SWALI: Nini maana ya Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
JIBU: Mithali hii hulenga hasaa watawala, iwe ni serikalini, kwenye mataasisi, makanisa n.k. endapo waongozao ni waovu, basi hufanya hata watu (hususani wale wema) kujificha, Au kutoonekana kabisa.
Ndio kama ilivyokuwa katika kipindi cha mfalme Ahabu, alipoiharibu nchi yote ya Israeli kwa kuweka miungu migeni, akichochewa na mkewe Yezebeli. Wakati huo Manabii wengi wa Mungu waliuliwa, na wale waliosalia walijificha wasionekane kabisa, wakabakia tu makuhani wa baali na wenye dhambi. Kiasi kwamba Eliya akadhani ni yeye tu peke yake nabii aliyebakia Israeli. Kuonyesha ni jinsi gani wenye haki, walivyokuwa adimu wakati huo. Lakini Mungu alimwambia Eliya, nimejisazia watu elfu saba wasiopigia goti baali.
Warumi 11:3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu. 4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali. 5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
Warumi 11:3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.
4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.
5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
Ni kama leo tu ulimwenguni, tunavyoona kiwango cha watenda maasi na maasi kinavyozidi kuongezeka, ndivyo inavyokuwa ngumu kukutana na watakatifu halisi, na hiyo inaweza pelekea pengine ukajidhani mpo wachache, au hakuna kabisa kama wewe.
Ukiwa katika mazingira kama haya usipumbazike, ukafanana na ulimwengu. Bali fahamu kuwa wapo, isipokuwa Mungu amewaficha tu. Siku watakapoondolewa waovu duniani ndipo utajua kuwa Mungu anao watakatifu wake, wengi.
Ndio maana ya hilo neno Bali “waangamiapo wasio haki, wenye haki huongezeka”.
Binti ambaye unatembea kwa kujisitiri barabarani, na huwenda huoni aliye kama wewe mtaa mzima, usife moyo, ni kwasababu wasio haki ni wengi. Kijana uliyeamua kuishi maisha ya mbali na uzinzi na anasa usijidhani upo peke yako, songa mbele tambua, ni Mungu amewaficha tu watu wake.
Kwasababu ni Neno la kweli kabisa wasio haki wastawipo, wenye haki hujificha, (sio kwamba wamekufa, bali wapo). Wakati utafika waovu wataondolewa, na sisi tutamiliki na kuangaza. Usiwe mfauta wimbi, nyakati hizi ni za hatari. Ni sawa na kichuguu tu, waweza kudhani hakina kumbikumbi ndani, kina huoni chochote kinachotoka humo, lakini wakati wa mvua, unastaajabia wingi wao umetoka wapi. Vivyo hivyo na wewe endelea kutembea kwa ujasiri katika wokovu wako. Unyakuo umekaribia. Tambua Bwana analo jeshi lake.
Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Miungu wasio na kikao pamoja na wenye mwili.
Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani.
Semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; (Luka 17:10)
Rudi Nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya Mithali 27:15 Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
JIBU: Neno Kutona-tona kama lilivyotumika hapo, ni “maji yanayovuja darini”.
Hivyo anaposema Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi. Anamaanisha kitendo cha kuvuja sana kwa dari siku ya mvua nyingi, na kitendo cha kukaa na mwanamke mgomvi ndani ni sawasawa.
Kwa namna gani?
Tunajua ukikaa kwenye nyumba ambayo dari lake halikujengwa vizuri, mvua kubwa inaponyesha maji mengi huchuruzika na kuingia ndani. Wakati umelala utashangaa maji yanakudondekea kitandani mwako, yanachuruzikia kwenye makochi, yanakwenda mpaka kwenye makapeti, jambo ambalo litakufanya usitulie hata kidogo humo ndani utakuwa tu bize, kusogoza vitu ovyo ovyo visilowe, na mbaya ni pale mvua inapokuwa kubwa, na maji kuongezeka ndani, mwisho huwa ni kutoka kabisa nje na kuiacha nyumba.
Ikiwa umeshawahi kupitia changamoto kama hiyo ya kuvujiwa nyumba, unaelewa ni kero kiasi gani.
Ndivyo anavyofananisha kutendo hicho na kuishi na mwanamke mgomvi. Ikilenga hasaa wanandoa. Kumbuka aliyeandika mithali hizi ni Sulemani, alikuwa anatambua anachokisema, kwasababu aliishi na wanawake elfu moja(1000) kama wake zake, na alijua masumbufu yao. Alikutana na changamoto za baadhi yao.
Mwanamke mgomvi, kibiblia ni Yule asimheshimu mumewe, ni Yule anayemwendesha mumewe, anayemkaripia, asiyekuwa msikivu, kila jambo analolifanya mumewe ni kulikosoa tu, mwenye kiburi na mwenye maneno mengi, asiye na staha.
Wanawake wa namna hii, huwataabisha waume zao sana, na hatimaye wengine huwafanya wahame kabisa nyumba, kukaa mbali na familia zao. Ni dari linalovuja utawezaje kukaa kwenye nyumba hiyo?
Andiko hilo limerudiwa pia katika;
Mithali 19:13 Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.
Uonapo familia zenye migogoro ya namna hii ni kuziombea sana Bwana aziponye.
Maandiko hayo yamewekwa sio kuonyesha mabaya kwa jinsia ya kike, hapana, bali imetoa tahadhari ili yasitokee kwa wanawake wa kikristo.
Biblia imetoa mwenendo wa mwanamke halisi wa kikristo, inasema awe ni wa kumtii mume wake. Awe ni mwenye kiasi, na MPOLE, na adabu. Akifanya hivyo atasimama vema kwenye nyumba yake, badala ya kuiharibu kinyume chake ataijenga.
1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
Soma pia.
1Petro 3:1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
1Petro 3:1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
Hivyo wewe kama mwanamke ukitembea katika hayo, utakuwa katika upande salama wa Mungu.
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Wokovu wa milele/ Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?
HUIJUI KAZI YA MUNGU, AFANYAYE MAMBO YOTE.
ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.
Swali: Je kazi ya udalali ni dhambi, na Mkristo anaruhusiwa kuifanya?
Jibu: Dalali ni yule mtu anayeuza kitu kwa niaba ya mwingine na kisha kuchukia asilimia fulani ya faida ya kile kilichouzwa.
Au pia dalali anaweza kuwa mtu mwenye kutafuta soko la bidhaa ya mtu mwingine na kisha kuchukua asilimia ya faida inayopatikana.
Kama hiyo ndio maana au tafsiri ya udalali, basi mtu akiifanya “SI DHAMBI”, Kwani hata ununuaji wa bidhaa kiwandani na uuzaji masokoni kwa namna moja au nyingine ni “Udalali”, kwani utanunua kwa gharama ndogo na kuuza kwa gharama kubwa na kisha kuichukua ile faida….Hapo tayari umeshakuwa dalali wa wenye kuitengeneza ile bidhaa..
Kwahiyo udalali si dhambi ikiwa tu haujahusisha mambo yafuatayo.
1. UONGO.
Labda umepewa kazi ya kutafuta mteja wa bidhaa husika, halafu ukampata na kumwekea kiwango cha juu sana nje na mapatano na yule aliyekupa bidhaa (lengo la kufanya hivyo ni ili wewe upate faida kubwa na ya haraka)…
Au mteja amehitaji bidhaa au nyumba na wewe ukamlaghai kwa uongo na kumpa kitu ambacho kiko chini ya viwango na huku ukijua kabisa kuwa kitu hiko hakistahili hiyo gharama, Huo wote ni Uongo na udalali huo ni haramu.
2.Dhuluma.(Utapeli).
Unapomdhulumu mtu fedha au bidhaa yake, aidha kwa kumlipa kisasi au kwasababu nyigine yoyote udalali huo ni haramu.
3. Haifanyiki ndani ya nyumba ya Mungu..
Udalali unaofanyika ndani ya Nyumba ya MUNGU ni haramu..
Utaona Bwana YESU aliwafukuza wale madalali wote waliokuwa wanabadili fedha ndani ya nyumba ya MUNGU.
Yohana 2:15 “Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;”
Vivyo hivyo kanisani si sehemu ya minada, na udalali, ni sehemu ya Ibada takatifu ya roho na kweli.
Swali lingine je?…Fedha ya udalali inaweza kutolewa sadaka ikiwemo Zaka?.
Jibu ni Ndio!.. kama udalali huo haujahusisha mambo hayo hapo juu, basi inaweza kutolewa sadaka ikiwemo Zaka(yaani fungu la Kumi), na ikakubalika mbele za Mungu.
Na je mkristo anaweza kufanya kazi ya udalali??..
Jibu ni Ndio! Anaweza kufanya, ikiwa hatatumia Uongo, au dhuluma, au rushwa, au kufanya ndani ya kanisa la Mungu.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
KAMA MHUBIRI USIWE MFANO WA DIOTREFE.
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
TUZIJARIBU HIZI ROHO.
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
Jibu: Jibu la swali hili tutalipata katika ule mstari wa 22, sura ya 7 ya kitabu cha Mwanzo…
Mwanzo 7:22 “kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu”.
Hapo yanatajwa mambo mawili,
1. Kila chenye roho ya uhai puani kikafa.
Kufuatia andiko hili, ni wazi kuwa samaki hawapumui kupitia pua kwasababu wao wapo chini ya maji..
2. Pia Kila kilichokuwako katika nchi kavu.
Kupitia maneno haya ni wazi kuwa gharika haikuwahusu viumbe wa majini au baharini, kwasababu hao hawaishi nchi kavu.
Vile vile hatusomi popote kuwa Nuhu aliingiza nyangumi, au kambale ndani ya safina, badala yake tunaona ni wanyama tu peke yao, na tena walimfuata Nuhu mwenyewe na wala Nuhu hakwenda kuwatafuta, sasa kwa mantiki hiyo nyangumi wangemfuataje Nuhu safinani?.
Kwahiyo ni wazi kuwa gharika ile ilihusu viumbe waliooishi nchi kavu, ambao ni wanadamu ndege, wanyama na wadudu.
Mwanzo 7:20 “Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. 21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu”
Mwanzo 7:20 “Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.
21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu”
Sasa kama ni hivyo, basi samaki walihifadhiwa wapi wakati wa gharika?
Jibu ni kwamba samaki waliendelea kubaki majini wakati wa gharika.
Lakini pamoja na hayo biblia inatabiri ujio wa gharika nyingine ambayo si ya maji tena bali ya moto, ambapo viumbe vyote vitafumuliwa na hakuna kitakachosalia..
2 Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. 8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa”.
2 Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa”.
Bwana atusaidie tukae katika mwenendo wa UTAKATIFU na UTAUWA.
Maran atha.
NAYE AKASIMAMA JUU YA MCHANGA WA BAHARI.
NUHU WA SASA.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Makasia ni nini? (Yona 1:13).
Jibu: Ili tuweze kuelewa vizuri, turejee mistari hiyo (kuanzia ule mstari wa 16 -22).
Mathayo 23:16 “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga. 17 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu? 18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga. 19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka? 20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake. 21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake. 22 Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake”.
Mathayo 23:16 “Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga.
17 Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu?
18 Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga.
19 Vipofu ninyi; maana ni ipi iliyo kubwa, ile sadaka, au ile madhabahu iitakasayo sadaka?
20 Basi yeye aapaye kwa madhabahu, huapa kwa hiyo, na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
21 Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo, na kwa yeye akaaye ndani yake.
22 Naye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa yeye aketiye juu yake”.
Shabaha kubwa ya Bwana YESU hapo si kuhalalisha VIAPO, Kwamba ni halali Mtu kuapa kwa Hekalu au kwa maadhahabu!.. La! Hiyo haikuwa shabaha yake kwani tayari alishaonya kuhusu viapo katika Mathayo 5:33-37.
Mathayo 5:33 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34 lakini mimi nawaambia, USIAPE KABISA; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu”.
Mathayo 5:33 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, USIAPE KABISA; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu”.
Na Pia Mtume Yakobo akaliandika jambo hilo hilo katika Yakobo 5:12.
Kwahiyo lengo la Bwana YESU halikuwa kuhalalisha viapo, bali ni kuonyesha UOVU na UNAFIKI wa viongozi hao wa kiyahudi (Mafarisayo na Masadukayo na waandishi) kupitia viapo vyao!. Kwamba wanavipa nguvu viapo vya sadaka Zaidi ya viapo vya Hekalu ambalo ndani yake lina Mungu na sadaka pia…Lakini wenyewe wanatazama sadaka tu!.
Maana yake ni kwamba kama Mtu ameapa kutoa sadaka (dhahabu au kitu kingine chochote) basi amejifunga (maana yake ni lazima atimize kiapo chake hicho, na asipotimiza ni dhambi kubwa)..lakini kama ameapa tu kwa kwa hekalu (labda kuabudu siku hiyo hekaluni, na asiabudu), basi sio kosa kubwa sana!!..
Ila kwa upande wa dhahabu (sadaka), ni kosa kubwa! Pasipo kuona kuwa Hekalu/Madhabahu ni kuu kuliko sadaka! Kwamba aliyeapa kwa Hekalu kaapa jambo kubwa sana kuliko yule aliyeapa kwa sadaka (dhahabu) peke yake itolewayo Hekaluni… kwasababu ndani ya Hekalu ndiko kwenye taratibu zote za matoleo, na si ndani ya matoleo ndio kwenye Hekalu…Ila Mafarisayo walikuwa hawalioni hilo, na ndio maana Bwana YESU anawaita vipofu.
Na kwanini walikuwa wamevipa hadhi kubwa viapo vya sadaka kuliko vya Hekalu??… Hakuna sababu nyingine Zaidi ya kwamba walikuwa wanapenda fedha!!!, walijua ya kwamba wakiwabana watu katika matoleo basi watanufaika Zaidi, hivyo walijali matoleo kuliko Hekalu la Mungu pamoja na madhabahu yake..
Na jambo hilo hilo utaona Bwana YESU alilirudia juu ya “vile vipasavyo kuwasaidia wazazi”..ambapo Mafarisayo walisema endapo mtu akipata chochote na kile anaweza kukifanya chote wakfu (yaani Korbani) na wala asiwape chochote wazazi, na isiwe dhambi!… jambo ambalo ni baya sana! (soma Marko 7:11).. na kwa maelezo marefu juu ya habari hiyo ya Korbani fungua hapa >>>>Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)
Mfano kamili wa baadhi ya viongozi wa kiimani wa leo??…. Utaona wanathamini Matoleo Zaidi ya Hekalu la Mungu na taratibu zake. Utaona mtu akiahidi kuja kanisani na asije, haiwi shida….lakini hebu mtu aahidi kutoa halafu asitoe!, inakuwa ni vita vikali na ni laana kubwa!…pasipo kujua kuwa nyumba ya Mungu ni kuu kuliko sadaka, kwasababu ndani ya nyumba ya Mungu kuna matoleo!.. (Na mtu akiiheshimu nyumba ya Mungu ataheshimu pia matoleo).
Bwana atusaidie sana.
Ipi tofauti kati ya matoleo na sadaka?
WEWE NI HEKALU LA MUNGU.
JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?
UJIO WA BWANA YESU.
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.
SWALI: Naomba kufahamu tafsiri ya Yakobo 1:13-17, hususani pale anaposema “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu”
Yakobo 1:13-17,
[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. [14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. [15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. [16]Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. [17]Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
[16]Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike.
[17]Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
JIBU: Katika hiyo mistari ya juu kabisa, tunasoma mtume Yakobo akitoa ufafanuzi wa mawazo ya watu kuhusu Mungu ambayo sio sahihi. Wakidhani kuwa majaribu yampatayo mtu hutolewa na Mungu, kwasababu chanzo chake ni Mungu.
Chukulia mfano labda mpendwa kabarikiwa na Mungu kwa shamba la mizabibu, likawa linasitawi sana, hata kumfanya afungue kiwanda chake cha juisi na kuuza na kupata faida nyingi..Sasa baada muda fulani watu wakamfuata na kuulizia bidhaa ya mvinyo, mwanzoni alikataa, lakini baadaye alipopiga hesabu na kuona faida itakuja mara nne,.akaingiwa na tamaa akaanza kutengeneza divai akauza na yeye mwenyewe akaanza kuwa mlevi, hatimaye maisha yake ya wokovu yakaporomoka akawa amekufa kabisa kiroho. Mwishowe akaanza kumlaumu Mungu amemletea jaribu la kumpa shamba la mzabibu na kumbariki sana, ndio maana akawa mlevu. Sasa mtu wa jinsi hii Mtume Yakobo anasema asiseme amejaribiwa na Mungu.
Ni sawa na tamaa za mwili,.Mungu aliziweka mahususi kwa ajili ya furaha ya wanandoa lakini imebadilika na kuwa uzinzi, na watu hutumia kisingizio kuwa Mungu ameziweka kama jaribu kwao. kumbe Mungu alichowapa ni chema isipokuwa wao wenyewe wamekigeuza kuwa uovu.
ndo maana sasa ya vifungu vinavyofuata vinasema. “kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu. Kwa lugha rahisi anamaanisha chochote kitolewacho kilicho chema hutoka kwa Mungu, lakini tu sio kilicho chema bali pia chochote kilicho kikamilifu, hutoka juu kwa Baba yetu.
Mungu sikuzote hutupa sisi vitu vizuri. Na si vizuri tu bali pia vilivyo vikamilifu hutoka kwake. tujengwe na tufurahie, isipokuwa sisi huvipindua na kuvitumia kwa tamaa zetu.
Pesa ni kitu kizuri, chakula ni kitu kizuri, usingizi ni kitu kizuri, ndoa ni kitu kizuri, kazi ni kitu kizuri, muziki ni kitu chema.
Lakini watu wanapovitumia kinyume ndio huzaa uzinzi, anasa, ulevi, uvivu, ufisadi.n.k.
Vitu vyote vyema vimetoka kwa Mungu na hajatupa ili kutujaribu..anaendelea kusema..
“hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka”.
Baba wa mianga, akijifananisha na jua ambalo huangaza kotekote, isipokuwa yeye amelizidi jua, hana misimu wala majira ya kuangaza, yeye wakati wote hutoa vilivyo vyema, hifadhili majira yote kwa watu wake.
Hata leo, uonapo Mungu amekupa kitu chema, halafu baadaye kikakuletea matatizo makubwa.. Tafakari hapo kuna mahali ulimpa nafasi shetani kukujaribu. Kwasababu Mungu hawezi kumpa mtu jiwe aliyemwomba mkate.
“kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu.
Ubarikiwe.
YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.
EPUKA KUTOA UDHURU.
SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.
SWALI: Katika Yakobo 1:5 inasema tuombapo Mungu hakemei, maana yake ni nini.
JIBU:
Yakobo 1:5
[5]Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Kabla ya kuona maana hilo neno “wala hakemei naye atapewa”. Tuone kwanza tafsiri ya kifungu chote.
Hapa mtume Yakobo kwa uongozo wa Roho, anandika juu ya suluhisho la kupungukiwa kwa jambo muhimu sana ndani ya mwanadamu. Nalo ni Hekima.
Haandiki ikiwa mtu amepungukiwa na mali, au na umaarifu au na fursa, au watoto…hapana bali na hekima, na aombe dua.
Lakini hekima aisemayo sio hekima ya duniani, bali hekima ya ki- Mungu. Ambayo ni ufahamu wa Ki-Mungu unaoingia moyoni mwa mtu kumsaidia aweze kupambanua vema mambo yote, katika ufasaha wote ili kuleta matokeo aliyoyatarajia.
Hivyo sisi wote tunaihitaji hekima katika yote tuyatendayo. Vinginevyo hatutaweza kuzalisha chochote.
Lakini bado anatoa kanuni ya kuipata, hasemi tukae chini tuwaze, au tukahubiri, au tukatoe sadaka, au tuende kwenye shule za biblia. Hapana anasema na tuombe dua kwa Mungu.
Tunaipata kwa kuomba. Kwa kuchukua muda kupiga magoti na kuomba. Sio kuomba dakika mbili, na kusema Amen au yale maombi ya kumalizia siku unapokwenda kulala. Hapana bali ni maombi yaliyochanganyikana na kiu ya dhati kupata hekima ya Ki-Mungu katika eneo fulani, unalotaka Bwana akusaidie.
Vilevile hatupaswi kuomba bila dira. Kwamfano kusema.. “Mungu naomba unipe hekima”.. Hapana tunaomba tukielekeza eneo ambalo tunataka Bwana atusaidie kupata hiyo hekima ya kupambanua.
Kwamfano hekima katika kuyaelewa maandiko, hekima katika kuhubiri, hekima katika kufundisha, katika kuombea wagonjwa, katika kufanya biashara, katika kuimba. n.k.
Na hapo ndipo Mungu mwenyewe anaongeza ufahamu wake juu ya hicho unachokiomba na hatimaye utaona tu, mabadiliko, au njia ya kitu hicho unachotaka akusaidie.
Sasa tukirudi kwenye swali, pale anaposema
“awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa”
Maana yake, kwasababu Mungu ana ukarimu, basi hachagui wa kumpa, anawapa wote. Hii ahadi yake kuwa kila aombaye humpa. Haleluya.
Na tena anasema “hakemei”. Tofauti na sisi wanadamu
Kwamfano sisi tuwafuatapo wazazi wetu na kuwaomba kitu, wakati mwingine, hutugombeza, au huwa wakali, au kutaka utoe kwanza hesabu ya kile cha nyuma ulikitumiaje, kabla ya kukupa hichi kingine. Na ndio maana ulikuwa na hofu, kujifikiria mara mbili mbili hicho unachotaka kwenda kuomba, ukiulizwa hivi, ujibu vipi. Sio tu kwa wazazi, lakini kwa wanadamu wote, sifa hiyo wanayo tuwafuatapo kuwaomba kitu, si kivyepesi vyepesi kama tunavyodhani.
Lakini kwa Mungu wetu sio, hakemei, haangaali ya nyuma kukushutumu, hakuuliza makosa yako. Anakupa tu, bila sharti lolote.
Ni furaha iliyoje. Mimi na wewe tuliomwamini tunapokwenda kumwomba Mungu hekima, hatushutumiwi kwa lolote, au kwa madhaifu yetu. Bali kinachohitajika tu ni kumwamini yeye asilimia mia, bila kutia shaka katika hilo unaloomba, kwasababu ukitia shaka, maombi hayo hayaendi kwake bali kwa mungu mwingine asiyeweza yote.
ndio maana anataka tumfuatapo tusiwe na shaka ya kutojibiwa, ili maombi yetu yafike kwake kwelikweli, yeye aliyemweza wa yote.
Anasema hivyo katika vifungu vya mbeleni.
Yakobo 1:6-8
[6]Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. [7]Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. [8]Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
[6]Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
[7]Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
[8]Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.
WhatsApp
SWALI: Ayubu alimaanisha nini kusema..Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Aliwezaje kurudi tena tumboni mwa mama yake tena uchi je hilo jambo linawezekana?
JIBU: Kauli hiyo aliisema Ayubu baada ya kupotelewa na familia yake na mali zake. Lakini Kwa ujasiri akamtukuza Mungu katika hali hiyo pia, kwa kusema maneno hayo;
Ayubu 1:21
[21]akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Lakini swali lipo hapo, katika kurudi tumboni mwa mama yake uchi. maana yake ni nini?
Ikumbukwe kuwa sisi hatukutoka tu katika tumbo la wanamke bali pia katika tumbo la ardhi, hiyo ndio mama wa ulimwengu. yaani mama wetu wa kwanza.
soma;
Zaburi 139:15
[15]Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
[15]Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
Mhubiri 12:7
[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Hivyo Ayubu aliposema nami nitarudi tena huko huko hakumaanisha mama yake mzazi, bali mama wa ulimwengu wote yaani ardhi.
Na ndivyo ilivyo kwa kila mmoja wetu, hukuja na kitu, utaondoka bila kitu chochote. Ukiwa uchi vilevile.
lakini jambo lingine la kufahamu kuwa, wale walio ndani ya Kristo, wafikapo kule ng’ambo hawataonekana uchi, bali watapewa vazi jipya la rohoni la Kristo Yesu, ndio ile miili mipya ya utukufu isiyoona uharibifu idumuyo milele.
2 Wakorintho 5:1-3
[1]Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. [2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; [3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
[1]Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
[2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
[3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
Swali ni je! Umeandaliwa vazi lako baada ya kuondoka?
Kumbuka unalipokea kwa kumwamini Yesu Kristo leo, okoka tubu dhambi zako, ubatizwe, kisha upokee kipawa cha Roho Mtakatifu. vazi lako liwe limekamilika., ili siku ile usionekane uchi.
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MFUNGO.
SWALI: Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? Kama tunavyosoma katika 2Samweli 5:6-9. Je! habari hiyo tunaielewaje?
2 Samweli 5:6-9
[6]Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo. [7]Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. [8]Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani. [9]Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.
[6]Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
[7]Lakini Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.
[8]Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani.
[9]Basi Daudi akakaa ndani ya ngome hiyo, akaiita mji wa Daudi. Kisha Daudi akajenga toka Milo na pande za ndani.
Habari hii inazungumzia wakati ule ambao Daudi alikwenda kuiteka Yerusalemu na kuufanya kuwa mji wa Mungu.
Alipofika na kukutana na wenyeji wa mji huo, walimdharau na kumsema kimafumbo kwa kauli ya mzaha kumwambia “Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe;”
Wakiwa na maana vita yake ni ya kupambanishwa na watu dhaifu kabisa wa mji, mfano wa vipofu na viwete, hao ndio apambane nao, lakini sio majemedari wa nchi ile. Akiweza hao walau ndio aingie sasa kujaribu kuuteka, huku wakijua kuwa hata hilo Daudi hataweza kwasababu walimwona ni dhaifu.
Na ukweli wakati huo Daudi hakuwa na nguvu yoyote, kwasababu ndio kwanza ametoka kuupokea ufalme. Hawakujua kuwa nguvu zake tangu zamani zina Mungu, ndio zile zilizomwangusha Goliathi ni silaha zake kwa jiwe moja.
Lakini Daudi aliipowafuatia na kuwapiga, na kuwaangamiza, naye alitumia pia jina hilo hilo la vipofu na viwete kimizaha akiwaita wayebusi waliomwonyeshea dharau..pamoja na hilo Daudi alionyesha kuwachia sana.
Lakini mistari hiyo hakumaanisha kuwa anawachukia viwete na vipofu. Hapana Kama ingekuwa hivyo asingemkaribisha Mefiboshethi mtoto wa Yonathani katika nyumba yake ya kifalme kuketi mezani pake daima..(2Samweli 9). Na ikumbukwe kuwa Daudi alikuwa anamcha Mungu na kuwakumbuka sana wanyonge.
Lakini pale inaposema….
“Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani”.
Ni kwamba kufuatana na Daudi kuwasema viwete na vipofu akiwarejea wayebusi, ukazuka msemo huo, ‘vipofu na viwete hawana ruhusu kuingia nyumbani mwa Mungu;. Lakini haikuwa hivyo’..
Misemo na namna hii ilikuwepo tangu zamani hata kuhusu ile habari ya mfalme Sauli, ya kutabiri (1Samweli 19:24), na kuhusu ike habari za mtume Yohana, pale wale mitume wengine waliposikia Kauli ya Bwana Yesu inayosema ikiwa nataka huyu awepo mpaka nijapo, wakadhani kuwa Yohana hata onja mauti kamwe, mpaka Yesu atakaporudi kumbe hawakumuelewa Bwana Yesu, hakumaanisha vile.(Yohana 21:22-23)
Na ndivyo ilivyodhaniwa kwa Daudi kwamba anawachukia vipofu na viwete, kumbe aliwamaanisha wayebusi.
Lakini ni nini hasaa tunaweza jifunza..katika tukio hilo?
Ni kawaida ya adui yetu anapokaribia kushindwa hunyanyua ujasiri wake kwa kiwango cha juu sana. Mji ambao uligeuzwa kuwa wa Bwana, na mwema kuliko yote, ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kukatisha tamaa. Hata ukuta aliokuwa anaujenga Nehemia, ambao sehemu yake iliendelea kudumu kwa mamia ya miaka mbeleni ulitanguliwa na dhihaka nyingi za kuvunjishwa moyo. wakisema hata mbweha akipita juu yake utaanguka.
Silaha hiyo hiyo anaitumia adui leo, unapoona maono makubwa ya kuitenda kazi ya Bwana ndani yetu, vitisho vya adui huanzia hapo, aah wewe huna upako, wewe huwezi kuhubiri, huna pesa, huna elimu ya kukutosha, huna uzoefu, utafungwa..hizo zote ni dhihaka, Daudi alishazitambua toka kwa Goliathi, ndio maana akawashinda wayebusi.
Hivyo ni kusimama imara kuitetea injili, kwa imani tukijua hakuna linaloshindikana kwake yeye aaminiye. Na palipo na dhihaka nyingi ndipo palipo na mafanikio makubwa.
Wayebusi walikuwa ni watu gani?
Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
Katika agano la kale, Israeli walikuwa na makusanyiko mengi, ambapo walikutanika kumfanyia Mungu ibada, na kuzishika sikukuu. Lakini pia yalichaguliwa makusanyiko mengine yaliyoitwa mikutano/makusanyiko ya makini. Makusanyiko haya yalifanyika katika siku ya saba ya sikukuu ya Pasaka, na siku ya nane, baada ya sikukuu ya vibanda. Katika siku hiyo hawakuruhusiwa kufanya kazi yoyote. Bali ilitengwa kwa ajili ya kujitakasa, au kujisogeza karibu na Mungu,
Hivi ni vifungu baadhi vinavyoielezea siku hiyo;
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; 36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba. Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. 36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Hesabu 29:35 Tena siku ya nane mtakuwa na kusanyiko la makini sana; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi;
36 lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng’ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba.
Walawi 23:34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
36 Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi
Kumbukumbu 16:8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Huo mkutano mtukufu ndio kusanyiko la makini.
Hekalu la kwanza pia lilipomalizika liliwekwa wakfu katika siku hii ya kusanyiko la makini
2Nyakati 7:9 Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku saba, na sikukuu siku saba.
Sehemu nyingine mikusanyiko hii iliitishwa rasmi, kwa lengo la kujimimina kwa Mungu kuomba, kwa ajili ya maovu na majanga ambayo yanaipata nchi. (Yoeli 1:14 – 2:15). Kusanyiko hili liliitwa pia kama kusanyiko kuu.
Je! Ufunuo wake ni upi leo?
Kama vile tulivyo na mikusanyiko ya aina mbalimbali leo, mfano ya shule ya jumapili, ya semina, ya injili n.k. Vivyo hivyo hatuna budi kuwa na makusanyiko ya makini. Ambayo ni mikusanyiko ya mifungo na maombi. Ambapo tunapata muda wa kujimimina kwa undani kabisa uweponi mwa Mungu, kumtaka aingilie kati mambo yetu.
Je! unaithamini? Mungu aliyesema tusiache kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25). Hakumaanisha tu mikusanyiko ya jumapili, lakini pia ya mifungo na maombi.