Title April 2019

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

Mithali 20:14 “Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.”

Ni wazi kabisa kwa jinsi tunavyozidi kuwa hapa duniani kuna mambo ambayo hayakwepeki, mfano kama hatutakuwa wauzaji, basi tutakuwa wanunuzi wa vitu fulani, Mungu karuhusu iwe hivyo ili kutufundisha sisi kwa nadharia mambo yanayoendelea rohoni, na kama tunavyofahamu siku zote ile lugha ya biashara, muuzaji atataka kupandisha thamani ya ile bidhaa yake juu kidogo kwa kiwango ambacho si chake, ili kusudi kwamba ikitokea mnunuzi ataitaka bidhaa ile kwa gharama ya chini kidogo, basi asimpoteze mteja wake atampunguzia mpaka kwenye kiwango cha thamani halisi aliyokusudia kuiuza hapo mwanzo, Na hivyo yule mteja atakapoona amepunguziwa bei basi hiyo itamfanya aridhike na kununua bidhaa ile, pasipo kujua kuwa kile alichokitoa ndio thamani halisi ya bidhaa ile.

Hali kadhalika na mnunuzi naye, anataka kwenda kwa muuzaji tayari kichwani ameshajipanga kuwa atakapofika kwa muuzaji ni lazima ashushe kidogo thamani ya kile kitu, hata kama anajua thamani yake inaweza ikawa ni ile ile iliyowekwa na muuzaji, lakini ni lazima afanye hivyo, hiyo ni ili tu aipate ile bidhaa kwa bei ya unafuu kidogo, na mwisho wa siku anaipata, hivyo hayo ni mambo ya kawaida kabisa na yapo siku zote masokoni…Ili biashara ifanyike ni lazima kuwe na mapambano ya bei.

 

Vile vile na Sisi (mimi na wewe) kama wahubiri tunafanya biashara, na biashara tunayoifanya ni ya kuuza Wokovu kwa watu wenye dhambi, ili tumpatie Kristo faida za watu, ikiwa tutauweka sokoni wokovu wetu katika thamani ya chini, basi tujue kuwa wale watakaovutiwa na kuja kuununua watautaka kuunua kwa thamani ya chini zaidi ya hiyo unayouza, haiwezekani waupokee kwa mara ya kwanza kwa gharama zile zile unazozitaka wewe, kwa viwango vile vile unavyovitaka wewe,..ni hatua kwa hatua..

Sasa injili zetu na mafundisho yetu, yakiwa ni manyonge, mtu unamvuta kwa Kristo leo, halafu unamwambia kuvaa suruali ni sawa, kuweka makucha ya bandia mfano wa mnyama kenge ni sawa, kuimba miziki ya kidunia ni sawa wala hakuna shida yoyote, hatukemei dhambi, hatumuhubirii mtu utakatifu, ambao pasipo huo tunajua kabisa hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao biblia inasema hivyo katika (Waebrania 12:14) muda wote sisi tunamfundisha mafundisho ya jinsi ya kufanikiwa hapa duniani, huku tunapuuzia mafanikio ya Roho yake ambayo ni kwa kumjua Kristo na wokovu wake kamili..anachokifamu tu tangu siku ile tumemvuta kwa Kristo ni “pokea kwa jina la YESU”, Anafahamu tu shuhuda za kichawi zaidi kuliko shuhuda za Yesu, hajui hata baada ya kifo ni nini kinafuata, hajui unyakuo ni kitu gani, hajua maandiko, yeye tunachomuhubiria tu ni kwamba “watapigana nawe lakini hawatashinda”…..

Ni kweli kabisa hapo tumefanikiwa kuwavuta, ni sawa na tunawaudhia bidhaa zetu za wokovu tulizopewa na Kristo, lakini tunategemea vipi watu kama hao wataununua kwa gharama ile ile unayoitazamia wewe, kwamba wawe watakatifu kama wewe au kuliko wewe, hilo haliwezekani kinyume chake wataupokea wokovu wako kwa thamani ya chini kidogo, na ndio hapo utakuta japo ulimleta mtu kwa Kristo lakini maisha yake yapo mbali na Kristo, utasikia ni mzinzi, ni mlevi, utasema mbona nilimhubiria mimi akaokoka?..Ndio ulimhubiria lakini ulimpa viwango hafifu vya wokovu, na hivyo kama ilivyo desturi ya mnunuzi si jambo la kushangaza kuinunua bidhaa yako kwa kiwango cha chini kidogo, na matokeo yake ndio akawa kama alivyo, mtukanaji, mzinzi, mvaaji vimini barabarani, msengenyaji, anajulikana mtaani kwa utapeli, n.k…

Ndugu, biblia inasema kazi ya kila mtu itapimwa, usifurahie watu wengi kukimbilia bidhaa zako, zilizo hafifu za bei ya chini, (mfano wa bidhaa za kichina) zinazotengenezwa na majani tu, ambazo hata jua haziwezi kustahimili, ni kweli utaziuza nyingi kwa wakati mmoja lakini faida yake itakuja kidogo, tofauti na mtu Yule anayefanya biashara ya DHAHABU, atapata mteja mara moja kwa mwezi lakini faida yake ni mara 1000 ya zaidi ya Yule wa mchicha.

1Wakorintho 3: 11 “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedhaau mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.

13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto”.

Unaona hapo?..Tunapaswa tujitathimini ni wokovu upi tunawapelekea wenye dhambi, ili siku ile tusije tukajikuta wote tunaangukia katika hasara na majuto, na kazi zetu na taabu zetu zikaonekana kuwa ni bure…Tuupe wokovu thamani yake, tuwafundishe watu UTAKATIFU na NENO la Mungu, na TOBA! tusiwafiche juu ya hukumu inayokuja, tuwaambie ukweli njia inayokwenda UZIMANI ni nyembamba nayo imesonga nao wanayoiona ni wachache, na inayoenda mautini NI PANA, tuwaambie kulingana na maandiko wanawake kuvaa vimini, suruali, mapambo, ni dhambi na vinapeleka wengi kuzimu. Ni kweli mambo kama hayo hayapendwi lakini mnunuzi atakayekuja kuununua wokovu wa namna hiyo..Atakuwa ni wa uhakika, na ndio hao biblia inasema mbingu nzima na malaika juu mbinguni wanawafurahia wakitubu..Lakini sio wokovu tu mwepesi ambao huo kila mtu anasema anao lakini roho yake ipo mbali ni Kristo.Hatupaswi kuhubiri vile watu wanavyovitaka, bali kile Kristo anachokitaka, hilo ndio jukumu letu.

Naamini, utakuwa umeongeza kitu katika vile ulivyojaliwa kuvijua, Bwana akubariki na atuongezee Neema yako sote tuzidi kumjua yeye. 

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

 


Mada Zinazoendana:

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

LULU YA THAMANI.

MAMA WA MAKAHABA


Rudi Nyumbani

Print this post

MWAMUZI WA KWELI:

Shalom mtu wa Mungu, ni siku nyingine tumepewa neema ya kuishi, Hivyo karibu kwa pamoja tushiriki kujifunza maneno ya uzima, ambayo ndio msingi hasaa wa sisi kuwa hapa duniani.

Tukisoma biblia tunaona jinsi Mungu alivyowanyanyua waamuzi wengi tofauti tofauti kwa udhihirisho tofauti tofauti katika vipindi vya awali kabisa baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri,Na Mungu aliwanyanyua kwa lengo lile lile moja la kuwarejesha watoto wake katika njia sahihi, kuwarejesha mahali ambapo walipaswa wawepo.Hivyo kitu alichokifanya Mungu kwa wakati ule ni kumtia “mafuta ya kipekee” mtu mmoja ili aende kushughulika ipasavyo na yule adui yao mtekeaji, na mwisho wa siku wanapata ukombozi wao kuwa yule mtu Mungu aliyemtia mafuta..

Kwa mfano tunaweza kumwona Musa, Mafuta yaliyokuwa juu ya Musa ni ISHARA NA MIUJIZA na yale MAPIGO. Hivyo kwa kupitia huduma hiyo aliweza kukishusha kiburi cha Farao na Misri nzima na hivyo wakaweza kuwaacha wana wa Israeli waende katika nchi yao Mungu aliyokusudia wafike ili wakamtumikie Mungu. Lakini japo ishara zile kubwa zilionekana kwa mkono wa Musa bado watu wale hawakupata ukombozi mkamilifu ambao ungewafanya wawe huru kabisa kabisa mbali na maadui zao wote.

Tunaona pia wakati mwingine Mungu aliwanyanyanyulia mwamuzi mwingine baada ya kutumikishwa na maadui zao kwa muda mrefu kutokana na dhambi zao wenyewe ndipo Mungu akawaletea Gidioni kwa Roho(Mafuta) ya ushujaa ili kuwaamua kwa upanga,(Waamuzi 6)..Ni kweli mwisho wa siku walipata ukombozi, lakini ukombozi ule ulikuwa ni wa kitambo tu, baada ya muda kidogo watu walirejea katika dhambi zao za kumwasi Mungu.

Hali kadhalika tunaona wakati mwingine Mungu alimtia mafuta Samsoni katika upako wa “Nguvu za kibinadamu”…Hivyo kwa nguvu zile za kimwili aliweza kuwashida wafilisti mpaka kuwafanya wawaache huru kabisa wana wa Israeli. Lakini ukombozi ule ulidumu kwa muda tu, haukuweza kutoa ulinzi wa kudumu kwa wana wa Israeli,kwa wakati ujao.Ndivyo ilivyokuwa siku zote waamuzi zaidi ya waamuzi 12 walipita juu ya Israeli.

Hali kadhalika wakati ulipofika walipohitaji kiongozi, Mungu aliwanyanyulia mtu mwenye Hekima atakayeweza kuwaamua katika mambo yote. Na hivyo akatokea Sulemani, wakamfurahia kwa muda lakini alipokengeuka kwa muda nchi ilitetereka kwa kasi sana, na kusababisha watu kurejea katika hali zao za zamani.

Vivyo hivyo tunaona kwa manabii kama Samweli, Eliya, Elisha, Samweli, Yehu, Yohana mbatizaji ambaye Yesu alisema watu waliifurahia nuru yake kwa kitambo tu (Yohana 5:35) na baadaye ikazima..wote hao Mungu aliwatia mafuta kwa namna tofauti tofauti ili kuwaokoa au kuwarejesha wana wa Israeli katika mstari waliopaswa wawe, lakini hakukuwa na hata mmoja aliyefanikiwa kuleta ukombozi mkamilifu wa kudumu kwa watoto wa Mungu, licha ya kuwa walikuwa hodari na mashujaa.

Lakini tunasoma katika biblia wakati ulipofika wa Mungu kumleta KRISTO duniani, hakuja na kauli mbiu ya mapanga au nguvu za misuli kama Samsoni, hapana badala yake alikuja kutumbua JIPU ambalo lilikuwa limekaa kwa muda mrefu kwa SIRI tangu zamani ambalo ndio lilokuwa linawafanya watoto wa Mungu wajione ni wananafuu kwa kipindi kifupi tu pale wanapookolewa na waamuzi lakini kumbe ugonjwa bado upo ndani yao, na ndio maana mwisho wa siku wanaishi kurudia kumuudhi Mungu..

Waamuzi wote waliotangulia walikuwa wanatoa tu dawa za kutuliza maumivu (Pain-killer), lakini YESU alipokuja kuutibu ugonjwa wote,kutoa mpaka mzizi wa mwisho na kisiki, wala hakikusalia chochote si hata kovu la alama.

Na ugonjwa huo si mwingine zaidi ya DHAMBI ambayo chimbuko lake ni SHETANI.

Na ndio maana ukisoma agano la kale utaona Shetani akitajwa mara chache sana, utaona shetani akijidhihirisha mara chache sana, tofauti na ilivyo katika agano jipya…Hivyo BWANA alivyokuja ilikuwa ni kwa lengo la kumweka huru mwana yoyote wa Mungu, tena kuwa huru kweli kweli, na sio nusu nusu kesho utumwa unajirudia… na ndio maana baada yake yeye hakuna mkombozi mwingine yeyote anayehubiriwa, hata hapa hatumuhubiri mtu mwingine zaidi ya YESU yule aliyesulibiwa miaka 2000 iliyopita na aliyeandikwa kwenye biblia takatifu kwamba yeye ndiye anayeweza Kumwokoa mtu na kumfanya kuwa huru kweli kweli, hana mshirika na yeye ndiye mwanzo na mwisho, hakuna mwingine.

Yeye mwenyewe anasema.. Yohana 8:36 “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.

YESU anakomesha dhambi kwa mtu yeyote anayemwamini, kumbuka dhambi ndio chimbuko la kila kitu; dhambi, ndio chimbuko la magonjwa, ndio chimbuko la mateso, ndio chimbuko la tabu, ndio chimbuko la kuteswa na mapepo, ndio chimbuko la kukosa raha, na kukata tamaa ya kuishi ndio chimbuko la masumbufu ya kila namna unayoyofahamu wewe huku duniani, ndio chimbuko la mauaji na vitendo vyote viovu vinavyoendelea huku duniani…n.k.

Dhambi ndio “control tower” ya shetani, ndio dira yake hiyo kukumaliza wewe na mimi..Wana wa Israeli walikuwa wanapata ukombozi wa miili yao kutoka kwa maadui zao, lakini hawakujua kuwa bado hajawekwa huru kweli kweli kwani yao dhambi bado zilikuwa zinawatawala, na shetani ametulia kimya asiwafunulie siri hiyo..na ndio maana baadaye waliendelea kurudi katika mateso yao ya siku zote, lakini mtu anayemwamini YESU KRISTO leo hii, hatarejea tena katika mateso yake ya kwanza.

Kumbuka wale waamuzi walipoondoka habari zao ziliishia pale pale lakini YESU wakati alipokuwa duniani alitujali na kutuombea kwa Baba tulindwe na yule mwovu, halikadhalika na alipopaa juu kwa Baba amesimama mpaka sasa kama kuhani mkuu akituombea kwa Mungu..Hivyo unaweza kuona hapo mtu aliye ndani ya Kristo kweli kweli sio wale mguu mmoja nje mwingine ndani hapana bali yule aliyekusudia kutembea na Kristo anayo faida nyingi kiasi gani!…Shetani anafahamu kabisa mtu wa namna hiyo hawezi kumpata tena milele, kwasababu mwamuzi wake, mkombozi wake anasimama mbele yake daima masaa 24, kumuamua na kumlinda.

Leo hii watu watashangaa inawezekanikaje mtu kuishi bila kuzini, mtu kuishi bila kutazama pornography, kuishi bila pombe, kuishi bila sigara, kuishi bila kuongoa matusi, inawezekanikaje mtu kuishi maisha ya furaha wakati huna pesa, inawezekanikaje unapitia shida zote hizo lakini bado tumaini lako lote lipo kwa Kristo, inawezekanikaje katika kizazi hiki cha Sodoma na Gomora, kutokuvaa suruali kwa mwanamke, na kuweka mawigi na ma-lipstick na marangi usoni, wala kupaka uwanja kama Yezebeli, inawezekanikaje unadumu katika imani bila kutetereka…

Hawajui kuwa nguvu hizo si zake bali ni za yule mwamuzi wake YESU KRISTO aliyemchagua maishani mwake, laiti zingekuwa ni zake asingekuwa vile alivyo leo…..

Maneno ya YESU yana nguvu ndugu, hilo tunalithibitisha kwa maombi yake aliyomwomba Baba akiwa hapa hapa duniani akisema..

Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, KWA JINA LAKO ULILONIPA UWALINDE HAWA, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyowa ulimwengu.

15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; BALI UWALINDE NA YULE MWOVU.

16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli”.

Unaona hapo?, YESU aliwaombea wale waliomwini kuwa Baba awalinde na yule mwovu,na si watu wote..Sasa kama Kristo amekataa kukuombea mtu mwingine akikuombea ina faida gani?? ni sawa na bure tu!….hivyo mtu yeyote anayemwamini Kristo sasa kwa kumaanisha kabisa kumfuata na kujikana nafsi yake kama mitume na sio kwa maneno tu , hapo hapo bila kupoteza muda Neno hilo linakuwa linaanza kufanya kazi ndani yake, na ndio hapo anajikuta anao uwezo wa kuvishinda vishawishi vyote vya shetani vile ambavyo hapo mwanzo alikuwa hawezi kuvishinda kwasababu nguvu za shetani zinakuwa hazijakaa juu yake kumtawala.

Vile vile, hiyo haiishii hapo tu bali mtu huyo hata akihitaji lolote kutoka kwa Mungu, mwamuzi wake wakati wote yupo kumtetea huko juu mbinguni..Ni faida juu ya faida.

Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; TENA NDIYE ANAYETUOMBEA”.

Sasa kama Mungu hapokei mashtaka yako…mtu mwingine akikushtaki yadhuru nini?

Unaona Faida zote hizo ni kwa mtu yule aliyemwamini Kristo,lakini ikiwa upo nje ya wokovu, au upo vuguvugu leo huku kesho kule, usijidanganye fahamu kuwa hutakaa uishinde dhambi milele, itaendelea kukusumbua na huku shetani akiichochoa zaidi na zaidi, utaendelea tu kutazama pornography, kufanya mustarbation na kuwa mzinzi, na kuvaa mavazi machafu ya kikahaba na kwako mambo hayo yataendelea kuwa magumu kuyaacha hata kama utatamani kuyaacha hutaweza kwasababu Kristo hajakamilika ndani yako..Na mwisho utakufa katika hali hiyo hiyo ya dhambi na kujikuta kuzimu. Kwasababu biblia hiyo hiyo inasema mshahara wa dhambi ni MAUTI!

Ni maombi yangu sote tutamtazama huyu MWAMUZI mkuu, aponyaye roho zetu na miili yetu kuanzia sasa, kwake kuna raha, kwake kuna amani, kwake kuna tumaini, kwake kuna utulivu…

Kwa kumalizia yatafakari maneno yake haya..

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Ubarikiwe sana. Tafadhali “SHARE” ujumbe huu na wengine. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

TUNAYE MWOMBEZI.

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

DHAMBI YA ULIMWENGU.


Rudi Nyumbani

Print this post

RACA

Mathayo 5: 20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; NA MTU AKIMFYOLEA NDUGU YAKE, ITAMPASA BARAZA; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.

Umewahi kujiuliza kumfyolea ndugu yako ni kufanya nini?

Siku moja, kuna mtu aliniudhi sana nikakasirika sikumwambia chochote ila nilimwonyesha hisia ya kukasirika… Sasa wakati naongea na mtu mwingine nikamtaja na kusema mtu fulani ameniudhi sana ni “mpumbavu sana” nikamtajia na sababu ya alichonifanyia…Baadaye kidogo hasira zilivyoanza kupungua nikaanza kusikia kukosa amani na kuhukumiwa ndani…

sikujua tatizo liko wapi lakini nilijua kuna tatizo…Nikaanza kujitafakari tukio lilolopita nikasema moyoni mimi ni mkristo sipaswi kuwa na hasira hivi..Baadaye nikaenda kutubu..lakini ndani nilikuwa bado najihisi sijatatua tatizo, Nikachukua biblia nikamwomba Bwana azungumze na mimi juu ya hii hali.

Nikafungua biblia mstari wa kwanza niliokutana nao ndio huo…”21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; NA MTU AKIMFYOLEA NDUGU YAKE, ITAMPASA BARAZA; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.

Baada ya kuusoma huo mstari, nilijisikia vibaya sana…nikaanza kujiuliza ni nini maana ya “kumfyolea ndugu yangu” kwamaana siku zote nasomaga lakini sielewi, maana ndio sentensi ya kwanza kukutana nayo nilipofungua biblia,Nikaenda kutafuta kwenye kamusi na kwenye biblia ya kiingereza na nyingine tafsiri yake…Nikapata tafsiri. Neno kufyolea linatoka kwenye Neno la Kigiriki linaloitwa “RACA”..Na maana ya Neno hilo “RACA” ni kichwa kisichokuwa na kitu, au kichwa maji kwa lugha zetu. Au “mpumbavu” kwa neno rahisi zaidi.

Kwahiyo maana ya kumfloyea ndugu yako ni kumpa Neno baya linaloonyesha udhaifu wake..kama vile mpumbavu, mjinga, tahira, mshenzi, mpuuzi…n.k Hayo ni maneno yanayoonyesha moja kwa moja udhaifu wa mtu, na Bwana katuonya tusiyatumie kabisa hayo..Na mtu anayeyatumia hayo itampasa Baraza, maana yake kikao cha hukumu, baada ya kujua hilo nikatubu tena kwa mara ya pili, nikaacha kutumia hayo maneno nikasema sitakaa tena nitumie hayo maneno na Bwana anisaidie…hata kama nimeona mtu ni kweli kafanya upumbavu lakini sitamwita mpumbavu….labda ninaweza kumwambia jambo ulilolifanya ni la kipumbavu kwa nia ya kumrekebisha sio kumkosoa ili abadilike lakini sio kumwita mpumbavu au mjinga au mshenzi.

Unajua ni kweli Biblia kwenye agano la kale sana sana kwenye kitabu cha Mithali na Zaburi imetaja sana juu ya watu wapumbavu na wajinga…Ni kweli Daudi na Sulemani walitoa hekima zao kwa wajinga na werevu…lakini hao hawakuwa utimilifu wa mambo yote..walimjua Mungu kwa sehemu, yupo mmoja ambaye aliyekuja kuitimiliza torati yote mwenye hekima kuliko Sulemani ambaye alimjua Mungu kwa utimilifu wote..”ndiye anayetuambia TUSIMWITE MTU YOYOTE MPUMBAVU WALA MJINGA”…Daudi aliua lakini yupo mmoja anayetuonya “hata tusimwonee ndugu yetu hasira kwasababu ni sawa na kuwa muuaji”…Musa alitoa ruhusa ya kuoa wake wengi lakini yupo mmoja anayetuambia “hapo mwanzo Mungu alimwumba mwanamke na mwanamume, kwahiyo ndoa ni mke mmoja na mume mmoja tu“

Kwahiyo tumsikilize Daudi au Musa au tumsikilize Yesu ambaye ni Bwana wa Daudi na Musa?..Yohana mbatizaji alisema “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua Yohana 3:30”…Na hata Daudi au Musa au Sulemani au Eliya wangekuwepo leo hii wangesema maneno hayo hayo..”kwamba sisi hatunabudi kupungua bali yeye kuzidi”.

Kwahiyo Ndugu unayesoma ujumbe huu,usitumie agano la kale, kuhalalisha laana juu ya ndugu yako wala kumdhihirishia udhaifu wake kwa kumwambia yeye ni mjinga, au ni mpumbavu, au mshenzi au kichwa maji au kichwa hewa n.k NI DHAMBI, hauhitaji uwe muuaji ndio ihesabike kuwa wewe ni muuaji! Kitendo cha chuki tu kujengeka ndani yako au Neno la kudhalilisha likitoka kinywani mwako tayari ni picha tosha ya mambo yaliyopo moyoni mwako, wewe na mtu anayeua hamna tofauti..wote wawili asili ya dhambi yenu ni moja! Chuki au hasira ndani ya moyo…isipokuwa mmoja hasira yake imeishia kutukana mwingine kuua! Kwahiyo wote ni sawa na wauaji tu! Maandiko yanasema hivyo.

Ni matumaini yangu kuwa umepata kitu, na Bwana atusaidie sote tuishi katika njia inayompendeza yeye kila siku. Tukue toka utukufu hata utukufu tukijifunza kutokana na makosa.

Mungu akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

KWANINI AWE NI PUNDA NA MWANA-PUNDA?

Tukisoma injili ya Mathayo 21:2-7, tunaona Bwana akiwaambia wanafunzi wake maneno haya:

“2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona PUNDA AMEFUNGWA, NA MWANA-PUNDA PAMOJA NAYE; wafungueni mniletee.

3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.

4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,

5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.

6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,

7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.”

*** Lakini tukirudi kusoma kwenye Injili ile ya Marko na Luka utaona waandishi wale wanamtaja mnyama mmoja tu kana kwamba hakukuwa na mwingine pamoja naye kwamfano tukisoma ile injili ya Luka 19:30 inatuambia ..

“30 akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.

31 Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji.

32 Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia.

33 Na walipokuwa wakimfungua mwana-punda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwana-punda?

34 Wakasema, Bwana ana haja naye.

35 Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana-punda, wakampandisha Yesu.

36 Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani”.

Unaona? Ni rahisi kusema maandiko yanajichanganya, lakini si kweli maandiko yapo sawa siku zote, embu jaribu kuwazia mfano huu, watu wawili walioshuhudia ajali iliyotokea mpanda wiki 2 zilizopita waliitwa kituo cha polisi ili kutoa taarifa ya tukio lilivyotokea..Mmojawapo akasema: niliona fuso iliyobeba mizigo ikienda moja kwa moja kuivaa gari ndogo ya abiria, na ghafla nilichokiona ni watu wakitoa nje ya vioo, wakirushwa huko na huko na wengine wakipondwa vibaya na ile fuso iliyokuja kulala juu ya lile gari la abiria hivyo ikapelekea kusitokee abiria yoyote aliyepona.,. Lakini shahidi wa pili naye alipoitwa atoe taarifa zake alisema, niliona gari kubwa likiwa katika mwendo wa kasi sana likitokea upande wa juu, lakini ghafla pikipiki ikakatiza mbele yake, na yule dereva alipokuwa katika harakati za kuikwepa pikipiki ile, alijikuta anaacha njia yake na kuingia upande wa pili na hapo ndipo alipokutana na lile gari dogo la abiria na kusababisha ajali.

Sasa kama ukiangalia mfano huo utaona mtu wa kwanza hakutoa habari za mwendesha pikipiki, yeye alitoa hasa maelezo ya ajali ilivyotokea lakini wapili alizungumzia zaidi chanzo cha ajali kuliko ajali ilivyokuwa, lakini hiyo haiwafanyi mashahidi wale wawili kuwa waongo kwasababu maelezo yanayotofautiana, wala hauufanyi ushuhuda wao kujichanganya.

Na ndivyo ilivyo katika habari hii ya punda, kulikuwa na sababu Mungu kuruhusu waandishi hao watoe taarifa kwa jinsi tofauti ili atufundishe sisi kitu..Ni kweli kabisa punda aliyechukuliwa pale hakuwa punda mmoja, Bwana aliwaagiza mitume wake wamlete Punda,akiwa na mtoto wake, japo shabaha yake ilikuwa ni Yule mtoto wa punda, na sio Yule punda mkubwa na ndio maana waandishi wale wengine hawakusumbuka kueleza habari za wote isipokuwa yule mwana-punda tu peke yake kwasababu yeye ndio ilikuwa shabaha kubwa katika habari ile , lakini tukisoma huku kwingine kumbe Bwana hakuona vema aende peke yake, bali pamoja na mama yake..

Hiyo ni kutupa sisi picha zaidi, juu ya mazingira yaliyokuwa yanamzunguka mwana-punda yule, kutuonyesha ni jinsi gani yule mwana-punda alivyokuwa bado ni mdogo, bado ni mchanga hawezi pengine kwenda mahali popote peke yake bila mama yake,hajafikia hatua bado ya kutumia katika utumishi wowote, bado ananyonya, hivyo alihitaji msaada mkubwa sana wa mama yake pembeni au kama si msaada basi alihitaji walau faraja ya mamaye.

Biblia inatuambia alikuwa bado hajakomaa kuweza kubeba mizigo wala kupandwa na mtu yeyote.

Bado alikuwa ni mchanga kabisa, lakini ndiye huyo Bwana aliyemuhitaji. Tunaweza kujiuliza ni Kwanini Yesu hakumwonea huruma walau angempanda mama yake, Yule mtoto apumzike pembeni mwa mamae…Lakini hilo halikuwa chaguo lake mambo yalikuwa kinyume chake..

Ndugu/Kaka, kumbuka mahali ulipo, katika udogo wako, katika uchanga wako wako uwe ni wa kimwili au wa kiroho kiasi cha kwamba huwezi kuenenda mwenyewe bila kutegemea msaada wowote kwa walio juu yako, hujawahi kutumika katika utumishi wa aina yoyote ile, lakini Bwana anakuita umtumikie katika hali hiyo hiyo uliyopo, chini ya huyo huyo kiongozi wako wa kiroho ambaye anakufundisha..Bwana anakuita ukamtumikie, hivyo usikwamishwe na chochote, Bwana aliyemwita Yule ndiye anayekuita na wewe, (wote wawili amewaita)….Yeye hana upendeleo wala jicho lake si kama macho yetu, haangalii cheo, umaarufu wala uzoefu…

Lakini tukiurudi kwenye hiyo habari…kiukweli hawezi kuwapanda wote wawili kwa wakati mmoja, bali amekuchagua wewe ULIYE MDOGO UMTUMIKIE, Ili Yule mkubwa asimame pembeni yako kukufariji ,.. Bwana hawezi kumtumia Yule kwa viwango vya sasa anavyovihitaji kwasababu kashatumika tayari..Ni zamu yako sasa, leo hii wewe bado ni fresh, anakuhitaji sana katika utumishi wake, wa kumtukuza yeye katika nyakati hizi za mwisho za kumalizia, Mteule wa Bwana.

Umekuwa ukiwaangalia viongozi wako kama kitu cha kurejea, ni jambo jema, sio jambo baya,umekuwa ukijiona hujafikia bado viwango vya kutumika mbele za Mungu, mpaka utakapipitia pengine madarasa Fulani au chuo fulani au hatua Fulani kama za mchungaji wako au mwalimu wako, hiyo ni kweli kabisa, lakini Yesu amekuchagua wewe sasa katika udogo huo, ukamtukuzwe katikati ya mataifa. Hivyo Ndivyo ilivyompendeza yeye…Bwana Yesu alisema hivi.

“Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, UKAWAFUNULIA WATOTO WACHANGA. 26  Naam, Baba, KWA KUWA NDIVYO ILIVYOPENDEZA MBELE ZAKO.(Mathayo 11:25).

Unaona? Hivyo ndugu ikiwa utausikia ujumbe huu, ikiwa utasikia wito wa Mungu ndani yako, usikawie kawie, wala kujiuliza uliza mara mbili eti mimi nafaa, au nitaweza?, ingia gharama ya kumfuata Kristo, jitwike msalaba wako, umfuate sasa, neema hiyo haitadumu milele juu yako ukichelewa chelewa shetani naye yupo pembeni kutaka kukutwika mizigo yake, au akupande ili akutumie katika mambo yake maovu, na kama unavyofahamu Kristo hatampanda punda Yule ambaye tayari kashatumiwa, wakati ndio huu uusikiapo ujumbe huu.. chukua uamuzi sasa. Kwasababu yeye mwenyewe alisema..

Mathayo 28:29 “JITIENI NIRA YANGU, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Sasa usisubiri shetani akutie nira yake ngumu katika uchanga wako, huu ni wakati wa kusema mimi na YESU tumefunga pingu za maisha milele..Na kuanzia sasa namaanisha kumfuata YESU katika hali zote zitakazokuja mbele yangu. Na hakika atakuangazia wema wake kwa wakati wake aliouweka juu yako..Kumbuka Punda Yule mdogo aliyekuwa akikaa mabandani tu na kula majani, muda mfupi baadaye tunamwona akitembea juu ya red-carpet, Hiyo ni kututhibitishia kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtumikia Bwana akaja kujuta maishani.

Na kumbuka leo Tarehe 14, mwazi huu wa Nne ni sikukuu ya Mitende…wakristo wote duniani wanaadhimisha siku ile kuu Bwana aliyoingia Yerusalemu huku akiwa amempanda mwana-punda…Hebu huyo mwanapunda leo awe wewe…Mwambie Bwana nipo mimi, nitwae jinsi nilivyo, niwe chombo chako, wewe Mfalme wa wafalme, Na hakika utauona wema wa Mungu kwa viwango ambavyo havipo.

Marko 11: 7 “Wakamletea Yesu yule mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.

8 Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani.

9 Nao watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana;

10 umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. HOSANA JUU MBINGUNI.”

Ni matumaini yangu, utafanya hivyo sasa.

Bwana akubariki na Jina la BWANA YESU libarikiwe daima. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MSHAHARA WA DHAMBI:

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Shalom Mtu wa Mungu karibu tujifunze Maneno ya Mungu wetu, kama wengi wetu tunavyojua hakuna maisha nje ya Yesu Kristo, yeye pekee ndio sababu ya sisi kuendelea kuishi leo hii hapa duniani kama tulivyo, tunaishi kwa ajili yake, na hata tukifa tunakufa kwa ajili yake..

Warumi 14: 7 “Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.

8 Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.

9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.” 

Yesu Kristo pekee ndiye aliyepewa mamlaka yote ya vitu vya mbinguni na vya duniani..utasema mbona biblia inasema “shetani ndiye mungu wa ulimwengu huu”…Ndio! Shetani ni mungu wa ulimwengu huu, kwa ruksa maalumu..Amepewa mamlaka atawale kwa kitambo tu, na mamlaka hayo kapokea kutoka kwa Yesu Kristo, …lakini itafika wakati leseni yake itaisha muda..atafungwa kwa miaka 1000, kupisha utawala wa Amani wa Bwana wetu YESU KRISTO kufanya kazi hapa duniani, na baadaye atafunguliwa kidogo ili kutimiza kusudi fulani na kisha atatupwa katika lile ziwa la moto. Hivyo tunaposema anamaliki sasa ulimwengu haimaanishi anafanya lolote kwa kujiamulia hapana! Anayo mipaka akitaka kufanya jambo lazima apate kibali kutoka juu kama alivyokwenda kufanya kwa Ayubu..

Kwahiyo unaweza ukauona ukuu alionao Bwana wetu Yesu Kristo sasa…kwamba vitu vyote sasa vipo chini ya himaya yake..kakabidhiwa kila kitu, yaaani tunaposema kila kitu maana yake hakuna kilichosalia…hata wanyama wa porini, hata mimea, hata waovu, hata yule mbwa au paka, au bundi au yule fisi unayemwona kule porini, hata kuzimu na malaika wote…vyote kwasasa vipo chini yake (anavimiliki) ana uwezo wa kufanya chochote atakacho juu yao. Nimependa kulizungumza hili kwasababu wapo wachache ambao bado hawajapata Neema ya kulielewa hili kwa undani..yaani mamlaka Yesu Kristo aliyonayo sio ya kimlinganisha na kitu kingine chochote.

Alisema katika Mathayo 28: 18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.

Lakini leo kwa Neema za Bwana..hatutaingia sana huko, bali tutajifunza juu ya MSHAHARA WA DHAMBI.

Siku moja nilikuwa napita mahali Fulani mahali walipokuwa wanauza mahindi karibu na mashine ya kusaga..sasa pembezoni mwa mtaro nikaona baadhi ya punje za mahindi zimeanguka na nyingine zilikuwa zimeshaanza kumea. Nikajiuliza kwa nini zile mbegu zimeota pale na wakati hakuna mtu aliyekusudia kuzipanda pale? Wakati natafakari hilo kitu kikaingia ndani mwangu na nijikuta ninasema…”hakika apandacho mtu ndicho atakachovuna kama watu wanavyosema”…haijalishi hiyo mbegu ilipandwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, kwa kujua au kwa kutokujua lakini mwisho wa siku kile kilichopandwa kitamea tu..

Wengi wetu tunafikiri mkulima ni Yule tu aliyetoka na mbegu zake nyumbani na kwenda kuzipanda shambani..lakini ni zaidi ya hapo, mkulima ni hata Yule aliyeangusha mbegu njiani pasipo yeye kujijua na ikamea…Naye pia anastahili kupata malipo ya kazi yake..Ni majibu ya Mungu kwa kile alichokipanda…hata kama alikuwa hajui..Mungu ameshamjibu! Ndio maana ile mbegu ikamea hata kama alikuwa hajui.

Hali Kadhalika na sisi katika maisha yetu..Yapo mambo mengi tunayapanda ambayo aidha kwa kujua au kwa kutokujua..hiyo haizuii chochote ni lazima yalete majibu. Ukipanda mbegu njema utavuna mema…na ukipanda mbegu mbaya utavuna hizo hizo..

Ukitenda dhambi kwa kutokujua kuwa umetenda dhambi au ukitenda dhambi kwa kujua…zote mbili zinaleta matokeo yanayofanana…na matokeo yenyewe ni mauti…kwasababu biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Ni sawa na mtu aliyepanda mbegu yake shambani na mwingine aliiangusha pasipo kujua mtaroni na kuendelea na shughuli zake…wote wawili mbegu zao zitamea tofauti ni kwamba mmoja atakuwa anaona na kufuatilia hatua za ukuaji, mwingine atakuwa haoni wala hafahamu kuwa alichokipanda kinaendelea kuota huko…lakini utakapofika msimu wa mavuno, mavuno yote yatakomaa kwa wakati mmoja.

Kama wewe ni mwasherati, na unajua kabisa uasherati ni dhambi, au ni mlevi, au mtazamaji pornography, au mwizi, au mlawiti, au mfanyaji masturbation, au msagaji, au mtoaji mimba, au msengenyaji..na unafanya hayo kwa makusudi kabisa..kuwa na uhakika kabisa mbegu hizo Mwisho wa siku mbegu hizo zitakuzalia mauti..

Halikadhalika kama mwingine ni mwizi, au muasherati, au mfanyaji masturbation, au mtukanaji au mlevi, na hana habari kuwa mambo hayo ni mabaya na ni dhambi mbele za Mungu..huyo naye ni sawa na mtu aliyeiangusha mbegu yake kwenye mtaroni kando ya barabara pasipo kujijua..ambapo itamea na wakati ukifika kazi yake itaonekana na watu wote hata kama yeye hajui..Hivyo na yeye pia mbegu zake zitamzalia MAUTI!! Atakufa katika roho na katika mwili.

Mfano leo hii ukienda kubaka mwanafunzi, serikali haitaki kujua kuwa ulikuwa unaifahamu sheria au la, hiyo si kazi yao…Kazi yao ni moja tu kukuhukumu kulingana na sheria inavyosema ,utakwenda gerezani miaka 30.

Biblia inasema katika

Wagalatia 6: 7 “MSIDANGANYIKE, MUNGU HADHIHAKIWI; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.

Unaona? Mungu hadhikiwi biblia inasema hivyo…uwe umepanda kwa bahati mbaya au kwa makusudi, kwa kujua au kwa kutokujua…sheria ni ile ile ni lazima uvune ulichokipanda ni sheria Mungu aliyoiweka katika mambo yote hata mambo ya asili.

Biblia inaposema mshahara wa dhambi ni mauti…haimaanishi adhabu ya dhambi ndio mauti!…hapana bali MSHAHARA! Zingatia hilo neno “mshahara”…adhabu maana yake unapewa mateso kulingana na kile kitu kibaya ulichokifanya…mshahara maana yake ni “unalipwa kulingana na kazi uliyoifanya”….Kwahiyo dhambi ni “kazi”..na ina mshahara haina adhabu bali mshahara…

Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Ufunuo 22:12..

“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Kwahiyo kitakachotokea siku ya hukumu sio watu kwenda kusomewa adhabu, bali kwenda kulipwa MISHAHARA YAO. Kila mtu kama kazi yake ilivyo…waliofanya kazi ya dhambi ndio watalipwa mauti ya milele, kadhalika waliofanya haki watalipwa uzima wa milele.

Kwahiyo ndugu, unayesoma ujumbe huu ambaye bado upo nyuma ya wakati (Yaani Kristo yupo mbali na wewe), na unafanya dhambi za makusudi au pengine sio za makusudi bali kwa kutokujua…Nataka nikuambie maisha nje ya Yesu Kristo, ni sawa na kuangusha mbegu barabarani na kwenda zako pasipo kujua kuwa zinaendelea kujiotea zenyewe huko ulikoziangusha. Na ujira wako upo! Vivyo hivyo dhambi zako ziwe za kwa kujua au kwa kutokuja zitafikishwa HUKUMUNI! Na zitapewa ujira wake.

Ni maombi yangu kuwa Bwana atakujalia kuliona hilo na kuweka mambo yako sawa sasa na kujitengenezea mshahara ulio bora wa uzima wa milele, kumchagua Yesu Kristo kuwa fungu lako lilolo bora, mkuu wa uzima, Biblia inasema mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla haijakaribia miaka utakaposema sina furaha katika hiyo. Hii ikiwa na maana kuwa utafikia miaka fulani hutaweza tena kumkumbuka muumba wako, kama unamsikia sasa na kumkataa.

Bwana akubariki katika Jina la Yesu, naye akupe kila haja ya moyo wako wewe uliyemchagua yeye.

Amina.

Tafadhali shiriki ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA DHAMBI, UOVU NA KOSA KIBIBLIA!


Rudi Nyumbani

Print this post

MWAMUZI WA KWELI:

Shalom mtu wa Mungu, ni siku nyingine tumepewa neema ya kuishi, Hivyo karibu kwa pamoja tushiriki kujifunza maneno ya uzima, ambayo ndio msingi hasaa wa sisi kuwa hapa duniani.

Tukisoma biblia tunaona jinsi Mungu alivyowanyanyua waamuzi wengi tofauti tofauti kwa udhihirisho tofauti tofauti katika vipindi vya awali kabisa baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri,Na Mungu aliwanyanyua kwa lengo lile lile moja la kuwarejesha watoto wake katika njia sahihi, kuwarejesha mahali ambapo walipaswa wawepo.Hivyo kitu alichokifanya Mungu kwa wakati ule ni kumtia “mafuta ya kipekee” mtu mmoja ili aende kushughulika ipasavyo na yule adui yao mtekeaji, na mwisho wa siku wanapata ukombozi wao kuwa yule mtu Mungu aliyemtia mafuta..

Kwa mfano tunaweza kumwona Musa, Mafuta yaliyokuwa juu ya Musa ni ISHARA NA MIUJIZA na yale MAPIGO. Hivyo kwa kupitia huduma hiyo aliweza kukishusha kiburi cha Farao na Misri nzima na hivyo wakaweza kuwaacha wana wa Israeli waende katika nchi yao Mungu aliyokusudia wafike ili wakamtumikie Mungu. Lakini japo ishara zile kubwa zilionekana kwa mkono wa Musa bado watu wale hawakupata ukombozi mkamilifu ambao ungewafanya wawe huru kabisa kabisa mbali na maadui zao wote.

Tunaona pia wakati mwingine Mungu aliwanyanyanyulia mwamuzi mwingine baada ya kutumikishwa na maadui zao kwa muda mrefu kutokana na dhambi zao wenyewe ndipo Mungu akawaletea Gidioni kwa Roho(Mafuta) ya ushujaa ili kuwaamua kwa upanga,(Waamuzi 6)..Ni kweli mwisho wa siku walipata ukombozi, lakini ukombozi ule ulikuwa ni wa kitambo tu, baada ya muda kidogo watu walirejea katika dhambi zao za kumwasi Mungu.

Hali kadhalika tunaona wakati mwingine Mungu alimtia mafuta Samsoni katika upako wa “Nguvu za kibinadamu”…Hivyo kwa nguvu zile za kimwili aliweza kuwashida wafilisti mpaka kuwafanya wawaache huru kabisa wana wa Israeli. Lakini ukombozi ule ulidumu kwa muda tu, haukuweza kutoa ulinzi wa kudumu kwa wana wa Israeli,kwa wakati ujao.Ndivyo ilivyokuwa siku zote waamuzi zaidi ya waamuzi 12 walipita juu ya Israeli.

Hali kadhalika wakati ulipofika walipohitaji kiongozi, Mungu aliwanyanyulia mtu mwenye Hekima atakayeweza kuwaamua katika mambo yote. Na hivyo akatokea Sulemani, wakamfurahia kwa muda lakini alipokengeuka kwa muda nchi ilitetereka kwa kasi sana, na kusababisha watu kurejea katika hali zao za zamani.

Vivyo hivyo tunaona kwa manabii kama Samweli, Eliya, Elisha, Samweli, Yehu, Yohana mbatizaji ambaye Yesu alisema watu waliifurahia nuru yake kwa kitambo tu (Yohana 5:35) na baadaye ikazima..wote hao Mungu aliwatia mafuta kwa namna tofauti tofauti ili kuwaokoa au kuwarejesha wana wa Israeli katika mstari waliopaswa wawe, lakini hakukuwa na hata mmoja aliyefanikiwa kuleta ukombozi mkamilifu wa kudumu kwa watoto wa Mungu, licha ya kuwa walikuwa hodari na mashujaa.

Lakini tunasoma katika biblia wakati ulipofika wa Mungu kumleta KRISTO duniani, hakuja na kauli mbiu ya mapanga au nguvu za misuli kama Samsoni, hapana badala yake alikuja kutumbua JIPU ambalo lilikuwa limekaa kwa muda mrefu kwa SIRI tangu zamani ambalo ndio lilokuwa linawafanya watoto wa Mungu wajione ni wananafuu kwa kipindi kifupi tu pale wanapookolewa na waamuzi lakini kumbe ugonjwa bado upo ndani yao, na ndio maana mwisho wa siku wanaishi kurudia kumuudhi Mungu..

Waamuzi wote waliotangulia walikuwa wanatoa tu dawa za kutuliza maumivu (Pain-killer), lakini YESU alipokuja kuutibu ugonjwa wote,kutoa mpaka mzizi wa mwisho na kisiki, wala hakikusalia chochote si hata kovu la alama.

Na ugonjwa huo si mwingine zaidi ya DHAMBI ambayo chimbuko lake ni SHETANI.

Na ndio maana ukisoma agano la kale utaona Shetani akitajwa mara chache sana, utaona shetani akijidhihirisha mara chache sana, tofauti na ilivyo katika agano jipya…Hivyo BWANA alivyokuja ilikuwa ni kwa lengo la kumweka huru mwana yoyote wa Mungu, tena kuwa huru kweli kweli, na sio nusu nusu kesho utumwa unajirudia… na ndio maana baada yake yeye hakuna mkombozi mwingine yeyote anayehubiriwa, hata hapa hatumuhubiri mtu mwingine zaidi ya YESU yule aliyesulibiwa miaka 2000 iliyopita na aliyeandikwa kwenye biblia takatifu kwamba yeye ndiye anayeweza Kumwokoa mtu na kumfanya kuwa huru kweli kweli, hana mshirika na yeye ndiye mwanzo na mwisho, hakuna mwingine.

Yeye mwenyewe anasema.. Yohana 8:36 “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.

YESU anakomesha dhambi kwa mtu yeyote anayemwamini, kumbuka dhambi ndio chimbuko la kila kitu; dhambi, ndio chimbuko la magonjwa, ndio chimbuko la mateso, ndio chimbuko la tabu, ndio chimbuko la kuteswa na mapepo, ndio chimbuko la kukosa raha, na kukata tamaa ya kuishi ndio chimbuko la masumbufu ya kila namna unayoyofahamu wewe huku duniani, ndio chimbuko la mauaji na vitendo vyote viovu vinavyoendelea huku duniani…n.k.

Dhambi ndio “control tower” ya shetani, ndio dira yake hiyo kukumaliza wewe na mimi..Wana wa Israeli walikuwa wanapata ukombozi wa miili yao kutoka kwa maadui zao, lakini hawakujua kuwa bado hajawekwa huru kweli kweli kwani yao dhambi bado zilikuwa zinawatawala, na shetani ametulia kimya asiwafunulie siri hiyo..na ndio maana baadaye waliendelea kurudi katika mateso yao ya siku zote, lakini mtu anayemwamini YESU KRISTO leo hii, hatarejea tena katika mateso yake ya kwanza.

Kumbuka wale waamuzi walipoondoka habari zao ziliishia pale pale lakini YESU wakati alipokuwa duniani alitujali na kutuombea kwa Baba tulindwe na yule mwovu, halikadhalika na alipopaa juu kwa Baba amesimama mpaka sasa kama kuhani mkuu akituombea kwa Mungu..Hivyo unaweza kuona hapo mtu aliye ndani ya Kristo kweli kweli sio wale mguu mmoja nje mwingine ndani hapana bali yule aliyekusudia kutembea na Kristo anayo faida nyingi kiasi gani!…Shetani anafahamu kabisa mtu wa namna hiyo hawezi kumpata tena milele, kwasababu mwamuzi wake, mkombozi wake anasimama mbele yake daima masaa 24, kumuamua na kumlinda.

Leo hii watu watashangaa inawezekanikaje mtu kuishi bila kuzini, mtu kuishi bila kutazama pornography, kuishi bila pombe, kuishi bila sigara, kuishi bila kuongoa matusi, inawezekanikaje mtu kuishi maisha ya furaha wakati huna pesa, inawezekanikaje unapitia shida zote hizo lakini bado tumaini lako lote lipo kwa Kristo, inawezekanikaje katika kizazi hiki cha Sodoma na Gomora, kutokuvaa suruali kwa mwanamke, na kuweka mawigi na ma-lipstick na marangi usoni, wala kupaka uwanja kama Yezebeli, inawezekanikaje unadumu katika imani bila kutetereka…

Hawajui kuwa nguvu hizo si zake bali ni za yule mwamuzi wake YESU KRISTO aliyemchagua maishani mwake, laiti zingekuwa ni zake asingekuwa vile alivyo leo…..

Maneno ya YESU yana nguvu ndugu, hilo tunalithibitisha kwa maombi yake aliyomwomba Baba akiwa hapa hapa duniani akisema..

Yohana 17: 9 “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, KWA JINA LAKO ULILONIPA UWALINDE HAWA, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyowa ulimwengu.

15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; BALI UWALINDE NA YULE MWOVU.

16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli”.

Unaona hapo?, YESU aliwaombea wale waliomwini kuwa Baba awalinde na yule mwovu,na si watu wote..Sasa kama Kristo amekataa kukuombea mtu mwingine akikuombea ina faida gani?? ni sawa na bure tu!….hivyo mtu yeyote anayemwamini Kristo sasa kwa kumaanisha kabisa kumfuata na kujikana nafsi yake kama mitume na sio kwa maneno tu , hapo hapo bila kupoteza muda Neno hilo linakuwa linaanza kufanya kazi ndani yake, na ndio hapo anajikuta anao uwezo wa kuvishinda vishawishi vyote vya shetani vile ambavyo hapo mwanzo alikuwa hawezi kuvishinda kwasababu nguvu za shetani zinakuwa hazijakaa juu yake kumtawala.

Vile vile, hiyo haiishii hapo tu bali mtu huyo hata akihitaji lolote kutoka kwa Mungu, mwamuzi wake wakati wote yupo kumtetea huko juu mbinguni..Ni faida juu ya faida.

Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; TENA NDIYE ANAYETUOMBEA”.

Sasa kama Mungu hapokei mashtaka yako…mtu mwingine akikushtaki yadhuru nini?

Unaona Faida zote hizo ni kwa mtu yule aliyemwamini Kristo,lakini ikiwa upo nje ya wokovu, au upo vuguvugu leo huku kesho kule, usijidanganye fahamu kuwa hutakaa uishinde dhambi milele, itaendelea kukusumbua na huku shetani akiichochoa zaidi na zaidi, utaendelea tu kutazama pornography, kufanya mustarbation na kuwa mzinzi, na kuvaa mavazi machafu ya kikahaba na kwako mambo hayo yataendelea kuwa magumu kuyaacha hata kama utatamani kuyaacha hutaweza kwasababu Kristo hajakamilika ndani yako..Na mwisho utakufa katika hali hiyo hiyo ya dhambi na kujikuta kuzimu. Kwasababu biblia hiyo hiyo inasema mshahara wa dhambi ni MAUTI!

Ni maombi yangu sote tutamtazama huyu MWAMUZI mkuu, aponyaye roho zetu na miili yetu kuanzia sasa, kwake kuna raha, kwake kuna amani, kwake kuna tumaini, kwake kuna utulivu…

Kwa kumalizia yatafakari maneno yake haya..

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Ubarikiwe sana. Tafadhali “SHARE” na wengine.


Mada Nyinginezo:

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

ADAM NA EVA.

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.

Tunasoma katika Matendo 17 Mtume Paulo, alipofika Athene mji mkuu wa Ukigiriki, mji ambao ulikuwa umejaa wasomi wengi ambao hata sasa historia ya dunia inarekodi sehemu kubwa ya Elimu na Sayansi tuliyonayo leo hii chimbuko lake lilikuwa ni huko Ugiriki, Wanafalsafa maarufu ambao wanafahamika kwa akili zao na hekima zao nyingi walizowahi kuzionyesha duniani mfano Aristotle, Xenophon, Plato,Pythagoras,Socrates,Plotemy, n.k. wote hao Walitokea huko huko Ugiriki, hivyo tangu zamani hawa watu walijulikana kama ni watafiti wakubwa (Great thinkers), na wagunduzi wa vitu vingi, na hivyo hawakuwa watu wa kubabaishwa tu na habari zinazovuma au maneno ya kutungwa yasiyoweza kuthibitishwa uhalisia wake yanayokuja katika jamii zao…

Na ndio hapa tunaona Mtume Paulo anaingia Athene sasa baada ya kuzunguka mataifa mengi na nchi nyingi kuhubiri, nchi hii kwake ilikuwa ni ya tofauti kidogo Kama Biblia inavyotuleza watu hawa wa Athene walikuwa hawana muda wa kufanya mambo mengine yoyote isipokuwa kutoa habari tu na kusikiliza juu ya taarifa mpya zinazowafikia (Soma Matendo 17:21), hii inaonyesha ni jinsi gani walivyokuwa wamejikita katika masuala ya utafiti na usomi ili kujua nini maana ya mambo yote na uhalisia wake zaidi ya kuganda katika mambo yale yale wanayoyaona kila siku..

Hivyo mtume Paulo alipoingia katika mji ule alianza kuupeleleza ili aone ni mambo gani yanayoendelea kule, lakini alipokuwa akizunguka huko na kule alikutana na madhahabu kubwa sana, iliyoandikwa maneno haya KWA MUNGU ASIYEJULIKANA..Hilo likateka sana fikra zake kupelekea kutaka kufahamu ni kwanini waandike vile, ni kwanini watengeneze madhabahu kwa Mungu wasiyemjua,

Kumbuka kama tulivyoona hapo mwanzo Wagiriki hawakuwa kama watu wa mataifa mengine mfano wa warumi au wamedi, hapana hawa ni watu waliokuwa wanafikiria sana, na wadadisi na wachunguzi wa kina wa mambo yote, hivyo kuandika vile sio kwamba walijisikia tu kuandika au walibuni wazo hilo kisha watengeneze madhabahu ya Mungu asiyejulikana kisha waabudu juu yake, hapana badala yake, ni kweli walitazama mambo yote,na kutathimini kwa kina na kwa utaratibu wakagundua kuwa katikati ya vitu vyote vilivyopo duniani na vinavyoabudiwa hakuna hata kimoja kinachoweza kuleta ufasaha wa mambo yao yote, isipokuwa kwa Mungu asiyejulikana asifanya vikao na wanadamu. hii ikiwa na maana japo kulikuwa na miungu mingi ugiriki watu wanayoiabudu wakati ule, lakini hakuna hata mmoja aliyefikia viwango vya kustahili kupokea Ibada zote za kiungu kwa kazi zake zote zinazoonekana ulimwenguni kote..

Walijua kabisa kipo kitu kingine zaidi ya wao wanavyoweza kukifikiri au kikitafsiri kiitwacho Mungu au vinginevyo, kinachoendesha shughuli zote za ulimwenguni, na wanadamu na kitu hicho hawawezi kuwasiliana nacho kwa njia za kawaida kwasababu ni kikuu sana, zaidi ya upeo wa kufikiri wa wanadamu, ni cha elimu ya juu sana, hakijulikani kama kipo mbali na sisi au karibu na sisi, ni kwamba tu hakina ushirika na wanadamu, wala hakielezeki, wala hakifananishwi, njia zake hazieleweki hali kadhalika hazichunguziki na makao yake hayafahamiki, na hivyo wakaona ili kufanya habari zake kuwa fupi basi wakaweka madhabahu yake mahali pa juu sana kuliko madhabahu nyingine zote na kuanza kumwabudu hivyo hivyo tu pasipo maarifa yoyote kumuhusu yeye..Ila walichokuwa wanajua ni kwamba ni kwa Mungu huyo anayeishi na ni mkuu kuliko vitu vyote.

Matendo 17:22 “Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.

23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.

24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;

25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.

28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.

30 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.

31 Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

32 Basi waliposikia habari za ufufuo wa wafu wengine walifanya dhihaka; wengine wakasema, Tutakusikiliza tena katika habari hiyo.

33 Basi hivi Paulo akaondoka akawaacha.

34 Baadhi ya watu wakashikamana naye, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao”.

Kama tunavyosoma tunaona mtume Paulo alifika na kuanza moja kwa moja kuwafunulia kwa utaratibu habari za Mungu huyo ambaye wanamwabudu pasipo wao kumjua, Mungu asiyejulikana. Na hivyo waliposikia habari za jambo hilo jipya masikioni mwao wengi wao walikaa chini na kumsikiliza.

Ndugu, hao watu walikuwa wapo sahihi kabisa kuenenda katika hali hiyo ni kweli kumwelewa ni kazi sana,au tunaweza kusema haiwezekani kabisa kumwelewa yeye au kumjua yeye kama hatutajua njia fasaha ya kumwendea…

Mambo hayo hayo ya Athene yanajirudia hata leo hii, Wanasayansi sio kwamba hawaamini kuwa hakuna nguvu ya kimiujiza (Supreme being) inayouongoza huu ulimwengu hapana wanaamini kabisa isipokuwa wao wanamtambua kwa jina lingine (nature) na hiyo inawafanya wasiamwamini kabisa Mungu tunayemwamini sisi, hawaamini kama huyo (nature) ambaye sisi tunamwita Mungu anaweza akawa dhaifu namna hiyo etu ajishughulishe na wanadamu na kutazama dhambi zao ili awaadhibu, angali yeye tunamfahamu anayo mambo makubwa sana yasiyokuwa na mwisho huko angani na ulimwengui kote yasiyoweza kuelezeka kwa fikra za kibinadamu iweje leo, eti udhaifu wa mtu umuudhi, huyo sio Mungu…Unaona? Ndivyo wanavyowaza na kuamini.

Mwanasayansi mmoja maarufu wa kizazi chetu ajulikanaye kama ALBERT EINSTEIN,ambaye dunia sasa inamwona kama mtu wa karne kwa mapinduzi yake makubwa aliyoyaleta katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia, yeye anasema hivi …..

“Mimi naamini katika Mungu, lakini sio katika Mungu huyu watu wanaomwita wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambaye yeye msingi wake ni kujishughulisha na vitu vidhaifu vya wanadamu, kama dhambi, na kuadhibu watu, huyu hawezi akawa ni Mungu ninayemfahamu: anaendelea kusema: mimi anasema naamini katika Mungu ambaye ni mkuu zaidi ya upeo wa kibinadamu muumba wa UNIVERSE, ambaye akili za kibinadamu hazijitoshelezi kumwelezea tabia zake”.. Yaani kwa ufupi anaamini kwa Mungu asiyeweza kufikiwa.

Unaona? Hali kadhalika jambo kama hilo tunaliona kwa ndugu zetu waislamu, wanasema Mungu tunayemwabudu ni Mungu mkuu sana (Allah), hajazaa, wala hajazaliwa, wala hana mtoto, wala hana USHIRIKA na mwanadamu yeyote wala kiumbe chochote, si mwanaume, wala si mwanamke, na hivyo mtu yeyote anayemwita Mungu baba, au mfalme wake anatenda dhambi kubwa sana ya kumshusha Mungu hadhi ya kumfananisha na Mwanadamu ambayo ni sawa na dhambi ya kukufuru…

Sasa hawa wote sio kwamba wanakosea kuamini hivyo, hapana, walichokiona kuhusu Mungu ni kweli kabisa, na ndivyo Mungu alivyo katika uhalisia wake, lakini kumbuka jambo hilo ndio kama lile lile lililowakuta watu wa Athene wao walitengeneza madhahaba na kumwabudu Mungu ndani yake lakini madhahabahu hiyo ilikuwa na jina la “KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.”

Unaona? Walimwabudu Mungu asiyejulikana, walimwabudu Mungu wasiyemjua, Sasa madhara yanayokuja kujitokeza kwa watu wa namna hiyo ni kwamba maisha yao yote wataishia kutokumwelewa muumba wao kabisa mpaka kufa kwao, pia hawatakaa wanufaike na chochote kutoka kwa muumba wao, Na mwisho wa siku wanaishi akutokumwelewa hata pale Mungu atakapotaka kusema nao hawatamwelewa na hivyo kupotea kabisa katika dira ya Mungu. angalia kwa makini utaona, watu na namna hiyo wanaishia kumwogopa, na kuwa na wasiwasi, na kumwendea kwa hofu zisizokuwa na maana yoyote, kwasababu wametaka kumwona yeye katika uhalisia wa ukuu wake lakini sio katika njia ambayo amewapangia wanadamu wote wamwone yeye.

Ndugu yangu Mungu kumleta Yesu Kristo duniani kulikuwa na manufaa sana, kwangu mimi na kwako wewe, ni kutufanya sisi tumwelewe yeye vizuri katika utimilifu wote, biblia inasema “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”(Wakolosai 2:9), Unaona pale ambapo tulikwama pasipo kumwelewa Mungu sasa tunamwelewa kwa kupitia mwana wake YESU KRISTO.

Na ndicho Paulo alichokifanya mara moja kwa wale watu wa Athene, Aliwahubiria Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye kwa huyo sisi tunahama moja kwa moja kutoka kuwa viumbe tu vya kawaida vya mwenyezi Mungu, na kufanyika kuwa WANA WA MUNGU aliye hai kama yeye alivyokuwa.. Na kwa kumwamini yeye basi tunakuwa na uwezo wa kumwelewa Mungu na mapenzi yake katika maisha yetu kwa urahisi kabisa, tunakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya madhabahu ya Mungu mbinguni na kuzungumza naye bila kutaabika kama wengine walivyo sasa hivi…

Na ndio maana alisema… (Yohana 14.6…”Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.)..Na pia alisema… Aliyeniona mimi amemwona Baba;….Hatuwezi kumjua Mungu kwa njia yoyote ile isipokuwa kwa kupitia mwana wake YESU KRISTO. Huo ni ukweli ndugu wala usihangaike pengine”

Waebrania 1:1”Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wautukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao”.

Tuchulie Mfano ulio hai ni sawa na leo hii unataka kuwasiliana na mimi bila kutegemea hicho kioo kilichopachikwa mbele ya simu yako, ni kweli kabisa Simu sio hicho kioo ambacho unakipangusa,na kuandika namba juu yake, …Simu ni ni kitu kingine cha ndani kilichojawa na Commands tofauti tofauti ili kufanya kifaa hicho kiweze kutumika kwa mawasiliano, sasa ikiwa utaondoa hicho kioo cha juu na ukataka kuwasiliana nami, basi jiandae kukukutana huko nambo ambayo hujayazoea maneno huko kama Galllery, au Contacts, au SMS, usitazamie utayakuta huko wala kidole hakitahitajika huko kufanya mawasiliano yaende.., ni wazi kuwa utakutana na vitu kama chips, cards,modems,processors,circuit board, na vinginevyo ambavyo hata kwa lugha ya Kiswahili havina tafsiri, ambavyo wewe kwa akili yako ya kawaida hutaelewa chochote isipokuwa yule mtaalamu wa hivyo vitu, yeye pekee ndiye anayeweza kupiga simu pasipo kioo kile, kwa vifaa na ujuzi alionao ..

Lakini sasa kwanini kile kioo kimewekwa, ni kwa faida yako wewe usiyejua hayo mambo magumu yaliyopo ndani ya hiyo simu, ili kufanya simu ionekane kuwa na maana kwako ndio hapo ukawekewa hicho kioo kizuri kwa nje chenye mpangilio mzuri wa mafile, kazi yako wewe ni kubofya tu au kupangusa, na moja kwa moja taarifa zako zinapelekwa ndani ya simu, na hivyo simu inafahamu kuwa ulimaanisha nini, na saa hiyo hiyo simu inapigwa kwenye minara kuungwa na mimi mahali nilipo kuwasiliana na wewe, Unaona hapo? jambo ambalo lingepaswa lifanywe na wataalamu wa hali ya juu, kuamrisha hizo code za simu lakini sasa linafanywa na wewe kirahisi tu kupitia kidole chako juu ya kile kioo.

Hivyo hivyo YESU ndiye kioo chetu kwa Mungu, ili tuweze kunufaika na Muumba wetu aliye mkuu sana, asiyechunguzika njia zake, asiyeelezeka kwa namna ya kibinadamu, asiyekuwa na mwanzo, aliye mwanadamu hatuna budi kumtumia yeye kama kirahisi chetu vinginevyo hatutakaa tumjue Mungu kwa kumchunguza.. Kwa kumwamini yeye na maneno yake,na sasa yale mambo yote ambayo tunayaona ni magumu kwetu, kumfikia Mungu wetu basi yanafanyika kuwa marahisi kabisa, embu fikiria kwa kuiamini tu damu ya Yesu unakuwa na nafasi ya moja kwa moja kusimama mbele za Muumba wa mbingu na nchi na kupata rehema ya kujibiwa maombi yako mambo ambayo watu wa agano la kale waliyatafuta kwa kafara nyingi lakini wasiweze kabisa kufikia hatua ya kuondolewa dhambi zao, au kusimama mbele ya madhabahu ya Mungu mbinguni…Unadhani hilo ni jambo dogo au rahisi, ukiwa nje ya Kristo hilo haliwezekani kabisa ndugu na ndio maana utaona hao wengine wanateseka huko nje, ni haki yao,kuwa hivyo japo wanamuheshimu Mungu kwa hofu lakini upendeleo huo hawataweza kuupata mpaka watakapoingia ndani ya KRISTO..

Wanamwamini Mungu lakini sio katika maarifa, wanamfahamu kuwa ni muweza wa yote lakini uweza wake hauna matunda yoyote ndani ya maisha yao, magonjwa yao hayaponywi, hawawezi kufunguliwa katika vifungo vya giza, hawawezi kupata faraha ya kudumu na amani ambayo ni YESU KRISTO tu pekee ndio anayeitoa, hawana uzima wa milele ndani yao, hawawezi kumwomba chochote kwasababu yeye huwa hajishughulishi na mambo ya wanadamu…Hana mshirika, ..Kwasababu hanawa ushirika naye kama wanavyosema…kwao ni Mungu asiyejulikana! Na asiyefanya vikao na wanadamu,..Lakini kwetu tuliomwamini Kristo Yesu, Mungu anafanya vikao na sisi, na anakuwa ni Mungu tunayemfahamu, tunakuwa ni watu wa Milki ya Mungu, ukuhani wa kifalme, uzao mteule haleluya!!

Hivyo ndugu yangu, ikiwa bado upo nje ya Kristo, wakati ndio huu, wewe mkristo-jina, wewe ni mwislamu, wewe ni asiye-na-dini mkabidhi leo maisha yako, utubu dhambi zako kabisa kwa kumaanisha kuziacha, kisha fanya hima ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na uwe ni kwa jina la YESU KRISTO, hapo ndipo utakapopokea uwezo wa kuwa mwana wa Mungu, na kuhesabiwa kuwa mtu wa kimbunguni kwasababu Roho wa Mungu atashuka ndani yako kuanzia huo wakati , kukusaidia wewe kumkaribia Mungu..na kumwelewa Mungu, Kwasababu atayatwaa yaliyo ya Kristo na kukupasha wewe habari.

Wakolosai 1:15 “naye (KRISTO) ni mfano wa Mungu asiyeonekana , mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

Lakini ikiwa utaendelea kubakia nje ya wokovu ufahamu kuwa hutakaa umfikie Mungu, wala kumjua wala maombi yako hayatakaa yamfikie yeye kama mwana, utakufa katika dhambi, utakufa katika kukosa maarifa ya kumjua Mungu hiyo haijalishi unaonyesha heshima nyingi kwake kiasi gani, utafanana na wale watu wa ATHENE wanamwabudu Mungu wasiyemjua.. na mwisho wake utaishia katika lile ziwa la Moto.Wakati ndio huu, fanya bidii uje kwa Kristo. Na Bwana atakusaidia.

Tafadhali “shiriki ” neema hii kwa wengine, ili nao waponywe na Neno la Mungu, na Bwana atakubariki.

Maran Atha. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

MWANA WA MUNGU.


Rudi Nyumbani

Print this post

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

Tujifunze siri mojawapo iliyopelekea habari za Bwana wetu Yesu Kristo kuenea kwa mafanikio makubwa sana ndani ya kipindi kifupi. Tunaweza kudhani kujisifia kwetu mbele za watu, au kuonyesha wema wetu mbele ya macho ya watu wengi kutatusaidia kuongeza umaarufu wetu, Utamwona mtu mfano ametoa msaada kidogo tu, au kamsaidia mtu kwa kitu kidogo,atatangaza kila mahali, na watu wote watajua kuwa yeye ndiye aliyefanya lile jambo.

Lakini embu tuangalie mbinu Yesu aliyoitumia. Nasi tupate kitu hapo kitakachotusaidia katika huduma zetu , na shughuli zetu tuzifanyazo kila siku, na mambo mengine yote.

Marko 1:40 “Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.

41 Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.

42 Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.

43 AKAMKATAZA KWA NGUVU, akamwondoa mara,

44 akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.

45 LAKINI AKATOKA, AKAANZA KUHUBIRI MANENO MENGI, NA KULITANGAZA LILE NENO, HATA YESU ASIWEZE TENA KUINGIA MJINI KWA WAZI; bali alikuwako nje mahali pasipokuwana watu, wakamwendea kutoka kila mahali”.

Unaona, sio kwenye habari hiyo tu peke yake alimzuia yule mtu asimtangaze, lakini kila mahali alipofanya miujiza yake alitumia kanuni hiyo hiyo, sio kana kwamba hakutaka UTUKUFU au habari zake zisienee kila mahali hapana! badala yake alifahamu kuwa “kumbe kumzuia mtu asikutangaze ndio kumruhusu atangaze”..

Marko 7:34 “akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. AKAWAONYA WASIMWAMBIE MTU; LAKINI KADIRI YA ALIVYOZIDI KUWAAGIZA, NDIVYO WALIVYOZIDI KUTANGAZA HABARI; wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme”

Tukitaka sifa zetu zienee katika nyanja yoyote ile maishani iwe ni katika Utumishi, au shughuli zetu, au chochote kile tukifanyacho, tuhakikishe tunatoa kilicho bora kwanza, kisha tukae kimya, tusijikweze, tukatae kutukuzwa tukuzwa na watu, Kwa kufanya hivyo ndio tutasifiwa, yule yule aliyekipokea ndiye atakayekisambaza kwa nguvu kuliko hata wewe unavyodhani..Hiyo ndio ilikuwa kanuni ya Bwana..alisema “ajikwezaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa”…Kwahiyo yeye mwenyewe alijishusha ili akwezwe.

Hali kadhalika mara nyingine Tunamwomba Mungu jambo kubwa, na huku tunatazamia jibu kubwa kutoka kwake. Tunamwomba Mungu atupe labda tuchukue mfano wa Gari, tunamwomba atupe gari, lakini kwa bahati mbaya haliji gari inakuja baiskeli tunaweza tukasema sio Mungu lakini tusipojifunza kanuni za Mungu kibiblia tunaweza tukakosa shabaha ya kupokea majibu yetu.

Embu mtafakari Eliya jinsi alivyofanya alimwomba Mungu mvua kubwa ya kutosha itakayoinyeshea nchi kame ya Israeli iliyokaa zaidi ya miaka 3 bila kupata hata tone moja la maji, lakini alipoomba kwa nguvu nyingi na kwa bidii mara 7 huku akitazamia kuona wingu zito jeusi, likitokea mashariki, lakini badala yake kilizuka kiwingu kidogo kama mkono wa mtoto mchanga. Lakini Kwa imani yeye alipoona vile hakushtuka kusema kuwa Mungu hajanisikia, kiwingu kile sio cha mvua, bali kijiupepo tu kimeuvumisha, badala yake alipokea vile vile katika udogo ule kwa Imani, na kuondoka mahali pale, lakini biblia inasema ghafla wingu zito likatanda juu ya nchi,na mvua kubwa sana ikanyesha.

Usidharau udogo wa majibu utokao Kwa Bwana juu yako, “usiidharau siku ya mambo madogo”…Ulimwomba nyumba kwa muda mrefu lakini umejikuta unapata pikipiki kwa sasa, usiseme Mungu hajakusikia pokea hiyo kwa Imani na kwa shukrani ukijua kuwa Mungu alishakusikia ulichomwomba na ghafla hiyo pikipiki moja itazaa nyumba 5 kwa muda mfupi sana usioutazamia…

Lakini pia usisahau, duniani sisi ni wapitaji tu! Hatujaitiwa kupata majumba, wala magari, wala mashamba…hayo ni ya muda tu! Pindi tukiwapo hapa duniani na yote yanapita…lakini tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya kama maandiko yanavyosema (2 Petro 3:13), mbinguni ndio kwetu, Hivyo Kila siku ni wajibu wetu, kutazama usalama wa roho zetu zaidi ya vitu vyetu tunavyomiliki. Kwasababu Biblia inasema 

“ Uzima wa Mtu haupo katika wingi wa vitu tulivyonavyo Luka 12:15” na tena inasema “itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake Marko 8:36”

Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

Print this post

MADHAIFU:

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe.

Mambo mengi yanayoendelea katika ulimwengu wa mwili ni ufunuo wa mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa roho..Uhusiano wa Baba na mtoto..ni ufunuo wa Uhusiano wa Baba yetu wa mbinguni na sisi watoto wake tuliopo hapa duniani…Kama Baba mzazi asivyoweza kumdharau mwanawe hata kama afanye jambo la kitoto kiasi gani ndivyo Baba yetu wa mbinguni asivyoweza kutudharau sisi watoto wake katika uchanga wetu. Na watoto wa Mungu ni wapi? Watoto wa Mungu ni wale waliomwamini Mwanawe mpendwa Yesu Kristo, hao ndio watoto wa Mungu…

Yohana 1: 11 “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika WATOTO WA MUNGU, NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE”

Kauli hiyo Ikiwa na maana kuwa kama mtu hajampokea bado Yesu Kristo bado hajapewa huo uwezo wa kufanyika kuwa mtoto wa Mungu, Hivyo sio mtoto wa Mungu bali anakuwa kama mtu tu au kiumbe cha Mwenyezi Mungu.

Upo usemi unasema “mtoto hakui kwa mzazi wake”…Na ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni..sisi ni watoto wake na tutabaki kuwa watoto wake tu milele…na Mungu hana wajukuu (wote sisi ni watoto wake).

Wapo watu wanapitia vita vya kiakili sana wanapokwenda kumwomba Mungu, kwasababu wanajiangalia ni jinsi gani wana madhaifu mengi, wanajiona hawajui kupangilia maneno wanaposali, wanakosa mtiririko mzuri wa maneno, Ningependa nikuambie kuwa Baba yetu haangalii wingi wa maneno au mpangilio mzuri wa Maneno tulionao mbele zake, bali anaiangalia nia yetu ya ndani, tamaa yenu au kusudi letu la ndani…kwasababu yeye mwenyewe alishasema anajua haja za mioyo yetu hata kabla ya sisi kwenda kumwomba. (Mathayo 6:8).

Mzazi anao uwezo wa kujua kuwa mwanawe anahitaji chakula na maji…kabla hata huyo mtoto hajajua kuzungumza wala kujua nini maana ya chakula wala maji..kwasababu upeo wake ni mkubwa zaidi ya huyo mtoto, ameishi muda mrefu na hivyo anafahamu mambo yote mtoto anapaswa ayapate hata kama hatazungumza..Ndivyo ilivyo kwa Baba wa mbinguni. Na pia Mungu hana kinyongo wala hatukinai. Madhaifu yetu hayamfanyi Baba yetu wa mbinguni atuchukie..kama tu madhaifu ya vichanga vyetu hayatufanyi tuwachukie…zaidi sana ndio tunawapenda, na kuwatengenezea njia kila siku ya wao kukua ili baadaye waachane na hayo madhahifu, hilo lipo wazi hakuna mzazi katika hali ya kawaida anamchukia mtoto wake mchanga..tena zaidi ya yote ndio anampenda zaidi.

Mathayo 7:11 “Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?”

Lakini tatizo kubwa linakuja ni wengi kutokuelewa tofauti kati ya MADHAIFU na DHAMBI. Mungu hachukizwi na madhaifu yetu lakini anachukizwa na dhambi…Kwasababu madhaifu ni kitu kinachotokana na uchanga au kukosa ufahamu, lakini dhambi ni kitu kingine…Wengi wanabadili dhambi kuwa madhaifu…Labda utasikia mtu ni mwasherati halafu atakwambia ni udhaifu wangu tu!, mtu anatukana halafu anakuambia ni udhaifu wetu wanadamu tumeumbiwa hayo kwahiyo Baba anaelewa, mtu ni mwizi au mlevi halafu anasema huo ni udhaifu wake..Ndugu huo sio udhaifu unaozungumziwa katika maandiko Hizo ni Dhambi na zinamchukiza Mungu, ambazo mshahara wake ni mauti. Hebu wewe mwenyewe tafakari mtoto wako akiwa mwizi au mtukanaji unaweza kwenda mbele za watu na kuwaambia walimwengu kuwa mwanangu anaudhaifu wa utukanaji au uzinzi?..kuna mtu atakuelewa kweli..Ni wazi kuwa watu wote watakuambia umfunze mwanao aache hizo tabia.

LAKINI NINI MAANA YA UDHAIFU?.

Udhaifu ni kitu mtu anakifanya kisivyopaswa, kwa kutokujua..lakini endapo akijua usahihi wa jambo hilo basi anajirekebisha mara…Kwamfano mtu aliyempa Kristo maisha yake kwa mara ya kwanza (Yaani kasikia injili na kuchomwa moyoni na kumwamini kuwa Yesu Kristo ni Kweli) anaweza kuwa na madhaifu mengi…anaweza akawa bado anatabia Fulani za kiulimwengu ambazo anakuwa anazionyesha..tabia za ubishi ubishi, wakati mwingine ugomvi, tabia za kupenda baadhi ya vitu vya kiulimwengu, vijitabia vya kutokujali n.k na hiyo yote ni kwasababu bado hajasikia mahali popote na wala hajasoma maandiko na kuelewa kuwa mambo hayo mtu aliyempa Bwana maisha yake hapaswi kuyafanya…Na inapotokea anausikia ukweli kuwa mambo hayo sio sahihi aliyokuwa anayafanya, haraka sana anakuwa ni mwepesi kugeuka…

Sasa mtu wa namna hiyo Mbele za Baba wa mbinguni alikuwa anaonekana kama ni mtoto tu! Mwenye madhaifu ambayo baadaye atakapokuja kujua ukweli atabadilika. Na hata angekufa katika ile hali ya madhaifu bado angeokoka kwasababu alikuwa anafanya mambo ambayo alikuwa hajui kama ni makosa…Na alikuwa hafanyi vile kwa makusudi…bali ni kwasababu alikuwa hajui! Ni sawa na mtoto wako mchanga anapojisaidia kwenye nguo zake za ndani..huwezi kumpiga au kumwadhibu kwa kosa lile au anapochukua kikombe na kukirusha kule? utamwekea kinyongo?…kwasababu unajua amefanya vile kwa uchanga wake wa akili…endapo angekuwa mtu mzima asingefanya vile. Na Baba wa mbinguni ni zaidi ya hayo, yeye anaangalia kwa jicho la ndani zaidi kuliko hata sisi tunavyoona.

Lakini sasa endapo mtu kashaujua ukweli kuwa uasherati ni dhambi, uzinzi ni dhambi, ulevi ni dhambi, rushwa ni dhambi, wizi ni dhambi, utazamaji pornography na utoaji mimba ni dhambi, ufanyaji masturbation ni dhambi,uvaaji mbovu ni dhambi..halafu bado anaendelea kufanya hivyo kwa makusudi, pengine kaujua kwa kusoma maandiko au kuhubiriwa….huyo mtu mbele za Mungu sio mdhaifu bali ni muasi na atahukumiwa..

Biblia inatuonya sana kuhusu dhambi za makusudi…ni hatari sana hizo…

Waebrania 10:26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;

27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”

Shetani amedanganya wengi kuwa uasherati ni madhaifu yetu sisi wanadamu, kwahiyo mtu anakwenda kufanya uzinzi akiamini moyoni mwake kuwa Bwana anaelewa, …akiamini kuwa huo ni udhaifu Mungu aliomwekea kila mwanadamu ndani yake..usidanganyike ndugu yangu hiyo ni tiketi ya kwenda kuzimu moja kwa moja…shetani anakushawishi kukuambia ufanyaji wa masturbation ni udhaifu, usidanganyike ndugu, huo ni muhuri wa kukupeleka kuzimu..Shetani anakushawishi kuamini kuwa utukanaji, chuki, kutokusamehe na vinyongo ni udhaifu na huku unajua kabisa ndani ya moyo wako mambo hayo ni machukizo mbele za Mungu..usidanganyike ndugu yangu mambo hayo ni njia panda ya Jehanamu ya moto..

Na moja ya dhambi kubwa inayowapeleka watu wengi kuzimu ni UASHERATI na nyingine ni KUTOKUSAMEHE…Uasherati ndio inayoshika namba moja na kutokusamehe inafuata hapo nyuma…Watu wengi wanakimbilia kuomba toba wasamehewe dhambi zao, lakini maandiko yanasema…

Mathayo 6: 14 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, WALA BABA YENU HATAWASAMEHE NINYI MAKOSA YENU,”..

Na unafikiri madhara ya kutokusamehewa na Bwana dhambi zako ni nini??..Ni ZIWA LA MOTO!!!..Kwahiyo ndugu kutokusamehe sio udhaifu bali ni dhambi..Kwaufupi jambo lolote unalolifanya huku unajua kabisa sio sahihi kimaandiko, jambo hilo ni dhambi.

Ni matumaini yangu kuwa utakuwa umeongeza kitu juu ya vile unavyovijua, na Kama hujampa Bwana maisha yako, mlango upo wazi leo, fanya hivyo leo kabla nyakati za hatari hazijafika..

Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?:

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

KITABU CHA UKUMBUSHO


Rudi Nyumbani

Print this post

RABONI!

Shalom mpendwa, karibu tujifunze Maneno ya Uzima.

Kama tukifakari kwa ukaribu matukio yaliyokuwa yanatokea baada ya Bwana wetu Yesu kufufuka, tutaona siri nyingi sana zimejificha ndani yake, kwamfano embu leo tuitazame siku ile ya kwanza kabisa ya Juma (Jumapili alfajiri), ambayo Mariamu Magdalene aliamka mapema sana kuliko hata watu wengine wote na kwenda kaburini kwa Yesu kutazama, Kwanza mpaka hapo hii inatuonyesha ni kwa jinsi gani huyu mama alikuwa anaupendo wa kipekee kwa Bwana zaidi hata ya watu wengine wote , lakini tunasoma alipofika tu makaburini kwa bahati nzuri au mbaya, alikuta tayari Kristo ameshamtangulia kufufuka, alichokiona ni jiwe tu la kabuni likiwa limeviringishwa pembeni na hakuna mtu ndani yake, wala chochote maeneo hayo, hivyo kwa hofu kubwa na kwa kuogopa akarudi haraka kwenda kuwaita mitume waje kulithibitisha hilo, ndipo tunaona Petro na mwanafunzi mmoja wakaondoka kwa kasi nyumbani pale, kuelekea makaburini,na walipofika kule ni kweli hawakuona mtu wala kitu chochote isipokuwa vitambaa vya sanda tu vimezongwa zongwa pembeni, hiyo iliwasikitisha sana lakini wakawa hawana namna isipokuwa kurudi tu nyumbani kuendelea kuomboleza…

Yohana 20:6 “Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala,

7 na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake.

8 Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini.

9 Kwa maana HAWAJALIFAHAMU BADO ANDIKO, YA KWAMBA IMEMPASA KUFUFUKA.”

Japo mitume ndio waliokwenda kuitwa lakini hawakuweza kudumu kwa muda mrefu pale makaburini kuangalia mwisho wake utakuwa vipi, badala yake wao moja kwa moja walirudi nyumbani, Lakini Mariamu aliendelea kubaki pale makaburini akijiuliza kwa uchungu moyoni mwake ni nini kinachoendelea mahali hapa na ni nani aliyeyafanya haya yote! Kwanini haya yote yampate Bwana?..Lakini wakati alivyokuwa anazidi kulia pale pembezoni mwa kaburi la Bwana, alirusha macho yake kwa mbali na ndani ya kaburi aliona malaika wawili wameketi mmoja kichwani na mwingine miguuni pa Yesu alipokuwa amelazwa, mahali pale pale wakina Petro walipokuwa wanapaangalia kwa makini wakizipapasa zile Leso,..Kumbe hakawajua mahali pale pale walikuwa wameketi malaika wa Bwana wakiwatazama tayari wakisubiria tu muda wa kusema nao, Lakini kwa kukosa kwao kuwa na subira waliondoka kwa huzuni, na ndio sasa tunamwona Mariamu akiwaona, na kuwauliza…

Yohana 20:12 “Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.

13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka”.

Hiyo habari hapo inatufundisha nini?..Tusiwe wepesi kuondoka uweponi mwa Bwana, Pale ambapo tunaona hakuna tegemeo kwa Mungu, tumaini lote la mwisho limepotea, kumbe hapo hapo ndipo Mungu kaketi ili kutuhudumia..Tusiwe wepesi kuondoka uweponi mwa Bwana.

Lakini tukirudi kwa Mariamu hilo peke yake halikutosha kumpa yeye majibu ya maswali yake, japo aliwaona malaika wa Bwana yeye alizidi kuendelea kulia tu, na muda kidogo mahali alipokuwa amekaa akasikia kama mtu anatembea maeneo ya karibu na pale alipokuwepo wala Mariamu hakuwa na muda wa kumtazama wala kumsemesha kwani alidhani atakuwa ni MTUNZA BUSTANI tu, hivyo Yule mtu akamfuata na kumwambia maneno haya:

Yohana 20:15 “Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, RABONI! (Yaani, MWALIMU WANGU).

17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo”.

Unaona hapo dakika za mwisho kabisa Mariamu anakuja kumwona na kumtambua Bwana Yesu, Lakini swali la kujiuliza hapo, ambalo hasaa ndio kiini cha somo letu la leo ni kwanini Bwana alimwambia “USINISHIKE; KWA MAANA SIJAPAA KWENDA KWA BABA”?

Sasa kama ukichunguza hapo, utaona Mariamu alipomwona Bwana, huyu mwandishi wa kitabu hichi cha Yohana Mtakatifu, hakunukuu maneno yale Mariamu aliyozungumza kwa kumuita Yesu Bwana au mwana wa Mungu au jina lingine lolote, wala hakutumia neno la moja kwa moja la mwalimu, badala yake aliandika kwa lugha ya kiebrania RABONI, ikiwa na maana MWALIMU WANGU..Sasa Uandishi huo haukuandikwa ili kutufundisha sisi maneno ya kiebrania, hapana kuna sababu kubwa kwanini hakuwenda moja kwa moja kuandika “mwalimu wangu” bali alianza na neno RABONI!, Hiyo ilikuwa ni kuweka msisitizo wa uzito wa kauli hiyo aliyoitoa Mariamu kwa BWANA…

Na ndio maana baada ya Maneno hayo kutoka kinywani mwa Mariamu tunaona Bwana akamwambia sasa USINISHIKE; KWA MAANA SIJAPAA KWENDA KWA BABA”?…Sasa hilo ni Neno usinishike, haimaanishi kuwa usinishike mwili wangu hapana bali Bwana alimaanisha kuwa.

“kwa kauli yako hiyo, ya kunifahamu mimi kama Raboni/mwalimu wako, usinijue mimi hivyo kwasasa, mpaka nitakapopaa kwenda kwa Baba…”

Na sio kwamba alimaanisha usinishike mwili wangu, kama wengi wanavyodhani,..Ikumbukwe kuwa kulikuwa na wakati mwingine walikuja kukutana naye yeye pamoja na Mariamu yule wa pili, na wote wakamshika miguu na kumsujudia (Mathayo 28:9). Sasa kama ingekuwa ni kumshika mwili asingeruhusu kitendo hicho kifanyike tena mahali hapo.

Hivyo Bwana alikuwa anamaana gani kusema vile?. Kumbe Japo walimwona YESU kama ni MWALIMU wao, lakini kiukweli walikuwa bado hawajamwelewa, na ndivyo Yesu alivyowaona….Lakini watakuja kumwelewa vizuri atakapopaa kwenda kwa Baba yake…Kwasababu kama wangekuwa wamemwelewa tangu zamani wasingekuwa wanapoteza muda kwenda kulia makaburini, badala yake saa ile ile wangepaswa wafurahie ushindi ambao wameupata kwa kufufuka kwake, kama alivyotabiriwa lakini wao kinyume chake walikuwa wanawaza habari za kuibiwa kwa mwili wake..Ni wazi kuwa walikuwa bado hawajamwelewa kama Mwalimu wao.

LAKINI NI KWANINI BWANA APAE KWANZA?

Jibu lipo wazi ndio hili kama tunavyosoma katika..

 Yohana 16:7 “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo MSAIDIZI hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.

8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.

9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;”

Umeona hapo? Kupaa kwa Bwana ni kwa ajili yetu sisi tupate msaidizi, ambaye kama tungemkosa huyo basi tungebaki katika mafumbo mengi ya kutomwelewa Kristo kama RABONI wetu, hata kama tungejifanya kumwita mwalimu kiasi gani,kama hatuna Roho mtakatifu haiwezekana kumwelewa Kristo. hata kama Kristo atatembea na sisi na kulala na kula na kunywa na sisi kila siku kama alivyofanya kwa mitume, kama tutakosa Roho Mtakatifu hatutakaa kamwe tumwelewe yeye..Huo ndio ukweli!

Na ndio maana Bwana Yesu aliweka wazi kabisa katika..

Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.”

Na ndivyo tunavyokuja kuona kwenye maandiko mara baada ya Kristo kuondoka Roho alipoachiliwa kwa wale wote waliotaka kumpokea siku ya Pentekoste, kuanzia huo wakati na kuendelea, tunaona jinsi mitume walivyomwelewa Kristo kwa namna ya kipekee hata zaidi ya ule wakati walipokuwa naye duniani..Tunaona jinsi gani walivyokuja kumwelewa sana KRISTO kama RABONI!, MWALIMU WAO MKUU, kwa Yule Roho tu Mtakatifu aliyeachiwa ndani yao……Unaona umuhimu wa kuwa na ROHO MTAKATIFU ndugu?

Vivyo hivyo na hata leo, haijalishi unampenda Bwana Yesu kiasi gani, haijalishi wewe ni mfuasi wa Yesu kiasi gani, haijalishi utajiita ni mwanafunzi wa Yesu kiasi gani, haijalishi utaona maono kiasi gani, haijalishi Yesu atakutokea mara ngapi, na kula na wewe na kutembea na wewe..KAMA hauna ROHO MTAKATIFU, basi fahamu kuwa bado upo mbali sana na KRISTO, kama vile Mashariki ilivyo mbali na Magharibi.

Kumbuka pia Roho Mtakatifu sio kunena kwa Lugha, ni zaidi ya hivyo vitu..Unaweza ukanena kwa Lugha na bado Roho wa Mungu akawa mbali na wewe vile vile…Uthibitisho wa kuwa na Roho Mtakatifu ni Matunda ya Roho katika tunavyoyasoma katika biblia Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”..yaani kwa ufupi “UTAKATIFU”….Kunena kwa lugha, maono, miujiza,uponyaji hivyo vyote ni vipawa vya Roho na sio matunda ya Roho…Na vipawa hivi havifanani kwa watu wote, kila mtu kapewa cha kwake, kwa jinsi roho alivyomjalia…Kwahiyo mtu anaweza akajazwa Roho na asinene kwa lugha bali akaonyesha karama nyingine labda uponyaji, imani au unabii, Neno la Maarifa n.k…

Kwahiyo uthibitisho pekee wa kujitambua kama unaye Roho Mtakatifu au la! ni UTAKATIFU ulionao..ambao ni upole, uvumilivu, huruma, fadhili,furaha, mwenye kiasi, mwaminifu n.k…Na sio kunena kwa lugha…Vipawa vya Roho ni uthibitisho namba mbili…lakini uthibitisho namba moja ni Utakatifu.

Biblia inasema..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Hivyo na wewe ndugu, hata sasa Roho wa Mungu anataka kuja juu yako maana ahadi hii ni ya kwako pia, na anataka akufanye uwe mwanafunzi wa YESU KRISTO kweli kweli ili afanyike kuwa RABONI! Kwako Katika maarifa yote..Unachopaswa kufanya ni kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha hapo ulipo, Unakusudia kuacha ulevi kama ulikuwa mlevi, unakusudia kuacha uasherati kama ulikuwa mwasherati, unakusudia kuacha usengenyaji kama ulikuwa msengenyaji, unakusudia kuacha utazamaji wa picha chafu mitandaoni kama ulikuwa unafanya hivyo n.k kisha hatua inayofuata ni kwenda kutafuta mahali wabatizwapo ubatizo sahihi wa kimaandiko, yaani ule wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe ni kwa JINA LA YESU KRISTO na si vinginevyo, Kumbuka hayo ni maagizo Bwana aliyoyatoa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu, na ikiwa hayo yote umemaanisha kuyafanya kwa kumaanisha kabisa kuanza kuishi maisha mapya matakatifu ya kumwishia Mungu, basi fahamu kuwa kuanzia huo wakati na kuendelea Roho wa Mungu atakuja juu yako kukufanya kuwa mwanafunzi wa KRISTO. Na kukupa uwezo wa kumwelewa mwana wa Mungu kwa mapana yake yote na marefu yake,..

Mafundisho hayo sio wote wanapewa isipokuwa wale tu waliopokea Roho wa Mungu.

Hivyo ni maombi yangu kuwa utachukua uamuzi huo leo. Na Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?


Rudi Nyumbani

Print this post