Tirano alikuwa nani na darasa lake lilikuwaje? (Matendo 19:9)

Tirano alikuwa nani na darasa lake lilikuwaje? (Matendo 19:9)

Swali: Huyu Tirano tunayemsoma katika Matendo 19:9 alikuwa ni nani, na darasa lake lilikuwaje?


Jibu: Tuanzie kusoma mstari ule wa 8 hadi ule wa 11 ili  tuweze kuelewe vizuri..

Matendo 19:8  “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa MUDA WA MIEZI MITATU, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.

9  Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika DARASA YA MTU MMOJA, JINA LAKE TIRANO.

10  Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.

11  Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.

Baada ya Paulo kuingia Efeso, aliingia katika sinagogi moja la wayahudi ili kuhubiri habari za BWANA YESU, na wachache walioamini na kuitii injili, lakini wengi walikaidi na hata kuitukana kabisa injili mbele ya watu wote..

Mtume Paulo alipoona kuwa wameikataa injili, aliliacha sinagogi hilo (la wayahudi) ambalo pengine lingekuwa ndio sehemu bora kwa watu kujifunzia habari za Bwana YESU, lakini kutokana na ubishi na ugumu wa watu wa sinagogi (wayahudi).. Paulo aliondoka pamoja na wale wachache walioamini (wanafunzi)..na kuhamia kwenye darasa lingine la mtu mmoja wa mataifa aliyeitwa TIRANO. (na kipindi ambacho Paulo alihudumu katika Sinagogi la wayahudi mpaka alipoondoka na kuhamia kwenye darasa la Tirano ni muda wa miezi 3)

Kumbuka hapo biblia inaposema “darasa la Tirano” inamaanisha “jengo” lililokuwa maalumu kwaajili ya kufundishia la mtu aliyeitwa Tirano.

Sasa swali huyu Tirano alikuwa nani?

Biblia haijaeleza kwa kina huyu Tirano alikuwa ni nani, lakini ni wazi kuwa alikuwa ni mmoja wayunani aliyeamini injili na hivyo akatoa darasa lake hilo liweze kutumika kama mahali pa kufundishia watu injili.. Kama tu Petro alivyoalikwa nyumbani kwa Simoni mtengeneza ngozi kule Kaisaria (Matendo 9:43).

Na mpaka atoe darasa hilo, maana yake hapo kwanza inawezekana alikuwa ni mwalimu wa Falsafa za Kiyunani (kwani wayunani walikuwa ni watu wasomi na wenye kutafuta elimu sana).

Na baada ya Paulo kuhama kutoka kwenye lile Sinagogi na kuhamia kwenye darasa hilo la Tirano, injili ilipata mafanikio makubwa sana, kwani baada ya miaka miwili tu, Watu wote wa Asia waliisikia injili na kuitii..

Matendo 19:10 “Mambo haya yakaendelea kwa MUDA WA MIAKA MIWILI, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.

11  Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida”.

Ikifunua kuwa kuna mambo au mifumo ndani ya masinagogi (au madhehebu) ambayo inazuia kutembea kwa Roho Mtakatifu, zipo tabia ambazo zinazuia injili kusambaa, ipo mienendo inayokinzana na nguvu za Roho Mtakatifu kutembea.. na mojawapo ya hiyo ni tabia ya kupingana na Neno la Mungu (kama ilivyokuwa kwa hawa wayahudi ndani ya Sinagogi)..walikuwa wanashindana na Paulo kutwa kuchwa.

Walikuwa wanaikejeli injili, hata kama wanaona kinachohubiriwa ni kweli kabisa..

Na hata katika madhehebu na makanisa leo ni hivyo hivyo, utakuta mtu au kiongozi anaweza kuiona kweli lakini bado akashindana nayo na kuipinga!..Kiongozi anaweza kuona jambo Fulani sio sawa lakini bado akalipalilia, na kushindana na ile kweli, watu wanaweza kufunuliwa maandiko lakini bado wakawa hawabadiliki wapo vile vile, bado maisha yao ni yale yale NA KWA MATENDO YAO WANAITUKANA INJILI (ingawa midomo yao inakiri).. mambo hayo yanazuia injili kusambaa na kutembea kwa Roho Mtakatifu.

Bwana atusaidie tuzidi kutembea katika kweli yake.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

Sinagogi kufumakana maana yake nini? (Matendo 13:43).

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments