Title July 2018

DANIELI: Mlango wa 2

Kulikuwa na sababu kwanini Mungu aliinyanyua Babeli kuwa taifa lenye nguvu kuliko yote duniani na kutawala falme zote za dunia kwa wakati ule, hata kudhubutu kulichukua taifa teule la Mungu Israeli kulipeleka utumwani, pamoja na kuteketeza mji na Hekalu la Mungu..Aliruhusu kwasababu alitaka kuonyesha kuwa ijapokuwa ni mji uliokuwa umetukuka sana, lakini siku moja kwa wakati ulioamriwa mji huo utaanguka na kuwa makao ya mbuni, na hayawani wote wa mwituni usioweza kukalika na watu . Hivyo ndivyo itakavyokuwa pia kwa BABELI YA ROHONI iliyopo leo ijapokuwa imetukuka sana, biblia inasema kwenye ufunuo 18 itaanguka na kuwa ukiwa na watu wote watauomboleza kwa kuanguka kwake.

Tunasoma miaka kadhaa kabla ya kuanguka kwake Mungu alishaanza kutoa maonyo kwa watawala wa Taifa hilo, na ndio maana tunaona ndoto zote na maono waliyoyaona yaliwafadhaisha sana, kwasababu walikuwa wanafahamu kwa namna moja au nyingine zinawahusu wao na utawala wao. Na kibaya zaidi ni kuona jinsi yale maono yalivyokuwa yanaishia.

Kama tunavyosoma katika sura hii ya pili Mfalme Nebukadneza aliota ndoto, ambayo ilimhuzunisha sana mpaka kufikia kwenda kuwaita waganga, na wachawi pamoja na watu wote wenye hekima waliokuwa Babeli wampe tafsiri ya ndoto ile, lakini hakuonekana hata mmoja ambaye angeweza kutoa tafsiri, waganga wote na wachawi walikiri kuwa hakuna awezaye kuingia katika vyumba vya ndani vya moyo wa mwanadamu isipokuwa Mungu peke yake. Na ni kweli ndivyo ilivyo shetani hana uwezo wa kuingia ndani ya mtu na kuyafahamu mawazo yake, ndio anaweza kutuma mawazo mabaya lakini hawezi kutambua fikra za mtu zikoje, mwenye uwezo huo ni Mungu tu,

Waebrania 4:12-13″ Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. “

Kwahiyo Mfalme alipoona hakuna mtu wa kumtafsiria ndoto yake, akakusudia kuwaangamiza waganga na wenye hekima wote wa Babeli lakini Mungu akamjalia Danieli na wenzake neema ya kufahamu tafsiri ya ile ndoto, na kuipeleka kwa mfalme. Tunasoma..

Danieli 2:26″ Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake.

27 Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu;

28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;

29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa.

30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.

31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha.

32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;

33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.

34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.

37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;

38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.

39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.

40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta.

41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.

42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.

43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.

45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.

46 Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danielii, akatoa amri wamtolee Danielii sadaka na uvumba.

47 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii.

48 Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.

49 Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme.

Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.

Katika ndoto hii tunaona Danieli akifunuliwa na Mungu Falme 4 zitakazokuja kutawala mpaka mwisho wa dunia, Kumbuka hakutakuwa na falme nyingine zaidi ya hizo, na ule wa tano ambao ndio uleule wa nne isipokuwa umechanganyikana na udongo ndio utakuwa wa mwisho kabla ya lile jiwe lilolochongwa mlimani pasipo kazi ya mikono kuupiga na kuuharibu kabisa.

Kama Danieli alivyomtafsiria mfalme kwamba kile kichwa cha dhahabu kinamwakilisha yeye(yaani ufalme wake wa Babeli),ambao kulingana na Historia ulidumu kuanzia mwaka 605BC hadi mwaka 539BC, Hichi ni kipindi cha miaka 66 , na baada ya hapo ukaanguka kama kitabu cha Danieli sura ya tano kinavyoelezea pale Mfalme Belshaza alipokuwa anafanyia anasa vyombo vya hekalu la Mungu kukatokea kiganja na kutoa hukumu juu ya kuanguka kwa ufalme wake, tunasoma katika usiku huo huo ufalme wake ulianguka.

Kisha ukanyanyuka utawala mwingine baada yake, tukisoma katika biblia ulikuwa ni utawala wa (Umedi na Uajemi) ambao ndio unawakilishwa na kile kifua na mikono ya fedha, Huu ulianza kutawala pindi tu Babeli ilipoanguka kuanzia mwaka 539BC hadi 331 BC. Nao ulienda kwa kipindi cha miaka 208, Pia kumbuka mwanzoni mwa utawala huu ndio Taifa la Israeli lilipokea Uhuru wake ili kutimiza unabii wa miaka 70 ya kukaa kwake utamwani kama Yeremia alivyotabiri, na kurejea tena katika nchi yake, ili kuijenga nyumba ya Bwana aliyokuwa imeharibiwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli.

Agizo hilo la kurejea na kuijenga tena nyumba ya Mungu, liliasisiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi. Tunasoma..

Ezra 1:1 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,

2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;

3 Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu.

4 Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. “

Lakini baadaye mwishoni historia inaonyesha ulikuja ukaanguka.

kisha baada ya huo ulikuja Utawala mwingine wa tatu chini ya Mfalme “Alexander the great” aliyekuwa mfalme mwenye nguvu, tunasoma katika historia na katika biblia ulikuwa ni utawala wa Uyunani ambao unawakilishwa na kile kiuno na shaba, Huu ulianza kutawala kuanzia mwaka 331 BC hadi 168 BC, Ni kipindi cha miaka 163,

Na baada ya huu ufalme wa Uyunani kuanguka ulinyanyuka utawala mwingine uliokuwa na nguvu kama za chuma, uliowakilishwa na ile miguu ya chuma, na huu haukuwa mwingine zaidi ya utawala wa RUMI ya kipagani.Utawala huu ulidumu tangu kipindi cha 168 BC hadi kipindi cha 476 AD, ni zaidi ya miaka 644 na huu ndio utawala uliomsulibisha Bwana Yesu, uliwaua watu wengi kikatili kwa kuwasulibisha misalabani, wengine kwa kuchomwa moto n.k. na ndio maana biblia inasema ulikuwa ni mgumu kama CHUMA.

Tukiendelea tunasoma utawala mwingine wa tano na wa mwisho ulifuatia ambao ni chuma kilichochanganyikana na udongo, huu ni utawala ule ule wa nne isipokuwa hapa unaonekana kama umechanganyikana na udongo, Hivyo ni ule ule wa Rumi lakini umechanganyikana ndio unaowakilishwa na zile nyayo na vidole vya miguu ..

JE! huu udongo uliochanganyikana na chuma ni nini?. 

Mstari wa 43 unasema..

43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

Kumbuka hapo kabla, Taifa la Rumi lilikuwa haliingiliani na Taifa la Mungu kiimani kwa kipindi chote lilipokuwa linatawala dunia kama chuma, wakati huo lilikuwa lipo kisiasa na kiuchumi zaidi, lakini lilikuja kubadilika baadaye na kubadili tasira yake kwa kupitia DINI ili kujiingiza katikati ya taifa la Mungu (wakristo na wayahudi) 

1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, TAIFA TAKATIFU, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, BALI SASA NI TAIFA LA MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Kumbuka hii ilikuwa ni agenda ya shetani alipoona mambo yamehamia Rohoni na yeye akahamia rohoni.

Kwahiyo ule UDONGO unawakilisha WATU WA MUNGU au TAIFA LA MUNGU, na ndio zile mbegu za wanadamu.

Hivyo taswira hii ya kujigeuza ilianza kujidhihisha wakati wa utawala wa Costantine, pale upagani wa kirumi ulipoingizwa rasmi katika Ukristo, hapo ndipo mafundisho ya kweli ya NENO la Mungu yalipoanza kuchanganywa na mafundisho ya kipagani ya kirumi ili tu kuwafanya watu wabebe taswira ya ufalme wa Rumi na wakati huo huo bado wabebe taswira ya Ufalme wa Mungu (Ukristo), Na ndio maana leo mtu akiulizwa wewe ni nani? atakuambia mimi ni MROMA, badala ya kuwa na utambulisho wa taifa lake la mbinguni (yaani kuitwa mkristo), atakuambia ndio mimi ni mkristo na pia ni Mroma, unaona hapo tayari ameshachanganyikana na ule ufalme wa chuma (ambao ndio Babeli ya rohoni ya sasa), na ndio wenye watu wengi duniani leo.

Kumbuka huu utawala ndio wa mwisho na hakutakuwa na mwingine baada ya huo (BABELI YA ROHONI) inayozungumziwa katika Ufunuo 17 & 18, Hivyo hii Rumi iliyochanganyikana na udongo ni UKATOLIKI. DINI hii imechukua desturi za Roma za kipagani ikazileta katikati ya watu wa Mungu, kwamfano ibada za sanamu ambazo Mungu alizikemea akilionya taifa lake lisifanye mambo kama hayo ni machukizo (Kutoka 20) lakini hili limeyaleta katikakati ya watu wa Mungu, ibada kama kusali rozari na kuomba kwa wafu, mafundisho ya kwenda toharani, kukataa uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuua karama za Roho na kuweka vyeo vya uongozi wa kibinadamu badala yake, n.k. Haya yote yalipenyezwa katika NENO la Mungu na kuleta mchanganyiko mkubwa sana katika Kanisa la Kristo.

Lakini mwisho wa lile ONO lilionekana JIWE likiwa limechongwa Mlimani na kushuka, tukisoma..

34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Na jiwe hili si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, yeye ndiye atakayebatilisha hizi falme zote mbovu kwa kuupiga ule ufalme wa mwisho kuleta utawala mpya Duniani ambao huo utadumu milele. Kwasababu yeye ni BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME. Haleluya!!..Na jiwe lile lilionekana likiwa milima mikubwa ikishiria kuwa Kristo atatawala duniani kote pamoja na wafalme wengi(wateule wake) milele na milele.

Mstari wa 44 unasema..

” Danieli 2:44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”

Hivyo ndugu kama tunavyosoma hakitasalia chochote katika ile sanamu?, na wewe je! upo kwenye ile sanamu kumbuka utawala wa shetani uliopo leo ndio ule wa tano uliojichanganyika yaani chuma na udongo(shetani ni mdanganyifu, haji kwako moja kwa moja,)..Udongo ni wewe unayejiita mkristo, na chuma ni ROMA, chini ya mwamvuli wa dini ya katoliki, je na wewe umejichanganya humo? kumbuka lile jiwe lilisaga saga chuma na udongo vyote kwa pamoja, hivyo kama na wewe umejichanganya naye utasagwasagwa kama yeye hakitasalia kitu.

Kumbuka yule mnyama anayezungumziwa kwenye Ufunuo 13 & 17 ni dola ya Rumi inayounda ile chapa ya mnyama, na yule mwanamke aliyeketi juu ya yule mnyama ni Kanisa Katoliki, na anafahamika kama mama wa makahaba, ikiwa na maana kuwa anao mabinti wenye tabia kama za kwake za kikahaba, na hawa mabinti si wengine zaidi ya madhehebu mengine yote yaliyoacha uongozi wa Roho wa mtakatifu na kufuata desturi zisizoendana na NENO LA MUNGU.

Na ndio maana NENO LA MUNGU linasema Ufunuo 18:4″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Kanisa tulilopo ni la mwisho linaloitwa LAODIKIA, na Bwana alilikemea kuwa ni kanisa vuguvugu (lililochanganyikana), na Bwana amesema atalitapika kama lisipotubu,

Ufunuo 3:14-20″14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “

Huu ni wakati wa kuwa bibi-arusi safi wa Bwana asiwe na mawaa, kwa kujitenga na mafundisho ya uongo pamoja na kuishi maisha matakatifu( waebrania 12:14″ Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;” ) ili BWANA atakapokuja tuwe tayari kwenda naye katika unyakuo.

Print this post

DANIELI: Mlango wa 1

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO na MKUU wa Dunia yote libarikiwe,

Karibu katika kujifunza kitabu cha Danieli, leo tukianza na ile Sura ya kwanza, Kwa ufupi tunasoma mlango huu wa kwanza kama wengi tunavyofahamu unaeleza jinsi wana wa Israeli walivyochukuliwa utumwani mpaka Babeli kutokana na wingi wa maovu yao, na Mungu kwa kupitia kinywa cha Nabii wake Yeremia alishawatabiria kuwa wangekaa huko kwa muda wa miaka 70 mpaka watakaporudi tena katika nchi yao wenyewe. Lakini mara tu ya kwenda utumwani tunasoma mfalme Nebukadneza alitamani kuwa na watu ambao watamsaidia katika Elimu za utafiti pamoja na utabiri wa mambo yanayokuja katika ufalme wake, hivyo akaazimu kwenda kuwatafuta watu wenye ujuzi mwingi na maarifa pamoja na wanajimu na wachawi wote waliosifikia, kutoka katika majimbo yote ya dunia aliyokauwa anayatawala.

Lakini taunaona walipofika kwa watu walioamishwa wa kabila la Yuda, walionekana huko vijana wanne, wenye sifa ya kuwa na ujuzi na hekima zilizotoka kwa Mungu nao ni Shedraki, Meshaki, Abednego pamoja na Danieli ambaye alikuwa na ujuzi katika ndoto na Maono yote.

Hivyo tunasoma walipopelekwa katika jumba la kifalme kwa mafunzo ya lugha na Elimu za wakaldayo, kama tunavyojua maeneo kama hayo havikosekani vyakula vya kila namna, vinono vyote kama nguruwe, nyama za wanyama wasiopasuka miguu kama bata, divai, na ng’ombe, kuku n.k vilikuwepo ambavyo vingi kati ya hivyo vilikuwa ni Najisi kwa Taifa la Israeli.

Kwahiyo Danieli na wenzake kwa kuwa walikuwa wanamcha Mungu hawakudhubutu kuvunja torati ya Mungu kwasababu ya vyakula, Hivyo wakaazimu kumuomba mkuu wa Matowashi wasivitumie vile vyakula, ndipo wakajaribiwa kwa mtama na maji kwa muda siku 10, na tunaona licha ya kwamba MTAMA na MAJI ni vyakula visivyokuwa na virutubisho kamili lakini tunaona waliweza kunona na kunawiri kuliko wale wengine wote waliokuwa wanajishibisha na vyakula vyote vya kifalme.

Na yule mkuu wa Matowashi alipouona muujiza ule na ujasiri wao, moja kwa moja aliwatolea ile posho ya vyakula najisi na kuwalisha vyakula walivyokuwa wanataka wao. Na baada ya ile miaka 3 kuisha ya mafunzo, walipowasilishwa mbele ya MFALME ili kuzungumza nao, hawakuonekana waliokuwa mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraki na Abednego watakaomfaa katika baraza lake la washauri.

Amen.

TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MAMBO HAYA?.

Tunapomuweka Mungu nyuma kwasababu ya fursa fulani au mazingira fulani yaliyopo mbele yetu, tukidhani kuwa ndio tutafanikiwa ukweli ni kwamba hatutafanikiwa tutakwama tu!!, Inawezekana mazingira yanayokuzunguka kama nyumbani au kazini au popote pale yanakulazimisha wewe mwanamke uvae vimini au suruali, au kuweka makeup, angali ukifahamu kuwa sheria ya Mungu hairuhusu hayo mambo, ni najisi, kwakuwa unaogopa kutengwa, au kufukuzwa kazi, au kuonekana wewe ni mshamba sio mzuri, unajitia unajisi kwa kufanya vitu ambavyo Mungu hakukuagiza ufanye ukidhani kuwa ndio utafanikiwa au utaonekana mzuri au utapandishwa cheo n.k., ukweli ni kwamba hautafanikiwa kwa lolote, safari yako ni fupi.

Danieli na wenzake, waliazimu kula mtama na maji tu, lakini ndani ya siku 10 tu walinawiri kuliko wale wengine wote, kuonyesha kuwa vyakula vya unajisi havimfanyi mtu kunawiri badala yake ndio vinamfanya mtu KUFUBAA.

Na sisi leo vyakula vyetu najisi ni nini??..Sio nguruwe, wala bata, bali ni Uasheratiibada za sanamu,UlevisigaraUfisadiusengenyaji,utukanaji,wiziRushwa, Fashion{vimini, suruali, makeup, wiggy}ushogapornoghaphymusterbation,discokamari,anasa, n.k. Hivi vyote vitakupelekea UFUBAE rohoni na mwilini,kwamaana vinatoka rohoni Bwana Yesu alisema..

Mathayo 15:16-20″ Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?

17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi;… “

Hivyo usidhani kwamba kwa kufanya hivyo utakubalika, au utaonekana mzuri, au utafanikiwa, la!! bali itakuwa ni kunyume chake.”

Kumcha Mungu ndio chanzo cha mafanikio yote na Hekima yote, kwa kadiri tutakavyozidi kuendelea kutazama sura zinazofuata tutaona jinsi Danieli alivyokuwa mwaminifu mpaka Mungu akampa kujua SIRI ya mambo yatakayokuja kutokea mpaka mwisho wa dunia, na kupewa cheo cha kuwa mkuu wa maliwali na waganga wote wa dunia.

Ni maombi yangu leo katika nafasi uliyopo, USIJITIE UNAJISI NA VITU VYA ULIMWENGU HUU, Bali uwe na msimamo kama Danieli na wenzake walivyokuwa, na watakapouona msimamo wako, watakuacha uendelee nao, lakini usipoonyesha msimamo wako, shetani atakuchezea kama anavyotaka.

Ubarikiwe na Bwana YESU

Kwa mwendelezo >>MLANGO WA PILI.


Mada Nyinginezo:

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

BIBLIA INAPOSEMA”VILIVYOTAKASWA NA MUNGU, USIVIITE WEWE NAJISI”. JE KAULI HIYO INATUPA UHALALI WA KULA KILA KITU?

JE! INAWEZEKANA MTU AKAWA ANAONA MAONO NA KUFANYA MIUJIZA NA BADO ASINYAKULIWE?

NINI MAANA YA KUBATIZWA KWA AJILI YA WAFU? (1WAKORINTHO 15:29)


Rudi Nyumbani:

Print this post

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Jina la BWANA wetu na mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe milele daima.

Karibu katika kujifunza maneno ya Mungu, leo tukiwa katika mwendelezo wa kitabu cha Yuda  tunapomalizia sehemu ile ya mwisho. Tunasoma.

Yuda 1: 14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.

16 Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

17 Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,

18 ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu.

19 Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.

20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

21 jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.

22 Wahurumieni wengine walio na shaka,

23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.

24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

25 Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina. “

Kama tulivyotangulia kusoma sehemu zilizopita tuliona watu wa aina TATU, mwovu aliowapandikiza katika kanisa la Mungu, waliofananishwa na nyota zipoteazo ambao weusi wa giza ndio akiba waliyowekewa milele, ambao wanafananishwa pia na miti ipukutishayo isiyo na matunda iliyokufa mara mbili, na visima visivyo na maji na miamba yenye hatari..wanafananishwa na magugu yaliyopandwa katikati ya ngano.

Na maonyo haya kumbuka waliandikiwa watu ambao wapo katika safari ya Imani, wakafananishwa na wana wa Israeli walipokuwa safarini, Na kama tunavyosoma wengi wao hawakuweza kuishindania Imani yao na kuilinda Enzi yao wakaishia kuanguka kwa makosa mengi, ikapelekea kutokuiona ile nchi ya AHADI Mungu aliyowaahidia.

Na tuliona watu waliotumiwa na shetani kuwakosesha wana wa Israeli Jangwani, walikuwa ni KORA na BALAAMU. Hawa walikuwa ni manabii, Na ndio maana kitabu cha Yuda kimewataja watu 3, na mwingine alikuwa ni KAINI. Tukisoma mstari wa 11 unasema 

“Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.

12 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ” .

Sasa huduma za watu hawa 3, ndizo zinazotenda kazi katika kanisa la Mungu leo, ili kuwapindua watu waliosimama katika Imani, na zinatenda kazi kwa udanganyifu wa hali ya juu kiasi kwamba ni ngumu kuzigundua. Katikati ya Huduma hizi ndipo kiti cha enzi cha shetani kilipo,(Ufunuo 2:13-14).

Wana wa Israeli walipokuwa kule jangwani wapo waliotii mafundisho ya Kora, ndio walioangamizwa naye, wapo pia waliousikiliza udanganyifu wa Balaamu nao pia wakaangamizwa, kadhalika katika kanisa wapo watakaopotea kwa kudanganywa na kwa kuyafuata mafundisho yatokayo kwa wachungaji wa uongo, mitume wa uongo, waalimu na manabii wa uongo, Huu ni wakati wa kuwa makini sana. Na utajuaje! kuwa hawa ni watumishi wa uongo? ni pale wanapoenda mbali na Neno, mfano wa Kora na Balaamu.

Biblia inasema katika ule mstari wa 18 “…….Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu”.

Jambo lingine  linalo tutambulisha kuwa tunaishi siku za mwisho, ni kutokea kwa watu wenye kudhihaki, na hawa hawatoki mbali! bali ni ndani ya kundi linalojiita kundi lililopo safarini, kumbuka waliomdhihaki Mungu ni Kora na wenzake baada ya kuona kuwa safari imekuwa ndefu, yenye shida, ambayo ingepasa ichukue wiki kadhaa tu kumaliza lakini imechukua miaka 40, wakaanza kudhihaki na kusema hiyo nchi tuliyoahidiwa mbona hatufiki hata sisi tunaweza tukajiongoza wenyewe??. Mfano huo huo wa baadhi ya watu wanaojiita wakristo, utasikia wanasema “Unakuja umekuwa YESU?“…”Yesu mbona haji?”.n.k. na cha kusikitisha huyu ni mtu anayejiita mkristo ndio anafanya hivyo, hawaogopi hata kulitamka hilo jina lililo kuu, katika mambo yao ya kipumbavu. Moja kwa moja utafahamu watu  kama hao wameshaanguka katika maasi ya Kora, na wala hawapo katika Imani japo wanajiita wakristo.

Mtume Petro pia alisema.

2Petro 3:1 “Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,

2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.

3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,

4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.

5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;

6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?

13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.

15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;”

Unaona hapo?. Uvumilivu wake Mungu ni kutuvuta sisi tutubu dhambi zetu, Lakini siku ya BWANA inakuja, inayotisha sana, kuwatekeza watu wote waasi, walioacha enzi yao. Wakati huo Bwana atakuja na watakatifu wake maelfu elfu, hao watakuwa ni wale waliokwisha nyakuliwa kabla, ndio watakaorudi na Bwana kuuhukumu ulimwengu wote, Kama HENOKO yule mtu wa 7 aliyenyakuliwa alivyoonyeshwa.(Ufunuo 19:11-20)

Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.”

Ndugu huu ni wakati wa kufanya wito wako, na uteule wako imara(2Petro 1:10), angali upo safarini, Sio wakati wa kutanga tanga huku na kule, kila wimbi la mafundisho unapokea..Unaweza ukaona mafundisho fulani ni mazuri yanavutia na kukupa faraja, lakini hujui kidogo kidogo yanakutoa katika njia ya IMANI,..Hapo mwanzoni ulikuwa unasali, ulikuwa unafunga, ulikuwa unawasaidia watu, ulikuwa mnyenyekevu,ulikuwa na huruma, ulikuwa unaogopa hata kuvaa mavazi ya aibu na kutembea nayo barabarani, ulikuwa ukisikia Neno la Mungu tu, unatetemeka lakini baada ya kufika sehemu fulani! na kusikia mahubiri fulani tu! kutoka kwa watumishi fulani, kuanzia hapo  hayo  mambo yote yakafa kabisa,Yesu kwako amekuwa kama kitu cha ziada, hana sehemu kubwa katika maisha yako kama zamani, hata ule uwepo wa ki-Mungu uliokuwa unausikia kwanza umetoweka, hamu ya kutamani mambo ya mbinguni imekufa. fahamu tu hapo umeiacha imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu! geuka haraka. kwasababu hapo ulipo ndipo penye kiti cha enzi cha shetani alipo Balaamu na Kora. Hivyo ondoka haraka sana, Rudi katika imani,..Ishindanie hiyo kwasababu shetani ndiyo anayoiwinda.

Tafuta uhusiano wako binafsi na Mungu, kwa kudumu katika maonyo ya biblia, Na BWANA ni mwaminifu safari aliyeianzisha mioyoni mwetu ataitimiliza..kama alivyosema.

Yuda 1: 24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;

25 Yeye aliye MUNGU PEKEE, MWOKOZI WETU, KWA YESU KRISTO BWANA WETU; UTUKUFU UNA YEYE, NA UKUU, NA UWEZO, NA NGUVU,TANGU MILELE, NA SASA, NA HATA MILELE. AMINA.

Mungu akubariki sana.

Unaweza pia uka-Share kwa wengine, mafundisho haya, ili nao pia wanufaike, na Mungu atakubariki.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

UPEPO WA ROHO.

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

NAPENDA KUJUA MAANA NA TOFAUTI KATI YA MYUNANI, MFARISAYO NA MSADUKAYO.

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Yuda, leo tukiendelea na sehemu ya pili. Kama tulivyokwisha kuona ile sehemu ya kwanza, Yuda mtumwa wa BWANA, alitoa angalizo na maonyo kwa watu wa Mungu kwamba waishindanie imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu, na kwamba maonyo hayo hawakupewa watu wote (yaani watu waovu na wema), hapana bali waraka ule uliandikwa kwa watu wa Mungu tu walioitwa peke yao (yaani wakristo). Hivyo ni vizuri ukafahamu hilo unapokisoma hichi kitabu,tukiendelea na mistari inayofuata tunasoma..;

“Yuda 1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

8 Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, HUUTIA MWILI UCHAFU, HUKATAA KUTAWALIWA, NA KUYATUKANA MATUKUFU.

9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

10 Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.

11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika NJIA YA KAINI, na KULIFUATA KOSA LA BALAAMU pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika MAASI YA KORA.

12 Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa;

13 ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao WEUSI WA GIZA ndio akiba yao waliowekewa milele”.

Kama ukichunguza watu hawa ambao Yuda anawazungumzia, ambao wanakataa kutawaliwa, wanaoenenda kwa kufuata mambo ya mwili, na wanaotukana matukufu, watu wanaofananishwa na nyota zinazotea ambao weusi wa giza ni sehemu yao waliowekewa milele, wanaonena maneno makuu magumu wasiyoyajua, Utaona kuwa Yuda amewapata kutoka katikati ya hawa watu watatu (yaani KAINI, BALAAMU na KORA). Kuna kitu kikubwa cha ajabu katikakati ya hawa watu.

Sasa tuwatazame ni kwa namna gani wamefananishwa na mawingu yasiyokuwa na maji, yachukuliwayo na upepo, na miamba ya hatari, na miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung’olewa kabisa; Kumbuka hawa watu wanaozungumziwa ni watu waliopo katikati ya kundi la Mungu waliojiingiza kwa siri.

NJIA YA KAINI;

Kumbuka Kaini hakuwa wa uzao wa Adamu kwa asili tangu mwanzo bali wa nyoka. Na nyoka kabla hajalaaniwa alikuwa hatembei kwa matumbo,bali alisimama wima kama mtu na alikuwa anazungumza kama mtu, ni kiumbe kilichokuwa karibu sana kufanana na mwanadamu, alikuja kuwa reptilia (nyoka tunayemwona sasa) baada ya kulaaniwa. Lakini Habili ndiye aliyekuwa mwana halisi wa Adamu, na uzao wake baada yake ndio ulioitwa “WANA WA MUNGU”, na uzao wa Kaini baada yake uliitwa “WANA WA BINADAMU “,

Na kama tunavyosoma tabia zote zilizokuwa kwa Kaini na uzao wake hazikutoka kwa Mungu, mfano tabia ya uuaji, alimuua ndugu yake kwasababu ya wivu, na ukichunguza uzao wake baada yake ulikuwa na tabia hiyo hiyo, mtoto wake Lameki alisema kama Bwana akimlipa Kaini kisasi mara 7 hakika Lameki atalipwa mara 77, sasa unaweza ukaona jinsi huyu mtu alivyokuwa muuaji kushinda hata baba yake.(Mwanzo 4:23), Ikiwa na maana kuwa kama baba yake aliweza kumuua mwenye haki mmoja (Habili), basi yeye ataua wenye haki 77.

Kadhalika tabia ya kuoa wake wengi ilianzia katika uzao wa Kaini, Ukisoma utaona huyu Lameki alikuwa na wake wawili jambo ambalo Mungu hakuliagiza. Lakini uzao wa Adamu (ambao ndio wana wa Mungu), walikuwa ni watu wanaomcha Mungu na kuutafuta uso wa Mungu siku zote soma(Mwanzo 4:25). Lakini agenda ya shetani siku zote ni kuwatafuta watu wa Mungu, na sio watu wa ulimwengu kwasababu hao tayari alishawapata. Na njia pekee anayoweza kutumia ni kuwakosesha wao na Mungu wao. Ili Mungu mwenyewe aamue kuwaangamiza, na ndio maana tunasoma katika mwanzo 6 utaona wana wa Mungu(yaani uzao wa Adamu) waliwatamani binti za binadamu (yaani uzao wa kaini) ambao ulikuwa ni mwovu, na kwenda kuwaoa na kusababisha kitendo cha kuchanganyika kwa mbegu. Hilo ndio likawa jambo pekee lililosababisha Mungu kuleta gharika kwa kuona mbegu takatifu imeharibika. Tunaona hapo japokuwa ulimwengu ulikuwa ni mwovu lakini hasira hasaa ya Mungu iliwaka juu ya wana wa Mungu kutoilinda enzi yao. Kumbuka “wana wa Mungu” kama wanavyozungumziwa pale sio malaika, kwasababu malaika hawazai wala hawazaliani. Na Mungu angewaadhibu malaika ingekuwa ndio wao waliozini, lakini badala yake waliadhibiwa wanadamu. Hivyo wana wa Mungu wanaozungumziwa pale ni wana wa uzao wa Adamu.

Ndio jambo linaloendelea leo katikati ya watu wanaojiita wakristo, shetani akishagundua upo katika mstari wa Imani, hali akijua wewe ni mzao mteule wa Mungu, atakuja kwa NJIA YA KAINI. Atakuletea jamii ya Viongozi wa Dini/Imani mfano wa Kaini, atakuletea wahubiri watakaokuhubiria kuoa wake wengi ni sawa watatumia Biblia kukuhakikishia jambo hilo, watakufundisha kuoa/kuolewa na mwanamke yeyote ni sawa tu! kumbuka hiyo ni njia mwovu siku zote wale binti wa Kaini ndio waliowakosesha wana wa Mungu, na ndio waliomkosesha pia na Sulemani,.Watakuhubiria kunywa pombe ni sawa biblia inaruhusu, watakufundisha Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo, hivyo hata ukivaa kimini na suruali na kupaka rangi usoni ni sawa….Na wewe hujui kwamba shetani ameshakumaliza..kukukosesha wewe na Mungu umeishindwa kuilinda enzi na IMANI yako uliyokabidhiwa mara moja tu! kwa kutokudumu katika maagizo yake, jambo litakalokutokea ni kuwekwa katika vifungo vya giza, kama watu wa Nuhu walivyofanywa na wale malaika walioasi..Na Bwana Yesu alisema kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu…….

KOSA LA BALAAMU:

Kama wewe ni mwanafunzi wa biblia utajua kabisa Balaamu alikuwa ni nabii lakini sio mwisraeli, Alikuwa ni nabii na bado alikuwa ni mchawi vile vile biblia inasema hivyo! sasa unaweza ukauliza je! Mtu anaweza akawa ni mchawi na bado akawa ni nabii?? JIBU NI NDIO!! (soma Kumbukumbu 13),ni nabii kabisa na anapokea mafunuo kutoka kwa Mungu lakini alikuwa ni mchawi. Sasa wakati wana wa Israeli walipokuwa jangwani wanakaribia kupita katika nchi ya Moabu, yule Balaki mfalme wa Moabu aliwazuia wasikatize katika nchi yao. Hivyo Wamoabu wakaongezea kwa kumuajiri Balaamu aje kuwalaania(kuwaloga) wana wa Israeli. Lakini Mungu alimwoonya asifanye hivyo, kama alivyomwonya Kaini tu, lakini kwasababu ni mtu aliyependa fedha, akatafuta njia mbadala ya kuwakosesha watu wa Mungu.

Ndipo akaja na wazo jipya la kishetani zaidi, kama lile linalofanana na uzao wa Kaini, Akamwambia Balaki mfalme wa Moabu watu hawa (Waisraeli) hawalaaniki kwa namna yoyote isipokuwa kwa njia ya kuwakosesha wao na Mungu wao. Na njia pekee ni kuwaalika na kuwapa binti zenu wale walio wazuri wakaolewe na wana wao, ili watoe sadaka kwa miungu yao, na kufanya karamu za anasa, kitu ambacho Mungu wao amewakataza wasifanye. Na baada ya hapo Mungu wao atakasirishwa nao na kuwaangamiza. Na kweli njama zao zilifanikiwa baada ya kitendo kile walidondoka waisraeli elfu 24, (Hesabu 22-25).

Unaona hapo balaamu ni aina ya wahubiri wa uongo waliopo duniani sasa, ni kweli wanaweza wakawa na karama za kinabii,wanaona maono saa nyingine wanakutabiria jambo na linatimia, lakini kumbe ni wachawi walioajiriwa na shetani kuwaharibu watu waliosimama katika imani. Agenda yao kubwa ni kwa wakristo wa kweli waliosimama. Mafundisho yao yanakupeleka moja kwa moja kufanya uzinzi wa kiroho,(Kumchanganya Mungu na ibada za sanamu), watakuhubiria ibada za miungu mingi, kuwaomba watakatifu waliokufa zamani na walio hai, watakufundisha kuna nafasi ya pili baada ya kifo, watakufundisha hakuna kuzimu, n.k na wengine wanakutabiria na inatokea..

Na ndio maana Bwana alisema katika 

Ufunuo 2: 13 Napajua ukaapo, NDIPO PENYE KITI CHA ENZI CHA SHETANI; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu WASHIKAO MAFUNDISHO YA BALAAMU, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa SADAKA KWA SANAMU, NA KUZINI.

15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Umeona hapo Bwana anazungumza na watu ambao wameishikilia IMANI, na akawaonya watubu watu wote wanaoshikilia mafundisho ya balaamu. Hivyo ndugu umeona kiti cha enzi cha shetani kilipo?? Hakipo freemason, kipo kwenye dini na mafundisho yote ya uongo katikati ya kanisa la Mungu. Hivyo kama unayashikilia toka huko, vinginevyo Bwana anasema atakuja kufanya vita na wewe kwa huo upanga wake.

MAASI YA KORA:

Kora naye alikuwa ni nabii kama Balaamu isipokuwa huyu sasa anatoka katikati ya wana wa Israeli tena katika uzao wa kikuhani (wana wa Lawi),alikuwa ni kuhani naye pia aliaminiwa na kupewa heshima kubwa katikati ya umati wa wana wa Israeli, Lakini aliinuka moyo na kuona kuwa MAMLAKA iliyowekwa na Mungu haistahili kuwaongoza, akaidharau TORATI ya Mungu na mtumishi wake, na kupeleka mashtaka juu ya mtu wa Mungu Musa,na kutoa maneno makuu ya kufuru, sasa kilichotokea alikusanya watu na kutaka kuwaundia MAMLAKA yake mwenyewe na kuwaongoza katika nchi yake ya ahadi anayoijua yeye. Lakini tunasoma mwisho wa siku ardhi ilipasuka na kummeza yeye pamoja na wafuasi wake wote waliomfuata (Hesabu 16).

Hii inafunua nini? Kora ni mfano wa viongozi wa dini wanaokataa MAMLAKA KUU, wanaokataa kutawaliwa na katiba maalumu ambayo Mungu kaiweka ambayo ni BIBLIA TAKATIFU. Wanayapinga yaliyoandikwa huko kwa faida zao wenyewe, Kama vile Kora, alivyoikinai njia Mungu aliyoiweka ya kupita nyikani, vivyo hivyo wahubiri hawa wataipinga njia ya msalaba kwa mafundisho yao,..hawawafundishi watu watubu, wajitwike misalaba yao wamfuate YESU, badala yake watawafundisha watu wajitwike mabunda ya pesa wamfuate Yesu ndio uthibitisho kwamba wanaelekea kaanani. Kumbuka Kora alikuwa anaona kama vile Musa anawatesa jangwani, wanapitia shida, na taabu, hiyo siyo njia ya Mungu..Vivyo hivyo na hawa wanapoona Watoto wa Mungu wanapitia magumu katika Imani zao wanakuja kuwavunja moyo na kuwafundisha,waache uongozi wa njia ya Mungu aliyoiweka, na wafuate uongozi wa kibinadamu.

Kora mahubiri yake yalikuwa ni kuwafariji kuwa wote ni watakatifu(Hesabu 16:3). Vivyo hivyo na hawa mafundisho yao ni kuwafariji watu na kuwaambia yote ni sawa, nyie ni watakatifu hata ukiishi maisha ya kawaida tu, utaenda mbinguni wewe bado ni mtakatifu kwanini kujiumiza kuishi maisha ya kilokole?.

Hivyo tukishafahamu tabia za hawa watu katikati ya kundi la Mungu, tunaonywa tujiepushe nao kwasababu ni nyota zipoteazo.

Biblia imerudia kuelezea habari hii ya kitabu cha Yuda katika kitabu cha 2Petro 2 soma kwa utaratibu itakusaidia sana kulinganisha yote mawili.

Inasema..

Mlango 2:1 “Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.

2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.

3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.

4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;

5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;

6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;

7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;

8 maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;

9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;

10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.

11 Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana.

12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;

14 wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;

15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;

16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.17 Hawa ni visimavisivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.

18 Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;

19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.

20 Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.

Hivyo ndugu, Kanisa tunaloishi ni la hatari sana, je! umeufanya imara wito wako na uteule wako?. Unaishindania imani?. Kama hujatubu dhambi zako fanya hivyo sasa.

Mungu akubariki.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Mada Nyinginezo:

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).

UZAO WA NYOKA.

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA.

UFUNUO: MLANGO WA 1

Biblia inamaanisha nini kusema Yeye aliye na sikio, na asikie?


Rudi Nyumbani:

Print this post

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Karibu katika kujifunza NENO la Mungu, leo tukikiangalia kitabu cha Yuda, kilichojaa maonyo makubwa kwa kanisa la leo. Yuda aliyeandika kitabu hichi sio Yule Yuda mwanafunzi wake YESU au yule aliyemsaliti hapana, bali ni Yuda yule aliyekuwa ndugu yake Bwana Yesu kwa kuzaliwa(Marko 6:3). Hivyo kwa uongozo wa Roho Mtakatifu aliuandika waraka huu mfupi kwa WATU WALIOITWA TU!! (yaani wakristo) na sio watu wote wa ulimwengu ambao sio wakristo, Leo tutasoma mstari wa 1-6″, Bwana akitupa neema tutaendelea na mistari inayofuata katika sehemu ya pili na ya tatu.

Biblia inasema…

Mlango 1:1-6″ Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, KWA HAO WALIOITWA, WALIOPENDWA, katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo.

2 Mwongezewe rehema na amani na upendano.

3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ILI NIWAONYE KWAMBA MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU.

4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI.

6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, AMEWAWEKA KATIKA VIFUNGO VYA MILELE CHINI YA GIZA KWA HUKUMU YA SIKU ILE KUU”.

Kama tulivyotangulia kusema waraka huu uliandikwa kwa watu walioitwa peke yao, yaani watu waliokwisha kumwamini Bwana Yesu Kristo, Ikiwa na maana wakristo wote (mimi na wewe). Hivyo tunaposoma maandiko haya tufahamu kuwa maonyo haya yanatuhusu sisi tunaojiona kuwa tupo katika IMANI na kwa namna moja au nyingine haziwahusu watu ambao wapo nje ya ukristo. Kwahiyo unaposoma usilichukulie kiwepesi wepesi na ndio maana Yuda alianza na kusema “Napenda kuwakumbusha ijapokuwa mmeyajua haya yote.” Kwahiyo inawezekana umeyajua, lakini unakumbushwa tena.

Sasa Tukisoma ule mstari wa 3 anasema 

“Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ILI NIWAONYE KWAMBA MWISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU. “

Umeona hapo anazungumza juu ya IMANI waliyopewa watakatifu, ambayo wamepewa mara moja tu! na kama ni mara moja inapaswa ishindaniwe kwa bidii na kushikiliwa kwa maana ikidondoka tu! hakutakuwa na nafasi ya pili ya kuipata tena. Huo ndio msisitizo mkubwa hapo.

Na kushindania Imani ni nini?. Ni kudumu katika kile ambacho umekiamini na kujiangalia usianguke, Na ndio maana ukiendelea kusoma Yuda aliuchukua mfano wa Wana wa Israeli akifananisha na safari ya wakristo (yaani walioitwa), alisema, ” Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, ALIWAANGAMIZA BAADAYE WALE WASIOAMINI. “

 

Sasa tukichunguza habari ya wana wa Israeli, tunaona wote waliokolewa kweli, wote walibatizwa, wote walikuwa wanashiriki baraka zote za rohoni, wote walikuwa chini ya Neema, wote walikula chakula cha Bwana n.k. lakini “WENGI” wa hao Mungu hakupendezwa nao na kuangamizwa jangwani, kumbuka sio wachache bali ni “WENGI”. Kama tunavyosoma katika biblia.

1Wakoritho 10:1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

3 wote wakala chakula kile kile cha roho;

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

5 LAKINI WENGI SANA KATIKA WAO, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.

6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.

7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.

8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.

9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.

10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.

11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Umeona hapo biblia inasema mambo hayo yameandikwa ili kutuonya sisi, Wana wa Israeli ni mfano wa wakristo wote ulimwenguni, ambao kwa pamoja tulipoamini tulitoka Misri na siku tulipobatizwa tulivuka bahari ya Shamu. Lakini huo ndio ulikuwa mwanzo wa safari yetu sio kwamba ndio tumefika, la! bali kuanzia hapo ndio IMANI INAANZA KUSHINDANIWA.

Kama tunavyosoma katika maandiko waliofika Kaanani, ni wawili tu kati ya mamilioni ya watu waliotoka Misri, Kadhalika na kanisa la siku za mwisho, japo kuna mamilioni ya watu wanaojiita wakristo na wameokoka, na wamebatizwa kweli katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa, wanaoupako, wanaona kabisa wakibarikiwa na Mungu katika mambo yao yote (huko ndiko kula mana kwenyewe kutoka mbinguni), wananena kwa lugha, wanatenda miujiza, wanayajua maandiko, n.k. lakini biblia imetabiri katika siku za mwisho watakaofika ng’ambo ya pili ni wachache sana kwasababu walioitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache. Lakini ni sababu ipi itakayowafanya watu wengi washindwe kuilinda imani, ni kwasababu kama hizo hizo tu za wana wa Israeli.

Tuzitazame:

> Ibada za sanamu: Wana wa Israeli walitengeneza sanamu za dhahabu wakiwa katikati ya safari yao ya Imani na kuanza kuziabudu, Hivyo Mungu akakasirishwa nao kuliko hata watu wa mataifa, ikapelekea kufanya dhambi isiyosameheka, mfano halisi wa leo mkristo upo safarini, Unafahamu kuwa ibada za sanamu, kuabudu picha au sanamu za watakatifu fulani waliokufa zamani angali unajua kufanya hivyo ni dhambi. Kuna hatari kubwa mno ya kuangamizwa na Mungu mwenyewe.

Sababu nyingine ni Uasherati: Wana wa Israeli walifika mahali wakasahau maagizo ya Mungu na kuanza kuzini na wanawake wa kimataifa: Kadhalika na watu wanaojiita wakristo kuzini au kufanya uasherati nje ya ndoa takatifu, pamoja na kuvaa mavazi ya kikahaba yanayowasababishia wengine kutenda dhambi za uzinzi nafsini mwao vile vile ni kujiangamiza mwenyewe, ipo hatari kubwa ya kuondolewa kabisa katika neema.

> Manung’uniko: Hili nalo liliwafanya wana wa Israeli wakataliwe na Mungu, japo ni kweli waliitwa na Mungu mwenyewe na kubatizwa lakini manung’uniko yalifamfanya Mungu achukizwe nao. Ni mfano halisi wa sasa wakristo wengi wanapopitia na mitikisiko kidogo tu, wanasahau fadhili zote Mungu alizowatendea nyuma. Pengine anapitia misiba, anaanza kutoa maneno ya makufuru, anapitia, kuugua kidogo anaanza kulaumu Mungu kamuacha, mtu kapungukiwa kidogo tu! anaanza kunung’unika moyoni mwake anasahau kuwa miaka mingine nyuma Mungu alikuwa anamfanikisha n.k.. Sasa mambo kama hayo ndio yanayosababisha safari kuwa fupi…Biblia inasema atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka..Safari ya ukristo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

Pia tabia ya kutamani mabaya na kumjaribu Mungu. Ni kikwazo kingine kilichowafanya wengi wa wana wa Israeli wasimalize safari yao. Kwa mfano Mungu aliwakusudia wale mana tu! mpaka wakati watakapoingia nchi ya ahadi, wao wakawa wanataka nyama tena kwa njia ya kumjaribu, wakijua kabisa Bwana anaweza kufanya hivyo. Vivyo hivyo watu wa leo Hawataki kuridhika katika njia Mungu aliowakusudia wapitie, wanataka wakiwa wakristo bado wafanane na watu wa kidunia, wanaenda kanisani leo kesho wanaenda disko, wanaongea vizuri leo kesho wanatukana n.k. Hizi zote ni sababu kubwa zinazokwamisha safari. Ni heri mtu kama huyo asingeanza safari kabisa, kuliko kuingia na kufanya machukizo, maana nafasi ya pili haipo kwasababu IMANI INAKABIDHIWA MARA MOJA TU.

Na ndio maana tukiendelea kusoma tunaona Yuda aliwafananisha watu hawa na watu WALIOJIINGIZA KWA SIRI katikati ya kundi la Mungu, ni magugu katikati ya ngano, Alisema;

” 4 Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

5 Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.

6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu “

Hivyo mtu yeyote anayefanya hayo na bado anajiita mkristo ni sawa na mtu aliyejiingiza kwa siri katikati ya kundi la Mungu mfano wa akina Kora, na dathani katikati ya wana wa Israeli ambao walishaandikiwa hukumu yao tangu zamani. Na biblia imewafanisha hawa na wale malaika walioasi (Shetani na malaika zake), ambao hawakuilinda enzi yao. sasa hivi wamefungwa katika vifungo vya giza wakisubiria ile hukumu ya siku ile watakapotupwa wote kwa pamoja katika lile ziwa la moto. Katika kanisa la kwanza walikuwepo watu waliojiingiza kwa siri, na hata sasa wapo wengi.

Hivyo ndugu kwanini unaendelea kuichezea au kuichukulia Imani yako juu juu, kumbuka upo safarini na imani umekabidhiwa mara moja tu, na wanaomuudhi na wanaompendeza Mungu siku zote huwa ni wale walio safarini na sio wasiomjua Mungu, hao Mungu atawahukumu mwenyewe siku ya mwisho. Na ndio maana anasema ni heri uwe moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu. Hatari kubwa ipo kwako wewe uliye mkristo vuguvugu, usipoilinda ENZI YAKO, na KUISHINDANIA IMANI utafananishwa na wale malaika walioasi ambao wameandaliwa ziwa la moto.

Huu ni wakati wa KUTUBU na kufanya IMARA WITO WAKO, NA UTEULE WAKO. Tunaishi katika siku za mwisho na Bwana yupo karibu kuja, Je! utaenda nae?.

Mungu akubariki.

Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

Mada Nyinginezo:

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

NGUVU YA UPOTEVU.

MTI UANGUKAPO, PAPO HAPO UTALALA.

EPUKA MUHURI WA SHETANI.

JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

YONA: Mlango wa 4

Bwana wetu YESU KRISTO atukuzwe.

Tunamshukuru Mungu kwa kutupa neema hii mpya ya kujifunza Neno lake. Leo tukiwa ukingoni kabisa wa kitabu cha Yona ile sura ya nne. Kama tulivyojifunza katika sura zilizotangulia, Nabii Yona anawakilisha kundi la wakristo pamoja na wahubiri walio vuguvugu wa Imani biblia inawaita wanawali wapumbavu, ambao walipaswa kuingia na Bwana wao katika karamu lakini kwasababu Taa zao hazikuwa na mafuta ya ziada wakaachwa. Kwasababu walikisia tu kwamba yale mafuta yaliyokuwa katika taa zao yangewatosha mpaka wakati wa Bwana wao kuja (Mathayo 25). Ni Mfano dhahiri wa wakristo wa kanisa hili la mwisho la Laodikia.

Na kiini cha sura hii ya mwisho tunaona ni Yona kutoa SABABU YA YEYE KUTOKWENDA NINAWI. Na haya yote tunayaona ni baada ya Bwana kughahiri mabaya yote aliyokuwa ameyakusudia kuyaleta juu ya Mji wa Ninawi, baada ya kuona kuwa matendo yao yamebadilika na kutubu, Tunasoma:

Yona 4

“1 Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika.

2 Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? HII NDIYO SABABU NALIFANYA HARAKA KUKIMBILIA TARSHISHI; KWA MAANA NALIJUA YA KUWA WEWE U MUNGU MWENYE NEEMA, UMEJAA HURUMA, SI MWEPESI WA HASIRA, U MWINGI WA REHEMA, NAWE WAGHAHIRI MABAYA.

3 Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.

4 Naye Bwana akasema, Je! Unatenda vema kukasirika?

5 Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje.

6 Na Bwana Mungu aliweka tayari mtango, akaufanya ukue juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumponya katika hali yake mbaya. Basi Yona akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango.

7 Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akaweka tayari buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakatika.

8 Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.

9 Mungu akamwambia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.

10 Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;

11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”

Kama tunavyosoma maandiko hapo juu, sababu pekee iliyomfanya YONA akaidi njia za Mungu, ni kumkadiria Mungu kwamba yeye anaweza yote, Yona alimsoma Mungu kwa muda mrefu akaona jinsi alivyokuwa analirehemu taifa la Israeli pindi walipokuwa wanamuudhi sana Mungu, na kutaka kuangamizwa lakini Mungu alikuwa akighahiri mabaya yote. Hata wakati Yona alipokuwa anaishi katika Taifa lake, uovu wa wana wa Israeli ulikuwa ni mwingi sana, lakini Bwana alikuwa akiwahurumia kwa kuwatumia manabii wake kuwaonya watubu. Hivyo Yona kwa kuyajua hayo yote, Neno la Mungu lilipomjia na kuambiwa aende Ninawi kawahubiria watu watubu vinginevyo wataangamizwa, yeye akajisema ndani ya moyo wake, ..’aa Mungu najua siku zote ni wa rehema, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa huruma, huwa anaghahiri mabaya, ni mwema, anatupenda sana. mwisho wa siku atasamehe tu!.Yona hakuona sababu ya kwenda kuwapa watu presha, wakati mwisho wa siku anajua wataponywa tu! Mungu ni mwingi wa rehema. Hivyo Yona kwa kulijua hilo akalifanya lile Neno kuwa jepesi sana, na kuendelea na mambo yake mwenyewe, na kama tunavyosoma habari yakamkuta mabaya yale pale alipopitia dhiki isiyokuwa ya kawaida tumboni mwa samaki siku tatu usiku na mchana….

Ndivyo ilivyo kwa wahubiri wa leo na wakristo walio vuguvugu, Wahubiri wengi mwanzoni walitumwa na Mungu kweli wawahubirie watu habari za TOBA, na kwamba wamgeukie Mungu na kuacha njia zao mbaya kwasababu hukumu ya Mungu inakuja. Lakini wengi wamegeuka sasa wanawahubiria watu mahubiri ya faraja angali wanajua kabisa Hakuna amani kwa mtu ambaye hajatubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi zake na kujazwa Roho Mtakatifu, Mahubiri yao siku zote ni …”Mungu ni wa rehema”…”Yote ni mema, “Haijalishi”..”Mungu ni Mungu wa upendo” “Hawezi kuteketeza dunia leo wala kesho,… tunaishi chini ya neema”..”Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo”n.k.

Wahubiri hawa kiini cha mafundisho yao ni faraja na mafanikio ya ulimwengu huu tu!..TOBA inatupiliwa nyuma kama kitu kisichokuwa na umuhimu sana. kwamba kwao laana kubwa ni mtu ambaye hajafanikiwa kimaisha, na sio mtu ambaye hajatubu dhambi zake. Lakini hawakusoma kwamba Neno la kwanza Yohana mbatizaji alilohubiri katika huduma yake ni TOBA, pia Hubiri la kwanza lililotoka katika kinywa cha Bwana wetu YESU KRISTO ni TUBUNI! kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Lakini wao neno lao la kwanza ni NJOO UPOKEE!!.. Na kundi kubwa la wakristo limeungana na hawa watu hawajui kuwa wote kwa pamoja wanaelekea Tarshishi kwa NJIA YA BAHARI ambapo humo yumo yule mnyama atokaye baharini mwenye vichwa 7 na pembe 10 (Ufunuo 13&17) aliyewekwa tayari kuwameza, katika kile kipindi cha dhiki kuu. Wakati huo unyakuo wa Bibi-arusi wa kweli wa Kristo utakuwa umeshapita.

Lakini ni kwasababu gani watayapata hayo yote?. Ni kwasababu walikisia kuwa Mungu ni Mungu wa rehema, si mwepesi wa hasira, kwani kuna watoto wasiojua mema na mabaya, kuna wanyama, kuna mimea, n.k. Bwana hawezi kuangamiza vyote hivyo. Lakini ndugu nataka nikuambie Bwana anaweza kama alifanya kwa wakati wa Nuhu, na wakati wa Luthu atafanya pia katika siku za mwisho kama watu wasipotubu.

Kuna wakati kilele cha maovu ya Israeli kilifika na Bwana akakusudia Yuda kuchukuliwa utumwani (BABELI). Na Bwana alimtumia nabii Yeremia kutoa unabii huo kwa mfalme wa Israeli na wakuu wake, na kuwaambia baada ya siku ambazo si nyingi watachukuliwa mateka waende Babeli, lakini alizuka nabii mmoja anayeitwa HANANIA yeye alinyanyuka na kutabiri kuwa Bwana ameghahiri mabaya hawataenda tena utumwani zaidi ya yote vile vitu vyao vilivyochukuliwa kabla vitarudishwa. Hivyo Israeli wote wakafurahi na kustarehe na kufarijika sana, wakijua ni habari njema, kumbe hawajui Hanania hakutumwa na Mungu ni nabii wa uongo. Na baada ya miezi 2 Mungu alimuua kwa kuwatumainisha watu uongo.

Yeremia 28: 15 ” Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini UNAWATUMAINISHA WATU HAWA MANENO YA UONGO.

16 Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana.

17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.”

Hivyo ndugu usidanganyike na Injili za matumaini kana kwamba hakuna hukumu inayokuja mbeleni. Tunaishi katika siku za mwisho hizi, Bwana Yesu yupo mlangoni kurudi, wakati umeenda sana, ishi maisha ya TOBA, na utakatifu, jiepushe na ibada za sanamu, uasherati, ulevi, anasa, mavazi ya kikahaba, rushwa, usengenyaji n.k.(Waebrania 12:14) ubatizwe katika ubatizo sahihi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, ujazwe na Roho wa Mungu. Huko ndiko kufanikiwa kwa kwanza kwa mkristo ndipo mafanikio mengine ya mwilini yafuate.

Mungu akubariki sana.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Tafadhali share ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki!.


Mada Nyinginezo:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

DHAMBI YA MAUTI

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ATUMIE MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO LAKE, JE! TUNARUHUSIWA KUTUMIA POMBE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

YONA: Mlango wa 3

Bwana wetu YESU KRISTO ahimidiwe milele na milele. AMEN.

Karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tukiwa katika ile sura ya 3 ya kitabu cha Nabii Yona. Katika sura zilizotangulia tuliona jinsi taabu na dhiki alizopitia Yona zinafananishwa na dhiki watakazokuja kupitia wakristo waliovuguvugu (wanawali wapumbavu mathayo 25) watakaokosa unyakuo. Pia tuliona kama vile Yona alivyomezwa na Yule samaki mkubwa atokaye baharini na kukaa muda wa siku tatu katika lile tumbo, hawa nao watamezwa na Yule mnyama atokaye baharini mwenye vichwa 7 na pembe 10 (ambaye ni Mpinga-kristo na mfumo wake) kwa muda wa miaka mitatu na nusu katika ile dhiki kuu.(soma Ufunuo 13&17). Hivyo habari ya Yona ni unabii halisi wa mambo yatakayokuja kutokea mwishoni.

Lakini tukiendelea katika hii sura ya 3 tunasoma:

Yona 3 “Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,

2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.

3 Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.

4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, BAADA YA SIKU AROBAINI NINAWI UTAANGAMIZWA.

5 Basi watu wa Ninawi WAKAMSADIKI MUNGU; WAKATANGAZA KUFUNGA, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.

6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.

7 Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;

8 bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, NAWAGEUKE, kila mtu AKAACHA NJIA YAKE MBAYA, na udhalimu ulio mikononi mwake.

9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?

10 MUNGU AKAONA MATENDO YAO, YA KUWA WAMEIACHA NJIA YAO MBAYA. Basi BAADA YA SIKU AROBAINIneno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende”.

Kama tunavyosoma habari hii baada ya Yona kutapikwa na yule samaki, Bwana alimtuma tena kwa mara ya pili Ninawi akawahubirie watu habari za Toba na kwamba wasipotubu baada ya siku 40, Ninawi itaangamizwa. Lakini tunaona watu wale walitii sauti ya Mungu na kutubu.

Lakini ni kitu gani kilichowafanya watubu kirahisi rahisi hivyo?.

Kumbuka kwa wakati ule Ninawi haikuwa na tofauti sana na mji wa Sodoma au Gomora, kwasababu ilikuwa yote ni miji ya kimataifa, watu wasiozijua sheria za Mungu wa mbinguni, ni mataifa yaliyoabudu maelfu ya miungu, yaliyojaa maovu ya kila namna, hivyo ingekuwa ni ngumu sana mtu kujizukia asiye na kitu na asiyejulikana na kuanza kuhubiri habari za kuteketezwa mji wao na mahubiri ya kubadilisha mtindo wa maisha yao. Hivyo ilihitajika kitu kingine cha ziada kuwashawishi wale watu waamini kuwa ni Mungu kweli wa mbinguni anazungumza na wao.

Hivyo Bwana kwa kulijua hilo akaruhusu Yona kwa makusudi akae katika tumbo la samaki siku tatu usiku na mchana bila kufa, kabla ya kwenda Ninawi. Pengine wale watu wa Ninawi walimuuliza Yona ni Ishara gani aliyonayo ili wasadiki kwamba ametumwa na Mungu wa mbinguni?. Na Yona akawasimulia ushuhuda wa maisha yake kwa muda wa siku tatu katika ule mji. Na pia mashuhuda wa jambo hilo walikuwepo, ambao ni wale mabaharia waliosafiri na Yona, ambao ndio baadaye walikuja kumtupa baharini, pengine baadaye walimwona ng’ambo ya pili akihubiri na kuwathibitishia watu kwamba ni kweli alikaa tumboni mwa samaki siku tatu. ndipo watu wa Ninawi wakaogopa sana, na kuchukua hatua ya kulia na kuomboleza juu ya dhambi zao, hivyo wakageuka na kuacha njia zao mbaya.

Vivyo hivyo hukumu ya Mungu ilipokaribia ya kuuteketeza ulimwengu wote tena, kwamba baada ya kipindi kisichokuwa kirefu kutokana na maovu ya watu ghadhabu ya Mungu itamwagwa juu ya ulimwengu mzima kama watu wasipotubu, Hivyo Mungu kwa kuwa ni wa rehema alianza kutanguliza kwanza manabii wake kuhubiri habari za TOBA kwa watu wote ambapo hapo kabla zilikuwa hazihubiriwi kama kiini cha wokovu, ndipo tunamwona Yohana mbatizaji akiwaonya watu watubu kwasababu hukumu ya Mungu imekaribia. Kadhalika na mwisho ya yote akamtuma nabii mfano wa Yona, mwenye ishara kama ya Yona, yamkini watu wa ulimwengu wakiiona hiyo WATUBU kama walivyofanya watu wa Ninawi lakini wasipotubu hukumu ya Mungu inakuja juu yao.

Ndipo Mungu akamtuma mwanae mpendwa Bwana Yesu ambaye kiini cha ujumbe wake kilikuwa ni TOBA ilioambata na ISHARA KUU. Tunasoma katika Mathayo 12:38 mafarisayo walio mfano wa watu wa Ninawi walimuuliza kwa ishara gani unatuonyesha tuamini kuwa hiyo hukumu inayokuja unayoizungumzia ni kweli, ili tupate kutubu…Tunasoma:

“38 Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako.

39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.

40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.

41 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. “

Umeona hapo? hukumu ya huu ulimwengu ilishatamkwa siku nyingi, na Yona wetu ni Bwana Yesu Kristo kitendo cha kufa na kufufuka kwake haikuwa bure, baada ya kumaliza kazi yake hapa duniani angepaswa apae juu moja kwa moja kama Eliya au Henoko, lakini kizazi hichi kingesadiki vipi kama kisingepewa ISHARA KAMA HIYO?. Hivyo kitendo cha kufa kwake na kukaa siku tatu kaburini na kufufuka ni ishara tosha ya kumfanya kila mwanadamu atubu kwa kuvaa magunia na kuomboleza kama watu wa Ninawi na kuacha njia zake mbaya. Lakini Bwana Yesu alisikitika sana na kusema katika siku ya hukumu watu watakaokihukumu kizazi hiki watakuwa ni wale watu wa Ninawi, Jaribu kutafakari Yona hakufanya miujiza wala kuponya watu, zaidi ya ile ishara ya kumezwa na samaki lakini watu wa Ninawi walitubu, lakini sisi watu wa kizazi hiki tumeona Ishara nyingi za Yesu Kristo licha ya hiyo ya kufa na kufufuka kwake, kuna miujiza na uponyaji wa kiungu vinaambatana naye kila siku lakini bado watu hawataki kutubu. Alisema pia..

Mathayo 11: 20 “Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, KWA SABABU HAIKUTUBU.

21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, WANGALITUBU ZAMANI kwa kuvaa magunia na majivu.

22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.

24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.

Na kumbuka pia watu wa Ninawi walipewa muda wa kutubu, nao ni siku 40, na si zaidi, baada ya hapo hakuna tena wokovu ghadhabu ikishamiminwa hakuna tena Toba. Vivyo hivyo na sisi tumewekewa muda wa kutubu, sio kila siku tutaliliwa Tubu! tubu! hapana, kuna muda utafika mlango wa neema utakuwa umefungwa, pale Bwana Yesu atakaposimama na kuufunga mlango.

Luka 13: 23 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, EE BWANA, TUFUNGULIE; yeye atajibu na kuwaambia, SIWAJUI MTOKAKO;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.

28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.

Ndugu huu ulimwengu unakaribia kutimiza 40 zake, na dalili zote zinaonyeshwa huu ni wakati wa siku za mwisho, utafika wakati hutaisikia tena injili ya Toba, na hata ukisikia haitakufaidia chochote kilichobaki kwako ni siku ile ya hukumu kusimama mbele ya watu wa Ninawi wakikuhukumu kwanini hukutubu kwa Ishara kuu kama hizi, na zaidi ya yote utakutana na watu wa sodoma na Gomora nao pia watakuhukumu kwamba umestahili adhabu kubwa kuliko wao kwa kuwa uliona ishara nyingi na miujiza mingi kuliko wao na bado haukutubu. Siku hiyo yatakuwa ni maombolezo na majuto kiasi gani.Na siku hiyo inakaribia.

 

TUBU leo ndugu angali muda upo kumbuka Kutubu maana yake ni KUGEUKA na kuacha njia mbaya, sio kusali sala ya toba tu, halafu basi, ndio maana tunasoma pale Mungu aliyatazama MATENDO ya watu wa Ninawi kama kweli wamegeuka au la!! . na sio maombolezo yao peke yake na alipoona matendo yao wamegeuka alighahiri mabaya yale.,Na wewe fanya vivyo hivyo, Kristo bado hajaja, ila hivi karibuni anakuja kumnyakua yule aliyekuwa tayari kwenda nae.

Mungu akubariki.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> YONA: Mlango wa 4


Mada Nyinginezo:

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

CHUKIZO LA UHARIBIFU

SAUTI NYUMA YA ISHARA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?


Rudi Nyumbani:

Print this post

YONA: Mlango wa 2

Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe.

Karibu katika mwendelezo wetu wa kitabu cha nabii Yona. Tukiwa katika sura ya pili, tulishaona katika sura iliyopita jinsi Yona alivyojitenga na mapenzi ya Mungu kwa kukataa kwenda katika njia zake, na kujikuta akingukia mambo mabaya badala ya mema kwa kumezwa na yule nyangumi mkubwa, na tukaona kuwa habari hiyo inafunua siri ya kanisa la Kristo katika wakati wa siku hizi za mwisho, kwa wale wakristo vuguvugu wa kanisa la mwisho la Laodikia ambalo ndilo tunaloliishi kuwa wataangukia katika tumbo la yule mnyama anayezungumziwa katika (Ufunuo 13&17) hapo itakuwa ni baada ya unyakuo kupita ambacho ndicho kile kipindi cha Dhiki kuu kitakachodumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu ya mwisho.

Lakini tunaona katika sura hii ya pili baada ya Nabii Yona kumezwa, kilichofuata akiwa ndani ya lile tumbo la samaki ilikuwa ni mapambano akiishindania NAFSI yake, isiteketee kabisa ndani ya lile tumbo la yule samaki, tunasoma Yona alipitia kipindi kilichokuwa kifupi lakini kigumu sana, kiasi kwamba kilimfanya awe katika MAJUTO makubwa sana, na MAOMBOLEZO yasiyoelezeka… Tusome.

Mlango wa 2

1 Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

2 Akasema, Nalimlilia Bwana KWASABABU YA SHIDA YANGU, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu NALIOMBA, Nawe ukasikia sauti yangu.

3 Maana ULINITUPA VILINDINI, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; MWANI ulikizinga kichwa changu;

6 NALISHUKA HATA PANDE ZA CHINI ZA MILIMA; HIYO NCHI NA MAPINGO YAKE YALINIFUNGA HATA MILELE; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,

7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nalimkumbuka Bwana; Maombi yangu yakakuwasilia, Katika hekalu lako takatifu.

8 WATU WAANGALIAO MAMBO YA UBATILI NA UONGO HUJENGA NA REHEMA ZAO WENYEWE;

9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa Bwana.

10 Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.

Amen. Hapo tunaweza kuona ni jinsi gani Yona alipitia taabu sana, ni rahisi kuisoma kama habari tu, lakini jaribu kutafakari kwa kina uelewe ni mateso ya namna gani, mtu kukaa kwenye tumbo la kiumbe ambacho hakijui, na kibaya zaidi kipo baharini ingekuwa heri kama kingekuwa ni cha nchi kavu, Yona anasema alipelekwa mpaka katika moyo wa bahari katikati ya vilindi, kwenye baridi kali huko chini, jaribu kifikiria mazingira ya tumboni, biblia inasema yule samaki alikuwa anakula pia na magugu ya baharini(mwani), ambayo yalikuwa yanamsumbua sana kule tumboni, jenga picha ni shida kiasi gani, kumbuka tumboni hamna mwanga, hata hewa yenyewe tunajiuliza alikuwa anapataje pataje katika tumbo lile, alikuwa hali wala hanywi muda wa siku tatu usiku na mchana, na tunafahamu kuna kemikali maalumu za kumeng’enya chakula ambazo ni lazima ziwepo ndani ya matumbo ya wanyama, hivyo mambo hayo yote yalimpata Yona. Na zaidi ya yote alifahamu kabisa hayo yote yalimpata kwasababu ya upumbavu wake, na ndio maana alipokuwa analia na kuomboleza alisema.. “8 WATU WAANGALIAO MAMBO YA UBATILI NA UONGO HUJITENGA NA REHEMA ZAO WENYEWE;”. Yona alijitenga na Rehema zake mwenyewe na ndio maana yakampata mambo hayo,

Mfano kamili wa mambo yatakayokuja kulipata hili kanisa la mwisho tunaloishi, siku ile Unyakuo utakapokuwa umepita, Kumbukua watu watakaonyakuliwa watakuwa wachache sana na sio watu wote wa dunia watafahamu kama wengi wanavyodhania, kwasababu zitaonekana kuwa kama habari za kutunga machoni pa watu wengi, na pia hakutaonekana mabadiliko yoyote mbinguni wala duniani, wala hakutakuwa na maajali, au viashiria vyovyote kwamba unyakuo umepita kwasababu litakuwa ni kundi ndogo sana litakalonyakuliwa.

Watakaokuja kufahamu kuwa unyakuo umepita na wao wameachwa, ni wale wakristo wapumbavu ambao nao pia watakuwa wachache, Hawa ndio wale waliokuwa wanajua kabisa unabii wa siku za mwisho, wanafahamu kabisa kuwa Bwana wao yupo karibuni kurudi lakini hawakutaka kujiweka tayari (wapo vuguvugu) leo wanamwabudu Mungu, kesho wanatenda maovu, mfano wa wale wanawali 5 wapumbavu (Mathayo 25) ambao hawakubeba mafuta ya ziada pindi Bwana wao alipokuja awachukue waende karamuni Hivyo kundi hili ndilo litakalolia na kuomboleza mfano wa Yona. Kumbuka hawatukuwa waislamu, au watu wasiomjua Mungu, au wasiojua unabii wa biblia kuhusu habari za siku za mwisho (hawa watapokea chapa ya mnyama kwasababu hawafahamu chochote). Lakini Itakaye muhusu ni yule mkristo anayejua sana maandiko kama wewe unayesoma ujumbe huu na hautaki kugeuka, siku ile mpinga-kristo atatafuta watu wa namna hii ili awameze pale watakapojaribu kukataa mfumo wake(Chapa ya Mnyama).

Kama vile Yona alivyopitia dhiki kuu ndani ya lile tumbo kadhalika hawa nao watapitia dhiki isiyo ya kawaida kama Bwana alivyosema kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu ulimwengu kuwako na wala hatakaa iwako. Usidhani itakuwa ni rahisi kuikataa ile chapa, usidanganyike ni heri usiwepo hicho kipindi kwasababu hutasalimika, kumbuka hutaweza kuajiriwa, kujiajiri kuuza wala kununua bila hiyo chapa, sasa utakula nini usipoweza kununua wala kuuza!..na utajifichia wapi katika jamii ya leo ni dhahiri kuwa mwisho wa siku utashikwa tu,(maana ule mfumo wa mpinga-kristo utashirikiana na vyombo vya dola,) na kupelekwa katika magereza maalumu ya mateso, huko hutakufa leo wala kesho, leo hii hayo magereza yapo tayari, kwasababu ni kikundi kidogo tu kitakacho kamatwa wengine wote watakuwa wanamfurahia mpinga-kristo kama mtu wa amani aliyekuja kuwaondolea watu waovu na wavuruga amani miongoni mwao, wakati huo wanawali wapumbavu walioachwa watakuwa wanalia na kuomboleza kwenye matumbo ya yule mnyama.

KAMA ILIVYOKUWA KATIKA SIKU ZA NUHU:

Siku hizo Bwana alizifananisha na kama zile za Nuhu, kumbuka kabla ya gharika haijaja duniani, HENOKO aliyekuwa mtu wa SABA (7) baada ya Adamu, alinyakuliwa juu asione uharibifu biblia inasema hivyo. Na aliyepata ufunuo wa kuondoka kwa HENOKO alikuwa ni Nuhu pekee yake, hivyo akalazimika kuingia katika ile SAFINA ili aiponye nafsi yake katika mawimbi na misukosuko ya MAJI MENGI kabla ya pepo hazijaanza kuvuma na madirisha ya mbinguni kufunguka.

Vivyo hivyo Henoko anawakilisha watu wa kanisa la 7, ambalo ndilo la mwisho, wakristo waliojiweka tayari bikira safi watakaoenda na Bwana kwenye unyakuo. Hawa Bwana atawaepusha na ile dhiki inayokuja. Lakini Nuhu na familia yake akiwakilisha Wale wanawali waliosalia wasiokuwa werevu iliwabidi waingie kwenye ile NYAMBIZI(SAFINA),hivyo wakagharimika kupitia misukosuko ya mafuriko makubwa katikati ya vilindi vya maji kama tu Yona alivyopitia misukosuko katika tumbo la yule mnyama. Wengi tunadhani Nuhu na familia yake walikuwa wamestarehe kwenye safina wakipata raha, kuna raha gani! kukaa katika kijumba kile chenye giza kwa siku 150, huku mkirushwarushwa na tufani na mafuriko,radi na mingurumo huko nje?..Ni dhahiri kuwa hofu ya Mungu iliwaangukia, kila siku ilikuwa ni kulia na kuomboleza, yamkini Mungu asiwajumuishe pamoja na wale wengine katika adhabu ile.Kumbuka pia ile safina ilikuwa haielei tu muda wote, kutoka na tufani kubwa ilikuwa inazamishwa chini ya maji na kupandishwa juu, na ndio maana biblia inasema ilipigwa LAMI NDANI na NJE, ili maji yasipenye ndani. Kadhalika kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa katika siku zetu, ni mmoja tu aliyeenda kwenye unyakuo ikifunua ni kundi dogo sana litakalonyakuliwa, na pia ni wachache tu waliostahimili misukosuko ambao ni watu 8 tu, ikifunua kuwa wataostahimili dhiki ya siku ile watakuwa ni watu wachache sana.

Hivyo ndugu usitamani uwepo kule, anza kuweka mambo yako sawa, hizo siku zimekaribia sana, ulimwenguni wote umeshadanganywa na shetani, ni kundi dogo la wakristo ndilo analolitafuta, na shabaha yake sio kukufanya uwe baridi la! bali ni kukufanya uwe vuguvugu na ndio tabia iliyotabiriwa kwa kanisa la LAODIKIA kwasababu anajua Bwana anamchukia zaidi mtu aliyevuguvugu kuliko aliye baridi kabisa. Tubu umgeukie Mungu, epuka ibada za sanamu, injili za mafanikio tu huku roho yako unaicha nyuma inaangamia zitakupoteza, acha mavazi ya kutokujisitiri hayo hayamfai kabisa bibi-arusi wa Kristo, tafuta utakatifu, ambao pasipo huo hakuna atakayemwona Mungu asipokuwa nao.Shika NENO la Mungu kwa kudumu katika mafundisho ya biblia tu.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Pia washirikishe na wengine mambo haya.

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>>> YONA: Mlango wa 3


Mada Nyinginezo:

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!


Rudi Nyumbani:

Print this post

YONA: Mlango 1

Yona alikuwa mmoja wa manabii wa Israeli wakati wa utawala wa Yeroboamu Mfalme wa Israeli, ambaye Mungu alimtumia sana kutoa unabii kadha wa kadha katika Israeli, kama tunavyomsoma katika (2Wafalme 14:21-25). Lakini ilifika wakati BWANA akataka kumtuma kwa watu wa Mataifa, Mji wa NINAWI uliokuwa mji mkuu wa Taifa la ASHURU ambalo kwa wakati ule lilikuwa ni moja ya ngome yenye nguvu duniani ndilo lililokuja baadaye kuhusika kuwachukua wana wa Israeli utumwani (2Wafalme 18:11), Mataifa mengine yakiwemo BABELI pamoja na MISRI. Kumbuka taifa la Ashuru liliyachukua yale makabila 10 na kuyapeleka Ashuru, na makabila mawili ya Israeli yaliyosalia (Yaani YUDA na BENYAMINI) Mfalme Nebukadneza, alikuja kuyachukua utumwani Babeli.

Hivyo mji wa NINAWI uliokuwa mji mkuu katika Ashuru ulijaa maovu mengi sana, mfano wa Sodoma na Gomora, mpaka kufikia wakati Bwana kutaka kuuangamiza mji wote na watu wote waliokuwepo kule, lakini Mungu alivyo wa rehema hawezi kufanya jambo lolote kabla hajawaonya kwanza watu wake, ili pengine waghahiri uovu wao wasiangamizwe, na ndivyo alivyofanya kwa kumtuma YONA nabii katika mji ule Mkubwa uliokuwa mbali sana na taifa la Israeli.

Lakini tunasoma habari haikuwa hivyo kwa nabii YONA, badala ya kwenda NINAWI mji wa ASHURU alioagizwa na Bwana, yeye akaamua kuubuni mji wake yeye alioupenda ili akakae huko, ndipo akakimbilia TARSHISHI mji uliokuwa nchi ya Lebanoni ili tu AJIEPUSHE NA MAPENZI YA MUNGU.

Lakini alisahau kuwa ili afikie malengo yake hana budi kupitia “NJIA YA BAHARI”.. Hivyo akaamua kupanda Merikebu zinazoelekea Tarshishi, Na kama tunavyosoma habari alipokuwa katikati ya safari yake bahari ilichafuka na mambo yakaanza kuharibika..

 
Yona 1: 4 “Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.

5 Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.

6 Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.

7 Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.

8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?

9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu.

10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.

11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka.

12 Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata.

13 Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana.

14 Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.

15 Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.

16 Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri.

17 Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku”.

Basi wakamkamata  nabii Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.

Bwana aliyaruhusu yote haya yampate YONA ili kutuonya sisi kwamba tusipotaka kuenda katika njia ambayo Mungu kaikusudia tuiendee,yatatukuta kama hayo hayo. Kama biblia inavyosema
 
1Wakoritho 10: 11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ILI KUTUONYA SISI, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.”
 

SWALI NI JE! NJIA YA BAHARI NI SALAMA?

Kibiblia BAHARI inawakilisha nini?…Ili kufahamu jambo hili ni vizuri tujue ni kitu gani kimo humo ndani yake .tukisoma. 

Ufunuo 13: 1 “KISHA NIKAONA MNYAMA AKITOKA KATIKA BAHARI, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.”

Unaona hapo?.

Kumbuka YONA anawakilisha kundi la wakristo wasiotaka kudumu katika mapenzi ya Mungu (yaani VUGUVUGU).leo wanaenda na Mungu, kesho wanaenda katika akili zao, leo anafanya ibada kesho anakula rushwa. N.k. Sasa Kama vile  nabii YONA alivyokimbia uso wa Mungu na kuelekea njia ya BAHARINI na hatimaye kumezwa na yule SAMAKI MKUBWA, vivyo hivyo na kundi hili la wakristo wasiotaka kutengeneza mambo yao sasa vizuri na Mungu, hawajui kama wanakimbilia baharini pasipo wao kujua, ambapo kule kuna Yule mnyama mwenye vichwa saba na pembe kumbi ameandaliwa kuwameza.

Na bahari inawakilisha nini?

Tukirudi kusoma Ufunuo 17: 15 Kisha akaniambia, YALE MAJI ULIYOYAONA, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Kumbuka huyu kahaba anayezungumziwa hapa ameketi juu ya Yule mnyama aliyetoka baharini ambaye tumemsoma katika Ufunuo 13.

Kwahiyo bahari au maji mengi inawakilisha mahali penye mkusanyiko wa watu wengi, hivyo Yule mnyama anatoka mahali penye mkusanyiko wa watu wengi, mahali ambapo amekubaliwa na wengi, tukizungumza katika roho leo hii mfumo wa mpinga-kristo unatenda kazi katikati ya mataifa, na dini nyingi za uongo.

Kama vile Yona alivyoiacha njia ya Mungu na kuchagua Njia ya BAHARI akidhani kuwa ni salama, vivyo hivyo na wakristo wa leo walio vuguvugu, wanamsahau Mungu na kushikimana na mambo maovu ya ulimwengu huu, nabii Yona alisinzia pale alipoona kuna utulivu mwanzoni mwa safari yake, kadhalika kundi hili la wakristo vuguvugu wanasinzia kwasababu wanajiona wapo salama, wanaona hata wakifanya hivyo hakuna dhara lolote wanatakalolipata lakini hawajui kuwa kuna mnyama ameshaandaliwa kwa ajili yao chini ya Merikebu yao. Pale PEPO zitakapovuma ndipo watakapotambua kwamba hawapo salama, wakati huo unyakuo umeshapita, ndugu unajiona upo salama katika ulimwengu, hata ukitenda dhambi unaona hakuna dhara lolote linalokupata, angali unafahamu kabisa moyoni mwako umeukimbia uso wa Mungu na unayoyafanya sio sahihi na bado unajiita Mkristo, hujui kwamba ni NEEMA ya Mungu tu, imekushikilia dhidi ya Yule Mnyama utubu, ugeuze njia uepuke madhara yaliyopo mbeleni ambayo yapo karibuni kuupata ulimwengu mzima. Ipo siku NEEMA inayokushikilia itakwisha na moja ya siku hizi PEPO ZITAANZA KUVUMA BAHARINI. Kama biblia inavyosema katika..

Danieli 7: 1 “Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.

2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, HIZO PEPO NNE ZA MBINGUNI ZILIVUMA KWA NGUVU JUU YA BAHARI KUBWA.

3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali”………

Wanyama hao Nabii Danieli alionyeshwa, watatu wa kwanza walishapitia na Yule wa mwisho wanne, ndiye aliyeko sasa chini ya MERIKEBU(NEEMA), na moja ya hizi siku pepo zitamwamsha kutenda kazi tukiendelea kumsoma:

“7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama,MNYAMA WA NNE, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.

8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazukia kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu”.

Kama vile Nabii Yona alikaa ndani ya tumbo la samaki siku tatu usiku na mchana, kadhalika Huyu mnyama atokaye baharini atalimeza hili kundi la watu, kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu ndio kile kipindi cha dhiki kuu, mpinga-kristo atakaponyanyuka na kuanza kuleta dhiki isiyoelezeka kwa wale waliouvuguvugu kwa kuupenda ulimwengu huu, na kuiacha njia Mungu aliyowawekea wao waiendee.

Hichi kipindi kipo karibuni kutokea, Yule mnyama sasa anatenda kazi katika siri na watu wa Mungu wanasinzia hawaoni kuwa wapo katika hatari, wanadanganyika na utulivu uliopo sasa hivi kama vile nabii Yona alivyodhani lakini biblia inasema 

1Wathesalonike 5: 2 “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile MWIVI ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.

Ndugu usileweshwe na ulevi wa hii dunia hata kulala usingizi, Bwana yupo karibu kulichukua kanisa lake BIBI-ARUSI WA KWELI anayedumu katika Neno lake na UTAKATIFU, Na hatua za unyakuo zimeshaanza Bwana anawakusanya watu wake toka kila mahali, watu ambao macho yao yapo mbinguni, duniani wao ni kama wapitaji tu, hao ndio watakaofunuliwa siri za unyakuo lakini wengine wote ikiwemo wakristo vuguvugu, hawatajua lolote isipokuwa kumtazamia Yule mpinga-kristo mnyama atokaye baharini. Utajisikiaje siku ile wenzako wapo mbinguni kwenye KARAMU YA MWANA-KONDOO na wewe upo katika dhiki kuu na zaidi ya yote watakuja kutawala na Kristo milele na milele kama wafalme na makuhani wa Mungu na wewe upo kwenye ziwa la moto??. Ni vizuri utengeneze mambo yako sasa hivi kabla siku ile haijafika. Tubu ukabatizwe kwa Jina la BWANA YESU upate ondoleo la dhambi zako na uanze kuishia wokovu..

Mungu akubariki..

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312

Kwa mwendelezo >>> YONA: Mlango wa 2

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: MLANGO WA 13

UFUNUO: MLANGO WA 17

DANIELI: MLANGO WA 7

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA


Rudi Nyumbani:

Print this post

ESTA: Mlango wa 8, 9 & 10. (SIKU KUU YA PURIMU)

Jina la YESU KRISTO BWANA wetu lisifiwe.

Karibu kwenye mwendelezo wa kitabu cha Esta, leo tukiwa katika sura za mwisho, yapo mambo mengi ya kujifunza yahusuyo safari yetu ya ukristo tunapopitia kitabu hichi, tunaona mara baada ya Hamani adui wa watu wa Mungu kuuawa, Malkia Esta ananyanyuka tena kumwomba mfalme ayaondoe madhara aliyokusudia juu ya wayahudi wote waliandikiwa kuuawa, tunasoma;

Mlango 8

“ 1 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.

2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.

3 Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi.

4 Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme.

5 Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.

6 Kwa maana niwezeje kuyaona mabaya yatakayowajia watu wangu? Au niwezeje kuyatazama maangamizo ya jamaa zangu?

7 Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani, naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono Wayahudi.

8 Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua.

9 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao”.

Kama tunavyosoma ule msiba mkuu na uchungu ambao ulikuwa juu ya wayahudi wote duniani Bwana aliugeuza na kuwa furaha na shangwe kwao, ile nyumba ya Hamani pamoja na cheo chake walipewa Mordekai na watu wake, wale walioonekana hawana heshima katikati ya mataifa Bwana aliwapa heshima kuliko jamii za watu wote duniani. wale walioonekana wadogo wakawa wakuu katikati ya mataifa. Biblia inasema kukawa nuru na furaha kwao;

Hata ile siku waliyopanga kuwaangamiza wayahudi wote tarehe 13 mwezi wa 12, ndio ikawa tarehe hiyo hiyo ya wayahudi wote duniani kuwaangamiza maadui zao waliowazunguka na kuwatawala. Hivyo tarehe 14. na 15 ya mwezi huo huo wa 12 wakaifanya kuwa sikukuu yao ya ushindi Bwana aliowapa dhidi ya maadui zao, wakaifanya kuwa sikukuu ya kupelekeana zawadi, pamoja na karamu na furaha waliyoiita sikukuu ya PURIMU.

Esta 8: 15 “Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.

16 IKAWA NURU na FURAHA na SHANGWE na HESHIMA kwa Wayahudi.

17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata FURAHA, na SHANGWE, KARAMU na SIKUKUU. HATA WENGI WA WATU WA NCHI WAKAJIFANYA WAYAHUDI, KWA KUWA HOFU YA WAYAHUDI IMEWAANGUKIA. “

Hivyo Bwana akawapa wayahudi wote kustarehe na kufurahi siku zote za ufalme wa Ahasuero.

Kumbuka habari yoyote tunayoisoma katika agano la kale ni kivuli cha mambo yatakayokuja kutokea mbeleni. Wakati wote shetani alipojaribu kuwaletea mateso na dhiki watu wa Mungu, Bwana alitolea wokovu na ushindi mkuu kwao, tunasoma habari ya wana wa Israeli jinsi walivyopiganiwa na Bwana dhidi ya maadui zao walipokuwa wanatoka Misri, wakati wa-Misri walipoona njia pekee iliyosalia ni kuwateketezea katika zile kingo za bahari ya shamu, kinyume chake, wao ndio walioteketezwa katika ile habari, ikawa shangwe kwa wayahudi, huo ulikuwa ni mfano wa PURIMU kwao.

Vivyo hivyo na sehemu nyingine zote, tunaona wakati wa wafilisti walipokuja kupigana na Israeli, wakati wa akina Shedraki, Meshaka, na Abadnego walipotupwa katika tanuru la moto, wakati wa Danieli alipotupwa katika tundu la simba, n.k. hata kwa Bwana wetu Yesu, tunaona jambo lile lile shetani alijaribu kumuua akidhani ameshinda, lakini ufufuo ulidhihirisha ushindi wake, wote hawa maangamizi yao yaligeuka kuwa wokovu mkubwa kwao…ikawa kama mfano wa PURIMU kwao.

Vivyo hivyo katika siku za mwisho shetani anashindana na UZAO wa Mungu, yaani wayahudi wa mwilini na wayahudi wa rohoni (wakristo), kama alivyofanya katika siku za kale, kumbuka HAMANI ni mfano wa mpinga-kristo atakayekuja, na Esta ni mfano wa BIBI-ARUSI wa Kristo. Kama vile HAMANI alivyokusudia kuwaangamiza wayahudi wote duniani, isipokuwa Esta kwasababu yeye alikuwa ni malkia..Vivyo hivyo na mpinga-kristo atakapotafuta kuwaua wayahudi wote (wa-mwilini na wa-rohoni) hatoweza kwa BIBI-ARUSI wa Kristo kwasababu wakati huo atakuwa ameshakwenda katika unyakuo yupo kwenye Jumba la kifalme mbinguni mfano wa Esta. Hivyo hayo madhara hayatamkuta yeye.

Mpinga-kristo (ambaye atakuwa ni PAPA wa wakati huo), atakusudia kuundoa uzao wote wa Mungu duniani kwa njia ya hila, kwa kisingizio cha kuleta amani duniani kama Hamani alivyofanya kuwasingizia wayahudi kwamba wamefarakana na watu wote wa dunia nzima, jambo ambalo si kweli. Hivyo katika siku hizo wayahudi wote, na wale wakristo wote waliokuwa vuguvugu waliokosa unyakuo watagharimika kuingia katika ile dhiki kuu Bwana aliyoizungumzia.

Japokuwa mpinga-kristo atafanikiwa kuua watu wengi, lakini haitakuwa kwa wote, kwasababu biblia inasema wapo watakaofichwa mbali naye,(Ufunuo 12) mpaka siku ile MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA, YESU KRISTO Atakapokuja na mawingu pamoja na bibi-arusi wake, kuwaokoa wateule wake walioko duniani, na kila jicho litamwona, atakaposhuka na kukusanya watu wake(wayahudi) toka pembe nne za dunia, hapo ndipo mataifa yote yatakapoomboleza kwa maana atakuja na upanga kinywani mwake, kama vile maadui wa wayahudi walivyoomboleza siku yao ilipofika, mbele ya Mordekai na Esta ndivyo itakavyokuwa siku ile mbele ya Bwana Yesu na watakatifu wake. Mataifa yaliyowatesa watu wa Mungu yataomboleza sana mbele zake.

Ufunuo 19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 NA MAJESHI YALIYO MBINGUNI WAKAMFUATA, WAMEPANDA FARASI WEUPE, NA KUVIKWA KITANI NZURI, NYEUPE, SAFI.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”.

Umeona hapo, ukirudi kwenye..
 Mathayo 24: 29 inasema….; Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu”.

PURIMU KWA WATU WA MUNGU.

Katika sura ya tisa ya kitabu cha Esta, kama vile tulivyoona jinsi wayahudi walivyosheherekea sikukuu ya PURIMU baada ya ushindi dhidi ya maadui zao, mpaka wale wasiokuwa wayahudi walijifanya kuwa kama wayahudi, kadhalika na katika siku hizo mpinga-kristo na mifumo yake yote mibovu pamoja na mataifa yote yaliyosalia wataangamizwa kwa maangamizo makuu katika vita vya Har-Magedoni. Wakati huo wengi watatamani kuwa kama watu wa Mungu lakini haitawezekana tena, kwao itakuwa ni MSIBA mkuu, wakati huo watoto wa Mungu kwao itakuwa ni KARAMU ya PURIMU. Kufarijiwa na kuburudishwa milele, na kufutwa machozi. Pale watakapomwona BWANA wao uso kwa uso akija kuwapigania na kuleta utawala mpya wa AMANI wa miaka 1000 usio wa shida wala uchungu.

Ufunuo 19:17 “Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane KWA KARAMU YA MUNGU ILIYO KUU;

18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.

19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.

20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

21 NA WALE WALIOSALIA WALIUAWA KWA UPANGA WAKE YEYE ALIYEKETI JUU YA YULE FARASI, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.”

Unaona hapo ndugu hii roho ya mpinga-kristo ilishaanza kutenda kazi tangu zamani, na shabaha yake si kwa kila mtu duniani bali ni kwa wale walio uzao wa Mungu tu.Iliwauwa wakristo wengi wakati wa zama za giza zaidi ya milioni 68, Na chombo chake teule anachotumia na atakachokuja kutumia kuyalaghai mataifa yote ulimwenguni ni dini na madhehebu huku akihubiri injili yake bandia yenye kivuli cha amani lakini nia yake sio kuleta amani bali kuangamiza uzao mteule wa Mungu. Hivyo ndugu ni wakati wa kujitathimini, je! Wewe ni mfuasi wa kweli wa Kristo au mfuasi wa dini au dhehebu?, je! Wewe ni mtakatifu au vuguvugu,.je! unahuakika wa kwenda mbinguni au unahisi tu?. Je! Wewe ni bibi-arusi wa kweli kama Esta au kama Vashti. Jibu lipo moyoni mwako. Kumbuka ndani ya kanisa yapo magugu na ngano, wapo wanawali wapumbavu na werevu..Je! wewe ni yupi kati ya hayo?.

Bwana wetu yuaja.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

UPUMBAVU WA MUNGU.

JE! MUNGU ATAIANGAMIZA DUNIA TENA BAADA YA GHARIKA YA NUHU?

MANENO HAYA YANA MAANA GANI? “..KWA SABABU HAMTOI ROHO KWA KIPIMO. (YOHANA3:34)”


Rudi Nyumbani

Print this post