Title November 2024

JE KUMWAMINI BWANA YESU PEKEE INATOSHA?

Swali: Neno la Mungu linasema Katika Yohana 3:18 na 36 ..amwaminiye mwana anao uzima wa milele, asiyemwamini hana uzima? .. Je kuna haja ya kutafuta jambo lingine tena baada ya kumwamini Bwana YESU?.


Jibu: Yapo maandiko katika biblia yanayokamilishwa na maandiko mengine, yako maandiko ambayo hayahitaji kukamilishwa na mengine kwani yanakuwa yamejitosheleza lakini yapo ambayo yanaelezwa kwa ufupi hivyo ni lazima yakamilishwe na maandiko mengine…

kwamfano andiko hilo la Yohana 3:18 na 36 ni kweli maandiko yanatuonyesha kuwa “tukimwamini Bwana YESU hatutahukumiwa bali tutapata uzima wa milele”.

Yohana 3:18 “AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu…..

36  Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Lakini tukirejea Marko 16:16 tunaona kuna jambo lingine linaongezeka..

Marko 16:16 “Aaminiye na KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa”.

Hapa kinachoongezeka ni “UBATIZO” Kwamba mtu akiamini pasipo kubatizwa bado hataurithi uzima wa milele, (ikiwa amesikia habari za ubatizo na hajataka kubatizwa).

Na ubatizo unaozungumziwa hapo sio ule wa MAJI TU, bali hata ule wa ROHO MTAKATIFU soma Luka 3:16.

Ili tuzidi kuelewe vizuri lugha hii, hebu tafakari kauli hizi mbili… “Ukipanda maharage utavuna maharage”… na kauli ya pili “Ukipanda maharage na kuyamwagilia maji utavuna maharage”.. Je kwa ni kauli ipi ipo sahihi kuliko nyingine?.. Ni wazi kuwa kauli zote zipo sahihi, isipokuwa ya pili imefafanua vizuri.. na inayofaa Zaidi ni hiyo ya pili, kwasababu ndio imekamilisha kauli ya kwanza.

Vivyo hivyo Neno linasema katika Yohana 3:18 kuwa amwaminiye YESU hatahukumiwa, lakini Marko 16:16, inakamilisha vizuri Zaidi kwamba Amwaminiye YESU na kubatizwa hatahukumiwa..Kwahiyo ya pili ni ya nzito Zaidi kwasababu imeikamilisha ile ya kwanza.

Sasa kwanini Imani pekee yake haitoshi ni lazima kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu??

Jibu: Kwasababu hata Mashetani yanaamini lakini bado hayana wokovu..

Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda VEMA MASHETANI NAO WAAMINI NA KUTETEMEKA.

20  Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai”

Kwa hitimisho ni kwamba “IMANI YA KUMWAMINI BWANA YEESU ni LAZIMA IENDE NA MATENDO”.. Na tendo la kwanza ni hatua ya ubatizo wa Maji na nyingine ni ya Roho Mtakatifu.

Mtu anapomwamini Bwana YESU na kubatizwa kwa maji na kwa Roho anakuwa amekamilika, na kukidhi vigezo vya kuuona ufalme wa Mungu, kwani maana pia ya kuzaliwa mara ya pili ni kuzaliwa kwa maji na kwa ROHO.

Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU.

6 KILICHOZALIWA KWA MWILI NI MWILI; NA KILICHOZALIWA KWA ROHO NI ROHO.

7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.


Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

UMUHIMU WA KUBATIZWA.

TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;

DHAMBI YA ULIMWENGU.

Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya neno kumwamba (Zaburi 78:19)

Zaburi 78:18-19

[18]Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao. [19]Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani? 

Kumwamba kama ilivyotumika hapo ni “kuzungumza kinyume”

Hivyo hapo anaposema 

“Naam, walimwamba Mungu, wakasema, Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?”

Ni sawa na kusema..

Naam, walizungumza kinyume na Mungu, wakisema Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?

Wana wa Israeli kule jangwani, vinywa vyao havikuwa vya shukrani au vya kuomba, bali vivywa vya kumjaribu Mungu na manung’uniko, ijapokuwa walijua uweza wake wote, lakini walijifanya kama Mungu wao hawezi kuwaokoa, wakawa wanauliza maswali yaliyoonekana magumu, kumbe nafsini mwao wanajua yote yanawezekana, wanafanya tu makusudi ili waone Yehova atafanya nini. Na ndio sababu iliyomfanya Mungu asipendezwe nao.

Na sisi pia tusiwe watu wa kumwamba Mungu, kwa kusema maneno ya kutoamini.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Kama Musa aliandika vitabu vya torati, Je! kifo chake alikiandikaje mule?

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?

Rudi Nyumbani

Print this post

JIFUNZE KWA SHUJAA YAELI.

(Ukarimu na maziwa)

Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mwokozi wetu. Karibu tujifunze maneno ya uzima. Haya ni mafunzo maalumu kwa ajili ya wanawake. Ikiwa utatamani kupata mengine mengi basi fungua link hii.. uweze yasoma..

https://wingulamashahidi.org/2021/07/21/masomo-maalumu-kwa-wanawake/

Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia, utakumbuka ile habari ya Debora na Baraka katika kitabu cha waamuzi.

Habari ile inaeleza jinsi Israeli ilivyo nyanyaswa na kutumikishwa  na maadui zao wakaanani kwa muda wa miaka ishirini, chini ya mfalme mmoja aliyeitwa Yabini, na jemedari wake mkali aliyeitwa Sisera.(Waamuzi 4)

Watu hawa walikuwa wameendelea sana kivita, hivyo Israeli hawakuweza kufanya lolote isipokuwa kukubali mateso, ndipo wakamlilia Bwana sana. Naye akawasikia akawainulia mtetezi. Ndio huyu Debora nabii pamoja na baraka shujaa wa Israeli.

Sasa huyu Sisera alikuwa ni jemedari kwelikweli, hata Neno la Mungu lilipomjilia Debora, kumwagiza Baraka jemedari wa Israeli, akapange vita nao, bado alisita, na alichofanya ni kuomba Debora aende naye vitani..

Ni jambo ambalo ni kinyume na asili, wanawake kuhusishwa kwenye vita, kwasababu hiyo Debora akapewa Neno na Bwana kwa Baraka..kufuatana na wazo lake la kutaka.mwanamke aende naye vitani..kuwa ushindi huo hautakuwa mkononi mwake bali mkononi mwa mwanamke.

Waamuzi 4:8-9

[8]Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. 

[9]Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi. 

Na kweli tunaona walipokwenda vitani kupigana nao. Yule Sisera jemedari wao, alifanikiwa kutoroka..Alipokuwa anakimbia alimwona mwanamke mmoja aliyeitwa Yaeli. Mwanamke huyo alimkaribisha kwake kwa ukarimu wa hali ya juu sana. Akampeleka sehemu ya maficho kabisa mahali ambapo si rahisi kugundulika, tena akamfunika ili kumuhakikishia ulinzi wote, 

Jambo lile la ukarimu usio wa kawaida lilimtuliza moyo Sisera, akajihisi kama amepona, ndipo akamwomba yule mwanamke maji kidogo anywe. Lakini yule mwanamke bado akaendelea kuonyesha ukarimu wa hali wa juu sana, akaenda kumletea MAZIWA badala ya MAJI.. Pengine akamwambia aah! bwana wangu, maji si mazuri ukiwa umefunguka tangu asubuhi, tena kwenye mbio na pilika pilika za vita, kutumia maji si vizuri kiafya,  kunywa kwanza maziwa haya, mwili uchangamke, upate nguvu, ndipo baadaye nitakupa maji unywe.  

Sisera kuona vile akaendelea ku-relax, zaidi kuona ukarimu wa ajabu wa yule mwanamke, akafanya kosa akanywa yale maziwa, yakamlewesha kwa haraka mpaka akapotelea usingizini akasahau kabisa kwamba yupo vitani anatafutwa.

Lakini mwanamke Yaeli alipoona shujaa Sisera amelala fofofo, akasema nimempata adui yetu, sasa  ninakwenda kumuua kirahisi kabisa.Akaenda kuchukua msumari mrefu, na nyundo. akavielekezea kichwani, akaupigilia ukaingia wote kichwani. Na mwisho wake ukawa umefikia pale pale.

Hata baadaye Baraka anakuja akakuta tayari mtu ameshakuwa marehemu.

Waamuzi 4:17-21

[17]Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni. 

[18]Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti. 

[19]Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika. 

[20]Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana. 

[21]Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa. 

Ni nini Kristo anataka wanawake wafahamu kwa ushujaa wa Yaeli? (Ni ukarimu na Maziwa)

Kumbuka vita vyetu sisi si juu ya damu na nyama, bali dhidi ya wakuu wa giza hili na ibilisi. Na mtu yeyote ambaye anahubiri injili, mtu huyo ni askari wa Bwana. Mfano wa akina Debora, na Baraka. Haijalishi jinsia yake ni ipi, wote ni watendakazi katika shamba la Bwana.

Lakini kama tunavyojua Mungu ameweka majukumu mbalimbali ndani ya mwili wa Kristo, wewe kama mwanamke hujaitwa kuwa mchungaji, au askofu, lakini umeitwa kuwa shujaa wa kumwangamiza adui kwa karama uliyopewa.  Debora na Yaeli hakuwa kama Baraka, maumbile yao hayakuumbwa kusimama na mikuki na ngao, na kukimbizana maporini usiku na mchana na maadui. Hapana.. bali ni kuwa katika utulivu. Na utulivu ukitumiwa vizuri huleta mlipuko mkubwa kuliko wingi wa makombora ya vita.

Aliyemuua shujaa Sisera alikuwa mwanamke, aliyekuwa nabii wa Israeli alikuwa mwanamke. Ushindi ulipatikana kwa mikono ya wanawake. Lakini bila kuvaa suruali, na mitutu vya vita.

Hata leo, ikiwa mwanamke ataitambua vema kazi ya injili kwa kufuata kanuni za kibiblia anaouwezo wa kuwavua watu wengi kwa Kristo zaidi hata ya mhubiri wa kusimama kwenye majukwaa makubwa.

Ukarimu, kwa wenye dhambi, upendo wa waliotekwa na mwovu, pamoja na maziwa (Ndio Neno la Mungu) ni Njia hii ya YAELI, ukiitumia itakufanya uwavute wale watu kwa Kristo wengi, na hatimaye kanisa la Kristo kukua na kuongezeka.

Ni watu wangapi unaweza wafadhili kichakula huku unawahubiria injili, unaweza wapelekea mavazi huku unawafundisha habari za Kristo, unaweza wafadhili kwa chochote huku unawaalika kanisani..kidogo.kidogo, upo kazini kwako, unazungumza nao kwa ukarimu, unawasaidia majukumu ambayo wangepaswa wayafanye wao wenyewe lakini wewe unawasaidia, lengo lako ni uwavute katika imani, huku ukihakikisha unawapa na maziwa, yaani maneno ya faraja ya Mungu,(1Wakorintho 3:2, 1Petro 2:2).

Wewe ni mamantilie, wateja wako, unawapa zaidi ya huduma, huku unawafundisha habari za Kristo, unawaeleza uzuri wa kukusanyika kanisani, n.k.

Ukiendelea hivyo baada ya kipindi fulani utashangaa watu hao wanavutika kwako, na kwa Kristo. Hata yule mpinga-kristo aliyekuwa na moyo mgumu kuliko wote anaokoka, yule boss wako ambaye alikuwa hataki kusikia masuala ya Mungu anaokoka. Wale ambao walirudi nyuma, wanaamka tena.

Onyesha tu ukarimu, lakini usiwe ukarimu wa bure, huo hautazaa chochote bali wenye injili nyuma yake.

Hivyo wewe kama mwanamke/binti wa kikristo simama katika eneo la utulivu, kiasi, kujisitiri, ni ukweli utaziangusha ngome sugu za adui.

1 Petro 3:1-5

[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 

[2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 

[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 

[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 

[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?

Maana ya Mithali 30:33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi

Rudi Nyumbani

Print this post

msalaba ni nini.

Msalaba ni kipande cha mti, kilichochongwa kwa kupishanishwa na kingine kwa juu. chenye lengo la kumuulia mwanadamu kwa kifo cha mateso.

Tofauti na sasa, ambapo adhabu nyingi za kifo kwa mataifa mbalimbali huwa ni kunyongwa, au kupigwa risasi, au kuwekwa kwenye kiti cha umeme, n.k.. Lakini katika falme za zamani watu waovu kupita kiasi, kwamfano wauaji, au wenye makosa ya uhaini, adhabu yao, ilikuwa ni kutundikwa au kugongelewa pale msalabani mpaka ufe. Ni mateso ambayo utataabika hapo kwa saa nyingi sana kabla ya kufa, hata siku mbili.

Hivyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema msalaba ni chombo cha kuulia mtu.

Kwetu sisi tuliomwamini Kristo. Msalaba ni ishara kuu ya ukombozi tulioupata kwa kifo cha mwokozi wetu. Kufahamu kwa undani ni kwanini fungua link hizi; usome..

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Nini maana ya sulubu/ sulubisha?

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> 

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.


Mafundisho mengine:

Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?

Print this post

Kaati na Nungu ni viumbe gani? (Isaya 34:11)

Isaya 34:11 “KAATI na NUNGU wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu”.

Jibu: “Kaati” ni “bundi wa jangwani” (wanaoishi majangwani), na chakula chao ni jamii za panya na wadudu..Tazama picha chini.

bundi wa jangwani

“Nungu” ni aina nyingine ya bundi wanaopatikana katika misitu yenye miti iliyozeeka, yenye matundu. Aina hii ya bundi hutoa mlio mkali wakati wa usiku wanapowasiliana na jamii zao, na ndio wanaosikika katikati ya jamii za watu (Tazama picha na video chini).

nungu

Lakini swali ni je? Bundi hawa (Kaati na Nungu) ni roho za kichawi/majini?.

Jibu ni la!.. Bundi ni ndege tu kama ndege wengine walioumbwa na Bwana MUNGU, kama wakiwa katika mazingira yao ya asili, ni ndege tu kama ndege wengine, wanaohitaji pia kutunzwa.

Lakini pia ndege hawa wanaweza kutumika na wachawi katika shughuli za kichawi, kama tu vile kuku anavyoweza kutumiwa katika kafara za kichawi, na bundi ni hivyo hivyo, ila kwa mtu aliyeokoka hakuna silaha yoyote yenye uhai, au isiyo na uhai itampata.

Lakini kwa mtu aliye nje ya KRISTO, basi ni haki yake kuogopa bundi, na viumbe wengine kwani ni kweli yupo hatarini kudhuriwa na ibilisi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Je! Ni dhambi kumpiga au kumuua mnyama bila sababu yoyote?

Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya “Hefsiba” na “Beula” (Isaya 62:4)?

Jibu: Tuirejee.

Isaya 62:4 “ Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Hii ni habari ya tumaini la kuinuliwa tena kwa Yerusalemu na Israeli kwa ujumla, Kwamba siku ile watakapomrudia Bwana kwa mioyo yao yote basi nchi yao hiyo Bwana aliyoikataa na kuiacha na kuifanya UKIWA, basi ataibarikia tena na kuifanya kuwa FURAHA yake na ILIYOOLEWA.

Sasa tafsiri ya Hefsiba na Beula tayari imeshatolewa pale..  Hefsiba/Hefziba maana yake ni “Furaha yangu iko kwake” na Beula maana yake ni “Aliyeolewa”.. Haya ni maneno ya kiebrania yenye tafsiri hiyo. Hali kadhalika tafsiri ya “Aliyeachwa” kiebrania ni “Abuba” na “Ukiwa” ni “Shemama”..

Kwahiyo kinyume cha aliyeachwa (Abuba) ni Hefsiba (furaha yangu iko kwake)…. Na kinyume cha shemama(ukiwa) ni aliyeolewa(Beula). Ni majina ya kiebrania yaliyotumika kwa jinsia ya kike (soma 2Wafalme 21:1)

Sasa swali kwanini Mungu atumie lugha hizo za “ndoa” kuzungumza na watu wake?.

Ni kwasababu watu wa Mungu wote kiroho wanafananishwa na “mwanamke aliyeolewa/bibi arusi”

Isaya 54:4 “Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.

5 KWA SABABU MUUMBA WAKO NI MUME WAKO; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote. 

6 Maana Bwana amekuita KAMA MKE ALIYEACHWA na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. 

7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya”.

Soma pia Yeremia 31:31-32, 2Wakorintho 11:2 na Ufunuo 21:9 utazidi kuliona jambo hilo..

Kwahiyo ujumbe huo haukuwa kwa Israeli peke yao, bali pia unatuhusu sisi, kwamba tumrudiapo Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, basi tunazo ahadi za Baraka na mafanikio, na majina yetu kiroho yatabadilika na kuwa Hefsiba na Beula…Na furaha ya Bwana itakuwa juu yetu nasi tutakuwa na muunganiko wa kiroho na Bwana YESU.

Isaya 62:1 “Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 

2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.

3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 

4 Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

Rudi Nyumbani

Print this post