Title 2024

USIIGE TABIA YA NAAMANI

Unajua Kwanini Naamani atake kuingia tena katika nyumba ya Rimoni baada ya kuponywa? (2Wafalme 5:18)

Turejee..

2Wafalme 5:18 “Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili”.

Katika kitabu hiki cha 2Wafalme 5, tunasoma uponyaji wa mtu mmoja aliyeitwa Naamani, aliyekuwa Jemedari wa jeshi la mfalme wa Shamu. Lakini huyu Naamani alikuwa ni mtu mwenye ukoma ingawa alikuwa shujaa wa vita.

Siku moja alienda kutafuta uponyaji kutoka kwa Mungu wa Israeli, kupitia taarifa alizozipitia kutoka kwa kijakazi wake aliyekuwa Mwishraeli kwa asili, na alipokutana na Nabii Elisha, kwa uongozo wa Roho wa Mungu aliagizwa akajichovye katika mto Yordani mara saba na ugonjwa wake (wa ukoma) utaondoka.

Mwanzo alikataa lakini baadaye alikubali na Bwana MUNGU akamponya ule ukoma, na ngozi yake ikarudi kama ya mtoto mchanga.

2Wafalme 5:14 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi”.

Kwa uponyaji huo alioupata aliahidi kutotoa tena sadaka kwa miungu aliyokuwa anaitumikia hapo mwanzo ambayo haikumsaidia kitu. (na mungu aliyekuwa anamtumikia hapo mwanzo kabla ya kuponywa na Bwana alikuwa anaitwa rimoni) .

2Wafalme 5:17 “Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.

Lakini pamoja na ahadi hiyo, aliona tatizo moja mbele yake..

Alijua atakaporudi kwa mfalme, bado atakuwa chini ya mfalme kama jemedari wake, na mara zote alikuwa anaongozana naye kuingia katika hekalu la mungu rimoni, naye pia alikuwa anasujudu.. Hivyo akajua atakaporudi hiyo desturi itaendelea.

Kwahiyo akatangulia kuomba radhi kwamba endapo jambo hilo likitokea basi Mungu amsamehe (yaani amwachilie), kwasababu hajadhamiria kufanya hivyo isipokuwa tu ni kwa kutimiza matakwa ya mfalme, lakini yeye ndani ya moyo wake au kwa hiari yake mwenyewe hajakusudia kumtolea mungu rimoni sadaka wala kumsujudia..

Hivyo Elisha akamruhusu aende na afanye kama anayoyaona moyoni mwake.

Ni jambo gani tunalojifunza?..

Ni kweli kwa Naamani tunajifunza Imani ya kupokea uponyaji baada ya kukubali mashauri, kwani kitendo cha kuamini tu taarifa kutoka kwa kijakazi, hiyo ni Imani kubwa, (kwamaana si wote wanaweza kuwasikiliza na kuwaamini watu walio chini yao kiuwezo, kielimu na hata kiufahamu), lakini Naamani aliweza hilo..Na hata sisi ili tuvute msaada wa Mungu na muujiza wake ni sharti tuwe watu wa Imani kama Naamani.

Na ndio Bwana YESU anakuja kurejea habari ya Imani yake katika kitabu cha Luka 4:27

Luka 4:27 “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.”

Lakini pamoja na hayo pia, lipo ambalo hatupaswi kujifunza kwa Naamani,..

NAAMANI MOYONI ALIMKIRI MUNGU WA ISRAELI kwa muujiza aliofanyiwa LAKINI KWA MATENDO ALIMTUMIKIA MUNGU RIMONI kwa heshima ya Mfalme.

Kwahiyo alikuwa ni VUGUVUGU..Moyo wake upo kwa Mungu wa Israeli,…lakini viungo vyake na utumishi wake upo kwa rimoni (mungu wa nchi yake).

Mfumo wa nchi yake ulimbana!, kazi aliyoifanya ilimfunga!..ijapokuwa alikuwa anatamani kweli kutotumika katika hekalu la mungu ambaye hakumsaidia, lakini tayari alikuwa ameshafungwa Nira, na hakuwa tayari kuikata hiyo nira.

Katika kitabu kile cha 2Wakorintho 6:15 Neno la Mungu linasema, tusifungwe Nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa.

2Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15  Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16  Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha”

Na sisi kama wakristo ni lazima tutoke katika mahekalu ya sanamu, ni lazima tutoke katika kazi zinazotulazimu kusujudia sanamu au kumwabudu shetani, ni lazima tuache makundi yanayoturudisha kumwabudu shetani.

Ni kweli inagharimu, lakini hiyo ndio maana ya “kuubeba msalaba na kujikana nafsi”, kama kazi inakuuzisha pombe, au mwili wako, au inakuabudisha sanamu…IACHEEE!!. Ili uondokane na uvuguvugu. Kwasababu Bwana YESU alisema atawatapika wale wote walio vuguvugu.

Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16  Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.

Orodha ya Miji ilivyojulikana Agano Jipya na inavyojulikana sasa

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi Nyumbani

Print this post

KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima.

Katika nyakati hizi za hatari na udanganyifu mwingi, ni vizuri kujichunguza sana, ni Roho ipi umeipokea ndani yako. Kwasababu tabia unazozionyesha ni matokeo ya roho iliyopo nyuma yake, ikiwa wewe ni mpenda dunia basi roho ya dunia ipo ndani yako.

1Wakorintho 2:12  Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

Vivyo hivyo ukijiona wewe ni mwizi, ujue roho ya wizi ipo nyuma yako.

Lakini maandiko yanasemaje kuhusu Danieli?

Yanasema ROHO BORA ilikuwa ndani yake.

Danieli 6:3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote

Maana yake ni kuwa Roho iliyozidi viwango, ndio iliyokuwa ndani yake.. Unajua mpaka inasema bora, maana yake zipo ambazo hazina ubora, kwa tafsiri nyingine “feki”, zenye mfano wa ile orijino. Ndicho shetani anachokibuni sana, ili awapoteze watu, wadhani wanaye Roho Mtakatifu, kumbe ni bandia.

Sehemu nyingine, inasema “Roho njema kupita kiasi”. Ilikuwa ndani yake..

Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.

Umeona sifa ya roho hiyo ni lazima iwe ya ‘kupita kiasi’, sio ya kawaida, vinginevyo ni feki. Sifa za Roho wa Mungu, anapita kiasi. Katika ubora na wema.

Ndio iliyomfanya Danieli awe mkamilifu kama tunavyomsoma kwenye maandiko. Kiasi cha watu kutafuta kosa ndani yake, bila mafanikio.

Danieli 6:4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.

Na mtu yeyote anayesema ameokoka,  Roho hii naye ni lazima imkalie. Roho iliyo bora, na njema kupita kiasi. Uthibitisho wa kwanza wa Roho uliyempokea ni Roho Mtakatifu, atakusukuma, kuwa Mtakatifu kama jina lake lilivyo.

Lakini iweje tunasema, tumepokea Roho, tunanena kwa lugha usiku kucha, tunatabiri, lakini Ubora wa huyo Roho hauonekani ndani yetu? Cha kushangaza utaona  huyo mtu anasema haiwezekani kuishi maisha matakatifu hapa duniani, ndio hapo tunamhubiri Kristo, wakati huo huo, tunaishi kidunia, tunafunga na kuomba wakati huo huo, tunavaa ovyo ovyo, tunaabudu pamoja lakini chini kwa chini tunavisasi na vinyongo. Tunatoa sadaka lakini nyuma kwenye biashara zetu ni za rushwa rushwa.

Je! Hiyo ni Roho bora?  Au imechakachuliwa?. Tumepewa ruhusu ya kujipima (1Yohana 4:1). Jihakiki, tangu ulipookoka hadi leo je, kuna mabadiliko yoyote ndani yako? Kama huna ni aidha ulimzimisha alipokuwa anaugua ndani yako ugeuke, au huna kabisa Roho Mtakatifu.

Habari njema ni kuwa Roho bora, ukimwita, huja ndani yako, au huamka tena. Ni wewe kuamini, na kutii kwa moyo wako wote. Kuwa tayari kuacha vyote(vya kidunia), na kumgeukia yeye. Na hatimaye atakuongoza na kukuweka sawa. Lakini sharti kwanza uaminifu kuwa utakatifu unawezekana, lakini pia ulimwengu utaukana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

Rudi Nyumbani

Print this post

Sheshaki ni wapi? (Yeremia 25:26)

Swali: Sheshaki inayotajwa katika Yeremia 25:26  ilikuwa ni wapi?


Jibu: Turejee..

Yeremia 25:26 “na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na wafalme wote wa dunia, wakaao juu ya uso wa dunia; na MFALME WA SHESHAKI atakunywa baada yao.

27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu”.

“SHESHAKI” ni jina lingine la Taifa la “Babeli”. Kama vile “YESHURUNI” ilivyo jina lingine la Taifa la Israeli.

Kumbukumbu 33:26 “Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake”.

Soma pia Kumbukumbu 32:15 na Isaya 44:2, utaona Zaidi kuhusu Yeshuruni, na kwa urefu Zaidi fungua hapa >> Yeshuruni ni nani katika biblia?

Na vivyo hivyo na “Babeli”, jina lake lingine aliitwa “Sheshaki”… Majina haya yalitumika mara nyingi kwenye mashairi na methali za kiyahudi. Utalisoma jina hilo tena katika Yeremia 51:41, ambapo imetaja kwa uwazi kuwa ni Babeli.

Yeremia 51:41 “Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa! Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa! Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa katikati ya mataifa.

42 Bahari imefika juu ya Babeli, Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.

43 Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu ye yote, Wala hapiti mwanadamu huko”.

Je Umeokoka?.. kama bado unasubiri nini?..

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:

Babeli ni nchi gani kwasasa?

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

UFUNUO: Mlango wa 18

Rudi Nyumbani

Print this post

HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.

Bwana ametupa agizo na wajibu wa kwenda kuihubiri injili ulimwenguni kote, na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake.(Mathayo 28:19)

Alisema pia mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache. Ikiwa na maana lengo lake ni yeye apate mavuno mengi kutoka kwetu. Lakini huwenda tukaona sisi ni shida, kufanya hivyo.

Hata kama itakuwa kwetu ni shida kuvuta watu, bado Yesu anaona ni rahisi kwetu..Kwani mahali pengine alisema mashamba yameshakuwa meupe tayari kwa mavuno, wapo ambao tayari walishayataabikia, sisi ni kumalizia tu. Hivyo ni rahisi sana.

Lakini ili injili yetu itoe matokeo aliyoyakusudia, yatupaswa tujifunze kanuni zote za kiuinjilisti na kuzitumia, kisha  miongoni mwa hizo Bwana azitumie kuleta matokeo yake. Kuliko kutegemea kanuni moja tu Fulani na kupuuzia nyingine.

Ni sawa na mvuvi ambaye anashikilia  uvuvi wa ndoano tu, lakini hajui kuna wa nyavu, au wa mkuki au wa kutegea, lakini pia kuna wa majira mbalimbali ya kuvua, kuna ya usiku, au ya mchana.

Na sisi katika utumishi wetu wa kuwavuta watu kwa Yesu, tufahamu pia njia zote.

Sasa kibiblia zipo kanuni kuu (8), zinazovuta watu.

1) Kutangaza/Kushuhudia.

Hii ndio njia kuu na ya kwanza, ambayo ndio inasimama kama uti wa mgongo wa uinjilisti. Kwamba ni sharti kila mmoja wetu atumie kinywa chake, ujuzi wake, elimu yake, ufahamu wake, kumuhubiri Kristo kwa watu kwa namna yoyote. Utashuhudia shuleni, nyumba kwa nyumba, masokoni, barabarani, vijiweni, mitandaoni n.k. Ni agizo la Bwana na linapaswa lifanywe na wote.

2) Kuangaza Nuru.

Mathayo 5:16

[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Wapo watu si rahisi kugeuka kwa kusikia unawaelezea habari za Yesu, ni rahisi kugeuka wanapomwona yule anayewahubiria mwenendo wake ni tofauti na wa kwao. Na hilo likamchoma moyo na kumfanya amgeukie Kristo moja kwa moja.

Hivyo angaza mwenendo wako, kwa watu, ikiwa hawataamini kwa lile Neno, basi waamini kwa mwenendo wako mzuri.

1Petro 3:1  Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2  wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu

3) Kujichanganya.

Ni ile hali ya kujaribu kuchukuliana na mawazo ya wale watu, na wakati mwingine hali zao, kana kwamba ni mmojawao, kisha kutumia fursa hiyo kuwaeleza habari za Yesu. Wengine huvitiwa kwanza na jinsi unavyothamini hali zao, sio kwa jinsi unavyo eleza vema Neno au mwenendo wako. Ni njia ambayo aliitumia Paulo na ikamletea matokeo mengi sana ya waongofu.

1Wakorintho 9:19  Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.

20  Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.

21  Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.

22  Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.

23  Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

Zingatia kujichanganya sio kushirikana na dhambi zao, hapana, bali kuwepo katikati yao ili kuwaondoa huko, huku wewe mwenyewe ukijilinda nafsi yako usitekwe na dhambi zao.

4) Kuifuata dira ya Roho Mtakatifu.

Unaweza kudhani kila eneo unaweza kuhubiri na kuleta matokeo unayoyatazamia. sio kweli, Mitume walivua samaki usiku kucha lakini hawakupata kitu, baadaye Yesu akawaambia tupeni jarife upande wa kuume mtapata (Yohana 21), sehemu nyingine aliwaambia waende vilindini. Na walipofanya vile walipata samaki wengi. Paulo mwanzoni aliegemea injili yake kwa wayahudi sana, akapitia ukinzani, lakini kumbe Mungu alimkusudia aende kwa mataifa, na alivyotii agizo lile matokeo yakawa makubwa. (Matendo 22:21)

Hivyo ni muhimu kuomba Bwana akupe dira, lakini pia katika kuhubiri kwako utaona eneo Fulani lina matunda mengi, basi ujue hapo ni dira yako. Au njia Fulani ukiitumia wengi huvutiwa kwa Kristo, basi fanya hivyo. Lakini hili ni kuendelea kuomba na kuhubiri Mungu mwenyewe ataielekeza dira yako, kama ni hapo au kwingine, kama ni njia hiyo au njia nyingine, la kuzingatia  ni kuwa mwepesi kutambua upepo wa Roho unakufanikisha wapi. Kisha ongeza nguvu nyingi sana hapo, kuliko kule kwingine.

5) Ishara na miujiza

Yapo makundi ambayo, Mungu anajua yakiona tu muujiza au ishara fulani huvutika kirahisi. Na hili pia ni eneo la kumwomba Bwana, ajalie kunyosha mkono wake kuponya maana lina mvuto mkubwa na wa haraka sana.

Kanisa la kwanza liliomba maombi ya namna hiyo.

Matendo 4:29  Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 30  ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu

Hivyo popote uendapo pia hakikisha unawaombea na watu, shida zao. Kwasababu kwa njia  hiyo Roho Mtakatifu hupata nafasi ya kupenyeza mvuto huo, kwao.

6) Busara.

Busara ni  namna nzuri kunena, hadi kuushawishi moyo wa mtu. Bwana Yesu anataka na sisi tujae busara ndani yetu aliyoifananisha na kama ile ya nyoka.

Mathayo 10:16  Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

Nyoka alijua akimwendea Hawa kwa ukali, au kulazimisha isingewezekana, lakini alijishusha na kujifanya kama mtu wa mashauri, afichuaye siri, Jambo ambalo ni uongo. Na sisi hatuna budi kujua kunena kwa hekima, ili wale tuwahubirio tuishawishi mioyo yao, mpaka kumgeukia Kristo ambaye ndiye kweli.  Tujifunze kueleza uzuri wa Yesu. Lakini pia tusiwe watu wa kauli mbaya kwa tunaowahubiria hata kama watatupinga.

7) Kujihatarisha: 

Kuna la watu hatutaweza kulipata kama hatutaingia gharama kubwa kwa ajili yao. Wakati mwingine hata kuhatarisha  maisha. Kwasababu mahali walipofungwa na adui, pana ngome nzito. Mfano wa hawa ni wale waliofungwa katika vifungo vikali sana vya kidini.

Kuwang’oa huko ni kujiandaa na dhiki. Cha kuomba hasaa hapa kwa Mungu ni ujasiri kwa kanisa la kwanza lilivyoomba.

Hichi ndio kilele cha juu kabisa cha kiuinjilisti. Ndio wito Yesu aliowaitia mitume wake utakaowafanya wafikie kona zote. Kuwa tayari kufa kwa ajili ya walio dhambini. Ndio maana si wote waliweza kuambatana nao, Bali walibakia tu kuwaadhimisha.

Matendo 5:12  Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;

13  na katika wote wengine hapana hata mmoja aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha;

8) Maombi.

Kuna wengine si rahisi kuokoka ki-uinjilisti tu, bali pia kuwaombea. Hii ni njia inayolegeza  nira za mwovu mioyoni mwa watu. Injili yako inaweza isiwe na shida lakini mioyo yao ya jiwe ikawa vile, hata uhubirije hawewezi kukuelewa.

Paulo alikuwa ni mtu wa kuwaombea sana watu wake wayahudi waokolewe. Maandiko yanasema ombeaneni ninyi kwa ninyi mpate kuponywa.

Warumi 10:1  Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.

2  Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.

Usione shida kuwaombea ndugu zako ambao hawajaokoka, wafanyakazi wenzako, majirani zako, jamii yako n.k. Ni maombi yasiyo  na ukomo fanya hivyo kila siku, maombi yako ni silaha kubwa sana ya kiuinjilisti.  Lakini usiombe tu na kukaa ukasema namwachia Bwana. Hapana unawaombea na huku unawahubiria.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, tukijifunza njia zote hizi, na kuziachilia katika maisha yetu ya kiutumishi ni hakika kuwa lipo kundi litaokoka tu.  Lakini kutegemea njia moja peke yake huubana utendaji kazi wa Roho Mtakatifu ndani yetu, . Ukihubiri changanya na hizo nyingine, kisha yeye aamue ni ipi itamvuta mtu kwa wakati huo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

UFUATILIAJI NI SEHEMU YA HUDUMA MUHIMU KWENYE UINJILISTI

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

JE UMEUPOKEA UWEZA WOTE WA UUNGU NDANI YAKO?

2 Petro 1:3

[3]Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 

Kuna mambo makuu sana ya kujifunza ndani ya vifungu hivi;

Hapo tunaonyeshwa kuwa Mungu anao Uweza wake. Kama vile tu mwanadamu alivyo na uweza wake usiokuwa sawa na mbwa. Kwamfano mwanadamu anaweza kuunda silaha, ambayo inaweza teketeza mji mzima kwa maarifa yake. Anauwezo wa kuruka angani zaidi ya kiumbe chochote duniani kwa vyombo alivyovibuni, anaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali sana hata na kuona uso wake kwa vyombo vya mawasiliana alivyojibunia.Mambo ambayo mnyama hawezi. Huo ni uweza wake wa kibinadamu.

Vivyo hivyo na Mungu wetu, anao uweza wake wa uungu, ambao ametukirimia sisi, Tunapoupokea huo  tunakuwa na sifa kama zake.

Ndio hapo anasema…

“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

Lakini sasa nataka uone hapo uweza huo umeshushwa juu yetu, si katika kila kitu bali  katika mambo mawili makuu.

1) La kwanza ni uzima.

2) la pili utauwa.

Yaani mambo yote yanayohusiana na uzima wetu, ametuwezesha yeye mwenyewe. Ndio maana kwa kumwamini Yesu tunapokea msamaha wa dhambi. Tunakuwa tumevuka kutoka  mautini kuingia uzimani. Hatuangamii, tunakuwa na uzima wa milele ndani yetu.

Kwasababu Hatuna kifo ndani yetu, tunalala tu, kupumzishwa ili baadaye tuamshwe. Lakini Uzima huu hauwezi kuupokea kwa juhudi zako, au kwa elimu yako, au kwa matendo yako mema, au kwa dini yako nzuri, hapana..Ni zawadi ya Mungu kupitia Kristo Yesu. Pale unapomwamini tu, unapokea msamaha wa dhambi zako, kwa neema, huu ni uweza wake wa ajabu, ambao wanadamu wanausumbukia hawaupati, kwasababu mwanadamu hana matendo mema ya kutosha kuununua uzima. Isipokuwa Yesu tu peke yake alitununulia kwa damu yake.

Yohana 3:36

[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. 

Lakini sio tu Uzima, uweza huo umetukirimia pia na katika Utauwa wote. Utauwa ni utakatifu. 

Mtu ambaye hajaokoka hawezi yatoa maisha ya utakatifu ndani yake. Vinginevyo atajitahidi sana kwa kuutumikisha mwili kwa nguvu, na hatimaye atashindwa, au atafanya kinafki kama mafarisayo na waandishi, ambao walikuwa wananena mambo ambayo hawayatendi,.kwasababu uweza huu haukuwa ndani yao.

Utauwa haswaa ni kazi ya Mungu mwenyewe mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu. Ni pale mtu anapompokea Kristo kama mwokozi wake, kisha kukubali kumtii, kwa kujikana nafsi yake. Ndio hapo hapo yeye mwenyewe anakuongezea nguvu, ambayo inakufanya uyakimbie yale maisha ya kale ya dhambi. Lakini kumbuka hiyo inakuja kwa kukubali kumtii Yesu, kukubali kuwa kiumbe kipya. Wakristo wengi wanataka Bwana awasaidie lakini hawataki kujikana nafsi zao wasaidiwe na Bwana. Ukimpokea kwa mdomo tu uweza huu hautakuwa na matunda ndani yako. Lakini ukiwa ni wa geuko la kweli, uweza huo ni lazima utende kazi ndani yako.

Utaweza kushinda zile dhambi ambazo ulikuwa huwezi ziacha.

Yohana 1:12

[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 

Unaposema Yesu ni BWANA wangu. Ni lazima, ujue unajifanya kuwa mtumwa wake.. sikuzote bwana yoyote humiliki mtumwa, chochote anachoagizwa.huwa ni amri kwake sio ombi. Kumbali kuongozwa na Yesu, acha kabisa wokovu wa mdomoni.

Kama mkristo, kuwa mtakatifu ni lazima sio chaguzi, ndio kitambulisho chako kuwa umepokea uzima wa milele. Kwasababu pasipo huo huwezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14).

Hakikisha uweza wote huu umeupokea ndani yako. Usiseme hicho kingine cha utakatifu hakinihusu, vinginevyo utakuwa hujakamilika

Shalom.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.

Je! Utatu mtakatifu upo kibiblia?

Rudi Nyumbani

Print this post

MKATAE MWAJIRI HUYU MBAYA.

Hebu tengeneza picha umeajiriwa, halafu aliyekuajiri anakutumikisha kwa mateso makali na mwisho wa siku anakulipa mshahara wa kifo!, Je kabla ya kuanza hiyo kazi, utakubali kutia sahihi mkataba huo??

Bila shaka kwa mtu mwenye akili timamu, hawezi kukukubali.

Lakini ajabu ni kwamba Zaidi ya nusu ya wanadamu wa kizazi chetu, wametia sahihi na huyu boss, ambaye anawatumikisha halafu anawalipa mshahara wa kifo. Je unataka kumjua huyu boss mkatili, na tena mwenye mshahara mbaya wa kifo?.. Biblia imemtaja ni nani katika Yohana 8:34-35 na Mshahara wake ni upi katika Warumi 6:23.

Yohana 8:34 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni MTUMWA WA DHAMBI”.

Mtu anayetenda dhambi, tajiri wake ni DHAMBI!.. Dhambi ni boss mbaya asiye na huruma…na huu ndio mshahara wake..

Warumi 6:23 “Kwa maana MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI….”.

Huyu boss hamdhulumu mtu, bali “anamlipa mtu mshahara tena kwa wakati”… kwasababu kila anayefanya kazi anastahili malipo biblia inasema hivyo katika (Luka 10:7 na 1Timotheo 5:18).

Dhambi inaua.., dhambi inaua.., dhambi inaua…, dhambi inaua..! Dhambi inaua,..Dhambi inaua…

> Dhambi inaua ule Upendo mdogo uliopo ndani yako

> Yale mahusiano madogo uliyoyaanza na Mungu wako, dhambi inayaua, inakusababisha kabisa usioune uso wa Mungu,… Tena biblia inasema inasema “Inafarikisha”…kufarikisha sio “kufarakanisha”… Kufarikisha inatokana na neno “kufariki” yaani “kufa/kutengwa”

Isaya 59:2 “lakini maovu yenu YAMEWAFARIKISHA ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”

> Dhambi inaua “furaha” ndogo na kubwa uliyonayo..

> Dhambi inaua “amani” na kuleta hofu.

> Dhambi inaua “wema” mtu alionao.

> Dhambi inaua “ndoa”

> Dhambi inaua huduma/karama/kipawa.

> Dhambi inaua “Heri” za mtu.

> Dhambi inaondoa “Baraka” za mtu

Mwisho dhambi inaua “Mwili”….. huyu ni boss asiyefaa, mwenye mkataba Mbovuuu!!!!…Tumkimbie! Na kumwendea Bwana YESU, ambaye yeye anasema Nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, nasi tutapata raha nafsini mwetu (Mathayo 11:28).

Tukimkimbilia Bwana YESU anatufungua kutoka kwa huyu mwajiri mbaya (dhambi) na kutuweka huru.

Yohana 8:35  “Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.

36  Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”

Bwana YESU anatulipa UZIMA badala ya KIFO…. na si Uzima tu, bali UZIMA WA MILELE.

Bwana anamlipa mtu uzima katika Nafsi yake.

Unaongeza uzima juu ya upendo wa mtu, lakini dhambi inaua!

Bwana YESU anaongeza Uzima juu ya Amani ya mtu, lakini dhambi inaua!

Bwana YESU anaongeza Uzima juu ndoa ya mtu na maisha kwa ujumla, lakini dhambi inaua!

Na Zaidi ya yote, Bwana YESU anamlipa Mtu UZIMA WA MILELE (Yaani maisha baada ya hapa)..Kwanini tusimchague huyu??.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Je unaye tayari?..kama bado unangoja nini?.. kwanini dhambi ikukaushie uzima wako wa hapa duniani na ule wa milele ujao??..na matunda ya dhambi ni yale yote yaliyotajwa katika Wagalatia 5:19-20.

Wakati uliokubalika ni sasa, mkaribishe YESU leo maishani mwako akuweke huru.

Ikiwa bado hujampokea Bwana YESU na unahitaji msaada huo basi wasiliana nasi, tutakusaidia buree.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TENDA JAMBO LA ZIADA.

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?

UFALME WAKO UJE.

Rudi Nyumbani

Print this post

NAMNA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA

bofya, juu, “download” ufungue makala yake usome..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

KILINDI CHAPIGIA KELELE KILINDI.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kisonono kinachozungumziwa katika Mambo ya Walawi 15:2 ni kipi?

Jibu: Turejee..

Walawi 15:1 “Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2 Haya, semeni na wana wa Israeli, mkawaambie, Mtu ye yote atakapokuwa na kisonono kimtokacho mwilini mwake, atakuwa najisi kwa ajili ya kisonono chake.

3 Na unajisi wake katika kisonono chake ni huu; kama mwili wake unachuruzika kisonono chake, au kama kisonono chake kimezuiwa mwilini mwake, ni unajisi wake.

4 Kitanda cho chote akilaliacho mwenye kisonono kitakuwa najisi; na kitu cho chote ambacho akiketia kitakuwa najisi”.

Moja ya magonjwa yaliyotajwa kwenye biblia ni pamoja na huu wa “kisonono” lakini kisonono hiki ni Zaidi ya hiki tukujuacho ambacho kipo mingoni mwa magonjwa ya zinaa (Maarufu kama Gonorrea).

Mistari mingine iliyotaja ugonjwa huo ni (Walawi 22:14 na Hesabu 5:2)

Kisonono kilichozungumzwa katika biblia ni mjumuiko wa magonjwa yote yanayosababisha kutokwa na uchafu katika njia za haja ndogo (kwa jinsia zote), yawe yanasababishwa na zinaa, au yasiyosababishwa na zinaa….na uchafu huo ni pamoja na (usaha, damu au mchanganyiko).

Kwahiyo katika biblia mtu yeyote aliyetokwa na chochote kati ya hivyo katika viungo vyake vya uzazi alihesabika kuwa na kisonono na alikuwa najisi mpaka atakapopona ugonjwa huo (hawezi kukusanyika katika kusanyiko la Bwana, na alikuwa anatengwa).

Lakini je hata sasa mtu wa namna hii anapaswa kutengwa?

Katika agano jipya hakuna agizo la kuwatenga wagonjwa wa aina yoyote, au wanawake walio katika mzunguko wa hedhi. Wote wanaweza kukusanyika katika nyumba ya Mungu (kwasababu kimtokacho mtu katika mwili hakimtii unajisi, bali kile kimtokacho kutoka moyoni, ndicho kinachomtia mtu unajisi, sawasawa na Marko 7:20-22).

Marko 7:20  “Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

21  Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

22  wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

23  Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.

Ikiwa mtu huyo amejitakasa moyoni kwa viwango vya kustahili kumfanyia Mungu ibada, hata akiwa na maradhi mwilini, bado ibada yake itapokelewa na Bwana.

Ikiwa kisonono mtu alichokipata ni matokeo ya zinaa, huyu mtu anapaswa atubie kwanza zinaa yake aliyoifanya kwa kumaanisha kuacha hiyo dhambi (kwa ufupi aokoke), na baada ya toba akiwa katika hatua za kutafuta uponyaji, anaweza kujumuika na wengine katika majumuiko ya kumwabudu Mungu.

Vile vile ikiwa ameupata kwa njia nyingine isiyohusisha zinaa, atajitakasa nafsi yake kwa toba na rehema kwa makosa mengine na atajiunga na wengine katika kumwabudu Mungu.

Mwisho: Mshahara wa dhambi ni mauti..ikimbie dhambi, na sehemu salama ya kukimbilia ili upate msaada ni msalabani, kwasababu msaada kamili upo msalaban, Kama hujampokea Bwana YESU upo hatarini…na hauwezi kushindana na dhambi.

Ni heri leo ukayasalimisha maisha yako kwake, na yeye atakuokoa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?

Tatizo la Bawasiri kibiblia

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.

Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?

Rudi Nyumbani

Print this post

OMBA, TAFUTA NA BISHA.

Mwokozi wa ulimwengu (BWANA YESU KRISTO) atukuzwe.

Bwana YESU alisema katika Mathayo 7:7, maneno yafuatayo..

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa”

Na kwanini aseme hivyo??…anaendelea mstari wa nane (8) kwa kusema..

“kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.

Kwahiyo kwanini tunapaswa tuombe?…jibu tumepata “kwasababu kila aombaye atapewa”… Lakini kwanini “Tutafute”..kwasababu kila “atafutaye ataona” na kwanini tubishe??… ni kwasababu “kila abishaye atafunguliwa”.

Kwahiyo matokeo ya Kuomba, Kutatufa na kubisha ni  KUPEWA, KUONA, na KUFUNGULIWA.

Je unataka KUPEWA unachokitaka, na KUKIONA, na KUFUNGULIWA?...basi usikwepe mambo hayo matatu; Kuomba, kutafuta, na kubisha…usichukue moja na kuacha lingine??.. ipo sababu kwanini Bwana ayaorodheshe yote matatu.

Unataka kumjua Mungu, na kutembea katika kanuni zake? Kuwa mtu wa KUOMBA, lakini si kuomba tu bali pia na KUTAFUTA!… Unamtafutaje Mungu?, kwa kuhudhuria katika makusanyiko kila wakati kwa uaminifu, na kwa kuyasoma maneno yake usiku na mchana…na KUBISHA!..

Kubisha kunakozungumziwa hapo si “kulumbana” bali “kugonga mlango”..kwa lugha rahisi ni kitendo cha kutumia maarifa yoyote uliyonayo kufikisha ujumbe kwa aliye ndani kwamba unataka kuingia!.. Na katika kumtafuta Mungu, kubisha kwetu ni pamoja na kumtolea yeye sadaka, na kuhubiria wengine habari njema, na kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo.

Wengi wanapenda kuomba tu na kuombewa, lakini wao wenyewe kutenga muda wa kumtafuta Mungu hawawezi.. watu wa namna hii ni ngumu sana kumpata Mungu katika maisha yao..  wanaishi kwa YESU aliyeko ndani ya mchungaji wao, au kiongozi wao (ndio maana kila kitu wanasubiri kuombewa)…lakini si hawaishi kwa YESU aliyeko ndani yao.

Hawa wataishia kuomba/ kuombewa na kupata kile wakitakacho lakini hawatamwona YESU katika maisha yao (hawataijua sauti yake wala kuongozwa na yeye)..lakini kama wangeomba na kuombewa na wangeongeza bidii katika kumtafuta MUNGU, wangepata faida zote.. kupata na kuona.

Je unaomba, na kutafuta na kubisha?

Kama hayo bado huuyafanyi basi anza kuyafanya leo, na Bwana atajifunua kwako.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?

TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI

NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Rudi Nyumbani

Print this post

kiaramu ni lugha gani? je ilizungumzwa na Yesu?

Kati ya lugha tatu ambazo zinaonekana katika uandishi wa biblia Kiaramu (Aramaic), ni mojawapo nyingine zikiwemo Kiebrania na kiyunani.

Sehemu kubwa ya agano la kale imeandikwa katika lugha ya Kiebrania na maeneo machache machache sana yalikuwa na maandishi ya kiaramu, (Ezra 4:8 – 6:18, Danieli 2: 4 – 7:28)

 Lakini katika agano jipya sehemu kubwa imeandikwa katika lugha ya kiyunani (kigiriki), na mahali pachache pachache kuna maandishi ya kiaramu.

Hivyo lugha hii haipo kwa sehemu kubwa katika biblia

Je chimbuko la hii lugha ni wapi?. 

Ni lugha iliyozungumzwa na watu walioitwa Waaramu, ambao lugha yao ilienea kwenye mataifa mbalimbali ambayo kwasasa ni nchi za Lebanoni, Syria, Yordani, Iraq, na Uturuki, na sehemu nyingine za mashariki ya kati. Ni lugha ambayo ilikuwa na nguvu sana zamani za falme zenye  kama Ashuru, na ufalme wa Uajemi. 

Enzi za Bwana wetu Yesu Kristo, lugha hii ilizungumzwa pia maeneo ya Israeli hususani katika miji ya Galilaya, ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alilelewa. Huku kiyahudi ikiwa ni lugha ya asili, kidini na kisiasa.

Hivyo lugha kuu ya Bwana ilikuwa ni hii kiaramu, japokuwa alizungumza pia kiyahudi.

Baadhi ya maneno ya kiaramu ambayo yananukuliwa moja kwa moja kutamkwa na Bwana Yesu ni haya; (japo yapo na pia mengine)

Marko 5:41 “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka”. 

Marko 7:34 “akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. 

Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Maneno mengine ni kama “Hosana” (lenye maana ya okoa sasa), Mathayo 21:9

“Aba” (Marko 14:36), lenye maana ya Baba.

Lakini pia swali la kujiuliza ni nini sababu ya Bwana Yesu, kuipenyeza lugha hii katika baadhi ya matukio?

jibu ni kuwa hakuna jambo la muhimu sana katika hiyo lugha, isipokuwa ni maongozo  ya Roho Mtakatifu ndani yake kwa wakati huo. Kama tu sehemu nyingine alipoongozwa kutema mate chini atengeneze tope apake mtu machoni ili apone. 

Hivyo Bwana Yesu alikuwa ni mtu aliyetega sikio kuisikia sauti ya Roho. Vivyo hivyo na sisi, misukumo mbalimbali yaweza kuja ndani yetu. Wakati mwingine hutaomba kwa akili, utaomba kwa kunena kwa lugha, utaomba kwa nyimbo, utaomba kwa kuugua na kulia, kwa jinsi Roho atakavyokusukuma ndani.

Ni kutuonyesha kuwa Bwana hakuwa na fomula fulani pekee katika kutenda kazi, alitegemea maongozo ya Roho Mtakatifu.

Vivyo hivyo na sisi tunapojawa Roho vema. Atatugusa kwa namna mbalimbali na hivyo tutatimiza makusudio yake vizuri, katika jina lake kuu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

SEMA KWA LUGHA NYINGINE.

ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Print this post