Kanuni ya kufunga na kuomba inafananishwa na kanuni ya Kuku kuyaatamia mayai yake mpaka kufikia hatua ya kutotoa vifaranga.
Ili mayai yaweze kuanguliwa na vifaranga kutokea ni lazima Kuku ayaatamie mayai kwa siku 21, na ili aweze kuyaatamia kwa mafanikio, basi hana budi kujizuia kula kwa kipindi kirefu ili asipoteze joto la mayai yale. Ndio hapo utaona itampasa atoke mara chache chache kwenda kutafuta chakula kisha kuyarudia mayai yake, na atafanya hivyo kwa siku zote 21.
Maana yake kama kuku hatajiingiza katika hiyo adhabu ya kuutesa mwili wake na kujizuia na milo kwa siku 21, hawezi kupata vifaranga!.
Vile vile kuna mambo ambayo yanahitaji “Joto la kiroho” kwa siku kadhaa za MIFUNGO na MAOMBI na KUJITESA. Ili tuweze kuyapata…Vinginevyo hayatatokea kabisa haijalishi tutayatamani kiasi gani!.
Bwana YESU alisema mambo mengine hayatoki pasipo Maombi na Mifungo..
Mathayo 17:21 “[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”
> Ukiona umejaribu kutafuta kitu na hujakipata, ingia kwenye mfungo!
> Ikiwa umeomba na bado hujapata, ongezea na mfungo juu yake!.
> Ikiwa umetafuta na hujapata ongezea na mfungo wa maombi juu yake!.
> Ikiwa unataka Amani, Furaha, au Nguvu za kuendelea mbele, usikwepe mfungo! N.k
Ukiwa ni mtu wa kuomba pamoja na kufunga, utakuwa ni mtu wa mafanikio kiroho na kimwili. Utaangua vingi kwa wakati.. Lakini ukiwa ni mtu wa kukwepa mifungo basi utatumia nguvu nyingi sana kupata baadhi ya mambo.
Danieli 9:2 “katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka KWA MAOMBI, na dua, PAMOJA NA KUFUNGA, na kuvaa nguo za magunia na majivu.………………………. 21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. 22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danielii, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. 23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya”.
Danieli 9:2 “katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.
3 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka KWA MAOMBI, na dua, PAMOJA NA KUFUNGA, na kuvaa nguo za magunia na majivu.……………………….
21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danielii, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.
23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya”.
Na kuna Toba nyingine zinahitaji Mfungo kabisa ili mtu aweze kufunguliwa.
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; 13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya”.
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya”.
Usikwepe mifungo!
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je unaruhusiwa kufanya tendo la ndoa ukiwa katika mfungo?
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.
Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
IJUE FAIDA YA KUFUNGA PAMOJA NA WANYAMA WAKO.
Rudi nyumbani
Print this post
Swali: Je mtu aliyeishi miaka mingi kwenye biblia alikuwa nani?..na Mtu aliyeishi miaka mingi duniani ni nani?.
Jibu: Katika biblia mtu aliyeishi miaka mingi kuliko wote, ni METHUSELA, mwana wa Henoko aliyetwaliwa na Mungu..Biblia inasema huyu Methusela aliishi miaka 969, na hakuna mwingine aliyerekodiwa kuishi miaka mingi kuliko yeye.
Mwanzo 5:25 “Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. 26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. 27 Siku zote za Methusela ni miaka MIA KENDA NA SITINI NA KENDA, AKAFA”.
Mwanzo 5:25 “Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
27 Siku zote za Methusela ni miaka MIA KENDA NA SITINI NA KENDA, AKAFA”.
Wengine walioishi miaka mingi katika biblia ni pamoja na;
Baada ya “Gharika ya Nuhu” miaka ya wanadamu ilishushwa mpaka kufikia miaka 120.. Ambapo ni wachache sana walivuka miaka hiyo, wengi waliishi chini ya hiyo..
Mwanzo 6:3 “Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini”.
Lakini kwajinsi siku zinavyozidi kwenda Miaka ya mwanadamu kuishi duniani ilizidi kushuka.. kutoka 120 mpaka 80
Zaburi 90:9 “Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite. 10 Siku za miaka yetu ni MIAKA SABINI, NA IKIWA TUNA NGUVU MIAKA THEMANINI; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara”.
Zaburi 90:9 “Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10 Siku za miaka yetu ni MIAKA SABINI, NA IKIWA TUNA NGUVU MIAKA THEMANINI; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara”.
Lakini swali kuu ni hili; kwanini miaka ya wanadamu inazidi kupungua siku baada ya siku? Je ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa au mabadiliko ya vyakula?
Jibu rahisi ni kwasababu ya “kuongezeka kwa Maasi”. Wala si mabadiliko ya hali ya hewa! Bali ni DHAMBI!.. Kitu cha kwanza kilichopunguza miaka ya Adamu na Hawa kutoka kuishi MILELE mpaka kufikia kuishi miaka 930 si kingine Zaidi ya DHAMBI!.. wala si kwasababu walikuwa hawazingatii mazoezi au milo kamili!..La!! bali ni dhambi!..
Na kanuni hiyo hiyo ndiyo inayopunguza maisha ya mwanadamu inaendelea mpaka sasa… Na wakati huo huo upande wa pili shetani anajaribu kuwaaminisha watu kuwa ni “Milo wanayokula ndiyo inayopunguza miaka” kwamba wapunguze ulaji wa nyama, na mafuta, na wazingatie mazoezi wataishi miaka mingi.
Mambo hayo ni mazuri, na yanafaa..lakini hayafai katika kuongeza UREFU WA MAISHA YA MTU, Kwani kuna wengi ambao wamezingatia hayo yote lakini wamewahi kuondoka duniani!.. na kuna ambao hawajazingatia hayo yote lakini wanayo miaka mingi duniani.
Kanuni ya kuishi miaka mingi na ya heri NI KUMCHA MUNGU NA KUEPUKANA NA UOVU, hiyo tu… Zishike Amri, fanya mapenzi ya Mungu, maisha yako yatakuwa marefu, hapa na katika ulimwengu ujao.
Kutoka 20: 12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako”.
Bwana akubariki.
Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.
NIFANYE NINI ILI NISILALE NINAPOSOMA BIBLIA.
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya Mungu ya uzima.
Kama kichwa cha somo kinavyosema. “Kuumbwa tu haitoshi”. Ikiwa na maana yapo mengine yanapaswa yafanyike ili uumbaji huo ukamilike.
Ukisoma kitabu cha Mwanzo mstari wa kwanza kabisa wa kitabu kile unasema.
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Lakini cha ajabu ni kuwa uumbaji ule haukukamilisha ulimwengu wetu, ndio maana ukisoma vifungu vinavyofuata anasema..
Mwanzo 1:2a “ Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;…”
Dunia Ilikuwa ni Utupu, na ukiwa. Na yenye giza, kitu cha kutisha. Ndio hapo Mungu anachukua hatua nyingine kuu MBILI (2), ili kuikamilisha. Ya kwanza ni “ROHO WA MUNGU” kutua juu yake, na ya pili kutamka “NENO” lake.
Baada ya hapo ulimwengu ukaanza kuumbika vizuri, na kuwa makao ya mwanadamu, pamoja na kila kiumbe kilichohai kilichoumbwa na mwenyezi Mungu, kama alivyokusudia yeye.
Mwanzo 1:2b…Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza
Kwamba kiumbe chochote kilichoumbwa, Kikikosa Roho wa Mungu, na Neno la Mungu. Kiumbe hicho ni Ukiwa na utupu haijalishi kitakuwa hodari, kikubwa, kina utashi kiasi gani.
Mimi na wewe tumeumbwa na Mungu tukaitwa wanadamu, ni vizuri. Lakini hiyo haitoshi. Bado hatujakamilika kama Neno La Mungu halijafunuliwa ndani yetu. Na Neno hilo si mwingine zaidi ya YESU. Yeye ndio ile sauti ya Mungu tangu pale mwanzo, iliyosema na iwe NURU. Ambayo baadaye ikaja kufanyika mwili, likakaa na sisi;
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, NAO ULE UZIMA ULIKUWA NURU YA WATU. 5 NAYO NURU YANG’AA GIZANI, WALA GIZA HALIKUIWEZA”
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, NAO ULE UZIMA ULIKUWA NURU YA WATU. 5 NAYO NURU YANG’AA GIZANI, WALA GIZA HALIKUIWEZA”
Maana yake ni kuwa kama huna KRISTO YESU maishani mwako. Wewe ni bure.
Vilevile na Roho wake MTAKATIFU kuwa juu yako.
Warumi 8:9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.
Ndio maana kwanini upo umuhimu wa mtu kuzaliwa mara ya pili. Kwa kumpokea Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, ili apate msamaha wa dhambi. Lakini pia kupokea Roho wake Mtakatifu.
Ukikamilisha hayo mawili wewe hapo unakuwa mtu KAMILI na HALISI, aliyeumbwa na Mungu. Unayeweza kumzalia Mungu matunda yote anayotaka.
Okoka ndugu, Fahamu kuwa hakuna maisha nje ya Kristo, hizi ni siku za mwisho. Kristo anakaribia kurudi, ulimwengu upo ukingoni. Umejiandaaje na karamu ya mwanakondoo mbinguni? Ukamilifu wako upo wapi?
Shalom.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
NJIA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.
Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?
AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi.
Waamuzi 16:13 Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. 14 Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande. 15 Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.
Waamuzi 16:13 Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo.
14 Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande.
15 Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.
Mtande ni kifaa maalumu kinachotumika kufumia nyuzi za nguo, kwa kuzisokota pamoja ili kuunda nguo. Tazama mfano wa picha.
Hivyo nyuzi za nguo zilipitishwa katikati ya kamba hizo ngumu za mtande, kisha kuvutwa na kukazwa na mfumaji.
Katika habari hiyo tunaona Delila kazi yake huwenda ilikuwa ni ya ufumaji. Kwasababu ya uwepo wa kifaa hicho katika nyumba yake. Lakini katika harakati zake za kutaka kujua asili ya nguvu za Samsoni, biblia inatuambia, Samsoni alimdanganya kwa kumwambia ikiwa atavifuma vishungi vyake saba vya nywele katika mtande ule, basi, hatakuwa na nguvu za kujinasua, mahali pale.
Delila kusikia vile akaamini ni kweli, kwasababu kwa kawaida mtu ukishikwa tu nywele zako, si rahisi kuleta vurugu kwasababu utakuwa unajiumiza mwenyewe. Delila akizingatia kuwa alijua pia namna ya kufuma nyuzi vizuri. Hivyo alijihakikishia kuwa hilo linawezekana. Na cha kuongezea akapigilia na msumari kabisa, ili atakapojaribu kuzivuta nyewe zake, kutoka pale ashindwe. Kisha wafilisti waje kumchukua.
Lakini bado tunaona hilo halikuwezekana. Samsoni aling’oa misumari ile na kuuvunja mtande ule, Delila alipomwamsha.
Ni nini Tunajifunza katika habari hiyo kama waaminio?
KATIKA USINGIZI MUNGU ANAUMBA, NA SHETANI NAYE ANANASA.
Jiulize kwanini majaribio hayo yote Delila aliyafanya wakati ambao Samsoni amelala?. Alijua kabisa wakati akiwa macho Samsoni hawezi kukubali. Lakini pia swali lingine watu wanalojiuliza, iweje Samsoni, asisikie lolote wakati anatendewa vitendo vile. Kwamfano mpaka Delila anachukua nywele zake na kuziingiza kwenye mtande na kuzibana na kuzipigia misumari, asisikie chochote, ni usingizi wa namna gani?
Ndugu Mitego ya shetani, si rahisi kuigundua, kwasababu anaoutashi wa kuiweka kiasi cha kukufanya wewe usiwe mwepesi kuitambua, au kuisikia. Utashutukia tu umeshanaswa. Hivyo kama mwaminio ni kukimbia usingizi wowote wa kiroho kwa hali zote. Kwa kumtazama na kumfuata Yesu wakati wote. Unapomtazama Yesu, na kumtii kwa kuyakimbia machafu ya dunia. Hapo hujalala kiroho.
Lakini Pia katika usingizi Mungu pia hufanya jambo, na hilo si lingine zaidi ya kuumba. Utalithibitisha hilo kipindi kile alipomuumba Adamu, Mungu anasema.
Mwanzo 2:21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Mwanzo 2:21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Umeona? Ukitulia kwa Bwana, akapumzika kwa Bwana, ukalala kwake. Jiandae kuumbiwa jambo lako bora kuliko yote katika maisha yako. Kama vile Mungu alivyomuumbia Adamu, msaidizi bora kuliko wote.
Kulala kwa Bwana ni kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako, akupe ondoleo la dhambi. Kisha kuamua kuacha mambo yote ya kidunia na kumfuata yeye kwa uaminifu kwa kulitii Neno lake baada ya hapo. Na hapo ndipo unakuwa umelala kwake.
Hivyo chagua leo “Kuumbwa” badala ya “Kunaswa”. Mpokee Yesu sasa, ikiwa upo tayari kufanya hivyo. Basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
KITENDAWILI CHA SAMSONI
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
Je Bwana Yesu alikuwa na nywele ndefu?
Rubani ni nani katika biblia? (Ezekieli 27:8)
Mahali pekee ambapo maandiko yanaeleza kuchoka kwa Yesu, ni siku ile alipokuwa anatoka Uyahudi anakwenda Galilaya. Kwasababu safari yake ilikuwa ndefu, ya saa nyingi, ilibidi waweke kituo kwanza kwenye mji wa mmoja wa wasamaria, wapumzike. Yeye na wanafunzi wake kwenye kile kisima cha Yakobo.
Yohana 4: 5 Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. 6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu AMECHOKA KWA SAFARI YAKE, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Jua la mchana likiwa kali, anasikia mwili ni mchovu hautaki, kufanya kazi yoyote, njaa zinauma, mpaka mitume wakaondoka kwenda kutafuta chakula mjini. Lakini katika mazingira hayo hayo Analetewa na Mungu mtu mwenye dhambi amshuhudie habari za neema ya wokovu. Ndio Yule mwanamke msamaria.
Lakini Yesu hakuwa na udhuru kwa kusema, huu ni muda wangu wa kupumzika, ni muda wangu wa kulala, ni muda wangu wa lunch nile na wanafunzi wangu. Alitii vilevile katika uchovu wake, akaanza kuongea na Yule mwanamke habari za ukombozi, kwa kipindi kirefu kidogo.
Lakini mwisho wa mazungumzo yao haukuwa bure, Yule mwanamke aliondoka, lakini baada ya muda mfupi alirudi na jopo la watu, ili kuja kumsikiliza Bwana Yesu, maneno aliyoshuhudiwa na yeye (Yohana 4:1-42). Na baada ya hapo tena, Samaria yote ikamwamini, sehemu nyingine mpaka wakawa wanataka hata kumfanya mfalme.
Lakini ni nini tunapaswa tujifunze katika habari hiyo? Wengi wetu hatujui kufanikiwa kwa huduma ile ya Yesu pale ndani ya mwanamke Yule zaidi ya wengine wengi, kulitokana na gharama ambazo Yesu aliingia. Yaani katika kipindi cha KUCHOKA kwake, alikuwa tayari kulitimiza kusudi la Mungu. Kitendo hicho rohoni huwa kinageuka na kuwa IMANI, kubwa sana mbele za Mungu.
Je! Na sisi, tunaweza kujifunza jambo hili kwa Bwana. Je! visingizio cha kuchoka, tumeshindwa kutimiza makusudi mangapi ya Mungu, yenye matokeo makubwa kama haya? Nimetoka kazini, nimefanya kazi wiki nzima, hivyo nimechoka siwezi kwenda kuomba. Weekend ni siku yangu ya kupumzika, siwezi kwenda kwenye ushuhudiaji?
Hatujui kuwa hapo ndipo Mungu anapathamini, tunataka siku ambayo tupo “free” tu.
Ukweli ni kwamba tukiwa watu wa kungojea siku ambazo tuna nafasi ya kutosha, au tuna afya, au tuna fursa, au tume-relax si rahisi kuzalisha vema kama wakati ambao tutajiona sisi ni dhaifu. Katika dunia hii ya masumbufu na mahangaiko ya maisha, utajikuta mpaka unamaliza maisha yako hujapata hata huo muda wa kupumzika vema. Hivyo tumia fursa hiyo sasa.
Isaya 40:29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Hubiri injili nyakati zote, omba nyakati zote, soma Neno nyakati zote. Kumbuka wakati wa kuchoka, ipo nguvu ya Mungu kukusaidia. Jenga ufalme wa Mungu. Na Bwana atakutia nguvu.
WALIKUWA WAMECHOKA NA KUTAWANYIKA KAMA KONDOO WASIO NA MCHUNGAJI.
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
YESU HAYUPO KATIKA MAZINGIRA YALEYALE TU SIKUZOTE, USIJISAHAU.
Tunaposikia kuhusu uweza wa Mungu wa kufanya mambo “nje ya wakati” moja kwa moja tunafikiria, juu wa wakati ambao umepitiliza muda wake. Lakini hatufikirii juu ya wakati ambao “bado haujafikiwa” ambao nao pia huitwa “nje ya wakati”.
Kwamfano Elisabethi alipokea ujauzito nje ya wakati, (yaani katika wakati uliopitiliza), wakati ambapo viungo vya uzazi havipo tena, mfano tu wa Sara. Lakini wakati huo huo Mariamu (mamaye Yesu), alipokea pia ujauzito nje ya wakati(Lakini wakati ambao haujafikiwa).
Ikiwa na maana kabla hata hajamkaribia mwanamume, alionekana tayari mimba imeshatungishwa tumboni. Huo ni uweza wa Mungu wa ajabu.
Ni lazima ufahamu kuwa katika maisha yako ya wokovu wewe kama mwaminio, majira yote mawili Bwana atakupitisha kwa mpigo. Fahamu kuwa kuna mahali utacheleweshwa kidogo,lakini pia kuna mahali utawahishwa haraka kabla ya wakati wake. Vyote viwili vitakwenda sambamba, Hivyo hupaswi kuwa na mashaka naye, kwasababu matokeo aliyoyatazamia Mungu juu ya maisha yako ya wokovu yatatokea tu.
Umtazamapo Mungu, usimweke kwenye kipimo tu cha “ndani ya wakati” ulichokizoea. Jiandae kwa lolote. Lakini mpango wake ni lazima utimie.
Maandiko yanasema..
Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Na pia anasema..
Warumi 11:33 “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!”
Ubarikiwe.
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
Maandiko hayaelezi moja kwa moja kifo cha Farao. Lakini baadhi ya hivi vifungu vinatuonyesha Farao alizama na jeshi lake katika bahari ya shamu.
Zaburi 136:15
[15]Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Kuonyesha kwamba sio tu jeshi lake, lakini pia pamoja na yeye..walizamishwa baharini.
Pia vifungu hivi…
Kutoka 14:28
[28]Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
Maandiko hayo, hapo mwishoni yanasema hakusalia hata “mtu mmoja”. Ikiwa na maana hata Farao mwenyewe alikwenda na maji.
Lakini pia andiko linaendelea kusema zaidi…
Kutoka 15:19
[19]Kwa maana farasi za Farao na magari yake na wapanda farasi wake waliingia ndani ya bahari, BWANA akayarudisha maji ya bahari juu yao; bali wana wa Israeli walikwenda katika nchi kavu katikati ya bahari.
Maana yake ikiwa kama magari yake mwenyewe yalizama baharini, ni uthibitisho kuwa hata na yeye mwenyewe alikuwa juu ya gari lake. Haiwezekani yeye kama mfalme aruhusu gari lake liende halafu abakie kwa miguu.
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Farao alikufa katika bahari ile, pamoja na jeshi lake. Na Mungu ilimpasa awahakikishie wokovu kamili watu wake. Kwa kumwangamiza aliye kichwa cha adui zao. Kwasababu tangu mwanzo, masumbufu yote yalishinikizwa na Farao, hivyo alikuwa hana budi kuondolewa na yeye. Ili Israeli waufurahie wokovu mkuu wa Mungu.
Kutufundisha nini?
Mungu huwa anawahakikishia wokovu kamili watu wake, hata sasa tunao ukombozi mkamilifu ndani ya Yesu Kristo kwa kumwimini yeye, adui yetu shetani na mapepo yake yanafukuzwa,mbali na sisi. Lakini yatupasa tusiwe watu wa kutokuamini kama wana wa Israeli jangwani kwa kuishi kama wapagani, kwasababu ijapokuwa Mungu aliwaahidia nchi nzuri iliyobubujika maziwa na asali, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuiingia isipokuwa wawili. Vivyo hivyo na sisi hatuna budi kuishindania Imani yetu. Ili tusionekane tumekosa kuingia kwenye ufalme wa Mungu wetu.
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
YONA: Mlango 1
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
USIMWABUDU SHETANI!
Swali: Je zamani marubani wanaoendesha ndege walikuwepo kama tunavyosoma katika Ezekieli 27:8?
Jibu: Turejee mstari huo..
Ezekieli 27:8 “Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio WALIOKUWA RUBANI ZAKE”.
“Marubani” wanaozungumziwa hapo si Marubani wanaorusha ndege kwamaana kipindi hicho ndege zilikuwa hazijavumbuliwa…bali marubani wanaozungumziwa hapo ni wana-maji (manahodha)..Kwasababu asili ya neno hilo rubani si mwana-anga, bali ni mwana-maji.
Isipokuwa kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na kumavumbuzi mengi kuibuka, basi maneno mengi yanakuwa yanapata maana Zaidi ya moja.
Kwamfano katika biblia yametajwa magari (Mwanzo 45:21)..sasa magari ya zamani si sawa na haya sasahivi, ingawa yote ni magari… vile vile katika biblia kuna mahali pametajwa “Risasi” (Kutoka 15:10) lakini Risasi hiyo si sawa na hii inayojulikana sasa.. Vile vile pametajwa neno “Ufisadi“ (2Petro 2:7).. Lakini ufisadi huo wa biblia ni tofauti kabisa na huu unaofahamika sasa. N.k
Kwahiyo tukirudi katika Rubani, anayetajwa hapo katika Ezekieli 27:8, ni rubani mwana-maji, na si mwana-anga. Ndio maana ukiendelea mbele Zaidi katika mstari wa 29 utaona biblia imeweka sawa…
Ezekieli 27:29 “Na wote wavutao kasia, wana-maji, na RUBANI ZOTE WA BAHARINI, watashuka katika merikebu zao, na kusimama katika nchi kavu”.
Hapo anasema “Rubani zote za baharini” ikiashiria kuwa ni wana-maji na si wana-anga.
Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?
Ufisadi una maanisha nini katika biblia?
EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.
Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
WhatsApp
Swali: Je kuna ubani katika biblia?.. Na kazi ya Ubani ni nini?
Jibu: Ubani ni moja ya viungo vilivyotumika zamani kutengenezea manukato matakatifu yaliyoitwa “Uvumba”..
Viungo hivi (ubani) vinatokana na utomvu unaozalishwa na mmea ujulikanao kama “Boswelia” (Tazama picha juu). Mti wa Boswelia unaanza kutoa utomvu kati ya miaka 8 mpaka 10 baada ya kupandwa kwake, miti hii pia inastawi Zaidi sehemu zenye ukame.
Katika biblia “ubani” ulichanganywa pamoja na viungo vingine vitatu (3) ambavyo ni NATAFI, SHEKELETHI na KELBENA, kutengeneza Manukato matakatifu yaliyoitwa Uvumba ambapo Kuhani mkuu aliyachoma pamoja na kisha kuvukiza moshi ndani ya ile Hema kabla ya kufanya shughuli za upatanisho.
Na uvumba wa aina hiyo, haukuruhusiwa kutengenezwa mfano wa huo kwa matumizi yoyote yale tofauti na hayo ya nyumba ya Mungu.. (maana yake haikuruhusiwa mtu kutengeneza kwa fomula hiyo na kufanya kama marashi nyumbani kwake, au ibada nyumbani kwake, ilikuwa ni kosa).
Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja; 35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu; 36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana. 37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana. 38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake”
Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;
35 nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu;
36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.
37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana.
38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake”
Sasa kuelewa kwa upana Zaidi kuhusu “Uvumba” na maana yake kiroho basi fungua hapa >>KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?
Lakini swali ni je! Sisi wakristo tunaruhusiwa kuchoma Ubani katika ibada au manyumbani mwetu?
Jibu ni La!.. Wakristo hatujapewa maagizo yoyote ya kuchoma ubani wala kujishughulisha nao. Manukato ya Ubani yalitumika katika agano la kale katika hema ya kukutania, na baada ya agano jipya kuanza, mambo hayo yakawa ni ya KIROHO na si ya kimwili tena, hivyo hakuna Uvumba, wala ubani wala hivyo viungo vingine unaopaswa kuhusishwa na ibada yoyote katika agano hili jipya.
Kwanini Ibada hizo za Kuvukiza uvumba na ubani hazipo tena sasa?
Ni kwasababu ile ile za kuondoka ibada za kafara za wanyama.. Hatuwezi sasa kutumia Ng’ombe au kondoo kwaajili ya utakaso wa dhambi zetu, na wakati kuna damu ya YESU, ambayo inatusafisha sasa katika ulimwengu wa roho.
Vile vile hatuwezi kuchoma ubani, na kuvukiza uvumba kama njia ya kuvuta uwepo wa Mungu na wakati tunaweza kufanya hivyo kwa njia ya sala na maombi.
Zaburi 141:2 “Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni”
Sasa Kafara za wanyama (Ng’ombe, mbuzi, kondoo na njiwa) na kuchoma ubani zimebaki kuwa ibada za miungu!… Wote wanaofanya hizo, wanavuta uwepo wa mapepo na si wa Mungu! Hivyo ni muhimu kuwa makini.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
SISI TU MANUKATO YA KRISTO.
MADHABAHU NI NINI?
Chetezo ni nini katika biblia? (Walawi 10:1)
NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?
Dhamiri au Dhamira ni nini kibiblia?
“Dhamiri” au kwa lugha nyingine “Dhamira” ni hisia ya ndani ya mtu (ya asili) inayompa kupambanua lililo jema na lililo baya, lililo zuri na lisilo zuri, linalofaa na lisilofaa. Hisia hii kila mtu anayo na haitokani na mafundisho au maelekezo, bali mtu anakuwa anazaliwa nayo.
Dhamiri ni kama mtu mwingine wa pili, aliyeko ndani yako ambaye anasahihisha hisia zako au maamuzi yako, kabla hujayafanya au baada ya kuyafanya. Kama jambo halipo sawa basi dhamiri inakushuhudia aidha kwa kukosa Amani au raha au ujasiri..
Vile vile kama jambo lipo sawa basi dhamiri yako ya ndani inakushuhudia kwamba kile ufanyacho ni chema, aidha kwa kupata furaha Fulani au Amani au ujasiri.
Kwamfano mtu anapofikiri “kuua/ kumwaga damu” au “kuiba”.. kabla ya kufanya kile kitu “dhamiri” ya ndani itamshuhudia kuwa kile kitu si sawa! Pasipo hata kuambiwa na mtu au kuhubiriwa, kuna kitu tu ndani yake kinamwambia hicho si sawa!.. Na kama ni mtu wa kujali basi haraka sana atahairisha maamuzi yake hayo.
Katika biblia neno Dhamiri limeonekana mara kadhaa.
Sehemu ya kwanza maarufu ni ule wakati ambao baadhi ya Waandishi na Mafarisayo walimletea Bwana YESU mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, kwa lengo la kutaka kumwua lakini pia kumjaribu Bwana. Lakini maandiko yanasema walipopewa ruhusa ya kumtupia mawe, wote walichomwa dhamiri zao na hakuna aliyemhukumu.
Yohana 8:3 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 9 Nao waliposikia, WAKASHITAKIWA NA DHAMIRI ZAO, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? 11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”
Yohana 8:3 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
9 Nao waliposikia, WAKASHITAKIWA NA DHAMIRI ZAO, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”
Vile vile biblia inatabiri kuwa katika siku za mwisho, watatokea watu ambao watasema uongo ijapokuwa dhamiri zao zinawashuhudia, lakini hawatazisikiliza, na watu hawa watawafundisha watu mafundisho ya mashetani.
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”
1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli”
Mistari mingine ihusuyo dhamiri ni pamoja na Matendo 23:1, Warumi 2:15, Warumi 9:1, Warumi 13:5, na 1Timotheo 1:9.
Ikiwa ndani yako unahisi “Dhamiri yako imekufa” au “imepungua nguvu”… maana yake husikii chochote kikikuzuia au kukuhukumu unapofanya jambo lisilo sawa, basi fahamu kuwa adui kaharibu utu wako wa ndani, na hivyo unamhitaji Bwana YESU akuhuishe utu wako wa ndani kwa damu yake.
Unapompokea BWANA YESU, na kubatizwa na kujazwa na Roho wake mtakatifu, ule utu wako wa ndani uliokufa au uliofifia yeye (Bwana YESU) anauhuisha upya…na hivyo Dhamiri yako inafufuka na inakuwa safi. Hivyo fanya maamuzi leo ya kumsogelea yeye karibu na imarisha mahusiano yako naye.
Waebrania 9:14 “basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
Nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.