Category Archive maswali na majibu

Nini maana ya 1Wakorintho 4:7?

SWALI: Naomba kufahamu maana ya 1Wakorintho 4: 7 

Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?


JIBU: Ukianza kusoma tokea sura ya kwanza utaona Paulo, anakemea sana baadhi ya tabia ya matengano ambayo ilionekana katika kanisa hili la wakorintho. Iliyozuka kutokana na aina ya mafundisho au utendaji kazi wa waasisi wa huduma, au waliowabatiza, na sana sana kati ya Paulo na Apolo.

Hivyo matabaka haya yakawafanya wajivunue wanadamu, na mafundisho yao. Bila kufahamu kuwa kanisa ni la Kristo na si la wanadamu.

Ndipo Paulo, akaweka wazi kuwa kila mmoja aliitwa kwenye utumishi wa Kristo Yesu, ambao una mchango wake katika kanisa, lakini si kwamba huduma ya mmoja ni bora kuliko nyingine. Akasema mmoja anapanda mwingine anatia maji, lakini mkuzaji ni Mungu.

Sasa katika vifungu hivi anaendelea kuwaambia tabia ya kupambanua watumishi, au huduma, si sawa.  Ndio hapo anasema “Nawe una nini usichokipokea?. Akiwa na maana je! Kuna kipawa gani, au kitu gani chema katika kanisa ambacho hawakukipokea kutoka kwa Mungu,?

Lakini anasema..

Iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?. Yaani kama vyote vilitoka kwa Mungu na sio kwa wanadamu, mbona basi mnajisifia kana kwamba vimekuja kwa uweza wa kibinadamu?.

Kama tumepewa kwa neema iweje sasa tujisifie, kana kwamba tumevipokea kwa nguvu zetu na utashi wa watumishi wetu, na ukuu wao, na uwezo wao wa kuhubiri vizuri? Karama hizi za rohoni hakuna hata mmoja imetoka kwa mwanadamu, wenyewe wamefanyika vyote tu. Hivyo wa kujivunia hapo na kusifiwa hapo ni Mungu wala si Paulo au Apolo.

Jambo ambalo hata leo huonekana kwa baadhi ya watu wa kanisa la leo. Ikiwa tuna msingi katika Kristo, iweje kujivunia makanisa au huduma, na kujiona sisi ndio bora zaidi ya wale wengine?

Ni kweli zipo huduma ambazo si za kweli, hazina msingi sahihi wa Kristo Yesu. Lakini ikiwa wote Injili yetu ni ya Kristo aliyesulubiwa kutukomboa sisi, basi tofauti za kiutendaji kazi, au kiujuzi, zisitufanye tujione bora, kwasababu sio hao wanadamu walitoa hivyo vipawa bali ni Roho Mtakatifu. Na anatenda kazi kama apendavyo yeye, anampa huyu hiki, anampa Yule kile.

Mmoja atapanda, mwingine atatia maji, mwingine mbolea, mwingine mvunaji, lakini atakuzaye ni Mungu mmoja, katika shina la Yesu Kristo Bwana wetu.

Kama mkristo ukijiona una vita vya kiuhuduma, ujue bado ni mchanga kiroho, bado unatabia za mwilini.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

MAUMIVU  NYUMA-YA-HUDUMA.

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Rudi nyumbani

Print this post

Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.(Yakobo 5:9)

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango”.

Yakobo 5:9  Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


JIBU: Neno la Mungu halitoi nafasi ya sisi, kunung’unikiana kwasababu yoyote. Aidha ya kuonewa, au kudhulumiwa, kuaibishwa au kufanyiwa jambo ambalo halikupasa utendewe, Manung’uniko ni zao la kutokuwa na uvumilivu. Na kwamba tukifanya hivyo basi, tafsiri yake ni kuwa tunamfanya Mungu naye aghahiri uvumilivu wake kwetu.

Lakini anatoa, suluhisho, kwamba hayo tuyaache mikononi mwake. Kwasababu yeye ndio mwamuzi wetu. Na kwamba, sio tu mwamuzi lakini  ni mwamuzi ambaye yupo mlangoni. Akiwa na maana kuwa Kristo yupo karibu sana na maonevu, au dhuluma hizo, na kwamba yeye mwenyewe atalipa, wala hatakawia, kwasababu yupo mlango.

Atalipa aidha kwa wakati huu huu duniani,  au siku ile ya mwisho wa Hukumu. Kwake yeye ni lazima haki itendeke. Pia kwa upande mwingine anataka uogope kwasababu ukinung’unika yeye hayupo mbali kukusikia.

Wafilipi 4:5  Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, popote tusimamapo kutoa malalamiko, laumu, kuhesabu makosa, n.k. basi tutambua kuwa Kristo yupo hapo hapo katikati yetu kutusikia. Hivyo tusiwe wepesi ya kunena, bali tujifunze kuwa wavumilivu katika mambo yote. Ili Mungu atuachilie neema yake.

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je, umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo? Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, tubu dhambi zako, kwa kumwamini Yesu upokee ondoleo la dhambi zako, Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Ikiwa upo tayari kumkabidhi leo maisha yako. Basi  fungua hapa kwa mwongozo huo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MWAMUZI WA KWELI:

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Rudi nyumbani

Print this post

JE! MWAMBA HALISI NI NINI KULINGANA NA BIBLIA?

Je! Umejengwa kweli juu yake?

Ukimuuliza mtu, mwamba ni nini, ni rahisi kukujibu YESU. Jibu ambalo ni sahihi, maandiko yanatuthibitishia hilo Yesu kuwa Yesu ni mwamba (Mathayo 21:42, 1Wakorintho 10:4). Lakini lazima ufahamu pia  MWAMBA mwenye anasemaje, kuhusu yeye mwenyewe alivyo.

Ni maneno ambayo tunayasoma lakini si rahisi kuyatafakari kwa ukaribu, embu tusome tena, halafu utaona mwamba alimaanisha nini. (Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa) Soma kwa utulivu.

Mathayo 7:24  Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

28  Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29  kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Umeelewa? Vema hayo maneno?

Kumbe mtu  yeyote anayesikia maneno ya Yesu. Hapo hapo huwa anaanza ujezi.

Lakini tofauti inakuja mahali anapokwenda kujengea,. Yule aliyejenga kwenye mchanga tafsiri yake Yesu anasema, anasikia, lakini hayatendei kazi (Hayafanyi), aliyoyasikia. Hivyo hapo Mchanga, ni KUTOTENDA.

Lakini Yule mwingine aliyekwenda kwenye mwamba tafsiri yake ni anasikia lakini pia anatenda. Hivyo MWAMBA, ni kutenda.

Mwamba sio kumjua Yesu ndugu, mwamba sio kusoma sana biblia na kujua mafumbo na siri zote zilizo katika biblia, mwamba sio kujua kujua tafsiri zote za kigiriki na kiebrania kwenye maandiko, mwamba sio kujua kufundisha vema biblia,.. Sio hivyo vyote.

Mwamba ni KULITENDEA KAZI NENO, Unalolisikia kwake. Hilo tu. Sio kumjua Yesu.

Hatari iliyopo leo, miongoni mwa wakristo wengi, ni kwamba tumejengwa juu ya mafundisho mengi. Lakini hatujajengwa juu ya kutendea kazi mafundisho tunayofundishwa. Ndugu fundisho halikusaidii kuyashinda majaribu, au tufani za mwovu, au dhoruba, au pepo, hapo unafanya kazi ya kuchosha tu,kudumu katika kusikia, kusoma, kusikiliza, bado si suluhisho, kusema nimebarikiwa, nimefunguliwa ufahamu, bado hakukufikishi popote, kama HUTALIISHI hilo Neno.

Ukiwa ni wa kufanya bidii kuliishi NENO moja, wewe ni imara sana kuliko Yule mwenye kujiona anaijua biblia yote

Penda Utakatifu, penda usafi wa moyo, penda kupiga hatua rohoni. Penda matendo mema.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

NAYAJUA MATENDO YAKO.

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

Rudi nyumbani

Print this post

Kuna tofauti gani kati ya “Mwivi” na “Mwizi”?

Swali: Kwanini katika biblia lisitumike neno “Mwizi” na badala yake linatumika neno “Mwivi”…Mwivi ni nini?


Jibu: Mwivi na Mwizi ni Neno moja, lenye maana moja.. isipokuwa ni lugha mbili za nyakati mbili tofauti.

Kiswahili kilichotumika katika kutafsiri biblia ni Kiswahili cha zamani, kilichoitwa “kimvita” ambacho ndicho kimebeba maneno ambayo hatuyaoni katika Kiswahili cha sasa, na mojawapo ya maneno ndio kama hayo “Mwivi na wevi” ikimaanisha “mwizi na wezi”. Ndio maana katika biblia yote huwezi kukuta neno Mwizi, badala yake utakuta mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoeli 2:9, Luka 12:39 n.k )

Maneno mengine ya kimvita (Kiswahili cha zamani) ambayo mengi ya hayo hayatumiki sasa ni pamoja na “jimbi” badala ya “Jogoo”“Kiza” badala ya “Giza”….”Nyuni” badala ya “ndege”…. “Kongwa” badala ya “Nira” na mengine mengi.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “Mwivi” na “Mwizi” ni Neno moja, lenye maana ile ile moja (ya mtu anayeiba).

Lakini mbali na hilo, maandiko yanatufundisha kuwa Bwana YESU atakuja kama “Mwivi”..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”

Je umewahi kujiuliza ni kwanini aje kama Mwivi na si Askari?.. Kwa upana juu ya hilo basi fungua hapa >>ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.

Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

Nini maana ya ELOHIMU?

Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).

Rudi nyumbani

Print this post

Ipi tofauti kati ya Kalvari na Golgotha?

Swali: Je Neno “Kalvari” tunalisoma wapi katika biblia?, na tofauti yake na Golgotha ni ipi?


JIbu: Katika biblia ya Kiswahili hakuna neno “Kalvari”, bali kuna neno “Golgotha” ambalo tunalisoma katika kitabu cha Yohana 19:17

Yohana 19:17 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, GOLGOTHA.

18  Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati”.

Maana ya Neno “Golgotha”, tayari biblia imeshatoa tafsiri yake hapo  kwenye mstari wa 17 kuwa ni “Fuvu la Kichwa”

Sasa neno “Kalvari” maana yake ni nini?

Neno Kalvari linapatikana katika tafsiri chache za lugha ya kiingereza, ambalo asili yake ni lugha ya Kilatini “CALVARIAE” lenye maana ile ile ya “Fuvu la kichwa cha mtu”.

Hivyo “Kalvari” na “Golgotha” ni Neno moja lenye maana moja, isipokuwa lugha tofauti, ni sawa na neno  “church” na “kanisa” ni kitu kimoja ila lugha tofauti.

Kufahamu kwa upana ufunuo uliopo nyuma ya Golgotha, (Fuvu la kichwa), basi fungua hapa >>>FUVU LA KICHWA.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)

Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

Biblia inaposema Yesu ameketi mkono wa kuume inamaana gani?

Rudi nyumbani

Print this post

Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).

Swali: Je wale waliowekewa tayari ni akina nani na kwanini Bwana Yesu aseme maneno yale?


Jibu: Tuanzie kusoma mstari wa 20..

Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

21  Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22  Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23  Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, SINA AMRI KUWAPA, BALI WATAPEWA WALIOWEKEWA TAYARI NA BABA YANGU”.

Ili tuelewe vizuri, hebu tafakari mfano huu.. “wanafunzi wawili wamemfuata mwalimu wao wa darasa na kumwomba washike nafasi ya kwanza kitaifa na mwingine ashike ya pili kitaifa katika mitihani yao ya mwisho wa kuhitimu”.. Unadhani jibu la mwalimu litakuwa ni lipi?..

Bila shaka mwalimu atawauliza.. je! Mtaweza kusoma kwa bidii??.. Na kama wale wanafunzi watajibu NDIO!.. Bado Mwalimu hataweza kuwapa hizo nafasi, bali atawaambia mimi sina mamlaka ya kuwapa bali “Wasahishaji watakaosahisha mitihani ya wote ndio watakaotoa majibu ya mitihani yenu na kuwapanga kama mmestahili hizo nafasi au la”..

Ndicho Bwana YESU alichowaambia hawa wana wa Zebedayo!.. ambao walienda kumwomba nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake.. na jibu la Bwana YESU likawa, ni “kukinywea kikombe”.. maana yake kukubali mateso kwaajili yake!.. Na wao wakajibu “wataweza”.. Lakini jibu la Bwana likawa “Nafasi hizo watapewa waliowekewa tayari”..maana yake waliostahili.

Na hao waliostahili ni akina nani?

Ni wale watakaofanya vizuri Zaidi ya wengine wote katika mambo yafuatayo.

   1. KUKINYWEA KIKOMBE.

Kikombe alichokinywea Bwana Yesu ni kile cha Mateso ya msalabani (Soma Mathayo 26:39), kutemewa mate, kupigwa Makonde, kuvikwa taji ya miiba, na kugongomelewa misumari mikononi..

Na yeyote ambaye atakubali kuteswa kwaajili ya Kristo, na si kwaajili ya mtu au kitu kingine chochote, basi yupo katika daraja zuri la kumkaribia Kristo katika siku ile kuu.

  2. KUBATIZWA UBATIZO WA BWANA YESU.

Marko 10:38  “Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au KUBATIZWA UBATIZO NIBATIZWAO MIMI?”

Swali Ubatizo aliobatizwa Bwana YESU KRISTO ni upi?…. si mwingine Zaidi ya ule wa kufa, kuzikwa na siku ya tatu kufufuka, na kupaa juu (soma  Luka 12:50), Na ubatizo huu mpaka sasa hakuna rekodi ya wazi ya yoyote aliyeupitia..

Ubatizo tubatizwao sasa ni ule wa maji mengi, ambao ni ishara ya kufa na kufufuka na Kristo (Wakolosai 2:12), kwamba tunapozamishwa katika maji mengi na kuibuka juu, ni ishara ya kufa pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye… Lakini Ule hasa wa kufa na kufufuka na kupaa, hakuna rekodi ya wazi ya aliyeupitia.

Isipokuwa unawezekana ndio maana tunasoma katika Ufunuo 11, kuwa wale washahidi wawili, ni miongoni mwa watakaoupitia..

Ufunuo 11:10 “….Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.

11  NA BAADA YA SIKU HIZO TATU U NUSU, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.

12  WAKASIKIA SAUTI KUU KUTOKA MBINGUNI IKIWAAMBIA, PANDENI HATA HUKU. WAKAPANDA MBINGUNI KATIKA WINGU, ADUI ZAO WAKIWATAZAMA”.

Je umempokea YESU?, Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Kristo yupo mlangoni.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

USIWE ADUI WA BWANA

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

UWE KIKOMBE SAFI 

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Rudi nyumbani

Print this post

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Swali: Wenye kutia Kalafati ni watu gani?

Jibu: Neno “Kalafati” limeonekana mara mbili tu katika biblia, katika Ezekieli 27:9 na Ezekieli 27:27.

Na maana yake ni “Kamba nyembamba iliyotengenezwa kwa pamba” ambayo inawekwa katikati ya mianya ya mbao za merikebu, ili kuzuia maji yasipenye katika ile miunganiko. (Tazama picha juu)

Hivyo watu wanaofanya hiyo kazi ndio waliotajwa hapo katika Ezekieli 27:9,

Ezekieli 27:9 “Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, WENYE KUTIA KALAFATI; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako”.

Lakini habari hii inahusu nini?

Ukisoma kitabu hicho cha Ezekieli mlango wa 27 kuanzia mstari wa kwanza, utaona ni unabii unamhusu mfalme wa Tiro. (Kwa urefu kuhusu Taifa la Tiro fungua hapa >>>Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa? 

Lakini hapa ni unabii wa Mfalme wa Tiro, Kwamba kwa kiburi chake na biashara zake nyingi alizozifanya juu ya nchi na katika bahari kupitia merikebu zake, siku inakuja ambapo ataanguka na kushuka chini kwasababu ya dhambi zake nyingi.

Na biashara za baharini alizokuwa anazifanya kupitia merikebu zake kubwa ambazo ndani yake kulikuwa na wana-maji, na “watiao Kalafati” na manahodha, zitaanguka na shughuli zao hizo zitaisha!

Ezekieli 27:27 “Mali zako, na bidhaa yako, na utajiri wako, wana-maji wako, na rubani zako, na WENYE KUTIA KALAFATI WAKO, na wafanya biashara wako, na watu wako wa vita wote, walio ndani yako, pamoja na jeshi lako lote lililo ndani yako, wataanguka katika moyo wa bahari katika siku ya kuangamia kwako”.

Ufunuo kamili pia kwa anguko la ulimwengu pamoja na dini zake za uongo katika siku za mwisho..

Ufunuo Ufunuo 18:2  “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3  kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake………………..

9  Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

10  wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

11  Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

12  bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;

13  na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

14  Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

15  Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza”

Je Umeokoka kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa, sawasawa na Marko 16:16?. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Kristo amekaribia kurudi.

Kwa msaada Zaidi katika kumpokea Kristo fuatiliza sala hii ya Toba >>KUONGOZWA SALA YA TOBA  au wasiliana nasi kwa namba zetu zilizoanishwa mwisho wa somo hili.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).

Kuna tofauti gani kati ya  “Edeni” na “Adeni”?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

SWALI: Je!  Mithali 6:30 inamaana gani?

Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;  31 Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.

JIBU: Chukulia mfano mtu hajala siku tatu, halafu akaona kuna duka lipo wazi pale jirani, na mwenyewe ametoka, akashawishika kuingia haraka  na kubeba mkate, ili akale. Lakini mwenye duka aliporudi na kuona mkate umeibiwa, alianza kumfuatilia, mwishowe akamkuta amejificha mahali Fulani anakula akiwa katika hali mbaya.

Kibinadamu, atakapoona hali halisi ya mwizi, huwenda ataishia kukasirika tu, au kumgombeza, au kwenda kumwajibisha, kwa mambo madogo madogo. Kwasababu anaona alichokifanya ni kwa ajili ya kusalimu maisha yake tu, ale asife, lakini sio kwa lengo la kuchukua vya watu, akauze, au kuleta hasara kwa wengine.

Lakini sehemu ya pili ya mstari huo anaendelea kusema kama “akipatikana atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake”.

Maana yake ni kuwa kama “atapatikana na kosa”, basi atalipa mara saba. Atagharimikia vyote alivyoviiba mara saba. Sasa kauli hiyo haimaanishi kwamba mwizi huyo huyo aliyeiba kwa ajili ya kujishibisha tumbo lake ndio atalipa mara saba, hapana, vinginevyo mstari huo ungekuwa unajipinga unaposema “watu hawamdharau mwizi akiiba kwa kujishibisha”, bali  anamaanisha kama akipatikana na hatia tofauti na hiyo..mfano aliiba vitu ili akauze, aliiba fedha ili akajiendeleze kwenye mambo yake, alete hasara kwa wengine. Huyo atalipa gharama zote mara saba.

Ndio maana utaona adhabu nyingi za wezi huwa ni kubwa sana zaidi ya vile walivyoviiba, wanapigwa faini kubwa, wengine mpaka wanauliwa, kwa wizi tu mdogo. Hapo ni sawa na wamelipa mara saba.

Je! Hili linafunua nini rohoni?

Kama njaa ya mwilini, inaweza kumfanya mwizi asihesabiwe kosa. Kwasababu watu wanaelewa umuhimu wa kunusuru uhai kwa chakula, vipi kuhusu rohoni. Hata kuna wakati Daudi alikula mikate ya makuhani ambayo  hawakupaswa watu wengine kula, lakini kwasababu alikuwa na njaa yeye na wenzake haikuhesabiwa kwake kuwa ni kosa (1Samweli 21).

Vivyo hivyo rohoni, Mungu anatufundisha sio kwamba tuwe wezi, hapana, lakini anataka tuthamini sana roho zetu, pale zinapokuwa hazina kitu, zina njaa. Iweje mtu unakaa hadi unakufa kiroho halafu unaona ni sawa kuwa hivyo hivyo kila siku. Hufanyi jambo Fulani la kujinasua katika hiyo hali yako mbaya rohoni, unaendelea tu hivyo hivyo. Tafuta kwa bidii chakula cha kiroho usife ndugu. Jibidiishe.

Iba muda wako wa kufanya mambo mengine ili ukipate chakula cha kiroho. Ni kweli ulipaswa kuwepo mahali Fulani pa muhimu, embu ghahiri muda huo, nenda kasome biblia, nenda kaombe, nenda kasikilize mahubiri yatakayokujenga. Ulipaswa uwepo kazini, lakini kwasababu ibada ile ni muhimu embu usione shida kughahiri.

Huna biblia Iba hata pesa yako ya matumizi ya muhimu kanunue, acha uonekane mjinga nenda kanunue biblia au vitabu vya rohoni vikujenge. Tafuta ile MANA iliyofichwa.

Siku hizi ni za mwisho. Na Bwana alishatabiri duniani kutakuwa na njaa, sio ya kukosa chakula au maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Mungu ya kweli. Usipojiongeza katika eneo la ukuaji wako kiroho.  Ni ngumu kuvuka hizi nyakati mbaya  za manabii wengi wa uongo, na mafundisho ya mashetani. Usipoyajenga maisha yako ya kiroho, shetani akusaidie kuyajenga kwake.

Amosi 8:11 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana”

Penda biblia, penda kujifunza, penda maombi zaidi ya vingine.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.

NJAA ILIYOPO SASA.

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.

(Opens in a new browser tab)KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

Makasia ni nini? (Yona 1:13).

Swali: Kuvuta Makasia maana yake nini?


Likiwa moja linatiwa ”Kasia”, yakiwa mengi ni “Makasia” … Hizi ni  “Zana” ya kukisaidia chombo kutembea juu ya maji. Zana hii kwa mwonekano ni kama “Mwiko mkubwa”, (tazama picha juu), ambapo mabaharia walipoyavuta basi chombo kilisogea mbele..

Yona 1:13 “Lakini wale watu WAKAVUTA MAKASIA kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana”.

Unaweza kusoma Zaidi kuhusu makasia katika mistari ifuatayo; Marko 6:48, Yohana 6:19,  Isaya 33:21, na Ezekieli 27:6.

Je ni nini tunajifunza katika habari ya Yona na mabaharia hawa kuvuta makasia kurudi pwani?.. Fungua hapa >>>YONA: Mlango 1

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

YONA: Mlango wa 2

HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

YONA: Mlango wa 3

YONA: Mlango wa 4

Rudi nyumbani

Print this post

Upepo wa Mbisho maana yake nini? (Mathayo 14:24)

Swali: Pepo za Mbisho ni nini?


Jibu: Turejee kuanzia mstari wa 23.

Mathayo 14:23 “Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.

24  Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; MAANA UPEPO ULIKUWA WA MBISHO.

25  Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.

26  Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu”.

Maana ya neno “Mbisho” ni “Ukinzani”. Hivyo hapo aliposema “Upepo ulikuwa wa Mbisho”, maana yake upepo ulikuwa ni wa ukinzani, (yaani ulikuwa unavuma kinyume na uelekeo waliokuwa wanauendea).

Utasoma tena aina ya upepo huu ikitajwa katika Matendo 27:4,

Matendo 27:4 ”Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana PEPO ZILIKUWA ZA MBISHO”.

Safari yoyote ya majini, ikikutana na pepo za mbisho, safari hiyo inakuwa ni ngumu sana.. Kwasababu upepo utakuwa unavuma kinyume na ile merikebu na hivyo kuchelewesha safari au hata kuirudisha nyuma.

Lakini pepo za Mbisho zinafunua nini kiroho?

Pepo za mbisho kiroho ni kila aina ya matatizo, na shida na dhiki na vikwazo kutoka kwa yule adui vinavyokawisha au kurudisha nyuma safari yetu ya Imani hapa duniani.

Ndio maana utaona katika habari hiyo ya Mathayo 14:23-36, kabla wanafunzi wa Bwana YESU kufika nchi ya Wagerasi kwaaijli ya huduma ya kufundisha na kuponya wagonjwa na kuwafungua walioteswa na shetani, adui aliwatumia “Upepo huu wa mbisho”, lengo ni ili wasifanikiwe safari yao hiyo.

Lakini BWANA YESU alipoingia ndani ya chombo kile ule upepo ukakoma na misuko suko yake, kufunua kuwa zile zilikuwa ni hila za ibilisi.

Hivyo hata sisi tunapokutana na pepo za namna hii katika Imani, suluhisho ni kuzikemea kwa Imani na kwa jina la YESU, na zitatii.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?

Rudi nyumbani

Print this post