Monthly Archive Septemba 2019

Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?

JIBU: Hilo neno SHEHE lisikusumbue sana..kama tunavyofahamu lugha yetu ya Kiswahili maneno mengi yametoholewa kutoka katika lugha ya kiharabu..kwamfano neno shukrani, marhaba, salamu, sultani, sadaka, simba, msalaba,jehanamu, sheria, raisi,uasherati, hekalu, adhabu, adui, askari, lawama, dhamira,roho,damu, giza, tufani n.k. theluthi ya Lugha ya Kiswahili ni kiharabu.  (Hivyo kuna Neno shehe katika biblia pia)

Sasa kwasababu waarabu walikuwepo katika nchi yetu huku zamani zile na lugha yetu ilikuwa bado haijajitosheleza hivyo tukajikuta tunatumia maneno yao katika lugha zetu, na sio kiharabu tu hata na lugha nyingine za kigeni za watu waliotawala nchi yetu… Kwahiyo hilo neno SHEHE asili yake ni kiharabu, likiwa na maana ya Kiongozi, au mwalimu hususani anayehusiana na mambo ya kidini..na ndio maana ukisoma katika tafsiri nyingine za biblia mfano za kiingereza utaona linatumiwa neno Lords, or rulers badala yake…Neno hili unaweza ukaliona katika kitabu cha Yoshua 13:3,21, 17:7, 1Samweli 5:7,11, 6:4, Ezra 9:2 Nehemia 2:16.

Hivyo kwasababu ni Neno la kiharabu viongozi wa dini ya kiislamu walilitumia sana katika dini yao na ndio maana linaonekana kama ni neno la kiislamu lakini kiuhalisia sio..   kadhalika kama tu neno Rabi ni neno linalomaanisha mwalimu kwa kiyahudi, lakini kwasababu ni neno la lugha ya kiyahudi na linatumiwa sana na viongozi wa dini ya kiyahudi basi inachukuliwa hivyo mtu yeyote anayejiita Rabi yeye ni kiongozi wa dini ya kiyahudi lakini kiukweli sio hivyo hata kiongozi wa dini nyingine yoyote tofauti na ya kiyahudi anaweza kuitwa Rabi kwasababu maana halisi ya neno Rabi ni mwalimu…  

Kadhalika na Neno Mchungaji limezoeleka kutumiwa na viongozi wa dini ya kikristo, na halitumiwi na wengine lakini kiuhalisia hata kiongozi wa dini ya kibuddha anaweza kuitwa mchungaji.. Na ndivyo ilivyo hata kwa Neno shehe, kwahiyo pale katika maandiko neno hilo linasimama kama kiongozi wa imani wa dini husika kwa wayahudi na kwa wasio wayahudi.…  

Na pia katika agano jipya halijatumika sana hilo neno lakini badala yake yametumika maneno kama waalimu na wachungaji lakini kwa lugha ya kiharabu ndio hao hao.  

Ubarikiwe sana.


Mada zinazoendana:

KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?

IMANI “MAMA” NI IPI?

UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.

EPUKA KUTOA UDHURU.

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

UFUNUO: MLANGO WA 11


Rudi Nyumbani:

Print this post

SAYUNI ni nini?

JIBU: Tukirudi Mwanzo kabisa Daudi alipoenda kuiteka Yerusalemu,na kufanikiwa eneo lile liliitwa ngome ya SAYUNI (2Samweli 5:7).Hivyo Sayuni kwenye biblia imetumika kama Mji wa Daudi au Mji wa Mungu (YERUSALEMU).. 

Kadhalika na lile eneo la mlima ambalo hekalu la Mungu lilijengwa liliitwa pia mlima Sayuni, ambalo lipo hapo hapo Yerusalemu (Yeremia 31:6,12). 

Sehemu nyingine biblia imetaja Sayuni kama watu wa Mungu yaani wayahudi;

 Isaya 60: 14 “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako [Israeli] na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli” 

Unaweza kuona hapo. Kadhalika ukisoma pia (Zakaria 9:9, Sefania 3:14-19),biblia inamtaja Israeli kama binti Sayuni. Yote haya yanaonyesha pia Wayuhudi mbele za Mungu ni sawa na SAYUNI yake. Lakini tukirudi katika agano jipya neno Sayuni limezungumziwa kama ufalme wa watu wa Mungu wa rohoni. 

Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,” 

Hapo Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho anaonyeshwa Sayuni hasaa ambayo Mungu aliikusudia kwa watu wake tangu zamani yaani hiyo Yerusalemu ya mbinguni kanisa la Mungu. Mtume Petro pia aliandika katika…

 1Petro 2: 6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.”

 Habari hiyo nayo inathibitisha kuwa kanisa ndiyo Sayuni ya Mungu na ndio pia Yerusalemu ya mbinguni,..na tunafahamu Kanisa msingi wake ni Yesu Kristo, na hapo hiyo Sayuni jiwe kuu lake la pembeni linaonekana nI YESU KRISTO BWANA WETU. Kwahiyo na sisi pia tujitahidi tuwe na sehemu katika hiyo SAYUNI/ YERUSALEMU mpya ya Mungu ambayo Mungu alishaanza kuiandaa na anaendelea kuiandaa hapa hapa duniani. 

Ubarikiwe.

MLIMA WA BWANA.

JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

Rudi nyumbani:

Print this post