Category Archive Home

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.

Luka 10: 25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 

29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?

30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.

33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.

36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?

37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo”.

Kuna kitu kidogo cha kujifunza katika hichi kisa…Mwanasheria mmoja alisimama kumwuliza swali la kumjaribu Bwana Yesu…kumwangalia atajibuje! Lakini Bwana alimjibu kwa kumrudisha kwenye Torati na kumwuliza imeandikwaje! Akamjibu “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako”.

Bwana akampongeza akamwambia afanye hivyo naye utaupata huo uzima wa milele. Lakini Yule mwanasheria hakuishia hapo…akataka kuendelea kumpima ufahamu Bwana Yesu kwa kumwuliza jirani yake ni nani??.

Sasa kumbuka huyu mtu hakuwa na lengo la kutaka kujifunza bali kwa lugha ya sasa hivi tunaweza kusema ni mtu aliyekuwa anajifanya mjuaji…Kwasababu alikuwa anajua kabisa vigezo vya kuupata uzima wa milele ni kumpenda Mungu kwa moyo wote na akili zote na pia kumpenda jirani kama nafsi yake, lakini bado alikuwa anamwuliza Bwana kwa kumjaribu…Na hapa anamwuliza tena Bwana jirani yangu ni nani…Na wakati Bwana ameshamjibu kuwa anapaswa ampende jirani yake kama nafsi yake..Kwahiyo alikuwa anajua kabisa jirani yake ni nani lakini alitaka kumwonyesha Bwana yeye ni mjuaji zaidi….

Na hicho kiburi alikipata kutokana na kusoma kwingi, alifahamu mambo mengi ya torati na dini yake kwasababu hapo juu biblia inasema alikuwa ni mwanasheria…Sasa hakuwa mwanasheria kama hawa wanasheria tunaowajua sasahivi wanaotumia katika ya nchi kuhukumu…Hapana bali yeye alikuwa ni mwanasheria aliyesoma sheria zote za Mungu kupitia Torati za Musa…Kwahiyo alikuwa anajua kufumbua maswali yote yanayohusiana na torati…kukitokea jambo Fulani anaweza kukupatia ufumbuzi kamili kwa kurejea kwenye Torati…atakwambia Aya Fulani ya torati, kipengele Fulani kinasema hivi na hivi…Kwahiyo ni watu ambao ulikuwa huwezi kuwadanganya kitu chochote kinachotoka kwenye Torati, walikuwa wanaijua yote.

Ndio maana alikuja kwa ujasiri kumjaribu Bwana akiwa tayari na majibu sahihi ya maswali yake kichwani.

Wakati yeye anadhani anajua kumbe mbele za Mungu alikuwa anaonekana hajui chochote.

Sasa katika mfano huo hapo juu Bwana Yesu alioutoa, alikuwa anataka kumwonyesha Yule mwanasheria kuwa “dhana ya kufikiri kuwa wayahudi ndio majirani zao pekee ni uongo”..Kama Torati ilivyowafundisha kuwa… “jirani yako ni Mwisraeli mwenzako”..Mtu mwingine tofauti na mwisraeli (Myahudi) sio jirani yako. Hivyo mtu unayepaswa kumpenda kama nafsi yako ni mwisraeli mwenzako tu!…Ndivyo huyu mwanasheria alivyokuwa anajua kichwani mwake na ndivyo torati ilivyokuwa inasema. Lakini ashukuriwe Mungu Bwana Yesu ndiye ukamilifu wa Torati Haleluya!!. Ndio maana Biblia inatuonya tutoke katika kamba za madhehebu kwasababu zinatufungia mlango wa kumjua Mungu…kamba za madhehebu zinatufanya tusimwelewe Mungu wala tusimsikie Mungu kwa kisingizio tu! Dini yetu inasema hivi, dhehebu letu linasema hivi. Zinatufanya tujione tunajua kila kitu kumbe hatujui chochote kama huyu mwanasheria hapa!.

Sasa tukirudi kwenye Torati ya Musa, Baada ya Mungu kuwatoa wana wa Israeli Misri na kuwaingiza nchi ya Kaanani aliwaambia…wapendane wao kwa wao, yaani wayahudi kwa wayahudi kama nafsi zao, pia walionywa wasichangamane na watu wa mataifa, hata wasioe watu wa mataifa. Na waliambiwa pia wasitozane riba wao kwa wao, wanaweza kuwatoza riba watu wa mataifa lakini sio wao kwa wao. Hivyo ilikuwa inaaminika na kufahamika kuwa sheria hiyo Musa aliyoitoa ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako, inawahusu tu wayahudi kwa wayahudi, kwamba wao tu watapendana kama nafsi zao, kwamba mtu mwingine tofauti na Taifa lao ni ruksa kutokumjali..ni ruksa kutojishughulisha naye. Lakini mwisraeli mwenzako ndio unapaswa umpende kama nafsi yako. Ukisoma kitabu cha Mambo ya Walawi utaweza kuelewa jambo hilo vizuri kwa undani, lakini moja ya mstari unaozungumzia upendo kwa wayahudi tu ni huu..

Walawi 19:18 “Usifanye kisasi, WALA KUWA NA KINYONGO JUU YA WANA WA WATU WAKO; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana”.

Umeona?..Biblia inasema hapo “juu ya watu wako”..ikiwa na maana watu wengine (yaani watu wa mataifa) ni ruksa kuwawekea kinyongo endapo wamefanya jambo la kukwaza.

Kwahiyo ndivyo ilivyokuwa inaeleweka miaka na miaka…Na huyu mwanasheria ndivyo alivyokuwa anajua…Lakini tunaona Bwana alimwambia kitu kipya..kuhusu JIRANI YAKE KUWA NI NANI?…Alitegemea aambiwe kuwa jirani yake ni myahudi mwenzake, (aidha mlawi au kuhani au mwisraeli wa kawaida tu)..lakini Bwana alimwonyesha Msamaria ndiye ndugu yake.

Sasa WASAMARIA wakati huo hawakuwa watu wa Taifa la Israeli, walikuwa ni watu wa mchanganyiko na watu wa mataifa…Kwahiyo hawakuwa uzao wa Ibrahimu hata kidogo..Lakini Bwana alitoa mfano huo kuonyesha kuwa watu wa mataifa wanaweza kuwa majirani wa kweli kuliko hata hao waisraeli wanaojiona wamestahili kupendana wao kwa wao tu!.

Katika mfano ule tunaona…Alikuja kwanza kuhani ambaye alikuwa myahudi lakini alipita kando hakutaka kumsaidia myahudi mwenzake mtu wa Taifa moja na yeye…Baadaye kidogo alipita Mlawi ambaye alikuwa myahudi pia lakini hakutaka kumsaidia myahudi mwenzake aliyekuwa amepatwa na matatizo…Lakini alipopita Msamaria ambaye hakuwa hata myahudi wala hamjui Mungu wa Israeli, alimsaidia kwa msaada mkubwa Myahudi ambaye alikuwa hata hamjui..Na hivyo huyo Bwana ndiye akasema ni JIRANI mwema anayepaswa kupendwa kama nafsi yake.

Bila shaka baada ya mfano huo, Yule mwanasheria aliondoka kwa hasira kwasababu ni kama aliambiwa amri mpya awapende pia watu wa mataifa aliokuwa anaishi nao, (makafiri) kama nafsi yake.

Na sisi kuna jambo tunaweza kujifunza hapo….Udini na Udhehebu ni mbaya sana, unaweza kutufanya tudhani tunampendeza Mungu kumbe hatumpendezi hata kidogo…Ni mara ngapi umeona watu wanaojiita wakristo wakiwachukia watu wasio wa Imani yao?…Utaona wanatoa mpaka maneno ya laana kwasababu tu sio wakristo kama wao…Wakati hao wanaowashutumu ndio Mungu anawaona ni MAJIRANI ZAO WAZURI kuliko hata wakristo wenzao..

Kama umefanya utafiti, utagundua kuwa fursa nyingi au msaada mwingi, Mungu anawatumia watu wasio wa Kristo au watu wa kiulimwengu kutusaidia kuliko watu wa ki-Mungu, Utaona watu ambao ni wakidunia wakati mwingine ni wakarimu na wanaojali kuliko hata watu wanaomjua Mungu. Hao Bwana anatuambia tuwapende kama nafsi zetu..hao ndio wasamaria wema..ndio majirani zetu, sio wakuwachukia na kuwasema bali kuwapenda kama nafsi zetu….

Sio kwasababu hamjui Mungu wako basi ndio awe sababu ya kuwa adui yako na kusema watu wa imani yangu tu ndio marafiki zangu, wakati mwingine Bwana anawatumia hao watu wasiomjua Mungu wako kukuletea wewe msaada kama ilivyokuwa kwa huyu myahudi aliyeangukia katikati ya wanyanganyi badala asaidiwe na watu wa dini yake na imani yake anakwenda kusaidiwa na watu hata wasioijua Torati..

Biblia imetuonya tu tusichangamane kufuata njia zao zisizofaa, kama ni walevi hatuenendi katika njia zao, kama ni waasherati vivyo hivyo, kama ni wacheza dansi, kama ni waabudu sanamu tusishirikiane nao hata kidogo…lakini sio tusiwapende na kuwachukia, wakitaka kukopa kwako usiwape kisogo, wakikuaribisha kwao usikatae, wakikupa zawadi pokea, wakiumwa uwatembelee… ili kwa matendo yetu mazuri na upendo wetu tuwavute waje upande wetu, na tuonekane tumeweza kuyafanya mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni.

Hivyo jawabu la mambo yote ni upendo, kwetu sisi kwa sisi na kwa wale walio nje.

Bwana atusaidie sote .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

UPENDO

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

BIBLIA ITUAMBIA TUSALIMIANE KWA BUSU TAKATIFU. HILI BUSU NDIO LIPI?

HAWA ALIPOLAANIWA ALIAMBIWA “TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO”.NI TAMAA IPI INAYOZUNGUMZIWA HAPO?


Rudi Nyumbani

 

Print this post

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

Hapo nyuma, kabla sijampa Kristo maisha yangu, na wakati ambao bado ni mchanga kabisa wa masuala ya wokovu, niliaminishwa kuwa kigezo kikuu kinachomtambulisha mtu huyu kuwa anazo nguvu nyingi za rohoni ni kiwango chake cha UPAKO, pengine na wewe ulifahamu hivyo au unafahamu hivyo, yaani mtu kuwa na uwezo wa kufanya miujiza,au kuona vitu katika ulimwengu wa roho kama vile mapepo, wachawi,majini, kuona maono, kuota ndoto, kunena sana kwa lugha, au kufanya sana ishara.n.k. Kwamba mtu kama huyo ni mtu mwenye nguvu nyingi sana rohoni na hivyo shetani anamwogopa sana. Jambo hili lilinifanya nione shauku kutatufa Upako kuliko kitu kingine chochote.

Lakini je! Kwa mujibu wa biblia hizo ndizo nguvu za rohoni?. Leo tutajifunza juu ya hilo, na ni kitu gani tufanye ili nguvu zetu za rohoni ziongezeke. Sasa Ili kuelewa nini maana ya nguvu za rohoni, ni vizuri tujifunze kwanza juu ya nguvu nyingine, Tunajua siku zote kitu chochote chenye nguvu huwa kinakuwa na uwezo wa “kuteka na kutawala”, Simba ni mnyama mwenye nguvu na ndio maana ameteka pori lote, hivyo nguvu ya aina yoyote ile huwa inateka na kutawala, tunafahamu pia mtu mwenye nguvu ya kiuchumi huwa anatawala, mwenye nguvu ya kisiasa huwa anateka na kutawala, mwenye nguvu ya kiteknolojia huwa na uwezo pia wa kuteka na kutawala, na ndio maana tunaona mataifa kama Marekani na Ulaya, yanatawala dunia sio kwasababu ni makubwa hapana, bali kwasababu yana nguvu Fulani zinazowazidi wengine.

Vivyo hivyo na kwa mwenye nguvu za Rohoni, ni lazima mtu awe na uwezo wa kuteka na kutawala, na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya.

Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”,

 Unaona nguvu anazozizungumzia sasa hapo ni NGUVU ZA ROHONI. Ikiwa na maana kuwa mtu mwenye nguvu nyingi za Rohoni ndiye atakayeweza kuuteka ufalme wa mbinguni, ukiwa na nguvu chache utakuwa mnyonge tu. Na leo nataka ujue hizi nguvu za Rohoni zinapatikana wapi.

Sasa tukirudi kwenye huo huo mstari hapo juu, lazima tujiulize swali moja, ni kwanini Bwana alisema “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa”, kwanini hakusema tangu siku za Ibrahimu au za Musa hadi sasa? Badala yake anasema “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa”, . Utagundua kuwa Bwana alitaka tujifunze kitu Fulani kwa Yohana mbatizaji katika masuala ya kupata nguvu za rohoni. Hivyo embu tumwangalie kidogo Yohana alikuwa ni mtu na namna gani tangu utoto wake.

Maandiko yanatuambia:

Luka 1:80 “Yule mtoto akakua, AKAONGEZEKA NGUVU ROHONI, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli”.

Unaona kumbe Yohana tangu utoto wake alikuwa akiongeza nguvu rohoni kwa kasi sana, mpaka alipokuwa mtu mzima alipoanza huduma yake. Lakini hakuwahi kufanya muujiza hata mmoja, wala kutoa ishara yoyote kutoka mbinguni kama vile Eliya, Biblia inasema hivyo (Yohana 10:41), Na ndio maana tunasema Upako wowote kulingana na maandiko sio kitambulisho kuwa mtu huyo anazo nguvu za rohoni. Mtu unaweza akawa na uwezo wa kuona maono yote duniani lakini rohoni ukawa mdhaifu kuliko hata mtu aliyempa Kristo maisha yake leo.

Sasa tunaona Yohana alipoteza muda wake mwingi kukaa mbali na makazi ya watu ili tu kuongeza nguvu zake rohoni tangu utoto wake,(baadaye kidogo tutaona ni kitu gani alichokuwa anakifanya alipokuwa anakwenda kule jangwani) mpaka kufikia kilele cha nguvu za rohoni mpaka Bwana Yesu Kumshuhudia vile katika:  

Mathayo 11:11 “Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; 

12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”.

Kwa Nguvu alizokuwa nazo rohoni, hakukuwahi kutokea nabii au mtu yoyote katika agano la kale aliyeweza kumfikia, sio Ibrahimu, sio Musa, sio Eliya, sio Daudi sio mtu yoyote Yule aliyefanya mambo makubwa unayemsoma katika agano la kale aliyeweza kuwa na nguvu zaidi yake (Yohana) kuuteka ule ufalme. Lakini Leo utafahamu SIRI imelala wapi nawe uanze kujishughulisha nayo.

Sasa kumbuka Yohana tangu utoto wake hakuwahi kujishughulisha na jambo lingine zaidi ya kutafuta kumjua huyu MASIHI ALIYETABIRIWA NI NANI?. Ambaye ndiye kiini cha dini yao kiyahudi, ndiye kiini cha wokovu uliokuwa unatarajiwa wa ulimwengu mzima, wakati wengine wanang’ang’ania kukariri torati huyu aling’ang’ania kumtafuta Kristo ambaye Mungu alimshuhudia tangu enzi za kale za manabii. Na hiyo ndiyo iliyomfanya mbinguni aonekane kila siku nguvu zake za rohoni kuongezeka kwa kasi sana.

Alianza kutafuta kwa bidii katika torati habari zake, tangu mwanzo mpaka mwisho, kwa jinsi alivyokuwa anamtafuta kwa bidii akachunguza akaona kuwa kumbe kwa mfano ule ule wa wana wa Israeli walivyookolewa utumwani Misri ndivyo mwokozi atakavyouokoa ulimwengu wote kwa jinsi hiyo hiyo..

Kwa hatua zile tatu, ambapo hatua ya kwanza, ilikuwa ni Yule mwanakondoo kuchinjwa, ili damu ipatikane kwa pigo la mzaliwa wa Kwanza Misri, akajua kumbe damu ilihitajika kufungua vifungo. Na pigo lile lililegeza kweli vifungo vya maadui zao kuwapa ruhusu wa kutoka Misri, lakini lile halikutosha kuwafanya maadui zao wasiwafuatilie, hivyo ilihitajika hatua nyingine ya pili na ndio ile ya nguzo ya moto, ambayo ilikuwa inawatangulia mbele yao sasa ilibidi irudi nyuma yao kuweka wigo wasiwafuate.. Yohana akagundua kumbe moto ulipitia juu yao kuwatakasa pasipo wao kujijua.

Lakini moto ule haukutosha kumaliza kabisa adui yao ulipoondolewa, bado walitaka kuwafuata na ndipo tunaona maji yalifuata kuwatakasa tena, nako ndiko kule kuvuka bahari ya shamu Kubatizwa, na hapo ndipo maadui zao walipomalizwa moja kwa moja walipotoswa na yale maji.

Hatua hizo tatu (yaani damu ya mwana-kondoo, moto-wa-Roho Mtakatifu, na Maji), ndizo Yohana alitambua kuwa Masihi ajaye atazitumia kumkamilisha mwanadamu kwa wokovu wake.

Sasa hapo ndipo Yohana alipopatia ufunuo wa ubatizo wa Maji akaanza kuufundisha na kuwaambia watu wabatizwe, huku akitazamia kuwa mwanakondoo atakajua ambaye atakamilisha yaliyobakia yaani maji na moto wa Roho Mtakatifu,

Yohana 1:26 “Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.

27 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

28 Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.

29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, MWANA-KONDOO WA MUNGU, AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU!

30 HUYU NDIYE NILIYENENA HABARI ZAKE YA KWAMBA, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

31 Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.

32 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.

33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.

36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!

37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu”.

(Soma pia Mathayo 3:11)..

Unaona hapo Yohana alimtambua YESU na Kazi yake atakayokuja kuifanya kabla hata hajawasili, alimtengenezea njia, Hivyo mbinguni akaonekana mtu mkuu sana, mwenye nguvu nyingi za rohoni japo duniani watu walimwona maskini amerukwa na akili.

Leo hii nataka nikuambie ndugu usifurahie tu kuwa YESU ameyaokoa maisha yako, halafu ukaridhika, mahali ulipo, unaendelea na mambo yako, YESU KRISTO ni zaidi ya unavyomfikiria, Mungu kaweka Heshima yake yote pale, ndio hekima ya Mungu na NGUVU YA MUNGU (1Wakorintho 1:24), na ndipo utajiri wote, na hazina zote za maarifa zilipolala. Hapo ndipo Yohana alipopatia heshima yake na ukuu wake.

Wakolosai 2:2 “….wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo;

3 ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”

Kwa mtu Yule leo hii anayejishughulisha kutafuta kumjua YESU usiku na mchana, mtu huyo nguvu zake za rohoni zinaongezeka kwa kasi sana pasipo hata yeye kujijua. Na mwisho wa siku anajikuta anauteka ufalme wa Mbinguni kirahisi kabisa kwasababu amefahamu mahali lulu ya thamani ilipo.

Itafute hii LULU ndugu. Nataka nikuambie vita kubwa ya shetani ipo hapo, watu wasimjue Kristo ni nani hasaa na uweza wake, yeye anataka watu wamwone kama mtu wa kawaida tu, kwasababu anafahamu mtu akishamwelewa vizuri Bwana Yesu ni nani, basi atajijengea daraja zuri mbinguni na atamsababishia madhara makubwa sana katika ufalme wake.

Anza leo mwanzo mpya, maanisha kumfauta Kristo…usitafute upako wala miujiza..Bwana akikujalia hizo ni vizuri lakini sio jawabu la kuwa na nguvu za rohoni…Ikiwa unapenda kuwa mkuu hata zaidi ya Yohana, machoni pa Mungu,wala usijishughulishe na jambo lingine lolote, JISHUGHULISHE KATIKA KUMTAFUTA KRISTO, acha kuzisumbukia karama, acha kutafuta maombezi, acha kukesha kwa ajili ya upako, kesha kwa ajili ya KUMSOMA KRISTO. Sisemi usizitumie hizo karama, hapana zitumie maadamu Mungu kakupa, lakini huku nyuma usisahau kuwa ufalme wa mbinguni unatekwa na wenye nguvu za mafunuo ya YESU Kristo. Tumeaswa tumjua sana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu mpaka tufikie kimo cha utimilifu wake.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”

Unapoyatafakari maandiko, jenga mtazamo wa Kristo ndani yake, wengi wakifungua maandiko wanayatazama kwa sura ya mafanikio ya kidunia, hivyo wanapata ufunuo kulingana na walichokitazamia, lakini ukimsoma Kristo kwa lengo la kutaka kumjua zaidi…atakujaza maarifa na nguvu za rohoni, atajifunua kwako na kuanza kukufundisha kanuni zake zote kwa namna ya ajabu sana.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

JINA LA MUNGU NI LIPI?

Shalom mtu wa Mungu. Wengi wanajiuliza swali hili, jina la Mungu hasaa ni lipi kwasababu kwenye biblia tunaona yanatajwa majina mengi tunashindwa kuelewa ni jina lipi la kusimamia. Ni kweli hili ni swali zuri, ambalo mtu aliyemaanisha kweli kumtafuta Mungu atatamani kufahamu jina halisi la Mungu ni lipi?.

Hili si swali gheni kwetu sisi, ni swali ambalo lilianza kuulizwa na wana wa Israeli tangu zamani kabla hata hawajatolewa katika nchi ya Misri, walikuwa wanajiuliza huyu Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka na Yakobo tunayemtumainia siku zote jina lake ni Nani?..Na ndio maana utaona jambo la kwanza ambalo Musa alimuuliza Mungu kabla ya kwenda kuwaokoa wana wa Israeli, ni kuwa “watu hawa wakiniuliza jina lako ni nani niwajibuje”?. Unaona alijua kabisa ndio swali atakalokumbana nalo la kwanza kabla ya mambo mengine kwa wayahudi waliokuwa wanateseka kule Misri. Hivyo leo tutajifunza Jina hasaa la Mungu ni lipi kwa mujibu wa majibu aliyopewa Musa na Mungu katika maandiko… tusome:

Kutoka 3:13 “Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?

14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

15 Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.”

Hilo ndilo lilokuwa jibu la Mungu, jina lake wakimuuliza ni MIMI NIKO AMBAYE NIKO, au NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA…Lakini leo nataka tujiulize swali moja je hili jina “NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA”, Ni jina kweli?. Ukweli ni kwamba hili sio “jina”. Lakini kulikuwa na sababu kubwa Mungu kujitambulisha kwa Musa kwa namna hiyo mwanzoni kabisa, nataka nikuambie na hapo ndipo siri ya jina lake ilipolala.

Aliposema NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA…kwa Lugha nyepesi ni sawa na kusema, siku hiyo ikifika Nitajifunua au nitajulikana kama nitakavyokuwa.. hiyo siku ndio litajulikana, kwahiyo hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu jina lake la si la mara moja tu kama ya kwetu sisi wanadamu yalivyo, bali linajifunua katika maumbile tofauti kulingana na wakati na majira… Ukimwelewa kwa hapo Mungu basi hutapata shida huko mbeleni.

Na ndio maana kipindi kifupi tu mbeleni mara baada ya Musa kwenda kumwonyesha Farao zile Ishara alizopewa na Mungu, na kukataa kuwaachia wana wa Israeli waende zao, kinyume chake akawazidishia utumwa, mpaka wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa, na Musa akarudisha malalamiko yake kwa Mungu, ndipo tunaanza kuona sasa hatua ya kwanza ya “NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA” ilipoanza kutenda kazi. Tunaona Mungu alimwambia tena Musa mimi ni YEHOVA.

Kutoka 6:1 “Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.

2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.

5 Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.

6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;

7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.”

Unaona hapo alimtokea Ibrahimu, na Isaka na Yakobo kama Mungu mwenyezi, (EL shadai) ukisoma mwanzo 17:1 utaona..Sasa Kwa utambulisho huu wa kumjua yeye kama mwenye enzi yote, mwenye Nguvu zote na uweza wote, ndio uliowafanya Ibrahimu na Isaka na Yakobo, wamwamini Mungu kwa kiwango kile cha juu namna ile, Unadhani mpaka mtu akuamini hivi hivi tu kuwa utakuja kumfanya kuwa taifa kubwa na mataifa yote duniani yatajibarikia kwako, na huku umeshazeeka, hapo inahitaji Mungu ajifunue kwako kama Mungu-mwenyezi vinginevyo hutaweza kuamini mpaka mwisho..

Lakini sasa Jina hili YEHOVA lilizuka mara baada tu ya Farao kuonyesha kiburi,..Na kama tunavyosoma habari Hiyo hatuna muda wa kuuleza moja moja hapa lakini kwa mapigo yale yaliyomfuata mpaka dakika ya mwisho, tunafahamu sio tu Farao na wayahudi walikiri kuwa Yule ni YEHOVA, bali pia mataifa yote duniani yalimtambua na kumwogopa Mungu kwa jina hilo.

Hata baada ya kuingia nchi ya kaanani Jina hili liliendelea kutumika kwa wana wa Israeli, lilichukua maumbile tofuatitofauti kulingana na wakati waliokuwa wanaupitia:

⧫Mfano utaona Mungu alijifunua kwao kama YEHOVA-RAFA: Maana yake Mungu-Nikuponyaye. (Kutoka 15:26.) Mungu aliwaahidia yale magonjwa yaliyokuwa Misri hayatawapa tena ikiwa watazishika amri zake..

⧫Alijifunua tena kama YEHOVA-NISI: Ikiwa na maana kuwa Mungu ni Bendera yetu (Berani ya vita) (Kutoka 15:26).

⧫Alijifunua tena kama YEHOVA-SHALOMU: Mungu ni Amani (Waamuzi 6:24). Gideoni alijenga madhabahu na kuiita jina hili baada ya kudhani kuwa Mungu angemuua pale alipokutana na malaika.

⧫YEHOVA-MEKADISHKEMU: Bwana atutakasaye (Kutoka 31:13)

⧫YEHOVA-ROHI: Bwana ndiye mchungaji wangu (Zab 23)

⧫YEHOVA-YIRE: Mungu atupaye (Mwanzo 22:14)..

Na mengine mengi hatuaweza kuyataja yote hapa.. Mungu alikuwa akijifunua kwa wana wa Israeli, akionyesha uweza wake na ukuu wake kwao, katika mazingira mbali mbali waliyokuwa wanapitia.

Hivyo hiyo ikaendelea mpaka wakati wa waamuzi,na wafalme na manabii..miaka mingi sana ilipita…

Na ulipofika wakati sasa wa Mungu kuikomboa dunia yote, sio kwa Taifa moja tena kama hapo mwanzo, bali dunia nzima ilimpasa ajichagulie jina la wakati huo.. Haleluya!! Na jina hilo ni lazima libebe sifa zote za majina yaliyotangulia, ili kusudi kwamba kusiwe na kitu chochote cha kando kilichosalia, Jina la dunia nzima…Jina ambalo manabii wa zamani mpaka Musa mwenyewe alitamani lifunuliwe wakati wao lakini ilishindakana…na jina hilo si lingine zaidi ya YESU KRISTO

Tafsiri ya YESU ni “YEHOVA-MWOKOZI” hiyo ndiyo tafsiri yake..Hivyo jina hili limebeba ukombozi mkamilifu wa viumbe vyote, sio wanadamu tu bali mpaka wa wanyama..tabia ya majina yote ya kwanza yamo ndani yake, jina hilo linaponya, linachunga, linatoa Baraka, linahuisha, linaokoa, linashindania vita, linaumba, linafunga, linafungua, linafanya kila kitu..Lile la kwanza lililishia kwa maadui wa mwilini lakini hili limechimba kwenye mizizi kabisa kwenye kiti cha enzi cha shetani huko kuzimu na kumshinda, na kumnyang’anya mamlaka yote na kumpa mwanadamu. Hivyo mwanadamu yoyote akipata ufunuo wa jina hili hakuna jambo lolote litakaloweza kumshinda hapa duniani.

Na ndio maana sasa biblia inasema..Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”

Jina hilo ni jina la YESU KRISTO. Utauliza ni wapi tena kwenye maandiko panaposema jina la Yesu ni jina la Mungu…Bwana Yesu alisema maneno haya..

Yohana 5:42 “Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.

43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo”.

Hivyo ndugu jina la Mungu Yule ambaye anasema NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA sasa ndio hili YESU KRISTO. Uponyaji wako utaupata kwa kupitia hili, kushukuria utashukuria kwa jina hili, kutolea mapepo utatolea kwa jina hili hakuna jina lingine hapo..Vile vile kubatizwa utabatizwa kwa jina hili..Wapo watu wanaobatiza kwa jina la Baba na mwana na Roho Mtakatifu, (Mathayo 28:19). Wanakosa ufunuo Yesu alimaanisha nini pale kusema vile..Hawajui kuwa jina la (Baba na mwana na Roho Mtakatifu) ni jina moja hilo nalo ni jina la YESU. Na ndio maana mitume wote baada ya kulitambua hilo utaona mahali pote walikuwa wanabatiza kwa jina hilo la YESU KRISTO, soma (Mdo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5) sehemu zote hizo mitume hawakubatiza kwa vyeo vya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Bali kwa jina la YESU KRISTO…

Kwa akili ya kawaida tu kwanini pepo ukikemea hulikemei kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu? Badala yake unatumia jina la Yesu, ukiumwa unatumia jina la YESU likuponye iweje leo unapoenda kubatizwa unatua vyeo badala ya JINA?. Ni vizuri tuifahamu kweli na tuifuate, Dini zisitukwamishe.

Natumaini utakuwa umemfahamu MIMI NIKO AMBAYE NIKO kwa sasa jina lake ni lipi?.

Lakini Pia, fahamu kuwa Hili jina la YESU nalo halitadumu milele, kuna wakati unafika Mungu atabalika na kuja na jina jipya, na hilo litatumika katika ule utawala wa miaka 1000, pale Kristo atakapokuwa kama Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme. Jina hilo litakuwa sio la ukombozi tena kama sasa, kwasababu ukombozi utakuwa umekwisha wakati huo…bali litakuwa na tabia nyingine ambazo tutazijua vizuri tukifika huko. Hivyo ni vizuri usiichezee neema tuliyonayo sasa ya ukombozi kupitia jina la Yesu, upo wakati utatamani kuokoka utashindwa kwasababu neema itakuwa imeshaondoka.

Ufunuo19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; NAYE ANA JINA LILILOANDIKWA, ASILOLIJUA MTU ILA YEYE MWENYEWE.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.”

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

JINA LAKO NI LA NANI?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 9.

Shalom.Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, ni vizuri ukakisoma kitabu hichi peke yako kwanza kwa utulivu, na katika uwepo wa Bwana, na kufuatilia mfululizo huu tangu mwanzo ili tunapoendelea katika sura hizi zinazofuata usibakie nyuma twende pamoja.

Katika sura iliyopita tuliona jinsi wale malaika 7 walivyopewa baragumu zao na  pindi walipozipuliza/kuzipiga ni nini kilitokea, Na tulishaona baragumu nne za mwanzo…kama hujapitia pia ni vizuri ukapitia au bofya hapa⏩ Ufunuo:Mlango wa 8. Na tuliona kuwa baragumu hizo ni kama mwanzo wa utungu tu! Wa vile vitasa saba vitakavyokuja kuachiwa huko mbeleni katika siku ile kuu ya Bwana.…Ni sawa na mtu anayenawa uso kwa muda tu! Lakini baadaye atakuja kuoga mwili mzima.

Vile vile tuliona  pia  hizi baragumu zitaanza kupigwa mara baada ya unyakuo kupita tu! Na zile tatu za kwanza Zitawaathiri sana wayahudi walioopo Israeli (na watu wanaoishi mashariki ya kati), isipokuwa lile la 4 ambalo litaathiri dunia nzima, kwasababu jua likipigwa ni dunia nzima itaathirika na sio sehemu tu!..na mapigo hayo yatatekelezwa kupitia wale mashahidi wawili waliozungumziwa katika ufunuo 11.

Ufunuo 11:3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.

6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo”.

Unaona Mashahidi hawa wawili wataleta mapigo hayo kwa amri ya Bwana kama vile Musa alivyoleta mapigo juu ya Farao kwa Amri ya Bwana.

Na mwishoni mwa sura ya 8, tuliona pia kulikuwa na malaika (Tai) aliyeruka katika anga na kutangaza ole kwa wote wanaokaa juu ya nchi kwasababu ya sauti ya zile baragumu 3 zilizosalia, yaani baragumu la 5,6 na la 7.

Hivyo leo tunaendelea na sura ya 9 kwa Neema za Bwana..ambayo inaelezea juu ya baragumu zilizosalia isipokuwa ile ya saba tu.

Ufunuo 9: 1 “Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.

2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.

4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

5 Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.

8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.

9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.

10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.

11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni”.

Kama tulivyotangulia kujifunza, Nyota iliyoanguka kutoka mbinguni si kimondo bali ni ‘shetani’ na Ufunuo 12:12 inasema.. “hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. OLE WA NCHI NA BAHARI! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”

Na pia sehemu nyingine Bwana Yesu anasema: Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. (Luka10:18)

Ikiwa na maana kuwa kuanguka kwa shetani, na kutupwa chini duniani ni LAANA! Sio kitu kizuri..viumbe vyote vikaavyo baharini vitaathirika na kadhalika vikaavyo juu ya nchi…sasa wanadamu ndio wanaokaa juu ya nchi, hao ndio waathirika wakuu!.

Katika baragumu hili tunaona shetani kama nyota iliyoanguka kutoka juu…akipewa funguo za kuzimu…sasa kumbuka kuzimu zimegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni sehemu ambapo roho za watu waliokufa katika dhambi zipo, ni sehemu ya mateso sana, roho za watu hawa zipo zikiwa katika hali ya vifungo, zikiteseka zikingoja ufufuo wa hukumu.

Na sehemu ya pili ya kuzimu, ni sehemu ambayo roho za baadhi ya malaika walioasi mbinguni zimefungiwa…Kumbuka sio mapepo yote yaliyoasi yanatenda kazi leo duniani, hapana, yapo mengine mabaya kuliko haya yaliyopo sasa, ambayo yalifungwa katika hii kuzimu ya pili, kwa makosa yaliyofanywa na hata kuna mengine yanaweza  kutupwa huko hata leo, ndio maana utaona kuna yale yaliyomsihi Bwana Yesu asiyapeleke shimoni..Huko shimoni kunakozungumziwa ni “kuzimu ya malaika walioasi’’ ni sehemu ya vifungo vya giza na mateso ambapo roho hizo zimefungwa huko mpaka siku zitakapotupwa katika ziwa la moto…ambapo tutakuja kuona katika ufunuo 20 shetani naye atakuja kutupwa huko na kufungwa kwa miaka 1000.

Sasa pia kumbuka shetani alinyanganywa funguo za mauti na kuzimu na Bwana Yesu mwenyewe, kwasababu hapo kwanza alikuwa nazo alikuwa na uwezo wa kuzileta juu roho za watu waliopo kuzimu na baadhi ya mapepo,! Ndio maana maana unaona aliweza hata kumleta Nabii Samweli juu aliyekuwa amekufa kuzungumza naye. Lakini Baada ya Bwana Yesu kuja, mamlaka yote ya wafu yakawa chini ya Yesu Kristo, hakuna kiumbe chochote hata shetani chenye mamlaka juu ya wafu au roho zilizopo kuzimu au peponi. Lakini tunaona hapa! Shetani anapewa ufunguo za kuzimu…na kama unavyoona ni ANAPEWA!! Ikiwa na maana kuwa hakuwa nazo hapo kabla…alikuwa amenyanganywa lakini hapa anapewa tena kwa muda.. sasa hapewi funguo za kuzimu mahali wanadamu walioasi walipo hapana bali anapewa funguo za kuzimu mahali malaika walioasi walipo?..hizo ni sehemu mbili tofauti.

Na kwasababu ana ghadhabu nyingi na lengo lake ni kuiharibu dunia kwasababu anajua muda wake umeisha….funguo atakazopewa atafungua kuzimu na kuyafungulia mapepo ambayo Bwana Yesu aliyafunga yasifanye kazi duniani kwa kipindi Fulani kwasababu yangeleta uharibifu mkubwa sana ambao haujawahi kuwepo!!..Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kumshukuru Mungu kwaajili ya Yesu Kristo, maana kama si yeye sijui tungekuwa wapi leo. Shetani angetupepeta vya kutosha.

Kwahiyo shetani atapewa funguo na atayafungua hayo mapepo yaliyokuwa kifungoni, ambayo ni mabaya kuliko haya yaliyopo huru sasa duniani..Sasa biblia imeyafananisha hayo mapepo na hao nzige tunaowasoma kwenye sura hii…Kumbuka sio nzige kama nzige hawa wadudu tunaowajua watakaotoka kuzimu hapana! Bali ni maroho! Biblia imefananisha mara nyingi roho chafu na roho za wanyama au wadudu..(Kwamfano Ufunuo 16:13 unaweza ukaona jambo hilo….Inasema:  “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote…”).

Maumivu yao ni kama ya ng’e..roho hizi zitaleta madhara makubwa katikati ya watu..pigo hili litakuwa ni kwa watu wa dunia nzima…Unajua sasahivi kila uovu Fulani unaasisiwa na roho Fulani (au pepo fulani)..Kwamfano ushoga ni mapepo Fulani ya aina hiyo yanawaingia watu na kuwapeleka kwenye ushoga…yasingekuwepo hayo watu kwa hali ya kawaida wasingeweza kuwa mashoga..kadhalika na usagaji, utafanyaji masturbation, uuaji, wizi, usengenyaji, n.k yote hayo ni mapepo.

Ili kuelewa vizuri kama wewe ni mdadisi wa kifaa kinachoitwa computer au simu, utagundua kuwa unaponunua computer au simu inakuwa na mambo machache sana…ili kuiongezea uwezo inakubidi kudownload baadhi ya programs au softwares ili iweze kwenda kama unavyotaka wewe..utagundua kuwa ili sauti iweze kusikika vizuri, au ili uweze kuongeza milio ya simu, au uweze kuwasiliana na watu kisasa n.k inakubidi udownload applications au software kwenye simu yako au computer yako..sasa hizo applications au softwares unazoziongeza kwenye simu yako ndio mfano wa mapepo ambayo shetani anayaongeza ndani ya watu ili waweze kuwa mashoga, wauaji, wazinzi, walawiti n.k

Sasa katika siku hizo yatakapofunguliwa, zitazalika tabia duniani ambazo hazipo duniani leo…pengine utaanza kuona watu wanaanza kula nyama za watu, au utaanza kuona watu wanaanza kuwa na uwezo wa ajabu wa kipepo, ukatili wa ajabu utaongezeka ambao haujawahi kuonekana hapo kabla, pengine utaona watu wanafanya uzinzi mabarabarani bila aibu,..na kuzuka baadhi ya magonjwa ambayo ni mapya, ya mateso kushinda saratani au ukimwi,..pengine utaanza kuona na wanyama pia wanabadilika tabia, hawafugiki tena, nk n.K, siku hizo ndizo  watu watatamani kufa lakini biblia inasema mauti itawakimbia. Kila mtu ataona hakuna maana ya maisha tena, duniani hakukaliki hofu ya kila kitu.

Na kwenye ule mstari wa mwisho biblia inasema wanaye mfalme naye ni malaika wa kuzimu..jina lake kwa kiebrania ni Abadoni na kwa kiyunani ni Apolioni…Abadoni maana yake ni “MAHALI PA UHARIBIFU”. …na Apolioni maana yake ni “MUHARIBIFU”…Majina yote haya mawili yanamzungumzia ‘shetani’ ambaye ndiye mwaribifu na kila aina ya uharibifu unatoka kwake. Yeye ndiye mfalme wa kuzimu na mfalme wa hawa malaika walioachiwa kutoka kuzimu.

Na ndio maana ni vizuri kutengeneza mambo yako sasa, angali neema ya Kristo ipo, huko mbeleni ni vilio na maombolezo kwa watakaokosa unyakuo.

Tukiendelea na mistari inayofuata biblia inasema…

Ufunuo 9: 12 “Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.

13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao”.

Katika mstari wa 14 tunaona ikitolewa amri ya kufunguliwa kwa wale malaika wanne waliokuwa wamefungwa katika Mto Frati. Na hawa lengo la kuzuiwa katika Mto Frati ni ili wasilete madhara waliomriwa kuleta kabla ya wakati kufika, kwamba wakati ukifika waue theluthi ya wanadamu wanaoishi juu ya nchi…Ili tujue hawa malaika ni wapi…turudi nyuma kidogo kwenye ufunuo Mlango wa 7.

Ufunuo 7: 1 “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao”.

Malaika hao wanne waliokuwa wamezuiwa kwenye mto Frati ndio hawa hawa ambao walionekana wamesimama kwenye pepo nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, Na pepo hizi nne ni upepo wa KI-SIASA, upepo wa KI-DINIKI-UCHUMI na KI-JESHI. Hizo ndio pepo 4 za nchi.

Malaika hawa waliwekwa kuzuia vita vikuu vya Harmagedoni visitokee juu ya nchi.. Kwahiyo walikuwa wanazuia shughuli zozote za kipepo zisifanye kazi juu ya siasa ya dunia, uchumi wadunia, dini ya dunia wala jeshi la dunia, lakini sasa wakati huu, wataruhusu shetani aingie kuvuruga siasa ya dunia, uchumi, dini pamoja na jeshi…Yale mapepo yaliyotoka kuzimu yatawaingia wanasiasa wa dunia, sasa kuanzia wakati huu kutakuwa hakuna kuelewana duniani, kutakuwa hakuna kuvumiliana tena…mipango ya vita itawekwa, na amani itavurugika kwa kiwango kikubwa sana…Na ndio maana unajiuliza kwanini Leo mataifa makubwa yanagombana lakini hayapigani, nikwasababu malaika hawa wameamuriwa wazuie machafuko, lakini wakati utafika hakutakuwa na kuzuiwa tena, vitendo vitafuata.

Biblia inasema zaidi ya wanajeshi milioni 200 (elfu ishirini mara elfu kumi), watahusika katika mapambano ya vita hiyo ya Harmagedoni… “na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.” Mstari huu unazungumzia aina za silaha zitakazotumika wakati huo, farasi anawakilisha silaha za kijeshi kama ndege za vita, vifaru, helicopter za mabomu ya atomiki n.k na kama hapo inavyosema katika midomo yao inatoka moto, moshi na kiberiti…inazungumzia mabomu, na makombora yatokayo kwenye vifaru hivyo, ndege hizo, nk na walikuwa na vichwa kama vya simba, kama vile simba angurumapo atafutapo wawindo na silaha hizi zitakuwa na mingurumo zitumiwapo.

Kwahiyo katika baragumu hili la sita ndio utakuwa mwanzo wa maandalizi ya vita ya tatu ya dunia…Vita ya Mungu mwenyezi, (Harmagedoni). Ambayo tutakuja kuisoma vizuri katika Kile kitasa cha sita katika Ufunuo ule mlango wa 16. Wakati huu machafuko ya mataifa yatakuwa mengi sana duniani. 

Kristo yupo mlangoni, umefanya uteule wako na wito wako Imara sawasawa na 2 Petro 1:10?. Kama sivyo jitazame mara mbili, kisha chagua mwisho mwema, mambo haya sio hadithi tu za zale ni mambo ambayo yatakuja kutokea dhahiri mbele ya macho ya watu wengi.

Bwana akubariki. Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 10. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

DANIELI: MLANGO WA 1

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

UFUNUO:Mlango wa 8

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, leo kwa Neema za Bwana tutajifunza sura hii ya 8.

Ufunuo 8:1 ‘Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa’.

Katika mstari huu wa kwanza, Tunaona Yohana anaanza kwa kuonyeshwa ono la kufunguliwa kwa  Muhuri wa saba. Kwenye mlango wa sita wa kitabu hichi tulishaona ni nini maana ya mihuri, na ilipofunguliwa ni nini kilitokea,kwahiyo kama hujapitia Mlango wa 6, ni vizuri ikaipitia ili tuweze kwenda pamoja katika sura hizi zinazofuata…Lakini kwa ufupi tuliona Muhuri huu wa saba umebeba siri ya Ujio wa Yesu Kristo mara ya pili…Na utatimizwa kipindi kifupi sana kabla ya unyakuo, ambapo ndani ya muhuri huo wa saba tuliona ndio umebeba siri ya zile ngurumo saba zilizozungumziwa katika Ufunuo 10:3 ambazo Yohana aliambiwa asiziandike. Kwa kupitia siri hizo kanisa la Kristo (linalojulikana kama bibi-arusi safi) litapata Imani ya kwenda kwenye unyakuo.

Tukiendelea ni mistari inayofuata biblia inasema…

Ufunuo 8:2 ‘Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.

3 Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu,akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu yadhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.

4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika’’.

Hapa tunaona Yohana akioneshwa maono mengine..Aliona Malaika saba wanaosimama mbele za Mungu..wakipewa baragumu saba…Sasa hawa malaika Yohana aliowaona sio malaika wa sifa au makerubi hapana! Bali ni malaika wa hukumu. Na utaona wanapewa baragumu saba…kila mmoja baragumu moja..Maana ya Baragumu ni ‘Mbiu’ kwa lugha ya sasa hivi..Kwahiyo kila mmoja alipewa mbiu yake…Sasa kazi za hizi mbiu ni kutoa sauti ya tukio Fulani la ghafla kuanza au kutokea…Zamani vita ilikuwa Ikisikika baragumu (au mbiu) vitani ni ishara ya kuwa vita vimeanza..au mapambano yameanza, au kuna kitu cha hatari kinakuja…Kwahiyo na hawa malaika wanaonekana hapa wakiwa na baragumu kufunua kuwa watakapopuliza tu basi kuna kitu cha hatari kinafuata.

Lakini katika mstari wa tatu, tunaona Yohana anakatishwa yale maono ya wale malaika saba, anapelekwa kwenye maono mengine anaonyweshwa madhabahu na malaika mwingine tofauti na wale saba, anakuja na chetezo pamoja na uvumba ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu iliyokuwa mbele ya kiti cha enzi.

Sasa uvumba unaashiria maombi ya watakatifu, watakatifu tunapoomba maombi yetu yanaenda kama harufu ya uvumba mzuri mbele za Mungu, Daudi alisema katika Zaburi 141:1-2 ‘’Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo. Sala yangu ipae mbele zako KAMA UVUMBA, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.’’..ukisoma pia Ufu.5:8 utaona jambo hilo, kuwa uvumba siku zote unawakilisha maombi ya watakatifu.

Kwahiyo Malaika huyu kazi yake ilikuwa ni kuchukua maombi ya watakatifu wote..kuanzia agano la kale hadi mwisho wa dunia na kuyapeleka mbele za Mungu, na yote yalikuwa yanajibiwa kwa wakati..Lakini sasa hapa mwisho utaona kazi yake ya kupeleka maombi ya watakatifu mbele za Mungu inaisha, na inaishia kwa kukichukua kile ‘chetezo’ na kukiweka makaa ya moto yatokayo madhabahuni na kuyatupa juu ya nchi (yaani duniani). Ikiashiria kuwa hakuna tena huduma ya kupeleka maombi ya watakatifu mbele za Mungu, kwani watakatifu wote wameshaondolewa duniani(katika Unyakuo)…kilichosalia ni hukumu tu.

Yule malaika mara baada ya kumaliza kuvukiza uvumba ule mwingi alichokua moto uliokuwa kwenye madhabahu na kuuweka kwenye chetezo chake na kuumwaga juu ya nchi…chetezo ni kifaa kidogo kilichokuwa kinatumika kuwekea ubani (uvumba)..ambacho ndani yake kinawekwa mkaa

wa moto na ubani na kilikuwa na mkono wa Kamba au mnyororo hivi ambacho kuhani mkuu alikuwa ana uwezo wa kutembea nacho ndani ya hekalu wakati wa kufanya upatanisho, na kinakuwa kinatoa moshi wa ule ubani unaochomeka mule ndani(Kutoka 30:5-9) …Hivyo kuhani alipochoma ubani moshi unatoka kwenye kile chetezo na kukijaza chumba chote moshi wa manukato.

 Ufunuo 8:5 ‘Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, KUKAWA RADI NA SAUTI NA UMEME NA TETEMEKO LA NCHI.6 Na walemalaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.’’

Hivyo huyu malaika alipotupa ule moto katika roho duniani kukawa na radi na sauti ya umeme na tetemeko la nchi. Sasa hivyo vitu vitatu, radi, sauti na tetemeko la nchi..Tafsiri yake ndio ipo katika wale Malaika 7 waliopewa baragumu wazipige…, hawa malaika saba ndio walioleta hizo radi, sauti na matetemeko ya nchi, kila mmoja kwa sehemu yake mpaka saba wote walipokwisha kupiga/kupuliza hizo baragumu.

Ufunuo 8:7 inasema:..‘Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea’.

Sasa kabla ya kuingia kwenye baragumu ni muhimu kujua kuwa Baragumu hizo zitaanza Kupigwa baada ya unyakuo kupita, yaani baada ya kanisa kunyakuliwa na kwenda mbinguni..wakati ambapo Mpinga-Kristo atanyanyuka duniani, na kwenda kuketi katika Hekalu la Mungu, katika nchi ya Israeli na kutaka kuabudiwa yeye kama Mungu (ukisoma 2Wathesalonike 2:1-10 utaona jambo hilo).

Kumbuka sasa wayahudi/waisraeli wengi leo hii hawamwamini Yesu kama ndiye Masihi, hivyo wengi hawajawa wakristo bado wanashika desturi za Torati ya Musa, huku wakimsubiria Masihi mwingine aje kuwaokoa, Kumbuka ni Mungu mwenyewe ndio kawafumba macho wasimtambue Bwana Yesu kuwa ndiye Masia wa kweli, hivyo mpaka unyakuo unapita watabakia katika hali hiyo hiyo ya upofu, hivyo wataikosa mbingu… 

Lakini Mungu atawahurumia wao tu na kuwafumbua macho baada ya unyakuo kupita Sasa Wakati huo ndio Israeli watagundua kuwa Yesu Kristo waliyemkataa Zaidi ya miaka 2000 iliyopita ndiye Masihi wao waliokuwa wanamtazamia, watatubu ndipo Bwana atawafungua macho..(saa hiyo watu wamataifa walioachwa kwenye unyakuo wataendelea kudanganyika na kupotea) kwasababu kutakuwa hakuna tena mlango wa Neema kwa watu wa mataifa, Zaidi ya kusubiria kuipokea ile chapa ya mnyama na kuingia katika siku ya ghadhabu ya Bwana..na watu wa mataifa kumbuka ni watu wote tofauti na Taifa la Israeli (yaani waafrika, wahindi, wazungu, wachina na wengine wote).

Hivyo baada ya unyakuo kupita Bwana atawatumia mashahidi wake wawili kwa Roho ya Musa na Eliya, kuwarejesha Israeli kwenye mstari na kuihukumu dunia kwa sehemu Fulani…Kwa uelewa Zaidi juu ya urejesho wa Israeli na huduma ya hawa mashahidi wawili…(fungua mfululizo huu katika sura ya 7 na ya 11 au bofya hapa⏩Ufunuo 7&11…soma yote vizuri kisha ndipo uendelee na hapa)…Kwasababu sehemu kubwa ya baragumu hizi saba zinahusu huduma ya hawa mashahidi wawili. Na baragumu hizi saba zitakuwa ni mwanzo wa UTUNGU, wa siku ile kuu ya BWANA..

Sasa tukirudi kwenye zile baragumu biblia inasema…

Ufunuo 8:7 ‘Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea’.

Kipindi kifupi sana baada ya unyakuo kupita Bwana atawanyanyua Mashahidi wawili na atawapa amri ya kuipiga dunia kama watakavyo ukisoma katika Ufu.11,utaona hilo, mambo haya yatatekelezwa na mashahidi hawa wawili, kutatokea na mtikisiko katika anga, kutakuwa na matukio ya mvua za mawe, ingawa pia katika roho mvua ya mawe inaashiria kitu kingine..Lakini kutakuwa na vipindi vibaya sana vya mvua ya mawe, kama ile ilivyotokea wakati wa wana wa Israeli walipokuwa Misri, ambayo iliharibu mimea yote na mazao yote ya chakula katika nchi ya Misri, na tunasoma ni Musa ndiye aliyeleta pigo lile kwa amri ya Mungu, na kadhalika katika baragumu la kwanza litakapopigwa wale mashahidi wawili ndio watakaoleta mapigo hayo..

Ufunuo 8:8 ‘Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto,

kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu.

9 Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa’’.

Katika pigo hili bado litatekelezwa na hao hao mashahidi wawili, kama vile Musa alivyogeuza maji kuwa damu mbele ya Farao, ndivyo mashahidi hawa wawili watageuza maji kuwa damu mbele ya yule mnyama (Ufu.11:6)..na theluthi ya bahari itakuwa damu…theluthi inayozungumziwa hapo..ni sehemu ndogo ya bahari yaani eneo la mashariki ya kati pale! (Bahari ya Mediterenia na maziwa yaliyo kando kando) Eneo la mashariki ya kati Ndio litakaloathirika na mapigo hayo kwa sehemu kubwa…mahali ambapo yule mnyama atakuwepo, kama vile kipindi cha Farao sio maji yote ya dunia nzima yaligeuzwa kuwa damu hapana isipokuwa ni yale tu ya Misri, ndivyo itakavyokuwa siku hizo,watu wote waliopo mashariki ya kati, maji yatageuka kuwa damu.Na samaki watakufa na shughuli za usafirishaji zitasimama…Huo ni mwanzo wa utungu tu wa hukumu ya Mungu itakayoijilia dunia nzima,

Katika siku za mwisho mara baada ya baragumu kuisha vitakuja vitasa saba, ambavyo hivyo ndio vinabeba hukumu ya Mungu katika utimilifu wote, ndani ya hivyo vitasa sana, maji yote ya dunia nzima yatageuzwakuwa damu, na chemichemi haitakuwa theluthi tena kama tunavyoona hapa katika baragumu hizi.
Tuendelee..

Ufunuo 8:10 ‘Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 

11 Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu’.

Nyota inayozungumziwa hapa sio kimondo..kwasababu haiwezekani kimondo kimoja kiangukie mito yote na chemchemi zote za maji…Nyota inayozungumziwa hapo ni ‘shetani’ yeye ndiye nyota iliyoanguka kutoka mbinguni..Na kwasababu yake yeye mito na bahari na nchi vimepigwa na vinapigwa kwa laana ya Mungu…Ndio maana ukisoma kwenye kitabu cha ufunuo 12:12, utaona inasema… ‘ Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na

bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana

wakati mchache tu’.

Unaona hapo anasema ole wa nchi na bahari, ikimaanisha kuwa kuanguka kwa shetani duniani, bahari itaathirika pia, itageuka kuwa damu, na maji kuwa machungu na

katika pigo hili…la Baragumu ya tatu…Bwana ataipiga mito na chemichemi za maji..Maji yatatiwa uchungu..kama yale wana wa Israeli waliyokutana nayo mahali palipoitwa ‘mara’

Kutoka 15: 22 ‘’Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. 

23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.

 24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa,wakisema, Tunywe nini?’’

Watu wengi wanaokaa katika mashariki ya kati na baadhi ya maeneo duniani..watateseka, lakini pigo hili halitauwa la dunia nzima. 

Ufunuo 8: 12 ‘’Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo’’.

Unazidi kuona, bado ni theluthi inayopigwa sio kitu kizima…Ikifunua kuwa ni mwanzo tu wa Utungu! Itafika wakati sio theluthi tena itakayopigwa bali yote…Malaika huyu wanne alipopuliza baragumu lake, Jua theluthi ya jua ikapigwa…na mwezi, na kama tunavyofahamu jua likipungua nguvu kitu gani kitatokea…ni wazi kuwa kutakuwa na baridi isiyokuwa ya kawaida na baadhi ya shughuli zitasimama…Ndicho kitakachotokea siku hiyo, watu wataona jua limepungua nguvu sasa hapa dunia nzima itaathirika na pigo hili…Na hiyo Itatangaza kuwa kipindi kifupi sana baadaye jua lote litazima..kama tutakavyojifunza tutakapofika kwenye vitasa saba katika Ufunuo mlango wa 16.

Ufunuo 8:13 “Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga”.

Hapa Yohana anaoneshwa Tai akiruka katikati ya mbingu, sasa huyu Tai sio ndege tai, bali ni mmoja wa malaika anayebeba tabia kama za Tai katika roho, ukisoma kwenye tafsiri nyingine utaona ni ‘’angel’’ yaani malaika ndio maana utaona hata Katikati ya wale wenye uhai wanne kulikuwa na mmoja mwenye uso kama wa Tai.

Sasa Malaika huyu Yohana alimwona katika roho akisema…ole wao wakaao juu ya nchi! Kwasababu ya sauti za baragumu za malaika watatu waliobakia..Ikifunua kuwa madhara yatakayoletwa kwa baragumu za hao malaika watatu waliosalia yatakuwa mabaya zaidi ya hao wanne waliotangulia.

Na kama tunavyosoma hapo, inasema ole wakaao juu ya nchi!!…Ikifunua kuwa ni madhara yatakayosababishwa na kuanguka kwa shetani, yatakuwa juu ya hao wakaao juu ya nchi kulingana na ufunuo 12:12 “Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu’’…Madhara juu ya bahari yameshapita…theluthi ya bahari, chemichemi na mito kuwa damu, na viumbe vya majini kufa…sasa yanayofuata ni kwa wale wakaao juu ya nchi..Tutayaona hayo zaidi katika sura inayofuata..

Swali ni je! Umempa Kristo maisha yako?..Una uhakika akija leo utakwenda naye mbinguni?, kama hauna uhakika basi ni wazi kuwa utaachwa akija, kwahiyo utii ushauri wake leo unaosema…

Ufunuo 3:18 “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.

Mfungulie mlango wa moyo wako leo kwa kutubu na kumaanisha kuziacha dhambi zako na yeye atakupokea…Toka kwenye kamba za madhehebu ambazo zinakufungia mlango wa maarifa na kukufanya usimjue Mungu kama anavyotakiwa kumjua.

Bwana akubariki sana..Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 9

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara,  kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani

Print this post

UKWELI UNAOPOTOSHA.

Jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe!..Maandiko yanatuambia Yesu ndiye njia, kweli na Uzima mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye. Ikiwa na maana kuwa hakuna namna yoyote ya kuiona mbingu nje ya Yesu Kristo, yaani unapoizungumzia mbingu unamzunguzia Bwana Yesu. Yeye ndio lile lango na ufunguo wa kuingia mbinguni(Yohana 10:9-16).

Kwa Neema za Bwana leo tutajifunza juu ya UKWELI UNAOPOTOSHA. Si kila ukweli unaozungumzwa lengo lake ni kumwelekeza mtu katika njia ya kweli…Ukweli mwingine lengo lake ni kupotosha!…Kwahiyo upo ukweli unaompeleka mtu kwenye njia sahihi na upo ukweli unapompeleka mtu kwenye njia ya upotofu.

Hebu tafakari hili tukio lifuatalo…

Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.

17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.

18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile”.

Katika tukio hili unaona Mtume Paulo na mwenzake walikutana na mwanamke mmoja kijakazi aliyekuwa na pepo la uaguzi, kwasasa tunaweza kusema alikuwa ni mganga wa kienyeji..Na Yule mwanamke alipowaona tu wakina Paulo, akawatambua hivyo akapaza sauti na kusema ‘hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu wenye kuwahubiria watu njia ya wokovu’…Sasa hapo alikuwa hawaambii wakina Paulo, bali alikuwa anawaambia watu waliokuwa karibu kando kando ya hilo eneo.

Lakini kama tunavyosoma Paulo alihuzunika, akalikemea lile pepo likamtoka?…Unaweza ukajiuliza kwanini Paulo ahuzunike?…angepaswa afurahi kwasababu Yule mtu kazungumza ukweli kuwa wao ni wakina nani, isitoshe kakiri hadharani mbele ya watu wote kuwa wao ni watumishi wa Mungu. Lakini Paulo hakufanya hivyo kwasababu aliijua nia na lengo shetani.

Sasa endapo Mtume Paulo na mwenzake wangekubali zile sifa…ni wazi kuwa moja kwa moja Yule mwanamke angezidi kuaminiwa na watu zaidi ya wakina Paulo wenyewe…Watu wangemheshimu Yule mwanamke kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kujua siri za ndani,..na hivyo watu endapo wangepatwa na matatizo wasingewatafuta wakina Paulo watumishi wa Mungu..wangemtafuta Yule mwanamke mwenye uwezo wa kutambua mambo ya ndani sana, Na matokeo yake mwanamke Yule angezidi kupata jina kuliko wakina Paulo..Hilo ndilo lilikuwa lengo la shetani.

Unajua kuna njama Fulani huwa wanazozitumia wafanya biashara waliofanikiwa ili wawavutie wateja kwao…wanachofanya ni kuwaambia wateja wao ukweli, utakuta mtu atafika labda katika duka lake, na endapo mteja akikosa hiyo bidhaa aliyokuwa anaitafuta…utaona Yule mwuzaji anamwelekeza sehemu nyingine iliyo sahihi ya kuipata hiyo bidhaa…na Yule mteja akienda hiyo sehemu aliyoelekezwa na kupata alichokuwa anakitafuta…hataliamini lile duka alilokwenda kununulia bidhaa bali atamwamini zaidi Yule aliyemwelekeza kwenye hilo duka…kwahiyo mwisho wa siku Yule mteja atakuwa kila akihitaji kitu anamrudia Yule mtu wa kwanza, kwasababu anajua ni muwazi na mwaminifu. Na wafanyabiashara werevu huwa wanajua kabisa ukitaka upoteze soko lako poteza uaminifu na uwazi kwa wateja wako…

Na ndio haya mapepo yalichokuwa yanataka kufanya hapa…yalikuwa yanataka kutengeneza jina (GOODWILL) kwa wateja wake.

Ndio maana Paulo alilikemea lile pepo mara moja na lilipotoka ndipo uwezo wa Mungu ukadhihirika, watu wote wakajua kuwa kumbe nguvu zilizokuwepo ndani ya Yule mwanamke ni ndogo kuliko zilizokuwepo ndani ya Paulo na wenzake…na hivyo lengo la shetani likaharibika palepale. Kwahiyo si kila ukweli unaozungumzwa unakuwa na lengo zuri.

Ndio maana utaona sehemu nyingi sana Bwana Yesu aliyazuia mapepo yasimdhihirishe…utaona sehemu nyingi alizokuwa akipita yalikuwa yanapiga kelele “wewe ndio mwana wa Mungu” n.k na Bwana alikuwa anayakemea, yanyamaze.

Na pia utaona Edeni jambo lililotokea ni hilo hilo, nyoka alimwambia Hawa ukila matunda utakuwa kama Mungu ukijua mema na mabaya…ni kweli hakumwambia uongo, alimwambia ukweli kabisa! lakini ukweli wenye kupotosha maana alipokula lile tunda alikuwa kweli kama Mungu kwa kujua mema na mabaya hata Mungu mwenyewe alishuhudia hilo, lakini ni ukweli ulioambatana na kifo…madhara yake utaona ndio yale utaona alishushwa na kuwa mdogo zaidi hata ya mume wake…ndio maana akaambiwa atatawaliwa na mumewe. Halikuwa lengo Mungu mwanadamu amtawale mwanadamu mwenzake. Hayo ndio madhara ya ukweli unaopotosha.

Na pia lengo lingine la shetani lilikuwa ni kutaka kupandikiza roho ya kiburi ndani ya wakina Paulo, mioyo yao inyanyuke ili wajione kuwa wanaupako..Na shetani anajua Mungu hapendi kiburi au mtu anayejikweza na hivyo wangeshushwa.

Lakini hebu leo hii, mapepo yazungumze na mtumishi yeyote na kuanza kumsifia uone kama mtu huyo hatanyanyuka moyo, utaona ndio atatumia hiyo fursa hata kuyauliza maswali, kumbe hajui huku nyuma nia ya shetani ni nini..Ndugu usisikilize ukweli wa shetani, ni ukweli unaopotosha….usisikilize mahubiri ya shetani, ni mahubiri kweli ya Neno la Mungu lakini ndani yake yanalengo la kupotosha…

Wakati shetani anamjaribu Bwana Yesu kule jangwani alikuwa anamwambiaje??…alikuwa anazungumza ukweli kabisa wa kimaandiko kwamba “jitupe kwa maana imeandikwa atakuagizia malaika zake wakulinde usijikwae”…Huo ni ukweli kabisa shetani anaouzungumza…lakini ni ukweli wenye lengo lingine tofauti na lile lililokusudiwa kwenye huo mstari.

Hivyo biblia inatuonya tuwe waerevu…tuzichunguze roho, sio tuchunguze miili, hapana bali roho na sifa zinazoletwa mbele yetu…

Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

NGUVU YA HEKIMA NA AKILI

RACA

WATU WASIOJIZUIA.



Rudi Nyumbani

Print this post

MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lisifiwe, nakukaribisha mtu wa Mungu tujifunze Maneno ya uzima, na leo tutajifunza ni kwanini Mungu alitaka kumuua Musa mwanzoni kabisa mwa huduma yake japokuwa yeye mwenyewe ndio aliyemuita na kumthibitishia kuwa atakuwa pamoja naye. Tukilifahamu hilo kwa undani itatusaidia na sisi kuielewa tabia ya Mungu, na hivyo kuchukua hatua stahiki tusije tukajikuta tunaangamia kwa uzembe fulani.

Tunafahamu sababu kubwa iliyomfanya Musa akimbie kule Misri ni ile hali ya yeye kutetea chimbuko lake (yaani la Kiebrania), tunaona alipomuua Yule Mmisri aliyekuwa anapigana na Mwebrania alikimbilia nyikani kwa Wamidiani na hakurudi tena Misri mpaka miaka 40 ilipoishia, sasa huo wakati wote alipokuwa katika Ardhi ile ni wakati ambao Mungu alikuwa anampitisha Musa katika madarasa ya kimaisha afahamu vizuri chimbuko lake, Mungu “alimtweza”, hicho kipindi chote, hivyo akafahamu vizuri asili yake, huku akisaidiwa na mkwewe Yethro, ambaye ndiye alimpa binti yake aliyeitwa Sipora awe mkewe, Wote hawa walikuwa ni wazao wa Ibrahimu isipokuwa kwa mama tofauti, Waisraeli walitoka kwa Sara, lakini Wamidiani (yaani wakina Yethro mkwewe Musa), walitokea kwa mke mdogo aliyeitwa Ketura ambaye Ibrahimu alimtwaa baada ya Sara kufa.

Hivyo wote walikuwa ni ndugu, na wote walimwabudu Mungu mmoja, sasa kumbuka wakati huo Torati ilikuwa bado haijafika, kwani Torati ilikuja kutolewa na Musa, lakini lilikuwepo agizo moja KUU ambalo Ibrahimu alipewa na Mungu kwa wazao wake wote, kama dalili ya agano aliloingia yeye na Ibrahimu, na agizo hilo lilikuwa ni TOHARA kwamba wazao wake wote watahiriwe, Hivyo mtoto yoyote anayezaliwa bila kupoteza muda siku ya 8 anapaswa atahiriwe kisha apewe jina..Na kwa kufanya hivyo atakuwa tayari kashahesabika kuwa ni mazao wa Ibrahimu mrithi wa Baraka zote Mungu alizomwahidia Ibrahimu na uzao wake.

Hivyo watoto wote wa Ibrahimu walitahiriwa, haikujalisha ni wa mke yupi ni wa kijakazi Hajira, au wa Sara au wa Ketura…haikujalisha hiyo, wote walitahiriwa kufuata maagizo waliyopewa.. Hivyo ilikuwa ni jambo la ajabu na la kushangaza itokee mzao yoyote mpaka amefikia mtu mzima hajatahiriwa,kwanza ulikuwa unaonekana ni kafiri, na unatengwa na jamii yote, Kama tu walikuwa hawashirikiani kwa chochote na mataifa ambayo hawajatahiriwa unadhani ukiitwa mzao wa Ibrahimu halafu hujatahiriwa utachukuliwaje?. Sio tu wazao wa Ibrahimu watakukataa bali pia Mungu mwenyewe atakukataa.

Sasa Musa alilifahamu hilo, mpaka akazaa watoto, lakini hakuliweka akilini kuwa kila mzao wa Ibrahimu wa kiume anapaswa atahiriwe, yeye alipuuzia, alilichukulia kiwepesi wepesi tu, kama jambo lisilokuwa na umuhimu mkubwa kwenye mambo ya rohoni na hivyo mpaka akazaa mtoto,akakua mkubwa, siku ya 8 ikipita, mwezi ukapita, miaka ikapata yupo naye tu…

Wakati huo wote Mungu hakumsemesha chochote, mpaka ikafikia wakati Mungu alipomwita kule mlimani, na kumpa maelekezo ya kwenda kuwaokoa wana wa Israeli, Mungu akamthibitishia kuwa atakuwa naye, kwa miujiza na ishara kubwa..

Na ndivyo ilivyo leo hii watu wanaona Mungu akitembea nao kwa ishara kubwa na miujiza wanapumbazika wakidhani kuwa hiyo yote ni kwasababu Mungu amependezwa nao.

Lakini angalia kilichomtokea Musa, kumbe huku nyuma Mungu alikuwa amepanga kumuua, kabla hata hajafika mbali, akiwa njiani usiku, Yule malaika ambaye alienda kuwaua wazaliwa wa kwanza wa Wamisri alikuwa ameshaandaliwa kumamliza Musa habari yake iwe imeishia pale pale.

Lakini mke wake Sipora kuona vile aligundua kuwa ni lile kosa la mume wake kuwa mzembe kutotimiza maagizo ya Mungu kwa mwanae, hivyo alichofanya haraka, alidhubutu kwenda kinyume cha taratibu akachukua jiwe kali akakata govi la mwanae, japo Sipora hakupendezwa na kitendo kile na ndio maana akamwambia Musa “Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi.” Hayo tunayasoma katika kitabu cha Kutoka:

Kutoka 4:24 “Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, Bwana akakutana naye akataka kumwua.

25 Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi.

26 Basi akamwacha. Ndipo huyo mkewe akanena, U bwana arusi wa damu wewe, kwa ajili ya kutahiri.”

Unaona, Musa alipata neema tu kwa Mungu pamoja maono yake makubwa ya kwenda kuwaokoa wana wa Israeli lakini asingefika mbali. Mambo kama hayo hayo yalimtokea Balaamu, aliambiwa asiwalaani Israeli lakini yeye akakang’ang’ania kwenda kule kwa Balaki ambako Mungu amemwambia asiende….lakini yeye akakazana kung’ang’ania kwenda mwishowe Mungu akamruhusu aende na kumpa maagizo ya kufanya huko aendako…. lakini kumbe njiani Mungu a alikuwa amepanga kumuua, Ni Punda tu ndio aliyemsaidia vinginevyo safari yake ingeishia pale (Hesabu 22).

Ndugu, Ni vizuri tukaitambua tabia ya Mungu ili na sisi yasitukute kama hayo, Leo hii Sipora wala Punda hawapo. Kumbuka wakati ule Tohara ya mwili ilikuwa ni muhimu mpaka Mungu alitaka kumuua Musa kwa uzembe wa Tohara ambayo si ya kwake, itakuwaje wewe ambaye sasahivi unaipuuzia tohara ya Roho yako ambayo hiyo inanguvu mara nyingi sana kuliko ile ya mwilini.

Biblia inasema:

Warumi 2:28 “Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu”.

Utasema, mbona Mungu huwa ananionyeshaga maono?, mbona huwa kila siku ananishuhudia kwenye ndoto mimi ni mteule wake, Mbona huwa ananitumia kutenda miujiza na maajabu, mbona huwa anajibu maombi yangu, mbona huwa ananipigania katika biashara zangu na shughuli zangu na mambo yangu yote, ..Lakini nataka nikuambie kama hujatolewa govi katika moyo wako, KIFO KITOKACHO KWA BWANA KIPO MBELE KINAKUNGOJA.

Sasa swali TOHARA hii YA ROHO ZETU INAFANYIKAJE?

Wakolosai 2:11 “Katika yeye [YESU KRISTO] mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.

12 Mkazikwa pamoja naye katika UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.”

Unaona hapo, tohara iliyosahihi baada ya kuamini kwa mkristo, kwa kuyaacha maisha yake ya kale, ni KUBATIZWA, kama ishara ya kwamba umekufa pamoja naye na kufufuka pamoja naye. Watu wengi wanapuuzia haya maagizo marahisi wanayaweka kando halafu wanataka kwenda kumtumikia Mungu..

Wanapumbazika pale wanapoona ishara zikifuatana nao, lakini kumbe Mungu kaweka kifo mbele yao, ndugu weka kwanza msingi wako imara ndipo nyumba itasimama, utawahubiria nini watu wamfuate Kristo wakati wewe mwenyewe huamini katika tohara ya Roho yako na katika ubatizo ambao Bwana wako alikuwa ni mkamilifu aliuendea wewe ni nani usifanye?…

Ikiwa wewe ulishamwamini Kristo, au ndio unampokea leo hii, usikawie kwenda kubatizwa ipasavyo ili kutimiliza haki yote. Na kumbuka pia ubatizo sahihi ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi na uwe ni katika JINA LA YESU KRISTO ambalo ndilo jina la Baba na mwana na Roho Mtakatifu..sawasawa na mitume walivyobatiza (katika Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5).

Hivyo Ikiwa unajiiona wewe ni nabii mkuu zaidi ya Musa, au mtu wa rohoni, basi uyatumbue ya kuwa hayo ni maagizo ya Mungu.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 


 

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE! UNAWEZA KUBATIZWA NA USIPOKEE ROHO MTAKATIFU?. NA JE! UNAWEZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU KWA KUWEKEWA MIKONO?

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOA?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! KARAMA NI UTHIBITISHO WA KUWA NA MUNGU?

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe…Karibu tujifunze Neno la Mungu,.

Mojawapo ya jambo linalochanganya watu wengi wa Mungu..Na hata mimi lilikuwa linanichanganya mwanzoni sana wakati nampa Bwana maisha yangu…Ni jinsi ya “kuwatambua watumishi wa uongo”. Nilikuwa nachanganyikiwa kuona mtu anafanya miujiza kwa jina la Yesu, anatoa pepo, anamwombea mtu anapona, anaona maono, anatoa unabii n.k lakini bado mtu huyo huyo ni mkorofi, ni mtu mzinzi, mtukanaji, ni mtu wa majivuno n.k…Nilikuwa nipo njia panda sana inawezekanikaje mtu akawa hivyo na Mungu bado yupo naye. Nilipojaribu kuwashirikisha baadhi ya watu kwanini jambo hilo linatokea, wengi wakaniambia wanatumia nguvu za giza. Wanakwenda kwa waganga kupokea nguvu za kichawi kisha wanakuja madhabahuni kufanya wanayoyafanya.

Lakini baada ya kujifunza zaidi, nilikuja kufahamu kuwa wengi wao hawatumii nguvu za giza hata kidogo. Leo tutajinza kwa kutumia Biblia ni kwanini hawatumii nguvu za giza.

Ni kweli wapo ambao wanatumia nguvu za giza kufanya miujiza, lakini hao hatutawazungumzia kwasasa kwasababu si wengi sana kama wale ambao hawatumii nguvu za giza.

Tukisoma biblia tunamwona Nabii mmoja ambaye alikwenda kinyume na maagizo ya Mungu, kwani aliambiwa baada ya kutoa unabii kwa mfalme Yeroboamu aondoke na asirudie njia aliyoipitia, na pia asizungumze na mtu njiani. Lakini ukisoma habari ile utaona alidanganywa na nabii mwenzake akayaacha maagizo ya Mungu na hivyo ikawa mauti kwake. Hebu tenga muda usome hichi kisa kwa utulivu kisha tutaendelea.

1 Wafalme 13: 6 “Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.

7 Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu.

8 Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;

9 maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.

10 Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.

11 BASI NABII MMOJA MZEE alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao.

12 Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda.

13 Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda.

14 Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.

15 Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.

16 Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;

17 kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.

18 Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.

19 Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake.

20 Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha;

21 akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako,

22 bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.

23 Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda.

24 Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti”.

Sasa kama umeelewa habari hiyo utaona kuwa huyo Nabii Mzee alimdanganya huyo nabii mwingine…lakini baadaye Mungu akampa maono huyo nabii mzee amwambie huyo nabii mwingine aliyedanganywa kuwa atakufa kwa kulikaidi Neno la Mungu.

Sasa hapo unaweza ukajiuliza kwanini Mungu aendelee kumpa maono Yule nabii mzee aliyemwambia uwongo mwenzake na kumsababishia mauti..Hiyo inadhihirisha kuwa MTU ANAWEZA KUONA MAONO na Bado akawa mtenda dhambi..mtu anaweza kuwa mwongo au mwasherati na bado Mungu akaendelea kumpa maono. Unaona?..inaogopesha sana!. Huyu nabii Mzee hapa hakutumia nguvu za giza kumtabiria kuwa atakufa. Hapana bali alitabiri kwa uweza wa Mungu. Alifanya dhambi kuzungumza uwongo, lakini Mungu hakumpokonya karama aliyokuwanayo ya kinabii. Na kama hakutubia dhambi hiyo mpaka kufa basi siku ya hukumu atakwenda kwenye ziwa la moto.

Ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 7: 22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Hapo anasema “hatukufanya unabii kwa jina lako?”… ikiwa na maana kuwa sio kwa nguvu za mapepo bali kwa jina lake…Mfano wa huyo nabii aliyemdanganya mwenzake na baadaye akamtolea unabii kwa jina la Bwana…Lakini Bwana Yesu anasema watu wengi wa namna hiyo siku ile atawafukuza na kuwaambia siwajui kamwe…ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu.

Hivyo ndugu hapo tunajifunza kuwa, usiangalia karama uliyonayo au mtu mwingine anayejiita mtumishi aliyonayo…bali jiangalie matendo yako ndipo ujihukumu kuwa upo sawa na Mungu au la! Usijiangalie karama yako ya kuimba ukadhani hichi ndicho kinachompendeza Mungu, au karama yako ya kiualimu, au karama yako ya kunena kwa lugha, au karama yako ya kinabii, unaona maono mengi mpaka ya kitaifa ukadhani wewe ni spesheli sana kwa Mungu…badala yake jiangalie ndani yako je! Unayatenda mapenzi ya Mungu je! Kuna utakatifu ndani yako??.

Unaweza ukawa kila anayekuja kwako ukimwombea anapona au tatizo lake linaondoka…au kila anayekuja kwako Bwana anakufunulia tatizo lake kwenye maono…lakini bado ukawa mbali na Mungu…Unaweza ukawa umetokewa na malaika au Bwana Yesu mwenyewe lakini siku ile akakwambia sikujui…Mungu anaweza akawa anaongea na wewe kila siku na kukupa maagizo ya kufanya hichi na kufanya kile kama alivyompa huyu Nabii Mzee, lakini siku ile bado akakukataa..Balaamu alikuwa ni nabii anayezungumza na Mungu na kupokea maagizo kutoka kwa Mungu lakini bado alikuwa ni mchawi.

Biblia inasema wazi katika Waebrania 12:14 kwamba PASIPO UTAKATIFU HAKUNA MTU ATAKAYEMWONA MUNGU.

Hivyo ni wakati wa kutafuta kuyatenda mapenzi ya Mungu ambao ndio utakatifu, Na si kuangalia upako wala karama kama uthibitisho wa kuwa Mungu yupo pamoja na sisi.Ikiwa karama itafuata baada ya utakatifu hiyo ni vizuri sana. Vile vile si wakati wa kumhukumu mtumishi wa ukweli au wa uwongo kwa karama anazozidhihirisha..bali tutawatambua kwa matunda yao biblia inatuambia hivyo (Mathayo 7:16)…na Matunda yanayozungumziwa hapo ni matendo yao…

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?

 KARAMA YA ILIYO KUU NI IPI?

KARAMA YA MUNGU NI IPI?

JE KUNENA KWA LUGHA MPYA KUKOJE? NA HIZI LUGHA NI ZIPI, NA JE! NI LAZIMA KILA MKRISTO ALIYEPOKEA ROHO MTAKATIFU ANENE KWA LUGHA MPYA?.


Rudi Nyumbani

 

Print this post

JIPE MOYO.

Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, lisifiwe daima. Nakukaribisha tushiriki pamoja Baraka za rohoni. Leo tutaitazama kauli hii moja ambayo Bwana Yesu aliitoa siku ile kwa wanafunzi wake baada ya kuwaagiza mambo yote ya kufanya na kuwaaga, alimalizia na kusema..

Mathayo 28:20 “….. na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”.

Kauli ni nyepesi kuisikia ni ya faraja kuisikia lakini imebeba tafsiri kubwa sana nyuma yake…Kwa lugha rahisi ni hii kama mbeleni Bwana Yesu asingeona kuwa watahitaji msaada wake asingewaambia maneno hayo, asingeona kama mbeleni kuna shida, asingewaambia maneno hayo, kama asingeona mbeleni kuna milima na mabonde bado asingewaambia kauli hiyo, kwani wangekuwa na uwezo wa wenyewe kutembea katika raha mpaka siku atakapokuja kuwachukua tena.

Lakini aliona kuna vifungo vingi mbeleni vinawasubiria watu wake, na hivyo watahitaji mtu wa kuwatia moyo, aliona kuna magonjwa mengi mbeleni hivyo watahitaji mtu wa kuwaponya, aliona kuna kuchukiwa na kutengwa kwa ajili ya jina lake hivyo watahitaji mtu wa kuwafariji na kuwa nao karibu, aliona kuna wakati watu wake watashindwa kujua jambo la kufanya na hivyo watahitaji mshauri wa karibu, aliona wataonewa na wenye dhambi na hivyo watahitaji mtetezi, aliona watapita katika bonde la uvuli wa mauti hivyo watahitaji mchungaji wa kuwaongoza, aliona kuwa wakati watazungukwa na maadui pande zote hivyo watahitaji mlinzi,..n.k. Yote hayo Bwana aliyaona mbeleni na ndio iliyokuwa sababu ya yeye kuitoa kauli kama ile kwa wanafunzi wake.. “NA TAZAMA, MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, HATA UKAMILIFU WA DAHARI.” Dahari maana yake ni “nyakati au muda”..kwahiyo hapo Bwana alimaanisha atakuwa pamoja nao mpaka mwisho wa nyakati au muda, au kwa lugha nyepesi zaidi tunaweza kusema mpaka mwisho wa dunia.

Sasa utaona huko nyuma alishakwisha kuwaambia..katika Yohana 16.33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni MNAYO DHIKI; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu..”

Hii inatufundisha watakatifu wanaomngojea Bwana, kuwa wavumilivu…Ndugu usikatishwe tamaa na dhiki hizi za kitambo kifupi. Wakati mwingine katika safari yako utakapokutana na misukosuko kwa ajili ya YESU, wala usidhani unayo bahati mbaya, badala yake JIPE MOYO, kwani ni mambo yaliyokwisha tabiriwa yatawakuta waaminio wote, hivyo uwe na uhakika kuwa unapopitia hayo Bwana YESU yupo pembeni yako kukuhudumia kwa namna usiyoijua wewe, anakuwazia mawazo yaliyo mema siku zote, hatauacha mguu wako ujikwae kamwe, haijalishi mawimbi yamekuwa mazito kiasi gani Hutakufa UTAISHI! Nawe utayasimulia matendo ya Bwana (Zab 118:17) ikiwa bado unamshikilia tu huiachi imani, atakupa nguvu ya ajabu ya kuendelea mbele, ulimwengu utashangaa inakuwaje huyu mtu anapitia hali hii mbaya lakini hatetereki katika Imani, hiyo yote hawajui kuwa ni kwasababu ile Ahadi ya Kristo inatimia juu yako kuwa atakuwa pamoja nawe siku zote mpaka utimilifu wa dahari. Hivyo nataka nikuambie JIPE MOYO, mtazame Yesu songa mbele.

Lakini kumbuka ndugu ahadi hii ni kwa wale wanafunzi wa Kristo tu, sio kila mtu, swali Je! Wewe ni mwanafunzi wa Kristo?. ikiwa bado upo kwenye dhambi, ukweli ni kwamba huna mfariji, wala mwombezi, wala mtetezi, wala mshauri. Wewe ni yatima haijalishi una ndugu wengi wa mwilini kiasi gani… una utajiri wa nje mwingi kiasi gani bado ni maskini, au unayo afya kiasi gani, wewe ni bado ni mgonjwa tu!..huna ulinzi wowote ndani yako, ni nyumba isiyokuwa na msingi, ambayo siku yoyote inaweza kudondoka, Na ndio maana unashindwa kustahimili mawimbi yote ya ibilisi yanayokuja juu yako ni kwasababu hujajengwa juu ya MWAMBA.

Zaburi 1: 4 “Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo”.

Ufunuo 3: 17 “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja name”.

Lakini leo hii habari njema ni kuwa Yesu bado anagonga kwenye milango ya mioyo ya watu, mkaribishe sasa, ayageuze maisha yako, atembee na wewe , afanyike kuwa mchungaji wako mpaka siku ya ukombozi wako,ili utembee kwa ujasiri hata ukifa leo ujue unapokwenda.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu.

Kama wengi wetu tunavyojua kuwa hakuna wokovu nje ya Yesu Kristo, wala hakuna Maisha nje ya Yesu Kristo. Kama Mtume Paulo alivyoandika kwa uweza wa Roho kwamba ‘Mauti ilikuja kwa njia ya mtu mmoja(Adamu)…kadhalika uzima utaletwa kwa njia hiyo hiyo ya mtu mmoja (ambaye ni Kristo)’.

Kwahiyo yeye peke yake ndio njia iliyo sahihi na iliyothibitishwa ya kumfikia Mungu..njia nyingine zote tofauti na yeye ni za upotevu, haijalishi zina wafuasi wengi kiasi gani.

Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani, alizungumza kwa mifano mingi, yote ni kwa lengo la kumfanya mwanadamu aelewe mpango wa Mungu juu ya Maisha yake…Alitumia mifano ya miti, mashamba, wafanyabiashara, wakulima,familia, wageni, wafalme na mingine mingi ambayo hata haijaandikwa kwenye biblia, kwasababu kama yangeandikwa mambo yote aliyoyafanya moja moja…biblia inasema hata dunia isingetosha kwa jinsi vitabu vingekuwa ni vingi (Yohana 21:25)..

Lakini tunaona baada ya kuondoka alikuja tena kuzungumza na Mtume Yohana katika maono , alipokuwa katika kisiwa kile cha Patmo na kumpa mfano namna ambayo huwa anavyowajilia watu wake alimwambia…

Ufunuo 3: 20 ‘’Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami’’.

Mfano huo Bwana Yesu aliutoa kuonyesha ujio wake kwa mtu ni kama wa mgeni…Ujio huu sio wa kulichukua kanisa…kwasababu ujio wa kuja kulichukua kanisa alisema utakuwa kama ujio wa mwizi…hata kuja kwa kugonga na kusihi, bali atakuja usiku watu wakiwa wamelala na atachukua walio wake na kuondoka….ndio maana unyakuo ukipita sio watu wote watajua…Kwahiyo kuna kipindi Bwana Yesu atakuja kama mgeni na kuna kipindi atakuja kama mwivi.

Sasa katika mfano huu..anasema tazama nasimama mlangoni nabisha! Kubisha maana yake ni kugonga mlango huku unatoa sauti Fulani kama hodii hodii!! Hiyo ndiyo maana ya kubisha!..Kwahiyo hapa Bwana anasema nasimama nabisha, halafu anasema mtu akiisikia sauti yake na kuufungua mlango ataingia…hii ikiwa na maana kuwa mtu anaweza akaisikia sauti yake na asifungue…au mtu anaweza asiisikie kabisa sauti yake…labda kutokana na kwamba amelala au kutokana na usumbufu uliopo ndani ya nyumba kuwa mkubwa (labda kelele za miziki au watu).

Na baada ya kuingia utaona anasema…’nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami’…sasa tafakari hapo kwa makini, hasemi tutakula pamoja hapana!…bali anasema nitakula pamoja naye…na yeye pamoja nami…ikiwa na maana kuwa alipokuwa anangonga alikuja na chakula chake, hakuja mikono mitupu…kadhalika na yule mtu aliyemfungulia atamkuta na chakula chake…na hivyo kila mmoja atashiriki na mwenzake kile alichokiandaa.

Sasa ukiingia ndani Zaidi kuutafakari mfano huu utaona kuwa unahusu wakati wa jioni…lugha yetu ya Kiswahili haijajitosheleza katika maneno mengi…lakini kama ukisoma tafsiri nyingine kama zile za kiingereza au kigiriki utaelewa vizuri kuwa ni wakati wa jioni ndio Bwana alikwenda kugonga mlango.. ni wakati wa chakula cha jioni (evening supper).

Kwahiyo katika mfano huo Bwana anakuja kugonga mlango wakati wa jioni…akiwa na chakula chake, hajaja kudoea wala kula vya watu bure!…Inaashiria kuwa Kristo anapotaka kuja kuingia katika Maisha yetu sio kwa lengo la kutaka vya kwetu, au kutuharibia Maisha hapana! Bali ni kwa lengo la kutupa sisi faida. Na atakuja jioni, hizi ni nyakati za jioni, wakati wa kumalizia wa mwisho wa dunia ndugu.

Na kama tunavyojua tabia ya mgeni anapogonga, huwa hagongi mfululizo kama vile analazimisha mlango ufunguliwe…bali utaona anagonga kidogo kwa utaratibu kisha anatulia kidogo, akiona hasikiwi atarudia tena kwa sauti kidogo baada ya muda Fulani kupita..atafanya vile kwa kipindi Fulani, akiona hakuna kabisa majibu labda yule mtu amelala usingizi mzito hawezi kusikia hatavunja mlango ataondoka arudi tena baadaye au arudi wakati mwingine…Lakini akigundua yule mtu kule ndani anamsikia lakini hataki kumfungulia makusudi tu! Basi ataondoka asirudi tena…kwasababu anajua hahitajiki mahali pale.

Na Ndivyo hivyo Kristo anavyogonga mioyoni mwetu leo hii, atakutumia wahubiri pale mahali ulipo, kwa kukusihi umfungulie moyoni mwako aingie…akiona bado humsikii ataongeza watumishi kila mahali utakapokwenda hata kwenye mitandao utakutana na Neno lake, sauti yake utaisikia kila mahali ikikuita, utakapoitii ataingia, na vitu alivyokuja navyo kukuletea hutaamini macho yako kuvioona..Lakini endapo unajua kabisa huyu ni Kristo ananiita kupitia mahubiri, na kuwa hii ni sauti yake kabisa na unafanya makusudi kutokumfungulia…basi ataondoka na Neema hiyo itakwenda kwa wengine..

Ndugu usidanganyike kuwa utatubu uzeeni, Sauti ya Mungu itarudia kuita kwa wale watu ambao wakati Bwana amegonga wapo usingizini…wale watu ambao nguvu za giza zimewafunga kiasi kwamba hawawezi kuisikia injili…hao ndio Bwana ataendelea kuwaita kila wanapokwenda, mpaka watakapoamka usingizini, na kundi hili mara nyingi ni lile kundi ambalo halijawahi kabisa kupata nafasi ya kuujua msingi wa Imani ya kikristo, wale watu ambao wamezaliwa katika familia za kipagani, au familia za watu wasio wa dini, na hawamjui Kabisa Kristo…hawa ni sawa wapo usingizini au wapo kwenye makelele ya ulimwengu kiasi kwamba hawawezi kuisikia sauti ya Bwana Yesu..Hivyo Bwana ataiongeza sauti yake mpaka wasikie.Watapata Neema kubwa Zaidi.

Lakini kwa wengine ambao wamezaliwa katika Ukristo tangu udogoni, wamehubiriwa vya kutosha kuhusu msalaba, na wanaielewa kabisa sauti ya Yesu inapoita, na wengine mpaka wamemwona Bwana katika maono, na wamepewa ishara kadha wa kadha, Bwana akiwaita na hawataki kusikia…Kristo ataondoka kwao na asirudi tena kamwe. Wengi hawapendi kusikia hivi lakini huu ndio ukweli maandiko yanasema hivyo..Wana wa Israeli Taifa la Mungu yaliwatokea hayo, si Zaidi watu wa mataifa.. Bwana Yesu aliwaambia waisraeli maneno haya, baada ya kuwaonya mara nyingi na kushupaza shingo zao haya ndio aliyowaambia:

Mathayo 23:37 ‘’Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.

39 Kwa maana nawaambia, HAMTANIONA KAMWE TANGU SASA, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana’’.

Aliwaambia ‘’hamtaniona kamwe tangu sasa’’..Hili Neno ni kali sana na linaumiza…’’kutengwa na Mungu milele’’..Si ni afadhali tutengwe na wanadamu kuliko Mungu…Ni heri wanadamu wote wanichukie na kunitenga lakini sio Mungu, ni heri nichokwe na wanadamu wote lakini sio Mungu.

Hebu tafakari leo hii Kristo anakwambia haya maneno ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’!!!…Yaani wewe na Kristo ndio Basii!!…

Leo hii usikiapo maneno haya kwenye mtandao, na bado hutaki kuacha dhambi na ulimwengu, kumbuka haukuwa mpango wa Mungu usikie injili yake kwa njia hii ya mitandao..Mpango wake ulikuwa siku ile ile ulipoisikia injili kwa mara ya kwanza ulipohubiriwa na mtu aliyeshika biblia mkononi ungeamini, kulikuwa hakuna sababu ya wewe kuja kusikia tena injili hapa……lakini kwasababu Moyo wako ulikuwa mgumu, ndio maana amekufuata kwa njia nyingine hii ya mtandao..ili awe na uhakika kabisa unaisikia sauti yake. Lakini unaidharau..pengine hii ndio sauti yake ya mwisho kwako, isikie ufungue, asije akakwambia kama alivyowaambia wayahudi ‘HUTANIONA TENA KAMWE TANGU SASA’….Maneno haya yalizungumzwa na Kristo yule yule aliyesema ‘njooni kwangu nyinyi nyote’….hapa anasema ‘hamtaniona tena kamwe’…sehemu nyingine anasema ‘tokeni kwangu’.

Pale ulipo mwambie Bwana natubu dhambi zangu zote, na kukusudia kutokuzifanya tena, tubu kabisa kwa kudhamiria kabisa kuacha kuzifanya.Mfungulie mlango na yeye ataingia ndani yako haraka kukugeuza, hataanza kukulaumu kwanini nimegonga muda wote huo ukufungua, yeye si kama sisi, moja kwa moja atazungumza na wewe na muda wa kula ukifika atakufungulia hazina zake alizokuletea mshiriki pamoja, atakupa baraka zote za mwilini na rohoni, na kukufundisha maneno yake ya uzima. Utakuwa na tumaini la uzima wa sasa na ule wa baadaye.

Lakini usipotaka ataondoka, na siku moja atakuja kama mwivi, siku hiyo hatokuja kwako tu bali atakuja kwa ulimwengu mzima, atavunja atavunja mlango na kuwaiba waliowake ndani, na kwenda nao mbinguni, huku nyuma moto utawaka. Usitamani uwepo hicho kipindi cha dhiki kuu. FIKIA TOBA LEO!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001 312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Ni maombi yangu kuwa utakitendea kazi ulichokisikia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 


Mada Zinazoendana:

TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.


Rudi Nyumbani

Print this post