaa katika eneo la kubarikiwa na Mungu katika baraka za mwilini. ambazo huja ndani ya kipawa hichi cha Mungu.
2 Wakorintho 9:11
[11]mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.
Ni kweli hatuwezi kueleza kwa maneno haya jinsi gani Yesu alivyoleta ukombozi katika maeneo mengi zaidi ya yale tunayoyadhani, si tu katika roho zetu, bali mpaka miili yetu, dunia yetu, uchumi wetu, familia zetu, magonjwa yetu, wanyama wetu, jamii yetu, ardhi zetu, n.k. kipawa hichi kila mahali kinatibu.
Hivyo si rahisi kukisifu kwa jinsi ipasavyo. Ndio maana kwa Yesu tumetia nanga, yeye ndio utoshelevu wetu wote, hatuna haja kwa mtu mwingine yeyote zaidi yake, na ndivyo ilivyo. Hekima ya Mungu iliona hilo ndio maana hakutupa sisi wanadamu kitu kingine zaidi ya Yesu Kristo tu.
Ashukuriwe Mungu kwa zawadi hii. Utukufu heshima na shukrani vimrudie yeye milele na milele. Amina.
Maana ya 2Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote
Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)
SWALI: Nini tafsiri ya 2 Wakorintho 9:11-12
JIBU: Katika sura hii mtume Paulo analisisitiza kanisa la Wakorintho, uthamani wa huduma ya utoaji kama njia mojawapo ya utiifu katika kuikiri injili (9:13).
Na hapa anaongezea kuwa Mungu hutoa utajiri katika vitu vyote (si tu vya rohoni tu, bali pia vya mwilini). Na kwamba yeye ndiye huwapa watu mbegu za kupanda na chakula.
Hivyo atutajirishapo lengo lake ni tutumie utajiri huo kwa kutenda mema (9:8), (yaani kuwapa maskini hususani watakatifu), kwasababu ndivyo ilivyokuwa kwa Kristo(9:9). Na si tutumie katika anasa na ufahari, na ubinafsi.
Ndio hapo anasema “mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote”. Na kama tukifanya hivyo, mitume wanasema shukrani zinamfikia Mungu kwa kutii kazi yao hiyo ya kutuhimiza sisi kutoa.
2 Wakorintho 9:11-12
[11]mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. [12]Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
[12]Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;
Hivyo Bwana anatutaka kila atufanikishapo tujue amekusudia tuwasidie wengine walio maskini hususani watakatifu, kwasababu kwa njia hiyo shukrani nyingi humfikia Mungu.
Zaidi vifungu hivi vinasisitiza pia jinsi Mungu anavyoongeza baraka pale tunapotoa sana, akisema atoaye haba hatavuna haba,(9:6). kile tupandacho ndicho tutakachovuna kwake.
Bwana atusaidie tuwe watoaji katika hali zote.
ubarikiwe.
FAIDA NYINGINE MUHIMU YA KUMTOLEA MUNGU.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
Mistari ya biblia kuhusu shukrani.
Swali: Ni kwanini siku/saa ya kuja kwa Bwana YESU anaijua Baba peke yake na mwana haijui?, na ilihali pia YESU ni Mungu?
Jibu: Turejee..
Mathayo 24:36 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
Kipindi Bwana YESU yupo duniani, alikuwa hana budi kuwa kama wanadamu wengine, ingawa alikuwa na uungu ndani yake, Hivyo alikuwa anahisi maumivu kama watu wengine,… alikuwa anasikia huzuni kama tu watu wengine, na pia ilimpasa amtafute Mungu kama tu wanadamu wengine wanavyomtafuta, ndio maana alifunga na kukesha milimani kuomba kwa machozi, ili aweze kupokea mafunuo kutoka kwa Baba, kwaajili ya huduma yake na watu wake.
Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.
Hivyo Bwana YESU hakuzaliwa anajua vyote, ilimpasa ajifunze vitu.. alizaliwa hajui kutembea na hivyo ikampasa ajifunze kutembea kama watoto wengine, vile vile alizaliwa hajui kusoma na hivyo ilimpasa ajifunze kusoma na pia ajifunze torati.
Luka 2:46 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.”
Luka 2:46 “na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.”
Hivyo kwa tabia hiyo ya kuendelea kujifunza, ni wazi kuwa si vyote alikuwa anavijua kipindi yupo duniani, ndio maana akasema “ile siku hata yeye haijui”
Lakini alipokufa na kufufuka, mambo yakageuka… ALIJUA YOTE!!, kwani baada ya kufufuka alisema, amepewa mamlaka yote ya mbinguni na duniani.
Mathayo 28:16 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. 17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. 18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.
Mathayo 28:16 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.
Sasa hawezi kupewa mamlaka yote mbinguni, halafu asijue saa ya kuja kwake, ni jambo lisilowezekana…
Kiashiria kingine kinachoonesha kuwa Bwana YESU aliijua saa ya kurudi kwake, baada ya kufufuka ni lile neno alilomwambia Petro kumhusu Yohana kwamba “ikiwa anataka akae hata ajapo” soma Yohana 21:22.
Soma pia Ufunuo 3:3, Ufunuo 16:15, Ufunuo 22:12, na Ufunuo 22:20.. Utaona mamlaka ya YESU kuhusiana na kurudi kwake.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Bwana YESU KRISTO sasahivi anajua kila kitu, ikiwemo siku ya kurudi kwake mara ya pili, na mwisho wa dunia (Si wa kawaida kabisa!!)
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MCHE MWORORO.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
TUNAPASWA TUWEJE WAKATI WA KUJA KWAKE BWANA YESU?.
Maana ya Mhubiri 10:15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,
Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?
Swali: Kwanini pale Edeni pawekwe MITI, isimamie uzima au Mauti na si kiti kingine kama JIWE?.
Jibu: Ijapokuwa zipo sifa nyingi za MITI zinazoipa vigezo vya kuweza kuwakilisha UZIMA au MAUTI…Lakini sifa kuu inayoweza kusimamia nafasi hiyo ni UREFU wa MAISHA.
Mti ndio kiumbe hai pekee kilichoumbwa na MWENYEZI MUNGU kinachoishi muda mrefu kuliko vyote.
Tembo ni kiumbe hai lakini miaka yake ya kuishi ni 80 tu, Kasuku ni miaka 90, kunguru ni miaka 90, kobe ni miaka 200 lakini MITI inafika mpaka miaka 2,000..
Ipo miti yenye miaka zaidi ya elfu chini ya Jua, na bado inaendelea kuzaa matunda yenye ubora ule ule, na zaidi ya yote MITI haisogei ipo palepale, lakini unaishi muda mrefu.
Tofauti na Jiwe, lenyewe Lipo kwa muda mrefu (hata miaka elfu) lakini haliishi (halina uhai), halizai wala haliongezeki liko vile vile siku zote…kama tu mifupa ya mfu iliyopo kaburini kwa mamia ya miaka.
Sasa kwa sifa hiyo ya MTI kuishi muda mrefu, ikiwa bado inaendelea kuzaa matunda yale yale na ikiwa bado ipo eneo lile lile moja..ndio inayoifanya ichukue sifa ya kusimamia UZIMA wa Daima au MAUTI ya daima.
Kwamba tunapotafakari maisha ya MTI (jinsi yalivyo marefu na usivyosogea). Hali kadhalika Mauti ya mtu aliye katika dhambi ni ya DAIMA, na hukumu yake ni ya Daima, vile vile UZIMA wa MTU aliye ndani ya MUNGU ni wa daima na usio badilika.
Sasa huu MTI wa uzima ni nini? Au upo wapi?..
MTI wa uzima ni YESU KRISTO, leo lifahamu hili, Nitakuhakikishia hilo kimaandiko.
Maandiko yanasema Kristo ndiye hekima ya MUNGU.
1 Wakorintho 1:23 “bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni KRISTO, nguvu ya Mungu, na HEKIMA YA MUNGU”.
1 Wakorintho 1:23 “bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi;
24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni KRISTO, nguvu ya Mungu, na HEKIMA YA MUNGU”.
Umeona hapo?..KRISTO ni HEKIMA ya MUNGU na kama Kristo ni Hekima ya MUNGU, basi yeye ni MTI wa UZIMA kama maandiko yasemavyo katika Mithali 3:18.
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye HEKIMA, Na mtu yule apataye ufahamu…… 18 Yeye ni MTI WA UZIMA kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye HEKIMA, Na mtu yule apataye ufahamu……
18 Yeye ni MTI WA UZIMA kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”
Kumbe YESU KRISTO ni MTI wa UZIMA, na ana heri kila amshikaye!!!… naam si ajabu tuonapo anatajwa kama Mkuu wa Uzima (Matendo 3:15).
Si ajabu tusomapo kuwa hakuna mwingine mwenye Uzima zaidi yake yeye (Yohana 10:10) na yeye lpekee ndiye njia na Uzima (Yohana 14:6).
Si ajabu kusikia kuwa kila anayemkimbilia anapata uzima wa milele (Yohana 3:16, Yohana 6:47).
Kwaufupi hakuna UZIMA nje ya YESU KRISTO, aliyekufa na kufufuka na kupaa mbinguni, yeye ndiye MTI uishio Milele, na kwake yeye kuna Uzima.
Je unao uzima wa milele?…je umeupata huu Mti?..kama bado mkaribishe YESU maishani mwako na akufanye kiumbe kipya na ukabatizwe kwa maji tele na kwa jjina lake YESU.
Shalom.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
Uzima wa milele ni nini?
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
CHAGUA UPANDE WA UZIMA.
WhatsApp
SWALI: Kwanini mke wa Ayubu hakupitia matatizo?
JIBU: Ni vema kufahamu kibiblia si kila tendo au jambo lililoandikwa lina umuhimu kulijengea hoja, kana kwamba usipolijua litakupunguzia sehemu katika roho yako. Hapana, Kwamfano maswali kama Yohana alibatizwa na nani, Au mke wa Petro aliitwa nani au kaburi la Yesu lipo wapi kwasasa, haya hayatusaidii sana kwasababu sio fundisho au agizo tuliloamuriwa tulishike.
Lakini ikiwa ni kutanua upana wa fikra zetu, basi tunaweza jifunza mambo kadhaa kuhusu matukio kama haya mfano wa hili la mke wa Ayubu, kutohusishwa katika majaribu.
Ni swali ambalo watu huuliza, mbona watoto wote wa Ayubu, walikufa mifugo na mali pia viliondoka, lakini hatuoni mke wa Ayubu kuguswa.
Tukumbuke kuwa hakukuwa na agizo kwamba vyote alivyonavyo Ayubu ni LAZIMA viathiriwe…Hapana. Kwani tunaona hata miongoni mwa watumwa wake wapo walionusurika kifo. Na hao waliachwa wawe kama mashahidi wa yaliyotokea.
Ayubu 1:16
[16]Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
Vivyo hivyo hata katika eneo la familia ya Ayubu hwenda ilipasa abakie shahidi wa kueleza hali ya moyoni iliyokuwa inaendelea katika nyumba hiyo.
Mke wa Ayubu anatufunulia machungu yaliyowapata kiasi cha mwanadamu wa kawaida kushindwa kuvumilia, isipokuwa tu kumkufuru Mungu. Kikawaida mpaka mtu kufikia hatua ya kutoa maneno ya matusi, na kufuru kwa muumba wake, ujue kabisa jambo lililomkuta limeijeruhi sana nafsi yake mpaka kushindwa kuvumilia.
Ni Ayubu tu peke yake ndiye aliyeweza kustahimili hivyo, hata mke wake alipomshauri alikataa. Hii ni kutuonyesha jinsi gani mtu huyu alivyo mwogopa Mungu, zaidi ya matatizo yake. Kama tusingesikia aliyoyafanya mkewe, hakika tusingejua-fika hali waliyokuwa nayo Ayubu, na nguvu aliyojaliwa hata kutoa majibu kinyume na uhalisia wa kibinadamu.
habari ya Ayubu hutupa sisi funzo kubwa la uvumilivu katika Imani. Kwasababu tunapostahimili, sikuzote mwisho wake Mungu huwa anatupa faraja kubwa zaidi ya mwanzo.
Yakobo 5:11
[11]Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Kuguguna maana yake nini? (Ayubu 30:3 )
1 Nyakati 17:11-12 “Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake. 12 Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele”.
1 Nyakati 17:11-12 “Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake.
12 Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele”.
Unabii huu unamuhusu BWANA YESU KRISTO, na si SULEMANI. yeye (YESU) ndiye atakayetokea na kuijenga nyumba ya MUNGU (Hekalu) lililo kamilifu na takatifu, na nyumba hiyo ni MWILI wake (Yohana 2:19-22).
Lakini pamoja na hayo pia Hekalu la damu na Nyama, Mungu alimzuia Daudi asilijenge KWASABABU alimwaga damu nyingi za hatia na zisizo za hatia, na kwasababu hiyo Mungu hakumruhusu aijenge nyumba ile bali mwanae Sulemani.
1 Nyakati 28:3 “Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu ……………… 5 tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli. 6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye”
1 Nyakati 28:3 “Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu ………………
5 tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.
6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye”
Na ni damu za akina na Daudi alizozimwaga?.
1.DAMU ZA MAADUI.
Daudi alikuwa ni mtu wa vita tangu ujana wake, yeye pamoja na mashujaa wake walikuwa ni watu wa kuua maadui zao kwa upanga, hilo likawa kizuizi kwa Daudi kuijenga nyumba ya Bwana.
2. DAMU YA URIA.
Damu ya Uria, jemedari aliyoimwaga Daudi, ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha Daudi kupata ruhusu ya kuijenga nyumba takatifu ya Mungu atakayokaa..
Kwani laiti Daudi angeijenga nyumba ile pamoja na tendo lake hilo alilolitenda la kumuua Uria na kumchukua mke wake, basi maadui wa Bwana wangeiona hiyo nyumba aliyoijenga na kukumbuka Daudi aliyoyafanya, wangepata sababu ya kukufuru na kukashifu ile nyumba sawasawa na maneno ya Bwana.
2 Samweli 12:13 “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. 14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa”.
2 Samweli 12:13 “Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.
14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa”.
Ni lipi tunaloweza kujifunza hapo?
Bwana hakuwahi kupendezwa na mauaji tangu mwanzo, watu wa kale waliruhusiwa kuua kwasababu ya ugumu wa mioyo yao, lakini tangu mwanzo Bwana alikataza mauaji Soma Kutoka 20:13.
Hivyo hatuwezi kuishi sasa kwa kuyaangalia matendo ya Daudi, kama Daudi aliua basi na sisi ndio tuue, kama Daudi alioa wake wengi basi na sisi ndio tuoe wake wengi n.k.
Bali tunamtazama YESU KRISTO sasa aliye Ukamilifu na Utimilifu wa sheria, yeye anasema…
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Bwana alimaanisha nini kusema “Yeye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo”? (Mathayo 23:20)
Daudi alikuwa na wake wangapi, na je ni halali kuwa na wake wengi?
Je! Habari iliyo katika 1Nyakati 21:25, na 2Samweli 24:24, ya Daudi kununua kiwanja inajichanganya?
MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.
Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)
SWALI: Biblia humaanisha nini kwenye vifungu hivi?
Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.
JIBU: Ni vema kwanza kufahamu kwanini watu wanapigana vita?
Zipo sababu nyingi,baadhi ya hizo ni hizi,
Kujilinda, kutoelewana, kulipiza visasi, kutofautiana kiitikadi, au kutanua ngome.
Hivyo ili watu kufikia malengo hayo, njia pekee waionayo ni kutumia silaha, kuuana. Lakini biblia inashauri njia iliyo bora zaidi ambayo inaweza kutumiwa na hatimaye yote hayo yakatatulika. Na njia hiyo ni hekima.
Hekima ni uwezo wa kipekee utokao kwa Mungu, unaomsaidia mtu kuweza kupambanua, au kutatua, au kuamua jambo Fulani vema. Hivyo kupitia hekima mtu anaweza kuponya vitu vingi pasipo uharibifu wowote, na kuunda mfumo bora.
Sulemani ambaye ndiye aliyeyaandika maneno hayo alijaliwa amani katika ufalme wake, sio kwamba hakuwa na maadui wanaomzunguka hapana, bali alipewa hekima ya kuishi nao, na kuzungumza nao, na kukubaliana nao, hivyo Israeli hakukuwa na kumwagika damu kama ilivyokuwa kwa baba yake Daudi, ambaye yeye kutwa kuchwa alikuwa vitani. Kilichoweza kumsaidia ni hekima ya Mungu ndani yake.
Lakini sehemu ya pili ya mstari huo anasema;
‘Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi’. Akiwa na maana mkosaji mmoja (wa hekima), jinsi anavyoweza kuharibu mipango mingi mizuri ambayo huwenda ilikuwa tayari imeshaleta matokeo mema. Na kweli hili angalia mahali penye viongozi wabovu, huathiri jamii nzima, hata Israeli, Wafalme wa kule ndio waliisababishia Israeli kunajisika kwa muda mrefu hadi kupelekea kwenda utumwani Babeli mfano wa hao walikuwa ni Yeroboamu na Ahabu.
Kwa ufupi vifungu hivi vinatueleza uzuri wa hekima, lakini pia madhara yasababishwayo pale hekima inapokosekana, hata kwa udogo tu.
Hekima chanzo chake ni kumcha Mungu. (Mithali 9:10). Ambapo panaanzia kwenye wokovu, kisha kuendelea kuishi maisha ya utii kwa Kristo baada ya hapo.
Mtu wa namna hii, huvikwa, ujuzi huo wa ki-Mungu, na hivyo anakuwa na uwezo wa kuutibu ulimwengu kwa namna zote. Mioyo, Ndoa,kanisa, jamii, taifa, vyote huponywa kwa hekima msingi huu wa hekima ya ki-Mungu.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.
Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?
USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.
1Nyakati 28:17 “na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa MATASA ya dhahabu, kwa uzani kwa kila TASA; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa”.
Ukisoma kuanzia juu utaona kuwa hivyo ni vyombo ambavyo vingepaswa viwepo ndani ya MUNGU aliyokusudia kuijenga Mfalme Daudi.
Lakini kwasababu haikuwa mapenzi ya MUNGU mfalme Daudi aijenge ile nyumba bali mwanae (Sulemani)…hivyo ilimbidi Mfalme Daudi ampe maelekezo ya namna ya kuijenga ile nyumba na viwango vyake.
Moja ya maagizo aliyompa kulingana na alivyooneshwa na Bwana ni uwepo wa MATASA ndani ya nyumba hiyo..(kwamba atakapoijenga basi aweke Matasa ya dhahahu ndani yake).
Sasa Matasa yalikuwa ni nini?
Matasa yalikuwa ni “Makarai/mabeseni” ya dhahabu yaliyowekwa ndani ya Hekalu kwa kusudi la kutawadha (kunawa).
Kwasababu ndani ya Hekalu kulikuwa na makuhani wengi waliokuwa wanafanya kazi mbalimbali na kwa zamu, na kulingana na desturi za wayahudi ilikuwa ni lazima kila Kuhani anawe
(atawadhe) kabla ya kuanza kazi ya kikuhani na hata baada ya kumaliza.
Hivyo vyombo hivyo (MATASA) vilitumika kuhifadhia maji kwaajili ya shughuli hiyo.
Na pia vilikuwepo VITASA hivi vilikuwa ni vibaluli vidogo vya kuweza kushikwa kwa mkono, tofauti na Matasa ambayo yalikuwa yanabeba ujazo mkubwa wa maji, na vitasa ndio vile vinavyotajwa katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana mlango wa 15 na 16.
Ufunuo 15:5 “Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; 6 na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu 7 Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba VITASA SABA vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele”.
Ufunuo 15:5 “Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa;
6 na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu
7 Na mmoja wa wale wenye uhai wanne akawapa wale malaika saba VITASA SABA vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu, aliye hai hata milele na milele”.
Ni nini tunajifunza katika hayo?
Tunachoweza kujifunza ni kuwa matasa ya Hekalu la duniani yalijaa maji ya kuoshea makuhani lakini vile VITASA vya Hekalu la mbinguni vimejaa hasira na hukumu ya MUNGU kwa wanadamu wasiomcha yeye.
Bwana atusaidie tumtafute, tusipotee wala kuangukia katika hukumu yake.
Maran atha.
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?
YAKINI NA BOAZI.
Je wakati Bwana YESU anazaliwa shetani alikuwa amefungwa?
Vihekalu vya fedha vya Artemi vilikuwaje? (Matendo 19:24).