Jibu: Turejee,
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, UCHAFU, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, UCHAFU, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Dhambi zote ni “uchafu” lakini zipo dhambi ambazo ni “chafu Zaidi”, hizo ndizo zinazoitwa “Uchafu” Mfano wa hizo ni zile zilizotajwa katika Mambo ya Walawi 18 na 20…(Dhambi za kulala na mnyama na ndugu wa karibu).
Walawi 18:23 “Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; NI UCHAFUKO”. Walawi 20:12 “Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo UCHAFUKO; damu yao itakuwa juu yao”.
Walawi 18:23 “Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; NI UCHAFUKO”.
Walawi 20:12 “Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo UCHAFUKO; damu yao itakuwa juu yao”.
Utaona dhambi nyingine zimetajwa tu kama ni “Machukizo” lakini hizi zimetajwa kama “Uchafuko” maana yake zimezidi machukizo.. Ni uchafu mkuu mbele za Mungu.
Kulala na Mnyama, ni uchafu, vile vile kulala na mama mkwe au baba mkwe ni uchafu..na wachafu wote hawataurithi uzima wa milele sawasawa na maandiko hayo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
Ninyi ni chumvi ya dunia, Andiko hilo lina maana gani?
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
Rudi Nyumbani
Print this post
Swali: Huyu Tirano tunayemsoma katika Matendo 19:9 alikuwa ni nani, na darasa lake lilikuwaje?
Jibu: Tuanzie kusoma mstari ule wa 8 hadi ule wa 11 ili tuweze kuelewe vizuri..
Matendo 19:8 “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa MUDA WA MIEZI MITATU, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. 9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika DARASA YA MTU MMOJA, JINA LAKE TIRANO. 10 Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. 11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.
Matendo 19:8 “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa MUDA WA MIEZI MITATU, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.
9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika DARASA YA MTU MMOJA, JINA LAKE TIRANO.
10 Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.
Baada ya Paulo kuingia Efeso, aliingia katika sinagogi moja la wayahudi ili kuhubiri habari za BWANA YESU, na wachache waliamini na kuitii injili, lakini wengi walikaidi na hata kuitukana kabisa injili mbele ya watu wote..
Mtume Paulo alipoona kuwa wameikataa injili, aliliacha sinagogi hilo (la wayahudi) ambalo pengine lingekuwa ndio sehemu bora kwa watu kujifunzia habari za Bwana YESU, lakini kutokana na ubishi na ugumu wa watu wa sinagogi (wayahudi).. Paulo aliondoka pamoja na wale wachache walioamini (wanafunzi)..na kuhamia kwenye darasa lingine la mtu mmoja wa mataifa aliyeitwa TIRANO. (na kipindi ambacho Paulo alihudumu katika Sinagogi la wayahudi mpaka alipoondoka na kuhamia kwenye darasa la Tirano ni muda wa miezi 3)
Kumbuka hapo biblia inaposema “darasa la Tirano” inamaanisha “jengo” lililokuwa maalumu kwaajili ya kufundishia la mtu aliyeitwa Tirano.
Sasa swali huyu Tirano alikuwa nani?
Biblia haijaeleza kwa kina huyu Tirano alikuwa ni nani, lakini ni wazi kuwa alikuwa ni mmoja wa wayunani aliyeamini injili na hivyo akatoa darasa lake hilo liweze kutumika kama mahali pa kufundishia watu injili.. Kama tu Petro alivyoalikwa nyumbani kwa Simoni mtengeneza ngozi kule Kaisaria (Matendo 9:43).
Na mpaka atoe darasa hilo, maana yake hapo kwanza inawezekana alikuwa ni mwalimu wa Falsafa za Kiyunani (kwani wayunani walikuwa ni watu wasomi na wenye kutafuta elimu sana).
Na baada ya Paulo kuhama kutoka kwenye lile Sinagogi na kuhamia kwenye darasa hilo la Tirano, injili ilipata mafanikio makubwa sana, kwani baada ya miaka miwili tu, Watu wote wa Asia waliisikia injili na kuitii..
Matendo 19:10 “Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. 11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.
Matendo 19:10 “Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.
Ikifunua kuwa kuna mambo au mifumo ndani ya masinagogi (au madhehebu) ambayo inazuia kutembea kwa Roho Mtakatifu, zipo tabia ambazo zinazuia injili kusambaa, ipo mienendo inayokinzana na nguvu za Roho Mtakatifu kutembea.. na mojawapo ya hiyo ni tabia ya kupingana na Neno la Mungu (kama ilivyokuwa kwa hawa wayahudi ndani ya Sinagogi)..walikuwa wanashindana na Paulo kutwa kuchwa.
Walikuwa wanaikejeli injili, hata kama wanaona kinachohubiriwa ni kweli kabisa..
Na hata katika madhehebu na makanisa leo ni hivyo hivyo, utakuta mtu au kiongozi anaweza kuiona kweli lakini bado akashindana nayo na kuipinga!..Kiongozi anaweza kuona jambo Fulani sio sawa lakini bado akalipalilia, na kushindana na ile kweli, watu wanaweza kufunuliwa maandiko lakini bado wakawa hawabadiliki wapo vile vile, bado maisha yao ni yale yale NA KWA MATENDO YAO WANAITUKANA INJILI (ingawa midomo yao inakiri).. mambo hayo yanazuia injili kusambaa na kutembea kwa Roho Mtakatifu.
Bwana atusaidie tuzidi kutembea katika kweli yake.
Maran atha!
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
Sinagogi kufumakana maana yake nini? (Matendo 13:43).
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Swali: Mathayo 21:19 inasema “mtini ulinyauka mara (maana yake muda ule ule uliolaaniwa)”.. lakini katika Marko 11:20 biblia inasema “mtini ulinyauka kesho yake, na sio siku ile ile ulipolaaniwa”.. Je mwandishi yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.
Jibu: Awali ya yote ni muhimu kujua kuwa biblia haijichanganyi mahali popote na wala haijawahi kujichanganya mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, fahamu zetu na tafakari zetu ndizo zinazojichanganya pale tunaposoma pasipo kutafakari kwa kina.
Sasa turejee habari hizo moja moja na kisha tuzitafakari tena..
Mathayo 21:18 “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. 19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. MTINI UKANYAUKA MARA. 20 WANAFUNZI WALIPOONA, WALISTAAJABU, WAKISEMA, JINSI GANI MTINI UMENYAUKA MARA? 21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka”.
Mathayo 21:18 “Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.
19 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. MTINI UKANYAUKA MARA.
20 WANAFUNZI WALIPOONA, WALISTAAJABU, WAKISEMA, JINSI GANI MTINI UMENYAUKA MARA?
21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka”.
Hapa tunaona mtini ulinyauka “Mara”.. Lakini turejea kitabu cha Marko ni kama tunasoma habari tofauti…
Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. 13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. 14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”
Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.
13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”
Turuke mpaka mstari wa 19-23..
“19 Na kulipokuwa jioni alitoka mjini. 20 NA ASUBUHI WALIPOKUWA WAKIPITA, WALIUONA ULE MTINI UMENYAUKA TOKA SHINANI. 21 PETRO AKAKUMBUKA HABARI YAKE, AKAMWAMBIA, RABI, TAZAMA, MTINI ULIOULAANI UMENYAUKA. 22 Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake”
“19 Na kulipokuwa jioni alitoka mjini.
20 NA ASUBUHI WALIPOKUWA WAKIPITA, WALIUONA ULE MTINI UMENYAUKA TOKA SHINANI.
21 PETRO AKAKUMBUKA HABARI YAKE, AKAMWAMBIA, RABI, TAZAMA, MTINI ULIOULAANI UMENYAUKA.
22 Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.
23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake”
Hapa tunasoma “MTINI ULINYAUKA SIKU INAYOFUATA na si muda ule ule”.. Sasa swali? habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?
Jibu ni kwamba habari zote ni sahihi, waandishi wote wote wapo sahihi, hakuna hata mmoja aliye mwongo..…
Sasa kwa ufupi ni kwamba mtini haukunyauka muda ule ule Bwana alipoulaani, bali mpaka kufikia kesho yake ndio ulikuwa umekwisha nyauka kabisa..…Sasa swali, kama ni hivyo kwanini Mathayo aseme ulinyauka MARA?…
Jibu la swali hili ni kwamba…si kila mahali panapotumika neno “Mara” panamaanisha “dakika ile ile, au sekunde ile ile, au muda ule”… Hapana!.. Bali neno “Mara” linaweza kumaanisha kipindi fulani cha muda/wakati… ili tuelewe vizuri, tusome habari ifuatayo..
Marko 1:26 “Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. 27 Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii! 28 Habari zake ZIKAENEA MARA KOTEKOTE KATIKA NCHI ZOTE kandokando ya Galilaya”
Marko 1:26 “Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.
27 Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!
28 Habari zake ZIKAENEA MARA KOTEKOTE KATIKA NCHI ZOTE kandokando ya Galilaya”
Hapo biblia inasema habari za Bwana YESU zikaenena “MARA KOTE KOTE KATIKA NCHI ZOTE”… Sasa swali??…Je zilienea sekunde ile ile, au muda ule ule, aliotoa Pepo?..Jibu ni la!...bali ni baada ya kipindi Fulani cha wakati labda masaa kadhaa mbele au siku moja mbele au siku kadhaa???… Kwani isingewezekana ndani ya sekunde ile ile muujiza ulipotokea, habari zifike Galilaya yote ambayo ilikuwa na vimiji vidogo vidogo Zaidi ya 400 kulingana na historia na miji hiyo ikiwemo Nazareti, Kapernaumu, korazini na Bethasaida, Na tena si Galilaya tu!, na hata nje ya Galilaya, maana hapo anasema taarifa zilifika miji yote ya kandokando ya Galilaya (maana yake nje ya Galilaya).
Kwa mantiki hiyo basi tutakuwa tumeelewa kuwa Mathayo alipotumia neno “kunyauka Mara” hakumaanisha sekunde ile ile, bali alimaanisha kuwa ni kwa kipindi Fulani cha masaa kadhaa, (haraka sana, ambako sio kwa kawaida kwa desturi ya miti kunyauka)… kwa maana kikawaida mpaka mti unyauke unachukua siku kadhaa, na huo ni kama umekatwa…sasa ule haukuonekana kama umekatwa, lakini ulinyauka kabisa (Hivyo ni muujiza).
Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa mtini mpaka kufikia asubuhi ndio ulionyesha kunyauka na wanafunzi walishagaa hiyo asuhubi hivyo biblia haijichanganyi mahali popote..
Je unaliamini Neno la Mungu?.. Na je umeokoka?…Kama bado ni nini kinachokusubirisha usimpokee Bwana YESU??.. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na YESU yu mlangoni.. hivyo usiyachezee maisha yako wala mtu mwingine yoyote asiyachezee..
MTINI, WENYE MAJANI.
KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
BADO UPO YERUSALEMU TU..GALILAYA HUTAKI KWENDA?
Swali: Je biblia takatifu inajichanganya katika habari ile ya binti wa Yairo?.. kwamaana katika Marko na Luka inaonyesha kuwa Binti alikuwa katika kufa! (Marko 5:23) Lakini katika Mathayo 9:18 inasema binti alikuwa amekwishakufa, sasa habari ipi ni sahihi kati ya hizo mbili?
Jibu: Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa biblia haijichanganyi mahali popote, isipokuwa pambanuzi zetu, na tafakari zetu ndizo zinazochanganyikiwa. Sasa ili tuelewe vizuri, turejee mistari hiyo..
Marko 5:21 “Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari. 22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, 23 akimsihi sana, akisema, BINTI YANGU MDOGO YU KATIKA KUFA; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi 24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.”…..
Marko 5:21 “Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
22 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,
23 akimsihi sana, akisema, BINTI YANGU MDOGO YU KATIKA KUFA; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi
24 Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.”…..
Turuke mpaka mstari ule wa 35 na 36 ili tuimalizie habari hii kama ilivyoelezewa na Marko..
35 Hata alipokuwa katika kunena, WAKAJA WATU KUTOKA kwa yule mkuu wa sinagogi, WAKISEMA, BINTI YAKO AMEKWISHA KUFA; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? 36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu”
35 Hata alipokuwa katika kunena, WAKAJA WATU KUTOKA kwa yule mkuu wa sinagogi, WAKISEMA, BINTI YAKO AMEKWISHA KUFA; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?
36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu”
Katika kisa hiki ni kweli tunaona taarifa zinaanza na binti kuwa katika HALI YA KUFA, na zinaishia na BINTI KUFA.. Lakini tukirejea katika kitabu cha Mathayo tunaona habari nyingine ambayo inaonekana kama ni tofauti kidogo..
Turejee…
Mathayo 9:18 “Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, BINTI YANGU SASA HIVI AMEKUFA; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. 19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake”……….
Mathayo 9:18 “Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, BINTI YANGU SASA HIVI AMEKUFA; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.
19 Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake”……….
Hapa tunasoma kuwa Jumbe-Yairo anamwambia Bwana kuwa Binti yake amekwisha kufa, na si yu katika kufa!, hivyo aende kumwekea mikono afufuke.. sasa swali je! Biblia inajichanganya?
Jibu ni la!.. kama tulivyosema, biblia haijichanganyi, isipokuwa ni pambanuzi zetu.
Sasa ili tukiweke hiki kisa vizuri; ni kwamba Yairo alipotoka nyumbani mwake kumfuata Bwana YESU, binti yake alikuwa hajafa bado!, ila alikuwa katika hali ya kufa,..na alipokutana na Bwana akamwomba aende amwekee mikono ili apone, sawasawa na Marko alivyorekodi hapo katika Marko 5:23, tukio ambalo halijarekodiwa na Mathayo..
Lakini alipokuwa katika kumsihi Bwana kuna watu baadhi waliotokea nyumbani kwake na kumpa taarifa kuwa binti yake amekwisha kufa!…Sasa Yairo aliposikia kuwa mwanae kafariki hakukata tamaa, bali aliendelea kumsihi Bwana kuwa aende kumwekea mikono ili afufuke hata kama amekwisha kufa!, Na Bwana YESU aliposikia hayo akaahidi kwenda naye.
Lakini alipokuja mtu mwingine kutoka nyumbani mwake kumpa hizo hizo taarifa kuwa binti yake kashafariki hivyo asizidi kumsumbua mwalimu… (maana yake alikuwa anarudia rudia kumwambia, sasa hiyo kauli ya asizidi kumsumbua Marko 5:35) ndio iliyomfanya Bwana YESU amwambie ASIOGOPE!, kwani ndiyo inayokatisha tamaa, na yenye kuua Imani ya Jumbe (Marko 5:36).
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa Mwandishi wa kitabu cha Marko alianzia kuelekezea tukio kuanzia mwanzo kabla ya binti kufa, na kutaja kuwa watu walikuwepo Zaidi ya mmoja waliokuja kumpa taarifa Yairo za kifo cha mwanae (Marko 5:35),
Lakini mwandishi wa kitabu cha Mathayo alianzia kuelezea tukio katikati wakati ambao tayari binti amekwishakufa na hakuelezea kabla ya kufa kwake…..Hivyo hakuna mkanganyiko wowote hapo, na wala mahali pengine popote katika biblia.
Je umeokoka?.. Je unafahamu kuwa tunaishi katika majira ya siku za mwisho?, na Kristo yupo mlangoni?. Kama bado hujampokea unangoja nini?.. Mpokee leo na ubatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Shalom.
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
USIFE NA DHAMBI ZAKO!
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 2)
Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?
Swali: Kwanini biblia ikataze kujiongezea hekima, kwani kuna ubaya gani katika kuongeza hekima?
Jibu: Turejee..
Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.
Hekima inayozungumziwa hapo si hekima ya KiMungu, ambayo hiyo tumeagizwa tuitafute sana..
Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa”.
Tena maandiko yanasema mtu aonaye hekima (hiyo ya kiMungu), biashara yake ni Zaidi ya fedha..
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. 14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. 15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”.
Kwahiyo hekima iliyozungumziwa hapo katika Mhubiri 7:16b ambayo mtu akiwa nayo nyingi inamharibu si hekima ya kiMungu, bali ni HEKIMA YA KIDUNIA.. Ambayo hiyo kwa Mungu ni upuuzi sawasawa na 1Wakorintho 3:18
1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. 19 Maana HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”
1Wakorintho 3:18 “Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima.
19 Maana HEKIMA YA DUNIA HII NI UPUZI MBELE ZA MUNGU. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao.”
Umeona?.. kumbe hekima ya dunia ni upuuzi mbele za Mungu na hiyo mtu akijiongezea sana itamwangamiza!!!.
Sasa mfano wa hekima ya kidunia ni ile inayosema “mwanadamu asili yake ni nyani”.. sasa hii ni elimu/hekima ya kidunia..ambayo imetukuka miongoni mwa wasomi wengi wakubwa, kiasi kwamba mtu aliyezama sana katika hiyo hekima, anajiangamiza mwenyewe, kwani atafikia hatua ya kusema hakuna MUNGU.
Ndio maana hapo biblia inasema “usijiongezee mno”… Maana yake usizame sana katika kuzitafuta, kwani zimejaa upotofu mwingi na ukweli kidogo…
Kwa maarifa Zaidi kwanini biblia iseme “usiwe na haki kupita kiasi” fungua hapa >>>>>USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.
Kwanini Mungu alimkataa Sauli? (1Samweli 15:23)
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.
Mithali 24:17 inamaana gani kusema Tengeneza kazi yako huko nje?
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
SWALI: Naomba kuelewa tafsiri ya mithali 30:32-33, isemayo;
Mithali 30:32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. 33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
Mithali 30:32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
JIBU: Hekima inatueleza matokeo ya kila tendo linapofanyiwa kazi liwe ni zuri au baya litaleta majibu fulani tu. Hapa anatumia mfano wa siagi ambayo inatolewa katika maziwa. Kwa kawaida siagi huwa imejificha ndani ya maziwa, hivyo ili kuipata tu ile siagi, ni kitendo cha kuipiga basi hutokea kwa juu yote,
Sasa kupiga hapo sio kuyachapa maziwa hapana, bali kuyakoroga, ndani chombo Fulani maalumu kwa muda mrefu, baadaye maziwa na siagi hujitenga vyenyewe.
Halikadhalika, pia damu huwa ipo ndani ya pua, lakini haiwezi kutoka yenyewe tu bila kuisumbua pua kwa kuipiga. Kwamfano mtu akikupiga ngumi ya pua ni wazi kuwa damu itatoka tu.
Ndivyo anavyofananisha na ugomvi, kwamba ni jambo ambalo lipo tu, wakati wowote katikati yetu. Mfano tu wa siagi ndani ya maziwa na damu ndani ya pua. Lakini mpaka ugomvi huo ujitokeze, unahitaji kuchochewa, kukorogwa, korogwa, kupigwa pigwa.
Anasema hasira inapoanza, aidha kwa kuzungumza maneno mabaya, mwenzako akakereka, haraka sana, weka mkono wako kinywani, usiendelee kuzungumza, kwasababu kitakachofuata ukiendelea sana ni ugomvi, yaani mapigano, na kudhuriana.
Mauaji, visasi, chuki, asilimia kubwa vimetokana na hasira zilizochochewa.
Lakini, uwezo huu wa kujizuia, una nguvu endapo mtu yupo ndani ya Kristo. Je! Umemwamini? Kama bado na upo tayari kumpokea leo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu chini.
Bwana akubariki
UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
SIKU YA HASIRA YA BWANA.
Mathayo 5:21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
JIBU: Katika vifungu hivi tunaona Bwana Yesu anatoa mtazamo mpya kuhusiana na dhambi ya uuaji. Hapo mwanzo ilidhaniwa kuwa pale mtu anapochukua hatua ya kumchinja ndugu yake, au kumpiga mpaka kufa kama alivyofanya Kaini, ndio umehitimu kuwa muuaji. Lakini Bwana Yesu anasema..
Kitendo tu cha kumwonea hasira ndugu yako, kumfyolea, na kumwapiza, tayari ni kosa la uuaji.
Sasa alikuwa na maana gani kwa maneno hayo matatu. “Hasira, kufyolea na kuapiza?”
Hasira kwa ndugu, huzaa mambo kama kinyongo, uchungu, na wivu. Kwahiyo kama mtu akiwa na mambo kama hayo kwa ndugu yake, mbele ya Kristo amestahili kuhukumiwa.
Lakini pia akimfyolea. Kumfyolea ni kumwita mwenzako mjinga wewe, au mpumbavu wewe. Ukilenga mtu asiye na akili, Kwa urefu wa tafsiri hii fungua hapa>> RACA Hilo nao ni kosa lililostahili kuketishwa kwenye mabaraza ya wazee, utoe hesabu.
Lakini mbaya zaidi kumwapiza. Hichi ni kitendo cha kumtamkia kabisa maneno ya laana. Kana kwamba ni mtu mwovu sana aliyepindukia. Kwamfano kumwita ndugu yako mwana-haramu wewe, au kumwita ‘shoga wewe’, kumwita msenge (neno lenye maana mtu anayeshiriki uovu kinyume na jinsia yake), kumwita pepo, kafiri wewe, n.k. maneno ambayo hayawezi kutamkika, ni sawa na tusi kwa mwenzako. Huko ndio kuapiza.
Adhabu yake Kristo anaifananisha na kutupwa katika jehanamu ya moto.
Hivyo hatupaswi kudhani kuwa, kuua ni mpaka tumwage damu, lakini twaweza kufanya hivyo tokea moyoni mwetu hadi vinywani mwetu, kabla hata hatujafikia kwenye kitendo chenyewe.
Tujazwe Roho Mtakatifu, tuweze kuzishinda tabia hizi mbaya za mwili.
Katika agano la kale ilikuwa sio tu kumpiga mzazi wako, ilikupasa kifo (Kutoka 21:15), lakini pia kumwapiza, adhabu yake ilikuwa ni moja tu na hilo kosa la kwanza yaani kifo.
Kutoka 21:17 “Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa”
Je! Umeokoka? Fahamu kuwa usipomwamini Kristo, na kupokea msamaha wake wa dhambi, hauna uzima wa milele ndani yako. Kwasababu kamwe hutakaa umpendeze Mungu kwa nguvu zako au matendo yako mwenyewe. Na sababu ya Yesu kufa msalabani kwa ajili yako kukusaidia, kupokea msamaha wa dhambi, lakini pia nguvu ya kushinda mambo mabaya kwa Roho wake Mtakatifu tuliopewa. Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu akuokoe leo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya wokovu, Bwana akubariki >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Amen
Bwana alimaanisha nini kusema “atazamaye mwanamke kwa kumtamani” amezini naye?
Je ni sahihi kumwita mtu “Mkuu”?
UFANYE MOYO WA MUNGU UWAELEKEE WATU WAKE.
Jibu:Turejee,
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 13 KWA MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA”.
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13 KWA MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA”.
Mstari huo haumaanishi kuwa Torati yote na Manabii wote walimtabiri Yohana Mbatizaji.. kwamba atakuja kutokea na kuhubiri, na kwamba atakuwa nabii mkuu kuliko wote. Hapana, bali ilimaanisha kuwa Torati iliendelea kuwepo na kufanya kazi, na manabii waliendelea kutokea na kutoa unabii, mpaka wakati wa Yohana kutokea duniani.. na baada ya Yohana ndipo likaanza agano lingine jipya la ufalme wa Mungu kutangazwa na kila mtu kujiingiza kwa nguvu.
Maneno hayo yamewekwa katika Kiswahili kirahisi Zaidi katika kitabu cha Luka..
Luka 16:16 “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”.
Sasa kufahamu nini maana ya Torati na Manabii fungua hapa >>>Nini maana ya “Torati na manabii”?
Lakini ni kwanini aseme tangu wakati wa Yohana ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na watu wanajiingiza kwa nguvu??..Ni kuonyesha kuwa hapo kwanza ilikuwa haiwezekani mtu kujiingiza katika ufalme wa Mungu..ilihitaji kuingizwa.. na waliokuwa wamesimama kama waingizaji wa watu katika ufalme wa Mungu ni Manabii na Torati..
Watu walisubiri maagizo ya Mungu kupitia Nabii au kuhani ndipo wapatanishwe na Mungu… lakini baada ya Bwana YESU kufa na kufufuka kiti cha rehema kimefunguliwa.. Watu hawahitaji tena manabii wala makuhani kumkaribia Mungu… (Maana yake kila mtu ana uwezo wa kumkaribia Mungu kupitia damu ya YESU).
Hatuhitaji tena kwenda Yerusalemu kwa makuhani ndipo tumsikie Mungu, hatuhitaji tena sanduku la agano, hatuhitaji tena nabii atokee ndipo atupe maagizo ya Mungu.. bali kupitia Roho Mtakatifu ndani yetu tunamkaribia yeye.
Kwa kadiri tunavyotia bidii ndivyo tunavyoukaribia na kuuteka ule ufalme..na wenye hekima na bidii ndio wanaoukaribia Zaidi ule ufalme.
Maran atha.
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
MAJINA YA MANABII WANAWAKE
MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.
Mistari ya biblia kuhusu shukrani.
SWALI: Nini Maana ya Isaya 24:16-18, inapomzungumzia mwenye haki, na anaposema Kukonda kwangu!
Isaya 24:16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana. 17 Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani. 18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika
Isaya 24:16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.
17 Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.
18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika
JIBU: Vifungu hivyo vinazungumzia unabii wa Masihi (Yesu Kristo) mwokozi wetu.
Katika mstari wa 16, nabii Isaya anaonyeshwa maono, ya nyimbo za “mwenye haki” ambaye si mwingine zaidi ya Kristo, Kwamba atukuzwe. Jambo ambalo ni la furaha, Kristo kuja duniani, ni tendo ambalo lilishangaliwa sio tu na malaika (Luka 2:8-14), lakini pia na wanadamu (Yohana 12:12-13).
Lakini tunaona katika sentensi inayofuata nabii Isaya, anaonyesha masikitiko yake, kwa kusema Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu, watenda hila wametenda hila. Akifunua kimifano hali ya taabu na huzuni inayompelekea hata kupoteza afya kwasababu ya mienendo ya watu waovu baada ya pale. Yaani badala wampokee mwokozi, wengi walimpinga na kumkataa, wakamsulubisha, na kuukata wokovu, ulioletwa na huyo mwenye haki.
Hivyo katika vifungu vinavyofuata 17-18, Anaeleza hukumu itakayowapata waliopo duniani, kwa kosa la kumkataa masihi, akilenga hasaa siku ile kuu ya Bwana, siku ya mwisho ya ghadhabu ya Mungu ambayo hii dunia itaharibiwa kabisa pamoja na watu waovu. Ambapo kwa urefu wake, inaelezwa pia katika vifungu vinavyofuata.
Unabii ambao ni kweli kabisa, unapompinga Kristo leo, aliye mwenye haki, aliyekuja kukuondolea dhambi zako, huwezi kuikwepa jehanamu ya moto, kwasababu matendo yako pekee hayawezi kukufanya mkamilifu, vilevile katika siku za mwisho ikiwa utakuwepo duniani, huwezi kuyakwepa mapigo ya Mungu juu yako.
Hivyo mpendwa ni heri ukampokea Yesu leo, akusamehe dhambi zako. Jina lako liandikwe kwenye kitabu cha uzima. Mwisho umekaribia sana, Jiulize ukifa leo katika hali ya dhambi utaenda kuwa mgeni wa nani huko ng’ambo ufikapo?
Ikiwa upo tayari kuupokea wokovu leo, upate msamaha wa dhambi zako basi fungua hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
Nini maana ya Mithali 19:21Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.
“Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).
JIBU: Yesu ni mtu ambaye alizungukwa na makutano mengi, hivyo isingekuwa rahisi kwao kumkamata wakati wa mchana, kwasababu walijua watakutana na upinzani mkubwa wa makutano.. kama maandiko yanavyosema katika vifungu hivi;
Mathayo 21:45-46
[45]Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. [46]Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
[45]Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao.
[46]Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Hivyo njia pekee, ilikuwa ni usiku. Tena wakamwendea na marungu na mapanga kujidai kuwa wanakwenda kumtafuta mwizi, huku mioyoni mwao wakijua kabisa wanayekwenda kumfuata ni mtu wa haki.
Na hiyo ni kuthibitisha kwamba walikuwa hawajiamini kwa matendo yao, kwasababu waliyajua ni maovu ndio maana waliyafanya gizani.
Marko 14:48-49
[48]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Ni kama juu ya mnyang’anyi mmetoka wenye panga na marungu, kunitwaa mimi? [49]Kila siku nalikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikamate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia.
Hiyo ndio sababu kwanini wamfuate usiku, lakini hawakujua ndio walikuwa wanairahisisha njia ya wokovu. Kufunua kuwa giza kamwe haliwezi kuishinda nuru.
Yohana 1:4-5
[4]Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. [5]Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
Mwamini Kristo, Nuru yake ikuangazie moyoni mwako.
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani, kulifunua nini?
Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?