Title August 2019

Kulingana na 1Wakorintho 3:10-15, kama inavyosema..ni kwa namna gani kazi ya mtu itateketea, na kupimwa kwa moto?”

1Wakorintho 3:10-15 Inasema..

10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.

13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa wanaozungumziwa hapo ni watenda kazi (yaani watu wote wanaojiita watumishi wa Mungu), na kila mtu anapofanya kazi ya kuhubiri na kuwavuta watu kwa Kristo ni sawa na kama anajenga nyumba yake mwenyewe ya mbinguni. Kwahiyo wale watu anaowazaa kwa injili yake hiyo ndio kazi yake na ndio itakayojaribiwa kwa moto. Sasa moto ni nini, na unaijaribuje kazi ya mtu?.

Moto ni majaribu ya imani, misukosuko, adha, dhiki, au mateso shetani atakayoyaleta juu ya watu wako uliowazaa katika kazi ya kuhubiri injili.

Kwahiyo kama wale watoto wako uliowaowazaa uliwakuza katika mafundisho madhaifu wasiyowafanya wawe imara, itakapokuja dhiki, au misukosuko,au majaribu, watashindwa kusimama na mwisho wa siku wataanguka na kuteketea na kupotea kabisa. Hivyo katika siku ile Kazi yake mtu huyo itaonekana kama ni ya hasara kwasababu watu aliowazaa wote wameteketea na moto(majaribu misukosuko n.k.), Kwa mfano unakuta muhubiri injili yake siku zote imejikita katika mafanikio ya kimwilini tu,haweki mambo katika usawa hafundishi watoto wake kumjua Mungu zaidi na utakatifu na uweza wa Mungu na iMANI,na Upendo wa Mungu au mambo yahusuyo ufalme wa mbinguni, yeye mafundisho yake ni mafanikio tu ya kimwilini basi na mtumishi huyo utakuta yupo na maelfu ya wafuasi anawalea chini yake,

Sasa kipindi kitakapofika shetani naye atataka kuwajaribu wale watoto aliowazaa,..atawaletea aidha mtikisiko wa kiuchumi kidogo tu, au magonjwa, au vifungo, au wakati mwingine mafanikio makubwa kupita kiasi ili apunguze muda wake na Mungu ajikite katika mambo ya kidunia n.k. sasa kwasababu wale watoto hawakufundishwa uvumilivu, saburi na Imani, kiasi n.k.. haraka sana wataiacha ile Imani na kurudi nyuma. Na ndio hao wanafananishwa na zile mbegu zilizodondokea nyingine njiani, ndege wakapita wakazila, nyingine kwenye miamba zikakosa mizizi na kufa(Hawa ndio wale wakati wa kujaribiwa wanajitenga na Imani), wengine kwenye miiba(shughuli na udanganyifu wa mali vinawasonga, wanakuwa hawazai chochote) n.k.. Kwa namna hiyo basi safari yao ya Imani wanajikuta imeishia ukingoni. 

Hivyo kazi ya yule muhubiri mwisho wa siku yote aliyojisumbukia yanakuwa ni hasara tupu kwasababu hakuijenga nyumba yake(kondoo wake) katika ubora unaotakiwa… Kadhalika biblia inaposema yeye naye ataokoka lakini kana kwamba kwa moto, inamaanisha pia na yeye atapitia majaribu yale yale, na kama akiweza kuyastahimili yeye ataokoka lakini kazi yake itakuwa ni ya hasara, atakuwa kama mtu tu ambaye hajawahi kumtumikia Mungu kwa namna yoyote ile.

 Kwahiyo habari hiyo inatufundisha kuwa tufanye kazi ya Mungu kwa malengo, tukijua ya kuwa kazi zetu zitaenda kupimwa siku ile. Itatufaidia nini tupate maelfu wa washirika katika makusanyiko yetu kwasababu tu tunawahubiria injili laini, na siku ile tunakwenda kuonekana hatufanya chochote?. Ni heri awepo mmoja lakini chombo cha thamani chenye kumfaa Mungu kilichojengwa kwa dhahabu.kuliko kuwa na mabunda ya nyasi.

Hivyo Tusihubiri tu ilimradi kuwaburudisha washirika ili washirika waendelee kukaa katika makusanyiko yetu, hapana bali tuwajenge wawe kama mawe ya thamani ambayo moto utakapokuja kuyajaribu ndio yanazidi kuwa imara badala ya kuwa dhaifu. 

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UBATIZO WA MOTO

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

ROHO MBAYA KUTOKA KWA BWANA.

UPUMBAVU WA MUNGU.

IMANI NI KAMA MOTO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! mtu anapofunga kwa muda wa SAA 24,anapaswa kunywa maji au kitu chochote?

JIBU: Biblia haijatoa masharti yoyote ya kufuata katika kufunga kwamba ufunge masaa 12 au 26 au 36 au mwezi,nk.. hapana. Kwasababu kitendo chenyewe cha kufunga ni kitendo kinachotoka rohoni na sio mwilini. Hivyo kwa jinsi mtu atakavyoguswa moyoni au atakapoona yeye mwenyewe umuhimu wa kufunga kwa muda fulani, pengine kutokana na ugumu wa hali fulani anayopitia kiroho ama haja fulani anataka kupeleka kwa Mungu, ndipo anapolazimika kujichagulia mwenyewe aina ya ufungaji wake utakaoendana na haja zake, (isipokuwa labda awe ameagizwa na Mungu mwenyewe aina ya mfungo anaopaswa afunge).   Mfano tunaweza tukamwona mtu kama Danieli ukisoma katika

Danieli 10: 1 “Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danielii, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.

2 Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.

3 SIKULA CHAKULA KITAMU, WALA NYAMA WALA DIVAI HAIKUINGIA KINYWANI MWANGU,WALA SIKUJIPAKA MAFUTA KABISA, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.  

Hivyo kulingana na habari hiyo Danieli kwa kuona vita kubwa mbele yake na kutaka kufahamu mambo gani yatakayokuja kutokea huko mbeleni, ikamlazimu afunge wiki tatu, pasipo kula chakula kitamu wala kujipaka mafuta, Kadhalika na Musa, kwa kuwa alifahamu anakwenda kukutana na uso wa Mungu na kupokea amri za Mungu kule mlimani ilimlazimu afunge siku 40 usiku na mchana bila kula chochote, Pia wakati wa Esta wayahudi walipoona wanapitia hatari ya kuuawa walifunga siku tatu usiku na mchana bila kula chochote, kadhalika na wengine mfano Nehemia, Daudi, Mitume Pamoja na Bwana wetu YESU KRISTO hata yeye wakati wa kwenda kujaribiwa na shetani nyikani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa chochote. n.k.  

Hivyo unaona hapo inategemea na sababu ya mtu kuingia katika mfungo huo, ndio kinachopelekea aina ya kujinyima nafsi. wapo watu wengine wanafunga saa 24 au zaidi kwa kunywa maji tu pasipo chakula na wanaweza kwenda hivyo kwa siku tatu au zaidi,.Wapo wengine wanaweza kufunga pasipo kula chakula wala maji kwa siku kadhaa, wapo wengine wanafunga kwa kutokula chakula walichokizoea, mfano walikuwa wanakula nyama mara mbili kwa siku, wanaamua kujinyima kwa kutokula chakula kitamu kama nyama kwa muda wa labda mwezi mmoja hivi au zaidi wanakuwa wanakula tu pengine maji na mkate basi.n.k.   Vyovyote vile nawe ukiamua kufunga kwa kutokunywa maji saa 24, au kwa kunywa maji tu katika ufungaji wako wote, ni uamuzi wako, lakini kumbuka kwa jinsi unavyojinyima zaidi ndivyo unavyoongeza nguvu zako za kiroho, Biblia inaonyesha wengi walikuwa wanafunga pasipo kula wala kunywa kwa kiwango cha chini ni saa 12 (yaani jua linapochomoza mpaka linapozama). Hivyo kufunga kokote kule utapata thawabu kama kama ukizingatia yale Bwana aliyosema katika Mathayo 6:16.  

Hivyo unapofunga kumbuka kuzingatia pia viwango vya rohoni kama usafi, utakatifu,(kwa kujitenga na dhambi) n.k. vinginevyo mfungo wako utakuwa ni sawa na bure kama wapagani wanavyofanya, Kwa kulijua hilo zaidi soma mistari ifuatayo. Bwana akiwaambiwa watu wake;  

Isaya 58:3 ” Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.

4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu,

5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?

6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?

8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.

9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;

10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.

11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.

13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;

14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

BWANA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI KUSEMA MARKO 2:19″WALIOALIKWA HARUSINI WAWEZAJE KUFUNGA MAADAMU BWANA-ARUSI YUPO PAMOJA NAO?”

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

NINI MAANA YA HUU MSTARI ” NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?(2TIMOTHEO 4:7)

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! shetani ni mwenye mwonekano mzuri au mapembe?

SWALI: Shetani kwa sasa ni mzuri wa umbo kama malaika watakatifu au ni mwenye mapembe na makwato na makucha marefu ya kutisha?


JIBU: Udanganyifu mkubwa uliopo duniani leo hii, ni pale watu wanapodhani kuwa shetani ni kiumbe chenye mapembe ya kutisha tu na kinakaa makaburini na kuzimu, hivyo wanadhani endapo mtu akikutana na kitu kama hicho kinachotisha sana ndio wamemuona shetani, Lakini hawajui kuwa yule alikuwa ni malaika kama wale wengine na alipoasi yeye na malaika zake, ndipo akawa shetani(Kumbuka maana ya neno shetani sio mapembe hapana bali ni MSHITAKI. 

Hivyo mara baada ya kuanguka ndipo akageuka na kuwa mshitaki wetu akitushitaki mbele za Mungu ..na biblia inaposema amelaaniwa haimaanishi kalaaniwa kimaumbile(ya nje) hapana, bali katika roho, na ndio maaana hata leo hii wanadamu wakilaaniwa na Mungu hawabadilili maumbile yao na kuwa vitu vya kutisha vyenye mapembe au viumbe visivyoeleweka, hapana bali roho zao ndio zinazobadilishwa. Kwahiyo shetani na malaika zake vivyo hivyo, wapo vilevile na ndio maana wanao uwezo wa kujigeuza jinsi wapendavyo hata kijifanya kama malaika wa Nuru wa Mungu, kadhalika pia hawajaondolewa ujuzi wao wote waliokuwa nao, isipokuwa hawana uwezo wowote wa kumshinda mtu aliye ndani ya Kristo.. Ukisoma;

2Wakorintho 11:3 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.

14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 

Kwahiyo unaona hapo?..Hawa watu wote waasi pamoja na viumbe vilivyolaaniwa(malaika waovu), wapo tu kama walivyoumbwa, isipokuwa tabia za roho zao ndio zinazowatofautisha kwasababu hao tayari wameshalaaniwa wakiongejea mauti ya pili katika lile ziwa la moto..(Na tabia zao ndio zinazofananishwa na vitu vya kutisha). Kwahiyo ndugu kumbuka ni vita kubwa inayopigwa sasa hivi, haupigani na vibwengo, au majinamizi, n.k. bali unapigana na malaika na vita kubwa ni kukufanya wewe Uache Imani yako usiende mbinguni.Tujitahidi tufanye Imara wito wetu na uteule wetu, kwasababu shetani ni kama simba angurumaye.. 

1Petro 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.

 Ubarikiwe sana. Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye
namba hizi: +255789001312/ +255693036618 . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI, JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.

JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE? 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Kwa kuwa Bwana Yesu alipitia katika tumbo la Mariamu je! Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

JIBU: Mariamu alimzaa BWANA kwa namna ya mwili, hivyo wakati Bwana alipokuwa duniani ndio Mariamu alijulikana kama mama wa Yesu, na sio mama wa Mungu. Bwana Yesu alipokuja hapa duniani alikuwa ni Mungu katika mwili lakini hakuja kutafuta kuabudiwa na ndio maana hakuna sehemu yoyote alijiita yeye ni Mungu, zaidi sana alikuwa anawarudisha watu wamuabudu Baba.   Kumbuka Mungu alipouvaa mwili ilimpasa afananishwe na mwanadamu kwa namna zote, azaliwe, ale chakula, asikie maumivu, alie, aone huruma, n.k. kama mwanadamu mwingine yeyote, si ajabu kumuona akiwa na Baba au bibi, au babu au mjomba, lakini haimaanishi kuwa yeye (YESU) yupo chini ya hao wote hapana..

Biblia inatueleza vizuri juu ya jambo hilo tukisoma katika..

Mathayo 22:41 Bwana Yesu alizungumza maneno haya;  

“41 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?

46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena”.

Unaona hapo? jibu litakuwa pia hivyo hivyo kwa Mariamu kwamba Yesu atakuwaje mwanawe na wakati bado ni Bwana wake? na yeye ni binti wa Mungu (Kwasababu kama Daudi alikuwa mkubwa kuliko Mariamu aliambiwa hivyo je! si zaidi yeye?).  

Hivyo sisi wote tunaomwamini YESU KRISTO mbele zake ni ndugu na dada, Na yeye akiwa kama Baba yetu. Kwahiyo ni muhimu tujue kutofautisha jinsi Mungu anavyotenda kazi katika ofisi zake tofauti, Mungu anapoonyesha unyenyekevu (kuzaliwa kibinadamu) haimaanishi kuwa mwanadamu yupo juu yake. Hapana anafanya hivyo kutuonyesha sisi njia bora kama watoto wake.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MARIAMU

JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

UDHAIFU WA SADAKA!

SHUKURU KWA KILA JAMBO.

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Ubatizo wa moto ni upi?

JIBU: Ni kweli Yohana alibatiza kwa maji na alisema Bwana YESU atakapokuja atatubatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto..Sasa huu ubatizo wa moto ni upi?, kama tunavyofahamu moto hufanya kazi kuu tatu:

Ya kwanza: ni kuteketeza vitu dhaifu vyote visivyostahili. Kwamfano takataka..Vivyo hivyo Hatua hii ni ile Mungu anaichoma dhambi yote ndani ya mtu, hapo ndipo utakuta mtu tamaa ile ya kutenda dhambi aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma inakufa yote, alikuwa anavuta sigara ghafla kiu ya sigara inakufa, alikuwa anakunywa pombe ghafla kiu ya pombe inakata, alikuwa ni mzinzi ghafla hata ile hamu ya kwenda kufanya uzinzi inakufa, alikuwa mtukanaji,ghafla anaanza kuona uzito tena kufungua kinywa chake na kutukana watu, alikuwa ni mwizi anajikuta hapendi tena uwizi, alikuwa msengenyaji ghafla dhamiri inamsuta akitaka kusengenya, alikuwa anatembea nusu uchi, ghafla anaanza kuona aibu hata kuzivaa hizo nguo n.k.

Ya pili: ni kuimarisha vitu vilivyo vigumu ili viwe vigumu na imara zaidi. kama vile dhahabu inapopitishwa kwenye moto.  

Hatua hii Roho Mtakatifu anapitisha mtu kwa lengo la kumuimarisha, Kama wafuaji wanavyofanya huwa wanayeyusha madini kwenye moto mkali ili baadaye yakishaganda yawe na mng’ao mzuri zaidi. , japo kwa nje yataonekana kama yanapitia dhiki ya hali ya juu kwa kuwekwa kwenye tanuru lakini yakishamalizwa kuchomwa matokeo yake yanaonekana kuwa bora zaidi kuliko yalipokuwa pale mwanzoni (Na ndio maana tunaona matofali ya udongo huwa yanachomwa kwanza, na ndipo yapelekwe kwa matumizi ya kujengea nyumba nzito,)..Hivyo kadhalika na kwa watoto wa Mungu..Tunapopokea Roho Mtakatifu..Mungu mwenyewe anaruhusu tupitie moto wa majaribu, ili kuzihimarisha IMANI ZETU zisiwe dhaifu, hata tutakapopitia mambo magumu tusiweze kuanguka kirahisi.

Na ndio maana tunaona pale tu mtu anapoanza kuamini! mara anaanza kuona mambo ya nje yanabadilika, ghafla anachukiwa na ndugu au kutengwa, mwengine atapitia misiba, mwingine magonjwa, mwingine vifungo, mwingine mapigo, mwingine anadorora kiuchumi, mwingine atatengwa n.k. mfano kama walivyopitia akina Ayubu, Yusufu n.k….Lakini Mungu kumpitisha mtu hivyo huwa sio kwa ajili ya kumwangamiza hapana bali ni kumuimarisha hivyo mtu kama huyo Bwana huwa anampa neema ya ziada kuyashinda hayo majaribu, kwasababu Mungu hawezi kuruhusu tujaribiwa kupita tuwezavyo

1Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

  Na pia Ukisoma…  

1Petro 1: 6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba KUJARIBIWA KWA IMANI YENU, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

  Hivyo huo ndio ubatizo wa Moto unaozungumziwa hapo..Kwahiyo mtoto yoyote wa Mungu ni lazima aupitie huo(Mitume walipitia, manabii walipitia na Bwana wetu Yesu Kristo alipitia kadhalika na sisi pia)..yaani ubatizo wa Maji pamoja na ubatizo wa Roho na wa moto .  

Na Hatua ya tatu: Ni kuchochea. Kwamfano moto ukiwashwa ndani ya bunduki, ile risasi iliyo ndani yake ni lazima ifyatuke. Moto ukiwekwa chini ya sufuria yenye maji, yale maji ni lazima yatokote, Vivyo hivyo na moto wa Roho ukiachiliwa ndani ya mtu..Ni lazima atatoka na kwenda kuwahubiria injili wengine, hawezi kutulia..Na hicho ndicho kilichotokea ile siku ya Pentekoste mitume walipopokea ubatizo huu, muda huo huo walianza kuhubiri kwa kasi sana.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?

MELKIZEDEKI NI NANI?

SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

JIBU: Kwanza ni muhimu kufahamu kwamba ziwa la moto waliandaliwa shetani na malaika zake,(wale walioasi pamoja naye), kutokana na makosa waliyoyafanya huko nyuma kabla ya mwanadamu kuumbwa, ambapo shetani pamoja na kuonywa na Mungu abaki katika kweli lakini hakutaka, akaandaliwa adhabu hiyo,Na vivyo hivyo wanadamu ambao hawataki kukaa katika ile kweli, wao pia watatupwa katika lile ziwa la moto.

 lakini pia ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hamchomi shetani au mwanadamu kwenye ziwa la moto kama kuwakomoa au kuwakomesha au kuwalipizia kisasi, hapana! bali Bwana anafanya vile ili kuondoa uovu karibu naye kwasababu yeye ni mtakatifu, ili kuelewa zaidi tafakari mfano ufuatao, Wewe ni msafi hupendi uchafu halafu inatokea kuna uchafu umejitokeza pembeni yako au karibu na makazi yako, uchafu huo unakuletea harufu mbaya, na kichefuchefu, na kukufanya ujisikie vibaya sana, dawa pekee ya kuutoa uchafu huo ni lazima itakuwa ni kuukusanya pamoja na kwenda kuutupa au kuuchoma moto? swali ni je! umeuchoma uchafu huo kwasababu unakisasi nao? au kwasababu unataka kuukomoa? jibu ni hapana!! unauchoma uchafu kwasababu umekaa mahali pasipo stahili na wewe huwezi kuchangamana na uchafu, kwahiyo itabidi utengeneze tanuru ili kuundoa uchafu huo. Kadhalika na Mungu pia, yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu, biblia inasema tutakuwa watakatifu kwasababu yeye Mungu ni mtakatifu

1 Petro 15: 15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;

16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.

17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.  

Unaona hapo sababu pekee ya Mungu kuuteketeza Roho zote zilizoasi katika ziwa la moto ni kwasababu yeye ni MTAKATIFU na hawezi kuchangamana na uchafu, hawezi kukaa mahali pamoja na uchafu, watu waovu hawawezi kuzirithi ahadi za Mungu, hawawezi kuketi pamoja naye, na kama unavyojua takataka ngumu ndiyo inayochelewa kuteketea zaidi kuliko ile laini kadhalika nafsi iliyojichafua sana na mambo maovu ndiyo itakayoadhibiwa sana kuliko ile iliyojichafua kidogo. 

Luka 12: 47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.

48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”. 

Hivyo adhabu ya shetani haiwezi kuwa sawa na ya mwanadamu, yeye atapigwa zaidi, na adhabu ya aliyeua watu 100 haiwezi kuwa sawa na aliyeua watu 10 n.k Lakini mwisho wa yote roho zote zilizoasi(shetani na wanadamu walioasi) zitakufa katika lile ziwa la moto, kwasababu hazina uzima wa milele, hiyo ndiyo mauti ya pili biblia inayoitaja katika (ufunuo 2:11,ufunuo 20:14). Kwahiyo tujitahidi tumwishie Mungu, tukijua kuwa ipo hukumu mbeleni inatungojea. 

Ubarikiwe sana. . jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=DaH7IK-F324[/embedyt]


Mada zinazoendana:

MBONA MUNGU ANARUHUSU WATU WAPATE SHIDA, ILHALI ANA UWEZO WA KUTUEPUSHA?

JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?

NI NANI ANAYETAWALA DUNIA KATI YA MUNGU NA SHETANI?

MUNGU MWENYE HAKI.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

JIBU: Neno Malkia wa mbinguni limeonekana mara mbili katika biblia

Sehemu ya kwanza ni katika Yeremia 7:18-20

18 Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.

19 Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema Bwana; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?

20 Kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, hasira yangu na ghadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya miti ya mashamba, na juu ya mazao ya nchi; nayo itateketea, isizimike.

Na pia ukisoma sehemu nyingine katika kitabu cha Yeremia utamwona akitajwa tena..  

Yeremia 44:17-23 ” Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.

18 Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba MALKIA WA MBINGUNI, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.

19 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?

20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema,

21 Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! Bwana hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?

22 Hata Bwana asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.

23 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya Bwana, wala hamkuitii sauti ya Bwana, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo. ”

Tunaona habari hizo zote mbili zinaelezea juu ya miungu ya kipagani iliyowasababishia Israeli kuingia matatizoni kwa kwenda kuifukizia uvumba, na kumbuka haina uhusiano wowote na ukristo, kwahiyo mbinguni Mungu anapoishi hakuna malkia, biblia inamtaja MFALME TU!, Naye ni mmoja na si mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA yeye peke yake.

Hivyo Mariamu sio malkia wa mbinguni, alikuwa ni mwanamke kama wanawake wengine waliokuwa wanamcha Mungu na kupewa neema ya kipekee ya kumzaa Bwana wetu Yesu, lakini hilo halina uhusiano wowote na yeye kuwa malkia, desturi za kuabudu miungu wake ni za kipagani na zilikuwepo tangu zamani AShtorethi/Semiramisi/Artemi mungu mke alikuwa anaabudiwa zamani zile na ndiye aliyekuwa anajulikana kama malkia wa mbinguni.   Kanisa katoliki ndilo lililobeba tamaduni hizi za kipagani kumwabudu Mariamu na kuwa kama kipatanishi kati yetu na Mungu ambayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.   Kwahiyo mkristo yoyote hapaswi kujihusisha na ibada potofu zinazotaja kuabudu miungu “wake”. Ni YESU KRISTO pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana

MARIAMU

YESU KRISTO NI MUNGU NA KAPITIA TUMBONI KWA BIKIRA MARIAMU SASA NI SAHIHI KUMUITA MARIAMU MAMA WA MUNGU?

ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA (MATHAYO 2) . ZILIWAKILISHA NINI?

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

JE! NI SAHIHI MTU KUNING’INIZA PICHA NYUMBANI MWAKO KAMA YA YESU?

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

MAVAZI YAPASAYO.


Rudi Nyumbani:


 

Print this post

Ni kweli mtu anaweza akafa lakini roho yake ikawa inatumika kama msukule (kumilikiwa na mtu fulani kwa wakati) mahali pengine?

JIBU: Biblia inasema mtu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu, (waebrania 9:27). Hivyo mtu akishakufa, amekufa hawezi kurudi tena. Lakini hiyo unayosemea kwamba mtu kafa halafu anatumika mahali fulani, kiuhalisia ni kwamba mtu huyo bado hajafa, Kwasababu mtu akishaenda kuzimu au peponi kurudi tena huku haiwezekani . bali mtu huyo anakuwa amehamishwa tu, roho yake bado ipo hapa hapa duniani pamoja na mwili wake sehemu fulani.. Huo ni uchawi tu wa shetani(watu wengine wanaita kiini macho) na mambo kama hayo yapo tu, Hivyo watu wa namna hiyo jinsi ya kuwatambua inahitaji macho ya rohoni, au kama sio hivyo basi ni kuomba kwa imani kwa jina la YESU KRISTO na mtu huyo atarudi (sasa hapo ni kulingana na imani yako mwenyewe).

Kwasababu biblia inasema yote yawezekana kwake yeye aaminiye. Kumbuka pia hayo mambo sio ya kuyahofia kana kwamba shetani anayomamlaka ya kujiamulia kumteka kila mtu kwa jinsi apendavyo. Hapana bali watu wanaokutwa na mambo kama hayo sehemu kubwa wanakuwa ni watu waliombali sana na Mungu, au walishajihusisha na uchawi hapo kabla katika maisha yao Ndiyo inapelekea wigo mwepesi zaidi kwa shetani kuwachezea jinsi apendavyo. Lakini sio kwa kila mtu anayemwona. Na pia kuna vifo vingine vinatokea, ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili baadaye Bwana aje kudhihirisha uweza wake, na mfano huo tunauona kwa Lazaro. Na watu kama hao nao hawawi wamekufa kabisa(yaani kwenda sehemu za wafu) hapana bali wanakuwa wamelala (japo hata hilo linawezekana kwa Mungu). Hivyo nao pia kwa jina la YESU wanaarudishwa na kuwa hai tena. 

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

JE!MUNGU ANAWEZA KULETA MAJIBU KUPITIA NGUVU ZA GIZA KAMA ALIVYOFANYA KWA MFALME SAULI?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO.(MATHAYO 8:21)?

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?

NGUVU YA UPOTEVU.

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.


Rudi Nyumbani:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Watakaodanganywa baada ya miaka 1000,watatoka wapi?

Swali linaendelea….Angali tunajua ndani ya ule utawala kutajawa na watakatifu tu? sasa hawa watu ambao shetani atawadanganya watatokea wapi kama tunavyosoma katika Ufunuo 20:7 “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.”

JIBU: Katika utawala wa miaka 1000 biblia inarekodi kuwa wenye dhambi watakuwepo, lakini dhambi haitatawala dunia kwasababu mkuu wa ulimwengu ule atakuwa ni MFALME WA AMANI yaani Yesu Kristo, tofauti na dunia ya sasa ambayo mkuu wa ulimwengu huu ni shetani. Hivyo Dhambi na wenye dhambi watakuja kuondolewa wote mara tu baada hukumu ya kile kiti cheupe cha Mungu ambayo itakuja mara baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha. Kwahiyo kama vile biblia inavyosema Kristo atatawala kwa fimbo ya chuma pamoja na sisi ukisoma..

Ufunuo 2:26 ″Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.”

(fimbo ya ni kwa ajili gani? na ni kwanini iwe ya chuma?. >> Ni dhahiri kuwa Ufalme wowote ni lazima uongozwe kwa mamlaka fulani, na utii chini ya kila kitakachoamriwa pasipo majadiliano wala mahojiano na ndivyo itakavyokuwa katika utawala wa Bwana wa miaka 1000, hivyo kwa yeyote atakayekaidi atalazimika kutumikia adhabu kali ). Hautakuwa utawala wa kimabavu bali ni wa amani na utaratibu lakini kwa watakaokuwa wanaenda kinyume na sheria ya MFALME (KRISTO) na watakatifu wake wataangukia laana. Kwa muda wako binafsi unaweza ukasoma Zekaria 14 yote, inaelezea adhabu zitakazowakuta mataifa yote wasiokwenda kumwabudu mfalme mwaka kwa mwaka Yerusalemu,

Ukisoma pia Isaya 65:17-20 Inasema..;

“17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.

18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.

19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.

20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; BALI MTENDA DHAMBI MWENYE UMRI WA MIAKA MIA ATALAANIWA.”

Hivyo tunaona atakayetawaliwa hapo kwa fimbo ya chuma sio mkristo bali watakuwa ni watu wengine watakaokuja kuzaliwa ndani ya huo utawala wa miaka 1000. Na ndio maana huo mstari unasema “mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa” ikimaanisha kuwa ndani ya huo utawala kutakuwa na makundi mchanganyiko. Kwasababu kumbuka ile siku ya mwisho ya Bwana inayowaka kama Tanuru, atakayokuja pamoja na sisi(Bibi-arusi) kuuharibu ulimwengu wa sasa haitamaliza watu wote bali kuna watu wachache sana watakaosalia,soma Isaya 13:9-13

Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;

12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.

13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.”

Umeona hapo watu wataadimika kuliko dhahabu,ni jinsi gani watakavyobaki wachache sana na hao ndio watakaopata neema ya kuingia katika utawala wa miaka 1000 katika miili yao ya asili( Na hawa ndio watakaokuwa wakizaa na kuzaliana) lakini sisi tutakao kuja na Kristo kutakuwa hakuna kuzaa wala kuzaliana kwa sababu tutakuwa na ile miili ya utukufu iliyotoka mbinguni. Na pia wale waliouawa na mpinga-kristo (wanawali wapumbavu) nao watafufuliwa na kuhukumiwa kisha wataingia katika utawala wa miaka 1000. Ufunuo 20:4.

Sasa baadhi ya hawa watu (watakaozaliwa kwenye huu utawala) baadaye Shetani atakapokuja kufunguliwa kuwajaribu, shetani atawadanganya ndio watakaotaka kufanya vita dhidi ya watakatifu, kama biblia inavyosema moto utashuka kutoka mbinguni na kuwameza wote. ndipo hukumu ya kiti cheupe itafuata kwenye ufufuo wa pili. ambapo waovu wote watahukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto pamoja na shetani na kisha tutaingia katika umilele ambapo dhambi haitakuwepo tena wala waovu.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?

Wale Watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu WALIKUWA WAPI KABLA YA KUFUFUKA kwao je! walikuwa Peponi au ni wapi?.

Je! ni kweli dunia iliumbwa takribani miaka 6000 iliyopita? na je! Shetani alikuwepo duniani wakati dunia inaumbwa?

JINA LA MUNGU NI LIPI?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

JIBU: Hili ni swali watu wengi wanajiuliza ni Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, badala yake akamwacha Hawa ajaribiwe na yeye?.

Tunapaswa tufahamu wakati mwingine Mungu anaruhusu sisi wanadamu tujaribiwe kwa makusudi maalumu ili tuujue uweza wake na asili yake kwetu sisi na pia tumjue yeye zaidi, kwamfano jaribu kufikiria tungemjuaje kama yeye ni mwokozi kama tusingepotea katika dhambi?, tungejuaje yeye ni mponyaji kama tusingeumwa, tungejuaje yeye ni wa rehema kama tusingeanguka, tungejuaje yeye ni wa neema kama tusingekuwa hatuna haki, tungejuaje yeye ni mwenye msamaha kama tusingekuwa na makosa n.k…

Kumbuka pia sikuzote dhahabu ili ing’ae lazima ipitishwe kwenye moto mkali ijaribiwe na sisi kama watoto wa Mungu ni lazima tujaribiwe na ndio maana Mungu hakumuua shetani. Hata tulipokuwa shuleni, lengo la mwalimu kututungia mitihani migumu sio kutufanya sisi tufeli, hapana bali ni kutuimarisha zaidi ili tuweze kukabiliana na changamoto za mbeleni. Na ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni.   Mungu ana makusudi makubwa sana na sisi chini ya jua na ndio maana anatupitisha katika njia hiyo. Tunachopaswa kufahamu ni kuwa siku zote Mungu anatuwazia mawazo yaliyo mema  

Yeremia 29:11 ” Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”  

Yote haya Mungu kayaruhusu ili kutuwekea msingi mzuri wa maisha yajayo matamu ya umilele yasiyokuwa na mwisho.   Hiyo ndio sababu kwanini Mungu hakumuua nyoka mwanzoni kabisa pale Edeni kabla hajaasi.

Zaburi 103:12 “Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. 13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao. 14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. 15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo”.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

UZAO WA NYOKA.

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?

CHANZO CHA MAMBO.


Rudi Nyumbani:

Print this post