Neno hili utalisoma katika vifungu kadha wa kadha,
Hivi ni baadhi ya vifungu hivyo ambavyo utakutana nalo;
Mwanzo 37:6 “akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake”.
Walawi 23: 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Tafsiri ya Neno mganda, ni matita ya mazao yoyote yaliyovunwa ambayo yamefungwa pamoja. Kwamfano ngano zilipovunwa, katika mashamba, zilifungwa kwanza katika matita matita, baadaye zikakusanywa zote pamoja, ndipo zikaenda kukobolewa na kusagwa. Sasa hayo matita matita ndio huitwa miganda. (Tazama picha juu)
Kwamfano katika vifungu vifuatavyo utaelewa biblia ilimaanisha nini;
Kumbukumbu 24: 19 Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.
Maana yake ni kuwa ikitokea, umeenda shambani kuvuna, ukafanikiwa kukusanya miganda kumi, sasa wakati unaondoka ukasahau mmoja, Ilikatazwa kurudi nyuma na kuuchukua, bali uuache kwa ajili ya mayatima na wageni. Kwasababu maskini waliruhusiwa kuingia kwenye mashamba kuokota vile vinavyosalia.
Hii inatufundisha nini?
Wakati mwingine Mungu ataruhusu usichukue kila kitu ulichonacho / ulichokikusanya, ikawa umesahau fahamu kuwa ni Mungu ametaka, ili wengine wafaidike, usipende kukomba kila kitu, wakati mwingine utajiepusha na Baraka zako. Ukisafiri usiondoke na kabati lote la nguo, ulikuwa unakwenda mahali Fulani umebeba vingi, na kwa bahati mbaya ukakisahau kimoja, usiwe mwepesi kukirudia kukichukua, hujui ni kwanini Mungu amekusahaulisha.
Wewe ni boss, umeona, vichenji vimebaki, si lazima uvikombe vyote, waachie waajiriwa wako. Itakuwa ni Baraka kwako.
Lakini pia ni kutuelekeza mioyo yetu imtegemee yeye zaidi ya miganda yetu. Utakumbuka mitume wa Kristo, walipofanyiwa miujiza ya mikate, wakaagizwa wakusanye vipande, kisipotee hata kimoja, lakini baadaye walipoondoka, wakakumbuka wamesahau,wakaanza kulalamikiana wao kwa wao watakula nini. Lakini Yesu akawaambia mmesahau miujiza Mungu aliyowafanyia kama hiyo? Mna wasiwasi gani? Mungu anaweza kuwapa na vingine.
Mathayo 16:5 Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate. 6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate? 9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota?
Hivyo na sisi pia tusiwe na tabia ya kubeba miganda yote.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).
Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).
YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.
TUYATENDE MAMBO YOTE KWA UZURI NA UTARATIBU.
VIACHENI VYOTE VIKUE HATA WAKATI WA MAVUNO.
Rudi nyumbani
Print this post