Swali: Je ni kweli kwamba kiganja cha mkono wa kushoto au wa kulia kikiwasha basi ni ishara ya kupata pesa?
Jibu ni LA!.. hakuna uhusiano wowote kiganja kuwasha na fedha kumjia mtu. Labda kama mtu huyo ana pepo la utambuzi ndani yake..
Kama mtu ana pepo la utambuzi basi anaweza kuhisi kitu Fulani kikimjia, ikiwemo pesa kutoka katika chanzo kisicho cha kiMungu, au akahisi hatari kutoka katika upande wa maadui zake (maana yake upande wa Mungu), na ishara hizo anaweza kuzihisi kwa njia kama hizo za kuwashwa mkono, au kuwashwa sehemu nyingine ya mwili.
Lakini mtu mwenye Roho wa Mungu hisia zake zipo katika Neno la Mungu..Anaposoma Neno la Mungu na kudumu katika uwepo huo basi anaweza kuhisi Baraka zijazo, au hatari ijayo.
Kwamfano Neno hili katika biblia linaweza kukupa hisia za Baraka zijazo…
Mithali 13:11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.
Mtu akilisoma hili Neno la kulishika, tayari atakuwa anajua ni nini kitafuta katika shughuli anayoifanya.. lakini si kukisikilizia kiganja kinasema nini!.. Na maneno mengine yote ya Mungu ni hivyo hivyo..
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Elimu ya kusoma viungo vya mwili na kutabiri mambo yajayo ni elimu ya adui na ya kupotosha..
Lakini pia kumbuka si kila anayewashwa mkono basi ana pepo la utambuzi!.. La!, mkono unaweza kuwasha kwa sababu nyingine yoyote ya kibaolojia, na mtu asiwe na pepo!.. (Hata hivyo asilimia kubwa ya wanaowashwa mikono hawana mapepo). Hivyo kilicho kikubwa na cha msingi ni kudumu katika Neno la Mungu.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
KUOTA UNAPEWA PESA, KUNA MAANISHA NINI?
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
Je! fedha ni jawabu la mambo yote? (Mhubiri 10:19).
MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.
Biblia inaposema Yesu ameketi mkono wa kuume inamaana gani?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Naomba kufahamu nini maana ya Isaya 40:12 inaposema maji kwa konzi ya mkono, na mbingu kwa shubiri?
Isaya 40:12 “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani”?
JIBU: Ukianzia kusoma vifungu vya juu na kuendelea vile vya chini, utaona Mungu anawaambia watu wake Israeli kuwa atawajilia kama mchungaji awachungaye kondoo wake , na kuwalisha, na kuwakuongoza, na kuwakusanya kifuani mwake, hata wale walio wachanga, ndivyo atakavyowatendea watu wake na hilo litawezekana.
Lakini Israeli waliona kama jambo hilo linaweza lisiwe rahisi, Ndio hapo akawaambia sasa katika vifungu vifuatavyo maneno hayo. Kwamba “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake”? Maji anayoyazungumzia hapo ni maji mengi, mfano wa bahari, na maziwa Je! Kuna mtu yeyote anayeweza kuyakusanya maji mengi namna hiyo kwenye viganja vyake? Jibu ni hapana! Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana.
Vilevile anawauliza ni nani awezaye ‘kuzikadiri mbingu kwa shubiri’?. Shubiri ni kipimo cha urefu, wa kiganja, toka kidole gumba mpaka kile cha katikati vinaponyooshwa. Na ni wazi hakuna mtu anayeweza kupima ukubwa wa mbingu, toka sayari moja hadi sayari nyingine, kwa kipimo chochote kile cha kibinadamu. Lakini kwa Mungu hilo ni jambo dogo sana, ni kama kuzipima kwa shubiri.
Halikadhalika anauliza ni nani awezaye kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi?. Pishi ni kopo dogo, je kuna mwanadamu anaweza kuyakusanya mavumbi yote duniani, kama vile akusanyavyo yale machache kwenye kopo lake. Ni wazi hakuna awezaye kuwa na pipa la uwezo huo.
Vilevile anauliza ni nani anayeweza kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?. Je! Kuna mizani yoyote ya kibinadamu inaweza kuiweka milima juu yake, na kutoa vipimo?. Jibu ni hakuna. Lakini kwa Mungu ni jambo dogo sana. Milima ni kama vipunje vidogo sana vya mchanga.
Ikiwa haya yanaonekana magumu kwa mwanadamu, lakini kwa Mungu ni mepesi. Vivyo hivyo jambo la kuwakusanya watu wake, au kuwasaidia, lisitizamwe kibinadamu, kwasababu uweza wa Mungu ni mkuu sana usioweza kufikirika kibinadamu. Maswali ya namna hii ndio kama yale Mungu aliyokuwa anamuuliza Ayubu, (Ayubu 38-41), na katika Mithali 30:4
Yesu kama mchungaji wetu mkuu, anauwezo wa kutukusanya kama kondoo wake. Haijalishi tutaonekana tumetawanyika mbali kiasi gani, lakini akisema jambo ni lazima liwe. Halikadhalika na katika mambo yetu yote ya kiroho na kimwili.
Hivyo kitabu cha Isaya sura ya 40 yote, kinaeleza uweza wa Mungu, usiopomika kibinadamu. Lakini Swali ni Je! Kristo amekusamehe dhambi zako? Kama ni la! Basi nafasi bado unayo leo. Mwamini yeye akuokoe. Na kukupa ondoleo la dhambi zako.
Kwa mwongozo wa namna ya kupokea wokovu basi fungua hapa>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)
Kuna Mbingu ngapi?
Mbinguni ni sehemu gani?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 4: 7
Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?
JIBU: Ukianza kusoma tokea sura ya kwanza utaona Paulo, anakemea sana baadhi ya tabia ya matengano ambayo ilionekana katika kanisa hili la wakorintho. Iliyozuka kutokana na aina ya mafundisho au utendaji kazi wa waasisi wa huduma, au waliowabatiza, na sana sana kati ya Paulo na Apolo.
Hivyo matabaka haya yakawafanya wajivunue wanadamu, na mafundisho yao. Bila kufahamu kuwa kanisa ni la Kristo na si la wanadamu.
Ndipo Paulo, akaweka wazi kuwa kila mmoja aliitwa kwenye utumishi wa Kristo Yesu, ambao una mchango wake katika kanisa, lakini si kwamba huduma ya mmoja ni bora kuliko nyingine. Akasema mmoja anapanda mwingine anatia maji, lakini mkuzaji ni Mungu.
Sasa katika vifungu hivi anaendelea kuwaambia tabia ya kupambanua watumishi, au huduma, si sawa. Ndio hapo anasema “Nawe una nini usichokipokea?”. Akiwa na maana je! Kuna kipawa gani, au kitu gani chema katika kanisa ambacho hawakukipokea kutoka kwa Mungu,?
Lakini anasema..
“Iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?. Yaani kama vyote vilitoka kwa Mungu na sio kwa wanadamu, mbona basi mnajisifia kana kwamba vimekuja kwa uweza wa kibinadamu?.
Kama tumepewa kwa neema iweje sasa tujisifie, kana kwamba tumevipokea kwa nguvu zetu na utashi wa watumishi wetu, na ukuu wao, na uwezo wao wa kuhubiri vizuri? Karama hizi za rohoni hakuna hata mmoja imetoka kwa mwanadamu, wenyewe wamefanyika vyote tu. Hivyo wa kujivunia hapo na kusifiwa hapo ni Mungu wala si Paulo au Apolo.
Jambo ambalo hata leo huonekana kwa baadhi ya watu wa kanisa la leo. Ikiwa tuna msingi katika Kristo, iweje kujivunia makanisa au huduma, na kujiona sisi ndio bora zaidi ya wale wengine?
Ni kweli zipo huduma ambazo si za kweli, hazina msingi sahihi wa Kristo Yesu. Lakini ikiwa wote Injili yetu ni ya Kristo aliyesulubiwa kutukomboa sisi, basi tofauti za kiutendaji kazi, au kiujuzi, zisitufanye tujione bora, kwasababu sio hao wanadamu walitoa hivyo vipawa bali ni Roho Mtakatifu. Na anatenda kazi kama apendavyo yeye, anampa huyu hiki, anampa Yule kile.
Mmoja atapanda, mwingine atatia maji, mwingine mbolea, mwingine mvunaji, lakini atakuzaye ni Mungu mmoja, katika shina la Yesu Kristo Bwana wetu.
Kama mkristo ukijiona una vita vya kiuhuduma, ujue bado ni mchanga kiroho, bado unatabia za mwilini.
Bwana atusaidie.
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
MBINGUNI YUPO NANI SASA?
SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango”.
Yakobo 5:9 Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
JIBU: Neno la Mungu halitoi nafasi ya sisi, kunung’unikiana kwasababu yoyote. Aidha ya kuonewa, au kudhulumiwa, kuaibishwa au kufanyiwa jambo ambalo halikupasa utendewe, Manung’uniko ni zao la kutokuwa na uvumilivu. Na kwamba tukifanya hivyo basi, tafsiri yake ni kuwa tunamfanya Mungu naye aghahiri uvumilivu wake kwetu.
Lakini anatoa, suluhisho, kwamba hayo tuyaache mikononi mwake. Kwasababu yeye ndio mwamuzi wetu. Na kwamba, sio tu mwamuzi lakini ni mwamuzi ambaye yupo mlangoni. Akiwa na maana kuwa Kristo yupo karibu sana na maonevu, au dhuluma hizo, na kwamba yeye mwenyewe atalipa, wala hatakawia, kwasababu yupo mlango.
Atalipa aidha kwa wakati huu huu duniani, au siku ile ya mwisho wa Hukumu. Kwake yeye ni lazima haki itendeke. Pia kwa upande mwingine anataka uogope kwasababu ukinung’unika yeye hayupo mbali kukusikia.
Wafilipi 4:5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, popote tusimamapo kutoa malalamiko, laumu, kuhesabu makosa, n.k. basi tutambua kuwa Kristo yupo hapo hapo katikati yetu kutusikia. Hivyo tusiwe wepesi ya kunena, bali tujifunze kuwa wavumilivu katika mambo yote. Ili Mungu atuachilie neema yake.
Je! Umeokoka? Je, umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo? Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, tubu dhambi zako, kwa kumwamini Yesu upokee ondoleo la dhambi zako, Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.
Ikiwa upo tayari kumkabidhi leo maisha yako. Basi fungua hapa kwa mwongozo huo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
MWAMUZI WA KWELI:
“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?
Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”
Je! Umejengwa kweli juu yake?
Ukimuuliza mtu, mwamba ni nini, ni rahisi kukujibu YESU. Jibu ambalo ni sahihi, maandiko yanatuthibitishia hilo Yesu kuwa Yesu ni mwamba (Mathayo 21:42, 1Wakorintho 10:4). Lakini lazima ufahamu pia MWAMBA mwenye anasemaje, kuhusu yeye mwenyewe alivyo.
Ni maneno ambayo tunayasoma lakini si rahisi kuyatafakari kwa ukaribu, embu tusome tena, halafu utaona mwamba alimaanisha nini. (Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa) Soma kwa utulivu.
Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. 28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.
Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.
Umeelewa? Vema hayo maneno?
Kumbe mtu yeyote anayesikia maneno ya Yesu. Hapo hapo huwa anaanza ujezi.
Lakini tofauti inakuja mahali anapokwenda kujengea,. Yule aliyejenga kwenye mchanga tafsiri yake Yesu anasema, anasikia, lakini hayatendei kazi (Hayafanyi), aliyoyasikia. Hivyo hapo Mchanga, ni KUTOTENDA.
Lakini Yule mwingine aliyekwenda kwenye mwamba tafsiri yake ni anasikia lakini pia anatenda. Hivyo MWAMBA, ni kutenda.
Mwamba sio kumjua Yesu ndugu, mwamba sio kusoma sana biblia na kujua mafumbo na siri zote zilizo katika biblia, mwamba sio kujua kujua tafsiri zote za kigiriki na kiebrania kwenye maandiko, mwamba sio kujua kufundisha vema biblia,.. Sio hivyo vyote.
Mwamba ni KULITENDEA KAZI NENO, Unalolisikia kwake. Hilo tu. Sio kumjua Yesu.
Hatari iliyopo leo, miongoni mwa wakristo wengi, ni kwamba tumejengwa juu ya mafundisho mengi. Lakini hatujajengwa juu ya kutendea kazi mafundisho tunayofundishwa. Ndugu fundisho halikusaidii kuyashinda majaribu, au tufani za mwovu, au dhoruba, au pepo, hapo unafanya kazi ya kuchosha tu,kudumu katika kusikia, kusoma, kusikiliza, bado si suluhisho, kusema nimebarikiwa, nimefunguliwa ufahamu, bado hakukufikishi popote, kama HUTALIISHI hilo Neno.
Ukiwa ni wa kufanya bidii kuliishi NENO moja, wewe ni imara sana kuliko Yule mwenye kujiona anaijua biblia yote
Penda Utakatifu, penda usafi wa moyo, penda kupiga hatua rohoni. Penda matendo mema.
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
NAYAJUA MATENDO YAKO.
Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)
Ngome ni nini? Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?
JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?
Swali: Kwanini katika biblia lisitumike neno “Mwizi” na badala yake linatumika neno “Mwivi”…Mwivi ni nini?
Jibu: Mwivi na Mwizi ni Neno moja, lenye maana moja.. isipokuwa ni lugha mbili za nyakati mbili tofauti.
Kiswahili kilichotumika katika kutafsiri biblia ni Kiswahili cha zamani, kilichoitwa “kimvita” ambacho ndicho kimebeba maneno ambayo hatuyaoni katika Kiswahili cha sasa, na mojawapo ya maneno ndio kama hayo “Mwivi na wevi” ikimaanisha “mwizi na wezi”. Ndio maana katika biblia yote huwezi kukuta neno Mwizi, badala yake utakuta mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoeli 2:9, Luka 12:39 n.k )
Maneno mengine ya kimvita (Kiswahili cha zamani) ambayo mengi ya hayo hayatumiki sasa ni pamoja na “jimbi” badala ya “Jogoo”… “Kiza” badala ya “Giza”….”Nyuni” badala ya “ndege”…. “Kongwa” badala ya “Nira” na mengine mengi.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “Mwivi” na “Mwizi” ni Neno moja, lenye maana ile ile moja (ya mtu anayeiba).
Lakini mbali na hilo, maandiko yanatufundisha kuwa Bwana YESU atakuja kama “Mwivi”..
Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”
Je umewahi kujiuliza ni kwanini aje kama Mwivi na si Askari?.. Kwa upana juu ya hilo basi fungua hapa >>ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.
Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha
OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!
Nini maana ya ELOHIMU?
Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).
WhatsApp
Swali: Je Neno “Kalvari” tunalisoma wapi katika biblia?, na tofauti yake na Golgotha ni ipi?
JIbu: Katika biblia ya Kiswahili hakuna neno “Kalvari”, bali kuna neno “Golgotha” ambalo tunalisoma katika kitabu cha Yohana 19:17
Yohana 19:17 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, GOLGOTHA. 18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati”.
Yohana 19:17 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, GOLGOTHA.
18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati”.
Maana ya Neno “Golgotha”, tayari biblia imeshatoa tafsiri yake hapo kwenye mstari wa 17 kuwa ni “Fuvu la Kichwa”
Sasa neno “Kalvari” maana yake ni nini?
Neno Kalvari linapatikana katika tafsiri chache za lugha ya kiingereza, ambalo asili yake ni lugha ya Kilatini “CALVARIAE” lenye maana ile ile ya “Fuvu la kichwa cha mtu”.
Hivyo “Kalvari” na “Golgotha” ni Neno moja lenye maana moja, isipokuwa lugha tofauti, ni sawa na neno “church” na “kanisa” ni kitu kimoja ila lugha tofauti.
Kufahamu kwa upana ufunuo uliopo nyuma ya Golgotha, (Fuvu la kichwa), basi fungua hapa >>>FUVU LA KICHWA.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
Swali: Je wale waliowekewa tayari ni akina nani na kwanini Bwana Yesu aseme maneno yale?
Jibu: Tuanzie kusoma mstari wa 20..
Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. 21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. 22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. 23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, SINA AMRI KUWAPA, BALI WATAPEWA WALIOWEKEWA TAYARI NA BABA YANGU”.
Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.
22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.
23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, SINA AMRI KUWAPA, BALI WATAPEWA WALIOWEKEWA TAYARI NA BABA YANGU”.
Ili tuelewe vizuri, hebu tafakari mfano huu.. “wanafunzi wawili wamemfuata mwalimu wao wa darasa na kumwomba washike nafasi ya kwanza kitaifa na mwingine ashike ya pili kitaifa katika mitihani yao ya mwisho wa kuhitimu”.. Unadhani jibu la mwalimu litakuwa ni lipi?..
Bila shaka mwalimu atawauliza.. je! Mtaweza kusoma kwa bidii??.. Na kama wale wanafunzi watajibu NDIO!.. Bado Mwalimu hataweza kuwapa hizo nafasi, bali atawaambia mimi sina mamlaka ya kuwapa bali “Wasahishaji watakaosahisha mitihani ya wote ndio watakaotoa majibu ya mitihani yenu na kuwapanga kama mmestahili hizo nafasi au la”..
Ndicho Bwana YESU alichowaambia hawa wana wa Zebedayo!.. ambao walienda kumwomba nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake.. na jibu la Bwana YESU likawa, ni “kukinywea kikombe”.. maana yake kukubali mateso kwaajili yake!.. Na wao wakajibu “wataweza”.. Lakini jibu la Bwana likawa “Nafasi hizo watapewa waliowekewa tayari”..maana yake waliostahili.
Na hao waliostahili ni akina nani?
Ni wale watakaofanya vizuri Zaidi ya wengine wote katika mambo yafuatayo.
1. KUKINYWEA KIKOMBE.
Kikombe alichokinywea Bwana Yesu ni kile cha Mateso ya msalabani (Soma Mathayo 26:39), kutemewa mate, kupigwa Makonde, kuvikwa taji ya miiba, na kugongomelewa misumari mikononi..
Na yeyote ambaye atakubali kuteswa kwaajili ya Kristo, na si kwaajili ya mtu au kitu kingine chochote, basi yupo katika daraja zuri la kumkaribia Kristo katika siku ile kuu.
2. KUBATIZWA UBATIZO WA BWANA YESU.
Marko 10:38 “Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au KUBATIZWA UBATIZO NIBATIZWAO MIMI?”
Swali Ubatizo aliobatizwa Bwana YESU KRISTO ni upi?…. si mwingine Zaidi ya ule wa kufa, kuzikwa na siku ya tatu kufufuka, na kupaa juu (soma Luka 12:50), Na ubatizo huu mpaka sasa hakuna rekodi ya wazi ya yoyote aliyeupitia..
Ubatizo tubatizwao sasa ni ule wa maji mengi, ambao ni ishara ya kufa na kufufuka na Kristo (Wakolosai 2:12), kwamba tunapozamishwa katika maji mengi na kuibuka juu, ni ishara ya kufa pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye… Lakini Ule hasa wa kufa na kufufuka na kupaa, hakuna rekodi ya wazi ya aliyeupitia.
Isipokuwa unawezekana ndio maana tunasoma katika Ufunuo 11, kuwa wale washahidi wawili, ni miongoni mwa watakaoupitia..
Ufunuo 11:10 “….Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. 11 NA BAADA YA SIKU HIZO TATU U NUSU, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. 12 WAKASIKIA SAUTI KUU KUTOKA MBINGUNI IKIWAAMBIA, PANDENI HATA HUKU. WAKAPANDA MBINGUNI KATIKA WINGU, ADUI ZAO WAKIWATAZAMA”.
Ufunuo 11:10 “….Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.
11 NA BAADA YA SIKU HIZO TATU U NUSU, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.
12 WAKASIKIA SAUTI KUU KUTOKA MBINGUNI IKIWAAMBIA, PANDENI HATA HUKU. WAKAPANDA MBINGUNI KATIKA WINGU, ADUI ZAO WAKIWATAZAMA”.
Je umempokea YESU?, Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Kristo yupo mlangoni.
USIWE ADUI WA BWANA
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?
UWE KIKOMBE SAFI
Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?
Swali: Wenye kutia Kalafati ni watu gani?
Jibu: Neno “Kalafati” limeonekana mara mbili tu katika biblia, katika Ezekieli 27:9 na Ezekieli 27:27.
Na maana yake ni “Kamba nyembamba iliyotengenezwa kwa pamba” ambayo inawekwa katikati ya mianya ya mbao za merikebu, ili kuzuia maji yasipenye katika ile miunganiko. (Tazama picha juu)
Hivyo watu wanaofanya hiyo kazi ndio waliotajwa hapo katika Ezekieli 27:9,
Ezekieli 27:9 “Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, WENYE KUTIA KALAFATI; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako”.
Lakini habari hii inahusu nini?
Ukisoma kitabu hicho cha Ezekieli mlango wa 27 kuanzia mstari wa kwanza, utaona ni unabii unamhusu mfalme wa Tiro. (Kwa urefu kuhusu Taifa la Tiro fungua hapa >>>Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa?
Lakini hapa ni unabii wa Mfalme wa Tiro, Kwamba kwa kiburi chake na biashara zake nyingi alizozifanya juu ya nchi na katika bahari kupitia merikebu zake, siku inakuja ambapo ataanguka na kushuka chini kwasababu ya dhambi zake nyingi.
Na biashara za baharini alizokuwa anazifanya kupitia merikebu zake kubwa ambazo ndani yake kulikuwa na wana-maji, na “watiao Kalafati” na manahodha, zitaanguka na shughuli zao hizo zitaisha!
Ezekieli 27:27 “Mali zako, na bidhaa yako, na utajiri wako, wana-maji wako, na rubani zako, na WENYE KUTIA KALAFATI WAKO, na wafanya biashara wako, na watu wako wa vita wote, walio ndani yako, pamoja na jeshi lako lote lililo ndani yako, wataanguka katika moyo wa bahari katika siku ya kuangamia kwako”.
Ufunuo kamili pia kwa anguko la ulimwengu pamoja na dini zake za uongo katika siku za mwisho..
Ufunuo Ufunuo 18:2 “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; 3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake……………….. 9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; 10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. 11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu. 14 Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe. 15 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza”
Ufunuo Ufunuo 18:2 “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake………………..
9 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;
10 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.
11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;
12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;
13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.
14 Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.
15 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza”
Je Umeokoka kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa, sawasawa na Marko 16:16?. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Kristo amekaribia kurudi.
Kwa msaada Zaidi katika kumpokea Kristo fuatiliza sala hii ya Toba >>KUONGOZWA SALA YA TOBA au wasiliana nasi kwa namba zetu zilizoanishwa mwisho wa somo hili.
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.
Tarshishi ni mji gani kwasasa?
Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).
Kuna tofauti gani kati ya “Edeni” na “Adeni”?
SWALI: Je! Mithali 6:30 inamaana gani?
Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; 31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.
JIBU: Chukulia mfano mtu hajala siku tatu, halafu akaona kuna duka lipo wazi pale jirani, na mwenyewe ametoka, akashawishika kuingia haraka na kubeba mkate, ili akale. Lakini mwenye duka aliporudi na kuona mkate umeibiwa, alianza kumfuatilia, mwishowe akamkuta amejificha mahali Fulani anakula akiwa katika hali mbaya.
Kibinadamu, atakapoona hali halisi ya mwizi, huwenda ataishia kukasirika tu, au kumgombeza, au kwenda kumwajibisha, kwa mambo madogo madogo. Kwasababu anaona alichokifanya ni kwa ajili ya kusalimu maisha yake tu, ale asife, lakini sio kwa lengo la kuchukua vya watu, akauze, au kuleta hasara kwa wengine.
Lakini sehemu ya pili ya mstari huo anaendelea kusema kama “akipatikana atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake”.
Maana yake ni kuwa kama “atapatikana na kosa”, basi atalipa mara saba. Atagharimikia vyote alivyoviiba mara saba. Sasa kauli hiyo haimaanishi kwamba mwizi huyo huyo aliyeiba kwa ajili ya kujishibisha tumbo lake ndio atalipa mara saba, hapana, vinginevyo mstari huo ungekuwa unajipinga unaposema “watu hawamdharau mwizi akiiba kwa kujishibisha”, bali anamaanisha kama akipatikana na hatia tofauti na hiyo..mfano aliiba vitu ili akauze, aliiba fedha ili akajiendeleze kwenye mambo yake, alete hasara kwa wengine. Huyo atalipa gharama zote mara saba.
Ndio maana utaona adhabu nyingi za wezi huwa ni kubwa sana zaidi ya vile walivyoviiba, wanapigwa faini kubwa, wengine mpaka wanauliwa, kwa wizi tu mdogo. Hapo ni sawa na wamelipa mara saba.
Kama njaa ya mwilini, inaweza kumfanya mwizi asihesabiwe kosa. Kwasababu watu wanaelewa umuhimu wa kunusuru uhai kwa chakula, vipi kuhusu rohoni. Hata kuna wakati Daudi alikula mikate ya makuhani ambayo hawakupaswa watu wengine kula, lakini kwasababu alikuwa na njaa yeye na wenzake haikuhesabiwa kwake kuwa ni kosa (1Samweli 21).
Vivyo hivyo rohoni, Mungu anatufundisha sio kwamba tuwe wezi, hapana, lakini anataka tuthamini sana roho zetu, pale zinapokuwa hazina kitu, zina njaa. Iweje mtu unakaa hadi unakufa kiroho halafu unaona ni sawa kuwa hivyo hivyo kila siku. Hufanyi jambo Fulani la kujinasua katika hiyo hali yako mbaya rohoni, unaendelea tu hivyo hivyo. Tafuta kwa bidii chakula cha kiroho usife ndugu. Jibidiishe.
Iba muda wako wa kufanya mambo mengine ili ukipate chakula cha kiroho. Ni kweli ulipaswa kuwepo mahali Fulani pa muhimu, embu ghahiri muda huo, nenda kasome biblia, nenda kaombe, nenda kasikilize mahubiri yatakayokujenga. Ulipaswa uwepo kazini, lakini kwasababu ibada ile ni muhimu embu usione shida kughahiri.
Huna biblia Iba hata pesa yako ya matumizi ya muhimu kanunue, acha uonekane mjinga nenda kanunue biblia au vitabu vya rohoni vikujenge. Tafuta ile MANA iliyofichwa.
Siku hizi ni za mwisho. Na Bwana alishatabiri duniani kutakuwa na njaa, sio ya kukosa chakula au maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Mungu ya kweli. Usipojiongeza katika eneo la ukuaji wako kiroho. Ni ngumu kuvuka hizi nyakati mbaya za manabii wengi wa uongo, na mafundisho ya mashetani. Usipoyajenga maisha yako ya kiroho, shetani akusaidie kuyajenga kwake.
Amosi 8:11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana”
Penda biblia, penda kujifunza, penda maombi zaidi ya vingine.
YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.
NJAA ILIYOPO SASA.
(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
(Opens in a new browser tab)KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.(Opens in a new browser tab)