Category Archive Home

USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!

Jina la Bwana, Yesu libarikiwe.

Kuna tofauti ya Marhamu na Manukato, kujua tofauti yake fungua hapa >> Marhamu na manukato ni nini?.

Lakini kwaufupi ni kwamba Marhamu ni pafyumu.

Sasa maandalio ya wayahudi kabla ya kuzika, ilikuwa ni desturi ya kumpaka maiti Marhamu kichwani, kisha Manukato yanafungiwa katika sehemu nyingine ya mwili. Na manukato hayakuwa katika mfumo wa kimiminika.

Lakini tunaona Bwana Yesu alipokufa, Yusufu yule mtu Tajiri Pamoja na Nikodemo waliandaa tu Manukato!, bila Marhamu na kwenda kuyafungia ndani ya mwili wa Bwana Yesu.

Yohana 19:38 “Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake.

39 Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), AKALETA MACHANGANYIKO YA MANEMANE NA UUDI, YAPATA RATLI MIA.

40 Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na YALE MANUKATO, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika”.

Lakini desturi ni kwamba, Maiti lazima apakwe pia Marhamu.. Lakini hapa tunaona hawakufanya hivyo!. Na utaona wale wanawake  walipanga kurudia hilo zoezi la kuupaka uso wa Bwana Marhamu siku ya kwanza ya juma baada ya sabato kuisha!…wangeupaka siku ile ile lakini tayari sabato, ilikuwa imeshaingia na kulingana na desturi za wayahudi, ilikuwa si ruhusa kufanya shughuli yoyote siku ya sabato!, hivyo ikawapasa wasubiri mpaka jumapili asubuhi.

Lakini chaajabu ni kwamba asubuhi walipokwenda wakiwa na Marhamu zao, Pamoja na manukato mengine hawakumkuta Bwana kaburini..Hivyo Marhamu zao zikawa hazina kazi tena!.

Luka 23:54 “Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.

55 Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa.

56 Wakarudi, wakafanya tayari MANUKATO NA MARHAMU. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.

Luka 24:1 “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.

2 Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,

3 Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu”.

Umeona hapo?.. wenyewe walikuja kwa lengo la kuupaka uso wa Bwana Yesu  marhamu na  mwili wake kuufungia manukato!, lakini hawakumkuta!..walikuwa wamechelewa.. Kumbe nafasi ya kumpaka Marhamu kichwani ilikuwa ni kipindi yupo hai!, si kipindi amekufa kama wafu wengine wanavyofanyiwa..

Na utaona yule mwanamke wa kwanza alipata huo ufunuo, na akawahi kumpaka Bwana Marhamu ya thamani kichwani mwake, na Bwana Yesu akawaambia watu “AMEFANYA VILE KUMWEKA TAYARI KWA MAZIKO YAKE”..Na popote injili itakapohubiriwa.. itahubiriwa kwa kumbukumbu lake!.

Mathayo 26:6 “Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,

7 MWANAMKE MWENYE KIBWETA CHA MARHAMU YA THAMANI KUBWA ALIMKARIBIA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE ALIPOKETI CHAKULANI.

8 Wanafunzi wake walipoona, wakachukizwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?

9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini.

10 Yesu akatambua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi.

11 Kwa maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote.

12 MAANA KWA KUNIMWAGIA MWILI WANGU MARHAMU HIYO, AMETENDA HIVYO ILI KUNIWEKA TAYARI KWA MAZIKO YANGU.

13 Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake”.

Na kwa heshima yake, utaona Bwana Yesu alipofufuka, vile vitambaa vya sanda vilifunguliwa na kuachwa pale, lakini ile LESO ya kichwani, maandiko yanasema “ilizongwa zongwa pembeni (Yohana 20:7)”.. maana yake ilikunjwa vizuri na kuwekwa pembeni..

Sasa kwanini ikunjwe na kuwekwa pembeni?, ni kuonesha uthamani wa leso ile, kwamba isitupwe, bali iwekwe ije itumike tena!!..kwasababu bado inafaa kwa matumizi, na kufaa huko ni kutokana pia na ile Marhamu yule Mwanamke aliyompaka Bwana siku chache nyuma kabla ya kufa kwake!

Nini tunajifunza hapo?

Kuna wakati unaofaa wa kumfanyia jambo Bwana, na pia upo wakati usiofaa!!.. Ukipata nafasi ya kumtolea Bwana fedha zako, au mali zako, au muda wako.. Mtolee sasa usingoje siku Fulani mbeleni ifike. Huo muda unaoungoja ukifika, utakapokwenda kumfanyia Bwana huduma utakuwa sio muda unaofaa..

Akina Mariamu Magdalene na wenzake, ni kweli walikuwa wana nia nzuri ya kwenda kumpaka Bwana Marhamu lakini walikuwa wamechelewa, Bwana havihitaji tena hivyo vitu kwa wakati huo!!…

Aliwaambia wale watu, “maskini mnao siku zote, lakini mimi hamnami siku zote”.

Ndugu, Watoto wako unao siku zote, ndugu zako wenye shida unao siku zote, Rafiki zako wenye matatizo unao siku zote, lakini kazi ya Bwana haipo kwako siku zote!, mfanyie Bwana kitu leo usingoje kesho.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

LIPI TUNAJIFUNZA KWA WALIOMWONA YESU ALIYEFUFUKA?

LIPI TUNAJIFUNZA KWA WALIOMWONA YESU ALIYEFUFUKA?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?

Rudi nyumbani

Print this post

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?

1) Marhamu ni nini?

Marhamu kwa lugha ya kiingereza ni “perfume”..kwa lugha ya kiswahili iliyozoeleka ni “pafyumu”. Pafyumu inatengenezwa kutoka katika mimea mbali mbali na inakuwa katika mfumo wa kimiminika, matumizi yake ni kukifanya kitu kiwe  chenye kutoa harufu nzuri, na kufukuza wadudu na baadhi ya viumbe viharibifu, Viwango na ubora wa pafyumu (marhamu) unatofautiana.

Zipo Marhamu za gharama kubwa, ambazo hazipungui nguvu yake ya harufu haraka! (Mfano wa hizo ndio zile Bwana Yesu alizopakwa kichwani na yule mwanamke, kipindi yupo nyumbani mwa Simoni, mkoma).

Mathayo 26:6 “Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,

7 mwanamke mwenye KIBWETA CHA MARHAMU YA thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.

8 Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?

9 Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini”.

Na zile akina Mariamu, Magdalene walizoziandaa kwaajili ya kumpaka Bwana siku ile ya kwanza ya juma

Luka 23:56 “Wakarudi, wakafanya tayari manukato na MARHAMU. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa”.

Lakini pia zipo Marhamu za gharama ndogo!, ambazo hazidumu sana katika mwili wa mtu.

Kwa urefu juu ya Marhamu Mwanamke aliyompaka Bwana kichwani na ujumbe wake kiroho unaweza kufungua hapa>> MARHAMU KICHWANI MWA BWANA

2) Manukato ni nini?

Manukato ni viungo ambavyo havipo katika mfumo wa kimiminika, ambavyo vikichomwa, au kupikwa au kuwekwa mahali basi vinatoa harufu Fulani inayovutia, au inayowakilisha jambo Fulani. Mfano wa manukato ni UDI, UVUMBA, na MANEMANE.. Kwasasa kuna maelfu ya aina za Manukato!

Kwa maelezo marefu kuhusu Manukato aina ya UVUMBA, na jinsi wakuhani walivyofukiza uvumba na ujumbe wake kiroho unaweza kufungua hapa >> KUVUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

LIPI TUNAJIFUNZA KWA WALIOMWONA YESU ALIYEFUFUKA?

MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!

Ratli/ Ratili ni nini katika biblia?

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Rudi nyumbani

Print this post

Moabu ni nchi gani kwasasa?

 1) Moabu ni nchi gani kwasasa? 2) Wamoabu walikuwa ni akina nani? 3) Na waamoni walikuwa ni watu gani na wa nchi gani?


1) Moabu ni nchi gani kwasasa?

Moabu ni Mji uliokuwepo maeneo ya nchi ya YORDANI kwasasa. Yordani ni nchi iliyopakana na Nchi ya Israeli kwa upande wa Mashariki.

2) Wamoabu walikuwa ni akina nani?

Asili ya Wamoabu na Waamoni ni kutoka kwa LUTU, aliyekuwa ndugu yake Ibrahimu (Baba wa imani). Mabinti wawili wa Lutu, walilala na Baba yao na kila mmoja kubeba mimba, Watoto hao waliozaliwa mmoja aliitwa MOABU na wa PILI aliitwa AMONI.

Mwanzo 19:30 “Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.

31 Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.

32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.

33 Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.

34 Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye.

35 Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.

36 Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.

37 Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.

38 Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo”.

3) Na waamoni walikuwa ni watu gani na wa nchi gani?

Kama tulivyosoma hapo Mwanzo 19:38, kwamba walikuwa ni kutoka uzao wa Lutu.

Taifa la Moabu ni moja ya mataifa yaliyolisumbua sana Taifa la Israeli, hususani katika safari yao ya kutoka Misri, utakumbuka Mfalme wa Moabu alimwajiri BALAAMU MCHAWI ili awalaani Israeli (yaani awaloge!).. lakini mpango huo ulishindikana!.

Bwana hakupendezwa na Taifa hilo, na alililaani.

Kwa maelezo marefu kuhusu Balaamu na uchawi wake unaweza kufungua hapa >> Balaamu mchawi

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

USIJITUMAINISHE JUU YA SIRA YAKO ANGALI UPO KATIKA DHAMBI.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Babeli ni nchi gani kwasasa?

KUSAMBAA KWA ROHO YA MPINGA-KRISTO.

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?

Marko 3:16 “Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;

17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo”.

Wana wa Zebedayo (yaani Yakobo na Yohana), walipewa jina hilo la Boarnege kwasababu ya ukaribu wao kwa Bwana.

Ikumbukwe kuwa ni wanafunzi watatu tu! Peke,e ndio waliobadilishwa majina na Bwana, na hao ni Petro, Yohana na Yakobo, Ambao biblia inawataja kama NGUZO! (Soma Wagalatia 2:9). Wakati Bwana akienda mlimani kusali hawa nao walikuwa Pamoja naye! (Soma Mathayo 17:1)..hawa walimpenda Bwana sana kuliko wale wanafunzi wengine 9 waliosalia.

Yakobo na Yohana ulifika wakati walikwenda kumwomba Bwana awaketishe mkono wa kuume na wa kushoto katika ufalme wake siku ile.

Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu”.

Umeona?

Hivyo hawa wana wa Zebedayo Pamoja na Petro siku zote walikuwa wanatamani kumsogelea Bwana sana, na Bwana aliijua mioyo yao!.

Kutokana na mapenzi hayo kwa Bwana, walikuwa ni watu wasiopenda kuona Bwana anakataliwa mahali popote!.. Utaona Petro, alimkata mtumwa wa kuhani mkuu sikio, kipindi ambacho walikwenda kumkamata Bwana. Halikadhalika Yohana na Yakobo walitaka Bwana ashushe moto kuwaangamiza watu wa Samaria kipindi kile walichomkataa.

Luka 9:51 “Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;

52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.

54 wanafunzi wake YAKOBO NA YOHANA walipoona hayo, walisema, BWANA, WATAKA TUAGIZE MOTO USHUKE KUTOKA MBINGUNI, UWAANGAMIZE; [KAMA ELIYA NAYE ALIVYOFANYA]?

55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]

56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.

Umeona hapo?.. Tabia hiyo ya “kutaka Moto ushuke kutoka mbinguni” ni tabia za KUNGURUMA.. Moto hauwezi kushuka kabla mbingu hazijanguruma, sauti ya Ngurumo ni sauti ya Hukumu iliyokaribu au ya adhabu!.

Hivyo Bwana aliiona tabia hiyo ndani yao, kwamba siku za mbeleni baada ya kuondoka kwake, watakuja kunguruma juu ya kazi zote za shetani, na kuziteketeza!.. kipindi hicho watakuwa hawafanyi vita juu ya damu ya nyama, kama walivyotaka kufanya juu ya hawa watu wa Samaria,(kutaka kuwaua kwa moto) bali wakati huo, watanguruma juu ya kazi zote za shetani katika ulimwengu wa roho na kuzichoma na kuwaacha watu wa Bwana huru!.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

NGURUMO SABA NI NINI?

KAMA VILE UMEME UTOKAVYO MASHARIKI UKAONEKANA HATA MAGHARIBI.

Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?

UFUNUO: Mlango wa 1

Maswali na Majibu

Rudi nyumbani

Print this post

Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?

SWALI: Naomba kuelewa kwa undani Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?


JIBU:

Mbinguni,

Sehemu nyingi Biblia inaposema mbinguni, huwa inamaanisha moja kwa moja kule Mungu alipo Pamoja Malaika zake, Kule ambako Bwana Yesu alikwenda kutuandalia makao. Mahali ambapo sisi kama watakatifu bado hatujafika hata mmoja.

Ndio mbingu ya Tatu, ambayo Mtume Paulo alinyakuliwa kuonyeshwa baadhi ya vitu vilivyopo kule vipo kule ambavyo havielezeki kibinadamu, kwasababu upeo wetu ni mdogo. (2Wakorintho 12:1-4)

Ni juu sana, ambako, hatuna maelezo ya kutosha kupaelezea, mpaka tutakapofika.

2Nyakati 6:18 “Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!”

Peponi/Paradiso:

Ni mbingu ya mangojeo, ambayo sio makazi yetu ya kudumu. Mtakatifu anayekufa sasa hivi anakwenda mahali panapoitwa Peponi/Paradiso, akisubiria, siku ya unyakuo ifike, arudi kaburini achukue mwili wake, kisha aungane Pamoja na wale watakatifu watakaokuwa hai wakati huo, na moja kwa moja safari ya kwenda mbinguni ianze, kule Bwana Yesu alipo.

Yule mwizi pale msalabani, Bwana alimwambia maneno hayo;

Luka 23:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.

Wengine wanaiita mbingu ya pili, lakini vyovyote vile iitwavyo, bado ni mahali pa mangojeo pa watakatifu, Ndio kifuani pa Ibrahimu, yule maskini Lazaro alikwenda (Luka 16:19-31), ndio kule ambazo zile Roho zilizo chini ya madhahabu zilikuwa zinalia, zikiomba zilipiziwe kisasi kwa watesi wao.

Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.

Vilevile huku ndio kule wale wafu waliofufuka na Bwana Yesu walipoelekea kwa mara ya kwanza. (Mathayo 27:52-53)

Hivyo leo, hii ukifa katika Kristo, basi unakwenda katika eneo hili la mbingu, ambalo ni lizuri sana. Ukisubiri ufufuo wa mwisho.

Kuzimu:

Kuzimu kibiblia ni Neno lililomaanisha makao ya wafu  Au kaburini. Ambapo, waovu na wema walikuwa wanakwenda kabla ya Kristo kuja duniani, kuwatenganisha moja kwa moja kimakao,

Ayubu anasema

Ayubu 14:13 “Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!”

Daudi pia alipazungumzia, (Zaburi 16:10), kwamba Bwana hatomwacha huko milele.

Lakini baada ya Bwana Yesu kuja, wakatifu walitoka huko  makaburini, na kwenda peponi/ Paradiso. Mahali pa raha Zaidi pa juu na si makaburini tena. Hivyo wanaobakia makaburini au kuzimu ni waovu.

Jehanamu:

Ni mahali pa mangojeo pa waovu, ni mahali pa mateso, kama vile Paradiso palivyo mahali pa raha pa mangojeo kwa watakatifu, vivyo hivyo jehanamu nako, ni mahali pa mangojeo pa watu waovu wanaokufa sasa. Wanaadhibiwa huko, wakingojea siku ile ya hukumu ya mwisho ifike. Ili wapewe hukumu yao, katika hukumu ya kile kiti cheupe cha enzi cha mwanakondoo, kisha wakatupwe kwenye lile ziwa la moto, ambalo ndio mauti ya pili ilipo.

Ni sawa na mhalifu anayekamatwa sasa hivi, kabla ya kuhukumiwa kifungo, huwa anawekwa kwanza mahabusu, akisubiria siku ya kupandishwa kizimbani ifike, ahukumiwe kisha akatumikie kifungo chake Jela, Ndivyo ilivyo kwa watu waovu wanaokufa sasa, na waliokufa zamani. Wanakwenda katika sehemu hii ya mateso, ambayo si ya kawaida.

Bwana Yesu alisema..

Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [

46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]”

Je! Wewe ni wa makao yapi?

Swali, la kujiuliza ni Je! Tukifa leo, au Unyakuo ukitukuta leo, mimi na wewe tutakuwa wa upande upi? Katika mambo ambayo hupaswi kuyachukulia juu juu tu, basi ni mambo ya Maisha yako ya milele. Kwasababu ukishakufa hakuna nafasi ya pili tena. Kama umestahili Jehanamu basi utaendelea kuishi humo milele.

Ni heri ukamgeukie Kristo, maadamu muda mchache bado unao. Acha kutazama, mambo ya ulimwengu, kwani huwa yanapumbaza sana, kukufanya usione kama kuna mabaya yanakuja mbele, Moja ya hizi siku utajutia Maisha yako, uliishije endapo hukumpa Kristo Maisha yako leo.

Tubu dhambi zako, maanisha kumfuata Yesu.

Bwana atusaidie, kuyafahamu haya.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?

MILANGO YA KUZIMU.

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

Rudi nyumbani

Print this post

Babeli ni nchi gani kwasasa?

Eneo ambalo mji wa Babeli ulikuwepo, ni maeneo ya nchi ya IRAQ kwa sasa, Mji huu ndio uliokuwa maarufu kwa kuwa na “bustani zinazoelea”, lakini kwasasa mji huu haupo tena, wala maajabu yake hayapo!!,

kwasababu mji huo ulikuwa mji wa kishetani na ulifanya dhambi nyingi, na Mungu akauadhibu.. mahali ulipokuwepo pamebakia tu mbuga!!, sawasawa na unabii Mungu alioutoa juu ya mji huo.

Isaya 13:19 “Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.

20 Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.

21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko.

22 Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka”..

Kwahiyo leo hii hakuna kilichosalia pale!, pamebakia tu kuwa sehemu ya makumbusho ya kale.

Kumbuka shetani aliinyanyua Babeli ya kwanza, ambayo Mungu aliiharibu kwa kuchafua lugha za wajenzi wao!, na kazi ya ujenzi ikaishia pale! (Mwanzo 11), Lakini hakukata tamaa bali aliitengeneza Babeli nyingine, ambayo ndiyo iliyokuja kuangushwa na falme za Umedi na Uajemi, ikawa jaa!!

Lakini sasa shetani katengeneza Babeli nyingine ambayo ni ya KIROHO, hii iliyopo sasa ndio mbaya kuliko mbili zilizotangulia, na ndio kitovu cha machukizo na machafuko yote yan chi (sawasawa na Ufunuo 17).

Kwa urefu juu ya Babeli hiyo ya rohoni iliyopo sasa, fungua hapa >>> BABELI YA ROHONI.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

JE WEWE NI LAZARO YUPI, WA KWANZA AU WA PILI?

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)

TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.

Rudi nyumbani

Print this post

Yohana Mbatizaji alibatiza watu kwa jina gani?.

Tunasoma Matendo 2:38, kuwa watu walibatizwa kwa jina la YESU. Lakini biblia haijataja Yohana Mbatizaji alitumia jina gani kumbatizia Bwana Yesu, Pamoja na makutano waliomjia ili awabatize?.


Jibu: Yohana Mbatizaji hakutumia jina lolote katika Ubatizo. Ubatizo wake ulikuwa ni ubatizo wa Toba, ambapo baada ya watu kusikia mahubiri yake na kutubu, aliwazamisha kwenye maji mengi kwa ishara ya kuoshwa dhambi zao kwa maji. (Hakuna jina lolote lililohusika).

Lakini baada ya Bwana Yesu kuja, maandiko yanasema mambo yote tunayafanya kwa jina lake (Jina la Yesu).

Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, KWA NENO au KWA TENDO, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.

Umeona hapo?.. anasema lolote lifanyikalo kwa “Neno” au kwa “Tendo”.

Mfano wa mambo yafanyikayo kwa neno, ni kuomba, kutoa pepo, kubariki, kuimba, kutoa unabii n.k Hayo yote tunayafanya kwa jina la YESU. Ndio maana leo Pepo linatoka kwa jina la Yesu, vile vile tunapoomba tunatumia jina la YESU, n.k Mambo haya hapo kabla hayakuwepo, kwamba pepo linamtoka mtu kwa kutaja tu jina la mtu Fulani!.. Lakini yamekuja kuwezekana kwa mmoja tu, ambaye ni Bwana YESU, kwa jina lake tunafanya yote!.

Lakini sio hilo tu, bali maandiko yanasema pia, lolote tufanyalo kwa TENDO. Sasa mfano wa tendo, ndio huo Ubatizo!.) Kwamba tunazamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU. Yohana hakutumia jina la Yesu, ndio maana ubatizo wake ukakoma, lakini ubatizo wa jina la Yesu umedumu siku zote!! Na ndio unaoondoa dhambi!.

Matendo 19:1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;

2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.

3 AKAWAULIZA, BASI MLIBATIZWA KWA UBATIZO GANI? WAKASEMA, KWA UBATIZO WA YOHANA.

4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu

5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.

6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”.

Umeona hapo?. Watu hao walirekebisha ubatizo wao, wakabatizwa tena kwa jina la BWANA YESU

Na sisi leo hii hatuna budi kubatizwa kwa jina la Bwana Yesu ili tupate ondoleo la dhambi.

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Ubatizo ni nguzo muhimu sana na ya awali katika Ukristo, (Kila Mtu aliyemwamini Yesu ni lazima abatizwe). Na kumbuka lengo kuu la ubatizo sio wewe kupewa jina jipya. Hilo sio lengo la ubatizo, lengo la ubatizo ni kuzikwa kwa utu wako wa kale, na kufufuka katika upya.

Swali ni Je!  umebatizwa inavyopaswa kwa kuzamishwa na kwa jina la Bwana Yesu? Kama bado unasubiri nini?..Fanya hima ubatizwe ili uitimize haki yote!.na kumbuka pia ubatizo sio wa kunyunyiziwa wala wa uchangani, bali ni maji mengi! Na wa utu uzima.

Hivyo kama ulibatizwa pia utotoni, huna budi kubatizwa tena sasa, baada ya kujitambua, kwasababu wakati ule hukuwa umeokoka!, hukuwa umetubu..lakini sasa umejitambu, hivyo huna budi kubatizwa.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga Namba hizi…

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

UMUHIMU WA KUBATIZWA.

UFUNUO: Mlango wa 1

Watu wajikatao ni watu wa namna gani? (Wafilipi3:1).

Rudi nyumbani

Print this post

Dameski ni wapi kwasasa?

Dameski ni mji ambao mtume Paulo alitokewa na Bwana Yesu, wakati akiwa anaelekea kuwaua wakristo ndani ya mji huo (Matendo 9:2-7). Mji wa Dameski mpaka leo upo!.. Ni moja ya miji ambayo haijabadilika jina lake mpaka leo, mingine mfano wa hiyo ni Yerusalemu na Bethlehemu.

Mji wa Dameski upo katika nchi ya SYRIA kwasasa. Tamaduni za watu waliopo Dameski ni tofauti na za watu wa enzi za kale… Hivyo mji upo Pamoja na watu, lakini tamaduni ni nyingine si ile ya zamani.

Nabii Isaya alipewa ufunuo juu ya mji huo kuja, kuondolewa kabisa katika siku za mwisho..

Isaya 17:1 “Ufunuo juu ya Dameski. TAZAMA, DAMESKI UMEONDOLEWA USIWE MJI, NAO UTAKUWA CHUNGU YA MAGOFU.

2 Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.

3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi”.

Pia vita vya Ezekieli 38, vilivyotabiriwa kuja kupiganwa kati ya Israeli na mataifa ya kandokando Pamoja na Gogu, itaifuta kabisa mji huo.

Kwasababu kwasasa ni mji unaopinga Yerusalemu kama mji mtakatifu wa Mungu mwenyezi na urithi wa Israeli, na unafanya vita dhidi ya Taifa h. Kwasababu hiyo utaondolewa Pamoja na miji mingine baadhi kulingana na biblia.

Isaya 49:23 “Habari za Dameski. Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia; Maana wamesikia habari mbaya; Wameyeyuka kabisa; Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.

24 Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake.

25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu?

26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi.

27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi”.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

Bwana Yesu alizaliwa mwaka gani?

MAMA, TAZAMA, MWANAO.

Nyungu ni nini kibiblia?(Ayubu 41:20,31, Waamuzi 6:19)

Rudi nyumbani

Print this post

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI (Kujua Mierezi ni miti gani fungua hapa >> MIEREZI).

Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi. (Kwa urefu juu ya mji wa Tarshishi na biashara zake na Taifa hilo linafunua nini kiroho, fungua hapa >>Tarshishi).

Asili ya mji wa Tarshishi ni mwana wa Yafethi aliyeitwa Yavani, ambaye huyu Yavani ndiye aliyewazaa wenyeji wa Tarshishi.

Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.

2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.

3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.

4 NA WANA WA YAVANI NI ELISHA, TARSHISHI, Kitimu, na Warodani”.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Ashuru ni nchi gani kwa sasa?

MADHARA YA KUFUATA MAMBO YAKO TU!

Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?

BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA

Rudi nyumbani

Print this post

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Ninawi ni wapi?

Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru. (Kujua Taifa la Ashuru ni wapi kwasasa fungua hapa> ASHURU).

Mji wa Ninawi ndio Mji Nabii Yona aliagizwa na Mungu akahubiri Injili, ili watu wa mji ule watubu, lakini alikataa na kukimbilia mji wa Tarshishi. Kujua Mji wa Tarshishi kwasasa ni nchi gani basi fungua hapa> TARSHISHI.

Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.

Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;

11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”

Ijapokuwa Mungu alikusudia kuuadhibu mji huu lakini wenyeji wake walitubu kwa mahubiri ya Yona. Na Bwana Yesu alikuja kutoa unabii kwa vizazi hivi vya siku za mwisho kuwa..

Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; KWA SABABU WAO WALITUBU KWA MAHUBIRI YA YONA; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.

Na sisi tunapaswa tutubu kwa mahubiri ya Bwana Yesu, ili tusije kuangukia hukumu siku ya Mwisho.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10


Mada Nyinginezo:

Babeli ni nchi gani kwasasa?

NINI MAANA YA KUTUBU

YONA: Mlango wa 4

Rudi nyumbani

Print this post