Huu ni mwendelezo wa Mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.
Mwanamke aliyepoteza shilingi moja.
Luka 15:8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? 9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
Bwana Yesu alipenda kutumia mifano halisi ya kimaisha kutufundisha habari za rohoni. Kwamfano katika habari hiyo tunafahamu mfano huo ulikuwa analenga mambo ya ufalme wa mbinguni, jinsi Mungu anavyomthamini mtu wake mmoja aliyepotea katika dhambi, pindi atubupo na kurejea. Kwamba tendo hilo linamfanya yeye pamoja na malaika zake mbinguni kufurahi sana.
Lakini leo nataka tujifunze kuhusu mfano huo katika uhalisia wake wa kimaisha kama ulivyoandikwa. Kuna maswali lazima ujiulize kwanini amtaje mwanamke na sio mwanaume. Kisha aipoteze shilingi yake pale NYUMBANI kwake, na sio sehemu nyingine, labda barabarani au sokoni? Tofauti na mfano uliotangulia ambao unamzungumzia Yule mtu aliyepotelewa na kondoo mmoja akawaacha wale 99 akaenda kumtafuta Yule mmoja huko maporini.
Na hatua ambazo alitumia kuitafuta shilingi ile hadi kuipata, kuna funzo gani pia?.
Kumbuka kimaandiko aliyekabidhiwa nyumba aisimamie ni mwanamke, ndio maana biblia inasema,
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Na hazina yake inapatikana humo, lakini pia ikipotea, basi hupotelea humo humo.
Tukisema nyumba hatumaanishi, gorofa, na sebule na jiko. Hapana, bali tunamaanisha wale waliomo mule. Hao ndio hazina yake hasaa.
Sasa katika mfano huo mwanamke huyu alikuwa na shilingi 10, labda tuseme hao ni watoto 10, au ndugu 10, lakini mmoja akapotea, huwenda akawa mtundu, au mwizi, au kibaka, au shoga, au jambazi n.k. Lakini Mwanamke huyu hakukata tamaa na kukaa chini na kusema, Ahh! Ninao hawa 9, wenye kujitambua na wenye nidhani. Embu ngoja niachane na Yule pasua kichwa mtukutu, mwenye kiburi, asinipe presha, nifarijiwe na hawa wanangu 9 wazuri. Hapana, bali alilazimika kufanya jambo ili kuhakikisha amempata na Yule.
Hivyo kama tunavyosoma, hakukaa tu hivi hivi, na kuzungumza. Bali alichukua hatua fulani, na hatua zenyewe ndio hizi tatu.
Hii ikiwa na maana gani? mpaka anafikia hatua ya kuwasha tamaa, maana yake ni kuwa chumba hicho kilikuwa na giza, hivyo asingeweza kuipata shilingi yake katika mazingira yale. Tafsiri yake ni nini? Alimkaribisha Kristo. Ambaye ndio Nuru ya ulimwengu katika nyumba yake.
Hivyo hatua ya kwanza katika kutatua tatizo lake, alimtambua Kristo kwenye nyumba yake. Na sasa Nuru ilipomulika ndipo akatambua kuwa nyumba ilikuwa chafu. Kama asingewasha taa, kamwe asingeweza kugundua kuwa Vitu havipo katika mpangalio wake. Hivyo ikampasa aanze kwanza kuifagia nyumba ile, aipangilie vizuri. Makombo yaliyodondoka sakafuni ayafagie, vikombe na vijiko vilivyokaa hoe hae, aviweke mahali pake, nguo ambazo hazijakunjwa aziweke kabatini, uwazi uwepo. Hakukimbilia kuitafuta shilingi yake katika hatua hiyo. alijua hawezi kuipata katika mazingira yale, machafu, imejificha sana.
Hivyo ikamchukua muda Fulani mrefu kuisafisha nyumba yake, mpaka hatimaye, pengine baada ya saa 6, ikawa safi. Kila kitu kikawa katika mpangilio wake.
Ndipo sasa akaenda katika hatua ya mwisho ya “kuitafuta kwa bidii ile shilingi”. Akaanza kupita eneo moja baada ya lingine, hakutoka nje ya nyumba kwenda kuitafuta barabarani, hapana bali pale pale ndani kwasababu alijua fedha zake hazijawahi kutoka nje ya nyumba.
Na hatimaye akaipata. Na mwisho wa siku akawaalika na marafiki zake, wakafurahi pamoja. Kwasababu ilimgharimu kuipata tena.
Hii ni kufunua nini?
Wanawake wengi wanapoona aidha ndugu zao nyumbani, au watoto wao, au ndoa zao zimeharibika,. Wengine wanakimbilia kwa waganga ili wasaidike, hapo umepotea, wengine wanakimbilia kwa washauri wa kijamii, bado hujapata suluhisho. Suluhisho pekee ni Nuru ya ulimwengu. Yesu Kristo, aimulikie kwanza nyumba yako.
Na Yesu anachokifanya ni kukuonyesha madhaifu uliyokuwa nayo, uchafu uliomo nyumbani mwako, ili urekebishe (ndio ufagie). Sasa wengine wanapofikia hatua hii, wanapoona wanahubiriwa waishi maisha ya utakatifu, wawe watu wa ibada majumbani mwao, wawe waombaji, wafungaji, wafukuze tabia zisiojenga majumbani mwao, waweke mipaka Fulani kwenye familia zao. Wanaona kama wanatwikwa mzigo juu ya mzigo. Wanamkimbia Kristo, wanabakia kulia tu, na kuhuzunika..
Wanachofikiria tu, ni utatuzi wa tatizo, mume aache pombe (aokoke), watoto wawe wasikivu, nyuma iwe na amani, n.k. lakini hawataki wao wenyewe kurekebisha baadhi ya mambo makwao. Hapo ndugu ukikwepa hatua hii, sahau kukipata unachokitafuta. Hata upewe bahari nzima ya mafuta ya upako, na pipa la chumvi. Unapoteza muda, hutatui jambo lolote.
Kristo anataka usafi kwanza, ndipo akupe jicho la kuiona shilingi yako iliyopotea. Sasa ikiwa utatimiza mambo hayo mawili yaani KRISTO ndani yako, na usafi wako. Kinachofuata ni kutafuta ulichokipoteza.
Hii ndio hatua sasa ya kumuhubiria, kumshauri, kumwonya, kumvuta kwa Bwana. Sasa ukiendelea hivyo hivyo, muda si mwingi utampata kiwepesi sana haijalishi alikuwa amepotea kiasi gani, au alikuwa sugu namna gani. Hakuna linaloweza kujificha mbele ya Nuru. Tatizo lolote sugu unalolijua wewe la kifamilia, kwa kufuata kanuni hizo litatatulika tu.
Hivyo wewe kama mwanamke, itambue huduma hii iliyopewa na Bwana, laiti kama wanawake wote, wangekuwa ni wa kujiwajibisha kwa namna hii, jamii zetu na familia zetu zisingekuwa na migogoro mingi,wala injili isingekuwa ngumu sana kuihubiri kwasababu tayari walishatangulia walioweka misingi bora nyuma. Hii ni huduma kubwa sana kwa mwanamke na Bwana anaithamini sana.
Simama katika nafasi yako wewe kama mama, wewe kama Dada, nyumba au familia itasimama, endapo wewe utasimama.
Bwana akubariki
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mafundisho mengine:
MAFUNDISHO KWA WANAWAKE
MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
BADO TUTAHITAJI TU KUSAIDIANA.
Je Mungu anaketi katika giza? (1Wafalme 8:12)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
Rudi nyumbani
Print this post
(Masomo maalumu kwa watumishi).
Jina la Mwokozi YESU KRISTO Lihimidiwe daima.
Je unajua namna yakujipima kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu na Kristo yu pamoja nawe?
Je unadhani ni ishara na miujiza ndio utambulisho pekee ya kwamba Kristo yu pamoja nawe?
Nataka nikuambie La!..Ishara na miujiza si uthibitisho wa kwanza wa Kristo kuwa pamoja nawe, kwasababu biblia inasema Yohana Mbatizaji hakufanya ishara hata moja lakini bado alikuwa mkuu kuliko manabii wote waliotangulia.
Yohana 10:41 “Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli”.
Na pia wapo watakaofanya ishara lakini atawakana kuwa hawajui…
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Umeona kumbe kufanya ishara au kutofanya si tija!..Si uthibitisho wa kwanza kuwa Kristo yu nawe!.
Sasa ni kipi kinachotupa uthibitsho kuwa tunatembea na YESU katika utumishi tunaoufanya?.
Jibu tutalipata katika maandiko yafuatayo..
Yohana 12:26 “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu”.
Hapo Bwana anasema mtu akitaka kumtumikia, yani kuwa mtumishi wake BASI AMFUATE!!… Na yeye alipo ndipo na mtumishi wake alipo, au kwa lugha nyepesi “Yeye yupo pamoja na wale waliomfuata”.
Sasa tunamfuata vipi YESU?.
Tusome tena maandiko yafuatayo..
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote AKITAKA KUNIFUATA, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote AKITAKA KUNIFUATA, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.
24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.
Kumbe ili tuwe watumishi wa kweli wa Mungu, ambao Kristo atakuwa nasi muda wote ni lazima TUJIKANE NAFSI KILA SIKU??.
Sasa swali ni je tumejikana nafsi zetu? au tunazipenda nafsi zetu na kuzishibisha kwa kila tunachokitaka.
Huwezi kumtumikia Mungu na huku hutaki kuacha mila, huwezi kumtumikia Mungu na huku unaupenda ulimwengu.Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na huku hutaki kuacha mizaha, na wala dhambi.
Huwezi kumtumikia Mungu na bado unaishi na mke/mume asiye wako. Fahamu kuwa Kristo hayupo na wewe hata kama unaona ishara na miujiza katika maisha yako..hiyo ni kulingana na maneno ya Kristo mwenyewe.
Kanuni ya kutembea na Kristo, itabaki kuwa ile ile MILELE! Nayo ni KUJIKANA NAFSI, KUBEBA MSALABA NA KUMFUATA YEYE!. Kwasababu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).
Na hiyo ni kwa faida yetu na si yake! (Ayubu 35:7).
Huenda umeshamwamini Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako!.. Hiyo ni nzuri sana, lakini bado haitoshi, ni lazima uongezee hapo “KUJIKANA NAFSI!”. Na baada ya kufanya hivyo pia ujiandae kwa dhiki kwaajili yake.
Jiandae kuchekwa, kudharaulika, kuonekana mshamba, mjinga na usiyejielewa. Usiogope maana hizo ndizo chapa zake Yesu, (Wagalatia 6:17), na wewe sio wa kwanza, zilianza kwa Kristo BWANA WETU NA AKAZISHINDA.
Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”
Bwana akubariki.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.
Yapo makazi ambayo si rafiki sana kwaajili ya uponyaji wa maisha yako!.
Kuna mahali/vijiji/mitaa ambayo ukikaa ni ngumu kupokea chochote kutoka kwa Mungu, isipokuwa Mungu mwenyewe amekuambia uishi hapo!. Lakini kama hakuna msukumo wowote wa KiMungu kuishi hapo, basi kuwa makini na mahali utakapopachagua!, kama ni mtaa, mji au kijiji.
Utauliza kwa namna gani?
Utakumbuka yule kipofu aliyepelekwa kwa Bwana ili aponywe!, biblia inasema “Bwana Yesu alimtoa nje ya kijiji kabla ya kumponya” na hata baada ya kumponya alimzuia asirudi kile kijiji alichokuwepo!.
Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. 23 Akamshika mkono yule kipofu, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? 24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. 25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. 26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, HATA KIJIJINI USIINGIE”
Marko 8:22 “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.
23 Akamshika mkono yule kipofu, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.
25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.
26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, HATA KIJIJINI USIINGIE”
Umeona?..sababu ya Bwana kumtoa huyu kipofu nje ya kijiji si kwasababu ya ghasia ya watu!, hapana bali ni kutokana na hali ya kiroho ya mahali pale, maana yake mazingira ya kile kijiji yalikuwa ni magumu kwa yule mtu kupokea uponyaji! (Maana yake ukinzani uliokuwepo pale ulikuwa ni mkubwa sana), Ndio maana Bwana akamtoa kwanza nje ya kijiji kabla ya kumponya!
Hali kama hiyo inaendelea hata leo!, ipo mitaa ambayo ina vita vikali vya kiroho kuliko mingine, vipo vijiji vilivyo vizito kuliko vingine, na sisi kama wana wa Mungu ni lazima tuongozwe na roho mahali pa kwenda na mahali pa kuishi.
Aina ya vijiji/mitaa ifuatayo kuwa makini nayo!
1. Yenye watu wengi wasio na hofu ya Mungu.
Ukiona mtaa/kijiji hakuna hofu ya Mungu, maana yake watu wa mahali hapo ni watu wasiojali, na hata kuidharau injili, na kuipinga kazi ya Mungu, kuwa makini na huo mtaa au hicho kijiji. Kwasababu mitaa inayoikataa Injili mara nyingi inakuwa chini ya vifungo vya laana (Mathayo 10:14-15), na mwisho wake huwa inaharibiwa na Mungu aidha kwa mapigo ya magonjwa au majanga au hali za kiuchumi!.
2. Yenye kiwango kikubwa cha ushirikina na uasherati.
Uchawi na uasherati ni ibada kuu mbili za shetani. Mahali palipojaa kiwango kikubwa cha uasherati na ushirikina fahamu kuwa hiyo ni kambi ya adui asilimia zote. Kuwa makini na mahali hapo!. Kama Roho wa Bwana amekuongoza uishi, basi ishi hapo na utafanikiwa, maana ni mapenzi yake!..lakini kama sio, basi usiishi hapo, ili ubaki salama na familia yako!, (mara nyingi adui anatumia mitaa/vijiji kuharibu watoto au ndoa), hivyo kuwa makini!
Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake”
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.
Aina za dhambi
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Ikiwa wewe umeokoka, na una kiu kweli ya kumkaribia Mungu wako katika viwango vya juu. Basi fahamu huna budi ujikuze kiroho. Na ukuaji huo hutegemea mambo mawili makuu “Neno pamoja na maombi”. Katika tovuti hii yapo mafundisho mbalimbali yatakayokusaidia kupiga hatua hizo.
Makala hii imeegemea zaidi katika Maombi. Hivyo huu ni mwongozo wa Wiki kwa Wiki, mfululizo wa vipengele muhimu vya kuombea. Uwapo nyumbani, uwapo kanisani. Jiwekee ratiba Kisha kuwa mwombaji. Na hakika baada ya wakati fulani utaona matokeo makubwa sana ndani yako.
Mwendelezo utakuja…
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Orodha ya mafundisho yote.
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Makwazo ni mambo yanayozuia mwendelezo wa jambo Fulani lililokuwa limekwisha anza, au linalotaka kuanza. Kwamfano ulikuwa unasafiri lakini ghafla kwenye safari yako unakutana na mto mpana, unaokufanya ushindwe kuvuka, hicho kinaitwa kikwazo. Au ulikuwa unapika chakula chako, halafu ghafla gesi ikaishia katikati na chakula bado hakijaiva, hicho kinatiwa kikwazo.
Na rohoni pia vivyo hivyo yapo makwazo ambayo yanamzuia mtu asimalize mwendo wake wa imani, au asiendelee mbele tena katika kumtafuta Mungu. Na muhimu sana kuyajua na kujiepusha nayo.
Kibiblia makwazo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu.
Tukianzana na hilo kundi la kwanza, wapendwa tunaowazungumzia hapa ni wale ambao hawajasimama vema katika kweli. Ndio hawa ambayo Bwana Yesu anawazungumzia katika vifungu hivi;
Luka 17:1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. 3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. 4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Kwa namna gani hawa wanaweza kumkosesha ndugu. Kwamfano ni pale, Mpendwa mwezako anaposikia umemsengenya, Sasa Kama ni mdhaifu kiimani Hili linaweza kuwa ni kwazo kubwa sana kwake ambalo likamfanya hata nguvu yake ya kuendelea kudumu katika kusanyiko ikapoa. Zipo shuhuda nyingi sana za wapendwa ambao wamerudi nyuma kiwokovu kwasababu ya maisha haya. Hivyo kama mwanaminio hakikisha, kinywa chako, unakichunga. Jifunze kuwa na kiasi na uvumilivu. Jifunze kujiepusha na mambo mabaya Kwa wapendwa wenzio.
Kwazo hili linaweza pia kuwa katika ufahamu wa kiroho .
Utakumbuka Ayubu, alipopitia majaribu yake mazito, hakuna mahali popote alinena maneno yasiyo faa, lakini wale marafiki zake watatu, yaani Sofari, Elifazi na Bildadi, (ambao wanawawakilisha watumishi wa Mungu), walipofika, walitumia ujuzi wao wa kibinadamu kumuhukumu Ayubu, kwamba ni kwasababu alitenda dhambi, hiyo ikampelekea Ayubu kunena hata maneno yasiyofaa.
Kama mtumishi wa Mungu, epuka hukumu ya macho,ukiletewa tatizo la mtu/ watu, usiangalie kwa jicho la nje, mwingine ni Mungu mwenyewe anampitisha katika madarasa yake, ukajikuta badala ya kutatua tatizo ndio unaongeza tatizo juu yake. Usianze kuhukumu matukio, bali kuwa katika Roho, tegemea zaidi uongozo wa Roho Mtakatifu. Hekima itakusaidia.
Pia lipo katika ujuzi.
Ukisoma Warumi 14, maandiko yanaeleza kwa upana jinsi ujuzi wetu unaweza kuwa kwazo kwa wengine wadhaifu was imani, kwamfano wewe ukipewa chakula ambacho umesikia kimepitishwa kwenye matambiko, ukashukuru, ukakila, ukijua kabisa chakula hakiwezi kukuondoa kwenye mpango wa Mungu. Lakini kwa ujuzi huo mwingine mwenye imani haba akakuona, na yeye akaanza kula vyakula vya kimatambiko na mila, akajikuta anashirikiana na uganga na mizimu, utakuwa umemsababishia kwazo kubwa kwa Mungu.
Lolote tunalolifanya, lazima tuangalie wengine wanaiga nini kwetu sisi wenye ujuzi. Uvaaji wako, wewe kama mkristo, unaweza ukajiona hauna shida kwako, lakini wengine wakaona ni sawa, hata kuvaa mavazi hayo ambayo hayana utukufu mbele za Mungu, utakuwa umefanyika kwazo kwao
Wapagani wanaweza kuzuia injili, isihubiriwe mahali, wakawapiga au wakawafunga watu wa Mungu n.k. Utaona Herode alimpinga Yohana akamweka gerezani hakuweza tena kuhubiri injili, wapagani waliwapinga watakatifu wengi. Hata mitume katika ziara zao walikutana na vikwazo vingi kutoka kwa watu wa mataifa, mahali pengine hawakuweza kuhubiri kwa utulivu (1Wakorintho 15:32, 1Wathesalonike 2:2).
Watu ambao hawajakamilika katika imani. Kwamfano ni mpendwa lakini mzinzi, sasa wale watu wa nje, ambao walikuwa wanakaribia kuvutwa katika imani, wanapoona matendo ya watu kama hawa, wanasema kama ukristo wenyewe ndio huu ni heri niendelee kuwa mpagani. Hayo ni makwazo. Au unakuta mwingine ni tapeli, mwingine ni mtukanaji, mambo kama haya hufanyika kwazo kubwa sana kwa wapagani kuihubiri injili.
2Wakorintho 6:3 Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; 4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;
Hitimisho:
Hivyo wewe kama ni mkristo jitahidi sana kuyaepuka makwazo kwa waaminio wenzako au kwa wapagani. Lakini pia kama ulikwazwa na ndugu yako, basi, suluhisho sio kuvunjika moyo au kuuacha wokovu, bali ni kunyanyuka tena na kuendelea mbele. Biblia inasema;
Mithali 24:16 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
Amka tena, mtumikie Bwana, kwasababu alishatujuza tangu mwanzo kwamba hayana budi kuja, hivyo hilo liwe ni jambo la kawaida kwako, jitie nguvu uendelee mbele.
Mpagani ni nani?
USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.
Kutoka 21:10 ina maana gani?
Biblia inasema tusiwe kwazo kwa yeyote, je! inawezekanikaje kwa dunia hii ya sasa?(2Wakorintho 6:3).
MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.
Jibu: Tusome,
1 Wafalme 9:12 “Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala haikumpendeza. 13 Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita NCHI YA KABULI, hata leo”.
1 Wafalme 9:12 “Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala haikumpendeza.
13 Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita NCHI YA KABULI, hata leo”.
Nchi hiyo iliitwa “Nchi ya Kabuli” na sio “Nchi ya Kaburi”.Kuna tofauti ya “Kabuli” na “Kaburi”.
Maana ya “kaburi” ni shimo la kuzikia mtu aliyekufa, lakini “Kabuli” maana yake ni “isiyofaa kitu”. Kwahiyo hapo inaposema Nchi ya Kabuli, maana yake ni nchi isiyofaa kitu.
Sasa kwanini nchi hiyo iliitwa hivyo na huyu Hiramu?. Na ni funzo gani tunapata?.
Kipindi Sulemani anaijenga nyumba ya Mungu pamoja na nyumba yake mwenyewe, aliingia makubaliano na Mfalme wa Tiro kwamba Mfalme wa Tiro atampa Sulemani Malighafi za ujenzi (Miti ya Mierezi na mawe pamoja na malighafi nyingine baadhi, 1Wafalme 5:17-18), kwa makubaliano ya kwamba Mfalme Sulemani atampa Hirimu, mfalme wa Tiro ardhi kama malipo.
Sasa baada ya Sulemani kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo mbili, ambapo alitumia miaka 20 (1Wafalme 9:10), aliazimu kumlipa Hirimu malipo yake.
Hivyo Sulemani akaamua kumpa Mfalme wa Tiro miji 20, (maana yake kila mji mmoja kwa mwaka mmoja aliotumikiwa). Zaidi ya hayo Sulemani alimpa Hiramu mwaka kwa mwaka kori nyingi za mafuta na ngano.
1Wafalme 5:10 “Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka. 11 Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka”.
1Wafalme 5:10 “Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka.
11 Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka”.
Lakini tunasoma Hiramu, Mfalme wa Tiro hakupendezwa na miji hiyo 20 iliyokuwa kaskazini mwa Israeli (Galilaya, mpakani na Tiro), na biblia haijataja sababu za yeye kutopendezwa na miji hiyo, huenda pengine aliona si mizuri na yeye alitegemea kupewa miji mingine mizuri yenye kupendeza, ambayo huenda ipo katikati ya Israeli.
Na kwasababu hakupendezwa nayo, aliipokea tu hivyo hivyo, na kuiita “miji isiyo na faida” yaani “Kabuli”
Lakini yote katika yote biblia haijaelezea kwa kina sababu ya Sulemani kufanya vile, au sababu ya Hiramu, Mfalme wa Tiro kutopendezwa nayo na hata kuiita nchi ya Kabuli (Maana yake isiyofaa kitu).
Ni nini tujajifunza kupitia habari hiyo na miji hiyo?.
Tunachoweza kujifunza ni kuwa tunapotenda wema “tusitegemee malipo kutoka kwa wanadamu, bali kutoka kwa Mungu”. Malipo ya wanadamu siku zote yana mapungufu mengi.
Mfalme huyu wa Tiro, alikuwa ni mtu mwema sana kuliko wafalme wote waliowahi kutokea Tiro, na zaidi sana alikuwa ni rafiki yake Mfalme Daudi, baba yake Sulemani, na hata alivyosikia kuwa Sulemani anataka kumjengea Mungu nyumba alifurahi sana na kumtukuza Mungu wa Israeli, (1Wafalme 5:7) hivyo akamtia nguvu Sulemani kwa sehemu kubwa sana, lakini pamoja na hayo alitazamia kupewa thawabu nyingi (malipo mengi) kutoka kwa Sulemani, kwasababu alijua Sulemani alikuwa Tajiri sana, Zaidi ya wafalme wote duniani, lakini kinyume chake akapewa vichache tofauti na alivyotegemea, hivyo moyo wake ukauma!, lakini Laiti kama angetegemea vichache ni wazi kuwa asingeumia kwa vile alivyopewa badala yake angeshukuru na thawabu yake ingezidi kuwa kubwa mbele za Mungu.
Hivyo na sisi hatupaswi kutegemea malipo kutoka kwa watu, pale tunapotenda wema bali tunapaswa tuwe na nia ya kiasi, ili wakati wa Bwana ukifika tupate thawabu kulingana na kile tulichokitenda.
Bwana atubariki.
Maran atha.
Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
Je! Sulemani alienda mbinguni?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 14 (Yoeli, na Obadia).
Neno hilo utalisoma katika andiko hili;
Yohana 19:13 Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha
Maana ya Gabatha ni “eneo lililoinuka”. Ni sehemu iliyojengwa mbele ya jumba la kifalme la Pilato ambapo hukumu zake alizitolea hapo. Kama biblia inavyosema paliitwa sakafu ya mawe. Maana yake palikuwa ni eneo la sakafu iliyojengwa kwa mawe. (Tazama picha juu).
Hapo ndipo hukumu ya Bwana wetu Yesu Kristo ilipotolewa ya yeye kusulibiwa.
Lakini jambo ambalo unapaswa utafakari kuhusiana na tukio hilo, ni kuwa Mungu, ambaye ndiye muhukumu wa wanadamu wote, anasimama mbele ya kiti cha hukumu cha wanadamu kuhukumiwa. Mungu kukubali kuhukumiwa Ni ishara ya unyenyekevu usiokuwa wa kawaida. Na hapo tunathibitisha kuwa hukumu za wanadamu hazitendi haki. Lakini utafika wakati na yeye mhukumu mkuu ataketi katika kiti chake cha enzi kuwahukumu wanadamu wote. Ambapo kwa haki kila mtu atalipwa sawasawa na matendo yake.
Jiulize wakati huo utakuwa upande upi?. Kwake hakuna upendeleo wa kibinadamu kama alivyofanya Pilato kwa wayahudi, kwake hakuna rushwa, kwake hakuna siri, yote yatamulikwa na kuwekwa wazi, na kama jina lako halipo katika kitabu cha uzima, utatupwa katika lile ziwa la moto, ambapo utateketea huko usiku na mchana.
Ufunuo 20:11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Je! Umejiandaaje kukutana na mhukumu wa haki? Kumbuka huwezi kuokoka, ikiwa bado upo nje ya Kristo Yesu. Unachopaswa kufanya ni kutubu leo, ili upate ondoleo la dhambi zako. Ndipo kuanzia huo wakati na kuendelea uwe na amani na Mungu wako,. Hakuna ukombozi kwa yoyote Yule zaidi ya Yesu Kristo.Huwezi kuokoka kwa nguvu zako mwenyewe. Yesu alikufa tayari kwa dhambi zako, ili aziondoe, akuhesabie sio mkosaji.
Ikiwa upo tayari leo kumkabidhi Bwana maisha yako ayaokoe na kuyaongoza, Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.
Wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?
Chetezo ni nini katika biblia? (Walawi 10:1)
“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?
Kila mwanadamu, kuna aina Fulani ya mizigo anayo. Mizigo tunayoizungumzia hapa sio mizigo ile ya dhambi n.k. Hapana, bali ile ya kimajukumu. Kama vile utafutaji wa rizki, kodi, ada, elimu, ujenzi n.k. Hii ni mizigo ambayo inatufanya tusiwe katika hali Fulani ya utulivu.
Wakati mwingine haiepukiki, ni lazima tukumbane nayo. Lakini kosa linafanyika ni pale tunapotaka kuibeba mizigo hiyo yote ndani ya siku moja. Au tuyatatue matatizo yote kwa kipindi kifupi.
Ukiwa mtu wa namna hiyo hata ukiwa tajiri wa namna gani, Bado utaona maisha ni magumu, tena yenye shida na taabu isiyokuwa ya kawaida, na wengine wanaishia hadi kujinyonga kwa namna hii. Kwasababu gani? Kwasababu Mungu hajatuumbia tuibebe mizigo kwa namna hiyo? Leo tutaona ni kwa namna gani tunaweza kuibeba mizigo yote.
Kwamfano unapofikiria, changamoto za chakula cha mwaka mzima uzimalize leo, hivyo unafikiria ni wapi utapata pesa ya kununua mapipa 5 ya mahindi, wakati huo huo unafikiria ada za watoto za miaka 5 mbele itakuwaje, hivyo unahangaika uzipate nazo leo, tena wakati huo huo unafikiria uende katika mafunzo ya kujiongezea aina 7 za elimu, ambazo ungepaswa uzisomee kwa miaka 10, unataka uzimalize ndani ya miezi 3. Tena uanze kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanja vya watoto wako watano, ambapo ndio kwanza wananyonya, na wengine wapo tumboni.
Yaani kwa ufupi ufanye mambo yote chap-chap ndani ya kipindi hiki hiki kifupi. Ukweli ni kwamba kamwe hutakuwa na raha katika maisha yako. Utaona maisha ni mazito sana, hayabebeki, hata kama utakuwa unapata vingi kiasi gani. Kumbuka, Kusema hivi haimaanishi tusifikirie kuwekeza, hapana, lakini fikiria hivyo tayari kipo mkononi, lakini kama hakipo, usijijengee akili hiyo.
Hivyo Mungu ametusaidia kwa kutupa njia ya kuibeba mizigo hiyo yote. Nayo si nyingine zaidi ya ile ya “kuimega siku kwa siku”.
Luka 11:3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
Bwana ameivunja vunja mizigo yetu katika siku. Ametaka kukupa rizki ya siku, kesho usiwe na presha nayo sana, Bwana ataifungulia milango yake, amekupa ada ya muhula mmoja, shukuru, ile ya muhula wa pili ikifika atakupa, usiwe na wasiwasi wa ada ya miaka 3 mbele, utapata ugonjwa wa moyo. Acha hata kufikiria kodi ya miaka 2 mbele, ikiwa umejaliwa ya mwezi mmoja, shukuru. Hujui mwaka ujao utahama hapo, au Bwana atakufungulia milango ya Baraka zaidi ukanunua pako.
Jukumu lolote ulilonalo, embu livunje vunje kwenye vipindi vifupi, Kwasababu hujaumbiwa uibebe mizigo yote kwa wakati mmoja. Ukiitabikia sana “kesho yako” leo, ujue unajijengea mazingira ya stress.
Ni kwa faida yako mwenyewe., Lakini ukiwa mtu wa kushughulika na siku yako utashangaa tu mbeleni umeweza litatua hilo tatizo kubwa kirahisi, kwa njia mbalimbali Mungu atakazokufungulia, kwasababu ni hekima ya Mungu imetumika hapo si ya mwanadamu.
Mathayo 6:31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wasikisaze chakula?
JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?
Fahamu Namna ya Kuomba.
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
Watu wenye kuvunja maagano ndio watu wa namna gani? (Warumi 1:31)
Mungu mara nyingi huwa anatumia lugha ya picha au maumbo, ili kutupa sisi uelewa mzuri kuhusiana na mambo ya rohoni. Kama tunavyojua inapotokea mtawala, labda raisi amekualika uketi pamoja naye meza moja ule chakula, ni wazi kuwa kwa tendo hilo litakuwa limekupandisha hadhi sana.
Sasa zamani, za wafalme ilikuwa mtu aliyepewa heshima kubwa aliwekewa kiti chake kidogo pembeni mwa mfalme upande wake wa kuume. Na hiyo ilikuwa inamaana kubwa zaidi ya heshima peke yake, bali pia ilimaanisha kupewa mamlaka.
Hivyo katika biblia unapokutana na “mkono wa kuume” Mungu ametumia picha hiyo kumaanisha aidha mambo haya makuu matatu;
1. HESHIMA.
Maandiko kutuambia Kristo, ameketi mkono wa kuume wa Mungu, ni kutuonyesha, hadhi na ukuu alionao sasa. Mbinguni wapo malaika wengi wenye nguvu, wapo wenye uhai wanne, wapo maserafi na mamilioni ya malaika, lakini hakuna hata mmoja alipewa hadhi ya kuwa karibu/sawa na Mungu zaidi ya Kristo, Bwana wetu.
Waebrania 1:13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Kwahiyo, aliyepokea heshima, ya juu zaidi ya viumbe vyote ni Kristo Yesu Bwana wetu. Na ndio maana tunamwabudu na kumtukuza. Na heshima zote na shukrani zinamwelekea yeye tu peke yake. Ndiye Mfalme wa Wafalme, na Bwana wa Mabwana. Hafananishwi na mwanadamu yoyote duniani, au malaika yoyote mbinguni.
2. MAMLAKA.
Lakini pia mkono wa kuume sio tu heshima bali pia huwakilisha mamlaka, Kuketi kwake kule, ni kuonyesha mamlaka ya kumiliki na kutenda jambo lolote na kutiisha vitu vyote chini yake anayo.
Waefeso 1:20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote
> Vilevile anayo mamlaka ya kutuombea na kutuondolea dhambi, kama kuhani mkuu,
Warumi 8:34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
>Mamlaka ya kutumwagia vipawa vya rohoni na nguvu ya kushuhudia habari njema.
Matendo 2:33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia,
Luka 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo
3. ULINZI.
Uwapo karibu na mfalme, maana yake upo salama, chini ya mfumo wa ulinzi wake. Hivyo Mungu kumweka Kristo kuumeni mwake ni kutuonyesha sisi,ufalme wa Kristo hauhasiki. Na wanaompinga kazi yao ni bure. Na Mungu atawaweka maadui zake chini ya miguu yake.
Zaburi 110:1 Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Lakini jambo ambalo watu wengi hawajua ni kwamba Bwana anataka na sisi tumweke yeye mkono wetu wa kuume, maana yake tumpe heshima yake, katika mambo yetu, na yeye, atatuheshimisha, atatuinua, na atatulinda.
Matendo 2:25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.
Usiweke Mali kuumeni kwako, usiweke elimu, au mwanadamu kuumeni kwako. Bali Kristo tu peke yake.
Unaweza pia kupitia vifungu hivi Kwa maarifa zaidi; Mathayo 22:44 , Matendo 7:55, Wakolosai 3:1, Waebrania 1:3,13, 10:12, 1Petro 3:22.
Je! Kristo yupo kuumeni kwako? Fahamu tu ili Kristo awe pembeni yako, na wewe pembeni yake wakati wote, ni sharti uwe umeokoka. Na wokovu unakuja kwanza kwa kutubu (, yaani kukubali kuacha njia mbaya), na hapo hapo unaupokea msamaha wa dhambi, kisha Kristo anaingia moyoni mwako. Na baada ya hapo unaitimiza haki yote kwa kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu, na Roho atakuwa tayari ameshakuja ndani yako kuanzia huo wakati na kuendelea. Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo akusamehe dhambi zako, basi fungua hapa kwa mwongozo mfupi wa sala ya toba>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ubarikiwe.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume, maana yake nini?
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Je! waliokufa kabla ya Bwana Yesu wataokolewaje?
NI KWASABABU YA YESU KRISTO.
SWALI: Siku ya kwanza Mungu aliumba Nuru, Je ilitokea wapi wakati Tunafahamu jua ambalo ndio lenye kutoa Nuru liliumbwa siku ya Nne?(Mwanzo 1:14-19)
Mwanzo 1:3-5
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. [4]Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. [5]Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
JIBU: Mungu si kama sisi wanadamu ambao tukitaka kuunda jambo ni lazima tuwe na chanzo Fulani husika. Kwamfano hatuwezi kumleta mtu duniani Kwa kumchukua mwanamke na kumfungia ndani tu peke yake bila mwanaume tukitarajia baadaye ajifungue .
Lakini Mungu ni tofauti anaweza kumpa uzao pasipo kumkutanisha na mwanaume. Tunaona alifanya Kwa Mariamu. Lakini ameamua kuunda njia rasmi ya sisi kuzaliana, ambayo ndio hiyo ya watu wawili kukutana.
Vivyo hivyo na pale mwanzo Mungu kutanguliza Nuru, SI jambo la kushangaza kwake. Yeye ni mweza wa yote, Dunia hii ingeweza kumulika sikuzote Daima pasipo kutegemea jua Wala mwezi Wala nyote.
Lakini aliamua aviundie na chanzo chake, Kwa lengo la kutenganisha majira.
Lakini pia ni vema tukapata ufunuo, wa tukio lile, Nuru Ile ilimwakilisha nani. SI mwingine zaidi ya Yesu. Kumbuka Yesu katika agano la kale alijifunua katika maumbo. Lakini katika agano jipya waziwazi. Hivyo ilihitaji Nuru iwepo ili shughuli zote za uumbaji ziendelee.
Yohana 1:1-5
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.[2]Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. [3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. [4]Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. [5]Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
Je! Kristo Ameangaza ndani Yako? Tambua kuwa pasipo Kristo hakuna maisha, hakuna uhai, Tubu Leo mgeukie Kristo Akusamehe dhambi zako.Ili uumbwe upya na Mungu. Hivyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa fungua hapa Kwa mwongozo wa Sala ya Toba>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
Nini maana ya huu mstari Ayubu 23:10 ‘Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’?
Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?
JE UMEKUFA PAMOJA NA NANI?
JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?
Je ni sawa kuomba novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia?