Swali: Je mkristo aliyeokoka kwenda “Gym” / kunyanyua vyuma na kufanya mazoezi mengine ya viungo ni dhambi?.
Jibu: Kufanya mazoezi kwa asili si dhambi, kwasababu hata kutembea kutoka nyumbani kwenda kanisani kumwabudu Mungu au kwenda kazini tayari hayo ni mazoezi hata kama hujarasimisha. Bwana hajatuumba kutulia sehemu moja kama vile “MTI”, bali kujongea.
Na kujongea kuna faida katika mwili endapo kukiambatana na “Kuyafanya mapenzi ya Mungu”. Maana yake ni hii, kama utakuwa upo sawa na MUNGU aliyekuumba kimahusiano, basi mazoezi utakayoyafanya yatakuwa na faida katika mwili wako.
Lakini kama Mahusiano yako na Mungu ni hafifu au hayapo kabisa, basi hata mazoezi utakayofanya hayatakuletea matokeo yoyote katika mwili wako.
Lakini suala la Msingi, ni je.. Aina gani ya Mazoezi Mkristo anayopaswa kuyafanya?? Hili ndilo SWALI LA MSINGI.
Mazoezi Mkristo anayopaswa kuyafanya ni yale yasiyo na NIA YA KIDUNIA, wala YASIYOJIFUNGAMANISHA NA MIFUMO YA KIDUNIA. Tuangalie moja baada ya nyingine.
1. MAZOEZI YENYE NIA YA KIDUNIA NI YAPI?
Mfano wa mazoezi yaliyobeba Nia ya kiduani ni yale yote yanayochochea tamaa za kimwili..mfano wa hayo ni yale ya kunyanyua vyuma ili kutanua misuli kwa lengo la kutazamwa na watu, au kuvutia jinsia nyingine…mazoezi ya namna hii ni haramu kwa mkristo.
Lakini kama mkristo atafanya mazoezi ya kutanua misuli aidha kwasababu kazi yake ya mikono aifanyayo itahitaji ukakamavu, hiyo sio kosa.
Mfano mwingine wa mazoezi haramu ni yale ya kupunguza mwili kwa lengo la kutumia mwili huo kama kivutio cha matangazo ya urembo au mitindo.(Maarufu kama Umiss, au Umodel), mazoezi ya namna hii mkristo hapaswi kufanya..
Lakini kama lengo lake si hilo, bali anafanya tu mazoezi ya kupunguza mwili kwa lengo la kujiongeza wepesi katika viungo vyake afanyapo kazi au aendeleapo na majukumu yake ya kila hapo afanyi kosa.
2. MAZOEZI YALIYOJIFUNGAMANISHA NA MIFUMO YA KIDUNIA.
Mazoezi yaliyojifungamanisha na mifumo ya kidunia ni yale yote yaliyobeba tamaduni za kidunia kuendesha/kuongoza mazoezi hayo…(Mazoezi ya dizaini hii haijalishi yana NIA nzuri, lakini maadamu tu tayari yamejifungamanisha na mifumo ya kidunia, basi yanakuwa Najisi kwa mkristo).
Mfano wa mazoezi haya ni yale ambayo Mtu atakimbia barabarani huku kavaa nguo ya kubana au nguo ya ndani tu peke yake!!…kwasababu tu ndio mfumo wa ukimbiaji ulioidhinishwa au ulio katika wakati. Mkristo kwa vyovyote vile hapaswi kufanya mazoezi kwa mtindo huo… haijalishi nia yake ni kupunguza mwili ili awe mwepesi katika kazi au kuongeza ili imsaidia katika kazi zake.
Maana yake kama wewe ni mkristo na unataka kufanya mazoezi ya kukimbia ili kupunguza mwili, na kujifanya mwepesi, vaa nguo zako za kujisitiri, (Uwe mwanamke au mwanaume) na fanya mazoezi yako kwa staha.. na tena si sehemu za kujionyesha onyesha..
Mfano mwingine wa mazoezi yaliyochanganyikana na udunia ni yale yanayofanyika katika majumba maalumu almaarufu kama “Gym”. Majumba ya Gym hayana tofauti na DISKO, kwani kama vile disko kulivyo na kule kumo vivyo hivyo, Disko utakuta watu wamevaa nusu uchi, na GYM ni hivyo hivyo.
Disko utakuta watu (wakike na wakiume) wanaserebuka na midundo ya miziki, na Gym ni hivyo hivyo, utakuta wamepanga mistari na wanafanya mazoezi huku wanaongozwa na ile midundo wakiwa nusu uchi, na hata wakati mwingine kupapasana kana kwamba wanaelekezana au kusaidiana kanuni za mazoezi n.k
Sasa mazoezi kama hayo, Mkristo hapaswi kushiriki wala kufanya kwasababu yamejifungamanisha na mifumo ya kidunia. (1Yohana 2:15)
Kama mkristo ni lazima kuenenda tofauti na dunia siku zote. Kwasababu mambo yanayofanyika duniani karibu yote maudhui yake ni ya kishetani.
Lakini jambo la mwisho la kuzingatia ni kwamba, hata kama umeokoka usitie kipaumbele sana kufikiri kutengeneza mwili, lakini ni heri kufikiri kutafuta afya ya rohoni, kwani ukiipata hiyo hata hiyo ya mwilini itajiweka tu katika uwiano..
1Timotheo 4:8 “Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
USIWE ADUI WA BWANA
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?
Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
Rudi Nyumbani
Print this post
Jibu: Turejee..
Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu”.
Msikwao ni Kiswahili cha “Mgeni aliyetoka nchi nyingine”… Mtu aliyetoka Taifa lingine na kuingia katika Taifa lisilo lake ndio anayeitwa “Msikwao”.
Hivyo katika hilo andiko, aliposema nimekuwa Msikwao kwa wana wa mama yangu, maana yake amekuwa kama mgeni asiye wa nchi ile mbele ya ndugu zake (wana wa mamaye).
Maneno hayo Daudi aliyaandika kumhusu yeye, lakini pia yalikuwa ni unabii wa maisha ya Bwana YESU KRISTO. Ukisoma Zaburi nyingi za Daudi zilikuwa ni unabii wa maisha ya BWANA YESU, Kwa mfano Zaburi ya 22 ule mstari wa kwanza unasema…
Zaburi 22:1 “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?”
Maneno hayo utayaona Bwana YESU anayataja alipokuwa pale msalabani (soma Mathayo 27:46).
Vile vile unabii wa Yuda kumsaliti Bwana YESU, umeandikwa katika Zaburi 41:9..
Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.”
Na Bwana YESU anakuja kunukuu maneno hayo katika Yohana 13:18…
Yohana 13:18 “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake”
Sasa tukirejea katika Zaburi hiyo ya 69, ilikuwa inaelezea maisha ya BWANA YESU KRISTO, kwamba kuna wakati ataonekana mbele ya ndugu zake kama mtu aliyetoka nchi ya mbali, maana yake hata ndugu zake watamkataa.. (na ndugu zake wa kwanza ni Taifa la Israeli, na wa pili ni ndugu zake wa damu).
Utauliza ni wakati gani ndugu zake walimwona kama mtu wa ajabu asiye wa kwao (msikwao)?..
Marko 3:21 “Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili”.
Soma pia Yohana 7:5.
Hivyo Zaburi hiyo ya 69 ni unabii wa maisha ya Bwana YESU asilimia zote… Na tunazidi kulithibitisha hilo katika mstari unaofuata wa 9, ambao tunaona baadaye Bwana YESU anakuja kuurejea..
Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. 9 MAANA WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata”.
Zaburi 69:8 “Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
9 MAANA WIVU WA NYUMBA YAKO UMENILA, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata”.
Utaona hapo aliposema “Wivu wa nyumba yako umenila”.. panakuja kujifunua katika Yohana 2:16-17.
Yohana 2:1 “Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. 17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, WIVU WA NYUMBA YAKO UTANILA.”
Yohana 2:1 “Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, WIVU WA NYUMBA YAKO UTANILA.”
Ni nini tunajifunza?..
Kikubwa tunachojifunza ni UNABII uliopo katika kitabu cha Zaburi, kwamba kumbe sehemu kubwa ya kitabu hiko ni unabii wa maisha ya BWANA YESU, ili kutumiza yale maneno yake aliyoyasema katika Luka 24:44.
Luka 24:44 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii NA ZABURI”.
Hivyo tukisoma kitabu hiko kwa uongozo wa ROHO MTAKATIFU, Tutaona mambo mengi sana yamhusuyo YESU.
Lakini pia mambo mengi yaliyoandikwa katika kitabu hiko yanatuhusu pia sisi, kwani Kristo akiwa ndani yetu nasi tunafanana na yeye, na hivyo sehemu ya maandiko hayo pia yanatimia juu ya maisha yetu..
Maana yake ni kwamba kama KRISTO alionekana Msikwao mbele ya ndugu zake kwasababu anafanya mapenzi ya Baba wa mbinguni, hali kadhalika na sisi tutakutana na vipindi kama hivyo tukiwa katika kuyafanya mapenzi ya Mungu, hivyo endapo yakitokea hayo hatuna budi kusimama na kujitia moyo, kwasababu tayari yalishatabiriwa.
Yohana 16:32 “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU”.
Yohana 16:32 “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.
33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU”.
BWANA YESU AKUBARIKI.
KUMBUKA KUSOMA NENO LA MUNGU KILA SIKU!!!!
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?
NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.
NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.
Biblia haielezi moja kwa moja kama waliokoka, au hawakuokoka, kwasababu Neno “Kuokoka”, tunalisoma kwenye agano jipya, likimaanisha kukombolewa kutoka katika uharibifu wa hukumu ya Mungu kwasababu ya dhambi kwa kupitia kifo cha Yesu Kristo mwokozi wetu.
Lakini tunaweza kufahamu watu wa agano la kale waliokolewa, kwa kutii kwao ile ahadi ya Mungu aliyoahidi ya kumletea mkombozi duniani baadaye, yaani Yesu Kristo. Hivyo wote waliotembea katika mpango huo wa Mungu, waliokoka. Na mpango wa Mungu wote ulimuakisi Yesu Kristo.
Kwamfano ile safina aliyoijenga Nuhu ilikuwa ni Yesu Kristo, Ule mwamba walionywea wana wa Israeli jangwani ulikuwa ni Kristo, wote waliokataa kuunywea walimkataa Kristo, (1Wakorintho 10:4), Yule nyoka wa shamba alikuwa ni Kristo waliokataa kuitazama, walimkataa Kristo(Yohana 3:14), zile mbao mbili (Amri 10), zilikuwa ni Kristo waliozikataa kuzitii, walimkataa Kristo. Yule melkizedeki aliyemtokea Ibrahimu alikuwa ni Kristo, wale malaika wawili walioshuka sodoma kuhubiri alikuwa ni Kristo ndani yao, waliowatii walimtii Kristo. Wale wanyama waliochinjwa na damu zao kunyunyizwa katika madhabahu kwa ajili ya upatanisho wa dhambi za watu walimfunua Kristo, wote waliotii,. Walimtii Kristo ajaye.
Hivyo kila mahali walipotembea, Kristo alijidhirisha kwao kwa lugha ya maumbo na vivuli, na mifano, na maagizo, ili wamwamini yeye. Kwahiyo wote waliomtii katika nyakati zote, waliingizwa katika jopo la watu ambao Kristo atakapofunuliwa basi wataokolewa. Ndio maana baada ya Yesu kufufuka katika wafu miili mingi ya watakatifu ikatoka makaburini, wakahamishiwa peponi, rahani mwa Yesu, kwani hapo kabla watakatifu wote waliokufa walikuwa chini makaburini.
Hivyo kwa msingi huo, tutachunguza kama Adamu na Hawa walimtii Kristo au la, baada ya anguko. Biblia inatuonyesha walipojiona wapo uchi, hawakuendelea kufurahia anguko lile, bali walijificha, kuonyesha majuto ya dhambi zao, ndipo Mungu akamchinja mnyama Yule, akawavika vazi lake. Sasa Mnyama Yule alimfunua Kristo,(Mwanzo 3:21) lakini kama wangekataa basi wasingeweza kuokoka, ndio maana Yesu alisema..pia maneno haya haya kwetu sisi wa siku za mwisho, tuvikwe vazi lake, ili aibu yetu iondoke.
Ufunuo 3:18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona
Halikadhali, biblia inataja uzao wa mwanamke kwamba utauponda kichwa uzao wa nyoka. Kuashiria kuwa Hawa hakuwa mwana wa Adui (Mwanzo 3:15). Bali ni zao mbili tofauti kabisa.
Lakini pia watoto wao, mpaka sethi, tunaona walifundishwa njia ya kumtolea Bwana sadaka, na sadaka zile zilikuwa ni Kristo katika maumbo. Ni wazi kuwa wasingeweza kufanya vile kama hawakupokea au kuona kwa wazazi wao.
Na sababu nyingine ya mwisho, Kristo anatajwa kama mwana wa Adamu, hata katika vizazi vile vilivyoorodheshwa anatajwa kama “wa Adamu” (Luka 3:23-38). Asingeitwa hivyo wa Adamu kama angekuwa ni wa ibilisi,. Mungu hawezi anza na mguu usio sahihi. Atashinda mwanzo, vilevile atashinda mwisho.
Kwa hitimisho ni kwamba Adamu na Hawa hawakupotea, bali walimwamini Kristo, baada ya anguko.
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?(Opens in a new browser tab)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?(Opens in a new browser tab)
Nini Maana ya Adamu?
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)
Je unaielewa vyema hii sentensi? “..Naye Neno alifanyika Mwili”.
Yohana 1:14 “Naye NENO alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.
Je ulishawahi kuzungumza na mtu kwa simu?.. Je anapozungumza na wewe huwa unamwona?? Au unayasikia MANENO YAKE TU?.. Ni wazi kuwa humwoni ila unasikia MANENO YAKE.
Lakini atakapokujia na kusema nawe ana kwa ana..hapo utakuwa UNAMWONA na pia UNAYASIKIA MANENO YAKE YANAYOTOKA KATIKA KINYWA CHAKE.
Hivyo tunaweza kusema kuwa wakati anaongea nawe kwenye simu yalikuwa ni Maneno tu (Pasipo yeye kumwona), lakini alipokujia na kusema nawe ana kwa ana yalikuwa ni Maneno yale yale isipokuwa yanatoka ndani ya mwili unaoonekana..KWA LUGHA NYINGINE TUNAWEZA KUSEMA NI MANENO YALIYOUVAA MWILI.
Na siri ya UUNGU wa YESU, inaanzia hivyo hivyo… Kwamba hapo Mwanzo Mungu alisema nasi kwa NENO LAKE pasipo yeye kuonekana… Lakini baadaye yeye mwenyewe akaja katika mwili na kuonekana na kusema MANENO YALE YALE kupitia mwili unaoonekana…
Mtume Paulo kaielezea vizuri hiyo siri katika 1Timotheo 3:16
1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.
Lakini sio tu Mtume Paulo aliyefunuliwa hiyo siri, bali pia Mtume Yohana, aliyekuwa mwanafunzi wa BWANA YESU, alifunuliwa hiyo siri ya MUNGU kudhihirika katika mwili..
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika………… 14 NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika…………
14 NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”
Na huyu Neno aliyevaa mwili alikuwa si mwingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO, MKUU WA UZIMA!!!.
Tena Mtume huyu huyu Yohana kazidi kuliweka hili wazi katika nyaraka yake nyingine aliyoiandika kwa watu wote.. na kusema kuwa lile NENO lililokuwa linasikiwa zamani, limefanyika mwili, na wakaushika ule mwili na kuupapasapasa (yaani mwili wa BWANA YESU).
1Yohana 1:1 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima”
Kumbe hili Neno lilianza kwa kusikiwa, baadaye likaonekana (maana yake lilivaa mwili)..na Mitume wakalipapasa (maana yake waliushika mwili wa BWANA YESU) kabla na baada ya kufufuka.
Kwahiyo KRISTO ni Neno la MUNGU na ni MUNGU pia aliyeuvaa mwili, ni Mungu pamoja nasi (Imanueli) ndio maana katukuka kuliko vitu vyote na viumbe vyote.
Je umemwamini na kumpokea maishani mwako?..kama bado fahamu kuwa hakuna njia nyingine yoyote ya kufika mbinguni isipokuwa kwa njia ya yeye. Na pia hakuna mtu wala malaika, wala kiumbe kingine chochote kitakachoweza kukupenda wewe au mimi katika viwango atupendavyo BWANA YESU.
Sasa ni heri umtumainie huyu YESU ambaye si mnafiki katika upendo, mwanadamu anaweza kukunafikia, mchungaji anaweza kukunafikia, lakini YESU, ni wa UPENDO USIO NA UNAFIKI NDANI YAKE. Yasikilize maneno yake, yakubali na yapokee.
BWANA AKUBARIKI.
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”
Roho Mtakatifu ni nani?.
Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu katika kujifunza Neno la Mungu. Leo tutaona mambo Makuu sita (6), ambayo Mungu anatumia kuondoa uovu ndani ya mtu, na kumfanya awe mtakatifu kabisa kama yeye alivyo. Ikiwa wewe umemfuata Kristo basi tarajia mambo haya matano atayatumia katika maisha yako, kukukamilisha.
Tukianza na
Kumbuka sisi sote tulizaliwa na deni la dhambi. Hivyo tulistahili hukumu ya mauti, (Warumi 6:23), Lakini deni hilo lilikuja kulipwa na Bwana wetu Yesu kwa kifo chake pale msalabani (Warumi 5:8). Kumwagika kwa damu yake, sote tumepokea “msamaha wa dhambi” bure kwa neema. Hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kukubaliwa na Mungu, kwa uweza wake mwenyewe. Kwahiyo damu ya Yesu imekuwa hatua ya kwanza ya sisi kukubaliwa na Mungu.
Sasa tunaweza kupokea msamaha kweli, tukasemehewa, lakini dhambi bado ikawepo ndani yetu. Na hilo sio kusudu la Mungu atusemehe tu, halafu atuache tuendelee kuwa watumwa wa dhambi ndani kwa ndani. Si lengo la Mungu, hata mtu mwenye upendo wa dhati wa Yule aliyekosewa naye, anapoona amemsamehe, huwa hamwachi tena kesho arudie kosa lile lile ili, amsamehe, hapana, bali humwonyesha njia ya kuepuka makosa ili yeye mwenyewe aweze kusimama kwa ujasiri mbele zake. Na ndivyo ilivyo kwa Mungu mara baada ya kupokea msamaha wa dhambi, huyo mtu anaanza hatua ya utakaso wa Mungu ambao sasa hufanywa na Roho Mtakatifu aliyeingia ndani yake, Ndio hapo inakuja hatua ya pili,
Biblia inasema Neno ni kama maji, ambayo yanasafisha.
Waefeso 5:26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Umeona, Kristo hulisafisha kanisa lake, kwa Neno, ndio maana wewe kama mtu uliyempokea Yesu, Ni lazima uwe na juhudu nyingi sana za kusoma Neno la Mungu kila siku, usikie maonyo, fundisho, agizo, njia, (2Timotheo 3:16), Na kwa jinsi unavyojifunza sana, ndivyo unavyosafishwa moyo wako na roho yako, hatimaye unaanza kujiona mtu ambaye huna hatia ndani yako. Na hapo ndipo unapojikuta unaacha baadhi ya mambo uliyokuwa unafanya huko nyuma. Kumbuka biblia uliyonayo sio kitambulisho cha mkristo au pambo la mkoba, bali ni maji hayo ya kukusafisha, hivyo oga kila siku, uwe msafi. Kwasababu usipofanya hivyo utakuwa mchafu tu sikuzote.
Kwa kawaida sio kila uchafu hutoka kwa maji, mwingine huitaji moto ili kuundoa. Kwamfano ukiupata mwamba wenye dhahabu ndani yake ukipitisha maji huwezi toa uchafu uliogandamana nao,hivyo wale wafuaji, wanaupitisha kwenye moto, kisha unayeyuka na baada ya hapo uchafu na dhahabu hujitenga kisha wanaikusanya dhahabu. Ndivyo ilivyo na Mungu kwa watoto wake. Upo moto ambao wewe kama mwana wa Mungu ni lazima tu utapitishwa hata iweje, kuondoa mambo sugu yaliyogandamana na wewe yasiyoweza kutoka kwa Neno tu bali kwa hatua ya kimaisha, ndio huo unaoitwa “ubatizo wa moto”. Mfano wa huu ndio ule uliompata mfalme Nebukadreza (Danieli 4), kukaa miaka saba maporini kula majani ili tu aondolewe kiburi ndani yake. Ni aina Fulani ya maisha ambayo kwako yatakuwa kama moto, lakini mwisho wake hukuletea faida ya roho yako.
1Petro 1:6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Zipo tabia nyingine ambazo Mungu anaona mwanawe anakuwa nazo kwa ujinga tu, hivyo, ili kuundoa ujinga huo, haihitaji maji wala moto, bali kiboko. Anapoona unafanya jambo Fulani kwa makusudi na alishakukataza hapo awali fahamu pia kiboko kitapita juu yako.
Waebrania 12:6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Waebrania 12:6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Biblia inasema pia..
Mithali 22:15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Yohana mbatizaji kwa uvuvio wa Roho aliandika maneno haya kuhusu Bwana Yesu..
Mathayo 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Mathayo 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Yesu akija kwako, fahamu kuwa mkononi ameshika pepeto pia, na wewe utawekwa juu yake, Anajua kabisa ulipo wewe makapi pia yapo, uliyotoka nayo huko shambani (ulimwenguni), hivyo ili kukutenga nayo, ataanza kukupepeta, kama vile ngano, utarushwa juu, utashushwa chini, utarushwa juu utashushwa chini, huwezi kuachwa utulie, lengo ni kuhakikisha makapi yote yanapeperushwa na upepo, iwe ni watu, vitu, utaona tu unapelekwa mbele, unarudishwa nyuma..baadaye akishaona ni ngano tu imebakia chini, hapo ndipo anapokuacha, unaanza kuona ushwari. Hii ilimkuta Ibrahimu, Bwana anamtoa Uru, anampeleka kaanani, mara anakimbilia Misri, mara anarudisha, lakini baadaye Mungu alimpa pumziko, baada ya kuona wote waliokuwa wameshikamana naye hawapo naye.
Usishangae kutokuwa na utulivu katika nyakati fulani za maisha yako wokovu, wakati Fulani unafanikiwa, halafu unarudi chini, wakati Fulani unapata amani kotekote, gafla inaondoka, unapata, ghafla tena unapoteza, tulia tu, kuwa na amani ndani ya Kristo, utakuwa tu, imara, wala hiyo misukosuko haitakuwepo tena, ni kwanini iwe hivyo? Ni kwasababu makapi yanapeperushwa na upepo.
Kaa ukifahamu Yesu anajulikana pia kama tabibu,(Marko 2:17) na anajua maovu mengine unayoyafanya yanatokana na magonjwa na majeraha ya rohoni, anajua hali yako ilivyo hivyo anachokifanya ni kukutibu yeye mwenyewe, ndio hapo unashangaa tu mwingine anatokwa na mapepo yaliyokuwa yanamsumbua na kumpelekea kutenda dhambi mwingine anapona udhaifu fulani, uliokuwa unamfanya amkosee Mungu, mwingine anapokea faraja, amani, utulivu usio wa kawaida, anashangaa kuona tofauti kubwa ya sasa na hapo kabla. Hili nalo mtu aliyempokea Kristo ataliona kwenye maisha yake. Na atimaye anakuwa mwema yeye tu mwenyewe, asukumwi tena na presha ya dhambi fulani. Kwasababu tabibu mkuu ameshamponya, ambaye akikuweka huru, unakuwa huru kwelikweli.
Ufunuo 3:18
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na DAWA ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
Hivyo, wewe kama mwana wa Mungu, tambua yote hayo yatapita katika sehemu Fulani ya maisha yako. Usidhani kusafishwa tu na damu ya Yesu ndio basi, utatakaswa na hiyo ni katika maisha yako yote. Haiwezekani mtu aliyeokoka ambaye amepokea Roho maisha yake yote awe Yule Yule wa zamani, hizo sio kanuni za wokovu, wala sio kusudi la Mungu. Ukubali utakaso, au usiwe mkristo kabisa. Kwasababu hivi viwili huenda sambamba wala haviwezi kutenganishwa. Huo ndio upendo wa Mungu.
Utukufu na heshima ni vyake milele na milele.
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> hhttps://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
(Opens in a new browser tab)UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
Ipi tofuati kati ya UTAKATIFU na UKAMILIFU?
Yezebeli alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya nchi ya Lebanoni, mahali pajulikanapo kama Sidoni (1Wafalme 16:31), karibu sana na mji wa Tarshishi, ule ambao Nabii Yona alienda kuhubiri, na alikuwa ni binti wa kifalme, hivyo alitokea katika familia tajiri.
Mwanamke huyu hakuwa Mwisraeli, ila aliolewa na Mfalme wa Israeli aliyeitwa AHABU, ikambidi ahame kutoka katika Taifa lake hilo na kuhamia Israeli, katika mji wa Samaria pamoja na miungu yake, na tamaduni zake.
Mfalme wa Israeli akamfanya kuwa Malkia, jambo ambalo BWANA Mungu alishalikataza kwa kinywa cha mtumishi wake Musa kuwa wana wa Israeli wasioe wanawake wa kimataifa, kwasababu watawageuza mioyo waabudu miungu mingin, Lakini Mfalme Ahabu alifumba macho yake asione hilo, na badala yake akamwoa YEZEBELI.
Na Yezebeli kwakuwa si Mwisraeli, bali alitoka Taifa lingine lenye miungu mingine, basi aliingia Israeli na miungu yake hiyo, na makuhani wake.. Hapo ndipo mambo yalipoanza kuharibika kwa wana wa Israeli!.. shida ikawa kubwa mpaka Bwana MUNGU kumnyanyua Eliya Nabii.
Sasa zifuatazo ni roho (3) alizokuwa nazo Malkia Yezebeli, zilizoliharibu Taifa la Israeli, na zinazofanya uharibifu leo katika kanisa na nje ya kanisa.
1. UKAHABA
Hii ni sifa ya kwanza ya Malkia Yezebeli,..Biblia inasema alikuwa ni “Mzinzi”, kwani ndiye mwanamke pekee aliyeonekana katika biblia kapaka UWANJA usoni na KUJIPAMBA KICHWA! Kwa lengo la kuvutia ukahaba..Hakuna mwanamke mwingine yoyote katika biblia yote anayetajwa kufanya mambo hayo..
2Wafalme 9:30 “Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; AKATIA UWANJA MACHONI MWAKE, AKAPAMBA KICHWA CHAKE, akachungulia dirishani”
Yezebeli anamwona YEHU anakuja, kwa tabia yake ya uzinzi, anaanza kujipaka uwanja machoni, na kupamba kichwa ili amlaghai YEHU apate kulala naye!. Na wala hata hakuwa na uchungu kwa kifo cha mwanae, yeye anawaza uzinzi tu.
Roho hii inatenda kazi hata leo… huoni hata watu leo wanaenda misibani wamejipodoa… mahali pa kwenda kutafakari mwisho wa safari ya mtu ulimwenguni, wengine wanaenda wamejipodoa kwa lengo la kuvutia ukahaba kama alivyofanya Yezebeli, katika msiba wa mwanae..
Roho hii imeingia mpaka makanisani, utaona wanawake na mabinti sehemu za ibada wanaingia kwa mionekano kama ya YEZEBELI, bila aibu wala hofu!..viungo vyao vipo wazi, nguo walizovaa ni za nusu tupu, nyuso zimejaa rangi, na vichwa vimepambwa kama Yezebeli, na hawaambiwi chochote, na wala wenyewe hawasikii chochote ndani yao kikiwahukumu… pasipo kujua kuwa hiyo ni roho ya YEZEBELI, inaishi na kutenda kazi, kama ilivyokuwa enzi za mfalme Ahabu.
Dada, Mama acha kupamba uso!!!, ndani na nje ya kanisa, hiyo ni roho ya YEZEBELI, ya Ukahaba…usidanganywe na shetani kwa kukuambia kuwa ni urembo tu.. ni urembo tu!!.. hakuna urembo ndani ya sare ya kikahaba.. Utavaaje sare ya askari na ukasema ni urembo tu!!..
Na hii roho ya Yezebeli imeingia pia kwa wanaume,..kama mwanaume anasuka nywele zake, na kupaka uwanja usoni, na kuvaa nguo nusu tupu, na kujichora mwili wake… roho ya Yezebeli inatenda kazi ndani yake.
2. UCHAWI
Pamoja na kwamba Yezebeli alikuwa ni kahaba, biblia inasema pia alikuwa ni mchawi.
Na Uchawi wa Yezebeli ulianzia nchini kwake alikotoka, kutokana na aina ya miungu aliyokuwa anaiabudu. Kwani alikuwa anaabudu “mungu baali”, ambaye kwa asili makuhani wake wote walikuwa ni wachawi na Yezebeli ndiye aliyekuwa mkuu wao.
2Wafalme 9:22 “Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na UCHAWI WAKE NI MWINGI?”
Na uchawi wa Yezebeli mbali na kuloga, alikuwa pia ni mkaidi
3. NABII WA UONGO.
Ufunuo 2:20 “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule MWANAMKE YEZEBELI, yeye AJIITAYE NABII na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ILI WAZINI na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu”.
Roho ya Yezebeli inawafundisha watu “Kuzini”.. Inawafundishaje?.. si kwa njia nyingine isipokuwa kwa injili ya kwamba “Mungu haangalii mwili anaangalia roho”… Injili hii, inawafanya watu wavae watakavyo..ili lile neno Bwana YESU alilolisema kuwa “amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye nafsini mwake” litimie juu yao kupitia yale mavazi ya kikahaba wavaayo.
Dada/mama fahamu kuwa uvaapo mavazi ya kikahaba kama Yezebeli halafu mwanaume akikutamani tayari umekwisha kuzini naye, hata kama hajakushika mkono. (wewe na yeye wote mmezini, na si yeye tu!.. bali hata na wewe, ambaye hujui kama umetamaniwa kwa mavazi yako). Sasa jiulize unapotembea mtaani umevaa nguo hizo za nusu uchi, umezini na wanaume wangapi!
Hii roho ya Yezebeli ipo makanisani leo!.. ipo kwa wengi wanaotambulika kama watumishi wa Mungu, hii ni roho ya Unabii wa Uongo, inayowafundisha watu UZINZI!, kwa kujua na kutokujua.
Hivyo jihadhari na injili hiyo ya adui, isemayo “Mungu anaangalia roho na haangalii mwili”.. Ulinde mwili wako usiwe chanzo cha kuipoteza roho yako moja kwa moja.
Na tabia ya hii roho ya YEZEBELI ni kushindana na Roho ya kweli ya Mungu.. Ndio maana utaona Malkia Yezebeli katika Uzinzi wake, na uchawi wake na unabii wake wa uongo, hakuwahi kamwe kupatana na Nabii Eliya, wala kujinyenyekeza kwake..zaidi sana utaona Yezebeli baada ya kusikia ishara Eliya aliyoifanya ya kushusha moto na kuwaua manaabii wake wa baali, aliapa kumlipa kisasi Eliya, na wala hakumwogopa hata Mungu. (Ni roho ya kiburi).
Roho hii ikishakita mizizi ndani ya mtu, inamfanya kuwa na kiburi, na mkatili hususani katika matumishi wa kweli wa Mungu, na inakuwa inamfanya mtu kuichukia njia ya kweli na watumishi wa Mungu wa kweli.
Jivue roho ya UYEZEBELI.. Mvae BWANA YESU (Warumi 13:14). Hizi ni siku za Mwisho na Bwana YESU anarudi.
Maran atha!
YEZEBELI ALIKUWA NANI
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
KIMBIA! KIMBIA! KIMBIA!
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
UTANGULIZI: Neno la MUNGU ni DAWA, iponyayo Nafsi, Mwili na Roho.. Maombi yanayosimamiwa na Neno la MUNGU yanakuwa na nguvu kuliko yasiyo na msingi wa NENO, Hivyo wakati wa kuomba au kuombea jambo fulani, ni vyema Mwamini akawa na maandiko machache ya kusimamia wakati wa Maombi.
MAOMBI YASIYO NA NENO LA KUSIMAMIA ni kama BENDERA ISIYO NA MLINGOTI!!….Hivyo ni vyema kulijua Neno la kulitumia wakati wa Maombi.
AMANI:
Ikiwa Amani imepungua au imepotea kabisa katika nyumba, ambapo inafikia hatua Baba haelewani na Mama, au wazazi hawaelewani na watoto, au watoto kwa watoto hawaelewani, vurugu imekuwa nyingi jambo ambalo hapo mwanzo haikuwa hivyo…. Na wewe kama Baba, au Mama, au Mtoto uliye na Kristo unaliona hilo na unatamani msaada kutoka kwa Baba wa mbinguni, kurejesha mambo yote yawe sawa.
Basi mistari ifuatayo inaweza kukufaa wakati wa maombi baada ya kuitafakari kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Zaburi 4:8 “KATIKA AMANI nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama”.
Zaburi 29:11 “Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana ATAWABARIKI WATU WAKE KWA AMANI”.
Zaburi 122: 7 “AMANI NA IKAE NDANI YA KUTA ZAKO, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, AMANI IKAE NAWE”
Zaburi 122: 7 “AMANI NA IKAE NDANI YA KUTA ZAKO, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, AMANI IKAE NAWE”
Zaburi 147: 14 “Ndiye afanyaye AMANI mipakani mwako, Akushibishaye kwa unono wa ngano”
Ayubu 25:2 “Enzi na hofu zi pamoja naye; HUFANYA AMANI katika mahali pake palipoinuka”
Zaburi 35:27 “Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na AMANI YA MTUMISHI WAKE”.
Zaburi 37: 37 “Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, MAANA MWISHO WAKE MTU HUYO NI AMANI”.
Zaburi 72:7 “Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, NA WINGI WA AMANI hata mwezi utakapokoma”
Zaburi 85:8 “Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, MAANA ATAWAAMBIA WATU WAKE AMANI, Naam, na watauwa wake pia, Bali wasiurudie upumbavu tena”.
Zaburi 85: 10 “Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana”
Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani”.
Ikiwa utaomba maombi hayo kwa Imani, na kwa ufunuo, na ukiwa umejihakika kwamba njia zako zimetakasika mbele zake basi tegemea majibu yake, kwamaana Neno la MUNGU halijawahi kupita kamwe!, wala kushindwa.
Usikose sehemu inayofuata juu ya Mistari ya kusimamia katika MAOMBI YA UPENDO WA FAMILIA.
FAMILIA TAKATIFU: Marimu na Yusufu.
TUNA WAJIBU WA KUOMBEA MAHALI TULIPO.
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake
Umoja katika Ukristo ni jambo linalokimbiwa na wengi lakini ndilo jambo pekee lililobeba UTUKUFU WA MUNGU wa moja kwa moja. Na maana ya Utukufu wa Mungu ni “MUNGU KUTUKUZWA”.. Maana yake Mungu anatukuzwa katika Umoja.
Labda utauliza ni kwa namna gani?.. Tusome maandiko yafuatayo..
Yohana 17:22 “Nami UTUKUFU ULE ULIONIPA nimewapa wao; ILI WAWE NA UMOJA kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”
Yohana 17:22 “Nami UTUKUFU ULE ULIONIPA nimewapa wao; ILI WAWE NA UMOJA kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”
Kumbe Utukufu Kristo aliotuachia lengo lake la kwanza ni ili tuwe na UMOJA.. Na si kutenda miujiza, na maajabu.. Maana yake Mungu anatukuzwa Zaidi katika UMOJA kuliko katika MIUJIZA na ISHARA. Na ndicho kitu pekee kilicho na nguvu ya kuwafanya watu wamwamini Mungu kuliko ishara na miujiza.
Watu watakapoona umoja wetu katika Mungu, ndipo watavutwa kumwamini Mungu kuliko hata kuona ishara na miujiza halafu hamna Umoja… Na ndicho kitu pekee kinachotufanya sisi tumwamini BWANA YESU, ni kwasababu alikuwa na Umoja na Baba.
Laiti Bwana YESU asingelikuwa na umoja na Baba, ingelikuwa ngumu kumwamini kwa ishara na miujiza pekee, lakini ule Umoja wa Roho kati yake na Baba, umetutengenezea sisi Upendo wa ajabu, na Imani kuu kwa BWANA YESU KRISTO, Kwamba yeye ni kweli na hamna uongo ndani yake.
Na vile vile sisi tukiwa na Umoja na Mungu, na tukiwa na umoja sisi kwa sisi ndipo USHUHUDA WETU UTAKAPOTHIBITIKA ZAIDI kuliko kukaa katika matengano.
Yohana 17:21 “WOTE WAWE NA UMOJA; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ILI ULIMWENGU UPATE KUSADIKI YA KWAMBA WEWE NDIWE ULIYENITUMA. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.
Yohana 17:21 “WOTE WAWE NA UMOJA; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ILI ULIMWENGU UPATE KUSADIKI YA KWAMBA WEWE NDIWE ULIYENITUMA.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi”.
Hapo mstari wa 21 anasema.. “WOTE WAWE NA UMOJA ….ILI ULIMWENGU UPATE KUSADIKI YA KWAMBA WEWE NDIWE ULIYENITUMA”.
Kumbe UMOJA WETU ndio utakaowaaminisha watu kuwa KRISTO ni BWANA! Na si mahubiri yetu kuwa mengi, au miujiza yetu kuwa mingi…ni UMOJA TU!.
Tukilikataa Neno hili, na kufuata njia zetu za matengano, tutakuwa tunajipunguzia wenyewe utukufu wa Mungu, kwasababu KRISTO hakujitenga na Baba, wala hakujitenga na wanafunzi wake.
> Unapochagua kuomba peke yako kila mara na huku ipo nafasi ya kuomba na mwingine mmoja au wawili ni roho ya matengano inayoondoa utukufu wa Mungu. (Bwana wetu YESU KRISTO mara nyingi alipanda mlimani kuomba na wanafunzi wake, na hata katika sehemu za faragha soma Mathayo 17:1, na Marko 14:33-34).
> Unapochagua kila mara kwenda kuhubiri peke yako na wakati kuna nafasi ya kwenda na mwingine mmoja au wawili, ni roho ya matengano ambayo inapunguza utukufu wa Mungu juu yako (Bwana YESU aliwatuma wawili wawili kuhubiri katika miji na vijiji soma Luka 10:1 na Matendo 13:2).
> Unapochagua kila mara kutosema na ndugu yako, kumfariji, au kumtia moyo au kukaa karibu naye, ili hali ni mtu wa Imani moja nawe, mnamwamini Bwana mmoja, mmepokea roho mmoja, na hata ubatizo mmoja hiyo ni roho ya matengano inayoharibu utukufu wa Mungu juu yetu.
Hivyo ni lazima tuuhifadhi Umoja wa Roho kama Neno la Mungu linavyotufundisha ili tusipungukiwe na utukufu wa Mungu.
Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”
Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”
Bwana atusaidie na kutuwezesha.
TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.
JE UNAMHUBIRI KRISTO KATIKA KWELI YOTE?.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
MARINDA KATIKA BIBLIA NI KITU GANI?
BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)
SWALI: Nini maana ya Mithali 21:30 Hapana hekima, wala ufahamu, Wala shauri, juu ya Bwana ?
JIBU: Mstari huo unaweza ukasemwa hivi; “Hapana hekima, wala ufahamu, wala shauri linaloweza kufanikiwa/kusimama kinyume na Mungu”.
Ikiwa na maana iwe ni mwanadamu au malaika, atumie uwezo wake wote, kufanya jambo la hila kinyume na yeye haliwezi kufichika kwasababu yeye ni mkuu zaidi ya vyote. Mpango wa shetani kuliharibu kanisa huawezi kufanikiwa hata azidishe kufanya kazi mara elfu zaidi ya mwanzo hilo haliwezekani kama lilivyoshindikana mbinguni.
Mambo yote yanayotokea hayafiki kwake ghafla tu bila hodi, kama ilivyo kwetu sisi wanadamu. Elimu ya darasani haiwezi pindua ukweli wake wa uungu, wajaposema mwanadamu ametokana na nyani, mwishoni wanarudia kule kule kwenye ukweli wa uumbaji wa kiungu, kwasababu atabakia kusimama kuwa Mungu wa daima, na ataabudiwa vizazi vyote haijalishi dunia itaelimika kiasi gani.
Mungu Anajua mawazo yetu yote tokea mbali, wewe kama mwanadamu huwezi mficha dhambi zako, ukajifanya mbele zake umesahau, au ulikuwa hujui, hata utumie hekima nyingi kiasi gani kuficha ukweli bado anatambua nia ya mioyo yetu.
Anasema;
Zaburi 50:17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi. 19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. 21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako. 22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya.
Zaburi 50:17 Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 18 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.
19 Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila. 20 Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21 NDIVYO ULIVYOFANYA, NAMI NIKANYAMAZA; UKADHANI YA KUWA MIMI NI KAMA WEWE. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane mwenye kuwaponya.
Pale tunapomwona Mungu ni kama sisi ndio unakuwa mwanzo wa kuto-mhofu yeye. Unapokuwa na udhuru wa kuifanya kazi yake halafu unasingizia sina muda, lakini una muda wa kufanya mambo yako, ukidhani yeye hajui nia yako ya ndani, unajidanganya mwenyewe. Unapoepuka maombi, kwa kisingizio umechoka, na bado unataka Mungu akuhudumie, fahamu Mungu anakuelewa vizuri sana, atakuonyesha ambao wanachoka zaidi yako, lakini hawana udhuru. Jambo lolote tulifanyalo, tutambue kwanza kwa Mungu halifichiki.
Kwasababu Hapana hekima, wala ufahamu, wala shauri litakalosimama kinyume cha Mungu
Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.(Opens in a new browser tab)
Je shauri la kuipepeleza Kanaani lilitoka kwa wana wa Israeli au kwa BWANA?(Opens in a new browser tab)
Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?
(Opens in a new browser tab)Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake(Opens in a new browser tab)
SWALI: Nini maana ya Mithali 21:17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
JIBU: Mstari huo unamaana mbili.
Maana ya kwanza ni ya mwilini, ni ukweli watu wanaopenda maisha ya anasa, mwisho wao huwa ni kutofanikiwa. Kwasababu kile wanachokipata ambacho kingepaswa kiwekwe akiba kwa wakati wa baadaye au kiwekezwe kizalishe zaidi, wao hutumia chote katika starehe mfano wa pombe, uasherati, na kununua vitu vya gharama kubwa, lengo tu asionekane amepitwa na wakati, au aonekane wa kisasa.
Hapo anaposema apendaye mvinyo na mafuta, hayo mafuta yanayozungumziwa hapo ni marashi ya gharama ambayo zamani waliokuwa wananunua ni matajiri. Ni sawa na leo labda mwajiriwa analipwa mshahara wa laki tatu (3) kwa mwezi, halafu anakwenda kununua perfume (marashi), ya laki 2, ili tu aonekane wa kisasa, hiyo ni anasa, na mwisho wake ni umaskini.
Anasa ni tunda la majivuno, na kukosa adabu. Hivyo biblia inamfundisha mwanadamu yoyote kuwa, anasa ni kinyume cha mafanikio.
Lakini pia rohoni, anasa ni zao la ufukara wa ki-Mungu. Mtu wa anasa, hutumia muda wake vibaya, kwasababu nyakati zake za ziada huishia kwenye starehe za kimwili na sio kwenye mambo ki-Mungu.
Bwana alisema;
Luka 8:14 Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.
Umeona? Anasa husonga mbegu ya Mungu ndani yako.
Katika kizazi cha sasa anasa ni pamoja na kushinda kwenye tv kutazama muvi kila kukicha, ni pamoja na kushinda mitandaoni kufuatilia vipindi vinavyokupa raha za kimwili na kihisia lakini havikujengi rohoni, ni kuwekeza muda wako katika matanuzi ya mijini na kwenye sherehe-sherehe za kila mara ambazo hazina mpangalio. Muda wote akili yako ipo katika kile kitu wanachosema “ku-party weekend” na marafiki. Ushikapo simu yako, usiku wote ni kuchat, na wale wanaowaita ma-boyfriend na ma-girlfriend. Muda ambao ungepaswa kusoma Neno na kuomba.
Sasa ikiwa wewe umeokoka, na una mwenendo huo wa maisha, usitazamie hapo utazalisha kitu. Utabakia kuwa Yule Yule milele. Biblia inasema ni heri kuona kwa macho kuliko kutangatanga kwa tamaa(Mhubiri 6:9). Sio kila taarifa uifuatilie, sio kila kitu ukitende, viache vingine vikupite, ili upate nafasi ya kuwa karibu na Mungu wako, uwe mtu wa matunda. Komboa wakati.
Shalom..
Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa.
(Opens in a new browser tab)APENDAYE FEDHA HASHIBI FEDHA.
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)