JIBU: Mafarisayo na Msadukayo chimbuko lao ni moja dini zao zimeegemea katika Torati ya Musa, wote hawaamini maagizo mengine nje ya torati isipokuwa tofauti inakuja katika kuamini kiama cha wafu.. Mafarisayo wanaamini kuwa kuna kiama cha wafu (yaani maisha baada ya kufa, wanaamini yote yaliyoandikwa katika torati hata tumaini ya kuja kwa Masihi duniani) lakini masadukayo hawaamini kama kuna kufufuliwa kwa wafu, wanaamini kuwa mtu akishakufa, amekufa hakuna chochote baada ya hapo, wala hakuna malaika wala ulimwengu wa roho wala mbingu.
Ukisoma Mathayo 22:24-34 utaona Bwana Yesu akiwajibu hao mafarisayo kuhusu mitazamao wao hafifu ya maandiko Na kuwaambia kuwa Mungu asingesema yeye ni Mungu wa Ibrahimu, na Isaya na Yakobo kama watu hao ni wafu sasa. Kwasababu siku zote Mungu si Mungu wa wao bali wa wanaoishi..Hivyo Neno hilo linathibitisha kuwa kiama kipo. Ukisoma tena Matendo 23 Utaona Mtume Paulo akiyagonganisha madhehebu hayo mawili.
Matendo 23: 6 “Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. 7 Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana. 8 Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote. 9 Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesemanaye, ni nini? 10 Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paulo asije akararuliwa nao, akaamuruaskari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.”
Matendo 23: 6 “Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.
7 Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana.
8 Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote.
9 Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesemanaye, ni nini?
10 Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paulo asije akararuliwa nao, akaamuruaskari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.”
Hivyo kwa maandiko hayo utapata kuelewa tofauti ya watu hawa ipo wapi.. MYUNANI: Sio dini au imani, bali ni watu wa taifa la uyunani, kwasasa ni Ugiriki.Hivyo katika agano jipya mahali popote anapotajwa myunani, linalenga watu wa aina mbili, aina ya kwanza ni aidha wayahudi wanaotokea katika nchi za wayunani, na hivyo wanajulikana kama wayunani lakini kiasili ni wayahudi, kwa mfano wale watu waliotaka kumwona Bwana zamani zile ni wayahudi lakini sio wa kuzaliwa Israeli. tunasoma:.
Yohana 12:20 “Palikuwa na WAYUNANI kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. 21 Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya,wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu “
Yohana 12:20 “Palikuwa na WAYUNANI kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.
21 Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya,wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu “
Unaona? Kadhalika pia wale watu waliokuwa Yerusalemu siku ile ya Pentekoste, (Matendo 2) wakishangaa matendo makuu ya Mungu, biblia inasema walikuwa Warparthi na Wamedi na Waelami,n.k. wote hawa hawakuwa watu wa mataifa mengine (yaani watu wasio wayahudi) hapana bali walikuwa ni Wayahudi waliotoka katika hayo mataifa yaliyotajwa hapo,Na aina ya pili: ni Wayunani ambao asili yao ni Uyunani kabisa, watu wa mataifa. Mfano tunaweza kumwona mwanamke huyu aliyezungumziwa hapa ni myunani lakini hana uyahudi wowote ndani yake:
Marko 7:24 “Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba,akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika. 25 Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake,akajaakamwangukia miguuni pake. 26 Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katikabinti yake. 27 Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto,na kuwatupia mbwa 28 Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hulamakombo ya watoto. 29 Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. 30 Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.”
Marko 7:24 “Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba,akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.
25 Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake,akajaakamwangukia miguuni pake.
26 Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katikabinti yake.
27 Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto,na kuwatupia mbwa
28 Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hulamakombo ya watoto.
29 Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako.
30 Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.”
Kadhalika tunaona watenda kazi wa Mungu wengine kama Tito, mwanafunzi wa Paulo (Wagalatia 2:3).
Na Timotheo (Matendo 16:1) hawa wote biblia inawataja kama ni Wayunani, na sio wayahudi.
Ubarikiwe sana.
Mada Nyinginezo:
MATOWASHI NI WAKINA NANI?
WANA WA MAJOKA.
NIFANYAJE ILI NIJUE KUWA UAMUZI NINAOKWENDA KUCHAGUA KUFANYA NI MAPENZI YA MUNGU?
USIWE SABABU YA WATU KUMKUFURU MUNGU.
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?
MASHEHE NI WAKINA NANI?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Ufafanuzi mzuri sana