Kama tukisoma biblia katika agano la kale, tunaona kuwa mambo yaliyokuwa yanamkasirisha sana Bwana Mungu na kumtia wivu, sio maovu yaliyokuwa yanatendeka katikati ya WATU WA MATAIFA, La! bali ni yale yaliyokuwa yanaendelea katikati ya watu wake (ISRAELI), watu alioingia nao agano. Na ndio maana zile amri 10 zilitolewa kwa wana wa Israeli tu! Na sio kwa watu wa mataifa yote ulimwenguni,.
Hivyo hao ndio watakaohusika na adhabu kwa Mungu endapo watakiuka mojawapo ya amri hizo. Kwa mfano mwanaume aliyemuoa mke wake kamwe hawezi kuona wivu kwa wanawake wengine wasiokuwa wake anapowaona wanafanya ukahaba, lakini akimwona mke wake aliyempenda na kumtolea mahari anafanya hivyo ni lazima aingiwe wivu na hasira na ghadhabu nyingi na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu na Israeli.(Yeremia 3:14)
Kuna wakati ulifika maovu yalizidi sana katika nyumba ya Israeli ndipo Mungu akamuonyesha Ezekieli maono ya mambo yaliyokuwa yanaendelea kwa siri katikati ya watu wake. Alionyeshwa watu wakiabudu JUA katika ya nyumba yake, wengine walikuwa wanamlilia TAMUZI,(miungu ya wakaldayo), wengine wanaabudu vinyago kwa siri katika nyumba zao, na makuhani wanavukiza uvumba kwa miungu migeni,(Ezekieli 8:1-18), alionyeshwa dhuluma katika mji na umwagaji damu,na upotoshaji hukumu umejaa, na zaidi sana kulinyanyuka manabii wa uongo waliokuwa wanawatabiria watu amani wakati hamna amani. Yote haya yalimchukiza Mungu sana mpaka kuifikia kilele cha Mungu kuleta hukumu kwa watu wake wote.
Lakini kabla maangamizi hayajaja Mungu huwa anawatenga waovu na wema katikati ya watu wake kwa kuwatia ALAMA..kumbuka hawatengi hao watu katikati ya ulimwengu wote, hapana bali ni katikati ya watu wake(ISRAELI)..watu wa ulimwengu tayari Mungu alishawawekea hukumu yao katika siku ile. Na ndivyo alivyoonyeshwa Ezekieli katika habari hii..Tunasoma.
Ezekieli 9:1-11
“1 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru WALE WANAOUSIMAMI MJI wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake CHA KUANGAMIZA mkononi mwake. 2 Na tazama, watu SITA wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. 3 Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. 4 Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWASABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE. 5 Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; 6 Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote MWENYE HIYO ALAMA; TENA ANZENI KATIKA PATAKATIFU PANGU. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba. 7 Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji. 8 Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu? 9 Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; MAANA HUSEMA, BWANA AMEIACHA NCHI HII, NAYE BWANA HAONI. 10 Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao”. 11 Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.”
“1 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru WALE WANAOUSIMAMI MJI wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake CHA KUANGAMIZA mkononi mwake.
2 Na tazama, watu SITA wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
3 Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
4 Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWASABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE.
5 Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma;
6 Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote MWENYE HIYO ALAMA; TENA ANZENI KATIKA PATAKATIFU PANGU. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
7 Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji.
8 Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
9 Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; MAANA HUSEMA, BWANA AMEIACHA NCHI HII, NAYE BWANA HAONI.
10 Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao”.
11 Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.”
Hukumu hii iliyoletwa na hao malaika 6 ilikuja kutimia pale wa-babeli walipokuja kuuteketeza mji na kuwauwa wayahudi vijana, wazee na watoto, na kuiacha nyumba Israeli ukiwa isipokuwa kikundi kidogo sana kilichokuwa kinaugua na kulia juu ya maovu ya Israeli hao tu ndio waliosalimika(Ndio wale waliotiwa Alama katika roho) wengine wote walikufa na kuchukuliwa utumwani. Soma 2Wafalme 25:8-12, Sefania 3:11-13. utaona jambo.
Ndivyo ilivyo hata sasa hivi, Maovu makubwa yanayopelekea hasira ya Mungu kumwaga sio yatokanayo na watu wasiomjua Mungu.Hapana bali ni kwasababu ya maovu yanayoendelea katika nyumba ya Mungu (yaani kanisa), Katikati ya WAKRISTO aliowanunua kwa damu ya thamani nyingi wivu wake ndimo ulimo.
Kumbuka wana wa Israeli walidhani kuwa Mungu haoni waliyokuwa wanayafanya kwa siri, japo aliwapa muda mrefu wa kutubu lakini hawakugeuka mpaka kikombe cha ghadhabu kilipojaa hata kukawa hakuna kusamehewa tena, pale walipotengwa WEMA kati ya WAOVU.
Na katika kanisa la Kristo vivyo hivyo maovu yanayoendelea sasa hivi ni mengi mno vitu kama Siasa, ibada za sanamu ( sanamu za watakatifu waliokufa zamani mfano bikira Maria zikiabudiwa n.k.), kanisani kuna vichekesho na mizaha, mchungaji ni mlevi, mwasherati, na mpenda fedha, mtu anajiita mkristo lakini ni vuguvugu, leo yupo kwa Mungu kesho yupo kwa shetani, leo anaenda kanisani kesho disko, leo anavaa vizuri kesho kimini,.leo anamwimbia Mungu kesho anaimba nyimbo za kidunia, leo anasali kesho anasengenya. n.k.
Sasa mambo kama haya ndiyo yanayochochea ghadhabu ya Mungu, ni heri haya yangetendeka kwa mtu asiye mkristo kuliko mtu anayesema yeye ni mkristo na kakombolewa na damu ya Mungu na bado anatenda mambo kama hayo huko ni kumtia Mungu wivu mkubwa sana.
Lakini pamoja na hayo kabla Mungu hajashusha ghdhabu yake huwa anawatia ALAMA kwanza WATU WAKE waaminifu katikati ya wanaojiita wakristo, hawa anawatenga na kuwaepusha na mabaya yanayokuja mbeleni. Ndio kitu kinachoendelea sasahivi katika kanisa. Japo yanaonekana mambo ya ajabu na yasiyofaa katika Kanisa, Mungu anaendelea kuwatia muhuri wale waliojazwa Roho na waliowaaminifu na kuwaepusha na ile ghadhabu kwa KUWANYAKUA mbinguni kisha baadaye wale waliosalia wasiotiwa muhuri/alama wataangamizwa, katika siku ile kuu ya Bwana inayotisha.
Biblia inasema Nuhu na Luthu walikuwa ni watu wenye haki wakilia juu ya maovu yaliyokuwa yanaendelea katika nchi, hivyo Bwana akawaepusha na Hukumu iliyokuwa inakuja..Kadhalika Bwana YESU pia alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Luthu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.
Hivyo ndugu, Kanisa tunaloishi sasa ndilo la mwisho linaloitwa LAODIKIA. Na ujumbe Bwana alioutoa kwetu sisi ni huu;
Ufunuo 3: 14-20
” Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “
” Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “
Wanaozungumziwa hapa ni wanaojiona kuwa ni wakristo, na sio watu wasiomjua Kristo, ule mfano wa magugu na ngano unawakilisha kundi lililopo kanisani..mfano wa wanawali 10, watano werevu na watano wapumbavu wote ni wanaojiona kuwa ni wakristo na sio watu wa wasiomjua Mungu. Hivyo Bwana alishatoa ONYO kwa wakristo wote wa kanisa hili tulilopo sasa wote walio vuguvugu kuwa ATAWATAPIKA, tena anasema ni HERI kuwa baridi kabisa au moto kuliko kuwa hapo katikati.
Huu ni wakati wa kufanya IMARA WITO wako na UTEULE wako. Kitu kinachoendelea sasahivi katika roho ni BWANA kuwatia alama wale wanaenenda katika ukamilifu na UTAKATIFU, wasiojitia unajisi na mambo ya ulimwengu huu, walioamua kumwishia Bwana tu na si kingine. Iogope ghadhabu ya Mungu inayokuja tubu sasa uyaweke mambo yako vizuri unyakuo usikupite.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
CHAPA YA MNYAMA
WITO WA MUNGU
SABATO HALISI NI LINI, JE! NI JUMAPILI AU JUMAMOSI?, NI SIKU GANI ITUPASAYO KUABUDU?
Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)
MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?
Rudi Nyumbani
Print this post
Wakati ule baada ya watu kumuudhi sana Mungu hata kufikia hatua ya BWANA kuleta GHARIKA juu ya dunia nzima, Na kama tunavyoijua habari ni Nuhu tu na familia yake ndio waliopona, lakini baada ya hapo BWANA akaweka UPINDE kama ishara ya agano aliloingia na Nuhu pamoja na uzao wake kwamba hataiteketeza tena dunia kwa maji..Tunasoma;
Mwanzo 9: 8 “Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, 9 Mimi, tazama, NALITHIBITISHA AGANO LANGU NANYI; tena na uzao wenu baada yenu; 10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. 11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi. 12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; 13 MIMI NAUWEKA UPINDE WANGU WINGUNI, nao utakuwa ni ISHARA YA AGANO kati yangu na nchi. 14 Hata itakuwa NIKITANDA MAWINGU JUU YA NCHI, upinde utaonekana winguni, 15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. 16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. 17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.”
Mwanzo 9: 8 “Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,
9 Mimi, tazama, NALITHIBITISHA AGANO LANGU NANYI; tena na uzao wenu baada yenu;
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
13 MIMI NAUWEKA UPINDE WANGU WINGUNI, nao utakuwa ni ISHARA YA AGANO kati yangu na nchi.
14 Hata itakuwa NIKITANDA MAWINGU JUU YA NCHI, upinde utaonekana winguni,
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.”
Ni rahisi kulichukulia agano hili kivyepesi vyepesi kwamba linafanya kazi pale tu tufani na gharika kubwa inapotaka kushuka juu ya nchi. Ni kweli kabisa Bwana alimwambia Nuhu ishara hii ya UPINDE wa RANGI SABA, Utaonakana mawinguni, lakini swali! je! ni kweli huu upinde unaonekana mawinguni tu peke yake??.
Kama ulishawahi kuona au kama hujawahi jaribu kufanya utafiti, utagundua kuwa huu upinde upo kila mahali palipo na asili au dalili ya maji. Mimi huwa nikinyeshea bustani kwa mpira nauona ukijiunda maji yanapochuruzika,,wakati mwingine nikiwa naoga na maji ya juu, unaonekana, ukiangali hata sehemu zenye maporomoko ya maji unaonekana, hata katika mito hususani pale jua linapopiga maji n.k. naamini nawe pia ulishawahi kuuona huo upinde mahali fulani tofauti na angani?. Lakini ulishawahi kujiuliza nikwanini unauona hata katika mambo madogo na sio tu mbinguni kwenye mawingu mengi ya mvua?, Hapo kuna jambo Mungu anatufundisha.
Biblia inasema Zaburi 12:6 “Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; ILIYOSAFISHWA MARA SABA”. Hii ikiwa na maana kuwa AGANO Mungu analoingia na watu wake alilolinena kutoka katika kinywa chake ni thabiti kama madini ya fedha yaliyohakikiwa mara 7, si ajabu hata tunauona UPINDE ukiwa na rangi SABA(7). Ikionyesha kwamba ni agano lililothibitishwa sana..Na ndio maana unaweza ukaliona katika mambo makubwa na madogo, unaweza ukaliona mbinguni na bado ukaliona kwenye ndoo ya maji.
Kumbuka upinde huu unafunua agano Mungu aliloingia na watu wake kwa kupitia damu ya YESU KRISTO mwana wake. Ni Agano lililo thabiti na kuhakikiwa sana, ni Imara kiasi kwamba kwa yeyote atakayeingia katika hilo, iwe ni katika MAMBO MAKUBWA AU MADOGO litakuwa naye kumwepusha na tufani shedtani atakayoileta. Mtu aliye ndani ya hilo agano, Iwe ni katika kushiba au njaa, iwe yupo katika raha au shida, iwe katika kupungukiwa au kuwa ni vingi litakuwa nawe, maadamu tu ameingizwa humo, HAKUNA GHARIKA yoyote ITAKAYOMGHARIKISHA. Na ndio maana biblia inasema;
Warumi 8: 33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? KRISTO YESU NDIYE ALIYEKUFA; NAAM, NA ZAIDI YA HAYO, AMEFUFUKA KATIKA WAFU, yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. 35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! NI DHIKI au SHIDA, au ADHA, au NJAA, au UCHI, au HATARI, au UPANGA? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Warumi 8: 33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? KRISTO YESU NDIYE ALIYEKUFA; NAAM, NA ZAIDI YA HAYO, AMEFUFUKA KATIKA WAFU, yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! NI DHIKI au SHIDA, au ADHA, au NJAA, au UCHI, au HATARI, au UPANGA?
36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Unaona hapo? Unapokuwa katika hilo agano ule upinde ambalo ni agano uliloingia na Bwana kwa kupitia damu ya Yesu Bwana utakupigania usijitenge na Mungu katika hali yoyote ile utakayokuwepo…
Ndugu unapokuwa mkristo fahamu kuwa upo safarini, na kama tunavyofahamu uthibitisho ya kwamba upo safarini ni kukatisha katika mazingira tofuati tofauti, kuna wakati utakutana na milima, kuna mahali utafika utakutana na mabonde, mahali pengine tambarare, kuna mahali utakuta mvua, sehemu nyingine joto n.k. lakini ukiona mazingira hayabadiliki nje basi ujue haupo safarini..upo pale pale…Hivyo usishangae kukutana na hizo hali ni jambo la kawaida.
Mkristo kupitia dhiki, shida, wakati mwingine magonjwa, au kupungukiwa, au njaa haimaanishi kuwa Mungu kakuacha kama wengi wadhanivyo, maadamu upo katika lile AGANO THABITI la Damu ya YESU KRISTO, fahamu kuwa wewe ni MBARIKIWA, japo utapitia hayo tena kwa kitambo tu, Mungu hataruhusu chochote kikugharikishe kabisa..ukumbuke ule upinde unaonekana katika mambo makubwa na madogo.
Wapo watu wanahubiri kipimo kwamba kipimo cha kwamba upo katika lile agano ni mafanikio ya kimwili tu wakati wote, kwahiyo mtu yeyote asiyefanikiwa kifedha amelaaniwa..ni safari gani hiyo isiyokuwa na mabonde na milima? biblia inasema;
Mhubiri 3:3……… kuna wakati wa Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; 4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; 5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; 6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
Mhubiri 3:3……… kuna wakati wa Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
Vile vile mambo mengine unaweza ukayaona ni madogo au usiyaone kabisa shetani aliyoyapanga dhidi yako, lakini Mungu anakuepusha nayo pasipo hata wewe kujua, kwa mfano wachawi kwa siri wamepanga kuidhuru familia yako, lakini Mungu anawaepushia mbali na Mungu hakwambii, wakati mwingine unakatisha njiani na nyoka anapita pembeni yako pasipo kukuuma, na wewe hujamwona, pengine utasema mimi sijawahi kukutana na nyoka maisha yangu yote, lakini fahamu umeshapishana nao wengi na kwamba wangekung’ata ungepata madhara makubwa mpaka leo..
Wakati mwingine umekula chakula chenye sumu pasipo hata wewe mwenyewe kujua, lakini Mungu anakiponya, utasema mimi mwaka mzima nina afya, ninazidi kunawiri lakini kumbuka mfano angeutoa ule UPINDE WAKE katika mambo madogo kama hayo ungekuwa umeshakufa siku nyingi. kila siku kwenye shughuli zako unakutana na mamilioni ya mapepo na majini pengine kukusababishia ajali, wakati mwingine kukuletea uchonganishi, ugomvi, visa, malumbano yasiyokuwa na maana, tamaa, uasherati n.k. vyote hivi Mungu anakuepusha navyo pasipo hata kukwambia. Kwako wewe siku inakuja siku inaenda upo salama…Hujui kuwa ni ule UPINDE wa Agano unatenda kazi ndani yako katika mambo madogo usiyoyajua wewe.
Kwahiyo ndugu ikiwa wewe ni Mkristo nikimaanisha kuwa umeokolewa kwa kumwamini BWANA YESU, na kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa kuzamishwa kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi na kujazwa Roho mtakatifu na kuishia maisha matakatifu fahamu tu kuwa upo katika mahali salama kabisa kwasababu lile AGANO LA UPINDE linafanya kazi sehemu zote, halipo kwenye tufani kubwa tu, hata katika ndogo.
Ni thabiti katika hali zote katika utajiri na umaskini. Lakini kwa yeyote aliye nje ya hilo Agano la Damu ya Yesu hana ulinzi wowote iwe katika utajiri atagharikishwa tu, iwe katika umaskini atagharikishwa tu, iwe katika raha, shida, mafanikio, afya, magonjwa vyovyote vile gharika ikija hata ikiwa ndogo kiasi gani itampeleka tu …Kwa sababu hakuna UPINDE wa Agano katika maisha yake la kumfanya Mungu akumbuke agano aliloingia na yeye ili amrehemu.
Ndugu nje ya YESU KRISTO hakuna uzima. Yeye ndio njia kweli na uzima, na kumbuka kumwamini Bwana Yesu sio kuongozwa sala ya Toba tu, bali ni kuchukua uamuzi wa kutubu kwa kumaanisha kuziacha kabisa dhambi zako na maisha yako ya zamani, hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili, na ndipo lile AGANO LA UPINDE litakapoanza kuonekana katika maisha yako, likitenda kazi katika nyakati za mambo makubwa na mambo madogo.
Ubarikiwe sana.
NUHU WA SASA.
FAHAMU KINACHOMGHARIMU MUNGU, KUTOA URITHI WAKE.
UTIMILIFU WA TORATI.
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?
Mathayo 24:23-28 “23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”
Mathayo 24:23-28
“23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”
Luka 17: 23 “Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate;
Bwana alipoykuwa anayazungumza maneno hayo alimaanisha kabisa kwamba kuna wakati wa hatari utafika ambapo mtoto yeyote wa Mungu atalazimika kubaki mahali alipowekwa kwa usalama wa roho yake, kwasababu alisema watatokea manabii wengi wa uongo na makristo wa uongo kudanganya watu yamkini hata walio WATEULE. Kumbuka wateule ni watu waliosimama katika imani kweli kweli ndio katika siku za mwisho watakaokuja kujaribiwa na sio tu kila mtu wa ulimwengu hao walishadanganyika siku nyingi..
Hivyo ni muhimu sana kujua ni wapi tulipoonywa tubaki tusiondoke?. Ni dhahiri kuwa patakuwa ni sehemu moja, Kumbuka alipokuwa anazungumza hizi habari kwa wanafunzi wake hapo mwanzo aliwaambia; kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakavyo kuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu. Sasa tujifunze kidogo siku za Nuhu zilikuwaje..
Tunasoma habari kwamba kabla ya gharika kuanza Nuhu na familia yake waliambiwa na Mungu waingie ndani ya SAFINA, na walipomaliza kuingia tu wote, Mungu mwenyewe ndiye aliyeufunga mlango, ikiwa na maana kuwa hakutakuwa na mazingira ya mtu yeyote kutoka mpaka utakapofikia wakati wa Mungu mwenyewe kuufungua tena, kutokana na hatari iliyopo nje. Kwa lugha rahisi alikuwa anamaanisha kuwa WASITOKE MAHALI WALIPO mpaka utakapofika wakati wa Mungu mwenyewe kuwafungulia mlango watoke.
Lakini tunakuja kuona baadaye mara baada ya mvua kuacha kunyesha na maji kuanza kupungua Nuhu alishawishika kufungua mlango ambao BWANA hakumwambia aufungue..Ni Yeye mwenyewe kwa kuwaza kwake, alikisia tu kwamba nje kutakuwa kumeshaanza kuwa salama, matokeo yake alipofungua tu madirisha yale Mungu aliyoyafunga ZIKATOKA ROHO MBILI.
Na hizi roho ni zipi?
Si nyingine zaidi ya KUNGURU na NJIWA. Kwa ufupi hizi roho zilitoka ili kuwaongoza katika njia waliyotaka kuiendea. Tunasoma alitoka kwanza Kunguru, na hakurudi tena, kuashiria kwamba huko nje ni SALAMA KABISA, chakula sasa kipo tele nje, maji yamekauka, ardhi ni kavu kabisa hivyo ni wakati wa kutoka na kuanza kufurahia nchi, pengine wakina Nuhu walishaanza kujiandaa kutoka wakidhani kuwa nje ni salama, kumbe ile ilikuwa ni roho idanganyayo,
Maana kama mfano wangetoka nje,wasingeweza kurudi tena katika safina pengine wangekutana na tope kubwa sana ambalo lingewazamisha ndani yake, na pia wasingekutana na jani lolote kama walivyotegemea kutoka katika ile injili ya kunguru hivyo wasingeweza kuishi kwa namna yoyote..Lakini Bwana kwa huruma zake na rehema zake hakupenda Nuhu aangamie akaruhusu Roho nyingine iwatangulie nje nayo ni NJIWA.
Lakini kama tunavyoisoma habari, yule njiwa hakuona mahali pa kutua na kurudi safinani, kuashiria kuwa huko nje hakuna maisha, Hivyo Nuhu akalazimika kungojea tena siku saba nyingine, na yule njiwa alipotoka tena, akarudi na TAWI LA MZEITUNI mdomoni mwake kuashiria kuwa nje ni salama kijani kimeshatokea..sasa huo ndio wakati wa KUTOKA.
Mwanzo 8:6 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya; 7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi. 8 Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi; 9 bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani. 10 Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili, 11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi. 12 Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe”.
Mwanzo 8:6 “Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
8 Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;
9 bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
10 Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,
11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
12 Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe”.
Habari hii ni ya siku hizi za mwisho kama Kristo alivyosema, Bwana kwa kuiona hatari iliyopo katika majira haya alitangulia kutufungia mahali fulani ili tukae huko mpaka wakati wetu na majira yaliyokusudiwa yafike. Na kifungo hicho ni NENO LA MUNGU (Biblia). Kumbuka unapokuwa mkristo na umezaliwa kweli mara ya pili, Mungu analazimika kukufunga katika misingi ya Neno lake kwamba udumu huko usitoke. Na yule njiwa ni Roho Mtakatifu(Waefeso 4:30) na yule kunguru ni mfano wa roho zidanganyazo zinazotenda kazi katika siku hizi za mwisho kuwadanganya yamkini hata walio wateule.
Kumbuka unapofungua mlango ambao Mungu alishaufunga kwako unaruhusu roho zidanganyazo zilizofananishwa na yule kunguru kukuongoza. Na roho hizi zitakuhubiria huko nje hakuna shida siku zote ni raha, kuna amani, kuna maisha, hakuna tena gharika, Mungu kashaibariki nchi, hizi roho zitakuwa zinakuambia njoo!! njoo!! njoo!! zinakuita sana ujiunge nazo kuliko zenyewe kukuletea chakula, mfano ya yule kunguru, zitakufundisha dunia haiishi leo wala kesho, zitakwambia chakula kipo tele cha kukutosha huku nje!! .Ndugu yangu na kama hutadumu katika maagizo ya NENO LA MUNGU hakika zitakuchukua.
Tunaishi katika kizazi kile alichokisema Bwana cha kuzuka kwa makristo na manabii wengi wa uongo, wanaohubiria watu injili nyingine, na Yesu mwingine, ambaye hakuhubiriwa na mitume. Mitume walihubiri watu watubu, wakabatizwe kwa jina la Yesu kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao na wapokee Roho Mtakatifu. lakini wao hilo halina maana sana kwao, unaweza ukawa na Yesu tu(umeokoka) hata ukiwa unavaa nguo za nusu uchi,unapaka wanja,lipstick, unaabudu sanamu, n.k. Mungu haangalii mavazi anaangalia moyo.
Biblia pia inasema Yesu ndiye njia kweli na uzima, wao wanasema zipo njia nyingi za kumfikia Mungu kipimo ni upendo tu, unaweza ukawa dini nyingine na ukaenda mbinguni bila hata kumwamini Bwana Yesu, Injili zao siku zote ni za kumfariji mtu katika hali ya dhambi aliyopo. Hazilengi kumwelekeza mtu mbinguni, bali zinalenga kumwelekeza mtu kufanikiwa tu katika mambo ya mwilini, hazihubiri hukumu inayokuja kwa watu ambao wapo kwenye dhambi zinafundisha mtu ambaye hajafanikiwa ndio kipimo halisi cha kulaaniwa na Mungu..n.k.
Hizi zote ni roho za kunguru zinazotangulia kudanganya watu wa kweli wa Mungu. Lakini Roho wa Mungu kwa mfano wa yule njiwa anakuletea tumaini ukiwa ndani ya safina yako akiwa na TAWI LA MZEITUNI mdomoni mwake. Huo ndio utakuwa uthibitisho tosha kuwa nje ni salama. Yule njiwa Hatakupigia kelele nenda sehemu fulani,yeye ndio yupo, bali atakuambia tazama ufalme wa Mungu haupo kule wala huku, bali upo ndani yako.
Ndugu yangu hili kanisa tunaloishi ndilo la mwisho linaloitwa LAODIKIA,(ufunuo 3) na ndilo Bwana alilolitolea habari hizo na kusema;
“Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele wakiwaambia Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate”; Usizifuate hizi roho bali dumu katika kile BIBLIA inasema, na sio kile DINI au DHEHEBU,au MCHUNGAJI, au NABII au mtu yeyote anachosema kwasababu hizi ni nyakati za hatari sana. Itafika wakati Bwana mwenyewe atatoa ishara kwa watu wake kutoka..na ndio maana wanafunzi wake wakamuuliza Bwana… “Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai”.
Utakuja wakati ambao ni hivi karibuni, karibia na unyakuo nao utakuwa ni mfupi sana, kwa wale wateule wa Mungu kutoka, utapita UAMSHO WA ROHO MTAKATIFU duniani kote,ambao utakuwa wa kipekee sana, mfano wa yule njiwa alipolileta tawi la mzeituni kwa Nuhu na kumpa IMANI KAMILI ya kutoka nje ya SAFINA, kadhalika Roho Mtakatifu ataachilia UFUNUO FULANI WA KIPEKEE KWA WATU WAKE TUU (ndiyo zile ngurumo 7 ambazo hajifanuliwa bado kwa kanisa (ufunuo 10:4)) ndizo zitakazokuja kumpa IMANI bibi-Arusi wa Kristo ya kwenda kwenye UNYAKUO. Kumbuka hii ni IMANI ile Bwana Yesu aliyoiulizia kwamba akija je! ataiona? katika luka 18:8.
Hivyo ndugu hizi ni siku za mwisho, JE! UMEOKOLEWA!, NI NANI ANAYEKUONGOZA SASA, NJIWA AU KUNGURU?. biblia inasema Roho Mtakatifu ndio Muhuri wa Mungu , na wote wasio na Roho wa Mungu hao sio wake(warumi 8:9). TUBU sasa mgeukie Yesu Bwana aliye mkuu wa uzima wako.
NEEMA YA YESU, HAITADUMU MILELE.
JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI
KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI ,JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?
Jina kuu la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe daima.
Ni rahisi kudhania kuwa pindi unapoonza kufanya kazi ya utumishi wa Mungu hapo ndipo Mungu anaanza kupendezwa na wewe. Mfano pale mtu anapoanza kuhubiri, au kuwaleta watu kwa Kristo, au kufanya maombezi au huduma ya namna yoyote ile n.k. kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea ndio wakati Mungu anapendezwa na mtu huyo?!. Lakini je! hilo ni kweli kwa wakati wote?.
Tujifunze kwa kiongozi wetu Bwana Yesu kwa maana yeye mwenyewe alituambia..“..TUJIFUNZE KWAKE (Mathayo 11:29)”. Je! ni wakati upi Bwana Yesu alishuhudiwa kwamba kampendeza Mungu?. Tunasoma katika Marko 1:11 “na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; NIMEPENDEZWA NAWE “.
Sauti hii ilisikika wakati Bwana Yesu alipokuwa anabatizwa na Yohana katika ule mto Yordani, kabla hata hajaanza huduma yake.Unaona hapo alikuwa ameshashuhudiwa kwamba amempendeza Mungu Na alikuwa ameshapewa vitu vyote na baba yake kabla hata hajaanza kuhubiri wala kufanya muujiza wowote.
Kumbuka kumpendeza huko au kupewa vyote na Baba, hakukuja kwasababu tu yeye alikuwa ni Mungu, hapana, Bali kuna vitu vingine vilivyomfanya afikie kiwango hicho kikubwa sana cha kumpendeza Mungu. Nacho hatukipati pengine zaidi ya ndani ya ile miaka 30 BWANA YESU aliyoishi kabla ya kuanza huduma yake.
Injili hazijarekodi kwa urefu maisha hayo aliyoishi miaka 30, isipokuwa matukio machache sana, ambayo ni yale alipokuwa anazaliwa, na lile tukio alipokuwa na miaka 12, na sehemu nyingine alipokuwa anamsaidia baba yake kazi za useremala. Lakini sehemu kubwa ya maisha yaliyobakia Mungu aliyaficha kwa makusudi maalumu ili sisi tutafute kufahamu ni nini hasa kilichomfanya Mungu apendezwe naye kabla hata ya kuanza huduma yake.
Wengi tunadhani Bwana alipokuwa anafufua wafu,anatenda miujiza,anaponya wagonjwa, anahubiri n.k. ndio kipindi hicho ambacho Mungu alianza kupendezwa na yeye sana. Hapana alipendezwa kwanza kwa maisha aliyoishi ambayo hayajarekodiwa kwenye Injili zile nne lakini yapo kwenye biblia.
Sasa tutapataje kuyajua maisha yake.?
Kama tunavyofahamu ili kufahamu tabia ya mtu, ni vizuri kuangalia historia ya familia yake, au jamii ya watu aliyotokea, ndio maana watu sana sana wanapenda kuangalia tabia za baba, babu, n.k.ili kulinganisha na tabia ya mtoto. kwasababu wanajua kwa namna moja au nyingine kuna aina fulani ya mwenendo au tabia itakuwa imerithiwa kutoka kwao.
Hivyo tukirudi kwenye biblia tunaousoma pia ukoo wa Bwana Yesu . Ukoo ule haukuandikwa kutufurahisha tu, bali ulikuwa unamaana kubwa ili kutusaidia sisi kuyajua maisha ya YESU mwokozi wetu yalivyokuwa kabla hajaanza huduma na yanatufundisha nini.. Hivyo ni vizuri kusoma biblia kwa kujifunza, kuliko kusoma kama hadithi tu.. Embu tuusome huu ukoo kidogo..
Mathayo 1:1-17 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; 3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; 6 Yese akamzaa mfalme Daudi; Daudi akamzaa Suleimani kwa yule mke wa uria; 7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; 8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; 9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; 10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; 11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli. 12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; 13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. 17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Mathayo 1:1-17
1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
6 Yese akamzaa mfalme Daudi; Daudi akamzaa Suleimani kwa yule mke wa uria;
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;
14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;
15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Laiti Kama mafarisayo na masadukayo wangefuatilia kwanza historia ya Yesu katika ukoo wake kabla ya kuzaliwa wasingepata shida kumtambua au kumwamini YESU kama yeye ndio Mwokozi. Mfano tukisoma habari ya Ibrahimu na Isaka, mwanzo kabisa wa ukoo, tunaona Ibrahimu alimtoa mwanawe pekee, kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu, ikifunua kuwa masiya atakayekuja atabeba tabia zinazofanana na hizo kwamba Isaka ni mfano wa Bwana Yesu na Ibrahimu kama Mungu, kwahiyo wasingepaswa washangae wamwonapo Bwana kujitoa nafsi yake kama mwanakondoo kwa wengine.
Kadhalika na maisha ya wale wote walioandikwa katika ule uzao, walibeba tabia fulani zinazomtabiri Bwana, hatuna muda wa kupitia mmoja mmoja lakini tumwangalie mmoja wa mwisho Daudi, yeye alikuwa ni Mfalme, lakini ufalme wake ulipatikana kwa taabu na shida nyingi maadui zake walimzunguka kila pande, ikampelekea kuandika zile zaburi alipokuwa katika shida, Kama vile Daudi alivyopitia shida kutoka kwa maadui zake, vivyo hivyo Bwana Yesu kabla ya kuupokea ufalme ilimpasa apitie taabu nyingi na kukataliwa. Na ndio maana kitabu cha zaburi ni maisha ya Bwana Yesu mwenyewe mwanzo mwisho.
Tunaona pia Daudi alipokuwa anapitia tabu na kuonekana kama hakuna msaada wowote alisema, Mungu wangu! Mungu wangu mbona umeniacha? (zaburi 22) ..alisema pia “hutaucha mwili wangu uone uharibifu(akiwa na maana kuwa kutokufa)“,.aliposalitiwa na watu wake wa karibu alisema “aliyekula mezani pangu amenigeuzia kisigino chake “…alisema pia, “wameyapigia kura mavazi yangu..” na maneno mengine mengi…Na mengi ya hayo tunaona yakijirudia kwa Bwana Yesu alipokuwa anapitia tabu kama za Daudi katika maisha yake, na alipokuwa msalabani. Ukiwa ni mchunguzaji wa maandiko utaona mambo hayo.
Hivyo ukitaka kufahamu maisha na tabia ya BWANA YESU alipokuwa duniani kabla na baada ya huduma kuanza rudi katika historia ya ukoo wake, utayaona mwanzo mwisho jinsi alivyoishi hapa duniani. Ndio maaana alipokuwa anaondoka aliwaambia wanafunzi wake..
Luka 24: 44 ” Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima YATIMIZWE YOTE NILIYOANDIKIWA KATIKA TORATI YA MUSA NA KATIKA MANABII, NA ZABURI. 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. 46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.
Luka 24: 44 ” Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima YATIMIZWE YOTE NILIYOANDIKIWA KATIKA TORATI YA MUSA NA KATIKA MANABII, NA ZABURI.
45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.
Umeona hapo maisha ya Bwana yaliandikwa katika TORATI, ZABURI na MANABII ukizingatia kusoma hizo utamwona Yesu lakini kwa kawaida maisha yake yatabakia kuwa fumbo machoni pa mtu.Kwa mfano utatafuta katika biblia yote mahali pameandikwa masihi atakufa na kufufuka siku ya tatu hutaona kwasababu mambo hayo yameandikwa katika mafumbo ambayo yanahitaji msaada wa Roho kuyafahamu.
Mahali pengine kwenye zaburi Daudi katika taabu zake alisema ;
Zaburi 69: 7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. 8 Nimekuwa MGENI KWA NDUGU ZANGU, NA MSIKWAO KWA WANA WA MAMA YANGU. 9 Maana WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. 10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. 11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. 12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. 13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. 14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.
Zaburi 69: 7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.
8 Nimekuwa MGENI KWA NDUGU ZANGU, NA MSIKWAO KWA WANA WA MAMA YANGU.
9 Maana WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu.
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao.
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.
“Ndio sababu Bwana Yesu aliitwa mwana wa Daudi japokuwa YESU ndiye aliyekuwa Bwana wake
Ukichunguza maandiko utaona maneno hayo pia yalimuhusu Bwana. Yeye hata ndugu zake hawakumwamini kama anaweza mtu kama yeye kuwa MFALME wa Israeli, alionekana kama mgeni katikati ya ndugu zake, kisa tu ameamua kutenda mapenzi ya baba yake, japokuwa alikuwa ni mtu wa dua nyingi akiwaombea maadui zake kwa kufunga na kulia (Waebrania 5:7), marafiki pia wasingeweza kukaa naye kwasababu alionekana kama mtu wa itikadi fulani za kidini ngumu, maana kama angekuwa na marafiki bila shaka hao hao marafiki zake wangeweza kuja kuwa wanafunzi wake…
Biblia inasema pia alikuwa hana UMBO LA UZURI kama wengi tunavyodhani (Isaya 53:3-4)..ni mtu ambaye asingeweza kulinganishwa na vijana wengine kwa uzuri. Lakini mbele za Mungu alikuwa ni mzuri kuliko watu wote duniani…Alifikia umri wa kuoa lakini hakuoa kuwa mke ni kitu cha maana sana kwake zaidi ya kumtazama Baba yake kila wakati.
Maisha yake yalikuwa hivyo hivyo siku zote, kabla ya kuanza huduma, tafakari hata nyumba yake binafsi alikuwa hana, wala kiwanja, kwa dunia ya sasa watu wangeweza kusema mtu asiyekuwa na malengo…Lakini alikuwa ni mtu mwenye malengo makubwa kuliko watu wote duniani na ndio maana tunasoma habari zake mpaka leo. kazi yake,chakula chake, kuishi kwake ilikuwa ni KUTENDA MAPENZI YA MUNGU TU!! na kuzingatia utakatifu wa hali ya juu..Na ndio hapo baada ya Mungu kumuhakiki kwa muda mrefu wa miaka 30 …Ndipo akaona huyu ndiye mwana wake pekee aliyempendezwa naye akampa vyote na kumtangaza hadharani..HUYU NDIYE MWANA WANGU, MPENDWA WANGU NILIYEPENDEZWA NAYE…HALELUYA….
Unaona hapo Bwana Yesu hakumpendeza Mungu baada ya kuanza huduma, hapana bali kabla ya kuianza..japokuwa maisha yake mbele za watu yalidharaulika lakini ulipofika wakati Mungu alimtukuza na kumweka juu ya vitu vyote.Vivyo hivyo na sisi Mungu hatuangalii tunapokuwa wahubiri bali anataka tumpendeze katika maisha tunayoishi siku zote sasa katika hali yoyote tunayopitia, katika kutengwa, au kupendwa, katika kuradhaulika au kukubalika… JE! TUNAISHI SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU KATIKA UTAKATIFU WOTE?.
Je! tunampenda Mungu wetu kwa akili zetu zote na mioyo yetu yote kama Yesu alivyofanya?. Tukifanya hivyo basi BABA atapendezwa na sisi na kutupa vyote kabla hata hatujaanza kumtumikia katika viwango vingine.Hivyo ndugu huu ni wakati wa kuanza kuchukua uamuzi katika hatua tulizopo na kuyatenda mapenzi ya Mungu..usiongoje uwe muhubiri au mtumishi anza sasa, na Bwana akishakwisha kukushuhudia atakutukuza. MUNGU ATUSAIDIE SOTE.
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?
TUMEAMBIWA TUNAPOSALI TUSIPAYUKE-PAYUKE, JE! HUKO KUPAYUKA PAYAUKA NDIO KUPI?
JE! WAYAHUDI WOTE WATAOKOLEWA HATA KAMA NI WATENDA DHAMBI KWASABABU WAO NI UZAO MTEULE?
Amri ya kwanza tuliyopewa na Bwana, ni kumpenda yeye kwa mioyo yetu yote, kwa nguvu zetu zote na kwa akili zetu zote, na nyingine inayofanana na hiyo ni kupendana sisi kwa sisi. Kila mmoja kumchukulia mwenzake bora kama nafsi yake mwenyewe. Lakini mtu mmoja alimuuliza Bwana, jirani yangu ni nani…akiwa na maana kuwa nini maana ya ujirani?.
Ndipo Bwana akatoa mfano ambao tunausoma katika Luka 10.
Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, NA JIRANI YANGU NI NANI? 30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31 Kwa nasibu KUHANI mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. 32 Na MLAWI vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 33 Lakini, MSAMARIA mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. 36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? 37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo”.
Luka 10:25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, NA JIRANI YANGU NI NANI?
30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.
31 Kwa nasibu KUHANI mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
32 Na MLAWI vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
33 Lakini, MSAMARIA mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo”.
Katika mfano huu tunajifunza, makundi matatu ya watu, wa kwanza ni KUHANI, wa pili MLAWI, na watatu ni MSAMARIA.
Kama tunavyofahamu kuhani ni mtu aliyekuwa ametiwa mafuta na Mungu kuhudumu katika nyumba ya Mungu, ni mtu aliyemkaribia Mungu sikuzote, kwa kazi ya kufukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa makosa ya watu wa Mungu, katika patakatifu. Ni mtu mwenye bidii ya kumtumikia Mungu usiku na mchana, kiufupi ni mtu aliyeheshimika mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Lakini ilipokuja katika jambo dogo kama hili, aliikosa shabaha, pengine alijua kumtumikia Mungu ni hekaluni tu na kwenye masinagogi! mahali penye mikusanyiko mikubwa ya watu wengi. Hakufanya vibaya, ni kwasababu hakupata ufunuo wa neno “JIRANI HASA NI NINI?”. Yeye alidhani kuwa kule aendako ndipo majirani zake walipo.
Kadhalika na yule Mlawi nae, kumbuka mlawi naye anafanya kazi zinazofanana na za kikuhani katika nyumba ya Mungu, isipokuwa yeye haingii katika patakatifu pa Mungu, tofauti ya Mlawi na Kuhani ni kwamba Kuhani yeye ni Mlawi aliyeteuliwa kutenda kazi katika patakatifu pa Mungu, hivyo kwa cheo huwa anaanza Mlawi, kisha kuhani, na mwisho kabisa ni Kuhani Mkuu. Sasa huyu naye alipomuona yule mtu mwenye majeraha, pengine huruma ilimjia kidogo, lakini alipogundua kuwa hizo sio kazi za Walawi, akaamua naye kupita kando. Naye pia hakufanya kosa, ni kwasababu tu hakupata ufunuo wa “JIRANI HASA NI NANI?”.
Lakini tunamsoma mwingine wa mwisho ambaye ni MSAMARIA. Kumbuka katika Israeli kulikuwa na Eneo linaloitwa Samaria na watu waliokuwa wanaishi kule walikuwa ni watu ambao sio wayahudi kamili, ni kama mchanganyiko wa watu wa mataifa na wayahudi, hivyo walikuwa nao wanaishika torati ya Musa japo wayahudi walikuwa hawawaatambui wala kuchangamana nao. Ni watu ambao hawakuruhusiwa kuingia au kuhudumu katika nyumba ya Mungu kwa namna yoyote ile, ni kama watu-baki au najisi mbele za wayahudi lakini walikuwa wanamjua Mungu na baadhi yao wanamcha.
Hivyo huyu Msamaria naye alipokatiza katika njia ile. alimuona yule mtu mwenye majeraha na “KUMUHURUMIA”, na pasipo kujali yule mtu ni wa namna gani, au ni kwasababu gani kapata hayo matatizo, yule msamaria akaghairi yote, pengine shughuli zake za kumwingizia kipato, ili tu aokoe maisha ya yule mtu kwa ule wakati. Hivyo kama tunavyosoma akayafunga majeraha yake, na kuyatia MAFUTA NA DIVAI. Kisha akaona hiyo tu haitoshi akampeleka hospitali, kwa gharama zake mwenyewe akamuuguza mpaka alipopona.
Na ndipo baada ya mfano huo Bwana Yesu akamuuliza yule mwanasheria ni yupi aliye JIRANI YAKE?. Naye akajibu; NI yule aliye MUHURUMIA(Msamaria).
Na sisi tunajifunza nini hapo?.
Katika hali tulizopo ni rahisi kudhani kuwa kuhudumu katikati ya umati mkubwa ndio chachu ya kudhani Mungu anakuona una upendo kwa jirani zako! lakini nini maana hasa ya kuwa JIRANI kwa mwenzako?.. Tukijifunza katika hiyo mifano hapo tunaona ni yule aliyekaribu sana na wewe, na unaona anahitaji msaada wa haraka sana kutoka kwako huyo ndiye jirani yako. Yule Kuhani na yule Mlawi walidhani umati mkubwa wa watu wanaowatumikia kule kila siku ndio wanaweza wakawa majirani zao. Lakini mtu alipotokea mbele yao ghafla mwenye uhitaji mkubwa na wa haraka kuliko wale, wakapita kando. Na mtu asiyemjua Mungu sana ndiye akaja kumsaidia.
Vivyo hivyo na sisi hatuhitaji tuwe wahubiri wakubwa, tunahubiria mamilioni ya watu ndipo tuonekana tuna upendo mkubwa kwa ndugu zetu mbele za Mungu.. Hauhitaji kwenda masafa ya mbali kuhubiri ukidhani kuwa hichi ni kipimo cha kuonyesha kuwa una upendo mkubwa kwa ndugu zako wakati jirani yako hapo karibu nawe yupo katika hali ya dhambi, na hamjui huyo Mungu unayekwenda kumuhubiri ulaya.
Unao rafiki zako ni makahaba, au walevi au waabudu sanamu. unawaacha waangamie unasema mimi nataka nikahubiri makanisani na kwenye makongamano tu…unachofanya sio dhambi lakini bado hujaonyesha ule upendo kwa jirani yako kama Mungu anavyotaka.
Lakini yule msamaria alimpaka mafuta na divai na kufunga majeraha yake, na baadaye akampeleka kwa matabibu wamtunze. Kadhalika na sisi tunapaswa tuwatazame ndugu zetu wote waliokaribu na sisi sana ambao wapo katika dhambi wamepigwa na kutiwa majeraha na shetani, tunapaswa kuwatia mafuta na divai, kwa kuwahubiria habari njema ili wapokee Roho Mtakatifu kisha wakishapokea Roho ndipo tuwapeleke kwa viongozi wa kiroho wawakuze. Na kwa kufanya hivyo Tutakuwa tumekidhi vigezo vya kuwapenda jirani zetu kama nafsi zetu. Japo mbele za wanadamu unaweza ukaonekana hujafanya kitu lakini mbele za Mungu, ni mtu mwenye maana sana.
Mungu akubariki.
MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
WALE WATU AMBAO SHETANI ATAWADANGANYA KATIKA MWISHO WA UTAWALA WA MIAKA 1000, WATATOKA WAPI, ANGALI TUNAJUA UTAWALA ULE UTAKUWA UMEJAWA NA WATAKATIFU TU?
Rushwa inapofushaje macho?
Ili kuelewa uzito wa Neno hili “KUZALIWA MARA YA PILI”, Ni vizuri tukarejea katika maisha ya kawaida kujifunza vitu gani vinaambatana na kuzaliwa kwa mtu. Mtu kabla hajazaliwa sehemu kubwa ya maisha yake yanakuwa yameshaandaliwa na vizazi vilivyomtangulia ni machache sana ambayo atakuja kuyaongeza yeye mwenyewe atakapozidi kukua, lakini asilimia kubwa mambo yake yanakuwa yameshakamilika.Na ndio maana inakuwa rahisi kumtabiri mtu atakuja kuwa wa namna gani kabla hata hajazaliwa.
Kwamfano wewe kabla hujazaliwa ndugu zako walishajua kabisa utakuja kuwa mwafrika mwenye rangi nyeusi, na nywele za katani, na sio mchina au mzungu! na ndivyo ilivyokuja kuwa baada ya kuzaliwa kwako, hivyo hawakushangaa kukuona wewe uko jinsi ulivyo leo. Lakini Kwanini hawakustaajabia kukuona hivyo, ni kwasababu mababa zako na wenyewe wako hivyo hivyo kama wewe,
Kadhalika kama jamii yenu ni watu warefu au wafupi, ni rahisi watu kutabiri kimo chako kabla hata hujazaliwa. Pia Kama familia yenu ni ya kifalme, ni rahisi watu kutabiri kuwa utakuwa mfalme kabla hata hujazaliwa..na siku utakapokuwa mtu mzima na kuwa mfalme hawatastaajabia kukuona wewe hivyo.
Ni kwasababu gani?. Jibu ni kwamba wameweza kusoma ukoo wako, na kuangalia tabia za mababa zako na mwenendo wao, na vyeo vyao wakaweza kuhitimisha maisha yako yatakavyo kuja kuwa. kadhalika na vitu kama majina,mtu kabla hajazaliwa watu wataishiakumuita majina ya ukoo kama Massawe, Wambura, Lema, Laiza, n.k. ni kwasababu gani?. Jibu ni kwasababu ni lazima aje kuyarithi kutoka kwa mababa zake, Vivyo hivyo kama mababa wana magonjwa fulani ya kurithi, au tabia au laana fulani ni rahisi kutabiri hali ya mtoto atakayezaliwa itakuwaje mbeleni.
Tukirudi katika mambo ya rohoni kuna kuzaliwa pia mara ya pili. Na ukishazaliwa mara ya pili moja kwa moja unaingizwa katika ukoo husika ambao utakufanya urithi kila kitu kinachohusiana na ukoo huo. Kuanzia jina, tabia, cheo, mwenendo n.k.
Ukiamua leo hii kwa moyo wako wote kujiunga na Dini ya UBUDHA, kwa kufata taratibu zao walizokuwekea moja kwa moja utakuwa umezaliwa na kujiingiza katika Ukoo wa Budha, hivyo mambo yote yamuhusuyo Bhuda utabeba na ndio maana huwezi kushangaa kwanini wale mabudha wote wanafanana,. kimavazi, kimienendo na kitabia ni kwasababu wamezaliwa humo katika roho..Kadhalika na dini nyingine zote na vikundi vyote viwe vya kishirikina n.k..
Lakini pia kuna kuzaliwa mara ya pili katika ukoo unaoitwa UKOO wa YESU KRISTO. Huu ni ukoo ulio juu sana kuliko koo zote, ni uzao mteule, wa kifalme wa Mungu mwenyewe, Huku nako watu wanazaliwa. Lakini kabla mtu hajaamua kuzaliwa katika huu ufalme ni lazima ajue ni nani anayemzaa, pili jina la ukoo wake ni lipi, tatu tabia za huo ukoo ni zipi, nne, je! ataweza kuendana nazo?. Kumbuka jina la ukoo huo Ni YESU KRISTO huo ndio msingi kukutambulisha kwamba wewe ni unamilikiwa na mwenye huo ukoo. kwasababu biblia inasema.
Matendo 4: 12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. “
Hivyo hatua ya kwanza ya kuzaliwa kama tunavyojua wakati wa utungu kwa mwanamke huwa yanaanza kutoka kwanza maji, kisha damu baadaye kiumbe, kadhalika katika roho mtu anapodhamiria kuzaliwa mara ya pili kwa KUTUBU kabisa kwa kumaanisha kuziacha dhambi, anapaswa akabatizwe kwanza katika ubatizo sahihi wa MAJI MENGI.. Na ni lazima abatizwe kwa JINA LA YESU KRISTO..Zingatia hilo JINA YESU huo ndio msingi wa kukutambulisha wewe kuwa umezaliwa katika ukoo wa Yesu. Kumbuka wengi wanabatizwa kwa jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu kimakosa. Mitume hawakufanya hivyo soma
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Soma pia (Matendo 8:16, 10:48, na 19:5) utathibitisha jambo hilo. Hivyo unapobatizwa kifasaha baada ya kutubu dhambi zako, zinakuwa zinaondolewa na unakuwa umeingizwa katika Ukoo wa kifalme, Sasa hatua ya mwisho ni kupokea Roho Mtakatifu mpaka hapo utakuwa una uhakika kuwa wewe ni mwana wa YESU KRISTO.
Kuanzia hapo unakuwa umepanda daraja una haki zote za kukanyaga nguvu zote za yule adui, kwa Jina la YESU na hakuna lolote litakalokusumbua kwasababu umepewa mamlaka yote ya kifalme. Lakini haishii hapo, baada ya kuzaliwa unaanza kurithi zile tabia za ukoo huo uliouingia. Mfano BABA yako YESU KRISTO alipenda kuishi maisha matakatifu, wewe nawe utaanza kujiona mwenyewe unachukia maisha ya uovu, utaanza kuona hamu ya pombe, sigara, uasherati, rushwa, wizi, utukanaji, tamaa vinaanza kuisha, ndani yako pasipo hata kujilazimisha au kutumia nguvu,..
Ni kwasababu gani? jibu ni kwamba zile tabia za Baba yako YESU zinaanza kujidhihirisha ndani yako pasipo hata wewe mwenyewe kuamua hivyo. Huu ndio uwezo wa kufanyika mwana unaotoka kwa Mungu aliouzungumzia katika
Yohana 1: 12 ” Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”.
Yohana 1: 12 ” Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”.
Kadhalika kama Baba yako(YESU), na mababa (mitume na manabii) walikuwa wanatabia za unyenyekevu, tabia za kusali, kufunga, kuwapelekea wengine habari njema, n.k. vivyo hivyo na mtoto naye atarithi tabia hizo, na zitatoka zenyewe ndani pasipo kulazimishwa kwasababu hizi unazaliwa nazo, haujifunzi..na ndio maana ya Neno hatuishi chini ya sheria, kwasababu sheria ya Mungu imefungwa ndani ya mioyo yetu haitutawali inatoka yenyewe.
Kadhalika pia kama baba yetu YESU alichukiwa na ulimwengu, vivyo hivyo na watoto pia watarithi na hayo..kwasababu yeye mwenyewe alitangulia kuwaonya akisema “mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu”..
Lakini huu UWEZO hauji hivi hivi na ndio maana tunasema kuna watu WALIOJIUNGA na watu WALIOZALIWA. Wengi wanasema wamezaliwa mara ya pili, lakini hawajazingatia hatua za kuzaliwa mara ya pili, ikiwa na maana kuwa hawajatubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha, na hawajabatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa, na kwa jina la YESU KRISTO.
Hivyo zile tabia za kurithi maisha ya YESU KRISTO haziwezi kuonekana ndani yao, hawa ndio waliojiunga badala ya kuzaliwa. Watajilazimisha kuwa kama wakristo, watajilazimisha waache uasherati watashindwa, watajilazimsha waache sigara, pombe, watashindwa kwasababu wao wamejiunga na sio kuzaliwa.
Biblia inasema
1Yohana 3:9 “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, KWA SABABU UZAO WAKE WAKAA NDANI YAKE; wala hawezi kutenda dhambi KWA SABABU AMEZALIWA KUTOKANA NA MUNGU ”.
Unaona hapo? Ule UZAO WA MUNGU unakaa ndani yako. Lakini kama haupo ndani yako kamwe hutakaa uweze kuishinda dhambi au kumshinda shetani.
Hivyo ndugu, kumbuka dunia nzima na vizazi vyote vinajua, kuwa hakuna UFALME mwingine zaidi ya Ufalme wa YESU KRISTO. Huo ndio unaomiliki sasa dunia, na ndio utakaokuja kumiliki baadaye. Ndugu BWANA YESU sio mtu wa kawaida kabisa, sasahivi tunavyoongea anamiliki Mbingu zote, malaika wote, na sayari zote, na dunia yote, na kuzimu yote, na tunavyovijua na tusivyovijua,.amekaa katika mbingu za mbingu asikoweza kufika mtu yeyote huko sio malaika yoyote au mwanadamu. Na atakuja tena kuwachukua walio wake ikiwa na maana ule UZAO WAKE. kwenda kumiliki vyote naye, watu wa milki yake milele na milele..
Kwanini ukose baraka zote hizo, kwa mambo yasiyokuwa na maana ya kitambo tu?. Siku ile wenzako wanaenda kung’aa kama Jua kama yeye alivyo wewe utakuwa wapi ndugu?. Bwana Yesu alisema dhahiri kabisa, katika..
Yohana 3: 5 ” Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Hivyo ndugu fanya juu chini uzaliwe mara ya pili kabla mlango wa neema haujafungwa.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
MIHURI SABA
JE! MKRISTO ANARUHUSIWA KULA NGURUWE, NA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE?
JE! NI SAHIHI KWENDA KUMFUATA KIONGOZI WA DINI KWA MFANO PADRE NA KUMPIGIA MAGOTI KUMWELEZA DHAMBI ZAKO AKUSAMEHE?.
Unyenyekevu ni nini?
Utaketi pamoja na Ibrahimu katika ufalme wa Mungu katika siku ile?. Ni vigezo gani vitakufanya ukidhi viwango vya kufanana na Ibrahimu. Jibu lipo dhahiri ni IMANI. Unapaswa uwe na imani kama ya Ibrahimu, Ikiwa na maana kuwa uyachunguze maisha yake, Jinsi alivyoenenda mbele za Mungu kwa IMANI na uyaige. Sio kuiga alichokifanya, bali ni kuiga mwenendo wake.
Ibrahimu alimchukulia Mungu, au ALIMUHESABIA Mungu kuwa anauwezo wa kufanya mambo yote. Aliweza kuamini vitu visivyowezekanika, na ndio maana aliweza kutembea na Mungu kwa muda wote ule pasipo kujikwa kwaa, aliamini Mungu angeweza kumpa mtoto hata kama akiwa na miaka 100 au 1000, kwasababu aliufahamu ukuu wake, hivyo hakudhubutu kumwekea Mungu mipaka, kwamba hapa anaweza, na hapa hawezi. Na alipopewa mtoto Bwana akamuhitaji kwa ajili ya dhabihu,.Lakini Ibrahimu hakusua sua kuuliza mara mbili, kwasababu alijua Mungu anaweza hata kumfufua tena mtoto wake na kumrudisha kutoka katika wafu.
Waebrania 11: 17 ” Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, 19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano. “
Waebrania 11: 17 ” Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;
18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,
19 AKIHESABU YA KUWA MUNGU AWEZA KUMFUFUA HATA KUTOKA KUZIMU; akampata tena toka huko kwa mfano. “
Ibrahimu alizingatia vitu kama hivyo AKIMUHESABIA Mungu anaweza mambo yote, na ndio maana hadi leo hii anaitwa Baba wa Imani. Na wote wenye Imani zinazofanana na hiyo yake wataitwa WANA WA IBRAHIMU, na watarithi ahadi zile zile Ibrahimu alizoahidiwa na Mungu.
Hivyo Mungu anapendezwa na watu wenye kumwamini kwa asilimia zote, Kuna mahali Bwana Yesu alipokuwa anafuatwa na makutano makubwa ya watu, alikutana na akida mmoja, aliyemshangaza sana..tusome.
Mathayo 8:5-13 “5 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, 6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. 7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. 8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; LAKINI SEMA NENO TU!, na mtumishi wangu atapona. 9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. 10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, SIJAONA IMANI KUBWA NAMNA HII, KWA YE YOTE KATIKA ISREALI. 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao WATAKETI PAMOJA NA IBRAHIMU, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 13 Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile”.
Mathayo 8:5-13
“5 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; LAKINI SEMA NENO TU!, na mtumishi wangu atapona.
9 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, SIJAONA IMANI KUBWA NAMNA HII, KWA YE YOTE KATIKA ISREALI.
11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao WATAKETI PAMOJA NA IBRAHIMU, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
13 Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile”.
Kumbuka akida huyu hakuwa myahudi (mwisraeli), au mtu aliyeijua torati ya Musa, hapana bali alikuwa ni mtu wa mataifa, tena Mrumi, jamii ya watu wa Pontio Pilato isipokuwa yeye alikuwa na hofu ya Mungu tofauti na wale wengine. Wakati huo aliposikia kidogo tu ya Kwamba Bwana YESU anaponya wagonjwa na kufufua wafu na kutenda miujiza… moja kwa moja akafahamu ule ni uweza mkubwa wa Mungu. Hivyo akamwamini kwa KUMUHESABIA, kuwa ataweza kufanya pia na mambo ambayo yanaonekana hayawezekani machoni pa watu.
Tofauti na desturi za watu wengine, ambao walitaka mpaka waende kuwekewa mikono na Bwana Yesu, ndio waamini kwamba wataponywa, wengine mpaka watembelewe manyumbani kwao ndipo waamini, wengine mpaka waone kwanza ishara ndipo waamini.
Lakini huyu moja kwa moja alisema “sema Neno tu na mtumishi wangu atapona”..Na jibu la Bwana lilikuwa ni ” Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. “…Imani hii iliwavuka wayahudi wote wa Israeli, iliwapita makuhani wote ambao kwa wakati huo walikuwa wanavukiza uvumba katika nyumba ya Mungu..Imani kama ya Ibrahimu Iliwapita mitume wa Yesu ambao kila siku walikuwa wanatembea naye..Iliwapita mafarisayo na waandishi na wazee wote wa Israeli wenye hekima na ujuzi wa torati, iliwapita hata yale makutano makubwa yaliyokuwa yanamfuata Yesu pale.
Na haikuishia hapo tu, Bwana alisema pia.
” 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno “
” 11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno “
Umeona hapo, watatoka wengine wengi kutoka pembe 4 za dunia, ikiwa na maana kuwa watatoka watu sehemu zisizojulikana zilizodharauliwa, sehemu ya watu wasiokuwa na maana, pengine wasiojulikana na kanisa, watu wasio na umaarufu n.k. hao wote watakuja kuketi na Ibrahimu yaani watashiriki pamoja baraka Mungu alizomuahidia Ibrahimu. kwasababu wameonekana kuwa na Imani kama ya Ibrahimu mfano wa yule akida.
Ukichunguza kwa karibu utaona kuwa Bwana alikuwa katika utaratibu wa kuwaponya watu wote waliokuwa wanamfuata lakini hakuwa anazungumza chochote baada ya kuwaponya, kwasababu hakuona kitu kingine cha ziada ndani yao. Lakini kwa akida aliona kitu cha ziada, vivyo hivyo na kwa yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda wa miaka 12 (Luka 8:43), aliona makutano wote wanataka njia zile zile za kuponywa tu, kuwekewa mikono, kutembelewa nyumbani, kuombewa, wengine walishatuma maombi ya kumwona Bwana pengine mwezi mmoja kabla, wengine walikuwa wameshamaliza ngazi za chini, wameshatoka kuwaona mitume, sasa wanakaribia ngazi ya juu ya kumfikia YESU, n.k.
Lakini yeye alisema kwanini nipitie shida zote hizo,pengine angetaka kusubiria mpaka zamu yake ifike ingemchukua mwaka mzima, isitoshe kulikuwa na watu wenye matatizo makubwa hata kuliko yeye, lakini yeye alisema “nikishika pindo la vazi lake tu nitapona saa hiyo hiyo”, ALIMUHESABIA kuwa kama mikono yake inaponya kwanini na vazi lake lisiponye pia?. Kadhalika na yule mwanamke wa Tiro (Mathayo 15:21), Kadhalika na Zakayo naye. n.k.
Lakini leo hii wengi, tunataka tumfikie BWANA kwa njia zile zile za makutano, kumbuka hata leo jambo lile lile linajirudia Bwana Yesu kazungukwa na makutano mengi,(Mabilioni ya watu duniani) kila mtu anataka kumwona Bwana, kila mtu anataka kuponywa, kila mtu anataka kupewa hitaji la moyo wake. n.k. Fahamu tu, mpo wengi wenye shida za kukutana na BWANA. Na wote amewaahidia kuwaponya kwa majira yake, lakini je! ni wangapi kati ya hao wanaugusa moyo wa BWANA, kwa mfano wa yule AKIDA, au yule mwanamke aliyekuwa anatokwa damu? Kiasi cha kufikia kuahidiwa kuketi pamoja na Ibrahimu katika ufalme wa mbinguni?.
Unapopata shida, au unapokuwa na mahitaji fulani kwanini jambo la kwanza unakimbilia kwa watumishi au wachungaji wakuombee?, Wewe kwani Mungu wako hayupo?, kwanini unakimbilia mataifa mengine au Israeli kutafuta suluhisho la matatizo yako, angali Bwana wako yupo karibu na wewe hapo ulipo? Fanya tu kitu cha ziada ndugu, MUHESABIE BWANA, kama anauwezo wa kumtumia mtumishi fulani kuniponya, vivyo hivyo anaweza akanitumia mimi mwenyewe kwa kinywa changu kunitimizia mahitaji yangu. Mungu hana ngazi, kwamba ukitaka umfikie yeye sharti uanze kwanza kwa shemasi kisha mchungaji halafu Mungu. hapana. Akitoka Mungu ni wewe. Sio Padri, wala kasisi wala Nabii anapaswa kuwa kiunganishi chako wewe na Mungu. Yesu pekee ndiye anayesimama hapo katikati.
Pengine watu walimdhihaki yule akida, anachezea nafasi ya kipekee ya kutembelewa na Bwana nyumbani kwake, lakini badala yake Mungu ndiye aliyependezwa na yeye kuliko watu wote. Vivyo hivyo wengine wanatamani mpaka watokewe na YESU au Malaika,au watembelewe na mchungaji ndipo waamini, na kuanza kumtumikia Mungu, wakidhani kuwa hayo ndio mapenzi ya Mungu. Lakini wapo ambao hawatayaona hayo wala hawatayahitaji hayo yote, na watakumpendeza Bwana na kuketi pamoja na Ibrahimu siku ile. Na wana wa Ufalme (ambao wangepaswa wenyewe ndio wawe vielelezo) watatupwa nje.
Hivyo ndugu yangu, tujitahidi sote, tupige mbio tufikie vile viwango vya IMANI kama ya ibrahimu ya kumpendeza Mungu kwa kufanya kitu cha ziada kwake, njia ambazo hazijazoeleka na wengi na hii haiji isipokuwa kwa KUMUHESABIA Mungu kuwa anaweza yote, anaweza kufanya mambo yasiyowezekanika.
Tafadhali share kwa wengine ujumbe huu na Mungu wetu atakubariki.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
JIWE LA KUKWAZA
JE! INAKUBALIKA KUMTOLEA MTU MWENGINE DAMU?(BLOOD TRANSFUSION).
Habari za Elifazi, Sofari, na Bildadi tunazipata katika kitabu cha Ayubu, kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka kuwa walikuwa ni marafiki wa Ayubu wa karibu sana waliokuja kumlilia pale alipopatwa na yale matatizo ambayo tunayoyasoma kwenye biblia. Lakini kabla ya hao kuja tunasoma pia Ayubu alikuwa ni MWELEKEVU sana aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu wa kila namna, na baada ya shetani kuona wivu juu yake,ndipo akaamua kwenda kumshitaki kwa Mungu, ajaribiwe ili aiache Imani yake. Kama tunavyofahamu, baadaye Mungu alimruhusu shetani amjaribu Ayubu. Na ndipo shetani akaenda kuzimu kuandaa MAJARIBU yake mazito MATATU(3), ambayo katika hayo alipata uhakika kabisa kwamba Ayubu hawezi kunusurika ni lazima amkane Mungu na kuachana na uelekevu wake. Embu tuyapitie kwa ufupi.
Jaribu la kwanza lilikuwa ni la nje ya mwili wake na nafsi yake:
Hili lilihusisha vitu vyote vilivyomzunguka Ayubu, vitu kama mali zake, wanyama wake, biashara zake pamoja na watumwa wake, n.k. Hawa wote shetani aliwapiga kama tunavyosoma habari katika Ayubu sura ya 1, lakini hakuishia hapo alizidi kupiga kufikia hatua kuwaua mpaka na watoto wake, na kumfanya Ayubu abaki peke yake, Lakini shetani alipoona hayo majaribu bado hayamtikisi Ayubu kwa namna yoyote zaidi ya yote aliishia kulibariki jina la BWANA. ibilishi akakusudia kubadilisha kinyago na kuamia kwenye ngazi ya juu iliyo nzito zaidi. (lile Neno linatimia mtu hujaribiwa kulingana na Imani yake.)
Jaribu la Pili lilikuwa ni katika mwili wake:
Tunasoma shetani alianza kumpiga Ayubu kwa magonjwa ya ajabu, majipu yaliyozuka mwili mzima yalimfanya Ayubu kufikia hatua ya kukonda sana na kukaa kwenye majivu muda wote akijikunia vigae. Kumbuka hili ni jaribu baya zaidi kuliko lile la kwanza kwasababu hili lilimuhusu yeye moja kwa moja. Afya yake ilidorora ghafla hivyo aliona kama mlango wa mauti unamwita muda wowote. Lakini pamoja na hayo Ayubu aliushikilia uelekevu wake, hatua hii ndiyo iliyomfanya hata mke wake Ayubu amkufuru Mungu, kwa kuona kuwa huyo Mungu waliyekuwa wanamtumainia kwa hatua hiyo waliofikia sasa hana msaada wowote kwao, kwa mume wake na kwa familia yake, Hivyo hakuna sababu ya kumtumikia tena. Lakini alizidi kuvumilia kwa muda mrefu na shetani alipoona ameshindwa, akaamia kwenye hatua nyingine ya juu zaidi ambayo ndiyo ngumu na ya hatari kuliko zote kiasi kwamba ingekuwa ni rahisi Ayubu kuchukuliwa na shetani kama asingesimama kikamilifu na Mungu wake. Hii ndio silaha ya mwisho shetani anayoitumia kuwamaliza watu wa Mungu. Na hakuna nyingine iliyojuu ya hiyo.
Jaribu la Tatu lilikuwa la rohoni:
Kule Ayubu alipokuwa anapashikilia ndipo, hapo hapo shetani alipopajia. Kumbuka kitabu cha Ayubu sehemu kubwa kinaeleza juu ya hili jaribu la tatu, ambalo ndio msingi na kila mtu anapaswa afahamu kwasababu hapo ndipo siri hii ilipokaa, (hivyo unaposoma biblia soma kwa kujifunza vinginevyo masomo makuu na ya msingi yaliyo ndani yake yatakupita kama utakuwa unasoma tu kama gazeti). Sasa hapa tunaona ni mapambano ya moja kwa moja kati ya Shetani na Ayubu. Sasa kama tunavyosoma mara baada ya Ayubu kuzidi kushikilia msimamo wake na Mungu wake licha ya kwamba ana magonjwa na kufiwa na watoto wake, lakini bado yupo na Mungu wake. Shetani ndipo sasa akaingia kazini kwa kawatia mafuta watumishi wake wa uongo, ili waende kumgeuza moyo Ayubu kwa mafundisho ya udanganyifu. Na hawa si wengine zaidi ya ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI.
Hawa walikuwa ni marafiki zake na Ayubu wa Karibu, ni watu pia waliomcha Mungu lakini sio kwa kiwango cha Ayubu. walikuwa ni Wazee wenzake, washauri wenzake, ambao pengine kwa wakati wakiwa pamoja waliweza kuwafundisha hata watu wengine njia za haki, na ukamilifu. Walipata sifa nzuri kwa Ayubu na ndio maana Ayubu aliweza kuwachagua wao tu! kuwa kama marafiki zake na washauri wake wa karibu. Lakini katika hatua kama hii walionekana kama wapo kinyume na Ayubu. Hii inadhihirisha kuwa mtazamo wao juu ya UKAMILIFU ulikuwa ni tofauti na wa AYUBU. Sasa kama tukichunguza habari zao kwa karibu tunaona moja kwa moja kwa kumtazama Ayubu katika hali aliyokuwa nayo wakaanza kumuhukumu kuwa, hakika kuna mahali amemkosea Mungu. Lakini sababu zao walizozitoa za Ayubu kumkosea Mungu hazikuwa za “rohoni” bali za nje tu, lakini wenyewe waliangalia vya “mwilini” wakilinganisha na vya rohoni (kwamba ndio kigezo cha kukubaliwa na Mungu). Na hii ndio sababu kubwa iliyowafanya wapishane na Ayubu.
Sasa ukitazama moyo wa Ayubu utaona yeye alijua kuwa ushahidi mkubwa wa kukubaliwa na Mungu upo katika moyo wake(uhusiano binafsi alionao na Mungu wake, na si vinginevyo.) pasipo kujali anapitia hali ya namna gani ya nje! iwe ni umaskini, shinda, njaa, uchi, magonjwa n.k. na ndio maana vilipotokea aliweza kustahimili kwasababu alijua ndani ya moyo wake hakijaharibika kitu, hajaona kama amefanya jambo la kumkosea Mungu. Uwepo wa Mungu ndani yake ulikuwa upo pale pale. Lakini wale marafiki zake watatu ambao wao walitumiwa na shetani kutenda kazi ile, walitazama kwa jicho lingine lisilo la ki-Mungu, na kuhitimisha kwamba kigezo pekee cha Mtu kukubaliwa na Mungu, ni kufanikiwa katika mambo yote, afya, familia, mali,mifugo umri, n.k.basiii!!! sasa ukiona umepungukiwa na hayo yote basi ni dhahiri kuwa Mungu amekukataa na hayupo na wewe hivyo unapaswa UTUBU. ndio yalikuwa mahubiri yao kwa Ayubu kuanzia mwanzo mpaka mwisho (Pata muda taratibu mwenyewe upitie kitabu cha Ayubu chote), na kibaya zaidi waliyathibitisha hayo waliyokuwa wanayasema kwa kutumia maandiko matakatifu, na mengine kufunuliwa kupitia maono usiku. Kiasi kwamba unaweza ukadhani ni Mungu kweli anazungumza na wewe kupitia watumishi wake. Embu Tusome baadhi ya maneno yao waliokuwa wanamuhubiria Ayubu..
Elifazi alianza kwa kumwambia Ayubu tukisoma Ayubu 4:6-9..
“6 Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako? 7 Kumbuka, tafadhali, NI NANI ALIYEANGAMIA AKIWA HANA HATIA? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? 8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo. 9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika. “
“6 Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
7 Kumbuka, tafadhali, NI NANI ALIYEANGAMIA AKIWA HANA HATIA? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? 8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika. “
Akiwa na maana kuwa kwamba Ayubu angekuwa ni mwelekevu kweli asingepatikana na shida zote hizo kwasababu walijua maandiko kwamba mwenye haki hawezi kukatiliwa mbali,(Na ni kweli ndivyo yanavyosema lakini yalitumika mahali pasipoyapasa)na pia waliongezea “watu wapandao madhara huvuna hayo hayo” hivyo Ayubu kuwa vile ni kwasababu huko nyuma alikuwa ni mkaidi, hivyo kavuna alichokipanda.
Bildadi rafiki yake wa pili naye akaongezea na kumwambia Ayubu:
Mlango 8 “1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema, 2 Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? 3 Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? 4 KWAMBA WATOTO WAKO WAMEMFANYIA DHAMBI, NAYE AMEWATIA MKONONI MWA KOSA LAO; 5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; 6 UKIWA WEWE U SAFI NA MWELEKEVU; HAKIKA YEYE SASA ANGEAMKA KWA AJILI YAKO, NA KUYAFANYA MAKAZI YA HAKI YAKO KUFANIKIWA. 7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. 8 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; 9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) 10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? 11 Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? 12 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. 13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia; 14 Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui. 15 Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu. 16 Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake. 17 Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe. 18 Lakini, aking’olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona. 19 Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi. 20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. 21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. 22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena”.
Mlango 8
“1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema, 2 Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? 3 Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? 4 KWAMBA WATOTO WAKO WAMEMFANYIA DHAMBI, NAYE AMEWATIA MKONONI MWA KOSA LAO; 5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; 6 UKIWA WEWE U SAFI NA MWELEKEVU; HAKIKA YEYE SASA ANGEAMKA KWA AJILI YAKO, NA KUYAFANYA MAKAZI YA HAKI YAKO KUFANIKIWA. 7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. 8 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; 9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) 10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? 11 Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? 12 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. 13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia; 14 Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui. 15 Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu. 16 Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake. 17 Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe. 18 Lakini, aking’olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona. 19 Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi. 20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. 21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. 22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena”.
Unaona hapo tunaona Bildadi anamwambia Ayubu sababu pekee ya watoto wake kuangamizwa ni kwasababu watoto wake walikuwa ni waovu. Lakini tunasoma Ayubu alikuwa kila siku anaamka alfajiri kuwaombea watoto wake rehema na dua kwa Mungu. Yaani kwa ufupi Bildadi alimaanisha kuwa kifo, misiba, wakati wote ni matokeo ya kutokuwa mwelekevu mbele za Mungu. Bildadi aliendelea kumlaumu Ayubu kwamba kama kweli angekuwa ni mkamilifu mbele za Mungu, basi Mungu mwenyewe angenyanyuka amtete, lakini sasa mbona bado anaonekana hali yake iko vile vile tena ndio ikizidi kuwa mbaya zaidi. Kwahiyo matatizo yale ni ushahidi tosha kwamba maisha yake hayapendezi hata kidogo mbele za Mungu.
Na rafiki yake wa mwisho Sofari aliendelea kumvunja moyo Ayubu na kusema..
Mlango 20 “1 Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema, 2 Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu. 3 Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu. 4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi, 5 YA KUWA SHANGWE YA WAOVU NI KWA MUDA KIDOGO, NA FURAHA YA WAPOTOVU NI YA DAKIKA MOJA TU?. 6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni; 7 HATA HIVYO ATAANGAMIA MILELE KAMA MAVI YAKE MWENYEWE; HAO WALIOMWONA WATASEMA, YUKO WAPI? 8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku, 9 Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena. 10 Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake. 11 Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini. 12 Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake; 13 Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake; 14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake. 15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake. 16 Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua. 17 Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi. 18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi. 19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga. 20 Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia. 21 Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu. 22 Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia. 23 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula. 24 Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili. 25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake. 26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake. 27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake. 28 Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake. 29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu”.
Mlango 20
“1 Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema, 2 Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu. 3 Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu. 4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi, 5 YA KUWA SHANGWE YA WAOVU NI KWA MUDA KIDOGO, NA FURAHA YA WAPOTOVU NI YA DAKIKA MOJA TU?. 6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni; 7 HATA HIVYO ATAANGAMIA MILELE KAMA MAVI YAKE MWENYEWE; HAO WALIOMWONA WATASEMA, YUKO WAPI? 8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku, 9 Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena. 10 Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake. 11 Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini. 12 Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake; 13 Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake; 14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake. 15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake. 16 Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua. 17 Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi. 18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi. 19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga. 20 Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia. 21 Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu. 22 Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia. 23 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula. 24 Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili. 25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake. 26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake. 27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake. 28 Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake. 29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu”.
Kama tunavyosoma hapo, Sofari naye hakuona haya kumwambia Ayubu kwamba yeye alikuwa katika “shangwe za watu waovu ambazo hazidumu ni za muda tu”. Akiwa na maana kuwa Mali Ayubu alizokuwa nazo kwanza zilikuwa ni za muda tu! kwasababu hazikuwa ni za haki, akimaanisha kuwa uthibitisho pekee wa Mungu kuwa na Ayubu ni mali zidumuzo na kama hazidumu basi hizo ni shangwe za waovu. Hivyo hatuwezi kueleza habari zao zote lakini ukiwa na muda pitia kitabu cha Ayubu chote utaona Injili ya hawa watu ilivyokuwa kwa Ayubu na jinsi walivyoweza kutumia maandiko na maono kuthibitisha uongo wao ili tu wamfanye Ayubu auache uelekevu wake mbele za Mungu. Hawa ndio walimfadhaisha Ayubu mara mia elfu zaidi hata ya kupotelewa na watoto na mali zake, kwasababu walikuwa wanataka kumfanya Ayubu atilie shaka uelekevu wake mbele za Mungu. walifanyika kama vyombo vya shetani kumjaribu Ayubu.
Mambo hayo yameandikwa ili kutuonya sisi watu wa zamani hizi, Shetani anapomaliza kumjaribu mkristo kwa magonjwa, kwa dhiki, kwa misiba, kwa udhaifu, kwa kupungukiwa na mali, kwa vifungo, kwa mateso, kwa shida, kwa njaa, n.k na kuona kuwa mtu huyo bado kasimama katika imani yake na uelekevu wake kama Ayubu basi huwa anabadilisha mfumo wake wa majaribu, na kuleta majaribu magumu zaidi, na ya hatari zaidi, anakuletea watu aliowatia yeye mafuta, mfano wa akina ELIFAZI,SOFARI, NA BILDADI ambao watatumia maandiko kukushawishi na kukuhakikishia kwamba njia unayoiendea sio sahihi, na kama hauna Roho wa Mungu ni rahisi sana kuchukuliwa na uongo wa watu hao, watakwambia KIGEZO PEKEE cha Mungu kukukubali ni wewe kuwa na MALI, kigezo pekee cha kuwa Mungu hajakutupa ni kutokupitia shida kabisa, watakwambia ukipitia misiba basi kuna tatizo kwenye imani yako, watakwambia ukipitia magonjwa basi kuna mahali umemuudhi Mungu, ukiwa na ulemavu fulani basi kuna laana fulani inakufuata kwasababu wenye haki lazima wawe na afya, watakuhakikishia kwa maandiko kabisa “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. “
watu kama hawa hata siku moja hawataangalia AFYA YA ROHO YAKO, kwamba je! unaishi maisha matakatifu?, au unayo imani? au una upendo? au je! unamzalia Mungu matunda ya haki?? au unamfanyia Mungu ibada ya kweli? wao wataangalia AFYA YA MWILI wako tu! na siku ikitetereka kidogo tu, basi umekwisha chukuliwa nao utaishia kuudharau ukristo na kusema ni ulokole tu,
Ndugu jiepushe nao, wanaipotosha kweli ya Mungu, ni shetani kawainua kuwajaribu watu wa Mungu, na kuwavunja moyo na kuwakatisha tamaa ili waiache imani, kwasababu laana kubwa mbele za Mungu sio kupungukiwa mali, au kukosa afya,au kupitia misiba au dhiki, hapana bali laana kubwa mbele za Mungu ni kutomwamini yeye aliyetumwa na yeye (yaani Yesu Kristo),na kukosa uhusiano binafsi na Mungu kwasababu biblia inasema..
Warumi 8: 35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Warumi 8: 35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Hivyo ndugu yatangeneze maisha yako kwa kumpenda Bwana Mungu wako pasipo kupelekwa na upepo huku na huku au kundi hili la waalimu na manabii wa uongo,(Hao ndio manabii wa uongo wa siku za mwisho) Biblia inasema kila jambo na majira yake wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kujenga na wakati wa kubomoa, mkumbuke Ayubu baada ya yale majaribu Bwana alimrudishia mara mbili ya vile alivyovipoteza, lakini kama angewasikiliza wale rafiki zake leo hii angekuwa wapi?. Si angeishia kumwangalia Mungu katika kioo cha mafanikio tu??. lakini hakuruhusu imani yake ipotee na zile mali za kwanza alizokuwa nazo, alitunza uhusiano wake binafsi na Mungu katika hali yoyote aliyopo, nasisi vivyo hivyo tuwe matajiri, au maskini, tuwe na vitu au tusiwe na vitu, tuwe wazima au tuwe wagonjwa, uhusiano wetu na Mungu unapaswa uwe pale pale kama Ayubu, usiyumbishwe na mazingira ambayo shetani anayaleta kupitia watumishi wake wa uongo ambao ndio sasahivi wamezagaa kila mahali kuwarubuni watu na mafundisho yao ya kujigamba.
Bwana akubariki sana.
AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
‘’MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI’’..NA NDIVYO ILIVYO KWA UASHERATI
AYUBU ALIJARIBIWA KWA MUDA GANI?.
KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?
KWANINI SAMWELI ALIRUHUSIWA KUHUDUMU HEKALUNI KAMA VILE WALAWI WAKATI YEYE NI MU-EFRAIMU?
Licha ya kuwa na INJILI YA MSALABA,ambayo ndio kiini cha kila mwanadamu ipo injili nyingine pia ijulikanayo kama INJILI YA MILELE, hii ni tofauti na injili ya msalaba. Injili ya msalaba yenyewe inatangaza wokovu kwa mwanadamu tu, kwa kupitia mmoja naye ni YESU KRISTO BWANA wetu. Kwahiyo injili nyingine yeyote inayodai kumkomboa mwanadamu na haimweki Bwana Yesu kama kiini cha injili yenyewe, basi injili hiyo ni batili, kwasababu yeye pekee ndiye Njia, kweli na uzima, hakuna mtu yeyote atakayemwona Mungu, pasipo kupitia kwake yeye biblia inasema hivyo(Yohana 14:6).. Kwahiyo zipo injili nyingi zinazodai zinaweza kumkomboa mwanadamu lakini kati ya hizo ni moja tu itakayoweza kumkomboa mwananadamu! Nayo ni Kwa kupitia Yesu Kristo, na ndio maana Mtume Paulo alisema|:
2Wakoritho 11: 4 “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au INJILI NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”
Unaona hapo? Biblia inasema kuna Yesu mwingine, roho mwingine na injili nyingine tofauti na ile iliyohubiriwa na mitume. Kwahiyo injili yoyote inayohusishwa na ukombozi wa mwanadamu inapaswa imlenge YESU KRISTO ALIYESULIBIWA,akafa na kufufuka kama kiini cha Ukombozi wenyewe, kwa asilimia mia yeye peke yake na sio pamoja mtu mwingine.
Lakini leo kwa ufupi tutaitazama INJILI YA MILELE ambayo ipo na imezungumziwa katika biblia..kama tunavyosoma katika;
Ufunuo 14: 6 “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye INJILI YA MILELE, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji”.
Ufunuo 14: 6 “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye INJILI YA MILELE, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji”.
Sasa hii injili ya milele ni ipi?
Kama jina lake lilivyo “Milele” inamaana kuwa ni injili ambayo Ipo milele yote, ilikuwepo kabla ya mwanadamu kuumbwa, ipo sasa, na itaendelea kuwepo milele na milele, Kumbuka INJILI YA MSALABA ilikuwa na mwanzo, na itakuwa na mwisho, mwanzo wake ilikuwa ni Kalvari, na mwisho wake itakuwa katika Unyakuo. Baada ya hapo hakutakuwa na nafasi tena ya ukombozi, kwasababu mlango wa neema utakuwa umefungwa. Kitakachokuwa kimebaki ni ile ile injili ambayo ilikuwepo milele na milele.
Na ndio maana ukisoma mstari huo hapo juu utaona kuwa yule malaika(mjumbe) anapita kuitangaza hiyo injili ambapo kwa wakati huo unyakuo wa kanisa utakuwa umeshapita na mlango wa neema ya kuokolewa utakuwa umefungwa kwa watu wa mataifa.
Kwahiyo injili hii ni tofauti na ya msalaba tuliyonayo sasa, hii ya msalaba tunaifahamu kwa “kuhubiriwa”. Hatuwezi kuifahamu pasipo kuhubiriwa ndio maana biblia inasema katika;
Warumi 10: 13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana{YESU KRISTO} ataokoka. 14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? TENA WAMSIKIEJE PASIPO MHUBIRI? 15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!{INJILI YA MSALABA}”
Warumi 10: 13 “kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana{YESU KRISTO} ataokoka.
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? TENA WAMSIKIEJE PASIPO MHUBIRI?
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!{INJILI YA MSALABA}”
Kwahiyo unaona hapo, ni lazima awepo mtu wa kuihubiri ndipo watu waokolewe.
Tofauti na ilivyo INJILI YA MILELE. Injili hii haisambazwi kwa kuhubiriwa na mtu yeyote, Ni Mungu mwenyewe anaiweka ndani ya mtu, katika eneo maalumu la moyo wa mwanadamu linaloitwa “DHAMIRA”..ambayo kila mtu anazaliwa nayo. Na inafanya kazi ya kuhukumu njia zote mbaya zinazokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu ndani ya mtu..Na Injili hii haipo tu kwa wanadamu, ilikuwepo hata kwa malaika, kwasababu ni ya milele, ilikuwepo huko enzi na enzi, ipo na itakuwepo.
Kwahiyo sasa kitendo tu cha mtu kuwa mwanadamu, tayari moja kwa moja kuna kitu ndani yake kitakuwa kinamshuhudia mambo yanayofaa na yasiyofaa, bila hata kuhubiriwa na mtu yeyote, au kukumbushwa na mtu yeyote, kwamfano, kila mtu anafahamu kuwa uuaji sio sawa, iwe anayo hofu ya Mungu au hana hofu ya Mungu, kila mtu anafahamu kuwa dhuluma ni mbaya, hata kama sheria isingesema hivyo, ndani ya moyo wake dhamira inamuhubiria kuwa kitendo hicho ni kibaya, Kadhalika haihitaji kuifahamu biblia kujua kuwa uonevu ni makosa, wizi ni makosa, utukanaji, ubakaji, rushwa ni makosa hayo yote hata kama mtu hajawahi kumsikia Mungu, au chochote kinachoitwa Mungu anajua kabisa hayo mambo hayafai kufanya, pia haihitaji kwenda katika vyuo vya biblia kutambua kuwa kulala na ndugu yako wa damu ni makosa, kadhalika na ushoga au usagaji ni makosa, utajikuta tu wewe mwenyewe unachukia kufanya hivyo au unalipinga hilo wazo ndani yako pale linapokuja kwasababu unajua kabisa kuwa hayo ni makosa.
Sasa hiyo ndio inayoitwa INJILI YA MILELE, Mungu anayoihubiri ndani ya moyo wa mtu. Na ndiyo hiyo siku za mwisho itakuja kukumbushwa kwa watu, wamche Mungu.wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita.
Kwahiyo usidhani kuwa wale watu ambao hawajasikia habari za YESU(Injili ya msalaba) mahali popote, hawatahukumiwa. Hapana Watahukumiwa tu kama wale wengine kwa injili hiyo. Watu wa kipindi cha Nuhu hawakuwa na sheria waliyopewa na Mungu kama watu wa Musa na kuendelea,Na ndio maana Mtume Paulo alieleza habari za watu hawa kama tunavyosoma katika…
Warumi 1: 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. 18 Kwa maana GADHABU YA MUNGU imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 19 Kwa kuwa MAMBO YA MUNGU YANAYOJULIKANA YAMEKUWA DHAHIRI NDANI YAO, KWA MAANA MUNGU. 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; YAANI, UWEZA WAKE WA MILELE NA UUNGU WAKE; hata wasiwe na UDHURU; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. 24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. 28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. 29 Wamejawa na UDHALIMU, UOVU na TAMAA na UBAYA; wamejawa na HUSUDA, na UUAJI, na FITINA, na HADAA; watu wa NIA MBAYA, wenye KUSENGENYA, 30 wenye KUSINGIZIA, wenye KUMCHUKIA MUNGU, wenye JEURI, wenye KUTAKABARI, wenye MAJIVUNO, wenye KUTUNGA MABAYA, WASIOTII WAZAZI WAO, 31 wasio na UFAHAMU, wenye KUVUNJA MAAGANO, WASIOPENDA JAMAA ZAO, WASIO NA REHEMA; 32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
Warumi 1: 17 Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.
18 Kwa maana GADHABU YA MUNGU imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
19 Kwa kuwa MAMBO YA MUNGU YANAYOJULIKANA YAMEKUWA DHAHIRI NDANI YAO, KWA MAANA MUNGU.
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; YAANI, UWEZA WAKE WA MILELE NA UUNGU WAKE; hata wasiwe na UDHURU;
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na UDHALIMU, UOVU na TAMAA na UBAYA; wamejawa na HUSUDA, na UUAJI, na FITINA, na HADAA; watu wa NIA MBAYA, wenye KUSENGENYA,
30 wenye KUSINGIZIA, wenye KUMCHUKIA MUNGU, wenye JEURI, wenye KUTAKABARI, wenye MAJIVUNO, wenye KUTUNGA MABAYA, WASIOTII WAZAZI WAO,
31 wasio na UFAHAMU, wenye KUVUNJA MAAGANO, WASIOPENDA JAMAA ZAO, WASIO NA REHEMA;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
Umeona hapo ndugu, biblia inasema wakijua kabisa watendao mambo kama hayo wamestahili mauti lakini bado wanayatenda. Dhamira zao zikiwashuhudia ndani kuwa wanayoyafanya sio sahihi lakini wanaendelea kuyafanya, Na wewe je! Ambaye upo kwenye dhambi utahitaji mhubiri siku moja aje kukuthibitishia kwenye biblia kwamba, uvutaji sigara ni dhambi, au uasherati ni dhambi?? Angali ndani ya moyo wako dhamira inakushuhudia kabisa unachofanya ni makosa?..hakika unaweza usilione lakini fahamu kuwa hukumu inakungojea.!
Wewe unayevaa vimini, na kutembea nusu uchi barabarani unasema Mungu haangalii mavazi lakini moyo wako unakuambia kabisa hayo ni makosa unayoyafanya na bado unaweka moyo mgumu, wewe unayevaa suruali,unayepaka wanja, na kupaka lipstick, na kuvaa wig na hereni, Hukumu ipo mbeleni dada!, wewe unayesengenya, wewe ambaye ni shoga, wewe unayejisaga, wewe unayetoa mimba, wewe uliye mwasherati, wewe uliye mlevi, wewe unayetazama pornography, wewe unayefanya masturbation, wewe unayeabudu sanamu za watakatifu waliokufa zamani angalia biblia inavyokuambia hapo juu < wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu(sanamu), na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo >..Unaona unajua kabisa Mungu hawezi kufananishwa na mfano wowote wa kinyago cha kuchonga lakini wewe bado unakwenda kuvipiga magoti na kuviabudu..
2Wakorintho 6: 16 inasema “Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu?”..
Lakini biblia inaendelea kusema kwa jinsi utakavyozidi kuweka moyo wako mgumu, kuna kipindi kitafika Mungu anakuacha uendelee hivyo hivyo kwasababu umekataa kuitii hiyo sauti inayosema ndani yako, mpaka ile siku ya hukumu ije na utaingia kuzimu!! Alisema “”28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”.
Kwahiyo dada/kaka hukumu ya Mungu haikwepeki hata uwe nje ya kanisa, njia pekee ni kujisalimisha maisha yako kwa BWANA YESU ambaye yeye ndiye aliyetoa uhai wake ili akuokoe, Tubu geuka, ukapewe uwezo wa kushinda dhambi. Muda umekwenda kuliko unavyodhani, na Injili ya msalaba sio ya milele utafika wakati utatamani uingie utakosa, muda ndio huu, mpe Bwana maisha yako tangu sasa.
Tafadhali “Share” kwa wengine na Mungu atakubariki.
JE! KUBET NI DHAMBI?
MLINZI, NI HABARI GANI ZA USIKU?
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
KATIKA KITABU CHA UFUNUO 16:5, TUNAONA AKITAJWA MALAIKA WA MAJI SWALI HUYU MALAIKA WA MAJI NI NANI? NAJE! KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?
HABARI ILE YA PILATO KUCHANGANYA ZILE DAMU ZA WAYAHUDI NA PAMOJA NA DHABIHU ZAO,(LUKA 13) ILIHUSU NINI?
WhatsApp
Yapo maswali kadha wa kadha umekuwa ukijiuliza kama mkristo (tukisema mkristo tunamaanisha mtu aliyegeuka na kudhamiria kwa gharama zake zote kubeba msalaba wake na kumfuata Kristo). Wakati mwingine unajikuta aidha ndani ya moyo wako au nje na maswali unayokosea majibu!!.
Kwamfano pengine unasema tangu nilipompa Bwana maisha yangu ni kweli ndani ya moyo wangu nilipata amani kubwa ya ki-Mungu lakini nje! Naona mambo mengi hayapo sawa, nilipojaribu kuishi maisha matakatifu marafiki na ndugu wakanitenga , nilipojaribu kuacha usengenyaji ndipo nilipoanza kuonekana mbele ya marafiki zangu ninajidai,
Nilipoacha rusha ndipo visa vikainuka kazini na kupelekea kuongeza idadi ya watu wanichukiao, niliposaidia watu badala ya kupokea shukrani ndio napokea lawama, nilipoanza kufunga na kuomba badala ya matatizo kupungua ndio yaliendelea kuwa vile vile, nilipoanza kufanya kazi ya Mungu ndipo matatizo ya kiuchumi yakanyanyuka zaidi,
Mpaka unafikia hatua ya kusema mbona huku kuishi maisha ya kujinyima na mambo ya dunia hakuna faida yoyote ninayoipata, zaidi ya kuwa vile vile tu siku zote!, mbona wale wasiomcha Mungu wana raha siku zote, ni matajiri pamoja na kwamba wanamkana Mungu, wanazidi kufanikiwa katika mambo yao,mbona wazinzi ndio wanao afya nzuri?.
Mimi pamoja na utakatifu wangu wote na wema wangu wote, Mungu kama hanioni na kunipa raha kama hao wengine, japo ninafanya mema kushinda wao?, kwani ni laana gani ninayo hadi yanipate hayo yote, au wao wana kitu gani cha ziada cha kushinda mimi mpaka wao wayapate hayo yote?,..Kumbuka Hayo ni mawazo yaliyopo ndani ya watakatifu wengi wa Mungu, Hata Daudi naye pia alizungumza maneno kama hayo tusome katika:
Zaburi 69: 7 “Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. 8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. 9 Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. 10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. 11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. 12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki”.
Zaburi 69: 7 “Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
9 Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki”.
Zaburi 73:1 “Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao. 2 Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza. 3 MAANA NALIWAONEA WIVU WENYE KUJIVUNA, NILIPOIONA HALI YA AMANI YA WASIO. 4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na mwili wao una nguvu. 5 Katika TAABU YA WATU HAWAMO, Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu. 6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Jeuri huwavika kama nguo. 7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao. 8 Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu. 9 Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutanga-tanga duniani. 10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao. 11 Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu? 12 Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi”.
Zaburi 73:1 “Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.
2 Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.
3 MAANA NALIWAONEA WIVU WENYE KUJIVUNA, NILIPOIONA HALI YA AMANI YA WASIO.
4 Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na mwili wao una nguvu.
5 Katika TAABU YA WATU HAWAMO, Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.
6 Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Jeuri huwavika kama nguo.
7 Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.
8 Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.
9 Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.
10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao.
11 Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?
12 Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi”.
Zaburi 42: 3 “Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako”.
Kama tunavyosoma Daudi pamoja na wema wake wote wa kuwaombea watu wengine fadhili mbele za Mungu kwa kufunga na wakati mwingine kwa machozi lakini bado alionekana kuwa kama ni kituko na mgeni mbele zao. Mpaka kufikia hatua ya kuwaonea wivu watu waovu.
Kadhalika na mambo haya haya yanawazwa na watakatifu walioko leo duniani , Wanasema aidha kwa midomo yao au kwa mioyo yao: Mungu wetu yuko wapi? Mbona hatuoni faida yoyote ya kumtumikia, mbona hatuoni faida yoyote ya kuacha kuvaa vimini, hereni, suruali, kuacha kupaka lipstick na wigi, wale wanaoendelea kufanya hivyo hao ndio wanaolewa kwa harusi nzuri, wana watoto wazuri lakini mimi bado nipo vile vile tu!.
Utasema mbona sioni faida yoyote ya kuacha pombe na sigara, mbona sioni faida yoyote ya kuacha uasherati, disco, anasa,na kucheza kamari na ku-bet, wenzangu wanafanikiwa kirahisi mimi nipo vile vile tu, Mbona sioni faida yoyote ya kuacha kula rushwa, zile pesa nilizokuwa ninapata mwanzoni sizioni tena nikizipata sasahivi, wale wenzangu tuliokuwa tunakula nao rushwa zamani wanazidi kunawiri na kusomesha watoto wao na kujenga majumba makubwa na mimi nimebaki katika hali ile ya kawaida tu!.n.k.
Haya yote yamekuwa ni maswali ya WATAKATIFU tangu zamani, Lakini Bwana naye aliyasikia na kuyatolea majibu yake: Kama tunavyosoma katika Malaki 3 Bwana anasema.
Malaki 3:13 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? 14 MMESEMA, KUMTUMIKIA MUNGU HAKUNA FAIDA; na, TUMEPATA FAIDA GANI KWA KUYASHIKA MAAGIZO YAKE, NA KWENDA KWA HUZUNI MBELE ZA BWANA WA MAJESHI? 15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. 16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. NAYE BWANA AKASIKILIZA, AKASIKIA; na KITABU CHA UKUMBUSHO KIKAANDIKWA MBELE ZAKE KWA AJILI YA HAO WAMCHAO BWANA, NA KULITAFAKARI JINA LAKE. 17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. 18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia”.
Malaki 3:13 “Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani?
14 MMESEMA, KUMTUMIKIA MUNGU HAKUNA FAIDA; na, TUMEPATA FAIDA GANI KWA KUYASHIKA MAAGIZO YAKE, NA KWENDA KWA HUZUNI MBELE ZA BWANA WA MAJESHI?
15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.
16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. NAYE BWANA AKASIKILIZA, AKASIKIA; na KITABU CHA UKUMBUSHO KIKAANDIKWA MBELE ZAKE KWA AJILI YA HAO WAMCHAO BWANA, NA KULITAFAKARI JINA LAKE.
17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia”.
Unaweza ukaona hapo?. Hakuna wema wowote wa mtakatifu atakaoufanya ukapita bure bure tu! , mbinguni kuna KITABU CHA KUMBUKUMBU kimewekwa kwa watu maalumu, kinarekodi mambo yote mema watakatifu wanayoyafanya kila siku huku duniani.
Na kama ni kitabu basi inaamanisha ili kiwe kitabu kamili ni lazima kiwe na kurasa nyingi na sio chache, na kitabu hichi cha watakatifu, ni matendo mema tu ndio yanayoandikwa huko, na sio kingine. Kwahiyo wingi wako wa kumcha Mungu na matendo yako mema mbele za Mungu kila siku yanarekodiwa katika kitabu kile na ndio yatakayoelezea wingi wa thawabu utakazopewa mbinguni katika siku ile ya mwanakondoo.
Hivyo ndugu/dada ukiwa ni mkristo kweli kweli uliyedhamiria kusimama katika Imani huu sio wakati wa kudhani kumtumikia hakuna faida yoyote,Faida zipo nyingi sana utazijua kwa marefu na mapana utakapofika katika urithi uliowekewa na Mungu wako.
Mambo ya ulimwengu huu sio urithi wetu, wewe upate usipate, uwe tajiri uwe maskini, uwe una afya usiwe na afya, vyovyote wewe endelea kumcha Mungu bila kujali lolote lile ukijua siku ile ni Mungu wako aonaye taabu yako ndiye atakayekulipa, maadamu unajiona upo sawa na Mungu wako usikwamishwe na kitu kingine chochote,songa mbele! endelea kuliweka Kumbukumbu lako sawa mbinguni, usidanganyike na mafundisho ya watumishi bandia kwamba kuwafanikiwa au kutokufanikiwa kifedha ndio uthibitisho kwamba Mungu yupo na wewe au Mungu amekuacha, hapana uthibitisho pekee ni maisha unayoishi ya kumpendeza Mungu wako sikuzote, kwasababu kitabu cha kumbukumbu kipo mbinguni.
Ongeza bidii, ikiwa umekataa rushwa endelea kuipinga, ukiwa umekataa uasherati endelea kufanya hivyo kwa bidii zaidi, ikiwa umekataa kuenenda kama mfano wa watu wa ulimwengu huu kuvaa vimini, suruali endelea hivyo hivyo kumbukumbuku lako kila siku linawekwa na thawabu yako ya siku haitapita bure..Bwana aliyeumba macho anaona yote!.
Lakini ukisema nitafanya hivyo nikifika umri fulani au wakati fulani, hujui kesho yako itakuwaje, na utakosa kumbukumbuku bora siku ile wakati wenzako wanafarijiwa kwa mambo mazuri yasiyoelezeka ya umilele na wewe haupo.Usiwaige watu waovu katika njia zao?
Na ni kwasababu gani Mungu anaruhusu waovu wafanikiwe sasa? .
Ni kwasababu urithi wao upo katika dunia ya sasa iliyoharibika na hawana sehemu yoyote katika urithi katika ulimwengu unaokuja. Hivyo faraja yao ipo katika mambo ya ulimwengu wa sasa kule hawana sehemu ndio sababu Bwana karuhusu wapate faraja yao hapa.
Bwana alimwambia Daudi.
Zaburi 92:7 “WASIO HAKI WAKICHUPUKA KAMA MAJANI NA WOTE WATENDAO MAOVU WAKISTAWI. NI KWA KUSUDI WAANGAMIZWE MILELE”
Kwahiyo sababu pekee ya waovu kufanikiwa sio kwasababu wanampendeza Mungu, ni ili waangamizwe milele, je! Na wewe unapenda kuwa miongoni mwao?, unafanikiwa katika rushwa yako ili uje uangamizwe milele?, unafanikiwa katika uasherati wako,na ulevi wako, na biashara yako haramu ili uje uwe miongoni mwa hao watakaoangamizwa milele?
Unafanikiwa katika utapeli wako na kamari yako na betting yako, ili uje uangamie milele?? Biblia inasema ITAKUFAIDIA NINI UPATE ULIMWENGU MZIMA, NA KUPATA HASARA YA NAFSI YAKO?, itakufaidia nini uonekane ni wakisasa kuliko watu wote duniani, kwa kujichora, kwa kuvaa vimini, na suruali na mawigi na kisha upate hasara ya nafsi yako? Ndugu KUMBUKUMBU LA WENYE HAKI LINAANDIKWA MBINGUNI kamwe usitamani mambo yao wala njia zao, kama hujampa Kristo maisha yako ni vema ukafanya hivyo sasa angali wakati upo, kabla mlango wa Neema haujafungwa.
Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu, na Mungu atakubariki.
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
KITABU CHA UZIMA
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
JE! NI SAHIHI MTU KUBATIZWA KWENYE MAJI YA KISIMANI?
KWANINI KUNA WATU WANAFANYIWA DELIVERANCE (MAOMBI YA KUFUNGULIWA), LAKINI BAADA YA MUDA WANARUDIWA TENA NA HALI ILE ILE SABABU NI NINI?