Luka 14:12 “Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.
13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, 14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki”.
13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,
14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki”.
Katika habari hii, tunaona Bwana Yesu alialikwa na mtu mmoja mkuu sana miongoni mwa Mafarisayo ale chakula cha mchana nyumbani kwake, na bila shaka mtu huyu alikuwa ni tajiri, na katika karamu yake alialika watu wakuu, watu wa maana, na si watu wa kawaida kawaida tu, Lakini kuna kitu ambacho Bwana Yesu alikiona kimepunguka katika ukarimu wake mwema wa kuwaalika watu na wageni katika shughuli zake, kwani si wote wenye moyo kama huo.Wengine wanaweza wakawa ni matajiri na wakuu, lakini wakala vitu vyao peke yao, lakini huyu alikuwa watofauti kidogo.
Lakini pamoja na hayo, Bwana Yesu aligundua watu aliowaalika walikuwa ni matajiri tu, watu wenye uwezo kama yeye, Hivyo Bwana Yesu kwa kuliona hilo ili kumsidia kuifanya taabu yake isiwe bure, ndipo akamwambia kwa kumshauri wakati mwingine, kuwa atakapofanya sherehe awaalike watu wasiokuwa na uwezo wa kumlipa mfano wa hicho alichokifanya..Kwasababu akiwaalika watu wenye uwezo, wale watu nao watarudisha mapigo siku moja, watamwalika na yeye kwenye karamu zao na thawabu yake itakuwa imeshalipwa na wao, lakini mbinguni hatakuwa na kitu, hivyo ili taabu yake na wema wake uwe na nguvu idumuyo, siku nyingine akifanya karamu kubwa kama hiyo, asiiachie thawabu yake ilipizwe na wanadamu bali ije ilipizwe na Mungu katika siku ya ufufuo wa wenye haki, hivyo awaalike watu wasiokuwa na uwezo wa kumfanyia kama kile alichowafanyia.
Hata leo hii, yapo mambo mengi tunayafanya tukidhani tutalipwa tutakapofika mbinguni kwa ukarimu tunaoufanya..Kwa mfano leo hii labda kutokee mchango wa sherehe fulani ni rahisi kuchangia harusi ya boss wako, au mfanyakazi mwenzako kwasababu unajua kuna siku moja na wewe utahitaji wakuchangie kwenye sherehe yako, au ya ndugu yako. Lakini ukisikia yupo jirani yako ambaye ni maskini hana mbele wala nyuma kipato chake ni kidogo hata hakimtoshelezi yeye mwenyewe, halafu mwanawe anataka kuoa, hivyo anahitaji sapoti yako kidogo, Ukweli ni kwamba wengi wetu tutakuwa tayari kuingia mitini, ni kwasababu gani?, Ni kwasababu tunaona mbeleni huyu anaweza asiwe na msaada kwangu siku shughuli yangu, hivyo hata nisipomsaidia hainiathiri chochote.
Kiuhalisia Mungu hatakulaumu ulipochangia sherehe ya Yule boss wako na kuiacha hii ya huyu maskini, zaidi Mungu atakulipa, na kukulipa kwake kutakuwa ni kwa kupitia wao, na habari thawabu yako itakuwa imeishaipata hapa hapa duniani, juu mbinguni utakuwa huna kitu chochote. Ukinunua zawadi si zote uzipeleke kwa marafiki na ndugu, nyingine tenga wapelekee wasio na uwezo wa kukulipa,watu wasio na faida yoyote kwako. Unapokopesha usikopeshe wale tu ambao watakupa na Riba juu yake..Kopesha hata na Yule ambaye hawezi kukulipa na Riba juu yake mwenye uwezo wa kukurudishia kiwango kile kile ulichompa.
Luka 6:35 “Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, NA THAWABU YENU ITAKUWA NYINGI; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu”.
Na ndio sababu ambayo Bwana alimshauri huyu mtu aliyemwalika, nasi tupokee ushauri huo, tutafute thawabu zinazodumu milele. Ni kweli wakati mwingine unaweza kuona ni mzigo kuwa msaada kwa wasiokunufaisha Lakini thawabu yake, utaiona siku ile utakapofika mbinguni. Maana kiwango cha hazina yako ndicho kitakachofunua utajiri utakaokuwa nao mbinguni.
“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. (Wagalatia 6:9)”
Bwana akubariki.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
KATIKA BIBLIA KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Maombi yamegawanyika katika sehemu kuu tatu 1) kushukuru 2) kuwasilisha mahitaji kwa mungu 3) Kutangaza.
1) MAOMBI YA SHUKRANI; Maombi haya ya shukrani ni Dhahiri na yanajulika na Wengi, kwamfano maombi ya kushukuru ni muhimu sana, na ni wajibu wa kila mtu, kuyafanya…Na haya yanahusisha kumshukuru Mungu kwa Uzima anaotupa, kumshukuru Mungu kwa afya anayotupa, ukizingatia wakati unapumua kuna wengine wapo ICU, wengine Mochwari n.k, pia maombi haya yanahusisha kumshukuru Mungu kwa mambo yote mabaya aliyokukingia katika wiki yote iliyoisha, mwezi wote uliopita na miaka yote iliyopita nyuma yako, njiani umepishana na mapepo mengi, shetani alikuwa amepanga mauti na ajali nyingi juu yako lakini Mungu kakuepusha nazo zote pasipo hata kukuambia, uthibitisho ni wewe kuimaliza wiki salama, na pia yanahusisha kumshukuru Mungu kwa riziki zote za kiduni anazotupatia, katika shughuli zetu na mapato yetu yote,..Kwahiyo maombi haya kwa ujumla yanahusisha kumshukuru Mungu kwa mambo yote anayoyafanya tunayoyaona na tusiyoyaona. Ni maombi yanayoonesha unyenyekevu wetu mbele za Mungu na kumwonesha Mungu wetu kuwa tunathamini na kuutambua na kuujali ulinzi wake na Fadhili zake juu yetu. Kwahiyo ni sehemu ya maombi ambayo ni muhimu sana.
2) Sehemu ya pili ya maombi ni ile ya KUWASILISHA MAHITAJI YETU MBELE ZA MUNGU. Hii inahusisha kumwendea Mungu kwa unyenyekevu kumwomba atufanyie au atupatie jambo Fulani katika Maisha yetu, Tunamwendea tukiamini kuwa yeye ndiye mpaji wetu (YEHOVA-YIRE). Tunamwomba azidi kutupa riziki zetu, azidi kuzifanikisha kazi zetu za mikono, azidi kutupa afya, azidi kutuepusha na yule mwovu na mipango yake yote, azidi kutupa Neema ya kumjua yeye Zaidi popote tuendapo atukutanishe na injili yake na kuitii, azidi kutupa mioyo ya nyama na si ya jiwe katika kutenda mapenzi yake, azidi kutupa hekima, tunamwomba Bwana azidi kutupa furaha, amani, upendo pamoja na kibali kila tuendapo, na kutufanikisha katika mambo yote katika masaa ya siku yaliyobakia, wiki na katika mwezi huu na unaokuja. Hapa tunamwomba Mungu atuepushe na kila jaribu lililopangwa na shetani kinyume chetu mbele yetu..Kama Bwana alivyosema mahali Fulani “Ombeni kwamba msiingie majaribuni. (Luka 22:40)”.
Ikiwa na maana kuwa usipoomba ni lazima utaingia majaribuni tu!..Wakina Petro usiku ule Bwana aliwaambia waamke kusali ili wasiingie majaribuni wakapuuza, wakalemewa na usingizi wakalala, masaa machache baadaye Petro alipojaribiwa na Ibilisi amkiri Yesu, alishindwa mwisho wake akamkana mara 3 lakini endapo angeomba usiku ule kama Bwana alivyomwambia na kuifunika siku yake wakati Ibilisi anamjaribu angeshinda lile jaribu, saa ile nguvu fulani ya ujasiri ingemshukia pale pale na angemkiri Bwana badala ya kumkana, au Mungu angemuepusha kabisa na jaribu hilo. Lakini kutokana na kwamba alikuwa hana hazina ya maombi ya kutosha, nguvu za roho zilikuwa chin alishindwa. Na aina zote za majaribu zinaweza kuzuiwa au kuepukwa kwa maombi… unapopita mahali na watu kukuudhi mpaka kukasirika na kugombana mpaka kutoa maneno machafu hilo ni majaribu ambalo ungeweza kulizuia kwa kuomba usiku mmoja kabla hujalala, au asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako.
Kadhalika unapojikuta unafanya kitu kisichofaa ambacho hukutarajia au hukupanga kukifanya hilo nalo ni jaribu ambalo lingeweza kuzuiliwa kwa kuomba kabla ya kuianza siku..Na dhambi nyingine zote za bahati mbaya zinasababishwa na upungufu wa maombi. Inapotokea safari ya ghafla ambayo ni ya hasara na si ya faida hilo nalo ni jaribu ambalo endapo ungeomba lisingekukuta.nk n.K.
3) Sehemu ya tatu na ya mwisho ya maombi ni maombi ya KUTANGAZA. Hii ni sehemu ya mwisho na ya muhimu sana kwa kila Mkristo kuifanya. Na faida yake kuu ya haya maombi ni ile ile ya KUTUEPUSHA NA MAJARIBU, Maombi haya ni maombi ya kimamlaka…Maombi haya na yale ya KUPELEKA MAHITAJI yanakazi moja tu nayo ni KUTUEPUSHA NA MAJARIBU.
Sasa kabla ya kuingia kujifunza juu ya jambo hili hebu kwanza tujifunze ulinzi wa kiMungu juu ya mtu aliyezaliwa mara ya pili.
Mtu anapozaliwa mara ya pili, na kuishi Maisha yanayompendeza Mungu asilimia zote, kunakuwa kuna ulinzi Fulani wa kiujumla ambao Mungu anauachilia juu yake, kiasi kwamba huyo mtu hata iweje hawezi kupotea, shetani hawezi kumtoa mkononi mwa Mungu, labda tu huyo mtu kwa hiyari yake mwenyewe aamue kujiuza kwa shetani, lakini kwa namna nyingine yoyote hawezi kutoka mikononi mwa Mungu, anakuwa analindwa kuanzia unywele wake mpaka unyayo wako, na anakuwa amevuka kutoka mautini kuingia uzimani, …Lakini pamoja na huo ulinzi wa kiujumla kuna sehemu ndogo sana ambayo Mungu kamwachia shetani aimiliki..na hiyo ni kutokana na kwamba bado tupo katika miili hii ya dhambi, sehemu yote ya ulinzi wa kiMungu tutakuja kuipata baada ya ukombozi wa miili yetu pale tutakapovaa miili mipya ya utukufu.
Ndio maana unaona sasa japokuwa umeokoka na unaishi Maisha ya kumpendeza Mungu kwa asilimia zote lakini bado utapitia wakati mwingine wa viudhaifu vya hapa na pale, utaumwa kichwa, utajisikia kichefuchefu, mafua yatakusumbua, wakati mwingine itakubidi umeze Panadol kupunguza maumivu au uende hospitali n.k. Sasa hiyo yote ni kuonesha kuwa Mungu hajaipa miili yetu hii asilimia 100 ulinzi…ingawa hivi viudhaifu haviwezi kutuathiri kiasi cha kututoa kwenye Imani, kwasababu Mungu hawezi kuruhusu tujaribiwe kupita tuwezavyo, alisema hivyo katika Neno lake.
1Wakoritho 10: 13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.
Kwahiyo haya majaribu madogo madogo ni lazima yaje! Na ni wazi kuwa yanaletwa na shetani kututesa tu! Na kutuhangaisha…Kwahiyo shetani anachokifanya ni kutumia hii nafasi aliyopewa ya sehemu ndogo ambayo Mungu kaiacha, kutujaribu…Na kwasababu anajua hawezi kumjaribu mwamini kwa asilimia zote, atahakikisha kuwa hiyo sehemu ndogo aliyopewa anaitumia ipasavyo.
Sasa swali? Anaitumiaje?
Anaitumia kwa KUTANGAZA, Anawatumia watu kutamka maneno Fulani Fulani juu yako, ambayo hayo yanaweza kutokea kama walivyozungumza, kwasababu Mungu alivyomuumba mwanadamu akizungumza kitu kwa Imani ni lazima kitokee hata kama mtu huyo sio mchawi. Ndio maana wazazi hata kama ni waabudu sanamu wanao uwezo wa kumbariki mtoto au kumlaani, na hizo baraka au laana zikampata huyo mtoto hivyo hivyo kama alivyozisema. Kwasababu hiyo basi shetani anaweza kutumia watu au wachawi au mapepo yake KUTANGAZA mambo Fulani mabaya juu ya mtu.
Kumbuka tena kwa msisitizo..kama umezaliwa mara ya pili na kuishi Maisha yampendezayo, haijalishi ni mambo gani makubwa watayatangaza juu yako, hayatatimia yote kwasababu kuna asilimia kubwa ya ulinzi wa kiMungu kwenye Maisha yako, lakini pia yapo baadhi madogo madogo yanayoweza kutimia na hiyo ni kwasababu hatujapewa dhamana wa ulinzi wa miili hii asilimia zote kama tulivyotangulia kusema..(huu ni msingi mkubwa ambao unahitaji kuelewa) Na sio kwamba Mungu kashindwa kutufunika asilimia zote, hapana ni kwasababu tu ndivyo imempendeza iwe hivyo…kwamba tujue kwamba bado tupo duniani?, tujue kuwa sisi bado ni wadhaifu mbele zake, na tujifunze kumtegemea yeye na kumwomba ulinzi…na pia tujue kuwa vita bado vinaendelea…mpaka siku tutakapovaa ile ya utukufu, ndipo vita vitaisha.
2Wakorintho 1:8 “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. 9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu, 10 aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;”
2Wakorintho 1:8 “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,
10 aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;”
Sasa ili kupunguza nguvu za shetani kwa majaribu yake anayoyatumia kwa NJIA YA KUTANGAZA…Na sisi tulioamini tuna wajibu huo huo, wa kuingia kwenye maombi ya kuzipunguza hizo nguvu ndogo ndogo za shetani zinazofanya kazi kwenye Maisha yetu…Na maombi hayo hatuyafanyi kwa kupeleka mahitaji mbele za Mungu, bali kwa KUTANGAZA kama yeye anavyotangaza..Ndio hapo sasa Kila siku kabla ya kuianza siku unatamka baraka katika siku hiyo, unalaani na kufuta kila kazi zote za Adui zilizopangwa katika siku hiyo kwa jina la YESU, Unalaani vidhiki na vijaribu vidogo vidogo vilivyopangwa na shetani…Na unatamka kwa maneno yanayosikika kabisa, kwasababu maneno yanaumba, kwa Mungu aliiumba dunia kwa Neno, Unatamka kwa kutangaza kuziharibu nguvu zote na kufuta maneno yote yaliyozungumzwa na watu, wachawi, au mapepo katika siku nzima…unalaani nguvu zote za giza zilizoachiwa siku hiyo zitakazokufanya uikane Imani, au upate hasara ya jambo Fulani, au zitakazokufanya ulumbane au ugombane na watu, unalaani kwa kinywa chako kila nguvu zote za giza zilizoachiwa na yule adui kukufanya usipate muda wa kusoma Neno,na kila ratiba isiyoeleweka iliyopangwa kuzimu kinyume chako na ndugu zako…Unahikikisha unagusa kila kipengele katika Maisha yako, afya yako,familia yako, kazi yako na Imani yako. Usiache kitu!, kwasababu na yule adui anajua anaomlango mdogo juu ya Maisha yako hivyo anakaza kuutumia vizuri.
Mithali 18:21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”
Kwa kufanya hivyo utakuwa umeharibu mipango yote midogo midogo ambayo shetani alikuwa amepanga kukusumbua katika siku hiyo na wiki hiyo. Na hivyo utakuwa umejiongezea Ulinzi wa kiMungu kwa asilimia nyingine kadhaa mbele. Kama alikuwa akuletee viugomvi, viugonjwa, unashangaa siku inaisha bila hivyo vitu, kama alikuwa amekusudia kukuletea vitabu vya hapa na pale visivyoeleweka vinatoweka.
Nakumbuka mwanzoni mwanzoni nampa Bwana Maisha, nilikuwa napitia changamoto nyingi sana na nilikuwa sijui chanzo chake ni nini?..lakini baada ya kujifunza somo la maombi, niliona mabadiliko makubwa sana…
Kwa hiyo ni maombi ya Muhimu sana na kila Mwamini anatakiwa aombe. Na ni moja ya silaha 6 tulizopewa katika biblia..
Waefeso 6: 11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE; 19 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; 20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.”
Waefeso 6: 11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 KWA SALA ZOTE NA MAOMBI MKISALI KILA WAKATI KATIKA ROHO, MKIKESHA KWA JAMBO HILO NA KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA WATAKATIFU WOTE;
19 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo;
hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.”
Kwa kumalizia kumbuka kuwa muda wa chini Bwana Yesu aliotuamuru tusali kwa siku ni LISAA LIMOJA.
Mathayo 26: 40 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”
Umeona hapo, roho zetu zipo tayari kuomba lakini miili ndio inayokataa, hivyo mambo mengine ni unalazimisha, kama Bwana asiyekuwa na dhambi aliomba Zaidi ya lisaa limoja, unafikiri inatupasaje sisi wenye dhambi?..unakataa usingizi na uvivu wa kuomba, unalazimisha mambo, utashangaa dakika za kwanza unapata shinda lakini baaada ya dakika 10-15 mbeleni unashangaa kuna nguvu Fulani inakuvaa unajikuta unazama kwenye maombi…Na kwa vipengele hivyo vitatu ukianza na kushukuru, kisha kupeleka maombi na kutangaza baraka..huwezi kuacha kumaliza lisaa na Zaidi..
Na pia kumbuka kuwaombea na wengine, katika vipengele vyote hivyo vitatu, hata hichi unachokisoma hakijapewa guarantee ya ulinzi asilimia 100, kinahitaji maombi kiweze kuendelea kuwepo, kwahiyo uombapo ukumbuke kugusia kila eneo, pamoja na sisi tunaoandika hizi habari, Ili injili ya Mungu izidi kwenda mbele, kwa Neema za Mungu.
Bwana akubariki sana.
NI JAMBO LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
SHUKURU KWA KILA JAMBO.
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.
Rudi Nyumbani
Shalom! Mtu wa Mungu, maandiko yanatuagiza tusiache kuonyana kila siku, maadamu iitwapo leo (Waebrani 3:13). Hivyo nakukaribisha tujifunze leo jambo moja lihusulo BIBLIA.
Nilipokuwa ninatafakari hili Neno linalosema “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.” Nikajiuliza hii njia ionekanayo kuwa sawa ni ipi?..Mtu akiwa mtukanaji, mtu akiwa muuaji, mtu akiwa ni fisadi n.k, njia yake haiwezi kuonekana ni sawa machoni pake, ni wazi kuwa anafahamu anapoeleka ni pabaya..Lakini njia inayoweza kuonekana ni sawa machoni pa mtu ni ipi?, ni ile inayotoka katika maandiko (BIBLIA), pale maandiko yanapomthibitishia mtu kuwa kitu hichi au kile anachokifanya kimeandikwa, basi hilo linampa amani ya kufahamu kuwa yupo katika njia sahihi.
Nataka nikuambie, biblia ni kitabu kitakatifu sana, kimekamilika na kujitosheleza kwa namna zote, hakiwezi kuongezwa wala hakiwezi kupungumzwa, lakini nataka nikuambie pia Biblia hii si ya watakatifu peke yao: Biblia si mti wenye tunda la aina moja, bali ni mti wenye matunda ya aina nyingi tofauti tofauti,. na kila mtu anachuma kinachomfaa na kuondoka kulingana na matakwa yake mwenyewe.
Na hiyo yote ni kwasababu biblia ni Neno la Mungu, na Neno la Mungu tunajua ndio lililoumba kila kitu (Yohana 1:1), halikuumba vyema tu bali hata na viovu pia, hivyo pumzi ya kila kitu inategemea hilo Neno. kwahiyo kila mtu na kila mmoja na inaweza kumnufaisha kulingana na matakwa yake mwenyewe. Shetani inamnufaisha katika lengo lake la kupoteza watu, na amefanikiwa kweli kupoteza mamilioni ya watu kwa kupitia biblia unayoisoma, hata alijaribu kuitumia hiyo hiyo kumwangusha Bwana akashindwa..
Madaktari wanaitumia hii kuwasaidia kubuni aina mbalimbali za matibabu, hata ukiangalia nembo yao kubwa maarufu inayotumiwa na Shirika la Afya ulimwenguni (WHO), utaona ni Yule nyoka wa shaba ambaye Musa aliwaagiza wana wa Israeli wamtazame ili wapone kutokana na sumu ya nyoka. Utamaduni huo ambao baadaye uligeuka kuwa wa kipagani, ulirithiwa na mataifa mengine ya kipagani kama Ugiriki wakahusisha na tiba za kienyeji na mambo hayo, na ndio huko huko mpaka ikawa maarufu katika masuala yote ya tiba duniani leo hii.
Biblia hii hii inayoisoma inatumiwa na majeshi, kubuni mbinu mpya za kupigani: Na wanafanikiwa vizuri sana. Wakati wewe unafurahia kusoma zile habari za vita vya Yoshua na waamuzi, wengine huko wanaiga mbinu za kivita. Biblia hii hii inatumiwa na wanasiasa kutengeza sera zao za kampeni na wanafanikiwa katika hilo, Msome mtu kama kwame Nkrumah raisi wa kwanza wa Ghana,si jinsi alivyoupindua utawala wa kikoloni kwa maandishi ya maandiko.
Biblia hii hii inatumiwa na wachawi na wanajimu, kuwasaidia kufanya uchawi wao: Wasingefahamu kitu kinachoitwa kafara na nguvu iliyokatika damu kama wasingesoma katika biblia..Katika Agano la kale kafara za Wanyama zilikuwa zinafanyika kwaajili ya upatanisho…Asili ya kuvaa hirizi si kutoka kwa wachawi…Wana wa Israeli waliagizwa na Mungu wazivae kwenye vipaji vya nyuso zao, ili kuwakumbusha sheria za Mungu, (vilikuwa ni viboksi vidogo vilivyokuwa vimebeba baadhi ya maneno ya kwenye Torati) lakini Baadaye shetani akaja kuiba huo utamaduni na kutengeneza za kwake kwa lengo la kulogea watu.
Wafanya-biashara na matajiri: Kanuni za kufanikiwa zote wanazitolea katika maandiko,kupanda na kuvuna. Kufanya kazi kwa bidii,n.k. zipo huko, wanazitumia na zinawaletea mafanikio makubwa sana.
Vile vile biblia hii hii inatumiwa na manabii wa Uongo, kutimiza matakwa yao: Wanasoma na kufahamu kuwa ndani ya jina la YESU, kuna uweza wa kipekee, kila kitu kinatii, hivyo hata mtu ambaye alishamkufuru Mungu siku nyingi, anaouwezo wa kulitumia hili jina ili kuamirisha chochote na kikamtii, hata kuamisha milima…hivyo anaweza kutumia fursa hiyo kujipatia mali, au kuwapoteza, kwa kisingizio cha miujiza, na anafanikiwa kabisa, na ndio maana Bwana Yesu alisema wengi watakuja siku ile wakisema Bwana Bwana…, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. (Mathayo 7:21).
Lakini pia biblia hii hii inatumiwa na watu wengine, na inawapa UZIMA WA MILELE.
Unaweza ukaona hapo, jinsi Biblia inavyofungua milango ya mambo mengi, hata yale maovu, lakini sio milango yote mtu akiingia kwa kupitia biblia inamletea mwisho mwema. Na ndio maana ukisoma maneno ya kwanza kabisa Bwana Yesu aliyoyahubiri ni haya, TUBUNI, KWA MAANA UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA(Mathayo 4:17)..Na habari zake zote zilikuwa zinalenga ufalme wa mbinguni, kama ukitafuta mahali Bwana Yesu anakufundisha utajiri na mafanikio ya kidunia nataka nikuambie unaweza ukavunjika moyo, zaidi ya yote watu waliojaribu kumfauta kujaribu kumuuliza kuhusu mambo kama hayo aliishia kuwaambia “Uzima wa mtu haupo katika mwingi wa vitu alivyonavyo”(Luka 12:15).
Alikuwepo kwa lengo moja tu la msingi, nalo ni kumpa mtu uzima wa milele. Na wote waliomfuata waliupokea bali waliomkataa hawakaupata bali walipata sehemu ya vipengele vingine katika maandiko.,Leo hii usifurahie na kusema biblia inahimiza hichi ninachokifanya..ukadhani kuwa upo sahihi wakati wote katika hiyo njia…Unapaswa ujiulize je! matokea ya hichi ninachokifanya mwisho wake ni nini?,..Ni uzima wa milele au Mauti, au huna-uhakika?. Ikiwa ni mauti au huna-uhakika, hata kama kuna vifungu vinakusapoti, achana nacho, tafuta kilicho cha msingi kwanza, na biblia imeshaturahisishia kufahamu kilicho cha msingi, nacho ni YESU KRISTO..
Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Ni heri ukakifanya hicho, lakini huku nyuma jambo la msingi la wokovu wako na uzima wa milele lipo pamoja na wewe, hiyo haina shida kabisa,lakini unaacha mambo ya wokovu na habari za kwenda mbinguni, unasema biblia inaniambia hivi au vile …Kumbuka Yesu anasema “hapa yupo aliye mkuu zaidi ya Sulemani”.
Hivyo kwa kumalizia ni vizuri tukajua jinsi ya kuyavunja vunja maandiko na kuchagua vile vilivyo vya muhimu kwanza, ambavyo ni vya UFALME WA MBINGUNI NA HAKI YAKE NA HIVYO VINGINE VILIVYOSALIA TUTAZIDISHIWA tu Bwana ameahidi hilo, yeye si mwongo. Tunajua hizi ni nyakati za kumalizia, Kristo yupo karibuni kurudi kushinda hata sisi tunavyoweza kufikiria..Ikiwa utasikia unyakuo umepita leo na wewe umebaki utakuwa katika hali gani?. Kumbuka atakayeona uchungu zaidi sio mlevi, au jambazi, atakayeona uchungu ni Yule mkristo aliye vuguvugu ambaye aliitupilia injili za wokovu na kwenda mbinguni akageukia injili za namna nyingine za faraji, ambazo thawabu zake zinaishia hapa hapa duniani…siku hiyo huyo ndio atakayeomboleza..Kwasababu alidhani kuwa ndio njia aindeayo uzimani..Lakini mwisho wake umekupeleka kuingia katika dhiki kuu.
Utasema siku ile, Hatukupata mali kwa jina lako Bwana?, hatukufunguliwa matumbo yetu yaliyokuwa tasa kwa jina lako?, hatukufungua biashara nzuri kwa unabii wako?.nk Ni kweli mambo hayo yote uliyafanya kwa jina la Yesu lipitalo majina yote na lifungualo vifungo vyote, lakini siku ile Bwana atasema ondokeni kwangu! Kwanini? kwasababu jina hilo ulipaswa ulitumie pia kukuletea wokovu wako wa milele, si tu vitu vya ulim:wengu huu vinavyopita, jina hilo ulipaswa pia ubatiziwe kwalo, kulingana na Matendo 2:38, Matendo 8:16, Matendo 19:5 na Matendo 10:48. ili upate ondoleo la dhambi zako na upokee kipawa cha Roho Mtakatifu..Umepata fahari zote na ulimwengu mzima kwa jina hilo lakini umekosa uzima kwa jina hilo, itakufaidia nini?.
Jihadhari na njia zinazoonekana ni nzuri, zinazopendwa na kufuatwa na wengi kwa kivuli cha biblia, nyingi zinaelekea upotevuni. kumbuka njia ni nyembamba ielekeayo uzimani
Ubarikiwe sana.Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
NJIA MUNGU ALIYOIWEKA KWA KILA JAMBO
NJIA YA MSALABA
NJIA YA BWANA INATENGENEZWA WAPI?
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, 17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. 18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. 19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. 20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. 21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. 22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. 23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. 24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Luka 14:16 “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi,
17 akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
18 Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe.
19 Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe.
20 Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
21 Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.
22 Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi.
23 Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa.
24 Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.
Bwana Yesu alitoa mfano huo wa karamu, kuelezea mambo yanayoendelea sasa katika roho, Kristo kama Bwana Arusi, anaalika watu sasahivi katika ufalme wake, anatuma watumishi wake huku na huko duniani kote…kuwaambia watu habari za uzima…Lakini kinachohuzunisha ni kwamba wengi ambao wangestahili kuwepo kwenye harusi ya mwanakondoo siku ile hawatakuwepo!, wengi ambao wangestahili kuwa wageni rasmi hawataingia kabisa karamuni.
Watu wengi wa dini, au wanaojiita wakristo hawataingia mbinguni, hiyo ni kulingana na maandiko! Hiyo yote ni kwanini?..Ni kutokana na kitu kimoja tu kinachoitwa UDHURU..Kutokuitikia mwaliko kutokana na visababu vidogo vidogo vya kutengenezwa.
Na maandiko yanasema pia, watoza ushuru na makahaba watawatangulia wengi kuingia katika ufalme wa mbinguni.. Ni kwanini?..Ni kwasababu hawana viudhuru katika kuitikia wito wa kumgeukia Mungu, Ni rahisi kumbadilisha kahaba amgeukie Mungu, kuliko kumrekebisha mtu ambaye ni wa kidini, ambaye tayari kashashiba na dhehebu lake, hataki tena kusikia kitu kingine, hata kama ni cha kweli vipi.
Ukiisoma tabia ya hawa watu walioalikwa Harusini na kukataa kuja, utaona kabisa walikuwa ni watu werevu, walikuwa wanatoa hoja za nguvu za kwanini wao kutokuja! Na kweli utaona kwa sehemu Fulani zinamashiko! Au ni za msingi…mwingine kwenda kujaribu ng’ombe, mwingine kaoa ni lazima akae na mke wake kidogo baada ya harusi, mwingine kanunua shamba, ni lazima akalitazame n.k.
Lakini kama ukichunguza sababu pekee za kutokuja sio hizo, lazima kutakuwa na vitu vingine ambavyo havijawapendeza kwenye hiyo karamu, labda pengine mfumo wa sherehe hawakupendezwa nao, au vinywaji wavipendavyo pengine havitakuwepo n.k…hivyo ili kuiepuka hawawezi kusema moja kwa moja hatuji, watatafuta visababu sababu vitakavyowapa kibali maalumu cha kutokufika, ili waeleweke, ndio hivyo vya kununua mashamba, kujaribu ng’ombe na kuoa na kuolewa.
Sasa umewahi kujiuliza kwanini Bwana Yesu alisema… “kama ilivyokuwa siku za Nuhu na za Lutu watu walikuwa wakiuza na kununua, wakipanda na kujenga, wakioa na kuolewa?” mpaka siku ile gharika na moto viliposhuka ghafla na kuwaangamiza wote?..Kuoa sio kubaya, wala kujenga sio kubaya, wala kuuza na kununua sio kubaya…Kibaya ni UDHURU unaoutoa wakati huu wa Neema. Unapofanya vitu vya ulimwengu kama kigezo cha kuepuka mwaliko Mungu anaokupa hicho ndicho kibaya..Na kumbuka Mungu anaujua moyo wako, haiwezekani unapata muda wa kuangalia sinema au kusikiliza umbea masaa 2 au zaidi kila siku lakini muda wa kumtafakari Mungu au kusoma Neno lake au kuhudhuria kwenye nyumba yake angalau mara moja kwa wiki huna…kwa kisingizio una majukumu Fulani? Wiki nzima ulikuwa buzy na kazi umechoka,..Biblia inasema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Wagalatia 6:7 “ Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.
Wagalatia 6:7 “ Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.
Unapoisikia Injili wakati huu ya kukualika kwenye ufalme wa mbinguni, inayokuambia utubu na uache dhambi na rushwa, na utapeli, na wizi, na ukahaba na wewe unaanza kusema siwezi kuacha kufanya hivyo vitu kwa wakati huu au kubadilika sasa, nina majukumu, Nipo kwenye mipango ya Harusi sina hela, Nipo nasomesha Watoto, Nina viwanja vimewekewa dhamana, nina mkopo ninatakiwa niushughulikie, hata jumapili nakuwa bize sana siwezi kuhudhuria kanisani, bado natafuta fedha za kujenga, mwezi wote huu nitakuwa bize sitapatikana, nitasafiri…
Ndugu, hicho ndio kitu kisichompendeza Mungu, kutoa UDHURU!..Nafasi yako ya wokovu atapewa mwingine! Ambaye asikiapo mara moja tu ataacha!..usidhani Mungu anafurahishwa na udhuru unaoutoa. Kaingia gharama kubwa kukuandalia Karamu yake mbinguni halafu leo, unamwangusha kwa udhuru wako, Vitu unavyovihangaikia vyote vinapita (1 Yohana 2:17)..Na mwaliko huu unaoalikwa leo ni wa muda tu! Hautadumu milele.
Kuna Neema kubwa sana sasa hivi Mungu kaiachilia katika Bara la Afrika, Roho wa Mungu sasahivi anafanya kazi sana Afrika kushawishi watu wamgeukie Mungu kwa nguvu kubwa sana ya ushawishi, ambayo hiyo haipo mabara mengine, ndio maana kwa sehemu kubwa utaona hofu kubwa ya Mungu humu Afrika, mabara mengine ni ngumu sana mtu kushawishika kuigeukia injili, ni kwasababu gani?…Ni kwasababu ile nguvu ya ushawishi (Neema) haipo kwa wingi kama huku, Injili ilianzia Asia na Ulaya na kuzunguka kwenye mabara yote na inamalizikia na Afrika…Na ikitoka huku inarudi Israeli, baada ya hapo ule mwisho unakuwa umefika..Ugumu wa kuiamini injili tunaouona sasa kwenye mataifa yaliyoendelea na utahamia huku pia hivi karibuni wakati kanisa limenyakuliwa, kutakuwa hakuna ile nguvu yakuvutwa tena kwa Mungu, Itahamia Israeli.
Sasa kwanini unaichezea hii Neema iliyopo Afrika sasa?..Neema ambayo inakupa Ushahidi wote ndani ya moyo wako kuwa Mungu yupo, utafika wakati itakuwa ni ngumu hata kuamini kuwa Mungu yupo,..ndicho kinachotokea kwa watu wa mabara mengine, kwasababu anayemfanya mtu amwamini Mungu ni Mungu mwenyewe, sasa akiondoka utamwaminije?, utamfuataje?, utatubuje? (Yohana 6: 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka).
Wakati utafika Bwana ataingiza kwa nguvu wale ambao hawaujui ukristo kabisa, usishange moja ya hizi siku kuwaona waislamu wengi wanamgeukia Kristo, wahindu wale ambao ni waabudu ng’ombe, wanaokoka ghafla ghafla tu, watu wasioamini Mungu wapagani wanamjia Kristo kwa kasi, ukishaona hivyo ujue kuwa, tayari watu wameshakatwa. Na mambo hayo tumeshaanza kuyaona sasahivi yakiongezeka kwa kasi. Hapo ndipo wengi watatamani kuingia lakini itashindikana,
Mathayo 22:10 “Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni. 11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. 12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. 13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.”
Mathayo 22:10 “Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.
11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.
12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.
13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.”
Kama hujatubu, usiuchezee huu muda, ambao wenzako waliokuzimu wanatamani hata dakika moja tu watengeneze mambo yao na Mungu wanakosa.. unayo nafasi sasa ya kufanya hivyo, pale ulipo tubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi ulizokuwa unafanya kisha tafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa mwili wote na kwa jina la Bwana Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi na Bwana mwenyewe atafanya yaliyosalia kwa kupitia Roho wake Mtakatifu. Nawe utakuwa umeanza mwendo mpya na Bwana, hata kufikia karamu yake kuu aliyowaandalia watu wake tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba hizi…
+225693036618 / +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.
Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30 na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. 32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,
30 na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.
31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Bwana Yesu aligusia vifo vya hawa watu wawili kama mfano alipokuwa anazungumza juu ya hukumu itakayowapata waandishi na mafarisayo na wote walio wanafki, (Ambao kwa sasa inawalenga viongozi wote wa kidini walio wanafiki katika kazi ya Mungu). Kama alivyosema Damu za wenye haki wote zitachanganywa na kuletwa juu yao. Ikianzia kwa Habili, mpaka kwa Zakaria bin Barakia. Wengi wetu tunafahamu habari ya Habili Jinsi ndugu yake alivyomuua kwa jambo moja tu ambalo ni wivu. Kaini baada ya kuona sadaka ya ndugu yake imekubaliwa na ya kwake imekataliwa, moja kwa moja akaamua kumuua ndugu yake, “tukose wote”. Hivyo kwa kuwa Habili alikuwa ni mwenye haki na damu yake imemwagika pasipo kuwa na sababu ya msingi au hatia yoyote, biblia inatuambia…japo alikufa lakini bado anaendelea kunena, kwa namna nyingine ni kuwa damu yake bado inalia katika ardhi…
Waebrania 11:4 “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, IJAPOKUWA AMEKUFA, ANGALI AKINENA.”
Soma pia Waebrania 12:24,..utathibitisha unenaji wa damu ya Habili. Yeye alikuwa ni mfano mmojawapo aliowakilisha watu wenye haki, waliouawa tangu kuweka misingi ya ulimwengu hadi mwisho wa dunia, na wote hao damu zao zinanena mfano huo huo kama ya Habili mahali Fulani.
Sasa mtu mwingine ambaye tunaona Bwana akimgusia tena katika habari hiyo ya mapatilizo ya damu, ni ZEKARIA, wengi wanamchanganya na Yule Zekaria mwana wa Berekia, aliyeandika kitabu cha Zekaria, lakini tukichunguza kwa undani habari Bwana Yesu aliyokuwa anaizungumzia hapa, haikumuhusu yeye bali ilimuhusu Zekaria aliyekuwa kuhani wa kipindi cha mfalme Yoashi wa Yuda , mwana wa Yehoyada enzi za wafalme. Huyu Yehoyada Mungu alimpa umri mrefu kwa jinsi alivyoijali nyumba ya Mungu na uzao wa Daudi na kuwaongoza watu katika njia za kweli, aliishi miaka 130, Hivyo Zekaria inawezekana alikuwa ni mjukuu wake, ikumbukwe kuwa biblia sehemu nyingi haielezi “Babu na mjukuu”, bali wote wanaitwa “watoto wa”. Hivyo Zekaria bin Barakia Bwana Yesu aliyekuwa anazungumzia hapo ni ndiyo huyu Zekaria mwana wa Yehoyada.
Sasa huyu Yehoyada ambaye alikuwa ni kuhani aliyemcha Mungu sana, kabla ya kufa kwake watu walimcha Mungu, lakini siku alipokufa tu, mfalme na watu wote wakakengeuka waakanza kuabudu masanamu, hata nyumba ya Mungu iliyokuwa inaendelea katika ukarabati ikasitishwa..Wakaanza kufanya maovu, ndipo Zekaria sasa mtoto wake akatumwa na Mungu kwenda kuwaonya, tusome:
2 Nyakati 24:17 “Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao. 18 Wakaiacha nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao. 19 Hata hivyo akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa Bwana; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza. 20 Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi. 21 Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Bwana. 22 Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.”
2 Nyakati 24:17 “Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.
18 Wakaiacha nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zao; wakatumikia maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao.
19 Hata hivyo akawapelekea manabii, ili kuwarudisha kwa Bwana; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.
20 Na roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama juu ya watu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za Bwana, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi.
21 Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya Bwana.
22 Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.”
Kama tunavyosoma hapo wakati Zekaria anakufa kwa kupigwa mawe, alisema maneno hayo “BWANA NA AYAANGALIE HAYA, AKAYATAKIE KISASI.”. Jambo hili hawakufahamu ni jinsi gani lilimuudhi Mungu. Ingekuwa ni heri waishie kuwaua tu wenye haki, lakini wanafika mpaka hatua ya kuwaua makuhani wake na kibaya zaidi wanawaua katika nyumba ya Mungu, mbele ya macho ya Mungu.
Na ndio maana tunaona mamia ya miaka mbeleni Bwana Yesu anawakumbushia wale mafarisayo habari ile ile wasidhani kuwa imesahauliwa, hakuna kilichosahaulika. Aliigusia hii mifano miwili iliyohai kuwakilisha na wengine wote waliotendewa na watakaokuja kutendewa huko mbeleni mambo kama hayo:
Tukisoma katika
Ufunuo,6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Ufunuo,6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Ndugu, Kumbuka kuwa wayahudi wakati wa Dikteta Adolf Hitler waliuliwa kikatili bila hatia yoyote, waliuliwa kwasababu wao ni wayahudi tu, kwasababu Mungu aliwachagua hao basi, hakuna kosa lolote walilolifanya ni WIVU tu kama ilivyokuwa kwa Habili, sasa hawa leo hii roho zao zinalia chini ya madhabahu, zikitaka kisasi kilipizwe..Na sio juu ya waliokufa, hapana bali juu ya hao waliojuu ya nchi, yaani wale waovu waliopo sasa.
Vilevile, tangu kipindi cha mitume hadi kipindi cha matengenezo ya kanisa, historia inarekodi, zaidi ya watakatifu wa Mungu milioni 68 waliuliwa kikatili, na kibaya zaidi asilimia kubwa waliotekeleza shughuli hiyo walikuwa ni viongozi wa kidini ya kikatoliki..Maneno yale yale ya Bwana yanatimia hapo..
Ndugu, tutawezaje kupona kama leo hii hatutauthamini wokovu, kumbuka, mtu yoyote asiye wa Kristo tayari huyo ni adui wake. Anatekeleza ilani ya ufalme wa giza, unashirikiana na matendo ya giza, hata kama hajui…hivyo na wewe pia ikiwa upo nje ya wokovu damu hizi nyingi za watakatifu zitatakwa juu yako. Tubu leo Bwana Yesu akufanye kuwa askari wa ufalme wa mbinguni. Shetani hakupendi, leo hii unayopumzi ni kwasababu Mungu amekuhurumia pengine utubu leo. Lakini wale wasiotaka kutubu tukiachilia ziwa la moto kuna wakati utafika wakiwa hapa hapa duniani watazinywa hizo damu za wenye haki.
Ufunuo 16:4 “Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili. 7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.”
Ufunuo 16:4 “Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.”
Bwana akubariki. Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +22589001312
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
UFUNUO: Mlango wa 6
Marko 8:31 “Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. 32 Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. 33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Marko 8:31 “Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.
32 Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea.
33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Katika habari hiyo tunajifunza mambo mengi, jambo la kwanza tunaloweza kujifunza hapo ni jinsi ya kushughulika na roho ya uadui inayotutafuta kila kona, shetani ni adui yetu mkubwa.. na anapenda kutumia Zaidi watu kutushambulia, kutuumiza, hata wakati mwingine kutafuta kutuangamiza na kutuua.. na sisi tukikosa ufahamu na shabaha tunaweza kujikuta tunajibu mashambulizi isivyopasa…tunakipiga chombo cha muhusika badala ya mhusika mwenyewe….badala ya kumdhuru mrusha mkuki, unajikuta unatafuta kuidhuru mikuki.
Katika tukio hilo tunaona Bwana Yesu haraka sana alishajua ni shetani anazungumza ndani ya Petro, pasipo hata Petro kujijua kama anatumika na shetani, yeye alijua tu Bwana Yesu anahuzuni hivyo anahitaji faraja..kwahiyo wazo lilimjia kuwa anahitaji kumfariji Yesu…lakini hakujua kuwa hilo wazo ni kinyume na maandiko…Maandiko yanasema “ni lazima mwana wa Adamu asulubiwe na siku ya tatu afufuke”..
kwahiyo wazo lingine lolote litakaloibuka kinyume na hilo ni kutoka kwa yule Adui……….Kumbuka sio kwamba shetani alimvaa Petro kama nguo na kuanza kuzungumza ndani yake hapana!, aliyekuwa anazungumza pale ni Petro mwenyewe isipokuwa hilo wazo ndio lilitoka kwa shetani, na kumbuka shetani ana uwezo wa kumtupia mtu yeyote mawazo yake, awe mtumishi wa Mungu asiwe mtumishi wa Mungu..na mtu asiyekuwa na Neno vizuri ndani yake ni rahisi kukubali wazo la shetani pasipo kujua kuwa ni wazo la shetani. Ndicho kilichomtokea Petro hakuwa na Neno la kutosha ndani yake kuweza kuchambua wazo la Mungu ni lipi na la shetani ni lipi.
Na Bwana alipojua ni wazo la shetani hilo ndani ya Petro, hakuanza kushughulika na Petro bali na roho iliyopo ndani ya Petro,..na baada ya kuikemea ile roho au lile wazo la ibilisi, aliendelea kutembea na Petro kama kawaida kwani alikuwa bado ni mwanafunzi wake aliyempenda…Na ile ilimsaidia Petro kuwa makini na chochote anachokizungumza, kukilinganisha na maandiko.
Hivyo na sisi tunajifunza hapo namna ya kushughulika na roho ya uadui, hatupaswi kushughulika na yule mtu, bali na lile wazo au roho ndani ya yule mtu, hapo ndipo vita vyetu vilipo…sio kumchukia yule mtu.
Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Lakini jambo la mwisho la kujifunza ambalo ndio kiini cha somo letu leo ni “MAWAZO YA SHETANI”…
Tukirejea hapo juu mstari wa 33 unasema.. “Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.
Hapo Bwana Yesu anafunua ni kitu gani shetani anachowaza au kilichopo ndani ya kichwa chake siku zote…yeye siku zote anafikiria mambo ya duniani tu! (mambo ya wanadamu)…mambo ya kimwili, anawaza siku zote ni namna gani mwanadamu atakuwa anafikiri mambo ya hapa duniani tu!..hatataka mtu awe anafikiria mambo ya kimbinguni ya wakati ujao, yeye ni Maisha ya hapa tu!…hataki mtu afikiri ni nini kitamtokea baada ya kufa! Hataki mtu afikirie kwamba kuna kifo cha ghafla! Hataki mtu afikirie habari za Maisha baada ya haya, ndio maana hapa akamrushia Petro wazo haraka sana kumwambia Bwana hatakufa!. Ili amshawishi ajiwekee hazina hapa duniani na asifikiri mambo yajayo.
Ndugu kama ulishawahi kukaa peke yako na kufikiri ni nini kitakukuta baada ya kufa, ni lazima utakuwa umeona Maisha hayana maana kabisa…hiyo ni hatua ya kwanza ya Mungu kukuvuta kwake, kama ulishawahi kuhudhuria msiba, ndio utajua kuwa Maisha haya hayana maana tunapita tu!..Usipende raha raha tu kila wakati! Kila siku kuhudhuria sherehe na party, hudhuria pia misiba, nenda mahospitini hata siku moja, pita tu! Ujifunze….. shetani hapendi! Wewe uende huko atakuambia aah unakwenda kujitoa kwenye mood tu!..atakurushia wazo la kwenda kujifariji na nyimbo Fulani za kidunia.
Hataki uhudhurie huko kwasababu anajua ukitoka pale utakuwa umepata funzo kubwa sana la Maisha, na hivyo atakukosa, na yeye hataki akukose…shetani anawaza yaliyo ya wanadamu tu! Hataki ufikirie mambo yajayo.
Siku moja jioni nilitoka nyumbani nikawa natembea mtaani tu, nikaenda mbali sana mitaa mipya kidogo, njiani nikawa natafakari Maisha yangu binafsi na mambo mengine ya kawaida..nilikuwa nina amani ya kawaida tu! Lakini nilipita sehemu nikakuta geti la nyumba moja limefunguliwa, na watu wanaingia ndani kwa huzuni, nilibahatika kumwona ndugu mmoja nafikiri atakuwa ni ndugu wa marehemu analia mpaka ameshikwa ndipo nikajua kuwa ulikuwa ni msiba, nami pia nilihuzunika kidogo…nikasema hiyo pia ingeweza kunitokea na mimi pia leo hii…
Kwa kitendo kile, kikanifanya nizidi kuingia kutafakari hatima ya Maisha haya zaidi, likanijia andiko kichwani kutoka katika kitabu cha Mhuhiri
Mhubiri 7:1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. 2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake. 3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo. 4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha”.
Mhubiri 7:1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.
2 Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.
4 Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha”.
Kujifunza juu ya hatima ya haya Maisha sio kukosa tumaini la Maisha hapana! Bali ni hekima..kwasababu hiyo inaonyesha unayapenda Maisha yako, leo utamwuliza mtu una mipango gani ya baadaye, atakupa mipango ya miaka mingi ya mbeleni sana, na ataanza kujiwekea hazina sasahivi…lakini hatakupa mipango ya maisha baada ya kifo, sasa huyu huwezi kusema anaona mbele kwasababu anayeona mbele lazima avuke Maisha haya, azidi kuona mbele Maisha baada ya kufa, huyo ndio anayeona future yake…
Sasa Huyu ni Sulemani ambaye alikuwa na plani kubwa sana za Maisha yake na aliyekuwa ni Tajiri na mwenye hekima ambaye hakuna mfano wake ndiye anayesema haya maneno …”heri kuiendea nyumba ya matanga kuliko nyumba ya karamu”. Ni heri kusikia habari za misiba kuliko kila siku kusikia habari za shangwe tu na sherehe. Kwasababu kwa habari hizo zitakupa chachu ya kutafakari Maisha baada ya hapa.
Usisikilize mawazo ya shetani ambayo hayo ni kukupa wewe tumaini la mambo ya kiulimwengu tu kila siku, anakwambia hutakufa! Utaishi! Na huku upo bado kwenye Maisha ya dhambi, anakuambia utakuwa na heri na kufanikiwa, wakati unaishi na mke/mume wa Mtu. Na wakati maandiko yanasema wazi kabisa roho itendayo dhambi itakufa…shetani atatumia watu kukufariji kwa kila aina ya faraja, atatumia mpaka wanaojiita watumishi wa Mungu kukupa wewe faraja kwamba hutapatikana na mabaya…na wakati maandiko yanasema kinyume na hayo.
Atasema pia, wakristo hawapitiagi dhiki..ndicho alichomwambia Bwana Yesu, kuwa hatakufa..na wakati maandiko yanasema “ulimwenguni mnayo dhiki (Mathayo 16:33)” na “ tena mtakuwa watu wa kuchukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu”..lakini shetani atakwambia mtapendwa na watu wote…tangu lini mafisadi wakawapenda watu wasio mafisadi kama wao?…Danieli alikuwa ni mtu apendwaye mbinguni lakini duniani alikuwa anachukiwa, na watu waliokuwa wanakula rushwa…Na katika Ukristo ni hivyo hivyo zipo dhiki za hapa na pale, ambazo Bwana alituambia mapema kabisa tutakutana nazo ili tuwe na Amani…zitakapotokea tusihuzunike sana.
Hivyo tunajifunza kuyakataa mawazo ya shetani ambayo yanatusukuma kuyatazama mambo ya ulimwengu huu tu, mambo ya kitambo! mambo ya wanadamu Na kutuzuia kutafakari mambo yajayo. Na tunayakataa mawazo hayo kwa formula moja! Iliyorahisishwa katika Neno lake na hiyo ni kwa kutubu kwa kumaanisha kwanza kuacha dhambi na pili ubatizo sahihi wa kuzama mwili wote na kwa jina la Yesu na tatu Roho Mtakatifu..Roho Mtakatifu akishaingia ndani yako ni kama mlinzi wetu, atayaathiri Maisha yako na kuyapeleka anakotaka yeye, kama vile upepo uvumapo usipojua wewe…
atakukumbusha juu ya hatima ya maisha haya na kukupasha habari ya mambo yajayo…
Na baada ya hapo kilichosalia ni kudumu katika kujifunza Neno la Mungu siku zote za wakati wako zilizosalia hapa duniani…ili uwe na uwezo wa kuzipambanua roho, Petro alikuwa hana uwezo wa kuzipambanua roho kwasababu Neno halikuwa ndani yake, laiti angekuwa analifahamu Neno linalosema kuwa “Mwana wa Adamu ni lazima afe kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu” yale mawazo yalipokuja kichwani mwake ya kumfariji Bwana angeyakataa…na yeye mwenyewe angesema moyoni mwake, shetani ondoka ndani mwangu na mawazo yako ya kibinadamu, kwasababu Neno linasema hivi na hivi. Na sisi tunapoyajua maandiko ni silaha tosha, biblia inasema Neno la Mungu ni Upanga wa Roho, linamkata kata shetani vipande vipande.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada basi Wasiliana nasi kwa namba hizi..
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
EDENI YA SHETANI:
Mhubiri 11:3b “…… Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.”
Maisha yetu yanafananishwa na mti, na tunajua siku mti unapoanguka aidha kwa uzee, au kwa kukatwa, kuanguka kwake kunategemea sana jinsi ulivyokuwa. Hata kama ni mnazi unaoonekana umenyooka kama rula, bado unayo sehemu Fulani umelemea upande mwingine, utajua hilo siku ile unapokatwa wakati unadondoka..Kamwe haiwezekani ukawa sawasawa pande zote, na pia ukishalala pale chini, ndivyo utakavyolala hapo hapo milele, kwasababu mti sio kama viumbe hai vingine vinavyoweza kujongea, hata vikianguka vitasimama..Lakini Mti hautembei wala hausogei, hivyo anguko lake ni la milele.
Vivyo hivyo na sisi tunavyoishi, hapa duniani kama unyakuo hautatukuta, basi tufahamu kuwa kifo tutakutana nacho siku moja..Wengi wanasema nikikaribia hicho kipindi nitatubu, nataka nikumbie unapolemea maisha yako yote leo hii ndipo utakapolalia milele siku ile ya kukatwa kwako, huwezi ghafla ghafla tu, ukageukia upande wa pili ingekuwa ni rahisi hivyo Bwana asingekuwa anawahubiria watu injili tangu utoto wao mpaka wanakuwa watu wazima wamgeukie yeye. Si angesubiri tu siku ile wanakufa awahubirie injili waende mbinguni..Haipo hivyo wokovu ni tendo linalogharimu maisha na sio tukio Fulani tu.
Na kama tulivyoona mti unapoanguka unalala hapo daima,iwe ni kaskazini, iwe ni kusini, ndivyo itakavyokuwa baada ya kifo, umeangukia katika uzima utakuwa katika uzima milele, umeangukia katika mauti, utakaa katika mauti daima..Hakuna nafasi ya pili, Wala hakuna nafasi ya katikati.
Hivyo pima maisha yako leo uangalie ni wapi yamelemea kwa sehemu kubwa, na uanze kuyatengeneza upya ili kusudi kwamba hata ikitokea kifo kimekukuta kwa ghafla basi unakuwa na uhakika wa kuangukia mahali salama. Kama bado hujampa Bwana maisha yako, nafasi bado unayo sasa, hapo ulipo tubu na kusema kuanzia leo Bwana ninataka kuegemea kwako, na yeye atakusamehe, kisha kama hujabatizwa nenda kabatizwe, katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji kwa jina la YESU KRISTO, kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na Bwana atakupa Roho wake Mtakatifu kukulinda na kukuongoza sikuzote.
Ubarikiwe sana.
+225693036618/ +225789001312
KIFAA BORA CHA MATUMIZI.
JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?
TUNAYE MWOMBEZI.
Moja ya kazi kubwa PIA shetani anayoifanya ni kuhakikisha watu hawaelewi dhambi ni nini?…Na hivyo anatumia nguvu kubwa kuwafanya watu waamini kuwa chanzo cha matatizo yote ni yeye!…hata mtu akifanya uasherati ni shetani! Mtu akiua ni shetani! Mtu akiiba ni shetani!…Lakini wengi hawajui kuwa shetani naye pia hakudanganywa na mtu, hakukuwa na mtu juu yake wa kumdanganya…alijidanganya mwenyewe (moyo wake ulimpoteza mwenyewe Yeremia 17:9).
Sababu ya kutenda dhambi watu wengi ambao hawaelewi huwa wanamtupia shetani…lakini kumbe ni wao..Shetani, anachokifanya yeye ni kupalilia UOVU tu duniani…lakini yeye sio aliyeuumba uovu, Uovu upo katikati yetu uliumbwa na Mungu, kwa makusudi maalumu ya kutambua wema, kwamfano uovu usingekuwepo basi hata wema usingekuwepo, ili kutambua kitu hiki ni kitamu lazima kiwepo kichungu, lakini kama hakuna kichungu, umejuaje kuwa kile ni kitamu?. (Vivyo hivyo na sisi tumeumbiwa tayari mema na mabaya ni sisi kuchagua)…..Na malaika nao waliumbiwa hicho kitu ilikuwa ni kitendo tu cha wao kuchagua…Na shetani na malaika zake wakachagua mabaya (na huko ndiko kuasi), na matokeo yake wakatupwa duniani…
Na huku duniani tayari kulikuwa kuna mti wa mema na mabaya pale Edeni…Kiasi kwamba hata kama shetani asingekuwepo bado Hawa alikuwa anao uwezo wa kuchagua mabaya, kama angetaka……kwahiyo asili ya uovu sio shetani! Uovu ulikuwepo tangu asili, ni kitendo cha watu kuchagua..(pale Edeni shetani alikuwa ni kama dalali tu! Wa kumvutia na kumshawishi mwanadamu achague uovu). Kwahiyo shetani anachofanya sasahivi yeye na malaika zake ni kuipalilia tu ile njia ya ouvu izidi kuwa pana kwa watu….Ukilijua hilo litakufanya kuwa makini kutokufikiria kila kitu chanzo ni shetani.
Kwahiyo mtu anayekwenda kufanya uasherati leo, ni yeye mwenyewe amechagua uovu kwa ushawishi wa nguvu za shetani…zingati hili (Ni huyo mtu kafanya na sio shetani kafanya kwa niaba yake)…Kwahiyo hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza ni huyo mtu, kwasababu kachagua kufanya mabaya…
Ni sawa leo uende sokoni kununua nguo, ukute maduka mawili mbele yako, moja linauza nguo nyeupe lingine nyeusi…na ndani kila mmoja anakushawishi ununue kwenye duka lake…maamuzi ya mwisho yanatoka kwako wewe, na sio kwa mwenye duka…hapo kama utachagua nyeusi au nyeupe na kwenda nyumbani kukuta kasoro, hapo anayestahili kulaumiwa wa kwanza sio muuzaji bali ni wewe ambaye ulikwenda kuchagua…ulipaswa ukague nguo yote kwa makini kabla ya kuinunua, sio kusikiliza tu maneno ya wauzaji na kuamini!
Na ndivyo ilivyo sasa hivi duniani kuna maduka mawili, moja linauza mavazi meupe(ya uzima wa milele), na lingine meusi ni jukumu lako wewe kuchagua lipi linakufaa…kila moja lina watu ndani yake wanaokushawishi na kukuvutia, maamuzi ya mwisho unatoa wewe..sio muuzaji!…Muuzaji anakazi tu ya kukudalalia basi! Mambo mengine unafanya wewe, uchaguzi unafanya wewe na gharama unaingia wewe.
Leo utasikia mtu anakwenda kuzini, halafu anakwambia ni shetani kafanya vile, atakuambia shetani kanipitia tu!… hajakupitia ndugu ni wewe umechagua mwenyewe uovu, kwa kukubali ushawishi wake…Kama ingekuwa ni shetani, basi Mungu asingesema “siku ile kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu kutoa hesabu ya mambo yake”…asingesema hivyo, badala yake angesema “shetani atasimama kueleza ni kwanini kawaingia watu na kuwalazimisha wafanye dhambi”…Lakini siku ile kila mtu atahukumiwa kwa aliyoyatenda…kwanini? kwasababu si shetani aliwalazimisha watu kutenda, bali ni watu kwa uchaguzi wao wenyewe walichagua uasi…
Yohana 3: 19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Kwahiyo mtu yeyote anayetenda dhambi, ni katenda dhambi kwa idhini yake mwenyewe baada ya kuzidiwa na ushawishi wa shetani kufanya hilo jambo. Hivyo hapo shetani ni mtu wa pili kulaumiwa baada yake yeye…wa kwanza kabisa kulaumiwa ni yeye na ndio afuate shetani.
Hebu tafakari juu ya hili ili upate kuelewa kuwa kuna upofu Fulani unaendelea…..Mtu atakapotenda jambo fulani jema, labda amsaidie maskini hatasema ni Mungu kafanya lile jambo…atasema ni yeye kafanya…ukimwuliza imekuaje umefanya hivyo, atakwambia nimeguswa tu kufanya hilo jambo! Na tena ukimwuliza ni wewe au Mungu ndio kafanya hilo jambo atakwambia ni yeye ndiye aliyefanya 100%….. Mungu ni kama kamsaidia tu…na tena ataamini kuwa anastahili baraka kutoka kwa Mungu kwa alichokifanya lakini huyo huyo mtu hebu afanye uasherati utasikia anasema ni shetani huyo!..sio mimi ni shetani, utaona malaumu yote na sababu zote anamtupiwa shetani na kuanza kumlalamikia Mungu kwanini hakumwua shetani…lakini alipotenda mema hakusema ni Mungu kafanya bali alisema ni yeye, tena alipokea utukufu kutoka kwa watu kuwa yeye ndiye aliyefanya ule wema!.
Ndugu kama ni haki yako kupata baraka kutoka kwa Mungu kwa kutenda mema…jua pia ni haki yako kupata laana kutoka kwa Mungu kwa uovu unaoufanya!..Uovu unaoufanya, Mungu wala shetani hawahusiki, ni wewe ndio unaoamua kuufanya..wao ni kama washauri tu!..Ndio maana Mungu pia atawapa thawabu watakatifu wake watakaoshinda mbinguni, siku ile hatajipa yeye thawabu, atawapa watakatifu kwasababu ni wao ndio walioamua kufanya mema, sio Mungu.
Kumbuka pia unapotenda mema ni Mungu ndiye atakubariki, na unapotenda mabaya ni Mungu ndiye atakulaani na sio shetani, kwasababu sio shetani aliyeuumba uovu, ndio maana unaona pale Edeni baada ya Adamu na Hawa kuasi ni Mungu ndiye aliyewalaani na sio shetani!…aliyesema tutakula kwa jasho sio shetani ni Mungu!…aliyesema tutazaa kwa uchungu sio shetani ni Mungu! Aliyeilaani ardhi sio shetani ni Mungu!. Kwahiyo ukitenda uovu leo hii ni umeuchagua kwa hiyari yako mwenyewe na hivyo utakuwa unaishi katika laana kutoka kwa Mungu. Shetani hahusiki hapo!.
Wengi wanawalaumu pia Adamu na Hawa kuwa ndio sababu ya mambo yote..Ni kweli wao walichangia kuifanya njia ya upotevu iwe pana Zaidi lakini ni vyema ukafahamu kitu kimoja…hata kama Adamu na Hawa wasingekula lile tunda, kusingemzia shetani kuwajaribu Watoto wao, na hata kama watoto wao pia wasingekula tunda kwa kukataa ushawishi wa shetani pia isingemzua shetani kuwajaribu wajukuu wao na vitukuu vyao…na ingeendelea hivyo hivyo mpaka mwisho wa vizazi vyote, shetani angekuwa anandelea kuwajaribu tu wanadamu….hata siku wewe unazaliwa ungemkuta shetani naye pia asingeacha kukujaribu kula tunda hata kama vizazi vyako vya nyuma vyote vimeshinda…Kwahiyo hata kama Adamu na Hawa wasingenaswa pengine ungeweza kunaswa wewe!…uthibitisho ni hizo dhambi za makusudi unazozifanya sasa….
Ndio maana huoni mahali popote kwenye Biblia Mungu akiwalaumu Adamu na Hawa, baada ya kutoka pale Edeni..kwasababu wote tumefanya dhambi… Hivyo geuza mtazamo wako wa kuwasingizia baadhi ya watu na shetani kuwa ndio chanzo cha matatizo Fulani, ni kweli wanaweza kuwa wamehusika kwa sehemu Fulani…lakini sehemu kubwa ya maamuzi ipo kwako!!.
Kristo leo anagonga moyoni mwako umegeukie kumbuka shetani anapenda umsingizie yeye ili siku ile ya hukumu ujute! Useme laiti ningepata huu ufahamu angali nipo duniani nisingekuwa mtu wa visingizio…Chagua mema leo usichague mabaya yaletayo laana. Ni rahisi kuchagua mema, yupo mmoja ambaye aliweza kuchagua mema, yeye ndiye anayeweza kutufundisha na sisi namna ya kuchagua mema…na huyo si mwingine Zaidi ya YESU KRISTO, aliyemzungumziwa mahali Fulani hivi…
Isaya 7: 14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. 15 Siagi na asali atakula, WAKATI AJUAPO KUYAKATAA MABAYA NA KUYACHAGUA MEMA”.
Isaya 7: 14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
15 Siagi na asali atakula, WAKATI AJUAPO KUYAKATAA MABAYA NA KUYACHAGUA MEMA”.
Huyu ndio Mkuu wa Uzima, aliyebeba wokovu, hakuna aliyemfuata yeye akajuta, alituambia maneno haya..
Mathayo 11: 27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11: 27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Hivyo tunamtii na kumfuata kama tulivyo, na mizigo yetu.. kama ni mwasherati unaenda kama ulivyo, kama ni mtazamaji wa pornography unaenda kama ulivyo, kama ni msengenyaji vivyo hivyo, kama ni mlawiti, shoga, mlevi, mtoaji mimba, mwizi,muuaji, mla rushwa, mcheza kamari, mwenye huzuni, mwenye msongo wa mawazo, uliyefungwa na nguvu za giza,..msogelee leo, utue mzigo wako pale… hapo ulipo Tubu kwa kumaanisha kuacha kabisa kufanya hayo mambo, na yeye ni mwaminifu atakusamehe…
Na baada ya kufanya hivyo ili ukamilishe toba yako nenda katafuta ubatizo sahihi wa kuzama mwili wote katika maji na kwa jina la YESU KRISTO, kwaajili ya ondoleo la dhambi zako kulingana na Matendo 2:38, dhambi zinakamilika kuondolewa kwa ubatizo sahihi…na baada ya Hapo Roho mwenyewe ataingia ndani yako na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia na kukusaidia katika kuchagua yaliyo mema na kukataa mabaya..na utakuwa na uhakika wa uzima wa milele.
Kumbuka tunaishi siku za mwisho, siku yoyote Parapanda inalia, na watakatifu watanyakuliwa kwenda juu mbinguni, tujitahidi mimi na wewe tuwe miongoni mwao walioalikwa Karamuni.
Bwana akubariki sana, Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAP
SHETANI NI NANI?
‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI
MKATAE SHETANI NA MAWAZO YAKE YA KIBINADAMU.
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
Yeremia 30:7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Biblia inasema ni siku ambayo haiwezi kufananishwa na siku yoyote katika historia ya siku zote za dunia ambazo zilishawahi kuwepo mambo ambayo yataenda kulikuta Taifa la Israeli, Hicho ndio kipindi cha taabu kuu ambacho Danieli alionyeshwa;
Danieli 12: 1 “ Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile”.
Na Bwana wetu Yesu Kristo alikuzingumzia pia, kuweka msisitizo wa uzito wa dhiki hiyo ..
Mathayo 24:21 “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”
Mathayo 24:21 “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”
Na cha kuzingatia ziadi ni kuwa dhiki hii haitakuja wakati wowote isipokuwa wakati ambapo Israeli imesharudi na kuwa kitu kimoja kama zamani za kale za mfalme Daudi na Sulemani.
Yeremia 30:1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, 2 Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia. 3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki………… 7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Yeremia 30:1 “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema,
2 Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.
3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki…………
7 “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”
Na jambo hilo lilitimia mwaka 1948, baada ya kukaa zaidi ya miaka 2500 bila kuwa taifa huru, Israeli sasa ni taifa huru, na sisi ni mashahidi kuwa tumeshaanza kuona mwanzo wa utungu wa mambo hayo, kipindi cha vita ya pili vya dunia jinsi wayahudi walivyouliwa kikatili na Dikteta wa kijerumani Adolf Hitler bila sababu yoyote, tafakari jinsi wanawake na watoto walivyokuwa wanachukuliwa uchi, na kudanganywa kuwa wanaenda kuogeshwa kumbe wanafungiwa kwenye mabafu ya gesi za sumu (Gas chambers), na huko ndani kwenye vyumba hivyo, vya giza inatupwa gesi moja kali ijulikanayo kama Zyklon B, inawaua watu kama kuku waliochinjwa, huku damu zikitoka midomoni na puani, ndani ya dakika 4 tu zinakuwa ni maiti zilizolala chini. Na mauaji mengine ya kikatili ukifuatilia katika historia utayaona. Wayahudi zaidi ya milioni 6 waliuliwa kwa namna kama hizo kikatili.
Sasa huo ni mfano mdogo sana,(mwanzo wa utungu) kwa hiyo dhiki itakayokuja huko mbeleni. Mambo yatakuwa mabaya zaidi, kutakuwa kuna mateso ya ajabu ambayo hayajawahi kufanyika popote, kama tu wakati wa Hitler watu walikuwa wanachukuliwa kwa marika tofautitofauti na wanawekwa kwenye barafu wakiwa uchi na wanaangaliwa mpaka wafe, huku wengine wakichukua data, kuchunguza ni rika lipi linawahi kufa katika hali ya ubaridi (na hiyo biblia inaiita tu ni mwanzo wa utungu)…unadhani itakuaje utungu wenyewe ukianza?….pengine watu watalishwa nyama za miili yao wenyewe wangali wakiwa hai….Dhiki hii Mungu atairuhusu kwa watu wake Israeli, na watu wa mataifa wachache ambao walibaki kwenye unyakuo….na hiyo yote Mungu ameruhusu kwa makosa ya Israeli ukiendelea kusoma mistari inayofuata ya hiyo Yeremia 30 utaona, na atakayetekeleza hilo zoezi ni mpinga-Kristo, Wayahudi (Waisraeli) wataadhibiwa hivyo lakini baadaye Mungu atawaokoa..
Lakini mpaka hayo yote yatokee, Kanisa la Kristo litakuwa limeshanyakuliwa, mbinguni, Bibi-Arusi sikuzote haandaliwi kupitia dhiki bali anaandaliwa kwa ajili ya sherehe, na ndivyo itakavyokuwa kwa Bibi-arusi wa Kristo, wakati wote huu ambao yupo duniani sasa anaandaliwa kwa ajali ya karamu ya mwana-kondoo, ambayo Kristo amekuwa akituandalia mbinguni kwa miaka 2000 sasa, Siku watakapoisikia paraparanda ya Mungu ikiwaita, muda huo huo watageuzwa kufumba na kufumbua na kuwa na miili ya utukufu ya kimbinguni, wataungana na wale watakatifu waliolala, kisha kwa pamoja watapaa zao mbinguni, kumfurahia Bwana wao. Hivyo watakaopitia hii dhiki ni wale wanawali wapumbavu, ambao hawakujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana wao akiwa hapa duniani….Hao ndio watakaojumuika na wayahudi,
Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Utajisikiaje, siku ile unaona wenzako wapo juu mbinguni karamuni, halafu wewe umeachwa?, umetengwa na uso wa Mungu milele, Ikiwa neema unaichezea leo, usidhani itakuwepo kipindi kile, wakati huo neema ya Mungu itakuwa kwa wayahudi watu wake, kupigwa kwao upofu leo ni ili wewe na mimi tutubu tumgeukie Mungu, (soma Warumi 11:8-36 )wakati ule ukifika Mungu hatakuwa na habari tena na wewe, au mtu yoyote wa mataifa, bali watu wake, wateule wake wayahudi. Na hao ndio Bwana atakaowakoa.
Hizi ni nyakati za mwisho ndugu, usipumbazwe na huu ulimwengu unaopita, angalia ni faida gani unakuahidia maisha baada ya hapa?, majira yanabadilika haya, matukio yanayotokea duniani, ni kuonyesha kuwa dunia imeshafika OMEGA. Acha kusuasua kwenye njia mbili, huu sio wakati wa kuhubiriwa injili ya kubembelezwa tena, mkabidhi Kristo maisha yako leo, tubu kabisa na umaanishe kumfuata, na yeye ni mwaminifu na mwenye huruma, hata kama dhambi zako ni nyingi kiasi gani ataziweka mbali na wewe. Tubu ukabatizwe, Upokee Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?.
WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA.
ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?
Ili kujua kama ku-BET ni dhambi au la! Ni vizuri kwanza kufahamu mapenzi ya Mungu ni yapi?…Huwezi kujua kipi kisichompendeza Mungu kama hujui kipi kinachompendeza…Sasa Mungu alivyotuumba watu wake na viumbe vyake vyote hata Wanyama, alituwekea kitu kinachoitwa dhamira ndani yetu…Hii dhamira kazi yake ni kutulinda sisi tusiende kinyume na mapenzi ya Mungu tunapoishi…Na ipo kwa viumbe vyote (wanadamu na wanyama)..Ndani ya hii dhamira kumefungiwa sheria za Mungu. Kwahiyo pasipo hata Mungu mwenyewe kuzungumza na mtu juu ya jambo Fulani tayari ile dhamira iliyopo ndani yake ina uwezo wa kukamata na kuhisi jambo ambalo sio sawa.
Kwamfano utaona, Simba anauwezo wa kula swala na kumrarua kikatili, lakini simba huyo huyo hamli mtoto wake…ni kwanini? Ni kwasababu dhamira iliyopo ndani yake inamshuhudia kuwa jambo hilo sio sawa…simba hajapewa sheria yoyote na Mungu, lakini ndani ya moyo wake kumefungiwa sheria, kwa kupitia dhamira aliyo nayo. Kadhalika huwezi kuona mbwa au mnyama yoyote analala na mnyama wa jinsia moja naye…
Ni kwanini? ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yao..inayowashuhudia kuwa jambo Fulani sio sahihi, sio kwamba hawana hisia! Wanazo hisia lakini hawawezi wakavuka hiyo mipaka.
Na wanadamu ni hivyo hivyo, kuna kitu kinaitwa dhamira ambayo hiyo imebeba sheria za Mungu ndani yake, kiasi kwamba mtu anaweza asizijue kabisa amri za Mungu, lakini bado akazitimiza vile vile..
Haihitaji biblia kujua kuwa uuaji ni mbaya, au kuwatesa Watoto wako ni vibaya…Hiyo sheria tayari mtu anazaliwa nayo moyoni mwake…ndo maana hata wanyama pamoja na ukatili wao wote hawayafanyi hayo, hawasomi biblia lakini wanazitimiza sheria za Mungu….Haihitaji biblia kujua kuwa utoaji mimba ni vibaya, au kumdhulumu mtu ni vibaya, hiyo tayari mtu angejua hata kama hajawahi kusikia habari za Mungu. Haihitaji sheria kufahamu kumuoa dada yako/kaka yako wa damu ni makosa, hiyo tayari ipo ndani yako, hata hizo hisia zenyewe hazipo licha tu ya dhamira kukushuhudia.
Sheria ilipokuja, kazi yake ni kuitoa hiyo hiyo sheria kutoka katika roho na kuileta katika maandishi..Na hiyo ni kutokana na ugumu wa mioyo yetu, unajua hata watoto wanapotumwa dukani, na wanaonekana ni wazito kidogo kuelewa au wanasahausahu sahau, basi wazazi wanaamua kuwaandikia kikaratasi kidogo cha maelekezo ili wasisahau. Na sheria ilikuja kwa namna hiyo hiyo. Ililetwa kutufanya tuyakumbuke yale tuliyokuwa tumeyasahau katika roho zetu na dhamira zetu..
Sasa Watu waliokuwa wanaishi wakati wa Nuhu, walikuwa hawana sheria yoyote, Maana sheria ililetwa na Musa miaka mingi sana baada ya gharika?..Sasa unaweza kuuliza kama kulikuwa hakuna sheria, wale watu walihukumiwa kwanini?…Walihukumiwa kwa dhamira iliyokuwepo ndani yao…walikuwa wanafanya mambo ambayo ndani ya dhamira zao walikuwa wanajua kabisa sio sawa…lakini waliendelea kuyafanya! Hivyo ikawa dhambi kwao,(Warumi 1:17-30) Na Mungu akawaangamiza wote kwa gharika. Kwahiyo sheria hii ambayo tayari ipo ndani ya dhamira zetu ndio inayojulikana kama INJILI YA MILELE (Ufunuo 14:6). Kwa maelezo marefu juu ya injili hii ya milele Bofya hapa >> INJILI YA MILELE
Sasa mpaka sasahivi hii INJILI YA MILELE ipo, Kuna vitu ambavyo havijazungumziwa hata kwenye Biblia takatifu lakini mtu akiona tu! Anajua hiyo sio sawa machoni pa Mungu..Mfano wa vitu hivyo ni Uvutaji wa sigara, utoaji mimba, mtu anayetoa mimba anajua kabisa ndani ya moyo wake anaua na anafanya jambo lisilo sahihi…ingawa ukitafuta mahali popote kwenye biblia palipoandikwa utoaji mimba ni dhambi huwezi kupata…Lakini mtu anayefanya hivyo anajua kabisa na anauhakika ndani ya moyo wake anamkosea Mungu, na ndivyo ilivyo…au mtu anayetumia madawa ya kulevya…anajua kabisa jambo afanyalo sio jema…
Jambo lingine ni mtu anayefanya masturbation, ukienda kumwuliza mtu anayefanya masturbation unajua ni kosa kufanya hivyo, wala hatakubishia Zaidi ataogopa na atakuuliza namna ya kuacha!…lakini ukienda kwenye maandiko ukitafuta mahali popote pamezungumzia suala la masturbation kuwa ni dhambi hutapaona!…lakini kwanini yule mtu ndani ya moyo wake anauhakika kuwa anachokifanya sio sahihi?..
Ni kwasababu ya dhamira iliyopo ndani yake! (Sheria ambayo Mungu alishaiweka ndani ya moyo wake) inayomshuhudia jambo sahihi na lisilo sahihi…Au leo hii ukimfuata mtu anayeangalia pornography, atakwambia kabisa mimi nafanya makosa, wala hatakubishia wala kukuuliza ni wapi pameandikwa hivyo kwenye biblia?…wala hatataka kujua, yeye anachojua kuwa anafanya dhambi, jambo lisilompendeza Mungu, hilo tu!…Au mtu anayecheza kamari, anajua kabisa jambo afanyalo sio sawa, na anajua kabisa huo mchezo ni wa kishetani, anajua kabisa ni mchezo wa dhuluma ambao wakati mwingine unaweza kuhatarisha, uchumi wake, na usalama wake, anajua kabisa Mungu hayupo katikati ya huo mchezo, Na dhambi nyingine nyingi zinazofanywa na wanadamu ndio hivyo hivyo, hazihitaji biblia kuzihakiki, tayari zimeshajihakiki zenyewe ndani yetu.
Sasa tukirudi kwenye suala la KU-BET na lenyewe ni hivyo hivyo, Kubet ni kamari, isipokuwa iliyohalalishwa na nchi.
Hakuna mahali popote katika biblia imezungumzia habari za kubet…Lakini ipo INJILI YA MILELE ndani ya kila mtu…Inayokushuhudia kuwa hichi kitu sio sahihi.
Kama ukichunguza kwa makini mtu anayebet kabla hajaanza kufanya hicho kitu kina kitu ndani yake kinamshtua kwanza, anaanza kukosa amani na anakuwa na mashaka mashaka na huo mchezo, ndio hapo ataanza kujiuliza, hivi kweli huu mchezo ni wa KiMungu? Hayo ndio maswali ya kwanza mtu anayoanza kujiuliza kabla ya kuingia…Na anapoikataa hiyo sauti na kuingia huko, baadaye haisikii tena ndio anaanza kuona ni mchezo wa kawaida tu usio na madhara yoyote, lakini siku za kwanza kwanza atakwenda mpaka kuuliza watu kama ni sawa kuucheza au la?..Ukishaona hali kama hiyo jua kabisa kuna kitu cha hatari unakiendea..
Na ni kwanini unaanza kusikia hivyo viashiria kabla hata hujajiingiza kwenye huo mchezo? Ni kwasababu mchezo huo ni wa kishetani, na unamwingiza mtu kwenye roho moja kwa moja..Mashirika yote ya betting ulimwenguni yanafanya kazi ya shetani kama ulikuwa hulijui hilo ndugu yangu.., yanafanya mambo mengi ya siri ambayo shetani hawezi kuruhusu watu wayajue, ndio mashirika yanayokusanya utajiri mkubwa kwa shetani..Na hayo ndiyo yatakuja kushirikiana na mpinga-Kristo katika kumpa nguvu.
Mashirika hayo mengi yanamilikiwa na vikundi vya kichawi vikubwa duniani kama freemason, brotherhood, yana kivuli cha kulipa kodi, lakini yana agenda nyingine za siri nyuma ya pazia, yanapokea maagizo kutoka kwa lusifa mwenyewe kufadhili mikutano ya hadhara ya ushoga ili kuipalilia roho ya ushoga duniani,..kufadhili haki za mashoga na wasagaji, kufadhili agenda za utoaji mimba n.k kwa nje yanaonekana ni mazuri, lakini wamiliki wa mashirika hayo ni mawakala wa shetani mwenyewe waliowekwa na shetani kwa kazi hiyo.
Na baadhi ya mashirika hayo pia yanafadhili ugaidi kwa siri, ili kuihimiza dunia ilete ustaarabu mpya wa ulimwengu, na pia yanatumia fedha nyingi kuyanyanyua mashirika mengine madogo madogo yanayofanya kazi kama hizo za kuiharibu dunia.…Shetani anafanya kazi kubwa kuachilia mapepo ambayo yatahakikisha watu wengi wanakwenda kubet na kuhakikisha wanakosa, ili aongeze fedha nyingi katika ufalme wake kwaajili ya kumwekea njia mpinga-Kristo. Biblia inasema shetani anampa aliyewake jinsi apendavyo, yeye ndiye anayechagua ni nani apate na ni nani akose, na kumbuka anawapa walio wake, hawezi kumpa ambaye anajua hamsujudii wala haongezi chochote katika ufalme wake..
Mtu anayekwenda kubet kuna pepo Fulani linamvaa, ambalo litamfanya Kesho arudi tena kufanya hivyo hata kama atakosa mara ngapi lakini hatachoka kubet…Mwisho wa siku unakuwa fukara, na bado taabu yako umempa shetani aitumie.
Kwahiyo Biblia inatuambia tutoke huko? (2 Wakoritho 6:15-18)..tutatokaje! Ni kwa kutubu na kudhamiria kuacha hivyo vitu…Biblia inasema shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, unapotamani kupata fedha za ghafla, tambua ni kama mtu aliyewasha WIFI kwenye simu yake, mtu aliyekaribu na yeye anaweza kuupata mtandao wake, na kadhalika mtu anayependa au kutaka kupata fedha za ghafla, anakuwa ni rahisi sana kuonekana kwenye mitandao ya mashetani na kuvaliwa na maroho…
1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. 10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.
1 Timotheo 6:9 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
10 Maana SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
11 Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole”.
Hivyo tunaonywa tusipende fedha za ghafla! huo ni mtego mkubwa sana shetani anaoutumia…Tembea huko barabarani kwenye nguzo za umeme uone vibao vya waganga,..wote kitu cha kwanza watakwambia…njoo upate utajiri!..Mpango wa Mungu ni kuchuma kidogo kidogo…Sio kwamba hapendi tupate kingi hapana! Ndio mpango wake tuwe na vingi Lakini tukusanye kidogo kidogo…….Tukusanye shilingi mia, mia, kuanzia asubuhi hadi jioni na kupata milioni kumi hiyo ni sawa!….lakini kupata milioni kumi ndani ya dakika moja ogopa sana hizo njia!..Vingi vya hivyo ni mitego ya shetani, Na ndio betting inachofanya.
Mithali 13: 11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
INJILI YA MILELE.
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
KUCHEZA KARATA NI SAHIHI KWA MTU ALIYE MKRITO?
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.