Title September 2019

Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema katika 1Wakorintho 15:31″…NIKAKUFA KILA SIKU?

JIBU: Katika ukristo KUFA kupo kwa namna mbili:  

>Aina ya kwanza ni kufa kwa habari ya dhambi.  

>Aina ya pili ni kufa kwa ajili ya Ndugu: Yaana kuwa tayari kuiponza roho yako, mpaka kufikia hatua ya kuweza kuitoa roho yako kwa ajili ya injili na kwa ajili ya Kristo.  

Ukristo sio wa leo na kesho halafu basi, Tunapokuwa wakristo inamaanisha tunajikana nafsi zetu kila siku, na kumwishia Mungu siku zetu zote zilizobakia na ndio maana Bwana YESU alisema:

Luka 9:23 “ Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate.

24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.”  

Unaona hapo, ni kuchukua msalaba wako na kumfuata KILA SIKU na sio siku moja au mbili kisha basi. Kwa lugha iliyo rahisi ni kwamba kila siku unapaswa UFE kwa habari ya ulimwengu na uwe hai kwa habari ya Kristo.

Unakufa kila siku kwa habari ya fashion za ulimwengu huu, unakufa kila siku kwa kampani za marafiki wabovu, unakufa kila siku kwa habari ya matusi, kila siku unakufa kwa habari ya uasherati na tama zake kwa kujiweka mbali nazo, unakufa kwa habari ya rushwa, unakufa kwa habari ya usengenyaji, na anasa n.k.  

Kadhalika pia tunapoona ndugu zetu walio wachanga na wanahitaji msaada wa kiroho wa injili kutoka kwetu nasi tunajua kabisa tusipofanya hivyo wataangamia, hapo pia tunagharimika kuwaendea kwa gharama zozote zile bila kujali ni hatari gani tutakumbana nayo huko mbeleni kama vile mtume Paulo alivyokuwa anasema..Bila kujali jamii itakutenga vipi, bila kujali serikali itapingana nawe vipi, bila kujali watu wenye chuki watakuvizia muda wowote kukuua, bila kujali watu wa dini wanakuchuliaje n.k.   Sasa huko ndio KUFA KILA SIKU WA AJILI YA KRISTO.

Lakini ikiwa maisha yetu kila siku yatakuwa hivyo hayana mabadiliko yoyote, kila siku tunaonakena hatuna tofuati na watu wa ulimwengu. Hiyo ni dalili tosha kutuonyesha kuwa bado hatujamfauta Kristo..

  Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

NJIA YA MSALABA

AGIZO LA UTUME.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

NGURUMO SABA

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia inasema usiongeze wala usipunguze Neno la Mungu, huko kuongeza na kupunguza kukoje?

JIBU: Hata katika hali ya kawaida mtu anapozungumza maneno mengine ya uongo ambayo wewe hujasema mtu huyo ni sawa na kakuongezea maneno… Kwamfano mtu anapokwenda kutoa ushahidi mahakamani ya kwamba amekusikia ukisema maneno Fulani na angali wewe hujasema hayo maneno,na anafanya vile kwa makusudi mtu huyo atakuwa ni kama amekuongezea maneno, Vivyo hivyo na kwa Mungu mtu anapotoa ushuhuda wa uongo kuhusu Mungu, au anapofundisha jambo la uongo kinyume na Neno la Mungu na anafanya vile makusudi kwa nia ya kupotosha, mtu huyo ni sawa na ameongeza neno katika maneno ya Mungu na Biblia inasema ataongezewa mapigo katika siku ile (Ufunuo 22:18).  

Kwamfano maandiko yanasema “Mtu ameandikiwa kufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu Waebrania (9:27)” Lakini inatokea mwalimu au mtumishi analijua hilo andiko na maana yake lakini badala ya kuwafundisha watu hilo, anawapotosha na kuwaambia hakuna hukumu baada ya kufa, au mtu baada ya kufa anakwenda toharani kutakaswa kisha mbinguni baadaye hata kama alikufa katika dhambi, Hivyo anaendelea kuwafariji watu wazidi kudumu katika dhambi zao..huyo ni sawa na ameongeza Neno katika maneno ya Mungu..  

Kadhalika kupunguza maneno inatokea pale mtu anapoujua ukweli na hauhubiri wote kama inavyopaswa, pengine kwa hofu Fulani, au kwasababu anaogopa kutengwa, au kuchukiwa…mtu kama huyo ni sawa na amepunguza Neno kati ya maneno ya Mungu, na hivyo atapunguziwa sehemu yake (yaani thawabu yake) katika ule mti wa Uzima, na katika ule mji Mtakatifu Yerusalemu ya Mungu katika siku ile.(Ufunuo 22:19).

  Kwamfano Maandiko yanasema Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; KWA MAANA KILA AFANYAYE MAMBO HAYO NI MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO. (Kumbu.22:5), sasa kwamfano Mwalimu, au muhubiri au mchungaji, akilijua hili na hawafundishi wanafunzi wake , au washirika wake,mambo kama hayo kwa hofu Fulani labda watamchukia, au watamkimbia sasa mtu kama huyu ni sawa na amepunguza Neno katika Maneno ya Mungu na hivyo sehemu yake pia itapunguzwa katika mji ule.

  Kwahiyo tunapaswa tulichukue Neno la Mungu kama lilivyo bila kupunguza makali yake, au kuongeza shuhuda zipinganazo na Neno la Mungu kwa lengo la kuwapotosha watu.  

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.

TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

UMEFUNULIWA AKILI?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Biblia inasema askofu anapaswa awe mume wa mke mmoja! Je! Wale wasiooa kwa ajili ya injili hawawezi kuwa maaskofu?

1 Timotheo 3:1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja,..” 


JIBU: swali zuri, na pia wengi wanachanganyikiwa kuhusu hilo, wakidhani kuwa mtu yeyote anayeitwa askofu ni lazima aoe…lakini unapaswa uelewe kuwa hapo Mtume Paulo alisema hivyo kwa mantiki ipi?, hakuwalenga wale ambao hawajaoa bado hapana, bali aliwalenga wale ambao wanao wake zaidi ya mmoja..kwamba hao ndio hawapaswi kuwa maaskofu, kwasababu ni lazima waonyeshe kielelezo kwanza wao wenyewe katika nyumba zao na ndio waje kuchunga wa nje, sasa kama mtu alikuwa na wake 6 kabla hajaamini na akaingia kwenye ukristo na ukristo unasema mtu anapaswa awe na mke mmoja, sasa unadhani wale atakaowachunga yeye kama askofu atakuwa anacho kielelezo gani? 

Na ndio maana haipaswi mtu yeyote anayeitwa askofu au mchungaji awe na mke zaidi ya mmoja…Lakini haikumaanisha pale kwamba ni lazima kila anayetaka kuwa askofu awe na mke, huo ni uelewa hafifu wa maandiko. Kumbuka mtume Paulo naye hakuwa na mke, lakini alikuwa mwangalizi wa makanisa yote, Kristo naye hakuwa na mke lakini yeye ndiye Askofu wa maaskofu. Hivyo hapo maneno hayo yaliwalenga wale ambao tayari wanao mke zaidi ya mmoja. 

1Wakoritho 7:32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe

Ubarikiwe.

Maran atha


Mada zinazoendana:

MATOWASHI NI WAKINA NANI?

JE! NI VIBAYA KUTAJA HUDUMA KWA KUJIPA CHEO? MFANO MIGHTY PROPHET, CHIEF APOSTLE N.K.?

NITAMJUAJE NABII WA UONGO?

MLINZI, NI HABARI GANI ZA USIKU?

BIDII YA MFALME YOSIA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?

JIBU: Sherehe yoyote ile iwe ni ya kuzaliwa, au mahafali, maadhimisho ya miaka ya ndoa, harusi, kumbukumbu n.k. Biblia haitatoa katazo lolote kufanyika, isipokuwa imetoa katazo tu kwa KARAMU ZA ULAFI.

Tukisema karamu za ulafi tunamaanisha karamu/sherehe zozote zinazovuka mipaka ya Neno la Mungu, kwamfano sherehe zinazochanganyikana na pombe,Disco, miziki ya kidunia, uvaaji mbovu, na mambo yote yafananayo na hayo ambayo ni kunyume na Neno la Mungu, hizo zote ni karamu za ULAFI ambazo biblia imezikataza. Ukisoma..  

1Petro 4: 3 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na KARAMU ZA ULAFI, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;”  

Unaona hapo pia ukisoma …  

2 Petro 2: 13 “Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu WAKIFUATA ANASA ZISIZO KIASI KATIKA KARAMU ZAO ZA UPENDO, wafanyapo karamu pamoja nanyi; ”

  Unaona pia hapo karamu/sherehe zenye mambo kama hayo ndani yake ni dhambi kwa mkristo kufanya, lakini ikiwa ni kwa ajili ya kuhitimu, au kuzaliwa, au ndoa, au mahadhimisho unaweza ukasheherekea upendavyo lakini hapo ndio kuzingatia lile neno linalosema Wakolosai 3: 17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.  

Na ndio maana Bwana YESU alitushauri pale tunapojisikia kufanya karamu au kusheherekea kwa namna yoyote ile tufanye kwa manufaa ya kimbinguni zaidi, yaani kuliko kuwaalika watu wenye cheo, ni vizuri kusheherekea na watu maskini, ili thawabu yetu iwe kubwa mbinguni (Luka 4:12)..Kuliko kukata keki na ndugu zetu au na marafiki zetu tu, ni vema tukaongeza pia kukata na yatima waliokaribu nasi pamoja na wajane.. Ndio karamu yenye harufu nzuri mbele za Mungu.

  Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

NI SAHIHI KUMUITA MARIAMU, MAMA WA MUNGU?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUNING’INIZA PICHA NYUMBANI MWAKO KAMA YA YESU?

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

KARAMA ILIYO KUU.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?

JIBU: Kufunga ndoa ni agizo la Mungu, lakini Harusi ni karamu/sherehe ya Ndoa mpya. Na hizo ni desturi tu ambazo zipo katika mataifa mbalimbali kulingana na chimbuko lao. Hata taifa la Israeli walikuwa na desturi za harusi ukisoma

Yohana 2:1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
2.2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

Hivyo ikiwa ndoa mpya itaambatana na harusi kwa Mungu hakuna dhambi, wala hakuna maagizo yoyote kwenye biblia kwamba mtu akioa au akiolewa ni lazima afanyiwe harusi au asifanyiwe…Ni jinsi mtu mwenyewe atakavyopenda isipokuwa tu, tumeagizwa lolote tufanyalo kwa Neno au kwa tendo tufanye kwa jina la Yesu Kristo. Ikiwa na maana kuwa hiyo arusi isivuke vigezo vya kikristo.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

NDOA NA TALAKA:

BIBLIA INAKATAZA KUAPA, LAKINI KATIKA VIFUNGO VYA NDOA?

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?

NINI TOFAUTI KATI YA UZINZI NA UASHERATI?

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?.


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?

JIBU: Biblia haijaeleza moja kwa moja kuhusu suala la uzazi wa mpango aidha utumike au la, kwasababu njia zinazotumika sasa hazikuwepo katikati ya watu wa kale, Lakini ni vizuri kufahamu lengo la kufanya hivyo ni nini, wapo wengine wanafanya hivyo kwasababu ya matatizo ya kiuchumi, wengine kwasababu ya mapungufu ya kimwili, wengine kwasababu ya kuzuia kuathiriwa kwa kazi yake Fulani, na pia wapo wengine ni kwasababu tu za kiasherati/zinaa n.k..

  Hivyo njia nyingi za sasa zitumiwazo kwa uzazi wa mpango zinachukuliwa kwa taswira ya kiasherati kwasababu iko wazi nyingi zinatumiwa hivyo. Lakini ikiwa ni kwa wana ndoa, na dhamira zao zikiwa ni safi mbele za Mungu, na malazi yao ni masafi siku zote, na wanazo sababu za muhimu zinazowalazimu kufanya hivyo labda kwasababu za uleaji wa watoto n.k. Si dhambi wanaweza kutumia. Kwasababu kumbuka pia maandiko yanasema Katika

1Timotheo 5: 8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”.

  Unaona hapo? Uzaaji wa watoto usio na mpango, hususani pale usipokuwa na uwezo wa kuwalea, ni sawa na umeikana Imani. Hivyo ni vizuri kama wewe ni mwanandoa, ukae chini katika maombi na kumuuliza Mungu, na mapatano na mwenzako, na kisha zitumike.

Lakini mambo hayo hayamuhusu mtu asiye mwana-ndoa.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOANA?

JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

WATU WASIOJIZUIA.

MWANZI ULIOPONDEKA.


Rudi Nyumbani:

 

Print this post

Kunena kwa lugha kukoje?

KUNENA KWA LUGHA. 

Kuna aina nyingi za lugha, zipo lugha za wanadamu na lugha za malaika, lugha za wanadamu ndio kama hizi tunazozifahamu na kuzizungumza; Kiswahili, kingereza, kiarabu, kizulu n.k..Na lugha za malaika nazo zipo nyingi, hatuwezi tukazielewa kwa upeo wetu wa kibinadamu.

 1Wakoritho 13: 1 “Nijaposema kwa LUGHA ZA WANADAMU na ZA MALAIKA, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao”.

 Sasa moja ya ishara kubwa kati ya nyingi ambayo Bwana aliichagua siku ile ya Pentekoste ijidhihirishe kama ushahidi kuwa Roho Mtakatifu amemwagwa juu ya watu wake ni ISHARA YA LUGHA. Kumbuka: angependa kutumia ishara nyingine pia angeweza, kama watu kutabiri, watu kung’aa nyuso zao kama Musa, n.k lakini yeye alipenda kutumia ishara ya lugha, kama tu alivyotumia ishara ya lugha kuwatapanya watu waliokuwa wanaujenga mnara wa Babeli. Sasa kilichotokea siku ile ya Pentekoste baada ya Roho Mtakatifu kushuka juu ya watu, watu kujikuta wanapata msukumo wa ajabu(au uwezo wa ajabu) kuzungumza lugha wasizozijua.

Na lugha hizo hazikuwa lugha za MALAIKA hapana! Bali zilikuwa ni lugha za WANADAMU. Ili tuelewe vizuri tujifunze kwa mfano ufuatao. Petro mwanafunzi wa Yesu alikuwa anaongea ki-galilaya lakini hawezi kuongea kiyunani, Roho aliposhuka juu yake siku ile ya Pentekoste, alisikia uwezo na msukumo wa ajabu ndani yake, na kujikuta anamtukuza Mungu kwa lugha nyingine pasipo kujua ile lugha anayoizungumza ni ya kiyunani. Na kadhalika Mathayo naye lugha yake ya asili ni ki-galilaya lakini nguvu ilipomjia akajikuta anamtukuza Mungu kwa lugha ya kiarabu, pasipo kujua kwamba anaongea kiarabu..na vivyo hivyo kwa wanafunzi wengine wote na wale wote waliokuwepo siku ile ya Pentekoste. 

Sasa wao pasipo kujua kwamba zile lugha wanazoziongea ni lugha halisi, wale watu wa nje ndio waliowasikia wanazungumza kwa lugha zao, labda tuseme kuliwepo na wayunani pale ghafla wanamsikia mtu akimtukuza Mungu huko ghorofani kwa lugha ya kiyunani, na hali anajua kabisa pale mjini wayunani wenzake ni wa kubahatisha, na Kadhalika kama palikuwepo na muarabu kafika pale mjini Yerusalemu kwa biashara yake, ghafla anamsikia mtu huko ghorofani anapaza sauti akimshukuru Mungu kwa lugha yake ya kiarabu, tena kiarabu kile cha ndani kabisa na hali anajua kabisa katika huo mji hakuna waarabu wenzake wengi, na cha ajabu akimtazama mtu anayenena hana hata dalili ya kufahamu tamaduni za kiarabu,ni wazi kabisa ataishia kuduwaa tu!. Sasa ndicho kilichotokea siku ya Pentekoste.

Ni mfano leo usafiri na kwenda Kijiji kimoja huko China, na wakati umefika huko, unamsikia mchina mmoja huko anaongea kichaga kile cha ndani kabisa, wakati unajiuliza hilo ni nini, unasikia mchina mwingine huko anamsifu Mungu kwa kimakonde! Bila shaka utashangaa na kujiuliza hawa wote si ni wachina! Imekuwaje basi mimi kuwasikia wakizungumza kwa lugha zetu za asili za kiafrika?. Sasa hiyo ishara ya lugha Bwana Yesu aliiachia siku ile ya Pentekoste ili watu wote wajue kwamba kuna kitu kipya kimemwagwa duniani (nacho si kingine Zaidi ya Roho Mtakatifu). Lakini Roho Mtakatifu mwenyewe sio lugha, kama tulivyosema hiyo ni ishara Roho Mtakatifu aliyoichagua tu kujidhihirisha yeye, anaweza akatumia ishara nyingine tofauti na hiyo, mtu akishindwa kuelewa hilo, atadhani kuwa asiponena kwa lugha basi hana Roho Mtakatifu ndani yake, Na ndio hapo inapelekea kulazimisha kufanya hivyo na asiponena mwisho wake anaishia kunena kwa akili zake tu, na sio kwa jinsi Roho anavyowajalia.

Kunena kwa lugha ni karama Roho wa Mungu anayoitoa kama yeye apendavyo na sio kila mtu anaweza kuwa nayo. Sasa nini kinatokea Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya Mtu?Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya mtu, hali atakayoisikia mtu yule kwa mara ya kwanza sio kunena kwa lugha, kwasababu lugha kazi yake ni ishara kwa watu wa nje wasioamini, kuwaonyesha kwamba kuna jambo jipya limeshuka juu ya huyo mtu, lakini kama Roho ameshuka juu ya mtu na yule mtu yupo peke yake, hakuna lugha hapo!.

 Jambo la kwanza atakalolisikia yule mtu ndani yake baada ya Roho Mtakatifu kushuka ni badiliko kubwa ndani ya moyo wake, atajisikia anaichukia dhambi, na maisha yake ya zamani, atajikuta anatamani na anakuwa na kiu ya KUWA MTAKATIFU, na huo ndio uthibitisho wa kwanza na sio kutamani kunena kwa lugha, au kuona maono, au kutabiri.Uthibitisho wa ROHO YA UASHERATI ndani ya mtu ni UASHERATI sio kuzungumza kingereza, vivyo hivyo uthibitisho wa ROHO YA MAUAJI ndani ya mtu ni MAUAJI anayoyafanya na sio elimu yake, huwezi kusema elimu ya mtu ndio uthibitisho wa Roho ya mauaji iliyopo ndani ya huyo mtu, Vivyo hivyo na ROHO MTAKATIFU kama jina lake lilivyo “MTAKATIFU” uthibitisho kwamba mtu yule anaye Roho Mtakatifu ndani yake ni UTAKATIFU ANAOUISHI, na sio lugha anazoziongea, Kwahiyo hizi lugha, ni ISHARA TU na Bwana anachagua nani wa kumpa hii na nani wa kumpa ile.

Hivyo jambo la kwanza mtu akipokea Roho Mtakatifu ni kuanza kuona ile kiu ya kupenda dhambi inakufa, anaanza kupenda kuwa MTAKATIFU na kuishi maisha ya kumcha Mungu, Sasa vya ziada ndio hizo ishara nyingine zinafuatana naye, labda anaona MAONO, lakini haneni kwa lugha, sasa mtu kama huyo anaweza akadhani hajapokea Roho Mtakatifu kwasababu tu hajanena kwa lugha, hajui kwamba Roho Mtakatifu yupo ndani yake, na amemchagulia ishara ya Maono iambatane naye badala ya ishara ya lugha.

Mwingine katubu dhambi na ghafla anaona kiu ya kupenda dhambi inakufa anatamani na anaanza kuishi maisha ya UTAKATIFU, lakini anajigundua kila anapolala anaota ndoto na zile ndoto zinakuja kutokea kama zilivyo, lakini hajanena kwa lugha, naye huyo Roho kapenda kumpa kipawa cha NDOTO badala ya lugha, Vivyo hivyo na wengine watapewa, karama za uponyaji badala ya LUGHA, wengine watapewa karama za unabii badala ya lugha, wengine watapewa karama neno la faraja, wengine karama za neno la maarifa, wengine watapewa uinjilisti badala ya lugha, wengine watapewa lugha badala ya uinjilisti, na maono, wengine waalimu, wengine wachungaji, N.k na wengine watapewa karama mbili mbili, wengine tatu tatu, wengine moja tu n.k Lakini wote hawatenena kwa lugha wala wote hawatakuwa manabii n.k na ndio maana Mtume Paulo ililisema hilo katika.. 

1Wakoritho 12: 28 “ Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.29 Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? WOTE WANENA KWA LUGHA? Wote wafasiri?”

Umeona hapo? Sio wote watanena kwa lugha. Hivyo usikazane kutafuta kunena kwa lugha, kama hiyo karama haipo ndani yako,[sisemi kama ukimwomba Mungu hatakupa,] lakini ikiwa haipo ndani yako zidi kujaa Roho Mtakatifu, na baki katika nafasi uliyoitiwa. 

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Print this post

Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?

JIBU: Kama tukisoma Marko 2: 17 tunaweza kuona Bwana Yesu aliwaambia watoza ushuru na Mafarisayo maneno haya, “…WENYE AFYA HAWAHITAJI TABIBU, BALI WALIO HAWAWEZI; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” Bwana alitumia mfano huo wa kidunia kueleza mambo ya rohoni, akimaanisha kuwa ni jambo la kawaida kwa mtu aliye mgonjwa kumtafuta daktari amuhudumie afya yake. Kwasasa tunaweza kusema kwenda hospitali. Hivyo mkristo kuumwa na kwenda hospitali hafanyi kosa lolote, maadamu anafanya tendo ambalo halimwathiri Imani yake.  

Kadhalika pia anaweza kutumia aina zozote za mimea ambazo anaweza kuona zitamsaidia kuimarisha afya ya mwili wake, mwingine anaona kutumia mwarobaini, au alovera ni nafuu zaidi kwake kuliko dawa za hospitalini kwasababu pia dawa nyingi za hospitalini zinatengenezwa kutoka kwenye hiyohiyo mimea ya asili. Lakini la kuzingatia mkristo anapotumia dawa hizo, hapaswi kuzihusisha na ibada zozote za Kiroho isipokuwa kwa Mungu wake.  

Kwamfano mtu anapewa dawa za miti shamba labda mwarobaini, halafu anaambiwa achinje kuku, au aweke uvunguni, au aseme maneno Fulani au afanye kafara kisha ndio anywe, sasa hizo tayari ni ibada za sanamu ambazo ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Lakini mtu akiwa na mwarobaini wake nyumbani, akatengeneza akanywa kwa jina la YESU hakuna tatizo lolote. Akizingatia tu lile Neno katika

Wakolosai 3: 17 “Na kila mfanyalo, KWA NENO au KWA TENDO, fanyeni yote KATIKA JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.

Lakini pia kuna mwingine kwa Imani yake anaamini kuwa Mungu ndiye mponyaji wake kwa asilimia zote pasipo kupitia nyenzo yeyote, hivyo anaposikia kuumwa anaamini kuwa Mungu atamponya pasipo kwenda hospitali, akiliamini lile Neno (Mathayo 8:17 “…Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” )

hivyo mtu wa namna hii pia hafanyi kosa, Kwasababu Mungu ni yule yule anayeweza kumponya mtu kwa kupitia daktari au pasipo daktari..Hapo ni kulingana na Imani ya mtu kwa Mungu wake.  

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

YESU MPONYAJI.

HADITHI ZA KIZEE.

MADARAKA YA WAKATI MKAMILIFU.

MKUU WA GIZA.

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je ni sahihi kulima mazao, ambayo hutumiwa kutengenezea pombe?

SWALI: Kwamfano tunajua kuna pombe zinazotengenezwa na mtama Je! ni sawa kwa mkristo wa kweli kulima mtama na kuuza na hata hiyo hela kuitumia kutolea sadaka?


JIBU: Hakuna zao lolote lililoumbwa na Mungu lenye ubaya wowote ndani yake, zao linafanyika kuwa baya pale tu linapotumiwa kwa matumizi yasiyo sahihi, kwamfano mtama ni zao la chakula, wengine wanatumia kama ugali, lakini baadhi ya watu wanatumia fursa ya zao hilo ili kuunda pombe. Hivyo mtu anayeligeuza zao kuwa hivyo , au kupanda kwa ajili hiyo, atakuwa na hatia mbele za Mungu.

Lakini zao lenyewe kama zao halina shida kama mtu akilipanda kwa ajili ya matumizi ya asili, kwasababu yapo mazao mengine mengi tu kwamfano zao kama miwa, ambayo ingetumiwa kutengenezea sukari wengine wanaundia pombe, minazi ambayo ingetumika kuzalisha nazi na mafuta wengine wanaigema kutolea pombe, ulezi na ndizi ambazo zingetumika kama chakula wengine wanatumia kutengeneza pombe n.k. Lakini biblia ilishasema katika, 

Isaya 5:20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; WATIAO UCHUNGU BADALA YA UTAMU, NA UTAMU BADALA YA UCHUNGU!.

Unaona hapo? Biblia imetoa onyo kali kwa wale wote wanaopenda kupundia, vitu ambavyo Mungu aliviumba vitumike ipasavyo katika uhalisia wake, Kuzalisha mtama kwa ajili ya kutengenezea pombe ni sawa na kutia uchungu katikati ya jamii badala ya utamu. Kuzalisha ulezi na ndizi kwa dhumuni la kuviuzia viwanda vya utengenezaji pombe, ni sawa na kutia uchungu katikati ya jamii badala ya utamu. Kadhalika na mambo mengine yote ambayo yangepaswa yatumike kwa matumizi ya asili lakini watu wanayageuza, kwamfano wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake ni sawa na kutia nuru badala ya giza..Bwana alishasema OLE WAO wafanyao hivyo. 

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

JE! TUNARUHUSIWA KUNYWA MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO KAMA PAULO ALIVYOMWAMBIA TIMOTHEO?

MATUMIZI YA DIVAI.

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

JE! MABALASI BWANA YESU ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA KWA KAZI HIYO TU?

JE! MTU ANAPOFUNGA KWA MUDA WA SAA 24,ANAPASWA KUNYWA MAJI AU KITU CHOCHOTE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?

SWALI: Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika hivi vifungu?

Luka14:26 “kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake,na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; na naam, na hata nafsi yake mwenyewe , hawezi kuwa mwanafunzi wangu ”.


JIBU: Bwana Yesu aliposema yeye “asiyemchukia” baba yake na mama yake, hakumaanisha, kumdharau, au kuweka uadui naye, hapana kwasababu Bwana Yesu hawezi kufundisha upande mmoja upendo na mwingine chuki, bali pale alimanisha kupenda mapenzi ya wazazi au ya mtu binafsi Zaidi ya mapenzi ya Mungu, mtu wa namna hiyo hawezi kuwa mwanafunzi wake.

Leo hii mtu atafahamu kabisa kuwa mlevi au kufanya matambiko ya kimila ni dhambi sawa sawa na Neno lake katika

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

lakini kwasababu mzazi wake anamshurutisha afanye vile kwasababu wazee wa ukoo wameagiza ,na asipofanywa hivyo atatengwa na ukoo, yeye anaamua awe mlevi, au apige ramli ili tu kuwaridhisha wazazi wake. Mtu wa namna hiyo biblia inasema hawezi kuwa mwanafunzi wa YESU.

Kadhalika Bwana anasema mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni, lakini mtu kwasababu dini ya wazazi wake haiamini hivyo, anaona vema abaki hivyo hivyo tu, angali akijua kabisa ubatizo sahihi ule wa kuzamishwa katika maji tele tena katika Jina la YESU KRISTO ndio Bwana anaouhitaji kwa mtu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake, lakini yeye hataki kutii akiwaogopa wazazi au ndugu zake..Sasa mtu kama huyu hawezi kuwa mwanafunzi wa YESU.

Na maagizo mengine yote Bwana aliyotupa, hatupaswi tutazame kwanza wanadamu wanatoa maoni gani kuhusu hayo.Kama ni Bwana kasema moja kwa moja tunatii pasipo kuwatazama wanadamu wanasema nini.

Ili kufanyika wanafunzi kweli kweli wa Kristo hatuna budi kuingia gharama, Hivyo Bwana atupe rehema tuweze kuzishinda hatua zote.

Amen.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP

Mada zinazoendana:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

UBATILI.

WANA WA MAJOKA.

RACA


 

Rudi Nyumbani:

Print this post